Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1115 | 1116 | (Page 1117) | 1118 | 1119 | .... | 1897 | newer

  0 0

   
  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali itahakikisha inawasaka watu wote waliohusika na upotevu wa mali za kiwanda cha chai cha Lupembe na kuwachukulia hatua.

  Hata hivyo amesema Serikali haitoipa nafasi migogoro yote ya uwekezaji inayopelekea wananchi kutopata ajira bali itatatuliwa bila ya kusimamisha uzalishali.

  Pia amewataka wawekezaji mbalimbali waliomilikishwa viwanda wahakikishe wanafuata kanuni na sheria ili kufikia malengo yaliyokusudiwa na wananchi waweze kupata tija.

  Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Jumatano, Januari 25, 2017) wakati alipotembelea kiwanda cha chai cha Lupembe akiwa katika ziara yake ya kikazi mkoani Njombe.

  Mali za kiwanda hicho vikiwemo vipuli na vyombo vya usafiri yakiwemo maroli na magari madogo 17 vilipotea baada ya Ushirika wa wakulima wa chai Muvyulu kuvamia kiwanda.

  Kiwanda hicho kinakabiliwa na mgogoro kati ya muwekezaji wa kiwanda hicho Lupembe Tea Estate na Ushirika wa wakulima wa chai Muvyulu ambao ameahidi kuitafutia ufumbuzi.

  “Migogoro yote inayopelekea watu kutopata ajira haitapewa nafasi. Tutaisikiliza na kuipatia ufumbuzi bila ya kusimamisha uzalishaji,”.

  “Ushirika nchini uliyumba na umekuwa ukiharibiwa na waliopewa dhamana na ndiyo sababu tuliamua kuufumua uongozi kuanzia juu na tutashuka hadi chini,” amesema.

  Waziri Mkuu amesema Serikali itaendelea kufuatilia viongozi wa vyama vya ushirika na wenye uwezo wa kuviendesha wataendelea na wasioweza wataondolewa.

  Amesema Serikali itayafanyia kazi maelezo yote yaliyotolewa na uongozi wa kiwanda hicho pamoja na ya wanaushirika na kisha itayatolea ufafanuzi wakati kiwanda kikiendelea na kazi.

  Waziri Mkuu amesema Serikali itahakikisha mwenye haki anapata haki yake na haitakubali kuona kiwanda hicho kikisimamisha uzalishaji. Pia inafuatilia muwekezaji huyo alipataje kiwanda.

  “Lupembe ni miongoni mwa viwanda ambavyo vilikufa na sasa kimeanza uzalishaji hatutakubali kife kutokana na migogoro ya wanaushirika na muwekezaji. Kiwanda hakitasimama ng’o,”.

  “Hatuwezi kukubali migogoro iendelee kwani haina tija inaumiza wananchi. Najua ushirika ni wa wakulima tunataka uwe imara hatutaki ushirika wenye mizengwe mizengwe,” amesema.

  Katika hatua nyingine Waziri Mkuu amemtaka Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kuja na kufanya uchunguzi wa kiwanda hicho.

  Amesema Serikali imedhamiria kuwaletea wananchi maendeleo na haitamvumilia mtu atakayevuruga uendeshaji wa viwanda. “ Tunataka viwanda vifanye kazi”

  Waziri Mkuu amesema Serikali imedhamiria kupiga hatua kiuchumi kutoka katika uchumi wa chini hadi wa kati kwa kupitia sekta ya viwanda.

  Awali Waziri Mkuu alipokea taarifa ya kiwanda hicho kutoka kwa muwekezaji pamoja na taarifa ya uongozi wa Ushirika wa wakulima wa chai Muvyulu ambao ameahidi kuitafutia ufumbuzi.

  Waziri Mkuu leo ameendelea na ziara yake mkoani Njombe baada ya kuikatiza Januari 22 mwaka huu na kwenda mkoani Dar Es Salaam kwa shughuli za kikazi.

  IMETOLEWA NA:

  OFISI YA WAZIRI MKUU,

  JUMATANO, JANUARI 25, 2017.

  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akihutubia mamia ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam wakati wa hafla ya uzinduzi wa Miundombinu na Huduma za mabasi yaendayo haraka Dar es Salaam, awamu ya kwanza leo jijini Dar es Salaam.
  KOPA 2
   Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akifafanua jambo wakati wa hafla ya uzinduzi wa Miundombinu na Huduma za Mabasi yaendayo haraka Dar es Salaam, awamu ya kwanza leo jijini Dar es Salaam.
  KOPA 3
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais _TAMISEMI George Boniphace Simbachawene akizungumza jambo wakati wa hafla ya uzinduzi wa Miundombinu na Huduma za Mabasi yaendayo haraka Dar es Salaam, awamu ya kwanza leo jijini Dar es Salaam.
  KOPA 4
  Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika Makthar Diop akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Miundombinu na Huduma za Mabasi yaendayo haraka Dar es Salaam, awamu ya kwanza leo jijini Dar es Salaam.
  KOPA 5
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Miundombinu na Huduma za Mabasi yaendayo haraka Dar es Salaam, awamu ya kwanza leo jijini Dar es Salaam.
  KOPA 6
   Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Joseph Nyamhanga aakimtambulisha Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Augustine Mahiga(aliyesimama) wakati wa hafla ya uzinduzi wa Miundombinu na Huduma za Mabasi yaendayo haraka Dar es Salaam, awamu ya kwanza leo jijini Dar es Salaam.
  KOPA 7
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiwaongoza viongozi na wananchi wa Dar es Salaam kuimba wimbo wa taifa wakati wa hafla ya uzinduzi Miundombinu na Huduma za Mabasi yaendayo haraka jijini Dar es Salaam leo. Kutoka kulia ni Mbunge wa Ilala Mussa Zungu, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam Ramadhan Madabida,Waziri wa OR – TAMISEMI George Simbachawene, Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika Makthar Diop, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, Waziri wa Mambo ya Nje Balozi Augustine Mahiga na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda.
  KOPA 8
   Baadhi ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam wakifuatilia hotuba mbalimbali za viongozi wakati wa hafla ya uzinduzi wa Miundombinu na Huduma za Mabasi yaendayo Haraka awamu ya kwanza leo jijini Dar es Salaam.
  KOPA 10
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akitazama jiwe la msingi mara baada ya kuzindua rasmi Miundombinu na Huduma za Mabasi yaendayo Haraka awamu ya kwanza leo jijini Dar es Salaam.Kutoka kulia kwa Rais ni Waziri wa Nchi OR – TAMISEMI George Simbachawene na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa.
  KOPA 11
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli (wa pili kulia), akiwa na Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhandisi Mussa Iyombe (katikati) na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika Makthar Diop wakimwagilia maji mti uliopandwa kama kumbukumbu za uzinduzi wa Miundombinu na Huduma za mabasi yaendayo haraka Dar es Salaam, awamu ya kwanza leo jijini Dar es Salaam.
  KOPA 12
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akipeana mkono na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika Makthar Diop wakati wa hafla ya uzinduzi wa Miundombinu na Huduma za mabasi yaendayo haraka Dar es Salaam, awamu ya kwanza leo jijini Dar es Salaam.
  AWU 11
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akieenda kumtumza msaani wa muziki Mrisho Mpoto na Banana Zoro   wakati wa hafla ya uzinduzi wa  Miundombinu na Huduma za mabasi yaendayo haraka jijini Dar es Salaam leo. Uzinduzi huo umefanyika katika kituo cha mabasi yaendayo haraka cha Gerezani Kariakoo amba Mpoto na Banana waklitumbuiza wimbo wao unaohamasisha wananchi kufanya kazi hali iliyomvutia Rais Magufuli.
  KOPA 15
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiwa katika picha na baadhi ya viongozi wa kiserikali na siasa wakati wa hafla ya uzinduzi wa Miundombinu na Huduma za mabasi yaendayo haraka, awamu ya kwanza leo jijini Dar es Salaam.Aliyemshikana naye mkono ni Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita.
  KOPA 17
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiendesha Basi la Mwendokasi mara baada ya kuzindua Miundombinu na Huduma za Mabasi yaendayo Haraka, awamu ya kwanza leo jijini Dar es Salaam.
  KOPA 18
  Baadhi ya wanacnhi wakiwa katita mageti ya kuingilia katika Kituo cha Mabsi yaendayo haraka cha Gerezani Kariakoo walipokuwa wakimshuhudia Rais Magufuli akiendesha Basi kama ishara ya kuzindua Miundombinu na Huduma za Mabasi yaendayo Haraka leo jijini Dar es Salaam.
  KOPA
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiwasili katika kituo cha mabasi yaendayo haraka Kariakoo Gerezani alipoenda kuzindua Miundombinu na Huduma za mabasi yaendayo haraka jijini Dar es Salaam leo.Kulia ni Makamu wa Rais wa Benki ya Diunia kwa Ukanda wa Afrika  Maktahar Diop

  Picha zote na Frank Shija – MAELEZO.

  0 0

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa kiwanda cha chai cha Lupembe, Mussa Kefa (kushoto kwake) wakati alipotembelea kiwanda hicho akiwa katika ziara ya mkoa wa Njombe Januari 25, 2017.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na aliyewahi kuwa Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo wakati alipowasili kwenye kiwanda cha chai cha Lupembe kukagua kiwanda na kuzungumza na wafanyakazi akiwa katika ziara ya mkoa wa Njombe Januari 25, 2017.

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wafanyakazi wa kiwanda cha chai cha Lupembe akiwa katika ziara ya mkoa wa Njombe Januari 25, 2017.


  Wasanii kutoka kijiji cha Kanitelele mkoani Njombe wakicheza ngoma ya Limdoya wakati Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipowasili kwenye kiwanda cha chai cha Lupembe kukagua kiwanda na kuzungumza na wanyakazi Januari 25, 2017.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama ngoma kutoka kijiji cha Kanitelele mkoani Njombe ikicheza ngoma ya Limdoya wakati alipowasili kwenye kiwanda cha chai cha Lupembe akiwa katika ziara ya mkoa wa Njombe Januari 25, 2017. Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Christopher Ole Sendeka.

  0 0

   Madaktari Bingwa wa Moyo wa  Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na Madaktari Afrika wa nchini Marekani wakitoa huduma kwa mgonjwa ya kuzibua mshipa wa moyo uliokuwa umeziba  bila ya kupasua kifua (Catheterization). Kulia ni Dkt. Peter Kisenge, akifuatiwa na Dkt. Peter O’brien na kushoto ni Afisa Muuguzi Ayoub Mchau.
   Daktari Bingwa wa Moyo kutoka Madaktari Afrika wa nchini Marekani Dkt. Peter O’brien na Afisa Muuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Ayoub Mchau wakitoa huduma kwa mgonjwa ya kuzibua mshipa wa moyo uliokuwa umeziba  bila ya kupasua kifua (Catheterization).
   Madaktari Bingwa wa Moyo wa  Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na Madaktari Afrika wa nchini Marekani wakiendelea na kazi ya kutoa  huduma kwa mgonjwa ya kuzibua mshipa wa moyo uliokuwa umeziba  bila ya kupasua kifua (Catheterization).
  Madaktari Bingwa wa Moyo wa  Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na Madaktari Afrika wa nchini Marekani wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumalizi kutoa  huduma kwa mgonjwa ya kuzibua mshipa wa moyo uliokuwa umeziba  bila ya kupasua kifua (Catheterization). Picha na Anna Nkinda – JKCI

  0 0

  BEN MWAIPAJA -WFM
   BENKI ya Dunia imekubali kuikopesha Tanzania fedha kwaajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo ukiwemo mkopo wa Dola Milioni 350 kwa ajili ya Mradi wa Upanuzi wa Bandari ya Dar es salam.
  Waziri wa Fedha na Mipango, Dokta Philip Mpango, amewaambia waandishi wa Habari mara baada ya kumalizika kwa Mazungumzo kati yake na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anaye shughulikia Kanda ya Afrika, Mhe. Makhtar Diop, Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es salaam.
  Amesema kuwa kukamilika kwa upanuzi wa Babdari hiyo kutasaidia kuongeza ubora wa huduma zinazotolewa na Bandari hiyo hatua itakayo chochea ukuaji wa  uchumi wa nchi.
  Kwa upande wake Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayeshughulikia Kanda ya Afrika Mhe. Makhtar Diop, amesema kuwa Benki yake imefurahishwa na hatua zinazochukuliwa na Serikali ya awamu ya tano katika kukuza uchumi na kwamba Benki hiyo itaendelea kushirikiana na serikali kuhakikisha kuwa malengo yaliyokusudiwa yana fikiwa kwa haraka
  Ameishauri Serikali kuongeza ushirikiano kati yake na Sekta Binafsi katika kuchochea  biashara na uwekezaji pamoja na kutupia jicho sekta ya kilimo kwa kuboresha uzalishaji wa mazao ya kilimo na mifugo pamoja na kuongeza thamani ya mazao hayo ili kuwawezesha wananchi wengi zaidi kuondokana na umasikini na kuchochea uwekezaji katika sekta hiyo

  0 0

   Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi, Humphrey Polepole, leo amefanya ziara ya kikazi katika Vyombo vitatu vya Habari vya Kampuni za Uhuru Publications Ltd, Wachapishajiwa Magazeti ya Uhuru,Mzalendo na Burudani, Peoples Media ya Uhuru FM na New Habari Corporation, Wachapishaji wa Magazeti ya Mtanzania, Rai na Dimba. Pichani, Polepole akizungumza na Wafanyakazi na viongozi wa kampuni ya Uhuru Publications Ltd, wakati wa ziara hiyo.
   Polepole akiingia katika Ofisi za Uhuru Publications Ltd, zilizopo Mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam, leo. Kulia ni Kaimu Katibu Msaidizi Mkuu wa Idara ya Itikadi na Uenezi, Gabriel Athuman
   Polepole akimsalimia Suleiman Jongo alipokuwa akisalimia wafanyakazi wa Uhuru Publications Ltd, baada ya kuwasili kwenye Ofisi za Kampuni hiyo leo
   Polepole akimsalimia Grace alipokuwa akisalimia wafanyakazi wa Uhuru Publications Ltd, baada ya kuwasili kwenye Ofisi za Kampuni hiyo leo
   Polepole akimsalimia mmoja wa wafanyakazi wa Uhuru Publications Ltd, baada ya kuwasili kwenye Ofisi za Kampuni hiyo leo
   Kaimu Mhariri Mtendaji wa Uhuru Publications Ltd, Ramadhani Mkoma (kushoto) akimtambulisha baadhi ya Viongozi wa UPL kwa Polepole
   Polepole akifafanua jambo alipokuwa akizungumza Ofisi kwa Kaimu Mhariri Mtendaji wa UPL 
   Polepole (kulia) akizungumza na Kaimu Mhariri Mtendaji Ramadhani Mkoma (kushoto) alipokuwa katika ziara hiyo leo
   Wafanyakazi wa UPL wakisimama kumlaki Polepole alipoingia kwenye chumbacha habari ili uzungumza nao
   Katibu wa NEC, Itkadi na Uenezi Polepole akizungumza na wafanyakazi wa UPL leo
  UHURU FM
   Katibu wa NEC Itkadi na Uenezi, Humphrey Polepole akipanda ngazi kuingia katika Ofisi za Uhuru FM leo
   Kaimu Mkurugenzi wa Uhuru FM, Angel Akilimali akimpa Polepole kitabu cha wageni ili asaini
   Akilimali akitoa maelezo machache kumkaribisha Polepole
   Akilimali akimkabidhi Polepole taarifa kuhusu Uhuru FM
   Baadhi ya Maofisa Kutoka Makao Makuu ya CCM, na wafanyakazi wa Uhuru FM wakiwa katika Ofisi ya Akilimali
   Polepole akiwa tayari kuzungumza na Wafanyakazi wa Uhuru FM
   Akilimali akitambulisha ugeni wa Polepole kwa wafanyakazi wa Uhuru FM
   Polepole akizungumza na wafanyakazi wa Uhuru FM
   Wafanyakazi wa Uhuru FM wakimskiliza Polepole
   Wafanyakazi wa Uhuru FM wakimsikiliza Polepole
  NEW HABARI CORPORATION 
   Mhariti Mtendaji wa New Habari Corporation Absalom Kibanda akimkaribisha Polepole katika Ofisi za Kampuni hiyo, Sinza jijini Dar es Salaam
   Polepole akimsalimia Msanifu wa Habari wa kampuni hiyo, Hamis Mkotya
   Polepole akimsalimia Mwandishi wa siku nyingi Mzee Makaranga
   Polepole akizungumza na wafanyakazi na viongozi wa New Habari Corporation
   Baadhi ya wafanyakazi wa New Habari Corporation wakiwa wamesimama kumshuhudia Polepole 
   Polepole akiondoka katika Chumba cha Habari cha New Habari Corporation
   Polepole akimsalimia Mhariri Mkuu wa gazeti la Mtanzania
   Kibanda akizungumza na Polepole  katika Ofisi za New Habari Corporation
   Deus Mhagale na mfanyakazi mwenzake wakimfurahia mpigapicha aliyefuatana na Polepole 
  Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Humphrey Polepole akifafanua jambo katika mazungumzo na Mhariri Mtendaji wa New Habari Corporation Absalom Kibanda. Picha zote na Bashir Nkoromo)

  0 0


  Kaimu Meneja Mwandamizi udhibiti mifumo ya umeme TANESCO makao makuu, Mhandisi Abubakar Issa,(katikati), akionyesha kifaa kilicholipika (female connector), cha umeme wa 132kv kutoka Ubungo kwenda Chalinze. Kulia ni KaimunMeneja Uhusiano, Bi. Leila Muhaji na kushoto ni mwangalkizi mkuu wa kituo cha kupoza umeme cha Ubungo jijini Dar es Salaam, Bw,Deodatus Ngwanda

  NA K-VIS BLOG/Khalfan Said

  SHIRIKA la Umeme Tanzania, (TANESCO), limeeleza chanzo cha kukatika umeme leo Januari 25, 2017), ni kulipuka kwa kikata umeme,(Circuit breaker), baada ya kifaa kijulikanacho kama female connector ya umeme wa 132kv kutoka kituo cha kupoza umeme cha Ubungo jijini Dar es Salaam kwenda Chalinze mkoani Pwani kupata hitilafu.

  Kwa mujibu wa Kaimu Meneja Mwandamizi udhibiti mifumo ya umeme TANESCO makao makuu, Mhandisi Abubakar Issa,(pichani juu), alisema hitilafu hiyo iliyotokea majira ya saa 12;32 asubuhi, leo Januari 25, 2017  ilileta athari kwenye mfumo mzima wa gridi ya taifa na kufanya wateja wa TANESCO walio kwenye mikoa inayotumia gridi ya taifa kukosa umeme kwa takriban masaa mawili.
  "Napenda kuwahakikishia wateja wetu kuwa gridi ya taifa iko salama, hakuna tatizo lolote isipokuwa ilizima baada ya kikata umeme hicho kulipuka, lakini sasa mambo yamewekwa sawa na umeme unazidi kurejea katika hali yake ya kawaida kote nchini" alisema Mhandisi Issa, wakati waandishi wa habari walipopelekwa kujionea wenyewe hitilafu hiyo majira ya mchana leo.   Hata hivyo alisema kifaa kilichoharibika kinasafirishwa kutoka mkoani Tanga, na mara kitakapowasili kitafungwa mahala kilipoharibika kile cha awali.
   Hii ndiyo kikata umeme (Circuit breaker) iliyolipuka
   Female Connector inayotoa umeme hapo ubunge kupeleka Chalinze mkoani Pwani ambayo ililipuka
   Female connector (juu katikati) iliyolipuka
   Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO makao makuu, Bi Leila Muhaji, akiwa na baadhi ya waandshi wa habari waliotembelea eneo hilo leo mchana Januari 25, 2017

  0 0


  0 0

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira akipewa maelezo na Meneja Uzalishaji wa Kiwanda cha Urafiki kilichopo jijini Dar es Salaam Thomas Mushi,   juu ya bidhaa zinazozalishwa na Kiwanda hicho alipofanya ziara ya kikazi akiwa ameambatana na maofisa wa majeshi yaliyo chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ili kujionea ubora wa bidhaa zinazozalishwa  viwandani  humo kwa  kuwa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi inategemea kuanza kuagiza vitambaa vya sare za Majeshi yake kutoka viwanda vilivyopo nchini hapa.
  URAFI 2
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira akioneshwa hatua za awali za namna pamba inavyoandaliwa katika Kiwanda cha Urafiki kilichopo jijini Dar es Salaam kabla ya kutengeneza bidhaa. Katibu Mkuu huyo alitembelea kiwanda hicho akiambatana na baadhi ya maofisa wa majeshi yaliyopo chini ya wizara yake (hawapo pichani) ili kujionea ubora wa bidhaa zinazozalishwa kiwandani humo.

  URAFI 3
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira akioneshwa jinsi mitambo iliyopo katika kiwanda cha Urafiki inavyofanya kazi katika uzalishaji wa bidhaa zinazotoka kiwandani hapo na Salum Dailuga ambaye ni Meneja utiaji rangi na uchapishaji wa bidhaa. Wa kwanza kulia ni Kamanda wa Polisi Kamishna Msaidizi wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Ilala Hamdan   Salum aliyeambatana na Katibu Mkuu huyo kwenye ziara hiyo iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
  URAFI 4
  Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira pamoja na Maofisa mbalimbali wa majeshi yaliyopo chini ya wizara hiyo wakitazama khanga iliyozalishwa kiwanda cha Urafiki wakati alipotembelea kiwanda hicho ili kujionea ubora wa bidhaa zao.
  URAFI 5
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira akioneshwa malighafi iliyopo katika hatua za mwishoni kabla ya kwenda kutengenezwa mashuka katika  kiwanda cha NIDA Textile MILLS (T) LTD, kilichopo Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam ambako alitembelea leo pamoja na baadhi ya maofisa wa majeshi yaliyopo chini ya Wizara hiyo, kwa lengo la kujionea ubora wa bidhaa zinazozalishwa viwandani humo.
  URAFI 6
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira akiangalia mfano wa vitambaa vinavyozalishwa na kiwanda cha NIDA Textile MILLS (T) LTD kilichopo maeneo ya Tabata jijini Dar es Salaam ambako alitembelea leo pamoja na baadhi ya maofisa wa majeshi yaliyopo chini ya Wizara hiyo, kwa lengo la kujionea ubora wa bidhaa zao.
  URAFI 7
  Baadhi ya maofisa wa Majeshi yaliyo chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi waliokuwa wameambata na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (Hayupo pichani), wakiwa na sampuli zao za vitambaa vya sare zao.
  URAFI
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira akielekea katika maeneo ambayo Kiwanda cha Urafiki kilichopo jijini Dar es Salaama kinazalisha bidhaa zake. Katibu Mkuu huyo alitembelea kiwanda hicho leo akiwa na baadhi ya maofisa wa majeshi yalipo chini ya wizara yake kwa ajili ya kuangalia ubora wa bidhaa zinazozalishwa viwandani  humo.Mwenye suti nyeusi ni Shedrack Mkelebe ambaye ni Naibu  Meneja Mkuu wa kiwanda hicho. Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi inategemea kuanza kuagiza vitambaa vya sare za Majeshi yake kutoka viwanda vilivyopo hapa nchini.

  ……………
  Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira amefanya ziara katika Viwanda vya NIDA na Urafiki vinavyotengeneza nguo vilivyopo jijini Dar es Salaam. Lengo la ziara hii ni kuangalia ubora wa bidhaa zinazozalishwa viwandani humo kwa kuwa Wizara inategemea kuanza kuagiza vitambaa vya sare za Majeshi yaliyopo ndani ya  wizara hii kutoka viwanda vilivyopo hapa nchini.
  Katika ziara hii Meja Jenerali Rwegarisa  aliambatana na baadhi ya maofisa wa majeshi yaliyopo chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi wakiwa na sampuli za aina za vitambaa wanavyohitaji kwa ajili ya sare za majeshi yaliyoko chini ya wizara hii.
  Uamuzi wa Ofisi ya Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi  kuwafuata watengenezaji moja kwa moja na hivyo kuacha kutumia wazabuni kutapunguza gharama zilizokuwa zikiongezwa na mtu wa kati. Mbali ya Viwanda alivyotembelea bado atatembelea viwanda vingine vilivyopo mikoani kama vile Arusha, Mwanza na Morogoro.
  Aidha viwanda vya ndani vitainuliwa kwa kuviunga mkono kwani bidhaa zinazozalishwa na viwanda vya ndani zina ubora mzuri hivyo kuzifanya  hata nchi za jirani mfano Kenya na Zambia kuendelea kuagiza bidhaa kutoka viwanda vya hapa nchini.
  Hata hivyo, viwanda vya ndani vya kutengeneza nguo vinaweza kupewa zabuni bila upendeleo wowote kitakachoangaliwa ni ubora wa bidhaa zinazozalishwa kama zinakidhi mahitaji ya sare za majeshi yaliyopo chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
  Imetolewa na
  Christina R. Mwangosi
  Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali
  Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

  0 0

  Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), akiagana na Mgeni wake, Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayeshughulikia Kanda ya Afrika, Bw. Makhtar Diop, mara baada ya kumalizika kwamazungumzo kati yao, ambapo Benki hiyo imeahidi kuendelea kushirikiana na Tanzania kwa kuipatia Mikopo yenye mashari Nafuu kwaajili ya miradi mbalimbali ya kiuchumi na kijamii.
  Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) (wa Pili kutoka kulia) akisisitiza jambo wakati wa alipokutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayeshughulikia ukanda wa Afrika Bw. Makhtar Diop, makao makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar salaam.
  Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayeshughulikia Kanda ya Afrika, Bw. Makhtar Diop, (wa nne kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Watendaji wa Wizara na Taasisi zake baada ya kumalizika kwa mazungumzo kati yake na mwenyeji wake, Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), Makao Makuu ya Wizara hiyo, Jijini Dar es salaam.
   
  Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayeshughulikia Kanda ya Afrika, Bw. Makhtar Diop, akisaini kitabu cha wageni katika ofisi ya Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (Mb), walipokutana kwaajili ya mazungumzo Makao makuu ya Wizara hiyo, Jijini Dar es salaam. Wanao shuhudia ni Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia anaye hudumia nchi za Tanzania, Malawi, Burundi, Bella Bird na Msaidizi wa Waziri wa Fedha na Mipango, Bw. Edwin Makamba (aliyesimama).
  Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) (Kushoto) akizungumza na mgeni wake, Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayeshughulikia kanda yas Afrika, Bw, Makhtar Diop, (wa kwanza kulia) pamoja na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia anaye hudumia nchi za Tanzania, Malawi, Burundi, Bella Bird, na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James.
  Ujumbe wa Tanzania na Benki ya Dunia, ukiwa katika kikao kilichojadili masuala mbalimbali yanayogusa Serikali na Benki hiyo, wakiongozwa na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayeshughulikia Kanda ya Afrika, Bw. Makhtar Diop, pamoja na Mwenyeji wake, Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (Mb), Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango,Jijini Dar es salaam
  Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), (Wa Pili kulia), akisisitiza jambo wakati wa mkutano wake na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayeshughulikia Kanda ya Afrika, Bw. Makhtar Diop, Makao makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es salaam.
  Baadhi ya Watendaji wakuu wa Serikali kutoka Wizara ya Fedha na Mipango na Benki Kuu ya Tanzania (BOT) wakiwa katika Mkutano kati ya Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (Mb) na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayeshughulikia Kanda ya Afrika, Bw. Makhtar Diop ( hawapo Pichani), Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es salaam.(Picha na Kitengo cha cha Mawasiliano Serikalini-WFM)


  0 0


  Na Humphrey Shao, G lobu ya Jamii

  Msanii wa muziki wa kughani, Mrisho Mpoto amemuinua Rais Dk John Pombe Magufuli mara baada ya kuimba mashairi yenye mvuto na kutoa hamasa kwa watanzania kujenga nchi na kufanya kazi katika serikali hii ya awamu ya tano.

  Mpoto ambaye leo alikuwa mmoja wa watumbuizaji katika shughuli ya uzinduzi wa mradi wa mabasi yaendayo haraka jijini Dar es Salaam na kuimba mashairi ambayo yaliweza kuwafurahisha watanzania na Rais John Pombe Magufuli na kuamua kuinuka kwenye kiti na kwenda kumpongeza wakati akiimba.

  Mara mpoto alipoanza kuimba aliweza kuinua baadhi ya viongozi na kwenda kumtunza na wadau mbalimbali na hatimae kupitia ushiri huo ambao ulimfurahisha Rais Dk John Pombe Magufuli na ujumbe wake wote na kunyanyuka kwenye kiti na kuamua kwenda kumpongeza

  Wimbo huo ambao ulikuwa na maneno yanayosema ,amka tujenge nchi, amka tufanye kazi,na mashairi kadha wa kadha ambayo yanaleta hamasa kwa watanzania nchi nzima.

  Mpoto ambaye alikuwa ameambatana na msanii mahiri hapa nchini banana zoro ambaye alikuwa amesimama katika upande wa uimbaji wa kiitikio.

  0 0

  Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

  Rais John Pombe Magufuli ametoa siku tano kwa uongozi wa jiji la Dar es Salaam na halmashauri zake pamoja na waziri wa Tamisemi George Simbachawene kuhakikisha wanapata majibu ya matumizi ya kiasi cha shilingi bilioni tano zilizolipwa na Simon Group.

  Rais Magufuli amesema hayo jijini Dar es Salaam leo alipokuwa akifungua rasmi mradi wa mabasi yaendayo haraka .

  “nimemsikiliza waziri jinsi alivyonieleza juu ya pesa hizo kiasi cha shilingi bilioni tano ziweze kutumika kwa ajili ya maendeleo ya wana Dar es Salaam hivyo natoa siku tano mnipe taarifa ni namna gani mtatumia fedha hizo,ama kama mtashindwa ofisi yangu itakuja na maelekezo mapya” amesema Magufuli.

  Aidha Rais Magufuli ameagiza wakala wa barabara nchini kuhakikisha wanatenga eneo la kuegeshea magari na kituo cha daladala katika eneo la kimara na kubomoa nyumba zote ambazo zimejengwa katika hifadhi ya barabara na badala yake hifadhi hiyo ya barabara itumike kwa manufaa ya wananchi wote.

  Pia amesema kuwa serikali ipo katika mchakato wa kujenga Interchange katika eneo la ubungo ili kuweka uhalisia wa jina lenyewe la mradi huu wa mabasi yaendayo haraka kuliko hivi sasa Trafiki anayeongoza magari anaweza kuamua tu kusimamisha magari hayo kutokana na mapenzi na kupoteza maana halisi ya mradi.

  Ameweka wazi kuwa Dar es Salaam lazima ibadilike na lazima liwe jiji la kisasa kwa kuwa na miundombinu ambayo inawawezesha watu kufika katika shughuli zao kwa haraka.

  Aidha ametaja kuwa mradi huo unataraji kuendelea katika awamu nyingine ya pili ya tatu mpaka tano katika barabara tofauti za mkoa wa Dar es Salaam.

  0 0

  Bingwa wa mbio za mita 100 upande wa wanaume Usain Bolt atalazimika kurudisha dhahabu moja miongoni mwa dhahabu tisa alizoshinda baada ya mwanariadha mwenza Nesta Carter kupatikana alitumia dawa za kusisimua misuli.

  Carter alikuwa miongoni mwa wanariadha wanne wa Jamaica walioshinda mbio za mita 100 kupokezana vijiti katika michezo ya beijing 2008.

  Ni miongoni mwa wanariadha 454 waliochukuliwa violezo vyao na kamati ya kimataifa ya Olimpiki IOC mwaka uliopita na amepatikana alitumia dawa ya aina ya methylhexaneamine.

  Bolt mwenye umri wa miaka 30 alishinda dhahabu tatu katika michezo ya Olimpiki ya Rio msimu uliopita.

  Alishinda dhahabu katika mbio za mita 100, 200 na 400 kupokezana vijiti na kuongeza mafanikio yake katika mbio hizo mwaka 2008 na 2012.

  Carter mwenye umri wa miaka 31 alikuwa miongoni mwa wanariadha walioshinda dhahabu katika mbio hizo mjini London miaka mitano iliopita na kuisadidia Jamaica katika mbio za dunia miaka ya 2011, 2013 na 2015.

  Alikuwa wa kwanza kukimbia katika mbio za rilei za 4 mara 100 mjini Beijing ambazo zilimuhusisha mwanariadha Michael Frater, Asafa Powell na Bolt.

  Jamaica ilishinda kwa kuvunja rekodi ya dunia baada ya kumaliza kwa sekunde 37.10 mbele ya Trinidadad and Tobago na Japan ,ambao sasa medali zao zitaongezwa.Brazil itajipatia medali ya shaba.
   

  0 0

  Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) akimsikiliza mmoja wa wataalam walioambatana na Balozi wa Norway nchini Tanzania Mhe. Hanne Marie Kaarstad (watatunkulia) walipomtembelea ofisini kwake leo( 10/01/2017) jijini Dar Es Salaam.
  Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Katiba na Sheria Prof. sifuni Mchome (wapilikulia) akifafanua jambo wakati wa kikao na Baloziwa Norway na ujumbe wake (hawapopichani) walipotembelea Wizara hiyo leo ili kujadili namna wataalam hao wanavyoweza kusaidia kiteknolojia katika kurahisisha upatikanaji wa haki kwa wananchi.


  Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akiagana na Balozi wa Norway nchini Tanzania Mhe. Hanne Marie Kaarstad na ujumbe wake baada ya kumaliza kikao leo jijini Dar es salaam.

  (Picha na Wizara ya Mambo ya Katiba naSheria)

  0 0

  Naibu Waziri wa Nchi TAMISEMI Mhe. Suleimani Jafo (Mb) akitoa hotuba katika kikao cha kazi katika ukumbi wa mikutano Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini mjini Dodoma akiwaasa wanasheria kuhakikisha sheria ndogo hazikinzani na sheria mama kwa kuzingatia uandishi wa taaluma ya sheria kwani katika baadhi ya ziara zake amebaini kuwepo mogogoro ya wakulima na wafugaji, kesi nyingi za halmashauri kushindwa mahakamani na uandishi mbovu wa mikataba inayoingia halmashauri
  Naibu Waziri wa Nchi TAMISEMI Mhe. Suleimani Jafo (Mb) akisisitiza jambo kuhusu uendeshaji wa vikao vya Halmashauri kwamba Madiwani wanapaswa kuelekezwa kanuni na sheria za Halmashauri ili kuepuka migogoro ambayo mingi inaibukia wakati wa vikao vya mabaraza katika Mamlaka hizo. Kushoto kwake ni Sarah Barahomoka (Mwandishi Mkuu wa sheria bungeni) na Mwanasheria wa Idara ya Sheria OR TAMISEMI
  Naibu Katibu Mkuu OR TAMISEMI Bw. Benard Makali akisisitiza jambo juu ya makosa yanayofanywa na Mamlaka za Serikali za Mitaa nchini kama ukiukwaji wa utendaji kazi wa kisheria ambapo wanasheria wanapaswa kusimamia masuala yote ya kisheria katika utendaji wa kazi za Serikali
  Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kishapu (Shinyanga) ambaye pia ni Mwanasheria Bw. Stephen M.Magoiga akimshukuru Naibu Waziri OR TAMISEMI Mhe. Suleimani Jafo (Mb) kwa niaba ya Wanasheria ambapo amewaasa Wanasheria wenzake kuacha kufanya kazi kwa mazoea na kuzifanyia kazi sheria ndogo kwa ustawi wa Mamlaka za Serikali nchini.
  Baadhi ya Wanasheria wa Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa wakimsikiliza Naibu Waziri wa Nchi TAMISEMI Mhe. Suleimani Jafo (Mb) wakati akitoa hotuba katika kikao cha kazi katika ukumbi wa mikutano Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini mjini Dodoma ambapo amewaasa kufanya kazi kwa bidii na umuhimu wa sheria ndogo katika uendeshaji wa Mamlaka za Serikali za Mitaa.

  …………….

  NAIBU Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Seleman Jafo, amefungua mafunzo ya siku tatu ya wanasheria kwenye Halmashauri zote nchini huku akioneshwa kukerwa na tabia ya wanasheria hao kushindwa kesi na kuisababishia hasara serikali kwa kuwalipa fidia washindi.

  Akifungua mafunzo hay oleo mkoani Dodoma, Jafo amesema zipo kesi nyingi zinazohusu halmashauri mbalimbali, lakini zinashindwa kutetewa na kusababisha serikali kulipa fidia.

  Amebainisha pamoja na kuwepo wanasheria ndani ya halmashauri hizo, lakini wanashindwa kusimamia kesi zinazowakabili hali inayochangia serikali kulipa gharama kubwa kwa washindi wakati fedha hizo zingetumika kwa maendeleo ya wananchi.

  “Fedha zinazolipwa na serikali mara baada ya kushindwa kesi, zingeweza kusaidia maendeleo ya wananchi ndani ya halmashauri hizi kutokana na wanasheria kutokuwa makini,”amesema Jafo.

  Amewataka kuhakikisha wanasimamia vyema kesi za ardhi zinazowakabili wananchi wa chini ambao wengi wao hudhurumiwa na wenye uwezo na kusababisha malalamiko kwa wasimamizi wa sheria.

  Mbali na hilo, pia Jafo amesema sheria nyingi za halmashauri zinatofautiana na maeneo husika ma kuwa na matatizo makubwa ya kimaandishi kutokana na kukinzana na sheria mama.

  Amesema kutokana na sheria hizo kutoeleweka, inasababisha mikataba mingi ndani ya halmashauri hizo kutokuwa na umakini kwa kutoipendelea serikali na kuwapa kipaumbele walioingia mikataba hiyo, hali inayoonyesha kama hawapo wanasheria.

  0 0


  0 0

  Na Rhoda Ezekiel Kigoma.

  MKUU wa wilaya ya Buhigwe mkoa wa Kigoma kanali Marco Gaguti amewaonya wakimbizi wenye historia ya uhalifu nchini Burundi  wanaoingia Nchini  Tanzania, kwa kigezo cha kuomba hifadhi ya ukimbizi kwa kuhofia wasikamatwe kwa uhalifu walioufanya Nchini mwao, kuwa ikibainika  hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

  Aidha, Gaguti aliuomba uongozi wa Nchi ya Burundi kutoa ushirikiano kwa vyombo vya ulinzi na usalama vya   Wilaya hiyo iliyopo Mpakani, kuwabaini waomba hifadhi  hao wanaoingia Nchini kwa kukimbia uhalifu walioufanya Nchini mwao na kuja kuendeleza vitendo hivyo wanapo ingia Nchini.

  Hayo yalibainika jana wakati wa Kikao cha majadiliano baina ya Mkuu huyo na Mkuu wa Wilaya ya Mabanda Mkoa wa Makamba Nchini Burundi, alipokuwa akihoji ni kwanini wahamiaji wengi wanaongezeka Nchini wakidai wanakimbia vurugu zinazo endelea Nchini mwao ambapo kwa Mwezi january  waliingia waomba hifadhi 2230, ambapo ilibainika wengi wao wanadai wanakimbia kukamatwa kwa kujihusisha na uhalifu na wengine kukimbia njaa iliyopo majumbani kwao.

  Gaguti alisema kumekuwa na ongezeko kubwa la wahamiaji wanaoingia Nchini wakidai kukimbia vitisho wanavyo pewa na kikundi cha Vijana wa chama tawala kinacho julikana kama  ( IMBONELAKULE),  ambapo wanakuja kuomba hifadhi katika Nchi ya Tanzania ilihali Nchi yao ina amani ya kutosha  na wengine kukimbilia kambini kupata huduma za bure kwa kuhofia njaa nchini mwao . 

  Hali iliyopelekea Waziri wa Mambo ya ndani kusitisha zoezi la Waomba hifadhi kuingia Nchini kwa kigezo cha kukimbia njaa Nchini mwao na kukimbilia Tanzania ili waweze kupata Msaada wa chakula , ni lazima Afanyiwe mahojiano na atoe sababu zilizo mfanya akimbie iliaweze kupatiwa kibali cha kuwa mkimbizi.

  Hata hivyo Kanali Gaguti aliwaomba viongozi hao kutoa ushirikiano kwa vyombo vya ulinzi na usalama kuwabaini wahalifu hao waweze kurudishwa Nchini mwao kuepukana na vitendo vinavyo endelea na ongezeko la waomba hifadhi kuingia Nchini bila kufuata utaratibu.

  '' leo nilikuwa natembelea vituo na kuona ongezeko la wahamiaji lakini serikali imetoa maelekezo mapya ikiwemo kuwatambua na kujua sababu za kukimbia Nchini mwao, lakini kama atakuwa na sababu za Msingi hata pata fursa ya kuwa mkimbizi, lakini pia nikuombe ushirikiano kama kuna taarifa za watu ambao ni wahalifu upewe taarifa mapema kabla ya mambo kubadilika ili tuweze kuchukua tahadhari mapema kwa pande zote mbili" alisema kanali Gaguti.

  Naye mkuu wa Wilaya ya Mabanda Mkoa wa Makamba (Musitanteri)Niyonkuru Laetitia alisema kwa sasa nchi ya Burundi ni tulivu na wanaokimbia nchini  mwao ni wale wanaokimbia njaa na wengine kukimbia uhalifu aliofanya nchini Burundi na kuja Tanzania kuomba hifadhi.

  Alisema wengi waliofika Tanzania ni wale waliokimbia kwa mambo yao binafsi na wengine ni wale wakimbizi waliorudishwa BUrundi kipindi cha nyuma wanaokimbia wengi wanakuja kwa kigezo cha kupelekwa nje ya Nchi kama vile America na Ulayana Nchi nyingine ilikuwafuata ndugu zao walio pelekwa huko .  

  Aidha aliuomba Uongozi wa Tanzania kabla ya kuwapokea wahamiahi hao kuchukua vitambulisho vyao ilikubaini walio kimbia tuhuma zinazo wakabili, pia kumekuwa na tetesi wengi wao wanaoingia kuomba hifadhi wanakuja makambini kujifunza namna wanavyo weza kwenda kuipindua Nchi kwa kupigana pindi wanapo wabaini waweze kuwakabidhi kwa Serikali ya Burundi.

  Kwa upande wao baadhi ya Waomba hifadhi waliofika katika maeneo ya kupokelea waomba hifadhi hao kwa mahojiano waweze kuingia kambini ,wengi wao walidai wanakimbia vikundi vya IMBONELAKULE vinavyo wafuata Nyumbani kwao usiku na kuwapiga na kuwatishia usalama wao hali inayo walazimu kukimbilia Tanzania , suala lililo kanushwa na Mkuu wa Wilaya ya Mabanda.

  Nizigimana Silivesta ni moja kati ya  waomba hifadhi kutoka Burundi, alisema kinacho wapelekea kukimbia Nchini mwao ni hali ya kiusalama kuwa ndogo kumekuwa na tabia ya vikundi vya watu vinavyo wafuata kuwatisha kutokana na baadhi ya ndugu zao walio kimbilia nchini kuwa wanamahusiano nao na wanaipinga serikali.
   MKUU wa wilaya ya Buhigwe mkoa wa Kigoma kanali Marco Gaguti   akifafanua jambo mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Mabanda Mkoa wa Makamba nchini Burundi,(Musitanteri) Niyonkuru Laetitia, pamoja na kamati ya Ulinzi na Usalama ya Tanzania na Burundi katika kujadiliana sakata la Wahamiaji wengi wengi kuanza kuingia nchini Tanzania kwa kasi tangu Januari,2017.
  MKUU wa wilaya ya Buhigwe mkoa wa Kigoma kanali Marco Gaguti  akisalimiana na  Mkuu wa Wilaya ya Mabanda Mkoa wa Makamba nchini Burundi,(Musitanteri) Niyonkuru Laetitia
   Mkuu wa Wilaya Ya Buhigwe akisalimiana Na Wanajeshi wa Burundi mpakani mwa Tanzania na Burundi
   Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe akiongozana na kamati ya ulinzi na usalama kuingia mpakani mwa Burundi na Tanzania

  0 0

   MAKABIDHIANO: Mwenyekiti Mstaafu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Mstaafu Damian Lubuva (kulia) akimkabidhi  Mwenyekiti wa sasa wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji wa Rufaa Mhe. Semistocles Kaijage (kushoto) taarifa ya utendaji Kazi wake kwa kipindi miaka 5 alichokuwa madarakani.

   Mwenyekiti Mstaafu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Mstaafu Damian Lubuva akizungumza na Wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Sekretarieti ya Tume hiyo mara baada ya kukabidhi taarifa ya utendaji Kazi wake kwa kipindi miaka 5 alichokuwa madarakani

   Mwenyekiti wa sasa wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji wa Rufaa Mhe. Semistocles Kaijage akizungumza na Wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Sekretarieti ya Tume hiyo mara kupokea taarifa ya utendaji Kazi wa Mwenyekiti Mstaafu wa Tume hiyo Jaji Damiani Lubuva jijini Dar es salaam.

   Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Bw. Ramadhan Kailima akizungumza jambo wakati wa makabidhiano hayo jijini Dar es salaam.Katikati ni Mwenyekiti Mstaafu wa Tume Jaji Mstaafu Damian Lubuva na Kulia ni  Mwenyekiti wa Sasa wa NEC, Jaji wa Rufaa, Semistocles Kaijage.

  Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji wa Rufaa Mhe. Semistocles Kaijage akiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti Mstaafu wa Tume Jaji Damiani Lubuva , Wajumbe wa Tume na Secretarieti ya Tume hiyo.


  Picha na Aron Msigwa - NEC.

  0 0

  BENKI ya Dunia imekubali kuikopesha Tanzania fedha kwaajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo ukiwemo mkopo wa Dola Milioni 350 kwa ajili ya Mradi wa Upanuzi wa Bandari ya Dar es salam.

  Waziri wa Fedha na Mipango, Dokta Philip Mpango, amewaambia waandishi wa Habari mara baada ya kumalizika kwa Mazungumzo kati yake na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anaye shughulikia Kanda ya Afrika, Mhe. Makhtar Diop, Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es salaam.

   

  Kama ulipitwa na story ya mtu aliyekufa na nyoka yake tumekusogezea hapa


  0 0

   Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akisaini daftari la wageni baada ya kuwasili wilayani Momba Mkoani Songwe, kwa lengo la  kutembelea na kukagua uingiaji na utoakaji wa raia na wageni katika mpaka wa Tunduma unaotoa huduma kwa watu wanaoingia na kutoka katika nchi za Zambia, Zimbabwe, Botswana, Afika Kusini, Namibia na DRC Congo.Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Momba, Juma Irando. (Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
   Afisa Uhamiaji Mpaka wa Tunduma akimuelekeza jambo Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati), wakati wa ziara ya kutembelea mpaka huo unaotoa huduma kwa watu wanaoingia na kutoka katika nchi za Zambia, Zimbabwe, Botswana, Afika Kusini, Namibia na DRC Congo.Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Momba, Juma Irando.
   Mkuu wa Wilaya ya Momba, Juma Irando akizungumza na Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, walipotembelea jiwe (linaloonekana pichani) linalotenganisha nchi ya Tanzania na Zambia.Wengine ni Wakuu wa Idara za Uhamiaji, Magereza, Zimamoto na Polisi walioambatana na Naibu Waziri katika ziara hiyo mkoani Songwe.
   Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama mpakani Tunduma huku akiwaasa kushirikiana kwa pamoja katika kudhibiti uingiaji wa wahamiaji haramu wanaoingia  nchini kupitia mpaka huo. Kulia  ni Mkuu wa Wilaya ya Momba, Juma Irando.
  Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wanne kulia) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Serikali na Wakuu wa Idara za Uhamiaji, Magereza, Zimamoto, Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) na Polisi baada ya kutembelea mpaka wa Tunduma.Ambapo aliwaasa kushirikiana kwa pamoja katika kudhibiti uingiaji wa wahamiaji haramu wanaoingia  nchini kupitia mpaka huo. Wapili kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Momba, Juma Irando.


  IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI-WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI


older | 1 | .... | 1115 | 1116 | (Page 1117) | 1118 | 1119 | .... | 1897 | newer