Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live

Mwakyembe atembelewa na Uongozi wa TLS

$
0
0
Serikali imekiasa Chama cha Wanasheria cha Tanganyika (TLS) kibaki kuwa chombo cha kitaaluma cha kulinda weledi, viwango na maslahi mapana ya uanasheria na kisikubali kuyumbishwa na mihemko ya uanaharakati wa kisiasa isiyo na tija kitaaluma.

Akiongea na ujumbe wa TLS kwenye ofisi yake ndogo ya Dar es Salaam leo (15/2/17), Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria, Dk. Harrison Mwakyembe amesema TLS ibakie njia kuu kama ilivyo kwa vyama vingine vya kitaaluma nchini, isighilibiwe na michepuko.

Amesema uanzishaji na uendeshaji wa TLS kwa sheria ya Bunge umesukumwa miaka yote na dhamira njema ya Serikali ya kutaka kuilinda na kuilea taaluma ya uanasheria ili ikue na ijenge weledi stahili na hivyo itoe mchango bora katika ujenzi na uendeshaji wa utawala wa sheria nchini.

"Ikiwa TLS sasa inajiona imekua kiasi cha kutosha na sasa inataka iingie kwenye majukumu ya ziada ya uanaharakati wa kisiasa, Serikali haitasita kuifuta sheria iliyoanzisha TLS ili chama hicho kijisajili chini ya Sheria ya Vyama kama NGOs zingine nchini au ikiwezekana chini ya Sheria ya Vyama vya Siasa kama vyama vingine vya siasa nchini".

Ameongeza kusema harakati zinazoendelea ndani ya TLS zenye mwelekeo wa kisiasa, zimeifanya ofisi yangu isimame kidogo kukamilisha marekebisho kadhaa ya sheria ya TLS maana hatma ya TLS haieleweki, "it remains in the balance".

Awali, waziri huyo aliueleza ujumbe huo wa TLS ukiongozwa na Mtendaji Mkuu wa TLS, Wakili Lameck Calleb, kuwa Serikali imefarijika sana kwa ushirikiano mkubwa uliotolewa na chama hicho katika maandalizi ya muswada wa sheria ya huduma ya msaada wa kisheria ambayo imepitishwa na Bunge na sasa unasubiri saini ya Rais wa Nchi kuwa sheria.

Aliongeza kuwa Wizara inaitegemea sana ushirikiano wa TLS hata katika utungaji wa Kanuni za sheria hiyo mpya, mchakato wake ambao tayari umeanza.

KIPINDI CHA BBC DIRA YA DUNIA JUMATANO

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AHUTUBIA MKUTANO WA HADHARA MJINI KITETO

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa michezo wa Kiteto akiwa katika ziara ya mkoa wa Manyara, Februari 15, 2017. 
Wananchi wa Kiteto wakimshangilia Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipowahutubia mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa michezo wa Kiteto Februari 15, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea kutoka Mzee Mbambire Oloi Kurukur, jani la mti ikiwa ni ishara ya amani ya kukomesha mapigano kati ya wakulima na wafugaji wilayani Kiteto kabla ya kuhutubia mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa michezo wa Kiteto, Februari 15, 2017.. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea kutoka kwa Katibu wa Baraza la Amani la Kiteto, Salum Mambo, jembe la asili ikiwa ni ishara ya kukoma kwa mauaji kati ya wakulima na wafugaji wilayani Kiteto katika mkutano wa hadhara aliouhutubi kweye uwanja wa michezo wa Kiteto, Februari 15, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia mikono wananchi katika mkutano wa hadhara aliouhutubi kweye uwanja wa michezo wa Kiteto, Februari 15, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

MUSEUM ART EXPLOSION POSTER

VIJUSO VYA MAGAZETI Y ALEO ALHAMIS FEBRUARY 16,2017

13 countries sits in Dar to discuss education

$
0
0

The Minister for Education, Science, Technology and Vocational Training Prof Joyce Ndalichako delivering key note address to officiate Ministerial SDG4 Regional Forum for Eastern African in Dar es Salaam.
Chair of the Ministerial SDG4 Regional Forum for Eastern African in Dar es Salaam and Head Office and country Representative of UNESCO, Zulmira Rodrigues welcomes invited guests, dignitaries and key speakers during Ministerial SDG4 Regional Forum for Eastern African in Dar es Salaam.(All photos by Zainul Mzige.
Unesco Regional Office for Eastern Africa, Director Mrs Ann Therese Ndong-Jatta addressing Ministerial SDG4 Regional Forum for Eastern African in Dar es Salaam.
UNHCR Head Regional Services Center, Mrs Victoria Akyeampong, gives her statement at the National Forum Session during the Ministerial SDG4 Regional Forum for Eastern African in Dar es Salaam.
Linda Madete from UNESCO Office Dar es Salaam gives out some of the education materials and brochures to invited guests during the Ministerial Sustainable Development Goals numbers 4 that focuses on ensuring inclusive and equitable quality education and promote lifelong learning opportunities for all at the Regional Forum for Eastern African in Dar es Salaam.
The Minister for Education, Science, Technology and Vocational Training, Prof Joyce Ndalichako (far left) arrives at Julius Nyerere International Convention Centre (JINCC )to attend the Ministerial SDG4 Regional Forum for Eastern African in Dar es Salaam.
Norwegian Ambassador to Tanzania, Hanne-Marie Kaarstad tete-a-tete with the UNHCR Representative to Tanzania, Chansa Ruth Kapaya at the Ministerial SDG4 Regional Forum for Eastern African.
Swedish Ambassador to Tanzania H.E Katarina Rangnitt gives a welcome remark on behalf of Diplomatic Corps at the Ministerial SDG4 Regional Forum for Eastern African. Katarina emphasized on the importance of equipping young people with proper education and relevant skills to make them competent.
A cross section of ministers from Eastern Africa, Unesco officials and the SDG4 co- conveners (ILO, UNFPA, UNDP, UNICEF, UN Women, UNHCR and World Bank) listening attentively on various speakers at the ongoing Ministerial SDG4 Regional Forum for Eastern African in Dar es Salaam.
Some of the invited dignitaries attending the Ministerial SDG4 Regional Forum for Eastern African in Dar es Salaam.
The Minister of State in the President's Office responsible for Regional Administration and Local Government (TAMISEMI), Hon  George Simbachawene and Norwegian Ambassador to Tanzania, Hanne-Marie Kaarstad (right)  follows  the Ministerial SDG4 Regional Forum for Eastern African in Dar es Salaam.
Deputy Minister for Education, Science, Technology and Vocational Training Eng. Stella Manyanya exchanging contacts with a disabled teacher Madam Sophia Mbeyela (centre) at the ongoing Ministerial SDG4 Regional Forum for Eastern African in Dar es Salaam.
Group Photo.
The Minister for Education, Science, Technology and Vocational Training Prof. Joyce Ndalichako elaborates a point to reporters about the prons and cons of the Ministerial SDG4 Regional Forum for Eastern African in Dar es Salaam.
The Minister of State in the President's Office responsible for Regional Administration and Local Government (TAMISEMI), Hon. George Simbachawene making a point during the press conference at the Julius Nyerere International Conference Centre.
 A cross section of Ministers and Journalists.
Zanzibar Minister of Education and Vocational Training Hon.Riziki Pembe shares her experience on how they have prioritized Sustainable Development Goals on Education in the Island.
Minister of Education &Human Resources  Tertiary Education & Scientific Research to the Republic of Mauritius, Leela Dookon Luchoomon gives testimony on her country achievement on education.
Minister of State for Primary Education in Uganda, Hon. Nansubuga Rosemary Seninde explains to reporters what it means to deal with children who do not want to attend schools in a bid to pursue compulsory education for all.
Minister of National Education and Vocational Training in the Republic of Djibouti, Hon. Moustapha Mohamed Mahamoud explaining challenges encounters in the education sector during the press conference.

13 Ministers from Eastern Africa, Unesco and the SDG4 co- conveners (ILO, UNFPA, UNDP, UNICEF, UN Women, UNHCR and World Bank) are in Dar es salaam to identify priorities and policy recommendations for a regional roadmap for the implementation of the SDG4- Education 2030 agenda and linkages with other SDGs;

In two days meeting opened yesterday at Julius Nyerere International Convention Centre (JINCC) various people made different remarks on how to ensure inclusive and equitable quality education and promote lifelong learning opportunities for all.

Opening the floor to welcome all participants including ministers from Comoros, Djibout, Eritrea, Ethiopia, Kenya, Madagascar, Mauritius, Rwanda, Seychelles, Somalia, South Sudan, Tanzania and Uganda, Swedish Ambassador to Tanzania  H.E Katarina Rangnitt spoke about Young people being given proper education with relevant skills to make them competent.

She talked about unlocking the potential of the people by keeping children in school and managing drop out with full knowledge that education is the tool to reach development goals.

“With the growing frustrations among the youth on lack of employment, climate change and disasters she asked participants to come out with practical solutions making sure that nobody is being left behind with a keen attention to kids with disabilities.” She said.

She asked the participants to look at how global SDGs will be achieved in accordance to the national policies targets and plans.

Speaking at the same meeting Mrs Victoria Akyeampong, UNHCR Head Regional Services Center spoke about the need to support people of concern so as to reach the goal as the agenda 2030 spoke about leaving no body behind.

She said refugees and migrants are in dire need of support because of the fragile situation they are. She said less than one percent of those people are enrolled in education. She asked the participants to increase access to refugees through digital education.

She also asked East Africans to look at the best way of including refugees in their national school as is being done in Cameroon Chad and Pakistan.

Unesco Regional Office for Eastern Africa, Director Mrs Ann Therese Ndong-Jatta addressing the forum posed several question to the participants on priorities and what makes good education.

She said the forum was initiated to deal with the missing link by focusing difficult questions which are still puzzling the community.

On education, she asks about the environment, investment and if people are happy with the current education set up. She examined critically what does examinations do to the kids. If it is not only creating competitions and not happiness.

 She wanted the participants to look and come out with the statement what are we supposed to do to have a true education. She said kids and the rest, learning should be joy and not otherwise and teaching should be joy too.

She remembered Mwalimu Nyerere, Tanzania Founding father, for his courage to insist on using local language to teach. She said by using local language as other nation like China and Japanese did we will create confidence to our people and allow mothers to teach their kids.

In her Key note address Hon Prof Joyce The Minister for Education, Science, Technology and Vocational Training, insisted the importance of the platform in transforming the East African society. She said the platform is an important platform and step in the construction of a common vision for the education 2030 agenda.

“This is an important platform and step in the construction of a common vision for the Education 2030 Agenda, and for our countries to share National Road maps, to identify emerging common areas, and to identify common challenges and opportunities", said Ndalichako.

She said Tanzania is ready to engage in achieving the targets of SDG4.
She further added that the successful implementation of the SDG4 like any other programme, depends much on political will and support.

Unafahamu kuwa unaweza kujitengenezea pesa kupitia blogu yako?

$
0
0

Na Jumia Travel Tanzania

Ulishawahi kujiuliza iwapo itafika siku moja kwamba utakuwa unapata pesa kutokana na blogu uliyoifungua mtandaoni? Najua pengine wazo hilo halikuwepo awali wakati unaianzisha kwa sababu wengi wetu hufanya hivyo ili kujijengea wasifu mzuri hususani tuliomo kwenye tasnia ya uandishi wa habari.

Kila mtu anataka pesa na anatumia mbinu mbalimbali kuhakikisha anapata pesa. Jumia Travel ingependa kukufahamisha kuwa mbinu zifuatazo zinaweza kukufanikishia kujitengenezea pesa nzuri kupitia blogu yako.

Kupitia matangazo ya CPC au CPM

CPC/PPC Ads (Cost per click or pay per click), ni matangazo ambayo huwekwa kwenye maudhui au pembezoni mwa blogu. Kila wakati ambapo msomaji hubonyeza tangazo hilo, wewe utakuwa ukilipwa kutokana na kitendo hiko.

Kwa upande mwingine, CPM Ads (cost per 1,000 impressions ads), ni aina ya matangazo ambayo hukulipa kiasi fulani cha pesa kutokana na kiasi gani cha watu waliolitembelea tangazo hilo kwenye mtandao wako.

Mitandao maarufu ambayo unaweza kujiunga na kufaidika na aina hiyo ya matangazo ni Google AdSense, Chitika, Infolinks na Media.net

Uza matangazo binafsi

Endapo utakuwa na wasomaji au watu wengi wanatembelea blogu yako basi wenye matangazo wenyewe watakufuata kukuomba uwawekee matangazo yao. Utofauti wa njia hii na ya hapo juu ni kwamba hakuna mtu wa kati au dalali, hii inamaanisha kwamba unaweza kuweka viwango vyako mwenyewe vya kutangaza.


Itumie blogu yako kama njia ya kujitangaza kibiashara

Inawezekana pia ukaitumia blogu yako kama njia ya kuuza na kutangaza bidhaa zako mwenyewe. Hivyo basi badala ya kufikiria blogu yako itumike kukuingizia pesa pia unaweza kuitumia kama daraja kuwavuta wasomaji wako watembelee tovuti ya biashara yako.


Itumie blogu yako kujijengea jina na uaminifu

Kwa mfano, ukaanzisha blogu ambayo inahusu masuala ya benki pekee. Watu wataanza kusoma blogu yako na itaanza kupata umaarufu. Hatimaye utakuwa mtu mashuhuri na unayefahamika kwenye sekta ya benki. Hali hii inaweza kukupa fursa ya watu kukutaka ushiriki kwenye uandishi wa vitabu, kulipwa ili uzungumze kwenye midahalo au kuendesha semina kwa wafanyakazi.

USHAURI WA KUZINGATIA: Kuanzisha blogu tu pekee yake sio sababu ya kukuingizia pesa, lazima uwekeze muda katika kuhakikisha inafanya vema. Hivyo basi, kabla ya kujikita katika uandishi wa blogu hakikisha unazingatia mambo yafuatayo:

Tengeneza maudhui yenye ubora

Blogu yako haitotengeneza pesa kama watu hawaisomi. Kwa sababu wao ndio watakaokuwa wanakuletea pesa kupitia kubonyeza matangazo au kununua bidhaa zako. Hivyo basi huna budi kuhakikisha unachokiandika kinawavutia watu kusoma.

Usipende kutumia muda mwingi kwenye blogu yako pekee

Safari ya kuwa na blogu yenye mafanikio makubwa inakwenda sambamba na kujijengea mahusiano mazuri na wadau mbalimbali. Wadau hao ni kama vile wadhamini, washirika wa kibiashara, pamoja na wanablogu wenzako ambao wanaweza kupendekeza wasomaji kuitembelea blogu yako.

Usiogope kujaribu

Sio lazima njia hizo zote zilizotajwa hapo juu za kukuingizia kipato zitakufaa au kufanya kazi. Kwa hiyo usiogope kubadili mbinu kama haitofanya kazi kwako na kwa wasomaji wako.

Kwa ujumla, mpaka blogu ianze kukuingizia kipato inahitaji bidii na jitihada za hali ya juu. Kwa hiyo Jumia Travel inakushauri wewe anza bila ya kuhofia kitu chochote kwani hatimaye itakuja kukulipa siku za usoni. Cha msingi ni kukumbuka kwamba sio lazima kuzitumia hizo njia zote zilizoorodhesha hapo juu, tazama wengine wanafanya nini kisha nawe anzia hapo.



Do you know that you can earn money through your blog?

JE WEMA SEPETU ATAFUNGWA AU ATALIPA FAINI.

$
0
0
Na  Bashir  Yakub.

Sheria  inayoshughulikia   habari  nzima  ya  madawa  ya  kulevya  inaitwa “The  Drug  Control  And  Enforcement  Act”.  Ni  sheria  namba  5  ya  mwaka  2015.  Ni  sheria  mpya  kabisa. Msanii  Wema  Sepetu  ni  kati  ya  Watu  walioko  mahakamani  tayari  kuamuliwa  kwa  mujibu  wa  sheria  hii.

1.AINA  YA  DAWA  ZA  KULEVYA.
Sheria  hii  inataja  aina  nyingi  mno  ya  vitu  ambavyo  imeviita  dawa  za  kulevya. Vipo  jamii  ya  kimiminika,  jamii  ya  unga,  jamii  ya  miti,  majani, mbegu  n.k.
Kifungu  cha  2   cha  sheria  hiyo  kinachosomwa  sambamba  na Schedule  ya 1  ya  sheria  hiyohiyo  kimeorodhesha  zaidi   ya  sampuli  100  ya  vitu  ambavyo  vinahesabika  kuwa   ni  dawa  za  kulevya hapa  Tanzania. Humo  imo  pia  bangi,  mirungi, cocaine, heroine na  aina  nyingine  nyingi.  Katika  hizi  Msanii  Wema  anatuhumiwa  kukutwa  na  misokoto  ya  bangi.

2.   JE  ILIKUWA  SAWA  WEMA  KUPEWA  DHAMANA  ?.
Ndio  ilikuwa  sawa.  Wako  watu  wanasema  kuna  mtu  amemkingia  kifua  akapata  dhamana. Hili si  kweli .  Dhamana  katika   kesi  za  madawa  ya  kulevya  hunyimwa  kutokana  na  kiwango  ulichokutwa au  unachotuhumiwa  nacho.   Kifungu  cha  29  cha  Sheria  hiyo  ya  kupambana  na  dawa  za  kulevya  kimeeleza  hilo  kama  ifuatavyo;.

( a ) Kama  ni  cocaine, heroine, mandrax, morphine, cannabis  resin au  opium   kuanzia gramu  200  au  zaidi  hakuna  dhamana.  Ni  pote  polisi  na  mahakamani.
( b ) Kama  ni  dawa  aina  ya  majani  au  mimea  kama  bangi n.k  kuanzia  kilo  100  au  zaidi  hakuna  dhamana. Ni  pote  polisi na  mahakamani.
( c ) Kama  ni  dawa  zenye  mfumo  wa  kemikali  kuanzia  lita  30 au  zaidi au  kilo  100  ikiwa  zimewekwa  katika  mfumo  wa  unga au  vinginevyo  hakuna  dhamana.  Ni  pote  polisi na  mahakamani.
Wema  Sepetu  alikutwa  na kiwango  kidogo kwa  taarifa  zilizotolewa,  ni  kama  msokoto  mmoja  hivi.  Ukiangalia  hapa  juu  hakuna  popote  ambapo kiwango  hicho  kimetajwa  kuwa hakidhaminiki.  Kwa  hiyo  kosa  lake  lilikuwa  la  kudhaminika  kabisa  kwa  mujibu  wa  kifungu  hiki.

3.   JE   WEMA  ANAKABILIWA  NA  ADHABU  ZIPI ?.

Kifungu  cha  17 ( 1 )  cha  Sheria  ya  Kuzuia  na  Kupambana  na  dawa  za  kulevya   kinaeleza  adhabu  ya  miaka  mitatu  jela, au  faini  isiyopungua  laki  tano   au  vyote  viwili.
Kwahiyo  panapo  kupatikana  na  hatia   atatakiwa  kwenda  jela  miaka  mitatu,  au  asiende  jela  iamuliwe  alipe  faini  inayoanzia  laki  tano  za  Tanzania,  au   aende  jela  miaka  mitatu  na  hapohapo  alipe na  faini  inayoanzia  shilingi  laki  tano  kwenda  mbele.

KUSOMA  ZAIDI  sheriayakub.blogspot.com.



MAJALIWA AZUNGUMZA NA WATUMISHI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA SIMANJIRO

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro kwenye Ikulu ndogo ya Orkesimet akiwa katika ziara ya Mkoa wa Manyara, Februari 16, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea taarifa ya wilaya ya Simanjiro kutoka kwa Mkuu wa wilaya hiyo, Mhandisi Zephania Chaula baada ya kusomewa taarifa hiyo kwenye Ikulu ndogo ya Orkesimet akiwa katika ziara ya Mkoa wa Manyara, Februari 16, 2017.
Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro, Mhandisi Zephania Chaula akisoma taarifa ya wilaya hiyo mbele ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwenye Ikulu ndogo ya Orkesimet Februari 16, 2017
 
Baadhi ya Watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Simanjiro wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao kwenye Ikulu ndogo ya Orkesimet akiwa katika ziara ya Mkoa wa Manyara , Febuari 16, 2017.


(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

HATUTAKUBALINA NA WACHOCHEZI - WAZIRI MKUU

$
0
0
*Asisitiza amani kwanza, masuala mengine baadaye

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali haitakubali kuona watu wachache wanachochea vurugu na kusababisha watu wengine wapoteze maisha ilhali wao hawadhuriki.

Ametoa kauli hiyo jana jioni (Jumatano, Februari 15, 2017) wakati akizungumza na maelfu ya wananchi waliohudhuria mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa michezo wa mjini Kibaya, wilayani Kiteto, mkoani Manyara.

Waziri Mkuu ambaye alikuwa katika siku ya kwanza ya ziara yake ya siku sita mkoani Manyara, alisema: “Hatutakubaliana na wachochezi. Hatutakubaliana na yeyote atakayesababisha kifo. Tukibaini kuna uchochezi, tutawasaka wahusika na kuwashughulikia,” alisema.

“Hapa kulikuwa na majina ya ajabuajabu, hatutakubali Kiteto iitwe Soweto au Kossovo, hapa ni Tanzania. Hatuwezi kuishi kwa kubaguana, ni lazima tuheshimu maamuzi ya wazee wetu wa kimila ambao wamesimamia zoezi hili ili kurejesha amani ya Kiteto,” alisema.
Alisema zamani Kiteto kulikuwa hakuna lugha ya amani lakini hali kwa sasa imebadilika na kuwa nzuri na akasisitiza kwamba hakuna kurudi nyuma.

Alisema anamshukuru Waziri Mkuu mstaafu, Mhe. Mizengo Pinda kuwa kufuatilia suala hilo na kuunda tume ya kutafuta amani wilayani Kiteto. “Nilipoingia madarakani, nami nilianza kufuatilia suala hilo ili nijue chanzo hasa ni nini. Nikabaini kuwa mgogoro mzima umechangiwa na chokochoko tu za watu wachache,” alisema.

Mapema, viongozi wa kimila walimkabidhi Waziri Mkuu rungu, jembe dogo na jani la mti wa asili (Kimasai unaitwa elisibie) ikiwa ni ishara amani ya kukomesha mapigano baina ya wafugaji na wakulima. Pia alishiriki dua ya kuombea amani ambayo iliongozwa na viongozi wa dini.

Mzee Mbambile Oloi Kurkur (65) ambaye amejiita ni msimamizi wa mila za Kimasai alisema Mungu yuko na anaweza kusimamia na kudumisha amani ambayo wameiombea. Alisema Mungu ameumba mti wa ajabu ambao haukauki kwa mwaka mzima na majani na hubaki ya kijani hata wakati wa kiangazi kikali. “Jani hili tunakukabidhi ikiwa ni ishara ya makubaliano yetu kuwa ya kudumu,” alisema.

Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Baraza la Amani la Wilaya ya Kiteto, Mzee Abubakar Mrisho alisema kamati hiyo iliundwa na wazee 70 ambao walipita katika tarafa saba za wilaya hiyo na kutoa elimu kwa wakazi wa vijiji vyote 23 juu ya umuhimu wa suala kudumisha amani.

Ili kuhitimisha kazi yao, Mzee Mrisho alimweleza Waziri Mkuu kwamba jana asubuhi, waliwachagua wazee kutoka makabila manne ya Wamasai, Wanguu, Wakamba na Wagogo ili wawakilishe makabila yote ya wilaya hiyo kwenye tambiko la kuoza ardhi.

“Baada ya tambiko tulitoa tamko la Baraza la Amani kwamba mauaji hapa Kiteto sasa basi.Yeyote atakayeona anabanwa, Kiteto haina nafasi naye tena,” alisema.

Kwa upande wao, viongozi wa dini walitumia mkutano huo wa Waziri Mkuu kuomba dua kwa ajili ya kuombea amani, haki, vita dhidi ya rushwa, ufisadi na dawa za kulevya na pia kuombea mvua ya kiasi na yenye kuleta neema.

Askofu Isaiah Chambala wa CCT alimuomba Mumgu awashe moyo wa upendo, amani na udugu miongoni mwa wakazi wa Kiteto, mkoa wa Manyara na Tanzania kwa ujumla.

Padre Filbert Moita wa Kanisa la Roma aliombea kuwe na haki na amani kwa watu wote na Mungu awasaidie watu wake ili waheshimiane kidugu katika wilaya hiyo na mkoa mzima.

Mwalimu Juma Hicha wa BAKWATA mbali ya kuombea amani wilayani humo, aliwaombea viongozi wa kitaifa wapewe hekima ya kuongoza nchi na Mungu awajalie nguvu ya kupambana na ufisadi, dhuluma na dawa za kulevya na zaidi ya yote Mungu awatie nguvu ya kuikamilisha vita hiyo.

Leo Waziri Mkuu anaendelea na ziara yake katika wilaya ya Simanjiro.

TAARIFA YA MKUTANO MKUU WA MWAKA WA WADAU WA MFUKO WA PENSHENI WA LAPF

NISHATI JADIDIFU KUCHANGIA UPATIKANAJI WA UMEME WA UHAKIKA

$
0
0
Na Greyson Mwase, Arusha
Imeelezwa kuwa vyanzo vya nishati jadidifu kama vile upepo, jua, jotoardhi vitachangia upatikanaji wa nishati ya uhakika ya umeme kwa kila  kijiji ifikapo mwaka 2030 kama mpango wa nishati kwa wote unavyofafanua.

Hayo yameelezwa na Kamishna Msaidizi- Nishati Jadidifu kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Styden Rwebangila katika mafunzo  kwa  wadau wa nishati jadidifu kuhusu matumizi ya mfumo mpya  wa uhifadhi data  na utoaji taarifa kwa ajili ya  nishati jadidifu ujulikanao kama Tanzania Renewable  Energy  Management Information System (TREMIS) yaliyofanyika jijini Arusha leo.

Mhandisi Rwebangila alisema kuwa ili nchi ya Tanzania kuingia kwenye orodha ya nchi za kipato cha kati ifikapo mwaka 2025, nishati ya uhakika ya umeme inahitajika hususan katika kuchochea uwekezaji katika viwanda na kukuza uchumi wa nchi.

Alisema mbali na gesi iliyogunduliwa katika mkoa wa Mtwara na maeneo mengine, nishati ya umeme kutokana na vyanzo vingine kama vile upepo, jua, joto ardhi vinahitajika ili kuongeza kiwango cha umeme katika Gridi ya Taifa.

“ Kuna maeneo ambayo hayajafikiwa na miradi mikubwa ya  Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na Shirika la Umeme  Tanzania (TANESCO) kama visiwani, ambapo Wizara ya Nishati na Madini imeweka utaratibu wa kutumia vyanzo vya nishati mbadala kama jua, upepo na jotoardhi kulingana na maeneo husika ili kila mwananchi afikiwe na huduma ya umme,” alifafanua Mhandisi Rwebangila.

Aliendelea kusema kuwa ili kuvutia fursa za uwekezaji, Wizara imeanzisha mfumo mpya wa uhifadhi data  na utoaji taarifa kwa ajili ya  nishati jadidifu ujulikanao kama Tanzania Renewable  Energy  Management Information System (TREMIS) utakaowezesha wawekezaji kutoka ndani na nje ya nchi kupata taarifa kuhusu fursa za uwekezaji katika nishati jadidifu, sera na taratibu.

Alisema kuwa taarifa za kampuni zote zinazojihusisha na nishati jadidifu, fursa za uwekezaji, sera, sheria na taratibu zitawekwa katika mfumo huo utakaounganishwa na tovuti ya Wizara ili wadau kupata uelewa kabla ya kuwekeza.

Aliendelea kusema kuwa  hatua iliyofikiwa kwa sasa katika maandalizi ya mfumo huo, ni utoaji wa mafunzo na ukusanyaji wa maoni kutoka kwa wadau mbalimbali wa nishati mbadala nchini ambapo mpaka sasa wamekwishafanya zoezi hilo katika Kanda ya Ziwa.
Kamishna Msaidizi- Nishati Jadidifu kutoka Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi, Styden Rwebangila (kulia) akibadilishana mawazo na Mtaalam kutoka Kitengo cha Teknolojia ya  Habari na Mawasiliano (TEHAMA)- Wizara ya Nishati na Madini, Danford Phiri (kushoto) katika mafunzo yaliyokutanisha wadau wa nishati jadidifu jijini Arusha Februari 16, 2017
Wadau wa nishati jadidifu  wakiendelea na majadiliano katika mafunzo hayo

KATIBU MKUU WA WIZARA YA UJENZI ATEMBELEA BANDA LA MAMLAKA YA USAFIRI WA ANGA TANZANIA (TCAA)

$
0
0
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Dkt.  Leonard Chamliho (kushoto)  akiangalia moja ya chapisho la vitabu  wakati  alipotembelea  banda la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) jijini Mwanza jana, kwenye  maonyesho ya kongamano la Mazingira la  watafiti za kisayansi na mazingira  zilizofanywa kwenye bonde la ziwa Victoria (Environmental Research and Science), Kulia ni Afisa Habari wa Mamlaka hiyo   Bestina Magutu.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi,u chukuzi na Mawasiliano Mhandisi Dkt.  Leonard Chamliho( wasita waliosimama kutoka kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa  Mamlaka ya Usafriri wa Anga Tanzania (TCAA)  mara baada ya kutembelea banda la TCAA kwenye  maonyesho ya kongamano la Mazingira la  watafiti za kisayansi na mazingira  zilizofanywa kwenye bonde la ziwa Victoria (Environmental Research and Science),yaliyofanyika mwanza jana.

RICHARD MUYUNGI ATEULIWA KUWA MKURUGENZI WA IDARA YA MAZINGIRA KATIKA OFISI YA MAKAMU WA RAIS

$
0
0
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Profesa Faustin Kamuzora amemteua Bwana Richard Muyungi kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Mazingira katika Ofisi hiyo.

Awali Bwana Muyungi alikua ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Mazingira katika Ofisi ya Makamu wa Rais. Bwana Muyungi pia ni mjumbe wa Bodi ya Dunia ya mfuko wa mabadiliko ya tabianchi akiwakilisha Afrika. Pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ushauri wa Marais wa Afrika kuhusu masuala ya mabadiliko ya tabianchi (CAHOSCC)

Uteuzi wa Bwana Muyungi umeanza mara moja tarehe 8/2/2017

KONGAMANO LA UTAFITI LA KISAYANSI LA BONDE LA ZIWA VICTORIA LAFANYIKA JIJINI MWANZA

$
0
0
Katibu Mkuu, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (sekta ya Uchukuzi), Dkt Leonard Chamuriho (kushoto) akisalimiana na Meneja wa Kiwanja cha Ndege cha Mwanza, Bi. Esther Madale kwenye banda la Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), katika maonesho ya Washiriki wa Kongamano la Mazingira la Wanasayansi Watafiti wa Bonde la Ziwa Victoria linalofanyika jijini Mwanza.
Katibu Mkuu, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (sekta ya Uchukuzi), Dkt Leornard Chamurho (kushoto), akifurahia maelezo yanayotolewa na Meneja wa Kiwanja cha Ndege cha Mwanza, Bi. Esther Madale kwenye banda la Mamlaka ya Viwanja vya ndege Tanzania (TAA), katika maonesho ya Washiriki wa Kongamano la Mazingira la Wanasayansi Watafiti wa Bonde la Ziwa Victoria linalofanyika jijini Mwanza. 
 Raia wa Kenya, John Osodo (kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Mhandisi Diana Munubi (kulia) alipotembelea banda la Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), kwenye maonesho ya Washiriki wa Kongamano la Mazingira la Wanasayansi Watafiti wa Bonde la Ziwa Victoria linalofanyika Jijini Mwanza.
Mhandisi Diana Munubi (wa kwanza kulia) akitoa maelezo yaliyomfurahisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi), Dtk. Leonard Chamurho (wa kwanza kushoto), akifuatiwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Prof. Faustine Kamuzora, Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Emmanuel Kalobelo na Afisa Usafirishaji Mkuu wa Uchukuzi, Alphonce Mwingira katika maonesho ya Washiriki wa Kongamano la Mazingira la Wanasayansi Watafiti wa Bonde la Ziwa Victoria linalofanyika jijini Mwanza.
Wafanyakazi wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi) kutoka taasisi za TAA, TCAA, TMA na DMI wanaoshiriki kwenye maonesho ya washiriki wa Kongamano la Mazingira la Wanasayansi Watafiti wa Bonde la Ziwa Victoria, linalofanyika Mwanza, wakiwa kwenye picha ya pamoja na Katibu Mkuu Uchukuzi, Dkt. Leonard Chamurho, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Prof. Faustine Kamuzora, na Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maji na Umwagiliaji Mhandisi Emmanuel Kalobelo.
Frank Mgeta wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza, Sekou-Toure (kulia), akipata maelezo mbalimbali yanayohusu mazingira kutoka kwa Mhandisi Diana Munubi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), kwenye maonesho ya washiriki wa Kongamano la Mazingira la Wanasayansi Watafiti wa Bonde la Ziwa Victoria, jijini Mwanza.


WAZIRI MWIJAGE AZINDUA KIWANDA CHA UTENGENEZAJI VIUNGO MBALIMBALI WA VYAKULA,BAGAMOYO MKOANI PWANI,

$
0
0
Mgeni rasmi akiwa waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Mh.Charles Mwijage wa tatu kushoto,akikata utepe kuashiria uzinduzi wa kiwanga cha utengenezaji wa viungo,Vegata Podravka Ltd,kilichojengwa kwa gharama ya shilingi bilioni 16,Kushoto ni Mbunge wa jimbo la Bagamoyo,Mh.Shukuru Kawambwa na kulia ni Makamu wa Rais wa Kampuni ya Podravka Group kutoka nchini Croati,Bi..Olivia Jakupec
  waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Mh.Charles Mwijagea akipata maelekezo mbalimbali kuhusiana na baadhi ya bidhaa ambazo ziko tayari kutoka kwa Makamu wa Rais wa Kampuni ya Podravka Group kutoka nchini Croati,Bi..Olivia Jakupec.
 Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda cha Vegeta Podravka Ltd,Bw-Tanzania,.Davor Svar akizungumza kwa ufupi wakati wa uzinduzi wa kiwanda hicho cha viungo mbalimbali,jana mjini Bagamoyo,huku mgeni rasmi akiwa waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Mh.Charles Mwijage.

Davor alisema kuwa wameamua kuwekeza nchini Tanzania kwa sababu imeonekana ni kiungo muhimu katika mambo ya uwekezaji hasa kutokana na eneo lake, miundo mbinu yake,ukuaji wake wa kiuchumi na pia kuwa kiungo muhimu kwa kuwa mwanachama hai wa nchi za Afrika Mashariki na Kati,kufuatia vigezo hivyo,hurahisisha mambo ya kibiashara kufanyika kwa urahisi zaidi.

Davor alisema kuwa kufuatia kuanzishwa kwa kiwanda hicho,kimefanikiwa kutoa ajira za kazi zaidi ya 200 katika Wilaya ya Bagamoyo ikiwemo kazi ya uuzaji na usambaji wa bidhaa za kiwanda hicho.
 Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda cha Vegeta Podravka Ltd-Tanzania,Davor Svar akifafanua jambo kwa Mgeni rasmi,Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Mh.Charles Mwijage,kabla ya hafla fupi ya uzinduzi wa kiwanda hicho,uliofanyika mjini Bagamoyo mkoa wa Pwani na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali.
Makamu wa Rais wa Kampuni ya Podravka Group kutoka nchini Croatia ,ambayo ni kampuni mama ya Vegeta Tanzania,Bi.Olivia Jakupec akizungumza mbele ya wageni waalikwa mbalimbali wakati wa uzinduzi wa kiwanda hicho cha utengenezaji wa viungo mbalimbali,mjini Bagamoyo mkoani mkoani Pwani.

Olivia alisema kuwa wao kama wawekezaji wametembea nchi kadhaa za Afrika ikiwemo Uganda,Kenya,Burundi,Zambia,Rwanda,Sudani Congo,Afrika Kusini na nyinginezo,lakini wakabaini Tanzania ndio mahali sahihi kwa uwekezaji."Hivyo tukafanya utafiti,tukabaini eneo la Bagamoyo linafaa kujengwa kiwanda cha aina hiyo,hivyo tukaamua kujenga kiwanda ndani ya mwaka mmoja na nusu,ambacho kimetumia kiasi cha shilingi bilioni 16 mpaka kukamilika.

"Tunaishukuru Serikali ya Tanzania inayoongozwa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt John Pombe Magufuli,Waziri Mkuu Kassim Majaliwa,Waziri wa Viwanda Mh.Charles Mwijage,Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) na wengineo kwa ujumla, kwa kuweka mazingira wezeshi ya uwekezaji,kiasi kwamba hata nasi tukaiona furasa hiyo na tukachukua hatua ya kuwekeza kiwanda hiki hapa nchini",alisema Olivia.
 Baadhi ya Wageni waalikwa mbalimbali waliohudhuria hafla hiyo ya uzinduzi wa kiwanda cha Viungo wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.
  Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Mh.Charles Mwijagea  akizungumza mbele ya wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye hafla ya uzinduzi wa kiwanda hicho wilayani Bagamoyo,Pwani.Waziri Mwijage alisema kuwa serikali ya awamu ya Tano imeamua kujenga Uchumi wa Viwanda,ili kuchochea mageuzi ya kiuchumi na maendeleo ya Watu.

"Tanzania sasa tunajenga  viwanda na si Tanzania ya viwanda inawezekana,hiyo ilikuwa kauli mbiu ya zamani,kwa hiyo sasa tunajenga viwanda,mwenye macho haambiwi Tazama"alifafanua Waziri Mwijage.Waziri Mwijage amewashuruku wawekezaji hao kwa kuamua kuja kuwekeza nchini Tanzania,ikiwa ni sehemu ya kumuunga mkono Rais wa awamu ya tano ,Dkt John Pombe Magufuli katika kuhakikisha Uchumi wa Viwanda unakwenda kwa kasi na kufanikiwa.
 Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Mh.Charles Mwijage akipeana mkono na  Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda cha Vegeta Podravka Ltd,Bw-Tanzania,.Davor Svar mara baada ya kusoma hotuba yake iliyowahamasisha wakati wa Wilaya ya Bagamoyo kuchangamkia fursa mbalimbali zitokazo na ujenzi wa viwanda vya aina mbalimbali vinavyoendelea kujengwa wilyani humo mkoani Pwani.
 Sehemu ya meza kuuu
 Wageni waalikwa kutoka kituo cha Uwekezaji nchini (TIC),wakifautilia kwa makini yaliyokuwa yakijiri
 Baadhi ya wageni waalkwa wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye hafla hiyo
 Makamu wa Rais wa Kampuni ya Podravka Group kutoka nchini Croatia ,ambayo ni kampuni mama ya Vegeta Tanzania,Bi.Olivia Jakupec akimkabidhi Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Mh.Charles Mwijage cheti cha heshima ya ushiriki wake mkubwa katika uzinduzi wa kiwanda hicho
  Makamu wa Rais wa Kampuni ya Podravka Group kutoka nchini Croatia ,ambayo ni kampuni mama ya Vegeta Tanzania,Bi.Olivia Jakupec akimkabidhi Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Mh.Charles Mwijage cheti cha heshima ya ushiriki wake mkubwa katika uzinduzi wa kiwanda hicho.Pichani kati ni  Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda cha Vegeta Podravka Ltd-Tanzania,Davor Svar
 picha ya pamoja
 Picha pamoja




 Baadhi ya Wawakilishi kutoka Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC) wakipewa maelezo mafupi namna ya bidhaa hizo zinavyotengenezwa kiwandani hapo
Baadhi ya wafanyakazi wakiendelea na usindikaji wa viungo kiwandani humo

PROFESA NTALIKWA AKUTANA NA UJUMBE WA WAZIRI MKUU WA UINGEREZA

$
0
0
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa Justin Ntalikwa (katikati) akiongoza kikao baina ya Ujumbe kutoka nchini Uingereza ukiongozwa na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania  Sarah Cooke pamoja Watendaji mbalimbali wa Idara ya Nishati katika Wizara ya Nishati na Madini.

 Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa Justin Ntalikwa (kulia) na Mwakilishi wa  Waziri Mkuu wa Uingereza anayehusika na masuala ya Biashara nchini Kenya na Tanzania,  Lord Hollick  wakimsikiliza mmoja wa Wataalam wa Wizara ya Nishati na Madini (hayupo pichani) wakati wa kikao kilichofanyika katika Ofisi za Wizara ya Nishati na Madini jijini Dar es Salaam.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa Justin Ntalikwa (kulia) akimsikiliza Balozi wa Uingereza nchini Tanzania  Sarah Cooke, (kushoto)  aliyeambatana Mwakilishi wa  Waziri Mkuu wa Uingereza anayehusika na masuala ya Biashara nchini Kenya na Tanzania,  Lord Hollick (katikati). kikao kilifanyika katika Ofisi za Wizara ya Nishati na Madini jijini Dar es Salaam.

Na Teresia Mhagama, Dar es Salaam

Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa Justin Ntalikwa tarehe 16 Februari, 2017  amekutana na Ujumbe kutoka Ubalozi wa Uingereza nchini Tanzania ukiongozwa na Balozi,  Sarah Cooke,  aliyeambatana  na Mwakilishi wa  Waziri Mkuu wa Uingereza anayehusika na masuala ya Biashara nchini Kenya na Tanzania,  Lord Hollick na Mshauri wa Hali ya Hewa na Mazingira.

Katika kikao hicho walijadili masuala mbalimbali ikiwemo upunguzaji wa madeni ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) ili Shirika hilo liweze kujiendesha lenyewe kwa ufanisi pamoja uendelezaji wa miradi ya uzalishaji, usafirishaji na usambazaji wa umeme.

Profesa Ntalikwa pia aliueleza Ujumbe huo kuhusu mipango inayofanywa na Serikali ya kuendeleza miradi mbalimbali ya umeme ikiwemo uandaaji wa kabrasha litakaloainisha  miradi yote ya umeme inayohitaji wawekezaji.
Alisema kuwa kabrasha hilo litasambazwa kwa wadau mbalimbali na wawekezaji ili waweze kulisoma na kufanya maamuzi ya kuwekeza kwenye miradi husika.

“Kabrasha hilo limeshaandaliwa na Wataalam na kwa sasa linapitiwa na baadhi ya Taasisi za Serikali  kabla ya kulisambaza kwa wadau wetu kupitia njia mbalimbali kama Tovuti na magazeti,” alisema Profesa Ntalikwa.

Kwa upande wake,  Mwakilishi wa  Waziri Mkuu wa Uingereza anayehusika na masuala ya Biashara nchini Tanzania,  Lord Hollick alisema kuwa kipaumbele cha nchi hiyo ni kuwekeza kwenye miradi ya nishati kwani Tanzania ina vyanzo vingi vya nishati jadidifu  ikiwamo, Jotoardhi, maporomoko madogo ya Maji, Tungamotaka, Jua na Upepo.

“ Tunao mtaji wa kuwekeza kwenye miradi ya umeme na pia tunaweza kusaidia kiutaalam ili kuifanya TANESCO kufanya kazi kwa ufanisi ili kupunguza changamoto mbalimbali zinazochelesha uwekezaji,” alisema  Hollick.

TANZANIA ITAENDELEA KUWA MWENYEJJI WA PROGRAMU YA URITHI WA UKOMBOZI WA BARA LA AFRIKA.

$
0
0
 Mwenyekiti  wa Programu ya  Urithi wa Ukombozi   wa  Bara la Afrika  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akitoa maelezo kuhusu Programu hiyo kwa wajumbe katika kikao kilichofanyika jana Jijini Dar es Salaam.
  Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo  Prof.Elisante Ole Gabriel akiwasilisha mchango wake kwa wajumbe  wakati wa kikao cha Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika kilichofanyika jana Jijini Dar es Salaam.
 Mtaalamu wa Programu  ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika Dkt Daniel Ngagala akiwasilisha mada wakati wa  kikao na wajumbe wa Programu hiyo kilichofanyika jana Jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe.Dkt Hussein Mwinyi akichangia mjadala wakati wa kikao cha Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika kilichofanyika jana Jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.William Lukuvi akiwasilisha mchango wake katika kikao cha Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika kilichofanyika jana Jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya Wataalamu wa Program ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika wakiwasilisha mawazo yao katika kikao cha Programu hiyo kilichofanyika jana Jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akiwa katika picha ya pamoja na Baadhi ya Mawaziri na manaibu Mawaziri,Viongozi  na Wajumbe wengine wa Program hiyo baada ya kumaliza kikao kilichofanyika jana Jijini. Dar es Salaam.

UMOJA WA ULAYA WASAIDIA MRADI WA LISHE NA USALAMA WA CHAKULA WA WFP KATIKA MIKOA YA KANDA YA KATI, TANZANIA

$
0
0
Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula  Dunini (WFP) limepokea mchango wa Euro (€) milioni 9.5 kutoka Umoja wa Ulaya (EU) kwa lengo la kuunga mkono Mradi wenye thamani ya Euro milioni 24.5 (takribani Shilingi za Tanzania bilioni 50) wa kusaidia kukuza Usalama wa Chakula na Lishe katika mikoa ya kati nchini Tanzania.

Mradi umeandaliwa ili kuimarisha usalama wa chakula na lishe kwa watu wapatao 40,000  na wakati huohuo ukichangia katika kupunguza utapiamlo katika wilaya zinazolengwa za Bahi na Chamwino mkoani Dodoma na Ikungi na Singida Vijijini katika mkoa wa Singida. 

Mchango wa EU umetangazwa leo wakati wa hafla ya kutiliana saini makubaliano katika Jengo la Umoja jijini Dar es Salaam uliofanywa na Dr. Mpoki Ulisubisya, Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Michael Dunford, Mwakilishi wa WFP nchini Tanzania na Roeland Van De Geer, Mkuu wa Ubalozi wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania.

“Licha ya kuimarika kwa viashiria vingi vya afya katika muongo uliopita, bado hakuna hatua kubwa katika kuimarisha hali ya lishe ya watoto na wanawake nchini Tanzania,” Roeland Van De Geer, Mkuu wa Ubalozi wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania, alisema wakati wa hafla hiyo".

“Viwango vya juu vya kudumaa, kukosa uzito wa kuridhisha na upungufu wa viinilishe nchini kunaashiria dharura ya kimyakimya. Utayari wa kisiasa katika safu ya viongozi wa juu katika kukabili lishe duni nchini Tanzania kwa mtazamo wa sekta nyingi kwa hakika ni mageuzi makubwa. Kupitia mradi huu, EU pamoja na WFP ziko katika nafasi nzuri ya kubaini na kuunga mkono uhusiano kati ya kilimo, afya, usalama wa chakula na lishe, ambao hapo kabla haukuwa umeelezwa kwa kina au kufuatiliwa kikamilifu.”

Mradi huu unatumia uwepo wa muda mrefu wa WFP katika mikoa ya kati nchini Tanzania na uzoefu wake katika kutoa chakula chenye lishe na mawasiliano yenye lengo la kubadilisha tabia ya kijamii kupitia vituo vya afya. Shughuli hizi zitakamilishwa na jitihada katika sekta nyingine ili kutoa mtazamo ulio kamili zaidi wa kupunguza kudumaa nchini. Viwango vya Taifa vya kudumaa viko katika asilimia 34 ambapo kwa Dodoma ni asilimia 36.5 na Singida ni asilimia 29.2

“Tunashukuru kwa mchango huu kutoka Umoja wa Ulaya kwani umeiwezesha WFP kuendelea na programu hii bunifu inayolenga kukidhi mahitaji ya watu walio hatarini zaidi, hasa watoto katika kile kipindi muhimu sana cha ukuaji wao, yaani siku 1,000 za mwanzo tangu kubebwa mimba hadi kutimiza miaka miwili,” Mwakilishi wa WFP Michael Dunford alisema katika hafla hiyo. “Programu hii itatoa ushahidi ambao utatoa mwongozo kwa jitihada za baadaye, na kwa hiyo ina uwezekano wa kuleta mabadiliko ya kudumu nchini Tanzania.”

Nchini Tanzania, viwango vya utapiamlo sugu miongoni mwa watoto unatokana na umaskini, ukosefu wa usalama wa chakula na ukosefu wa chakula cha kutosha kwa watoto wachanga na unyonyeshaji watoto. Mradi utalenga kukuza maarifa kuhusu lishe, mtawanyiko wa lishe na taratibu za kutumia maji, usafi wa mazingira na usafi wa mwili (WASH). Shughuli hizi zitapewa nguvu kwa kuhamasisha ufugaji wa idadi inayofaa ya mifugo, kupanda mazao tofautitofauti na kuhamasisha vijiji kuanzisha vikundi vya kuweka akiba na kukopa, yote yakilenga kukuza uwezekano wa kupata mtaji.

Shirika la Save the Children ni mshirika wa WFP katika kuimarisha ushirikiano na uwezo wa asasi zilizojikita katika jamii ili kuhamasisha uwezeshaji wa jinsia na uhusiano wa sekta mbalimbali katika suala la lishe, pamoja na kuratibu utekelezaji wa kipengele cha kilimo katika mradi.

Kwa kuratibu shughuli hizi chini ya mwamvuli wa WFP, Umoja wa Ulaya na Shirika la Save the Children zitakuwa zikishughulikia changamoto nyingi zinazolenga kuimarisha usalama wa chakula na lishe nchini Tanzania.

Mradi huu ni sehemu ya majukumu ya WFP katika kufanikisha Lengo la 2 katika Malengo ya Maendeleo Endelevu: Kufuta Njaa. Ili Kuondoa Njaa kabisa ifikapo mwaka 2030, WFP inashirikiana na washirika mbalimbali kama vile serikali, sekta binafsi na vyama vya kiraia.

YANGA VS NGAYA NI BUKU TATU TU, KUWAKOSA WACHEZAJI WATATU

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

UONGOZI wa Klabu ya Yanga umetangaza viingilio vya mechi yao marudiano dhidi ya Ngaya unaotarajiwa kufanyika wikiendi hii.

Akizungumnzia viingilio hivyo, Afisa Masoko wa klabu hiyo, Omar Kaaya amesema kiingilio cha chini kitakuwa ni shiilingi 3000 kwa majukwaa ya mzunguko na viti vya machungwa,  VIP A  ni Tsh  20,000, VIP  B  ni Tsh  10,000 na VIP  C itakuwa Tsh  10,000.

Kaaya amewataka mashabiki wa Yanga kuja kwa wingi uwanjani ili kuishan gilia timu yao na zaidi amani inatakiwa itawale kwenye mchezo huo ambao ni muhimu sana kwao.

Kwa upande wa Benchi la Ufundi wa Yanga, Kocha msaidizi wa Juma Mwambusi amesema kuwa katika mchezo huu hawatabweteka na ushindi walioupata mwazoni zaidi wanataka kuona wanapata ushindi mwingine.

Mwambusi amesema, hawatabweteka na ushindi uliopita kwani ni hazina tosha ila kila kitu inakuja na mbinu yake kwahiyo lazima tucheze kwa umakini mkubwa sana na kuweza kutokuruhusu goli.

"Tunajivunia ushindi mnono tulioupata ugenini kwani ni hazina tosha kwetu lakini tunatambua umuimu wa mchezo wetu wa marejeano ambao utafanyika siku ya jumamosi kwenye uwanja wa Taifa,kikubwa nawaomba mashabiki wetu na wanamichezo wajitokeze kwa wingi kuipa sapoti timu yao." amesema Mwambusi.

Kuelekea mchezo huo wachezaji watakaokosekana kwa sababu ya kuwa majeruhi ni Donald Ngoma,Amisi Tambwe na Haruna Niyonzima.
                   
Tayari Ngaya wamewasili asubuhi ya leo kwa ajili ya mchezo wa marudiano dhidi ya Yanga ambao kwenye mechi iliyofanyika nchini Comoro Yanga walifanikiwa kutoka na ushindi wa goli 5-1.
 Kocha msaidizi wa Yanga Juma Mwambusi (kushoto) akizungumza na wanahabari kuelekea mchezo wao wa marudiano na timu ya Ngaya utakaofanyika Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa, katika mechi ya kwanza Yanga walifanikiwa kutoka na ushindi wa goli 5-1 nchini Comoro.
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live




Latest Images