Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46397 articles
Browse latest View live

KATIBU WA SUKI KANALI MSTAAFU LUBINGA AKUTANA NA MKURUGENZI MKAZI WA FES

$
0
0
 Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, anayeshughulikia Siasa na Uhusiano wa Kimataifa (SUKI), Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga (kulia), akizungumza na Mkurugenzi Mkazi hapa nchini wa Taasisi ya Fredrich Ebert Stiftung (EFS) ya Ujerumani, Michael  Schultheiss, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, leo, Januari 19, 2017. (Picha na Bashir Nkoromo).

MAJALIWA ATEMBELEA SHAMBA LA NG'OMBE LA ASAS LILILOPO IRINGA

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akisalimiana na Mkurugenzi wa Kampuni ia SAS, Bw. Salim Abri  wakati alipokwenda kwenye shamba la ng'ombe la ASAS lililoko nje kidogo ya mji wa Iringa Januari 19, 2017. (Picha na Ofisi ua Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama ukamuaji ng'ombe wa maziwa katika shamba la Ng'ombe la ASAS nje kidogo ya mji wa  Iringa Januari 19, 2017.  Wapili kushoto  ni Mkuu wa mkoa wa Iringa, Amina Masenza.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wakurugenzi wa kampuni ya ASAS  baada ya kutembelea shamba la ng'ombe la ASAS nje kidogo ya mji wa Iringa Januari  19, 2017.   Kulia ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).


MARUFUKU KULIMA, KUINGIZA MIFUGO NDANI YA VYANZO VYA MAJI-MAJALIWA.

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka wakuu wa mikoa ya Singida, Mbeya, Iringa na Dodoma wawasimamie wananchi wao na kuhakikisha hakuna shughuli za kibinadamu zinazofanyika ndani ya vyanzo vya maji.

Ametoa kauli hiyo leo (Alhamisi, Januari 19, 2017) alipozungumza na watumishi wa kituo cha kuzalisha umeme cha Mtera alipotembelea bwawa la Mtera akiwa njiani kwenda mkoani Njombe kwa ziara yake ya kikazi.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo baada ya Kaimu Meneja wa Kituo cha kuzalishia umeme cha Mtera, Mhandisi Edmund Seif kutaja baadhi ya changamoto zinazokikabili kituo hicho kuwa ni pamoja na kuongezeka kwa shughuli za kibinadamu ndani ya vyanzo vya maji.

Kufuatia hali hiyo Waziri Mkuu ameagiza vifanyike kwa vikao vya ujirani mwema ili wananchi waelimishwe umuhimu wa kutunza vyanzo vya maji na ni marufuku kuendesha shughuli za kibinadamu ndani ya kilomita 60 kutoka kwenye chanzo.

"Marufuku wafugaji kuingiza ng'ombe ndani ya vyanzo vya maji na badala yake utafutwe utaratibu wa kuwachimbia mabwawa pembeni. Pia wakulima nao wazuiwe kulima ndani ya vyanzo vya maji. Lazima tushirikiane kulinda vyanzo vyetu," amesema.

Awali, Mhandisi Seif alisema kituo hicho cha Mtera kinazalisha megawati 80 kwa siku ambazo zinaingizwa kwenye gridi ya Taifa. Alisema bwawa hili kwa sasa lina maji ya kutosha kuzalisha umeme hadi msimu ujao wa mvua.

Mhandisi hiyo alisema bwawa hilo linategemea kupata maji kutoka mto Ruaha Mkuu, mto Ruaha Mdogo na Vyanzo vyote hivyo vinaathiriwa na shughuli za kibidamu ambapo watu wanalima na kuingiza mifugo.

Baada ya kutoka kituoni hapo Waziri Mkuu alitembelea shamba la Igingilanyi ambalo ni moja kati ya mashamba matatu ya kufugia ng’ombe yanayomilikiwa na kiwanda cha kuzalisha bidhaa za maziwa ya Asas kilichoko mkoani Iringa.

Akiwa shambani hapo Waziri Mkuu aliwaagiza wakurugenzi wa halmashauri zote nchini kuhakikisha wanasimamia vizuri mgawanyo wa ardhi ndani ya halmashauri zao pamoja na kusimamia mipaka kati ya wilaya na wilaya.

“Wekeni mipango bora ya matumizi ya ardhi. Pimeni ardhi na mgawe hati ili kumaliza migogoro ya ardhi hata kwa waliopewa mashamba makubwa nao wapimiwe na ardhi yao na wapewe hati kwa mujibu wa muda uliowekwa kisheria,” amesema.

Pia aliwataka Maofisa Mifugo kuongeza kasi ya kutambua mifugo iliyoko kwenye maeneo yao na kuiwekea alama ili kuzuia uhamiaji holela wa mifugo kwa lengo la kuzuia migogoro kati ya wafugaji na wakulima.

Kwa upande wake mmoja wa Wakurugenzi wa kiwanda cha Asas, Bw. Fuad Abri alisema kiwanda hicho kina mashamba matatu yenye jumla ya ekari 2,000 na ng’ombe 1,010 kati ya hao 350 hukamuliwa maziwa na kutoa wastani wa lita 5,000 kwa siku.
Alisema katika mashamba hayo wameajiri wafanyakazi 175 na wamefanikiwa kutumia njia ya uhamilishaji (Artificial Insemination) katika mashamba yote na njia hiyo inawasaidia kuchagua jinsia ya ng’ombe wanayohitaji.


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU, 
ALHAMIS, JANUARI 19, 2017.

RAIS WA FIFA INFANTINO ATAKA SHERIA ZA SOKA KUBADILISHWA

$
0
0
Rais mpya wa FIFA Gianni Infantino anaonekana kutaka kubadili soka kabisa kwa kutaka kuondoa kila kitu cha Sepp Blatter na kuleta vyake hasa baada ya kupelekea mapendekezo ya kuongeza timu zitakazoshiriki kombe la dunia 2026 kufikia timu 48 na sasa amekuja na mpya ya kutaka kubadili namba ya kupiga penati.

Kwa kumtumia mkurugenzi wa mambo ya ufundi wa FIFA Marco Van Basten wamependekeza baadhi ya sheria mpya katika soka.
Kuondoa offside.

Akihojiwa na gazeti la Ujerumani liitwalo Bild,Van Basten amesema wanawaza kuondoa mchezo wa kuzidi katika soka.Alisema “sipati picha soka isipokuwa na ofside,washambuliaji watapata nafasi nyingi sana za kufunga”.Van Basten alisema mpira wa miguu utakuwa wakuvutia sana kama offside itaondolewa na anaamini jambo hilo litawafurahisha mashabiki na washambuliaji.

Kingine ni kubadili upigaji wa penati, Van Basten pia anaona kuna haja kubwa kwa FIFA kubadili aina ya upigaji wa penati na adhabu ya penati mchezaji ambapo upigaji wa penati ni mita kadhaa karibu na goli na kuupiga lakini sheria mpya anataka mpiga penati auweke mpira mita 25 kabla ya goli na kama anaweza atembee nao kuelekea golini kwa muda usiozidi sekunde nane.Aina hii ya upigaji penati sio ngeni kwani mwaka 1999 ilishafanyiwa majaribio nchini Marekani.

Kupunguza adhabu mipira ya kushika, Van Basten anaona kama adhabu ya kadi nyekundu ni kali mno kwa tukio hilo na  wanaliona kama tukio dogo lisilohitaji adhabu hiyo na wanazani inapaswa ipunguzwe kusitolewe kadi nyekundu mpira ukishikwa. Adhabu kam ile ya tukio la Luis Suarez mwaka 2010 wakicheza dhidi ya Ghana aliposhika mpira wakati ukiingia golini na kutaka ibadilishwe na kuwa ya njano.

Kapteni awe mtu pekee kuongea na mwamuzi, kama katika Rugby ni kapteni tu anayeongea na mwamuzi,asiruhusiwe mtu yeyote,mchezaji yeyote kuongea na mwamuzi.Aina  ya faulo ya mchezo wa kikapu pale mchezaji anapocheza madhambi matano anatakiwa atoke uwanjani na  sasa Van Basten anaamini staili hiyo inapaswa kuletwa katika soka.

Kupunguza idadi ya mechi, hii itafurahiwa sana na makocha wageni Uingereza. Alianza Van Gaal akaja Jurgen Klopp walilalamikia idadi ya mechi kuwa nyingi Epl.Van Basten anataka idadi ya mechi zipunguzwe kutoka mechi 80 kwa msimu hadi 50 kwa msimu.

Kuongeza idadi ya Substitution.Van Basten anatamani kuongeza idadi ya wachezaji wa sub kuanzia 5-7,kwa muda mrefu wadau wa soka wamekuwa wakizungumzia kuhusu suala la kuongeza wachezaji wa akiba na sasa FIFA inatarajia kuliangalia suala hili.

Kuzifanya dakika 10 za mwisho kutumika ipasavyo.”Tunajua kutokana na kuongeza idadi ya wachezaji wa akiba pamoja na aina ya upigaji penati vitachukua mda mrefu uwanjani na itatubidi kuhakikisha dakika 10 za mwisho zinatumika kiuhakika” Van Basten alisema watahakikisha hakuna upotezaji muda katika dakika zamwisho za mchezo.

Hayo ni mapendekezo tu kutoka kwa mkurugenzi wa ufundi wa FIFA na  sasa atawasilisha mapendekezo hayo katika kamati ya FIFA yaweze kujadiliwa.

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA ATEMBELEA KITUO CHA KUZALISHA UMEME MTERA

$
0
0
Gari lililombeba  Waziri  Mkuu, Kassim Majaliwa likipita kwenye daraja la bwawa la kuzalisha umeme  Kituocha Kuzalisha Umeme cha  Mtera kwenye mpaka wa mkowa Dodoma na Iringa  Januari 19, 2017. Mheshimiwa Majaliwa alifanya ziara fupi  ya kukagua kina cha maji kwenye bwawa hilo . (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na wafanyakazi wa Shirika la Umeme Nchini (TANESCO)  katika bwawa la Kituo cha Kuzalisha Umeme cha Mtera lililoko kwenye mpaka wa  mkoa wa Dodoma na Iringa wakati alipofanya ziara fupi ya kukagua kina cha maji kwenye bwawa hilo  Januari 19, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akipata maelezo kuhusu kina cha maji kwenye bwawa la  Kituo cha Kuzalisha Umeme cha Mtera lililoko kwenye mpaka wa mkoa wa Dodoma na Iringa  wakati alipofanya ziara fupi ya kukagua kina cha maji kwenye bwawa hilo Januari  19, 2017.  Kushoto ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na maendeleo ya Makazi, William Lukuvi.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akikagua kina cha maji kwenye bwawa la  Kituo cha kuzalisha Umeme cha Mtera lililoko kwenye mpaka wa mkoa wa Dodoma na Iringa Januari 19, 2017.   Kushoto ni Kaiu Meneja wa Kituo hicho,  Mhandisi Edmund Seif. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua kina cha maji kwenye bwawa la  Kituo cha Kuzalisha Umeme cha Mtera  lililoko  kwenye  mpaka wa mkoa wa Iringa na Dodoma  wakati alipokwenda kukagua kina cha maji kwenye bwawa hilo Januari  19, 2017.

SERIKALI YAONYA WAWEKEZAJI WANAOCHOCHEA MIGOGORO

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amesema kuwa serikali haitasita kuwachukulia hatua wawekezaji wanaochochea migogoro katika wilaya ya Ngorongoro na kusababisha uvunjifu wa amani hivyo kuchangia kuzorota kwa shughuli za maendeleo. 

Gambo ameyasema hayo katika ziara yake wilayani Ngorongoro inayolenga kutatua migogoro wa pori tengefu lenye ukumbwa wa kilomita za mraba elfu kumi na tano ambapo amekutana na wadau mbalimbali ikiwemo wawekezaji,wafugaji pamoja na viongozi wa kiserikali. 

Amesema kuwa serikali itawaondoa wawekezaji wanaochochea migogoro na kuwagombanisha wananchi na serikali yao jambo ambalo halitafumbiwa macho,Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro Rashid Taka amesema kuwa wako baadhi ya watu wanaonufaika na migogoro hiyo hivyo kumalizika kwa migogoro hiyo kutaleta manufaa kwa wananchi wengi kuliko kunufaisha kundi la watu wachache 

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Wizara ya Mifugo,Kilimo na Uvuvi ambaye pia ni Mbunge wa Ngorongoro Wiliam Ole Nasha na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha Lekule Laizer wamesema kuwa utatuzi wa mgogoro huo utasaidia kuepusha migongano ya kimaslahi na kuchochea shughuli za kimaendeleo badala ya kutumia muda mwingi katika usuluhishi wa miigogoro hiyo 

Mkuu wa Mkoa ameanza Ziara yake leo Wilayani Ngorongo na kesho atatembelea katika vijiji mbalimbali ikiwa ni katika juhudi za kutatua mgogoro wa pori tengefu katika wilaya hiyo.

Mufuruki na ujumbe wake wamtembelea Waziri Makamba ofisini kwake jijini Dar leo

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano na Mazingira Mh. January Makamba akijadili jambo na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Taifa wa Dhamana ya Hifadhi ya Mazingira Bw. Ali A. Mufuruki alimpotembelea Waziri Makamba Ofisini kwake mapema hivi leo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano na Mazingira Mh. January Makamba (wa kwanza kushoto) akiwaongoza kupitia Makabrasha ya masuala ya Mazingira, Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Taifa wa Dhamana ya Hifadhi ya Mazingira Bw. Ali A. Mufuruki, Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Prof. Faustin Kamuzora na Kaimu Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais.
Wakifurahia jambo kwa pamoja Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano na Mazingira Mh. January Makamba, Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Taifa wa Dhamana ya Hifadhi ya Mazingira Bw. Ali A. Mufuruki, Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Prof. Faustin Kamuzora na Kaimu Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais.

NAIBU WAZIRI MASAUNI AKUTANA NA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA MAMBO YA NJE, ULINZI NA USALAMA JIJINI MBEYA

$
0
0
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akijibu maswali yaliyoulizwa na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama wakati wa ziara ya kikazi iliyofanyika leo jijini Mbeya.Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Kanali Mstaafu Masoud Ally.
Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Kapteni Mstaafu Goerge Mkuchika, akizungumza wakati wa kipindi cha kuuliza maswali yaliyoelekezwa kwa Idara zilizopo ndani ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.Kamati hiyo imekutana jijini Mbeya kwa ziara ya kikazi.
Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Juliana Shonza (katikati) akizungumza wakati wa kipindi cha kuuliza maswali yaliyoelekezwa kwa Idara zilizopo ndani ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi .Wengine ni wajumbe wa kamati hiyo.Kamati hiyo ya Bunge iko jijini Mbeya kwa ziara ya kikazi
Mkuu wa Wilaya ya Chunya, Rehema Madusa akizungumza wakati wa mkutano na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama,iliyokutana jijini Mbeya kwa ziara ya kikazi.
Mkuu wa Idara ya Uhamiaji mkoa wa Mbeya, Kamishna Msaidizi , Asumsio Achachaa, akijibu maswali yaliyoelekezwa kwenye Idara yake na wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama(hawapo pichani), wakati wa mkutano na kamati hiyo iliyokutana Jijini Mbeya kwa ziara ya kikazi.( Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)


IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI-WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

WAZIRI MBARAWA AFANYA ZIARA KUANGALIA UTEKELEZAJI WA MRADI WA UJENZI WA JENGO LA TATU LA ABIRIA KATIKA KIWANJA CHA NDEGE CHA KIMATAIFA CHA JNIA

$
0
0
 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania, Salim Msangi akimkaribisha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa alipofanya ziara leo Januari 19 kuangalia Ujenzi wa Jengo la Tatu la Abiria (TB III), katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere 
 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania, Salim Msangi akitoa maelezo ya Utekelezaji wa Mradi wa Ujenzi wa Jengo la Tatu la Abiria (TB III), katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa. 
Kukagua Mradi wa Ujenzi.
 Waziri Mbarawa (katikati), akisikiliza kwa makini maelezo ya Mhandisi Mohamed Millanga kuhusu ujenzi huo.
 Mkurugenzi wa Mradi Mhandisi Mohamed Millanga akitoa maelezo kwa Waziri Mbarawa.
 Waziri Mbarawa akikagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa jengo la tatu la abiria (TB III) katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere.  
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliamo, Prof. Makame Mbarawa (kushoto), akipata maelezo kuhusu ujenzi wa jengo la tatu la abiria katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), kutoka kwa Mkurugenzi wa Mradi Mhandisi Mohamed Millanga wakati waziri alipofanya ziara jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania, Salim Msangi.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliamo, Prof. Makame Mbarawa akizungumza mara baada ya kukagua ujenzi wa ujenzi wa jengo la tatu la abiria (TB III) katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere.  Kulia ni Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania, Salim Msangi.

FES YA UJERUMANI YAMFAGILIA DK. MAGUFULI KWA KUINOA UPYA CCM

$
0
0
NA BASHIR NKOROMO.

Asasi ya Fredrich Ebert Stiftung (FES) ya Ujerumani, imeelezea kuvitiwa kwake na hatua anazofanya Rais Dk. John Magufuli, kukifanya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwa kipya zaidi.

Taasisi hiyo imesema, inavutiwa na hatua hizo zinazofanywa na Rais Dk. Magufuli ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi, kwa kuwa sasa zitakifanya kuwa cha watu zaidi badala ya kuwa mali ya viongozi kama kilivyokuwa kimeanza kuonekana.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkazi wa Taasisi hiyo ya EFS hapa nchini, Michael  Schultheiss, alipokutana na kuwa na mazungumzo na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, anayeshughulikia Siasa na Uhusiano wa Kimataifa (SUKI), Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, leo.

Amesema, hatua hiyo ya Rais Dk. Magufuli, itakiimarisha zaidi Chama Cha Mapinduzi, na kuendelea kuaminiwa na Watanzania wengi hivyo kukipa ridhaa ya kuunda serikali kwa kuwa na matarajio kuwa serikali inayoundwa na CCM itaweka mikakati iliyo bora katika kuwainua kiuchumi katika nyanja mbalimbali na kuifanya nchi kuwa yenye uchumi unaokua haraka.

Naye kanali Mstaafu, Lubinga alisema, CCM inaipongeza FES kwa kuendelea kuwa karibu na vyama vyote vya siasa hapa nchini, kwa kuwa hatua hiyo inavisaidia hasa vyama vichanga kuimarika katika misingi ya kujielewa kuwa vinayo majukumu ya kuwafanyia wananchi katika kusaidia kuleta maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika nchi.

Ameisihi FES kuendelea na jitihada zake hizo, hasa kwa Chama Cha Mapinduzi kwa kuwa kufanya hivyo ni moja ya njia zinazoimarisha uhusiano wa miaka mingi ulipo baina ya Chama na Taisisi hiyo.
 Katibu Msaidizi Mkuu Idara ya Siasa na Ushirikiano wa Kimataifa, Mama Juliana Chitinka akitoa maneno ya Utangulizi, kabla ya mazungumzo kuanza kati ya Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga na Mkurugenzi Mkazi wa FES, Michael Schulttheiss, leo katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam.
 Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga na Mkurugenzi Mkazi wa FES, Michael Schulttheiss, wakiwa tayari kwa mazungumzo leo katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mratibu wa Taasisi FES,  Amon Petro.
Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga (kulia) akisisitiza jambo wakati akizungumza na Mkurugenzi Mkazi wa FES, Michael Schulttheiss, leo katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam. Picha:Bashir Nkoromo)

SEMINA YA KUPEANA TAARIFA KUHUSU UTOAJI MIMBA USIO SALAMA NA HALI ILIVYO KATIKA SHERIA ZA NCHI, MIKATABA YA KIKANDA NA KIMATAIFA YAFANYIKA

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Chama Cha wanasheria wanawake TAWLA Bi Tike Mwambipile akifungua semina ya kuhamasisha wadau wa Kutetea haki za wanawake na kujadili madhara ya utoaji mimba usio salama hapa Tanzania kwa kushirikishana matokeo ya utafiti uliofanyika hivi karibuni wa matukio ya utoaji mimba usio salama pamoja na huduma za baada ya utoaji mimba usio salama hapa Tanzania.
2
Baadhi ya washiriki wa semina hiyo wakifuatilia mada kadhaa zilizokuwa zikitolewa katika semina hiyo.
3
Dk. Pensiens Mapunda Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Afya na Tiba Hurbert Kairuki HKMU akielezea jambo wakati wa semina hiyo.
4
Baadhi ya washiriki wakisikiliza kwa makini mambo mbalimbali yaliyokuwa yakijadiliwa katika semina hiyo.
7
5
Washiriki wa semina hiyo wakiwa katika picha ya pamoja.
...........................................................................

Lengo la semina hii ni kujadili swala nyeti linaloigusa jamii yetu ya Kitanzania na wadau muhimu katika kutetea haki za wanawake katika kuhakikisha ustawi wa mwanamke unaendelea vizuri katika jamii yetu
Pamoja na kazi tunazofanya za kutoa huduma ya msaada na ushauri wa kisheria kwa wanawake na watoto, TAWLA imejikita pia katika kupigania haki za wanawake na usawa wa kijinsia hapa nchini ikiwemo Haki ya Afya ya Uzazi. Hii ni kwa sababu, TAWLA inatambua umuhimu wa haki za kijinsia na Afya ya Uzazi katika kuleta maendeleo ya kiuchumi na kijamii na zaidi sana kuondoa imani potofu kuhusu afya ya uzazi.

TAWLA kupitia vituo vyake vya msaada wa kisheria na mijadala ya kijamii (Community Conversation) tulipata taarifa za madhara na vifo vitokanavyo na utoaji mimba usio salama ambazo zilitushtusha na kutugusa sana na ndio maana tukaonelea kuwa ni vyema takafanya utafiti juu ya suala hili ili kuona ni kwa namna gani tunaweza kuisaidia jamii yetu kwa kushirikiana na wadau muhimu katika swala hili, ili kupunguza au kuondoa kabisa vifo vya akina mama na wasichana vitokanavyo na utoaji mimba usio salama.
Takwimu za tafiti ya Guttmacher zinaonyesha kwamba utoaji mimba usio salama ni sababu ya pili ya vifo vya akina mama na wasichana hapa nchini kwa maana kwamba:

(1) Kila mwaka wanawake wa Kitanzania 405,000 hutoa mimba kwa usiri karibu wote na kwamba 40% hupata matatizo ambayo yanahitaji matibabu:
(2) Kila mwaka wanawake wa Kitanzania milioni moja hupata mimba zisizotarajiwa ambazo 39% ya wanawake hao huishia kwenye utoaji mimba:
(3) 60% ya wanawake wa Tanzania wenye matatizo ya utoaji mimba hawapati huduma ya matibabu wanayoihitaji:
(4) Kila mwanamke 1 kati ya wanawake 5 nchini Tanzania ana mahitaji yasiyofikiwa ya uzazi wa mpango
Ni kwa misingi hiyo basi kongamano hili lina malengo makuu yafuatayo:
(1) kuhamasisha washiriki na kujadili madhara ya utoaji mimba usio salama hapa Tanzania kwa kushirikishana matokeo ya utafiti uliofanyika hivi karibuni wa matukio ya utoaji mimba usio salama pamoja na huduma za baada ya utoaji mimba usio salama hapa Tanzania:
(2) Kushirikishana matokeo ya utafiti uliofanyika hivi karibuni wa matukio ya utoaji mimba usio salama pamoja na huduma za baada ya utoaji mimba usio salama hapa Tanzania:

(3) Kubadilishana uzoefu:
(4) Kufanya uchechemuzi wa kuingizwa kwenye Sheria za Tanzania vipengele vinavyohusu haki ya Afya ya Uzazi vilivyopo kwenye Mkataba wa Nyongeza wa Afrika (Maputo Protocol) juu ya Haki za Wanawake:
(5) Kuwakutanisha wadau muhimu juu ya swala hili ili kujadili kuhusu Sheria na Sera zinazohusu Haki ya Afya ya Uzazi na utoaji mimba ulio salama hapa Tanzania.

Pamoja na madhumuni yaliyoiainisha hapo juu, semina hii inakusudia kutambua aina ya michango ambayo wadau mbali mbali waliopo hapa leo wanaweza kutoa katika kupunguza vifo vya akina mama vinavyotokana na utoaji mimba usio salama na madhara yake hapa Tanzania

Chama Cha Wanasheria Wanawake Tanzania kinaamini kwamba, kutambua Haki ya Afya ya Uzazi ni muhimu katika kufikia lengo la kupigania haki za wanawake na usawa wa kijinsia hapa nchini.. Lengo hili linaweza kukamilika endapo tu kila mmoja wetu katika ukumbi huu atajitoa katika kuhakikisha kuwa, wototo wetu wa kike, dada zetu, mama zetu na wanawake wote hapa nchini hawafi kwa sababu ya utoaji mimba usio salama.

Tunatambua kazi za Taasisi/ofisi zenu katika kuletea haki za binadamu, haki za wanawake na usawa wa kijinsia hapa Tanzania, ndio maana tumeomba ushiriki wenu ili kufanikisha lengo hili la kuleta haki katika jamii yetu.

Washiriki wa semina hii ni Baadhi ya wadau kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Wizara ya Katiba na Sheria na baadhi ya Asasi zisizo za kiraia zinazoshughulikia maswala ya haki za wanawake Nchini Tanzania.

KAMATI YA BUNGE YA ARDHI, MALIASILI NA UTALII YATEMBELEA MAKAO MAKUU YA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII, MPINGO HOUSE

$
0
0
Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (wa tatu kushoto) akizungumza katika kikao cha Kamati ya Bunge, Ardhi, Maliasili na Utalii  katika ukumbi wa Ngorongoro wizarani hapo jana. Kutoka kulia ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhandisi Ramo Makani, Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Kemilembe Lwota, Mwenyekiti wa Kamati, Mhandisi Atashasta Nditiye, Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Jenerali Gaudence Milanzi na Naibu Katibu Mkuu, Dkt. Aloyce Nzuki.
Kikao kikiwa kinaendelea katika ukumbi wa Ngorongoro, Makao Makuu ya Wizara hiyo, Mpingo House, Jijini Dar es Salaam.
 Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Kitengo cha Kupambana na Ujangili wa Idara ya Wanyamapori, Bw. Robert Mande akiwasilisha taarifa kuhusu taratibu za uhifadhi wa ghala la meno ya tembo kwa Kamati ya Bunge, Ardhi, Maliasili na Utalii katika ukumbi wa Ngorongoro makao makuu ya Wizara hiyo Jijini Dar es Salaam leo.
 Baadhi ya wajumbe wa kamati ya bunge Ardhi, Maliasili na Utalii katika kikao hicho. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu, Maliasili na Utalii, Dkt. Aloyce Nzuki.
 Baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo.
Baadhi ya wakurugenzi wa Idara katika Wizara ya Maliasili na Utalii, wakifuatilia mjadala kwenye kikao hicho.
Baadhi ya wajumbe wa Kamati hiyo ya Bunge.
 Baadhi ya wajumbe wa Kamati hiyo ya Bunge.
 Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Aloyce Nzuki (kulia) akisalimiana na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge Ardhi, Maliasili na Utalii, Mhandisi Atashasta Nditiye baada ya kuwasili makao makuu ya Wizara hiyo Mpingo House Jijini Dar es Salaam jana huku akiongozana na wajumbe wa kamati hiyo.
NA HAMZA TEMBA - WMU
...........................................................................

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imetembelea makao makuu ya Wizara ya Maliasili na Utalii, Mpingo House jijini Dar es Salaam leo na kuzuru ghala la nyara za Serikali kuona utunzaji wa meno ya tembo na changamoto zake.


Kabla ya kutembelea ghala hilo kamati hiyo ilipokea taarifa maalum ya wizara juu ya mchakato mzima wa taratibu za ukusanyaji wa meno ya tembo, usafirishaji, uhakiki, usajili kwenye mfumo maalum wa kielektroniki, uhifadhi wake na ulinzi thabiti wa ghara hilo.


Akizungumza wakati wa kuwasilisha taarifa hiyo, Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Kitengo cha Kupambana na Ujangili wa Idara ya Wanyamapori, Bw. Robert Mande alisema meno yanayohifadhiwa katika ghala hilo ni yale yanayotokana na vifo asilia, kuuawa kutokana na uharibifu wa mali na maisha ya binadamu na yale yanayotokana na ujangili.


Waziri wa Maliasili na utalii, Prof. Jumanne Maghembe akijibu moja ya swali la wajumbe wa kamati hiyo ambao walitaka kujua uwezekano wa kuuza meno hayo ya tembo yaliyohifadhiwa ili kulipatia taifa mapato,  amesema msimamo wa Serikali ya Tanzania kwa sasa sio wa kuuza wala wa kuchoma meno hayo.


"Msimamo wetu ni kama ule wa nchi za Kenya, Uganda, Zambia, Malawi na Msumbiji wa kutokuuza meno haya kwa sasa kwasababu mbalimbali za kimsingi kabisa, moja ikiwa ni sababu za kiutafiti ambapo vinasaba vya meno ya zamani vinaweza kutumika kubaini mambo mbalimbali ikiwemo utafutaji wa dawa ya magonjwa ya tembo”, alisema.


Alisema kitendo cha kuuza meno hayo pia ni kuchochea zaidi biashara hiyo kwakuwa kitaongeza upatikanaji wa bidhaa hiyo kwenye masoko hivyo kuendelea kuipa uhai biashara hiyo haramu duniani.


Hapo awali, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Generali, Gaudence Milanzi akizungumza kwenye kikao cha kamati hiyo mkoani morogoro kilichohusisha uongozi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) alisema ujangili hapa nchini kwa sasa umepungua kwa kiasi kikubwa na kwamba nyara zinazokamatwa kwa sasa ikiwemo meno ya tembo ni za zamani zilizokuwa zikisubiria kusafirishwa nje ya nchi.


Alisema hatua hiyo ya kupungua kwa uhalifu huo imefanikiwa kutokana na kazi kubwa inayofanywa vikosi maalum vya Askari wa wanyamapori vya kudhibiti ujangili kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama nchini.


Alisema hatua ya Serikali ya China kupiga marufuku biashara ya meno ya tembo nchini humo ni jambo la kupongezwa na kwamba uamuzi huo utasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza msukumo wa vitendo vya ujangili nchini na barani Afrika kwa ujumla.


Naye mwenyekiti wa kamati hiyo ya bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Mhandisi Atashasta Nditiye amewapongeza viongozi wa Wizara ya Maliasili na Utalii namna walivyojipanga katika utekelezaji wa majukumu ya Wizara hiyo na kuwaahidi ushirikiano kutoka kwa kamati yake.


Aliahidi kutoa ushirikiano kwa uongozi wa wizara hiyo katika kuhakikisha kuwa wanaikabili changamoto kubwa ya uvamizi wa mifugo kwenye maeneo ya hifadhi. "Sisi tunaungana na nyie, hatukubali mifugo kwenye hifadhi zetu, kwakuwa zinaharibu ubora wa hifadhi hizo, tunawaahidi ushirikiano wa kukabiliana ma changamoto hiyo"


Kamati hiyo ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii ilitembela pia makao makuu ya Wakala ya Mbegu za Miti Tanzania (TTSA), Mamlaka ya Wanyamapori Tanzania (TAWA) na Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania (TAFORI) zote za mkoani Morogoro.



WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AWASILI MAKAMBAKO KUANZA ZIARA YA MKOA WA NJOMBE

$
0
0

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na ULinzi na Usalama ya Mkoa wa Njombe baada ya kuwasili Makambako kuanza ziara ya mkoa huo Januari 19, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea maua kutoka kwa Skauti baada ya kuwasili Makambako kuanza ziara ya mkoa wa Njombe Januari 19, 2017. Kulia ni Mkuu wa Mkoa huo Christopher Ole Sendeka. (Picha na Ofisi ya Wiri Mkuu)

NEWS ALERT: RAIS DKT MAGUFULI ATEUA MABALOZI SITA KUWAKILISHA TANZANIA NCHI MBALIMBALI

MHE. MHAGAMA ASHAURI CHAMA CHA AKIBA NA MIKOPO OFISI YA WAZIRI MKUU (MAKAMU SACCOS) KUWA WABUNIFU

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama ameshauri uongozi wa Chama cha Akiba na Mikopo cha Ofisi ya Waziri Mkuu (Makamu Saccos) kuwa na ubunifu katika utendaji ili kuleta manufaa zaidi kwa wanachama wake.

Mhe. Mhagama ameyasema hayo wakati wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Wanachama wa Chama hicho uliofanyika Januari 19, 2017 mkoani Dodoma.

Katika Mkutano huo Mhe. Waziri alisisitiza kuwepo na mikakati madhubuti ya kubuni miradi itakayowezesha chama kuwa na vyanzo vyake vya mapato na kuwa na mikakati ya kuongeza wanachama wapya kwa kuzingatia umuhimu wa chama hicho.“Ni muhimu kuwa na mikakati madhubuti ya kubuni miradi, kuongeza wanachama pamoja na kuwa na vitu vya kiupekee na vya kiufanisi vitakavyokisaidia chama kuwa imara katika utendaji wake”, alisema Waziri Mhagama.

Aliongeza kuwa chama hicho kimekuwa msaada mkubwa kwa wanachama wake amabapo wengi wao wamekuwa na maendeleo mbalimbali kutokana na uwepo wa fursa za mikopo isiyokuwa na masharti magumu.

“Chama kimekuwa mkombozi mkubwa kwa wanachama wake kwani wamekuwa wakikopa na kusaidia katika shughuli za kimaendele, ikumbukwe kuwa asilimia kubwa ya wafanyakazi wana maendeleo kwakuwa wanachukua mikopo mbalimbali inayowasaidia kuwepo na maendeleo ya kiuchumi kwa mtu mmoja mmoja”, alisisitiza Mhe.Mhagama.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama hicho Bw. Joseph Muhamba aliahidi kuyachukua mapendekezo yote yaliyotolewa na Mhe.Waziri na kuyaweka katika vitendo ili kuhakikisha chama kinaongeza mbinu za ubunifu ikiwemo eneo la kuongeza wanachama wapya na kuweka mazingira mazuri zaidi kwa wanachama waliopo.

Mhe. Mhagama aliahidi kutoa ushirikiano wake kwa Chama hicho na kueleza kuwa chama kiitumie fursa ya Serikali kuhamia Dodoma kama chachu ya kuongeza wanachama wapya.

 “Ninawaahidi kuwapa ushirikiano wa hali na mali na kuamini kuwa chama hiki ni msaada mkubwa kwa wafanyakazi wa Ofisi ya Waziri Mkuu kwani kipo kisheria kabisa na zipo kanuni zinazoelekeza juu ya uwepo wa chama na kwa kuonesha mfano mimi na Naibu Waziri Mhe. Dkt. Possi tunajiunga rasmi hii leo ili kuwa mstari wa mbele kukisaidia chama hiki”. Alisema Mhe. Mhagama.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (katikati) akisalimia wanachama waChama cha Akiba na Mikopo Ofisi ya Waziri Mkuu (hawapo pichani) wakati wa Mkutano wao wa mwaka Uliofanyika Ukumbi wa Mikutano Ofisi ya Waziri Mkuu Dodoma tarehe 19 Januari, 2017.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akizungumza jambo wakati wa Mkutano Mkuu wa mwaka wa Wanachama wa Chama cha Akiba na Mikopo Ofisi ya Waziri Mkuu Januari 19,2017 katika Ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu Dodoma.
 Baadhi ya wajumbe Chama cha Akiba na Mikopo Ofisi ya Waziri Mkuu wakifuatilia maelekezo ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani) wakati wa Mkutano wa kwanza wa mwaka Januari 19, 2017 Mkoani Dodoma.
 Mkurugenzi Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu Ofisi ya Waziri Mkuu Bw.Issa Nchasi akizungumza jambo wakati wa Mkutano wa Mwaka wa Wanachama wa Akiba na Mikopo wa Ofisi hiyo Mkoani Dodoma Januari 19, 2017.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akikabidhi ada ya uanachama na hisa zake kwa Katibu wa chama Bi. Algensia Ngalapa mara baada ya kuamua kujiunga rasmi na Chama cha Akiba na Mikopo Ofisi ya Waziri Mkuu wakati wa Mkutana wao Januari 19, 2017 Dodoma.
 Mwenyekiti wa Chama cha Akiba na Mikopo Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Joseph Muhamba akitoa neno la shukrani kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama wakati wa Mkutano wa chama hicho mkoani Dodoma tarehe 19 Januari, 2017.
 Naibu Waziri Ofisi ya Waziri (watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi akizungumza wakati wa mkutano wa Wanachama wa Chama cha Akiba na Mikopo cha Ofisi ya Waziri Mkuu kilichofanyika Ukumbi wa Mikutano hiyo Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (wa pili kutoka kulia waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na wanachama wa Chama cha Akiba na Mikopo cha Ofisi ya Waziri Mkuu, Kulia kwake ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri (watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi na kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Chama hicho Bw. Joseph Muhamba. PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU

TAARIFA KWA UMMA: KAMBI ZA UPASUAJI WA BILA KUFUNGUA KIFUA KWA WAGONJWA WA MOYO


OMBI LA UANACHAMA WA ZANZIBAR KUJADILIWA CAF

$
0
0

Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limepitisha ombi la Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) la Zanzibar kuwa mwanachama kamili wa CAF. Katika kikao chake cha Kamati ya Utendaji kilichoketi Januari 12, mwaka huu kiliamua kupitisha ombi hilo kuwa moja ya ajenda za Mkutano Mkuu wa CAF utakaofanyika Machi 16, 2017 huko Addis Ababa, Ethiopia.

Hivyo sasa Mkutano Mkuu huo utapiga kura na kama Zanzibar itapata idadi ya kura theluthi mbili yaani 2/3 ya wanachama wote, itatangazwa kuwa mwanachama mpya kamili wa CAF ambako atakuwa na haki mbalimbali za kama mwanachama.

Haki hizo ni pamoja na kushiriki michuano yote inayoandaliwa na kusimamiwa na CAF na hii ni pamoja na Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON), fainali za Afrika Wanawake (AWCON), fainali za vijana (AFCON U17 na AFCON 20)na pia kuhudhuria mikutano mbalimbali ya CAF kama mwanachama kamili, kupokea na kusimamia kozi mbalimbali za CAF nakadhalika.

Pia itakuwa na fursa ya kupiga kura katika masuala muhimu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) tofauti na sasa ambako inapata fursa ya klabu zake zinazoshika nafasi ya juu katika Ligi Kuu ya Zanzibar kushiriki Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho.

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linatoa shukrani kwa Mheshimiwa Nape Nnauye – Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wa Jamhuri ya Muungano Tanzania pamoja na Mheshimiwa Rashid Ali Juma - Waziri wa Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo wa Serikali ya Mapinduzi Zanizbar (SMZ) kwa kufanikisha hatua hiyo.

Pia, TFF inatoa shukrani kwa Rais wa Chama cha Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFA), Ravia Idarus Faina pamoja na Rais wa Heshima wa TFF Leodegar Chilla Tenga ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji wa CAF na Marais wa Heshima wa TFF Said Hamad El Maamry ambaye ni Mjumbe wa kudumu wa CAF na Mzee Muhiddin Ndolanga na wadau wote wa familia ya mpira wa miguu kwa mafanikio ya hatua hii.

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa sasa linajikita kwenye kampeni nzito ya kuomba kura za kutosha kuhakikisha kwamba Zanzibar inapata nafasi hiyo ya uanachama kamili.

Kadhalika Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kupitia viongozi wake wako kwenye mchakato wa kumfanyia kampeni Rais wa Heshima wa TFF, Bw. Leodegar Chilla Tenga kuhakikisha anashinda nafasi ya Ujumbe wa Kamati ya Utendaji (Council) ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA).

Leodegar Tenga anawania nafasi hiyo kutoka nchi za Afrika zinazozungumza lugha ya Kiingereza akishindana na Rais wa zamani wa Shirikisho la Mpira wa Miguu la Zambia, Kalusha Bwalya na Kwesi Nyantakyi wa Ghana.

TFF inaomba Watanzania wote na wadau wote wa mpira wa miguu nchini kutuunga mkono katika juhudi na jitihada zetu za kuona Zanzibar inapata nafasi hiyo kadhalika Tenga anakuwa mjumbe kwenye baraza la ushauri huko FIFA.

UONGOZI WA WILAYA MPYA YA KIBITI PWANI YAAHIDI KULIVALIA NJUGU SUALA LA WIMBI LA UMASIKINI KWA VIJANA NA WAKINAMAMA

$
0
0
Mkurugenzi mtendaji wa halmasjauri ya Wilaya ya Kibiti mkoani Pwani Alvera Ndabagoyo wa katikati akiwa katika boti ikiwa ni moja ya safari yake kwa ajili ya kuweza kukagua shughuli mbali mbali za maendeleo na changamoto za wananchi (PICHA NA VICTOR MASANGU)


NA VICTOR  MASANGU, KIBITI

KATIKA kuunga juhudi za  serikali awamu ya tano  katika kupambana na wimbi la umasikini hususan kwa upande wa vijana na wakinamama halmashauri ya Wilaya mpya ya Kibiti mkoani Pwani imejiwekea mipango madhubuti kwa ajili ya kuweza  kuwasaidia katika vikundi vya ujasiriamali kwa lengo la kuweza kuondokana na dhana ya kuwa tegemezi na badala yake wafanya kazi ili kuweza kueta maendeleo.

Hayo yalibainishwa na Mkurugenzi mtendaji wa  halmashauri ya Wilaya ya Kibiti Alvera Ndabagoyo wakati alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi katika mahojiano maalumu  kuhusiana na changamoto ya siku nyingi ya wimbi la umasikini kwa vijana wa wakinamama pamoja na mikakati yao waliyojiwekea ili kuondokana kabisa na hali hiyo.

Mkurugenzi huyo alisema kwamba kwa sasa anatambua kuna baadhi ya vijana na wakinamama katika Wilaya hiyo ya Kibiti wanakabiliwa na tatizo la kutokuwa na ajira hivyo uongozi wa halmashauri hiyo imeshaanza kufanya jitihada za hali na mali katika kuhakikisha fedha ambazo zitakuwa zikitengwa kwa ajili yao zinawafikiwa walengwa  ili waweze kuzifanyia shughuli halali za kimaendeleo  na kujipatia kipato.

“Kama unavyofahamu ndugu mwandishi wa habari nadhani umejionea wewe mwenyewe katika Halmashauri yetu hii ya Wilaya ya Kibiti ni mpya kwa sasa na haina muda mrefu, lanini pamoja na upya wake tumeshaanza kujiweka sana na watendaji wangu ili kuhakikisha kuwa vijana na wakinamama tunawawezesha kwa kuwapatia fedha endapo wakiwa katika vikundi ili kuweza kupamaba na wimbi la umasikini nadhani kwa hili tutaweza kufanikiwa  na kufikia malaengo tuliyojiwekea,”alisema Alvera.

Pia Alvera alibainisha kuwa katika mwongozo wa serikali inatakiwa kila halmashauri katika kila bajeti yake  ya  mwaka  inatenga  asilimia 10 cha fedha    kwa ajili ya kuweza  kuvisaidia vikundi mbali mbali vya wakinamama pamoja na vijana ili waweze kuendelea kufanya shughuli zao mbali mbali za kijasiriamali lengo ikiwa ni kuweza kupamabana na umasikini.

Aidha aliongeza kuwa ana imani kubwa endapo  vikundi vya vijana na wakinamama katika Wilaya ya Kibiti vikijiunga kwa pamoja na kuwezeshwa kwa kupatiwa fedha kwa ajili ya kufanyia biashara  vitaweza kufika mbali na kuweza kuleta mabadiliko  chanya ya kimaendeleo kuanzia ngazi za familia zao hadi kuwasaidia na wananchi wengine .

Katika hatua ngingine Mkurugenzi huyo alitoa wito kwa wananchi wote wa Wilaya ya Kibiti kuachana na kuwa na tabia ya kuwa tegemezi kila kukicha na badala yake sasa wabadilike na kujiunga katika vikundi mbai mbali vya ujasiliamari ili pindi fedha inapotolewa na halmahsuari iwe rahisi kuwafikia walengwa kuliko kuwa  mtu mmoja mmoja.

Hata hivyo Mkurugenzi huyo aliahidi kushirikiana bega kwa began a baraza la madiwani, watendaji, pamoja na wadau wa maendeleo katika kuhakikishwa wanapambana vilivyo katika kuzitatua kero na changamoto mbali mbali ambazo zimekuwa zikiwakabili  kwa kipindi kirefu wananchi wa Wilaya mpya ya Kibiti mkoani Pwani.

UJENZI WA DARAJA LA KIJICHI NA TUANGOMA KUANZA

$
0
0
Serikali ya Manispaa ya wilaya ya Temekee na kampuni ya Ujenzi ya China CRJE  wametiliana saini mkataba wa Ujenzi wa Daraja litakalo unganisha  eneo la kijichi na Tuangoma  wilayani humo.

Akizungumza katika hafla hiyo mwakilishi wa Mkuu wa wilaya ya Temeke   ambaye pia ni katibu tawala  Wilaya hiyo Hashim Komba  , amesema daraja hilo linajengwa ili kuondo usumbufu wanaoupata  wananchi wanaoishi  maeneo hayo kwa kuzunguka Kigamboni na kongowe wakati wa masika.

Aidha afafanua kuwa Daraja hilo litakuwa na urefu wa Mita 800 na barabara za mitaa zaidi ya kumi zenye urefu wa Kilomita 1.8   na  barabara  nyingine zenye urefu wa kilomita 84 zote zitajengwa kwa kiwango cha lami na kitapimwa viwanja zaidi ya mianane kuzunguka eneo  la mradi huo.

Naye Mkurugenzi wa kampuni ya Ujenzi CRJE Zhao Yefang ameshukuru kupewa kazi hiyo ana ameahidi kufanya kwa viwango kama walivyo jenga Daraja la Kigamboni watahakikisha ubora na thamani ya hela vinazingatiwa na ndani ya mwaka mmoja watakabidhi Daraja hilo.
Wakisaini Mkataba katikati ni Mstahiki Meya Wa Manispaa ya Ilala Bw Abadallah Chaulembo,Kulia ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke Bw Nassib Mbaga na Kushoto ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Ujenzi CRJE Bw Zhao Yefang
  Katibu mkuu wa Wilaya ya Temeke Bw Hashim Komba akiongea na Wananchi wa Kijichi kuhusu swala zima la Utengenezwaji wa Daraja hilo ili kuondoa Usumbufu wanaoupata wananchi kuzunguka Kigamboni na Kongowe wakati wa Msimu wa Masika.
Mstahiki Meya wa Temeke Bw Abdallah Chaulembo akizungumza na wananchi wa Kijichi kuhusu ujenzi wa Daraja unaotarajia kuanza mapema Mwaka huu katika Eneo hilo
Baadhi ya Wananchi wa Kijichi wakiwa Katika Mkutano huo.
 

WAKUU WA MASHIRIKA YA UMEME KUTOKA NCHI KUMI ZA EASTERN AFRICA WAKUTANA ARUSHA KUJADILI NAMNA YA KUUNDA MIFUMO YA USAFIRISHAJI UMEME KWA NCHI HIZO

$
0
0
Na Woinde Shizza,Arusha

Wakuu wa mashirika umeme kutoka katika nchi kumi za Afrika zinazozalisha umeme (Eastern Africa Power pool (EAPP) zimekutana jijini arusha kwa malengo ya kujadili mfumo wa usafirishaji wa umeme ikiwa ni pamoja na namna wananchi wao watakavyoweza pata nishati ya umeme kwa urahisi tofauti
na sasa .

Hayo yamesemwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Dkt.Juliana Palangyo alipokuwa akizungumza katika ufunguzi wa mkutano wa wakuu wa mashirika ya umeme katika nchi hizo za Eastern Africa power pool (EAPP) mapema leo.

Palangyo alisema kuwa lengo halisi ni kuweza kujadili mambo mbalimbali yahusuyo nishati ya umeme kwa watumiaji wake kwani kuna uwezekano mkubwa wa nchi zote zilizo kwenye umoja huo. 

Alisema kwa sasa yapo baadhi ya makampuni ambayo yalikuwa yanauza umeme kwa gharama kubwa hasa kwa wananchi ambao hawajapata huduma hiyo ya umeme lakini kupitia umoja huo wataweza kupata nishati hiyo kwa gharama nafuu.  "Hizi nchi za eastern tumekutana hapa ili tujadili namna ambayo tunaayo wanayoweza kutafuta namna ya kuzalisha umeme kwa bei nafuu na kisha nchi hiyo itaweza kuuza umeme kwa bei ndogo"aliongeza Palangyo. 

Hata hivyo kwa upande Kaimu Meneja Uhusiano wa Shirika la Tanesco,Bi Leila  Muhaji alisema kuwa katika mkutano huo pia watajadili namna ambavyo Tanzania itajenga njia ya usafirishaji wa umeme wa njia ya maji ambayo itatoka nchi ya Tanzania kwenda nchini Kenya,Zambia,pamoja na nchi nyingine .

Muhaji alisema kuwa Tanzania itanufaika na ujenzi wa njia hizo hivyo jamiiiitanufaika kwa kiwango kikubwa sana kama ilivyo kwenye nchi ambazozimeeendelea Duniani. 

"Hata hivyo mara baada ya mkutano huo,Wakuu wa nchi zinazozalisha umeme tunatarajia pia kuwepo na wadau wengine ambao ni Mawaziri kutoka nchi zote ambao nao sasa wataweza kuweka mambo sawa ili huduma iweze kumfikia mlengwa"aliongeza Muhaji

Alimalizia kwa kutaja nchi ambazo zina unda umoja huo kuwa ni Tanzania ,Kenya,Uganda ,Rwanda ,Burundi ,Sudan , Dr congo, Ethiopia ,Djbout, Libya pamoja na Egypt.

HAKI ELIMU YAZINDUA MPANGO KAZI WA MWAKA 2017-2021

$
0
0
 Mwenyekiti ya bodi ya taasisi ya Haki elimu nchini, Profesa Martha Qorro akifungua pazia kuashira uzinduzi wa dira ya mwaka 2017 mpaka 2021 nchini.
 Mwenyekiti ya bodi ya taasisi ya Haki elimu nchini, Profesa Martha Qorro akihutubia wakati wa mkutano wa uzinduzi wa Dira ya tasisi hiyo kuanzia 2017-2021.

 Mkurugenzi wa taasisi ya haki elimu nchini,John Kalaghe akizungumza wakati wa mkutano wa uzinduzi wa Dira ya haki elimu 2017-2021.

 Baadhi ya wahariri mbalimbali wa vyombo vya habari walioshirikikatika uzinduzi huo wakifatilia kwa makini.
 Picha ya Pamoja ya wajumbe wa bodi wa taasisi ya Haki elimu na wadau muhimu kwa tasisi hiyo.
 Picha ya pamoja ya watendaji wa taasisi ya Haki elimu na mkurugenzi wa tasisi hiyo John Kalaghe mara baada ya kumalizika kwa uzinduzi huo.
 Wadau wa vyombo vya habari na wahariri kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini wakifatilia kwa makini mjadala.
 Baadhi ya wanafunzi wakiwa na walimu wao wakifatilia mjadala kabla ya uzinduzi wa mpango kazi wa taasisi ya haki elimu.
Wanazuoni wakijadili jambo mara baada ya kumalizika kwa uzinduzi wa mpango kazi wa tasisi ya haki elimu kuelekea 2017-2021.
Viewing all 46397 articles
Browse latest View live




Latest Images