Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live

WATAALAMU WA AFYA WATAKIWA KUPIGANIA AFYA YA MAMA NA MTOTO.

$
0
0
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu afungua mkutano wa mwaka wa huduma za Afya na uzazi na mtoto unaofanyika mjini Dodoma
TUTA 3
Waziri Ummy Mwalimu kwenye picha ya pamoja ya mkutano huo wa siku tatu unaojumuisha waratibu wa Afya ya uzazi wa kanda na mikoa, wenyeviti wa kanda Afya ya uzazi na watoto pamoja na wadau wa maendeleo katika Afya ya uzazi na mtoto kote nchini
TUTA
Baadhi ya wajumbe wa mkutano huo wakimsikiliza Waziri Ummy Mwalimu(hayupo pichani) wakati wa ufunguzi
TUTA 1
Mjumbe kutoka UNICEF bi Hafsa Khalfani akifuatilia mkutano huo
……….

WATAALAMU  wa  afya  wametakiwa kutumia utaalamu na wajibu wao katika kuokoa maisha ya mama na mtoto ili kuepuka vifo vitokanavyo na uzazi  kwa ajili ya kujenga taifa lenye kizazi imara.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya ,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati wa ufunguzi wa mkutano katika ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa huduma za afya ya uzazi na mtoto uliofanyika Mkoani Dodoma.
“Tumieni utaalamu wenu na wajibu mliopewa kuleta mabadiliko ya kiutendaji na ufanisi katika kuboresha afya ya uzazi na mtoto” alisema Waziri Ummy.
Aidha Waziri Ummy amesema kuwa wataalamu na wasimamizi wa huduma za afya ya uzazi na mtoto, wana nafasi kubwa ya kuleta mabadiliko chanya, kwa kuhakikisha kuwa, huduma zinaboreshwa zaidi na kutolewa kulingana na viwango vilivyowekwa.
Kwa mujibu wa Waziri Ummy amesema kuwa idadi ya vifo vitokanavyo na uzazi na vifo vya watoto wachanga imeendelea kuwa juu.  Mathalani, vifo vitokanavyo na uzazi mwaka 2010 vilikuwa vifo 454 kwa kila vizazi hai 100,000 na mwaka 2015 viliongezeka hadi vifo 556 kwa kila vizazi hai 100,000.
Aidha Waziri Ummy alisema kuwa kiwango cha vifo vya watoto wachanga kimeendelea kupungua kwa kasi kidogo kwani mwaka 2010 vilikuwa vifo 26 kwa kila vizazi hai 1,000 na mwaka 2015/16 vilipungua hadi kufikia vifo 25 kwa kila vizazi hai 1,000 .
Waziri Ummy alisema kuwa  yapo maendeleo yanayotia moyo kwa upande wa kupungua kwa kiwango cha vifo vya watoto walio na umri chini ya miaka mitano kutoka vifo 112 kwa kila vizazi hai 1,000 hadi kufikia vifo 67 kwa kila vizazi hai 1,000 mwaka 2015/16.
“Tumeweka baadhi ya mikakati ikiwemo kujengea uwezo vituo vya afya ili viweze kutoa hudumaza dharura  za upasuaji wa kutoa mtoto, kuhamasisha wanawake kujifungulia katika vituo vya kutolea huduma ya afya na  kuhakikisha upatikanaji wa huduma bora wakati wa kujifungua” alisema Waziri Ummy.
Mkutano huo wenye lengo la kujadili mafanikio na mikakati ya utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Kuboresha Afya ya Uzazi, Vijana na Watoto (One Plan II) umebeba kauli mbiu isemayo “Kutoa Taarifa na kufanya Mapitio ya Vifo vitokanavyo na Uzazi na Vifo vya Watoto wachanga; ni jukumu letu sote, Tuwajibike”.

MAONYESHO YA WASANII WA TANZANIA YAANZA NAIROBI

$
0
0
Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Bi. Talha Mohamed Waziri (kulia) akimkaribisha Balozi wa Msumbiji kwenye maonesho hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa maonesho wa Village Market Nairobi nchini Kenya.
Ofisa wa Ubalozi wa Venezuela Nairobi, Jose Gregorio Ayila Torres (katikati) akibadilishana mawazo na Kaimu Balozi wa Tanzania (kulia). Kushoto ni mmoja wa wasanii wa Tanzania, Raza Mohamed.
Raia wa Uswisi waliofika kwenye maonesho wakijadiliana jambo wakati wa maonesho hayo yaliyoshirikisha wasanii 14 kutoka Tanzania wa uchoraji yaliyoanza toka jana katika ukumbi wa maonesho wa Village Market Nairobi.
Wapenda sanaa wa Kenya wakikagua kazi za wasanii wa Tanzania kwenye ukumbi wa maonesho wa Village Market Nairobi.
Wadau wa sanaa wakifurahia maonesho yaliyowakutanisha Wasanii wa sanaa ya uchoraji 14 kutoka Tanzania huku yakihudhuliwa na wadau mbalimbali kutoka nchini Kenya

KAMATI YA BUNGE YA PIC WAKAGUA UJENZI WA JENGO LA TATU LA ABIRIA KIWANJA CHA NDEGE KIMATAIFA CHA JULIUS NYERERE (JNIA)

$
0
0
Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC), wakipata taarifa mbalimbali za ujenzi wa jengo la tatu la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA).BAHA 1
Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC), wakiendelea kuchukua maelezo mbalimbali ya ujenzi wa jengo la tatu la abiria la Kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere kutoka kwa Mkurugenzi wa Mradi huo, Mhandisi Mohammed Millanga (hayupo pichani).
BAHA 2
Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC), Mhe. Sophia Simba (mwenye sketi ndefu), akiwa na wajumbe wenzake wakikagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la tatu la abiria la Kiwanja cha ndege cha kimataifa cha Julius Nyerere.
BAHA 3
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC), Mhe. Albert Obama (mwenye shati la maua mbele), akiongoza wajumbe wa kamati hiyo kukagua ujenzi wa jengo la tatu la abiria la Kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere.
BAHA 4
 Mhe. Joseph Haule ‘Prof. Jay’, (kulia) akiongozana na Mkurugenzi wa mradi wa jengo la tatu la abiria la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere, Mhandisi Mohammed Millanga, walipotembelea jengo hilo hivi karibuni.
BAHA 5
Mkurugenzi wa mradi wa jengo la tatu la abiria la Kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere Mhandisi Mohammed Millanga (aliyenyoosha mkono), akitoa maelezo ya ujenzi kwa Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) walipotembelea hivi karibuni.
BAHA 6
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC), Mhe. Albert Obama (kulia) akiwa na wajumbe wa kamati hiyo walipotembelea maendeleo ya ujenzi wa jengo la tatu la abiria la Kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere.
BAHA 7
Mhandisi Mohammed Millanga (aliyenyoosha mkono), akiwaeleza wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC), maendeleo ya ujenzi wa jengo la tatu la abiria la Kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere, ambapo likikamilika litakuwa na uwezo wa kuhudumia abiria milioni sita kwa mwaka.
BAHA 8
Wajumbe wa kamati ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC), wakiondoka katika jengo la tatu la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere, baada ya kutembelea maendeleo ya ujenzi huo. Jengo hilo linatarajiwa kukamilika Disemba 2017.

VIJUSO VYA MAGAZETI YA LEO IJUMAA JANUARI 27

Waziri mkuu Mhe Majaliwa asema wanaojichomeka eneo la mgodi ili wapate Fidia hawatolipwa

$
0
0



Waziri mkuu wa tanzania Mhe. Kassm Majaliwa (Katikati) akizungumza na baadhi ya viongozi mkoani Njombe katika eneo la Liganga nyuma yake ni Mawe yanayo daiwa kuwa na Chuma Cha liganga
Waziri Mkuu Wa Tanzania Kassm Majaliwa Akizungumza na wakazi wa Ludewa Mkoani Njombe ambako anatoa onyo wa wanao jifanya wananchi na kuvamia migodi la Liganga

Ngomba ya Kinyakyusa ikimpokea waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa katika viwanya vya shule ya mpira Ludewa Mjini ambako amezingunza na wananchi


Na Mwandishi wetu

SERIKALI imesema kuwa itahakikisha kuwa wananchi wanao zunguka mradi wa Machimbo ya Liganga machimbo ya chuma ambao unatarajia kuanza hivi karibuni ambapo kunatarajiwa wananchi hao kulipwa na kuanza Machimbo katika eneo hilo ambapo onyo kwa wale ambao wameanza kuanza kujichomeka na kupata fidia.

Waziri Mkuu ametembelea eneo la machimbo ya Liganga wilayani Ludewa ambapo mbunge wa jimbo la Ludewa anaomba kwa waziri wananchi wake kulipwa fidia na kuwekwa kwa lami barabara ya kutoka Mkiu kuingia mpaka katika mladi wa Liganga.

Waziri akielekea wilayani ludewa anakutana na wananchi wanao msimamisha katika kijiji cha Lusitu ambapo wananchi wanamfikishia kilio chao kwa kutumia nyimbo.

Kabla ya kuingia ludewa mjini waziri anaingia Liganga ambako chuma litachimbwa kwenye mlima wa mawe ya chuma lenye ukubwa wa kilomita kumi ambapo akiwa hapa anazungumza na viongozi wa mkoa wa Njombe.

Baada ya kumaliza kutembelea mradi huu waziri mkuu anakutanan ana wananchi ambapo suala ya fidia mbunge analisema mele ya mkutano wa hadhana huku barabara nayo ikiombwa kuwa ya lami kutoka Mkiu hadi Liganga.

Na haya ndio majibu ya waziri mkuu huhusu umeme, fidia na huduma zinginde za za kijamii.Kuhusu kukamilika kwa kulipa fidia na kuanza kwa mradio huo waziri anaongeza.

Baada ya kutoka eneo la mgodiwaziri mkuu anaelekea mjini Ludewa kwaajili ya Mkutano wa Hadhara na kuzungumza na wakazi wa mjini Ludewa ambapo suala la maji na barabara linaibuka tena.

DIWANI SAIDI FELLA MGENI RASMI UZINDUZI WA KUMPENI INAYOPINGA UKATILI WA WANAWAKE NA WATOTO

$
0
0
Mgeni rasmi, Diwani ya Kata ya Kilungule Saidi Fella (kushoto) akizungumza jambo wakati wa ufunguzi wa hafla ya ufunguzi wa Kampeni ya Tunaweza inayopinga ukatili wa wanawake na watoto, wakwanza kulia ni  Afisa Mtendaji wa Kata ya Sandali, Engerasia Lyimo na  Diwani wa Kata ya Sandali,  Abel Tarimo.
 Afisa Maendeleo Kata ya Sandali, Anuciatha Kayombo akizungumza jambo katika hafla ya  ufunguzi wa Kampeni ya Tunaweza inayopinga ukatili wa wanawake na watoto uliofanyika Kata ya Sandali Dar es Salaam jana kabla ya ufunguzi huo.
 Afisa Mtendaji wa Kata ya Sandali, Engerasia Lyimo akisalimia wananchi na kutambulisha viongozi meza kuu
 Diwani wa Kata ya Sandali, Abel Tarimo (wa pili kulia) akimkaribisha mgeni Rasmi ambaye ni Diwani wa Kata ya Kulungule na Mkurugezi wa  Yamoto Bend, Said Fella (wa kwanza kulia) wakati akiwasili katika hafla ya  ufunguzi wa Kampeni yaTunaweza inayopinga ukatili wa wanawake na watoto uliofanyika Kata ya Sandali Dar es Salaam jana kabla ya ufunguzi huo.
 Mkurugenzi wa Kikundi cha ngoma ya Hisia Theater Group, Hamisi Kussa (kushoto) akicheza na nyoka wakati wa  hafla ya  ufunguzi wa Kampeni Tunaweza inayopinga ukatili wa wanawake na watoto uliofanyika Kata ya Sandali Dar es Salaam  kabla ya ufunguzi huo. 
 Mkurugenzi wa Kikundi cha ngoma cha Hisia Theater Group, Hamisi Kussa akicheza na nyoka wakati wa  hafla ya  ufunguzi wa Kampeni Tunaweza inayopinga ukatili wa wanawake na watoto uliofanyika Kata ya Sandali Dar es Salaam  kabla ya ufunguzi huo.
Nyoka
 Diwani wa Kata ya Sandali,  Abel Tarimo (wa pili kushoto) akizungumza jambo wakati wa  hafla ya  ufunguzi wa Kampeni ya Tunaweza inayopinga ukatili wa wanawake na watoto uliofanyika Kata ya Sandali Dar es Salaam  kabla ya ufunguzi huo  na kupata nafasi ya kumkaribisha mgeni rasmi, kuanzia kulia ni  Afisa Maendeleo Kata ya Sandali, Anuciatha Kayombo,  Afisa Mtendaji wa Kata ya Sandali, Engerasia Lyimo na kushoto ni Diwani ya Kata ya Kilungule, Said Fella
Diwani Fella katika picha ya pamoja na kikundi cha ngoma cha Hisia Theater Group
 Mkurugenzi wa Kikundi cha ngoma cha Hisia Theater Group, Hamisi Kussa akisalimiana na Diwani Kata ya Sandali Abel Tarimo
 Mkurugenzi wa Kikundi cha ngoma cha Hisia Theater Group, Hamisi Kussa (kulia) akisalimiana na Mgeni rasmi ambaye ni Diwani wa Kata ya Kilungule, Saidi Fella
Kikundi cha wacheza ngoma cha Hisia wakitowa burudani wakati wa hafla ya  ufunguzi wa Kampeni ya Tunaweza inayopinga ukatili wa wanawake na watoto uliofanyika Kata ya Sandali Dar es Salaam
Msanii wa Yamoyo Band akitowa burudani katika hafla hiyo

Wapiga ngoma wakitumbuiza wakati wa hafla hiyo
Msanii wa Kikundi cha ngoma cha Hisia, Theo Leonald  awa kivutio katika hafla ya ufunguzi wa Kampeni ya Tunaweza inayopinga ukatili wa wanawake na watoto
Mcheza Sarakasi wa Kikundi cha Hisia, Omary Said akitowa burudani ya mchezo wa Yoga katika hafla ya ufunguzi wa Kampeni ya Tunaweza inayopinga ukatili wa wanawake na watoto
Mcheza Sarakasi wa Kikundi cha Hisia, Omary Said akitowa burudani ya mchezo wa Yoga katika hafla ya ufunguzi wa Kampeni ya Tunaweza inayopinga ukatili wa wanawake na watoto
Wananchi wakifuatilia kwa umakini
Msanii wa Kikundi cha ngoma cha Hisia, Theo Leonald  akionyesha umahiri wake katika hafla ya ufunguzi wa Kampeni ya Tunaweza inayopinga ukatili wa wanawake na watoto


Afisa Msajili Cecilia Nyandindi (kushoto) akiendelea na kusajili wananchi wanaopinga Ukatili wa wanawake na watoto
Baadhi ya wasanii wa Sarakasi wa Kikundi cha Hisia  wakizunguuka mfano wa tairi wakati wa ufunguzi wa hafla ya Kampeni ya Tunaweza inayopinga ukatili wa wanawake na watoto,




(PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA)

MWAKYEMBE KUWASILISHA MUSWADA WA KIHISTORIA BUNGENI

$
0
0
Dodoma.

Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria, Dk. Harrison Mwakyembe atawasilisha Bungeni wiki ijayo muswada wa kihistoria wa msaada wa kisheria kwa wananchi wasio na uwezo wa kumudu gharama za mawakili katika kutetea na kupigania haki zao nje na ndani ya mahakama.

Jumatano wiki hii Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria ilimaliza zoezi lililochukua wiki nzima la kukutana na wadau mbalimbali wa sheria kubadilishana nao mawazo kuhusu muswada huo na baadaye kumwita Dk. Mwakyembe kujibu baadhi ya changamoto zilizojitokeza.

Katika kuhitimisha zoezi hilo, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mohamed Mchengerwa, alimpongeza waziri huyo kwa kuzingatia kwa karibu maoni ya wadau na Kamati, hatua ambayo itawezesha muswada huo kupita bila upinzani mkubwa.

Sheria ya Msaada wa Kisheria itawezesha kwa mara ya kwanza katika historia ya Tanzania wananchi wasio na uwezo wa kuhudumiwa na mawakili kwenye masuala ya kisheria kupata msaada huo kutoka kwenye vikundi mbalimbali vya msaada wa kisheria vitakavyokuwa na wasaidizi wa kisheria nchi nzima.

Maelfu ya vijana waliomaliza sekondari na vyuo mbalimbali watapatiwa mafunzo maalum ya kisheria na kutambuliwa rasmi kuwa wasaidizi wa kisheria watakaosambazwa mijini na vijijini kutoa huduma hiyo.

Mitaala ya mafunzo hayo iliishaandaliwa na Chama cha Wanasheria cha Tanganyika (TLS) na hadi sasa zaidi ya vijana 4,700 wameshapitia mafunzo hayo.

Akihojiwa mjini Dodoma jana, Dk. Mwakyembe alisema sheria hiyo itakuwa mkombozi kwa wanawake wengi nchini wanaonyanyaswa na taratibu za kimila zilizopitwa na wakati kwenye masuala ya ndoa, talaka, mirathi, umiliki wa ardhi, uasilia wa watoto na kadhalika.

“Itakuwa mkombozi kwa wanyonge wote wakiwemo watoto yatima, wazee, wajane, walemavu na kadhalika, wanaodhulumiwa kwa kutokujua sheria na haki zao”.

WAZIRI MUHONGO NA UJUMBE WAKE KUTEMBELEA BOMBA LA MAFUTA LA TAZAMA

$
0
0
 Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo na Ujumbe wake wamewasili nchini Zambia kwa ajili ya kufanya ziara ya kutembelea njia nzima ya Bomba la Kusafirisha Mafuta Ghafi  la TAZAMA ili kukagua miundombinu yake pamoja na kuzungumza na wafanyakazi wa vituo vinavyotumika kusukuma mafuta hayo.

Ziara hiyo ya kutembelea Mkuza wa Bomba inaanza rasmi leo Tarehe 27 Januari huko Ndola nchini Zambia na kumalizika Tarehe 31 Januari, 2017 Jijini Dar es Salaam..

Ziara hiyo inafuatia makubaliano ya Marais wa nchi husika, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na Mhe. Edgar Lungu ya Tarehe 28 Novemba, 2016 kuhusu kuboresha Bomba hilo la TAZAMA kwa manufaa ya nchi zote mbili.

Imeelezwa kuwa Ziara hiyo itafanyika kwa kufuata njia ya Mkuza kwa kupitia vituo vyote vinavyosukuma mafuta na baadaye kikao cha pamoja cha viongozi hao kitakachofanyika jijini Dar es Salaam. 

Ziara hii imechagizwa pia na  ziara ya Rais Lungu  kwenye kituo cha TAZAMA Jijini Dar es Salaam ambapo ilielezwa kuwa ufanisi wa Bomba hilo umeshuka ikilinganishwa na hapo hapo awali kwani lilikuwa na uwezo wa kusafirisha tani milioni 1.1 za mafuta kwa mwaka lakini kwa sasa linasafirisha tani 600,000 tu.  

Hivyo ili kuboresha miundombinu ya TAZAMA, nchi hizo zimekubaliana kushughulikia kwa pamoja chanzo cha kuzorota kwa utendaji kazi wa TAZAMA ili Bomba hilo liweze kuendeshwa kwa faida kwa kunufaisha pande zote mbili.

Ziara  hiyo pia imelenga kufanya tathmini kwa kukagua Mkuza wa Bomba na maeneo yanayopendekezwa kujengwa bomba la kusafirisha Mafuta Safi (Finished Product) na Gesi Asilia kutoka Tanzania hadi Zambia kupitia njia ya Mkuza huo (wayleave) wa Bomba la TAZAMA.

Imeelezwa kuwa ziara hiyo itafanywa kwa ushirikiano wa Mawaziri wa Nishati kutoka Tanzania na Zambia wakiambatana na Makatibu wakuu, pamoja na viongozi waandamizi kutoka nchi zote mbili sambamba na uongozi wa TAZAMA.

Bomba la kusafirisha mafuta ghafi la TAZAMA linaloanzia nchini Tanzania hadi mji wa Ndola nchini Zambia lina urefu wa kilomita 1,710 na kipenyo cha inchi 8 hadi 12 na lilianza kazi Mwaka 1968.
 Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kushoto) akizungumza jambo alipowasili katika Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kenneth Kaunda Jijini Lusaka, Zambia. Kulia ni Balozi wa Tanzania Nchini Zambia, Balozi Grace Mujuma.
 Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (wa pili kulia) na ujumbe wake kutoka Tanzania walipowasili Lusaka Nchini Zambia. Kutoka kushoto ni Balozi wa Tanzania Nchini Zambia, Balozi Grace Mujuma, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati ya Zambia, Brigedia Jenerali Emelda Chola na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini kutoka Tanzania, Profesa Justin Ntalikwa.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (katikati) akizungumza jambo alipowasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kenneth Kaunda Jijini Lusaka, Zambia.  Kulia ni Balozi wa Tanzania Nchini Zambia, Balozi Grace Mujuma na kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa Justin Ntalikwa.

 Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kushoto) akiongozana na  Balozi wa Tanzania Nchini Zambia, Balozi Grace Mujuma (kulia) alipowasili Jijini Lusaka, Zambia kwa ajili ya ziara ya kutembelea Bomba la TAZAMA.

RC Rukwa awacharukia Wakurugenzi kuhusu TASAF,aagiza waliokula fedha wakamatwe

$
0
0

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen amewaagiza wakurugenzi, waratibu wa Tasaf, watendaji wa kata, watendaji wa vijiji na wenyeviti wa vijiji Mkoani humo kuhakikisha kwamba haki inapatikana katika kufanya mchujo kwa zile kaya ambazo hazistahili kuingizwa katika mpango wa kuzinusuru kaya masikini (TASAF)

Ametoa agizo hilo baada ya kufanya ziara yake ya siku ya nne katika wilaya za kalambo na Nkasi Mkoani humo kwa kuzitembelea kaya za walionufaika na mpango wa TASAF ambao bado wanaendelea kunufaika na wale ambao waliondolewa katika mpango huo baada ya kukosa vigezo na hatimae kutakiwa kurudisha pesa hizo.

“nimezunguka nimebaini kuwa zoezi hili limekuwa likifanyika hovyo hovyo, hakuna umakini, hakuna usimamizi, hakuna ufuatiliaji, matokeo yake kwenye mradi wameingizwa watu wenye sifa na wasio na sifa, Wakurugenzi na waratibu wasimamie zoezi hili, wasiwaachie wenyeviti na watendaji wa vijiji peke yao katika hili,”

Zelote Stephen alifanya ziara hiyo ili kujiridhisha kuwa kaya ambazo hazistahili kuingizwa katika mpango wa TASAF wanatendewa haki katika kuondolewa kwenye mpango huo lakini pia kujua sababu zilizopelekea kaya hizo kuingizwa kwenye mpango bila ya kuwa na vigezo na kuachwa kaya zenye vigezo.

“Wale wote ambao hawana vigezo na kweli ionekane kwamba hawana vigezo vya kuwepo basi watolewe kwasababau sehemu zingine utakuta kwenye mpango huo wameingizwa wastaafu, mke wa mwalimu, mjumbe wa smc yumo humo humo, hii haifai,” Zelote alifafanua.

Katika ziara yake hiyo iliyolenga kufuatilia mchujo wa kaya hizo, Zelote Stephen alibaini kuwa wakurugenzi pamoja na waratibu wa TASAF wilaya wanakosa umakini katika kuzifanya shughuli zao na hatimae kubaki maofisini kusubiri ripoti zitokazo vijijini bila ya kufuatilia kwa kina kwa kufika katika maeneo husika ili kujua hali halisi.

“Mimi nina taarifa kwamba fedha za ufuatiliaji wa TASAF zikifika tu katika Ofisi ya Mkurugenzi, kama zimefika asubuhi basi mchana tu hakuna senti tano, zote zimeshanyanganyiwa na hatimae makusudio ya fedha zile hayatimii na ufuatiliaji haufanywi,” Alisisitiza.

Nae mratibu wa TASAF Mkoa wa Rukwa, James Kapenulo aliongeza kuwa kaya zote ambazo zilinufaika na TASAF kwa kuwa na mashamba na nyumba nzuri ambazo kabla ya TASAF hawakuwa nazo, familia hizo ndio ziwe za mfano na ziendelee kuwezeshwa ili tathmini itakapokuja kufanywa ioneshe hali halisi ya mafanikio ya mpango huo.

“Hatuwezi tukaendelea kuwaweka wale ambao wakipewa pesa za TASAF wanaishia kwenye vilabu vya pombe na kumuacha yule ambae akipewa pesa hizi ananunua kuku au mbuzi au bati na kuwapeleka watoto shuleni, hayo sio madhumuni ya mpango huu, huyu aliyefanikiwa baada ya TASAF ndiye ametoka weye umaskini.

Naye mnufaika wa TASAF aliyetolewa kwenye mpango huo Mathias Mwanakatwe alimshukuru Mkuu wa wa Mkoa kwa kuweza kuliona hilo na kulishughulikia kabla hali haijawa mbaya zaidi kwa wale wananchi wenye wivu na chuki kwa wale waliofanikiwa kutokana na kuwepo kwa mpango huo wa TASAF.

Kaya 550 mbazo hazistahili kuwepo katika mpango huo kwa Mkoa wa Rukwa.

DC KAKONKO KANALI NDAGALA ABAINI MADUDU MPANGO WA KUSAIDIA KAYA MASIKINI (TASAF),WAMO WAHAMIAJI HARAMU

$
0
0

Na Rhoda Ezekiel Kigoma,

MKUU wa Wilaya ya Kakonko Mkoa wa Kigoma kanal Hosea Ndagala ameitaka mamlaka ya uhamiaji kuharakisha kufanyia Uchunguzi kwa kaya 180 ambazo zilibainika kuwa na baadhi ya wakuuu wa kaya wanadhaniwa kuwa ni wahamiaji haramu walioingizwa kwenye mpango wa kusaidia kaya maskini TASAF kinyume cha sheria.

Pia kanali Ndagala aliwataka Wanufaika na walengwa wa TASAF Kutumia fedha wanazo zipata kuanzisha miradi midogomidogo itakayo wasaidia kutoka katika wimbi kubwa la umasikini, na kuacha kutumia fedha hizo kinyume na utaratibu uliokusudiwa kwa kufanyia mambo ya anasa.

Kauli hiyo alitolewa jana wakati wa ziara yake vijijini ya kutembelea wanufaika wa Mradi huo katika Vijiji vya Nyabibuye na vijiji vya kata ya Nyaronga, ambapo alisema lengo la serikali kuanzisha Mfuko huo ni kusaidia Watanzania wanaoishi katika Mazingira magumu waweze kupata fedha za kuwapeleka Shule watoto, kupata chakula milo mitatu kwa siku na kuboresha afya zao na kuanzisha miradi itakayo wasaidia kujikwamua na umasikini.

Alisema katika uhakiki uliofanyika wa kuhakiki watu wasio stahili kuwemo katika mradi huo, iligundulika kwa Wilaya ya Kakonko kuna baadhi ya kaya 180 zinazo nufaika na mradi huo ambapo baadhi ya wakuu wa kaya hizo mmoja wao ni Raia kutoka Nchi ya Burundi wanao endelea kunufaika na mradi kinyume na utaratibu uliowekwa kwa Wanufaika wa Mradi huo.

Ndagala alisema kuwahudumia wahamiaji haramu kwenye mpango wa TASAF ni kuhujumu uchumi wa serikali , endapo itagundulika Watu hao tunao wadhania sio raia ikithibitishwa na Maafisa wa Uhamiaji Watatakiwa kurudisha fedha zote walizo kwisha kuzichukua na kwa Wale wajumbe wa Kijiji walio shiriki kupitisha majina yao yaingizwe kwenye mradi watatakiwa kuchukuliwa hatua .

"Leo nimepita mimi mwenyewe kujionea Wanufaika wa Mradi wa TASAF na nimebaini mambo machache moja wapo ikiwa wahamiaji haramu kuingizwa kwenye mpango, Wanufaika kutumia fedha kama inavyo takiwa wengi wao wanarumia kunywea pombe na mambo mengine nimekuja kuwahamasisha watumie fedha hizo kwa kuwajenga kiuchumi na kwa wale walio bainika kwenye uhakiki majina tumeyafikisha kwa idara ya uhamiaji waweze kufanya upembuzi yakinifu ilikuweza kubaini uraia wao",alisema Kanali Ndagala.

Sauda Lumala ni Mmoja kati ya Wanufaika alisema kwa upande wake alipo pokea fedha za TASAF alinunua Mbuzi na bata ambapo Mpaka sasa anajumla ya Mbuzi watatu na bata kumi alizo zalisha kupitia miradi ya kusaidia Kaya masikini.

Alisema changamoto wanayo kumbana nayo katika suala zima la kuanzisha miradi baadhi ya Wanawake wengi wakipokea fedha hizo waume zao wanawanyang'anya na kuzifanyia mambo yao binafsi hali inayopelekea kushindwa kutumia fedha hizo kwa shughuli zilizo kusudiwa.

Nae Mratibu wa TASAF Wilaya ya Kakonko, Maria Tarimo alisema mpaka sasa kuna jumla ya wanufaika 7775 katika wilaya ya Kakonko zinanufaika na mpango huo ambao umeleta manufaa makubwa na wengi wao wameanza kufikia malengo yaliyopangwa na wameanzisha miradi endelevu itakayo wasaidia kupambana na umasikini.

Alisema katika uhakiki wa Kuwaondoa watu wasio stahili katika Mpango huo waliobainika ni watu 180 wanaozaniwa kuwa sio Raia ambao wataondolewa kwenye mpango huo na watatakiwa kurudisha fedha walizo kwisha kuzichukua kinyume na utaratibu.
MKUU wa Wilaya ya Kakonko Mkoa wa Kigoma kanal Hosea Ndagala  akisalimiana na mmoja wa wanakijiji cha Nyabibuye,wakati Ndagala alipofanya ziara yake kutembelea wanufaika wa Mradi wa TASAF,katika Vijiji vya Nyabibuye na vijiji vya kata ya Nyaronga
 MKUU wa Wilaya ya Kakonko Mkoa wa Kigoma kanal Hosea Ndagala  akimsikiliza mmoja wa wanakijiji cha Nyabibuye,aliyenufaika na mradi wa Kaya Masikini wa TASAF,wakati  alipofanya ziara yake kutembelea wanufaika wa Mradi wa TASAF,katika Vijiji vya Nyabibuye na vijiji vya kata ya Nyaronga.
 Baadhi ya Wanakijiji cha Nyaronga wakimsikiliza MKUU wa Wilaya ya Kakonko Mkoa wa Kigoma kanal Hosea Ndagala  (hayupo pichani) wakati alipofanya ziara yake kutembelea wanufaika wa Mradi wa TASAF,katika Vijiji vya Nyabibuye na vijiji vya kata ya Nyaronga


SERIKALI YAWAKALIA KOONI WATUMISHI WA HALMASHAURI YA LUDEWA

$
0
0
Wananchi wa kijiji cha Lusitu wilayani Ludewa wakilizuia gari la Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakimtaka asimame na kuwasalimia alipokuwa akienda mjini Ludewa kutoka mgodi wa chuma wa Liganga Januari 26, 2017. Mheshimiwa Majaliwa alisimama na kuwahutubia.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwasalimia wananchi wa kijiji cha Lusitu wilayani Ludewa walioziba barabara wakitaka asimame na kuwasalimia alipokuwa akitoka kwenye mgodi wa chuma wa Liganga kwenda mjini Ludewa Januari 26, 2017. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na viongozi wa dini baada ya kuhutubia mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa Halmashauri, mjini Ludewa Januari 26, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

*Ni wale waliohusika na upotevu wa sh. milioni 700

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Njombe Bw. Christopher Ole Sendeka kuwachukulia hatua watumishi  Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa waliohusika na upotevu wa fedha za maendeleo.

Amesema zaidi ya sh. milioni 700 zilizopelekwa katika halmashauri kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo zikiwemo sh. milioni 300 za ujenzi wa Ofisi ya Halmashauri hiyo.
Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo jana jioni (Alhamisi, Januari 26, 2017) wakati akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Halmashauri alipokuwa katika ziara yake katika  Wilaya ya Ludewa mkoani Njombe.

“Mkuu wa Mkoa watu wote waliohusika na upotevu huu watafutwe popote walipo na kuchukuliwa hatua na kisha nipewe taarifa ya hatua ulizochukua. Hatuwezi kuwavumilia watu hao ambao wanachora ramani kwa sh milioni 200  na sh. milioni 100 zingine hazijulkikani zilipo,“ alisema.

Pia Waziri Mkuu alimuagiza Mkuu huyo wa Mkoa  kufuatilia kiasi kingine cha sh milioni 400 zilizopelekwa wilayani hapo kwa ajili ya maendeleo ambazo nazo hazijulikani zilipo. “Tafuta waliohusika popote walipo hata kama ni nje ya Njombe waje kutueleza ziliko fedha zetu,”

Mbali na kutoa agizo hilo kwa Mkuu wa Mkoa, pia Waziri Mkuu ameuagiza uongozi wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa nchini (TAKUKURU) kuhakikisha inashirikiana nayo inafanya uchunguzi ili kubaini watu waliohusika na upotevu huo.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu alisema Serikali haitowavumilia watumishi wote wanaojihusisha na vitendo vya ubadhilifu wa fedha za umma, hivyo amewataka watumishi wafanye kazi kwa kuzingatia sheria na maadili.

Waziri Mkuu aliwataka watumishi wa umma nchini kuacha tabia ya kudokoa fedha za maendeleo zinazopelekwa katika Halmashauri zao kwa sababu Serikali iko macho na itawashughulikia wote watakaobainika kujihusisha na vitendo hivyo.

Aidha, Waziri Mkuu alitoa wito kwa Wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini kusimamia vizuri fedha za maendeleo zinazopelekwa kwenye maeneo yao na kuhakikisha zinatumika kama ilivyokusudiwa.

Awali akiwa njiani kuelekea Ludewa Mjini akitokea katika kata ya Mundindi Waziri Mkuu alisimamishwa na wananchi wa kijiji cha Mlangali ambao waliiomba Serikali iwasaidie kuzipatia ufumbuzi changamoto mbalimbali zinazowakabili ikiwemo ya maji.

Mwenyekiti wa kijiji hicho Bw. Michael Lameck alisema alimueleza Waziri Mkuu kwamba awali walikuwa wanapata maji ila kwa sasa hayatoki kutokana na uchakavu wa miundombinu hali iliyowafanya kuchangishana na kupata sh. milioni 95 kati ya 200 zinazohitajika.

Kufuatia hali hiyo Waziri  Mkuu alimuagiza Mhandisi wa Maji wa Wilaya hiyo, Bw. Nasib Mlenge kwenda kijijini hapo leo  Januari 27 kukutana na Bw. Lameck ili kushirikiana naye na kuangalia alipofikia na kuendeleza uboreshaji wa miundombinu hiyo ili wananchi hao wapate maji.

“Mwenyekiti amechangisha sh. milioni 95 na kununua baadhi ya vifaa nyinyi mnashindwa nini. Lazima muwe makini na matatizo ya wananchi na Serikali haitaki masuala ya urasimu. Watu wana shida ya maji na mnajua tatizo mmekaa tu,” alisema.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
IJUMAA, JANUARI 27, 2017.

WAZIRI LUKUVI ATOA HATI 810 ZA ARDHI KWA WANAKIJIJI MKOANI IRINGA

$
0
0
Wakazi wa Kijiji cha Kinywang’anga Mkoa wa Iringa wakiwa na hati zao za umiliki wa ardhi mara baada ya kukabidhiwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa William Lukuvi (aliyevaa miwani) akifuatiwa na Mkurugenzi wa Shirika la Misaada la Watu wa Marekani (USAID) Ndugu David Thompson na Mkuu wa Mkoa wa Iringa Richard Kasesela.
Baadhi ya hati miliki za ardhi zikiwa zinaandaliwa ili kugawiwa kwa wananchi wa Kijiji cha Kinywang’anga Mkoani Iringa.
Ndugu Yohanes Keng’ena na Mkewe Elizabeth Makang’olo wakipokea hati miliki ya ardhi kutoka kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa William Lukuvi.
Bibi Catherine Abdallah akipokea hati miliki ya ardhi kutoka kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa William Lukuvi.
Ndugu Petro Wilson na Mkewe Leila Mlawa wakipokea hati miliki ya ardhi kutoka kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa William Lukuvi.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa William Lukuvi akiongoza ukataji utepe katika ufunguzi wa masijala ya ardhi ya kijiji cha Kinywang’anga Mkoa wa Iringa.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa William Lukuvi akiongoa na wakazi wa Kijiji cha Kinywang’anga Mkoani Iringa.
Mkurugenzi wa Shirika la Misaada la Watu wa Marekani (USAID) Ndugu David Thompson akiongoa na wakazi wa Kijiji cha Kinywang’anga Mkoani Iringa.
Moja ya shamba la mkazi wa Kijiji cha Kinywang’anga Mkoani Iringa.



Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa William Lukuvi amewakabidhi hati miliki 810 za ardhi kwa wananchi wa Kijiji cha Kinywang’anga kilichipo Mkoani Iringa.

Wananchi hawa wamekabidhiwa hati hizo za umiliki wa ardhi baada ya kupimiwa maeneo yao ya viwanja na mashamba wanayoyamiliki na kuandaliwa hati miliki ambazo walikabidhiwa na Waziri wa Ardhi Mheshimiwa William Lukuvi kijijini hapo.

Katika tukio lingine Mheshimiwa William Lukuvi amezindua masijala ya ardhi ya kijiji cha Kinywang’anga Mkoa wa Iringa ili kuboresha huduma ya utoaji na uhifadhi wa hati miliki za ardhi.

Akizungumza na wakazi wa Kijiji hicho mara baada ya kuwakabidhi hati miliki zao za ardhi na kuzindua baraza hilo Waziri Lukuvi aliwasihi wananchi hao kuzihifadhi na kuzitunza hati zao hizo ili kuepukana na migogoro ya ardhi inayowakabili wananchi wengi wasio na hati miliki nchini.

Nae Mkurugenzi wa Shirika la Misaada la Watu wa Marekani (USAID) walioshirikiana na Serikali kuwezesha uandaaji wa hati miliki hizo Ndugu David Thompson amemshukuru Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa William Lukuvi kwa kuja na kuwakabidhi Wananchi hati hizo na kuwaombaa Wananchi kuzitumia kwa maendeleo yao.

Wananchi wa Kijiji cha Kinywang’anga wamemshukuru Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa William Lukuvi pamoja na shirika la USAID linaloendesha mradi wa ‘Tanzania Land Tenure Assistance’ kwa kuwaaezesha kupata hati hizo maana ilikuwa kero kubwa katika kata yao.

Aidha, Waziri wa Ardhi ametoa hati miliki hizo ili kutekeleza Programu ya Kitaifa ya kupima na kumilikisha ardhi na kuzuia migogoro ya ardhi yenye lengo la kutekelezwa nchi nzima. Utekelezaji huu utahusisha kuhakiki mipaka ya Mitaa na Vijiji pamoja na maeneo mengine yote nchini na kupima kila kipande cha ardhi kwa lengo la kumilikisha ardhi hiyo kwa wananchi, taasisi na Kampuni.

Sambamba na hilo, Matangazo ya Serikali yanayotambulisha mipaka ya mikoa, Wilaya, Hifadhi za Taifa na vijiji yatafanyiwa marekebisho baada ya mipaka yote nchini kuhakikiwa na kukamilika.

Aidha mpango huu unalenga kuwaunganisha wadau wa sekta ya ardhi katika kupanga, kupima, na kumilikisha ardhi nchini na kuweka kumbukumbu za vipande vya ardhi ili kuongeza thamani ya ardhi na kuondoa migogoro ya ardhi kwa ajili ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

Serikali ya awamu ya tano imeweka adhma ya kumaliza migogoro ya ardhi iliyopo sasa na kuzuia kasi ongezeko la migogoro ya ardhi ndani ya miaka mitano kwa kuandaa mpango kabambe wa matumizi na usimamizi wa ardhi kwa kuharakisha na kurahisisha upatikanaji wa hati za umiliki wa viwanja na mashamba.


Na Hassan Mabuye (Kitengo cha Mawasiliano Serikalini – Wizara ya Ardhi)

UNFPA YAKABIDHI MAGARI SITA NA VIFAA TIBA KWA WIZARA YA AFYA ZANZIBAR

$
0
0
Dkt. Hashina akimkabidhi Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo moja ya funguo za magari hayo kwenye sherehe zilizofanyika Wizarani kwake Mnazimmoja Mjini Zanzibar.
Kaimu Muwakilishi Mkaazi wa UNFPA Tanzania Dkt. Hashina Begum na Waziri wa Afya wa Zanzibar Mahmoud Thabit Kombo wakisaini makabidhiano ya magari manne ya kubebea wagonjwa na mawwili ya huduma yaliyotolewa na Shirika hilo katika sherehe zilizofanyika Mnazimmoja Mjini Zanzibar.
 
Gari nne za kubebea wagonjwa na mbili za huduma zilizotolewa msaada na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu Ulimwenguni (UNFPA) kwa ajili ya kutoa huduma katika Hospitali na vituo vya Afya Zanzibar zikiwa mbele ya Wizara hiyo Mnazimmoja Mjini Zanzibar.
Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo akiwa na Kaimu Muwakilishi Mkaazi wa UNFPA Dkt. Hashina Begum akilijaribu moja ya gari lilililotolewa msaada na UNFPA akwa ajili ya kuhudumia wagonjwa.
Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo na Kaimu Muwakilishi wa UNFPA Tanzania Dkt. Hashina wakinyanyua moja ya vifaa tiba vilivyotolewa na UNFPA kwa ajili ya wodi ya mama wajawazito na watoto.

Picha na Makame Mshenga/Maelezo.

SBL yawapatia Watanzania milioni mbili maji ya uhakika, salama

$
0
0
 
Moja ya mradi wa maji uliodhamiwa na kampuni ya Serengeti Breweries Limited uliozinduliwa mapema Novemba mwaka jana katika Kijiji cha Makanya wilayani Same katika programu ya hisani ya kusaidia jamii inayoendeshwa na kampuni hiyo inayolenga kuboresha maisha.


Mkurugenzi wa Mahusiano wa SBL, John Wanyancha akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu mradi wa maji ulioweza kuwafikia watanzania milioni 2 katika programu ya hisani ya kusaidia jamii inayoendeshwa na kampuni hiyo inayolenga kuboresha maisha katika mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika mapema jana katika hoteli ya Morena Mkoani Dodoma.
Waandishi wa habari wa mkoani Dodoma wakichukua matukio wakati wa mkutano uliofanyika mapema jana katika hoteli ya Morena mkoani Dodoma.
Kampuni ya Bia ya Serengeti imewapatia Watanzania zaidi ya milioni mbili kote nchini maji safi na salama bure katika kipindi cha miaka sita iliyopita kupitia programu ya hisani ya kusaidia jamii inayoendeshwa na kampuni hiyo inayolenga kuboresha maisha.

Kupitia programu yake inayofahamika kama Maji kwa Uhai, SBL imechimba visima vya kisasa 16 katika mikoa minane na kuwezesha jamii katika maeneo hayo kupata maji ya uhakika na salama.

Akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari mjini Dodoma leo, Mkurugenzi wa Mahusiano wa SBL, John Wanyancha alisema kwamba kampuni hiyo ya bia imejikita katika kupunguza uhaba wa maji katika maeneo ambayo kwa muda mrefu yamekuwa yakitaabika kutokana na uhaba wa bidhaa hiyo.

“SBL ina sera iliyojikita katika ustawi wa jamii yetu ambapo Maji ya Maisha ikiwa ni moja ya maeneo manne ya kipaumbele ambayo kampuni yetu imeyafafanua katika malengo yake ya kutoa msaada kijamii kwa jamii inamofanya shughuli zake, alisema Wanyancha akifafanua maeneo mengine ya kipaumbele kama Kutoa Stadi za Maisha, Mazingira Endelevu na Kuhamasisha Unywaji wa Kistaarabu.

Wanyancha aliongeza kwamba kwa kutoa huduma ya maji ya uhakika katika jamii, SBL imewawezesha watu kutumia muda mwingi zaidi katika uzalishaji kuliko kusafiri umbali mrefu kutafuta maji.Aliongeza, “licha ya kuboresha afya za wakazi wa maeneo hayo, upatikanaji wa maji safi na salama ndani ya jamii unahakikisha kuwa watoto hususani watoto wa kike wanaosoma shule wanapata muda mzuri wa kuhudhuria shuleni kwa uhuru zaidi bila usumbufu”.

Mkurugenzi huyo wa Mahusiano alieleza kwamba mpango wa Maji ya Maisha kwa mwaka 2017 ni kuanzisha miradi zaidi katika maeneo ya Ngare Nairobi, wilayani Siha, Chang’ombe B wilayani Temeke (Dar es Salaam) na Karatu na Likamba katika mkoa wa Arusha ambapo miradi yote itawanufaisha wakazi zaidi ya 300,000.

RC MAKALLA ATENGA MUDA WA KUSIKILIZA KERO ZA WANANCHI MKOANI MBEYA.

$
0
0
 Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mh. Amos Makalla akizungumza na wananchi pamoja na wadau mbalimbali wa maendeleo ikiwa ni utaratibu wake wa kusikiliza kero za wananchi wa mkoa wa mbeya kila Alhamis ya mwanzo na mwisho mwa mwezi na jana Alhamis ya Tarehe 26 ya mwezi Januari amekutana na baadhi ya wananchi wa watokao maeneo tofauti mkoani Mbeya na kueleza kero zao na kutatuliwa papo kwa papo na idara husika.PICHA NA MR PENGO-MMG MBEYA
Bi. Fidea Lukas Mwakanyamale akitoa kero kwa mkuu wa mkoa kuhusu  jinsi alivyo mwagiwa tindikali na muajili wake Wilayani Chunya mkoa wa Mbeya..
 Baadhi ya wananchi wa mkoa wa Mbeya wakitua kero zao mbele ya mkuu wa mkoa alipokutana na wananchi hao
  Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla akitolea majibu maswali pamoja na hoja za wananchi waliofika kuwasilisha kero zao kwa mkuu wa mkoa huyo katika ukumbi mdogo wa Mkapa jijini Mbeya.
 Baadhi ya wananchi na wadau wa mkoa wa Mbeya wakimsikiliza mkuu wa Mkoa alipokuwa akijibu hoja za wananchi kwenye ukumbi mdogo wa Mkapa jijini Mbeya .
Mkutano ukiendelea

ZIARA YA NAIBU WAZIRI MASAUNI MKOANI RUKWA ATEMBELEA IDARA ZILIZOPO CHINI YA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

$
0
0
Naibu Waziri wa Wizar ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akisindikizwa na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Zelote Stephen mara baada ya kumaliza kupokea taarifa ya mkoa na ya vyombo vya usalama wa mkoa huo wakati wa ziara ya kikazi mkoani hapo.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Zelote Stephen akitoa taarifa ya mkoa na ya vyombo vya usalama wa mkoa huo kwa Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(kulia), wakati wa ziara ya Naibu Waziri kutembelea idara zilizopo chini ya wizara yake.
 
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza wakati alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi la Magereza mkoa wa Rukwa kwa ziara ya kikazi.Kulia ni wakuu wa jeshi hilo mkoani hapo wakimsikiliza.
Afisa Uhamiaji Mkoa wa Rukwa, Kamishna Msaidizi Selemani Kameya akisoma taarifa ya utendaji kazi ya Mkoa huo kwa Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, ACP George Kyando akizungumzia Mradi wa Ujenzi wa ofisi wakati Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni alipotembelea jengo hilo kuona maendeleo ya mradi huo na kuwataka kutumia rasilimali watu ya wafungwa waliopo mkoani hapo ili kuweza kukamilisha ujenzi huo wakati wa ziara ya kikazi aliyoifanya mkoani hapo.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akipokea risala kutoka kwa askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoani Rukwa aliyoisoma kwa niaba ya wenzake ikiwa na maombi mbalimbali yaliyoelekezwa kwa wizara.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akisalimiana na aliyewahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Simiyu, Paul Mzindakaya baada ya kumaliza kupokea taarifa ya hali ya usalama mkoani Rukwa wakati Naibu Waziri alipokuwa mkoani humo kwa ziara ya kikazi.(Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)

IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI-WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

Uwanja wa Taifa Ruksa kutumiwa na Simba na Yanga

Jumia Travel committed to bolster the tourism sector

$
0
0
Jumia Travel CEO, Paul Midy.
By Jumia Travel Tanzania

2016 was a successful year to the tourism sector across the world as it recorded a number of 1.2 billion people who traveled the world. Out of these, 58 million people travelled to Africa, according to a report released by the United Nations World Tourism Organization (UNWTO).

That report was presented during the 8th edition of the FITUR, the Spanish Tourism Fair organized by INVESTOUR on January 19th, 2017 in Madrid, Spain in a joint initiative of the UNWTO and Casa Africa. It involved stakeholders and over 20 Ministers of Tourism  from different African countries.

The conference focused on two main agendas: ‘Technology and design of new touristic products’ and ‘Capacity development for youth and women in tourism.’

Speaking as part of the participating panelists, Jumia Travel CEO, Paul Midy commented that, “That huge number of people who travelled within their borders is the sign that they are increasingly embracing domestic tourism thus frequenting  local tourist attractions. Therefore, immediate measures by tourism stakeholders should be taken in promoting tourist attractions. Meanwhile, facilitating easy access to accommodation services is a key point as is price-cut in accommodation which would be a huge relief to travellers.

According to the report, there is a high possibility for domestic tourism to bolster. This is because  as part of the 1.2 billion people who travelled the world, 6 billion people toured within their borders. This indicates that immediate efforts must be taken to promote and encourage people to visit local tourist attractions.  

In an effort to make sure Tanzanians tour destinations they desire,  Jumia Travel has been offering dream deals every Wednesday which lasts until Friday every week. The offers are a relief to most travellers who love to travel but perceive a high price in some hotels as a major setback.

All the hotels which are in Travel Wednesday deals are located in tourist attractions such as conservation areas, mountains, clean and attractive beaches along the Indian Ocean, birds life, as well as delicious dishes and cultural life of indigenous.

Jumia Travel yajizatiti kujikita zaidi katika utalii

$
0
0

Afisa Mtendaji Mkuu wa Jumia Travel, Bw. Paul Midy.


Na Jumia Travel Tanzania


Mwaka wa 2016 ulikuwa wenye mafanikio makubwa kwa sekta ya utalii duniani ambapo kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Utalii Duniani (UNWTO), watu bilioni 1.2 walisafiri duniani huku waliotembelea Afrika wakiwa milioni 58.

Taarifa hiyo ilitolewa katika mkutano wa nane uliondaliwa wa INVESTOUR Januari 19, 2017 jijini Madrid nchini Hispania, kwa ushirikiano wa UNWTO na Casa Afrika ambao uliwakutanisha wadau na mawaziri zaidi ya 20 wa utalii kutoka barani Afrika.

Ajenda kuu za mkutano huo zilikuwa mbili ambazo ni; ‘Tekinolojia na uundaji wa bidhaa mpya za kitalii’ pamoja na ‘Kuendeleza uwezo kwa vijana na wanawake katika utalii.’

Akiwa na mmojawapo wa washiriki waliounda jopo la wazungumzaji katika mkutano huo, Afisa Mtendaji Mkuu wa Jumia Travel, Bw. Paul Midy alibainisha kwamba, “Idadi kubwa ya wasafiri wa ndani ni ishara nzuri kwamba watu wanavutiwa na vivutio walivyonavyo. Zinahitajika jitihada za wadau wa utalii katika kuwaelimisha na kuvitangaza vivutio hivyo huku tukiwarahisishia miundombinu kama vile malazi ambayo huwezi kuiweka kando pindi unapozungumiza usafiri na utalii. Naamini kwa gharama za malazi kupunguzwa, watu wengi watahamasika kusafiri kwani mahali zilipo hizo hoteli ndipo vivutio vilipo.”

Kwa mujibu wa ripoti hiyo kuna fursa kubwa kwa utalii wa ndani kwa sababu mbali na idadi ya watu bilioni 1.2 waliosafiri duniani, watu bilioni 6 walifanya utalii wa ndani. Hii inamaanisha kwamba zinahitajika kufanyika jitihada za makusudi katika kuhamasisha na kutangaza vivutio vya nyumbani ili kuwavutia watu wengi zaidi.

Katika kulifanikisha hilo Jumia Travel imekuwa ikitoa punguzo kubwa la bei kila ifikapo siku ya Jumatano na kudumu mpaka siku ya Ijumaa kila wiki. Ofa hii hutoa fursa na kuwarahisishia watu wanaotamani kwenda kutalii sehemu fulani lakini wakihofia bei ya malazi kuwa juu.

Hoteli zote ambazo zimo kwenye orodha ya ofa hii zinapatikana kwenye maeneo ambayo yana vivutio vya kitalii kama vile mbuga za wanyama, milima, fukwe safi na za kuvutia za bahari, ndege wa kuvutia pamoja na vyakula na utamaduni wa eneo husika.

SERIKALI WILAYANI HANDENI YAZINDUA MRADI WA KUDHIBITI VITENDO VYA UKEKETAJI (KIJANA WA LEO “STOP FGM” (ELIMISHA) KWA WATOTO NA WANAWAKE

$
0
0
Mradi umeandaliwa na AMREF shirika lisilo la kiserikali,umezinduliwa Wilayani Handeni katika ukumbi wa Kanisa la KKT na Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mhe. Godwin Gondwe. Kuzinduliwa kwa mradi huo kumekuja Kufuatiwa kuwepo kwa jamii nyingi za wafugaji na jamii nyingine za kawaida zinazodumisha Mila potofu ya ukeketaji wa watoto na wanawake bila kutambua athari wanazokumbana nazo walengwa. Tathmini iliyofanyika imeonesha Asilimia 70% ya wafugaji wanafanya ukeketaji na 30% ni jamii ya kawaida ambayo inadumisha mila hizo.

Akizungumza kwenye uzinduzi huo, Mhe. Gondwe alisema kuwa jamii hazikatazwi kudumisha mila na kufanya sherehe za kimila, lakini serikali na jamii kwa ujumla haitakuwa tayari kuona tamaduni potofu kama ya Ukeketaji inaendelea kukumbatiwa na kuathiri watoto na wanawake wa Wilaya Handeni.”

Aliongeza kuwa Vitendo vya ukeketaji vinamuathiri mtoto kisaikolojia ,kiafya, kiuchumi na Kielimu, hali inayopelekea utoro uliokithiri shuleni na watoto wengi kutomaliza shule na kuolewa katika umri mdogo , kutokana na mazingira wanayojengewa na mangariba wakiwa kwenye sherehe hizo za kiutamaduni.

Mhe. Gondwe alieleza kuwa mradi huu ambao AMREF wameuleta kwetu tuna wajibu wa kuumiliki, kuufanya wa kwetu na endelevu hata baada ya mwaka mmoja kufika ukomo . Alieleza kuwa Kila mtoto anahaki ya kuishi na kupata haki zake za msingi ikiwemo elimu kama mtoto mwingine na kwamba jamii nzima ya Handeni iungane na kutoa ushirikiano kuanzia ngazi ya vitongoji hadi Halmashauri kwa shirika la AMREF kuondokana na vitendo hivyo kutoka 14% iliyopo sasa hadi 0%.

Akielezea muundo mzima wa mradi huo, Dokta Aisha Bianaku Meneja wa Mradi alisema kuwa, Mradi huo wameamua kuuleta Handeni baada ya kufanya tahmini na kuona kwamba katika mkoa wa Tanga ikitoka wilaya ya Kilindi, Handeni ni wilaya inayofuata kwa kushiriki vitendo hivi vya ukeketaji. Alisema kuwa kata tano ndizo zitakazopewa elimu na kutoa njia mbadala kwa mangariba ambao wamechukulia kukeketa ni njia mojawapo ya wao ya kujipatia kipato.

Elimu itatolewa kuanzia shuleni kwa waalimu na wanafunzi, mitaani , kwa viongozi wa kata na vitongoji, matabibu wa vituo vya afya, morani na wazee wenye ushawishi mkubwa katika jamii. 

Alisema kuwa lengo ni kuwaelimisha madhara ya vitendo vya ukeketaji na kuondoa kabisa desturi hii ambayo inamadhara makubwa ya kiafya na kielimu kwa ujumla kwa watoto na wanawake hasa wakati wa kujifungua. Akaongeza kuwa AMREF imeona ni vyema kutumia jamii zetu kuleta mabadiliko katika jamii.

Mradi huu umedhaminiwa na mdhamini anayejulikana kwa jina la Sternstunden chini ya shirika la AMREF GERMAN ili kuongezea nguvu mradi wa kupinga ukeketaji ambao kwa awamu ya kwanza utafanyika kwa kipindi cha mwaka mmoja kuanzia Januari 1/2017 hadi Desemba 31/2017. Kata zitakazonufaika na mradi huu kutokana na tathimini ya uwepo wa jamii ya wafugaji wengi na kukithiri kwa tamaduni hii ya ukeketaji ni pamoja na Segera, Malezi, Konje, Kwamagome na Ndolwa ambapo kiasi cha uro 176,634.22 sawa na milioni miatatu za kitanzania zitatumika kutekeleza mradi huo.

Alda Sadango
Afisa Habari
Halmashauri ya Wilaya Handeni.
  Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mhe. Godwin Gondwe akizungumza na wakuu wataalamu wa Wilaya ya Handeni wakati wa uzinduzi huo.
  Baadhi ya wataalamu wa Wilaya ya Handeni walioshiriki uzinduzi huo.

 Kamati ya ulinzi na usalama  wakimsikiliza  Mhe. Mkuu wa Wilaya kwenye ufunguzi wa mradi huo.
Daktari Aisha Bianaku ambaye pia ni mratibu wa mradi  akiwaelezea wataalamu kuhusu mradi na mikakati iliyowekwa kuwafikia walengwa.
Bw. Henry Bendera mwezeshaji wa mradi kutoka AMREF akizungumza wakati wa uzinduzi huo. 
 Daktari Sarafina Mkua Mratibu wa afya ya uzazi kwa mama na mtoto AMREF kitaifa akielezea baadhi ya athari za ukeketaji. 

Viewing all 46389 articles
Browse latest View live




Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596344.js" async> </script>