Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1129 | 1130 | (Page 1131) | 1132 | 1133 | .... | 1904 | newer

  0 0


  Habari ilizoifikia Globu ya Jamii jioni ya leo kutoka Mkoani Kilimanjaro,zinaeleza kuwa watu zaid ya watano wanadaiwa kupoteza Maisha,akiwemo mwandishi wa habari wa gazeti la Habarileo na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Hai,
  Anord Swai,katika ajali ya gari dogo.Ajali hiyo inaelezwa kuwa imetokea maeneo ya Mwika Mawanjeni maarufu kama Bar Mpya Moshi mkoani Kilimanjaro.

  Inaelezwa kuwa ndani ya gari hiyo walikuwemo watu sita wakiwemo viongozi wa CCM wakitoka kushiriki sherehe za miaka 40 ya CCM kimkoa yaliyofanyika katika ukumbi wa shule ya Msingi Shauri Tanga wilayani Rombo.Chanzo cha ajali inaelezwa kuwa ni fuso kufeli breki na kuligonga gari dogo.

  “Waliofariki ni Mwenyekiti wa Uvccm wilayani Hai na Mwandishi wa habari Leo Arnold Swai, mjumbe wa NEC ya CCM na Katibu wa CWT mkoa wa Kilimanjaro Ally Mmbaga na wanafunzi makada wa CCM kutoka vyuo vikuu vya ushirika na KCM.
   
   Majeruhi wa ajali hiyo ni Jackson Kimambo ambaye inaelezwa kuwa amekimbizwa Hospitali kwa matibabu,Watu hao walikuwa wakitoka kwenye maadhimisho ya kilele cha miaka 40 ya kuzaliwa CCM wilayani Rombo”
  Pichani ni aliyekuwa  Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Hai na mwandishi wa habari wa gazeti la serikali la Habari leo,enzi za uhai wake,Arnold Swai ambaye pia ni mmojawapo kati ya watu waliopoteza maisha katika ajali hiyo.
   
  Globu ya Jamii itazidi kuwaletea habari zaidi kutoka katika mamlaka husika,hususani Jeshi la Polisi.
   
  Mungu azilaze Roho za Marehemu Mahali pema peponi-Amin,

  0 0

    Meya wa jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kushiriki ibada ya jumapili kwenye kanisa la ufunuo lililoko kimara jijini Dar es Salaam.
  Mchungaji wa kanisa  la Ufunuo, Nabii Paul Bendera akifafanua jambo kwa waandishi wa habari.
   Mchungaji wa Kanisa  la Ufunuo, Nabii Paul Bendera akiongoza ibada katika kanisa hilo lililoko Kimara jijini Dar es Salaam kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi  Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita Charles kuzumgumza na waumini wa kanisa la ufunuo aliposhiriki ibada ya jumapili leo.
   Mchungaji wa kanisa  la Ufunuo, Nabii Paul Bendera (kushoto) akimtambulisha mgeni rasmi kwa waumini Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita Charles kuzumgumza na waumini wa kanisa la ufunuo na kujumuika kwenye ibada ya jumapili leo.
    Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita Charles akizungmza na waumini wa kanisa la Ufunuo  wakati aliposhiriki ibada ya jumapili.
   Waumini wa kanisa la Ufuno wakipiga makofi kumpongeza  Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita Charles wakati akizunguza.
   Waumini wa kanisa la ufunuo wakishikishiriki kwenye ibada.
   Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita (kulia) pamoja na Mchungaji wa kanisa   la Ufunuo, Nabii Paul Bendera
  (katikati) wakiwa kwenye ibada ya jumapili.
    Waumini wakiwa kwenye maombi ya ibada ya jumapili .
   
  …………………..
  Meya wa jiji la Dar es salaam Isaya Mwita amewasihi wazazi kushirikiana  na serikali katika maswala ya elimu ili  kuweza kutatua tatizo la kufeli katiaka shule za Serikali.
  Kauli hiyo ameitoa leo hii wakati akifanaya aliposhiriki ibada katika Kanisa   la Ufunuo linaloogozwa na Nabii Paulo Bendera,  lililopo Kimara Jijini Dar es salaam amesema wazazi wanatakiwa kuchunguza watoto wao katika masomo kwakuwa baadhi ya  watoto wanaaga wanakwenda shule lakini hawafiki hivyo inapelekea watoto kutokufanya vizuri.
  ”Nawasii wazazi  na walezi waendelee kushirikiana na serikali pamoja na bodi ilikuweza kupunguza matokeo mabaya katika mkoa wetu lakini wazazi wawakataze watoto wao kutumia simu kwa sababu watoto wengi wanatumia simu muda mwingi  kuliko muda wa kusoma”amesema Mwita
  Nae  Mchungaji wa kanisa  hilo la Ufunuo Nabii Bendera  ameliombea Taifa amani na kuwahasa  watanzania kushirikiana ili waweze kuwa na maendeleo ya kiuchumi.
  ” Nawaomba watanzania waandelee kuitunza  amani na kuwaombea viongozi wetu  kwakuwa tusipokuwa na amani na ushirikiano hatutoweza kufikia maendeleo tunayo yaitaji” amesema Bendera

  0 0
  0 0

  Mtaalam wa Maendeleo ya Watu Mayrose Kavura Majinge akieleza umuhimu wa Kanuni ya Dhahabu "The Golden Rule" Katika kuondoa Ufisadi na maovu mbalimbali katika jamii yetu. Fuatilia Habari kamili: maadilikitaifa.blogspot.com
  Profesa Nicholls Boas wa Chuo Kikuu Maryland Marekani akiwa miongoni mwa wadau Watanzania waishio Marekani akifurahia jambo wakati wa Siku Maalum ya Kuwezesha Kampeni ya Kuinua Maadili Kitaifa iliyofanyika Katika ukumbi wa Quality One Care, Maryland Marekani.
  Baadhi ya wadau wa Kampeni ya Kuinua Maadili Kitaifa kutoka maeneo mbalimbali nchini Marekani wakifuatilia kwa makini Maudhui ya Siku Maalum ya Kuwezesha Kampeni ya Kuinua Maadili Kitaifa iliyofanyika Katika ukumbi wa Quality One Care Silver Spring, Maryland Nchini Marekani
  Baadhi ya wadau wa Kampeni ya Kuinua Maadili Kitaifa kutoka maeneo mbalimbali nchini Marekani wakifuatilia kwa makini Maudhui ya Siku Maalum ya Kuwezesha Kampeni ya Kuinua Maadili Kitaifa iliyofanyika Katika ukumbi wa Quality One Care Silver Spring, Maryland Nchini Marekani.

  0 0

  Je, kwa wale wanaotumia vilevi kama bia, unajua kuwa chupa moja ya bia unatakiwa kunywa kwa saa moja?

  Tumsikiliza mtaalam wa Daktari wa Afya ya Jamii na Familia Dr Ali Mzige hapa chini akizungumza na The Beauty TV juu ya suala hilo na usisahau ku-subscribe kupata updates zaidi. 

  0 0

  Afisa Programu na Uchambuzi wa TGNP, Deogratius Temba (kulia) akiwasilisha mada katika semina kwa baadhi ya madiwani, watendaji na wenyeviti wa Serikali za mitaa kutoka Wilaya tatu za Mkoa wa Dar es Salaam, yaani Temeke, Ilala na Kinondoni. Semina hiyo liyofanyika Mabibo Jijini Dar es Salaam iliandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) Afisa Programu na Uchambuzi wa TGNP, Deogratius Temba (kulia) akifafanua jambo katika semina kwa baadhi ya madiwani, watendaji na wenyeviti wa Serikali za mitaa kutoka Wilaya tatu za Mkoa wa Dar es Salaam, yaani Temeke, Ilala na Kinondoni. Semina hiyo liyofanyika Mabibo Jijini Dar es Salaam iliandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) Baadhi ya washiriki katika semina kwa baadhi ya madiwani, watendaji na wenyeviti wa Serikali za mitaa kutoka Wilaya tatu za Mkoa wa Dar es Salaam, yaani Temeke, Ilala na Kinondoni wakichangia mada anuai katika Semina hiyo Sehemu ya washiriki wa semina kwa baadhi ya madiwani, watendaji na wenyeviti wa Serikali za mitaa kutoka Wilaya tatu za Mkoa wa Dar es Salaam, yaani Temeke, Ilala na Kinondoni wakifuatilia mada anuai. Semina hiyo liyofanyika Mabibo Jijini Dar es Salaam iliandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP). Baadhi ya washiriki katika semina kwa baadhi ya madiwani, watendaji na wenyeviti wa Serikali za mitaa kutoka Wilaya tatu za Mkoa wa Dar es Salaam, yaani Temeke, Ilala na Kinondoni wakiwasilisha kazi za vikundi baada ya majadiliano. Baadhi ya washiriki katika semina kwa baadhi ya madiwani, watendaji na wenyeviti wa Serikali za mitaa kutoka Wilaya tatu za Mkoa wa Dar es Salaam, yaani Temeke, Ilala na Kinondoni wakichangia mada anuai katika Semina hiyo. Baadhi ya washiriki katika semina kwa baadhi ya madiwani, watendaji na wenyeviti wa Serikali za mitaa kutoka Wilaya tatu za Mkoa wa Dar es Salaam, yaani Temeke, Ilala na Kinondoni wakichangia mada anuai katika Semina hiyo.

   BAADHI ya madiwani, watendaji na wenyeviti wa Serikali za mitaa kutoka Wilaya Tatu za Mkoa wa Dar es Salaam yaani Temeke, Ilala na Kinondoni wameviomba vyama vya siasa kutoa fursa za uongozi kwa wanawake ili waongezeke katika nafasi za uongozi ngazi mbalimbali. 

  Ombi hilo limetolewa na viongozi hao katika maoni yao walipokuwa katika semina kuangalia usawa wa kijinsia katika nafasi mbalimbali za uongozi iliyoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP). 

  Baadhi ya viongozi hao na watendaji walisema kumekuwa na changamoto nyingi ndani ya vyama vya siasa ambazo zinaendelea kuwa vikwazo kwa wanawake kushiriki katika nafasi za uongoni katika vyama anuai, hivyo kama zikiangaliwa zinaweza ongeza hamasa kwa wanawake kupata nafasi za uongozi. Semina kwa baadhi ya madiwani, watendaji na wenyeviti wa Serikali za mitaa kutoka Wilaya tatu za Mkoa wa Dar es Salaam, yaani Temeke, Ilala na Kinondoni ikiendelea. Baadhi ya washiriki katika semina kwa baadhi ya madiwani, watendaji na wenyeviti wa Serikali za mitaa kutoka Wilaya tatu za Mkoa wa Dar es Salaam, yaani Temeke, Ilala na Kinondoni wakiwasilisha kazi za vikundi baada ya majadiliano.

   Hata hivyo wamewataka wanawake kuendelea kujitokeza, kujiunga na vyama mbalimbali vya siasa pia kushiriki kugombea nafasi ili waweze kuonekana na kukwaa nafasi hizo. "Mbali na Vyama vya siasa kutakiwa kuregeza masharti na kutoa fursa kwa kundi la wanawake, wao pia wanatakiwa kujitokeza kushiriki katika siasa...na hata kugombea nafasi mbalimbali ili waonekane," alisema mmoja wa washiriki wa semina hiyo. 

  Kwa pamoja viongozi hao walikubaliana kuendelea kuwaunga mkono kundi hilo katika ushiriki wa siasa ili kujenga usawa wa kijinsia katika nafasi za maamuzi kuanzia ngazi za chini na kuendelea. Kwa upande wake Afisa Programu na Uchambuzi wa TGNP, Deogratius Temba akiwasilisha mada katika semina hiyo alisema wanawake ni wadau muhimu katika shughuli zote za kisiasa na maendeleo ya jamii hivyo kuna kila sababu ya kupewa nafasi ili waingie katika vyombo vya maamuzi. 

  Alisema yapo matamko mbalimbali ya juu ya umuhimu wa kundi hilo kushiriki katika uchaguzi, japokuwa utekelezaji wake kivitendo umekuwa na changamoto kadhaa. Aidha alitolea mfano matamko hayo ni pamoja na Tamko la Kimataifa Kuhusu Haki za Binadamu (U 1948), Mkataba wa Kimataifa wa Kutokomeza aina zote za ubaguzi dhidi ya wanawake (CEDAW: 1979) na mpango kazi wa Beijing (1995). 

  Pamoja na hayo alisema licha ya kundi hilo kusahaulika lakini limekuwa likitumiwa na vyama vya siasa kuhamasisha na kueneza sera zao ikiwemo kuongeza wanachama jambo ambalo linapaswa kuangaliwa kwa umuhimu hivyo kupewa fursa katika ushiriki.

  0 0

  Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL Waziri W.Kindamba akikabdhi msaada wa dawa na vifaa tiba kwa ajili ya Kituo cha Afya cha Tandale kwa Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Tandale Dkt Emmanuel Kazimoto na kushuhudiwa na Mkuu wa Wilaya Kinondoni, Mheshimiwa Ally Hapi.
  Mkuu wa Wilaya Kinondoni, Mheshimiwa Ally Hapi akizungumza kwenye hafla ya kupokea msaada wa dawa na vifaa tiba kutoka Kampuni ya Simu Tanzania(TTCL). Katika Haflya hiyo ilihudhuriwa na Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu, Bw Waziri W.Kindamba, Dr Zuhura Majapa Mratibu wa BRN Manispaa ya Kinondoni na Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Tandale Dkt Emmanuel Kazimoto. 
  Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL Waziri W.Kindamba akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi msaada wa dawa na vifaa tiba kwa Kituo ch Afya cha Tandale, wilayani Ilala, jijini Dar es salama

  Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) imeahidi kuendelea kushirikiana na Serikali katika kutatua changamoto katika sekta mbali mbali nchini ili kuboresha huduma za Kijamii zinazogusa maisha ya kila siku ya Wananchi kwa lengo la kuyaboresha na kuongeza kasi ya Nchi kupiga hatua za Maendeleo.

  Ahadi hiyo imetolewa Jijini Dar Es Salaam na Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL Bw Waziri Kindamba alipokuwa akikabidhi msaada wa dawa na vifaa tiba kwa Kituo cha Afya cha Tandale, kilichopo Wilaya ya Kinondoni, mkoa wa Dar es salaam mwishoni mwa wiki hii. 

  Msaada huo umekabidhiwa kwa Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya cha Tandale Dkt Emmanuel Kazimoto, tukio lililoshuhudiwa na Mkuu wa Wilaya Kinondoni Mheshimiwa Ally Hapi ambaye ndie aliwezesha kupatikana kwa vifaa hivyo kupitia program yake maalumu ya kuwasiliana na Taasisi za Umma na Binafsi ili zisaidie kuboresha huduma za kijamii Wilayani kwake.

  Akizungumza kwenye hafla ya makabidhiano hayo iliyofanyika katika Kituo hicho, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ally Hapi ameishukuru Kampuni ya Simu TTCL kwa msaada iliotoa na kubainisha kuwa, msaada wa dawa na vifaa tiba utasaidia sana kuboresha huduma katika kituo hicho chenye kuhudumia idadi kubwa ya Wananchi wa kipato chini.

  “Juhudi hizi za kusogeza huduma kwa wananchi ni muhimu sana katika kipindi hiki ambacho serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Rais wetu Dkt John Pombe Magufuli imedhamiria kuboresha maisha ya watu wa hali ya chini na kuwaondoa katika unyonge unaowafanya kushindwa kutoa mchango stahiki katika jitihada za nchi kujiletea Maendeleo” Amesema Mhe Hapi

  Aidha Mkuu huyo wa Wilaya ameutaka uongozi wa Kituo cha Afya Tandale kuhakikisha kuwa unasimamia vyema matumizi ya dawa hizo ili zitumike kwenye malengo yaliyokusudiwa ambayo ni kuboresha huduma kwa Wananchi.

  Naye Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Bw. Waziri W.Kindamba amesema, TTCL imekuwa mstari wa mbele katika kusaidia Jamii kwenye sekta mbalimbali kama vile elimu, afya, michezo, matumizi ya teknolojia ya Habari na Mawasiliano, makundi maalum na wakati wa maafa.

  “TTCL imetoa msaada huu wenye thamani ya shilingi milioni 5, dawa zilizotolewa ni pamoja na Paracetamol Syrup, Paracetamol Tabs, Diclofenac, Amoxicillin, Amoxicillin Granules, Folic Acid, Gloves Surgical, Bandage, Magnesium Trisilicate, Methylated Spirit na nyinginezo nyingi. Tunaamini kuwa msaada huu utatumika kwa malengo yaliyokusudiwa na utasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza uhaba wa dawa kwenye kituo hiki” amesema Waziri K.Kindamba. 

  Aidha, Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Bw. Waziri W.Kindamba ametoa rai kwa taasisi na makampuni mengine kukusaidia juhudi za Serikali katika kusaidia huduma za Kijamii hali itayoimarisha uhusiamo mwema na Wananchi na kutoa suluhisho kwa changamoto zinazoikabili jamii katika maeneo mbali mbali nchini.

  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye mkutano wa Jopo la Kuwawezesha Wanawake Kiuchumi linalofanyika jijini Dubai.
  Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza jambo na mmoja wa washiriki wa mkutano wa Jopo la Kuwawezesha Wanawake Kiuchumi linalofanyika jijini Dubai.
   Washiriki wa mkutano wa Jopo la Kuwawezesha Wanawake Kiuchumi likiendelea kufanyika jijini Dubai.
   Pichani kushoto ni Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na baadhi ya Washiriki wa mkutano wa Jopo la Kuwawezesha Wanawake Kiuchumi linalofanyika jijini Dubai.

  0 0

  Mgeni Rasmi kwenye hafla ya uzinduzi wa Bodi ya tano (5) ya Wadhamini wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF Waziri wa Nchi – Ofisi ya Rais (TAMISEMI) Mh. George Simbachawene (Mb) alipokea maelezo ya utangulizi. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi Prof. Faustine Karani Bee na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mh. Mrisho Gambo. Kulia ni Mkurugenzi mkuu wa LAPF Bw. Eliud Sanga na Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mh. Gabriel Daqarro.
  Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini iliyozinduliwa pamoja na Menejimenti ya Mfuko wa LAPF wakisilikiza kwa makini hotuba ya uzinduzi wa Bodi toka kwa Mgeni Rasmi Mh. George Simbachawene, Waziri wa Nchi – Ofisi ya Rais (TAMISEMI).
  Mwenyekiti wa Bodi ya tano (5) ya Wadhamini Prof. Faustine Karani Bee akitoa maelezo ya msingi kuhusu Mfuko wa LAPF mbele ya Mgeni Rasmi kwenye uzinduzi wa Bodi ya Wadhamini wa Mfuko tarehe 04 Februari, 2017.
  Waziri wa Nchi – Ofisi ya Rais (TAMISEMI) Mh. George Simbachawene (Mb). akitoa hotuba ya uzinduzi wa Bodi mpya ya Mfuko wa LAPF mbele ya Mwenyekiti wa Bodi, Wajumbe wa Bodi, Menejimenti ya Mfuko na wanahabari, tarehe 04 Februari, 2017.
  Mmoja wa Wajumbe wapya wa Bodi ya Wadhamini wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF Ndg. Tumaini P. Nyamuhokya akijitambulisha mbele ya Mgeni Rasmi wakati wa uzinduzi wa Bodi ya tano (5) ya Mfuko wa LAPF.
  Mgeni Rasmi kwenye uzinduzi wa Bodi ya tano (5) ya mfuko wa LAPF Waziri wan chi – Ofisi ya Rais (TAMISEMI) Mh. George Simbachawene (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mh. Mrisho Gambo, Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mh. Gabriel Daqarro, Mwenyekiti wa Bodi Prof. Faustine Bee, Wajumbe wa Bodi pamoja na Menejimenti ya Mfuko mara tu baada ya uzinduzi wa Bodi.

  0 0

  Mama wa mtoto huyo, Julieth Daudi

  Na Dotto Mwaibale

  SAKATA la Julieth Daudi (19) mkazi wa Tabata Relini pamoja na ndugu zake kususia kuchukua mwili wa mtoto aliyejifungua kwa madai kuwa mtoto huyo hakuwa wake baada  ya kubadilishiwa na wauguzi wa Hospitali ya Amana katika Manispaa ya Ilala  jijini Dar es Salaam baada ya kujifungua limechua sura mpya kufuatia wazazi hao kutaka kwenda kumuona Waziri wa Afya kufikisha kilio chao.

  Akizungumza na Jambo Leo nyumbani kwao  Dar es Salaam jana, Daudi alisema tunahitaji kwenda kumuona  Waziri waAfya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu  kwa hatua zaidi kutokana na kitendo hicho walichofanyiwa na wauuguzi hao.

  "Mimi pamoja na ndugu zangu tutakwenda kumuona waziri ili kumpelekea malalamiko yetu" alisema Daudi.Akizungumzia mkasa huo Daudi alisema  alifika Hospitalini hapo Februari 2 jioni akiwa amesindikizwa na mama yake Veronica Lucas na shangazi yake Judith Christopher.

  "Nilipofika daktari aliponipima aliniambia kuwa hasikii mapigo ya mtoto isipokuwa ya kwangu hivyo alishauri siku iliyofuata nipate kipimo cha utrasaund lakini kabla ya
  kipimo hicho nilijisia uchungu na kujifungua" alisema Daudi.

  Daudi alisema baada ya kupita muda kidogo muuguzi aliyemzalisha alimfuata na kumueleza kuwa mtoto wake alikuwa amefariki na alipomuuliza alikuwa wa jinsia gani muuguzi huyo alimweleza kuwa alikuwa hajui kama alikuwa wa kiume au wa kike.

  Aliongeza kuwa wakati yupo wodini alimuona kijana mmoja aliyevalia koti la hospitali akiwa amembeba mtoto ambaye hakujua alikokuwa amempeleka.

  Alisema baada ya kuambiwa mtoto wake amefariki aliomba aonyeshwe lakini hakuoneshwa tangu saa tatu asubuhi ambapo alilazimika kwenda kuomba simu kwa mlinzi wa hospitali hiyo na kuwajulisha ndugu zake walipofika nao waliomba kuonyeshwa mwili wa mtoto huyo bila mafanikio.

  Shangazi wa Julieth Judith Christopher alisema baada ya kutokea tukio hilo walikwenda kumuona Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo ambaye aliitisha kikao baina ya ndugu pamoja na maofisa wengine wa hospitali hiyo ambacho hakikufikia muafaka baada ya ndugu hao kukataa kuuchukua mwili wa mtoto huyo wakidai si wa kwao.

  Aliongeza kuwa mganga mkuu huyo aliwaeleza kuwa mtoto huyo alikuwa amefia tumboni baada ya mimba hiyo kuharibika na ndiyo sababu mtoto huyo alizaliwa akiwa mfu.

  "Wanafamilia tumegoma kuuchukua mwili wa mtoto huyo na maamuzi yaliyofikiwa ni kufanyika kipimo cha DNA" alisema Christopher.

  Alipopigiwa simu Muuguzi Mkuu wa Hospitali hiyo, Beauty Mwambebule alisema hawezi kulizungumzia tukio hilo kwenye simu njia ya simu badala yake alimtaka mwandishi wetu kwenda hospitali kupata undani wa jambo hilo.


  0 0

  Kazi ya kuwawezesha vijana na akinamama katika wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi,imeanza rasmi. 
   
  Mkuu wa Wilaya hiyo ya Tanganyika  Mh.Saleh Mhando akiwa sambamba na viongozi wengine mbalimabli,leo wameshirki kupalilia shamba la Karanga la kikundi cha vijana ktk kijiji cha Kabungu pamoja na kukabidhi hundi ya Milioni 56. 75 kwa ajili ya vikundi 24 vya wanawake na vikundi 8 vya vijana. 
   
  DC Mhando amesema kuwa lengo ni kuhakikisha hadi Juni 2017 kiasi cha milioni 150 zinatotewa na Halmashauri ya Wilaya kuwawezesha vijana na akinamama watakaojiunga katika vikundi dani ya Wilaya ya Tanganyika.
  Mkuu wa Wilaya hiyo ya Tanganyika Mh.Saleh Mhando (shati jeupe) akiwa sambamba na viongozi wengine mbalimabli wakishiriki kupalilia shamba la Karanga la kikundi cha vijana ktk kijiji cha Kabungu pamoja na kukabidhi hundi ya Milioni 56. 75 kwa ajili ya vikundi 24 vya wanawake na vikundi 8 vya vijana.  
   Mkuu wa Wilaya hiyo ya Tanganyika Mh.Saleh Mhando (shati jeupe) akiwa sambamba na viongozi wengine mbalimabli wakikagua shamba la Karanga la kikundi cha vijana ktk kijiji cha Kabungu Wilayani Tanganyika.
   Mkuu wa Wilaya hiyo ya Tanganyika Mh.Saleh Mhando (tatu kulia) akikabidhi hundi ya Milioni 56. 75 kwa ajili ya vikundi 24 vya wanawake na vikundi 8 vya vijana katika kijiji cha Kabungu wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi.

  0 0

  CHAMA Cha CCM Mkoa wa Kigoma kimevuna jumla ya Wanachama wapya 868 kutoka vyama mbalimbali vya siasa akiwemo mwenyekiti wa chama cha ACT-Wazalendo Venasi Busunzu wa wilaya ya Kakonko na Mwenyekiti wa CUF Kilembwe Omari mgombea udiwani kata ya Sinuka wamekabidhiwa kadi ya chama hicho jana, katika hitimisho ya sherehe za madhimisho ya kutimiza miaka 40 ya CCM.

  Akihitimisha sherehe hizo jana zilizo fanyika Kimkoa Katika kijiji cha Mwakizega Wilayani Uvinza Mwenyekiti wa CCM kigoma Amani Kabourou , alisema katika maazimisho waliyafanya Mkoa mzima katika Wilaya zote walipatikana wanachama wapya 726 na kutoka vyama vya upinzani ni wanachama 146 ambao walikabidhiwa kadi katika sherehe za maazimisho zilizo fanyika jana katika Kijiji cha Mwakizega kata ya Mwakizega Wilaya ya Uvinza.

  Alisema wanachama hao Waliamua kurudi katika Chama hicho kutokana na Shughuli kubwa zinazo fanywa na chama hicho , ambapo mpaka sasa kuna Maendeleo Makubwa yaliyo fanyika katika Kipindi cha Mwaka mmoja cha uongozi wa serikali unaongozwa na Serikali ya Chama cha Mapinduzi.

  Kabourou alisema Kwa sasa Viongozi wa chama hicho wameweka mikakati wa kukisafisha chama hicho kwa kuondoa viongozi wote wasio na sifa wanaokichafua sana na kuifanya CCM kuwa mpya na Serikali mpya kutokana na Misingi iliyo wekwa na waanzirishi wa Chama hicho.
   
  Akizungumzia hatua hiyo, aliyekuwa mwenyekiti wa ACT wazalendo Bususnzu alisema amegundua mapungufu makubwa katika chama cha awali hali ,iliyomshawishi kujiunga na ccm ni pamoja na viongozi kuhamasisha misuguano kwa jamii ,ili nchi isitawalike lakini kwa awamu ya serikali ya wamu ya tano ya John Magufuli ni kigezo cha upinzani kukubali uwajibikaji wake wenye tija kwa wananchi.

  Akizungumzia hilo Kilembwe Omari alisema amerudi kundini akiwa na wananchama 34 kutoka chama cha ACT wazalendo ,akidai amerudi kwa baba na mama yake akiwa na wenzake hao,sababu aminiye na kubatizwa ameokoka na anatumaini atakuwa mumini mzuri wa chama hicho.

  Akiongezea hilo Aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF,wilaya ya Kakonko Amana Ramadhani alisema anapokea kadi kwa hiari japokuwa amekulia katika upinzani akiwa mwenyekiti wa kina mama kwa miaka 15 wa chama cha CUF,kwa sababu ya sera zake akijua kitawakomboa wananchi,kumbe kipo kwa ajili ya kupata ruzuku ya serikali.

  Alisema tangu mwaka 1990 wapo wanachama wawili hali inayokwamisha jitihada za kuleta maendeleo ,awali aliamini ujio wa UKAWA ni kuimarisha vyama lakini kilichotokea ni ubaguzi wa udini na kugombea maslai binafsi na si wananchi,hivyo hana budi kujiunga na ccm ili kutimiza ndoto za kuinua uchumi .

  Kwa upande wa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Emanuel Maganga alisema kwa awamu ya tano ya serikali ya leo,imetatua kero mbalimbali za wananchi,hususani katika sekta ya elimu kigoma imepiga hatua 2015/16 wilaya ya kakonko ilishika nafasi ya kwanza matokeo ya kidato cha pili na kidato cha sita kigoma ilishika nafasi ya kwanza kitaifa.

  Maendeleo hayo ni pamoja na sekta ya miundombinu ya barabara ,miradi ya maji zimetengwa kiasi cha sh.milioni 10 kwa kila wilaya ya kigoma kwa ajili ya kukamilisha miundombinu ya maji iliyokuwa ikisuasua sanjari na umalizwaji wa barabara ya Kidahwe hadi kasulu na nyakanazi Kakonko huku Uvinza hadi Tabora fungu la fedha zimepangiwa bajeti katika mwaka wa 2016/17.

   


  0 0  0 0

  Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimepokea kwa majonzi na masikitiko makubwa taarifa za vifo vya watu saba wakiwemo viongozi na wanachama wanne wa CCM ambao ni Ndg Ally Mmbaga, mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa na mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Mkoa, Ndg Arnold Swai, Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana (UVCCM) Wilaya ya Hai, Ndg Anastazia Innocent Malamsha, Mwenyekiti wa UWT Tawi la Chuo Kikuu cha Ushirika (Moshi) na Ndg Edwin Msele, Katibu wa Hamasa wa Shirikisho la Vyuo Vikuu Mkoa wa Kilimanjaro vilivyosababishwa na ajali ya barabarani katika eneo la Mwika, Wilaya ya Moshi Vijijini, Mkoa wa Kilimanjaro siku ya Jumapili ya tarehe 05th Februari 2017.

  Ajali hiyo ilitokea majira ya jioni ikihusisha gari ya mizigo aina ya Fuso na Toyota Hilux Surf iliyokuwa imewabeba Viongozi wa CCM waliokuwa wakitoka katika kutekeleza majukumu ya Chama ya Maadhimisho ya Miaka 40 ya Kuzaliwa kwa CCM yaliyofanyika kimkoa Wilayani Rombo na kusababisha vifo vyao.

  Kutokana msiba huo, Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu Abdulrahman Kinana amemtumia salamu za rambi rambi Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kilimanjaro, Ndugu Iddy Juma, familia, ndugu, jamaa, marafiki pamoja na wanachama wa CCM Mkoa wa Kilimanjaro kufuatia vifo vya Viongozi wetu. 

  Wana CCM nchi nzima, tunawaombea majeruhi kupona haraka, na tunamuomba Mwenyezi Mungu aziweke mahali pema roho za Marehemu.  Amina.
  Imetolewa na,

  HUMPHREY POLEPOLE
  KATIBU WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA, ITIKADI NA UENEZI
  06/02/2017.

  0 0

  Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa akipokelewa na Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza alipowasili Makao Makuu ya Jeshi hilo baada ya kuapishwa rasmi kuwa Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, Ikulu Jijini Dar es Salaam Februari 6, 2017.
  Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa akipokea salaam ya heshima toka katika Gwaride Maalum lililoandaliwa na Maofisa na askari(hawapo pichani) kwa ajili yake kwa heshima.
  Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa akikagua Gwaride Maalum lililoandaliwa na Maofisa na askari wa Jeshi la Magereza kwa ajili yake kwa heshima kama inavyoonekana katika picha.
  Kamishna wa Fedha na Utawala wa Jeshi la Magereza, Gaston Sanga(kulia) akiteta jambo na Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa kabla ya kuongea na Maafisa na askari wa Jeshi hilo Makao Makuu ya Magereza mara baada ya kutoka kuapishwa kuwa Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza.
  Baadhi ya Askari wa Jeshi la Magereza wakimsikiliza Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa mara baada ya kutoka kuapishwa kuwa Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, Ikulu Jijini Dar es Salaam Februari 6, 2017.
  Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakimsikiliza Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa mara baada ya kutoka kuapishwa kuwa Kamishna Jenerali wa Jeshi hilo, Ikulu Jijini Dar es Salaam Februari 6, 2017.
  Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa akiongea na Maafisa, askari na Watumishi raia wa Jeshi la Magereza baada ya kutoka kuapishwa kuwa Kamishna Jenerali wa Jeshi hilo, Ikulu Jijini Dar es Salaam Februari 6, 2017.
  Sehemu ya familia ya Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, Dkt. Juma Malewa waliohudhuria kuapishwa kwake leo Ikulu, Dar es Salaam wakiwa katika picha ya pamoja(katikati) ni Mke wa Kamishna Jenerali wa Jeshi hilo Bi. Fatuma Malewa(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).
  Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa akiwasili Makao Makuu ya Jeshi la Magereza mara baada ya kuapishwa rasmi kuwa Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, Ikulu Jijini Dar es Salaam Februari 6, 2017.

  0 0

  Mkuu wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) Jenerali Venance Mabeyo akila kiapo cha utii mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanznaia Dkt. John Pombe Magufuli leo Ikulu jijini Dar es Salaam. Katikati ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi.
  Mkuu wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) Jenerali Venance Mabeyo akiweka saini katika hati ya kiapo cha utii mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanznaia Dkt. John Pombe Magufuli wakati wa hafla ya kuapishwa kuwa Mkuu wa Jeshi la Wananchi Tanzania (CDF) leo Ikulu jijini Dar es Salaam. Katikati ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanznaia Dkt. John Pombe Magufuli akiweka saini katika hati ya kiapo cha utii wakati wa hafla ya kumwapisha Mkuu wa Majeshi la Majeshi ya Ulinzi Tanzania (JWTZ) Jenerali Venance Mabeyo leo jijini Dar es Salaam.
  Mkuu wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) Jenerali Venance Mabeyo akipokea salamu ya utii kutoka kwa kikosi maalumu cha Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) mara baada ya kuapishwa kuwa Mkuu wa Majeshi leo Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Mnadhimu Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Meja Jenerali James M. Mwakibolwa akila kiapo cha utii mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanznaia Dkt. John Pombe Magufuli leo Ikulu jijini Dar es Salaam. Katikati ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi.
  Mnadhimu Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Major Jenerali James M. Mwakibolwa akiweka saini katika hati ya kiapo cha utii mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanznaia Dkt. John Pombe Magufuli wakati wa hafla ya kuapishwa kuwa Mkuu wa Jeshi la Wananchi Tanzania (CDF) leo Ikulu jijini Dar es Salaam. Katikati ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanznaia Dkt. John Pombe Magufuli akiweka saini katika hati ya kiapo cha utii wakati wa hafla ya kumwapisha Mnadhimu Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Meja Jenerali James M. Mwakibolwa leo jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanznaia Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi vutendea kazi Mnadhimu Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Major Jenerali James M. Mwakibolwayo wakati wa hafla ya kuwapisha wateule hao leo jijini Dar es Salaam.
  Kamishna Jenerali wa Magereza Dr. Juma Malewa akila kiapo cha utii mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanznaia Dkt. John Pombe Magufuli leo Ikulu jijini Dar es Salaam. Katikati ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanznaia Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi vitendea kazi Kamishna Jenerali wa Magereza Dr. Juma Malewa wakati wa hafla ya kuwapisha wateule hao leo jijini Dar es Salaam.
  Balozi Paul Mella ambaye ataiwakilisha nchi ya Tanzania nchini katika Jamhuri ya Demokrasia ya Congo akila kiapo cha utii mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanznaia Dkt. John Pombe Magufuli leo Ikulu jijini Dar es Salaam. Katikati ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi.
  Balozi Samweli William Shelukindo ambaye anakwenda kuiwakilisha Tanzania nchini Ufaransa akila kiapo cha utii mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanznaia Dkt. John Pombe Magufuli leo Ikulu jijini Dar es Salaam. Katikati ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi.
  Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma Nyakimura Mathias Mhoji akila kiapo cha utii mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanznaia Dkt. John Pombe Magufuli leo Ikulu jijini Dar es Salaam. Katikati ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi.
  Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) Kamishna Robert Boaz Mikomangwa akila kiapo cha utii mbele ya Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania Inspekta Jenerali Ernest Mangu katika hafla ya kuwaapisha baadhi ya viongozi walioteuliwa na Mhe. Rais kushika nyazifa mbalimbali leo Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanznaia Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Jenerali Venance S. Mabeyo ( kulia) mara baada ya hafla ya kumuapisha leo jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Mnadhimu wa Jeshi hilo Meja Jenerali James Mwakibolwa, Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dkt. Mohamed Shein na Waziri Mkuu wa Kassim Majali.
  Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania (JWTZ) Jenerali Venance S. Mabeyo akifurahia jambo na Mkuu wa Majeshi Mstaafu Jenerali Davis Mwamunyage wakati wa hafla ya kuapishwa kwake leo jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Makamishna wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama ya Tanzania wakati wa hafla ya kuwaapisha Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania, Mnadhimu Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, Mabalozi pamoja na Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma leo jijini Dar es Salaam.

  Picha zote na: Frank Shija – MAELEZO

  0 0


  0 0

  Na: Lilian Lundo – MAELEZO – Dodoma
  Serikali haina mamlaka ya kuweka ukomo wa riba au riba elekezi itakayotumiwa na mabenki katika kutoa mikopo.
  Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji ameeleza hayo leo Bungeni, Mjini Dodoma alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Baraza la Wawakilishi Machano Othman Said juu ya lini Serikali itaweka utaratibu wa kupunguza riba ya mikopo walau kufikia asilimia 10 – 12 badala ya sasa ambayo ni asilimia 17 – 20.
  “Mabadiliko ya Sekta ya Fedha ya mwaka 1991 yalipelekea Serikali kujitoa katika uendeshaji wa moja kwa moja wa shughuli za kibenki nchini ili kuruhusu mfumo wa soko huria, hususan nguvu ya soko kuamua viwango vya riba za mikopo, riba za amana na gharama nyingine za huduma za kibenki,” alifafanua Dkt. Ashatu Kijaji.
  Aliendelea kwa kusema kuwa viwango vya riba za mikopo na riba za amana pamoja na riba za mikopo kati ya benki na benki hupangwa kwa kuzingatia gharama za upatikanaji wa fedha, gharama za uendeshaji, riba za dhamana za Serikali, sifa za mkopaji na hatari ya mkopaji kutolipa mkopo pamoja na kasi ya mfumuko wa bei.
  Aidha Dkt. Ashatu Kijaji amesema kuwa kutoa maelekezo kwa mabenki kutumia viwango fulani vya riba katika biashara zao, kutaifanya Benki Kuu kukosa nguvu na mamlaka ya kuyachukulia mabenki hatua endapo yatapata hasara kwa kutumia riba ambayo Benki Kuu imeelekeza.
  Vile vile amesema kuwa kiwango cha hatari ya kutolipa mkopo ni miongoni mwa vigezo vinavyotumiwa na mabenki katika kupanga viwango vya riba za mikopo, ambapo kwa sehemu kubwa gharama za riba za mikopo hutegemea zaidi gharama za upatikanaji wa fedha pamoja na gharama za uendeshaji.
  Pia amesema kuwa, ni muhimu kutambua kwamba kadri riba za mikopo zinapokuwa juu, ndivyo riba za amana zinapokuwa juu pia, ambapo wastani wa riba za kukopa kwa mwaka mmoja mwezi Juni, 2016 ulikuwa asilimia 13.67 wakati wastani wa riba za amana za mwaka mmoja ulikuwa asilimia 11.52 ikiwa ni tofauti ya asilimia 2.25.

  0 0

  Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

  Wizara ya afya na maendeleo ya Jamii,Jinsia wazee na watoto imezindua vipindi maalum vya radio katika radio ya 100.5 Times fm kuhusu utekelezaji wa mpango kazi wa Taifa wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto nchini.

  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Katibu mkuu wa maendeleo ya jinsia na watoto , Sihaba Nkinga amesema tatizo la ukatili dhidi ya wanawake na watoto hapa nchini ni kubwa na linaaathiri maendeleo yao katika taifa.

  “takwimu za jeshi la Polisi zinaonyesha kuwa vitendo vya ubakaji kwa mwaka 2015 vilifikia 3,444 na matukio ya shambulio ,kujeruhi na matusi vilikuwa 14,561”amesema katibu Nkinga.

  amesema kuwa taarifa ya utafiti wa idadi ya watu na afya ya 2010 inaonesha kuwa asilimia 39 ya wanawake wa umri wa miaka 15-49 walifanyiwa ukatili wa shambulio na kutaja kuwa ukatili dhidi ya watoto ya mwaka 2011 ilibainisha kuwa asilimia 72 ya wasichana na asilimia 71 ya wavulana walifanyiwa ukatili wa vipigo.

  Katibu Nkinga alitumia fursa hiyo kumponeza meneja vipindi wa radio ya Times Amani Misana kwa kuwa tayari kushirikiana na wizara katika kusimamia na kuratibu na maandalizi ya uendeshaji wa vipindi vya elimu na stadi za kuzuia ukatili.

  Amemaliza kwa kusema kuwa anawataka kufuatilia matangazo ya vipindi hivi ili kupata ufafanuzi wa kutosha kutoka jopo la waelimishaji watakaoshirikiana na watangazaji

  0 0


  Aliyekuwa meneja wa wema Martin Kadinda akiwa katika mahakama ya hakimu mkazi kisutu pamoja na wanasheria


  Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

  Mwanamitindo maarufiu nchini, Martin Kadinda amesema kuwa yeye sio meneja wa Wema Sepetu kwa sasa, bali amefika mahakamani hapo kama rafiki wa karibu wa msanii huyo.

  Kadinda amesema hayo katika maongezi maalum na mwandishi wa globu ya jamii juu ya uhusiano wake na Wema Sepetu kwa sasa. hasa mara baada ya kuhusishwa na tuhuma za matumizi na uuzwaji wa dawa za kulevya.

  “kwa sasa mie sio meneja wa wema,mimi ni rafiki yake tu wa karibu hivyo nimeamua kuja hapa kwa ajili ya kujua rafiki yangu amefikia wapi katika kipindi hiki ambacho anapitia magumu” amesema Kadinda

  Ametaja kuwa yeye kwa sasa anaendelea na biashara yake ya kushona suti tu ili aweze kujipatia ugali wake wa kila siku na sio kujihusisha na makundi ambayo sio sahiii.Hata hivyo kadinda ameonekana akisubiri kwa hamu kubwa kuona rafiki yake anafikishwa mahakamani hapo,lakini haikuwa hivyo Wema hakufikishwa tena mahakamani hapo.
  baadhi ya wafuasi wa wema wakiwa wamesimama kusubiri msanii huyo kuletwa mahakamani
  Mmoja wa wasanii mahiri atambulikae kwa jna la kisanii Jike shupa na wenzie wakiwa wamekata tamaa mara baada ya kuambiwa Wema haletwi mahakamani hapo

older | 1 | .... | 1129 | 1130 | (Page 1131) | 1132 | 1133 | .... | 1904 | newer