Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live

KAMATI YA BUNGE YA MALIASILI YAFANYA ZIARA MOROGORO

$
0
0
Mbaolojia wa Mbegu, kutoka Wakala wa Mbegu za Miti Nchini (TTSA), Ndugu Fandey Mashimba akiwalezea wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii namna ambavyo Wakala huo unavyozalisha mbegu za miti.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Mhe. Atashista Nditiye akisikiliza maelezo kutoka kwa Mbaolojia wa Mbegu, kutoka Wakala wa Mbegu za Miti Nchini (TTSA), Ndugu Fandey Mashimba ya jinsi ya uoteshaji wa mbegu za miti.
Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii walipotembelea Ofisi za Wakala wa Mbegu Nchini (TTSA) leo Mjini Morogoro.


Na Debora Sanja, Bunge.

WAKALA wa Mbegu za Miti Tanzania (TSSA) unakabiliwa na uhaba wa fedha hali inayokwamisha uaandaji wa mbegu bora.

Taarifa hiyo ilitolewa Mjini Morogoro jana wakati Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii ilipotembelea Ofisi za Wakala huo.Akiwasilisha mada katika mkutano wa wafanyakazi wa Wakala huo na wajumbe wa Kamati ya Bunge, Mkurugenzi wa TSSA, Edger Masunga alisema kwa sasa fedha inayoapatika kwa ajili ya kuandaa mbegu bora za miti ni kidogo.

Alisema kwa sasa Wakala huo unakusanya mbegu Tani 12 badala ya tani 40 kwa mwaka na kwamba mbegu hizo wamekuwa wakiziuza katika nchi na taasisi mbalimbali nchini.

“Changamoto nyingine tunayokabiliana nayo ni uchomaji wa misitu na miti ya asili ambapo zipo baadhi ya mbegu ambazo zipo hatarini kutoweka,” alisema.Aidha, alisema Wakala huo unao mipango ya muda mrefu na muda mfupi ikiwemo ufunguzi wa mashamba makubwa ya mbegu za miti.

Akizungumzia majukumu ya Wakala huo, Mkurugenzi huyo alisema ni kuzalisha na kusambaza vyanzo bora vya mbegu na kuziuza.Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii Mhe. Atashista Nditiye alisema ziara hiyo ya Kamati ni ya kawaida kwa ajili ya kupokea na kujadili taarifa ya majukumu na changamoto za Wakala huo.

“Tumefanya ziara hii hapa kwa kuwa tunajua umuhimu wa Wakala huu hapa nchini,” alisema.

WAZIRI MWIJAGE AZINDUA BODI YA MAMLAKA YA MAENDELEO YA BIASHARA TANZANIA

$
0
0

Mhe Charles Mwijage akimkabidhi vitendea kazi Mhandisi Christopher Chiza Mwenyekiti mpya wa bodi ya Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara ya Tanzania baada ya uzinduzi wa bodi hiyo


Mhe Charles Mwijage, Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji asisitiza mageuzi ya kiuchumi kwa maendeleo ya watu yanayolenga katika kujenga viwanda na kupunguza biashara ya kuuza malighafi na ilenge kwenye kuhamasisha biashara za kuuza bidhaa zilizoongezwa thamani. 

Hayo aliyasema kwenye uzinduzi wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Maendelo ya Biashara Tanzania (TanTrade) uliofanyika tarehe 16 Januari, 2017 katika ofisi za TanTrade zilizopo kwenye kiwanja cha Mwl J.K Nyerere barabara ya Kilwa. 

Mhe Mwijage amesema kuwa kazi kubwa ya Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) ni kuhamasisha shughuli za biashara Tanzania na wizara ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji ni wizara ambayo matumaini mengi ya watanzania yameangalia huko hivyo watu wanategemea matumaini makubwa sana. 

Akaendelea kwa kusema kuwa kwa mwaka 2017 kwenye maonesho ya 41 ya kimataifa ya biashara ya Dar es Salaam (DITF) yawe ya tofauti kwa watakaokuja kuonyesha bidhaa zao kutoka nchi za nje, waoneshaji hao waje na mashine za viwanda vidogo ili watanzania watakaokuja kuona na kununua mashine hizo ziweze kusaidia kuongeza thamani za bidhaa zao ili kasi ya kuuza malighafi nje ya nchi ipungue bali bidhaa za viwandani ziweze kuongezewa thamani ili kuweza kuuza nje ya nchi. 

Mhe Mwijage aliendelea kuiambia Bodi ya Wakurugenzi iliyoteuliwa kuwa kazi zote ambazo zilisimama zifanyiwe kazi mapema ili kueza kukamilisha maamuzi yote usiku na mchana akaongeza kwa kusema kuwa maamuzi ambayo hayakufanyika ni mabaya mno na gharama zake ni kubwa afadhali maamuzi ambayo yamefanyika ila mabaya hivyo asingependa kufanya maamuzi ya bodi bila bodi kumshauri ili aweze kufanya kazi yake kwa ufanisi. 

Akaongeza kwa kusema kuwa tunapoelekea kwenye uchumi wa viwanda Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) yapaswa kwenda kuwafundisha watanzania ili waelewe kile wanachopaswa kwenda kukiuza nchi za nje na kuwashawishi wale wanaokuja kuonesha bidhaa zao nchini waje kuonesha vitu gani kwetu vyenye tija. Natamani maonesho ya kimataifa ya biashara Dar es salaam (DITF) kuwe na viwanda vidogovidogo vingi, tuwashawishi wanaokuja kuonesha kwa kutumia teknolojia zao ila yatupasa kufanyaTantrade kutumia mwenyekiti wao wafanye survey kwa kuhusisha wataalam kama teknolojia zao zinakidhi haja ya mazingira ya nchi yetu na matakwa ya wananchi.

Mhe Mwijahe akatoa maagizo kwa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) kuulizia ofisi zote za serikali na za watu binafsi ni maonesho gani yaliyopo mwaka 2017 sababu kisheria maonesho yote Tanzania yanasimamiwa na tantrade hata wanaokwenda nje ya nchi kwenye maonesho mbalimbali wapate Baraka za TanTrade kwa kutambulika hivyo asionekane asionekane mtu anaenda bila kupata kibali kupitia TanTrade na pia kuhakikisha taasisi hiyo haitawanyi rasilimali zilizopo bali ikazane kuongeza trade volume za bidhaa za viwanda ziende kwa wingi nje ya nchi. 

Nae mhe Mhandisi Christopher Chiza Mwenyekiti wa bodi mpya ya wakurugenzi kutoka Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) alisema kuwa nguzo kubwa atakayotumia katika kutekeleza majukumu ni sheria iliyoanzisha mamlaka ya kuendeleza Biashara Tanzania ya mwaka 2009 na sheria zingine za nchi. 

Akaendelea kusema kuwa kwa uchache majukumu ambayo atakayosimamia ni pamoja na kusimamia na kujiridhisha kwamba mali za mamlaka zinazohamishika na zisizohamishika zinatunzwa na zinatumika vzuri kwa manufaa ya Umma, Kuelekeza mamlaka kubuni na kutafuta vyanzo mbalimbali vya fedha na kwa fedha zote zitatumika kwa manufaa ya umma, kusaidia mamlaka kubuni na kubaini fursa za biashara na kuziunganisha fursa hizo na wadau mbalimbali ili zijulikane ndani na nje ya nchi kuwawezesha wadau wengine wazichangamkie. Hivyo kama taasisi ya muungano ambayo sehemu kubwa inawagusa makundi mbalimbali ya wazalishaji hawana budi kupanua wigo wa huduma hizo ilikuwafikia kwa ukaribu. 

Mnamo Desemba 17, 2016 Mhe Dkt John Magufuli Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alifanya uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania na kumteua Mhandisi Christopher Kajolo Chiza kuwa mwenyekiti wa Bodi hiyo na kufuatiwa uteuzi wa wajumbe wa bodi hiyo uliofanywa na Mhe Charles Mwijage Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji.

MKUU WA MKOA WA ARUSHA MRISHO GAMBO AONGOZA KIKAO CHA WADAU KUMALIZA MGOGORO WA PORI TENGEFU LOLIONDO

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo akiongoza kikao cha wadau wa kutafuta suluhu ya mgogoro wa matumizi ya ardhi katika Pori Tengefu la Loliondo uliofanyika Kijiji cha Wasso ukiwa ni utekelezaji wa maagizo ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aliyotoa katika ziara yake hivi karibuni mkoani humo.

Mbunge wa Jimbo la Ngorongoro ambaye ni Naibu Waziri wa Kilimo,Ufugaji na maendeleo ya Uvuvi,William Ole Nasha akizungumza katika mkutano huo ,kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo na Mwenyekiti wa CCM mkoa,Lekule Michael Laizer.
Mkuu wa mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo akipokea nyalaka kutoka kwa Mkazi wa Kijiji cha Wasso ,Tina Timan zilizowahi kutumika kutafuta suluhu ya mgogoro huo ambao eneo la Kilometa za mraba 1,500 lilitengwa kwaajili ya kuruhusu shughuli za uhifadhi ya wanyapori jambo linalopingwa na wenyeji.

Afisa Ardhi wa halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro,Kasema Samawa akifafanua namna wilaya hiyo ilivyopanga matumizi bora ya ardhi.





Diwani wa Viti Maalumu katika halmashari ya wilaya ya Ngorongoro,Kijoolu Kakeya akizungumza kwenye kikao kilichowakusanya wadau wote kujadili namna ya kupata suluhu ya mgogoro wa Pori Tengefu la Loliondo mkoa wa Arusha.
Mkazi wa Arash ,Rafael Long’oi akizungumzia namna anavyoufahamu mgogoro huo na namna ya kuumaliza kwa njia ya mazungumzo.

MRADI WA UMWAGILIAJI WA MILIONI 300 KUJENGWA NJOMBE.

$
0
0
Na: Lukelo Mshaura, Njombe.

Halmashauri ya Wilaya ya Njombe imesaini mkataba wenye thamani ya zaidi milioni 300 kwa ajili ya ujenzi wa mradi mkubwa wa umwagiliaji katika kijiji cha Itipingi kilichopo Kata ya Ingongolo Wilayani Njombe,

Mradi huo unafadhiliwa na Shirika la JAICA kutoka nchini Japani ambao utekelezaji wake unaanza januari mwaka huu, utajengwa na mkandalasi Engineering Plus kutoka Dar es Salaama na utatekelezwa kwa kipindi cha miezi nane huku ukisimamiwa kwa pamoja baina ya wataalamu wa umwagiliaji kutoka kanda ya Mbeya na wa Halmashauri ya Njombe. 

Akizungumza wakati wa utiaji saini wa mkataba huo uliohudhuriwa na meneja uendeshaji wa kampuni ya Engineering Plus, wawakilishi wa kikundi cha umwagiliaji skimu ya Itipingi, wataalamu kutoka ofisi ya mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Njombe, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Njombe , Bi Monica PZ Kwiluhya, amewataka wakandalasi kutekeleza mradi huu kwa wakati na ubora unakubalika.

“Kawaida mimi huwa siongezi muda wa kutekeleza mradi kwa kuwa pesa tayari ipo hivyo hakuna visingizio, siko tayari kuona mradi unacheleweshwa pasipokuwa na sababu za msingi maana pesa hizi ni za wafadhili na mradi ukicheleweshwa zinatakiwa zirudi” alisema Kwiluhya. 

Amewataka wakandalasi kushirikiana na wananchi kwa kazi zile ambazo zinaweza kufanywa na wananchi pamoja na kujiepusha na vitendo vitakavyopelekea kukosa ushirikiano kutoka kwa wananchi ambao ndio wamiliki wa mradi..

Kwa upande wake mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Njombe Bw. Valentino Hongoli amewataka wakandalasi kufanya kazi kwa mujibu wa makubaliano yaMkataba kwa kuzingatia tarehe ya kuanza utekelezaji na tarehe ya kumaliza.

“Naomba mfanye kazi kwa kuzingatia thamani ya fedha na kwa viwango vinavyokubalika ili kuweza kutoa mtokeo chanya kwa wananchi” alisema Hongoli.

Kusainiwa kwa mkataba huu kunatoa matumaini kwa wananchi wa Itipingi ambapo awali walikuwa wakitumia mifereji katika kufanya kilimo cha uzalishaji wa mazao mbalimbali ikiwemo chakula na mboga mboga.

Mradi ukikamilika unatarajia kuwanufaisha zaidi ya wakazi 1500 ambao watakuwa wakilima mazao ikiwemo, mahindi, nyanya, vitunguu pamoja na mboga mboga. Mradi huu umekuja wakati muafaka ambapo Halmashauri iko katika hatua za mwisho kukamilisha kituo cha kuzuia upotevu wa mazao ya mboga mboga na matunda ili kuyaongeza thamani ambacho kimejengwa kwa ufadhili wa shirika la MIVARAF mjini Njombe.

Sambamba na hilo mradi huu ukikamilika utasaidia kuinua kipato cha wakulima, kuongeza lishe kwa jamii pamoja na kuiongezea Halmashauri Mapato.


Lukelo Mshaura
Afisa Habari 
Halmashauri ya Wilaya ya Njombe.

MUONGOZO WA MATUMIZI YA MIHURI KWA WENYEVITI WA MITAA NA VIJIJI WASITISHWA.

$
0
0
Na Beatrice Lyimo-MAELEZO

Serikali imesitisha waraka wa muongozo uliotolewa kuhusu matumizi ya mihuri kwa wenyeviti wa Mitaa na vijiji mpaka pale itakaposhirikiana na kukubaliana namna bora ya kuendesha masuala ya kuhudumia wananchi.

Akizungumza na baadhi ya wenyeviti wa mtaa, Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. George Simbachawene amewataka wenyeviti wa mitaa nchini kufanya kazi kwa kuzingatia Sheria na taratibu zilizopo.

Mhe.Simbachawene alisema kuwa nia ya kusitisha waraka huo ni kuweka utendaji mzuri baina ya Serikali na watendaji wake wa chini.

“Utaratibu uliopo uendelee mpaka pale Serikali itakapotoa utaratibu mwingine wa matumizi mbalimbali ya mihuri hiyo baada ya kujadiliwa na kushirikiana vya kutosha” alifafanua Waziri Simbachawene.

Mhe.Simbachawene alisema kuwa kuna baadhi ya wenyeviti wa mitaa wamekuwa wakitumia vibaya mihuri hiyo na kupelekea migongano na migogoro ya ardhi katika vijiji na mitaa ikiwemo maeneo ya Ununio, Temeke.

Mbali na hayo alisema kuwa katika Tangazo la Serikali namba 3 lililotolewa 5 Septemba, 1994 limeeleza baadhi ya vitendea kazi vya mwenyekiti wa mtaa ni bendera yenye nembo ya Halmashauri, daftari ya kutunza kumbukumbu na rejista ya makazi.

Alisema kuwa mamlaka ya mwenyekiti haitokani na mihuri, bali utendaji uliopo ndani ya mtaa au kijiji husika, hivyo mamlaka ya mwenyekiti ipo pale pale na haibemwi na muhuri bali muhuri huonesha nguvu ya ofisi baada ya kuwashirikisha watendaji tofauti ndani ya kijiji katika kutoa maamuzi.

 “Mhuri si mali ya mwenyekiti binafsi, hivyo kwa yeyote atakayekiuka matumizi ya mihuri hiyo Sheria itachukua mkondo wake” alisisitiza Mhe. Simbachawene.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Wenyeviti wa Serikali za Mitaa Wilaya ya Temeke Bakiri Makele, ameahidi kushirikiana na Serikali kwa kutumia mihuri hiyo kwa kufuata Sheria na taraibu zilizopo.

Naye Katibu wa Wenyeviti hao, Marium Machicha alimshukuru Waziri mwenye dhamana kwa kauli aliyoitoa baada ya kuliona tatizo hilo na kuahidi kulifanyia kazi.

Serikali ilitoa Muongozo huo wa namna wa matumizi ya mihuri kwa wenyeviti wa mitaa na vijiji kwa sababu ya matumizi mabaya ya mihuri kwa baadhi ya wenyeviti wa mtaa na vijiji nchini.

JKCI YAOKOA SHILINGI MILIONI 174 KWA KUFANYA UPASUAJI WA MOYO NCHINI.

$
0
0
Daktari wa Taasisi ya Jakaya Kikwete,JKCI, Bashiru Nyangasa katikati akizungumza na waandishi habari juu ya taasisi hiyo inavyofanya kazi leo jijini Dar es Salaam.kulia ni Daktari wa Hospitali ya Apollo, Sathyaki Nambala 

Na: Lilian Lundo - MAELEZO

Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) imeokoa kiasi cha shilingi Milioni 174 kwa kuwafanyia  upasuaji wa moyo wagonjwa 6 katika taasisi hiyo. 

Hayo yameelezwa leo Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Upasuaji JKCI ambaye pia ni Daktari Bingwa Upasuaji wa Moyo  Dkt. Bashir Nyangasa wakati wa mkutano na waandishi wa habari kuhusu mafanikio yaliyotokana na upasuaji huo.

“Kwa mwaka 2017 tumeanza kwa kufanya kambi ya kwanza ya upasuaji kwa kushirikiana na timu ya wataalamu kutoka hospitali ya Apollo, Bangalore ya nchini India na kufanya upasuaji wa moyo kwa wagonjwa sita (6) kati ya hao wanaume ni wanne na wanawake wawili,” alifafanua Dkt. Nyangasa.

Aliongeza kuwa badala ya kuwapeleka wagonjwa hao nje ya nchi, wamewaleta madaktari wa Apollo nchini ambapo imesaidia kupunguza gharama wakati huo huo wataalamu wa JKCI wameweza kujifunza aina mpya ya upasuaji wa magonjwa wa moyo.

Dkt.Ngangasa alifafanua kuwa kama Serikali ingewasafirisha wagonjwa hao 6 kwenda kupata matibabu nje ya nchi gharama ya shilingi milioni 174 ingetumika ambapo kwa kuwafanyia wagonjwa hao hapa nchini gharama ambayo imetumika haizidi shilingi milioni 60.

Upasuaji uliofanyika ni upasuaji wa kuvuna mishipa ya damu mguuni na kuipandikiza katika mishipa ya moyo iliyokuwa imeziba (CABG-Coronary Artery Bypass Graft) ambapo upasuaji huo uliweza kufanyika bila kutumia mashine ya mapafu na moyo.

Aliongeza kuwa upasuaji mwingine uliofanyika ni wa kubadilisha milango ya moyo (Valves) ambayo haikuwa inapitisha damu vizuri. Pia mgonjwa mmoja amefanyiwa upasuaji wa milango miwili ya moyo ambayo iliharibika sana, milango hiyo ilibadilishwa na kupanuliwa kwa kishina cha mshipa mkubwa wa moyo kwa kutumia mfuko wa moyo (Aorta).

Kwa upande wa Mshauri Mwandamizi kutoka hospitali ya Apollo Dkt. Sathyaki Nambala alisema kuwa ni mara ya nne amekuja Tanzania, lakini kwa sasa amekuta kuna jengo jipya kwa ajili ya wagonjwa wa moyo ambalo lina vifaa vyote muhimu na vya kisasa kwa ajili ya upasuaji wa moyo. 

Alongeza kuwa hatua hiyo imesaidia Serikali ya Tanzania kupunguza kiasi kikubwa cha fedha kwa kuwafanyia wagonjwa upasuaji ndani ya nchi badala ya kuwapeleka nje ya nchi.

Vile vile, Mkurugenzi wa Tiba ya Moyo JKCI Peter Kisenge alisema kuwa Taasisi hiyo  inategemea kupokea madaktari kutoka  Afrika na Saudi Arabia kwa  ajili ya upasuaji wa kutanua mishipa ya moyo iliyoziba, kutanua milango ya moyo iliyoziba na kuziba matundu ya moyo.  

Kambi ya madaktari wa Afrika  itakuwepo katika Taasisi hiyo kuanzia tarehe tarehe 23  mpaka 29 mwezi huu, ambapo wagonjwa 15 watafanyiwa upasuaji wa bila kufungua kifua(Catheterization Procedure).

Kambi ya madaktari bingwa kutoka Saudi Arabia  watafanya upasuaji wa bila kufungua kifua (Device Closure) ambapo wagonjwa zaidi ya 55 wenye umri kuanzia miaka 12 na kuendelewa watafanyiwa upasuaji kuanzia tarehe 04/02/2017.

Aidha Madaktari wote nchini na wanachi wa Dar es Salaam na mikoa ya jirani wenye wagonjwa wa moyo ambao wana matatizo hayo ya moyo wameombwa kuwatuma wagonjwa katika Taasisi hiyo ili kupatiwa matibabu. Pia wanaweza kuwasiliana na Dkt. Kisenge kuitia namba 0713 236 502 au 022-2151379.

Introducing Od Y ft Chief Ally Tatizo Moyo Official Video

MASAUNI AFANYA MAZUNGUMZO NA VIONGOZI WA MAHAKAMA YA UMOJA WA MATAIFA (UNMICT-TAWI LA ARUSHA), JIJINI DAR LEO

$
0
0
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) akizungumza na Mkuu wa Mahakama ya Umoja wa Mataifa (UNMICT), Ofisi ya Arusha, Samwel Akorimo (wapili kushoto) na Msajili wa Mahakama hiyo, Dk. Elias Olufemi (kushoto), wakati walipomtembelea Wizarani kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya UNMICT na Wizara hiyo.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto) akimsikiliza Mkuu wa Mahakama ya Umoja wa Mataifa (UNMICT), Ofisi ya Arusha, Samwel Akorimo (kulia) wakati alipokuwa akifafanua jambo kuhusiana na masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya UNMICT na Wizara hiyo. Wapili kulia ni Msajili wa Mahakama hiyo, Dk. Elias Olufemi. Mazungumzo hayo yalifanyika ofisini kwa Naibu Waziri, jijini Dar es Salaam leo.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (watatu kulia), Mkuu wa Mahakama ya Umoja wa Mataifa (UNMICT), Ofisi ya Arusha, Samwel Akorimo (wapili kulia), Msajili wa Mahakama hiyo, Dk. Elias Olufemi (watatu kushoto), wakiwa katika picha ya pamoja na maafisa wengine mara baada ya Mhandisi Masauni kufanya mazungumzo na ujumbe huo, ofisini kwake, jijini Dar es Salaam leo.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) akimkaribisha Mkuu wa Mahakama ya Umoja wa Mataifa (UNMICT), Ofisi ya Arusha, Samwel Akorimo wakati viongozi wa Mahakama hiyo walipomtembelea kiongozi huyo wa Wizara, ofisini kwake, jijini Dar es Salaam leo, kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya UNMICT na Wizara hiyo. Katikati ni Msajili wa Mahakama hiyo, Dk. Elias Olufemi.


MAKUSANYO YA KODI KIPINDI CHA NUSU MWAKA WA FEDHA 2016/17

$
0
0

Katika kipindi cha miezi sita ya mwaka wa Fedha 2016/17 yaani kuanzia Julai hadi Disemba 2016, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imekusanya kodi jumla ya shilingi trilioni 7.27 ikilinganishwa na shilingi trilioni 6.44 ambazo zilikusanywa kipindi kama hicho mwaka wa fedha  2015/16.

Ukusanyaji wa mapato katika kipindi cha nusu mwaka wa fedha 2016/17 umeongezeka kwa asilimia 12.74. Mlinganisho wa makusanyo ya mapato kwa mwaka wa fedha 2015/16 na 2016/17 ni kama ifuatavyo:

MWEZI
MWAKA 2015/16
MWAKA 2016/17
Ongezeko
JULAI
925,384.7
1,069,458.5
15.57
AGOSTI
923,316.9
1,154.222.5
25.01
SEPTEMBA
1,132,310.3
1,378,048.9
21.70
OKTOBA
1,037,179.8
1,131,094.9
9.05
NOVEMBA
1,027, 939.6
1,123,509.7
9.30
DISEMBA
1,403, 189.8
1,414,921.8
0.84
JUMLA
6,449,321.1
7,271,256.26
12.74

Jitihada mbalimbali zinafanywa ili kuhakikisha TRA inaongeza makusanyo kwa kuongeza ufanisi katika ukusanyaji, kuhimiza maadili mema kwa watumishi, kuboresha mifumo ya ukusanyaji, kushirikiana na vyombo vingine vya dola na wananchi katika kuziba mianya ya upotevu wa mapato pamoja na kufuatili, kuhimiza matumizi ya mashine za kielektronik na kuhimiza ulipaji wa kodi ya majengo.  

TRA inaendelea kuhimiza wafanyabiashara wote waliosajiliwa na Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kuwasilisha ritani za VAT kabla ya tarehe 20 ya kila mwezi kama ilivyobadilishwa katika Sheria ya Fedha ya 2016.

Pamoja na hayo tunawakumbusha na kuwahimiza wananchi wa Dar es Salaam ambao hawajafanya uhakiki wa taarifa za Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN) kuhakiki taarifa zao kabla ya tarehe 31 Januari 2017 ili zoezi hilo liweze kuanzishwa katika mikoa mingine.

TRA inatoa wito kwa wafanyabiashara kulipa kodi stahiki kwa hiari na wakati ili serikali ipate mapato yake ambayo yataiwezesha kuwahudumia wananchi wake kikamilifu.

Kwa wafanyabiashara wenye madeni ya nyuma wanashauriwa kujitokeza kuonana na Mameneja wa Mikoa na Wilaya kujadiliana jinsi watakavyolipa madeni yao bila kuathiri biashara zao.

Wamiliki wa majengo wanaaswa kutoa ushirikiano kwa kulipia ankara zao za kodi ya majengo kwa hiari. 

Pamoja Tunajenga Taifa Letu’
Richard M. Kayombo
MKURUGENZI WA HUDUMA NA ELIMU KWA MLIPAKODI


Hukumu kesi ya kutorosha msichana yapigwa kalenda

$
0
0
Na Khadija Khamis –MAELEZO ZANZIBAR 17/01/2017.

MAHAKAMA ya Wilaya ya Kusini Unguja iliyoko Makunduchi, Januari 31, 2016, inatarajia kusoma hukumu ya kesi ya kutorosha msichana aliye chini ya uangalizi wa wazazi wake inayonmkabili mzee wa miaka 58, Khatib Mohammed Khatib.

Mtuhumiwa huyo pamoja na msichana anayedaiwa kumtorosha, wote ni wakaazi wa shehia ya Ngannai Makunduchi, Wilaya ya Kusini Unguja.

Akielezea hatua ya kuakhirishwa kwa hukumu hiyo iliyokuwa ikitarajiwa kusomwa leo Januari 17, 2017, Hakimu wa Mahakama hiyo Ali Abdulrahman, alisema kuna taratibu kadhaa zinahitaji kukamilishwa kabla ya kusomwa kwake.

Katika kesi hiyo iliyoanza kusikilizwa mahakamani Septemba 5, 2016, ilidaiwa kuwa mnamo Agosti 23, 2016, saa 2:30 asubuhi, mtuhumiwa Khatib alimtorosha msichana wa miaka 14 akiwa chini uangalizi wa wazazi wake na kwenda nae hadi Bondeni, shehia ya Nganani Makunduchi.

Kitendo hicho ni kosa kwa mujibu wa kifungu 130 (a) cha sheria ya makosa ya jiani namba 6, ya mwaka 2004, sheria za Zanzibar.

Kufuatia kuakhirishwa kwa hukumu, mshtakiwa huyo anaendelea kuwa nje kwa dhamana hadi siku hiyo ya Januari 31, 2016.

Taarifa zilizopatikana mahakamani hapo, zimeeleza kuwa, hiyo ni kesi ya pili kwa mshtakiwa huyo kushtakiwa kwa kosa kama hilo ikiwemo pia kukashifu, dhidi ya msichana huyo huyo.

Imeelezwa kuwa, katika kesi hiyo ya awali mnamo mwaka 2014, mtuhumiwa Khatib aliachiwa huru na mahakama, baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha makosa yake.

Wakati huo, kesi ilisikilizwa na kutolewa hukumu na Hakimu Mohammed Amour Haji.

MAJALIWA AFUNGUA DUKA LA DAWA LA MSD KATIKA HOSPITALI YA MPANDA

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifungua duka la dawa la MSD katika hospitali ya Mpanda Januari 17, 2017.    Kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Meja Jenerali Mstaafu, Rafael  Muhuga na kulia kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurean Bwanakunu. Kulia ni Waziri wa Nishati na Madini , Profesa Sospeter Muhongo, Wapili kulia ni Mbunge wa mapanda Mjini, Sebastian Kapufi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
1A2800    Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kakitazama dawa za bibadamu baada ya kufungua duka la dawa la MSD katika hospitali ya Mpanda Januari 17, 2017.  Watatu kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurean Bwanakunu na wapili kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Katavi, Muselem Said Abdallah.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipiga makofi  baada ya kufungua duka la dawa  la MSD katika hospitali ya Mpanda  Januari 17, 2017. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurean Bwanakunu na kulia ni Mbunge wa Mapanda Mjini Sebastian Kapufi.

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kakitazama dawa za binadamu baada ya kufungua duka la dawa la MSD katika hospitali ya Mpanda Januari 17, 2017.  Kushoto  ni Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurean Bwanakunu .
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipiga makofi  baada ya kufungua duka la dawa  la MSD katika hospitali ya Mpanda  Januari 17, 2017. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurean Bwanakunu na kulia ni Mbunge wa Mapanda Mjini Sebastian Kapufi.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na viongozi wa dini baada ya kufungua duka la dawa la MSD katika hospitali ya Mpanda Januari 17, 2017
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akizungumza na Elizabeth Zephania , mmoja wa wazazi waliojifungua katika hospitali ya Mpanda  wakati alipotembelea wodi ya wazazi ya hospitali hiyo Januari 17, 2017.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimfariji Bw. Mussa Matemela anayemuuguza mwanae Emmanuel Sahani (3) wakati alipotembelea wodi ya watoto katika  hospitali ya Mpanda Januari 17, 2017.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimfariji  wanawake waliolazwa katika hospitali ya Mpanda wakiuguza watoto wao wakati alipotembelea wodi ya watoto katika hospitali hiyo Januari 17, 2017.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitembelea wodi ya watoto katika hopitali ya Mpanda ili kuwafariji wagonjwa na kusikiliza kero zao Januari 17, 2017.
 Wananchi wa Mpanda wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati aliopowahutubia  kabla  ya kuzindua duka la dawa  la MSD  katika hospitali ya Mpanda Januari 17, 2017.

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi wa Mpanda kabla ya  kufungua duka la dawa la MSD katika hospitali hiyo Januari 27, 2017.

Waziri Mkuu, Kassim  Majaliwa akiwapungia wananchi baada ya kufungua duka la dawa la MSD katika hospitali ya Mpanda Januari 17, 2017. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Meja Jenerali Mstaafu, Rafael Muguga baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Mpanda Januari 17, 2017  ambako  alifungua duka la dawa la MSD.  Wpili kushoto ni Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo na kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Katavi, Muselem  Said Abdallah. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa  akisalimiana na Mbunge wa Mpanda Mjini, Sebastian Kapufi baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Mpanda Januari 17, 2017 kufungua duka la dawa la MSD.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na viongozi na watumishi wa Halmashauri na Manispaa ya Mpanda  na wananchi  kwenye Ikulu ndogo ya Mapanda Januari 17, 2017.

SERIKALI KUENDELEA KUSHIRIKIANA NA VYOMBO VYA HABARI KATIKA UTOAJI WA TAARIFA KWA UMMA

$
0
0
 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza na uongozi na  baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya IPP Media yenye vituo vya Televisheni vya ITV, EATV na Capital Tv alipotembelea na kujionea utendaji kazi wa vituo hivyo Leo January 17, 2017 Jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abass(kushoto) akifafanua jambo kwa uongozi na wafanyakazi wa IPP Media upande wa Televisheni wakati Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye  alipotembelea Kampuni ya IPP Media kwenye vituo vya Televisheni vya ITV, EATV na Capital Tv Leo January 17, 2017 Jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza mara baada ya kuwasili katika kampuni ya IPP media kwa ajili ziara yake ya kujionea utendaji kazi wa vituo vilivyo chini ya Kampuni hiyo Leo January 17, 2017 Jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akipata maelekezo kutoka kwa mmoja ya wafanyakazi wa Ipp Media kuhusuana na ufanyaji kazi wa vituo vya Televisheni vya ITV, EATV na Capital Tv alipofanya ziara kujionea utendaji kazi wa vituo hivyo Leo January 17, 2017 Jijini Dar es Salaam.



  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akiangalia studio ya kutangazia habari katika kituo cha Televisheni cha ITV alipofanya ziara kujionea utendaji kazi wa vituo vilivyo chini ya IPP Media Leo January 17, 2017 Jijini Dar es Salaam.
  Mkuu wa Sahara Media kwa upande wa Dar es Salaam Bw. Cyprian Musiba akifafanua jambo kwa Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye alipotembelea Sahara Media kwa upande wa Dar es Salaam kujionea utendaji wake wa kazi Leo January 17, 2017 Jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza na uongozi na baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Sahara Media alipotembelea na kujionea utendaji kazi wa vituo chini ya kampuni hiyo Leo January 17, 2017 Jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa Masuala ya Utangazaji kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA)  Frederick Ntobi akifafanua jambo kwa uongozi na wafanyakazi wa Sahara Media wakati Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye  alipowatembelea Leo January 17, 2017 Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akiwa katika picha ya pamoja na uongozi na wafanyakazi wa Sahara Media kwa tawi la Dar es Salaam mara baada ya kumaliza ziara yake kwa vituo vilivyo chini ya kampuni hiyo Leo January 17, 2017 Jijini Dar es Salaam. Picha zote na Raymond Mushumbusi WHUSM

Na Raymond Mushumbusi WHUSM.

Serikali imeahidi kuendelea kushirikiana na vyombo vya habari nchini katika kutoa habari kwa ajili ya kuhabarisha umma kuhusiana na mambo mbalimbali yahusuyo Serikali katika kutekeleza majukumu yake.

Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye alipotembelea na kujionea utendaji kazi wa Kampuni ya IPP Media kwenye vituo vya Televisheni vya ITV, EATV na Capital Tv pamoja na Sahara Media kwa tawi la Dar es Salaam.

Katika ziara hiyo Mhe. Nape Moses Nnauye amehaidi kuendeleza ushirikiano baina ya Serikali na vyombo vya habari katika utoaji wa habari ambazo ni muhimu kwa wananchi kujua zikiwemo hatua ambalimbali zinazochukuliwa na Serikali katika kutekeleza majukumu yake katika kuwaletea wananchi maendeleo.

“Niseme kwa kipindi cha nyuma kumekuwa na urasimu wa utoaji wa taarifa muhimu kutoka kwetu kuja kwenu vyombo vya habari lakini niwahakikishe kuwa sasa Serikali imefungua milango kwenu na tuendelee kushirikiana katika kuhabarisha umma wa watanzania” Alisistizia Mhe. Nnauye.

Kawa upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abass amevihakikishia vyombo vya habari nchini ushirikiano mzuri katika kupata habari za Serikali kutoka katika vitengo vyote vya Mawasiliano Serikalini.

Dkt Abass ameeleza kuwa kwa sasa wako katika mpango wa kuboresha vitengo vya Mawasiliano serikali ili kuboresha upatikanaji wa habari zinazohusu Serikali.

“Niwahakikishieni ndugu zangu wanahabari kuwa suala la upatikanaji wa habari kutoka Serikali litakuwa si la kusumbuana tena na tunatengeneza mfumo katika vitengo vyote vya Mawasilaino Serikalini ili iwe rahisi kupata taarifa kutoka kwetu” alisisitiza Dkt Abass.

Aidha Mkurugenzi wa ITV/Radio One Bibi. Joyce Mhavile ameishukuru Serikali kwa kuendelea kushirikiana na Vyombo vya Habari vya binafsi nchini katika kutoa taarifa kwa umma ambazo zimesaidia kuelimisha, kuburudisha na kutengenza mazingira ya watu kuamini yale yanayotolewa na vyombo vyao.

Naye Mkuu wa Sahara Media kwa upande wa Dar es Salaam Bw. Cyprian Musiba ameipongeza serikali kwa kuona umuhimu wa vyombo vya habari nchini  na kuahidi kuongeza ushirikiano baina yao na Serikali katika upashanaji habari.

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye yupo katika ziara ya siku sita kutembelea vituo vya Televisheni kujionea utendaji kazi wa vituo hivyo ikiwa pamoja na changamoto zilizopo ili kupata namna bora ya kuiendeleza sekta ya habari kwa manufaa ya taifa.

WAZIRI MKUU AFUNGUA DUKA LA DAWA MPANDA

$
0
0
*Ni la MSD litahudumia mikoa mitatu ya kanda ya Tabora

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amefungua duka la dawa la Bohari Kuu ya Dawa (MSD) katika hospitali ya Manispaa ya Mpanda lilogharimu sh. milioni 55 litakalohudumia mikoa mitatu ya Kigoma, Katavi na Tabora.

Pia duka hilo itatoa huduma kwa vituo vya kutolea huduma za afya 580 ikiwa ni pamoja na hospitali za rufaa za mikoa miwili ya Kigoma na Tabora, Hospitali za wilaya sita za Nzega, Igunga, Urambo, Kobondo, Kasulu na Mpanda Mji. 

Waziri Mkuu amefungua duka hilo la dawa la MSD, lililoko  katika hospitali ya Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi leo (Jumanne, Januari 17, 2017) ikiwa ni utekelezaji wa agizo alilolitoa kwa MSD Agosti 20, 2016 alipokuwa katika ziara yake ya kikazi mkoani Katavi. Aliuagiuza  uongozi MSD kujenga duka hilo ili kurahisisha upatikanaji wa dawa katika mkoa huo pamoja na mikoa jirani.

Aidha, Waziri Mkuu amesema baada ya kufunguliwa kwa duka hilo Serikali haitarajii kusikia tena katika vituo vya afya na Zahanati zilizoko mkoani Katavi na mikoa jirani  zinakosa dawa. Amewaagiza Wakurugenzi kusimamia suala hilo na kuhakikisha vituo vyote vya afya vinakuwa na dawa za kutosha.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu ameziagiza Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto kukutana na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) ili kutafuta namna bora ya kutumia fedha za huduma za afya zinazipatikana katika halmashauri nchini. 

Aidha, Waziri Mkuu amesema Serikali imetoa sh. bilioni 1.5 kwa ajili ya kuanza ujenzi wa hospitali ya mkoa wa Katavi ili kupunguza msongamano wa wagonjwa katika hospitali ya Manispaa ya Mpanda. 

Amesema lengo la Serikali ni kuwa na Hospitali ya Rufaa kwa kila mkoa, hivyo, Mkoa wa Katavi ni miongoni mwa mikoa mipya itakayojengwa Hospitali ya Mkoa ili kusogeza huduma za afya karibu na wananchi.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Bw. Laurean Bwanakunu amesema ujenzi waduka hilo la Mpanda hadi kukamilika umegharimu sh. milioni 55, huku benki ya CRDB ikitoa sh. milioni 50 na MSD imeweka dawa na vifaa tiba vya sh. milioni 104.45 na vifaa vya TEHAMA vya sh. milioni tano.

Amesema kuanzishwa kwa duka hilo kutaongeza upatikanaji wa dawa na vifaa tiba kwa wagonjwa hasa dawa ambazo hazimo katika orodha zilizoidhinishwa na Serikali kutumika katika vituo vyake vya kutolea huduma za afya ila zimeidhinishwa kutumika nchini na Shirika la Afya Duniani (WHO).

Amesema dawa na vifaa tiba vilivyomo katika orodha ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) zinapatikana katika duka hilo kwa bei nafuu, hivyo kuondoa usumbufu kwa wagonjwa kwenda kuzitafuta katika maduka ya mbali na kwa bei ghali.

“Nitoe mfano mdogo wa tofauti ya dawa katika ya maduka ya MSD na maduka ya mitaani, hapa dawa ya sindano ya kutibu fungus aina ya Fluconazole inauzwa sh. 2,300 na mitaani sh. 4,500 na dawa ya sindano kwa ajili ya kushusha kisukari (Insulin) chupa moja MSD ni sh. 8,500 na mitaani sh. 20,000,” amesema.
(Mwisho)

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMANNE, JANUARI 17, 2017.

Kikundi cha Yamoto Band hakitatumbuiza tamasha la Sauti za Busara

$
0
0
 
JANUARY 16, 2017 — MJI MKONGWE,  ZANZIBAR:  Harakati za kukamilisha taratibu za ushiriki wa kikundi cha Yamoto Band hazikufanikiwa kutokana na changamoto za ugumu wa mawasiliano baina ya uongozi wa kikundi hicho na Uongozi wa Sauti za Busara. Sauti za Busara  imesitisha taratibu za kuruhusu ushiriki wa kikundi cha Yamoto Band kwenye tamasha la mwaka huu kama ilivyotangazwa awali.
Yusuf Mahmoud, Mkurugenzi wa tamasha amesikitishwa na ugumu wa kufanya mawasilaino ndani ya muda husika kutengeneza mazingira mepesi ya uandaaji wa taratibu zote za kuhakikisha kikundi hicho kinakamilisha mahitaji yote ndani ya muda uliopangwa.

“Kuna vipaji vingi sana vya muziki Tanzania.  Vipaji hivi hufifia kwa sababu ya uhaba wa ujuzi kwa mameneja ambao hawajibu barua pepe, wanakataa kusaini mikataba, hawafiki kwenye mikutano hata baada ya kuthibitisha kuwa watashiriki, na hawapokei simu,’’ Yusuf alikaririwa akisema hayo wiki iliyopita kwenye gazeti la Sunday News.

Journey  Ramadhan, Meneja wa tamasha amesema kuwa jitihada za makusudi za kuhakikisha  Yamoto Band wanashiriki tamasha hazikuzaa matunda baada ya yeye kufika Dar es Salaam na kumsubiri meneja wa Yamoto Band afike kwa ajili ya maongezi lakini alisema yuko nje ya mji  na asingeweza kuonana naye.

“Ili kuibua, kung’arisha  na kukuza vipaji vya muziki Tanzania tunahitaji mameneja wenye kuheshimu mawasiliano yatakayowezesha wanamuziki kupata nafasi ya kuonesha vipaji vyao kupitia wadau wa muziki nchini. Pia ni vema msanii apate naasi ya kushiriki kwenye matamasha ya kimataia ni lazima aanye mawasiliano kwa njia ya kieletroniki,’’ amesema Ramadhan.

Uzoefu wa kufanya kazi na mameneja wa wanamuziki  tofauti hapa nchini unaonesha ugumu wa kupokea simu, kushindwa kujibu barua pepe, kuhundhuria kwenye mikutano baina ya wadau wa muziki ili kujadili njia sahihi za kuhakikisha wasanii wanapata nafasi ya ushiriki ni changamoto kubwa zinazorudisha nyuma harakati za kukuza muziki Tanzania, amesema Ramadhan.

Yusuf ametoa wito kwa wasanii na mameneja wao kutumia tamasha la SzB  ambayo ni nafasi pekee  na sahihi ya  kutangaza na kuonesha kazi zao na kupanua wigo wa kung’arisha taaluma zao na kuongeza mawasiliano na wasanii na wadau wa muziki  kutoka sehemu mbali mbali duniani ambao hukutana kwenye tamasha hilo la siku nne mfululizo.
 

BARAZA LA MADIWANI WILAYA YA KAKONKO LAMSIMAMISHA KWA MUDA DIWANI WA CHADEMA KWA UTOVU WA NIDHAMU

$
0
0
Na Rhoda Ezekiel Kigoma,
BARAZA la Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko limemsimamisha kwa muda Diwani wa kata ya Gwalama Elia Kanjero (CHADEMA),kutohudhuria kikao kimoja cha Baraza la madiwani, kwa kosa la utovu wa nidhamu kwa baadhi ya Viongozi wa Serikali na Madiwani.

Adhabu hiyo ilitolewa jana katika kikao cha baraza la madiwani la halmashauri hiyo, ambapo Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Juma Maganga alisema adhabu hiyo imetolewa na kamati ya maadili ya baraza hilo ili kujenga nidhamu kwa madiwani wengine kuwa na nidhamu kama viongozi wanao waongoza Wananchi.

Maganga alisema kosa moja wapo lilopelekea adhabu hiyo ni pamoja na Diwani huyo kwenda kutolea ufafanuzi katika kipindi cha kipimajoto cha ITV wa Rasimu ya kodi ya majengo ambayo ilikuwa haijapitishwa katika halmashauri hiyo na kudai sheria hiyo inayowakandamiza Wananchi bila kibali cha mwenyekiti wa Halmashauri hiyo.

Alisema Katika adhabu hiyo imeshuhudiwa na Mwenyekiti wa halmashauri pamoja na Katibu wake ambae ni Mkurugenzi wa halmashauri na Mtuhumiwa atakabidhiwa barua yake ya adhabu kupitia kwa Afisa utumishi wa halmashauri.

Kwa upande wake Diwani wa kata ya Gwarama Elia Kanjero(CHADEMA) alisema yeye kama kiongozi wa uponzani kuadhibiwa kwasababu ya Wananchi ni faraja kwangu na nitaendelea kuwatetea Wananchi kwa uwezo wangu na nitaitumikia adhabu hiyo.

Kanjero alisema kosa lililopelekea kuadhibiwa ni pamoja na kuwashawishi madiwani kupinga rasimu ya Wananchi kulipa kodi ya majengo pamoja na kwenda kutoa maoni dhidi ya kutoshirikishwa Wananchi katika Baadhi ya mambo yanayo endelea katika halmashauri, jambo ambalo sioni kama ni kosa la kunifanya niadhibiwe.

"Suala lingine lililopelekea Kuadhibiwa ni baada ya Mtendaji wa kata ya Garama kugushi saini yake na kusaini fedha za Mfuko wa maendeleo ya kata baada ya kuleta malalamiko kwa Mkurugenzi wamuhamishi ikawa chanzo cha Mimi kuonekana sina nidhamu suala ambalo nilikuwa nikipigania haki yangu na Wananchi walio nichagua",alisema Kanjero.


RC RUKWA AZUNGUMZIA HALI YA KUTOKUWEPO KWA NJAA MKOANI KWAKE

VIJUSO VYA MAGAZETI YA LEO JUMATANO JANUARI 18, 2017

KAMATI YA BUNGE YA ARDHI, MALIASILI NA UTALII YATEMBELEA MAKAO MAKUU YA TTSA, TAWA NA TAFORI

$
0
0
Mtaalam wa Baiolojia ya mbegu wa Wakala wa Mbegu za Miti Tanzania, Fandey Mashimba (kulia) akitoa ufafanuzi wa namna ya uaandaaji wa mbegu na miche ya miti kwa wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii walipotembelea wakala huyo jana Mkoani Morogoro kwa ajili ya kuona shughuli na miradi ya wakala huyo. Kushoto ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe.
Meneja wa Kanda ya Mashariki na Kati wa Wakala wa Mbegu za Miti Tanzania, Frida Mngulwi (kulia) akitoa maelezo kwa wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii namna mashine za kuandaa mbegu za miti zinavyofanya kazi. Wa pili kushoto ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe.
 Wajumbe wa Kamati ya Bunge, Ardhi, Maliasili na Utalii wakikagua vitalu vya miche ya miti vya wakala wa mbegu za miti Tanzania (TTSA) walipotembelea makao makuu ya wakala huyo mkoani Morogoro jana.
 Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mbegu za Miti Tanzania (TTSA), Edigar Masunga (mbele kushoto) akiongoza wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii kukaga shamba la miti la wakala huyo mkoani Morogoro jana. 
Mkurugenzi wa Mipango na Matumizi Endelevu ya Rasilimali za Misitu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, Mohammed Kilongo (kulia) akifafanua jambo kwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (wa pili kulia) wakati wa kukagua shamba la miti la Wakala wa Mbegu za Miti Tanzania (TTSA) mkoani Morogoro jana.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania (TAFORI), Laurence Mbwambo (kushoto) akitoa maelezo kwa wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii namna taasisi hiyo ilivyojipanga kuendesha tafiti zake na kuhifadhi taarifa za utafiti kwa njia ya mtandao.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (kushoto) akisistiza jambo kwa wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii walipotembelea ofisi za Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania (TAFORI) mkoani Morogoro jana.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (wanne kushoto) akitoa maelezo ya mtandao (kulia) wa kugundua matukio ya moto kwenye maeneo ya misitu nchini unavyofanya kazi kwa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii. Mtambo huo upo chini ya usimamizi na utafiti wa Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania (TAFORI).
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), Martin Laibooki akiwasilisha taarifa ya mamlaka hiyo kwa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii ilipotembelea makao makuu ya mamlaka hiyo mkoani Morogoro jana. Katika taarifa yake ameeleza kuwa katika kipindi cha mwezi Julai hadi Agosti 2016 mamlaka hiyo ilitoa jumla ya shilingi bilioni 2.2 kama faida ya mgao wa mapato ya utalii kwa Halmashauri za Wilaya, vijiji pamoja na Jumuiya za Uhifadhi wa Wanyamapori nchini (WMAs). Hata hivyo alisema changamoto kubwa ya mamlaka hiyo kwenye uhifadhi kwa sasa ni uvamizi wa mifugo ndani ya maeneo ya hifadhi.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utali, Dkt. Aloyce Nzuki (kulia) akiteta jambo na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki wa Wizara hiyo, Dkt. Ezekiel Mwakalukwa wakati kamati ya bunge, Ardhi, Maliasili na Utalii ilipotembelea makao makuu ya TAFORI NA TAWA mkoani Morogoro jana.

Picha ya pamoja ya Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii na viongozi wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Mamlaka ya Wanyamapori Tanzania na Taasisi ya Utafiri wa Misitu Tanzania (TAFORI).
Mtaalamu wa maabara wa Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania (TAFORI) akieleza namna tafiti za misitu zinavyofanywa kwenye maabara ya taasisi hiyo kwa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii.
Baadhi ya watumishi wa Mamlaka ya Wanyamapori Tanzania (TAWA) wakiwa kwenye mkutano wa kamati hiyo ya bunge. 

Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (wa pili kushoto) na Katibu Mkuu wa Wizaya hiyo, Meja Generali Gaudence Milanzi (kushoto) wakiwakaribisha wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii walipowasili katika ofisi za Wakala ya Miti za Mbegu Tanzania (TTSA) mjini Morogoro jana kwa ajili ya kuona kazi na miradi ya wakala huyo. Kushoto ni wajumbe wa kamati hiyo, Silafi Maufi ambaye ni Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Rukwa na Godwin Molel (wa pili kushoto), Mbunge wa jimbo la Siha.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Mhandisi Atashasta Nditiye (kulia) akisalimiana na Mkurugenzi wa Mipango na Matumizi Endelevu ya Rasilimali za Misitu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, Mohammed Kilongo alipowasili na kamati yake katika ofisi za Wakala wa Miti za Mbegu Tanzania mkoani Morogoro jana. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Mipango, Wizara ya Maliasili na Utalii, Marry Faini na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki, Dkt. Ezekiel Mwakalukwa (wa pili kulia).
Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe akiwakaribisha wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii katika ofisi za makao makuu ya Wakala wa Mbegu za Miti Tanzania (TTSA). Kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhandisi Atashasta Nditiye.
Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mbegu za Miti Tanzania (TTSA), Edigar Masunga (wa pili kulia) akiwasilisha taarifa ya wakala huyo kwa Kamati ya Bunge ya Ardhi ya Maliasili na Utalii mkoani Morogoro jana. Alisema wakala huyo huzalisha aina 195 za mbegu, kati ya hizo asilimia 60 ni miti ya kienyeji na asilimia 40 ni miti ya kigeni. Kushoto ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe na kulia kwake ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Mhandisi Atashasta Nditiye.
Katibu Mkuu wa Wizaya ya Maliasili na Utalii, Meja Generali Gaudence Milanzi (kulia) na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Aloyce Nzuki wakifuatilia mada iliyokuwa ikiwasilishwa na Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mbegu za Miti Tanzania (TTSA), Edigar Masunga kwa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii mkoani Morogoro jana. Meja Generali Milanzi alisema Ujangili nchini kwa sasa umepungua kutokana na kasi ya udhibiti wa vitendo hivyo inayofanywa na askari wa wanyamapori kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama. Alisema nyara nyingi zinazokamatwa kwas sasa ni zile za zamani na kwamba uamuzi wa China kuzuia biashara ya meno ya tembo utasaidia kupunguza zaidi ujangili nchini.

(PICHA ZOTE NA HAMZA TEMBA - WMU)

TIZAMA GOLI LA YANGA , PAMOJA NA MAKOCHA WA TIMU ZOTE MBILI WAKIZUNGUMZIA MCHEZO

$
0
0

Timu ya maji maji (WANALIZOMBE) wameshindwa kuutumia uwanja wake wa nyumbani baada ya kufungwa bao moja na YANGA katika mchezo uliochezwa uwanja wa MAJI MAJI mjini SONGEA mkoani RUVUMA, Hapa tumekusogezea goli la YANGA pamoja na mahojiano na makocha wa timu zote mbili.

WAZIRI MBARAWA NA ZIARA YAKE YA KUSHTUKIZA SHIRIKA LA POSTA

$
0
0
Waziri Profesa Mbarwa (kushoto), akimweleza jambo Meneja wa Posta Mkoa wa Dar es Salaam, Margret Mlyomi (katikati), wakati akitembelea Posta Kuu, maeneo ya Posta Mpya jijini Dar es Salaam leo, wakati wa ziara hiyo. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Usalama cha Shirika la Posta Tanzania, George Mwamgabe.
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta, Dk. Harun Kondo (katikati), akimweleza jambo Waziri Profesa Mbarawa, akitembelea vitengo mbalimbali vya Ofisi za Posta Kuu jijijini katika ziara hiyo.
Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Fortunatus Kapinga, akizungumza wakati Waziri Profesa Mbarawa alipokutana na wafanyakazi na kuzungumza nao Makao Makuu ya shirika hilo, wakati akimaliza ziara yake hiyo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta, Dk. Harun Kondo (kulia), akizungumza kabla ya kumkaribisha Waziri Profesa Mbarawa, kuzungumza na wafanyakazi, Makao Makuu ya shirika hilo, wakati wa kumaliza ziara yake hiyo.
Waziri Profesa Makame Mbarawa, akizungumza na wafanyakazi wa Shirika la Posta, Makao Makuu ya shirika hilo, wakati wa ziara yake hiyo.
Ofisa Mwandamizi wa Shirika la Posta, Makao Makuu, David Hango, akizungumza wakati akimweleza Waziri Profesa Mbarawa baadhi ya changamoto zinazolikabili na kukwamisha shirika hilo katika kupiga hatua za kimaendeleo.
Mmoja wa wafanyakazi wa shirika hilo kutoka Chama cha Wafanyakazi cha Tewuta, Ahmed Kaumo, akimweleza Waziri Profesa Mbarawa baadhi ya changamoto ambazo angependa kuwa na kikao cha pamoja cha Viongozi wa shirika hilo na wa chama hicho cha wafanyakazi katika kukabiliana nazo ili kulikwamua shirika hilo.
Mmoja wa wafanyakazi wa shirika hilo, upande wa Masoko, Joyce Kagose, akimweleza Waziri Profesa Mbarawa changamoto mbalimbali zinazolikabili shirika hilo.
Mmoja wa wafanyakazi wa zamani wa shirika hilo, akimweleza kwa uchungu Waziri Profesa Mbarawa jinsi changamoto wanazozipata kutoka kwa baadhi ya watendaji wa shirika hilo, ambao hujifanya wasomi na kuwazarau wale wa zamani kutokana na elimu zao.
Waziri Profesa Makame Mbarawa (katikati), akisikiliza maelezo yaliyokuwa yakitolewa na wafanyakazi hao.
Waziri Profesa Makame Mbarawa, akijibu baadhi ya hoja na ushauri wa wafanyakazi wa shirika hilo, wakati wa ziara yake hiyo.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano,Profesa Makame Mbarawa akiwasili Ofisi za Posta Kuu ya Shirika la Posta maeneo ya Posta Mpya wakati alipofanya ziara ya kushtukiza Dar es Salaam leo. Kulia ni Postamasta Mkuu, Fortunatus Kapinga.(Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (kushoto), akipatiwa maelezo na Meneja wa Posta Mkoa wa Dar es Salaam, Margret Mlyomi (katikati), wakati alipofika katika ziara ya kushtukiza kwenye Ofisi za Shirika la Posta, Posta Kuu jijini Dar es Salaam leo kuangalia shughili mbalimbali zinavyofanyika ofisini hapo.
Mkuu wa Kitengo cha Usalama cha Shirika la Posta Tanzania, George Mwamgabe (kushoto), akimpatia maelezo Waziri Profesa Mbarwa kuhusu mambo ya usalama kwenye mtandao wa shirika hilo. Kulia ni Kaimu Meneja Mkuu wa Shirika la Posta, shughuli za biashara, Janeth Msofe.
Waziri Profesa Mbarwa, akimsikiliza mteja wa shirika hilo, Mhandisi Nungu Allanus kutoka DIT, kuhusu ubora wa utoaji huduma wa shirika. 
Waziri Profesa Mbarwa (kulia), akisikiliza maelezo kutoka kwa Msaidizi Meneja wa Fedha na Huduma wa shirika hilo, wakati alipotembelea kitengo kipya cha kutolea huduma mbambali za kifedha cha Jamii Centre. Katika Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika, Dk. Harun Kondo.
 
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live




Latest Images