Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1106 | 1107 | (Page 1108) | 1109 | 1110 | .... | 1898 | newer

  0 0

  Mhakama ya mwanzo ya RUANGWA mkoani LINDI, Imewahukumu watu 21 kifungo cha kwenda jela miaka miwili au kulipa faini ya shilingi elfu 40 kwa kila mmoja.

  0 0

   Kamanda Muroto na wezake wakikagua bustani ya mboga.
   Wana JKT wakilima.
   Kamanda Muroto akiwaangalia wanaJKT katika shmba.
   Kamanda Muroto (kushoto) na wezake wakijadiliana jambo.
   Wana JKT wakilima shamba lao.
   Bwawa la maji yanayotumika kumwagilia kwenye bustani ya mboga.
   Makamanda wakiangalia bwawa lenye maji yanayotumika kumwagilia katika bustani ya mboga.
   Kamanda Muroto akiingia ndani ya nyumba wanayoishi wana JKT katika Kambi yao ya Lugwadu.
   Kamanda Muroto (wa tatu kushoto) na Makamanda wezake wakiwa katika nyumba wanayohishi  wana JKT.
   Mwenyekiti wa wana JKT,Palale Kiwango (kushoto) akizungumza na Makamanda eneo la shamba la Mahindi, Mbaazi na Karanga.
   Wana JKT kazini.
   Mwenyekiti wa wana JKT,Palale Kiwango (kushoto) akizungumza na Kamanda Muroto.
   Mwenyekiti wa wana JKT,Palale Kiwango (kushoto) akizungumza na Makamanda waliowatembelea.

   Hiki ni choo wanachotua wahitimu katika makazi yao.
   wahitimu wa JKT wakishusha chakula.
   Wahitimu wakishusha chakula kutoka ndani ya gari.
   Sehemu ya chakula.
   Kamanda Muroto akikabidhi Chakula akiwa na makamanda wezake na Mama Jamila Nzota akiangalia.
   Dada mhitimu wa JKT akiandaa chakula.
   Wahitimu wa JKT wakiingiza chakula ndani ya nyumba yao.
  Wahitimu wa JKT wakiingiza chakula ndani ya nyumba yao.

  0 0

  Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.

  Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam DIT, imesema kuwa katika kufikia uchumi wa viwanda lazima vijana waandaliwe kwa ujuzi wa kuweza kutumika katika sekta hiyo.

  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati wa akisaini makubaliano na Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera ,Bunge, Kazi, Ajira na Wenye Ulemavu, Mkuu wa Taasisi ya DIT, Profesa Preksedis Ndomba amesema sekta ya viwanda inahitaji watu wenye ujuzi hivyo Taasisi ya DIT itakwenda na kasi ya kufua vijana wenye kwenye mafunzo mbalimbali.

  Profesa Ndomba amesema kuwa makubaliano ni kwa ajili ya kuwapa mafunzo vijana 1000 katika chuo cha DIT Mwanza katika utengenezaji wa bidhaa za ngozi kutokana na Tanzania kuwa na mifugo mingi Afrika hivyo vijana watazalishwa na kuweza kujiajiri au kuajiriwa katika sekta ya ngozi.

  Amesema DIT itakuwa bega kwa bega na serikali katika kuwaandaa katika sekta ya viwanda wakiwa na ujuzi ambao utawezesha viwanda hivyo viweze kukua katika uzalishaji wa bidhaa mbalimbali.

  Nae Mkurugenzi wa Ajira wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera ,Bunge, Kazi, Ajira na Wenye Ulemavu, Ally Msaki amesema makubaliano hayo yatakuwa endelevu kutokana na nia ya serikali katika kufikia vijana kuwa na ujuzi ambao unaweza kutumika na taifa likapata maendeleo.

  Amesema katika utafiti uliofanywa na hiyo pamoja na Ofisi ya Taifa ya Takwimu, inaonyesha kuwa watu walioko katika soko la ajira wanaujuzi mdogo.

  Msaki amesema katika uandaji huo ni pamoja na VETA kuwa na mafunzo mbalimbali ya kutambua watu wenye ujuzi na kuwapa vyeti ili waweze kutambulika katika kufanya shughuli zao.

  Aliongeza kuwa katika bajeti ya mwaka wa fedha 2017/2018 serikali imetenga bilioni 15 kwa ajili ya kutolea mafunzo kwa vijana ili waweze kuwa sehemu soko la ajira.
  Mkuu wa Taasisi ya DIT, Profesa Preksedis Ndomba akizungumza na waandishi wa habari juu ya mafunzo wanayotoa katika taasisi hiyo na umuhimu wa ushiriki katika uchumi wa viwanda leo jijini Dar es Salaam.
  Mkuu wa Taasisi ya DIT, Profesa Preksedis Ndomba na Mkurugenzi wa Ajira wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera ,Bunge, Kazi, Ajira na Wenye Ulemavu, Ally Msaki wakisaini makubaliono ya Mafunzo kwa vijana 1000 katika Chuo cha DIT Mwanza.
  Mkuu wa Taasisi ya DIT, Profesa Preksedis Ndomba akibadilishana hati za makubaliano na Mkurugenzi wa Ajira wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera ,Bunge, Kazi, Ajira na Wenye Ulemavu, Ally Msaki leo jijini Dar es Salaam.
  Sehemu ya waandishi habari wakiwa katika mkutano huo.

  0 0

   Madaktari Bingwa wa Upasuaji wa Kituo cha Moyo cha Jakaya Kikwete (JKCI), Dk. Evarist Nyawawa (kushoto) na  Dk Hussein Hassanali wakimfanyia upasuaji mmoja wa wagonjwa ambapo wengine huwapandikiza mishipa ya damu kwenye moyo juzi katika kituo hicho kilichopo Muhimbili, Dar es Salaam.PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
   Madaktari mbalimbali wakiendelea na kazi katika chumba cha upasuaji moyo
   Mmiliki wa Blog hii ya Kamanda wa Matukio, Richard Mwaikenda (katikati) akiwa na wanahabari wenzie wakijiandaa kufanya coverage kwenye chumba cha upasuaji
   wakiendelea na upasuaji
   Mtaalamu wa Usingizi wa Kituo cha Moyo cha Jakaya Kikwete (JKCI), Dk. Edwin Lugazia akitumia kompyuta kuhakikisha hakuna hitilafu yoyote inatokea kwa mgonjwa aliyekuwa anapandikizwa mishipa ya damu kwenye moyo  katika kituo hicho kilichopo Muhimbili, Dar es Salaam.

   Watalaaamu wa mashine ya mapafu na moyo Sophia Lukonge na Sylvester Mbunda wakiwa makini kuhakikisha mashine hizo hazipati hitilafu   Wasaidizi wa chumba cha upasuaji wakiwa wamejipanga tayari kwa kazi. Kutoka kulia ni Hildegard Karau, Hania Bwahama na Faustina Mwapingo
  0 0


  Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji nchini-TIC,Clifford Tandari akizungmza na Globu ya Jamii kuhusu Kongamano la Uwekezaji baina ya Makampuni ya Tanzania na Uturuki litakalofanyika Januari 23 mwaka huu katika Ukumbi wa Mikutano wa Benki Kuu ya Tanzania(BOT).

  Kongamano hilo litahususha Makampuni 157 kutoka Uturuki ambayo yatakuwa katika Sekta mbalimbali kama vile Nishati, Madini, Afya, Uchukuzi, Utalii, Maliasili, Kilimo, Mifugo, Chakula na Vinywaji.Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.

  0 0

   Mwenyekiti wa  Kamati ya  Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC)  Mhe. Albert Obama (Mb) akizungumza wakati Kamati yake ilipokwenda kukagua mradi wa Ujenzi wa Nyumba katika eneo la Kawe na Morroco Jijini Dar es Salaam.
   Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba NHC Bw. Nehemia Mchechu akiwaelezea Wajumbe wa Kamati ya PIC kuhusu mradi wa ujenzi wa Nyumba katika eneo la Kawe.
   Mwenyekiti wa  Kamati ya  Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC)  Mhe. Albert Obama (Mb) akielezea jambo wakati Kamati yake ikikagua ujenzi wa nyumba unaofaywa na NHC katika eneo la Kawe
  Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba NHC Bw. Nehemia Mchechu akifafanua jambo kwa Wajumbe wa Kamati ya PIC wakati wakikagua ujenzi wa Nyumba katika eneo hilo la Kawe.
  (Picha na Ofisi ya Bunge)


  0 0

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii Morogoro.

  Timu ya Simba imeshindwa kuondoka na ushindi kwenye Uwanja wa Jamhuri Mjini Morogoro  baada ya kulazimishwa sare ya kutokufungana na wakata miwa wa Morogoro  mtibwa Sugar mechi iliyochezwa leo.

  Baada ya matokeo hayo Simba wanaendelea kusalia kileleni wakiwa na alama 45 akiwa  mebel kwa alama mbili dhidi ya mahasimu wao Yanga wenye alama 43 baada ya mechi yao ya jana kushinda dhidi ya Majimaji Songea.

  Baada ya mchezo huu Simba wanakutana na Azam Januari 28 kwenye Uwanja wa Taifa.
  Henry Joseph akipambana na mchezaji wa Simba Mwinyi Kazimoto katika mchezo wao wa ligi kuu uliomalizika kwa suluhu ya kutokufungana mechi iliyochezwa kwenye Uwanja wa Jamhuri Mkoani Morogoro.
   Kipa wa Mtibwa akiondosha mpira langoni mwake  katika mchezo wao wa ligi kuu uliomalizika kwa suluhu ya kutokufungana mechi iliyochezwa kwenye Uwanja wa Jamhuri Mkoani Morogoro.
  Wachezaji wakiwa wanasubiri kupigwa kwa mpira langoni mwa Simba.
   Mshambuliaji wa Simba Shiza Kichuya akiwa amemfanyia madhambi Rashidi Mandawa  katika mchezo wao wa ligi kuu uliomalizika kwa suluhu ya kutokufungana mechi iliyochezwa kwenye Uwanja wa Jamhuri Mkoani Morogoro.


   Mshambuliaji wa Simba Juma Luizio akiwa anapambana na beki wa Mtibwa Henry Joseph  katika mchezo wao wa ligi kuu uliomalizika kwa suluhu ya kutokufungana mechi iliyochezwa kwenye Uwanja wa Jamhuri Mkoani Morogoro.
   Kiungo wa Mtibwa Ally Shomari akipambana na beki wa Simba Hamad Juma  katika mchezo wao wa ligi kuu uliomalizika kwa suluhu ya kutokufungana mechi iliyochezwa kwenye Uwanja wa Jamhuri Mkoani Morogoro.
   Mshambuliaji wa Simba Laudit Mavugo akiutuliza mpira pembeni mwa mabeki wa Mtibwa  katika mchezo wao wa ligi kuu uliomalizika kwa suluhu ya kutokufungana mechi iliyochezwa kwenye Uwanja wa Jamhuri Mkoani Morogoro.
  Kipa wa Simba Daniel Aggey akidaka mpira uliopigwa na Rashid Mandawa wa Mtibwa Sugar  katika mchezo wao wa ligi kuu uliomalizika kwa suluhu ya kutokufungana mechi iliyochezwa kwenye Uwanja wa Jamhuri Mkoani Morogoro.Picha zote na Zainab Nyamka.

  0 0

  Mkuu wa wilaya ya Iringa, Richard Kasesela(kulia) akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa Dr. William Mafwele, mwenye miwani ni mhandisi wa Manispaa, Eng. Lihamba .

  Mkuu wa wilaya ya Iringa, Richard Kasesela leo alitembelea mradi wa ujenzi wa daraja la Tagamenda linalofadhiriwa na serikali ya Uingereza kupitia shirika lake la DFID. Wakati wa ziara hiyo aliyoongazana na Mkurugenzi wa manispaa ya Iringa Dr William Mafwele pamoja na mhandisi wa Manispaa, Eng. Lihamba.

   Akipokea taarifa ya kazi, aliambiwa kuwa Mhandisi msimamizi wa Mradi amekuwa kikwazo cha utendaji na utekelezaji wa majikumu ikiwemo hata kunyanyasa wafanyakazi. Ndio maana mradi umekuwa unasua sua.

   Mkuu wa wilaya aliamuru Mhandisi Raymond Swai aondolewe haraka na asikanyage kabisa eneo la mradi akionekana mita 100 achukuliwe hatua. " 
  OCD mtafute haraka Raymond Swai mpe amri amri hii kama anabisha atatakiwa aondoke Iringa" Alisema Mkuu wa wilaya. Muda huo saa 5 asubuhi bado Mhandisi huyo alikuwa hajafika kazini kufanya kazi na kupelekea kazi kutoanza kwa wakati.

  Mkurugenzi wa Manispaa Dr Mafwele alionyesha wasiwasi wa mradi kumalizika kwa wakati kwani mkandarsai amekuwa anaishiwa vifaa mara kwa mara . Mkuu wa wilaya alimuagiza Mkandarasi kuleta vifaa haraka wiki ijayo atapita kukagua tena. 
  Mradi huo wenye thamani wa 5.3 bilioni unatarajiwa kukamilika mwisho wa mwezi wa 3 kama mkandarasi atafuata ratiba.​

  0 0


    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimuapisha Profesa Ibrahim Hamisi Juma kuwa Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumatano Januari 18, 2018.  Anayeshuhudia kushoto ni Jaji Mkuu mstaafu Mohamed Chande Othman. 
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimkabidhi nyenzo za kazi baada ya kumuapisha Profesa  Ibrahim Hamisi Juma kuwa Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumatano Januari 18, 2018. 
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimpongeza baada ya kumuapisha Profesa  Ibrahim Hamisi Juma kuwa Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumatano Januari 18, 2018. 
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan  na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Katibu Mkuu Wizara ya Sheria na Katiba Profesa Sifuni Mchome na Naibu wake Mhe. Amon Mpanju wakiwa katika picha ya pamoja na majaji wa mahakama ya Rufaa, Majaji wa Mahakama kuu baada ya kumuapisha Profesa  Ibrahim Hamisi Juma kuwa Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumatano Januari 18, 2018. 
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, katika picha ya pamoja na majaji wa mahakama ya Rufaa na Majaji wa Mahakama kuu baada ya kumuapisha Profesa  Ibrahim Hamisi Juma kuwa Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumatano Januari 18, 2018. 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, katika picha ya pamoja na watendaji wa Mahakama baada ya kumuapisha Profesa  Ibrahim Hamisi Juma kuwa Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumatano Januari 18, 2018. 

  PICHA NA IKULU

  0 0  0 0

  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza na uongozi na baadhi ya wafanyakazi wa Clouds Media group wakati alipofanya ziara kujionea utendaji kazi wake na changamoto wanazozipata katika kutekeleza majukumu yao.

  Waziri wa Habari utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza na uongozi na baadhi ya wafanyakazi wa Mlimani Media wakati alipofanya ziara kujionea utendaji kazi wake na changamoto wanazozipata katika kutekeleza majukumu yao.

  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akiangalia sehemu mbalimbali za studio za Mlimani Tv na Redio iliyo chini ya Mlimani Media wakati alipofanya ziara kujionea utendaji kazi wake na changamoto wanazozipata katika kutekeleza majukumu yao.

  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza na uongozi na baadhi ya wafanyakazi wa Uhuru Production inayomiliki vituo vya azam Tv na Redio wakati alipofanya ziara kujionea utendaji kazi wake na changamoto wanazozipata katika kutekeleza majukumu yao.

  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akiangalia sehemu mbalimbali za studio za Azam Tv na Redio iliyo chini ya Uhuru Production wakati alipofanya ziara kujionea utendaji kazi wake na changamoto wanazozipata katika kutekeleza majukumu yao.

  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza katika Kipindi cha Alasiri Lounge kinachorushwa na Azam Tv iliyo chini ya Uhuru Production wakati alipofanya ziara kujionea utendaji kazi wake na changamoto wanazozipata katika kutekeleza majukumu yao.

  Picha zote na Raymond Mushumbusi WHUSM.


  ………….


  Na Beatrice Lyimo-MAELEZO

  Serikali imevitaka vyombo vya habari nchini kuwa chachu ya mabadiliko katika kipindi hiki ambacho nchi inaelekea katika uchumi wa kati.

  Hayo yamesemwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye katika ziara yake kwa vyombo vya habari vya Clouds, Mlimani na Azam, ziara inayolenga kuimarisha mahusiano yaliyopo baina ya Serikali na vyombo vya habari nchini.

  “Serikali ya Awamu ya Tano imejikita katika ajenda mbalimbali ikiwemo kutoka katika hali ya uchumi tuliona nao sasa kuelekea uchumi wa kati hivyo vyombo vya habari vinatakiwa kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha suala hili linawafikia na kuleta uelewa kwa wananchi”alisema Mhe. Nnauye.

  Waziri Nape alisisitiza kuwa, kumekuwa na mitazamo tofauti katika vichwa vya wananchi au jamii kwa ujumla kuhusu suala zima la kuelekea uchumi wa kati, hivyo ni jukumu la vyombo vya habari nchini kuweza kuwaelewesha nini maana halisi ya uchumi unaolengwa kuufikiwa.

  “tumesikia ya kwamba uchumi wa nchi umekuwa kwa asilimia saba, mwananchi wa kawaida hawezi kuwa na uelewa wa kujua ni vipi uchumi wa nchi unakuwa, hivyo vyombo vya habari vina mchngo mkubwa katika kuifanya jamii kuwa uelewa juu ya ukuaji wa uchumi” alisisitiza waziri Nape.

  Mbali na hayo Waziri Nape amesema kuwa vyombo vya habari ni chanzo cha wananchi kuwa kitu kimoja katika kulinda amani ya nchi na utamaduni uliopo, hivyo vina budi kuzidi kutunza utamaduni uliopo pamoja na kuwafanya wananchi kupenda utamaduni wao.

  Waziri Nape alisisitiza kuwa vyombo vya habari viifanye jamii kwa ujumla kuwa na utamadumi hasa wa utamaduni wa ulipaji wa kodi katika nyanja tofauti na kuwa wazalendo kwa maendeleo ya nchi.

  “sisi kama wanahabari na vyombo vya habari kwa ujumla tunatakiwa kutengeneza vijana ambao kwao kulipa kodi ni fahari, vijana ambao kazi kwao ni heshima pamoja na kutengeneza vijana ambao hujivunia uzalendo wa nchi yao”Alisema Waziri Nape.

  Hata hivyo Waziri Nape ameahidi kuendeleza ushirikiano uliopo baina ya Serikali na vyombo vya habari nchini katika nyanja tofauti ikiwemo utoaji wa habari muhimu za utekelezaji wa Serikali katika kuleta maendeleo nchini.

  0 0

  Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Merard Kalemani,(kushoto) akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza( kulia) mara baada ya kuwasili mkoani huo kwa ziara ya kukagua utekelezaji wa Miradi ya Umeme Vijijini katika Mkoa huo.
  Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Merard Kalemani,(kulia) akisamilia na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali ( PAC), Livingstone Lusinde( kulia) walipowalisi mkoani wa Iringa, kwa ziara ya kukagua utekelezaji wa Miradi ya Umeme Vijijini mkoani huo.
  Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Merard Kalemani,(kushoto) na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Livingstone Lusinde( kulia) wasikiliza hoja za Wajumbe wa Kamati ya PAC, (hawapo pichani) kabla ya kuanza ziara ya kukagua utekelezaji wa Miradi ya Umeme Vijijini mkoani Iringa.
  Wajumbe wa Kamati ya PAC, wakisikiliza taarifa ya Mkoa wa Iringa, kabla ya kuanza ziara ya kukagua utekelezaji wa MIRADI ya Umeme vijijini mkoani Iringa.
  Wajumbe wa Kamati ya PAC,wakikagua Miradi ya Umeme Vijijini katika kijiji cha Nyamahana mkoani Iringa.
  Mjumbe wa Kamati ya PAC, Shally Raymond( kulia) akisisitiza jambo kwa wanafunzi wa shule ya Sekondari Idodi, wakati wa ziara ya kukagua utelezaji wa Miradi ya Umeme Vijijini.
  Mwenyekiti wa Kamati ya PAC, Livingstone Lusinde ( kushoto) akiruka pamoja na wanafunzi wa shule ya Sekondari Idodi, wakati wa ziara ya kukagua Miradi ya Umeme Vijijini.
  Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Merard Kalemani,(kulia) akisalimiana na wanafunzi wa shule ya Sekondari Idodi, wakati wa ziara ya kukagua Miradi ya Umeme Vijijini.

  ………………………..


  Na Zuena Msuya, Iringa

  Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) imeridhishwa na utekelezaji wa Miradi ya Umeme Vijijini, Unaotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) katika Awamu ya kwanza na ya Pili ili kuona thamani halisi ya matumizi ya fedha za Serikali katika mradi huo.

  Mwenyekiti wa PAC, Livingstone Lusinde alisema hayo mkoani Iringa wakati wa ziara ya kukagua utekelezaji wa mradi wa REA, katika vijiji na Taasisi mbalimbali zilizopitiwa na Mradi huo.

  Lusinde alifafanua kuwa wameridhishwa na utekelezaji wa miradi hiyo baada ya kuona miundombinu iliyotumika na maendeleo ya wananchi katika maeneo ambayo yamepitiwa na miradi hiyo.

  ” Tumepita katika vijiji mbalimbali hapa Iringa ambayo nimepitiwa na REA,tumeona namna ambavyo mradi huo umetekelezwa na tumeona miundombinu iliyotumika na maendeleo yake hivyo hatuna budi kusema wazi kuwa tumeridhishwa na utekelezaji wa mradi huu”, Alisema Lusinde.

  Lusinde aliwasisitiza wakandarasi wanaotekeleza Mradi wa Umeme vijijini, kutumia miundombinu imara inayokwenda sambamba na thamani halisi ya matumizi ya fedha za Serikali katika kutekeleza wa miradi hiyo ili kutimiza malengo yaliokusudiwa na kuondoa hasara za makusudi zinazoweza kujitokeza.


  Vilevile aliwataka wakandarasi hao kukamilisha zoezi za kuwaunganisha na huduma ya umeme wananchi na Taasisi zilizoomba huduma hiyo katika maeneo machache yaliyosalia ili kila mwananchi aliyeomba huduma hiyo aweze kuipata kwa wakati na kuitumia.

  Kwa upande wake Naibu Waziri wa Nishati na Madini DKt. Medard Kalemani alisema kuwa Awamu ya Tatu ya utekelezaji wa Mradi wa Umeme wa Vijijini utashirikisha Viongozi Serikali za mitaa, Madiwani,Wabunge, Wakuu wa Wilaya na Wakuu wa Mikoa.

  Alifafanua kuwa lengo la kufanya hivyo ni kutoa fursa kwa wananchi kutoa vipaumbele vya maeneo wanayotaka kufikiwa kwa huduma ya umeme kwa wakati na kuvifikia vijiji vyote nchini.

  ” Mradi wa REA Awamu ya Tatu utakuwa shirikishi, kwakuwa kabla ya mkandarasi kuanza kazi yake, atatakiwa kuwasiliana na Viongozi wa Serikali ya mitaa, Madiwani, Wabunge , Wakuu wa Wilaya na Wakuu wa Mikoa ili wao watoe vipaumbe cha maeneo wanayotaka kufikiwa na mradi huo”, alifafanua Dkt. Kalema.

  Dkt. Kalemani alibainisha kuwa utaratibu huo utawezesha kuviunganisha vijiji vyote nchini na huduma ya umeme ili kutimiza azma ya Serikali ya kufikia ya uchumi wa Kati ifikapo mwaka 2025.

  Kamati ya Kudumu ya Hesabu za Serikali ( PAC) inafanya ziara ya kukagua Miradi ya Umeme Vijijini inayotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA)kwa kushirikiana na Shirika la Umeme Nchini ( Tanesco) kwa lengo la kuona thamani hali matumizi ya fedha ya Serikali katika mradi huo.

  0 0

  Afisa  maendeleo ya  jamii Manispaa   ya  Iringa  Josephina Mwaipopo  akiwa na mtoto aliyebakwa
  DC  Richard  kasesela  akiwa amemnyanyua  mtoto  aliyebakwa  akitokanae kuchukuliwa  vipimo Hospitali ya  Rufaa ya  mkoa wa Iringa

   Watuhumiwa  baba  na mwanae  wakiwa   chini ya  ulinzi

  Na MatukiodaimaBlog

   YAWEZEKANA ikawa  ni  moja ya  sababu ya  mvua  kuchelewa kunyesha  mkoani Iringa tofauti  na  ilivyozoeleka  miaka  mingine  ni  kutokana na laana kama  hizi  baada  ya kikosi  maaalum kinachoongozwa   mkuu  wa  wilaya ya  Iringa  Richard Kasesela  kwa  kushirikiana na OFM kufanikiwa  kumkamata  kijana Emmanuel Mkiwa  (19) kwa tuhuma  za kumbaka mara kwa mara mdogo wake  wa miaka (4)


  Imedaiwa   kuwa kijana  huyo  ambae  ni mwenyeji  wa mtaa  wa Omary  Matrekta kata ya  Mtwivila  katika  Manispaa ya  Iringa alikuwa akiishi nyumba  moja  na babake pamoja na wadogo  zake watatu  wawili  wa  kiume na mmoja  ni  mtoto   huyo  wa  miaka 4  ambaye alitelekezwa  na mamake  mzazi kutokana na mambo ya  kifamilia kati  yake baba  wa  mtoto .

  Mashuhuda  wa  tukio   hilo  lililotokea January 16 majira ya  saa 2 usiku walimweleza  mwandishi  wa  OFM  Iringa  kuwa kijana   huyo mara  kwa  mara  alikuwa  akimbaka  mdogo wake  huyo  ambae baba  mmoja  na mama  tofauti kabla  ya  mtoto   huyo kuwaeleza majirani   kuwa kakake  huyo  amekuwa akimkandamiza na  kijiti sehemu  zake  za  siri (Akimbaka)

  Kutokana na  maelezo ya  mtoto   huyo ndipo taarifa  za  raia  wema  hao  zilipofikishwa kwa mkuu  wa  wilaya  na OFM na  kuamua  kufika  katika eneo la  tukio na  kufanikiwa  kumkamata kijana   huyo  na baba mzazi  wa  watoto  hao  Shukuru Mkiwa kwa malezi mabaya  ya  watoto.

  Akizungumza  baada ya  kukamatwa  kwa  kijana   huyo  mkuu  wa  wilaya ya  Iringa Richard  Kasesela   pamoja na  kuwashukuru raia wema  kwa  kufikisha taaarifa  ya  kunyanyaswa  kwa mtoto   huyo  bado  alitoa wito kwa  wananchi  wengine  ambao  wanataarifa  za  kunyanyaswa  kwa  mtoto  yeyote  katika  wilaya ya  Iringa  kutoa taarifa  ili  wahusika   wakamatwe  na  kufikishwa  katika  vyombo  vya sheria.

  Kasesela  alisema  kuwa uchunguzi   uliofanywa baada ya  vipimo katika  Hospitali ya  Rufaa ya  mkoa  wa  Iringa umeonyesha mtoto   huyo kashaondolewa  usichana wake   na  hivyo kulazimika  kulazwa  kwa  matibabu  katika Hospitali   hiyo huku akiahidi kumsaidia mtoto  huyo  kumsomesha .

  Alisema  kuwa yawezekana  moja ya  sababu ya  mvua  kuchelewa  kunyesha katika  mkoa  wa Iringa  ni  pamoja  na matukio ya  kinyama kama haya ya ubakaji  watoto na  kuwa  hatakubali kuona mbakaji  anaendelea   kuishi  uraiani wilaya ya  Iringa kwani tayari  mkuu  wa  mkoa  wa  Iringa Amina Masenza  kupitia  kikao  cha makati ya  ushauri ya  mkoa (RCC)  aliagiza wabakaji wote wasakwe kwa udi na uvumba na yeye ameanza  kutekeleza agizo hilo.

  Japo  alisema alishangazwa  na hatua ya baba  mzazi wa  kijana  huyo  kumficha mbakaji ndani na  kudanganya  kuwa  hayupo wakati  kijana  wake  alikuwepo  ndani hivyo  mzazi  huyo  kukamatwa pamoja na kijana  wake yeye kwa  kosa la  kumchifa  mharifu  na kijana wake kwa kosa la ubakaji .

  "Hiki  ni  kikosi  kamili  ambacho kitaendelea  kuendesha  misako  mbali mbali kwa kushirikiana na oparesheni  Fichua Maovu (OFM) ya Global Publishers hivyo kwa  yeyote  anayejua  wapi  mtoto anafanyiwa  vitendo  vya kikatili piga  simu hii mwandishi wa OFM Iringa 0754 026 299 tutakufikia ulipo na  kuchukua  hatua"

  Jeshi la  polisi  mkoa  wa Iringa  kupitia kwa  kamanda wa  polisi  mkoa (RPC) Julius Mjengi limethibitisha  kukamatwa kwa mtuhumiwa   huyo na  kuwa baada ya  upalelezi  atafikishwa mahakamani  huku  likiwataka  wananchi  kuendelea  kufichua  waharifu  zaidi


  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan  Januari 18, 2017, amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Bw. Masha Mshomba Ikulu jijini Dar es Salaam. Pichani, Makamu wa Rais, akipiga picha na Bw. Mshomba mara baada ya mazungumzo yao. (PICHA NA OFISI YA MAKAMU WA RAIS).
  Makamu wa Rais, Mh. Samia Suluhu Hassan, (kulia), akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Bw. Masha Mshomba Ikulu jijini Dar es Salaam, Januari 18, 2017
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan, (kulia), akimsikiliza Mkurugenzio Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Bw. Masha Mshomba, Ikulu jijini Dar es Salaam, Januari 18, 2017.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan, akimkaribisha ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mmkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Bw. Masha Mshomba Januari 18, 2017.

  0 0

  Na Fatma Salum-MAELEZO

  Serikali imepanga kutumia bilioni 15 kuwapatia vijana stadi za kazi zitakazowawezesha kujiajiri na kushiriki katika ujenzi wa uchumi wa Viwanda.

  Kauli hiyo imetolewa leo Jijini Dar es salaam wakati wa kutiliana saini makubaliano ya ushirikiano kati ya Taasisi ya Teknolojia Dar es saalam (DIT) na Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu.

  Akizungumzia makubaliano hayo Mkurugenzi wa Ajira kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Bw. Ally Msaki amesema kuwa yatasaidia kuiwezesha Taasisi hiyo kutoa mafunzo kwa vijana hasa ya kuzalisha bidhaa zitokanazo na ngozi ili waweze kushiriki katika ujenzi wa uchumi wa viwanda.

  “Vijana 1000 wataanza kupata mafunzo mwezi Februari mwaka huu na yatakayohusu utengenezaji wa bidhaa za ngozi na program hii ipo ndani ya mpango wa miaka mitano.” Alisema Msaki.

  Mafunzo hayo ya stadi za kazi kwa vijana yatagharimiwa na Serikali na yatahusisha vijana walio katika mfumo rasmi na wale wasio katika mfumo rasmi wa elimu lengo likiwa ni kuwakwamua vijana ili washiriki kikamilifu katika ujenzi wa taifa.

  Akifafanua Msaki alisema kuwa dhamira ya Serikali ni kuwawezesha vijana baada ya mafunzo hayo kujiajiri na kuwaajiri wenzao hivyo kuondokana na tatizo la ajira na kuongeza nguvukazi ya taifa kwenye uzalishaji.

  Kwa upande wake Mkuu wa Taasisi ya Teknolojia Dar es salaam (DIT) Prof.Preksedis Ndomba alibainisha kuwa Taasisi hiyo imejipanga vyema kuwawezesha vijana kwa kutoa mafunzo yanayoendana na mahitaji ya soko na kuweka msisitizo katika mafunzo kwa vitendo.

  Taasisi ya Teknolojia Dar es salaam (DIT) ipo imedhamiria kutekeleza kwa vitendo azma ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kujenga uchumi wa viwanda na kufikia uchumi wa kati.

  Mkuu wa Taasisi ya Teknolojia Dar es salaam (DIT) Prof.Preksedis Ndomba (kushoto) na Mkurugenzi wa Ajira kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Bw. Ally Msaki wakisaini makubaliano ya ushirikiano kati ya Serikali na Taasisi hiyo utakaowezesha vijana kupata mafunzo ya uzalishaji wa mazao ya ngozi katika Taasisi hiyo Kampasi ya Mwanza ili kuchochea uchumi wa viwanda nchini.
  Mkuu wa Taasisi ya Teknolojia Dar es salaam (DIT) Prof.Preksedis Ndomba (kushoto) akibadilishana hati ya makubaliano ya ushirikiano na Mkurugenzi wa Ajira kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Bw.Ally Msaki (kulia), makubaliano hayo ni kati ya Taasisi hiyo na Serikali ili kuwawezesha vijana kupata mafunzo ya uzalishaji wa mazao ya ngozi.
  Mkuu wa Taasisi ya Teknolojia Dar es salaam (DIT) Prof.Preksedis Ndomba (kulia) akifafanua kwa waandishi wa Habari kuhusu mikakati ya taasisi hiyo kushiriki katika ujenzi wa uchumi wa viwanda kwa kuzalisha wataalamu wenye ujuzi na stadi zinazoendana na mahitaji ya soko. Kushoto ni Meneja Rasilimali Watu na Utawala wa DIT Bw. Sebastian Ndahani.
  Mkurugenzi Msaidizi anayeshughulikia Taarifa za Soko la Ajira Bw.Ahmed Makbel toka Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu akieleza umuhimu wa vijana kutumia fursa zinazotolewa na Serikali katika kuwajengea uwezo ili waweze kushiriki katika ujenzi wa uchumi wa Viwanda. Kushoto ni Mkurugenzi wa Ajira, Bw. Ally Msaki kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu. 
  Mkurugenzi Msaidizi anayeshughulikia Taarifa za Soko la Ajira Bw.Ahmed Makbel toka Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu akieleza umuhimu wa vijana kutumia fursa zinazotolewa na Serikali katika kuwajengea uwezo ili waweze kushiriki katika ujenzi wa uchumi wa Viwanda. Kushoto ni Mkurugenzi wa Ajira, Bw. Ally Msaki kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu.Picha na Frank Mvungi (MAELEZO)

  0 0

  Mkurugenzi wa sekta ya uzalishaji kutoka Jumuia ya Afrika Mashariki Jean Baptiste Havugimana akimkabidhi Mfamasia Mkuu wa Zanzibar Habib A. Shariff Mashine 6 za uchunguzi wa Dawa kutoka Ujerumani kwa kupitia mradi wa EAC, MRH Projat.
  Professa. Richard Jahnke kutoka Ujerumani akitoa maelezo ya matumizi ya vifaa vipya vya uchunguzi wa dawa (Minilab Kid) kwa washiriki wa mafunzo ya siku 5 ya uchunguzi wa dawa kutoka nchi za Afrika Mashariki yaliyofanyika Mbweni.

  Washiriki wa mafunzo ya uchunguzi wa dawa kujua kuwa ziko salama kwa matumizi ya binadamu wakiwa katika mafunzo ya vitendo yaliyofanyika katika Kitivo cha Madaktari cha Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar kilichopo Mbweni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
  kurugenzi wa sekta ya uzalishaji kutoka Jumuia ya Afrika Mashariki Jean Baptiste Havugimana akimkabidhi cheti mshiriki wa mafunzo hayo, Hidaya Juma ambae ni Mratibu wa Mradi wa uwiano wa udhibiti wa dawa wa nchi za Afrika Mashariki ambae pia ni Mfamasia kutoka Bodi ya Chakula, Dawa na Vipodozi Zanzibar.
  Washiriki wa mafunzo ya uchunguzi wa Dawa kujua kama ipo salama kawa matumizi ya binadam kutoka nchi wanachama wa Afrika Mashariki wakiwa katika picha ya pamoja na wakufunzi wao na walikwa.Picha na Makame Mshenga.

  0 0

  shinda-nyumba-awamu-ya-pili-1
  Meneja Mkuu wa Kampuni ya Global Publishers, Abdallah Mrisho akimkaribisha Mgeni Rasmi, wanahabari na wageni wengine kwenye hafla fupi ya Uzinduzi wa Shindano la Bahati nasibu ya Shinda Nyumba Awamu ya Pili ya Kampuni hiyo.
  shinda-nyumba-awamu-ya-pili-2
  Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Global Publishers, Eric Shigongo, Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji na Sheria wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, James Mbalwe na Kiongozi Mwandamizi wa bodi hiyo, Sadick.
  shinda-nyumba-awamu-ya-pili-3
  Abdallah Mrisho akitoa maelekezo ya namna ambavyo mshiriki wa shindano hilo anapaswa kufanya. shinda-nyumba-awamu-ya-pili-4shinda-nyumba-awamu-ya-pili-7Eric Shigongo, akitoa ufafanuzi kuhusu maandalizi maboresho yaliyofanyika kwenye Shinda Nyumba Awamu ya Pili.shinda-nyumba-1
  Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Global Publishers, Saleh Ally akifuatilia kwa karibu uzinduzi huo.shinda-nyumba-2
  shinda-nyumba-3
  Wafanyakazi wa Kampuni ya Global Publishers, wageni na waandishi wa habari wakifuatilia uzinduzi huo.
  shinda-nyumba-awamu-ya-pili-8Mrisho akimkaribisha Bwana Mbalwe.shinda-nyumba-awamu-ya-pili-9shinda-nyumba-awamu-ya-pili-10James Mbalwe akizungumza jambo wakati alipozindua Shinda Nyumba Awamu ya Pili ya Global Publishers.
  shinda-nyumba-awamu-ya-pili-12 Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji na Sheria wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, James Mbalwe (katikati) akizindua Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba Awamu ya Pili na kumkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Global Publishers, Eric Shigongo kipeperushi chenye maelekezo ya namna ya kushiriki.
  shinda-nyumba-awamu-ya-pili-11James Mbalwe, akimkabidhi Mrisho kipeperushi.shinda-nyumba-awamu-ya-pili-13....Akimkabidhi kipeperushi Bwana Sadick.shinda-nyumba-awamu-ya-pili-14James Mbalwe na viongozi wa Global Publishers wakielekea kwa wanahabari kwa ajili ya kuwagawia vipeperushi hivyo.shinda-nyumba-awamu-ya-pili-15shinda-nyumba-awamu-ya-pili-16shinda-nyumba-awamu-ya-pili-17James Mbalwe akiendelea kugawa vipeperushi.shinda-nyumba-awamu-ya-pili-18Wanahabari wakifuatilia na kuchukua matukio wakati wa hafla hiyo.shinda-nyumba-awamu-ya-pili-19Mwanahabari akiuliza swali kwa Meneja, Abdallah Mrisho.shinda-nyumba-awamu-ya-pili-20
  Mwandishi wa Kituo cha Televisheni cha Channel 10, Said Makala akiuliza swali kwa Mkurugenzi, Eric Shigongo.shinda-nyumba-awamu-ya-pili-21shinda-nyumba-awamu-ya-pili-22Baada ya kuzindua Shinda Nyumba Awamu ya Pili.shinda-nyumba-awamu-ya-pili-24
  shinda-nyumba-awamu-ya-pili-25Viongozi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Viongozi wa Kampuni ya Global Publishers pamoja na wafanyakazi wake na wanahabari waliofika kwenye uzinduzi huo wakiwa, hapa wakiwa kwenye picha ya pamoja nje ya Lango Kuu la Ofisi za Global Publishers.shinda-nyumba-awamu-ya-pili-26shinda-nyumba-awamu-ya-pili-27Sebene likiuungurumishwa nje ya lango la ofisi hizo. 

  DAR ES SALAAM: Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba Awamu ya Pili inayoendeshwa na Kampuni ya Global Publishers, wachapishaji wa Magazeti ya Uwazi, Ijumaa, Ijumaa Wikienda, Amani, Risasi na Championi, imezinduliwa rasmi leo kwenye ofisi za Global Publishers, Bamaga- Mwenge jijini Dar es Salaam ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji na Sheria wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, James Mbalwe.

  Akizungumza katika uzinduzi huo, Mkurugenzi wa Global Publishers, Eric Shigongo alisema wameamua kutoa nyumba kama sehemu ya kurudisha wanachokipata kutoka kwa wasomaji na kuwahakikishia kwamba, mchakato mzima huendeshwa kwa umakini, haki na kuzingatia sheria kwa hiyo watu wasiwe na wasiwasi kwamba mshindi atapendelewa.

  "Niwahakikishie wasomaji na Watanzania wote kwamba shindano hili lipo 'fair' kabisa na maombi yangu ni kwamba kweli nyumba iende kwa mtu anayeihitaji, kama mjuavyo kujenga nyumba Dar es Salaam ni ghali sana na watu wengi wanapenda kuishi Dar es Salaam.

  "Awamu hii tumeyafanyia kazi mapungufu yote yaliyotokea kwenye shinda nyumba iliyopita, nyumba imeboreshwa na ipo karibu na barabara, pia samani zote za ndani zimeboreshwa pamoja na mfumo mzima wa ukusanyaji wa kuponi ambapo utamfikia msomaji karibu zaidi sehemu yoyote alipo nchini," alisema.

  Kwa upande wa mgeni rasmi, aliwahakikishia washiriki wote kwamba amekuwa akifanya kazi na Global Publishers na ana uhakika kuwa huwa wanazingatia sheria na ndiyo maana wamewapa kibali cha kuendesha shindano hilo.

  "Nimefanya kazi kwa muda mrefu na Global Publishers, huwa hakuna kupanga matokeo wala upendeleo, anayeshinda anakuwa ni yule kweli aliyestahili, nawasihi watu wote washiriki kwa sababu shindano limefuata taratibu zote za kisheria," alisema.

  Kwa upande wa Meneja Mkuu wa Global Publishers, aliwataka watu wengi washiriki kwa sababu yeyote anaweza kuibuka mshindi na kueleza kuwa namna ya kushiriki kuwania nyuumba hiyo iliyopo Bunju, Dar, mshiriki anatakiwa kununua magazeti la Global Publishers, kukata kuponi iliyopo ukurasa wa pili na kuijaza kisha kuikusanya kwa wakala aliye karibu naye nchi nzima au kwenye ofisi za Global Publishers, Bamaga- Mwenge jijini Dar.
  Picha na Richard Bukos na Amani Madebe/GPL
  shinda-nyumba-ii

  0 0

  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

  OFISI YA WAZIRI MKUU

   

  KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU


  MAOMBI YA NAFASI 1000 ZA MAFUNZO YA STADI ZA KUTENGENEZA VIATU

  1.         Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu (OWM-KVAU) inatekeleza Programu ya Kukuza Stadi za Kazi Nchini ya miaka mitano (2016 -2021) ambayo imelenga kuwezesha nguvu kazi ya Taifa kupata ujuzi na stadi za kazi stahiki ili kumudu ushindani katika soko la ajira. Hivyo, OWM-KVAU imeingia makubaliano na

  Taasisi ya Teknolojia Dar Es Salaam Kampasi ya Mwanza iliyo eneo la Ilemela Mwanza, kutoa mafunzo ya stadi za kutengeneza viatu na bidhaa za ngozi. Lengo ni kuhakikisha nchi inakua na nguvu kazi ya kutosha yenye ujuzi unaohitajika katika soko la ajira katika kutengeneza bidhaa za ngozi nchini.

  2.         Ofisi inapenda kutangaza nafasi 1,000 za mafunzo yatakayoanza ifikapo tarehe 20 Februari, 2017 katika Taasisi ya Teknolojia Dar es salaam Kampasi ya Mwanza. Vijana wa Kitanzania, wenye elimu ya msingi na kuendelea na umri kati ya miaka 18 hadi 35 wanaopenda kujiunga na mafunzo wawasilishe maombi yao kuanzia tarehe 22/ 01/2017 hadi 04/02/2017 yakiambatana na nyaraka zifuatazo:

  (i)      Barua ya maombi yenye anuani kamili ikiwa na namba za simu pamoja na barua pepe;

  (ii)      Nakala ya Cheti cha Elimu uliyohitimu
  (iii)       Nakala ya cheti cha kuzaliwa au kadi ya mpiga kura;
  (iv)      Barua  ya utambulisho kutoka Serikali ya Mtaa anaoishi mwombaji; na
  (v)      Picha nne za paspoti.

  3.         Maombi yawasilishwe kwa Mkuu wa Kampasi, TAASISI YA TEKNOLOJIA DAR ES SALAAM – KAMPASI YA MWANZA, S.L.P. 2525, Mwanza au kwa barua pepe: info@mwanzacampus.dit.ac.tz

  4.         Watakao kuwa na sifa na vigezo wataitwa kwenye usaili kuanzia tarehe 8 hadi 11 Februari, 2017.

  IMETOLEWA NA:
  KATIBU MKUU
  18 Januari, 2017

  0 0


  Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Prof. Elisante Ole Gabriel (kulia) akiongea na Waandishi wa habari kuhusu namna Wizara yake ilivyopokea kwa furaha vifaa hivyo na jinsi gani imejipanga kuvitumia katika kuhakikisha kuwa inawahudumia Wananchi kwa kuwapa huduma bora. Kushoto ni Afisa wa Masuala ya Utamaduni toka Ubalozi wa China nchini Tanzania Bw. Gao Wei. Makabidhiano hayo yamefanyika leo 19/0/2017 katika Ukumbi wa Wizara hiyo Jijini Dar es Salaam.

  Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Jianexi-Geo Engineering Group Corporation, Bw. Chen Xianghua (kulia) pamoja na Afisa wa Masuala ya Utamaduni toka Ubalozi wa China nchini Tanzania Bw. Gao Wei wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Prof. Elisante Ole Gabriel wakati akiongea na Waandishi wa habari kabla ya hafla ya makabidhiano ya samani za ofisi kwa ajili ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo iliyofanyika leo 19/01/2017 Jijini Dar es Salaam.  Baadhi ya Waandishi wa Habari pamoja na Maafisa wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Prof. Elisante Ole Gabriel (hayupo pichani) wakati akiishukuru Kampuni ya Jianexi-Geo Engineering Group Corporation kwa msaada wa samani za ofisi iliyoutoa kwa Wizara hiyo leo 19/01/2017.
  Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Jianexi-Geo Engineering Group Corporation, Bw. Chen Xianghua (kulia)

  akiongea na Waandishi wa habari kuhusu dhamira ya Kampuni yake ya kushirikiana na Serikali katika kusaidia kuleta maendeleo kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo hususani Sekta ya Sanaa na Utamaduni. Kushoto ni Afisa wa Masuala ya Utamaduni toka Ubalozi wa China nchini Tanzania Bw. Gao Wei, leo 19/0/2017 Jijini Dar es Salaam.

  Afisa wa Masuala ya Utamaduni toka Ubalozi wa China nchini Tanzania Bw. Gao Wei akiongea na Waandishi wa habari kuhusu dhamira ya Kampuni Jianexi-Geo Engineering Group Corporation pamoja Ubalozi wa Jamhuri ya Watu wa China ya kushirikiana na Serikali katika kusaidia kuleta maendeleo kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo hususani Sekta ya Sanaa na Utamaduni. Kushoto ni Afisa wa Masuala ya Utamaduni toka Ubalozi wa China nchini Tanzania Bw. Gao Wei, leo 19/0/2017 Jijini Dar es Salaam.
  Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Sanaa wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bibi. Leah Kihimbi (kushoto) pamoja Afisa Utamaduni (Kitengo cha Sanaa) Bi. Amney Kassam wakichukua taarifa za aina ya samani walizopokea kutoka kwa Kampuni ya Jianexi-Geo Engineering Group Corporation wakati wa hafla ya makabidhiano ya samani za ofisi kwa ajili ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo iliyofanyika leo 19/01/2017 Jijini Dar es Salaam.

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Prof. Elisante Ole Gabriel (kulia) akipokea moja ya samani za ofisi toka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Jianexi-Geo Engineering Group Corporation, Bw. Chen Xianghua wakati wa hafla ya makabidhiano ya samani hizo kwa hiyo iliyofanyika leo 19/01/2017 Jijini Dar es Salaam.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Prof. Elisante Ole Gabriel (kulia) pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Jianexi-Geo Engineering Group Corporation, Bw. Chen Xianghua wakiweka saini Hati za Makabidhiano ya Samani za ofisi mbele ya Waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla ya makabidhiano ya samani hizo kwa hiyo iliyofanyika leo 19/01/2017 Jijini Dar es Salaam.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Prof. Elisante Ole Gabriel (kulia) pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Jianexi-Geo Engineering Group Corporation, Bw. Chen Xianghua wakibadilishana Hati za Makabidhiano ya Samani za ofisi mbele ya Waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla ya makabidhiano ya samani hizo kwa hiyo iliyofanyika leo 19/01/2017 Jijini Dar es Salaam.

  (Picha zote na Benedict Liwenga-WHUSM).

  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimlaki Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Mhe. Benjamin William Mkapa ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi Januari 19, 2017.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akizungumza na Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Mhe. Benjamin William Mkapa ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi Januari 19, 2017.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimsindikiza Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Mhe. Benjamin William Mkapa baada ya maongezi yao ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi Januari 19, 2017.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri wa Maendeleo wa Denmark Mhe. Martin Bille Herman ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi Januari 19, 2017.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzi na Waziri wa Maendeleo wa Denmark Mhe. Martin Bille Herman ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi Januari 19, 2017.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli katika picha ya kumbukumbu na Waziri wa Maendeleo wa Denmark Mhe. Martin Bille Herman na ujumbe wake pamoja na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Philip Mpango na Katibu Mkuu Wizara hiyo Mhe. Dotto James Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi Januari 19, 2017.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiagana na Waziri wa Maendeleo wa Denmark Mhe. Martin Bille Herman wakiwa pamoja na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Philip Mpango na Katibu Mkuu Wizara hiyo Mhe. Dotto James Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi Januari 19, 2017.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimlaki Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Mhe. Benjamin William Mkapa ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi Januari 19, 2017.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akizungumza na Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Mhe. Benjamin William Mkapa ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi Januari 19, 2017.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimsindikiza Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Mhe. Benjamin William Mkapa baada ya maongezi yao ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi Januari 19, 2017.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri wa Maendeleo wa Denmark Mhe. Martin Bille Herman ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi Januari 19, 2017.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzi na Waziri wa Maendeleo wa Denmark Mhe. Martin Bille Herman ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi Januari 19, 2017.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli katika picha ya kumbukumbu na Waziri wa Maendeleo wa Denmark Mhe. Martin Bille Herman na ujumbe wake pamoja na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Philip Mpango na Katibu Mkuu Wizara hiyo Mhe. Dotto James Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi Januari 19, 2017.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiagana na Waziri wa Maendeleo wa Denmark Mhe. Martin Bille Herman wakiwa pamoja na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Philip Mpango na Katibu Mkuu Wizara hiyo Mhe. Dotto James Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi Januari 19, 2017.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimlaki Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Mhe. Benjamin William Mkapa ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi Januari 19, 2017.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akizungumza na Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Mhe. Benjamin William Mkapa ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi Januari 19, 2017.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimsindikiza Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Mhe. Benjamin William Mkapa baada ya maongezi yao ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi Januari 19, 2017.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri wa Maendeleo wa Denmark Mhe. Martin Bille Herman ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi Januari 19, 2017.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzi na Waziri wa Maendeleo wa Denmark Mhe. Martin Bille Herman ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi Januari 19, 2017.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli katika picha ya kumbukumbu na Waziri wa Maendeleo wa Denmark Mhe. Martin Bille Herman na ujumbe wake pamoja na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Philip Mpango na Katibu Mkuu Wizara hiyo Mhe. Dotto James Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi Januari 19, 2017.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiagana na Waziri wa Maendeleo wa Denmark Mhe. Martin Bille Herman wakiwa pamoja na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Philip Mpango na Katibu Mkuu Wizara hiyo Mhe. Dotto James Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi Januari 19, 2017


older | 1 | .... | 1106 | 1107 | (Page 1108) | 1109 | 1110 | .... | 1898 | newer