Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46334 articles
Browse latest View live

MAHAKAMA YAWAONYA MAWAKILI WA KESI YA 'MPEMBA' ANAYETUHUMIWA KUKUTWA NA NYARA ZA SERIKALI

$
0
0
Karama Kinyuko-Globu ya Jamii.

Mahakama imewataka mawakili wa utetezi katika kesi ya kukutwa na nyara za serikali zenye thamani ya sh. Milioni 785.6 inayomkabili Yusufu Yusufu maarufu kama Mpemba kuacha kuwaeleza washtakiwa lugha tamu tamu kana kwamba kesi yao imeiva.

Hakimu Mkazi Thomasi Simba wa mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu aliwaambia mawikili hao kuwaeleza ukweli washtakiwa na siyo kuwapa lugha tamu wakati wakijua fika safari yao bado ni ndefu na mbele kuna shubiri.

Hatua hiyo ilikuja wakati kesi hiyo asubuhi ilipofika mahakamani hapo kwa ajili ya kutajwa na Wakili wa serikali Elia Athanas kuieleza Mahakama kuwa jalada la kesi liko kwa RCO.

"Mheshimwa kesi leo imekuja kwa ajili ya kutajwa lakini jalada bado liko kwa RCO kwenye utaratibu wa kuandaliwa vijarada mbali mbali kwa ajili ya kupeleka mahakama ya mafisadi.

Lakini kabla kesi haijaahirishwa mawakili wa utetezi wakiongozwa na Nehemia Nkoko waliwataka Jamuhuri kumpa presha RCO ili amalize kuandaa hayo majarada na kesi iende mahakama ya mafisadi.

" kutokana na kauli za jamuhuri inaonekana kuwa upelelezi haujakamilika tu naomba wawe na kauli moja kuwa upelelezi bado", walisema.

Baada ya hoja hizo hakimu Simba aliwataka mawakili wawe wawazi kwa washtakiwa, waache kuwafanya wajue kwamba jalada likitoka kwa RCO linarudi moja kwa moja mahakamani wakati wanajua fika kuwa ni lazima liende kwa DPP kisha Kisutu kwa Committal tayari kwa kwenda mahakama ya mafisadi.

"Safari bado ni ndefu sana kwa washtakiwa, acheni kuwaeleza lugha tamu tamu wakati unajua mlolongo mzima" alisema hakimu Simba.Awali, upande wa Jamhuri uliiambia Mahakama hiyo kuwa jalada hilo liko kwa Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Siro analifanyia kazi ili liende ngazi zingine kwa hatua zaidi.

Mkuu huyo akishamaliza kulifanyia kazi atalipeleka kwa Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), Biswalo Mganga kwa hatua zaidi za kulitolea uamuzi atakaoona unafaa katika kesi hiyo.Mbali na Mpemba ambaye ni mkazi wa Tegeta, washitakiwa wengine ni Charles Mrutu (37) wa Mlimba, Morogoro, Benedict Kungwa (40) wa Mbagala Chamazi, Jumanne Chima (30) wa Mbezi, Ahmed Nyagongo (33) dereva na Pius Kulagwa (46).

Washitakiwa hao wanadaiwa kujihusisha na mtandao wa ujangili na biashara ya meno ya tembo yenye thamani ya Sh milioni 785.6.

Ilidaiwa kuwa katika tarehe zisizofahamika kati ya Januari 2014 na Oktoba, mwaka jana wakiwa Dar es Salaam, Tanga, Iringa na Mtwara, walikusanya na kuuza vipande 50 vya meno ya tembo vyenye thamani ya dola 180,000 sawa na Sh milioni 392.8 mali ya Serikali bila kibali cha Mkurugenzi wa Wanyamapori.

Aliendelea kudai kuwa katika mashitaka ya pili, Oktoba 26 mwaka jana washitakiwa wakiwa Mbagala Zakhem, Temeke walikutwa na vipande 10 vyenye uzito wa kilo 13.85 na thamani ya dola 30,000 sawa na Sh milioni 65.4.

Ilidaiwa kuwa katika mashitaka ya tatu, Oktoba 27 mwaka jana washitakiwa wakiwa Tabata Kisukuru, walikutwa na vipande vinne vyenye uzito wa kilo 11.1 na thamani ya dola 15,000 sawa na Sh milioni 32.7.


Pia Oktoba 29 mwaka jana walikutwa na vipande 36 vya thamani ya Sh milioni 294.6.

Kesi imeahirishwa hadi Februari 21 mwaka huu.

Sauti za Busara inakuza tasnia ya Muziki Afrika kupitia jukwaa la ‘Movers & Shakers’

$
0
0
Tamasha la Sauti za Busara 2017 liko tayari kutikisa tasnia ya muziki wa Afrika kwa mfufulizo wa vikao vyenye lengo la kukuza mafunzo ya sanaa. Wataalamu kutoka Dar es Salaam na Dakar watakutanishwa na Movers & Shakers na kutoa nafasi kwa viongozi wa tasnia ya muziki kukutana na kubadilisha mawazo ya kitaalama.

Ijumaa kutakua na mada inayohusu fursa za mitandaoni, changamoto na vitisho vinavuyoigusa tasnia ya muziki. Kutoka kwenye jopo la wageni Jude Clark, mwanzilishi wa Joose Digital na Eddie Hatitye, Mkurugenzi wa Music in Africa wataongelea ujuzi wao kwenye maeneo ya hatimiliki, utandawazi, digitali, soko la muziki duniani na maswala ya teknolojia ya mitandao. 

Kwa kutambua uwezo wa kidigitali ni muhimu kwenye taaluma, wahudhuriaji watashuhudia nguvu ya mitandao ya kijamii ilivyo na nguvu ya kuunganisha mashabiki na wawekezaji, na kuongeza masoko kwa kutumia mitandao ya kijamii.

Wanamuziki hujikuta mstari wa mbele kwenye harakati maarufu kwa kutumia sauti zao kwa niaba ya wasiosikika. Wakati mwingine wasanii hujikuta hatarini baada ya ujumbe wa muziki wao kuwatuhumu wasikilizaji na wenye mamlaka. Msanii anawezaje kutumia uhuru wa kuongea na kufungiwa kitaaluma? 

Mada ya Jumamosi itaeleza mtazamo huru wa ubunifu Afrika, ripoti imeandikwa na waandishi 25 kutoka Nchi 14 na kuchapishwa kwa ushirikiano wa Artwatch Afrika kama sehemu ya mtandao wa Arterial, wenye lengo la kulinda uhuru wa kujieleza. Jopo litajumuisha Nelson Mandela wa kundi la Sarabi Kenya, Mamou Daffe – Mkurugenzi,Tamasha la sur le Niger, Mali na Dr. Omar Abdalla Adam –Mkurugenzi, Bodi ya Udhibiti Zanzibar.

Jumapili wasanii wa tamasha wanakaribishwa kwa maswali na majibu ya kina. Washiriki wanatarajiwa kuwa Pat Thomas and Kyekyeku kutoka Ghana, Roland Tchakounte kutoka Cameroun, Bi Mariam Hamdani kutoka Zanzibar and Sahra Halgan kutoka Somaliland. Hii ni sehemu ya kipekee kwa wasanii kutoka bara la Afrika na sehemu mbalimbali kukutana na kubadilishana mawazo. Mada hii itaongozwa na Journey Ramadhan, meneja wa Tamasha.

Movers & Shakers imeandaliwa kutengeneza nafasi za kipekee kwa wasanii na kuwajengea uwezo ili tasnia ya muziki Afrika Mashariki isonge mbele. Mada zitatolewa kila siku kuanzia saa 8:00 mchana mpaka saa 9:30 jioni . Hotel ya Monsoon. Kuingia ni kwa mwaliko tu. Hovyo wasanii na mameneja wa ndani wanahamasishwa kuwasiliana na waandaaji wa tamasha la Sauti za Sauti za Busara kama watapenda kushiriki.

Wafanyabiashara wa Pombe za Kienyeji Wanatakiwa Kuwa na Leseni

$
0
0


Na: Lilian Lundo – MAELEZO – Dodoma

Wafanyabiashara wa Pombe za Kienyeji wanatakiwa kuwa na leseni ya kufanya biashara hiyo ambayo hutolewa na Halmashauri.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Selemani Jafo ameyasema hayo, Mjini Dodoma alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Najma Giga juu ya Serikali imejipangaje kukabiliana na tatizo la ulevi wa kupita kiasi kwa pombe za kienyeji pamoja na sheria ya vileo ya mwaka 1969 kuwa ya zamani hivyo kutokidhi mabadiliko ya hali halisi ya vileo.

“Pombe za kienyeji zimeanishwa katika kifungu cha 2 cha tafsiri katika Sheria ya Vileo, Sura ya 77 ambapo kwa mujibu wa sheria hiyo, wafanyabiashara wote wanatakiwa kuwa na leseni ambayo inatolewa na Halmashauri,” alifafanua Jafo.

Aliendelea kwa kusema kuwa, biashara hiyo hairuhusiwi kufanyika katika muda wa kazi. Muda unaoruhusiwa kisheria ni kuanzia saa 12:00 jioni hadi saa 5:00 usiku kwa siku za Jumattu hadi Ijumaa na kuanzia saa 05:00 asubuhi hadi saa 06:00 usiku kwa siku za Jumamosi, Jumapili na Sikukuu.

Vile vile amesema kuwa unywaji wa pombe kupita kiasi ni tabia ya mtu ambayo inawezekana kabisa haitokani na mapungufu ya Sheria.

Hata hivyo Wakuu wa Mikoa na Wilaya wameagizwa kusimamia taratibu za uendeshaji wa biashara za vileo na kuchukua hatua kwa watumiaji na wafanyabiashara wanaobainika kukiuka Sheria hiyo.

Aidha amesema kuwa, endapo ipo haja ya kuifanyia marekebisho Sheria ya vileo, Serikali itakuwa tayari kupokea mapendekezo kwa eneo ambalo litaonekana kuwa na mapungufu ili kufanyiwa marekebisho kupitia Bunge.

Jafo ametoa wito kwa Watanzania wote kutumia muda wao kufanya kazi kwa bidii ili kujiletea maendeleo kwa ustawi wa Taifa zima. Aidha Serikali haitasita kuchukua hatua kwa wanywaji pombe wasiozingatia utaratibu pamoja na wazururaji wakati wa kazi.

Ada za Uhakiki wa Filamu Zipo kwa Mujibu wa Sheria

$
0
0
Na: Lilian Lundo – MAELEZO – Dodoma.

Ada za uhakiki wa filamu hapa nchini zipo kwa mujibu wa sheria na kanuni, ambapo gharama hizo hulipwa kwa nakala mama na baada ya hapo mtayarishaji huzalisha nakala kwa idadi anayohitaji.

Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Anastazia Wambura ameyasema hayo leo Bungeni, Mjini Dodoma alipokuwa akijibu swali la mbunge wa Mafinga Mjini Cosato Chumi juu ya Serikali ina mpango gani wa kuwapunguzia wasanii gharama za ukaguzi ambapo kwa hivi sasa gharama hizo ni shilingi elfu moja kwa dakika.

“Nchi yetu hutoza ada ambazo ni rafiki ukilinganisha na nchi nyingine, kwa mfano, Nigeria ambayo ni nchi iliyopiga hatua kubwa kwa upande wa filamu, hutoza filamu yenye urefu wa dakika 60 (filamu ya lugha asili) Naira 30,000 sawa na zaidi ya dola 150 ambayo ni sawa na Sh. 337,950 za Kitanzania na Kenya, ni sawa na Sh. 190,000,” alifafanua Anastazia Wambura.

Aliendelea kwa kusema kuwa Tanzania hutoza filamu za Kitanzania zenye urefu wa dakika 60 kwa Sh. 60,000 (sawa na Sh. 1,000 kwa dakika) ambapo gharama hizo ni sawa na asilimia 18 ya gharama za Nigeria na asilimia 32 ya Kenya.

Hivyo basi Tanzania imekuwa ikitoza ada hiyo ya uhakiki wa filamu kwa gharama nafuu na rafiki ukilinganisha na nchi nyingine Afrika.Akijibu swali la namna gani Bodi hiyo imejipanga kuhakikisha huduma zao zinatambulika nchi nzima tofauti na sasa ambapo wasanii wachache ndiyo wanafahamu wajibu na majukumu ya Bodi hiyo, Wambura amesema kwamba Bodi hiyo imeendelea kujitangaza kwa wadau kupitia shughuli mbalimbali za kitaifa na Kimataifa kama vile kushiriki katika maonesho ya Sabasaba.

Vile vile bodi hiyo imekuwa ikishiriki katika wiki ya Vijana na Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru pamoja na Jumuiya ya Afrika Mashariki Utamaduni Festivals (JAMAFEST). Pia hutumia vyombo mbalimbali vya habari kama vile TBC1, E-FM, Clouds media pamoja na magazeti mbalimbali kueleza watanzania kazi zinazofanywa na Bodi hiyo.

Aidha Bodi hiyo imekuwa ikifanya warsha za kuwajengea wadau wake weledi katika masuala ya filamu sehemu mbalimbali ikiwemo mikoani na wilayani ikiwa ni moja ya maeneo ya kujitangaza.

AIRTEL NA TFF YAIPONGEZA SERIKALI KUFANIKISHA SERENGETI BOYS KUFUZU AFCON

$
0
0



Na Zainab Nyamka  Globu ya Jamii

Kampuni ya simu ya Airtel sambamba na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini Jamal Malinzi wamewataka wadau kujitokeza kuisapoti timu ya vijana ya chini ya miaka 17 Serengeti Boys ambao wamefanikiwa kwenda kombe la Mataifa Afrika kwa vijana (AFCON) nchini Gabon mwezi Mei mwaka huu.

Malinzi alisema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na kupata nafasi ya ushiriki kwa vijana hao baada ya timu ya Congo Brazaville kushindwa kumpelekea mchezaji wao Langa ambae alisadikiwa kuwa na umri mkubwa zaidi na kuchezeshwa kwenye mashindano ya vijana.

Malinzi amewataka wadau kwa pamoja kusaidiana nao katika kuaindaa timu ya vijana kwani hakika mashindano haya yanahitaji kiasi kikubwa cha fedha takribani dola laki tano (500,000) ili timu iweze kuweka kambi nje ya nchi na hata kupata vifaa vya kutosha na vya kisasa.

Meneja wa Mawasiliano  Airtel, Jackson Mmbando amesema kuwa wanawapongeza TFF kwa hatua kubwa waliyofikia ya kuifikisha hapa Serengeti Boys ila bado vijana hawa wanahitaji kupata sapoti kutoka kwa wadau na seriakali kwa ujumla.

Mmbando amesema kuwa,  vijana hawa wanahitaji kuangaliwa kwa umakini zaidi na kujengwa kisaikolojia ili waweze kufanya vizuri kwani waliona walishaondolewa  kwenye michuano hiyo.

"Vijana hawa wanahitaji sapoti kutoka kwa wadau ili waweze kufanikisha safari yao ya Gabon mwezi wa tano na sisi kama airtel tutasaidia katika kuitangaza timu hiyo,"amesema Mmbando

Airtel wamekuwa wadau wakubwa sana wa kukuza soka la vijana kwa kuanzisha mashindano ya Airtel Rising Star ambapo hivi karibuni waliweza kufanya usaili wa vijana na wengine wakiwa tayari kwenye kikosi cha vijana wa Serengeti Boys.
 Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu TFF akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na kufuzu kwa Serengeti kwenda Mataifa Afrika kwa vijana nchini Gabon, Kulia ni Meneja Mahusiano wa Airtel Jackson Mmbando.
Meneja wa Mahusiano Airtel Jackson Mmbando akizungumza na waandishi na kuwataka wadau kujitokeza kuisapoti Serengeti Boys ili waweze kufanya vizuri kwa mashindano ya Mataifa Afrika kwa Vijana nchini Gabon

MUHIMBILI YAADHIMISHA SIKU YA KIFAFA DUNIANI WILAYANI MKURANGA

$
0
0
  Profesa William Matuja wa Chuo Kikuu Kishiriki Cha Sayansi na Tiba (MUHAS) na Rais wa Chama Cha Wagonjwa wa Kifafa nchini (TEA) akiwakumbusha madaktari na wauguzi mambo yanayosababisha kifafa na kuwataka waongeze bidii katika kutoa huduma bora kwa wagonjwa hao.
HAO 1
Madaktari na wauguzi wakimsikiliza Profesa Matuja leo katika Hospitali ya Wilaya ya Mkuranga ambako maadhimisho yamefanyika.
HAO 2
 Wakazi wa Wilaya hiyo wakimsikiliza Profesa Matuja leo.
HAO 5
 Dk Njenje akitoa elimu kwa wananchi wa Mkuranga kuhusu ugonjwa wa kifafa na jinsi ya kutibu mtu mwenye ugonjwa huo leo.
HAO 6
Dk Yusuf  S. Jammagerwalla akizungumza na wananchi wa Mkuranga leo kwamba waache kuhusisha kifafa na imani za kishirikina ili kuokoa maisha ya watu wenye ugonjwa huo. Amewasisitiza kuwapeleka hospitali mapema kwa ajili ya kupatiwa matibabu.HAO 4
 Wakazi hao wakimsikiliza Dk Yusuf leo.
Picha na John Stephen, Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).
…………
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) Leo imeadhimisha siku ya kifafa duniani kwa kutoa elimu ya ugonjwa huo kwa madaktari, wauguzi na wakazi wa Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani.
Madaktari wa Muhimbili wameadhimisha siku hiyo ambayo hufanyika Februari 8 kila mwaka kwa kutoa elimu kwa jamii na wataalamu ili kupunguza vifo kwa watu wenye kifafa nchini.
Rais wa Chama Cha Wagonjwa wa Kifafa nchini (TEA), Profesa William Matuja amesema kwamba ugonjwa huo unatibika na amewataka wakazi hao kuacha imani za kishirikina na badala yake amewataka kuwapeleka wagonjwa hospitali mapema.
“Wengi wana imani potofu kwamba mtu mwenye kifafa, kimesababishwa na mashetani, lakini si kweli kwani karne ya 19 wanasayansi walibaini kuwa mshutuko wa ubongo ndio unasababisha kifafa kutokana na sababu mbalimbali,” amesema Profesa Matuja.
Naye Dk Njenje wa Hospitali ya Taifa Muhimbili amesema mtu anapata kifafa wakati anapozaliwa endapo ataumia sehemu ya kichwani, kukosa hewa au mtoto kuumizwa kichwani atapata  degedege.
“Mtu mzima anaweza kupata degedege endapo sukari yake itakuwa imeshuka sana na ukitibu kisukari anapona,”amesema Dk Njenje.Dk Njenje amesema kwamba ili kubaini mtu ana kifafa, lazima degedege itokee zaidi ya saa 24, degedege itokee zaidi ya mara mbili au mara kwa mara na wakati mwingine inatokea bila mtu kuwa na homa.

sakata la madawa ya kulevya:13 waachiwa kwa dhamana,huku Wema Sepetu akiendelea kusota Rumande

$
0
0
Na Karama Kenyunko,Globu ya Jamii 

Msanii Wema Abraham Sepetu (28), Ameendelea kusota Rumande huku wasanii wenzake 13 aliokuwa akishikiliwa nao kituoni hapo wameachiwa kwa dhamana na kutakiwa kuwa chini ya uangalizi wa polisi na mahakama kwa kipindi cha miaka minne. 

Miss Tanzania 2006 huyo anaendelea kushikiliwa kwa zaidi ya saa 72 kwa sasa kwa tuhuma za kukutwa msokoto mmoja wa bangi na kusubiri uchunguzi kukamilika . 

Taarifa kutoka chanzo makini cha habari kinasema wema ad anashikiliwa kwa uchunguzi Zaidi na muda wowote wiki hii anaweza kufikishwa mahakamani. 

Katika kesi hiyo iliyosikilizwa leo katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ilisikilizwa na mahakimu wawili ambapo watuhumiwa nane wa mwanzo walipewa dhamana ya milioni kumi (10,000,000) kila mmoja na watakuwa chini ya uangalizi wa polisi kwa kipindi cha mwaka mmoja. 

Watuhumiwa hao ni Hamidu Salum Chambuso (Dogo Hamidu), Rajabu Salum, Romeo George Bangura (Romy jons), Cedou Madigo, Khalid Salum Mohamed (TID), Johana Johanenes Mathysen (Director Joan), Rachael Josephat (Rachel) na Anna Patric Kimario (Tunda). 

Mbele ya Hakimu Mkazi , Huruma Shahidi washtakiwa walitakiwa kujibu maombi ya waleta maombi ambao ni upande wa Jamhuri yaliyowasilishwa chini ya kiapo kilichoapwa na Mrakibu Msaidizi wa Polisi ASP Dennis Mujumba wa kitengo cha dawa za kulevya. 

Sehemu ya kiapo hicho inadai kuwa wajibu maombi hao wanajihusisha na madawa ya kulevya hivyo kutokana na tabia hizo kuwaachia huru katika jamii bila kuwadhibiti kunaweza kusababisha uvunjifu wa amani katika jamii. 

Katika maombi hayo,upande wa Jamhuri uliiomba mahakama iwaamuru wajibu maombi (wasanii hao), kuweka dhamana ya kuwa na tabia njema kwa kipindi cha miaka mitatu na kuwamuru kuripoti katika kituo cha polisi cha kati kwa mwezi mara mbili kwa ajili ya kuangalia mwenendo wa tabia zao. 

Aidha Jamhuri waliiomba mahakama itoe amri yoyote nyingine itakayowafanya wajibu maombi hao kuwa na tabia njema na kuachana na kujihusisha na madawa ya kulevya. 

Upande wa utetezi uliokuwa ukiongozwa na wakili Albert Msando ulidai kuwa kifungu cha sheria 73B ambacho wasanii hao wameshtakiwa nacho hakuna sehemu inayoonyesha makosa ya uvunjifu wa amani na kwamba mtu anayejihusisha na madawa ya kulevya hawezi kuvunja amani. 

Akitoa amri, Hakimu Shahidi amewaamuru wasanii hao kuwa chini ya uangalizi wa mahakama kwa muda wa mwaka mmoja, wametakiwa kuwekewa dhamana ya kiasi cha milioni kumi (10,000,000) kila mmoja na pia wawe chini ya ulinzi wa polisi kwa ili waweze kujirekebisha na iwapo watakiuka watarudhishwa mahakamani. 

Aidha hakukubaliana na maombi ya kuwataka wasanii hao walipoti polisi kila mwezi mara mbili akisema kuwa watakuwa wakijiandaa. 

Wasanii Ahmed Hashim (Petitiman), Said Masoud Linnah (Said Alteza), Nassoro Mohamed Nassoro Bakar Mohamed Khelef and Lulu Abbas Chalangwe (Lulu diva) walifikishwa mbele ya Hakimu Mfawidhi Cyprian Mkeha. 

Katika amri zake, aliwataka wasanii hao kuweka dhamana ya kiasi cha shilingi milioni ishirini (20,000,000) kila mmoja na kutojihusisha na makosa ya dawa za kulevya kwa kipindi cha miaka mitatu na wanatakiwa kuripoti Kituo Kikuu cha Kati kwa mwezi mara mbili pamoja na kutakiwa wabadilike na kuacha kabisa matumizi ya dawa hizo. 

Hadi Globu ya Jamii inaondoka katika viwanja vya mahakama hiyo, wasanii hao walikuwa wamekamilisha taratibu zote za mahakama na walikuwa wakisubiri kurudishwa polisi kumalizia taratibu kabla hawajaachiwa huru. 
Watuhumiwa wa kesi ya dawa ya za kulevya wakishushwa ndani ya gari ya polisi katika mahakama ya hakimu mkazi kisutu.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Khalid Mohamed akiingia katika mahakama ya hakimu mkazi kisutu.
Watuhumiwa wa kesi ya dawa ya za kulevya wakiingizwa katika mahakama ya hakimu mkazi kisutu jijini Dar es Salaam.
Mama yake Diamond akiwa na familia yake wakifatilia kesi ya ndugu yao yao Peti Man wakuache
Petman wakuache akiwa na watuhumiwa wenzie akiwa katika mahakama ya hakimu mkazi kisutu

Wasanii wa muziki wa Bongo Fleva wakiwa katika mahakama ya hakimu mkazi kisutu.
Msanii wa bongo fleva Rachel akiwa na wenzie katika mahakama ya Hakimu mkazi kisutu

WAZIRI LUKUVI AWATAKA VIONGOZI WA MIKOA YA TANGA NA MANYARA KUTEKELEZA AGIZO LA WAZIRI MKUU

$
0
0
Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi,William Lukuvi akizungumza  kwenye kikao cha pamoja baina yake na viongozi wa mikoa ya Tanga na Manyara kuhusiana na mgogoro wa mipaka uliopo kati ya wilaya za kilindi na kiteto ili kuona namna ya kuumaliza
 Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella akizungumza kwenye kikao hicho.
 Mkuu wa Mkoa wa Manyara,Dokta Joel Bendera akizungumza kwenye mkutano huo kulia ni Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga,Monica Kinala 
Baadhi ya wenyeviti wa halmasahuri zote mbili na wakuu wa wilaya za Kiteto na Kilindi wakifuatilia kikao hicho
Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Kilindi,Sauda Mtondoo akifuatilia majadiliano hayo
WAZIRI wa ardhi Nyumba na maendeleo ya makazi William  Lukuvi amewataka viongozi kutoka Mkoa wa Manyara na Tanga kutekeleza agizo la Waziri Mkuu la kumaliza mgogoro wa mpaka katika ya Wilaya ya Kilindi na Kiteto kwa kuhakiki upya mpaka huo kupitia GN namba 65 ya mwaka 1961.

Lukuvi aliyazungumza hayo jana Mkoani hapa alipokutana na viongozi
  kutoka Mikoa ya Tanga na Manyara kuhusiana na mgogoro uliodumu kwa miaka mingi kati ya Wilaya hizo mbili ambapo aliwataka washirikiane kuhakikisha mgogoro huo unamalizika kama Waziri Mkuu alivyoagiza pindi alipofanya zira yake  mkoani hapa.

Aidha alisema kupitia Wizara ya ardhi imeteuwa wataalamu wa ardhi
  ambao hawatatoka kati ya Mikoa yenye mvutano wa mgogoro huo ili kujenga imani kwa wananchi na watakuwa na jukumu la kuhakiki upya mpaka huo kwa manufaa ya wananchi wa pande zote mbili.

"Timu ya wataalamu kutoka wizara yangu imekwishaundwa kwa kufanya kazi
  hiyo mategemo ya utekelezaji wa majukumu hayo tunatarajia kuanza rasmi machi 1 mwaka huu na zoezi hili litadumu kwa mwezi mmoja tu na wala hakuna ubabaishaji"Alisema Lukuvi.

Alisema hakuna mpaka mpya utakaokwenda kupimwa kati ya Wilaya hizo
  mbili zaidi ya kuhakiki ule wa awali ambao unatokana na ramani ya mwaka 1961,zoezi hili la uhakiki lazima wananchi na viongozi watambue kuwa linafanyika kwa  mara ya tatu na litakuwa la mwisho.

Pia aliwataka viongozi wote kuanzia ngazi ya mkoa mpaka Kijiji
 
kushiriki vema katika zoezi hilo ili kuweza kujadiliana hasa pale
panapotokea mapungufu na waache kutatua mgogoro huo huku wakiwa na matakwa yao binafsi na kufanya hivyo hakutamaliza mgogoro huo zaidi ya kuuwongeza.

"Kama kuna viongozi wanamatakwa yao basi watambue hawatapata nafasi na
  tayari tulishapokea agizo kutoka Waziri Mkuu na kinachotakiwa hapa ni utekelezaji wa kumaliza mgogoro huo"Alisema.

Kwa upande wake Mkuu wa mkoa Tanga Martin Shigela alisema jukumu kubwa
  lililopo mbele yao ni kutoa ushirikiano kwa timu iliyoundwa na Wizara hiyo na kuhakikisha wanafanikiwa kumaliza mgogoro huo kwa wakati kama Waziri alivyoagiza.

Nae Mkuu wa Mkoa wa Manyara Joel Bendera alisema lazima viongozi
  washirikiane kwa pamoja kutatua mgogoro huo ambao umekuwa ni tatizo kwa Wilaya hizo mbili na kupongeza hatua ya Serikali ya uhakiki upya hasa kwa kufuata GN ya namba 65 ya mwaka 1961 kama alivyoagiza Waziri Mkuu na si vinginevyo.

Ikumbukwe siku kadhaa zilizopita Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alifanya
  ziara Wilayani Kilindi katika Kijiji cha Mafisa na kuzungumza na wanachi Kijijini hapo kuhusiana na mgogoro huo na kutoa maagizo kwa viongozi wa kuchaguliwa kuacha kutumia nafasi zao vibaya kuongoza kwa mihemko au ushabiki kwa kuwa kufanya hivyo kunapelekea wananchi kufuata ushabiki na kuvunja sheria zilizopo.

Majaliwa alisema katika ziara yake hiyo kuwa Aidha alisema baadhi ya
  viongozi wa kisiasa na Serikali kwa kutokuwa wa kweli mbele ya wananchi kuhusiana na mgogoro huo na wanajaribu kufanya maamuzi kwa ajili ya maslahi yao ya kujiaminisha mbele ya wananchi hao.

Alisema lazima ramani ya mwaka 1961 ifuatwe na viongozi waache kuwa na
  agenda zao za siri na kuwadanganya wananchi kwa kuanza kurudia kupima mpaka huo mara kwa mara bila ya kupata majibu sahihi ramani na huu ni muda wa kuwael3za ukweli wananchi

"Ramani ipo ya mwaka 1961 na najiuliza sana hivi hao wanaokuwa na
  tabia ya kurudia kupima pima mara mbili agenda yao ni nini,huu si udanganyifu kwa wananchi?"Alihoji Majaliwa.

Alisema kuananzia sasa GN itakayotumika ni ile namba 65 ya mwaka
  1961,zaidi wanachotakiwa wataalamu kukifanya ni kuimarisha mpaka huo kwa kuwashirikisha  viongozi wa Serikali,wanasiasa na wananchi ili kuweka mustakabali mzuri juu ya mpaka huo
Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha Blog

Waziri Mahiga apokea hati za utambulisho za mabalozi wa Cuba, Zambia na Bundi

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akisalimiana na Balozi mteule wa Zambia nchini Tanzania Mhe.Benson Keith Chali alipowasili Wizarani Jijini Dar es Salaam kukabidhi nakala za hati za utambulisho
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akipokea nakala za hati za utambulisho kutoka Balozi Mteule wa Cuba nchini Tanzania Mhe.Lucas Domingo Harnandez Pelledo
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Augustine Mahiga (Mb.) akipokea nakala za hati za utambulisho kutoka kwa Balozi mteule wa Burundi Mhe. Gervais Abayeho alipoziwasilisha Wizarani Jijini Dar es Salaam.

SERIKALI INAENDELEA KUDHIBITI MATUMIZI HOLELA YA FEDHA ZA KIGENI

$
0
0
Serikali imesema kuwa katika kudhibiti matumizi holela ya fedha za kigeni, Benki Kuu kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania imeongeza usimamizi katika maduka ya kubadilishia fedha za kigeni ambapo taarifa za kila muamala wa fedha za kigeni unaofanywa zinapaswa kuoneshwa.

Kauli hiyo imetolewa Bungeni leo na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt Ashatu Kijaji, wakati akijibu maswali ya Mbunge wa Igunga Mhe. Dalaly Peter Kafumu aliyetaka kupewa ufafanuzi juu ya Kwanini Serikali isidhibiti matumizi holela ya dola nchini ili kupunguza utakasishaji wa fedha na kuimarisha ukuaji wa uchumi kama zinavyofanywa nchi nyingi duniani.

Aidha, Dkt Kijaji alifafanua hatua zimechukuliwa pia kuhakikisha kuwa miamala ya fedha za kigeni inayofanywa na mabenki ni ile inayohusu shughuli za kiuchumi tu ili kulinda thamani ya shilingi. 

Vilevile, tamko na mwongozo uliotolewa na Serikali mwaka 2007, ulieleza kuwa bidhaa na huduma zinazowalenga watalii au wateja wasio wakazi wa Tanzania, bei zake zinaweza kunukuliwa kwa sarafu mbili, yaani shilingi ya kitanzania na sarafu ya kigeni na malipo kufanyika kwa sarafu ambayo mlipaji atakuwa nayo. Pia, mkazi yeyote wa Tanzania asilazimishwe kulipia bidhaa au huduma yoyote hapa nchini kwa fedha za kigeni.

“Msingi wa kuruhusu soko huru la fedha za kigeni hapa nchini ni hatua ya makusudi ambayo ilichukuliwa na Serikali ili kuiwezesha nchi kuondokana na hali ya kuadimika kwa fedha za kigeni ilikuwa dola za Kimarekani milioni 4,093.7 wakati amana za fedha za kigeni za wakazi wa Tanzania zilikuwa dola za Kimarekani milioni 2,933.1 na rasilimali za fedha za kigeni za mabenki zilikuwa kiasi cha dola za Kimarekani milioni 1,021.1” alisema Dkt. Kijaji.

Dkt Kijaji ameeleza kuwa Tanzania ina urari wa biashara ya nje ambao umetokana na sera huru za kigeni, ambazo zimechangia kuimarisha uchumi kwa zaidi ya miaka 10 iliyopita, wastani wa ukuaji wa uchumi wa Taifa letu katika kipindi cha miaka kumi iliyopita ulikua ni asilimia 7, ikiwa ni wastani wa juu sana ikilinganishwa na nchi nyingine duniani. 

“Mfano, wastani wa ukuaji wa uchumi wa nchi za kusini mwa Jangwa la Sahara ni asilimia 5.4 katika kipindi hicho wakati ule wa nchi zinazoibukia kiuchumi ulikua ni asilimia 5.8” alisisitiza Dkt. Kijaji

Alisema kuwa njia zinazotumika kutakatisha fedha ni pamoja na kuziingiza haramu kwenye taasisi za fedha na kuziwekeza katika rasilimali halali kama ardhi na nyumba. Baadhi ya mambo yanayowapatia wahalifu fedha haramu ni pamoja na biashara ya dawa za kulevya, rushwa, ujangili, ujambazi, ukwepaji kodi n.k. Aidha fedha zinazotokatana na shughuli za kihalifu zinaweza kuwa shilingi za Kitanzania, dola za Kimarekani au fedha nyingine yoyote ile. 

Naibu Waziri huyo wa Fedha na Mipango amesema ziko kanuni ambazo zinafuatwa na vyombo vya fedha ili kuzuia utakatishaji wa fedha zote zilizopatikana kutoka vyanzo haramu na sio dola pekee huku akibainisha kuwa Benki Kuu ya Tanzania ina jukumu la usimamizi wa taasisi za fedha, hufuatilia mabenki ili kuhakikisha kuwa kanuni hizo zinafuatwa.

MAKAMU WA RAIS MAMA SAMIA SULUHU HASSAN ASHIRIKI HITIMISHO LA MKUTANO WA KUWEZESHA WANAWAKE KIUCHUMI MJINI DUBAI

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Profesa  Alicia Giron ambaye ni Profesa na Mtafiti wa uchumi katika Chuo Kikuu cha Mexico (UNAM) wakati wa hitimisho la mkutano wa kuwawezesha wanawake kiuchumi mjini Dubai. 
SUZANA
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na mwezeshaji Susan Monahan wakati wa hitimisho la mkutano wa kuwawezesha wanawake kiuchumi mjini Dubai. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Hitimisho la  mkutano wa kuwawezesha wanawake kiuchumi mjini Dubai ukiendelea leo (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Wa pili kushoto ni Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan sambamba na washiriki wengine wakifutilia yaliyokuwa yakijiri kwenye  Hitimisho la  mkutano wa kuwawezesha wanawake kiuchumi mjini Dubai ukiendelea leo (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).

DAWA YA MSONGAMANO WA MBAGALA YAPATIKANA-WAZIRI MKUU

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na viongozi wa wilaya za Mkuranga na Temeke, Ofisini kwake jijini Dar es salaam Februari 7, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifafanua jambo mbele ya viongozi wa wilaya za Mkuranga na Temeke, Ofisini kwake jijini Dar es salaam Februari 7, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka viongozi wa Wilaya za Temeke na Mkuranga kuangalia namna ya kupunguza msongamano uliopo katika eneo la Mbagala.

Moja ya hatua alizowashauri kuchukua ni pamoja na kuhamisha kituo cha mabasi ya mikoa ya kusini ya Lindi, Mtwara na Ruvuma kutoka Temeke hadi Mkuranga.Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Jumanne, Februari 7, 2017) alipokutana na viongozi wa wilaya hizo Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kutafua njia za kuondoa msongamano huo.

Amesema kwa sasa hakuna namna ambayo wataweza kuondoa msongamano huo zaidi ya kuhamishia kituo cha mabasi ya mikoa ya kusini wilayani Mkuranga.Waziri Mkuu amesema eneo la Mbagala kwa sasa lina msongamano mkubwa ambao ni lazima Serikali ichukue hatua za haraka za kuuondoa.

“Ikiwezekana mabasi ya mikoa ya kusini yaishie Mkuranga, hivyo kirikianeni kutafuta eneo la kujenga kituo kikubwa cha kisasa cha mabasi,” amesema.Amesema kituo hicho watakachokijenga kiwe na uwezo wa kuhudumia mabasi yote yatokayo mikoa ya kusini na kituo cha Mbagala kiwe cha daladala za kawaida.

Pia Waziri Mkuu amesema kukamilika kwa mradi wa ujenzi wa kituo hicho kutawezesha kuongeza mapato ya Halmashauri ya wilaya ya Mkuranga.Aidha Waziri Mkuu amewataka viongozi hao kwenda kujadiliana katika vikao vya mabaraza ya Madiwani juu ya mkakati huo na kisha kumpelekea taarifa ifikapo Februari 15 mwaka huu.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Mkuranga, Bw. Filberto Sanga amesema wazo hilo ni zuri na wilaya yake ina maeneo ya kutosha kujenga miundombinu hiyo.

“Ni kweli wilaya ya Temeke imeelemewa kwa maana ya maeneo kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya maendeleo na haina pa kupumulia zaidi ya Mkuranga , hivyo tupo tayari kushirikiana nao,” amesema.Wakati huo huo, Bw. Sanga ameiomba Serikali itakapoanza awamu ya tatu ya ujenzi wa mradi wa mabasi ya mwendo kasi ufike hadi Mkuranga mjini badala ya kuishia Vikindu.

Amesema kwa sasa wilaya yake ina viwanda 67 ambavyo kati yake vipo vinavyofanya kazi na vingine vikiwa katika hatua mbalimbali za ujenzi, hivyo mabasi hayo yatarahisisha usafiri kwa wafanyakazi.Naye Mkuu wa Wilaya ya Temeke Bw. Felix Lyaniva amesema amefurahishwa sana na mawazo hayo ya kuhamisha kituo cha mabasi cha Mbagala kwani katika vitu vilivyokuwa vinamnyima usingizi ni pamoja na msoingamano wa mabasi na wafanyabiashara wadogo wadogo katika eneo hilo.


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMANNE, FEBRUARI 7, 2017.

WIZARA YA HABARI YAZINDUA PROGRAMU YA WADAU TUZUNGUMZE

DKT SHEIN AZINDUA JENGO LA MAHAKAMA YA WATOTO

$
0
0




Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifungua pazia kuashiria uzinduzi wa Mahkama ya Watoto iliyopo Mahonda Wilaya ya Kaskazini B Unguja leo (kulia)Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe,Omar Othman Makungu.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akifuatana na Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe,Omar Othman Makungu (kulia) wakati alipotembelea jengo la Mahkama ya Watoto liliopo Mahonda Wilaya ya Kaskazini B,Unguja leo baada ya kulizindua rasmi,.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe,Omar Othman Makungu (katikati) wakitoka nje ya Jengo la Mahkama ya Watoto liliopo Mahonda Wilaya ya Kaskazini B,Unguja baada ya kulizindua rasmi leo.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe,Omar Othman Makungu wakiteta jambo wakati wa uzinduzi wa Jengo la Mahkama ya Watoto liliopo Mahonda Wilaya ya Kaskazini B,Unguja uliofanyika rasmi leo.

Wanafunzi wa Skuli ya Mahonda Wilaya ya Kaskazini B,Unguja ni miongoni mwa wananchi waliohudhuria katika sherehe za uzinduzi wa Mahkama ya Watoto,ambapo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) akiwa mgeni rasm.

Watoto wa Kijiji cha Mahonda Wilaya ya Kaskazini B,Unguja wakiwa katika sherehe za uzinduzi wa Mahkama ya Watoto ambapo imezuliwa leo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein.

Baadhi ya Viongozi na Wananchi waliohudhuria katika sherehe ya uzinduzi wa Mahkama ya Watoto,Kijiji cha Mahonda Wilaya ya Kaskazini B,Unguja,iliyozinduliwa leo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani).

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia)akisalimiana na Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe,Omar Othman Makungu alipowasili katika sherehe ya uzinduzi wa Jengo la Mahkama ya Watoto liliopo Mahonda Wilaya ya Kaskazini B,Unguja leo

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia)akisalimiana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Katiba,Sheria,Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe,Haroun Ali Suleiman (katikati)alipowasili katika sherehe ya uzinduzi wa Jengo la Mahkama ya Watoto liliopo Mahonda Wilaya ya Kaskazini B,Unguja leo,(kushoto) Waziri wa Kazi,Uwezeshaji,Wazee,Vijana,Wanawake na Watoto Mhe,Moudline Cyrys Castico.


Mwakilishi wa UNICEF katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bibi,Maniza Zaman akitoa salama zake kwa Wananchi na Viongozi wakati wa Uzinduzi wa Jengo la Mahkama ya Watoto liliopo Mahonda Wilaya ya Kaskazini B,Unguja leo.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Katiba,Sheria,Utumushi wa Umma na Utawala Bora Mhe,Haroun Ali Suleiman alipokuwa akizungumza machache na kumkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein kutoa hutuba yake kwa Wananchi wakati wa Uzinduzi wa Jengo la Mahkama ya Watoto liliopo Mahonda Wilaya ya Kaskazini B,Unguja uliofanyika leo

Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe,Balozi Seif Ali Iddi (kulia) na Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar Hamdani Omar Makame wakiwa katika sherehe za Uzinduzi wa Jengo la Mahkama ya Watoto liliopo Mahonda Wilaya ya Kaskazini B,Unguja leo.

Wasanii wa wakiigiza mchezo wa udhalilishaji Mtoto wa Skuli wakati wa sherehe za Uzinduzi wa Jengo la Mahkama ya Watoto liliopo Mahonda Wilaya ya Kaskazini B,Unguja leo,lililozinduliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akitoa hutuba yake kwa Wananchi wakati wa Uzinduzi wa Jengo la Mahkama ya Watoto liliopo Mahonda Wilaya ya Kaskazini B,Unguja uliofanyika leo,(kulia) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Katiba,Sheria,Utumushi wa Umma na Utawala Bora Mhe,Haroun Ali Suleiman na (kushoto) Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe,Omar Othman Makungu,[Picha na Ikulu.] 07/02/2017.

MNADA WA PILI WA KIMATAIFA KWA MADINI YA TANZANITE KUFANYIKA JIJINI ARUSHA, TAREHE 9-12, FEBRUARI 2017.

$
0
0
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA NISHATI NA MADINI

MNADA WA PILI WA KIMATAIFA KWA MADINI YA TANZANITE KUFANYIKA JIJINI ARUSHA, TAREHE 9-12, FEBRUARI 2017.

Serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini, inatoa Taarifa kwa Umma kuwa, itaendesha Mnada wa Pili wa Kimataifa kwa Madini ya Tanzanite ghafi na yaliyokatwa kuanzia tarehe 9 hadi 12, Februari 2017. Mnada huu utaendeshwa katika Kituo cha Jimolojia Tanzania (TGC) kilichopo Jijini Arusha. Kampuni mbalimbali za ndani ya nchi zitaleta madini kwa ajili ya kuuzwa kwa wanunuzi kutoka mataifa mbalimbali Duniani.

Mnada huu ni muendelezo wa mnada wa kwanza wa madini ya Tanzanite uliofanyika mwezi Agosti, 2016 ambapo jumla ya gramu 318,033.17 na Karati 3,274.70 za Tanzanite ziliuzwa na jumla ya Kampuni 43 kutoka mataifa mbalimbali Duniani zilihudhuria.

Lengo la mnada huu ni kuboresha ukusanyaji wa mapato ya Serikali katika Sekta ya Madini kwa kuhakikisha soko la uhakika kwa wauzaji wa madini hayo.

Imetolewa na:

KATIBU MKUU
WIZARA YA NISHATI NA MADINI
7 FEBRUARI, 2017


TAARIFA YA SERIKALI TOKA BUNGENI LEO JIONI 07/02/2017

VIJUSO VYA MAGAZETI YA LEO JUMATANO FEBRUARI 8, 2017

MKUU WA MKOA WA MJINI MAGHARIBI ATEMBELEA MAANDALIZI YA TAMASHA LA SAUTI ZA BUSARA 2017 MJINI ZANZIBAR

$
0
0
Mwenyekiti wa Tamasha la Sauti za Busara Zanzibar  Simai Mohammed Said akitowa maelezo ya kukamilika kwa maandalizi ya Tamasha hilo kwa Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe Ayoub Mohammed Mahmoud alipotembelea Ngome Kongwe kujionea maendeleo ya matayarisho ya Tamasha hilo litakalohudhuriwa na Wasanii wapatao 400 kutoka Zanzibar, Tanzania Bara na Nje ya Tanzania kwa kutowa burudani ya Sanaa yenye ubunifu kwa kutumia Tamaduni za Kiafrika. Hapo ni  Jukwaa la amphitheatre.
Mwenyekiti wa Tamasha la Busara Zanzibar Simai Mohammed Said akitoa maelezo kwa Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud, wakati alipofanya ziara kutembelea na kujionea maandalizi ya Tamaasha hiyo wakiwa katika Jukwaa kubwa litakalotumika kwa Wasanii kutowa burudani wakati wa maonesho mbalimbali ya Tamasha kwa Wasanii.
Fundi Mkuu wa Tamasha la Busara Zanzibar Hamza Omar Abbas akimuonyesha vyombo vya muziki vitakavyowawezesha Wasanii wakati wakiwa jukwaani wakiimba kujisikia wenyewe sauti zao wakati wa show zikiendelea. 
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe Ayoub Mohammed Mohamoud akizungumza na wafanyakazi wa Tamasha la Sauti za Busara Zanzibar alipofika kutembelea kujionea maandalizi ya Tamasha hilo na kuwataka kuitangaza Zanzibar kwa wageni wanaotembelea kujionea maonesho ya Tamasha hilo la Tamaduni za Kiafrika kuwakutanisha wasanii mbalimbali kutoka katika Nchi za Afrika.
Wafanyakazi wa Tamasha la Sauti za Busara wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe Ayoub Mohammrd Mahmoud akitowa nasaha zake kwa wafanyakazi hao wakati alipofika kutembelea maandalizi ya Tamasha hilo linalotarajiwa kufanyika keshokutwa Zanzibar tarehe 9-2-2017 

Sitakubali Tanesco Kupandisha Bei ya Umeme - Prof. Muhongo.

$
0
0
Na: Lilian Lundo – MAELEZO - Dodoma

Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo amesema kuwa msimamo wake juu ya  Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania (Tanesco) kutopandisha gharama za umeme kwa wateja wake upo palepale.

Prof. Muhongo ameyasema hayo leo Bungeni, Mjini Dodoma alipokuwa akijibu hoja zilizowasilishwa na wabunge  juu ya zuio la upandishaji bei ya umeme kwa shirika hilo wakati wa uwasilishwaji wa taarifa ya shughuli za Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini katika kipindi cha mwaka  2016/2017.

“Haiwezekani wakapandisha bei ya umeme wakati kuna watu ndani ya Shirika wanamiliki hadi hoteli nne, wakijaza lita 20 za mafuta  katika magari wanaandika lita 50 na kila mwisho wa mwaka wanagawana milioni 50 kama ‘bonus’,” alifafanua Prof. Muhongo.

Ameendelea kwa kusema kuwa Shirika hilo linadaiwa kiasi cha shilingi Bil. 820, katika deni hilo kiasi cha shilingi Bil.320 bado hazijachambuliwa. Hivyo shirika hilo haliwezi kujiamulia kupandisha gharama ya umeme wakati huo huo wakiwa bado hawajachambua baadhi ya madeni yao.

Aidha Prof. Muhongo amesema kuwa, Shirika hilo linahitaji kiasi cha Dola Bil. 12 kwa ajili ya uwekezaji ili ifikapo mwaka 2020 kiasi cha Mg 5000 za umeme ziweze kuzalishwa.

Hata hivyo, Prof. Muhongo amesema amekwisha anza kufanya mazungumzo na Benki ya Dunia ili kuona kama wataweza kufadhili kiasi hicho cha fedha ili kiweze kuwekezwa katika Shirika hilo.

Aliendelea kwa kusema kuwa Shirika hilo linahitaji mabadiliko ya hali ya juu ili kulifanya kuwa la kisasa na kuendana na dhima ya nchi ya  uchumi wa viwanda ambao kwa asilimia kubwa unahitaji nishati hiyo ya umeme.

WAZIRI MHAGAMA: VITA DHIDI YA DAWA ZA KULEVYA NI YETU SOTE

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama amesema kuwa mapambano ya kukabiliana na tatizo la Dawa za Kulevya ni jukumu la kila mwananchi na wala sio suala la kuiachia Serikali peke yake.

Ameyasema hayo bungeni jana wakati akijibu hoja za wabunge waliochangia juu ya Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya UKIMWI na Dawa za Kulevya iliyoibua maswali kwa Serikali kuendelea kupambana na wanaoshiriki katika biashara haramu ya dawa za kulevya nchini.

Waziri Mhagama alieleza kuwa dhamira ya Serikali ni kuhakikisha jamii yote kwa ujumla inakuwa mstari wa mbele katika kutokomeza tatizo hili linalowaathiri vijana kwa kiasi kikubwa.

“Mapambano haya ni yetu sote, yasichague mtu na iwe agenda ya Kitaifa inayowahusu Watanzania wote na ikumbukwe kuwa tatizo la dawa za kulevya lina historia tangu mwaka 1990 na Serikali imekuwa ikipambana kwa jitihada nyingi hivyo niombe watanzania wote tuunge mkono vita hii ili kumaliza kabisa tatizo hili”. Alisema Waziri

Aliongezea kuwa, dhamira hii ya Serikali ilianza kuonekana tangu kuwepo kwa sheria namba 9 ya mwaka 1995 hadi ilipofanyiwa marekebisho mwaka 2014 na kubaini kuwa asilimia 56 ya nguvu kazi ya vijana ndiyo imeathiriwa na tatizo la dawa za kulevya.

Aidha pamoja na mapambano hayo, tayari sheria namba 5 ya mwaka 2015 na miundo ya mapambano inaelekeza namna ya kupambana na vita dhidi ya dawa za kulevya.

Kwa upande wake Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Harrison Mwakyembe alieleza Bunge kuwa ziwepo jitihada za makusudi za kuunga mkono mapambano haya yawe ya Watanzania wote kwa kutoa wito kwa jamii kutoa ushirikiano na kumpongeza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe.Paul Makonda kwa namna alivyojidhatiti kupambana na wote wanaoshiriki katika biashara hizi za dawa ya kulevya.

“Nieleza wazi kuwa jitihada za Serikali pekee hazitoshi ni lazima jamii iunge mkono kwa kuwafichua wanaojihusisha na mtandao huu wa Dawa za Kulevya na Mhe.Paul Makonda nampongeza kwa kuthubutu kuingia kikamilifu katika vita hii”.Alisema Mwakyembe

Alimalizia kwa kueleza kuwa, kinachohitajika ni dhamira ya dhati na si fedha, hivyo Serikali imedhamiria kukomesha kabisa tatizo hili nchini.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akijibu hoja za wabunge mbalimbali waliochangia wakati wa kujadili Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Ukimwi Bungeni Dodoma. 


 
Viewing all 46334 articles
Browse latest View live




Latest Images