Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46334 articles
Browse latest View live

Utalii wa Tanzania Saudi Arabia

$
0
0
Baaadhi ya watu mbalimbali wakitembelea banda la Tanzania, nchini Saudi Arabia, katika maonyesho ya utalii ya '(Travel and Tourism Pioneers Forum - 2017).Maonyesho ya utalii nchini Saudi Arabia yaipaisha Tanzania

Na Mwandishi Maalum, Saudi Arabia
Ubalozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia mwishoni mwa juma hili ulishiriki katika maonyesho ya Safari na Utalii yajulikanayo kama '(Travel and Tourism Pioneers Forum - 2017).


Maonyesho ya TPF 2017 ambayo hufanyika kila mwaka kwa uandalizi Al Awsat Expo chini ya uhisani wa Mwana Mfalme HRH Prince Dr. Seif al Islam bin Saud bin Abdulaziz, yamefanyika kwa mafanikio huku ubalozi wa Tanzania ukifanikiwa kwa kiasi kikubwa kutangaza utalii wa Tanzania.


Akizungumza katika maonyesho hayo, Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, H.E Hemed Mgaza, alisema kwamba maonesho hayo yalikuwa maalumu kwa wafanya maamuzi na viongozi wa asasi za utalii (decision makers and leaders and tourisma leaders) nchini Saudi Arabia.
Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, H.E Hemed Mgaza, mwenye suti nyeusi akizungumza jambo na wageni waliotembelea katika banda la Tanzania kwenye maonyesho hayo.

Alisema kwamba kuwa banda la Tanzania lilifanikiwa kuonesha vivutio vya utalii vya Tanzania ikiwemo mlima Kilimanjaro, mbuga za wanyama, hifadhi za taifa, maeneo ya kihistoria ya Zanzibar, kilwa na Bagamoyo.
Mazungumzo yakiendelea yakiongozwa na Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia
Watu wakipata maneno juu ya utalii wa Tanzania nchini Saudi Arabia
Karibuni Tanzania.
“Tunashukuru kwa kiasi kikubwa kushiriki katika maonyesho haya sambamba na Tanzania kutangaza vivutio vya utalii wan chi yetu, tukiamini kuwa ni fursa adhimu kwa nchi yetu.


“Tunaendelea na juhudi za kutangaza nchi yetu ya Tanzania sambamba na kuwaonyesha watu wa Saudi Arabia juu ya umuhimu wa kutembelea nchini kwetu ili kujionea fursa mbalimbali za kiuchumi na utalii,” Alisema.


Kwa mujibu wa Balozi Mgaza, miadi na majadiliano kuhusu kukuza utalii (promotion of tourism) yalifanyika baina ya washiriki wa Tanzania na mawakala wa utalii (tour operators) na wa usafiri (travel agents).

JUKWAA LA BIASHARA MKOANI SIMIYU

$
0
0
Na Mroki Mroki, TSN Digital-Simiyu 
Ni ile siku iliyosubiriwa ya kuumulika kibiashara mkoa wa Simiyu ulioanzishwa mwaka 2012, ambao umejipambanua kuwa ‘mkoa  darasa’, mintarafu suala zima la ujenzi wa viwanda nchini.

Mwezi uliopita, Rais John Magufuli alipotembelea mkoa huu, alipongeza juhudi zinazochukuliwa na mkoa huu chini ya mkuu wake, Anthony Mtaka, katika kujenga uchumi wa viwanda na hivyo kuelekea kuifanya ndoto yake ya Tanzania ya viwanda kutimia.

Kupitia Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) inayochapisha magazeti ya Daily News na HabariLeo pamoja na mitandao mbalimbali ya kijamii, imeshirikiana na Mkoa wa Simiyu kuandaa Jukwaa la Biashara Simiyu likiwa na lengo la kuibua fursa za uchumi za mkoa huu darasa ambazo zitadadavuliwa na kuchambuliwa hii leo, na hivyo kuwasaidia wawekezaji wa ndani na nje kujua ‘kunani’ Simiyu.
 Mkuu wa Mkao wa Simiyu, Anthony Mtaka (kulia) akifurahia jambo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Prof. Elisante Ole Gabriel katika Jukwaa hilo la Biashara Simiyu.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka akizungumza wakati wa ufunguzi wa Jukwaa la Biashara Mkoa wa Simiyu ambapo alilisitiza kuwa Simiyu itajengwa na wana Simiyu wenyewe na si kutegemea watu kutoka nje.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Prof Elisante Ole Gabriel akitoa mada katika Jukwaa la Biashara Simiyu.Prof aliwataka wafanyabiashara kutambia biashara wanayoifanya maana wateja hawanunui biadhaa zao bali hununua thamani ya kitu kinachouzwa. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.
Mbunge wa Jimbo la Itim,ila Mkoani Simiyu na Mwenyekiti wa Wafanyabiashra Simiyu, Njalu Daudi Silanga akizungumza machache kuhusiana na Jukwaa hilo la Biashara Simiyu.
 Mbunge wa Busega, Dk Raphael Chegeni akizungumza na kupongeza jitihada hizo za kuutangaza mkoa wa Simiyu na fursa zake zilizopo katika kukuza uchumi na maendeleo ya wanasimiyu.
Mbunge wa Busega, Dk Raphael Chegeni akisoma gazeti la Habarileo.




 Meza Kuu.
 Washiriki wa Jukwaa hilo la Biashara Simiyu.
 Baadhi ya wafanyabiashra wa Mkoani Simiyu wakiwa katika Jukwaa hilo.
 Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Magzeti ya Serikali (TSN) wachapishaji wa magfazeti ya Daily News, Habarileo na Spotileo ambao pia ni wamiliki wa Kiwanda cha Uchapaji cha Standard Printer, DK Jim Yonazi akizungumza na kueleza kwanini wameanza na Simiyu katika kuvumbua fursa.
 Meza Kuu ikimsikiliza Mhariri Mtendaji wa TSN, Dk Jim Yonazi.
Washiriki

WANANDOA WAHUKUMIWA MIAKA 20 JELA KWA KUKUTWA NA MENO YA TEMBO

$
0
0
NA HAMZA TEMBA - WMU
...................................................................

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo imewahukumu kifungo cha miaka 20 jela Peter Kabi na Leonida Loi Kabi ambao ni wanandoa baada ya kukutwa na meno ya tembo 210 yenye uzito wa kilo 450.6 pamoja na mifupa mitano ya tembo.

Meno hayo yanayodaiwa kuwa ni sawa na idadi ya tembo 93 waliouwawa yalikutwa nyumbani kwa washtakiwa hao tarehe 27 Oktoba, 2012 eneo la Kimara Stop Over Jijini Dar es Salaam.


Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Huruma Shahidi amesema ametoa hukumu hiyo leo baada ya mahakama kujiridhisha na ushahidi wa upande wa Jamhuri ukiongozwa na mawakili Paul Kadushi na Elia Athanas ambao kwa pamoja umewatia hatiani washtakiwa hao.


Amesema katika kosa la kwanza kila mtuhumiwa atatumikia kifungo cha miaka 15 jela, kosa la pili na la tatu miaka 20 kila moja na kwamba hukumu hizo zitaenda kwa pamoja.


Akitoa ushahidi wa upande wa Jamhuri juu ya athari za ujangili nchini, Mtaalamu kutoka Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI), aliyefahamika kwa jina moja la Lymo amesema idadi ya tembo hapa nchini imepungua kwa kiasi kikubwa kwani sensa ya mwaka 2006 inaonyesha tembo walikuwa 1,034,000 tofauti na sesa ya mwaka 2012 ambayo ilionesha idadi hiyo kupungua na kufikia 43,000.


Alisema sensa ya mwaka 2013 ilionesha idadi ya tembo kuongezeka na kufikia 50,000 ambayo ni matunda ya jitihada za Serikali katika kukabiliana na ujangili kwa kuongeza nguvu katika doria na mikakati mbalimbali ya kudhibiti ujangili.


Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori Wizara ya Maliasili na Utalii, Prof. Alexandre Songorwa akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada ya hukumu hiyo amesema, kila mtanzania anapaswa kujifunza kupitia hukumu hiyo kwa kuwa binadamu wote hujifunza kutokana na makosa na kwamba ni jukumu la kila mtanzania kulinda na kuhifadhi rasilimali za taifa.


“Rasilimali hizi ni zetu sote watanzania, sio za Serikali, sio za Wizara ya Maliasili na Utalii, sisi ni vibarua wenu, tuwalindie watoto wetu na wajukuu zetu hizi rasilimali, wasijekututukana huko mwishoni kama hawatakuta chochote wakalazimika kupanda ndege kwenda kuangalia vitu vilivyokuwa hapa hapa, watatutukana hatuna sababu ya kusubiri matusi” alisema Songorwa. 
 Watuhumiwa wa Ujangili, Peter Kabi (wa pili kulia) na mke wake Leonida Loi Kabi (wa tatu kulia) wakielekea kusomewa mashtaka ya kukutwa na meno 210 na mifupa mitano ya tembo katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es Salaam leo, wote wamehukumiwa kifungo cha miaka 20 jela. 
 Mtuhumiwa wa Ujangili, Peter Kabi (wa pili kulia) akielekea kusomewa mashtaka ya kukutwa na meno 210 na mifupa mitano ya tembo katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es Salaam leo, mtuhumiwa huyo na mke wake Leonida Loi Kabi (hayuko pichani) wamehukumiwa kifungo cha miaka 20 jela.
 Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori Wizara ya Maliasili na Utalii, Prof. Alexandre Songorwa (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada ya hukumu hiyo leo katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara hiyo anaeshuulikia Maendeleo ya Wanyamapori, Kanisius Karamaga.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori Wizara ya Maliasili na Utalii, Prof. Alexandre Songorwa akizungumza na wanahabari katika moja ya ukumbi mahakamani hapo.

MKEMIA MKUU KUENDELEA NA MAFUNZO KWA WADAU WAKE

$
0
0
 Na jacquiline Mrisho - MAELEZO.

Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA) wamejipanga kuendelea kuendesha mafunzo kwa wadau wa Kanda ya Mashariki wanaohusika na kemikali ili kuhakikisha kemikali zinatumika vema na kwa njia salama.

Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Mkemia Mkuu wa Serikali, Prof. Samwel Manyele alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu wasafirishaji na watumiaji wa kemikali nchini.

Prof. Manyele amesema kuwa wakala hufanya usajili na ukaguzi kwa wadau wote wanaohusika na kemikali wakiwemo waagizaji, watengenezaji, wasafirishaji, watumiaji, wanaosafirisha nje ya nchi au yeyote yule anayehusika na kemikali kwa njia moja au nyingine. 

Pia ukaguzi huo unahusisha mahali ambapo kemikali zinatumika, zinatunzwa au kuhifadhiwa.

“Kuanzia mwaka 2012 hadi sasa, wadau wa Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani waliopatiwa mafunzo ni 642 wakiwemo Askari wa Jeshi la Polisi Usalama Barabarani Tanzania Bara, wasimamizi wa shughuli za uzalishaji kwenye viwanda, wasambazaji, wasafirishaji wa kemikali pamoja na madereva wanaosafirisha kemikali., hivyo baada ya kuona umuhimu wake tumeamua kuendelea na mafunzo haya kwa wadau wetu wengine,” alisema Prof.Manyele.

Prof. Manyele ameongeza kuwa mafunzo hayo yatatolewa kwa siku mbili kwa kila kundi katika makundi matatu yakiwemo ya wasimamizi wa shughuli zinazohusisha kemikali watakaoanza tarehe 21- 22/02/2017, Mawakala wa Forodha watakaoanza tarehe 23-24/02/2017 pamoja na madereva wanaosafirisha kemikali kuanzia tarehe 10-11/03/2017.

Aidha, Wakala Mkuu wa Serikali amefafanua kuwa Wakala hautaruhusu mdau ambaye hajapitia mafunzo hayo kuhusika katika shughuli yoyote ya kemikali kwa kutumia, kuhifadhi, kusafirisha, kutoa bandarini na hata kuagiza kutoka nje ya nchi hivyo akasisistiza umuhimu wa wahusika kuhudhuria mafunzo hayo.

Ametoa rai kwa wadau hao kuwahi kuhudhuria mafunzo haya ili kutekeleza matakwa ya Sheria Na. 3 ya mwaka 2003 ya Udhibiti na Usimamizi wa kemikali pamoja na kuepuka usumbufu utakaoweza kujitokeza kwa sababu ya kukosa mafunzo.

Mkemia Mkuu wa Serikali, Prof. Samwel Manyele (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Jijini Dar es Salaam kuhusu mafunzo ya wasafirishaji na watumiaji wa Kemikali nchini, kutoka kulia ni Kaimu Meneja wa Maabara ya Kanda ya Mashariki, Everlight Matinga na Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi na Udhibiti wa Kemikali nchini,Sabanitho Mtega, (kutoka kushoto), Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sayansi Jinai na Huduma za Vinasaba, David Elias pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Biashara,George Kasinga.

TID AWAOMBA RADHI WATANZANIA KWA UTUMIAJI WA DAWA ZA KULEVYA,AKIRI KUUNGA MKONO JUHUDI ZA KUPAMBANA NA DAWA ZA KULEVYA

$
0
0
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Msanii wa Bongo fleva Khalid Mohamed (TID) amesema kuwa hawezi kufumbia macho wala kuwaonea aibu kwa kuwataja watu wote ambao wanafanya biashara ya dawa za kulevya.

TID amesema hayo jijini Dar es Salaam katika mkutano wa mkuu wa mkoa na waandishi wa habari juu ya mapmbano dhidi ya dawa za kulevya kwa mara ya tatu.

“Mimi mnyama na mkuu wa mkoa kaonesha unyama katika kupambana na madawa ya kulevya, hivyo namshukuru sana kwa hatua ngumu aliyoamua kuichukua,basi wote kwa pamoja tuanze kupambana na kuhakikisha biasha hii inapungua kama sio kuisha kabisa,tushiriki kwa pamoja kukomesha biashara hii kwa kupinga janga hili ” amesema TID.

TID ambaye amekiri hadharani kuwa amekuwa akitumia dawa za kulevya kwa muda mrefu lakini zimekuwa zikimtesa ,hivyo RC Makonda amekuwa msaada kwake,akasema na kuongeza kuwa hahitaji nguvu ya dola kuacha uvutaji wa dawa za kulevya,hivyo ameamua kuacha mwenyewe ili awe mfano wa kuigwa .

Amesema yeye bado ni kijana hana kasoro yoyote wala ulemavu wowote,hivyo itakuwa ni aibu kwake kuonekana mtumiaji wa dawa za kulevya mbele ya mtoto wake, hivyo atakuwa hajengi familia bali atakuwa anaibomoa kwa kumfanya mtoto aendelee kuiga tabia mbovu za baba yake. 
 
TID ambaye aliiongea kwa ujasiri mkubwa bila kuhofu lolote akiwaomba Watanzania wamuelewe na kumpokea tena,kama kijana aliye amua kuacha matumizi ya dawa za kulevya.

WAZIRI PROF. MBARAWA AFANYA MAZUNGUMZO NA UJUMBE KUTOKA JAMHURI YA KIDEMOKRASIA YA CONGO

$
0
0

Stori na Biseko Ibrahim.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa amewataka watumishi wa Wizara hiyo Sekta ya Uchukuzi kutumia vizuri fursa ya kuhamia Dodoma kwa kuwatumikia watanzania kwa uadilifu na weledi.

Amesema hayo jijini Dar es Salaam wakati akiwaaga watumishi wa Sekta ya uchukuzi wa awamu ya kwanza ambao wameondoka leo kuelekea mjini Dodoma.

“Nawapongeza kwa kupata fursa ya kuwa katika awamu ya kwanza katika Wizara hii kuhamia Dodoma fahamuni hii ni fursa na si changamoto kwani hatua hii inasogeza huduma karibu na wananchi hivyo watumikieni kwa moyo”, amesema Prof. Mbarawa.

Prof. Mbarawa amesema kuwa nia ya Serikali ni kuhakikisha watumishi wake wanahamia Dodoma na kuendelea na utekelezaji wa majukumu yake kwa wananchi.

Kwa Upande wake Katibu Mkuu wa Sekta ya Uchukuzi, Dkt. Leonard Chamuriho amesema awamu ya kwanza ya watumishi zaidi ya 45 inahamia Dodoma mwezi huu na Awamu ya pili itaanza mwezi wa Machi na watumishi wote wa sekta ya uchukuzi watakuwa Dodoma ifikapo Agosti mwaka huu.

“Watumishi wa Sekta ya Uchukuzi wanaohamia Dodoma katika awamu ya kwanza ni pamoja na Katibu Mkuu Sekta ya Uchukuzi, Wakurugenzi na Wakurugenzi wasaidizi, wakuu wa vitengo na maafisa waandamizi”, amesisitiza Dkt. Chamuriho.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa akizungumza na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo (Sekta ya Uchukuzi), Dkt. Leornard Chamuriho kabla ya kuwaaga watumishi wa Wizara hiyo  wanaohamia Dodoma leo, jijini Dar es salaam. Picha na Biseko Ibrahim.

WANAHABARI TUMUUNGE MKONO RAIS KATIKA VITA DHIDI YA MADAWA YA KULEVYA.

$
0
0
Na Raymond Mushumbusi WHUSM.

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye amevishauri vyombo vya habari nchini kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Joseph Pombe Magufuli katika vita dhidi ya madawa ya kulevya nchini.

Ameyasema hayo wakati wa maadhimisho ya Siku ya Redio Duniani yaliofanyika katika Chuo Kikuu huria cha Tanzania na kusisitiza kuwa vyombo vya habari viwe sehemu ya kuwaunganisha watanzania katika mapambano dhidi ya madawa ya kulevya.

“Wanahabari tuliunganishe taifa letu tuwe kitu kimoja katika mapambano dhidi ya madawa ya kulevya” alisisitiza Mhe. Nnauye.

Ameongeza kuwa sasa ni wakati wa watu wote kuungana kwa pamoja zikiwemo tasnia zilizopo katika Wizara yake za Habari Utamaduni Sanaa na Michezo kwani vita hii ni ya watanzania wote na sio mtu mmoja au Serikali pekee.

Aidha Mhe. Nape amevitaka vyombo vya habari kutobaki nyuma katika mapambano dhidi ya madawa ya kulevya na kuhakikisha  haki inatendeka na vita dhodi ya madawa ya kulevya vinashinda.
 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza na wadau Redio na vyombo vya habari kwa ujumla katika maadhimisho ya Siku ya Redio Duniani yaliyofanyika katika Chuo Kikuu Huria cha Tanzania Jijini Dar es Salaam.

JAJI FATUMA HAMISI MASENGI AAGWA RASMI MAHAKAMA KUU KANDA YA ARUSHA LEO

$
0
0
Picha ya pamoja kati ya waheshimiwa majaji kanda ya Arusha na Kilimanjaro ,Wakwanza kulia ni mhe,Jaji Dkt.Modesta Opiyo,Wakwanza kushosto ni mhe,Jaji Salma Maghimbi,akifuatiwa na aliyeko kushoto kwake mhe,Jaji Sekela Mushi,akifuatiwa na mhe,Jaji mstaafu Fatuma Hamis Masengi wakiwa na majaji wengine pamoja na waheshimiwa mahakamu.Picha na Vero Ignatus Blog.
Mhe.Jaji Mstaafu wa mahakama kuu kanda ya Arusha Fatuma Hamis Masengi 
Mhe,Jaji Mstaafu wa mahakama kuu kanda ya Arusha Fatuma Hamis Masengi akiwa na waheshimiwa mahakimu wa mahakama ya mwanzo(waheshimiwa mahakimu hao wamelelewa na mhe,Fatuma Masengi)
Picha ya pamoja ya waheshimiwa majaji pamoja na mawakili wa serikali,na wale wa kujitegemea.Picha na Vero Ignatus Blog.




Na.Vero Ignatus.

Sherehe za kumuaga aliyekuwa Jaji mfawidhi wa mahakam kuu kanda ya Arusha Mhe,Fatuma Hamis Masengi ,zimefanyika leo katika mahakama kuu ya ndanda hiyo na kuhudhuriwa na wageni mbalimbali wakiwemo majaji,mahakimu,mawakili wasajili wa mahama watendaji pamoja na wageni waalikwa.

Sherehe hizo zimeanza majira ya saa asubuhi katika mahakama ya wazi ambapo Jaji Fatuma alianza kufanya kazi mnamo mwaka 1974 katika mahakama ya mwanzo na kuendelea kuitumikia mahakama hadi alipoteuliwa kuwa jaji mfawidhi mahakama kuu.

Amewataka majaji na mahakimu pamoja na wale wote wanaofanya kazi za kimahakama wafanye kazi kwa kumtegemea Mungu huku wakijua kazi yeyote ina changamoto zake hivyo ni vyema kufanya kazi kwa weledi zaidi na kwa kuzingatia sheria inavyosema,wakimtendea haki kila mtu kwa stahiki.

Amewataka wanawake kutokukata tamaa huku akisema kuwa wanawake wanaweza kuliko wanaume japo kuwa wakati mwingine wanaume wanaona kama vile wanawake ni wanyonge lakini mwanamke anaweza pale ambapo anasimama kwa nafasi yake na kulitumikia kusudi kwa wakati na weledi.

"Wanawake wenzangu msikate tamaa na kujiona wewe ni dhaifu ,tunaweza msibweteke unapopata nafasi itumie vizuri bila kuaharibu taratibu zilizowekwa ,fanya kazi kwa bidii na jamii itaona juhudi zako ,wanawake tunaweza "alisema masengi.

Aidha Jaji Fatuma amesema kuwa anamshukuru sana Mungu kwa kumuwezesha kwa wakati wote ambapo amekuwa akifanya kazi yenye majukumu mazito, amezishukuru Asasi za kiserikali na zile zisizo za kiserikali,amewashukuru wale wote walioshirikiana nae katika kipindi chote alichokuwa akitimiza majukumu yake ya kikazi.

MAMA MAGUFULI NA MAMA MAJALIWA ZIARANI SINGIDA KUTEMBELEA VITUO VYA WAZEE WASIOJIWEZA

$
0
0
 Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli na mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wakipokea msaada wa vyakula na vinywaji kutoka kwa Meneja wa tawi la Benki ya NMB Singida Bw. Abius Mlengwa katika Makazi ya Wazee Wasiojiweza Sukamahela wilaya ya Manyoni mkoani Singida leo Februari 13, 2017.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli na mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wakipokea msada wa vyakula na vinywaji kutoka kwa Meneja wa Tawi la CRDB Manyoni Bw. Richard Karatta katika Makazi ya Wazee Wasiojiweza Sukamahela wilaya ya Manyoni mkoani Singida leo Februari 13, 2017. PICHA NA IKULU


Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akisalimiana na mkuu wa mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi alipowasili wilayani Manyoni mkoani Singida leo Februari 13, 2017.
  Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli na mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wakilakiwa kwa furaha walipowasili katika Makazi ya Wazee Wasiojiweza Sukamahela wilaya ya Manyoni mkoani Singida leo Februari 13, 2017.
 Afisa Ustawi wa Jamii Yeremia Ngoo akiwapa maelezo Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli na mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa nyumbani kwa Bibi Agnes Kamota (75) walipotembelea Makazi ya Wazee Wasiojiweza Sukamahela wilaya ya Manyoni mkoani Singida leo Februari 13, 2017.
 Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli na mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wakiwa na Bibi Agnes Kamota (75) walipomtembelea nyumbani kwake katika Makazi ya Wazee Wasiojiweza Sukamahela wilaya ya Manyoni mkoani Singida leo Februari 13, 2017.
  Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli na mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wakitembelea  Zahanati ya Sukamahela katika Makazi ya Wazee Wasiojiweza Sukamahela wilaya ya Manyoni mkoani Singida leo Februari 13, 2017
 Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa akisalimia wananchi wakati yeye na Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli walipofanya ziara  katika Makazi ya Wazee Wasiojiweza Sukamahela wilaya ya Manyoni mkoani Singida leo Februari 13, 2017.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli na mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wakishiriki kucheza ngoma na vikundi vilivyojitokeza kuwalaki katika Makazi ya Wazee Wasiojiweza Sukamahela wilaya ya Manyoni mkoani Singida leo Februari 13, 2017.
 Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akihutubia wananchi wakati yeye na mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa walipotembelea Makazi ya Wazee Wasiojiweza Sukamahela wilaya ya Manyoni mkoani Singida leo Februari 13, 2017.
 Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa akihutubia wananchi wakati walipotembelea Makazi ya Wazee Wasiojiweza Sukamahela wilaya ya Manyoni mkoani Singida leo Februari 13, 2017.
 Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli na  mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wakioneshana kielele cha kilima cha Sukamahela ambapo inasemekana ndipo ilipo alama ya kuonesha katikati ya nchi ya Tanzania wakati wa ziara yao katika Makazi ya Wazee Wasiojiweza Sukamahela wilaya ya Manyoni mkoani Singida leo Februari 13, 2017
 Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli na mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wakitoa msaada wa vyakula tani 7.5  katika Makazi ya Wazee Wasiojiweza Sukamahela wilaya ya Manyoni mkoani Singida leo Februari 13, 2017

NA MWANDISHI MAALUM
MKE wa Rais Mheshimiwa Mama Janeth Magufuli pamoja na Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wametoa rai kwa Wanzania kujenga tabia ya kusaidia watu wasiojiweza na wenye mahitaji maalumu.

Wake hao wa viongozi pia wamewatahadharisha watumishi wanaofanya kazi katika vituo vya kulelea wazee wasiojiweza wahakikishe misaada inayotolewa na wadau mbalimbali inawafikia walengwa bila ya kuchakachuliwa.

Wameyasema hayo leo (Jumatatu, Februari 13, 2017) wakati walipotembelea Makazi ya Wazee wasiojiweza na walemavu watokanao na ugonjwa wa ukoma ya Sukamahela wilayani Manyoni Mkoani Singida.

Katika kituo hicho wamekabidhi tani 7.5 za vyakula mbalimbali ukiwemo mchele, unga wa sembe na maharage, ambapo Mama Janeth amewataka viongozi wa kituo kuhakikisha chakula hicho hakichakachuliwi.

Akizungumza na wazee wa makaazi hayo, viongozi mbalimbali na wananchi wanaozunguka eneo hilo Mama Janeth amesema “Naomba chakula hiki kitunzwe vizuri na hakikisheni kinawafikia walengwa na kisichakachuliwe hii ni sadaka,”.

Kwa upande wake Mama Mary amewaomba wadau mbalimbali kujitokeza na kuwasaidia wazee wanaoishi katika makaazi ya kulelea walemavu na wasiojiweza nchini kwa sababu wanakabiliwa na changamoto nyingi.
“Watanzania wote popote mlipo tukumbuke kutembelea vituo vya kulelea wazee kikiwepo na hiki tulichokitembelea leo cha Sukamahela na kutoa misaada mbalimbali kkwa kadri tutakavyojaaliwa,” amesema.

Awali Mkuu wa Makazi hayo Bw. Yeremia Ngoo alisema kituo hicho kilianzishwa mwaka 1974 chini ya Idara ya Ustawi wa Jamii kwa lengo la kuwasaidia watu wenye ukoma na wazee wasiojiweza mkoani Singida.

Bw. Ngoo alisema kituo hicho chenye wakazi 62 kinakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ya upungufu wa wapishi ambapo kwa sasa yupo mmoja huku mahitaji yakiwa ni wapishi wanne. Pia nyumba nyingi ni chakavu na zina nyufa.

Naye Mwenyekiti wa Wazee waishio katika makaazi hayo, Mzee Andrea Yohana aliwashikuru wake hao wa viongozi na kuwaomba waendelee na moyo huo wa kusaidia watu wasiojiweza.

RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA WAGENI MBALIMBALI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli akisalimiana na Balozi wa Uingereza hapa nchini Sarah Cooke aliyefika Ikulu kwa ajili ya Mazungumzo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli akiwa katika Mazungumzo na Balozi wa Uingereza hapa nchini Sarah Cooke Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli akiagana na Balozi wa Uingereza hapa nchini Sarah Cooke mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli akisalimiana na Mwakilishi Mkazi mpya wa Shirika la Fedha Duniani (IMF) Bhaswar Mukhopadhyay aliyefika Ikulu kwa ajili ya mazungumzo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli akizungumza na Mwakilishi Mkazi mpya wa Shirika la Fedha Duniani (IMF) Bhaswar Mukhopadhyay Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli akiagana na Mwakilishi Mkazi mpya wa Shirika la Fedha Duniani (IMF) Bhaswar Mukhopadhyay mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli akiwa na Spika wa Bunge la Afrika Mashariki Daniel Fred Kidega mara baada ya kuwasili Ikulu kwa ajili ya mazungumzo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli akiagana na Spika wa Bunge la Afrika Mashariki Daniel Fred Kidega mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli akisalimiana na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Balozi Liberat Mfumukeko  aliyefika Ikulu kwa ajili ya mazungumzo jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Balozi Liberat Mfumukeko  Ikulu 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli akiagana na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Balozi Liberat Mfumukeko mara baada ya kumaliza mazungumzo yao   Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli akiwa amemshika mkono Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Augustine Mahiga  wakati akijadiliana jambo na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Balozi Liberat Mfumukeko mara baada ya kumaliza mazungumzo yao   Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli akifurahia jambo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Augustine Mahiga mara baada ya kumaliza mazungumzo na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Balozi Liberat Mfumukeko Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

ORODHA YA MAHAKIMU NA MAJAJI WALIOVURUGA KESI ZA WAUZA UNGA KUTUA KWA JAJI MKUU

$
0
0
Kamishina wa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya nchini Rogers Sianga 

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.

JAJI Mkuu anatarajia  kupokea  orodha ya  majina ya mahakimu na majaji  ambao wanadaiwa kuvuruga kesi za watu wanaotuhumiwa kujihusisha na dawa za kulevya.

Hayo ameyasema leo  Kamishina wa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya nchini Rogers Sianga wakati wa mkutano wa viongozi mbalimbali wa kitaifa na waandishi wa habari ulioandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda  kwa ajili  kupambana na dawa za kulevya.

 Sianga amesema kuwa kesi zimevurugwa na mahakimu na majaji. hivyo wale wote watakaobainika kuhusika watashitakiwa na hata wawe na mali ambazo wamezipata kwa biashara hiyo zitataifishwa.

Amesema kuwa watazunguka katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam ili kuhakikisha mtandao huo unapatikana na kwenda hata Zanzibar na mbinu zote wanazijua katika kufanya biashara hiyo.

Nae Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amemkabidhi orodha ya majina 97 wanaojihusisha na dawa za kulevya na kuongeza kuwa moto umewashwa dhidi ya watu wanaojihusisha na dawa za kulevya.

Amesema kuwa kuna nyumba 200 zinajihusisha kufanya biashara ya madawa ya kulevya hapa jijini ambapo wote hao watafikiwa katika operesheni,ambayo mojawapo wanatarajia kuifanya usiku wa leo.

Nae Msanii wa muziki wa kizazi kipya Khalid Mohamed almaarufu kwa jina la kisanii TID , amesema kuwa sasa ni mnyama ambae yuko tayari kupambana na watu wanaouza pamoja na kutumia dawa za kulevya na amerudi kwa kufanya kazi na kuongeza kuwa kuimba hakuitaji dawa za kulevya.

Katika mkutano huo watu wawili wametakiwa kufika katika Kituo cha Polisi kati ambao ni Chidi Mapenzi,  Ayuob Mfaume Kiboko.

RC MAKONDA AMSHAURI SPIKA WA BUNGE,NDUGAI KUWAPIMA WABUNGE KUBAINI NAO KAMA WANATUMIA DAWA ZA KULEVYA AMA LA.

Alichokiongea Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za kulevya.

VIJUSO VYA MAGAZETI YA LEO JUMANNE FEBRUARY 14,2017

Wanahabari watakiwa kuacha kuamini kila kitu, wasome

$
0
0
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mh. Nape Nnauye (wa pili kulia) akimpongeza Meneja wa Redio Jamii Orkonerei  FM, Baraka David Ole Maika baada ya kuwasilisha risala ya mafunzo ya ufundi kwa Redio za Jamii wakati maadhimisho ya siku ya Redio Duniani yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Chuo Kikuu Huria jijini Dar es Salaam jana. Kulia  Mkurugenzi wa Utangazaji wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Fredrick Ntobi, Wa tatu kulia ni Mkuu wa Ofisi na Mwakilishili wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Zulmira Rodrigues, Wanne kulia Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu na Menejementi ya Teknolojia  wa Chuo Kikuu Huria (OUT), Dr. Edephonce Nfuka na Wa kwanza kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Mtandao wa Vyombo vya Habari vya Jamii (COMNETA), Prosper Kwigize.
 Mgeni rasmi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye akizungumza kwenye sherehe za maadhimisho ya siku ya redio duniani yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Chuo Kikuu Huria (OUT) jijini Dar es Salaam.
  Afisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Stella Vuzo akisheheresha kwenye sherehe za maadhimisho ya siku ya radio duniani yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Chuo Kikuu Huria (OUT) jijini Dar es Salaam
 Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini Zulmira Rodrigues akitoa neno la ukaribisho liliombatana na ujumbe maalum kwenye sherehe za maadhimisho ya siku ya redio duniani yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Chuo Kikuu Huria (OUT) jijini Dar es Salaam.
 Makamu Mwenyekiti wa Mtandao wa Vyombo vya Habari vya Jamii (COMNETA), Prosper Kwigize akisoma hotuba mbele ya mgeni rasmi Waziri Nape Nnauye (hayupo pichani) wakati wa sherehe za maadhimisho ya siku ya redio duniani, yaliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Chuo Kikuu Huria (OUT) jijini Dar es Salaam.
 Mgeni rasmi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye akiteta jambo na Mkuu wa ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini Zulmira Rodrigues (katikati) wakati wa sherehe za maadhimisho ya siku ya redio duniani yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Chuo Kikuu Huria (OUT) jijini Dar es Salaam. Kushoto ni  Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu na Menejementi ya Teknolojia  wa Chuo Kikuu Huria (OUT), Dr. Edephonce Nfuka
 Mgeni rasmi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye akimpongeza Makamu mwenyekiti wa Umoja wa Redio za Jamii (COMNETA) Prosper Kwigize kwa hotuba nzuri wakati wa sherehe za maadhimisho ya siku ya redio duniani yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Chuo Kikuu Huria (OUT) jijini Dar es Salaam. Kushoto ni  Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu na Menejementi ya Teknolojia  wa Chuo Kikuu Huria (OUT), Dr. Edephonce Nfuka na kulia ni Mkurugenzi wa Utangazaji wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Fredrick Ntobi.
 Mkurugenzi wa Utangazaji wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Fredrick Ntobi akizungumza kuhusu taratibu na sheria za utoaji leseni kwa redio za jamii nchini wakati wa sherehe za maadhimisho ya siku ya redio duniani yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Chuo Kikuu Huria (OUT) jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Dk. Ayoub Rioba akifafanua jambo wakati wa sherehe za maadhimisho ya siku ya redio duniani yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Chuo Kikuu Huria (OUT) jijini Dar es Salaam.
 Meneja wa Redio Jamii Orkonerei  FM, Baraka David Ole Maika akitoa neno la shukrani wakati wa sherehe za maadhimisho ya siku ya redio duniani yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Chuo Kikuu Huria (OUT) jijini Dar es Salaam.
 Washiriki kutoka redio za jamii nchini na waandishi wa habari waliohudhuria sherehe za maadhimisho ya siku ya redio duniani yaliyofanyika katika ukumbi wa Cho Kikuu Huria (OUT) jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa Utangazaji wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Fredrick Ntobi akiwasilisha mada kuhusu upashanaji wa vyombo vya habari na sheria wakati wa sherehe za maadhimisho ya siku ya redio duniani yaliyoratibiwa na UNESCO na kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa Chuo Kikuu Huria (OUT) jijini Dar es Salaam.
  Mshauri wa Masuala ya Uchumi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) Tanzania, Rogers Dhliwayo akizungumza kuhusu malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) na namna radio inavyowezesha hamasa ya utekelezaji wake kwenye sherehe za maadhimisho ya siku ya redio duniani yaliyoratibiwa na UNESCO na kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa Chuo Kikuu Huria (OUT) jijini Dar es Salaam.
Meza kuu kwenye sherehe za maadhimisho ya siku ya redio duniani zilizofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Chuo Kikuu Huria (OUT) jijini Dar es Salaam.
 Mgeni rasmi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye (katikati) katika picha ya pamoja na wawakilishi wa redio za jamii nchini wakati sherehe za maadhimisho ya siku ya redio duniani yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Chuo Kikuu Huria (OUT) jijini Dar es Salaam.
 Mgeni rasmi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye(katikati) na meza kuu katika picha ya pamoja na wajumbe wa bodi ya COMNETA wakati wa sherehe za maadhimisho ya siku ya redio duniani yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Chuo Kikuu Huria (OUT) jijini Dar es Salaam.
  Mgeni rasmi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye(katikati) na meza kuu katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa kwenye sherehe za maadhimisho ya siku ya redio duniani yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Chuo Kikuu Huria (OUT) jijini Dar es Salaam.
Maafisa wa UNESCO Dar Luiana Temba (kushoto) na Rose Mwalongo Mataifa wakifurahi jambo kwenye sherehe za maadhimisho ya siku ya redio duniani yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Chuo Kikuu Huria (OUT) jijini Dar es Salaam.

Na Mwandishi wetu

SERIKALI imewataka wanahabari kusoma sheria, taratibu na kanuni zinaogusa tasnia yao ili iweze kuendelea na kuachana na kuamini kila kitu wanachoambiwa na mtu mmoja.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye wakati  akizungumza katika siku ya radio duniani, hafla iliyofanyika Chuo Kikuu Huria jijini Dar es Salaam.

"Watu someni sheria, taratibu na kanuni kwa kina ili kujua na kuzielewa, mkielewa kama kuna sheria inakwaza ukuaji wa sekta ya habari tuseme tukae chini.. " alisema Waziri Nape akijibu hoja kuhusu sheria za habari zilizopo ambazo zinadaiwa kukwaza uhuru wa ukusanyaji wa habari.

Ilielezwa katika hafla hiyo kuwa sheria za sasa ya takwimu na habari  zinakwaza uhuru wa sekta hiyo muhimu kwa maendeleo ya taifa.
Katika hoja hiyo Makamu mwenyekiti wa Umoja wa Redio za Jamii (COMNETA) Prosper Kwigize katika hotuba yake kwa Serikali, alisema kwamba redio hizo zinachangamoto nyingi katika utendaji wake ikiwamo sheria zilizopo,watoa habari wasioeleweka na wanazuia upatikanaji wa habari.

Nape alisema kwamba sheria si msaafu na kwa kuwa asilimia 80 za habari zinazalishwa na serikali, waandishi wanahaki ya kupata habari hizo na kama kuna kikwazo ni lazima kitafutiwe suluhu.

"Tukae tushindane kwa hoja tukubaliane na kuhakikisha kwamba tunarekebisha.. Bunge kazi yake ni kutunga na kufuta sheria" alisema Nape ambaye alisema kwamba sheria ya sasa imetoa nguvu kwa watoa habari na kwamba si kila habari iliyopo serikalini ni classified.
Alisema pia ili kufanikisha upatikanaji wa habari maofisa habari wamepewa maagizo ya kushiriki vikao ili waweze kutoa taarifa bila woga na kwa ujasiri mkubwa.

Alisema ni kazi ya serikali ni kutengeneza mazingira mazuri ya kukua kwa tasnia ya habari na itaendelea kupigania hilo kwa kuwa inatambua umuhimu wa vyombo vya habari.

Pamoja na kuweka mazingira mazuri amewataka wanaoendesha redio za jamii kutafuta namna ya kujiunga na taarifa za kitaifa (habari) ili wananchi wasitengwe na matukio ya maeneo mengine.

Alisema kwa kuwa sehemu kubwa ya redio hizo ziko pembezoni ni vyema nguvu yake ikatumika pia kuhabarisha matukio ya kitaifa.
Akizungumzia dawa za kulevya, Waziri Nape alitaka wanahabari kuwa na uzalendo na kushiriki katika vita hiyo kwa kutumia vyombo vyao vyote.

Alisema ni vyema wananchi na wanahabari wakatambua kwamba vita hiyo ni yetu sote na kwamba wanahabari wanauwezo wa kuunganisha wananchi katika kushinda hiyo vita ambayo ni kubwa.

Akizungumzia redio alitaka watu wanaotumia vyombo hivyo kuangalia namna ya kutoachwa nyuma wakati huu wa mabadiliko makubwa ya teknolojia na sayansi ambapo matumizi ya mtandao ya utoaji wa habari papo hapo unaendelea.

Aliwataka watu kuzungumza nafasi ya radio katika kuleta maendeleo huku wakiangalia changamoto zinazoletwa na teknolojia ya habari.
Sherehe hizo ambazo ziliambatanishwa na midahalo kuhusu upashanaji wa vyombo vya habari na sheria iliwasilishwa na Mkurugenzi wa utangazaji wa TCRA Ntobi na pia watendaji wa UNDP kuhusu malengo ya maendeleo endelevu na namna radio inavyowezesha hamasa ya utekelezaji iliratibiwa na UNESCO.

Mkuu wa ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini Zulmira Rodrigues alisema akimkaribisha Waziri Nape kwamba washiriki katika sekta ya utangazaji wanatakiwa kuwa pamoja ili kukuza upashanaji wa habari katika maeneo ya pembezoni.

Alishauri kuwepo na kuaminiana ili kufanikisha malengo  ya kuleta maendeleo kwa kupeana nafasi na kushirikishana.
Alitaka watanzania kutumia nguvu ya radio kukabiliana na matatizo mbalimbali ya kitaifa na kuleta maendeleo yanayotakiwa.
Kukiwa na vituo vya radio 44,000 duniani Mwakilishi huyo wa UNESCO alisema kwamba  radio bado ina maslahi makubwa kwa wananchi kutokana na kutoa sauti kwa wakazi ili  kukabiliana na changamoto zilizopo.

MKUU WA WILAYA AELEZA SABABU ZA KUWAAMURU WAFANYA BIASHARA KUFUNGA MADUKA YANAYOLIZUNGUKA SOKO KUU - SONGEA

$
0
0

Mkuu wa wilaya ya Songea Mkoani RUVUMA Pololiti Mgema , aelezea sababu kuu za kuwaamuru wafanya biashara kufunga maduka yao, ambayo yana lizunguka soko kuu la Songea

MUHIMBILI KUFANYA UPASUAJI WA KWANZA KWA WATOTO KUPITIA MATUNDU MADOGO

USAFI HAUHITAJI SIASA- RC MAKALLA

TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE (JKCI) KWA KUSHIRIKIANA HOSPITALI YA BLK YA NCHINI INDIA WATOA HUDUMA YA MATIBABU YA MOYO BILA YA KUFUNGUA KIFUA KWA WAGONJWA 16

$
0
0
Madaktari Bingwa wa Moyo kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Peter Kisenge (kushoto) na Subhash Chandra (kulia) kutoka Hospitali ya BLK ya nchini India wakimwekea mgonjwa kifaa kitakachosaidia moyo kupata umeme kwa jina la kitaalam Pacemaker . JKCI kwa kushirikiana na BLK hospital kwa kutumia mtambo wa Cath Lab wamewafanyia wagonjwa 16 huduma mbalimbali za matibabu ya moyo ya bila kufungua kifua (Catheterization).
Madaktari Bingwa wa Moyo kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Peter Kisenge (kushoto) na Subhash Chandra (kulia) kutoka Hospitali ya BLK ya nchini India wakimwekea mgonjwa betri ambalo litatumiwa na kifaa kitakachosaidia moyo kupata umeme kwa jina la kitaalam Pacemaker . JKCI kwa kushirikiana na BLK hospital kwa kutumia mtambo wa Cath Lab wamewafanyia wagonjwa 16 huduma mbalimbali za matibabu ya moyo ya bila kufungua kifua (Catheterization).
Daktari bingwa wa Moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Peter Kisenge akimuhudumia Monica Mahenge ambaye amelazwa katika Taasisi hiyo baada ya kufanyiwa matibabu ya moyo kupitia mishipa ya damu bila kufungua kifua (Catheterization) kwa kutumia mtambo wa Cath lab . Monica ni mmoja kati ya wagonjwa 16 ambao JKCI kwa kushirikiana na wataalamu kutoka Hospitali ya BLK ya nchini India walitoa huduma za matibabu ya kuzibua milango ya moyo (Valve), balloon mitral valve procedure (Valvuloplasty), kuzibua mishipa ya damu ya moyo, kufunga kifaa kitakachosaidia moyo kupata umeme (Pacemaker) na kuangalia utendaji kazi wa Moyo.
Madaktari bingwa wa Moyo, Wauguzi, Technologists, wataalam wa dawa za usingizi wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumaliza kumpatia mgonjwa huduma za matibabu ya kuzibua milango ya moyo (Valve) bila kufungua kifua (Catheterization) kwa kutumia mtambo wa Cath lab .
Kazi ya kutoa huduma ya matibabu ya Moyo kwa mgonjwa kupitia mishipa ya damu bila kufungua kifua (Catheterization) kwa kutumia mtambo wa Cath lab ikiendelea.


Picha na Anna Nkinda – JKCI

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA APOKEA MADAWATI

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea mchango wa sh. milioni 5.5 kutoka kwa Mhasibu wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Rose Makange (katikati)ukiwa ni mchango wa watumishi wa TAMISEMI kwa ajili ya madawati wilayani Ruangwa. Makabidhiano hayo yalifanyika Ofisini kwa Waziri Mkuu, mjini Dodoma Februari 14, 2017. Kulia ni Rose Nyoni. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) baada ya kupokea Sh. milioni 5.5 ukiwa ni mchango wa watumishi wa Ofisi hiyo kwa ajili ya madawati wilayani Ruangwa. Makabidhiano hayo yalifanyika, Ofisini kwa Waziri Mkuu mjini Dodoma Februari 14, 2017. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) baada ya kupokea mchango wa watumishi hao wa sh. milioni 5.5 kwa ajili ya madawati wilayani Ruangwa. Makabidhiano hayo yalifanyika Ofisini kwa Waziri Mkuu mjini Dodoma Februari 14, 2017.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na baadhi ya watumishi wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) baada ya kupokea mchango wa watumishi hao wa sh. milioni 5.5 kwa ajili ya madawati wilayani Ruangwa. Makabidhiano hayo yalifanyika Ofisini kwa Waziri Mkuu mjini Dodoma Februari 14, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Viewing all 46334 articles
Browse latest View live


Latest Images