Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1139 | 1140 | (Page 1141) | 1142 | 1143 | .... | 1898 | newer

  0 0


  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari (TPA), Eng. Deusdedit Kakoko (Wa pili kushoto) na Mwanasheria Mkuu wa Shirika la uzalishaji Mali Jeshi la kujenga Taifa –SUMA JKT Kanali John Mbungo, (Wa pili kulia), wakitiliana saini mkataba wa ujenzi wa bandari kavu katika eneo la Kwala-Ruvu mkoani Pwani. Mkataba huo umesainiwa leo jijini Dar es salaam.


  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Nchini (TPA), Eng. Deusdedit Kakoko (Wa pili kushoto) akitoa maelezo kwa Waziri wa Ujenzi , Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (Wa pili kulia) kabla ya kutiliana saini mkataba wa ujenzi wa bandari kavu baina ya TPA na Shirika la uzalishaji Mali la Jeshi la kujenga Taifa –SUMA JKT jijini Dar es salaam.


  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari (TPA), Eng. Deusdedit Kakoko (kushoto) na Mwanasheria Mkuu wa Shirika la uzalishaji Mali Jeshi la kujenga Taifa –SUMA JKT Kanali John Mbungo (Kulia) wakikabidhiana mikataba ya ujezi wa wa bandari kavu katika eneo la Kwala-Ruvu mkoani Pwani. Katikati ni Waziri wa Ujenzi , Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akishuhudia makabidhiano hayo.
  Waziri wa Ujenzi , Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa(Katikati), akisisitiza jambo kwa watendaji wa Mamlaka ya Bandari (TPA) mara baada ya kutiliana saini mkataba wa ujenzi wa wa bandari kavu katika eneo la Kwala-Ruvu mkoani Pwani.

  Picha na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

  …………..

  Mamlaka ya Bandari nchini (TPA), imetiliana saini Mkataba wa ujenzi wa Bandari Kavu na Shirika la Uzalishaji mali la Jeshi la kujenga Taifa (Suma JKT), eneo la Kwala – Ruvu mkoani Pwani.

  Mkataba huo wa zaidi ya shilingi bilioni 7.2 unaitaka Suma JKT kukamilisha bandari hiyo katika kipindi cha wiki Tisa kuanzia sasa ambapo tayari eneo la Hekta 500 zimetengwa kwa ajili ya ujenzi huo.

  Akizungumza jijini Dar es salaam leo, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa amesema ujenzi huo utapunguza msongamano bandarini na katika jiji la Dar es salaam kwa kuwa magari mengi ya mizigo yanayokuja bandarini kuchukua mizigo sasa yataishia katika bandari hiyo.

  “Mizigo itasafirishwa kwa njia ya reli kutoka bandarini kwenda Ruvu, hivyo magari ya mizigo hayatafika Dar es salaam na hivyo kupunguza msongamano”, amesema Waziri Mbarawa.

  Aidha, Profesa Mbarawa ameitaka Suma JKT kufanya kazi kwa uadilifu na kwa muda mfupi ili kuiwezesha mipango na mikakati ya Mamlaka hiyo kufanikiwa kwa urahisi.

  Katika hatua nyingine, Waziri Mbarawa amesema Mamlaka hiyo itaanza ujenzi wa gati lenye urefu wa mita 300 katika bandari za Dar es salaam na Mtwara ili kuwezesha meli kubwa kuweza kutia nanga na kuongeza ufanisi wa Bandari nchini.

  “Upanuzi wa Bandari za Dar es salaam na Mtwara utavutia wasafirishaji wengi kutumia bandari hizi, hivyo wafanyakazi wote wa Mamlaka hii wafanye kazi kwa bidii na weledi”, amesisistiza Waziri Mbarawa.

  Kwa upande wake Mwanasheria mkuu wa JKT, Kanali John Mbungo, amemhakikishia Waziri huyo kuwa kazi ya ujenzi huo itafanyika kwa ubora na katika kipindi kilichopangwa.

  Ujenzi wa Bandari Kavu katika eneo la Ruvu ni mkakati wa Serikali wa kupunguza msongamano katika jiji la Dar es salaam.

  Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

  0 0

  Waziri wa Afya Mahmoud Thabi Kombo akipata maelezo kutoka kwa Dkt. Alona Roucher kuhusu matatizo ya moyo yanayomkabili Muslim Muhd Ali kutoka mtaa wa Jangombe ambae ni mmoja kati ya watoto watakaopelekwa Israel kwa matibabu.
  Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo akizungumza na madaktari wa maradhi ya moyo kutoka Israel ambao wapo nchini kuwafunyia uchunguzi watoto wenye m.aradhi hayo ambao baadhi watapelekwa Israel kufanyiwa upasuaji.
  Dkt. Yifat Brosh kutoka Shirika la Save a Child Heart la Israel akimfanyia vipimo mmoja ya watoto wanaosumbuliwa na maradhi ya moyo katika Hospitali Kuu ya Mnazimmoja.
  Baadhi ya wazazi wakiwa Hospitali Kuu ya Mnazimmoja wakisubiri zamu za kuwapeleka watoto wao kufanyiwa uchunguzi na madaktari bingwa wa moyo kutoka nchini Israel.Picha zote na Makame Shenga-Maelezo.

  0 0

  Wakazi wa jiji la Mwanza wamezifurahia simu za kisasa za Smart Bomba ambazo zilizinduliwa na kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania hivi karibuni,Simu hizo zinazidi kuchangamkiwa na wananchi wengi hususani wakazi wa maeneo ya jiji la Mwanza na wanaozunguka mkoa huo ambapo wameshukuru kwa hatua hiyo ambayo imeleta mapinduzi makubwa katika sekta ya mawasiliano nchini.

  Wakiongea kwa nyakati tofauti wakati wa promosheni ya mauzo ya simu hizo inayoendelea mkoani Mwanza,baadhi ya wananchi wamesema kuwa hatua ya kampuni hiyo kuingiza sokoni simu za kisasa za Smart Bomba zinazopatikana kwa gharama nafuu imedhihirisha dhamira ya kweli ya kampuni hiyo ya kuwapeleka watanzania katika ulimwengu wa kidijitali.

  Bw.Focus Phabian mmoja wa wananchi ambaye amenunua simu hiyo akiongea kwa niaba ya wenzake alisema kuwa Smart Phone ni mkombozi wa mawasiliano ya kisasa kwa kuwa licha ya kuwa na unafuu wa bei pia imetengenezwa kwa kuendana sambamba na mazingira halisi ya watanzania.

  “Simu ya Smart Bomba licha ya kuuzwa kwa shilingi 99,000 ambazo ni nafuu kwa watanzania wengi programu zake zinapatikana katika lugha ya taifa ya Kiswahili bila kusahau muundo wake unaowezesha kupata interneti yenye kasi kubwa ya Vodacom na kupiga picha zenye ubora wa hali ya juu .”Alisema.

  “Watanzania wengi hivi sasa wana kiu ya kupata taarifa mbalimbali zinazotokea papo kwa papo na kujiunga pia na progamu za simu zinazorahisisha mawasliano kama whasap hivyo kwa Smart Bomba wengi watamudu kutumia simu za kisasa za intanenti ambazo zinauzwa kwa bei nafuu na zilizotengenezwa kwa kulenga mazingira halisi ya kitanzania”,Alisema Phabian.

  Mkuu wa Mauzo na Usambazaji wa Vodacom Tanzania,kanda ya ziwa,Ayoub Kalufya,alisema kuwa tangu simu hizi ziingizwe sokoni wiki moja iliyopita kumekuwepo na mwitikio mzuri wa wananchi ambao wamekuwa wakizinunua ili kuingia katika ulimwengu wa kidigitali.

  “Smart Phone mbali na kuwa na unafuu wa bei pia inaambatana na ofa ya mteja anayenunua simu kuunganishwa na kifurushi cha intanenti chenye GB 10 za bure kwa mwezi na ofa hii inatolewa katika kipindi cha miezi 3 mfululizo kwa ajili ya kumuwezesha mteja kupata na kufurahia intanenti i yenye kasi kubwa ya Vodacom mahali popote na wakati wowote”,Alisema Kalufya.

  Kalufya aliongeza “wakati ni huu kwa wakazi wa jiji la Mwanza mikoa mingine ya kanda ya ziwa makundi kuchangamkia fursa hii pekee kwa kununua simu ya Smart Bomba kwa gharama nafuu na kufurahia mawasiliano ya kisasa”.
  Mkuu wa Vodacom Tanzania Kanda ya Ziwa ,Ayubu Kalufya akiitambulisha simu ya Smart Bomba kwa wakazi wa jijini Mwanza jana, kulia ni Mkuu wa Maduka ya Rejareja wa kampuni hiyo,Brigite Steven. 
  Baadhi ya wakazi wa jiji la Mwanza wakiiangalia simu aina ya Smart Bomba, wakati wa utambulisho wa simu hiyo jijini humo.
  Baahi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania kanda ya Ziwa wakiandamana kwenye barabara ya Kenyatta jiji Mwanza jana, wakati wa kuitambulisha wa simu aina ya Smart Bomba kwa wakazi wa jiji hilo jana. 
  Mkazi wa Nyasaka mkoani Mwanza Michael Alfred, akipokea simu
  aina ya Smart Bomba ikiwa ni zawadi kutoka kwa Mkuu wa Vodacom Tanzania Kanda ya ziwa ,Ayubu Kalufya,baada ya kununua moja ya simu hizo wakati wa kuzitambulisha simu hizo jijini Mwanza.

  0 0

  Meneja Masoko wa StarTimes Tanzania ,Felix Awino akizungumza na waandishi wa habari kabla ya kukabidhi zawadi kwa washindi hao
  Bwana na Bibi Alex wakifurahi mara baada ya kukabidhiwa zawadi kampuni ya Star Times Tanzania
  Meneja uhusiano wa kampuni ya Sar Times Tanzania Juma Suluhu akikabidhi zawadi kwa Bwana na Bibi Nuezy Fredrick 
  Wafanyakazi wa Star Times Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja wakiwa wameshika maua
  Meneja uhusiano wa kampuni ya Sar Times Tanzania Juma Suluhu na Meneja Masoko wa StarTimes Tanzania ,Felix Awinowakikabidhi zawadi kwa washindi wa Ni Valentine's na Star Times  Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii


  KAMPUNI ya Star Times imesheherekea siku ya wapendanao na wateja wake kwa kutoa zawadi kadhaa katika promosheni yake ya "Ni Valentine na Startimes".

  Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo jijini Dar es Salaam wakati wa kukabidhi zawadi hizo, Meneja Masoko wa kampuni hiyo Tanzania, Felix Awino amesema Star Times inasheherekea siku hii kwa kuwazawadia wapenzi kupata chakula cha jioni na malazi ya Hotel ya kisasa.

  “tunafurahi kusheherekea siku ya wapendanao na wateja kwa kuwa karibu nao kama sehemu ya upendo wetu kwao, kwa kuwapa promosheni na maudhui yanayoendana na wakati ,hivyo kwa wateja wetu wa Dar es Salaam watapata malazi SeaScape, Mwanza watalala katika hoteli ya Malaika , Meya wataenda Usungilo , Arusha Palece Hotel na kwa mkoa wa Dodoma watapata kupumzika katika Hotel ya Morena”amesema Awino.

  Kwa upande wake mmoja wa washindi wa promotion hiyo ya ni Valentine na Startimes, Nuezy Fredrick amesema kuwa ni furaha kubwa kwao kama wateja wa Star Times kupata nafasi hiyo ya kupelekwa sehemu ya kifahari kama hiyo hili waweze kufurahi na wapenzi wao kutokana na kutumia king’amuzi cha Star Times.

  Amesema kuwa star Times imemuheshimu na yeye ataendelea kutumia bidhaa za kampuni hiyo na kufurahia vipindi bomba vya kila siku.

  0 0
 • 02/14/17--07:36: TANZIA


 • 0 0

  MKE wa Rais Mheshimiwa Mama Janeth Magufuli na Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wametembelea Gereza la Mahabusu Tabora na kutoa zawadi mbalimbali kwa wafungwa na mahabusu gerezani hapo. 

  Wake wa viongozi wametembelea gereza hilo leo (Jumanne, Februari 14, 2017) wakiwa katika ziara mkoani Tabora, ambapo Mama Janeth amesema wameamua kuwatembelea wafungwa na mahabusu hao kwa nia ya kuwafariji kwa kuwa wao ni sehemu ya jamii. 

  “Vitabu vitakatifu vinasema kwamba ukiwasaidia watu wenye mahitaji utakuwa umetoa sadaka kubwa kwa Mwenyezi Mungu, hivyo tumeamua kuja kutembelea wafungwa na mahabusi kwenye gereza hili na kuwapa zawadi kwa kuwa nanyi mnahitaji faraja,” amesema. 

  Amesema wameamua kwenda kuwaona wafungwa na mahabusu hao kwa lengo la kuwafariji na kuwatia moyo kwa sababu wanaimani kwamba wakitoka watakuwa raia wema na hayo wanayopitia ni sehemu ya kufanya marekebisho ya tabia. 

  “Ni siku kubwa kwangu, nimejifunza mengi baada ya kufika hapa. Kitendo cha kwenda kuwaona wenye mahitaji wakiwemo wagonjwa, wafungwa ni jambo jema tunaamini hizi zawadi tulizozitoa zitawasaidia kwa sababu tunajua mnamahitaji mengi,” amesema. 

  Katika gereza hilo wake hao wa viongozi wamekabidhi zawadi mbalimbali kwa wafungwa na mahabusu, ambapo mwakilishi wa wafungwa hao Deo Kitave aliwashukuru kwa niaba ya wenzake. “Tunawashukuru kwa kutukumbuka, tunamuomba Mwenyezi Mungu muendelee kuwa na moyo huo,”. 
    Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akipokea risala toka kwa Kaimu Mkuu wa Magereza Mkoa wa Tabora Mkuu wa gereza SSP Nahman Koko wakati yeye na mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa walipotembelea Magereza ya mahabusu ya Tabora na kutoa zawadi mbalimbali kwa wafungwa mahabusu.

   Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akimkabidhi zawadi  Naibu Mkuu wa gereza la Mahabusu Tabora Mrakibu wa Magereza Godliver Makwaruzi  wakati yeye na mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa walipotembelea Magereza ya mahabusu ya Tabora na kutoa zawadi mbalimbali kwa wafungwa na mahabusu leo Februari 14, 2017.
   Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa zawadi  Naibu Mkuu wa gereza la Mahabusu Tabora Mrakibu wa Magereza Godliver Makwaruzi  wakati yeye na mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa walipotembelea Magereza ya mahabusu ya Tabora na kutoa zawadi mbalimbali kwa wafungwa na mahabusu leo Februari 14, 2017
   Mke wa Rais Mama Janeth magufuli na Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wakitoka katika gereza la wanawake Tabora walipotembelea Magereza ya mahabusu ya Tabora na kutoa zawadi mbalimbali kwa wafungwa na mahabusu leo Februari 14, 2017
   Mke wa Rais Mama Janeth magufuli na Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Aggrey Mwanri akiwashukuru sana kutembelea Magereza ya mahabusu ya Tabora na kutoa zawadi mbalimbali kwa wafungwa na mahabusu leo Februari 14, 2017

   Mke wa Rais Mama Janeth magufuli akiongea wakati yeye na Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa  walipotembelea Magereza ya mahabusu ya Tabora na kutoa zawadi mbalimbali kwa wafungwa na mahabusu leo Februari 14, 2017
   Mke wa Rais Mama Janeth magufuli na Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wakitoa zawadi kwa ajili ya wafungwa na mahabusu walipotembelea Magereza ya mahabusu ya Tabora na kutoa zawadi mbalimbali kwa wafungwa na mahabusu leo Februari 14, 2017
  Mke wa Rais Mama Janeth magufuli na Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wakiagana na askari magereza bada ya kutembelea Magereza ya mahabusu ya Tabora na kutoa zawadi mbalimbali kwa wafungwa na mahabusu leo Februari 14, 2017

  PICHA NA IKULU

  0 0


  0 0  Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo Akikagua ujenzi wa Kituo cha Afya cha Engorora,Akiwa ameambatana na baadhi ya viongozi mbalimbali kutoka Ofisi ya Mkoa

  Na Imma Msumba, Arusha
  Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Mashaka Gambo Amefanya ziara katika Kijiji cha Engorora leo february 14 na kujionea maendeleo mbalimbali hususani katika sekta ya Afya kijiji cha Engorora kilichopo Kata ya Kisongo.

  Mh: Gambo akiwa kwenye ziara hiyo amekagua Kituo cha Afya kilichojengwa kijini hapo kwa nguvu za Wananchi ambapo Mkuu wa Mkoa Alisema,

  " Nipende kuwapongeza wananchi wa kijiji hiki kwa kuweza kujitolea kwa nguvu zenu zote kwenye maendeleo ya kijiji hiki na Taifa kwa ujumla, Sisi kama Serikali inayoongozwa na Rais Dr. John Joseph Pombe Magufuli tumeamua kuchukua jukumu hili la kumalizia ujenzi wa Kituo hiki cha Afya,nipende tu kuwaambia wananchi wa kijiji hiki nitahakikisha kabla ya mwisho wa mwezi wa tatu, nitawaagiza watu wa Tanesco wajekuweka umeme kwenye zanahati hii,sambamba pia na watu wa Idara ya maji na wao pia wataleta huduma ya maji hapa haraka iwezekanavyo."

  Mkuu wa Mkoa amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Arusha Vijijini kuhakikisha kabla ya mwisho mwezi huu anaonana Mwenyekiti wa Kijiji hicho na kuweza kuweka utaratibu wa kifedha juu ya swala la kumalizia ujenzi wa Kituo hicho kwa upande wa kuweka Tiles pamoja na kufunga milango ambayo ipo tayari mpaka sasa.

  Pia mkuu wa Mkoa alimalizia kwa kuwapatia wananchi wa kijiji hicho saalamu za pongezi kutoka kwa Rais Magufuli
  " Mh:Rais anawasalimia sana na pia anashukuru kwa kura zenu nyingi za ndio na kumuwezesha kuwa Rais wa awamu ya Tano."HAPA KAZI TU"

  Wananchi wa Kijiji cha Engerora wakifuatilia Hotuba ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha kwa makini.

  Baadhi ya Wawekezaji wa Kata ya Kisongo waliojitokeza kwenye kumsikiliza Mkuu wa Mkoa

  0 0

  Wakazi wa mkoa Ruvuma wametakiwa kuwa mstari mbele kupinga matumizi ya madawa ya kulevya na kuwafichua wanaotumia kwani yamekuwa yakipunguza nguvu kazi ya taifa.


  0 0

   
  NAIBU Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI,Selemani Jafo,akizungumzia na wakurugenzi,wenyeviti wa halmashauri,waganga wakuu wa wilaya mkoani Pwani,jana.(Picha na Mwamvua Mwinyi)   Na Mwamvua Mwinyi,Kibaha

  NAIBU Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI,Selemani Jafo,amesema mkoa wa Pwani umepokea Bil.2.340 zitakazotumika kugawanywa kwenye vituo vya afya na zahanati 234 zilizopo mkoani hapo ili kuboresha na kutatua changamoto zilizopo.

  Amesema fedha hizo zimetolewa kutoka katika mpango wa malipo kwa ufanisi unaotekelezwa kwa ushirikiano baina ya bank ya dunia na serikali ya Tanzania kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.Aidha Jafo amewasihi wakurugenzi,wenyeviti wa halmashauri na mganga mkuu wa mkoa huo,kusimamia fedha hizo ili ziweze kuleta tija .

  Katika hatua nyingine,ametoa wiki moja hadi kufikia februari 21 mwaka huu,kwa waganga wakuu wa mikoa (RMO)na makatibu tawala wa mikoa (RAS)kote nchini,kuhakikisha wanapeleka account za bank zinazotumiwa katika vituo na zahanati zote.Alhaj Jafo,aliyasema hayo wakati akizungumza na wakurugenzi na wenyeviti wa halmashauri pamoja na waganga wakuu wa wilaya mkoani Pwani.

  Alisema kati fedha hizo kila zahanati na kituo cha afya kitapatiwa kiasi cha sh.mil 10 ili kuboresha na kutatua kero sugu zilizokuwa zikiwasumbua.“Kuna zahanati na vituo vya afya ambavyo havina magodoro,mapaa yamebomoka,,hakuna vyoo huku nyumba za mganga wa kituo nayo ikiwa haina choo”“Kuna maeneo mengine hayana hata vitanda vya kujifungulia,akinamama wanapata shida yaani unahofia wanaweza kuondoka hata na magonjwa mengine,hivyo kwa mazingira haya fedha hizi endapo zitatumika kikamilifu zitaondoa matatizo hayo”alisema Jafo.

  Alisema katika miaka iliyopita fedha hizo zilikuwa hakuna hivyo kutokana na mpango huo kuanza,wahakikishe wanaleta matokeo chanya kwa kujibu changamoto zilizokuwa zikiwakabili.Jafo alisema hatofurahishwa akisikia mradi huo haujafanikiwa katika mkoa wa Pwani na mikoa mingine 8 ambayo ipo kwenye mradi huo kwa majaribio hapa nchini.

  Akizungumzia suala la utoaji huduma bora za kiafya,alieleza kuwa ni tatizo kubwa na aibu kwani katika mkoa huo jumla ya vituo 153 vina nyota 0(0 star)kati ya vituo 234 vilivyopo .Alifafanua kuwa vituo vinavyokosa star kubwa ndivyo vinavyokosa mapato zaidi kwani endapo hospitali inafanya vizuri inapata mil.360,kituo cha afya mil.79.8 na zahanati mil.19.

  “Hili ni tatizo la nchi nzima,niwaombe waganga wakuu wa wilaya na mikoa kusimama kidete,kuhakikisha mnaondoa hizi 0,sifuri hizi hazina maana ,zinashusha mapato,kuanzia sasa mfanye juhudi mpate nyota 4 hadi 5”alisema Jafo.Alimtaka mganga mkuu wa mkoa wa Pwani,dk Beatrice Byarugaba,kuacha kukaa ofisini badala yake atoke kutembelea vituo na zahanati mbalimbali ili kujiridhisha na huduma inayotolewa.

  Wakati huo huo, Jafo alitoa wiki moja kwa makatibu tawala wa mikoa na waganga wakuu nchini kupokea account zote za vituo na zahanati zilizopo kwenye mikoa yao .Waziri huyo alisema endapo mkoa wowote utashindwa kutekeleza agizo hilo basi katibu tawala na mganga mkuu wa mkoa husika watatakiwa kutoa maelezo.

  Nae mchumi idara ya afya kutoka TAMISEMI,Nassoro Shemzigwa,alisema mpango huo unatekelezwa katika mikoa tisa ikiwemo Pwani,Shinyanga,Mwanza,Simiyu,Geita,Kagera na Mara .Alielezea kuwa lengo la mradi ni kuboresha huduma za afya ya msingi kuanzia hospital ya wilaya,zahanati na vituo vya afya.Shemzigwa alisema mpango huo utatekelezwa kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia mwaka 2015/2016 hadi 2020 na utakuwa ni endelevu.

  Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kibiti,Khatibu Chaurembo,alibainisha wamepokea maagizo na maelekezo waliyopewa na wataenda kuyafanyia kazi.Chaurembo aliiomba serikali kuangalia tatizo la uhaba wa watumishi katika zahanati mbalimbali hasa maeneo ya vijijini ambako zipo zahanati zenye mtumishi mmoja hivyo kusababisha huduma kuzorota.

  0 0

  Bweni la Wasichana la shule ya sekondari Itamba iliyopo katika tarafa ya Matamba wilayani Makete mkoani Njombe leo limeteketea kwa moto ambao chanzo chake bado hakijafahamika.


  Angalia video ya tukio hilo hapo chini:-

  0 0

   Katibu Mkuu Wizara ya Afya Bi. Asha Abdalla akifungua Mkutano wa siku tatu wa matayarisho ya Mpango wa kupambana na maradhi ya Polio Tanzania katika Ukumbi wa Zanzibar Beach Resourt Mbweni.
  Baadhi ya washiriki wa mkutano wa matayarisho ya Mpango wa kupambana na Polio wakifuatilia ufunguzi wa mkutano huo.
  Mwakilishi wa Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) kutoka Afrika Kusini Dkt. Mercy Kamupira akiwasilisha mada katika mkutano unaozungumzia maradhi ya Polio unaofanyika Zanzibar Beach Resourt Mbweni.
  Washiriki wa mkutano unaojadili ugonjwa wa Polio wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi, Katibu Mkuu Wizara ya Afya Bi. Asha Abdalla.Picha na Makame Mshenga-Maelezo.


  …………..


  Na Ramadhani Ali/Maelezo Zanzibar 


  Wadau wa chanjo wa Tanzania na nchi jirani wapo Zanzibar kwa ajili ya mkutano wa kutathmini maradhi ya polio na matayarisho ya kuandaa mpango wa kukabiliana na maradhi hayo iwapo yatajitokeza.

  Akizungumza katika mkutano huo unaofanyika Zanzibar Beach Hotel Mbweni, Mkurugenzi Kinga na Elimu ya Afya Zanzibar Dkt. Fadhil Mohd Suleiman amesema maradhi ya polio sio tatizao Tanzania kwa sasa, lakini bado hatupo salama kutokana na nchi jirani kuendelea kusumbuliwa na maradhi hayo.

  Amesema Tanzania mara ya mwisho kuwa na mgonjwa wa polio ni mwaka 1997 lakini nchi ya Somalia, Jamhuri ya Watu wa Kongo na Nigeria bado wanakabiliwa na maradhi hayo na watu wake wanakuja kwa shughuli mbali mbali za maisha hivyo matayarisho ya kujiandaa ni jambo muhimu.

  Amewashauri wazazi kuendelea na utaratibu wa kuwapeleka watoto wao katika vituo vya afya mara baada ya kuzaliwa kupatiwa chanjo zote ili kuhakikisha maradhi hayo na mengine yanayowasumbua hayarejei tena.Meneja wa Kitengo cha chanjo Zanzibar Dkt. Yussuf Haji Makame amesema hali ya chanjo iko vizuri baada ya asilimia 95 ya watoto wanaostahiki kupatiwa chanjo kupatiwa chanjo hizo.

  Amesema kitengo hivi sasa kinaendelea kufuatialia kwa karibu watoto wenye umri kuanzia miaka 15 wanapopata ulemavu wa ghafla ili kujua chanzo chake na amewataka wazee wanapobaini kijana wao kupata tatizo hilo kumpeleka hospitali mapema.

  Mwakilishi wa WHO Zanzibar Dkt. Andemichael Ghirmay ameipongeza Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa juhudi kubwa za kupambana na polio na kufanikiwa kupewa cheti maalumu mwaka 2015.Amesema Shirika hilo litaendelea kuunga mkono juhudi zinazoendelea kuchukuliwa na serikali na ametaka juhudi za pamoja za wadau na jumuiya za kimataifa kuhakikisha polio na maradhi mengine yanayozuilika kwa chanjo sio tatizo tena Zanzibar.

  Akifungua mkutano huo Katibu Mkuu Wizara ya Afya Bi. Asha Abdalla amewataka wadau wa chanjo kutoridhika na hatua iliyofikiwa ya kutokomeza Polio bali waendelee kuweka mikakati bora zaidi itakayo hakikisha maradhi hayo hayarejei.

  Mkutano huo wa siku tatu unaowashirikisha wataalamu wa chanjo kutoka Shirika la Afya ulimwengu (WHO) na Shirika la kuhudumia watoto (UNICEF) utaundaa Kamati ya Maafa ya polio ya kujiweka tayari wakati wote kukabiliana nayo yatakapo tokea.

  0 0


  Na Greyson Mwase, Manyara


  Wananchi katika Wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara wamepongeza kampuni ya kuzalisha umeme kwa kutumia nishati ya jua ya Rafiki Power iliyopo chini ya kampuni tanzu ya E.ON ya Ujerumani, kwa kuwapatia huduma ya umeme iliyopelekea kukua kwa kasi ya maendeleo katika wilaya hiyo.

  Waliyasema hayo leo katika ziara ya wataalam wa nishati jadidifu kutoka Wizara ya Nishati na Madini katika miradi ya umeme mkoani Manyara yenye lengo la kuangalia utekelezaji wa miradi ya umeme, changamoto zake na kutoa ushauri wa kitaalam.

  Akizungumza kwa niaba ya wenzake katika kijiji cha Komolo kilichopo wilayani Simanjiro mkoani Manyara, Thadeo Bura ambaye ni mmiliki wa duka la vifaa vidogo vya umeme jua na bidhaa nyingine, alisema kabla ya kampuni ya Rafiki Power kuwekeza katika kijiji hicho maisha yalikuwa ni magumu kwa kuwa hakukua na nishati ya kuwawezesha kuanzisha miradi midogo midogo.

  Alisema mara baada ya kupata umeme kupitia kampuni ya Rafiki Power, ameweza kuanzisha duka kwa ajili ya vifaa vidogo vya umeme jua, bidhaa nyingine na kutoa huduma nyingine kwa wanakijiji wenzake.

  Alisema huduma ya umeme imewekwa kwenye baadhi ya shule na hospitali hivyo kuboresha huduma za jamii.

  Naye Joseph Hango ambaye ni mmiliki wa saluni ya kunyoa nywele aliongeza kuwa uwepo wa nishati ya umeme kupitia kampuni ya Rafiki Power umepelekea kuongezeka kwa kipato kutokana na idadi ya wateja kuongezeka.

  Aliiomba kampuni hiyo kuendelea na juhudi za kusambaza umeme katika maeneo mengi ambayo hayajafikiwa na huduma ya umeme ili kukuza uchumi wa wilaya na mkoa kwa ujumla.

  Wakati huohuo, akizungumza katika ziara hiyo Meneja Mkuu wa Kampuni ya Rafiki Power, Joanis Holzigel alisema kuwa kampuni yake inatarajia kuongeza uzalishaji wa umeme ambapo kaya 20,000 nchi nzima zinatarajiwa kunufaika na huduma ya umeme ifikapo mwaka 2022.

  Alisema kwa kutambua umuhimu wa nishati ya umeme katika uchumi wa viwanda utakaopelekea nchi ya Tanzania kuwa kwenye orodha ya nchi za kipato cha kati ifikapo mwaka 2025, kampuni yake imeweka mipango ya muda mfupi na muda mrefu ambapo inatarajia kufikia wateja 20,000 ifikapo mwaka 2022.

  Akitaja miradi inayotekelezwa na kampuni yake, Meneja Holzigel alisema katika mkoa wa Arusha kampuni yake ina miradi minne katika maeneo ya Digodigo, Soitsambu, Ololosokowani, na Malambo yaliyopo wilayani Ngorongoro na miradi mingine miwili iliyopo katika maeneo ya Itaswi na Kwamtoro wilayani Kondoa, mkoani Dodoma.

  Aliongeza kuwa, mradi mwingine mmoja unaotekelezwa na kampuni hiyo ni wa Komolo/Temeke, uliopo Simanjiro mkoani Manyara.


  Meneja Mkuu wa kampuni ya kuzalisha umeme kwa kutumia nishati ya jua ya Rafiki Power, Joanis Holzigel (kushoto) akibadilishana mawazo na Mtaalam wa Nishati Jadidifu kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Emillian Nyanda (kulia) katika ziara ya wataalam wa nishati jadidifu kutoka Wizarani katika wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara kwa ajili ya ukaguzi wa miradi ya umeme.
  Mmiliki wa kioski kilichonufaika na huduma ya umeme jua kupitia kampuni ya Rafiki Power, Thadeo Bura (kushoto) akielezea manufaa ya mradi wake katika ziara ya wataalam wa nishati jadidifu kutoka Wizara ya Nishati na Madini katika wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara kwa ajili ya ukaguzi wa miradi ya umeme.
  Moja ya kioski kilichonufaika na huduma ya umeme jua kupitia kampuni ya Rafiki Power kilichopo katika kijiji cha Komolo wilayani Simanjiro mkoani Manyara.
  Mmiliki wa mghahawa wa chakula ambaye ni mmoja wa wanufaika wa huduma ya umeme jua kupitia kampuni ya Rafiki Power akionesha friji inayotumia nishati hiyo katika ziara ya wataalam wa nishati jadidifu kutoka Wizara ya Nishati na Madini katika wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara kwa ajili ya ukaguzi wa miradi ya umeme.
  Mmiliki wa kioski kilichonufaika na huduma ya umeme jua kupitia kampuni ya Rafiki Power, Thadeo Bura akielezea matumizi ya compressor inayotumia nishati ya jua kwa matumizi mbalimbali, katika ziara ya wataalam wa nishati jadidifu kutoka Wizara ya Nishati na Madini katika wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara kwa ajili ya ukaguzi wa miradi ya umeme.
  0 0

  Hussein Makame, NEC aliyekuwa Bukoba

  Tume ya Taifa ya Uchaguzi imewatahadharisha watu wanaochukua kadi za kupigia kura za wenzao na kuzizuilia au kubaki nazo kuwa ni kinyume cha Sheria.

  Hayo yamesema na Mkurugenzi wa Huduma za Kisheria wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Emmanuel Kawishe wakati akitoa elimu ya mpiga kura katika halmashauri ya manispaa ya Bukoba na Shinyanga hivi karibuni.

  Alisema kifungu cha 88 cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi kinasema kuwa ni kosa la jinai kwa mtu kuchukua kadi ya mpiga kura mwingine na kuiziulia, kukataa kuirudisha au kubaki nayo kwa uzembe.

  Bw. Kawishe alifafanua kuwa kumekuwa na malalamiko kwamba inapofikia karibu na kipindi cha uchaguzi, baadhi ya watu wanachukua kadi za wapiga kura wengine na kuzizuia kinyume cha Sheria.

  Hata, hivyo alisema kutokana na kutoa elimu ya mpiga kura kupitia mikutano na kuhudhuria maonesho mbalimbali, baadhi ya wananchi wameelewa umuhimu wa kadi hizo na kuahidi kutoampa mtu kadi zao za kupigia kura.

  “Kwa hiyo katika jambo hilo tumekuwa na mrejesho ambo ni chanya lakini tunachowaomba ukiandikishwa tunza kadi yako ya mpigia kura” alisema Bw. Kawishe na kuongeza kuwa;

  “Jambo la pili mwananchi usikubali mtu achukue kadi yako ya mpigia kura na wala usitumie kadi yako ya mpiga kura kwenye kuchukulia dhamana sehemu yoyote”

  “Kwa sababu itakwenda kuchukulia dhamana alafu utashindwa kwenda kupiga kura unapofika wakati wa kupiga kura, mwananchi ajue kwamba kupiga kura ni haki yake”

  Alisema mtu aliyejiandikisha asipokwenda kupiga kura anakosa haki ya kuchagua kiongozi anayemtaka na badala yake anawaacha wenzako wakuchagulie kiongozi.

  “Unaacha kupiga kura alafu baadaye anakuja kulalamika unasema huyu kiongozi simtaki kumbe kura moja inatosha kubadilisha matokeo ya eneo zima” alisema.

  Hivyo aliwasihi wananchi waendelee kuzingatia amani katika uchaguzi na kuwashukuru kwa jinsi uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 na uchaguzi mdogo uliofanyika Januari 22 mwaka huu kwa jinsi ulivyokuwa na amani na utulivu.

  ”Kwa kweli Watanzania tutambue kuwa amani ni yetu sisi sote na sisi ndio tutakaoilinda hiyo amani tuiweke Tanzania yetu kwanza alafu sisi baadaye” aliwakumbusha Watanzania.

  Akijibu swali la mmoja wa wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Bukoba aliyehoji anayepoteza kadi ya mpiga kura anachukuliwa hatua gani kumuwajibisha, Bw. Kawishe alisema hakuna hatua yoyote inayochukuliwa dhidi yake.

  Alifafanua kuwa wale wote wanaopoteza kadi ya mpiga kura wanatakiwa wafike kwenye kituo cha uboreshaji wa daftari la wapiga kura na kujieleza na watapatiwa kadi nyingine.
   
  Mkurugenzi waHuduma za Kisheria wa Tume ya Tiafa ya Uchaguzi Bw. Emmanuel Kawishe, akizungumza na Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Josephine Matirowakati alipomtembeleaofisinikwakemkoanihumo.
  Mkurugenzi waHudumaza Kisheria wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Emmanuel Kawisheakitoa Elimu ya Mpiga kurakupitia Kituo cha redioFarajaFm cha mkoaniShinyangamwishonimwa wiki hii.Kuliakwake ni mtangazaji wa redio hiyo FaustinKasala.
  Mkurugenzi wa Huduma za Kisheria wa Tume ya Tiafa ya Uchaguzi Bw. Emmanuel Kawishe, akitoa Elimu ya Mpiga kura kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Old Shinyangailiyopomanispaaya Shinyanga.Pichana Hussein Makame, NEC.
  Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji (R) Semistocles Kaijage (kulia) akisalimiana namwenyeji wake Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga Jaji Richard Kibelabaada ya mwenyeji wake kumpokea wakati akiwasilimkoaniShinyanya kutoa Elimu ya Mpiga Kura mkoanihumo.Kushoto niNaibuMsajili wa MahakamaKuu kanda ya Shinyanga Sekela Mwaiseje.
  Mkurugenzi waHuduma za Kisheria wa Tume ya Tiafa ya Uchaguzi Bw. Emmanuel Kawishe, akisamiliana na Mkurugenzi wa Halamashauri ya Manispaa ya ShinyangaBw. Geofrey Ramadhani Mwangulumbi baada ya kuwasili kwenye Halmashauri hiyo kutoa Elimu ya Mpiga kura.
   

  0 0

  Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (katikati) akimsikiliza mmoja wa washiriki katika kikao cha kuandaa Kanuni za Local Content. Wengine katika picha ni wenyeviti wa Bodi za Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Wakuu wa Mashirika pamoja na Viongozi Waandamizi kutoka Wizara ya Nishati na Madini na Taasisi zake na wawakilishi wa kampuni za Wachimbaji wa Mafuta na Gesi Asilia Nchini.
  Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (katikati) akisikiliza mada kuhusu Local Content iliyokuwa ikitolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Felix Mgamlagosi (hayupo pichani). Wengine ni washiriki walio hudhuria kikao hicho mjini Dodoma.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa James Ntalikwa (wa pili kulia) akiendesha kikao cha kujadili Kanuni za Local Content kwa niaba ya Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo. Wengine ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya BG, Marc Hartog (wa kwanza Kulia) Mwenyekiti wa bodi ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Profesa Sufiani Bukurura (wa tatu kulia), Kaimu Kamishna wa Nishati na masuala ya Petroli, Mhandisi Innocent Luoga (wa nne kulia), Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Uagizaji Mafuta kwa Pamoja (PBPA), Modestus Lumato (wa tano kulia) pamoja na Viongozi Waandamizi kutoka Wizara ya Nishati na Madini.
  Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akisikiliza mada kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Felix Mgamlagosi (hayupo pichani). Kutoka kushoto, Mwenyekiti wa bodi ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Profesa Sufiani Bukurura, wa pili ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa James Ntalikwa na wa tatu Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya BG, Marc Hartog wakiwa katika kikao hicho mjini Dodoma.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Felix Mgamlagosi (aliyesimama) akitoa ufafanuzi kuhusu mada zilizotolewa kwenye kikao cha kujadili Kanuni za Local Content kwenye Ukumbi wa Wizara ya Nishati na Madini mjini Dodoma. Wanaofatilia ni Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (wa kwanza kulia) pamoja na Wenyeviti wa Bodi za Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Wakuu wa Mashirika na Viongozi Waandamizi kutoka Wizarani.
  Washiriki wa kikao cha Local Content wakifatilia kikao kilicho jadili Kanuni za Local Content mjini Dodoma.


  ………….


  Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo amekutana na Wachimbaji wa Mafuta na Gesi Asilia nchini, Wenyeviti wa Bodi za Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania, Wakuu wa Mashirika pamoja na Viongozi Waandamizi kutoka Wizara ya Nishati na Madini na Taasisi zake ili kujadili Kanuni za Local Content kikao hicho kilifanyika tarehe 11-12 mjini Dodoma.

  0 0

  Forklift ikiwa kazini

  Na Dotto Mwaibale

  BOHARI ya Dawa (MSD) imekabidhiwa mashine za kupandishia mizigo juu na kushusha (Forklifts) sita, zenye gharama ya shilingi za kitanzania milion 531. 8, ambazo zimetolewa msaada na Mfuko wa Kimataifa wa Global Fund kupitia Shirika la Marekanila Ushirikiano wa Kimataifa (USAID).

  Msaada huo ni sehemu ya awamu ya pili ya maboresho ya maeneo  ya kuhifadhia dawa ya MSD yaliyokuwa ya kifanywa na Global Fund, ikiwa ni  pamoja na upanuzi wa maghala ya kisasa yaani WiB ya MSD Makao makuu, Dodoma na Mbeya, na ujenzi wa maghala ya Kisasa MSD Kanda ya Tabora na Kituo cha mauzoTanga.

  Wakizungumza katika makabidhiano hayo, yaliyofanyikaa jana katika utekelezaji wa awamu ya mwisho ya upanuzi na ujenzi wa maghala ya kisasa yanayojulikana kama Warehouse in -a –box, mashine hizo (forklifts), Naibu Mkurugenzi Mkazi wa JSI/SCMS Marasi Mwencha amesema fedha hizo ni zile zilizosalia kutoka kwenye ujenzi wa maghala ya kisasaya MSD, ambapo walikubaliana na menejimentiya MSD kununulia forklift.

  Mkurugenzi Mkuu wa MSD Laurean Bwanakunu amewashukuru wahisani hao kwa mashine hizo ambazo ni za gharama, na kueleza kuwa mashine hizo zitapelekwa kwenye kanda za MSD zenye uhitaji. 

  Hata hivyo ameeleza kuwa tayari MSD ina Kiwanja  maeneo ya Luguruni, wilayani Ubungo jijini Dar es Salaam,kwa ajili ya kujenga ofisi na ghala la kisasa kwa Kanda ya Dar es Salaam hivyo wanategemea kuendelea kushirikiana na wahisani kwa ajili ya ujenzi pindi taratibu zitakapokamilika.

  0 0  0 0

  Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini Alvaro Rodriguez akisalimiana na wakazi wa kijiji cha Maruwa wilaya ya Moshi vijijini mara baada ya kuwasili kwa ajili ya shughuli ya kuotesha miti 120 katika eneo la nusu maili lililopo katika Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro.
    Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini Alvaro Rodriguez na wageni wengine wakitizama mnara wa kumbukumbu uliowekwa katika eneo hilo baada ya kufanyika kwa shughuli za uoteshaji miti 1510 mwaka 2015.
  Kaimu Mwenyekiti wa Shirika lisilo la Kiserikali la kuhifadhi Mazingira (TEACA) Adoncome Mcharo akitoa taarifa fupi ya ukuaji wa miti iliyooteshwa katika eneo na nusu maili ,Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro kwa  Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini Alvaro Rodriguez na ujumbe wake (hawapo pichani)
  Kaimu Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya TAifa ya Mlima Kilimajaro (KINAPA) Charles Ngendo akizungumza kabla ya kuanza zoezi la uoteshaji miti katika eneo hilo.
  Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa kimataifa wa Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ,Kikanda na Kimataifa ,Balozi  Celestine Mushi  akionesha eneo ambalo lilipandwa miti na tayari imeanza kukua.
   Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini Alvaro Rodriguez akiwa na Mtaalamu wa Mawasiliano wa Shirika la Umoja wa Mataifa (UN) nchini Hoyce Temu wakitizama eneo lililooteshwa miti katika Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro. 
   Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa kimataifa wa Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ,Kikanda na Kimataifa ,Balozi  Celestine Mushi akitoa maelekezo eneo jingine lilaotakiwa kuoteshwa miti katika Hifadhi hiyo. 
   Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa kimataifa wa Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ,Kikanda na Kimataifa ,Balozi  Celestine Mushi  akiwa amebeba iche ya miti kwa ajili ya kutoesha katika eneo hilo. 
    Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa kimataifa wa Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ,Kikanda na Kimataifa ,Balozi  Celestine Mushi akiotesha miche ya miti katika eneo hilo.
    Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini Alvaro Rodriguez akiotesha miti katika eneo hilo la nusu maili lililopo katika Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro.
   Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini Alvaro Rodriguez akimwagia maji miti aliyootesha katika eneo hilo. 
  Kaimu Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro,Charles Ngendo akiotesha mti katika eneo hilo.
  Mtaalamu wa Mawasiliano wa Shirika la Umoja wa Kimataifa (UN) nchini ,Hoyce Temu akiotesha mti na kumwagia maji wakati wa zoezi la kuotesha miti katika eneo la Nusu Maili katika Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro.
  Wananchi wengine waliojitokeza katika ziezi hilo wakiotesha miti.
    Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini Alvaro Rodriguez akiotesha mti katika eneo hilo huku balozi Mushi akishuhudia.
     Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini Alvaro Rodriguez kwa pamoja na Balozi Mushi wakimwagia maji katika  mti uliooteshwa katika eneo la Nusu Maili katika Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro.
  Wananchi wengine wakiotesha miti katika eneo hilo.
    Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini Alvaro Rodriguez akiwa na Balozi Mushi katika alama ya kumbukumbu ya UN iliyokwa katika eneo hilo la nusu maili katika Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro.
   Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini Alvaro Rodriguez akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kulamizika kwa zoezi la uoteshaji miti ,eneo la nusu maili katika Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro.

  Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini. 

  0 0  • Wateja kujishindia vifaa mbalimbali vya majumbani kupitia droo ya Bahati nasibu
  ·         Airtel na Tecno wawazawadia wateja wake wa Smartphone

  Kampuni ya mkononi ya Airtel Kwa kushirikiana na Tecno mobile  leo imewazawadia wateja wake kupitia promosheni iliyozinduliwa maalumu kwa msimu wa sikukuu za crismass, mwaka mpaya na valentine kwa lengo la kuwahamasisha wateja kutumia simu za kisasa za smartphone na kujishindia

  Promosheni hiyo ilihusisha wateja wa Airtel wanaonunua simu aina ya TECNO N6 and TECNO W3  kwa kipindi cha sikukuu za krismasi, mwaka mpya na valentine na kisha kupata nafasi ya kuingia kwenye droo ili  kujishindia vifaa mbalimbali vya nyumbani vikiwemo , Televisheni, Mashine ya kutengenezea Juisi, Jiko la kuchoma nyama, Mashine ya kutengeneza Sandwich , Brenda mashine pamoja na simu za smartphone za TECNO W4 mbili

  Akiendesha droo hiyo iliyofanyika katika ofisi za makao makuu ya Airtel Morocco Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando alisema “Airtel tuefika mwisho wa promosheni yetu lakini bado smartphone zinapatikana katika maduka yetu zikiambatana na ofa kabambe.  Napenda kuwashukuru wote walijiunga na ulimwengu wa smartphone kupitia promosheni hii nakuwaomba wateja wetu wengine waendelee kutembelea maduka yetu ili kupata simu za kisasa kwa bei nafuu na kufurahia huduma zetu bora ikiwemo, Airtel Money Relax, huduma ya Inteneti na nyingine nyingi”

  Kampuni ya Airtel ilizindua promosheni ya shinda na Smartiphone mwishoni mwa mwaka jana ili kila mteja wake anaenunua simu aweze kupata nafasi ya kushinda. 
  Meneja wa Tecno Mobile Tanzania, Marco Wang akisoma jina la mshindi wakati wa kuendesha bahati simu ya jishindie Tecno smartphone kupitia promosheni maalumu iliyoendeshwa na Airtel pamoja na Tecno wakati wa msimu wa sikukuu ambapo mwisho wake ni leo na washindi 7 wamepatikana. Akishuhudia (wakwanza kulia) ni Meneja Uhusiano wa Airtel Bwn Jackson Mmbando, akifatiwa na msimamizi wa bodi ya michezo ya kubahatisha bwana Bakari Majid , na kushoto ni Mkurugenzi wa Kitengo cha huduma kwa wateja , Bi Adriana Lyamba.
  Afisa huduma kwa wateja wa Airtel , Bwn Pascal Maziku Akiokota jina la mshindi wakati wa kuendesha bahati simu ya jishindie Tecno smartphone kupitia promosheni maalumu iliyoendeshwa na Airtel pamoja na Tecno wakati wa msimu wa sikukuu ambapo mwisho wake ni leo na washindi 7 wamepatikana. Akishuhudia (wakwanza kulia) ni Meneja Uhusiano wa Airtel Bwn Jackson Mmbando, akifatiwa na msimamizi wa bodi ya michezo ya kubahatisha bwana Bakari Majid, na kushoto ni Mkurugenzi wa Kitengo cha huduma kwa wateja , Bi Adriana Lyamba
  Meneja Uhusiano wa Airtel Bwn Jackson Mmbando akitangaza majina ya washindi wa promosheni maalumu iliyozinduliwa wakati wa msimu wa sikukuu inayowawezesha wateja wa Airtel kujishindia zawadi mbalimbali pindi watakaponunua simu za smart phone za Airtel. Washindi 7 wamepatikana katika droo ya Bahati nasibu iliyochezeshwa leo katika makao makuu ya Airtel Morocco jijini Dar es saalam , akishuhudia kushoto ni Mkurugenzi wa Kitengo cha huduma kwa wateja , Bi Adriana Lyamba
  Mkurugenzi wa Kitengo cha huduma kwa wateja , Bi Adriana Lyamba akionyesha simu aina ya Tecno iliyokabithiwa kwa washindi wakati wa droo ya bahati nasibu iliyochezeshwa katika ofisi za makao makuu ya Airtel jijini Dar es Saalam
  Wafanyakazi wa Airtel na wafanyakazi wa Tecno wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa kuchezesha droo ya bahati nasibu,

   

  0 0


  Na: Genofeva Matemu – WHUSM

  Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo imeanza kutekeleza malengo iliyojiwekea ya kuifanya Lugha ya Kiswahili kuwa bidhaa yenye thamani ili iweze kupata soko na kutumika duniani kote katika kurahisisha mawasiliano ya watumiaji wa lugha hiyo.

  Rai hiyo imetolewa na Waziri mwenye dhamana ya Sekta na Utamaduni Mhe. Nape Moses Nnauye alipokua akizungumza na wadau wa Sekta hiyo jana Jijini Dar es Salaam.

  “Tumejipanga kuangalia changamoto zinazotokana na Sera na Sheria tulizonazo, changamoto za kirasilimali na mambo ya kiutashi kwani kwa kuzitafutia ufumbuzi changamoto hizo Kiswahili kitaendelea kuwa bidhaa ambayo itavuka mipaka ya nchi na kuitangaza nchi yetu” amesema Mhe. Nnauye.

  Akizungumza wakati wa Mkutano huo Katibu Mtendaji Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) Dkt. Selemani Sewangi amewataka waandishi wa vitabu vya Kiswahili kuzingatia weledi wa matumizi fasaha ya lugha ya Kiswahili wakati wa uandishi wa vitabu ili kuweza kuisaidia jamii hasa mashuleni kujua misamiati fasaha ya lugha hiyo.

  Kwa upande wake mdau wa Utamaduni nchini Dkt. Musa Hans ameiomba serikali kuhamasisha wageni wote wanaoingia nchini kujifunza lugha ya Kiswahili na kuandaa mwongozo kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu utakaowataka watoto wote wanaoingia sekondari kuwa na kamusi za Kiswahili na kamusi za Kiswahili Kingereza zitakazowasaidia kujua misamihati ya lugha ya Kiswahili.

  Naye Mdau wa Utamaduni mama Mipango ameipongeza serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuendelea kutafuta njia mbalimbali za kueneza na kukuza lugha ya Kiswahili ndani na nje ya nchi.

  Katika kuendeleza ukuaji wa Lugha ya Kiswahili Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amekua mstari wa mbele kutumia lugha ya Kiswahili katika shughuli mbalimbali za kiserikali kama vile Mkutano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na Mkutano wa Umoja wa Afrika (AU) ambapo kwa kufanya hivyo lugha hii imeweza kusambaa kwa kasi zaidi.
   Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza na wadau wa sekta ya Utamaduni walipokutana nao Jijini Dar es Salaam kujadili namna ya kukifanya Kiswahili kuwa bidhaa yenye thamani na kukisambaza nje ya mipaka ya nchi.
  Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia Wambura (katikati) akichangia wakati wa majadiliano jana  Jijini Dar es Salaam na wadau wa Sekta ya Utamaduni katika kukuza na kukifanya kiswahili kuwa bidhaa yenye thamani. Kushoto ni Waziri wa Habari Mhe. Nape Moses Nnauye na kulia ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bibi. Nuru Millao
  Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akizungumza na wadau wa Sekta ya Utamaduni (hawapo pichani) walipokutana jana Jijini Dar es Salaam kujadili namna ya kukifanya Kiswahili kuwa bidhaa yenye thamani ndani na nje ya nchi.
  : Baadhi ya Wadau wa Sekta ya Utamaduni wakifuatilia kwa makini hoja zilizokua zikiendelea wakati wa majadiliano na viongozi wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kujadili namna ya kukifanya Kiswahili kuwa bidhaa yenye thamani ndani na nje ya nchi jana Jijini Dar es Salaam
  Katibu Mtendaji Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) Dkt. Selemani Sewangi akitoa taarifa ya namna Kiswahili kinavoendelea kukua wakati wa majadiliano na wadau wa sekta ya Utamaduni kujadili namna ya kukuza na kukifanya Kiswahili kuwa bidhaa yenye thamani ndani na nje ya nchi  jana Jijini Dar es Salaam.
  Mdau wa Utamaduni Mama Mipango akichangia mada wakati wa majadiliano na wadau wa sekta ya Utamaduni kujadili namna ya kukuza na kukifanya Kiswahili kuwa bidhaa yenye thamani ndani na nje ya nchi jana Jijini Dar es Salaam.
  : Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (waliokaa katikati) katika picha ya pamoja na wadau wa sekta ya Utamaduni walipokutana kujadili namna ya kukifanya Kiswahili kuwa bidhaa yenye thamani jana Jijini Dar es Salaam. Wapili kulia waliokaa ni Naibu Waziri wa Habari Mhe. Annastazia Wambura, Wapili kushoto waliokaa ni Katibu Mkuu Wizara ya Habari Prof. Elisante Ole Gabriel, na wakwanza kushoto waliokaa ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari Bibi. Nuru Millao.

  Picha na: Genofeva Matemu – WHUSM

older | 1 | .... | 1139 | 1140 | (Page 1141) | 1142 | 1143 | .... | 1898 | newer