Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46397 articles
Browse latest View live

MAKAMU WA RAIS AHUDHURIA MKUTANO WA UMOJA WA MATAIFA WA KUWAWEZESHA WANAWAKE KIUCHUMI MJINI DUBAI

$
0
0

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akifuatilia kwa makini kwenye mkutano wa Kuwezesha wanawake kiuchumi ambapo wajumbe wa Jopo maalum walikutanna mjini Dubai kujadili Ripoti ya awali ya Jopo hilo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mkutano wa kuwawezesha wanawake kiuchumi pamoja na wajumbe wengine wa Jopo hilo mjini Dubai.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa pamoja na Siriel Shaidi Mchembe kwenye mkutano wa Kuwezesha wanawake kiuchumi ambapo wajumbe wa Jopo maalum walikutanna mjini Dubai kujadili Ripoti ya awali ya Jopo hilo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akifuatilia kwa makini kwenye mkutano wa Kuwezesha wanawake kiuchumi ambapo wajumbe wa Jopo maalum walikutanna mjini Dubai kujadili Ripoti ya awali ya Jopo hilo.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Mrithi wa Mtawala wa Dubai Sheikh Hamdan Bin Mohamed bin Rashid Al Maktoum pamoja na wajumbe wa Jopo wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Jopo la Umoja wa Mtaifa la Kuwawezesha Wanawake Kiuchumi ulioanza tarehe 6 februari mjini Dubai.

................................................................

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amehudhuria mkutano wa Jopo la Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa la Kuwawezesha Wanawake Kiuchumi kama mmoja wa wajumbe wa jopo hilo.

Mkutano huu umefanyika mjini Dubai, Falme za Kiarabu na Ufunguzi rasmi ulihudhuriwa na Mrithi wa Mtawala wa Dubai Mtukufu Sheikh Hamdan Bin Mohammed Bin Rashid Al Maktoum pamoja na viongozi na wakuu wa Serikali wa Falme za Kiarabu .

Lengo la Mkutano huu ilikuwa ni kupitia Ripoti ya Kwanza ya Jopo hilo iliyowasilishwa na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Ban Ki Moon kwenye Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, mwezi Septemba 2016. Mkutano huu wa Dubai, unategemea kutoa Ripoti ya Pili ambayo itatoa muelekeo wa namna Serikali zitashirikiana na wadau mbalimbali kama vile sekta binafsi, Asasi za kiraia na wadau wengine wa maendeleo katika jitahada za kumkwamua mwanamke kiuchumi.

Wajumbe wa Jopo hili, walipata fursa ya kujadili changamoto mbalimbali zinazomkabili mwanamke; pamoja na kubadilishana uzoefu na kutoa mapendekezo yatakayoleta matokeo chanya katika kumuinua mwanamke kiuchumi. Mbali na kupendekeza maboresho ya Ripoti hiyo, wajumbe walijadili na kupendekeza hatua ambazo wadau watatakiwa kuchukua ili kumkomboa mwanamke kiuchumi.

Tanzania kama nchi mwanachama ilipata fursa ya kutoa uzoefu wake jinsi Serikali imeweka mikakati mbalimbali ya kuwawezesha wanawake hususani wale walio katika sekta isiyo rasmi; hasa wakulima na wafanyabiashara wadogo wadogo wanawake ili kuhakikisha wanafaidika na mifumo ya kifedha na kijiditali kama vile kupata mikopo ya gharama nafuu; kuingizwa kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii na huduma zingine.

Makamu wa Rais alisema pamoja na kila bara kuwa na changamoto zake, bado kuna umuhimu wa dunia kuhakikisha inaweka misingi madhubuti ya kuinua wanawake kiuchumi hasa kwa wanawake wa ngazi za chini ambao wengi wao wanaishii vijijini.

Alitaja baadhi ya changamoto hizo kuwa ni pamoja na mifumo ya sheria na sera zilizopo kuwa bado zinawanyima wanawake haki ya kurithi na kumiliki ardhi hata kama haki hizo zimewekwa kisheria."Hii inatokana na utekelezaji mbaya wa sheria, inayosababishwa na kuwepo kwa mianya kwenye hizo sheria na utendaji wa kubagua ambapo unaondoa ule mfumo rasmi wa kisheria unaotegemewa," alisema Makamu wa Rais.

Aidha alisema ushiriki mdogo wa wanawake ambao wengi ni wajasiriamali, katika kutumia mifumo ya kifedha ikiwemo mifumo mipya ya teknolojia ya fedha mtandao inachangia kuwafanya wanawake wakose mapato na hivyo kushindwa kufanikisha azma ya kuwezesha wanawake kiuchumi. Aliwaasa wanawake waungane na kuinuana wenyewe kwa wenyewe ili kuweza kutoachwa nyuma kwenye kufikia malengo yao ya kiuchumi na kwamba sambamba na utekelezaji wa Malengo Mapya ya Maendeleo Endelevu na Ajenda ya mwaka 2030.

Jopo hilo linatakiwa kuwasilisha ripoti yake ya Pili kwenye Kamisheni ya Hali ya Wanawake Duniani mwezi Machi mwaka huu.

Mkutano huo ulileta washiriki takriban 45 kutoka sekta mbalimbali ikiwemo serikali, Taasisi binafsi, wachambuzi mbalimbali wa masuala ya kumwezesha mwanamke kiuchumi kutoka Jumuiya ya Kimataifa.

NEWZ ALERT: MOHAMED MATUMLA KUFANYIWA UPASUAJI WA KICHWA MOI

$
0
0
Bondia Mohamed Matumla anafanyiwa upasuaji wa kichwa muda huu baada ya ngumi aliyopigwa kuleta madhara kwenye kichwa chake na damu kubainika kuwa imevujia huku  hali yake ikiwa nzuri

Taarifa zilizotufikia ni kuwa Vipimo vya CT scan vimeonyesha kuvuja kwa damu na imejikusanya sehemu moja na madaktari wanahangaikia kunusuru maisha ya mwanamasumbwi huyo ambaye hali yake si nzuri.

Operation ilichelewa kufanyika mapema kwa kuwa alihitajika kuongezewa damu, "tumefanikiwa kupata damu ameshaongezewa na akitoka chumba cha upasuaji ataongezewa damu nyingine"

Wapenzi na wadau wa ngumi kwa muda huu tumuombee DUWA mwenzetu operation yake ifanikiwe

SADICK & CO LTD ipo na mgonjwa toka aliposhuka kwenye ulingo  na kusimamia matibabu yake yote

Tutaendelea kuwapa taarifa baada ya kutoka chumba cha upasuaji na hali yake itakavyokuwa inaendelea. 
Promota STONE                     

WAZIRI MWIGULU AFANYA MAZUNGUMZO NA MWAKILISHI MKAZI WA SHIRIKA LA WAKIMBIZI

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, akizungumza na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Wakimbizi(UNHCR), Chansa Kapaya(kushoto), alipofika ofisini kwake kujadili masuala ya wakimbizi wanaohifadhiwa katika kambi mbalimbali nchini Tanzania.Mazungumzo hayo yamefanyika leo jijini Dar es Salaam. 
Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, akiagana na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Wakimbizi(UNHCR), Chansa Kapaya (kushoto), baada ya kumaliza mazungumzo yaliyofanyika ofisini kwa waziri huyo,kujadili masuala ya wakimbizi wanaohifadhiwa katika kambi mbalimbali nchini Tanzania.Mazungumzo hayo yamefanyika leo jijini Dar es Salaam. 
Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, akiwa katika picha ya pamoja na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Chansa Kapaya (kushoto) ,baada ya kumaliza mazungumzo yaliyofanyika ofisini kwa waziri huyo,kujadili masuala ya wakimbizi wanaohifadhiwa katika kambi mbalimbali nchini Tanzania.Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi kutoka wizarani hapo, Harrison Mseke.Mazungumzo hayo yamefanyika leo jijini Dar es Salaam.(Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)

SERIKALI YAENDELEA KUBORESHA MAZINGIRA YA AJIRA KWA VIJANA

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama amesema kuwa Serikali imejipanga kusaidia vijana kutambua na kuchangamkia fursa mbalimbali za ajira zilizopo nchini ili kutatua changamoto ya ukosefu wa ajira na  kutimiza adhma ya kuleta maendeleo hususani kwa vijana.

Mhe. Mhagama ameyasema hayo jana wakati akijibu hoja ya Mbunge wa Kinondoni Mhe. Maulid Mtulia iliyohoji juu ya jitihada za Serikali katika kutatua tatizo la ukosefu wa ajira kwa vijana wakati wa Mkutano wa Tano wa Bunge unaoendelea Mkoani Dodoma.

Katika Mkutano huo Mhe. Waziri alisisitiza kuwa Serikali ina mipango na mikakati madhubuti inayokusudiwa yakusaidia vijana wa Kitanzania ili kujiletea maendeleo yao wenyewe na kuondokana na umasikini.

Serikali ya Awamu ya Tano imeendelea kuweka mikakati ikiwemo uwanzishwaji wa programu mbalimbali zitakazo saidia kutatua changamoto ya ajira kwa vijana kwa kuangalia matokeo ya tafiti mbalimbali ambazo zimepelekea kuwa na programu zinazolenga kukabili tatizo la ukosefu wa ajira kwa vijana” Alisema Waziri

Alisisitiza kuwa programu hizo ni pamoja na; kurasmisha ujuzi usio rasmi kuwa rasmi, mfumo wa mafunzo kwa vitendo, mfumo wa uanangezi pamoja na kukuza mafunzo kwa watanzania kulingana na soko lililopo kwa sasa.

Pamoja na juhudi hizo zinazotarajiwa kuzaa matunda bado Waziri aliwatoa hofu wananchi wote kwa kuwepo kwa fursa hizo za ajira zitakazo jali hali za watu pasipo kuangalia makabila yao, rangi wala dini.

“Katika kutatua changamoto ya ajira kwa vijana hatuta angalia kabila, rangi wala dini ya mtu bali kutakuwa na haki na usawa”.Alisisitiza Waziri

Aliongezea kuwa, Serikali pia inajitihada za kuvutia uwekezaji kwenye sekta mbalimbali na urasimishaji wa sekta isiyo rasmi ili kupunguza kiwango cha ukosefu wa ajira.

“Serikali itatumia sekta zenye uwezo wa kutoa ajira kwa wingi ikiwemo zile za Kilimo, majenzi, Mawasiliano na Utalii ili kuzitumia kuweka mazingira mazuri kwa vijana kupata fursa za ajira”.

Mhe. Mhagama alisisitizia bungeni kuwa kutokana na tafiti mbalimbali zilizofanyika zitatumika kama chachu ya kuangalia maeneo yanayohitaji kusaidia kwa haraka na kupunguza changamoto hiyo kwa vijana.

“Kwa kuangalia tafiti ya Hali ya Ajira Nchini ya mwaka 2014 imeonesha kuwa kiwango cha ukosefu wa ajira kimepungua kutoka asilimia 11.7 mwaka 2006 hadi asilimia 10.3 mwaka 2014 na ukosefu wa ajira kwa vijana umepungua kutoka asilimia 14.2 mwaka 2006 hadi asilimia 11.7 mwaka 2014”,alisema.

Hata hivyo, Waziri Mhagama alieleza kuwa pamoja na jitihada hizo Serikali bado ina wajibu wa kuongeza jitihada zaidi ili kuongeza kasi ya upatikanaji wa ajira na kuboresha maisha ya vijana.

Visiwa Ukerewe kupata umeme Juni 2018

$
0
0
Na Greyson Mwase, Dar es Salaam

Visiwa vidogo vilivyopo katika Ziwa Viktoria vinatarajiwa kupata umeme wa uhakika ifikapo Juni mwakani.

Hayo yalielezwa na Kamishna Msaidizi- Nishati Jadidifu kutoka Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Styden Rwebangila, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati alipokuwa akielezea mafanikio yaliyopatikana Sekta ya Nishati kupitia Nishati Jadidifu chini ya Idara ya Nishati katika upatikanaji wa umeme wa uhakika.

Alisema kuwa, wakandarasi wameshaanza kuweka miundombinu kwa ajili ya umeme wa jua ambapo miradi hiyo inatarajiwa kukamilika kwa asilimia mia moja ifikapo mwezi Juni mwakani.

Akielezea mipango ya Serikali katika kuhakikisha kuwa nishati ya umeme inakuwa ni ya uhakika Mhandisi Rwebangila alisema Wizara inahamasisha vyanzo vingine vya uzalishaji wa umeme kama vile jua, upepo, jotoardhi na kuongeza kuwa inakaribisha wawekezaji kutoka ndani na nje ya nchi kutafiti na kutumia vyanzo hivyo.

Alisema kwa upande wa jotoardhi utafiti ulifanyika na kuonesha maeneo ya Songwe na Ziwa Ngozi mkoani Mbeya na Mlima Meru mkoani Arusha yana viashiria vya jotoardhi.Aliongeza kuwa mara baada ya utafiti kukamilika mwishoni mwa mwaka huu, visima vinatarajiwa kuanza kuchimbwa kwa ajili ya uzalishaji wa nishati ya jotoardhi.

Aliendelea kutaja mipango mingine kuwa ni pamoja na uanzishwaji wa mwongozo kwa ajili ya mfumo wa umeme kwenye majengo na wa udhibiti wa matumizi ya umeme viwandani.

Alisema pia, Wizara inatarajia kuanzisha mfumo mpya wa uhifadhi data na utoaji taarifa za Nishati Jadidifu ujulikanao kama Tanzania Renewable Energy Management Information System (TREMIS) utakaowezesha wawekezaji ndani na nje ya nchi kubaini fursa za uwekezaji zilizopo katika sekta ya Nishati Jadidifu.

Alisema katika mfumo huo kutawekwa taarifa mbalimbali kuhusu, tafiti mbalimbali na fursa za uwekezaji katika nishati jadidifu , sera, sheria na taratibu ili kuvutia wawekezaji kutoka ndani na nje ya nchi.

“Kupitia mfumo huu kutakuwa hakuna haja ya mwekezaji kutoka nje ya nchi kufunga safari hadi Tanzania kwa ajili ya kupata taarifa, taarifa zote zitakuwepo katika mfumo huu utakaounganishwa na tovuti ya Wizara,” alisema Mhandisi Rwebangila.
Kamishna Msaidizi- Nishati Jadidifu kutoka Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Styden Rwebangila, (kushoto) akielezea mafanikio ya sehemu ya nishati jadidifu chini ya Idara ya Nishati katika upatikanaji wa umeme wa uhakika katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika jijini Dar es Salaam mapema tarehe 06 Februari, 2017. Kulia ni Mtaalam wa Nishati Jadidifu, Emillian Nyanda.

NAMAINGO WATAKIWA KUCHANGAMKIA UZALISHAJI WA MALIGHAFI YA VIWANDA

$
0
0
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mary Mashingo (katikati),akimkabidhi cheti Mwenyekiti wa Ushirika wa Vikundi vya Biashara Dar es Salaam (Vibidar Namaingo), Grace Lobulu katika sherehe iliyofanyika kwenye Uwanja wa Magereza, Ukonga juzi. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya ushirika huo, Ubwa Ibrahim. (PICHA, HABARI NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG)

Na Richard Mwaikenda
SERIKALI imeutaka Ushirika wa Vibidar Namaingo kuanza kuzalisha mazao mengi kwa ajili ya malighafi ya viwanda vilivyopo na vinavyotarajiwa kuanzishwa nchini.

Ushauri huo ulitolewa juzi na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mary Mashingo wakati wa sherehe ya kukabidhi cheti kwa ushirika huo wa Vikundi vya Biashara Dar es Salaam (Vibidar), kwenye Uwanja wa Magereza, Ukonga.

Mashingo, aliipongeza Kampuni ya Namaingo Business Agency Ltd,  kwa kuanzisha vikundi hivyo vya ujasiriamali na kuviatamia hadi kufikia kuunda ushirika wa Vibidar utakaoongeza viwango vya maarifa, taaluma pamoja na tija, jabo litakalowezesha wajasiramali wengi kuondokana na ujasriamali mdogo kwenda kwenye ujasiriamali mkubwa na hatimaye kuongeza pato la kaya na Taifa kwa ujumla.

Alisema kuwa ushirika huu umekuja wakati muafaka, wakati Serikali ya Awamu ya Tano, imekuwa ikitoa kipaumbele katika kuhamasisha maendeleo ya sekta ya viwanda, ambapo sekta ya kilimo kupitia vikundi shirikishi  inayo fursa kubwa ya kuweza kuzalisha malighafikwa ajili ya maendeleo ya viwanda.

"Ushirika wa vikundi mbalimbali kama Vibidar, vina uwezo wa kuzalisha malighafi ya kutosha kwa ajili ya kusindika mazao kutosheleza mahitaji ya viwanda, hivyo ushirika huu umeanzishwa katika muda muafaka wakati serikali inatilia mkazo katika kuchochea maendeleo ya sekta za kiuchumi zinazoweza kuchoche viwanda nchini," alisema Mashingo.

Mashingo, aliahidi serikali kuendelea kushirikiana na wadau kuimarisha ushirika ili kuzitatua changamoto mbalimbali kwa kutumia mikakati  na mbinu za kila aina. Alizija baadhi ya changamoto zinaikabili sekta ya kilimo kuwa ni;uongezaji wa tija katika uzalishaji, mifumo ya soko yenye mpangilio mzuri, kujenga mitandao thabiti ya mawasiliano na kuwaunganisha wadau katika mlolongo wa thamani.

Hakusita kumpongeza Mkurugenzi wa Kampuni ya Namaingo, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Vibidar,  Ubwa Ibrahim kwa bidii ya kuanzisha ushirika huo kwa Dar es Salaam tayari una vikundi 60 vyenye wanachama 4,000 waliotimiza vigezo, pia kwa kuanzisha Vikundi vya Biashara Vijijini (VIBIVI) katika mikoa ya Mtwara, Lindi, Pwani, Arusha, Kilimanjaro, Iringa, Ruvuma, Njombe, Tabora, Manyara, Kagera, Tanga, Kigoma, Mbeya, Songwe, Morogoro na Dodoma.

Akizungumza kabla ya kumkaribisha Katibu Mkuu Mashingo, Mkurugenzi wa Namaingo Business Agency, Ubwa Ibrahim, alisema kuwa kampuni hiyo kupitia Vibidar na Vibivi hutoa mafunzo kwa wajasiriamali ya jinsi ya kuendesha kilimo biashara na ufugaji wenye tija na kwamba hivi karibuni tayari wamezindua mradi wa ufugaji sungura wa kopa sungura lipa sungura katika eneo la Majohe, Dar es Salaam na Mradi wa kopa kuku lipa kuku katika Kata ya Miteja, Kilwa, mkoani Lindi.

Alisema kuwa hivi sasa Namaingo tayari imewafikia wananchi 400,000 nchi nzima  ambapo 10,000 kati ya hao wamweza kujiunga na kukidhi vigezo vya kuwa wanachama.


 Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mary Mashingo (katikati),akimkabidhi hati   Mwenyekiti wa Bodi ya Ushirika wa Namaingo Vibidar, Ubwa Ibrahim. (PICHA NA RICHARD MWAIKENDA)
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mary Mashingo (katikati),akimkabidhi cheti Mwenyekiti wa Ushirika wa Vikundi vya Biashara (Vibidar Namaingo), Wilaya ya Kinondoni, Loiruck Mollel  katika sherehe iliyofanyika kwenye Uwanja wa Magereza, Ukonga juzi. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya ushirika huo, Ubwa Ibrahim. (PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA)


 Mashingo akihutubia wakati wa sherehe hizo
 Wanachama wa Vibidar wakisikiliza kwa makini hotuba 
 Mashingo akitia saini kwenye vyeti vya ushirika alivyovikabidhi Vibidar
 Wanachama wa Vibidar Namaingo wakiwa katika sherehe hiyo




 Msanii akihutubia wakati wa sherehe hiyo
 Mkurugenzi wa Shitindi Poutry Farm, Shitindi akielezea kuhusu ununuzi wa mayai na kuku ambayo yeye atakuwa ndiyo mteja kutoka kwa wanaushirika
 Zaituni Mchata kutoka NSSF akielezea ushirikiano uliopo na Namaingo
 Ofisa wa NMB, Philimon Komu akielezea fursa za mikopo zilizopo katika benki hiyo
 Ofisa wa Benki ya CRDB Tawi la Banana, Anjela Mramba akiwakaribisha wanachama wa Vibidar Namaingo kufungua akaunti na kukopa kwenye benki hiyo

 Lobulu akifurahia kupata cheti cha ushirika
 Lobulu akimshukuru Mwenyekiti wa Bodi ya Vibidar Namaingo, Ubwa Ibrahim
 Mwenyekiti wa Vibidar Namaingo Wilaya ya Temeke, Regina Mutainulwa  (kushoto) akipongezwa na wanachama baada ya kukabidhiwa cheti cha ushirika.
 Ni furaha iliyoje
 Lobulu akitoa neno la shukrani kwa Katibu Mkuu, Mashingo
 Ubwa akitoa neno la shukrani kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Mashingo
 Mashingo na Ubwa wakielekea kukagua bidhaa za wajasiriamali wanachama wa Vibidar Namaingo
 Mashingo akinunua baadhi ya bidhaa za wajasiriamali
Bi Ubwa akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa vibidar Namaingo

Taarifa ya Serikali toka Bungeni

WALENGWA WA TASAF MKOANI SINGIDA WABORESHA MAKAZI YAO KWA KUTUMIA FEDHA ZA RUZUKU.

$
0
0

Na Estom Sanga

Baadhi ya walengwa wa Mpango wa kunusuru Kaya Maskini unaotekelezwa na serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF mkoani Singida wameanza kuboresha makazi yao kwa kutumia sehemu ya fedha zinazotolewa na mfuko huo kwa njia ya ruzuku .

Wakizungumza na Waandishi wa Habari walioko katika ziara ya mkoa huo kuona namna walengwa wa Mpango wa kunusuru kaya maskini wanavyonufaika kupitia utaratibu wa uhawilishaji fedha,baadhi yao wamewaeleza waandishi hao kuwa licha ya kutumia sehemu ya fedha hizo kununua chakula na sare za watoto lakini pia wameweza kununua mabati na kuezeka nyumba zao na hivyo kuboresha makazi yao.

“nimeepukana na shida ya kuvuja kwa nyumba yangu baada ya kununua mabati na kujenga nyumba ya matofali kutokana na fedha za TASAF”amesema mzee shaaban Mkondya anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 70 mkazi wa eneo la Mtipa nje kidogo ya manispaa ya Singida.

Naye bi.Mwajuma Omary amewaeleza waandishi wa habari kuwa tangu aanze kupata ruzuku ya fedha kutoka TASAF mwaka 2014 hali yake ya maisha imeboreshwa na kuwa na walau uhakika wa kupata chakula huku akitumia sehemu ya fedha hizo kununua mabati 10 yaliyomwezesha kuezeka nyumba yake na hivyo kuboresha makazi yake.

“ninaishukuru TASAF kwa kutufikiria sisi wanyonge kama mimi kwani tulikuwa na hali ngumu ya maisha lakini sasa walau tunauhakika wa kupata fedha kila mwezi kulingana na utaratibu uliowekwa” amesisitiza Bi Mwajuma Omary mwenye umri wa miaka 77.

Kwa upande wake Mzee Jumanne kinda amesema utaratibu wa Serikali kupitia TASAF kuwafikia watu maskini umeamusha ari ya wananchi hao kujiletea maendeleo kwani sasa wanaweza kuanzisha shughuli za uzalishaji mali ikiwemo ufugaji wa kuku na mbuzi ili kujiongezea kipato.”nimeweza kununua mbuzi watano na kuezeka nyumba yangu kwa mabati kutumia fedha nilizozipata kutoka TASAF, ninawashukuru sana ,sikuwahi kufikiria kuishi kwenye nyumba ya bati “ amesisitiza Mzee Jumanne Kinda .

Hata hivyo licha ya mafanikio wanayoendelea kupata walengwa hao wa TASAF,wameeleza kuwa jitihada zao za kujikwamua na umaskini zimekuwa zikiathiriwa na magonjwa hususani yale yanaokumba mifugo hasa kuku wa kienyeji.

Wameiomba TASAF kuangalia namna inavyoweza kutoa motisha kwa wataalamu wa mifugo ili waweze kuwatembelea walengwa kwenye maeneo yao na kutoa ushauri wa kitaalamu utakaosaidia kupunguza vifo vya kuku ambao hustawi vizuri mkoani Singida.

Zifuatazo hapo chini ni baadhi ya picha zinazoonyesha baadhi ya walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika manispaa ya Singida wakionyesha nyumba na mifugo walioipata baada ya kupokea ruzuku ya TASAF.


Sehemu ya mtaro uliojengwa katika eneo la Mtipa nje kidogo ya manispaa ya Singida kupitia utaratibu wa ajira ya muda unaotekelezwa na walengwa wa Mpango wa Kunusuru kaya maskini kupitia TASAF.
Mmoja wa walengwa wa Mpango wa kunusuru kaya maskini Mzee Shaaban Mkondya akiwa amesimama kando ya nyumba aliyoiezeka mabati kwa fedha za ruzuku ya TASAF na hivyo kuboresha makazi yake.
Mmoja wa walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini Mzee Shaaban Mkondya aliyesimama na mjukuu wake aliyevaa sare za shule akiwaonyesha waandishi wa habari nyumba yake ya zamani Kulia na ile mpya kushoto kwake aliyoezeka kwa mabati kwa ruzuku ya fedha za TASAF.
Bi. Mwajuma Omary (77) aliyeketi akiwaonyesha waandishi wa habari (hawapo pichani) nyumba yake mpya iliyoko kushoto kwake na kulia kwake ni nyumba yake ya zamani ikiwa katika mfumo wa tembe.
Mzee Jumanne Muhiyo akizungumza na waandishi wa habari juu ya ujenzi wa nyumba yake mpya kwa kutumia fedha za ruzuku kutoka TASAF.

Picha ya juu na chini inaonesha Mama wenye watoto chini ya miaka 5 wakiwa katika kituo cha afya cha Mtipa nje kidogo ya manispaa ya Singida wakitimiza moja ya sharti la Mpango wa kunusuru kaya masikini kuhudhuria kliniki.

WASTAAFU WANAOLIPWA NA HAZINA WASIOHAKIKIWA KUONDOLEWA KWENYE MALIPO YA PENSHENI

$
0
0
Na Benny Mwaipaja-WFM, Mtwara

WIZARA ya Fedha na Mipango, imesema kuwa wastaafu wanaolipwa na Wizara hiyo ambao hawatahakikiwa wataondolewa kwenye orodha ya malipo ya pensheni kwa kuwa watakuwa wamekosa sifa.

Kauli hiyo imetolewa Mjini Mtwara na Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali Msaidizi, Bw. Stanslaus Mpembe, wakati wa uzinduzi wa uhakiki wa wastaafu wanaolipwa pensheni zao na Wizara hiyo katika Mikoa ya Lindi na Mtwara.

Alisema kuwa lengo la uhakiki huo ni kuiwezesha Wizara kuhuisha taarifa za wastaafu ili kupata kanzidata (database) iliyo sahihi, kuwatambua wastaafu na kuiwezesha serikali kulipa wastaafu wanaostahili.

“Kwa kuwa zoezi hilo ni la lazima na kwa wale wastaafu ambao hawajahakikiwa kwa sababu mbalimbali katika mikoa ambayo uhakiki umekamilika watalazimika kufika katika ofisi za Hazina katika mikoa husika na kujiandikisha na baada ya uhakiki kukamilika wataelekezwa utaratibu utakaotumika kuwahakiki” aliongeza Bw. Mpembe

Aidha Bw. Mpembe alisisitiza wastaafu hao kufika wenyewe na sio kutuma wawakilishi, wakiwa na nyaraka zote muhimu zikiwemo barua ya tuzo la kustaafu, barua ya kustaafu au kupunguzwa kazini, nakala ya hati ya malipo ya kiinua mgongo au mkupuo, barua ya ajira ya kwanza, kitambulisho cha pensheni, barua ya kuthibitishwa kazini, kadi ya benki na picha mbili ndogo zilizopigwa hivi karibuni.

Akijibu kuhusu malalamiko ya pensheni ndogo kwa wastaafu, Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali Msaidizi, Bw. Stanslaus Mpembe, amesema kuwa watakapo kamilisha zoezi la uhakiki wataandaa taarifa namna zoezi zima lilivyo endeshwa na kuiwasilisha kwa uongozi wa juu wa Wizara, likiwemo suala hilo la malalamiko ya pensheni ya wastaafu.

Kwa upande wa wastaafu kutoka taasisi mbalimbali za Serikali wanaolipwa na Wizara ya Fedha na Mipango wameiomba Serikali iwaongezee viwango vya pensheni wanavyo lipwa ili waweze kujikimu kimaisha kutokana na hali ya maisha kuwa ngumu.

Akitoa maoni katika zoezi la uhakiki wa wastaafu linaloendelea katika mkoa wa Lindi na Mtwara, Mstaafu David Christopher Mtakula, amesema utaratibu wa kuhakiki taarifa za wastaafu ni njia nzuri ili kujiridhisha kuwa wanaolipwa ndio wanaostahili.

Zoezi hili la uhakiki linaloendelea katika mikoa ya Lindi na Mtwara lilianza Oktoba 20, 2016 katika mkoa wa Pwani na limeshafanyika katika mikoa 23 ya Tanzania Bara ambayo ni Mbeya, Iringa, Njombe, Ruvuma, Songwe, Katavi, Rukwa, Morogoro, Dodoma, Singida, Arusha, Kilimanjaro, Manyara, Tanga, Mwanza, Kagera, Mara, Shinyanga, Simiyu, Geita, Kigoma na Tabora.

Mkaguzi wa ndani wa Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara, Bw. Hussein Mussa, pamoja na maafisa wengine wakiendelea na zoezi la uhakiki wa wastaafu wanaolipwa na Wizara ya Fedha na Mipango, mkoani Mtwara.
Baadhi ya Wastaafu wanaolipwa na Wizara ya Fedha na Mipango, wakikagua nyaraka zao muhimu kabla ya kufika katika dawati la huduma kwenye zoezi la uhakiki linaloendelea mkoani Mtwara
Afisa TEHAMA Mwandamizi kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Jacqueline Nyamugali (wa kwanza kushoto) akiwa na maafisa wengine, wakitoa maelekezo kuhusu nyaraka muhimu za mmojawapo ya wastaafu wanaolipwa na Wizara ya Fedha na Mipango wakati wa zoezi la uhakiki linaloendelea mkoani Mtwara.
Kaimu Mhasibu Mkuu Pensheni, Scolastica Mafumba, akikagua nyaraka na kutoa maelekezo muhimu kwa mmojawapo ya wastaafu wanaolipwa pensheni na Wizara ya Fedha na Mipango waliofika kuhakikiwa mjini Mtwara.
Mkaguzi wa ndani wa Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara Bi. Imelda Mmbaga akimhudumia mmoja wa wastaafu wanaolipwa na Wizara ya Fedha na Mipango, wakati wa zoezi la uhakiki linaloendelea katika mikoa ya Lindi na Mtwara Mtwara.
Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali Msaidizi, Bw. Stanslaus Mpembe, akiongea na waandishi kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini kuhusiana na zoezi zima la uhakiki wa wastaafu wanaolipwa na Wizara ya Fedha na Mipango linaloendelea katika mikoa ya Lindi na Mtwara.

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-WFM)

MABUSHA, MATENDE NA USUBI BADO NI TATIZO MUFINDI

$
0
0
Halmshauri ya Wilaya ya Mufindi, italazimika kurudia zoezi la utoaji kinga tiba kwa magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele baada ya utafiti wa kitabibu kutoka wizara ya afya kubaini uwepo wa vimelea vya magonjwa hayo kwa asilimia kubwa ya wakazi wa halmashauri hiyo.

Taarifa ya idara ya afya kupitia Afisa habari na mawasiliano wa halmashauri ya Wilaya ya Mufindi Bw. Ndimmyake Mwakapiso , imeyataja magojwa hayo manne kuwa ni Ugonjwa wa Mabusha na Matende, Mivyoo ya tumbo sanjari na ugonjwa wa usubi ambao huathiri macho ya binadamu kwa kusababisha upofu.

Amesema baada ya kukamilika kwa zoezi la utoaji kinga tiba mapema mwaka jana, ni kawaida kwa wizara ya afya kuendesha utafiti kwa lengo kutadhimini na kujiridhisha kama kinga tiba iliyotolewa imekidhi matarajio au la, na ndipo ilipogundulika kuwa bado kunavimelea vya maabukizi ya magonjwa hayo miongoni mwa jamii ndani ya halmashauri hiyo.

Mwakapiso, ameongeza kuwa kinga tiba hiyo itatolewa na watoa huduma waliopo katika ngazi ya jamii husika ambao wamepata mafunzo maalum na kujengewa uwezo wa kutekeleza jukumu hilo kwa weledi mkubwa, zoezi ambalo litaendeshwa kuanzia jumatatu ya tarehe 06 mwezi huu na litadumu kwa muda wa siku 06 pekee.

Aidha, ametoa rai kwa wakazi wote wa halmashauri ya wilaya ya Mufindi kutoa ushirikiano wa kutosha kwa watoa huduma watakaofika katika kaya kuwapatia kinga tiba hiyo muhimu kwa ustawi wa afya zao na maendeleo ya taifa, kwa kuzingatia kuwa afya njema ndio chimbuko la maendeleo ya familia na taifa lolote duani.

WASOMI WAPONGEZA USAWA WA JINSIA UMOJA WA AFRIKA(AU)

$
0
0

Mwandishi Wetu,Arusha

Wasomi nchini wamepongeza uteuzi wa majaji wawili wanawake wa Mahakama ya Afrika na Haki za Binadamu(AfCHPR)uliofanywa na Wakuu wa Umoja wa Afrika(AU) katika mkutano wa 28 uliofanyika nchini Ethiopia kuwa unaelenga kujenga usawa wa kijinsia katika chombo hicho cha maamuzi.

Mkutano huo pamoja na mambo mengine ulipitisha majina ya majaji wawili ambao ni Jaji Bensaoula Chafika kutoka Algeria na Jaji Chizumila Rose Tujilane wa Malawi ambao wataitumikia mahakama hiyo kwa kipindi cha miaka sita ijayo.

Majaji hao wanachukua nafasi zilizoachwa wazi na Jaji Fatsah Ouguergouz(Algeria) na Jaji Duncan Tambala(Malawi)ambao utumishi wao ulikoma tangu Septemba 5,2016.

Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Sebastian Kolowa Memorial(Sekomu),Dk Happiness Rwejuna aliyewaongoza wanafunzi wa sheria kutembelea Mahakama hiyo yenye makao yake jijini hapa alisema uamuzi uliofanywa na AU ni mzuri na ufaa kuigwa na nchi wanachama katika uteuzi wa wanawake wenye uwezo katika nafasi za maamuzi.

“Naamini idadi ya wanawake wenye elimu ya juu wapo wengi na wanaweza kufanya kazi kwa umahiri mkubwa,isihishie katika ngazi ya AU tuu bali ishuke hadi kwa nchi moja moja kuona wanawake wana mchango muhimu katika maendeleo ya Afrika kwa ujumla,”alisema.

Majaji hao wanatarajiwa kuapishwa katika kikao cha 44 kinachotarajiwa kufanyika Machi 6,2017 jijini Arusha ikiwa ni mara ya kwanza kwa mahakama hiyo kuwa na majaji wanawake watano katika majaji 11 wa mahakama hiyo tangu ianze kazi zake mwaka 2004.

Naye Emmanuel Chipanta mwanafunzi wa mwaka tatu alisema uwepo wa mahakama hiyo una umuhimu katika kuimarisha utawala sheria kwani kumekua na makosa mengi yanayotendeka ambayo wahusika hawana budi kukabiliana na mkondo wa sheria.

Alisema uwiano wa kijinsia unatajwa katika itifaki iliyoanzisha mahakama hiyo katika ibara ya 12(2) na Ibara ya 14(3).

Kwa upande wake Mwanasheria wa Mahakama hiyo,Selemani Kinyunyu wakati akijibu hoja za wanafunzi hao waliotaka kufahamu uamuzi wan chi za Afrika kutaka kujiondoa katika Mahakama ya kimataifa ya makosa ya jinai alisema sula hilo lina sura mbili katika nchi zinazotaka kujiondoa na zinazotaka kubaki.
 
“Zipo nchi zinazoona mahakama hii imekua ikiwalenga viongozi wa Afrika zaidi badala ya kushughulikia jinai ulimwenguni kote hivyo kuona hamna sababu ya kuendelea kuwa mwanachama,lakini wapo wanaodhani ni muhimu kuendelea kuwepo ili kuotoa mapendekezo ya maboresho pale penye mapungufu jambo ninaloliunga mkono,”alisema
Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mahakama ya Afrika na Haki za Binadamu(AfCHPR)Sukhdev Chhatbar akizungumza na wanafunzi wa mwaka wa tatu kozi ya sheria katika Chuo Kikuu cha Sebastian Kolowa Memorial(Sekomu)kilichopo Lushoto mkoa wa Tanga wakati wa ziara ya masomo katika mahakama hiyo mkoani Arusha.Picha na Filbert Rweyemamu
Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mahakama ya Afrika na Haki za Binadamu(AfCHPR)Sukhdev Chhatbar akizungumza na wanafunzi wa mwaka wa tatu kozi ya sheria katika Chuo Kikuu cha Sebastian Kolowa Memorial(Sekomu)kilichopo Lushoto mkoa wa Tanga wakati wa ziara ya masomo katika mahakama hiyo mkoani Arusha. 
Wafanyakazi na wanafunzi wa sheria katika Chuo Kikuu cha Sebastian Kolowa Memorial(Sekomu)kilichopo Lushoto mkoa wa Tanga wakiwa kwenye chumba cha mahakama ya wazi katika Mahakama ya Afrika na Haki za Binadamu(AfCHPR) wakati wa ziara ya mafunzo. 

MHADHARA WA 8 WA KISAYANSI WAFANYIKA KATIKA HOSPITALI YA KAIRUKI MIKOCHENI

$
0
0
Dokta Winnie Mpanju-Shumbusho akitoa mada kwenye mhadhara wa 8 wa Kisayansi kuhusu Uimarishaji wa Mifumo ya Utoaji Huduma za Afya na Uzuiaji wa Magonjwa kwenye nchi za Kiafrika katika Zama za Maendeleo Endelevu wakati wa Maadhimisho ya 18 ya Kumbukizi ya hayati, Prof. Hubert Kairuki jijini Dar es Salaam. (Picha na Francis Dande). 
Dokta Winnie Mpanju-Shumbusho akitoa mada kwenye mhadhara wa 8 wa Kisayansi kuhusu Uimarishaji wa Mifumo ya Utoaji Huduma za afya na Uzuiaji wa Magonjwa kwenye nchi za Kiafrika katika Zama za Maendeleo Endelevu wakati wa maadhimisho ya 18 ya kumbukizi ya hayati, Prof. Hubert Kairuki jijini Dar es Salaam.
  Dokta Winnie Mpanju-Shumbusho akitoa mada.
 Prof. Moshi Ntabaye akizungumza katika mhadhara huo. 
 Prof. Moshi Ntabaye akizungumza katika mhadhara huo.
 Baadhi ya washiriki.
Prof. Moshi Ntabaye akizungumza katika mhadhara huo.
Baadhi ya washiriki. 
 Baadhi ya washiriki wa mhadhara wa 8 wa Kisayansi kuhusu Uimarishaji wa Mifumo ya Utoaji Huduma za afya na Uzuiaji wa Magonjwa kwenye nchi za Kiafrika katika Zama za Maendeleo Endelevu. 
Baadhi ya washiriki wa mhadhara huo. 
 Baadhi ya washiriki wa mhadhara wa 8 wa Kisayansi kuhusu Uimarishaji wa Mifumo ya Utoaji Huduma za afya na Uzuiaji wa Magonjwa kwenye nchi za Kiafrika katika Zama za Maendeleo Endelevu.
 Washiriki wa mhadhara wa 8 wa Kisayansi kuhusu Uimarishaji wa Mifumo ya Utoaji Huduma za afya na Uzuiaji wa Magonjwa kwenye nchi za Kiafrika katika Zama za Maendeleo Endelevu.
Dokta Winnie Mpanju Shumbusho akitoa mada. 
 Baadhi ya washiriki wa mhadhara wa 8 wa Kisayansi kuhusu Uimarishaji wa Mifumo ya Utoaji Huduma za afya na Uzuiaji wa Magonjwa kwenye nchi za Kiafrika katika Zama za Maendeleo Endelevu.
Washiriki wa mhadhara huo wakisikiliza mada.

Serikali Kupiga Marufuku Matumizi ya Pombe Aina ya Viroba Nchini

$
0
0
Na: Lilian Lundo – MAELEZO – Dodoma

Serikali inatarajia kupiga marufuku utengenezaji na uingizaji wa pombe za bei rahisi maarufu kama “Viroba” Nchini, ndani ya miezi mitatu ijayo.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamisi Kigwangalla ameyasema hayo leo Bungeni, Mjini Dodoma alipokuwa akijibu hoja za wabunge waliokuwa wakilalamikia  kilevi hicho kinavyopunguza nguvu kazi ya Taifa, wakati wa uwasilishwaji wa taarifa za kamati ya kudumu ya Bunge ya masuala ya Ukimwi pamoja na Huduma na Maendeleo ya Jamii kwa mwaka 2016/17.

Dkt. Kigwangalla amesema kuwa baada ya miezi mitatu kilevi hicho kitapigwa marufuku kutengenezwa au kuingizwa nchini pamoja na kuziba mianya yote ya uingizaji wa kilevi hicho ambacho kimekuwa kikitumiwa na vijana wengi, hivyo kuharibu nguvu kazi ya Taifa.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Tarime Mjini Esther Matiko amesema kwamba pombe hiyo inasababisha vifo vya vijana wengi nchini ambao ndio tegemeo kubwa na nguvu kazi ya Taifa.

“Katika kipindi hiki kifupi cha likizo yangu, nilikuwa jimboni kwangu na tumezika vijana wanne ambao wamefariki kutokana na matumizi ya viroba. Hivyo wananchi wa jimbo langu wameniagiza kuja kulieleza Bunge athari za pombe hiyo ili tuweze kujadili na kuona namna gani  ya kuliokoa Taifa hasa vijana kutoka katika janga hilo,” alifafanua Matiko.

Akiwasilisha taarifa ya Kamati, Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile amesema kuwa Kamati imebaini uwepo wa uhusiano mkubwa kati ya matumizi ya pombe hizo na kuongezeka kwa tabia hatarishi zinazochangia ongezeko la vijana katika matumizi ya dawa za kulevya.

Aidha amesema kuwa hali hiyo inaathiri ufanisi wa nguvu kazi ya Taifa kutokana na madhara ya matumizi ya dawa za kulevya. Hivyo Kamati imeishauri Serikali kufungia kabisa uzalishaji na uuzwaji wa pombe hizo za viroba ili kulinusuru Taifa.

VIJUSO VYA MAGAZETI YA LEO JUMANNE FEBRUARY 7, 2017

MATUKIO MBALIMBALI KUHUSU OFISI YA WAZIRI MKUU BUNGENI DODOMA JANUARI 2017

$
0
0

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akijibu hoja za wabunge mbalimbali waliochangia wakati wa kujadili Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Ukimwi Bungeni Dodoma Januari 6, 2017.


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (kulia) akizungumza na baadhi ya wabunge mara baada ya kuhairishwa kwa Mkutano wa Bunge Mjini Dodoma Januari 6, 2017 katikati ni Mbunge wa Singida Mhe. Ashyrose Matembe.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akiteta jambo na Mhe.Hawa Ghasia nje ya viwanja vya bunge Dodoma Januari 6, 2017.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Vijana), Mhe. Antony Mavunde (kulia) akizungumza na Mhe. Machano Othman nje ya ukumbi wa Bunge Dodoma mara baada ya kupitishwa kwa Taarifa ya Kamati ya Ukimwi na Dawa za Kulevya Januari 6, 2017.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira na Muungano Mhe.January Makamba baada ya kupitishwa kwa Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Masuala ya UKIMWI kuwa makadirio ya Bunge wakati wa Mkutano wa Sita wa Bunge linaloendelea Mkoani Dodoma.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akibadilishana mawazo na baadhi ya wabunge nje ya Ukumbi wa Bunge mara baada ya kuhairishwa kwa Mkutano wa Sita wa Bunge Januari 6, 2017 Dodoma.Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira na Muungano Mhe.January Makamba wakipongezana mara baada ya kupitishwa kwa Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Ukimwi na Dawa za Kulevya Januari 6, 2017. (PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU-DODOMA)

Ziara Ujumbe Shirika la Ndege Tanzania ATCL Visiwani Komoro

$
0
0
 Bw. Ladislaus Matindi akisamilimiana na Gavana wa Anjoun Mhe. Abdou Salam Abdou

 Mazungmzo yakiendelea katika ofisi ya Gavana
 Mhe Balozi akilakiwa na viongozi mbalimbali wa Kisiwa
 Mhe Balozi akiongoza kikao na wadau wa biashara kutoka Kisiwa cha Anjoun
 Mke wa Balozi Mama Irene Kilumanga akimsalim Gavana.
Wajumbe walipowasili Kisiwa cha Anjoun


TAARIFA FUPI ZIARA YA UJUMBE WA ATCL VISIWANI KOMORO TAREHE 06 FEBRUARI, 2017


Ujumbe wa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL Limited) uliwasili Visiwani Komoro tarehe 5 February, 2017. Ujumbe huo ukiongozwa na Bw. Emmanuel Korosso ulipokelewa na Mhe. Chabaka Kilumanga, Balozi wa Tanzania, Visiwani Komoro. Aidha Mwenyekiti huyo aliongozana pia na Bw. Ladislaus E. Matindi Mkurugenzi Mtendaji wa ATCL. 

Madhumini ya ziara hiyo ilikuwa ni kuja kuangalia namna gani ATCL inaweza kutanua wigo wa safari zake Visiwani Komoro. Hii ikiwa ni sehemu ya mkakati wa shirika hilo kuweza kulidhibiti kikamilifu soko la anga la Visiwa vya Komoro ambapo kwa sasa Soko hilo limekuwa na ushindani mkubwa kutoka kwa mashirika mengine ya Kimataifa kama vile  Ethiopian Airlines, Air Madagscar, Kenya Airways n.k.

Katika ziara hiyo, wajumbe walipata fursa ya kuongozana na Mhe. Balozi kwenda Kisiwa cha Anjoun na kufanya mazungumzo na Gavana wa Kisiwa hicho Mhe. Abdou Salami Abdou. Ifahamike kwamba Shirika la ndege la ATCL hufanya safari zake mara tatu kwa wiki Visiwani Komoro ambapo ndege hiyo hutua katika uwanja wa Kimataifa wa Prince Said Ibrahim Jijini Moroni. 

Komoro ni Muungano wa Visiwa Vitatu ambavyo ni Anjoun, Ngazidja na Moheli.  Hata hivyo imeonekana kuwa abiria wengi wanaosafiri kuja Tanzania kwa ajili ya shughuli za biashara hutokea Katika Kisiwa cha Anjoun.  Imejidhihirisha kuwa  abiria kutoka Ksiwa cha Anjoun hupata usumbufu kwa vile hakuna safari za moja kwa moja kutoka Kisiwa hicho kwenda Dar es Salaam, hali ambayo imeonekana kuongeza ghara za usafiri kwa abiria hao.

Aidha katika mazungumzo yao na Gavana wa Kisiwa cha Anjoun ujumbe huo uliwasilisha maombi ya ATCL kupewa kibali cha kutua Kisiwa cha Anjoun ambapo Gavana huyo aliridhia maombi hayo na kueleza kufurahishwa kwake na dhamira ya ATCL kufanya safari zake Kisiwani hapo. 

Mhe. Gavana alieleza pia safari za ATCL Visiwani hapo zitasaidia katika kukuza mahusiano ya biashara kati ya Tanzania na Komoro pamoja na kupunguza gharama za usafiri kwa abiria wanaotokea kwenye Kisiwa hicho. Kwa upande wake Balozi wa Tanzania Visiwani Komoro, Mhe. Chabaka Kilumanga alieleza pia kuwa jukumu kubwa la Ubalozi ni kuhakikisha kuwa mahusiano ya biashara kati ya Tanzania yanakuzwa na kwamba usafiri wa anga ni njia moja wapo ya kukuza mahusiano hayo. Mhe. Balozi aliendelea kwa kueleza kuwa lengo ni kuona Dar es Salaam inakuwa ni kitovu cha Biashara hivyo hakuna budi kukawepo ufanisi katika usafiri wa anga na usafiri wa maji.

Sambamba na hilo, Ujumbe wa ATCL pamoja na Balozi walipata fursa pia ya kufanya mazungumzo na wadau kutoka Sekta ya Biashara wa Kisiwa cha Anjoun ambapo pamoja na mambo mengine Mkurugenzi Mtendaji wa ATCL Bw. Ladislaus Matindi aliwahakikishia wana Anjouna kuwa shirika la Ndege la ATCL la sasa sio kama la zamani na kwamba shirika hilo limejidhatiti katika kuboresha huduma zake. 

Aidha Mkurugenzi huyo alieleza kuwa shirika hilo limeweza kuondoa usumbufu mwingi uliokuwa ukijitokeza hapo nyuma ikiwemo suala la upotevu wa mizigo, kufutwa kwa safari bila maelezo, ucheleweshaji wa abiria na mizigo yao,  alieleza kuwa shirika hilo linatambua umuhimu wa wadua wa biashara kutoka Kisiwa cha Anjoun na ndio maana ameeongozana na Mwenyekiti wa Bodi Visiwani hapa ili kuweza kusikiliza changamoto zinazowakabili wafanya biashara hao na kushauriana juu ya namna gani changamoto hizo zitapatiwa ufumbuzi.

Kw upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya ATCL Bw. Emmanuel Korosso alielekeza shukurani zange kwa wadau wa biashara Kisiwani Anjoun na kuendelea kusisitiza kuwa Shirika la Ndege la Tanzania limedhamiria katika kuboresha ufanisi kwenye utendaji wake na kwamba shirika hilo linasimama pamoja na Wakomoro katika kuhakikisha lengo hilo linafanikiwa. 

Mwenyekiti aliendelea kwa kueleza kuwa anatambua changamoto ambazo zimekuwa zikiwakabili abiria wa Anjoun na kwamba changamoto hizo siku zake zinahesabika. Aliahidi kuwa yale yote ambayo ATCL imedhamiria kufanya yatatekelezwa tena kwa wakati muafaka kwani Ofisi ya Ubalozi ipo kwa ajili ya kufanya hivyo.

Sekretarieti ya Ajira yatoa elimu ya masuala ya Ajira kwa wanafunzi wa Vyuo Zanzibar

$
0
0
 Naibu Makamu mkuu wa Chuo kikuu cha Zanzibar anayesimamia Utawala  Dkt. Zakia M. Abubakar (Kulia) akiongea na Ujumbe wa Sekretarieti ya Ajira uliotembelea Zanzibar kwa ajili ya kutoa elimu ya maswala mbalimbali ya Ajira kwa wanafunzi wa vyuo Vikuu vya Zanzibar.
Sehemu ya wanafunzi wa Chuo kikuu cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Tawi la Zanzibar wakisilizilza mada kuhusu namna ya kujaza Taarifa zao kwenye portal ya Ajira ili  kurahisihsa utumaji wa maombi ya kazi kwa njia ya Mtandao  (e-Application) wakati ajira zinapotangazwa.

Na Kassim Nyaki-PSRS

Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma imefanya ziara katika Vyuo vya Zanzibar ikiwa ni hatua ya utekelezaji wa utaratibu wake wa kuhamasisha na kuelimisha wanafunzi wa Vyuo mbalimbali nchini kuhusu utaratibu wa uendeshaji wa mchakato wa Ajira katika Utumishi wa Umma.

Ziara hiyo ambayo ilifanyika kwa ushirikiano kati ya Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma na Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Zanzibar ililenga kutoa hamasa na elimu kwa wanafunzi wa Vyuo kama sehemu ya wadau katika mchakato wa Ajira.

Katika ziara hiyo mada mbalimbali zimeweza kutolewa kwa wanafunzi hao ikiwemo taratibu za uendeshaji wa Mchakato wa Ajira katika Utumishi wa Umma na changamoto zake, Masharti ya msingi ya kuzingatiwa kabla na baada ya kuwasilisha maombi ya kazi, Matumizi ya TEHAMA hususani namna ya kujisajili katika mfumo wa maombi ya kazi.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Ajira Bibi Riziki Abraham akiongea na wanafunzi wa Vyuo mbalimbali alibainisha kuwa mada hizo zimelenga kutoa uelewa kwa wanafunzi wa Vyuo ili waweze kujua majukumu ya Sekretarieti ya Ajira, taratibu za kufuata kabla ya kuomba ajira Serikalini, namna ya kujiandaa kabla na wakati wa usaili pamoja na utaratibu wa uwasilishaji wa maombi ya kazi kwa njia ya mtandao ujulikanao kama Recruitment portal.

“Wanafunzi wa vyuo kama sehemu ya wadau wetu wakubwa katika masuala ya ajira ni mategemeo yetu kuwa mtakapohitimu masomo yenu mtaingia kwenye soko la ajira, hivyo ni vizuri mkafahamu taratibu za kuomba kazi, namna ya kuandaa wasifu binafsi (CV) namna ya kuandika barua za maombi ya kazi, jinsi ya kujiandaa kabla na wakati wa usaili na utaratibu mpya wa utumaji na upokeaji wa maombi ya kazi kwa njia ya Mtandao ujulikanao kama Recruitment portal” ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kuweza kushindana katika soko la ajira nchini, alisisitiza Riziki.

Vyuo Vikuu vilivyotembelewa ni pamoja na Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar-SUZA, Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Tawi la Zanzibar, Chuo cha Utumishi wa Umma Zanzibar pamoja na Chuo Kikuu cha Sumait.

Aidha, ziara hiyo pia ililenga kutoa uelewa kwa wanafunzi wa Vyuo kuzifahamu Wizara na Taasisi zinazotekeleza masuala ya Muungano ambapo katika mchakato wa Ajira kwa Wizara na Taasisi hizo waombaji kazi kutoka Tanzania Bara wanapata asilimia 79 na waombaji kazi kutoka Zanzibar asilimia 21 ya mgao wa Ajira kwenye Wizara na Taasisi hizo za Muungano.

Mkurugenzi wa Mipango na Rasilimali watu kutoka Wizara ya Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Zanzibar Bw. Hamis Haji Juma wakati akizungumza na wanafunzi wa vyuo hivyo alibainisha kuwa ziara hiyo imesaidia kuwaelimisha wanafunzi kujua fursa za Ajira kwa upana wake ikiwa ni pamoja na waombaji kazi kutoka Zanzibar kuomba nafasi za kazi zinatotangazwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Ajira zinazotangazwa kupitia Wizara na Taasisi zenye masuala ya Muungano.

Ziara hiyo pia imetumika kuwafahamisha wadau mbalimbali ikiwemo wanafunzi wa Vyuo hivyo juu ya uwepo wa Ofisi ya Sekretarieti ya Ajira katika eneo la Shangani Zanzibar ambayo itasaidia kuboresha utendaji kazi na kuratibu masuala mtambuka yanayohusiana na uendeshaji wa mchakato wa Ajira katika Utumishi wa Umma hasa katika Wizara na Taasisi za Muungano.

WAZIRI MKUU AZUNGUMZA NA MABALOZI, AWATAKA WAKATAFUTE WAWEKEZAJI

$
0
0

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka mabalozi wa Tanzania katika nchi mbalimbali kuhakikisha wanatumia uwakilishi wao kutafuta wawekezaji watakaokuja kuwekeza katika sekta ya viwanda nchini.
Amesema  mkakati wa Serikali ni kuimarisha uchumi  hadi wa kati kupitia sekta ya viwanda, hivyo jukumu la mabalozi hao ni kuhakikisha jambo hilo linafanikiwa.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Jumanne, Februari 7, 2017) alipokutana na mabalozi wa wanaoiwakilisha Tanzania katika nchi za Uturuki, Brazil, China, Italy, Ufaransa, Jamuhuri ya Kidemkrasi ya Congo (DRC) na Uswisi.

Mabalozi hao ni Balozi Dk. Emmanuel Nchini (Brazil), Balozi Elizabeth Kiondo (Uturuki), Balozi George Madafa (Italy), Balozi James Msekela (Uswisi),Balozi Samuel Shelukindo (Ufaransa), Balozi Paul Mella (DRC), Balozi Mbelwa Kairuki (China).

“Serikali inahitaji watu wa kuja kuwekeza katika viwanda ili kuongeza thamani ya mazao kabla ya kuyauza nje ya nchi, hivyo jukumu lenu ni kuhakikisha tunapata wawekezaji wenye sifa,” amesema.

Pia Waziri Mkuu amewataka mabalozi hao kutumia uwakilishi wao katika nchi hizo kwa kuhakikisha wanatangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini ili kuongeza idadi ya watalii wanaokuja Tanzania.

Aidha, Waziri Mkuu amewataka mabalozi hao kulinda maslahi ya Taifa katika nchi hizo ikiwa ni pamoja na kuimarisha uhusiano uliopo kati ya Tanzania na mataifa hayo.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amewataka mabalozi hao kuhakikisha wanawatambua Watanzania wanaoishi katika mataifa hayo na kushirikiana nao katika kutafuta wawekezaji wa kuja kuwekeza nchini.

Kwa upande wake Balozi Mella ambaye alizungumza kwa niaba ya mabozi wenzake alimuhakikishia Waziri Mkuu kwamba watakwenda kutekeleza wajibu wao ipasavyo.

       
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMANNE, FEBRUARI 7, 2017.
 WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa akizungumza na mabalozi ambao wanaiwakilisha Tanzania nje ya nchi na wanatarajiwa kuripoti kwenye vituo vyao vya kazi hivi karibuni, Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam, Februari 7, 2017 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa akizungumza na mabalozi ambao wanaiwakilisha Tanzania nje ya nchi na wanatarajiwa kuripoti kwenye vituo vyao vya kazi hivi karibuni, Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam, Februari 7, 2017 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa akizungumza na mabalozi ambao wanaiwakilisha Tanzania nje ya nchi na wanatarajiwa kuripoti kwenye vituo vyao vya kazi hivi karibuni, Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam, Februari 7, 2017 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa akizungumza na mabalozi ambao wanaiwakilisha Tanzania nje ya nchi na wanatarajiwa kuripoti kwenye vituo vyao vya kazi hivi karibuni, Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam, Februari 7, 2017 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali baada ya kuzungumza nao Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam, Februari 7, 2017. Kutoka kushoto ni Samwel Shelukindo (Ufaransa), Dkt. James Msekela (Uswisi), Mbelwa Kairuki (China), Paul Mella (DRC), Dkt. Emmanuel Nchimbi (Brazil) George Madafa (Italy) na Elizabeth Kiondo (Uturuki). (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

 WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa akisalimiana na mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania nje ya nchi baada ya kuzungumza nao Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam, Februari 7, 2017 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa akisalimiana na mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania nje ya nchi baada ya kuzungumza nao Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam, Februari 7, 2017 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

                       

WIZARA YA HABARI YAZINDUA PROGRAMU YA WADAU TUZUNGUMZE

$
0
0
Na: Genofeva Matemu 

Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo imebuni na kutanganza Programu ya kushirikisha wadau inayoitwa wadau tuzungumze itakayosaidia wizara kupata vionjo, maoni, mawazo na fikra za wadau katika kuhakikisha kwamba Wizara inafanya kama wadau wake wanavyotegemea.

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel alipokua akizungumza na waandishi wa habari kutangaza programu hiyo yenye kauli mbiu ya kuitoa wizara ofisini kuipeleka kwa wadau leo Jijini Dar es Salaam.

Prof. Gabriel amesema kuwa Wizara imekua na kauli mbiu ya kuitoa Wizara Dar es Salaam kuipeleka mikoani na sasa inaendelea na mkakati wa kuitoa wizara ofisini na kuipeleka kwa wadau kwani Shabaa kubwa ya wizara ni kuhakikisha kwamba yale yanayofanywa na wizara jamii iyafahamu katika kutekeleza nia na hari ya hapa kazi tuu ya serikali ya awamu ya tano.

“Mpango wa programu ya wadau tuzungumze utafanyika kisekta ambapo utakua ni mkutano utakaoshirikisha mmoja wa viongozi wa wizara kukutanana na wadau na utakua na utaratibu madhubuti kwa kila mwezi siku ya jumanne saa nne asubuhi ambapo viongozi hao watakutana na vyombo vya habari wakiwa na wadau kujadili mambo ya kisekta” amesema Prof. Gabriel.

Mpango huu utahusisha Jumanne ya kwanza ya mwezi sekta ya habari na wadau wote wa habari, jumanne ya pili ya mwezi ni kwa ajili ya sekta ya Utamaduni na wadau wote wa utamaduni, jumanne ya tatu ya mwezi ni kwa ajili ya sekta ya sanaa na wadau wote wa sanaa na mwisho jumanne ya nne ya mwezi ni kwa ajili ya sekta ya maendeleo ya michezo na wadau wake.

Pamoja na mambo mengine program hii itatoa fursa kubwa sana kwa wadau kuleta mawazo yao ili wizara iweze kuwaingiza kwenye mnyororo wa thamani wa shughuli zake kwani wizara inatamani ifanye kwa mlengo ambao wadau weke wanatamani ifanyike.

Progamu hii itazinduliwa rasmi tarehe 14 Mwezi Februari mwaka 2017 hapa Jijini Dar es Salaam ambapo itahushisha sekta ya Utamaduni na hapo baadaye mikutano hii inaweza kufikiriwa na kufanywa kwa kanda. Mpango huu utahusisha pia Taasisi zilizo chini ya wizara.

Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akizungumza na waandishi wa habari (hawapo Pichani) leo Februari 07, 2017 Jijini Dar es Salaam kuhusu mkakati wa Wizara kuanza kuzungumza na wadau katika sekta zinazosimamiwa na Wizara yake.

Waandishi wa Habari wakifuatilia mkutano wa Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (hayupo pichani) akizungumza leo Februari 07,2017 Jijini Dar es Salaa kuhusu mkakati wa Wizara kuanza kuzungumza na wadau wa sekta zinazosimamiwa na Wizara yake.Picha na Raymond Mushumbusi

Ni Wakati muafaka wa kulitumia Baraza la Taifa la Ujenzi katika ukaguzi na uendeshaji wa miradi.

$
0
0
Na Ismail Ngayonga,MAELEZO-Dar es Salaam


KATIKA mwaka 2014/15 Mamlaka ya udhibiti wa manunuzi ya umma (PPRA) ilifanya ukaguzi katika taasisi 70 za umma ili kuangalia iwapo taasisi hizo zilizingatia sheria na kanuni za manunuzi na matumizi ya nyaraka za miongozo iliyoandaliwa na PPRA.

Taasisi zilizoguswa na ukaguzi huo uliofanyika kati ya mwezi Aprili hadi Septemba ni pamoja na taasisi 15 zilizo katika kundi la Wizara, Idara na Wakala za Serikali, Mamlaka za Serikali za Mitaa 25 na mashirika ya umma 30.

Aidha jumla ya mikataba 21,313 ya manunuzi yenye thamani ya Tsh Trilioni 1.05 ilifanyiwa ukaguzi huo, ikiwemo mikataba 845 ya kazi za ujenzi, ambapo mikataba 130 yenye thamani ya Tsh 697 ikihusisha ukaguzi wa thamani halisi ya matumizi ya fedha.

Matokeo ya ukaguzi huo iliyohusisha miradi ya mbalimbali ya maendeleo yenye thamani ya Tsh. Milioni 964, ilibainika kuwa miradi 10 ya sekta ya ujenzi ilipata alama isiyoridhisha kutokana na thamani halisi ya fedha iliyotumika kushindwa kulingana na kiwango cha utekelezaji wa miradi iliyoainishwa.

Miradi iliyochaguliwa kwa ajili ya kufanyiwa ukaguzi wa kupima thamani ya fedha ilipatikana katika utekelezaji wa mikataba ya manununzi iliyothaminiwa kwa kutumia vigezo mbalimbali ikiwemo uandaaji, usanifu na uhifadhi wa nyaraka za zabuni, mchakato wa manunuzi pamoja na usimamizi wa kazi za ujenzi na mikataba.

Sekta ya Ujenzi ni miongoni sekta za kiuchumi zinaoongoza katika upotevu wa fedha za Serikali, na hivyo kuiingizia hasara Serikali kutokana na miradi mingi kutekelezwa chini ya kiwango na kukosekana kwa uwazi katika mikataba ya mkandarasi na taasisi.

Ili kukabiliana na changamoto hiyo, mwaka 2008 Serikali iliifanyia marekebisho sheria ya Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC) ili kuhakikisha kuwa sharia hiyo inaenda sambamba mazingira yaliyopo katika sekta ya ujenzi nchini hususani katika usimamizi na uendeshaji wa miradi inayosimamiwa na mamlaka za Serikali za Mitaa ikiwemo Mikoa na Wilaya.

Hivi karibuni Baraza hilo lilitoa taarifa yake kwa umma kuhusu tathimini ya ukaguzi wa kiufundi katika miradi 163 ya ujenzi yenye thamani ya Tsh. Bilioni 2.8 ikihusisha barabara, majengo na viwanja vya ndege.

Ukaguzi huo uliofanyika kati ya mwaka 2005-2009 ulilenga katika kufanya mapitio ya michakato ya manunuzi, utekelezaji wa miradi, ongezeko la gharama za miradi, ubora wa kazi zilizofanyika na gharama za malipo ya zabuni.

Kaimu Mkuu wa Idara ya Uhandisi wa NCC, Mhandisi Wambura Wambura anasema ukaguzi wa kiufundi katika utekelezaji wa miradi ya ujenzi ni uchunguzi maalum wa hatua mbalimbali za mradi, ambazo huwawezesha mamlaka ya maamuzi na wafadhili kujiridhilisha kwa kupata mrejesho halisia wa masuala mbalimbali ya mradi.

“Ukaguzi huu uhusisha mwenendo wa hatua mbalimbali za mradi hususani hatua za mwanzo za matayarisho ya mradi, upembuzi yakinifu wa mradi, usanifu, manunuzi na utekelezaji wa mradi” anasema  Mhandisi Wambura.

Anasema ukaguzi wa kiufundi katika miradi ya ujenzi huzisaidia mamlaka kuchukua hatua stahiki za maamuzi na tahadhari kwa wakati ili kuhakikisha ufanisi uliokusudiwa upatikana katika mradi husika.

Kwa mujibu wa Mhandisi Wambura anazitaja aina za kaguzi za kiufundi kuwa ni pamoja na ukaguzi wa kiufundi wakati wa matayarisho ya mradi, ukaguzi wa kiufundi wakati wa utekelezaji wa mradi, pamoja na ukaguzi wa kiufundi baada ya utekelezaji wa mradi.

Akizungumzia kuhusu taratibu za ukaguzi huo, Mhandisi Wambura anasema Baraza hilo hutoa miongozo maalum kwa ajili ya ukaguzi wa kiufundi katika, ambayo ni pamoja na kupokea maombi ya ukaguzi, uteuzi wa timu ya wataalamu, pamoja na kuandaa taarifa ya ukaguzi wa kiufundi.

Kwa mujibu wa Mhandisi Wambura anasema katika mwaka 2015/16, Baraza hilo lilifanya ukaguzi wa kiufundi wa miradi ya matengenezo ya barabara kwa halmashauri zote nchini pamoja na ukaguzi wa miradi ya majengo yanayomilikiwa na Benki ya NMB katika wilaya za Mwanga, Chalinze, Pangani, Mbulu na Arusha.

“Mwaka 2011 tulifanya ukaguzi katika miradi 14 ya ujenzi na vituo vya afya 36, yenye thamani ya Tsh. Bilioni 2.3 ambayo ilikuwa inatekelezwa na Halmashauri 20 nchini” anasema Mhandisi Wambura.

Baraza la Taifa la Ujenzi ni kitovu cha uratibu wa sekta ya ujenzi kwa taasisi zote zinazoshughulika na shughuli za ujenzi pamoja na wadau mbalimbali, likiwa na jukumu kuu la kusimamia na kuonogza juhudi za kukuza na kuendeleza sekta ya ujenzi ili kwenda sambamba na maendeleo na ushindani wa kimataifa.

Ni wajibu wa taasisi za umma na binafsi kushirikiana na Baraza hilo katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya ujenzi hususani katika shughuli za ukaguzi wa kiufundi wa miradi hiyo ili kuhakikisha kuwa thamani ya fedha inalingana na ubora wa miundombinu iliyojengwa.
Viewing all 46397 articles
Browse latest View live




Latest Images