Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46329 articles
Browse latest View live

KINANA ATEMBELEA KUWAFARIKI YATIMA KATIKA KIJIJI CHA MATUMAINI, ENEO LA KISASA DODOMA, LEO

$
0
0
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwakabidhi msaada wa vyakula watoto wa Kijiji cha Matumaini, kilichopo eneo la Kisasa Dodoma mjini alipotembelea kituo hicho kuwafariki watoto yatima, leo ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya miaka 40 ya CCM, ambayo kilele chake ni kesho. Kushoto ni mwanzilishi wa Kijiji hicho Padre Vincent Boseil
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwa na watoto wanaolelewa katika Kijiji cha Matumaini, kilichopo eneo la Kisasa Dodoma mjini alipotembelea kituo hicho kuwafariki watoto yatima, leo ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya miaka 40 ya CCM, ambayo kilele chake ni kesho. Kulia ni mmoja wa waanzilishi wa kituo hicho Sista Roselie
 Kinana akikaribishwa ndani na Mwanzilishi wa Kituo hicho, Padre  Vincent Boseili
 Kinana akisaini kitabu cha wageni alipowasili kwenye kituo hicho cha Kijiji cha Matumaini
 Padre Vincenti akionyesha wageni ramani ya Kijiji hicho cha Matumaini
 Sista Roselie akisoma risala
 Padre Vincent akitoa maelezo kuhusu kijiji hicho cha Matumaini
 Waziri Mavunde akizungumza alipokaribisha kuongea kwenye kijiji hicho cha Matumaini
 Mavunde akizungumza

Mavunde akipongezwa na Kinana baada ya kuzungumza neno la shukrani kwa mwanzilishi wa Kijiji hicho chenye kituo cha watoto yatima
Kinana akimpongeza Padre Vincent baada ya kuzungumza maneno ya shukrani
Kinana na ugeni wake wakienda kukagua sguhuli mbalimbali kwenye Kijiji hicho cha Matumaini
Kinana akiwasalimia watoto wanaolelewa kwenye kituo hicho ambao pia wanasoma
Kinana akiwasalimia wanafunzi wa Sekondari wanalelewa na kusomeshwa na Kijiji hicho cha Matumaini. Kushoto ni Padre Vincent wa Kijiji hicho
Watoto ambao ni wanafunzi wanaolelewa na kusomeshwa kwenye Kijiji hicho wakiimba wimbo wa Taifa Kinana alipowasili
Wanafunzi wa Kijiji hicho wakipiga ala wakati wimbo wa Taifa la Tanzania ukiimbwa
Kinana akifurahia jambo kwa kupiga kofi huku mtoto wa Kijiji hicho aliyempakata naye akipiga kofi
Wanafunzi wa Sekondari wanaolelewa na kusomeshwa na Kijiji hicho cha Matumaini wakiimba wimbo wao maalum
Kinana akiwafurahia wanafunzi ambao alitambulishwa kwao na Padre Vincent
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimfurahia mtoto anayelelewa katika Kijiji hicho cha Matumaini
Kinana akikabidhi zawadi kwa watoto
Kinana akifurahia watoto wa Kijiji hicho baada ya kuwapa zawadi
Kinana akishiriki kuimba wimbo maalum pamoja na wanafunzi wanaolelewa na kusomeshwa katika Kijiji hicho
Kinana akionyeshwa eneo ambako kinamama hujifungulia bure kwenye Kijiji hicho cha Matumaini
Kinana akizungumzana wageni kutoka Italia ambao nao walifika kutembelea Kijiji hicho cha Matumaini
Kinana akionyeshwa eneo ambako hutunza watoto wachanga, ambao ni yatima, kwenye Kijiji hicho cha Matumaini
Kinana akimchukua mtoto mmoja kumfurahia, katika eneo hilo la kulea watoto wachanga
Kisha Kinana akamchumu mtoto huyo kwa upendo mkubwa
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma mjini akimchukua mtoto kwa upendo
Watoto katika Kijiji hicho wakitazama kwa mshangao ugeni wa Kinana 
Katibu Mkuu Kinana akipewa maelezo kwenye mapokezi ya Hospitali ya Kijiji hicho cha Matumaini
Kinana akionyeshwa vifaa vya kupimia CD4 kwa wagonjwa wa Ukimwi
Kinana akimshukuru Padre Vincent baada ya kutembelea Kijiji hicho cha Matumaini
Kinana akiagana na Padre Vincnt kabla ya kuondoka
Mkuu wa wilaya ya Dodoma Mjini akiagana na Padre Vince pia kabla ya kuondoka. Picha zote na Bashir Nkoromo.  KINANA ASHIRIKI NA KUKAGUA SHUGHULI ZA MAENDELEO DODOMA LEO IKIWA NI SEHEMU YA MAADHIMISHO MIAKA 40 YA CCM
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Wilaya ya Dodoma mjini na mkoa huo, katika Ofisi ya CCM mkoa wa Dodoma, leo alipowasili kwenye ofisi hiyo, tayari kushiriki na kukagua shughuli za maendeleo ikiwa ni sehemu ya Madhimisho ya miaka 40 ya CCM ambayo kilele chake ni kesho. Akizungumza Kinana amesema, CCM imeamua kufanya Maadhimisho hayo mkoani Dodoma kwa kuwa imedhamiriwa kuisaidia Serikali katika kutekeleza ilani ya CCM, hivyo CCM imeamua kufanya hivyo ili kuunga mkono azma ya Serikali kuhamia Dodoma.
 Mkuu wa mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana akitoa salamu za shukrani, baada ya Kinana kuzungumza katika mkutano huo wa ndani. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM mkoa huo, Adam Kimbisa.
 Katibu  Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akiwasalimia mafundi alipowasili kukagua na kupanda miti kwenye mradi wa Ujenzi wa Dampo la Kisasa katika eneo la Kata ya Matumbulu wilaya ya Dodoma Mjini, leo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 40 ya CCM ambayo kilele chake ni kesho.
 Katibu  Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akipanda miti kwenye mradi wa Ujenzi wa Dampo la Kisasa katika eneo la Kata ya Matumbulu wilaya ya Dodoma Mjini, leo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 40 ya CCM ambayo kilele chake ni kesho.
 Mwenyekiti wa CCM, Wilaya ya Dodoma Mjini, akishiriki kupanda mji kwenye mradi huo
 Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini akishiriki kupanda mti kwenye eneo la mradi huo
 Mbunge wa Dodoma Mjini, Waziri Anthony Mavunde akishiriki kupanda mti katika eneo hilo
 Kinana akimpongeza kwa kupanda mti katika eneo hilo, Mzee Godfrey James
 Kinana akimsaidia kupanda mti mjumbe wa shina katika kata hiyo Ester Paschal
 Kinana na ujumbe wake wakiondoka katika upandaji mti na kwenda kukagua ujenzi wa dampo la kisasa katika eneo hilo. Kushoto ni Mavunde na kulia ni Kimbisa
 Mhandisi wa Manispaa ya Dodoma, Injinia John Nchilla akimpa Kinana maelezo kuhusu ujenzi wa dampo hilo la Kisasa katika Kata ya Matumbulu wilaya ya Dodoma Mjini
 Mwenyekiti wa CCM, Kata ya Nkuhungu, Dodoma Mjini, Pius Afa akimkaribisha Kinana kushiriki ujnezi na kupanda mti kwenye ujenzi wa Ofisi ya CCM ya Kata hiyo
 Wanachi wakimpokea Kinana kwa shamrashamra alipowasili katika Kata hiyo ya Nkuhungu
 Kinana akisalimia wananchi wa Nkuhungu
 Mwenyekiti wa CCM Kata ya Nkuhungu Pius Afa akimuonyesha Kinana ramani ya ujenzi wa Ofisi hiyo ya CCM ya Kata hiyo
 Kinana akipokea tofali alipokuwa akishiriki ujenzi wa Ofisi hiyo ya CCM Kata ya Nkuhungu
 Kinana akishiriki ujenzi wa Ofisi ya CCM Kata ya Nkuhungu, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 40ya CCM ambayo kilele chake ni kesho
 Kinana akishuka baada ya kushiriki ujenzi wa Ofisi hiyo kikamilifu
Kinana akizungumza na wananchi baada ya kushiriki ujenzi wa Ofisi ya CCM wilaya ya Mkuhungu, Dodoma leo. Picha zaidi  alipotembelea Kijiji cha Matumaini/>BOFYA HAPA

NDUGU WAGOMEA MAITI YA MTOTO HOSPITALI YA AMANA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Mzazi Julieth Daudi (19) mkazi wa Tabata Relini, akiwa Hospitali ya Amana jijini Dar es Salaam, alipozungumza na mwanahabari akidai amebadilishiwa mtoto aliyejifungua.
 Mama mzazi wa Julieth, Veronica Lucas akiwa ameshika shavu kwa masikitiko kufuatia tukio hilo.



 Shangazi yake Julieth, Judith Christopher akielezea tukio hilo 
kwa mwanahabari.
 Julieth Daud (kulia) akiwa na dada yake nje ya wodi ya wazazi katika Hospitali hiyo.

Julieth (aliyekaa kushoto), akiwa na ndugu zake nje ya
wodi ya wazazi katika Hospitali hiyo.

Na Dotto Mwaibale

MZAZI Julieth Daudi (19) mkazi wa Tabata Relini pamoja na ndugu zake wamegoma kuchukua mwili wa mtoto kwa madai kuwa mtoto huyo hakuwa wake kutokana na kubadilishiwa na wauguzi wa Hospitali ya Amana katika Manispaa ya Ilala  jijini Dar es Salaam muda mfupi baada ya kujifungua.

Akizungumza kwa masikitiko nje ya viwanja vya hospitali hiyo Dar es Salaam jana, Daudi alisema kitendo alichofanyiwa kimemuumiza sana pamoja na ndugu zake wengine.

Alisema alifika Hospitalini hapo Februari 2 jioni akiwa amesindikizwa na mama yake Veronica Lucas na shangazi yake Judith Christopher.

"Nilipofika daktari aliponipima aliniambia kuwa hasikii mapigo ya mtoto isipokuwa ya kwangu hivyo alishauri siku iliyofuata nipate kipimo cha utrasaund lakini kabla ya kipimo hicho nilijisia uchungu na kujifungua" alisema Daudi.

Daudi alisema baada ya kupita muda kidogo muuguzi aliyemzalisha alimfuata na kumueleza kuwa mtoto wake alikuwa amefariki na alipomuuliza alikuwa wa jinsia gani muuguzi huyo alimweleza kuwa alikuwa hajui kama alikuwa wa kiume au wa kike.

Aliongeza kuwa wakati yupo wodini alimuona kijana mmoja aliyevalia koti la hospitali akiwa amembeba mtoto ambaye hakujua alikokuwa amempeleka.

Alisema baada ya kuambiwa mtoto wake amefariki aliomba aonyeshwe lakini hakuoneshwa ambapo alilazimika kwenda kuomba simu kwa mlinzi wa hospitali hiyo na kuwajulisha ndugu zake walipofika nao waliomba kuonyeshwa mwili wa mtoto huyo bila mafanikio.

Shangazi wa Julieth Judith Christopher alisema baada ya kutokea tukio hilo walikwenda kumuona Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo ambaye aliitisha kikao baina ya ndugu pamoja na maofisa wengine wa hospitali hiyo ambacho hakikufikia muafaka baada ya ndugu hao kukataa kuuchukua mwili wa mtoto huyo wakidai si wa kwao.

Aliongeza kuwa mganga mkuu huyo aliwaeleza kuwa mtoto huyo alikuwa amefia tumboni baada ya mama yake kuiharibu mimba hiyo kwa nia ya kuitoa na ndiyo sababu mtoto huyo alizaliwa akiwa mfu.

"Wanafamilia tumegoma kuuchukua mwili wa mtoto huyo na maamuzi yaliyofikiwa ni kufanyika kipimo cha DNN na ili mama wa mtoto aruhusiwe kutoka hospitali inatakiwa ipelekwe barua ya mwenyekiti wa mtaa wake anakoishi" alisema Christopher.

Muuguzi Mkuu wa Hospitali hiyo, Beauty Mwambebule alipotakiwa kuzungumzia tukio hilo hakuwa tayari kuzungumza kwa njia ya simu badala yake alimtaka mwandishi wetu kwenda hospitali kupata undani wa jambo hilo.

Serikali Yaahidi Kufanyia Kazi Mapungufu Yaliyojitokeza Mradi wa TASAF

$
0
0
Na: Lilian Lundo – MAELEZO - DOdoma

Serikali imesema kwamba itafanya uchunguzi juu ya changamoto na matatizo ambayo yamejitokeza katika mradi wa TASAF ili kuja na mfumo mwingine bora zaidi kwa ajili ya wanufaika wa mradi huo.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah Kairuki ameyasema hayo leo Bungeni, Mjini Dodoma wakati wa uwasilishaji wa taarifa ya Kamati ya Utawala na Serikali za Mitaa kwa mwaka 2016/2017 ambapo wabunge waliulalamikia mradi huo kuwa na matatizo katika maeneo ambayo wanayasimamia.

Angellah Kairuki alisema kuwa wizara yake itafuatilia changamato zote ambazo wabunge wamezianisha ikiwemo utoaji wa fedha kwa kaya ambazo hazina sifa, matumizi mabaya ya fedha za mradi kwa baadhi ya wanufaika pamoja na usimamizi mbovu wa fedha za mradi kwa watendaji wa Halmashauri.

Kwa upande wake, Mbunge wa Jimbo la Nzega Hussein Bashe ameishauri Serikali kutafuta mfumo mzuri wa kuzitoa fedha hizo ili wanufaika waweze kuzitumia kwa kuanzisha biashara ndogondoga ambazo zitawasaidia kujikimu na kuziendeleza familia zao kiuchumi.

Aliendelea kwa kusema kuwa, kuwe na utaratibu wa wanufaika kutoa mchanganuo wa namna walivyozitumia fedha hizo ili kuleta nidhamu kwa wanufaika wanaotumia fedha hizo kinyume na malengo yaliyowekwa.

Aidha, Mbunge wa Jimbo la Nanyamba, Abdallah Chikota amesema kuwa katika jimbo lake kuna kaya ambazo zimetolewa katika mradi huo kwa kukosa sifa. Kaya hizo zimeagizwa kurejesha fedha zote ambazo walipatiwa kupitia mradhi huo, na wengi wao hawana uwezo wa kurejesha fedha hizo.

Hivyo basi, ameiomba Serikali kuwachukulia hatua Waratibu wa Mradi huo kwani ndio waliotoa fedha kwa watu wasio na sifa,  badala ya kuwaambia wananchi kurejesha fedha walizopewa  kwani wengi wao hawana huwezo wa kuzirejesha kutokana na vipato vyao kwa vya chini.

Akiwasilisha taarifa ya Kamati hiyo, Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Dkt. Pudenciana Kikwembe amesema kuwa, mpango wa TASAF wa kunusuru kaya maskini nchini umeonyesha mafanikio makubwa, licha ya kasoro kadhaa zinazotokana na baadhi ya Watendaji wa Halmashauri wanaohusika kukosa uwazi na uadilifu katika uwajibikaji wao.

Hivyo basi, hali hiyo imesababisha kubainika kwa Kaya 55, 692 zisizo na sifa stahiki  lakini zilikuwa zikinufaika na mpango hu o wa kunusuru Kaya Masikini.

Aidha Kamati imeishauri serikali kuimarisha uwezo wa Halmashauri katika kusimamia miradi ya TASAF ili itekelezwe kikamilifu na kwa ufanisi pamoja na kuimarisha mifumo ya kuwatambua walengwa wa Mpango huo na kuzuia kaya zisizo na sifa kunufaika.

Dk.Shei awaandalia chakula Maaskari walioshiriki Gwaride la Maadhimisho ya Miaka 53 ya Mapinduzi

$
0
0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akiwapungia mkono maaskari walioshiriki katika sherehe za Maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar wakati alipowasili katika  hafla ya chakula maalum kwa Askari hao iliyofanyika leo katika viwanja vya Kambi ya KVZ Mtoni (kulia) Brigedia Jeneral Sharif Sheikh Othman ,Kamanda wa Brigedi ya Nyuki Zanzibar
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akiwa na Viongozi mbali mbali wakisimama wakati Wimbo wa Taifa ukipigwa wakati wa hafla ya chakula maalum kwa maaskari walioshiriki katika sherehe za Maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar mara baada ya kuwasili katika   hafla hiyo  iliyofanyika leo katika viwanja vya Kambi ya KVZ Mtoni
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akiteta jambo na  Kamanda wa Brigedia ya Nyuki Zanzibar Brigedia Jeneral Sharif Sheikh Othman  wakati wa hafla ya chakula maalum kwa maaskari walioshiriki katika sherehe za Maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar mara baada ya kuwasili katika   hafla hiyo  iliyofanyika leo katika viwanja vya Kambi ya KVZ Mtoni
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) Makamo wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi, (wa pili kushoto) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa,Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ Haji Omar Kheir,(kushoto) Spika wa Baraza la Wawakilishi  Zubeir Ali Maulid na  Kamanda wa Brigedia ya Nyuki Zanzibar Brigedia Jeneral Sharif Sheikh Othman (wa pili kulia)  wakiwa katika   hafla ya chakula maalum kwa maaskari walioshiriki katika sherehe za Maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,hafla hiyo  iliyofanyika leo katika viwanja vya Kambi ya KVZ Mtoni
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akichukua chakula wakati wa hafla ya chakula maalum iliyoandaliwa kwa maaskari walioshiriki katika sherehe za Maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,iliyofanyika leo katika viwanja vya Kambi ya KVZ Mtoni Zanzibar
 Makamo wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi, (wa pili kushoto) na   Kamanda wa Brigedia ya Nyuki Zanzibar Brigedia Jeneral Sharif Sheikh Othman (wa pili kulia)  wakichukua chakula katika   hafla maalum kwa maaskari walioshiriki katika sherehe za Maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, hafla hiyo  iliyofanyika leo katika viwanja vya Kambi ya KVZ Mtoni
 Maaskari wa vikozi vya ulinzi walioshiriki sherehe za Maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,wakichukua chakula cha mchana kilichotayarishwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein leo  katika viwanja vya  Kambi ya KVZ Mtoni Zanzibar
 Maaskari wa vikozi vya ulinzi walioshiriki sherehe za Maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,wakichukua chakula cha mchana kilichotayarishwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein leo  katika viwanja vya  Kambi ya KVZ Mtoni Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akiagana na Brigedia Jeneral Sharif Sheikh Othman,Kamanda wa Brigedi ya Nyuki Zanzibar baada ya hafla ya Chakula  maalum aliyoiandaa kwa maaskari walioshiriki katika sherehe za Maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,Sherehe iliyofanyika leo katika kambi ya KVZ Mtoni Mkoa wa Magharibi Unguja. Picha na Ikulu. 





STATE HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE

Zanzibar                                                         4.2.2017
RAIS wa  Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein leo ameungana na Wakuu wa vikosi vya Ulinzi na Usalama wa SMT na SMZ pamoja na Maafisa na Askari katika hafla maalum ya chakala alichowaandalia kutokana na ushiriki wao katika gwaride la kutimia miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya Januari 12, 1964. 
Hafla hiyo ilifanyika huko katika viwanja vya Makao Makuu ya KVZ  Mtoni mjini Zanzibar na kuhudhuriwa na viongozi mbali mbali akiwemo Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd, Spika wa Baraza la Wawakilishi Zubeir Ali Maulid, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ, Haji Omar Kheir, na Vikosi wa na viongozi wengine. 
Akitoa neno la shukurani mara baada ya chakula hicho kwa niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Issa Haji  Ussi Gavu alitoa pongezi na shukurani kwa wapiganaji hao kwa ushiriki wao mzuri katika sherehe za kutimiza miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar. 
Katika maelezo yake, Waziri Gavu alisema kuwa Mapinduzi ndio yaliyowapa  uhuru wa kujitawala na kuendesha mambo yao wananchi wote wa Zanzibar, hivyo yataendelea kuenziwa, kutunzwa na kuthaminiwa kwa nguvu zote. 
Waziri Gavu aliendelea kutoa neno la shukurani kwa kueleza namna vikosi hivyo vilivyopamba sherehe hizo za miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa gwaride mwanana sambamba na nidhamu ya hali ya juu na kusisitiza kuwa mafanikio hayo yatakuwa ni muendelezo kwa sherehe za miaka ijayo. 
Aidha, Waziri Gavu alisema kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendela kusimamia umoja, mshikamano pamoja na amani na utulivu kwa wananchi wote wa Zanzibar kwani ndio rasilimali pekee inayoweza kusukuma mbele maendeleo ya Zanzibar. 
Mapema Brigedia Jenerali Sharif Sheikh Othman alitoa neno la shukurani kwa niaba ya wapiganaji wote kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Barza la Mapinduzi na kuipongeza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa jinsi inavyowajali na kuwathamini walinzi wake kwa kuwaandalia chakula hicho kutokana na ushiriki wao wa sherehe za kutimiza miaka 53 ya Mapinduzi ya Matukufu ya Zanzibar. 
Alisema kuwa mkusanyiko huo ni muhimu sana kwani unatoa fursa ya askari na wapiganaji wote kupata kubadilishana mawazo sambamba na kutathmini gwaride lililopita na kujipanga vyema kwa gwaride lijalo la mwaka 2018 la kutimiza miaka 54 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar jambo ambalo ni muhimu hasa kwa vikosi hivyo. 
Brigedia Generali Othman ambaye piandie Msimamizi Mkuu wa Gwaride hilo lililopita alieleza kuwa vikosi vya Ulinzi na Usalama vya SMT na SMZ vitaendelea kushirikiana zaidi na Serikali ikiwa ni pamoja na kushauriana na kusisitiza kuwa mda wote wako tayari kupokea maelekezo ikiwa ni pamoja na kufanya tahmini ya gwaride la sherehe za kutimiza miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar zijazo.

Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar
Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822 
 E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk

WAFANYAKAZI WA SERIKALI WILAYANI HANDENI WATAKIWA KUTOA USHIRIKIANO WAKIHITAJIKA KUTOA USHAHIDI MAHAKAMANI

$
0
0
Wafanyakazi wa Serikalini Wilayani Handeni wametakiwa kutoa ushirikiano kwa namna yoyote ile kama kuna eneo wanatakiwa kutoa ushahidi Mahakamani. Wametakiwa kuhudhuria mahakamani ili waweze kusaidia haki iweze kupatikana kwa wakati.
  
Kauli hiyo ilitolewa na Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mh. Godwin Gondwe alipokuwa akihutubia wananchi na wataalamu mbalimbali kwenye ukumbi wa Mahakama ya Wilaya ya Handeni jana katika maadhimisho ya  siku ya sheria Nchini  iliyoandaliwa na Mahakama ya Wilaya mwaka 2017 yenye kauli  mbiu ya  “ umuhimu wa utoaji haki kwa wakati kuwezesha ukuaji wa uchumi”.

Gondwe alisema “amani na utulivu ndio matunda ya Haki, sehemu yeyote iliyokosa amani na utulivu basi lazima kuna haki imepokonywa” Kuli mbiu yetu inatukumbusha wadau wote ambao tunasimamia sheria kuanzia jamii ya kawaida , wataalamu, mawakili, wanasheria ,TAKUKURU, uhamiaji na magereza tuweze kufanya kazi kwa pamoja ili haki iweze kutendeka kwa wakati na kukuza uchumi wetu.

Aidha alieleza kuwa TAKUKURU, Magereza, Uhamiaji , Wanasheria na Mawakili wa Serikali na kujitegemea hawataweza kufanikiwa katika kupambana na Rushwa na kutoa haki kama Mahakama haitakuwa mdau mkuu katika hili. Alisema kuwa kwa kuliona hilo Mahakama imetoa elimu kwa  wananchi wiki nzima juu ya umuhimu wa utoaji wa haki kwa wakati kuwezesha ukuaji uchumi.

Mahakama yenyewe imefahamu  nafasi ya kusimama na kuweza kushirikiana na wadau wote ili kuhakikisha kwamba wananchi wanoishi Handeni wanapata haki mbali na changamoto mbalimbali zinazoikumba Mahakama hasa ukosekanaji wa watoa ushahidi hali inayopelekea kuchelewa kwa kesi na maranyingine kufungwa kwa kukosa ushahidi uliojitosheleza. Mwananchi anapodai haki lazima afahamu kuwa anao wajibu wa kufanya ili haki hiyo aweze kuipata, alisema Mh. Gondwe.

Aliongeza kuwa Serikali inafahamu mabaraza ya ardhi yanamatatizo, kwa kuliona hilo wanasheria wa Halmashauri ya Mji Handeni  wameanza kuelimisha viongozi wa mabaraza ya ardhi namna bora ya kusimamia kesi na wameelezwa  jinsi gani ambavyo wakienda kinyume mabaraza hayo yanaweza kuvunjwa kwani zipo taasisi nyingine kama TAKUKURU ambazo wanaweza kushughulikia wakiukaji wa kanuni za mabaraza ya ardhi kama watu wengine ambao sio waadilifu katika mifumo ya kiserikali. Viongozi wa Serikali wasitumie mifumo ya kiserikali kujihalalishia mapato yasiyo halali. Upande wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Mkurugenzi na wanasheria waeanza mikakati ya  kutoa elimu kwa mabaraza ya ardhi.

Mh. Gondwe Alieleza kuwa nyaraka nyingi za serikali zinatengenezwa bandia, alivitaka vyombo vinavyohusika na utoaji haki kuhakikisha wanahakiki nyaraka/vielelezo kutoka malaka husika ili viweze kuwa halali kwa utoaji wa haki.

Mwisho alizitaka taasisi za Serikali kufanya kazi na kuhakikisha zinawezesha Mahakama kwenye kesi ili kusaidia kesi hizo ziweze kuisha kwa wakati na kuokoa muda ambao wananchi wanapaswa kushiriki katika kukuza Uchumi mbali na jiografia ngumu ya Wilaya ya Handeni.

Mh. Hakimu Mkazi Mfawidhi Wilaya Bw.Anorld Kileo alieleza kuwa Mahakama kama muhimili wa Serikali ndio chombo pekee kinachotoa Haki.  Dhima ya maadhimisho  haya inatutaka sisi kama watendaji wa Mahakama tuliokabidhiwa mamlaka ya kutoa haki tuweze kutoa haki kwa wakati ili kuwezesha jamii kuweza kuendelea na shughuli zao za Uchumi wa mtu binfsi na Taifa kwa ujumla.

Maadhimisho ya siku ya sheria Nchini  hufanyika kila mwaka wiki ya kwanza ya mwezi wa pili. Maadhimisho hayo yalijumuisha wadau  mbalimbali kutoka Halmashauri ya Mji na Vijijini Handeni wakiwemo Wanasheria, Mawakili, Idara ya Uhamiaji, Magereza, TAKUKURU na Polisi, yenye kauli mbiu ya  Umuhimu wa utoaji haki kwa wakati kuwezesha ukuaji uchumi”.

Alda  Sadango
Afisa habari
Halmashauri ya Wilaya ya Handeni.

 Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mh. Godwin Gondwe akihutubia wananchi na viongozi mbalimbali kwenye maadhimisho hayo
 Afisa upelelezi Bw. Paul Kimaro akitoa hotuba fupi wakati wa maadhimisho ya sheria
 Mkuu wa Wilaya na wataalamu mbalimbali wakati wa wimbo wa Taifa.
 Waendesha mashtaka wa Wilaya ya Handeni Bw.Joseph Hamisi na Nzagalila Kikwelele  wakisikiliza hotuba wakati wa maadhimisho.
 Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wikaya ya Handeni Bw. Noel Abel akisalimia wananchi.
 Wanasheria wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Bw. Amani Mangesho wa kwanza  kushoto na Bw. Joseph Vungwa wakijitambulisha kwa wananchi wakati wa maadhimisho
 Mh. Hakimu mkazi mfawidhi wa Wilaya ya Handeni na Kilindi Bw.Anorld kileo akitoa hutuba fupi wakati wa maadhimisho.
 Moja ya mwananchi akitoa hoja ya kupatiwa ufafanuzi.
Picha ya pamoja  Mkuu wa wilaya,  wataalamu  na wadau mbalimbali wa wanaosimamia Sheria.

The Embassy of Switzerland Contributes to East Africa’s Premier Music Festival

$
0
0



The Embassy of Switzerland Contributes to East Africa’s Premier Music Festival

 The Embassy of Switzerland has contributed over TZS 260 million to support the Sauti za Busara music festival for the next three years. The Swiss Ambassador to Tanzania, H.E. Florence Tinguely Mattli, met with the Chairman of the Busara Promotions Board of Trustees Hon. Simai Mohammed for the handover at the Swiss Embassy offices in Dar es Salaam on February 3.

The Sauti za Busara festival is one of Africa’s leading music events. This unique annual festival promotes respect for diversity by bringing people together to celebrate live music from across the continent. This festival’s mission is to increase visibility and accessibility for African music, develop skills and opportunities for those in the music industry and strengthen regional and international networking and partnerships.

“Switzerland has been promoting and supporting various initiatives and events within the arts and culture sector in Tanzania for over a decade now,” said Ambassador Tinguely Mattli. “The Sauti za Busara festival is a good example of a cultural event that brings people together to enjoy the arts while contributing to economic development.”

Honourable Simai expressed appreciation on behalf of the Busara Promotions Board of Trustees for the support. “The sustainability of most cultural organizations in Africa has mostly depended on support from donors. The support from the Swiss Embassy is a huge boost for this great festival,’’ he said.

The 14th edition of the Sauti za Busara music festival will be held between 9 and 12 February 2017 at the Old Fort in Stone Town, Zanzibar.

WAALIMU WAISHAURI SERIKALI KUTOCHANGANYA SIASA NA NA ELIMU

$
0
0

Na Anthony John Glob Jamii.
 
 Chama cha walimu wanaofundisha masomo ya uraia wameitaka serikali kutokuchanganya maswala ya siasa na elimu kwakuwa yanawaathiri wanafunzi .

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa miradi wa chama hicho Goodluck Moleli amesema kuwa walimu wameonekana kutokushirikishwa katika maswala ya mabadiliko ya mitaala ya elimu na badala yake kutokujua mambo yanayo endelea katika mabadiliko ya mitaala hiyo ya elimu.

‘’Leo hii tumekutana hapa katika warsha hii ya walimu iliyoandaliwa na Ceta ilikujadili ni jinsi gani ya kuboresha elimu ya Tanzania Lakini tunaiomba Serikali ipunguze maswala ya kubadilisha mitaala ya elimu mara kwa mara kwakuwa wanafunzi wengi wanashidwa kufanya vizuri katika masomo yao’’ amesema Moleli

Mbali na hayo Mwalimu wa shule ya sekondari ya Kibweheri iliyopo Kibamba Sabrina Makafu amesema mtawala bado unashida na silabasi bado haziendani na vile tunavyo fundisha darasani mfano katika somo la kingereza unakuta tunacho fundisha sio kile kinacho toka katika mitihani.

‘’Inatupa sisi ugumu wa kufundisha kwakuwa tunayofunsisha hatuna uhakika kama ni hayo yatakayo letwa hivyo tunaiomba serikali kulifanyia kazi swala hili’’ amesema Mkafu.
Mkurugenzi wa miradi wa chama cha walimu wanaofundisha masomo ya uraia Googluck moleli akizungumza na waandishi wa habari mapema leo,jijini Dar.
Mwalimu wa shule ya sekondari sabrina makafu akizungza na waandishi wa habari jijini hapa leo hii
 

VIJUSO VYA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI FEBRUARY 5,2017


DC Simanjiro aizindua Mazubu Grand Hotel ya Mji mdogo wa Mirerani

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, mhandisi Zephania Chaula amezindua uwekezaji mkubwa wa hoteli ya kisasa ambayo ndiyo kubwa kuliko zote Mkoani humo, Mazubu Grand Hotel iliyopo Mji mdogo wa Mirerani.

Akizungumza wakati akizindua hoteli hiyo, mhandisi Chaula amewataka wafanyabiashara na wachimbaji wa madini ya Tanzanite kuwekeza kwenye mji mdogo wa Mirerani kuliko kuchuma madini hayo na kwenda kuwekeza sehemu nyingine.

“Tunakupongeza mno ndugu yetu Elias Kipunile Maduhu kwa kufanikisha mradi huu kwani umetupa heshima kubwa watu wa wilaya hii ya Simanjiro kwani kwenye mkoa wote wa Manyara, hakuna uwekezaji mkubwa wa hoteli kama hii,” alisema mhandisi Chaula.

Hata hivyo, Mkurugenzi wa Mazubu Grand Hotel Elias Kipunile Maduhu, alisema uzalendo wa kuishi Mirerani ndiyo umesababisha yeye awekewe kwenye eneo hilo kwani mahali unapoishi inakubidi upathamanimi kama nyumbani kwako.

Amesema Mazubu Grand Hotel imeshatoa ajira kwa watu 26 na lengo lao ni kuwapatia ajira watu 40 hadi 50 kwa siku za baadaye.
 Zoezi la uzinduzi wa Mazubu Grand Hotel, likiwa limefanywa na Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, mhandisi Zephania Chaula kwa kukata utepe.
 Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara mhandisi Zephania Chaula na Mkurugenzi wa Mazubu Grand Hotel, Elias Kipunile Maduhu wakibadilishana mawazo baada ya kufanyika uzinduzi wa hoteli hiyo ya kisasa.
 Jengo la Mazubu Grand Hotel ya Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, ambao ni uwekezaji mkubwa kufanyika wa hoteli kwenye mkoa huo.
Mkugurenzi wa Mazubu Grand Hotel ya Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara Elias Kipunile Maduhu, akizungumza mara baada ya Mkuu wa Wilaya hiyo mhandisi Zephania Chaula kufanya uzinduzi wa hoteli hiyo ya kisasa.

IDADI KUBWA YA WAKAZI WA WILAYA YA IGUNGA WAPO HATARINI KUPAMTWA NA MAGONJWA YA SHINIKIZI LA DAMU

$
0
0
Na,Jumbe Ismailly,Igunga Feb,05,2017 Afya

IDADI kubwa ya wananchi wa Wilaya ya Igunga,Mkoani Tabora wapo hatarini kupatwa na magonjwa ya shinikizo la damu kutokana na kutokuwa na utamaduni wa kupima afya zao hali ambayo inachangia miili yao kuwa na uzito mkubwa kupita kiasi.

Mganga Mkuu wa Wilaya ya Igunga,Dk.Godfrey Mgongo aliyasema hayo wakati wa zoezi la kupima afya kwa watumishi,madiwani pamoja na wananchi ambao ni wanachama wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya afya (NHIF) wa Halmashauri ya wilaya hiyo lililofanyika kwenye viwanja vya Ofisi za Halmashauri hiyo.

“Kitu ambacho tumekigundua ni kwamba watumishi wengi au watu wengi wana uzito uliopitiliza,uzito mkubwa na hii inaweza ikapelekea ukapata magonjwa ambayo yatawaathiri katika maisha yao”alisema Dk.Mgongo.

Hata hivyo mganga mkuu huyo wa wilaya alivitaja vitu vilivyopimwa na wataalamu hao kutoka shirikisho la vyama vya magonjwa yasiyokuwa ya kuambukiza(TANCDA) kuwa ni uzito,shinikizo la damu,homa ya ini pamoja na kisukari na zoezi hilo limefanyika kwa siku nne ambapo lilianza kwa watumishi wa Halmashauri na baadaye huduma hiyo ilielekezwa kwa madiwani pamoja na wananchi.

Kwa mujibu wa Dk.Mgongo kati ya zaidi ya watumishi 60 wa Halmashauri hiyo waliopatiwa huduma ya upimaji wa afya, imegundulika kuwa tatizo kubwa linalowakabili watumishi hao ni uzito ingawa kuna tatizo la homa ya ini na ugonjwa wa kisukari ndiyo unaofuatia.

“Lakini pia kwa waheshimiwa Madiwani kuanzia asubuhi mpaka sasa wameshapimwa madiwani 61 na imegundulika kwamba robo tatu ya waliopima wanakabiliwa na tatizo la kuwa na uzito mkubwa kupitiliza,kisukari na homa ya ini vina asilimia ndogo sana”alisisitiza Mganga mkuu huyo wa wilaya.

Kuhusu madhara yatokanayo na uzito mkubwa kupitiliza,Dk,Mgonga hata hivyo aliyataja kuwa ni pamoja na shinikizo la damu,kisukari na magonjwa mengine yanayotokea baada ya kupata magonwa hayo na endapo ugonjwa mmoja ukitatuliwa unasaidia kuzuia magonjwa mengine mengi yanayoweza kutokea.

Akitoa ushauri kwa watumishi,wananchi na madiwani wanachama waliohudhuria katika zoezi hilo la kupima afya zao,Mganga Mfawidhi,Bi Elizabeth Mpangala aliwashauri wananchi hao kupunguza matumizi ya chakula kwani kwa kufanya hivyo kutasaidia pia uzito kupungua.

Aidha Bi Mpangala aliwasisitiza pia kwamba wazidishe matumizi ya mboga za majani,vyakula vya protini pamoja na kufanya mazoezi kutasaidia kupunguza uzito huku akionyesha kutoridhishwa na baadhi ya watu kutotumia mboga za majani ambazo zina sukari ndogo,tofauti na wanga na vyakula vyenye protini.

Naye diwani wa kata ya Iborogelo,Bwana Simbalugombi Ndali aliweka bayana kwamba baada ya kushiriki katika zoezi hilo la kupima afya aligundulika kuwa na kilo 93 na hivyo kutumia fursa hiyo kutoa wito kwa wananchi kuhakikisha wanafuata ushauri wa wataalamu wa afya ili kukabiliana na magonjwa hayo yanayotokana na kuwa na uzito mkubwa kupitiliza.
 Jengo la Ofisi za Halmashauri ya wilaya ya Igunga,Mkoani Tabora kulikofanyikia zoezi la upimaji wa afya kwa watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Igunga,Madiwani wa Halmashaurri hiyo pamoja na wananchi wa Halmashauri waliojiunga na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya(NHIF).
 Baadhi ya wataalamu wa sekta ya afya waliokuwa wakitoa huduma za upimaji afya kwa watumishi wa Halmashauri ya Igunga,Madiwani pamoja na wananchi wa kawaida waliojiunga na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya(NHIF)ambapo iligundulika kuwa idadi kubwa ya wakazi wake wapo hatarini kupatwa na magonjwa ya shinikizo la damu kutokana na kutokuwa na utamaduni wa kupima afya zao na hivyo kuchangia miili yao kuwa na uzito mkubwa kupita kiasi.
Baadhi ya Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Igunga,Mkoani Tabora wakiwa kwenye mkutano wa Baraza la kawaida la madiwani wa Halmashauri hiyo ambalo lilitumika pia kushiriki katika zoezi la upimaji afya kwa waliojiunga na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya(NHIF).(Picha Na Jumbe Ismailly)

NINAVYOIONA CCM YA SASA

$
0
0
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM),Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt John Pombe Magufuli akizungumza kwenye moja ya mikutano yake.

Nianze kwa kuitakia heri ya kumbukizi ya miaka 40 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi, chama kinachoendelea kushika dola ya Tanzania toka kiasisiwe mwaka 1977 ambalo ni zao la vyama vya TANU na ASP.

Misingi mizuri iliyojengwa na waasisi wa Taifa la Tanzania Mwalimu Julius Nyerere (Tanganyika- Bara) na Abeid Amani Karume (Zanzibar - Visiwani) imesababisha Wananchi wa Tanzania kwa muda mrefu kuishi kwa amani na utulivu huku wakifanya mambo yao kwa uhuru bila ya kuingiliwa na mtu yeyote Yule.

Tofauti na mataifa mengine Watanzania wako huru zaidi kwenda kokote kule ndani ya nchi na hata kuishi au kufanya kazi ama biashara bila ya bughudha yoyote endapo taratibu na sheria zitazingatiwa vyema.

Hali hii ni tofauti na nchi nyingine zikiwemo za jirani kama vile Kenya , Kenya Rwanda, Burundi, Kongo na hata Uganda ambapo ukabila umetalaki kuanzia ngazi ya kijiji hadi Taifa lakini kwa Tanzania hakuna ubaguzi wa rangi,dini wala kabila.

Hiyo inatokana na uongozi imara, sera safi, upendo na kila aina ya ubora uliotukuka ndani yake kwa jamii ya kitanzania. Jambo linaloendelea kutia faraja ni kuwa tangu ianzishwe CCM imeendelea kuwa ni chama kinachotawala na kuongoza nchi. Na siri yote ya mafanikio hayo ni kutokana na kuwa nguzo imara ambazo ni Wanachama, Ilani ya chama, na Viongozi wake.

Wanachama wake ambao ndio mtaji wa chama wapatao zaidi ya milioni nne na nusu na mashabiki wapatao ama zaidi ya milioni 10. CCM ni chama kisichozingatia uwepo au hata harufu ya ubaguzi wa rangi, kabila au dini ya mtu.

Hatua hio imewafanya Watanzania wengi kuanzia vijana kwa wazee, wake kwa wanaume kujivunia kuwa wanachama makini wa chama chenye mtazamo chanya wa kuwavusha kwenye neema. Ili kuhakikisha CCM inapata makada wa aina tofauti bila ya kujali umri, jinsia ilianzisha jumuiya za wazazi, wanawake (UWT) na vijana (UVCCM) ambazo ni viungo muhimu vya chama katika kuwaweka watu wote pamoja na karibu na hivyo kuendelea kuwa chama cha kishujaa katika kuwakomboa watu wake.

Pia kuna suala zima la uwepo wa ilani ya uchaguzi ambayo ni mkataba baina ya chama na wananchi au viongozi na wananchi ambao ndio wapiga kura wenyewe kupitia ilani, CCM inatoa ahadi zake mbalimbali za kutekelezwa katika muda uliopangwa wa miaka mitano.

Ni wazi kwamba ahadi hizo zimekuwa zikitekelezwa kwa kiwango kikubwa na cha kuridhisha kiasi cha kufanya Watanzania waendelee kuwa na imani nayo kila uchaguzi unapowadia. Hii inajidhihirisha wazi katika chaguzi kuu mbalimbali zilizofanyika mara tatu 1995, 2000, 2005, 2010 na 2015 ambapo CCM iliibuka na ushindi wa kishindo

Nguzo nyingine kuu ya CCM ni viongozi wake. Ndani ya CCM wenye dhamana ya chama ni wanachama wenyewe na wala si viongozi. Hali hii imesaidia kutokuwa na hata chembe au harufu ya umini wa mtu kujiona kuwa ana haki miliki ndani ya chama au ni kiongozi wa maisha. Ikumbukwe kuwa CCM ina haki zote kwa kiongozi yeyote yule aliyetokana na CCM.

Hiyo ni ishara kwamba ni chama chenye misingi imara ya uongozi na ndio maana kumekuwa na mabadiliko ya mara kwa mara ya uongozi kwa kufuata misingi ya katiba ya chama. Kila baada ya mitano hufanyika uchaguzi wa viongozi wa mashina hadi Taifa na katika uchaguzi huo ndipo watu huingia na kutoka.

Aidha hali hii ni tofauti na vyama vingine nchini ambavyo walivyoviasisi ni viongozi wa kudumu hadi hii leo. Wanapoambia kuna uchaguzi baadhi ya viongozi hao kufanya mizengwe kwa wale wanaonyesha nia ya kuleta mabadiliko na hata kuwafukuza.

Kwa sasa CCM ipo chini ya Uenyekiti wa Rais Dk. John Pombe Magufuli ambaye amekuwa mstari wa mbele kuhakikisha inaendelea kuongoza kupitia ridhaa ya Wananchi.

Ridhaa hii inatokana na CCM kuendelea kuwa na uongozi imara, sera safi, maendeleo bora na hivyo kuendelea kuwa tegemeo la kila Mtanzania anayependa haki na maendeleo pamoja na ustawi uliopo.

Hakuna binadamu aliyemkamilifu kwa kila kitu isipokuwa Mungu pekee. Kwa kulitambua hilo CCM iliona si vizuri endapo wataendelea kuwa peke yao. Mwaka 1990 uliletwa mswada na mwaka 1992 walio wachache (20%) wakapatiwa ushindi wa uletaji wa mfumo mpya ule wa vyama vingi.

Hivyo CCM ndiyo mkunga na mwanzilishi wa mfumo wa vyama vingi nchini. Tangu kuasisiwa kwake CCM imeendelea kuwa mkunga na kinara ndani ya utiriri wa vyama mbalimbali takribani 20 vya kisiasa vya hapa nchini.

Pia CCM hii imeendelea kuwa chama cha kimaskini kinachowakumbatia watu maskini na hii inajidhihirisha zaidi kupitia shughuli za kimaendeleo zinazofanywa na serikali za CCM zinazokuwa madarakani ambazo zote zina walenga watu maskini na watu wote kwa kuwa ujumla bila ya kujali rangi, dini wala kabila la mtu.

Lengo la kuanzishwa kwa CCM kulikuwa na malengo ya kumkomboa Mtanzania haswa Mkulima na mfanyakazi (kupitia nembo ya jembe na nyundo) ili kumfanya aweze kupiga hatua kimaendeleo. Hivyo hatutakosea endapo tutasema kuwa CCM ni chama cha kimapinduzi ya kweli na dhihiri mathalani CCM imekuwa daima chama tawala kinachopinga maradhi, ujinga na umasikini. Vile vile CCM kimeendelea kuwa mstari wa mbele kuleta maendeleo ya kiuchumi kijamii na kiutamaduni.

Mathalani katika elimu, kupitia mipango yake MMEM (Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi) na MMES (Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Sekondari) kumuwezesha kuwepo kea ongezeko la idadi ya Wanafunzi katika shule.

Hii inatokana na uwepo wa sera safi ya kuhakikisha kuwa kuna shule za Msingi katika kila kijiji na uwepo wa shule za Sekondari katika kila kata. Hali hii imesaidia uwepo wa shule 15,816 shule za msingi na shule 2,171 kwa shule za sekondari

Pia Serikali za CCM zimechakalikia uwepo wa vyuo mbalimbali ambapo mpaka sasa kuna jumla ya vyuo 47 hapa nchini toka vyuo 3 vilivyikuwepo wakati tunapata uhuru. Mfano ya vyuo hivyo ni chuo kikuu cha Dar es salaam “Mlimani” (UDSM) na matawi yake ambayo ni chuo cha Elimu Chang’ombe (DUCE) ;Chuo cha Madaktari Muhimbili; Chuo cha MKWAWA; Chuo cha ardhi (U-class).

Vyuo vingine vikuu ni pamoja na chuo cha kilimo cha Sokoine; Chuo kikuu cha Mzumbe, na chuo kikuu cha Dodoma (U – Dom) ambacho ni chuo kipya chenye uwezo wa kuchukua zaidi ya wanafunzi 40,000.

Upatikanaji wa maji vijijini 1961 ulikua 6% sasa ni 68%. Upatikanaji wa maji mijini 1961 ulikua 25% sasa ni 83%.

Upande wa huduma za kiafya; hospitali 1961 zilikua 48 sasa zipo 109. Zahanati 1961 zilikua 239 sasa zipo 6114.

Upande wa Elimu; Shule za msingi 1961 zilikua 3000 sasa zipo 16538. Walimu wa shule za msingi 1961 walikua 9885 sasa wapo 88905. Shule za sekondari 1961 zilikua 41 sasa zipo 4753. Walimu wa sekondari mwaka 1961 walikua 764 sasa wapo 88908.

Kwa mujibu wa Baraza la Mitihani NECTA ni kwamba mwaka 2016 ufaulu wa jumla umeongezeka kwa asilimia 2.56 kutoka asilimiq 67.53 mwaka 2015 hadi asilimia 70.09 mwaka 2016.

Upande wa Miundo mbinu, tulikua na km za barabara za lami 1300 zenye ukubwa wa kilomita 33,600 mwaka 1961 na sasa kuna kilomita 124,234 na zingine zinaendelea kukamilika kujengwa.

Serikali za CCM zimefanikiwa kuleta unafuu katika elimu na hata kuleta unafuu wa wanafunzi na kwa wazazi ama walezi wao kwa kuhakikisha kuwa elimu ya shule ya msingi ni lazima kila mtoto wa miaka saba na inatolewa bure; kila Mtanzania awe na elimu angalau ya kidato cha nne; kuondoa kero za ada za mitihani kwa shule za msingi na sekondari.

Wakati tunapata uhuru (1961) kulikuwa na Watanzania milioni 9 kati ya hao ni watu wasiozidi laki tatu waliobahatika kupata elimu ya darasani na waliokuwa darasani kipindi hicho hawakufika wanafunzi 1,500.

Takribani miaka 56 sasa baada ya uhuru, CCM imeendelea kuliongoza taifa letu lenye watu wapatao Milioni 45 (kwa mujibu wa sensa ya watu iliyofanyika nchini mnamo mwaka 2012) kwa kuhakikisha wanapatia elimu ya kutosha na yenye viwango. Leo hii asilimia kubwa ya Watanzania wameelimika hadi elimu ya ngazi ya chuo, na kwa mujibu wa takwimu za sasa kuna wanafunzi wapatao milioni 15 wakiendelea na masomo yao kwa ngazi mbalimbali kati ya hao kuna wanazuoni wapatao 120,000.

Hata kwa upande wa mikopo ya elimu ya juu nako CCM ipo bega kwa bega na jamii kwa kuhakikisha kuwa kila Mwanachuo anapatiwa mkopo wa gharama za elimu ya juu kwa kadri uwezo wa kifedha utakavyokuwa.Katika mwaka wa masomo wa 2005/2006 Bodi ya Mikopo ilitoa mikopo kwa  wanafunzi 42,729 iliyogharimu sh.  bilioni 56.1  na mwaka wa masomo wa 2016/2017 bodi ya mikopo ilitoa mikopo  iliyogharimu shilingi bilioni 487 kwa hapa nchini kuna changamoto kubwa cha kiwango hiki lakini tusisahau ya kwamba kiwango hiki na idadi hii ya wanafunzi wanaonufaika ni kikubwa mno ambacho hakiwezi kufikiwa na nchi yeyote ile ya Afrika Mashariki na kati. Nani kama CCM?

Hata kwenye mapambano ya dhidi ya ‘maradhi’ nako jitihada si za kubezwa. Tumeshuhudia ujenzi wa vituo vya afya kwenye kila kijiji na ujenzi wa zahanati kwenye kila kata Kwa mfano jumla ya Zahanati 5,422 na vituo vya afya 663 vimejengwa ndani ya utawala wa CCM. ; pia kuna uwepo wa hospitali kubwa kila mkoa mathalani Muhimbili hapa Dar es salaam, Bugando kule Mwanza na kadhalika.

Serikali za CCM hazina mzaha katika mapambano ya dhahiri dhidi ya Malaria, kifua kikuu, ukoma, matende trakoma, saratani za aina zote. Pia kuna mapambano dhidi ya magonjwa ya milipuko kama vile kipindupindu, kichocho, homa ya mafua ya ndege na yale mafua ya nguruwe.

Licha ya hapo, pia kumekuwa na maboresho ya dhati ya Afya ya mama na mtoto, upungufu wa vifo vya uzazi kwa utoaji wa elimu ya uzazi, kuongeza idadi ya wakunga na utoaji wa huduma ya kujifungua katika kiwango cha hali ya juu.

Katika kuhakikisha kuwa kila mtu maskini na asiyejiweza anapatiwa huduma sawa na sahihi kumekuwa na sera safi ya utoaji wa huduma bure za matibabu kwa makundi maalum kama vile walemavu ,vipofu, wazee wa zaidi ya miaka 60, na watu maskini wasiojiweza ilimradi tu apatiwe uthibitisho kutoka kwa Serikali za mitaa.

Pia kuna utoaji bure wa huduma za matibabu kwa magonjwa ya milipuko ndani ya jamii na hata pia wale wahanga wa majanga mbalimbali hawajasahaulika. Jamani kama haya si mafanikio ya Serikali za CCM ni kitu gani hasa?

Wahenga walisema, ‘Mnyonge mnyongeni, lakini haki zake mpeni’. Licha ya maneno mengi mno yasiyo na tija kusemwa semwa mitaani lakini kwa upande wa Serikali za CCM hawajavunjika moyo na daima wanazidi kusonga mbele kwa mbele. Baadhi ya viongozi kulumbana, ama matokeo ya uchaguzi kuteteleka ni sehemu tu mapito ya chama chochote kile cha kisiasa hapa Duniani ambapo unachukuliwa kama msingi mkuu wa maboresho ya chama husika.

Sote kwa pamoja tumeshuhudia na ujenzi na maboresho ya miundombinu, hakikisho la kilimo safi, mapambano dhidi ya ubadhilifu wa mali za umma, mapambano makali ya rushwa na ufisadi nchini, uanzilishwaji wa vyanzo vya ndani ya mapato ili tuweze kujitegemea wenyewe na kadhalika.

Tawala zote za CCM zilielewa ile dhana ya kuwa nchi haiwezi kuwa na mazingira mazuri ya kiuchumi iwapo miundombinu ya uchukuzi na usafirishaji itakuwa duni na isiyotosheleza mahitaji.

Katika serikali zake zimeendelea na ujenzi na uboreshaji wa miundombinu ya nchi bila ya kujalisha ni nani anaongoza na ni kwa awamu gani. Hata katika utawala wa awamu ya tano ya Rais Magufuli ameendeleza kazi nzuri na safi iliyofanywa na waliomtangulia.

Serikali za CCM hazina mzaha kabisa katika kuhakikisha kuwa rasilimali tulizonazo zinawasaidia Watanzania na kuhakikisha wanakusanya kodi ipasavyo kwa kukuimarisha vyanzo vilivyopo pamoja na kuanzisha vyanzo vipya ambapo mpaka mwaka huu 2017 mapato ya nchi yetu yameongezeka mara dufu hadi kufikia shilingi Trilioni 1.5 kwa mwezi mmoja. Nani kama CCM?

Serikali za CCM zimeendelea kufanya mengi mazuri ambapo kwa upande wa Zanzibar imefanikiwa kuondoa viashirio vya mvunjiko wa mshikamano, amani na utulivu waliokuwa nao kwa kuiondoa ile hali iliyotaka kuwatawala ya kununiana, kutokusalimiana, hadi ilifika kipindi watu walishindwa kuzikana. Leo hii hali ni tofauti kabisa kwani ile hali ya aibu imeshawaondoka na ule umoja wa Kitaifa, upendo, mshikamano na nguvu ya pamoja imerejea tena. Yote hayo yamewezekana chini ya himaya za utawala wa CCM.

Nyakati zote chama cha mapinduzi wameonekana kuguswa na kero na shida za Watanzania kwa kukata kiu ya kwikwi ya umaskini wa watu wake kwa kuwaletea maendeleo ya kweli. Hakika CCM ndio mama na mama ndio ajuaye uchungu wa mwana.

Mathalani kwa upande wa kilimo. Serikali za CCM haziko nyuma kwenye harakati za mapigano ya kilimo bora hapa nchini. Imefahamika kwamba zaidi ya asilimia 80 ya Watanzania ni wakulima ambao wanategemea kilimo kama nguzo ya maisha yao. Katika kuhakikisha kuwa kilimo kinaboreka zaidi na kuepusha mabalaa ya njaa kumekuwepo na uanzishaji wa kauli mbiu mbalimbali za kilimo.

Kauli mbiu hizo za kilimo ni kama vile, kilimo ni uti wa mgongo wa Taifa (1967); Siasa ni kilimo (1971); Kilimo cha kufa na kupona (1974); na kilimo kwanza (2009). Hakika matokeo chanya ya harakati za sera hizo zimekuwa zikionekana kwa dhahiri.

Katika idara ya ubadhilifu wa mali za umma nako harakati za mapambano hazikuwa nyuma. Tumeshuhudia idara mbalimbali zikibanwa mbavu kwa uthibiti imara kabisa tofauti na mitazamo hasi ya baadhi ya watu yalivyo. Mifano husika ni katika idara za maliasili, uvuvi, bandari, madini, chakula ambapo kote kumekuwa na uthibiti tulioshuhudia wa mapato na rasilimali za Watanzania.

CCM hii hii imekuwa mstari wa mbele kupambana na mafisadi (hawa ni wahujumu uchumi wanaotafuna rasilimali na mali za umma) Serikali za CCM imeweza kuvipa nguvu idara za kisheria ili kuweza kupambana na aina yeyote ilaya ubadhilifu na uhujumu uchumi. Kwa kutambua mgawanyo wa mihimili ya madaraka vimeachiliwa vyombo husika kufuatilia ili haki ipatikane bila kuhujumu upande wowote. Huu ndio utawala wa kisheria.

Mbali na hayo yapo mambo mengi ambayo CCM imefanya mapinduzi zaidi kupitia sera na ilani ambazo zipo kwa ajili ya kumlinda, kumtetea na kumkomboa mtu wa tabaka la chini na kati ambao ndio , asilimia kubwa ya Watanzania.

CCM inaundwa na Wanadamu ambapo inafahamika vyema kuwa Binadamu si Malaika hajakamilika na kwa kuwa CCM ipo kama Mwanadamu nayo pia haijakamilika, kuna sehemu imefanya vizuri sana, kuna sehemu imefanya vizuri na kuna sehemu pia haijafanya vizuri. CCM kama chama cha kisiasa chchote kile Duniani hakitaweza kumridhisha kila Mtu kwa kiwango kile kinachotaka.

Lakini hali hiyo haitaweza kufuta mazuri ambayo CCM kupitia serikali zake zilizokuwa na iliyopo madarakani kujivunia mafanikio yaliyopatikana toka enzi za kulikomboa Taifa letu toka kwa wakoloni Waingereza mpaka hapa ilipoifikisha.

Wakati CCM ikiadhimisha miaka 40 ya kumbukizi ya kuzaliwa kwake haina budi kubadilika na kuendana na kasi ya Mwenyekiti wake Rais Magufuli, kuendana na kasi ya Hapa Kazi Tu. Heri ya kuzaliwa Chama Cha Mapinduzi.

Na Emmanuel J. Shilatu

0767488622

TAARIFA YA KUANZA KUTUMIKA SHERIA YA HUDUMA ZA HABARI,2016 NA KANUNI ZAKE 2017

TRUMARK YAWEZESHA VIJANA KWA SEMINA ENDELEVU JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

Kampuni ya Trumark inayofanya mafunzo ya kuboresha ufanisi katika jamii imefanya mafunzo ya kujitoleta kwa kuwapatia Elimu ya kuwawezesha Wanawake Kiuchumi katika Chuo cha Ustawi wa Jamii Cha Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa TruMark Bi Agnes Mgongo ambaye pia ni Balozi wa Kuwawezesha Wanawake Kiuchumi Duniani kupitia Umoja wa Mataifa alisema kuwa ni muhimu vijana kutafuta na kukamata fursa mbalimbali kutoka kwenye jamii yao. Ikiwa ni pamoja na kujitolea kupitia vipaji vyao husuani elimu ili kuweza kuitumikia jamii.

Warsha hii iliyolenga kutimiza moja ya majukumu ya kuwa Balozi wa Kuwawezesha Wanawake Kiuchumi iliambatana na kutoa shuhuda mbalimbali za mafanikio, elimu na ajira huku wakiwajengea wanafunzi wa chuo hicho uwezo wa kutumia fursa mbalimbali zinazowazunguka katika jamii yao.

Mafunzo haya yalihimiza nguvu na matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii. Bi Agnes aliongeza kwa kusema kuwa mitandao ya kijamii ni mizuri hasa unapoamua ikuletee mafanikio katika maisha.

Jukwaa la Kimataifa la Kuwawezesha Wanawake Kiuchumi lina washiriki kutoka nchi 198, watazamaji 900,000, washiriki 18,500 na mabalozi 410 duniani kote.

Bi Agnes aliwashukuru Kampuni ya Kisima kwa kuweza kutambua umuhimu wakuwapatia vijana fursa nakuwezesha kufanikisha warsha hii muhimu. Na shukrani nyingine alizielekeza kwa uongozi wa chuo cha Ustawi wa Jamii cha Dar es Salaam kwa kuruhusu kutumia chuo cha kama jukwaa la kuwapatia elimu hii muhimu wanafunzi wa chuo hicho.

Tunategemea kufikia vijana wengi zaidi ili nao waweze kuwa mabalozi wazuri wa kuwawezesha wanawake kiuchumi hususan kwa nchi yetu ya Tanzania.
 Mkurugenzi wa TruMark Bi Agnes Mgongo  akizungumza na wanafunzi wa chuo cha Ustawi wa Jamii wakati wa semina ya kuwawezesha Wanawake Kiuchumi.
Muwezeshaji na Balozi wa Vijana kutoka East Community Youth Ambassador Platform Kamala Dickson akizungumza na wanafunzi wa chuo cha Ustawi wa Jamii wakati wa semina ya kuwawezesha Wanawake Kiuchumi.
Afisa habari wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania Stella Vuzo akizungumza na wanafunzi wa chuo cha Ustawi wa Jamii wakati wa semina ya kuwawezesha Wanawake Kiuchumi.
Wanafunzi wa Chuo cha Ustawi wa Jamii wakijiandikisha wakati wa semina ya kuwapatia Elimu ya kuwawezesha Wanawake Kiuchumi katika Chuo cha Ustawi wa Jamii Cha Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa TruMark Bi Agnes Mgongo  akiwa katika picha ya pamoja na wawezeshaji wa semina hiyo waliokaa na wanafunzi wa chuo cha ustawi wa Jamii.Picha na Zainab Nyamka.

WAZIRI NAPE NNAUYE ATANGAZA RASMI KUANZA KUTUMIKA KWA SHERIA ZA HUDUMA ZA HABARI NA KANUNI ZAKE

$
0
0

Na: Lilian Lundo – MAELEZO – Dodoma

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Nape Nnauye ametangaza rasmi kuanza kutumika kwa Sheria ya Huduma za Habari ya mwaka 2016 na kanuni zake za mwaka 2017.

Nape Nnauye ametoa taarifa hiyo leo katika ukumbi wa Bunge, Mjini Dodoma alipokuwa akiongea na vyombo vya habari juu ya kuanza kwa sheria hiyo na kanuni zake.

“Kwa mujibu wa kifungu cha 1 cha Sheria hiyo, ili ianze kutumika rasmi, Waziri wa Habari anatakiwa kuitangaza tarehe ya kuanza kutumika, hivyo napenda kuufahamisha Umma kuwa sheria hii imeanza kutumika tangu Desemba 31, 2016,” alifafanua Nape Nnauye.

Aliendelea kwa kusema kuwa kuanza kutumika kwa sheria hii ni jambo muhimu sana kwa tasnia hiyo kwa sababu inaihamisha taaluma ya habari kutoka fani ambayo mtu yeyote anaweza kujinasibu nayo hadi kuwa taaluma kamili yenye sifa mahsusi, maadili yanayojulikana pamoja na vyombo vya kusaidia kusimamia utekelezaji wake.

Vile vile amesema kuwa, sheria hiyo inaleta mfumo madhubuti wa kulinda haki za wanahabari kukusanya, kuhariri na kusambaza habari zao kwa uhuru.Pia sheria hiyo imeweka wajibu kwa wale watakaokiuka misingi na maadili ya taaluma hiyo, hivyo ukurasa mpya wa haki na wajibu umefunguliwa kupitia sheria hiyo.

Aidha amesema kuwa, Wizara imechambua maoni mbalimbali kuhusiana na sheria hiyo ambapo moja ya maoni hayo ilikuwa ni kiwango cha elimu cha mtu atakayeruhusiwa kufanya kazi ya taaluma hiyo. Ambapo wapo waliopendekeza kiwango cha elimu kiwe cheti, wengine diploma, digrii na hata PhD na wengine walitaka awe mtu yeyote anayejua kusoma na kuandika.

Amesema kuwa Serikali imesimama katikati ya maoni hayo, na sifa ya chini kabisa kwa kuanzia itakuwa ni Diploma ya uandishi wa Habari. Hivyo Serikali imetoa kipindi cha miaka Mitano kuanzia Januari, 01, 2017 kwa waandishi ambao hawana sifa hizo kujiendeleza na kufikia kiwango hicho cha elimu.

Hivyo basi, Idara ya Habari MAELEZO itaendelea kutoa “Press Card” bila kuwabana wanahabari kwa kuangalia vigezo hivi vya kitaaluma bali dhamana ya waajiri wao.

Sheria ya Huduma za Habari, 2016 ilisainiwa na Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli Novemba 16, 2016 na kuchapishwa kwenye gazeti la Serikali Novemba 18, 2016.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Moses Nnauye akioongea na Waandishi wa Habari kuhusu siku rasmi ya kuanza kutumika kwa Sheria ya Huduma za Habari ya Mwaka 2016 pamoja na Kanuni zake za 2017 katika Ukumbi wa Idara ya Habari Bungeni Mjini Dodoma 05/02/2017. Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Dkt. Hassan Abbasi.PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-WHUSM.

 

MTANZANIA NA MZAMBIA WANASWA INDIA NA MZIGO WA "UNGA" KILO NNE

$
0
0
Kushoto ni Mtanzania aliyejulikana kwa jina la Pamela David Kirrita (41) akiwa na mwanamke mwingine raia wa Zambia Thelma Mkandawire (38) wakiwa mbaroni kwa tuhuma za kukutwa na kilo 4 za madawa ya kulevya aina ya cocaine katika hoteli moja kusini mwa jiji la New Delhi, India. 

Naibu Mkurugenzi Mkuu wa kikosi cha kupambana na madawa ya kulevya cha New Delhi (NCB) Rajinder Pal Singh amesema watuhumiwa walikamatwa katika hoteli iliyopo eneo la Mahipalpur jana Februari 4, 2017. 

“Baada ya kupata taarifa kutoka vyanzo vyetu, timu yetu ikatega mtego kwa Mkandawire aliyewasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Indira Ghandi akitokea ughaibuni akiwa na mzigo huo. 

“Baada ya kuchekiwa uwanjani pale aliondoka na taxi hadi hotelini. Timu yetu ilimfuatilia na kumuona mara alipofika hotelini akakutana na Pamela David Kirrita aliyekuwa aupokee huo mzigo”, alisema Mkurugenzi wa NCB tawi la New Delhi. 

Amesema walipohojiwa Kirrita alibainisha kuwa alikuwa akiishi katika hoteli moja katika kitongoji kiitwacho Vasant Kunj tokea Januari, na kwamba alikuwa na mawasiliano na mtu mwingine raia wa kigeni ambaye ndiye angempasia mzigo baada ya kuuchukua toka kwa Mkandawire. 

Polisi wanasema mzigo ulifichwa kwenye uwazi wa begi la safari, na kwamba Mkabdawire aliwahi kukamatwa nchini Pakistani mwaka 2015 na kukaa mahabusu kwa zaidi ya miezi sita, huku Pamela akikiri kutembelea India zaidi ya mara sita tokea mwaka 2006.

Kwa sheria za India, mshtakiwa atayekutwa na hatia ya madawa ya kulevya yaliyokuwa ya kibiashara ni kifungo cha kati ya miaka 10 ama 20 gerezani na faini ya Rs 1 lakh (sawa na dola za Kimarekani 15,000) ama Rs 2 lakhs (dola 3000).

SHEREHE ZA KILELE CHA MAADHIMISHO YA MIAKA 40 YA CCM YAFANA LEO MKOANI DODOMA

$
0
0
 Katibu Mkuu wa CCM, Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akihutubia katika sherehe za Kilele cha Miaka 40 ya CCM mkoa wa Dodoma, zilizofanyika leo katika ukumbi wa CCM wa Dodoma Convertion Centre nje kidogo ya mji wa Dodoma.
 Makamu Mwenyekiti wa CCM-Bara Philip Mangula, akihutubia katika sherehe za Kilele cha Miaka 40 ya CCM mkoa wa Dodoma, zilizofanyika leo katika ukumbi wa CCM wa Dodoma Convertion Centre nje kidogo ya mji wa Dodoma. Kulia ni Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana
 Viongozi wakiwa meza kuu baada ya kuwasili ukumbini kuendelea na sherehe hizo
 Katibu Mwenezi wa CCM, Humphrey Polepole akihamasisha katika sherehe za Kilele cha Miaka 40 ya CCM mkoa wa Dodoma, zilizofanyika leo katika ukumbi wa CCM wa Dodoma Convertion Centre nje kidogo ya mji wa Dodoma.
 Katibu Mwenezi wa CCM, Humphrey Polepole akihamasisha katika sherehe za Kilele cha Miaka 40 ya CCM mkoa wa Dodoma, zilizofanyika leo katika ukumbi wa CCM wa Dodoma Convertion Centre nje kidogo ya mji wa Dodoma.
 Wanachama wa CCM wakiwa wamefurika ukumbini wakati wa sherehe hizo

 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akishauriana jambo na Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa wakati wa sherehe hizo leo katika ukumbi wa CCM wa Dodoma Convertion Centre nje kidogo ya mji wa Dodoma.
 Baadhi ya viongozi kwenye sherehe hizo
 Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa akisalimia wanacahama wa CCM wakati wa sherehe hizoleo katika ukumbi wa CCM wa Dodoma Convertion Centre nje kidogo ya mji wa Dodoma. PICHA ZINGINE KEM KEM KUHUSU SHEREHE HIZO/BOFYA HAPA 

WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII JINSIA WAZEE NA WATOTO YAKEMEA VITENDO VYA UKEKETAJI WANAWAKE NCHINI

$
0
0
Kaimu Mkurugenzi wa Maendeley ya Jinsia Bwana Julius Mbilinyi pamoja na   Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Watoto Bi. Margaret Mussai  k akifafanua jambo mbele ya  waandishi wa habari hawapo pichani kughusu siku ya kimataifa ya kuzuia ukeketaji
-------------------------------------------------------
Masuala ya ukatili wa kijinsia ikiwemo ukeketaji yameendelea kuwa tatizo kwa taifa na ulimwengu mzima na ili kukabiliana na tatizo hili, kumekuwa na mwitikio mkubwa wa kimataifa na kitaifa katika kukabilana na vitendo vya ukatili wa kijinsia.

Akiongea na vyombo vya Habari Jijini Dar es Salaam leo  Kaimu Mkurugenzi Idara ya Watoto wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Margaret Mussai amesema Serikali inalaani na kukemea vikali ukatili kwani unadhalilisha na kunyanyasa hadhi na utu wa mwanamke na mtoto wa kike akisema jambo hili halikubaliki.

Aidha aliongeza kuwa ni lazima jitihada za makusudi zichukuliwe na wadau wote kuhakikisha kuwa tunashiriki kwa pamoja kuzuia na hatimaye kutokomeza ukatili wa kijinsia katika jamii zetu, hususan kuzua ukeketaji.

Aidha kulingana na takwimu za Tafiti ya Idadi ya Watu na Afya (TDHS 2010)  inakadiriwa kuwa ukeketaji kwa wasichana na wanawake wenye umri wa miaka 15- 49 ni asilimia 14.6,  hii imepungua kidogo ukilinganisha na asilimia 17.9 mwaka 1996.     Aidha, takwimu hizo kwa mwaka 2015/16 zinaonyesha kiwango cha ukeketaji kwa wanawake na watoto kimepungua kutoka asilimia 14.6 ya mwaka 2010 hadi kufukia asilimia 10.

Margaret ametaja mikoa inayoongoza kwa vitendo vya ukeketaji ni Manyara (58%), ikifuatiwa na Dodoma (47%) na Arusha (41%) akitaja kuwa kupunguwa kwa vitendo vya ukeketaji  kunatokana na kampeni za uhamasishaji, uelewa na kujitambua kwa wasichana wanaofanyiwa vitendo hivyo, hofu ya kufungwa kutokana na uwepo wa sheria zinazotekelezwa, hivyo mangariba na wazee wa kimila kwa kiasi kikubwa wanaamua kuacha mila hii ya ukeketaji.  

Aidha Serikali inahimiza kuendeleza mila zenye manufaa na kujenga utamaduni chanya kwa jamii. Amewaomba  wadau mabalimbali wakiwemo wana habari, mashirika yasiyo ya kiserikali, Taasisi za dini, sekta binafsi na mamlaka za serikali za mitaa kuendelea kuongeza juhudi za kuelimisha jamii kuachana na mila zinazochochea ukeketaji.

Aidha Serikali imetunga sera, sheria, miongozo na kuandaa mikakati mbalimbali katika jitihada za kupambana na tatizo la ukatili wa kijinsia,ikiwemo ukeketaji, Sera ya Wanawake na Maendeleo ya Jinsia (2000) na Mkakati wa Maendeleo ya Jinsia (2005), Sera ya Maendeleo ya Mtoto (2008). Sheria ya Makosa ya Kujamiiana -SOSPA (1998) na Sheria ya Mtoto (2009) vyote vikiwa na lengo la kuzuia ukatili dhidi ya wanawake na watoto.

Katika kuongeza jitihada za kutokomeza ukeketaji serikali imeandaa Mpango wa kazi wa Taifa wa miaka mitano wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto (2017/18-2021/22). Mpangokazi umeanisha maeneo nane muhimu mojawapo ni la kuondoa mila na desturi zenye madhara. Kupitia mpango huu serikali imedhamiria kupunguza ukeketaji kwa wanawake kwa asilimia 50ifikapo mwaka 2022.

ZAIDI YA SHILINGI TRIONI 45 ZAHITAJIKA KUTOKA SEKTA BINAFSI ILI KUTEKELEZA MIRADI YA MAENDELEO NCHINI

$
0
0
Na Benny Mwaipaja-WFM, Dodoma 

 KIASI cha Shlilingi Trilioni 48 kinahitajika kutoka Sekta Binafsi ili kufanikisha ujenzi wa miradi mikubwa ya maendeleo kupitia Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa unaotekelezwa kuanzia mwaka wa fedha wa 2016/2017 hadi mwaka 2020/2021 .

 Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango, amesema hayo mjini Dodoma wakati akifunga semina ya siku moja iliyoandaliwa na Taasisi ya Sekta Binafsi hapa nchini-TPS iliyohusu zitaugharimiaji mkubwa wa miradi ya ubia kati ya sekta ya Umma na Sekta Binafsi kupitia mradi wa TVC (Tanzania Venture Capital and Private Equity Project) 
 "Imekadiriwa kuwa mahitaji ya fedha ya mpango huo ni takriban shilingi Trilioni 107, kati ya hizo shilingi Trilioni 59, sawa na asilimia 55, zitatokana na mapato ya Serikali na shiilingi Trilioni 48, sawa na asilimia 45 zitatokana na vyanzo vya Sekta Binafsi. 
 
 Amesisitiza umuhimu wa Sekta Binafsi kuwekeza zaidi kwenye kilimo na viwanda vitakavyosaidia kuongeza thamani ya mazao ya wakulima ili waweze kunufaika kiuchumi na kuendeleza nchi kwa ujumla Dkt. Mpango, ameahidi kuwa Serikali iko tayari kuhakikisha kuwa vitendea kazi muhimu vya utekelezaji wa mradi huo vinapatikana ili kuwezesha utekelezaji wa miradi hiyo ya ubia ukiwemo mradi wa ujenzi wa barabara ya njia sita kutoka Dar es salaam kwenda Chalinze.

 Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijabe (Mb), akizungunza wakati wa Semina iliyoandaliwa na Taasisi ya Sekta Binafsi hapa nchini-TPSF iliyohusu ugharimiaji mkubwa wa miradi ya ubia kati ya sekta ya Umma na Sekta Binafsi kupitia mradi wa TVC (Tanzania Venture Capital and Private Equity Project), mjini Dodoma
 Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), akihutubia washiriki wa semina  iliyoandaliwa na Taasisi ya Sekta Binafsi hapa nchini-TPSF iliyohusu zitaugharimiaji mkubwa wa miradi ya ubia kati ya sekta ya Umma na Sekta Binafsi kupitia mradi wa TVC (Tanzania Venture Capital and Private Equity Project), mjini Dodoma, ambapo waziri huyo ameitaka sekta binafsi kuwezesha upatikanaji wa Zaidi ya shilingi Trilioni 48 ili kusaidia ujenzi wa Miradi Mikubwa ya Maendeleo.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), (wa pili kulia) akiandika mambo mawili matatu yaliyojiri wakati wa semina  iliyoandaliwa na Taasisi ya Sekta Binafsi hapa nchini-TPSF iliyohusu zitaugharimiaji mkubwa wa miradi ya ubia kati ya sekta ya Umma na Sekta Binafsi kupitia mradi wa TVC (Tanzania Venture Capital and Private Equity Project), mjini Dodoma

BALOZI AAHIDI INDIA KUISAIDIA SEKTA YA ELIMU TANZANIA

$
0
0
Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda akiteta jambo na Meneja wa Kampuni ya uwakala wa vyuo vya nje, Global Education Link tawi la Dodoma, Hemed Mlapakolo (mwenye shati jeupe). Kushoto ni Balozi wa India Sandeep Arya.
Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda akiteta jambo na Meneja wa Kampuni ya uwakala wa vyuo vya nje, Global Education Link tawi la Dodoma, Hemed Mlapakolo (mwenye shati jeupe). Kushoto ni Balozi wa India Sandeep Arya. Picha na mpiga picha wetu. 
PINDAWaziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda akisaidia kitabu cha wageni alipotembelea banda ya maonyesho ya Kampuni ya Uwakala wa vyuo vya nje ya Global Education Link juzi. Kulia ni baadhi ya wafanyakazi wa kampuni hiyo.
………….

Na Mwandishi wetu, Dodoma

KUTOKANA na Tanzania kujikita kufufua uchumi katika sekta ya viwanda vya kati, Balozi wa India nchini, Sandeep Arya, ameihakikishia Tanzania kuisapoti kwenye suala la elimu kwa lengo la kuinua uchumi.

Akizungumza wakati akizindua maonyesho ya biashara yaliyoandaliwa na Chama cha Wafanyabiashara, Kilimo na Wenye Viwanda (TCCIA) mkoani Dodoma kwa kushirikiana na kampuni ya Global Education Link ya Tanzania juzi (jana), Balozi Arya alisema kukua kwa kasi uchumi wa India, kulitokana na kuwapo vyuo vingi vya elimu vyenye vifaa vizuri vya kufunduishia nchini humo.

“Kiwango cha elimu kinachotolewa India ni cha hali ya juu kutokana na upatikanaji wa vifaa vya kutosha vya kufundishia na kujifunzia, jambo linalowahakikishia wahitimu kutoka vyuo mbalimbali kupata kazi kwa urahisi,” alisema Arya na kuwashauri wanaotaka kusoma nje kuwasiliana na Global Education Link kwa vile wana ushirikiano wa karibu na ubalozi huo.

Alisema suala la utandawazi na mahusiano baina ya nchi hiyo na nyingine katika kurahisisha upatikanaji wa mahitaji muhimu, linachangia kuwakutanisha watu wa aina mbalimbali kupata elimu kutokana na kuwapo na vifaa vilivyopo.

Balozi Arya aliwahakikishia washiriki wa maonyesho hayo kuwa upatikanaji wa vifaa vya kisasa vya kufundishia nchini India, kumesaidia kutolewa kwa kiwango cha juu cha elimu.

Aidha, alisema baadhi ya mashirika makubwa duniani, viongozi wake walifanikiwa kusoma nchini India na kupata elimu iliyo bora.

Ubalozi wa India umeanzisha ushirikiano na GEL katika kuwasaidia Watanzania wanaotaka kusoma nje ya nchi hasa baada ya ubalozi huo kujiridhisha na namna kampuni hiyo ya uwakala wa vyuo vya nje inavyowafuatilia wanafunzi wake hata baada ya kuwaunganisha na vyuo vya nje kujua maendeleo yao.

Naye Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda aliyekuwa mgeni rasmi katika tukio hilo aliwataka watanzania kujiimarisha katika ujuzi akisema ndio msingi wa kila kitu.

Baadhi ya wanufaika wa elimu kupitia Kampuni ya Uwakala wa vyuo vya nje, Global Education Link (GEL), akiwamo Pelagia Mauma, alisema alifanikiwa kupata elimu bora nchini India kupitia kampuni hiyo kwa gharama iliyo nafuu zaidi.

“Gharama za elimu katika vyuo vyua India ni nafuu zaidi, hawa wenzetu hawaangalii ada bali wanachoangalia ni vipi mtu atafanikisha kupata elimu iliyo bora,” alisema Mauma.

Afisa Mtendaji wa TCCIA mkoa wa Dodoma, Fred Azaria pamoja na kueleza shughuli za chama chake, alisema wanalenga kupunguza umaskini kwa wananchi wa mkoa wa Dodoma baada ya kuandaa maonyesho ya vifaa vya shule na zana za kufundishia kutoka India.

“Nawaomba Watanzania waweze kutumia fursa iliyopo ya kupata elimu, huku wakiwaomba Watanzania kutumia fursa hiyo kujipatia elimu nchini India,” alisema.

Nae Meneja wa GEL tawi la Dodoma, Hemed Mlapakolo alisema sababu ya kushirikik maonyesho hayo ni kutoa nafasi kwa Watanzania kuhusiana na namna gani mtu anaweza kufanya uchaguzi sahihi wa kozi ya pale anapotaka kusoma nje ya nchi.

“Tumekuwa mawakala wa vyuo vya nje kwa zaidi ya miaka kumi sasa, wengi wamekuwa wakipitia kwetu kuunganishwa na vyuo vya nje, tumeona tuje hapa ili waweze kupata ufahamu zaidi kuhusiana na uchaguzi wa vyuo vya nje na uchaguzi wa masomo ya kusomea pia,” alisema Hemed.

Hemed alifafanua kuwa kumekuwa na changamoto kubwa kwa Watanzania katika uchaguzi wa nini cha kusoma. “Utakuta wengi wanachojua ni udaktari, lakini kwenye udaktari kuna wa aina nyingi, kuna udaktari wa magonjwa ufahamu, udaktari wa meno tu, udaktari wa mifupa na kadhalika, kazi yetu ni kutoa ushauri wa aina hii. Tunafanya hivi ili kukumbushana kwa sababu kama wengi watakuwa kwenye fani au utaalamu wa aina moja, maana yake ni kwamba fani nyingine zitakosa wataalam au zitakuwa na wataalam wachache,” alisema.

DK.SHEIN AWAANDALIA CHAKULA VIAJANA WA HALAIKI

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akisalimiana na viongozi mara alipowasili katika viwanja vya Kambi ya KVZ Mtoni Mjini Magharibi Unguja leo katika hafla ya chakula maalum kwa Vijana walioshiriki Halaiki ya sherehe za Maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akisalimiana na viongozi mara alipowasili katika viwanja vya Kambi ya KVZ Mtoni Mjini Magharibi Unguja leo katika hafla ya chakula maalum kwa Vijana walioshiriki Halaiki ya sherehe za Maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akisalimiana na viongozi mara alipowasili katika viwanja vya Kambi ya KVZ Mtoni Mjini Magharibi Unguja leo katika hafla ya chakula maalum kwa Vijana walioshiriki Halaiki ya sherehe za Maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,

Baadhi ya Viongozi walioshiriki katika hafla ya chakula cha mchana alichokiaandaa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kwa Vijana wa halaiki walioshiriki katika sherehe za Mapinduzi ya mwaka 2017kutimiza miaka 53 katika viwanja wa Kambi ya KVZ Mkoa wa Magharibi Unguja leo.

Wakufunzi wa Vijana walioshiriki halaiki wakiimba wimbo maalum wakati wa hafla ya chakula cha mchana alichokiaandaa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kwa Vijana wa halaiki walioshiriki katika sherehe za Mapinduzi ya mwaka 2017 kutimiza miaka 53 katika viwanja wa Kambi ya KVZ Mkoa wa Magharibi Unguja leo.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akiteta na Katibu wa Uhamasishaji Ali Mohamed Baraka (Shasha)(wa pili kulia) akiwepo Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe,Zubeir Ali Maulid (kulia) na Makamo wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi (kushoto) na Waziri wa nchi Ofisi ya rais tawala za Mikoa,Serikali za Mitaa na Idara maalum za SMZ Haji Omar Kheir, wakati wa hafla maalum ya chakula alichowaandalia Vijana walioshiriki katika Halaiki ya sherehe za maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar iliyofanyika leo katika viwanja Kambi ya KVZ Mkoa wa Magharibi Unguja leo.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati ) akitia chakula wakati wa hafla maalum ya chakula aliyowaandalia Vijana walioshiriki katika Halaiki ya sherehe za maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar iliyofanyika leo katika viwanja vya kambi ya KVZ Mkoa Magharibi Unguja.

Baadhi ya Viongozi walioshiriki katika hafla ya chakula cha mchana alichokiaandaa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kwa Vijana wa halaiki walioshiriki katika sherehe za Mapinduzi ya mwaka 2016 kutimiza miaka 53 katika viwanja wa Kambi ya KVZ Mkoa Magharibi Unguja iliyofanyika leo.
Baadhi ya Wakufunzi wakichukua Chakula kilichoandaliwa kwa Vijana walioshiriki katika halaiki ya maadhimisho ya Sherehe za Miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar hafla hiyo iliyoandaliwa kwa ajili yao na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein katika viwanja vya Kambi ya KVZ Mtoni Mkoa wa Magharibi Unguja leo.
Baadhi ya Vijana walioshiriki katika halaiki ya maadhimisho ya Sherehe za Miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar wakiwa katka hafla ya Chakula katika hafla ya kilichoandaliwa kwa ajili yao na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein katika viwanja vya kambi ya KVZ Mtoni Mkoa Mjini Magharibi Unguja leo.

Baadhi ya Vijana walioshiriki katika halaiki ya maadhimisho ya Sherehe za Miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar wakichukua Chakula katika hafla ya iliyoandaliwa kwa ajili yao na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein katika viwanja vya kambi ya KVZ Mtoni Mkoa Mjini Magharibi Unguja leo.
Baadhi ya Vijana walioshiriki katika halaiki ya maadhimisho ya Sherehe za Miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar wakichukua Chakula katika hafla ya iliyoandaliwa kwa ajili yao na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein katika viwanja vya kambi ya KVZ Mtoni Mkoa Mjini Magharibi Unguja leo.
Hawa ni miongoni mwa Vijana walioshiriki katika halaiki ya maadhimisho ya Sherehe za Miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar wakiwa katika hafla ya chakula kilichondaliwa kwa ajili yao na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein katika viwanja vya kambi ya KVZ Mtoni Mkoa Mjini Magharibi Unguja leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) pamoja na Viongozi na kamati Uhamasishaji Vijana wa halaiki walioshiriki katika sherehe za Mapinduzi kutimiza miaka 53 wakiwa katika picha ya pamoja katika viwanja Kambi ya KVZ Mtoni Mkoa wa Mjini Magharibi leo baada ya hafla ya chakula,[Picha na Ikulu.] 05/02/2017.
Viewing all 46329 articles
Browse latest View live




Latest Images