Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46206 articles
Browse latest View live

TAARIFA KUHUSU WATANZANIA WALIOPATA MATATIZO NCHINI MSUMBIJI.

0
0



NAPE KUONGOZA BONANZA LA WANAHABARI FEBRUARY 18 DAR ES SALAAM

0
0
 Ofisa Habari wa Idara ya Habari Maelezo Zamaradi Kawawa akizungumza juu ya Bonanza hilo
 Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Theophil Makunga akizungumza na waandishi wa habari juu ya Tamasha hilo

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Waziri wa habari Sanaa, utamaduni na Michezo, Nape Nnauye anataraji kuongoza  Bonanza la mazoezi na upimaji afya February 18 mwaka huu ulionadaliwa na Chama cha maofisa mawasiliano Serikalini (TAGCO) kwa kushirikiana na jukwaa la wahariri Tanzania na Dar es Salaam City Press Club.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Msemaji wa chama TAGCO, Abel Ngapemba ametaja kuwa lengo la Bonanza hilo ni kuhamasisha wananchi kujenga tabia ya kufanya mazoezi na kupima afya kama ilivyozoeleka kwa kuunga mkono kampeni iliyozinduliwa na Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan.

“washiriki wa bonanza hili ni pamoja na maofisa mawasiliano wa Serikali na wasekta binafsi ,Wahariri , Wahandishi wa habari na Bloggers na wananchi kwa ujumla kwa kuongozwa na Waziri Nape Nnauye na kuhudhuliwa na viongozi wa Wizara ya afya na ustawi wa jamii, jinsia wazee na watoto” amesema  Abel.

Ametaja kuwa mbali ya mazoezi taasisi zitakazo shiriki kutoa huduma siku hiyo ni pamoja na Tasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, Hospitali ya Saratani ya Ocean Road,Hospitali ya Sanitas,CCP Medicine Kinyerezi na Mfuko w Bima ya Afya (NHIF), Chama cha madaktari wa meno Tanzaniana tasisi ya wagonjwa wa mifupa MOI.

Abel ametoa wito kwa wahariri wa vyombo vya habar, waandishi wa habari , Bloggersna maofisa mawasiliano Serikalini, mashirika binafsi na tasisi za kimataifa kujitokeza kwa wingi katika bonanza hilo.

MAKAMU WA RAIS AFUNGUA MKUTANO WA MAZINGIRA JIJINI MWANZA

0
0

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Wadau wa Mazingira Wanasayansi na Watafiti wa Bonde la Ziwa Victoria uliofanyika kwenye Hoteli ya Malaika jijini Mwanza (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Wadau wa Mazingira Wanasayansi na Watafiti wa Bonde la Ziwa Victoria uliofanyika kwenye Hoteli ya Malaika jijini Mwanza (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

. Sehemu ya watu waliohudhuria wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Wadau wa Mazingira Wanasayansi na Watafiti wa Bonde la Ziwa Victoria uliofanyika kwenye Hoteli ya Malaika jijini Mwanza (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akitafakari jambo kabla ya kuanza kwa ufunguzi wa Mkutano wa Wadau wa Mazingira Wanasayansi na Watafiti wa Bonde la Ziwa Victoria uliofanyika kwenye Hoteli ya Malaika jijini Mwanza.
\
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na (kushoto) Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,Balozi Augustine Mahiga pamoja na (kulia),Waziri wa Maji na Umwagiliaji ,Injinia wakiwa wamesoma kwa pamoja kabla ya kuanza kwa ufunguzi wa Mkutano wa Wadau wa Mazingira Wanasayansi na Watafiti wa Bonde la Ziwa Victoria uliofanyika kwenye Hoteli ya Malaika jijini Mwanza (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,Balozi Augustine Mahiza akizungumza jambo wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Wadau wa Mazingira Wanasayansi na Watafiti wa Bonde la Ziwa Victoria uliofanyika kwenye Hoteli ya Malaika jijini Mwanza (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).

Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akitazama moja ya bidhaa iliyotengenezwa na wajasiliamali ndani ya jiji la Mwanza,alipokuwa akitembelea mabanda mbalimbali ya Wajasiliamali muda mfupi kabla ya kufungua mkutano. 
 Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mkurugenzi wa Habari Mawasiliano na Uenezi ( NEMC)Dr. Vedast Makota alipotembelea banda la Baraza la Mazingira muda mfupi kabla ya kufungua mkutano. 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amewataka wanasayansi, watafiti na wadau wa mazingira katika Jumuiya ya Afrika Mashariki kuibua mbinu mpya zitakazosaidia kukabiliana na changamoto zinazolikabili bonde la Ziwa Victoria ikiwemo uchafu wa ziwa hilo unaotokana na shughuli za kibinadamu.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo leo 15-Feb-2017 wakati anafungua mkutano wa siku Mbili unaojuisha wadau wa mazingira, wasayansi na watafiti wa bonde la Ziwa Victoria Jijini Mwanza.

Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amesema anaimani kubwa kuwa mkutano huo utakuwa ni chachu katika kuibua mbinu mpya na bora za kukabiliana na uharibifu wa mazingira unaoendelea katika Bonde la Ziwa Victoria.

Amehimiza kuwa kutokana na muhimu wa bonde hilo ni vyema wadau wote katika Jumuiya ya Afrika Mashariki kujumuika pamoja katika kulinda na kuendeleza uhifadhi wa bonde hilo kwa ajili ya manufaa ya wananchi wa jumuiya hiyo.

Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amesema bonde la Ziwa Victoria bado linakabiliwa na changamoto nyingi hasa kuibuka tena kwa magugumaji ambayo yameathiri shughuli za uvuvi, usafiri na kuchafua maji katika Ziwa hilo hivyo ni muhimu kwa makundi yote wakiwemo wanasayansi na watafiti kuweka mikakati mipya ya kukabiliana na changamoto hizo ambazo ni tishio kwa uhai wa Ziwa Victoria.

“Kufanya Maamuzi kwa kuzingatia ushauri wa kisayansi ni jambo zuri na la msingi katika kutunga sera ambazo zitasaidia kwa kiasi kikubwa kulinda na kuhifadhi Bonde la Ziwa Victoria kwa ajili ya manufaa ya wananchi wote”amesisitiza Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan.

Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amesisitiza anaimani kubwa kuwa majadiliano yatakayofanyika katika mkutano huo yatakuja na mbinu mpya ambazo zitatumika katika kuhifadhi na kuendelea Bonde la Ziwa Victoria.

Katika Mkutano huo wa siku Mbili unaofanyika Jijini Mwanza jumla ya mada 44 zitawasilishwa na kujadiliwa kwa kina na wadau wa mazingira, wanasayansi na watafiti.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan pia alitembelea mabanda mbalimbali ya maonyesho katika viwanja vya hoteli ya Malaika uliyopo Jijini Mwanza.

Imetolewa na
Ofisi ya Makamu wa Rais
Mwanza
15-Feb-2017

PROFESA MBARAWA ATETA NA BALOZI WA UINGEREZA HAPA NCHINI

0
0
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (Kulia), akipokea taarifa ya upembuzi yakinifu kuhusu uwekezaji katika miundombinu ya Madaraja kutoka kwa Bw. Lord Clire Hollich (Kushoto) wa Ubalozi wa Uingereza.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (Kulia), akipokea taarifa ya upembuzi yakinifu kuhusu uwekezaji katika miundombinu ya Madaraja kutoka kwa Bw. Lord Clire Hollich (Kushoto) wa Ubalozi wa Uingereza, katikati ni Balozi wa Uingereza hapa Nchini Sarah Cooke.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (Kulia) akijadiliana jambo na Balozi wa Uingereza hapa Nchini Sarah Cooke (Kushoto), walipokutana Jijini Dar es Salaam leo hii. Katikati ni Bw. Lord Clire Hollich.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (Kulia) akisisitiza jambo kwa Balozi wa Uingereza hapa Nchini Sarah Cooke (Kushoto), walipokutana Jijini Dar es Salaam leo. Katikati ni Bw. Lord Clire Hollich.

AfDB YAAHIDI KUENDELEA KUSHIRIKIANA NA TANZANIA KIMAENDELEO

0
0

Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) (kulia), akipeana mkono na Makamu wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), anayeshughulikia masuala ya Nishati na Mabadiliko ya Tabianchi, Bw. Amadou Hott, (kushoto) baada ya kumalizika kwa mkutano kati yao kuhusu ahadi zilizotolewa na Benki hiyo katika kuchangia maendeleo ya Tanzania kwa njia ya ruzuku na mikopo yenye masharti nafuu, katika ukumbi wa Wizara hiyo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) (kulia), akiwa kwenye mkutano na Makamu wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), anayeshughulikia masuala ya Nishati na Mabadiliko ya Tabia nchi, Bw. Amadou Hott (kushoto), ambapo Tanzania na AfdB, zimekubaliana kuendelea kushirikiana katika Nyanja mbalimbali za kiuchumi na hifadhi ya mazingira ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi, Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es Salaam.
Wajumbe wa mkutano wa kujadili ahadi zilizotolewa na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), kutoka Benki hiyo na Tanzania wakifuatilia maelezo kutoka kwa Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), (hayupo pichani) kuhusu umuhimu wa AfDB, katika utekelezaji wa miradi mbalimbali nchini. Mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Wizara hiyo jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Khamis Shaaban (kulia), Kamishna wa Fedha za Nje wa Wizara hiyo Bw. John Rubuga (katikati) na Afisa Mwandamizi wa Wizara Bw. John Mavura wakifuatilia mjadala kuhusu ahadi zilizotolewa na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), katika kufanikisha maendeleo ya Tanzania, katika ukumbi wa Wizara hiyo Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), akielezea kuhusu utekelezaji wa miradi ya nishati nchini alipokuwa katika kikao na Makamu wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), anayeshughulikia masuala ya Nishati na Mabadiliko ya Tabia nchi, Bw. Amadou Hott, katika ukumbi wa Wizara hiyo jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), anayeshughulikia masuala ya Nishati na Mabadiliko ya Tabia nchi, Bw. Amadou Hott, akifafanua jambo katika mkutano kati yake na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), katika ukumbi wa Wizara hiyo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (Mb), (Katikati) akiwa katika mkutano na ujumbe wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), ukiongozwa na Makamu wa Rais wa Benki hiyo anaye husika na masuala ya Nishati na Mabadiliko ya Tabia Nchi, Bw. Amadou Hott, na Ujumbe kutoka Tanzania, ambapo masuala kadhaa kuhusu uchumi, Nishati, Kilimo, Teknolojia jadidifu, yamezungumzwa ili kukuza uchumi wa nchi, Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) na Makamu wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), anayeshughulikia masuala ya Nishati na Mabadiliko ya Tabia nchi, Bw. Amadou Hott, wakiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wengine baada ya kumalizika kwa mkutano kuhusu ahadi zilizotolewa na Benki hiyo juu ya maendeleo ya Tanzania katika ukumbi wa Wizara hiyo jijini Dar es Salaam.




Makamu wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), anayeshughulikia masuala ya Nishati na Mabadiliko ya Tabianchi, Bw. Amadou Hott (kulia), akiwasili Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango kuonana na mwenyeji wake Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) jijini Dar es Salaam.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-WFM)

Tanzania Kushiriki Mashinda ya Mbio za Baskeri Nchini Afrika ya Kusini

0
0
Na: Lilian Lundo – MAELEZO

Washiriki watatu wa Tamasha la Majimaji Selebuka lililofanyika mkoani Ruvuma wanatarajia kushiriki mashindano ya Mbio za Baiskeli nchini Afrika Kusini Februari 19, 2017.

Hayo yamebainishwa leo na Muandaaji Mkuu wa Majimaji Selebuka Reinafrida Rwezaura wakati wa makabidhiano ya tiketi za ndege za kwenda Afrika Kusini kwa washindi hao yaliyofanyika katika ukumbi wa Idara ya Habari – MAEELEZO jijini Dar es Salaam.

“Kikubwa kilichotukutanisha hapa leo ni kuwaaga washindi wa Mbio za Baiskeli katika tamasha la Majimaji Selebuka 2016, zilizofanyika tarehe 04 Juni 2016 kutoka Mbinga hadi Songea umbali wa kilomita 100, ambao wanatakiwa kwenda kushiriki mashindano ya Mbio za Baiskeli Jijini, Johanesburg, Afrika Kusini,” alifafanua Rwezaura.

Rwezaura aliwataja washindi hao wanaotegemea kwenda Afrika Kusini kuwa ni Salum Miraji ambaye alikuwa mshindi wa kwanza , Allen Nyanginywa ambaye alikuwa mshindi wa pili na Ipyana Mbogela ambaye alikuwa mshindi wa tatu.

Kwa upande wake, mshiriki wa mashindano hayo Allen Nyanginywa ameishukuru Taasisi ya Songea Mississippi (SO-MI) kwa kuandaa mashindano hayo pamoja na kutimiza ahadi ya kuwasafirisha washindi wa kwanza hadi wa tatu kwenda nchini Afrika Kusini.

Aliendelea kwa kusema kuwa watahakikisha wanachukua ushindi nchini Afrika Kusini kwani huko wanaenda kufanya kazi na wamefanya mashindano hayo ya Baiskeli imekuwa ni kazi yao.

Majimaji Selebuka ni tamasha linalofanyika kila mwaka mjini Songea, mkoani Ruvuma ambalo huandaliwa na Taasisi ya Songea Mississippi (SO-Mi) ambapo kwa mwaka huu 2017 tamasha hilo linatarajia kufanyika kunzia Julai 23 hadi 30, 2017.

MKUU WA CHUO CHA ULINZI KUNDUCHI AZURU KENYA

0
0
Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi kilichoko Kunduchi Dar Es Salaam, Kanali Yacub Mohamed, yuko nchini Kenya kwa ziara ya kikazi.
Kanali Mohamed amesema atatembelea Chuo cha Taifa cha Ulinzi cha Kenya kuona miundombinu yake na kubadilishana uzoefu na wakuu wa chuo hicho kilichopo Karen katika viunga vya jiji la Nairobi.

Mkuu huyo wa Chuo ametembelea Ubalozi wa Tanzania Nairobi na kuonana na Kaimu Balozi, Bi. Talha Mohamed Waziri. Lengo kubwa la ziara yake ni kubadilishana uzoefu na Chuo cha Kenya kuhusu uendeshaji na uandaaji wa mitaala.
Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Bi Talha Waziri (Kulia) akifurahia zaidi aliyokabidhiwa na Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi, Kanali Yacub Mohamed (wa pili kushoto). Kushoto ni Mshauri wa Kijeshi wa Ubalozi wa Tanzania, Kanali Fabian Machemba.
Kanali Mohamed na Kaimu Balozi (Katikati) wakiwa kwenye picha ya pamoja. Wa pili kulia ni Mshauri wa Kijeshi Kanali Machema na kulia ni Kanali Maulid Surumbu kutoka Chuo cha Ulinzi. Kushoto ni Kanali Njoroge wa Jeshi la Ulinzi la Kenya.

TAKUKURU YAWABURUZA MAHAKAMANI WATUMISHI WA WIZARA YA ELIMU MANISPAA YA ILALA

0
0


Na Karama Kenyunko

Watumishi wanne wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi akiwemo Mkurugenzi na Mhasibu wamepandishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka saba ya kiwemo ya ubadhilifu na ufujaji wa fedha na kuisababishia wizara hasara ya zaidi ya Milioni 41.2

Akisoma hati ya mashtaka, Mwendesha Mashtaka, wakili wa serikali kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (PCCB), Emmanuel Jacob aliwataja washtakiwa hao kuwa ni Mkurugenzi Bakari Issa, Mhasibu Emmanuel Mayuma, Mkurugenzi Msaidizi Hellen Lihawa na Mhasibu Msaidizi Mbarouk Dachi.

Mbele ya Hakimu Mkazi, Wilbard Mashauri ilidaiwa kuwa washtakiwa hao kwa makusudi na kwa nia ya kudanganya walitumia malipo ya tarehe 16 Julai 2014 kwa jina la Emanuel Mayuma ambayo ilikuwa na taarifa ya uongo kuonyesha kuwa zaidi ya sh. Milioni 18.4 zilikuwa ni malipo kwa ajili wanafunzi waliohudhuria mafunzo ya michezo yaliyokuwa yamedhaminiwa na British Council huku wakijua siyo kweli.

Aidha watumishi hao wanadaiwa kufanya ubadhirifu na ufujaji wa fedha kati ya Agosti 30 na Septemba 10 mwaka 2014 na kujipatia kiasi hicho cha milioni 18 ambazo zilikuwa ni kwa ajili ya mpango wa walimu kwa mafunzo ya kadi za michezo zilizofadhiliwa na British Council.

Mhasibu Mayuma anadaiwa peke yake kuwa, kati ya Agosti 10 na Septemba 2014 wizarani hapo alitumia vibaya kiasi cha shilingi milioni 31.7 alizokuwa amekabidhiwa kwa ajili ya kugaramia mpango wa matumizi ya kadi za michezo.

Katika hatua nyingine watuhumiwa hao wote wanadaiwa kushindwa kutumia madaraka yao vibaya na kuisababisha wizara ya Elimu hasara zaidi ya shilingi milioni 18.4/- wakati Mhasibu Mayuma aliisababishia wizara hiyo hasara ya shilingi milioni 41.2.

Hata hivyo washtakiwa wamekana mashtaka na wako nje baada ya kuweka dhamana ya shilingi milioni 50 kila mmoja na kuleta wadhamini wawili wa uhakika. Aidha washtakiwa hao hawaruhusiwi kusafiri nje ya Dar es Salaam bila kupata kibali cha mahakama.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Machi 1, upelelezi bado haujakamilika.


Watuhumiwa wa ubadhilifu wa fedha wakifikishwa katika mahakama ya Hakimu mkazi kisutu jijini Dar es Salaam
 

SERIKALI YA JAPAN YAISAIDIA TANZANIA DOLA 80,234 KUENDELEZA MCHEZO WA BASEBALL

0
0
Mwenyekiti wa Chama cha Baseball Tanzania (TaBSA), Dkt. Ahmed Makata (aliyekaa kushoto mbele) akisaini Mkataba wa Ujenzi wa Uwanja wa Baseball, kulia ni Balozi wa Japan nchini Tanzania, Mhe. Masaharu Yoshida.Wanaoshuhudia nyuma ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye pamoja na Mjumbe toka Japan.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye (aliyesimama mbele) akiongea na Wageni waalikwa pamoja na Waandishi wa habari wakati wa hafla ya utiaji saini Mkataba wa Ujenzi wa kiwanja cha Baseball nchini kati ya Serikali ya Tanzania na Japan leo 15 Februari, 2017 Jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Japan nchini Tanzania, Mhe. Masaharu Yoshida (aliyesimama mbele kulia) akiongea na Wageni waalikwa pamoja na Waandishi wa habari wakati wa hafla ya utiaji saini Mkataba wa Ujenzi wa kiwanja cha Baseball nchini kati ya Serikali ya Tanzania na Japan leo 15 Februari, 2017 Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye akiwa katika picha ya pamoja na Wachezaji wa mchezo wa Baseball mara baada ya hafla ya utiaji saini Mkataba wa Ujenzi wa kiwanja cha Baseball nchini kati ya Serikali ya Tanzania na Japan leo 15 Februari, 2017 Jijini Dar es Salaam.

WAZIRI MKUU MAJALIWA AANZA ZIARA WILAYANI KITETO

0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewaagiza Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, Eng. Tumaini Magesa na Mkurugenzi wa Halmsahuri ya wilaya hiyo, Bw. Tamim Kambona waende kata ya Engusero Jumamosi wiki hii wakafanye mkutano wa hadhara na kujibu kero za wananchi wa kata hiyo.

Mkuu wa Wilaya hiyo na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo wametakiwa pia wafuatane na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Bw. Lairumbe Mollel wakatoe ufafanuzi bila kukosa.

Ametoa agizo hilo leo (Jumatano, Februari 15, 2017) katika kijiji cha Engusero wilayani kiteto baada ya kusimamishwa na wananchi wakati akiwa njiani kuelekea mjini Kibaya yalipo makao makuu ya wilaya hiyo ili aanze ziara ya kikazi ya mkoa wa Manyara.

Akijibu baadhi ya maswali aliyoulizwa na wananchi wa kijiji cha Engusero, Waziri Mkuu amesema analichukua ombi la wakazi hao la kupata kujengewa soko la kimataifa katika kata hiyo ili waweze kuuza mahindi hapo hapo.

“Nitaawagiza Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi wa Halmashauri waje hapa Jumamosi hii na kufanya mkutano ili wawaeleze wana mpango gani kuhusiana na ujenzi wa soko hilo,” amesema.

Awali , Mkazi wa kata hiyo Bw. Ali Athumani alimuomba Waziri Mkuu awasiaidie ili wajengewe soko la kimataifa kwa sababu wao ni wazlishaji wakubwa wa mahindi lakini hawafaidiki nayo kwa sababu yote yanaenda kuuzwa katika soko la Kibaigwa.

Naye Bw. Said Shabani alimuomba Waaziri Mkuu awasaidie kufuatilia upatikanaji wa gari la wagonjwa na ujenzi wa wodi nyingine ya wagonjwa pamoja na chumba cha kuhifadhia maiti kwenye zahanati yao.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amesema Serikali imeweka nia ya dhati ya kupambana na dawa za kulevya na amewataka watendaji wote kuanzia ngazi ya vijiji wadhibiti suala hilo.

“Serikali haiwezi kuona vijana wanaangamia kwa dawa za kulevya. Tumeamua kudhibiti hali hiyo. Hii vita ni ya nchi nzima. Kuanzia sasa, viongozi wa Serikali za vijiji wakamateni wale wote wanaojihusisha na biashara hii.”

“Tunataka vijiji vyetu, kata zetu, wilaya zetu na mikoa yetu iwe safi bila hata chembe ya dawa za kulevya. Tukikuona kijana unayumbayumba au kuweweseka, tunakupima na tukikuta umetumia ile kitu, tunakukamata ili utuambie ni nani amekupa,” amesema na kuongea:

“Sisi tunataka vijana wafanye kazi za kujiletea maendeleo. Kijana hawezi kuwa na maendeleo wakati hufanyi kazi, huwezi kuwa na ndoto za maendeleo wakati umelewa bangi au dawa za kulevya. Kila mmoja afanye kazi kwa ajili ya maendeleo ya nchi yetu,” amesisitiza.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi wa kijiji cha Engusero wilayani Kiteto waliofunga barabara wakitaka asimame kuwasalimia. Alikuwa kitoka Dodoma kwenda Kiteto kwa ziara ya kazi mkoani Manyara Februari 15, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akivalishwa skafu baada ya kuwasili mjini Kibaya kuanza ziara ya kazi wilayani Kiteto Februari 15, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Katibu Tawala wa mkoa wa Manyara, Eliakim Maswi baada ya kuwasili mjini Kibaya kuanza ziara ya wilaya ya Kiteto Februari 15, 2017.

Wizara yapokea mrejesho wa mradi wa afya ya uzazi wa Thamini Uhai na namna inavyoongeza matumizi ya vituo vya afya na kuokoa maisha

0
0

Wadau kutoka shirika la Thamini Uhai, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na Ofisi ya Rais - Tawala za Mkoa na Serikali za Mitaa wakimsikiliza kwa makini Waziri Ummy Mwalimu wakati wa mkutano wa mrejesho wa shirika la Thamini Uhai, leo jijini Dar-es-Salaam

 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto - Mh Ummy Mwalimu (katikati) na Dr Hussein Kidanto - kaimu mkurugenzi wa idara ya huduma za kinga Wizara ya Afya (kushoto) wakishauriana  na Mkurugenzi mtendaji wa Thamini Uhai, Dr Nguke Mwakatundu (Kulia) wakati wa mkutano wa mrejesho wa shirika la Thamini Uhai, leo jijini Dar-es-Salaam


Wadau kutoka shirika la Thamini Uhai, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na Ofisi ya Rais - Tawala za Mkoa na Serikali za Mitaa wakishauriana wakati wa mkutano wa mrejesho wa shirika la Thamini Uhai, leo jijini Dar-es-Salaam
 

Tokea 2008, Thamini Uhai imesaidia vituo vya huduma za afya 19 na zahanati 18 katika mikoa mitatu, na hivyo kujenga mfumo utakaokuwa mfano bora na inayoweza kutumika kokote nchini kuokoa maisha ya akina mama na watoto wachanga.

(Februari 15, 2017, Dar es Salaam, Tanzania)– Leo jijini Dar-es-Salaam, Thamini Uhai imetoa mrejesho wa shughuli zake tokea kuanzishwa kwake na kuwasilisha mipango yake kwa mwaka 2017 kwa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto pamoja na Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa.

Thamini Uhai (iliyoitwa World Lung Foundation hapo awali), imefanya kazi kwa karibu na wahisani pamoja na serikali za mikoa, kujenga mfumo ambao umepelekea ugatuzi wa huduma za dharura za kuokoa maisha ya mama na watoto wachanga kutoka hospitali kwenda kwenye vituo vya afya. Mfumo huu wa kipekee wa huduma ya afya umehusisha pia kuboresha vituo vya huduma za afya ili viweze kutoa huduma hizi za dharura, kuendeleza mafunzo ya jamii kupitia vyombo vya habari na waelimishaji jamii ili kuhamasisha jamii itumie vituo vya huduma za afya, kuboresha mifumo ya rufaa, kuhakikisha upatikanaji wa ushauri wa afya kila wakati. Pia shirika imetoa mafunzo, usimamizi na elimu endelevu kwa wahudumu wa afya, waganga wasaidizi (AMO) na manesi ambapo elimu hiyo inatolewa na madaktari bingwa ili kugatua huduma na ujuzi na hivyo kuongeza uwezo katika jamii zilizopo pemebezoni.

Akizungumzia mafanikio yao, Dr. Nguke Mwakatundu, Mkurugenzi Mtendaji wa Thamini Uhai,  amesema:
“Moja ya mafanikio yetu muhimu ni jinsi shughuli zetu zimeweza kuleta mabadiliko katika maisha ya wagonjwa katika nyanja zinayotuhusu. Tumeona vifo vya uzazi na rufaa zikipungua kwa kiasi kikubwa na kwa njia endelevu katika maeneo haya, pamoja na kuona ongezeko la maana katika idadi ya wanawake wanaoamua kujifungua katika vituo vya huduma za afya.”


Akitilia mkazo baadhi ya changamoto, Dr. Mwakatundu ameeleza kuwa ili mafanikio haya yawe endelevu kuna haja ya kupanga rasilimali za kutosha kwa ajili ya wafanyakazi wa afya na kuboresha mfumo wa usamabazaji wa vifaa na madawa.


Waziri wa Afya, Mh, Ummy Mwalimu akitoa mchango wake kuhusu kazi za Thamini Uhai, amesema: “Ningependa kutambua mchango wenu katika kuhakikisha akina mama wanajifungua kwa usalama katika mikoa husika. Naelewa kuwa mmefanya kazi kubwa kuboresha mifumo ya huduma za dharura katika vituo vya afya na hospitali, mmeanzisha kampeni za mawasiliano na kuimarisha mifumo ya rufaa kutoka vituo vya afya kwenda hospitali.”

Thamini Uhai imekwisha kabidhi serikalini shughuli zake za mradi wa afya ya uzazi katika mikoa miwili – Morogoro na Pwani, na imepanga mwaka 2017 kuanza utaratibu wa kukabidhi shughuli zake katika mkoa wa Kigoma.


# # #
Kuhusu Thamini Uhai
Tangu mwaka 2008, Thamini Uhai (zamani iliyojulikana kama World Lung Foundation Tanzania) imefanya kazi ili kusaidia kupunguza vifo vya wajawazito na watoto wachanga na kuboresha upatikanaji wa huduma bora za uzazi wa dharura (CEmONC) katika jamii, hasa katika maeneo ya vijijini na sehemu zilizo pembezoni ambapo wagonjwa awali walikuwa wanasafiri masaa tatu au nne kwenda hospitali ya karibu. Mpango mkakati wetu ni kusaidia mawasiliano bunifu na kampeni za  jamii ili kuongeza matumizi ya vituo vya afya na uzazi wa mpango; kuboresha miundombinu; na kutoa mafunzo na kusaidia kliniki zisizo na daktari kutoa huduma ya uzazi wa dharura. Kwa mikoa Kigoma, Morogoro, na Pwani:

       Thamini Uhai imeboresha kikamilifu, kukarabati au kujenga upya vituo vya afya 15 vijijini na hospitali za wilaya na inasaidia vituo 5 zaidi. Pia inasaidia zahanati 18 katika maeneo ya vyanzo vya maji, kuboresha upatikanaji wa mahudhurio ya uzalishaji wenye ujuzi kwa ubora wa juu na huduma za uzazi wa dharura na watoto wachanga.
       Zaidi ya wasaidizi 100, waganga wasaidizi, nesi-wakunga, na maafisa wa kliniki wamepata mafunzo ya kina kuhusu huduma ya uzazi wa dharura au nusu kaputi.
       Matumizi ya kituo cha afya kwa ajili ya uzalishaji yameongezeka kwa kiasi kikubwa kutoka wanawake 21,661 waliojifungua katika vituo vinavyoungwa mkono mwaka 2011, hadi wanawake 26,189 waliojifungua mwaka 2015.

Mpango huu umepokea msaada wa kifedha kutoka Bloomberg Philanthropies, Blue Lantern, Fondation H & B Agerup, na Svenska Postkod Stiftelsen na Thamini Uhai ni mshirika wa Vital Strategies.
Kwa maelezo zaidi tembelea tovuti:www.thaminiuhai.or.tzor Twitter @ThaminiUhai, or Facebook https://www.facebook.com/ThaminiUhai/


Kuhusu Vital Strategies
Vital Strategies ni shirika la kimataifa linalojishughulisha na masuala ya afya na linalenga kusaidia kuongeza kasi ya maendeleo katika kupambana na magonjwa yenye athari kubwa duniani.
Timu yetu inatumia mikakati iliyojikita katika ushahidi  na uvumbuzi ili kubuni na kutekeleza sera nzuri za afya ya umma, kusimamia mipango kwa ufanisi, kuimarisha mifumo ya data, kufanya utafiti, na kubuni kampeni ya kimkakati ya mawasiliano kwa ajili ya sera na mabadiliko ya tabia.
Kwa taarifa zaidi au kupanga mahojiano na mtaalam wa afya ya jamii au afya ya uzazi kutoka Vital Strategies, tafadhali wasiliana naTracey Johnston, Vital Strategies, at +44.7889.081.170 au tjohnston@vitalstrategies.org

ACACIA, UDSM INKS MOU TO IMPROVE ENGINEERING INDUSTRY IN THE COUNTRY

0
0

Vice Chancellor of the University of Dar es Salaam, Professor Rwekaza Mukandala, (L), and Deo Mwanyika, (R) , who is Acacia Vice President (Corporate Affairs), exchange documents after they had signed at the University’s Mlimani campus in Dar es Salaam late on Tuesday. The University of Dar es Salaam (UDSM) has signed a renewed Memorandum of Understanding (MoU) with Acacia Mining that would support 52 students and staff in various areas hence to improve quality of engineering sector. Right is Acacia's Chief Advisor, Learning and Training, Jannet Reuben Lekashingo, and UDSM's Acting Secretary to Council and Corporate Counsel who is also, the Intellectual Property Manager,
Dr. Saudin Mwakaje.
 K-VIS BLOG/Khalfan Said


THE University of Dar es Salaam (UDSM) has signed  a renewed Memorandum of Understanding (MoU) with Acacia Mining that would support 52 students  and staff in various areas hence improve quality of engineering sector .

Speaking shortly before signing of the MoU on Tuesday in Dar es Salaam , Deo Mwanyika , who is Acacia Vice President (Corporate Affairs) , said  there are a number of aspects that the company and University are partnering.

He mentioned some of aspects as a two year practical work experience for 2nd  and 3rd year students, funding for university laboratory equipment, sponsorship of postgraduate  mining/mineral process engineering students and bursary for six students.
He said the two year practical work experience for the mentioned students  in the chemical  and Mining engineering department  in various fields of significance to Tanzania’s development agenda in relation to the mining sector.
Mwanyika congratulated the first 52 students  who will be part of the program  and asked them to apply the knowledge and experience gained from practical training for the development of Tanzania.
Further more, he said Acacia  is committing more than 22m/- finances for purchase  of laboratory equipment, student site visit  and practical experience  at its mine sites and helps supervise final year students on their project works.
“This support , exposure and experience are critical  to our students the future professional workforce  of our country Acacia creates  that solid foundation one needs for their career ahead”, he said.
Under the two year signed Mou, he said the company has for the new study year allocated 6 scholarship for students at CoET.
Mwanyika noted that education is an important factor  for economic development , but most students are  not in a position to pay for their tertiary education due to lack of funds.
“As Tanzania’s leader in the mining sector , the firm  is committed  to further increase its investment in higher education ,” he assured.
He urged students at UDSM and other institutions  of higher learning in Tanzania to  realize that they are  honored a lot , having access to education that is distant dream to many others in the country.
“Whoever will be beneficiary of the next two years Acacia internship and  scholarship programs you have a responsibility to give back to our community  and county imparting the knowledge you have gained,” he said.
The  firm has run the scholarship program with UDSM since 2009 ,  which supported top  undergraduate students  and offered scholarships to  academic staffs to pursue postgraduate studies
Speaking earlier , the Principal of College of Engineering and Technology (CoET) Prof Ignas  Rubaratuka, said the support from Acacia has focused in practical training, industrial oriented students projects  and provision of engineering and design and modeling software.
He said the University through the CoET has always been seeking to forge productive and constructive partnership with the industry for the mutual benefits of all
He said the collaboration between UDSM and Acacia Mining has been an exemplary  partnership that they are proud of and need to be consolidated in order to continue training mining  engineers.
“This is huge obligation that if left alone, without support of the industry  like Acacia, we can hardly make meaningful contribution as it is understood all over the world that training of engineers is an expensive though necessary undertaking”, he said.
He added that, there fore most of time , universities are obliged  to seek partnerships with industry and tend to orient their training to solve problems of the industry so as to attract the industry to fund their activities which eventually benefit the industry.
Explaining further he said some of the graduates from mining programs have secured employment in various  countries namely Australia, South Sudan, Mali, Ghana, South America and South Africa.
He noted that one of the objectives of the MoU that has not been fully realized to the satisfaction of both sides is the component of  staff training.
Like any other organization, the University is constantly  striving to train younger staff as part of its succession plan.
“You will agree with me that the quality of the graduates will depend  partly on the quality of instructors that the University engages, we are committed to this and any funds set aside for training will be used only for this purpose,” he concluded.

Vice Chancellor of the University of Dar es Salaam, Professor Rwekaza Mukandala, (L), and Deo Mwanyika , who is Acacia Vice President (Corporate Affairs), sing the renewed Memorandum of Understanding (MoU) under which Acacia Mining will support 52 students  and staff in various areas hence to improve quality of engineering sector. The signing ceremony was held late on Tuesday at the University’s Mlimani Campus in Dar es Salaam
 Displaying the documents
 Deo Mwanyika delivers his message

Principal College of Engineering and Technology (coet), of the University of Dar es Salaam, Professor Ignas A. Rubaratuka gives his remarks

 Senior Officials of Acacia Mining, left is Buzwagi Gold Mine's General Manager, Asa Mwaipopo, and Acacia's Chief Advisor, (Government Relations), Alex Lugendo
 Acacia staff in attendance
 Exchanging ideas after the evenet, Professor Mukandala right and Deo Mwanyika
 Professor Mukandala, (L),  with Acacia's General Manager (Buzwagi Gold Mine), Asa Mwaipopo

UDSM’s Lecturer In the Department of Political Science and Public Administration, Dr. Bashiru Ally, (R), exchanges ideas with Acacia’s Vice President (Corporate Affairs), Deo Mwanyika

 Acacia's Chief Advisor, (Government Relations), Alex Lugendo, (L), with the firm's Chief Advisor, Learning and Training, Jannet Reuben Lekashingo
 Professor Rwekaza Mukandala, (R), UDSM's Vice Chancellor, listens to Acacia's Chief Advisor (Public Relations), Necta Pendaeli Foya
Group photo

ANNA ABDALLAH APONGEZWA KUWA MWENYEKITI WA BODI YA WADHAMINI YA TGGA

0
0
 Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Wadhamini ya Tanzania Girl Guids Association (TGGA), Anna Abdallah (kushoto), akipongezwa na Kamishna  Mkuu wa TGGA,  Symphorosa Hangi  (kulia) na Mwenyekiti wa Taifa wa TGGA, Profesa Martha Qorro baada ya kuchaguliwa Dar es Salaam jana. (PICHA ZOTE NA  NA RICHARD MWAIKENDAKAMANDA WA MATUKIO BLOG)
 Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Wadhamini ya Tanzania Girl Guids Association (TGGA), Anna Abdallah (kushoto),Kamishna  Mkuu wa TGGA,  Symphorosa Hangi  (kulia) na  Mwenyekiti wa Taifa wa TGGA, Profesa Martha Qorro  wakipiga makofi wakati wa mkutano huo wa kumtambulisha Anna. 
 Mwenyekiti mpya wa Bodi ya  Wadhamini ya Tanzania Girl Guids Association (TGGA), Anna Abdallah (kushoto), akipongezwa na Mjumbe wa Bodi hiyo, Zakia Meghji.
 Katibu wa Taifa wa TGGA, Grace Shaba (kulia) akimpongeza Anna Abdallah
 Mary akimpongeza Anna Abdallah
 Wakiwa na furaha kutoka kushoto ni Grace Makenya, Anna Abdalah, Profesa Martha Qorro na Hangi






 Baadhi ya Girl Guids wakiwa katika picha ya pamoja

KAMPUNI YA RED SEA YA KEKO JIJINI DAR ES SALAAM YAPEWA MWEZI MMOJA KUBOMOA UKUTA ULIOJENGWA JUU YA MTARO WA MAJI MACHAFU NA KUSABABISHA USUMBUFU KWA WANANCHI

0
0

NA Evelyn Mkokoi- Dar Es Salaam

Kampuni ijulikanayo kwa jina moja la Red Sea iliyopo katika Mtaa wa mafuta Keko Gerezaji jijini Dar Es Salaam, Imepewa mwezi mmoja wa kutakiwa kubomoa ukuta uliojengwa juu ya Mtaro wa maji machafu ambao pia ni eneo chepechepe, na kusababisha usumbufu kwa wakazi wa maeneo hayo na hatari ya kupata magonjwa hasa katika kipindi cha mvua.

Akifuatila utekelezaji wa Maagizo ya ziara yake aliyoifanya tarehe 20 mwezi wa December mwaka jana, Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina, amesema kuwa ujenzi huo holela, umekiuka sheria ya mazingira ya mwaka 2004 na kanuni zake na kumtaka mmiliki wa kampuni hiyo kubomoa ukuta huo ndani ya siku thelathini na kinyume na hapo serikali kupitia halmashauri ya wilaya ya Temeke na NEMC itabomoa ukuta ukuta huo kwa gharama za mmiliki wa kampuni hiyo.

Aidha, Naibu Waziri Mpina Ameitaka NEMC pamoja na Manispaa ya Temeke kuwasilisha kwake ndani ya siku tatu vibali vilivyomruhusu mmiliki mwingine wa kampuni ya KOBIL kujenga juu ya mtaro huo, kinyume na hapo hatua nyingine zitachukuliwa.

Kwa Upande wake Mkaguzi wa Wakala wa Barabara nchini TANROADS Bw.Dismas Nyoni, ameeleza kuwa, TANROADS ina mpango wa muda mvupi wa kufanyia usafi mtaro huo ulioziba na kupita chini ya barabara katika eneo la kilwa road, na kuzibua mtaro huo ili kuwapunguzia wananchi usumbufu katika msimu wa mvua zinazokuja.

Wakati huohuo Naibu Waziri Mpina, alitemebelea Gereza la Keko kujionea utekelezaji wa maagizo yake ambapo awali gereza hilo lilikuwa likiririsha maji taka katika maeneo ya makazi na kwa hivi sasa gereza la keko limekamilisha ujenzi wa miundombinu ya maji taka kwa asilimia 80, aliwapongeza na kuwapa muda wa wiki mbili kumalizia marekebisho yaliyobakia, nae Mkazi wa eneo la Keko Gerezani Bi ASha Hussein alisema gereza la keko likikamilisha ujenzi huo wa miundombinu ya maji taka wananchi wataepukana na magonjwa na watoto watacheza vizuri.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina, Akitoa Maelekezo kwa Uongozi wa Baraza la Taifa la Hifadhi na usimamizi wa Mazingira (NEMC) Hamlashauri ya Wilaya Ya Temeke, na TANROADS kuhusu suluhisho la muda na la kudumu la Mfereji wa Mtaa wa Mafuta keko Gerezani Jijini dar Es Salaam, wenye kuleta kero ya kimazingira kwa wakazi wa eneo hilo hususan katika kipindi cha mvua.



Katikati Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina na Uongozi wa Gereza la keko wakati wa Ziara ya Naibu Waziri Mpina ya ufuatiliaji wa utekelezaji wa maagizo yake gerezani keko ya ujenzi wa miundombinu ya majitaka ambayo ni rafiki kwa mazingira.( Picha na Evelyn Mkokoi)
 


SERIKALI YAWAPOKEA WATAALAM SITA WA KUJITOLEA KUTOKA JAPANI WALIOKUJA KUTOA HUDUMA NCHINI

0
0
 Mratibu wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japani (JICA) Bw. Owa Ichiro akizungumza na Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji Rasilimaliwatu, Bi. Roxana Kijazi wa Ofisi ya Rais-Utumishi (hayupo pichani) wakati wa hafla fupi ya kuwakaribisha Wataalam wa kujitolea kutoka Japani waliokuja kutoa huduma nchini, iliyofanyika katika Ukumbi mdogo wa Ofisi ya Rais-Utumishi leo.
 Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji Rasilimaliwatu wa Ofisi ya Rais-Utumishi, Bi. Roxana Kijazi akizungumza na Wataalam wa kujitolea kutoka Japani waliokuja kutoa huduma nchini wakati wa hafla fupi ya kuwakaribisha Wataalam hao iliyofanyika katika Ukumbi mdogo wa Ofisi ya Rais-Utumishi leo.
 Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji Rasilimaliwatu wa Ofisi ya Rais-Utumishi, Bi. Roxana Kijazi akipokea kalenda ya JICA ya mwaka 2017 toka kwa Mratibu wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japani (JICA) Bw. Owa Ichiro wakati wa hafla fupi ya kuwakaribisha Wataalam wa kujitolea kutoka Japani waliokuja kutoa huduma nchini, iliyofanyika katika Ukumbi mdogo wa Ofisi ya Rais-Utumishi leo.
 Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji Rasilimaliwatu wa Ofisi ya Rais-Utumishi, Bi. Roxana Kijazi akipewa maelezo kuhusu kalenda ya JICA ya mwaka 2017 toka kwa Mratibu wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japani (JICA) Bw. Owa Ichiro wakati wa hafla fupi ya kuwakaribisha Wataalam wa kujitolea kutoka Japani waliokuja kutoa huduma nchini, iliyofanyika katika Ukumbi mdogo wa Ofisi ya Rais-Utumishi leo.
Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji wa Rasilimaliwatu wa Ofisi ya Rais-Utumishi, Bi. Roxana Kijazi akiwa katika picha ya pamoja  na Wataalam wa kujitolea kutoka Japani waliokuja kutoa huduma nchini  mara baada ya hafla fupi ya kuwakaribisha Wataalam hao, iliyofanyika katika Ukumbi mdogo wa Ofisi ya Rais-Utumishi leo.  


MAMA MAGUFULI NA MAMA MAJALIWA WAWAOMBA WANANCHI WASAIDIE WATU WASIOJIWEZA

0
0
MKE wa Rais Mheshimiwa Mama Janeth Magufuli na Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wametoa wito kwa Watanzania kujengea utamaduni wa kutembelea vituo vya wazee na watu wenye mahitaji maalumu na kutoa misaada ili waweze kujikimu.

Wameyasema hayo leo (Jumatano, Februari 15, 2017) wakati walipotembelea Makazi ya Wazee wasiojiweza na walemavu watokanao na ugonjwa wa ukoma ya Amani Ipuli yaliyoko kwenye Manispaa ya Tabora mkoni Tabora.
Katika makazi hayo wamekabidhi tani 7.5 za vyakula mbalimbali ukiwemo mchele, unga wa sembe na maharage pamoja na mafuta maalumu kwa ajili ya watoto wenye ulemavu wa ngozi wanaosoma katika shule mbalimbali mkoni Tabora.

Hata hivyo, Mama Janeth amewapongeza watumishi wote wanaofanyakazi kwenye makazi ya kulelea wazee na watu wenye mahitaji maalumu kwa sababu kazi hiyo ni ngumu na ina changamoto nyingi.“Ibada si kwenda katika nyumba za ibada pekee bali hata kuwatembelea wazee, watu wenye mahitaji maalumu na wasiojiweza utakuwa umetoa sadaka kubwa kwa Mwenyezi Mungu. Nawaomba tujitahidi kuwatembelea,” amesema.

Kwa upande wake Mama Mary amewaomba wananchi wote wawe na utaratibu wa kuwasaidia wazee wanaoishi katika makaazi ya kulele wazee, walemavu na wasiojiweza nchini na kuwafariji kwa sababu wanahitaji upendo na faraja kutoka kwao.

Pia Mama Mary ameipongeza Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto pamoja na wadau mbalimbali kwa kujitoa kwa hali mali katika kuwahudumia wazee na watu wenye mahitaji maalumu.Naye Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala amesema Serikali itahakikisha huduma zinaboreshwa katika makazi ya kulelea wazee na watu wenye mahitaji maalumu nchini kwa kuwa vingi viko katika hali mbaya.

Awali Ofisa Ustawi wa Jamii mkoa wa Tabora, Bw. Baraka Makona alisema makazi hayo yalianzishwa mwaka 1969 kwa lengo la kuwasaidia watu wasiojiweza hususan walioathirika na ugonjwa wa ukoma ambao walitengwa na familia zao.

Bw. Makona alisema baada ya ugonjwa wa ukoma kupungua mkoani Tabora kwa sasa makao hayo yanahudumia wazee wasiojiweza wenye ulemavu na ambao wametengwa na jamii kutokana na sababu mbalimbali.

Katika hatua nyingine, Bw. Makona alisema makazi hayo yanakabiliwa na changamoto mbalimbali zikiwemo za uchakavu wa majengo, ukosefu wa gari la wagonjwa hali inayosababisha usumbufu mkubwa hasa inapotokea dharura nyakazi za usiku kwani hakuna zahanati karibu na makazi hayo.

Pia Bw. Makona amewapongeza wake wa viongozi hao kwa moyo wao wa dhati wa kuamua kutembelea makazi hayo na kutoa misaada mbalimbali vikiwemo vyakula kwa sababu wameonyesha matendo ya huruma na Mwenyezi Mungu atawabariki.

Naye Mwenyekiti wa Wazee waishio katika makaazi hayo, Mzee George Busambilo aliwashikuru wake hao wa viongozi kwa niaba ya wenzake na kuwaomba waendelee na moyo huo wa kusaidia watu wasiojiweza na wenye mahitaji maalumu.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli na Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wakiongea na mmoja ya wazee wasiojiweza wanaolelewa katika kituo cha wazee na watu walemavu watokanao na ugonjwa wa ukoma cha Amani Ipuli katika Manispaa ya Tabora mkoani Tabora leo Februari 15, 2017
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli na Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wakiongea na mmoja ya wazee wasiojiweza wanaolelewa katika kituo cha wazee na watu walemavu watokanao na ugonjwa wa ukoma cha Amani Ipuli katika Manispaa ya Tabora mkoani Tabora leo Februari 15, 2017
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli na Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wakiongea na mmoja ya wazee wasiojiweza wanaolelewa katika kituo cha wazee na watu walemavu watokanao na ugonjwa wa ukoma cha Amani Ipuli katika Manispaa ya Tabora mkoani Tabora leo Februari 15, 2017
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli na Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wakilakiwa kwa nderemo walipowasili katika kituo cha wazee na watu walemavu watokanao na ugonjwa wa ukoma cha Amani Ipuli katika Manispaa ya Tabora mkoani Tabora leo Februari 15, 2017
:Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Aggrey Mwanri na Mkuu wa Wilaya ya Tabora Mhe. Queen Mlozi wakati yeye na Mama Mary Majaliwa walipotembelea katika kituo cha wazee na watu walemavu watokanao na ugonjwa wa ukoma cha Amani Ipuli katika Manispaa ya Tabora mkoani Tabora leo Februari 15, 2017
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli na Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wakilakiwa kwa nderemo walipowasili katika kituo cha wazee na watu walemavu watokanao na ugonjwa wa ukoma cha Amani Ipuli katika Manispaa ya Tabora mkoani Tabora leo Februari 15, 2017
Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa akisalimia wananchi na wazee wasiojiweza wanaolelewa katika kituo cha wazee na watu walemavu watokanao na ugonjwa wa ukoma cha Amani Ipuli katika Manispaa ya Tabora mkoani Tabora leo Februari 15, 2017
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akihutubia wananchi pamoja na wazee wasiojiweza wanaolelewa katika kituo cha wazee na watu walemavu watokanao na ugonjwa wa ukoma cha Amani Ipuli katika Manispaa ya Tabora mkoani Tabora leo Februari 15, 2017
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akihutubia wananchi pamoja na wazee wasiojiweza wanaolelewa katika kituo cha wazee na watu walemavu watokanao na ugonjwa wa ukoma cha Amani Ipuli katika Manispaa ya Tabora mkoani Tabora leo Februari 15, 2017




Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli na Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa Pamoja na naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Hamisi Kigwangwalla wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa tabora Mhe. Aggrey Mwanri akianzisha harambe kwa ajili ya wazee wasiojiweza wanaolelewa katika kituo cha wazee na watu walemavu watokanao na ugonjwa wa ukoma cha Amani Ipuli katika Manispaa ya Tabora mkoani Tabora leo Februari 15, 2017
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli na Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wakiwakabidhi mafuta maalumu wawakilishi wa wanafunzi wenye ulemavu wa ngozi walioalikwa kwenye hafla iliyofanyika katika kituo cha wazee na watu walemavu watokanao na ugonjwa wa ukoma cha Amani Ipuli katika Manispaa ya Tabora mkoani Tabora leo Februari 15, 2017
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli na Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wakikabidhi sehemu ya msaada wao wa tani 7.5 ya vyakula katika kituo cha wazee na watu walemavu watokanao na ugonjwa wa ukoma cha Amani Ipuli katika Manispaa ya Tabora mkoani Tabora leo Februari 15, 2017

Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli na Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wakikabidhi sehemu ya msaada wao wa tani 7.5 ya vyakula katika kituo cha wazee na watu walemavu watokanao na ugonjwa wa ukoma cha Amani Ipuli katika Manispaa ya Tabora mkoani Tabora leo Februari 15, 2017
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli na Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wakikabidhi sehemu ya msaada wao wa tani 7.5 ya vyakula katika kituo cha wazee na watu walemavu watokanao na ugonjwa wa ukoma cha Amani Ipuli katika Manispaa ya Tabora mkoani Tabora leo Februari 15, 2017





DIWANI WA KATA YA KIJICHI TAUSI MILANZI AAPISHWA LEO.

0
0
Diwani mpya wa kata ya kijichi Tausi Milanzi akiapishwa katika kikao cha madiwani kilichofanyika leo.

Halmashauri ya Manispaa ya Temeke imefanya kikao cha baraza la madiani ambapo katika kikao hicho mada na ajenda mbalimbali za kimaendeleo zinazohusu wananchi zilijadiliwa.

Sambamba na hilo diwani mpya wa kata ya kijichi Tausi Milanzi alipata kuapishwa katika kikao hicho na kumfanya diwani kutambulika rasmi katika baraza la Madiwani la Halmashauri ya Manispaa ya Temeke.
Madiwani wakiwa katika kikao wakijadili ajenda mbalimbali za kimaendeleo za Manispaa ya wilaya ya Temeke

WAAMUZI TOKA UGANDA KUCHEZESHA MCHEZO WA YANGA VS NGAYA JUMAMOSI

0
0
Kikosi cha Yanga

Na Zainab Nyamka, Globu 

Mchezo wa marudiano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Young Africans ya Tanzania na Ngaya ya Comoro hatua ya awali utachezeshwa na Waamuzi kutoka Uganda.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), waamuzi hao ni Alex Muhabi Nsulumbi atakapuliza filimbi uwanjani.

Nsulumbi atasaidiwa na Ronald Kakenya na Lee Okello wakati Mwamuzi wa Akiba atakuwa Brian Nsubuga Miro huku Kamishna akitokea Afrika Kusini ambaye ni Monnyenyone Lucas Nhlapo.

Mchezo huo utafanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kama ambavyo Young Africans walithibitisha CAF majuma mawili yaliyopita kabla ya terehe ya mchezo huo ambayo ni Februari 18, mwaka huu.

ZIARA YA WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA WILAYANI KITETO

0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimfariji, Aziza Ibrahim wakati alipotembelea wodi ya wazazi katika hospitali ya wilaya ya Kiteto akiwa katika ziara ya mkoa wa Manyara, Februari 15, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiweka jiwe la Msingi la Jengo la Halmashauri ya wilaya ya Kiteto lililopo Kibaya, Februari 15, 2017. Yuko katika ziara ya mkoa wa Manyara. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipanda mti baada ya kuweka jiwe la Msingi la jengo la Halmashauri ya wilaya ya Kiteto akiwa katika ziara ya mkoa wa Manyara, Februari 15, 2017. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mwanahamisi Abdllah akiwa na mtoto Yusra Juma (3.5) katika eneo la mapokezi la hospitali ya wilaya ya Kiteto wakati alipotembelea hospitali hiyo akiwa katika ziara ya mkoa wa Manyara, Februari 15, 2017.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

MBUNGE WA SHINYANGA MJINI STEPHEN MASELE AFANYA ZIARA JIMBONI,ATEMBELEA MRADI MKUBWA WA DARAJA LA GALAMBA

0
0
Mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini mheshimiwa Stephen Masele kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) leo Jumatano Februari 15,2017 ameanza ziara ya kukagua miradi ya maendeleo na kuangalia miundo mbinu iliyopo katika jimbo hilo. 
Siku ya kwanza ya ziara ya mbunge huyo ilikuwa katika kata ya Kolandoto,Ibadakuli,Shinyanga Mjini,Kambarage na Ngokolo. 
Mheshimiwa Masele alikuwa ameambatana na Katibu Mwenezi wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Rajabu Makuburi pamoja na wataalam kutoka idara mbalimbali katika manispaa ya Shinyanga.
Mheshimiwa Masele ametembelea mradi mkubwa wa ujenzi wa daraja lililopo katika kijiji cha Galamba kata ya Kolandoto katika manispaa ya Shinyanga ambalo lipo kati mto mkubwa maarufu kwa jina la ‘Mto Simba’. 
Mbunge huyo pia amejionea jinsi barabara ya kutoka barabara kuu ya Shinyanga – Mwanza kwenda hospitali ya Kolandoto ilivyokatika na kusikiliza kero za wananchi katika kata ya Kolandoto.
Ziara ya Mbunge Masele pia ilifika katika masoko makubwa yaliyopo katika jimbo hilo ikiwemo soko la Kambarage lililopo kata ya Kambarage,Nguzo Nane lililopo kata ya Shinyanga mjini,soko kuu la mkoa wa Shinyanga na soko la Mitumba maarufu ‘Ngokolo Mitumbani’ lililopo kata ya Ngokolo katika manispaa ya Shinyanga.

Hapa ni katika Barabara ya Kolandoto- Wami ambayo inatoka katika barabara kuu ya Shinyanga- Mwanza-Kushoto ni Mhandisi wa Barabara wa Manispaa ya Shinyanga Injinia Stephen Manyangu akimuonesha mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini Mheshimiwa Stephen Masele (wa pili kushoto) jinsi barabara hiyo ilivyomong’onyoka hali inayotishia kukatika kwa barabara hiyo inayoelekea katika hospitali ya Kolandoto.
Mhandisi wa Barabara wa Manispaa ya Shinyanga Injinia Stephen Manyangu akiendelea kutoa maelezo ingawa hata hivyo mbunge Masele aliahidi kutengenezwa/kujengwa kwa barabara hiyo kwa kiwango kwa fedha za mfuko wa jimbo la Shinyanga mjini wakati wanafanya utarabu wa kujenga barabara hiyo katika kiwango cha lami.
Hapa ni katika Ofisi ya CCM Kata ya Kolandoto-Aliyesimama ni Katibu Mwenezi wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Rajabu Makuburi akizungumza wakati akimkaribisha mheshimiwa Masele aweze kuzungumza na baadhi ya wananchi wa kata hiyo huku akibainisha kuwa ziara hiyo inalenga kutekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM.
Diwani wa Kata ya Kolandoto mheshimiwa Agnes Machiya ambaye pia ni Naibu Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga akielezea changamoto ya gharama kubwa za matibabu katika hospitali ya Kolandoto hali inayosababisha wananchi wa eneo hilo wakose huduma ya afya kama inavyotakiwa matokeo yake kulazimika kusafiri umbali mrefu kwenda kutafuta huduma hiyo katika kituo cha Afya Kambarage au Zahanati ya Galamba.
Mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini mheshimiwa Stephen Masele kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) akizungumza na wananchi wa kata ya Kolandoto ambapo alisema ziara hiyo siyo ya siasa bali ni kiutendaji.
Mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini mheshimiwa Stephen Masele kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) alieleza kukerwa na changamoto ya gharama kubwa ya matibabu katika hospitali ya Kolandoto na kuahidi kuzungumza na mamlaka zinazohusika ili kumaliza tatizo hilo.Mheshimiwa Masele pia alisema serikali/Chama Cha Mapinduzi kinafanya jitihada zote ili kuhakikisha kuwa wananchi wa kata ya Kolandoto wanapata huduma ya maji safi na salama.
Diwani wa kata ya Kolandoto Agnes Machiya akimwelezea Mheshimiwa Masele changamoto zilizopo katika kata hiyo
Mkazi wa Kolandoto Kadesha Noniyaza akielezea kero ya maji katika kijiji cha Wami na Mwanubi 
Mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini mheshimiwa Stephen Masele kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) akizungumza na wananchi katika Senta ya kijiji cha Galamba kilichopo katika kata ya Kolandoto baada ya kumuomba asimame wamwelezee changamoto zinazowakabili ambazo ni maji na uhitaji wa daraja katika mto Simba
Mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini mheshimiwa Stephen Masele akizungumza na wananchi hao na kuwaeleza namna serikali inavyojitahidi kuhakikisha kuwa kero zao zinamalizika
Hapa ni katika Mto Simba ambapo mradi wa Ujenzi wa Daraja lililopo katika kijiji cha Galamba kata ya Kolandoto manispaa ya Shinyanga unaendelea.Pichani ni Mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini mheshimiwa Stephen Masele (CCM) akiangalia upande wa pili wa daraja linalojengwa na Mkandarasi M/S Pasons Co.Ltd tangu mwezi Juni mwaka 2016 na unatarajia kukamilika mwezi Machi mwaka 2017.
Mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini mheshimiwa Stephen Masele (CCM) akiangalia daraja hilo ambalo mpaka kukamilika kwake jumla ya shilingi milioni 429.8 zinatarajiwa kutumika. 
Mmoja wa wataalam katika ujenzi huo akimwelezea mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini mheshimiwa Stephen Masele namna ujenzi huo unavyoendelea. 
Daraja hilo lina urefu wa mita 26 na upana wa mita 8
Ujenzi wa daraja ukiendelea
Mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini mheshimiwa Stephen Masele akishindilia zege kwa kutumia mashine kwenye daraja hilo
Mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini mheshimiwa Stephen Masele akishiriki ujenzi wa daraja la Galamba
Diwani wa kata ya Kolandoto Agnes Machiya akishiriki ujenzi wa daraja la Galamba
Mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini mheshimiwa Stephen Masele akizungumza kwenye daraja la Galamba ambapo alisema ujenzi huo wa daraja ambalo litaboresha mawasiliano katika kata ya Kolandoto na manispaa ya Shinyanga kwa ujumla ni miongoni mwa ahadi ambazo aliahidi wakati wa kampeni za uchaguzi mwaka 2015 
Diwani wa kata ya Kolandoto Agnes Machiya (CCM) akizungumza ambapo alisema mradi huo unatekelezwa kupitia mfuko wa barabara 'Road Fund' huku akiongeza kuwa daraja hilo litaunganisha wilaya ya Shinyanga,Wilaya ya Kishapu na Meatu na kwamba kabla ya ujenzi huo eneo hilo lilikuwa kero hasa wakati wa masika
Mkandarasi George Nyanswe kutoka M/S Pasons Co.Ltd akielezea mradi huo wa daraja ambapo alisema mpaka sasa ameshakamilisha ujenzi wa vitako vyote vya daraja na ujenzi wa kuta/nguzo zote za daraja na kwamba anaendelea kutengeneza kindanda cha daraja ya upande mmoja na kwamba ujenzi umekamilika kwa asilimia 75.
Muonekano wa daraja hilo
Ujenzi unaendelea
Muonekano wa daraja na eneo ambapo mto Simba unapita
Mheshimiwa Masele akiteta jambo na Mkandarasi George Nyanswe kutoka M/S Pasons Co.Ltd
Hapa ni katika Shule ya Msingi Bugweto iliyopo kata ya Ibadakuli katika manispaa ya Shinyanga-Wanafunzi na walimu wakimpokea mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini mheshimiwa Stephen Masele
Mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini mheshimiwa Stephen Masele akimtambulisha Diwani wa viti maalum (CCM) kata ya Ibadakuli mheshimiwa Zuhura Waziri (katikati) na diwani wa kata ya Kolandoto mheshimiwa Agnes Machiya (CCM) ambaye pia naibu meya wa manispaa ya Shinyanga
Mheshimiwa Masele akizungumza katika shule ya msingi Bugweto na kuwataarifu wanafunzi na walimu wa shule hiyo kuwa ametoa mifuko 100 ya saraji kwa ajili ya ukarabati wa madarasa ya shule hiyo ambayo yamechakaa na hayana sakafu sambamba na ujenzi wa matundu ya vyoo katika shule hiyo
Mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini mheshimiwa Stephen Masele akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa shule ya msingi Bugweto
Mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini mheshimiwa Stephen Masele akiwa ndani ya darasa la saba katika shule ya msingi Bugweto
Darasa likiwa lina kokoto na vumbi sakafuni
Hapa ni katika Soko la Kambarage kata ya Kambarage katika Manispaa ya Shinyanga.Mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini mheshimiwa Stephen Masele akiwasili katika soko hilo kwa ajili ya kuzungumza na wafanyabiashara 
Mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini mheshimiwa Stephen Masele akisalimiana na mfanyabiashara katika soko la Kambarage katika manispaa ya Shinyanga
Mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini mheshimiwa Stephen Masele akizungumza na wafanyabiashara katika soko la Kambarage na kuwaeleza kuwa serikali ina mpango wa kujenga upya soko hilo hivyo kuwaomba wafanyabiashara wakae na viongozi wao na manispaa ya Shinyanga waangalie eneo ambalo litatumika wakati wakipisha ujenzi wa soko hilo pia kuangalia mazingira mazuri ya wafanyabishara hao kurudi na kuendelea na biashara katika soko hilo
Mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini mheshimiwa Stephen Masele akiteta jambo na katibu wa soko la Kambarage Daudi Kitila( wa kwanza kulia)
Hapa ni katika eneo la Stendi Mpya ya Mabasi Mjini Shinyanga ambapo ujenzi wa choo cha stendi hiyo unaendelea.Katikati ni Mhandisi wa Barabara wa Manispaa ya Shinyanga Injinia Stephen Manyangu akielezea ujenzi wa mfumo wa majitaka unaoendelea katika eneo hilo
Hapa ni katika soko la Nguzo Nane kata ya Shinyanga Mjini-Mheshimiwa Masele akizungumza na wafanyabiashara katika soko hilo
Mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini mheshimiwa Stephen Masele akisikiliza na kujibu kero za wafanyabishara katika soko hilo.Kero kubwa iliyotolewa ni ushuru mkubwa kwa mazao ambapo Masele aliahidi kukutana na uongozi wa manispaa ya Shinyanga kufuatilia kero hiyo na namna ya kuitatua
Ndani ya Soko Kuu la Mkoa wa Shinyanga.Mheshimiwa Masele akizungumza na wafanyabiashara katika soko hilo,kero kubwa ikiwa ni soko hilo kukosa wateja kutokana wafanyabiashara na wateja kukimbilia katika soko la Nguzo Nane na Kambarage
Hapa ni Ngokolo Mitumbani,kwenye soko la Mitumba lililopo kata ya Ngokolo katika manispaa ya Shinyanga.Mheshimiwa Mbunge akishangaa namna mabanda yalivyo wazi kutokana na wafanyabiashara kukimbia soko hilo na kufanyia biashara zao katika maeneo mengine mjini Shinyanga
Mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini mheshimiwa Stephen Masele akizungumza na wafanyabiashara wa nguo za mitumba katika soko la Mitumba,maarufu Ngokolo Mitumbani katika kata ya Ngokolo.
Mfanyabiashara wa Mitumba akielezea jinsi soko hilo lilivyokosa wafanyabiashara kutokana serikali kuruhusu masoko kila mahali mjini Shinyanga
Vibanda vikiwa havina nguo
Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog
Mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini mheshimiwa Stephen Masele akijadiliana na wafanyabiashara hao namna ya kurudisha wafanyabiashara waliokimbia .
Viewing all 46206 articles
Browse latest View live




Latest Images