Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1116 | 1117 | (Page 1118) | 1119 | 1120 | .... | 1897 | newer

  0 0

   Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akifurahia ngoma ya Limdoya iliyochezwa na wasanii kutoka kijiji cha Kanitelele wilayani njombe wakati alipohutubia mkutano wa hadhata kayika uwanja wa michezo wa Lupembe mkoani Mjombe Januari 25, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama  chai   katika shamba la wananchi wa kijiji  cha Lwangu , Njombe akiwa katika ziara ya mkoa huo Januari 25, 2017.Kulia ni Meneja wa Kampuni a kutoa huduma kwa wakulima wadogo wa Njombe  (NOSC),Bw.Filbert Kavia
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Askofu   Alfred Maruma wa jimbo Katoliki la Njombe,  wakati alipotembelea shamba ya chai ya wakulima wa kijiji cha Lwangu, Njombe Januari 25, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imejipanga katika kuhakikisha inaongeza thamani ya mazao yake kabla ya kuyauza nje ya nchi.

  Amesema kwa muda mrefu Serikali ilikuwa inapata hasara kwa kusafirisha malighafi nje nchi lakini kwa sasa inajenga viwanda ili iweze kuuza bidhaa.

  Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo jana jioni (Jumatano, Januari 25, 2017) wakati alikizungumza na wakulima wa chai katika kijiji cha Lwangu wilayani Njombe.

  “Miaka mingi Serikali imekuwa ikipata hasara kwa kuuza mazao nje ya nchi, tumeamua kujenga viwanda vitakavyoweza kuyachakata na kuuza bidhaa badala ya malighafi,”.

  “Ujenzi wa viwanda ni moja kati ya mikakati dhati ya Serikali ya kuhakikisha mazao  mnayolima yanakuwa na thamani kubwa  hivyo kuwaongezea tija,” alisema.

  Kutokana na mkakati huo Waziri Mkuu amewataka wananchi kuongeza juhudi katika kilimo. “Kuna anayetaka hela hapa? Kama mnataka mali mtazipata shambani. Limeni,”.

  Waziri Mkuu alisema mazao hayo ndiyo yatakayoweza kuleta tija kwa wakulima, hivyo aliwashauri waendelee kushirikiana katika vikundi ili wapate misaada ya kitaalam kwa urahisi.

  Aidha, alimuagiza mkuu wa wilaya hiyo, Ruth Msafiri na Maafisa kilimo kuwatembelea wakulima hao kwa lengo la kuwaelekeza namna bora ya kuendeleza mazao yao.

  Waziri Mkuu alisema hatua hiyo itawawezesha wakulima kupata mbinu bora za kilimo na hatimaye kuvuna mazao mengi yenye viwango vya ubora vinavyotakiwa kimataifa.

  Katika hatua nyingine Waziri Mkuu aliiagiza halmashauri ya wilaya ya Njombe kuwaunga mkono wakulima hao kwa kuimarisha barabara zinazoingia kwenye mashamba yao.

  “Tuwaunge wakulima wetu kwa kuwaimarishia miundombinu ya barabara ili kuwawezesha kupeleka chai yao kiwandani kwa gharama nafuu,” alisema.

  Naye Mbunge wa jimbo la Lupembe Mheshimiwa Joram Hongoli alisema kilimo cha chai ndio mkombozi kwa wananchi hao, hivyo aliwaomba waongeze juhudi.

  Awali Meneja Mkuu wa Kampuni ya Kutoa Huduma kwa Wakulima Wadogo Njombe (NOSC), Bw. Filber Kavia alisema kampuni inatoa huduma za kitaalam  kwa wakulima.

  Alisema wanalenga kuendeleza kilimo cha chai kwa kuongeza kuongeza uzalishaji kwa hao kutoka kilo 500 hadi kilo 2,000 za majani makavu ya chai kwa hekta kwa mwaka.

  Meneja huyo alisema kampuni inakusudia kuongeza mashamba mapya ya chai hadi kufikia hekta 3,800 kutoka hekta 614 ifikapo mwaka 2025.

  Bw, Kavia alisema huduma nyingine inayotolewa na kampuni hiyo ni utoaji wa mikopo nafuu ya pembejeo bila ya riba na mkulima hulipa muda mrefu kupitia mauzo ya chai.

  Pia kampuni hiyo inatoa huduma ya usimamizi wa mashamba makubwa ya chai ya vijiji na watu binafsi kwa mkataba maalumu ili kuongeza uzalishaji na tija.

  Awali Waziri Mkuu alikagua eneo litakalojengwa kiwanda cha kisasa cha kuchakata chai cha kampuni ya Unilever.

        
  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  ALHAMIS, JANUARI 26, 2017.


  0 0  0 0

  Mhariri Mtendaji wa kampuni ya magazeti ya Serikali (TSN), Dk Jim Yonazi (kushoto) na Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili la Taifa, Dk Selemani Sewange wakiweka saini makubaliano ya kukuza lugha ya kiswahili kupitia gazeti la Habari Leo wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka kumi ya gazeti hilo, jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia (kutoka kushoto waliosimama) ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, Naibu Mhariri Mtendaji wa TSN, Tuma Abdallah, Kaimu Mhariri wa  Habari Leo, Nicodemus Ikonko na Mwanasheria wa TSN, Mwadawa Sakware  (kulia)
   Mhariri Mtendaji wa kampuni ya magazeti ya Serikali (TSN), Dk Jim Yonazi (kushoto) na Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili la Taifa, Dk Selemani Sewange wakikabidhiana makubaliano ya kukuza lugha ya kiswahili kupitia gazeti la Habari Leo wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka kumi ya gazeti hilo, jijini Dar es Salaam. 
   Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye,akizungumza kwenye sherehe ya maadhimisho ya miaka 10 ya gazeti la HabariLeo,iliyofanyika leo katika uwanja wa Taifa,jijini Dar.Waziri Nape alisema kuwa Gazeti hilo lililoanza kuchapishwa rasmi Desemba 21, 2006,limekuwa na  mchango mkubwa sana katika juhudi za kuepuka migawanyiko ya kisiasa nchini, na kuimarisha juhudi za kuendeleza umoja wa kitaifa. 

  "Na hili likiwa ni mojawapo ya malengo ya msingi na kusudio la kuanzishwa kwa Gazeti la HabariLeo na kwa kweli niwapongeze kwa namna mlivyolifanya kwa kiwango cha juu kabisa,Muda wa miaka 10 sio mdogo kwa uhai wa gazeti hasa kutokana na ushindani mkubwa na changamoto mbalimbali zinazoikabili tasnia ya habari hapa nchini na duniani kote.",alisema Waziri Nape.
   Mgeni rasmi,Waziri Nape akizindua bahati nasibu ya watoto waliozaliwa desemba 21,2006,anaeshuhudia pichani kulia Mhariri Mtendaji wa kampuni ya magazeti ya Serikali (TSN), Dk Jim Yonazi 
   Uongozi wa TSN ukimkabidhi zawadi ya Picha Waziri Nape 
   Muda wa Cheers kwa meza kuu
   Chiaazzzzz
   Waziri Nape akiwasha mishumaa iliyowekwa kwenye keki maalum kwa ajili ya maadhimisho hayo
   Waziri Nape pamoja na uongozi wa TSN ,Mhariri Mtendaji wa kampuni ya magazeti ya Serikali (TSN), Dk Jim Yonazi (kushoto) na Naibu Mhariri Mtendaji wa TSN, Tuma Abdallah (kulia) kwa pamoja wakikata  keki maalum kwa ajili ya maadhimisho hayo
   Waziri Nape akiongoza meza kuu kukata  keki maalum kwa ajili ya maadhimisho hayo. 
   Waziri Nape akimlisha keki Mhariri Mtendaji wa kampuni ya magazeti ya Serikali (TSN), Dk Jim Yonazi

   Waziri Nape akionesha umahiri wake wa kupiga gitaa na kuimba ikiwa ni sehemu ya kuonogesha maadhimisho ya miaka 10 ya gazeti la Habarileo

  Wafanyakazi wa kampuni ya magazeti ya Serikali (TSN) na wageni mbalimbali wakifuatilia matukio ya maadhimisho ya sherehe za miaka kumi ya gazeti la Habari Leo, yaliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
  0 0

  Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
  Mmiliki mwenza wa kampuni ya Jamii Media, Mike Mushi amefikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi kisutu na kuunganishwa katika mashtaka yaleyale yanayomkabili mkurugenzi wa kampuni hiyo, Maxence Melo.

  Washtakiwa wote wawili walisomewa mashtaka mbele ya hakimu mkazi mkuu, Thomas Simba na Hakimu mkazi mkuu, Godfrey Mwambapa.

  Wakili wa serikali, Mohamed Salum alisema kuwa washtakiwa hao wakiwa eneo la mikocheni kwa nafasi zao wakijua jeshi la polisi linafanya uchunguzi wa mawasiliano kwa njia ya mtandao kufuatia chapisho lililochapishwa katika tovuti yao na waliamua kushindwakutoa ushirikiano kwa Jeshi la polisi kwa kuwanyima data walizonazo.

  Hata hivyo upelelezi wa kesi hizo mbili umekamilika na washtakiwa wote hawa watasomewa mashataka yao kuanzia Februari 9 na Februari 20.
  Mpaka sasa washtakiwa wote wawili wapo nje kwa dhamana kwa masharti ya bondi ya Milioni 10 kwa kila kosa na masharti ya kutosafiri nje ya nchi.

   Maxence Melo akijaribu kumueleza jambo mmiliki mwenza wa Jamii Forum Mike mushi ndani ya chumba cha Mahakama
   Maxence Melo na Mike Mushi wakimsikiliza wakili wao


  0 0

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) George Simbachawene akizindua kitabu cha Mwongozo wa Taifa wa Utekelezaji wa Sera za Huduma kwa watoto waliokatika mazingira hatarishi kwa Serikali za Mitaa leo jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia tukio kutoka kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Misaada na Maendeleo la Marekani (USAID) nchini Tanzania Tim Donnay, Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam Theresia Mmbando, Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa – TAMISEMI Dkt. Zainab Chaula
  Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam Theresia Mmbando akimkabidhi Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam kitabu cha Mwongozo wa Taifa wa Utekelezaji wa Sera za Huduma kwa Watoto waliokatika mazingira hatarishi kwa Serikali za Mitaa leo jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) George Simbachawene na Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa – TAMISEMI Dkt. Zainab Chaula (wapili kulia).
  Baadhi ya washiriki wa mkutano baina ya USAID na TAMISEMI uliofanyika katika ofisi za TAMISEMI jijini Dar es Salaam wakifuatilia hoja kutoka kwa wasilishaji wa mada leo jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa Sekta kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Dkt. Andrew Komba akichangia mada wakati wa mkutano baina ya TAMISEMI na USAID kuhusu Afya ya mama na motto leo jijini Dar es Salaam.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) George Simbachawene akiteta jambo na Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Misaada na Maendeleo la Marekani (USAID) nchini Tanzania Tim Donnay mara baada ya kumaliza mkutano kuhusu Afya ya Mama na Mtoto leo jijini Dar es Salaam.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) George Simbachawene akiwa katika picha ya pamoja washiriki wa mkutano baina ya TAMISEMI na USAID kuhusu Afya ya mama na mtoto leo jijini Dar es Salaam.Kutoka Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki, Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Misaada na Maendeleo la Marekani (USAID) nchini Tanzania Tim Donnay, Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa – TAMISEMI Dkt. Zainab Chaula na Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam Theresia Mmbando.

  Picha zote na: Frank Shija – MAELEZO.

  0 0

   Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala Omary Kumbilamoto akizungumza na mtoto mwenye ulemavu wa ngozi katika shule ya msingi Miembeni.
   Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala Omary Kumbilamoto akimkabidhi mifuko mwenyekiti wa kamati ya ujenzi wa shule ya miembeni, Kuruthumu Hamisi


  Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii.
  Katika kutekeleza sera ya elimu bure Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala na Diwani wa Vingunguti , Omary Kumbilamoto amekabidhi mifuko 12 ya Saruji kwa ajili ya ujenzi wa shule ya msingi Miembeni.

  Kumbilamoto amesema kuwa mifuko hiyo ya saruji ni kwa ajili ya ujenzi wa  sakafu ya madarasa mawili ambayo yamekamilika lakini yalikuwa ayana sakafu.
  “mimi nilipita hapa nikafanya ziara na kujionea mapungufu yaliyopo katika ujenzi wa madarasa haya ambayo yalianza kujengwa na kamati ya maendeleo ya shule kwa kushirikiana na wananchi hivyo nimeona nichangie hii mifuko 12 ya Saruji”

  Kumbilamoto amewashukuru wananchi waliofika katika hafla hiyo kwani wameweza kujichangisha  na kupata shilingi laki mojana ishirini ambazo zitaweza kununulia mchanga wa kujengea.Ametoa wito kwa wadau wengine wa maendeleo kuendelea kumuunga mkono Rais Magufuli kwa kuweza kusaidia maendeleo ya elimu katika kata ya vingunguti.
  Kwa upande wake mwalimu mkuu wa shule hiyo Hidaya Hamisi amemshukuru Naibu meya kwa msaada huo ambao utaweza kusaidia kukamilika kwa ujenzi wa madarasa hayo na kuondoa msongamano kwa wanafunzi.
   Naibu meya wa Manispaa wa Ilala, Omary Kumbilamoto akikabidhi mifuko ya saruji kwa mwalimu mkuu wa shule ya msingi Miembeni, Hidaya Hamisi
   Picha ya pamoja na ya Naibu Meya na wazazi wa wanafunzi wanaosoma Miembeni shule ya msingi


  0 0

  Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kindondoni Benjamin Sitta (katikati) akikata utepe wa kuzindua  huduma ya kipesa ya "DCB Jirani" na "DCB Pesa" sambamba na Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa DCB Prof Lucian Msambichaka (kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa DCB Edmund Mkwawa (kushoto).
  Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kindondoni Benjamin Sitta (kushoto) pamoja na Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa DCB Prof Lucian Msambichaka (katikati) wakizindua magari ya DCB Jirani na DCB Pesa  jana Jijini Dar es salaam, pembeni ni  Mkurugenzi Mtendaji wa DCB Edmund Mkwawa.
  Wafanyakazi wa Benki ya DCB wakiwa katika picha ya pamoja na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kindondoni Benjamin Sitta jana Jijini Dar es salaam.
  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

  Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Benjamin Sitta amewapongeza uongozi wa benki ya DCB kwa kuweza kuwasogezea huduma ya kipesa ya "DCB Jirani" na "DCB Pesa" kwani kwa hatua hiyo ni wanakuwa miongoni mwa benki zinazoanzisha huduma zinazoendana na teknolojia za kisasa.

  Akizungumza katika uzinduzi huo, Mstahiki Meya Sitta amesema kuwa kwa kuanzisha huduma hiyo ni moja ya maendeleo yanayohitajika katika tasnia ya kibenki na zaidi anautaka uongozi wa bodi ya DCB kuongeza juhudi na ubunifu katika kuileteta mafanikio zaidi siku zijazo na kuendelza sifa nzuri iliyopatikana.

  Ameongeza na kusema kuwa, kuna changamoto ,mbalimbali katika sekta za kibenki zinakabiliana nazo ila ametoa ushauri kwa manispaa za Dar es salaam kutumia benki hiyo katika shughuli zao za kibenki ili kuiwezesha kupata amana za kudumu na zaidi amesisitiza kuwa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni wataendelea kuwa mstari wa mbele kutumia DCB kwani wameweza kufaidika na gawio la kila mwaka.

  Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa DCB Prof Lucian Msambichaka amemshukuru mstahiki  meya kwa kukubali kuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa huduma ya kipesa ya 'DCB Jirani' na "DCB Pesa" na kumshukuru kwa hatua nzuri ya Manispaa za Mkoa wa Dar es salaam kwa kukubali kupitisha mfuko wa mkopo ya  wanawake na vijana katika benki ya DCB.

  Msimbachaka ameziomba manispaa hizo kuleta fedha za asilimia 10 ya mapato yao zinazotengwa na kila manispaa kwa ajili ya mfuko huu ili benki iendelee na mpango wake wa kuwakopesha wajasiriamali kwa niaba yao.

  Akieleza kuhusiana na DCB Jirani, Msambichaka amesema kuwa kwa kutumia huduma hii ya kisasa wateja wa DCB wanaweza kufaidika kwa kupata huduma za kibenki katibu na mahala anapoishi bila kufuata tawi la benki hiyo, kwa upande wa DCB Pesa mteja ataweza kutumia simu kulipia huduma mbalimbali kama Dawasa, Luku, DSTV, kununua muda wa maongezi, kukopa mikopo midogo midogo kwa ajili ya kuendeleza biashara na pia wafanyakazi wataweza kutumia kwa kuomba nusu ya mshahara.

  Mbali na hilo, pia DCB waliweza kuwakabidhi zawadi zao wateja waliofanikiwa kushinda kwenye droo ya awali ya Kampeni ya kufungua na kuweka amana na DCB benki ambapo washindi 20 waliweza kukabidhiwa zawadi zao za Tshirt, wawili walikabidhiwa simu za mkononi aina ya Smartphone na wengine watatu walipatiwa ada ya shule kwa ajili ya watoto.
  Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Benjamin Sitta akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma ya kipesa ya "DCB Jirani" na "DCB Pesa" na kuwapongeza kwa kuanzisha huduma hiyo ni moja ya maendeleo yanayohitajika katika tasnia ya kibenki jana Jijini Dar es salaam.
  Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa DCB Prof Lucian Msambichaka akizungumza wakati wa  uzinduzi wa huduma ya kipesa ya "DCB Jirani" na "DCB Pesa" na kuwapongeza kwa kuanzisha huduma hiyo ni moja ya maendeleo yanayohitajika katika tasnia ya kibenki jana Jijini Dar es salaam.
   Mkurugenzi Mtendaji wa DCB Edmund Mkwawa akizungumza wakati wa  uzinduzi wa huduma ya kipesa ya "DCB Jirani" na "DCB Pesa" na kuwapongeza kwa kuanzisha huduma hiyo ni moja ya maendeleo yanayohitajika katika tasnia ya kibenki jana Jijini Dar es salaam.

   Baadhi ya washindi wa zawadi ya Tshirt wakipokea zawadi zao walizokabidhiwa na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kindondoni Benjamin Sitta jana Jijini Dar es salaam.
   Washindi wa zawadi ya simu wakipokea wakikabidhiwa na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kindondoni Benjamin Sitta jana Jijini Dar es salaam.
  Washindi wa fedha taslimu wakikabidhiwa na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kindondoni Benjamin Sitta
  Wateja wa Benki ya DCB wakiwa wamejitokeza kwenye uzinduzi wa uzinduzi wa huduma ya kipesa ya "DCB Jirani" na "DCB Pesa" na kuwapongeza kwa kuanzisha huduma hiyo ni moja ya maendeleo yanayohitajika katika tasnia ya kibenki jana Jijini Dar es salaam. Picha zote na Zainab Nyamka.

  0 0

   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Naibu Mtendaji Mkuu wa Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC), Eric Mwingira kuhusu  sampuli ya chuma  kilichogunduliwa katika mgodi wa Liganga  wakati alipotembelea mgodi huo Januari 26, 2017.
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Naibu Mtendaji Mkuu wa Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC), Eric Mwingira kuhusu  sampuli ya chuma  kilichogunduliwa katika mgodi wa Liganga  wakati alipotembelea mgodi huo Januari 26, 2017. 
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama mlima utaoelezewa na watalaamu kuwa uana hazina kubwa ya madini ya chuma wakati alipotembelea mgodi wa chuma wa Liganga wilayani Ludewa Januari 26, 2017. Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Christopher Ole Sendeka. 
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitembelea eneo lenye mlima anaoelezewa na watalaamu kuwa una hazina kubwa ya madini ya chuma wakati alipotembelea   mgodi  wa chuma wa Liganga wilaya Ludea Januari 26, 2017. Kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC), Samuel Nyantahe.
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitembelea eneo lenye mlima anaoelezewa na watalaamu kuwa una hazina kubwa ya madini ya chuma wakati alipotembelea eneo la mgodi a wa chuma wa Liganga wilaya Ludea januari 26, 2017. Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Christopher Ole Sendeka na Kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC), Samuel Nyantahe.
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua eneo lenye mlima anaoelezewa na watalaamu kuwa una hazina kubwa ya madini ya chuma wakati alipotembelea eneo la mgodi a wa chuma wa Liganga wilayani Ludewa januari 26, 2017. Wapili kulia  ni Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC), Samuel Nyantahe  na kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Christopher Ole Sendeka.
    Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikaguaeneo lenye mlima anaoelezewa na watalaamu kuwa una hazina kubwa ya madini ya chuma wakati alipotembelea eneo la mgodi a wa chuma wa Liganga wilayani Ludewa januari 26, 2017. Wapili kulia  ni Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC), Samuel Nyantahe  na kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Christopher Ole Sendeka
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitembelea eneo lenye mlima anaoelezea na watalaamu kuwa una hazina kubwa ya madini ya chuma wakati alipotembelea eneo la mgodi  wa chuma wa Liganga wilayani  Ludewa Januari 26, 2017.
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifuhia wimbo wa kikundi cha ngoma cha kijiji cha Mundindi wialyani Ludewa wakati alipokwenda kijijini hapo kukagua maendeleo ya mgodi wa chuma wa Liganga Januari 26, 2017. 
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi wa kijiji cha  Mundindi wialyani Ludewa baada ya kutembelea mgodi wa chuma wa Liganga Januari 26, 2017. 
   Wanawake wa kijiji cha mundindi wilayani Ludewa wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipowahutubia baada ya kukagua mgodi wa chuma  wa Liganga Januari 26, 2017. 
   Mlima wenye mwamba ambao watalaamu wa madini wameeleza kuwa kwa zaidi ya asilimia 60  una  madini ya chuma  katika eneo   la Liganga lililotembelewa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  Januari 26, 2017.
   (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akisalimiana na Mwenyekiti wa Bodi la Shirika la Maendeleo la Taif (NDC), Samuel  Nyantahe baada ya kuwasili kwenye ueneo la mgodi wa Liganga wilayani Ludewa kukagua maendeleo ya  hatua muhimu zitakazowezesha kazi uchimbaji chumakuanza haraka.

  0 0

  Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii.

  Shindano la  wajasiliamali kwa vyuo vikuu mbalimbali nchini linategemea kuanza hivi karibuni likidhaminiwa na Benki ya Barclays nchini Tanzania.Kupitia benki hiyo kumezundiliwa mpango wake mpya wa udhamini kwa wanafunzi wa vyuo vikuu nchini.

  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo mratibu wa mradi huo Victor Mnyawami amesema kuwa wataweza kuzunguka vyuo vikuu vyote kwa ajili ya kupata washindani.

  “ujasiliamali ni muhimu sana katika uchumi wa taifa hili hivyo ni vyema tukawa na wahitimu wa vyuo vikuu ambao wataweza kujitengenezea ajira zao wenye kuliko kusubiri kuajiriwa” amesema Mnyawami.

  Kwa upande wake afisa uhusiano wa Barclays, Hellen Siria amesema kuwa mshindi wa shindano hilo atapata fursa ya kuungana na vijana wengine kutoka vyuo vikuu mbalimbali nchini ujerumani.

  Hellen amesema kuwa vijana watakaopata fursa ya kupita kwenye mchujo watapata nafasi ya kupata mafunzo ambayo yataweza kuwasaidia kujiajiri.
   Kiongozi wa Taasisi inayoandaa shindano la  wajasiliamali kutoka vyuo vikuu mbalimbali nchini, Victor Mnyawami akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na shindano hilo.
   Meneja uhusiano wa Benki ya Barclays nchini, Hellen Siria  wakijadiliana jambo na  Kiongozi wa Taasisi inayoandaa shindano la  wajasiliamali kutoka vyuo vikuu mbalimbali nchini, Victor Mnyawami kuhusu mchango wa Bank hiyo katika kusaidia jamii hasa wanavyuo. 
   Meneja uhusiano wa Benki ya Barclays nchini, Hellen Siria  akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam leo juu ya udhamini wa benki ya Barclays kuhusu shindano la wajasiliamali kutoka vyuo vikuu mbalimbali hapa nchini.

  0 0

   
  Bi Mindi akimkabidhi Bi. Sarah kombe la ushindi kwa niaba ya Wizara. Bi. Kibonde aliipokea zawadi hiyo kwa niaba ya Mamlaka ya Usimamizi wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii. 
   
  Meneja wa Mradi wa Mfumo wa Forodha wa TANCIS kutoka TRA akipokea zawadi ya cheti cha ushindi kutoka kwa Bi. Mindi Kasiga. 

   
  Picha ya pamoja ya Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje, TRA na SSRA. 
   
  Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Mindi Kasiga akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kwenye kikao kilichofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere, tarehe 26 Januari, 2016. Katika kikao hicho Bi. Mindi alizungumza kuhusu tuzo za ubunifu zilizotolewa na Umoja wa Afrika (AU) kwa Mamlaka ya Usimamizi wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii na Mamlaka ya Mapato Tanzania ambazo zilikuwa miongoni mwa taasisi zilizoshindanishwa na kuibuka washindi.Pia alitumia fursa hiyo kuwaarifu waandishi wa habari kuhusu Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Umoja wa Afrika unaoendelea nchini Ethiopia-Addis Ababa na Mkutano wa Tume ya pamoja ya ushirikiano kati ya Tanzania na Malawi unaotarajiwa kufanyika tarehe 3 hadi 5 Februari, 2017. 
   
  Kutoka kushoto ni Bw. Felix Tinkasimile Meneja wa Mradi wa Mfumo wa Forodha wa TANCIS, kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Richard Kayombo, Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi kutoka TRA, Bi. Sarah Kibonde kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) na Bw. David Nghambi kutoka Mamlaka hiyo 
   
  Bi. Sarah akizungumza kuhusiana na tuzo iliyotolewa kwa SSRA ambapo alieleza wameshinda Tuzo hiyo katika kipengele cha utunzaji data ambapo wamekuwa wakishirikiana na taasisi za Serikari zinashughulika na umma katika masuala mbalimbali kama Mamlaka ya Vitambulika, Mamlaka ya Mapato na RITA. 
   
  Bw. Richard Kayombo akizungumzia tuzo hizo ambapo aliishukuru Wizara ya Mambo ya Nje kwa uratibu na kutambua umuhimu wa huduma zinazotolewa na Mamlaka ya Mapato kwa umma katika kuboresha utendaji na kuongeza uwazi na uwajibikaji. 


  Taarifa kuhusu Mkutano wa Tume ya Pamoja ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Malawi, Tuzo za AU kwa SSRA na TRA na Mkutano wa AU-Addis Ababa

  Mkutano wa Nne wa Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano (JPCC) kati ya Tanzania na Malawi umepangwa kufanyika mjini Lilongwe, Malawi tarehe 03 hadi 05 Febuari 2017. Mkutano huo utawakutanisha viongozi na wataalamu wa sekta mbalimbali kutoka Tanzania na Malawi.

  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine P. Mahiga (Mb), anategemewa kuongoza ujumbe wa Tanzania katika mkutano huo. Aidha, Uongozi wa Mkoa wa Mbeya ambao umekuwa ukishiriki katika vikao vya maandalizi, unategemewa kushiriki katika mkutano huo.

  Lengo la mkutano huu ni kujadili na kutathmini hatua zilizofikiwa katika utekelezwaji wa makubaliano yaliyofikiwa katika Mkutano wa Tatu wa JPCC uliofanyika Tanzania, tarehe 24 hadi 30 Juni, 2003.

  Miongoni mwa mafanikio yaliyofikiwa kwenye utekelezaji wa makubaliano ya mikutano iliyopita kwa upande wa Tanzania ni pamoja na; Kuanzishwa kwa mradi wa Kituo cha Huduma za Pamoja Mipakani (One Stop Border Post – OSBP) katika mpaka wa Kasumulu/Songwe ambao umefikia katika hatua nzuri; Idara za Uhamiaji, Polisi na Forodha za nchi zetu mbili zinaendelea kushirikiana katika kutoa huduma na kudhibiti abiria na mizigo katika maeneo ya mpakani.

  Pia, Mamlaka ya Bandari Tanzania imeruhusu Mamlaka za Malawi kuwa na maeneo yao katika bandari zetu, kwa ajili ya kuhifadhia mizigo na bidhaa nyingine zinazopitia nchini kabla ya kwenda Malawi. 

  Aidha, mkutano huo utatoa fursa kwa nchi zetu mbili kujadiliana na kukubaliana kuhusu maeneo mapya ya ushirikiano. Miongoni mwa maeneo hayo (kwa upande wa Tanzania) ni pamoja na: Kuanzisha ushirikiano katika sekta ya usafiri wa majini, ambapo mbali na faida za kiuchumi, safari hizo zitaimarisha mwingiliano wa watu na kupunguza tofauti zilizopo. Kwa hivi sasa Serikali inajenga meli tatu, mbili kwa ajili ya kusafirisha mizigo na moja kwa ajili ya abiria. 

  Maeneo mengine ni kuanzisha Mkataba wa ushirikiano katika Sekta ya Usafiri wa Anga (BASA); Kuanzisha mfumo wa kurahisisha ufanyaji biashara kwa ajili ya kuwasaidia wafanyabiashara wadogo hasa katika maeneo ya mpakani; Kuanzisha ushirikiano katika uhifadhi wa mazingira na masuala ya afya ikiwemo magonjwa ya mlipuko hususan maeneo ya mipakani; na Kuanzisha ushirikiano katika sekta ya elimu ya vyuo vikuu na vyuo vingine vya amali.

  Tangu kuanzishwa kwa Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano (JPCC) kati ya Tanzania na Malawi nchi hizi mbili zimeshafanya vikao vinne vya Tume hiyo. Kikao cha mwisho kilifanyika hapa Dar es Salaam, Tanzania tarehe 24 hadi 30 Juni, 2003 na kuhudhuriwa na viongozi na wataalam wa sekta mbalimbali kutoka nchi zetu mbili.

  Wakati huohuo, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Mindi Kasiga kwa niaba ya Wizara amekabidhi tuzo kwa wawakilishi wa taasisi za Mamlaka ya Usimamizi wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Bi. Sarah Kibonde na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Richard Kayombo baada ya kuibuka washindi wa Tuzo zilizotolewa na Umoja wa Afrika (AU). 

  Akipokea kombe baada ya kuibuka mshindi kwenye kipengele B kuhusu “Innovative Partnership in Service Delivery for its National Social Security Collaborative Database Bridging Project" Bi. Kibonde alisema kuwa ushindi huo ni chachu ya taasisi yao kufanya vizuri zaidi katika kutoa huduma bora kwa wananchi wote kwa ujumla. 

  Naye Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi, Bw. Kayombo ambaye taasisi yake imefanikiwa kushika nafasi ya pili kipengele C kuhusu "Tanzania customs Integrated System" ameushukuru Umoja wa Afrika kwa kuandaa mashindano hayo ambayo ni muhimu katika kujenga uwazi kwenye eneo la ulipaji kodi. 

  Pia ameushukuru Ubalozi wa Tanzania kwa kupokea Tuzo hizo kwa niaba yao na kuishukuru Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirkiano wa Afrika Mashariki kwa kukabidhi ushindi huo kwao.

  Katika hatua nyingine, Bi. Kasiga alizungumzia juu ya Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Umoja wa Afrika (AU Summit) unaotarajiwa kufanyika Jijini Addis Ababa, Ethiopia tarehe 30 na 31 Januari, 2017. Mkutano huo umetanguliwa na kikao cha Kamati ya Wawakilishi wa Kudumu na Maafisa Waandamizi kilichofanyika tarehe 22 hadi 24 Januari, 2017 na kufuatiwa na kikao cha Baraza la Mawaziri kilichoanza tarehe 25 hadi 27 Januari, 2017.


  Imetolewa na:
  Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
  Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, 
  Dar es Salaam, 26 Januari, 2017  0 0

   Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Prof. Ibrahim Hamis Juma akiongea na wanahabari (hawapo pichani) kuhusu Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini kitakachofanyika hivi karibuni katika viwanja vya Mahakama vilivyopo jijini Dar es Salaam.
   Jaji Kiongozi wa Mahakam Kuu Tanzania Jaji Ferdinandi Wambali (kushoto) akiongea na wanahabari (hawapo pichani) kuhusu Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini kitakachofanyika hivi karibuni katika viwanja vya Mahakama vilivyopo jijini Dar es Salaam.
  Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Katrina Revocati akiongea na wanahabari (hawapo pichani) kuhusu Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini kitakachofanyika hivi karibuni katika viwanja vya Mahakama vilivyopo jijini Dar es Salaam.(Picha na Benjamin Sawe- Maelezo)


  Rais John Pombe Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kilele cha maadhimisho ya siku ya Sheria nchini zitakazofanyika mwanzoni mwa mwezi ujao katika viwanja vya Mahakama jijini Dar es Salaam.

  Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam Kaimu Jaji Mkuu Prof. Ibrahim Hamis Juma amesema mahakama itawaelimisha wananchi jitihada mbalimbali ilizochukua zenye lengo la kuboresha huduma zake kupitia mpango mkakati wa miaka mitano inaoutekeleza katika kutoa haki kwa wakati na kuwezesha ukuaji wa uchumi.

  Amesema kabla ya kilele cha maadhimisho hayo, mahakama itafanya matembezi maalum yatakayoongozwa na Rais Mstaafu Mh. Ali Hassan Mwinyi  na yataanzia Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kuishia katika viwanja vya Mnazi mmoja 

  Katika matembezi hayo Mhe. Rais Mstaafu Mwinyi atazindua rasmi maadhimisho ya wiki ya elimu ya sheria ikiwa ni sehemu ya sherehe za kuelekea maadhimisho ya kilele cha siku ya sheria nchini.

  Aidha ametoa rai kwa wananchi kutembelea sehemu zote zilizoandaliwa kwa ajili ya utoaji elimu ya sheria nchini kwa ajili ya kujifunza na kupata huduma mbalimbali za Kisheria 

  Alizitaja huduma hizo ni pamoja na taratibu za ufunguaji mashauri katika ngazi mbalimbali za mahakama, taratibu za kesi za mirathi, taratibu za kesi za dhamana, taratibu za rufaa, ndoa na talaka, taratibu za kupokea na kushughulikia malalamiko na Msaada wa Kisheria


  Maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini hufanyika kila mwaka mwanzoni mwa mwezi wa pili na mwaka huu yamebeba ujumbe wa Umuhimu wa Utoaji Haki kwa Wakati Kuwezesha Ukuaji wa Uchumi.


  0 0

  Wakulima wakipata maelezo kutoka kwa wataalamu namna ya kupata mazao bora 
  Mmoja wa wakulima wakiangalia mazao yaliyostawisha kwa kufuata kanuni za kilimo 
  Mkuu wa wilaya ya Arusha,Gabriel Daqarro akifungua maonesho ya siku mbili ya kimataifa unaofanyika kwenye viwanja vya taasisi ya Utafiti wa Kilimo Selian(Sari)jijini Arusha. 
  Sehemu ya mitambo iliyopo tayari kwaajili ya wakulima. 


  Mtaalamu wa Mawasiliano wa taasisi ya Agriculture Markets Development Trust(AMDT),Al-amani Mutarubukwa(kulia)akitoa maelezo kwa Mkuu wa wilaya ya Arusha,Gabriel Daqarro(wa pili kulia)kuhusu taasisi hiyo inayowajengea uwezo wakulima katika mazao ya Ufuta na Mahindi katika mikoa mbalimbali nchini. 
  Meneja wa Kampuni ya Monsanto nchini,Frank Wenga(kulia)akizungumza na wakulima waliofika kwenye maonesho hayo kujifunza mbinu za kilimo chenye tija. 
  Wakulima kutoka maeneo mbalimbali wakipata elimu ya matumizi ya kilimo bora na chenye tija.


  0 0


  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali lazima ijiridhishe ni kwa namna gani itafaidika na uwekezaji katika miradi ya makaa ya mawe na chuma kabla haijaanza.

  Amesema Serikali iko katika hatua za mwisho za mazungumzo na muwekezaji kabla ya kuanza uzalishaji kwenye miradi ya makaa ya mawe ya Mchuchuma na chuma cha Liganga.

  Miradi hiyo inatekelezwa kwa ubia kati ya Serikali ya Tanzania kupitia Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) na kampuni ya Sichuan Hongda (Group) Ltd (SHG) ya China. Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Alhamisi, Januari 26, 2017) wakati akizungumza na wananchi wa Kata ya Mundindi baada ya kukagua eneo la mradi wa chuma cha Liganga.

  “Madini haya yana viwango vya juu vya ubora, hivyo ni lazima tuwe makini kabla ya kuanza kwa uzalishaji wake. Kwani chuma chetu ni bora na tutachimba kwa zaidi ya miaka 50,”. “Hivyo maeneo haya ni nyeti na lazima Serikali ijipange vizuri na kujiridhisha kama vipengele vyote vya mkataba vimetengamaa ndipo mradi huo uanze,” amesema.

  Hata hivyo amesema mradi huo hautachukua muda mrefu utaanza hivyo wananchi wawe na subira. “Hatutaki kusikia tena suala la mikataba mibovu tunataka mikataba itakayoleta tija. Akizungumzia suala la fidia kwa wananchi wanaopisha mradi, amesema kabla haujaanza lazima walipwe fidia zao na tayari fedha zipo muwekezaji anasubiri ruhusa ya Serikali.

  Amesema kuna baadhi ya watu wamejipenyeza na kutaka kuiibia Serikali kupitia suala la ulipaji wa fidia. Serikali haiko tayari kuona wananchi hao wakitumika kama madaraja ya wizi. Waziri Mkuu amesema watu hao ambao hawahusiki na eneo hilo wamesababisha gharama za fidia kuwa kubwa, hivyo wataalam wanatathmini ili kubaini wahusika kabla ya kulipa.

  “Tunataka wananchi wenyewe waliokuwa hapa ndiyo tuwalipe fidia yao kwa mujibu wa tathmini husika. Fidia yenu mtalipwa baada ya kuwaondoa wezi wote waliojipenyeza. “Kuna watu wanataka kuiibia Serikali kwa mgongo wenu, hili hatutakubaliana nalo. Tupo makini vumilieni inalifanyia kazi suala letu. Hakuna haki ya mtu itakayopotea,” amesema.

  Naye Naibu Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Tanzania China International Mineral Resources Ltd (TCIMRL) Bw. Eric Mwingira amesema miradi ya Liganga na Mchuchuma inatekelezwa kwa mfumo unganishi ambayo ina vipengele vitano kikiwemo cha mgodi wa chuma cha Liganga.

  Amesema mgodi huo wa chuma una uwezo wa kuzalisha tani milioni 2.9 kwa mwaka huku kiwanda cha kuzalisha bidhaa za chuma Liganga kitazalisha tani milioni 1.1 kwa mwaka. Bw. Mwingira amesema kipengele kingine ni mgodi wa makaa ya mawe Mchuchuma wenye uwezo wa kuzalisha tani milioni tatu kwa mwaka.

  “Kipengele cha nne ni kituo cha kufua umeme cha megawati 600 huko Mchuchuma. Kati ya hizo megawati 250 zitatumika Liganga katika kuchenjua na kuzalisha chuma cha pua na megawati nyingine 350 zitaingizwa kwenye msongo wa Taifa ili kuiuzia TANESCO,” amesema.
   
  Pia kutakuwa na njia ya msongo wa umeme wa kilowati 220 kati ya Mchuchuma na Liganga na barabara ya mkato kutoka Mchuchuma hadi Liganga.

  Amesema gharama za uwekezaji katika mradi huo unganishi ni Dola bilioni tatu, ambapo dola milioni 600 ni mtaji wa muwekezaji na mkopo utakuwa dola bilioni 2.4. Awali Mbunge wa Jimbo la Ludewa Mheshimiwa Deo Ngalawa alimuomba Waziri Mkuu kuwaeleza wananchi hao ni lini watalipwa fidia za kupisha mradi wa chuma Liganga na mradi huo utaanza lini.


  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU, ALHAMISI, JANUARI 26, 2017.

  0 0


  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.

  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul  Makonda amekutana  na Umoja wa Madereva Tax Wilaya ya Ilala ilikusikiliza  kero zao zinazowakabili katika kazi yao.

  Makonda ameyasema hayo leo alipokutana na madereva hao, amesema kunahitaji madereva wa tax kuwa mfumo bora wa kusaidia jiji la Dar es Salaam kuwa na huduma bora ya usafiri wa tax na wenye usalama

  Amesema ni vyema kukawepo kifaa maalum kitakachoonesha umbali wa mteja anapokwenda ili alipe kulingana na umbali huo na ajue bei hiyo kuliko kukadiriana, pia amesema katika kufanikisha hayo serikali yake itaziondoa Tax bubu zote, na utaratibu wa kuweka rangi na namba kwenye magari utarudi ili Tax zote zitambulike.

  Aidha amesema madereva wa tax kutoa taarifa za matukio ya kiharifu pale wanapohisi abiria waliyempakia ni mtu wa kufanya matukio ya kialifu.
   Makonda amesema wakitoa taarifa za uhalifu watalisaidia Taifa kuwa katika hali ya usalama, huku akiwataka ndani ya wiki moja wakae wajadiliane waje na mapendekezo yatakayokuwa na tija kwa pande zote.

  Makamu Mwenyekiti wa Madereva  mkoa wa Dar es Salaam, Jacob Anyandwile amesema madereva hao wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo kutozwa kodi kubwa na Mamlaka ya mapato nchini (TRA) pamoja na uwepo wa huduma ya Tax kwa njia ya mtandao unafanywa na kampuni ya UBA ambayo  imechangia kuharibu  soko ya usafiri huo.
  Amesema kampuni ya UBA inatoza bei ndogo zaidi, pia gharama za uendeshaji hazilingani wanajikuta wao wanalipa kodi kubwa zaidi kuliko kampuni hiyo.

  Katibu Mkuu wa Umoja huo Ramadhani Ashiru ameeleza kuwa kampuni hiyo ya UBA inatumia Tax bubu ambazo hazitambuliki kisheria.
   Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza  na Umoja wa Madereva Tax na kusikiliza kero zao, ,leo jijini Dar es Salaam.Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.
   Katibu Mkuu wa Umoja wa Wamiliki wa Tax Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Ashiru akifafanua jambo katika mkutano uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
   Mkuu wa Usalama Barabarani Kanda Maalum ya Dar es Salaam (ZTO) ACP Awadhi Haji akitoa elimu kwa madereva wa Madereva Tax leo jijini Dar es Salaam.
  Mkutano ukiendelea

  0 0
 • 01/26/17--07:50: DC UYUI AACHIA NGAZI

 • Aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Uyui Bw.Gabriel Mnyele akizungumza na Mwandishi wa habari wa Azam tv Juma Kapipi wakati akiwa ofisi za CCM Wilaya ya Uyui ikielezwa kuwa alikuwa ameitwa na Uongozi wa chama hicho kufuatia kuwepo kwa taarifa kwamba ameamua kuachia ngazi nafasi ya Ukuu wa wilaya hiyo ya Uyui jambo ambalo alilithibitisha kwa Katibu wa CCM wilaya ya Uyui kwamba ni kweli amemwandikia barua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
  Bw.Gabriel Mnyele hakuwa tayari kuelezea maamuzi aliyochukua na kuwataka Waandishi waliokuwa wakihoji hatua ya maamuzi yake wasubiri tamko kutoka juu."Mimi sina la kusema kuhusu hilo nimeamua mwenyewe,kwani mmesikia kuwa nimetumbuliwa?Aliwahoji waandishi.

  0 0

   Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Dharura na Ajali katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dk Juma Mfinanga akiueleza ujumbe huo kazi zinazofanywa na idara yake.
   Mkuu wa Idara ya Mionzi katika hospitali hiyo, Dk. Flora Lwakatare akizungumza na ujumbe huo leo.
   Profesa wa Masuala ya Utafiti kutoka Chuo Kikuu cha Minnesota, Michelle Biros akiwa  na Mkuu wa Idara ya Mionzi wa Muhimbili, Dk. Flora Lwakatare wakati wakielekea katika chumba cha CT-Scan.
   Dk Lwakatare akitoa maelezo kwa ujumbe huo jinsi CT-scan inamvyofanya kazi. 
   Mmoja wa msimamizi wa wodi ya wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu wa hospitali hiyo, Trustworthy Majuta akifafanua jambo wa ujumbe huo leo.
   Mkuu wa Idara ya Wagonjwa wa Nje, Dk Raymond Mwenesano akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe huo leo. Picha na John Stephen, Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).

   Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru akizungumza na ujumbe wa watu watano kutoka Mennisota nchini Marekani. Ujumbe huo umetembelea maeneo mbalimbali ya hospitali hiyo Leo.
   Wageni hao wakiwamo wakurugenzi wa hospitali hiyo wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wakati akiwaeleza changamoto na mafanikio ya hospitali hiyo.  Kutoka kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji katika hospitali hiyo, Dk Julieth Magandi, Anne Hussian, Cheryl Grasmoen kutoka Chuo Kikuu cha Mennisota, Marekani na Mkurugenzi wa Tiba Shirikishi, Dk. Praxeda Ogweo wa Muhimbili.

  Ujumbe wa watu watano kutoka Chuo Kikuu cha Tiba cha Minnesota kutoka nchini Marekani leo wametembelea Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendajji wa hospitali hiyo, Profesa  Lawrence Museru.

  Ujumbe huo umeongozwa  na Mkuu wa masuala ya utafiti  katika Idara ya Magonjwa ya dharura kutoka Chuo hicho,  Profesa Michelle Biros .

  Katika mazungumzo hayo Profesa Museru ameuleza ujumbe huo mikakati na malengo mbalimbali ambayo MNH inafanya katika kuhakikisha huduma za kibingwa zinafanyika nchini ikiwa ni pamoja na upandikizaji wa figo, kuweka kifaa maalum cha usikivu  na kuongeza wodi kwa ajili ya wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalum.

  Kwa mujibu wa Profesa Museru, MNH inakabiliwa na changamoto ya wataalam  katika baadhi ya maeneo ikiwamo ICU.

  Maeneo waliotembelea ni  Idara ya Magonjwa ya  dharura na Ajali, Idara ya Mionzi, Mwaisela -wodi moja, Jengo la watoto na Jengo la wazazi namba mbili -Wodi 35.

  0 0

  Wajasiriamali toka vikundi mbalimbali mkoani Ruvuma wamehamasishwa kujiunga na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) ili kurahisisha matibabu wawapo katika shughuli zao za kawaida, Wajasiriamali watakaojiunga na mfuko huo na kuwa wanachama watalipia shilingi 76,800 kwa mwaka ili kupata matibabu kupitia mfuko huo.


  0 0

  Ushiriki wa wasanii watatu wa muziki aina ya Reggae na bendi zao kwenye  tamasha la 14 la Sauti za Busara  lenye kauli mbiu #AfricaUnited unaashiria kuwa ni wakati muafaka kwa wadau wa muziki Tanzania kuutazama muziki wa Reggae kwa jicho la pili.

  Kupitia jukwaa la Sauti za Busara  muziki wa Reggae umepewa uzito mkubwa kwa kuwa hubeba ujumbe mzito wa umoja, amani, upendo pamoja na kuibua mabaya yote yanayoendelea kwa jamii husika.

  Kupitia nafasi hizo tatu zilizotolewa na uongozi wa Sauti za Busara ni changamoto kwa wanamuziki chipukizi na mameneja wa muziki kuwekeza kwenye muziki wa Reggae Tanzania kama ilivyo kwa aina nyingine ya muziki.Vikundi hivi  ni miongoni mwa vikundi 40 vya muziki vitakavyotumbuiza ni pamoja na Rocky Dawuni kutoka Ghana, Sami Dan na Zewd band kutoka Ethiopia na Bob Magharib kutoka Morocco.

  Mkurugenzi wa tamasha Yusuf Mahmoud amesema, “wasanii hawa watatu wa Reggae wanawakilisha vema muziki wa Reggae kwa  bara la Afrika. Tuna hakika kuwa Watanzania wengi wanapenda Reggae  si kwa midundo yake tu bali ni pamoja na ujumbe wa matumaini kwa wote wanaopigania haki na uhuru,”.

  Bob Maghrib ni kundi lililozinduliwa mwaka 2011 lenye muunganiko wa wanamuziki wanaowakilisha tasnia ya muziki Morocco.  Kundi hili pia linamuenzi mwanamuziki maarufu wa Reggae  Bob Marley.

  Sami Dan ana taaluma ya uhandisi  mwenye  shauku na muziki.  Harakati zake za kimuziki  zilianza kwa kuandika nyimbo na kufanya kazi kwenye bendi  akiwa kidato cha tano na sita.
  Mwaka  2014, Sami Dan aliunda bendi ya  Zewd  nyimbo zake kama ‘Fikir Selam’ au ‘Love, Peace’  huburudisha mashabiki wake  kwa ujumbe wa amani na umoja.

  Tamasha la  Sauti za Busara lilitajwa na CNN kuwa ni kati ya matamasha 7 ya muziki  Afrika ya kutazamwa litafanyika tarehe 9-12 February Ngome Kongwe Zanzibar.

  0 0


  Imeelezwa kuwa teknolojia duni,rasilimali fedha,malighafi kuwa juu, uhaba wa mvua unaotokana na uharibifu wa mazingira ndio changamoto kubwa inayomkabili mkulima wa Tanzania kutofikia malengo ya kufanya kilimo biashara.


  Mkuu wa wilaya ya Arusha Fabian Daqarro akiongea kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gamba wakati wa kufungua maonyesho ya kilimo –Selian Arusha.


  ARUSHA.

  Hayo yamebainishwa na mkuu na mkoa wa Arusha Mrisho Gambo aliyewakilishwa na Mkuu wa Wilaya ya Arusha Fabian Daqarro kwenye Maonyesho ya zana za kilimo yanayojulikana AGRItech EXPRO TANZANIA yamefunguliwa jijini Arusha ikiwa ni mara ya kwanza kufanyika jijini hapo katika viwanja vya Taasisi ya Utafiti wa kilimo ya Seliani iliyopo mkoani hapa na kushirikisha wadau mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi.
  Wageni rasmi waliofika wakati wa ufunguzi wa maonyesho yanayojulikana kwa jina AGRItech EXPRO 2017 TANZANIA, kutoka kulia ni Daniel Loiruck –Afisa kilimo wa mkoa Arusha, Eric Ng’amaryo –Mwenyekiti TAHA Taifa, Fabian Daqarro –Mkuu wa wilaya ya Arusha, Dr, January Mafuru –Mkurugenzi utafiti wa kilimo kanda ya kasikazini (Sari)
  Mshauri wa mambo ya uchumi kutoka wizara ya kilimo na chakula Profesa Aden Nyange akiongea wakati wa ufunguzi wa maonyesho ya kilimo AGRItech.
  Baadhi ya wadau wa kilimo na wataalam ambao wamehudhulia ufunguzi wakisikiliza kwa makini mkuu wa wilaya alipokuwa akitoa hotuba ya ufunguzi.

  Alan Edwards meneja masoko kanda ya Afrika akitoa maelekezo kwa mkuu wa wilaya ya Arusha Fabian alipotembelea banda lao mapema leo.

  Mkuu wa wilaya ya Arusha Fabian Daqarro kushoto akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi mtendaji wa kampuni tanzu ya kilimo PASS huku meneja usimamizi maarifa na mawasiliano wa AMDT Al-amani Mutarubukwa akisikiliza akiwa kashika kifaa kimoja kinachohusika katika kilimo.
  Meneja wa masoko wa kampuni ya GSI Group ya Afrika kusini akimpa maelezo mkuu wa wilaya ya Arusha jinsi kampuni yao inavyozalisha vyakula vyenye uwezo wa kumfanya kuku kufikia uzito wa kilo 5!

  Mashine saidizi ya kubebea mizigo ambayo imetengenezwa na kampani ya BUV Tanzania, Scott Price aliyekaa juu ya pikipiki hiyo anamuonyesha mkuu wa wilaya (kulia) jinsi inavyofanya kazi.
  Mkuu wa wilaya ya Arusha pia alipata nafasi kutembelea banda linaloonyesha uzalishaji wa nyanya, hapa Butwa Godluck meneja masoko na mauzo akitoa maelezo.


  HABARI KWA UNDANI..


  Hayo yamebainishwa na mkuu na mkoa wa Arusha Mrisho Gambo aliyewakilishwa na Mkuu wa Wilaya ya Arusha Fabian Daqarro kwenye Maonyesho ya zana za kilimo yanayojulikana AGRItech EXPRO TANZANIA yamefunguliwa jijini Arusha ikiwa ni mara ya kwanza kufanyika jijini hapo katika viwanja vya Taasisi ya Utafiti wa kilimo ya Seliani iliyopo mkoani hapa na kushirikisha wadau mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi.

  Vilevile amesema kuwa serikali inawashukuru wadau kwa kuupa mkoa wa Arusha heshima ya kufanyika kwa maonyesho hayo ambayo yanafanyika kwa siku mbili, hivyo amewataka wananchi wajitokeze kwa wingi kujifunza teknolojia mpya za kilimo na ubunifu wa wataalamu mbalimbali, ukaowasidia kuendesha kilimo chenye tija.

  “serikali kwa kushirikiana na wadau wa kilimo wanaangalia ni kwa namna gani wataweza kuboresha sekta hii ya kilimo kwa kutoa elimu mbalimbali kwa wakulima ili kuepukana na kilimo duni ambacho kinasababisha hasara kwa wakulima nchini”, Amesema Fabian Daqarro.

  Amewataka wadau hao wa maonyesho hayo ya kilimo kuangalia namna bei za pembejeo za kilimo, kwani inaonyesha asilimia kati ya 75-80 ni ya wakulima wadogo wadogo hivyo ni vyema wakauza bidhaa zao kwa bei nafuu ili mkulima wa hali ya chini aweze kumudu kununua pembejeo hizo ili waweze kuendana na kasi ya kilimo cha kisasa.

  Kwa upande wake mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti ya Seliani amesema kuwa wamekua wakishirikiana na wadau mbalimbali wa kilimo, katika uzalishaji wa Teknolojia ,pamoja na kuwatafutia wadau wa kilimo masoko ya mazao yao.

  “Sisi Seliani tupo tayari kuwaunganisha wakulima na waonyeshaji wa teknologi taongezeka pamoja na wakulima watafahamu namna ya kuhifadhi mazao yao baada ya uvunaji ili wa mazao” amesema Dr. Mafuru.

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Singida Dr Rehema Nchimbi (wa pili kutoka kushoto) akishiriki kupalilia zao la mtama Mtama katika ziara aliyoifanya Mkoani humo.
   Mkuu wa Mkoa wa Singida Dr Rehema Nchimbi akishiriki kupanda Mihogo katika ziara aliyoifanya Mkoani humo.

   Mkuu wa Mkoa wa Singida Dr Rehema Nchimbi (wapili kutoka kulia) akishiriki kikamilifu katika shughuli za kilimo katika ziara aliyoifanya Mkoani humo.

  Mkoa wa Singida Dr Rehema Nchimbi akishiriki chakula cha mchana baada ya kukaribishwa na wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Mwenge Singida katika ziara aliyoifanya Mkoani humo.


  Na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Singida.

  Viongozi, Watendaji na Watumishi wa Halmashauri zote za Mkoa wa Singida wametakiwa kuhakikisha taarifa zote za mapato na matumizi zinawafikia wananchi wote katika ngazi ya Kata na Kijiji ili waweze kuelewa hasa kiasi cha fedha zilizoingizwa na Serikali katika Halmashauri na namna zinavyo tumika.

  Agizo hili limetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi katika ziara yake ya kuzitembelea Halmashauri zote za Mkoa huo kwa lengo la kujenga Uelewa wa pamoja, utumishi wa pamoja, na kasi ya pamoja ili kufikia lengo pamoja kwa maslai  mapana ya Taifa.

  Kwa upande wa Wakuu wa Idara na Vitengo Dkt Nchimbi amewaagiza wawe na taarifa za kila siku za watendaji na watumishi katika mnyororo wote wa kiutendaji na kiuongozi na kuepuka kutegemea taarifa za makaratasi na ili kuimrisha utendaji wa kuzingatia matokeo yanayo onekana.

  Niaibu sana kwa Mganga Mkuu wa Wiwala (DM) kushindwa kutoa takwimu pale unapo ulizwa swali nje ya ofisi yako juu ya idadi ya watoto waliozaliwa ndani ya siku tatu katika wilaya yako au Afisa Elimu wa Halamashari unashindwa kutoa jibu la ni Walimu wangapi katika Halmashauri yako hawakuingia kazini kwa sabau za kiafya. Sinto penda hali hii iendelee kujitokeza katika Mkoa wa Singida. Aliongeza Dkt Nchimbi.


  Mh Dkt Nchimbi pia amewataka Watumishi wa umma Mkoani Singida kuzinduka usingizini na kuacha kufikiri kuwa bado wapo katika kipindi cha uchaguzi na kuendekeza siasa badala ya kufanya kazi ya kuwatumikia wanchi kwa uaminifu na uadilifu kama inavyo taka serikali ya hawamu ya tano ya Tanzania chini ya Rais Dkt John Joseph  Pombe Magufuli.

  Sinto mvumilia mtumishi yeyote wa umma ndani ya Mkoa wangu wa Singida atakae shindwa kwendana na kasi ya Serikali ya hawamu hii ya Tano, sitaki kuendelea kusikia msamiati wa Chini ya Kiwango katika Ujenzi na wale wote watakao husika na ujenzi wa chini ya kiwango watakamatwa na kulazimika kulipa thamani ya fedha zote zilizotumika katika ujenzi huo, watumishi wa Umma ni lazima watambue kuwa wafanyapo kazi waweke mbele maslai ya umma kwanza yaana wananchi kwanza. Alisema Mh Dkt Nchimbi.


  Katika suala la usalama wa Chakula Mh Dkt Nchimbi amelitaja kuwa ni wajibu wa kila mmoja hivyo ni lazima Viongozi, Watendaji, Watumishi wa Halmashauri na Wananchi kwa Ujumla wawajibike kwa pamoja kuhakikisha kuna usalama wa chakula hasa kwa kulima Mazao yanayo tumia maji kwa ufanisi kama vile Mihogo, Mtama naViazi lishe.

   

   
  Dkt Nchimbi amesisitiza kuwa viongozi na watendaji wote walime mashamba yasio pungua nusu heka ya kilimo cha  mihogo, viazi lishe, mtama, Watumishi wa halmashauri zote wawe na mizinga isiyo pungua miwili ya ufugaji nyuki na kila shule iwe na heka moja au zaidi ya Mihogo, viazi lishe au Mtama, pia ziwe na nusu heka au zaidi ya mazao hayo kwaajili ya walimu.

  Ili kutatua changamoto ya upungufu wa makazi ya watumishi wa Umma katika Mkoa wa Singida Mh Mkuu wa Mkoa Dkt Nchimbi ameziagiza  Halmashauri zote za mkoa huo kuwapatia watumishi hasa walimu viwanja vya kujenga nyumba za makazi kwa utaratibu ambao ni rafiki na mishahara yao na licha ya kutatua changamoto ya makazi kwa watumishi pia utaratibu huo utasaida ustaafu mwema kwa watumishi wa Halmashauri hizo.

   Katika ziara hiyo Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi amezindua shughuli mbali mbali za kilimo zenye kuzingatia mazao yanayo tumia maji kwa ufanisi kama vile Mihogo, Mtama naViazi lishe na pia amezindua Huduma maalum ya Afya katika Halamashuri ya Mkoa huo


older | 1 | .... | 1116 | 1117 | (Page 1118) | 1119 | 1120 | .... | 1897 | newer