Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1108 | 1109 | (Page 1110) | 1111 | 1112 | .... | 1898 | newer

  0 0

  Mkurugenzi  Mtendaji wa Hospitali ya Taifa  Muhimbili ( MNH),  Profesa  Lawrence Museru  leo amekutana na wahudumu  wa  Afya  katika  hospitali hiyo pamoja na mambo mengine  amewasisitiza kufanya kazi kwa bidii na kwamba uongozi wa hospitali hiyo utaendelea kutatua changamoto zinazowakabili.Pia, mkurugenzi huyo amewataka wahudumu hao kuzingatia maadili ya kazi  ili kutoa huduma bora kwa wagonjwa.

  Profesa Museru  ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es salaam  katika  mkutano  na baadhi ya wahudumu wa afya  uliolenga kumpongeza  kwa kuteuliwa  kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali hiyo.

  Profesa Museru  amesema licha ya wahudumu hao kukabiliwa changamoto mbalimbali , lakini hawanabudi kufanya kazi kwa bidii kwani jukumu lao ni kutoa huduma bora.

  " Nawapongeza kwa kazi nzuri mnayofanya hatua ambayo imesaidia kupunguza malalamiko wakati wa kutoa huduma , ingawa bado kuna changamoto lakini hatua budi kutoa huduma bora  na sisi tutaendelea kutatua changamoto hizo kadiri inavyowezekana  ili kuhakikisha mazingira yetu ya kazi yanakua bora," amesema Profesa Museru.

  Katika mkutano huo wahudumu hao wamewasilisha ajenda  14 ikiwamo ombi la kupatiwa mafunzo  ili kuongeza  ufanisi na kuboresha utendaji kazi wao.
  Mwenyekiti wa TUGHE, Tawi la Muhimbili, Mziwanda Salumu Chimwege akimkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru zawadi kutoka kwa wahudumu wa hospitali hiyo leo.
   Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru akifafanua jambo kwenye mkutano huo.  Kulia ni Mkurugenzi wa Uuguzi, Agnes Mtawa wa hospitali hiyo.
   Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dk Mtemi Sufiani Baruani, Mkurugenzi wa Uuguzi, Agnes Mtawa, Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali hiyo, Profesa Lawrence Museru, Kaimu Mkuu wa Idara ya Utawala, Leila Komba,  Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Shirikishi, Dk. Praxeda Ogweo na Mkurugenzi wa Huduma za Tiba, Hedwiga Swai wakiwasikiliza wahudumu wa hospitali hiyo katika mkutano uliowahusisha viongozi hao. Mkutano huo umefanyika leo katika ukumbi wa jengo la maabara kuu.
   Mkurugenzi wa Uuguzi, Agnes Mtawa akisisitiza jambo kwenye mkutano huo. 
   Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Shirikishi, Dk. Praxeda Ogweo wa hospitali hiyo akizungumza na wahudumu leo katika mkutano.
    Mmoja wa wafanyakazi wa hospitali hiyo, Joseph Oloch akizungumza kwenye mkutano huo leo.
   Baadhi ya wahudumu hao wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru leo.
   Wahudumu wakifuatilia jambo kwenye mkutano huo leo.

  0 0

  Na Ali Issa, Maelezo Zanzibar.

  Wizara ya Afya Zanzibar kupitia kitengo cha maradhi ya yasio pewa kipaumbele (kichocho, matende, na Vikope)kimo katika harakati za kuyatokomeza kabisa maradhi hayo katika maeneo ya Zanzibar.

  Hayo yamesemwa leo huko Mkoa wa Kusini Unguja katika Hoteli ya visital inn Jambian na Dr.wa maradhi hayo Khalifan Abdalla Mohamed wakati wa semina ya mapitio wa mradi uliomaliza wa kuyatokomeza maradhi hayo .

  Amesema maradhi ya kichocho na matende yaliathiri sana wananchi wa visiwa vya zanzbar katika miaka ya thamanini na kupelekea wengine kupata maradhi ya matende hadi hii leo jambo ambalo kwasasa maradhi hayo yanaonekana kutoweka kutokana na jitihada za Serikali na washirika wake wa maendeleo kulivalia njuga tatizo hilo.

  Amsema kwa sasa hali hiyo inaridhisha kwakiasikikubwa na sehemuzilizo bakia nichache kuliitokomeza tatizohilo “Tuna tarajia kuyamaliza maradhi ya kichocgo na matende kwani imekuwa nadra kupokea wagonjwa wamaradhi haya ispokuwa niwale wale wagonjwa wazamani tu walioathirika na matende,kichocho,na  zipo baadhi ya maeneo ambayo hayajamalizika maradhi hayo kama vile kamgamba,kinyasini,moga,kizimkazi na kwapemba micheweni kwa”alisema DR Khalifan.

  Nae mwenyekiti wa mradi wa kutokomeza maradhi hayo kutoka Nchini giniva katika shirika Global Schistosomiasis Alliance Dr Lorenzo Savioli amesema mapitio ya semina hiyo ni kuangalia vipi kuisaidia Zanzibar  kwa kuwapatia madawa na kufikia lengo la kuyatokomeza maradhi hayo.
  Amsema  wananchi wazitumie dawa hizo kwa rika zote na hazina matatizo yoyote bali zinapoza zaidi maradhi mengine kama vile mapele mabaka na mipasuko mwilini.

  Alisema wazitumie dawa hizo bure na nifrusa kwao ,kwani nchini kwao dawa hizo ni ghali mno kwa mwananchi wa Tanzania.

  Nae mkurugenzi wa Maendeleo ya maji Zanzibar Muhamed Iliasa Mohamed alisema katika kuondoa tatizo la kichocho Zanzibar ni kuhakikisha kupeleka maji safi na salama katika maeneo yote ya zanzbar ili wananchi waweze kutumia maji safi na kuacha kutumia maji ya mito na mashimo.
  Aidha alisema wanalazimika maji kuyatia dawa yakuulia vimelea vya maradhi hayo ili visiwe na nafasi ya kuathiri wananchi wanapo yatumia.
   Washiriki mbali mbali wa Semina wakifanya mapitio ya Mradi wa kutokomeza Maradhi yasiopewa kipaumbele (Kichocho,Matende na Vikope) katika ukumbi wa Hoteli ya VISITAL INN iliopo Jambiani Mkoa wa kusini Unguija.
   Mwenyekiti wa kutokomeza Maradhi hayo kutoka  Shirika la Global Schistosomiasis Alliance (GSA) Dr Lorenzo Savioli,akizungumza na waandishi wa Habari namna walivyodhamiria kuyatokomeza maradhi haya katika Nchi ya Zanzibar.
  Mkurugenzi Maendeleo ya Maji Moh’d Iliasa Moh’d akizungumza na Waandishi wa Habari,  namna walivyokusudia kuwapelekea Wananchi huduma ya Maji maeneo yote ambayo yamegundulika na maradhi ya kichocho hayana maji salama watafikisha huduma ya Maji safi na salama haraka iwezekanavyo .

  0 0

  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

  WAZIRI Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye,amesema kuwa anafanya harakati za kapambana na kazi za wasanii ziweze kupata heshima na pamoja na masilahi kwa wasanii hao hili waweze kujiongeza kipato.

  Nape ameyasema hayo leo wakati alipokutana na Wasanii juu ya masuala mbalimbali yanayohusu sekta ya filamu, amesema wasanii wanafanya kazi ngumu lakini hawanufaiki na kazi wanayoifanya huku jamii ikiona mafanikio.

  Amesema katika kazi za filamu ziweze kupata heshima kunahitajika kutengeneza sera ambayo itamaliza malalamiko ya wasanii na wawekezaji wanaweza kuwekeza katika katika sekta hiyo.

  Nape amesema kuna watu wanakuja kutaka kuwekeza katika sekta ya filamu kutokana na kutokuwepo kwa sera wawekezaji hao wanakimbia na kwenda nchi nyingine zilizoweka sera.Aidha amesema kupatikana kwa sera kutapunguza maharamia wanaofanya kazi wasanii na kujipatia kipato kikubwa kuliko wale wanaofanya kazi halisi.

  "kazi za wasanii ambazo hazina stika ziko katika maghala ya TRA na kati hizo za wasanii zina kesi mahakamani.Nape amesema katika juhudi hizo kumekuwa na maneno kwa baadhi ya wasanii ya kumpiga vijembe huku akiwa anafanya kazi ya kukamata kazi hizo kwa gharama yake mwenyewe" amesema Waziri Nape.

  Hata hivyo amesema katika kupambana na maharamia baadhi ya wasanii wanashirikiana na ambao wameshiriki mkono na taarifa zote za mkutano huo wanaupata lakini hatajali na operesheni zingine zitaendelea.

  Hata hivyo ameitaka baraza la Sanaa la Taifa Basata kusajili kazi za wasanii licha ya kuwepo kwa sheria za ovyo ovyo.Katika Mkutano huo ubwabwa ulionunuliwa kwa wasanii na kuliwa uwanja wa taifa unadaiwa kutolewa na maharamia wa kazi za wasanii ambapo Waziri Nape amepinga kuwa hakuna kitu kama hicho.

  Waziri nape amewatahadharisha wasanii ambao wanajiona wana majina na kushindwa kushiriki mkutano huo na kufanya wasanii waliofika kuwa wao ndio wanashida huku akitaja kuwa jambo hilo ni la wasani wote hivyo kila mtu anapaswa kushiriki.
  Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye akiangalia mashine ya kudurufu santuri za muziki na video wasambazaji zilizopo katika ghala la kampuni ya madalali ya YONO iliyopo Ilala Bungoni. 
  Baadhi ya Wasanii wakiangalia kazi haramu za wasanii zilizokamatwa kwa wasambazaji zilizopo katika ghala la kampuni ya madalali ya YONO iliyopo Ilala Bungoni. 

  Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye akiongea na wadau katika sekta ya filamu alipokutana nao leo kujadili changamoto za sekta hiyo na jinsi ya kupambana na maharamia wa kazi za wasani na kuwatoa hofu juu ya wasiwasi wao wa Mali zilizowahi kukamatwa kuwa zimerudishwa kwa wahusika. 
  Wadau wa Sekta ya Filamu wakimsikiliza Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye alipokutana nao leo Jijini Dar es salaam. 
  Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye akimsikiliza Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF) Bw. Simon Mwakifamba 
  Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye akiangalia kazi haramu za wasanii zilizokamatwa kwa wasambazaji zilizopo katika ghala la kampuni ya madalali ya YONO iliyopo Ilala Bungoni.

  0 0

   Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango, akibonyeza kitufe kuashiria kuzinduliwa rasmi kwa Jina Jipya na Nembo Mpya yenye alama ya Kipepeo, (Tpb Bank Plc) vitakavyo tumiwa kibiashara na Benki ya Posta Tanzania Plc, kuanzia Januari 19, 2017. Tukio lililofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Jijini Dar es salaam
   Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango, (katikati), Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki hiyo, Prof. Lettice Rutashobya na Mtendaji Mkuu wa benki hiyo, Bw. Sabasaba Moshingi, wakiangalia Jina Jipya na Nembo Mpya iliyobuniwa na Benki hiyo baada ya kuizindua rasmi  Januari 19, 2017, Tukio lililofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Jijini Dar es salaam
   Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango, (wa pili kulia), akimpongeza Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania (Tpb Bank Plc), Bw. Sabasaba Moshingi, kwa kazi nzuri ambayo benki hiyo imefanya kubuni Jina na Nembo Mpya itakayoanza kuitambulisha Benki hiyo katika biashara ya Sekta ya Fedha kuanzia Januari 19, 2017, tukio lililofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Jijini Dar es salaam
   Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania (Tpb Bank Plc), Bw. Sabasaba Moshingi, akitoa hotuba ya mafanikio ambayo Benki yake imeyapata katika biashara ya Sekta ya Fedha ikiwemo kukuza mtaji, kupata faida na kufanikiwa kubuni Jina Jipya na Nembo Mpya ya Kipepeo, itakayoanza kutumika kuanzia leo Januari 19, 2017, baada ya kuzinduliwa rasmi na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Jijini Dar es salaam
   Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango, akitoa hotuba kabla ya kuzindua rasmi Jina Jipya na Nembo vitakavyo tumiwa kibiashara na Benki ya Posta Tanzania (Tpb Bank Plc), kuanzia  Januari 19, 2017. Tukio lililofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Jijini Dar es salaam.
   Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango, (aliyeketi kulia), Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Tpb Bank Plc, Prof. Lettice Rutashobya (katikati), Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango wa Serkali ya Mapinduzi Zanzibar Bw. Ally Khamis Juma, wakisikiliza kwa makini hotuba ama wasilisho la Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo Bw. Sabasaba Moshingi, (hayupo pichani) wakati wa hafla ya uzinduzi rasmi wa Jina na Nembo Mpya itakayoanza kuitambulisha Benki hiyo katika biashara ya Sekta ya Fedha kuanzia Januari 19, 2017, tukio lililofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Jijini Dar es salaam
   Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Tpb Bank Plc, Prof. Lettice Rutashobya (kushoto) akimkabidhi Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango, zawadi ya saa yenye Jina na Nembo Mpya ya Kipepeo, itakayoanza kuitambulisha rasmi Benki hiyo ndani na nje ya nchi baada ya kuzinduliwa rasmi kwa matumizi ya vitu hivyo, Januari 19, 2017, tukio lililofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Jijini Dar es salaam
   Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Tpb Bank Plc, Prof. Lettice Rutashobya (kushoto) akimkabidhi Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango, kadi ya benki hiyo mara baada ya kuzinduliwa kwa Jina na Nembo Mpya ya Kipepeo, itakayoanza kuitambulisha rasmi Benki hiyo ndani na nje ya nchi kuanzia Januari 19, 2017, Tukio lililofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Jijini Dar es salaam
   Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Jijini Dar es salaam, ambapo tukio la uzinduzi wa Jina na Nembo Mpya ya Benki ya Posta Tanzania (Tpb Bank Plc) limefanyika.
   Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt, Philip Mpango, (wa pili kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Posta Tanzania (Tpb Bank Plc), Prof Lettice Rutashobya, Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango wa Serkali ya Mapinduzi Zanzibar Bw. Ally Khamis Juma, (wa kwanza kushoto), Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo Bw. Sabasaba Moshingi (kulia), na Baadhi ya Watendaji wakuu wa Benki hiyo, baada ya kuzinduliwa rasmi kwa Jina na Nembo Mpya ya Benki hiyo, Katika Ukumbi wa Julius Nyerere, Jijini Dar es salaam, Januari 19, 2017
   Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt, Philip Mpango, (wa pili kulia) akiwa  katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Posta Tanzania (Tpb Bank Plc), Prof Lettice Rutashobya, (wa tatu kushoto), Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango wa Serkali ya Mapinduzi Zanzibar Bw. Ally Khamis Juma, (wa kwanza kushoto), Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo Bw. Sabasaba Moshingi (kulia), na baadhi ya wafanyakazi wa Benki hiyo, baada ya kuzinduliwa rasmi kwa Jina na Nembo Mpya ya Benki hiyo, Katika Ukumbi wa Julius Nyerere, Jijini Dar es salaam, Januari 19, 2017
  Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt, Philip Mpango, (wa pili kulia) akiwa  katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Posta Tanzania (Tpb Bank Plc), Prof Lettice Rutashobya, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (wa kwanza kushoto), Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo Bw, Sabasaba Moshingi (kulia), wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wanawake wa  Benki hiyo baada ya kuzinduliwa rasmi kwa Jina na Nembo Mpya ya Benki hiyo, Katika Ukumbi wa Julius Nyerere, Jijini Dar es salaam, Januari 19, 2017

  (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-WFM)

  0 0  0 0

  Kiongozi wa Kampeni ya Kuinua Maadili Kitaifa Bi Mayrose Kavura Majinge, siku ya Jumamosi Jan 14, ameweza kushirikiana na wadau mbali mbali jijini hapa Washington kwa lengo la kuinua Maendeleo Maalum ya Maadili Kitaifa, yaliyoanza rasmi kufanyika mwezi huu Januari hadi Disemba 2017, kwa lengo la kuinua na kudumisha maadili ya Watanzania ili kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazodhoofisha mfumo wa muundo wa jamii yetu ya Kitanzania.

  0 0

  Raundi ya tano ya mechi za kuwania Kombe la Shirikisho la Azam 2016/17 (Azam Sports Federation Cup - ASFC), utaanza Jamamosi Januari 21, 2017 kwa timu za Majimaji na Mighty Elephant za Songea kucheza kwenye Uwanja Majimaji mjini Songea.

  Ratiba ya ASFC inaonesha kwamba timu za Alliance na Mbao za Mwanza zitacheza pia keshokutwa Jumamosi kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, wakati Young Africans itacheza na Ashanti United kwenye Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam.

  Jumapili Januari 22, mwaka huu Ruvu Shooting itacheza na Kiluvya United kwenye Uwanja wa Mabatini ulioko Mlandizi mkoani Pwani wakati Toto Africans itacheza na Mwadui ya Shinyanga kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza huku Simba itakipiga na Polisi Dar kwenye Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam kadhalika Mbeya Warriors ikicheza na Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.

  Jumatatu Januari 23, mwaka huu Stand United itacheza na Polisi Mara kwenye Uwanja wa Karume Mara wakati Azam itacheza na Cosmopolitan kwenye Uwanja wa Chamazi wakati Ndanda itacheza na Mlale JKT kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona.

  Jumanne Januari 24, mwaka huu Mtibwa Sugar itacheza na Polisi Moro kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro wakati Kurugenzi ya Iringa itacheza na JKT Ruvu huko Mafinga huku Mbeya City ikipangwa kucheza na Kabela City Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya ilihali Madini na Panone zitacheza kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha.

  Januari 25, mwaka huu kutakuwa na mchezo kati ya Singida United na Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Namfua mjini Singida wakati mchezo mwingine utakaozikutanisha timu za African Lyon na Mshikamano utapangiwa tarehe mpya. Mechi hiyo imepangwa kufanyika Uwanja wa Uhuru

  0 0

  Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mh.Nape Nnauye amempongeza Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania ( TFF) baada ya kuteuliwa na CAF kuwa mjumbe
   

  0 0  0 0

  Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) walipotembelea na Kukagua Mradi wa Umeme uliopo moja ya kijiji kilichopo Wilaya ya Ileje Mkoani Songwe.(PICHA NA OFISI YA BUNGE).
  Mkuu wa Mkoa wa Songwe Mhe. Chiku Galawa (aliesimama) akizungumza mbele ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) pale kamati hiyo ilipofanya ziara ya kukagua miradi ya Umeme Songwe Vijijini, katika Kikao kilichofanyika leo katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mjini Songwe.
  Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) Mhe. Livingstone Lusinde akifafanua jambo mbele ya Wajumbe wa Kamati hiyo, pale walipotembelea Ofisi ya Mkuu wa Wilaya wa Ileje tayari ya kwenda kukagua Mradi wa Umeme uliopo kijijini hapo, Kushoto wake ni Naibu Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Dkt. Medard Kalemani na Kulia kwake ni Katibu Kamati wa Bunge anaehusika na Hesabu za Serikali (PAC) Ndg. Asmin Kihemba na anaefuata ni Mkuu wa Wilaya ya Ileje Mhe. Joseph M. Mkude. katika kikao kilichofanyika leo katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya wa Ileje Mkoani Songwe.
  Mkuu wa Wilaya ya Ileje Mhe. Joseph M. Mkude (aliesimama) akizungumza na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) pale kamati hiyo ilipomtembelea Ofisi kwake tayari kwa Ukaguzi wa mradi wa umeme katika moja ya kijiji kilichopo Wilaya ya Ileje, Katika kikao kilichofanyika leo katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya.

  0 0

  Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Nape Nnauye amekutana na wadau wa sekta filamu nchini na kuoneshwa kusikitishwa juu ya shutuma dhidi yake na serikali kuwa wamekamata bidhaa haramu za wasanii na kuzirudisha kwa wamiliki kupitia mlango wa nyuma.

  Akiongea wakati alipotembelea moja ya ghala la Kampuni ya Udalali ya YONO Waziri Nape amewatoa hofu wasanii na kuwaeleza kuwa bidhaa hizo za muziki na video ziko mahali salama na zitateketezwa bila kificho muda si mrefu.

  Akiongelea kuhusu sakata hilo Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF) Simon Mwakifamba amewaasa wasanii kuacha tabia ya kushutumu viongozi bila kuwa na ushahidi wa kutosha

  Katika Ziara hiyo Waziri Nape aliongozana na Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bi. Joyce Fissoo na Wawakilishi kutoka Mamlaka ya Mpato Tanzania (TRA),COSOTA,Tume ya Ushindani wa Kibiashara(FCC) na Baraza la Sanaa Tanzania(BASATA)

  0 0

  Mwenyekiti wa Wabunge wa Kamati ya Maliasili, Ardhi na Utalii, Eng. Atashasta Nditiye (wa kwanza kulia) akizungumza na wabunge na baadhi ya Viongozi na Watumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii wakati walipokuwa wakiangalia sanamu mtu wa kabila la Kimasai iliyochongwa kwa kutumia mti aina ya Mpingo kabla ya Wabunge wa kamati hiyo kuanza kutembelea Makumbusho ya Taifa, jijini Dar es Salaam, wa pili kulia ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Eng. Ramo makani.
  Mwenyekiti wa Wabunge wa Kamati ya Maliasili, Ardhi na Utalii, Eng. Atashasta Nditiye ( watatu kushoto) na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Eng.Ramo Makani (watatu kulia) akiwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Maj. Gen. Gaudence Milanzi (wa pili kulia) akizungumza na wabunge na baadhi ya Viongozi wa Wizara ya Maliasili na Utalii wakati walipokuwa wakiangalia zana za mawe zilizotumiwa na binadamu wa kale wakati Wabunge wa kamati ya Maliasili, Ardhi na Utalii walipokuwa wakitembelea Makumbusho ya Taifa, jijini Dar es Salaam.
  Mwenyekiti wa Wabunge wa Kamati ya Maliasili, Ardhi na Utalii, Eng. Atashasta Nditiye (wa kwanza kulia) akitia saini kwenye kitabu cha Wageni akishuhudiwa na baadhi ya Wabunge wa Kamati ya Maliasili, Ardhi na Utalii pamoja na baadhi ya Viongozi wa Wizara ya Maliasili na Utalii wakiwa kwenye chumba maalumu ( strong room) cha kuhifadhia urithi wa utamaduni wa thamani kubwa kama zamadamu (hominine remains), masalia ya akiolojia, historia pamoja na sanaa ya ethnografia) leo walipotembelea Makumbusho ya Taifa, jijini Dar es Salaam, 
  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Eng. Ramo makani (kushoto) akitia msisitizo jambo kwa Mwenyekiti wa Wabunge wa Kamati ya Maliasili, Ardhi na Utalii, Eng. Atashasta Nditiye (katikati) akiwa pamoja na Mbunge wa kamati hiyo, Mhe, Shabani Shekilindi ( wa kwanza kulia) mara baada ya kumaliza ziara ya kutembelea kijiji cha Makumbusho cha Kijitonyama, jijini Dar es Salaam.
  Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Maj. Gen. Gaudence Milanzi akiwaelezea Wabunge wa Kamati ya Maliasili, Ardhi na Utalii kuhusu meli ya kivita ya iliyozama baharini iliyotumiwa na jeshi la Kijerumani wakati wa vita vya kwanza duniani (1914-1919)
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Gaudence Milanzi akizungumza na Mwenyekiti wa Wabunge wa Kamati ya Maliasili, Ardhi na Utalii, Eng. Atashasta Nditiye wakati wakielekea kuangalia Nyumba ya wahehe iliyopo kijiji cha Makumbusho cha Kijitonyama, jijini Dar es Salaam,  ( Picha na Lusungu Helela- WMU)

  0 0

  Na Estom Sanga - Pemba.

  Kamati ya Kudumu ya Bunge Utawala Bora na Serikali za Mitaa imetembelea miradi inayotekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii –TASAF- Unguja na Pemba na kuridhishwa na hatua ya Maendeleo iliyofikiwa katika utekelezaji wake  kupitia Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini.

  Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mheshimiwa Mwanne Ismail Mchemba akizungumza na wananchi wa shehia ya Ndagoni Kisiwani Pemba baada ya kukagua ujenzi wa tuta la kuzuia maji chumvi ya baharini yasiathiri mashamba ya wananchi, ametaka walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini kutumia fursa ya Mpango huo kupunguza kero ya umaskini.

  Ametoa Mfano wa Miradi iliyojengwa kwa ufanisi kuwa ni pamoja na matuta ya kuzuia maji chumvi ,upandaji wa mikoko, uchimbaji wa mitaro ya maji ,uundwaji wa vikundi vya kuweka akiba, na ujenzi wa vyumba vya madarasa na zahanati miradi iliyotekelezwa na walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya maskini kwa utaratibu wa ajira ya muda kisiwani Unguja na Pemba.

  Kwa kutengeneza matuta ya kuzuia maji ya chumvi, walengwa hao wa TASAF wameweza kuokoa zaidi ya hekta 200 za mashamba ya mpunga katika shehia ya Ndagoni kisiwani Pemba kwa njia ya ushiriki kwenye ajira ya muda .

  Kwa Upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menenjimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mheshimiwa Angellah Kairuki amesema serikali inafuatilia kwa karibu utekelezaji wa shughuli za TASAF ili kuziboresha zaidi kwa manufaa ya wananchi.

  Aidha Waziri huyo ameiagiza TASAF kuviimarisha zaidi vikundi vya kuweka akiba na  kuwekeza vipatavyo 876 kwenye shehia 78 vilivyoundwa na walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini kisiwani humo kwa kuvipatia nyenzo muhimu hususani elimu na vitendea kazi ili vikundi hivyo viwe endelevu.

  Mmoja wa wajumbe wa kamati hiyo Mheshimiwa Mwita Mwikabe Waitara mbunge wa Ukonga amesema mfumo wa kuwashirikisha walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya kuibua na kutekeleza miradi unaotumiwa na TASAF umeamusha ari ya wananchi kushiriki katika shughuli za Maendeleo na kutatua kero zinazowakabili badala ya kuitegemea serikali pekee.

  Wakitoa ushahuda wa namna wanavyonufaika na Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika shehia ya Ndagoni na Shidi kisiwani Pemba ,baadhi ya walengwa wa Mpango huo wamewaambia wajumbe wa kamati hiyo ya bunge kuwa uwezo wao wa kuhudumia watoto hususani wanafunzi umeongezeka na hivyo kuboresha mahudhurio yao shuleni na hata kwenye vituo vya afya ili kutimiza masharti ya Mpango.

  Hata hivyo baadhi ya walengwa hao wamesema kwa sasa wanakabiliwa na soko la bidhaa wanazozalisha hususani mboga mboga kutokana na ongezeko la bidhaa hiyo kwenye maeneo yao.Mpango wa Kunusuru Kaya masikini unaotekelezwa na TASAF nchini kote pia  umeweka mkazo katika  shughuli za usalishaji mali kwa walengwa ili waweze kukuza kipato .

  Zifuatazo ni picha za wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Utawala Bora na Serikali za Mitaa wakati wa ziara yao kisiwani Pemba kukagua miradi inayotekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii - TASAF.  
   Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe.Angellah Kairuki akikagua bidhaa zilizotengenezwa na vikundi vya walengwa wa TASAF  
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe.Angellah Kairuki akikagua bidhaa zilizotengenezwa na vikundi vya walengwa wa TASAF 

    Matuta ya kuzuia maji chumvi ,upandaji wa mikoko na uchimbaji wa mitaro ya maji ni Moja ya Miradi iliyojengwa kwa ufanisi Mkubwa.
   Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe.Angellah Kairuki akipata maelezo mbalimbali alipokuwa akikagua bidhaa zilizotengenezwa na vikundi vya walengwa wa TASAF 

  0 0

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa polisi katika mji wa Makambako akiwa katika ziara ya mkoa wa Njombe Januari 19, 2017.
  Wananchi wa Makambako mkoani Njombe wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipohutubia mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa Polisi Januari 19, 2017.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na viongozi wa mkoa na wilaya ya Njombe baada ya kupokea taarifa ya mkoa huo katika siku ya kwanza ya ziara yake mkoani humo Januari 19, 2017. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Christopher Ole Sendeka.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua vibanda vya biashara vya Magegele vinavyomilikiwa na Halmashauri ya Mji wa Makambako akiwa katika ziara ya mkoa wa Njombe Januari 19, 2017.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewaagiza viongozi wa Idara ya Uhamiaji kuandaa semina za mafunzo ya elimu ya uraia kwa wahudumu ya hoteli na nyumba za kulala wageni nchini ili kudhibiti wimbi la wahamiaji haramu.

  Ametoa kauli hiyo jana jioni (Alhamisi, Januari 19, 2017) mara baada ya kuwasili katika Ikulu ndogo ya Njombe na kupokea taarifa ya mkoa wa Njombe iliyotolewa na mkuu wa mkoa huo Bw. Christopher Ole Sendeka.

  Katika taarifa hiyo Bw. Ole Sendeka alisema kwenye kipindi cha kuanzia Januari hadi Desemba, 2016 Idara ya Uhamiaji ilibaini kuwepo kwa raia 119 wa kigeni ndani ya mkoa huo, ambapo wahamiaji haramu 42 walikamatwa.

  Waziri Mkuu alisema ni hatari kwa mkoa huo kuwa na idadi kubwa ya raia wa kigeni walioingia nchini bila ya kufuata utaratibu hivyo aliitaka Idara hiyo ijipange vizuri ili kudhibiti watu wa aina hiyo.

  “Anzisheni utaratibu wa kutoa semina kwa wahudumu wa hoteli na nyumba za kulala wageni. Hawa wakipata elimu ya uraia watawasaidia katika kutoa taarifa za kuwepo kwa wageni ambao wana mashaka na uraia wao,” alisema.

  Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu aliwataka viongozi wa mikoa kujikita katika ukusanyaji wa mapato pamoja na kuzuia mianya ya rushwa pamoja na matumizi mabaya ya fedha za umma katika maeneo yao.

  Alisema lazima kuwe na nidhamu ya matumizi ya fedha za Serikali zinazopelekwa katika halmashauri nchini. “fedha hizo lazima zitumike kwa malengo yaliyokusudiwa yenye kuleta tija kwa wananchi na Taifa kwa ujumla,”.

  Aidha, Waziri Mkuu aliwataka watumishi wa umma kuibua maeneo mapya ya ukusanyaji wa mapato ambayo yatatumika katika utoaji wa huduma za jamii hivyo kuleta tija kwa Taifa.

  Pia aliwataka wakuu wa mikoa na wilaya kusimamia vizuri miradi ya maendeleo inayojengwa katika maeneo yao kuhakikisha kama inalingana na thamani halisi ya fedha zinazotolewa na wasikubali kupokea miradi iliyojengwa chini ya kiwango.

  Awali Mkuu wa mkoa huo alisema kati ya wahamiaji haramu 42 waliokamatwa 39 ni raia wa Ethiopia, wengine wanatoka Uganda (1), Burundi (1) na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (1). Wote walifikishwa mahakamani na kuchukuliwa hatua za kisheria.

  Alisema Idara ya Uhamiaji inaendelea na mikakati ya kuishirikisha jamii katika utoaji wa taarifa pindi wanapowatilia shaka kuhusu ukaazi wao ikiwa ni pamoja na kutoa elimu ya uraia na upanuzi wa huduma za uhamiaji.

  Akizungumzia kuhusu suala la ukusanyaji wa mapato mkuu wa mkoa alisema katika kipindi cha mwaka wa fedha 2015/2016 mkoa uliweza kukusanya kiasi cha sh. bilioni 7.07 sawa na asilimia 89.3 ya makisio ambayo yalikuwa sh. bilioni 7.92.

  “Kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2016/2017 halmashauri zilikisia kukusanya kiasi cha sh. bilioni 8.22 ambapo katika kipindi cha nusu mwaka (Julai hadi Desemba, 2016) wameweza kukusanya jumla ya sh. bilioni 4.37 sawa na asilimia 53.2 ya makisio ya mwaka,” alisema.

  Alisema mafanikio hayo yamechangiwa na ukusanyaji wa mapato kwa kutumia mashine maalumu za kielektroniki za kukusanyia mapato pamoja na kuondoa utaratibu wa ukusanyaji wa mapato kwa kutumia mawakala katika vyanzo vingi.

  Aidha, Ole Sendeka alisema halmashauri za mkoa huo zinaendelea kupitia upya sheria ndogo za ukusanyaji wa mapato ili kuongeza vyanzo vya mapato pamoja na baadhi ya viwango vya kodi na tozo mbalimbali.

  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  IJUMAA, JANUARI 20, 2017.

  0 0

  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akiwakaribisha wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Utawala na Serikali za Mitaa walipoitembelea ofisi ya Mfuko wa Rais wa Kujitegemea (PTF) ili kupata taarifa ya kiutendaji.
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akifafanua majukumu ya Mfuko wa Rais wa Kujitegemea (PTF) kwa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Utawala na Serikali za Mitaa ilipoitembelea ofisi hiyo ili kupata taarifa ya kiutendaji. Kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Utawala na Serikali za Mitaa, Mhe. Jason Rweikiza (Mb) na kulia ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Ikulu Bw. Peter Ilomo.
  Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Utawala na Serikali za Mitaa, Mhe. Jason Rweikiza (Mb) akitoa neno la utangulizi wakati Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Utawala na Serikali za Mitaa ilipoitembelea ofisi ya Mfuko wa Rais wa Kujitegemea (PTF) ili kupata taarifa ya kiutendaji. Kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb).
  Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Ikulu Bw. Peter Ilomo akitoa maelezo ya namna Mfuko wa Rais wa Kujitegemea (PTF) unavyotekeleza majukumu yake kwa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Utawala na Serikali za Mitaa ilipoitembelea ofisi hiyo ili kupata taarifa ya kiutendaji. Kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akimsikiliza kwa makini.
  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Rais wa Kujitegemea (PTF), Bi. Haighat Kitala akifafanua majukumu ya ofisi yake kwa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Utawala na Serikali za Mitaa ilipoitembelea ofisi hiyo ili kupata taarifa ya kiutendaji.
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Utawala na Serikali za Mitaa mara baada ya kumaliza kikao cha kupokea taarifa ya kiutendaji ya Mfuko wa Rais wa Kujitegemea (PTF).

  0 0


  Mkufunzi na mtaalamu wa masuala ya usalama barabarani kutoka Safe Speed Foundation, Henry Bantu akitoa mada kwa waandishi wa habari wanaohudhuria mafunzo ya uandishi wa habari za usalama barabarani yanayoendeshwa na TAMWABaadhi ya waandishi wa habari wanaoshiriki uandishi wa habari za usalama barabarani wakiwa katika mafunzo hayo. Baadhi ya waandishi wa habari wanaoshiriki uandishi wa habari za usalama barabarani wakiwa katika mafunzo hayo.Mkufunzi na mtaalamu wa masuala ya usalama barabarani kutoka Safe Speed Foundation, Henry Bantu akisisitiza jambo katika mafunzo hayo. Kushoto ni Mkufunzi wa mafunzo hayo, Valerie Msoka. Mkufunzi na mtaalamu wa masuala ya usalama barabarani kutoka Safe Speed Foundation, Henry Bantu akisisitiza jambo katika mafunzo hayo. Kushoto ni Mkufunzi wa mafunzo hayo, Valerie Msoka.Ofisa Miradi Mkuu wa TAMWA, Bi. Gradness Munuo (kushoto) akiwasilisha mada kwa washiriki wa mradi wa kampeni ya kupambana na ajali za vyombo vya moto barabarani. Kulia ni Ofisa Mradi wa TAMWA, Bw. Edson Sosten. Ofisa Miradi Mkuu wa TAMWA, Bi. Gradness Munuo (kushoto) akiwasilisha mada kwa washiriki wa mradi wa kampeni ya kupambana na ajali za vyombo vya moto barabarani. Kulia ni Ofisa Mradi wa TAMWA, Bw. Edson Sosten.Baadhi ya waandishi wa habari wanaoshiriki uandishi wa habari za usalama barabarani wakiwa katika mafunzo hayo. Baadhi ya waandishi wa habari wanaoshiriki uandishi wa habari za usalama barabarani wakiwa katika mafunzo hayo.Mafunzo hayo ya uandishi wa habari za usalama barabarani kwa waandishi wa habari yakiendelea. Mafunzo hayo ya uandishi wa habari za usalama barabarani kwa waandishi wa habari yakiendelea.

  0 0

  1
  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imetoa sh. bilioni 2.4 kwa ajili ya kuboresha mradi wa maji katika mji wa Makambako mkoani Njombe
  Ametoa kauli hiyo jana jioni (Alhamisi, Januari 19, 2017) wakati akizungumza na wananchi katika uwanja wa Polisi Makambako ulipofanyika mkutano wa hadhara akiwa katika ziara yake ya kikazi mkoani Njombe.
  Waziri Mkuu alisema lengo la Serikali ni kuhakikisha kila mwananchi anapata maji safi za salama katika umbali usiozidi mita 400 kama inavyosema sera ya maji.
  Hata hivyo aliwataka wananchi kutofanya shughuli za kijamii katika vyanzo vya maji ili kuvilinda. Alisema Serikali inatumia fedha nyingi kutafuta maji kwa sababu vyanzo vingi zimekauka kutokana na shughuli za kibinadamu.
  Katika hatua nyingine Waziri Mkuu alizungumzia suala la madai ya fidia kwa wananchi waliopisha ujenzi wa kituo cha ukaguzi cha pamoja na soko la kitamaifa katika eneo la Makambako aliahidi kuwa watalipwa.
  “Fidia zenu mtalipwa hivi katibuni baada ya Serikali kupitia Wizara ya Fedha na Mipango kukamilisha taratibu za ulipaji,” alisema. Wananchi hao walilalamikia ucheleweshwaji wa malipo ya fidia hizo kupitia katika mabango mbalimbali pamoja na mbunge wa Njombe, Mheshimiwa Deo Sanga.
  Serikali imeanzisha eneo la Idofi lililoko Makambako kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha ukaguzi wa pamoja wa magari ya mizigo ili kupunguza vikwazo vya kibiashara barabarani kwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki.
  Kituo hicho kitakuwa na vituo vidogo vya Polisi, Uhamiaji, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Maliasili pamoja na vituo vya mizani.
  Awali mbunge wa jimbo la Njombe Mheshimiwa Sanga alisema moja ya changamoto inayowakabili wakazi wa mji wa Makambako ni ucheleweshwaji wa malipo ya fidia kwa waliopisha ujenzi wa kituo hicho hali inayosababisha baadhi yao kwenda kudai fidia hiyo kwake.
  ”Mheshimiwa Waziri Mkuu leo na sisi wananchi wa Makambako tutapona. Baba Majaliwa hawa wananchi wanadai fidia yao kwa muda mrefu na baadhi yao wamefikia hatua ya kuja kulala nje ya nyumba yangu wakigoma kuondoka hadi niwape ufafanuzi wa malipo yao,” alisema.
  Mbali na kuwasilisha changamoto hiyo mbunge huyo pia aliishukuru Serikali ya Awamu ya Tano kwa jitihada zake za kuboresha maendeleo ya wananchi hususan wakazi wa jimbo la Njombe.
  Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Njombe, Bw. Christopher Ole Sendeka alisema Serikali imetenga sh. bilioni 2.8 kwa ajili ya ujenzi wa daraja la chuma lenye urefu wa mita 95 katika mto Ruhuhu.
  Alisema mkataba wa ujenzi wa nguzo za daraja tayari umesainiwa kati ya mkandarasi wa kampuni ya M/s Lukolo na Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) kwa gharama ya sh bilioni 6.17 na muda wa utekelezaji ni miezi 24.
  Akizungumzia mapambano dhidi ya ugonjwa wa ukimwi Bw. Ole Sendeka alisema mkoa unaendelea na kampeni za upimaji, zilizowezesha watu kufahamu afya zao na kuchukua tahadhari ya jinsi ya kujikinga na kuepuka maambukizi mapya.

  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  IJUMAA, JANUARI 20, 2017.

  0 0

         
       Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO.

  Sekta ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ni sekta muhimu sana katika kujenga uchumi wa nchi kwani bila rasilimali watu wenye afya njema, nchi haiwezi kuwa na uchumi ulio imara.

  Katika kuimarisha rasilimali watu itakayochochea maendeleo ya nchi, Serikali ya awamu ya tano kwa kushirikiana na wadau mbalimbali inajitahidi kuhakikisha huduma za afya za uhakika zinatolewa kwa wingi katika maeneo mbalimbali nchini.

  Kwa kutambua umuhimu wa suala hilo, Serikali ilianzisha ujenzi wa Hospitali ya kisasa katika Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi (MUHAS) kilichopo eneo la Mloganzila nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam ambayo tayari imekamilika na inatarajiwa kufunguliwa mwishoni mwa mwezi Januari mwaka 2017.

  Ujenzi wa Hospitali hiyo ya kipekee na ya aina yake katika eneo la Afrika Mashariki na kati ulianza mnamo Aprili 24 mwaka 2104 na kukamilika Agosti 31 mwaka 2016 ambapo kwa sasa wataalamu wanaendelea kuweka vifaa tiba na kufunga mifumo ya vifaa vya tehama ili kurahisisha kazi hospitalini humo.

  Hospitali hiyo ya kisasa ilijengwa kwa mkopo wa riba nafuu kutoka Serikali ya Korea Kusini pamoja na fedha ya Serikali ya Tanzania hivyo hadi kukamilika kwake imegharimu jumla ya dola za kimarekani milioni 94.5 ambazo ni sawa na Tsh.206.7 bilioni.

  Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo hicho (Muhimbili), Eligius Lyamula amesema kuwa Serikali iliamua kutoa kiwanja chenye ukubwa wa hekari 3800 kwa ajili ya kupanua shughuli za Chuo na kuweza kuzalisha wataalam wa kada mbalimbali za afya ili kuweza kutatua changamoto za afya zinazowakabili wananchi.

  “Hospitali hii ina uwezo wa kuweka vitanda 571 na inategemewa kutibu magonjwa makubwa hivyo tunategemea kupunguza idadi kubwa ya wagonjwa wanaotibiwa katika Hospitali yetu ya Taifa ya Muhimbili pamoja na kupunguza gharama kwa wanaoenda kutibiwa nje ya nchi,” alisema Lyamula.

  Aliongeza kuwa Hospitali hiyo inategemea kutoa huduma za kisasa pamoja na kutoa mafunzo kwa wanafunzi wanaosomea sekta ya afya ili kuondokana na tatizo la upungufu wa watumishi wa kutosha katika sekta ya afya na wasio na ujuzi katika taaluma hiyo.

  Lyamula alifafanua kuwa Serikali iliona tatizo la upungufu wa watumishi wa afya hivyo ikaamua kutafuta fedha kwa ajili ya kujenga chuo hicho ambacho kitakuwa na uwezo wa kudahili wanafunzi 15,000 kutoka wanafunzi 4000 wanaodahiliwa kwa sasa hivyo ni dhahiri kabisa kuwa wagonjwa watapata huduma za uhakika.

  Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mh.Paul Makonda alipotembelea Chuo hicho mnamo Novemba 26 mwaka 2016 kwa ajili ya kuangalia maendeleo ya ujenzi wa chuo hicho alitoa ushauri kwa Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kuweka sheria kwa wanafunzi wanaosomea masomo hayo kwa mkopo kupewa sharti la msingi la kufanya kazi katika hospitali za umma kwa miaka isiyopungua mitatu.

  Hiyo yote ikiwa ni njia ya kutatua changamoto ya watumishi wa afya katika hospitali za Umma kwani imeonekana kuwa wanafunzi wengi wa kada hiyo humaliza vyuo na kukimbilia kufanya kazi katika hospitali za binafsi au nje ya nchi na kuacha hoapitali hizo zikielemewa na idadi kubwa ya wagonjwa.

  Mhe. Makonda alikaririwa akisema kuwa,” wanafunzi wanaosoma sekta ya afya kwa mikopo wanatumia bajeti kubwa ya Serikali na hizo zote zikiwa ni fedha za kodi za wananchi lakini mwisho wa siku wanaondoka bila kuwatumikia wananchi hao waliojitolea fedha zao kuhakikisha wanapata elimu”.

  Aidha, Mhe Makonda aliupongeza uongozi wa Chuo hicho kwa kutenga eneo kwa ajili ya viwanda vya dawa na vifaa tiba pamoja na eneo litakalotumika kujenga kituo kikubwa cha utafiti wa masuala ya sayansi na liahidahidi kusaidiana nao kwa hali na mali katika kuhakikisha ujenzi wa chuo hicho unakamilika.

  Njia nyingine ya kuhakikisha kuna kuwa na watumishi wa kutosha katika hospitali hiyo inayotarajiwa kuwa na watumishi 1300 ni kuhamisha watumishi kutoka katika hospitali mbalimbali nchini ambapo kwa kuanzia watumishi 928 wa awali wameshahamishiwa Hospitalini hapo.

  Katika mkakati wa kuhakikisha wanaongeza idadi ya watumishi ili kuijengea uwezo na ufanisi hospitali hiyo serikali imetoa kibali cha kuajiri watumishi 50 katika mwaka wa fedha wa 2016-17  na wataendelea kuajiri kadiri bajeti itakavyoruhusu.

  Kwa upande mwingine, Serikali imeamua kuweka historia nyingine ya kujenga kituo cha utafiti, mafunzo na tiba za magonjwa ya moyo na mishipa ya damu kitakachojengwa ndani ya eneo hilo la Mloganzila ambapo ujenzi huo unategemewa kuanza mnamo mwezi Mei mwaka 2017.

  Mbali na kuongeza watumishi wa afya wenye weledi na kupunguza adha ya foleni katika hospitali zingine, nchi yetu pia itanufaika kwa kuwa na kituo hicho cha utafiti ambacho kitakuwa kikubwa katika ukanda wa Afrika Mashariki.

  Ujenzi huo unafadhiliwa na Serikali ya Tanzania pamoja na Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB) ambapo kwa awamu ya kwanza ya mradi Serikali imetoa jumla ya shilingi 7,055,000 na ADB imetoa mkopo wa jumla ya shilingi 9,500,000.

  Pia, ili kuhakikisha nchi yetu inapunguza gharama za wananchi kwenda kutibiwa nchi za nje, Serikali itachagua jumla ya wataalam 24 kutoka kada mbalimbali za magonjwa ya moyo na mishipa ya damu kwa ajili ya kupewa mafunzo ya kina kuhusu magonjwa hayo katika hospitali za nje na ndani ya nchi ili waweze kubobea katika kutibu magonjwa hayo hivyo kupelekea wagonjwa kutibiwa hapa hapa nchini.

  Kaimu Makamo Mkuu wa chuo hicho, Lyamula anaendelea kusema kuwa baada ya ujenzi huo kukamilika, uongozi wa chuo unajitahidi kwa hali na mali kutafuta mikopo na misaada mbalimbali nje na ndani ya nchi ili kuweza kuendeleza eneo lililobakia kwa ajili ya ujenzi wa chuo ambao ndio litakua chimbuko la wataalamu wa afya wenye utaalamu wa kutosha.

  Aidha, alifafanua kuwa jumla ya Dola za Kimarekani Milioni 510,696,243 zinaendelea kutafutwa kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za waalimu, madarasa, maktaba, majengo ya utawala, mabweni ya wanafunzi, kumbi za mikutano pamoja na maabara.

  Mkatati wa uboreshaji wa huduma za afya nchini hauishii tu kwenye kujenga hospitali mpya na za kisasa bali pia kuboresha maslahi ya wafanyakazi ili waendane na umuhimu wa kazi wanayoifanya kwaajili ya maendeleo ya nchi yetu.

  Kwakuwa suala la afya ni suala mtambuka ambalo wadau wengi wa maendeleo wanatakiwa kushiriki ni vyema hata sekta binafsi ikaiunga mkono serikali kwa kupeleka huduma za afya kwenye maeneo ambayo hazipatikani ili kuweza kusaidiana na Serikali katika kufanikisha adhma ya kuwa na huduma bora za afya kwa wananchi hasa katika maeneo ya vijijini.

  0 0


  Wakufunzi wanaoingia kufanya mtihani wa kupandishwa madaraja wakiwa katika picha ya pamoja wakisikiliza maelekeo kabla ya kuanza kufanya mtihani huo.

  Wakwanza kushoto ni Master Shihan Shalom Avitan 9th Dan Degree ambaye ni raisi wa shirikisho la West Shotokan Karate Internation duniani ,akifuatiwa na Mkufunzi wa West shotokan Karate Kanda ya kaskazini Dady K.Ramadhan.
  Master Shihan Shalom Avitan 9th Dan akiwa anawapa maelekezo wakufunzi wanaofanya mtihani wa kupanda madaraja kabla ya darasa kuaza rasmi .
  Master Shihan Shalom Avitan 9th Dan degree akiwa tayari kuanza kuwafanyisha mtihani wakufunzi ambao wanahitaji kupanda madaraja .

  wakufunzi wakiwa wanaendelea kufanya mtihani kwa njia ya vitendo mbalimbali ili waweze kupanda madaraja.
  Wakwanza kushoto Mkufunzi Hamis Abdallah akiwania Dan ya nne ,akifuatiwa na aliyepo katikati Sensei Taifa Liwewa naye akiwania Dan ya nne.Picha na Vero Ignatus Blog.
  Wakwanza kushoto ni sensei Hamis Wembo kutoka mkoani Kilimanjaro pamoja na Sensei Ally Iddy kutoka mkoani Arusha wakifanya mtihani wa kuwania Dan ya tatu kwa mujibu wa west Coast Shotokan Karate ASSN.

  Wakwanza kushoto Mkufunzi Hamis Abdallah akiwania Dan ya nne ,akifuatiwa na aliyepo katikati Sensei Taifa Liwewa naye akiwania Dan ya nne,na wa kwanza kulia ni sensei Dady K.Ramadhan akiwania Dan ya tano.Picha na Vero Ignatus Blog.
  Wakufunzi wakiwa katika picha ya pamoja na Master Shihan Shalom Avitan 9th Dan Degree baada ya kumaliza kufanya mitihani kwa vitendo katika hatua mbalimbali .

  Afisa michezo wa jiji la Arusha Mwamvita Okong'o ,akiwa pamoja na Afisa michezo wa Jiji la Arusha Benson Maneno akipokea zawadi kutoka kwa rais wa shirikisho West Shotokan Karate Internation duniani kwa Master Shihan Shalom Avitan 9th Dan Degree

  Wapili kushoto ni Afisa michezo wa Mkoa wa Arusha Mwamvita Okong'o ,walieko kulia kwake ni Afisa michezo wa Jiji la Arusha Benson Maneno,aliyepo katikati ni muwakilishi kutoka kampuni ya Benson ,akifuatiwa na Master Shihan Shalom Avitan na wa kwanza kulia ni Sensei Dady K.Ramadhan.
  Sensei Taifa Liwawa akikabidhiwa cheti cha kuwa Master of Art wa 27 katika shirikisho hilo ulimwenguni mwote .Picha na Vero Ignatus Blog

  Mmoja wa wakufunzi Ally Iddy akipokea cheti kwa kufaulu kuingia Done ya tatu.Picha na Vero Ignatus Blog.
  Na.Vero Ignatus ,Arusha.

  Mafunzo ya karate ya kimataifa yanayoambatana na kufanya mtihani wa kupanda madaraja yamefanyika Jijini Arusha yakiongozwa na Master Shihan Shalom Avitan, kutoka nchini Israel .

  Mafunzo hayo yamefunguliwa na Afisa michezo mkoa wa Arusha Mwamvita Okeng’o ambapo amesema kuwa serikali imeipa michezo kipaumbele ili kupunguza tatizo la ajira nchini na amewataka wanamichezo hao kuuambikiza katika jamii kwa ujumla

  Akijibu risala iliyoandaliwa na West coast Shotokan internation Karate( ASS'N) Afisa michezo huyo wa mkoa amesema kuwa serikali inafanya jitihada ili kuwapatia eneo la kudumu la kufanyia mazowezi kama walivyoomba.

  Naye afisa michezo wa Jiji la Arusha Benson Maneno amesema kuwa michezo inaimarisha afya ,ni ajira hivyo ameitaka jamii kushiriki kikamilifu huku akiwasisitiza vijana kutumia fursa hiyo ili waweze kujiajiri.


  Muandaaji wa mafunzo hayo hapa nchini Sensei Dady Ramadhan ambaye ni Mkufunzi kiongozi amesema kuwa wapo wanakarate wanaocheza Shotokan ambao wana daraja mbalimbali katika taaluma hiyo miongoni mwao wapo waliofanya mtihani na wamepanda daraja

  Aidha amesema kila mwaka wanamuita mwalimu na kufanya mitihani ,hivyo amewataka wale wote wanaotaka kuifunza mchezo huo wahakikishe wanajicfunza kupitia wataalamu ambao wamepitia mafunzo hayo na wenye uzoefu wa kutosha.

  “Unajua kwa sasa mchezo huu unawaalimu wengi ambao wamevamia hawana taaluma kabisa hivyo msikubali kuburuzwa na kufundishwa na hao watawapotosha na kuleta madhara kwani hawazifahamu kanuni na miiko ya karate.”alisema sensei Dady.

  Kwa upande wake sensei Taifa Liwewa ambaye ni Katibu wa shirikisho West Coast shotokan Karate ambaye kitaaluma ni msanifu jukwaa(Stage Craft designer amesema kuwa karate siyo mchezo wa kihuni wala wa watu wasio na elimu bali nimchezo wa watu wote.

  “kuna watu wananishangaza sana wanadhania kuwa watu wote waliokuja kucheza karate ni watu wasiokuwa na elimu,wahuni,siyo kweli mimi nimezaliwa nikaikuta karate nyumbani kwetu,mama yangu mzazi ana miaka 70 lakini bado anacheza karate ,baba yangu alikuwa naye anacheza ,kaka yangu vilevile ,mimi mwenyewe natamani watoto wangu wacheze karate.”alisema sensei Taifa.

  Amesema kuwa karate ina sheria na taratibu zake ,ameongeza kuwa mchezo huo wenye maadili,nidhamu,utiifu pamoja na uadilifu kwani unajenga mwili na kuimarisha afya,amesema zipo nguzo 5za mazowezi,nguzo 9 za mafunzo, pamoja na miiko ya karate 20.

  Wakufunzi walioshiriki katika kufanya mtihani idadi yao walikuwa 13 kutoka Arusha,Kilimanjaro 1,Dar es salaam 4 na imeshirikisha vilabu vitano,mafunzo hayo yalikuwa ya siku tatu kuanzia 18januari hadi 20 januari

  Mafunzo hayo yamefungwa rasmi na mwenyekiti wa chama cha karate mkoa wa Arusha Sensei Dady K.Ramadhani,ambapo amesema kuwa mafunzo ya mwaka huu yamekuwa mazuri na wanafunzi wamefanya mtihani kwa ufahaulu wa hali ya juu,mafunzo kama haya yanatazamiwa kufanyika tena januari 2018

  0 0  Chama chetu kinakabiliwa na chaguzi mbalimbali za kikatiba mwaka huu 2017.

   Yapo mambo mengi yatakayotawala harakati za chaguzi hizo, lakini kubwa la muhimu ni dhahiri wanaccm wangependa hatimaye ziletwe safu mpya kwenye sura za viongozi wa ngazi zote, yaani kuanzia kwenye Matawi, Wilaya,Mikoa hadi (Taifa). Na sala hizi (za mabadiliko) za wanaccm zinatokana na aina ya majukumu yaliyopo mbeleni katika kukabiliana na changamoto mpya zinazotukabili ndani ya chama na katika nchi yetu sisi kama taasisi ya siasa na pia chama tawala.

   MAJUKUMU:
   CCM lazima ifanye kazi kama taasisi yenye ubora wa hali ya juu  kulingana na mazingira ya sasa. Ubora katika kupanga na kutekeleza (Plan and Deliver) na ili kufanikisha hilo ni lazima chama kiwe makini na wale watakao jitokeza kuwania kujaza nafasi hizo ili kuwabaini kama wanakidhi vigezo vinavyohitajika na kuwa makada wanaoweza kuleta mipango endelevu ya siasa za ccm na hatimaye kusimamia utekelezaji wake pasipo na shaka kwa kutumia raslimali zitakazokuwepo.

  Siasa za Tanzania/Africa zinabadilika kwa haraka kutokana na wadau wanaoongezeka (New Generation) ambao mahitaji yao yanabadilika kila wakati na wanatumia nguvu kubwa katika kutaka kuyafikia mahitaji hayo! CCM ni lazima tuwe na safu zinazoweza kumudu kasi hiyo ya mahitaji ya jamii zetu. Lengo kamwe sio kupambana nao bali kutafuta mbinu na nguvu tendaji ya kuweza kutekeleza majukumu ya chama kwa kuzingatia upatikanaji wa matokeo bora.

  Matukio kadhaa yaliyojitokeza wakati wa harakati za kumpata mgombea wa uraisi kwa tiketi ya ccm miaka miwili iliyopita yametoa sura halisi kuwa sio wote waliokuwamo kwenye safu mbalimbali za uongozi wa chama chetu walikuwa na vigezo sahihi vya utumishi bora wa chama. Wengi wao walijionesha wazi kuwa wapo kwenye nafasi zile kwa bahati mbaya au kwa makusudi ya kujitafutia maslahi binafsi kupitia uongozi wa chama, na pengine walipandikizwa na wapinzani wa ccm ili waweze kuhujumu taratibu za chama!

   Na kasoro za kuwa na viongozi wa namna ile zipo kwenye taratibu za chama chetu hasa katika  KUPEMBUA wagombea wa nafasi hizo huko mikoani na hata kwenye jukwaa la taifa. Kamwe ccm isikubali kuendeleza dhana hiyo mbovu katika uchaguzi ujao wa viongozi wa ndani ya chama kwa vyovyote vile. Kama itabainika wagombea waliojitokeza hawana vigezo basi majina yasirudi na uchaguzi uitwe tena au watafutwe wenye sifa hata kama hawakujitokeza kujaza fomu mara ya kwanza.

  CHANGAMOTO:
  Changamoto tulizonazo kwenye chama ni nyingi kwani sisi ni chama tawala hivyo wajibu wetu ni mpana kuliko wenzetu. Lakini kwanza nianze kwa kubainisha mazingira yanayotuzunguka na hapa nitazungumzia mazingira ya nje ya chama.

  Chama kimepata Mwenyekiti mpya (Raisi wetu JPM) hivyo changamoto zimeongezeka kutokana na aina ya utendaji wa kazi wa kiongozi wetu huyo. Wapo pia maadui wapya walioongezeka kutokana na sababu hiyo hiyo ya aina ya msukumo (influence) aliyokuja nayo. Zipo pia sababu za kimaumbile ya siasa za nchi yetu na majirani zetu, na hata muungano wetu na mstakabali wake. Kwa leo nitajikita katika dhana mpya ya ujenzi wa uchumi wa VIWANDA, ambayo ndiyo agenda kuu ya Mhesh.Raisi kwa sasa na wapo tunaomuunga mkono na wale wanaopinga kwa sababu zao za kawaida kabisa. Kuna wengine wanapinga kwa sababu wamezaliwa nchi ikiwa haina viwanda hivyo wanaona kama ndoto isiyotekelezeka, Lakini tulio watu wazima tunakumbuka viwanda vingi vilivyokuwepo hapo zamani katika nchi yetu hivyo hatuna shaka kuwa inawezekana kabisa kuvijenga upya ikizingatiwa kuwa kuna jukumu pia la sekta binafsi katika azma hiyo ambayo itapunguza nakisi ya utendaji mbaya katika uendeshaji wa viwanda hivyo.

  Lakini lengo langu kubwa ni kutoa dokezo ambalo kwangu ni dhahiri ndio nguvu kubwa isiyoonekana katika kuhakikisha kuwa dhana ya viwanda nchini haisongi mbele, Nguvu hiyo haitoki ndani ya nchi pekee bali ipo nje ya mipaka yetu pia. Tukumbuke kuwa wakati wa ujamaa adui yetu alikuwa wale viongozi waliokuwa wanajilimbizia mali, sasa kwenye uchumi wa viwanda adui sio huyo tu, bali pia ni yale makampuni makubwa yaliyokuwa yanazalisha bidhaa nje ya nchi/jirani zetu na kuzileta kwetu kama soko. Hayo makampuni hayajalala usingizi toka Mhesh. Raisi aweke wazi kuwa nchi yetu sasa inaingia kwenye ushindani wa viwanda. Na makazi yao yanaweza kuwa ni nchi jirani zetu ila watatumia influence mbalimbali za ndani ya nchi ili kuyumbisha lengo hilo(distraction). Watafanya hivyo kwa kupenyeza vijisenti kwa watu wasiotutakia mema na kujenga dhana potofu ikiwemo ya uhaba wa chakula, tetemeko,udikteta n.k 

  Kwa hiyo majukumu ya chama kwa sasa ni lazima yaongezeke na kuwa na sura ya uelewa wa kimataifa kwani wabaya wetu hao wataingia hadi kwenye mikoa yetu ambako tunataka kuwekeza viwanda na kwa vile ni dhahiri viongozi wetu wa mikoa wa chama na serikali watahusika kwa namna moja au nyingine katika michakato husika na kama hatutakuwa makini huenda watatumika kuyumbisha dhana hii tukufu ya uchumi wa viwanda. Hivyo kuna kila sababu ya chama kujipanga kiutendaji ili kiweze kuwa mhimili wa mapinduzi haya ya viwanda.

  Wanaccm wenzangu mnapoona Raisi anapigwa madongo si kwa sababu ameshindwa kutekeleza kazi zake za uraisi la hasha, bali inawezekana kabisa ni kumyumbisha ili apunguze umakini (focus) kwenye dhana ya viwanda na uchumi mpya visiwezekane chini ya chama cha mapinduzi.
  Sisi kwenye matawi ya nje tunafuatilia nyendo hizi kwa karibu sana na hatutakubali upotoshaji unaotumia mitandao ya kijamii.

  Kidumu chama cha mapinduzi.

  Kangoma H.Kapinga
  Mwenyekiti-CCMUK.
older | 1 | .... | 1108 | 1109 | (Page 1110) | 1111 | 1112 | .... | 1898 | newer