Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46379 articles
Browse latest View live

Taasisi za umma marufuku kujenga vituo binafsi vya kuifadhi Data

$
0
0

Afisa Mkuu wa Ufundi wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Bw Senzige Kisenge (aliyenyoosha mkono), akitoa maelezo ya Utendaji wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe Prof Makame Mbarawa (Katikati) alipotembelea Makao Makuu ya TTCL leo jijini Dar es Salaam.Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe Prof Makame Mbarawa (Wa pili kushoto) akizungumza na baadhi ya wateja wa TTCL waliotembelea Kituo cha Huduma kwa Wateja kilichopo Makapo Makuu ya Kampuni hiyo mara baada ya kukitembelea Kituo cha Serikali cha Kuhifadhia Data na Kumbukumbu (NIDC) kilichopo kijitonyama Jijini Dar es Salaam leo. Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe Prof Makame Mbarawa (Wa pili kushoto) akizungumza na baadhi ya wateja wa TTCL waliotembelea Kituo cha Huduma kwa Wateja kilichopo Makapo Makuu ya Kampuni hiyo mara baada ya kukitembelea Kituo cha Serikali cha Kuhifadhia Data na Kumbukumbu (NIDC) kilichopo kijitonyama Jijini Dar es Salaam leo.Pichani ni Muonekano wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano unavyofanya kazi. Pichani ni Muonekano wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano unavyofanya kazi.Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe Profesa Makame Mbarawa akizungumza na menejimenti ya Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) leo alipotembelea Makao Makuu ya TTCL na Kituo cha Serikali cha Kuhifadhia Data na Kumbukumbu (NIDC) kinachoendeshwa na kampuni ya TTCL. Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe Profesa Makame Mbarawa akizungumza na menejimenti ya Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) leo alipotembelea Makao Makuu ya TTCL na Kituo cha Serikali cha Kuhifadhia Data na Kumbukumbu (NIDC) kinachoendeshwa na kampuni ya TTCL.Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Bw. Waziri Kindamba (kulia) akizungumza kabla ya kumkaribisha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe Prof Makame Mbarawa (hayupo pichani) alipotembelea Makao Makuu ya TTCL leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Kaimu Afisa Mkuu wa Fedha wa TTCL, Prygod Kimweri. Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Bw. Waziri Kindamba (kulia) akizungumza kabla ya kumkaribisha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe Prof Makame Mbarawa (hayupo pichani) alipotembelea Makao Makuu ya TTCL leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Kaimu Afisa Mkuu wa Fedha wa TTCL, Prygod Kimweri.Baadhi ya maofisa waandamizi wa TTCL wakiwa katika mkutano huo na waziri. Baadhi ya maofisa waandamizi wa TTCL wakiwa katika mkutano huo na waziri.Kaimu Mkurugenzi wa TEHAMA toka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Bi. Nikusubila Maiko (wa kwanza kulia) akiwa katika mkutano huo. Kutoka kushoto ni Meneja Ufundi wa NIDC, Kironde Kaijage pamoja na Katibu wa Waziri Prof. Makame Mbarawa wakiwa katika mkutano huo. Kaimu Mkurugenzi wa TEHAMA toka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Bi. Nikusubila Maiko (wa kwanza kulia) akiwa katika mkutano huo. Kutoka kushoto ni Meneja Ufundi wa NIDC, Kironde Kaijage pamoja na Katibu wa Waziri Prof. Makame Mbarawa wakiwa katika mkutano huo.

 SERIKALI imezitaka taasisi zake kote kuachana na mpango wa kujenga Vituo binafsi vya vya kuhifadhia kumbukumbu (Data Center) na badala yake kutumia Kituo cha Serikali cha kuhifadhia Data na kumbukumbu (NIDC) chenye uwezo na hadhi ya Kimataifa. Agizo hilo limetolewa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe Profesa Makame Mbarawa baada ya kufanya ziara ya kutembelea kituo hicho cha Kimataifa cha kuhifadhia kumbukumbu za kimtandao na Makao Makuu ya Kampuni ya Simu Tanzania TTCL. 

Mheshimwa Mbarawa amesema, Serikali imetumia fedha nyingi sana kujenga miundo mbinu ya kituo hicho mahiri katika eneo lote la Afika Mashariki na kusisitiza kuwa, Taasisi za Serikali ni lazima zitumie kituo hicho na kwa zile zenye mpango wa kujenga vituo binagsi, ziachane na mpango huo ambao ni matumizi mabaya ya fedha za Umma.

 'Natoa agizo kwa taasisi zote za Umma, ziachane kabisa na mpango wa kujenga Data Centres. Serikali imebeba jukumu hilo, imejenga kituo cha hadhi ya juu kabisa, sote tukitumie kituo hiki. Kila taasisi zijikite katika majukumu yao ya msingi, hili la Data Centre watuachie Serikali kwa kuwa tumeshalitekeleza, hatuwezi kuendelea kutumia fedha nyingine kwa eneo hili, tuelekeze fedha hizo katika maeneo mengine muhimu.' 

Akiwa katika Makao Makuu ya Kampuni ya Simu nchini TTCL, Mhe Mbarawa ameitaka Menejimenti ya Kampuni hiyo kuongeza kasi ya utendaji kazi na ubunifu ili kukabiliana na ushindani uliopo katika sekta hiyo sambamba na kukidhi kiu ya Wananchi ya kupata huduma Shirika lao.Mkuu wa Kituo cha Serikali cha Kuhifadhia Data na Kumbukumbu (NIDC), Abdul Mombokaleo (kulia) akimfafanulia jambo Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe Profesa Makame Mbarawa (kushoto) alipotembelea kukagua utendaji kazi wa kituo hicho. Mkuu wa Kituo cha Serikali cha Kuhifadhia Data na Kumbukumbu (NIDC), Abdul Mombokaleo (kulia) akimfafanulia jambo Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe Profesa Makame Mbarawa (kushoto) alipotembelea kukagua utendaji kazi wa kituo hicho.

'TTCL mna deni kubwa kwa Wananchi. Tumeondoa vikwazo vingi vilivyokuwa vikiwakwamisha na sasa tunataka kuona kasi ya uhakika ya utendaji kazi. Tumewalipa Bharti Airtel na kuvunja ubia nao, tumewafutia madeni, tumewakabidhi Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano na Kituo cha Kimataifa cha kuhifadhia kumbukumbu mviendeshe kwa niaba ya Serikali. 

Yote haya yamefanyika kwa nia moja ya kuwajengea uwezo ili mtimize majukumu yenu vizuri.' amesema Waziri Mbarawa. Katika hatua nyingine, Waziri Profesa Mbarawa amepongeza jitihada kubwa zinazofanywa na TTCL katika kuboresha huduma zake nchini. Aidha, Mhe Mbarawa ameeleza kuridhika kwake na kasi kubwa ya kusambaza huduma za mtandao wa 4G LTE na kujitangaza zinazofanywa na Kampuni hiyo katika maeneo mbali mbali nchini. 

 Awali katika taarifa yake fupi kwa Mhe Waziri, Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL Bw Waziri Kindamba amesema, hadi kufikia Januari 16, 2017 Mikoa 7 ya Tanzania bara inapata huduma kwa teknolojia ya 4G LTE ambayo ni Dar es Salaam, Dodoma, Pwani, Morogoro,Mwanza, Mbeya na Arusha. Tarehe 11 Januari 2017, siku moja kabla ya maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, TTCL ilizindua huduma za 4G LTE mjini Unguja. 

Bw Kindamba ameongeza kuwa, kutokana uhusiano wa shughuli za kiuchumi na kijamii baina ya Visiwa vya Unguja na Pemba, TTCL inakusudia kupeleka huduma za 4G LTE Kisiwani Pemba katika muda mfupi ujao ili kulifanya eneo lote la Tanzania Visiwani kufikiwa na huduma na kusaidia katika ukuaji wa shughuli za kiuchumi,huduma za kijamii,ulinzi na usalama katika maeneo hayo.

Waziri Makamba atoa maelekezo katika kikao kazi

$
0
0
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe  January Makamba akiwasili katika Chuo Kikuu cha Mzumbe kwa ajili ya Kikao kazi cha Menejimenti ya Ofisi yake.  Kushoto ni Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Prof. Faustin Kamuzora.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe  January Makamba (kushoto) akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Eng. Ngosi Mwihava mara baada ya kuwasili katika Chuo Kikuu cha Mzumbe kwa ajili ya Kikao kazi cha Menejimenti ya Ofisi yake.
 Sehemu ya Menejimenti timu wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe  January Makamba kabla ya kuanza kikao kazi katika Ukumbi wa Mikutano wa Chuo Kikuu cha Mzumbe mjini Morogoro.
 Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Prof. Faustin Kamuzora (kulia) na Eng. Bonaventure Baya Mkurugenzi Mkuu (NEMC) wakifuatilia hotuba ya ufunguzi katika kikao kazi kinachoendelea katika Ukumbi wa Chuo Kikuu cha Mzumbe.
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Sera na Mipango Bw. Ntime Mwalyambi akiwasilisha mada katika kikao kazi kinachoendelea katika Ukumbi wa Mikutano wa Chuo Kikuu cha Mzumbe.

NEWZ ALERT:RAIS DKT MAGUFULI AFANYA UTEUZI WA WABUNGE WAWILI NA BALOZI MMOJA.

VIJUSO VYA MAGAZETI YA LEO JUMANNE JANUARI 17, 2017

WENGI WAJITOKEZA KUMUAGA AMINA ATHUMAN DAR

$
0
0
 Waombolezaji wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Mwandishi wa Habari za Michezo wa Gazeti la Uhuru, Amina Athuman  walipokuwa wakioutoa nyumbani kwake Banana, Dar es Salaam leo, kuliingiza kwenye gari tayari kusafirishwa kwenda nyumbani kwao Lushoto kwa mazishi. (PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG)
 Mwili wa aliyekuwa Mwandishi wa Habari za Michezo wa Gazeti la Uhuru, marehemu  Amina Athumani ukiombewa dua nyumbani kwake, Banana, Ukonga.
 Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania, Juma Pinto (kushoto) akimzungumzia marehemu Amina kuhusu uchapakazi wake enzi za uhai wake
 Baadhi ya waombolezaji wakiwemo wanahabari wakiwa eneo la msiba nyumbani kwa marehemu Amina Athuman, Banana, Ukonga Dar es Salaam
 Mwili ukpelekwa kwenye gari

 Mhariri Msanifu Mkuu wa Gazeti la Jambo Leo, ambaye kabla ya kujiunga na gazeti hilo alikuwa Mhariri Mtendaji wa gazeti la Uhuru,Joseph Kulangwa (kushoto), na Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania, Juma Pinto wakiwa na huzuni wakati jeneza lenye mwili wa Amina Athuma likitolewa ndani tayari kusafirishwa kwenda Lushoto.
 Mgane wa marehemu Amina, Towfiq Majaliwa
 Ndugu wa marehemu
 Kiongozi wa kundi la wasapu la Waandishi wa Habari za Michezo Innocent Okamwa (kulia) akimkabidhi Baba mkubwa wa marehemu Amina Athuman, Athuman Kazukamwe mchango wa rambirambi sh. 600,000 zilizochangwa na wanahabari wa kundi hilo.Katikati ni mwanachama wa kundi hilo, Somoye Ng'itu.
 Kazukamwe akitoa shukrani kwa mchango huo

 Sehemu ya waombolezaji
 Mgane wa marehemu Amina, Towfiq Majaliwa akifarijiwa na Naibu Mhariri Mtendaji wa gazeti la Uhuru
Wanahabari wakiwa na huzuni

RITA KABATI: WAPINZANI HAWATASHINDA UCHAGUZI MDOGO WA KATA YA IGOMBAVANU NA IKWEA

$
0
0
 
Mbunge wa viti maalumu mkoani Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Rita Kabati akimpigia kampeni mgombea udiwani wa kata ya Igombavanu na kuwataka wapinzani kusahua kama watashinda katika kampeni za kuwania kiti cha udiwani katika kata ya Igombavanu tarafa ya Sadani wilayani Mufindi mkoani iringa zinaendelea kupamba moto huku uchaguzi ukitarajiwa kufanyika siku ya tarehe 22 /01 /2017.
 katibu wa chama cha mapinduzi wilaya ya Mufindi Jimson Mhagama amewataka wananchi kuwataa kabisa wapinzani kwa kuwa si waadilifu katika kuleta maendeleo
 Mbunge wa jimbo la Mufindi kaskazini Mahamood Mgimwa aliwaomba wapiga kura kumpigia kura nyingi diwani wa chama cha mapinduzi Rashidi Mkuvasa ili awe diwani wa kata ya Igombavanu na kuwa kiungo muhimu kuwaletea wananchi maendeleo
Mgombea udiwani wa kata hiyo kupitia chama cha mapindizi (CCM) Rashidi Mkuvasa amesema wananchi wanapaswa kuwa makini na mbinu chafu zinazotumiwa na wapinzani wake kwa kuwalaghai wananchi kwa kununua vitambulisho 

Na fredy mgunda,Iringa

MBUNGE wa viti maalumu mkoani Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Rita Kabati amewataka wapinzani kusahua kama watashinda katika kampeni za kuwania kiti cha udiwani katika kata ya Igombavanu tarafa ya Sadani wilayani Mufindi mkoani iringa zinaendelea kupamba moto huku uchaguzi ukitarajiwa kufanyika siku ya tarehe 22 /01 /2017.
 
Akizungumza wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika katika kijiji cha Makongomi mbunge Kabati aliwaambia wananchi kuwa jimbo la Mufindi kaskazini na wilaya ya Mufindi kwa ujumla ni ngome ya chama cha mapinduzi (CCM) hivyo wapinzani wasipoteze muda wa kupiga kampeni kwa kuwa hawawezi kushinda chaguzi zote za jimbo hilo.

Kabati alisema kuwa wananchi wa wilaya ya Mufundi bado wanakipenda chama cha mapinduzi na wanahakika watashinda kutokana na mapokeo mazuri kutoka wapiga kura ambao wanazikubali sera za chama cha mapinduzi na wanaendelea kumuamini rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

“Mimi nikiangalia naona nyuso za furaha tu hapa na nimepemda kuwa mmetukikishia kushinda uchaguzi huu basi furaha yangu itakuwa siku ile diwani wetu kutoka chama cha mapinduzi anatangazwa kuwa mshindi kwa kura nyingi,nawapenda na naomba mkipe kura nyingi chama cha mapinduzi”.alisema Kabati 

Naye mbunge wa jimbo la Mufindi kaskazini Mahamood Mgimwa aliwaomba wapiga kura kumpigia kura nyingi diwani wa chama cha mapinduzi Rashidi Mkuvasa ili awe diwani wa kata ya Igombavanu na kuwa kiungo muhimu kuwaletea wananchi maendeleo.

“Jamani nipeni huyu diwani ili tuendelee kufanya maendeleo kwa kuwa mimi mnaniamini basi naomba mpeni kura nyingi na kuondokana na maneno machafu kutoka kwa wapinzani kwani wapinzani hawana jipya saizi”.alisema Mgimwa 

Kwa upande wake katibu wa chama cha mapinduzi wilaya ya Mufindi Jimson Mhagama amewataka wananchi kuwataa kabisa wapinzani kwa kuwa si waadilifu katika kuleta maendeleo,alimalizia kwa kuwaomba wananchi wa kata hiyo kumchagua Rashidi Mkuvasa kwa kuwa ni kiongozi mzuri na atawaletea maendeleo wananchi wa kata hiyo.

“Tumeona wagombea wengi wakija hapa kupiga kampeni na kuomba kura kwa njia ya matusi na kuhamasisha kutomchagua kiongozi furani pasipo kutaja au kuongelea hata hoja za msingi kwanini wanaomba kura zetu” alisema Mhagama

Mgombea udiwani wa kata hiyo kupitia chama cha mapindizi (CCM) Rashidi Mkuvasa amesema wananchi wanapaswa kuwa makini na mbinu chafu zinazotumiwa na wapinzani wake kwa kuwalaghai wananchi kwa kununua vitambulisho au kunakili namba za vitambulisho hivyo
.
“Tuwakatae viongozi wa namna hiyo kwa kuwa lengo lao ni kutaka kununua uongozi kwa nguvu ya pesa na kuwa wao sio chaguo la wanachi hivyo wananchi msithubutu kufanya hivyo mtapoteza haki yenu ya msingi na hamtampata kiongozi atakaye waletea maendeleo”.alisema Mkuvasa

Aidha wananchi wa kata ya Igombavanu katika jimbo la Mufindi Kaskazini wamempongeza mgombea udiwani wa kata kupitia tiketi ya chama cha mapinduzi (CCM) Rashidi Mkuvasa kwa kufanya kampeni za kistaarabu na kuwapa matumaini kuwa atakuwa kiongozi mzuri na kuwaletea maendeleo katika kata hiyo.

SOKO LA PARETO NI UHAKIKA WANANCHI KILOLO LIMENI PARETO -DC ASIA

$
0
0

mkuu  wa  wilaya ya Kilolo  mkoani  Iringa Asia Abdalah  wa  tatu  kushoto  akishiriki  kupanda  miche  ya  Pareto  kwenye  shamba  la mtaalam  wa  Pareto Kilolo wakati wa  uzinduzi  wa kilimo  cha Pareto leo

DC  Kilolo katikati  akipata  maelezo ya miche ya Pareto
Mkuu  wa  wilaya ya  Kilolo na  timu ya uhamasishaji wa kilimo  cha Pareto  wakitoka  kutazama  vitalu  vya miche ya  Pareto
Mkuu  wa  wilaya ya  Kilolo Asia  Abdalah  akitazama  vitalu  vya  miche  ya  Pareto  miche ambayo inatolewa  bure kwa  wakulima
Mtaalam  wa  kiwanda  cha  Pareto Mafinga Godfrey  Mbeyela  kulia  akishirikiana na  Dc Kilolo  Asia Abdalah kupanda Pareto
Na MatukiodaimaBlog

MKUU wa wilaya ya Kilolo Asia Abdalah ameanza jitihada za kuhamasisha wananchi wa wilaya hiyo kulima zao la Pareto kama zao la biashara.

Akizungumza na wananchi wa Udekwa na Lulanzi leo, amesema kuwa Kampeni maalum ya kuhamasisha kilimo cha zao La Pareto zimeanza leo  kwa kupanda Pareto pia kuona vitalu vya miche ya pareto.

Alisema kimsingi miche hiyo itatolewa bure kwa kila Mwananchi anayehitaji kulima zao hilo.Alisema pamoja na kupanda mazao mengine ya Chakula na biashara wasiache kupanda japo hekari moja ya zao La Pareto.

Mkuu huyo alisema kuwa  zoezi La uhamasishaji upya wa zao La Pareto litafanyika katikati kata mbali mbali za Wilaya ya Kilolo.Kwani kati ya Wilaya ambazo zilikuwa zikilima zao La Pareto kwa mkoa wa Iringa Wilaya ya Kilolo ni moja ya wilaya ambazo zilikuwa zikilima zao hilo.

Kuhusu soko aliwataka wakulima kuondoa hofu kwani soko kwa sasa ni uhakika

"Nawaagiza mabwana shamba kutoka ofisini na kwenda kwa wananchi kuwapa Elimu juu ya kilimo cha Pareto"Alisema kuwa zao La pareto limekubali sana Wilaya ya Kilolo kutokana na hali ya hewa ya ubaridi na kuwa zao hilo halihitaji mbolea

Aidha aliwataka wananchi hao kuanzisha vikundi vya kulima zao hilo japo mtu mmoja mmoja anaruhusiwa kulima "Mimi mwenyewe nitatafuta eneo La kulima Pareto… ila sisemi muache kulima mahindi kwenye heka zako 10  tenga heka moja ya Pareto"

Katika hatua nyingine amewataka wakulima kutumia mvua zinazoendelea kunyesha kupanda mbegu za muda mfupi zaidi.Mtaalamu wa Kiwanda cha Pareto Mafinga Godfrey Mbeyela alisema kwa mbegu za Pareto zimeandaliwa na wanategemea wananchi zaidi ya 40 elfu kulima zao hilo.Alisema kwa wilaya ya Kilolo daraja La chini litanunuliwa kwa Tsh 2000 Kwa wakulima wa Pareto Kilolo

Alisema kuwa soko la Pareto liliyumba kutokana na mwekezaji aliyekuwepo ila sasa soko lipo La uhakika na kuwa pesa zitalipwa kijijini moja kwa moja.Alisema kuwa kuwa katika Wilaya nyingine kama Ludewa na Njombe  wanagombea kulima zao hilo.

Hivyo aliwaomba viongozi   wa dini mbali mbali kutumia Nyumba za ibada kuhamasisha wananchi kulima zao hilo.

Kwa  upande  wao  wananchi  wa Kilolo  wameeleza  kufurahishwa na utaratibu  huo  wa Kiwanda  kugawa  miche  bure na  kuwa  wapo tayari  kuanza  tena  kulima  zao  hilo ambalo awali  walikuwa  wakilima kwa  wingi  zaidi 











































WILAYA MPYA YA KIBITI YAANZA KUTEKELEZA AGIZO LA NAIBU WAZIRI SELEMAN JAFO KUBORESHA SEKTA YA AFYA VIJIJINI

$
0
0
NA VICTOR MASANGU, KIBITI

UONGOZI wa halmashauri mpya ya Wilaya ya Kibiti Mkoani Pwani imeanza kutekeleza maagizo yaliyotolewa Naibu waziri ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI) Seleman Jafo ya kuhakikisha wanaboresha sekta ya afya hususan katika maeneo ya Delta kwa kununua vifaa tiba, madawa, pamoja na vitanda maalumu kwa ajili ya kujifungulia wakinamama wajawazito.

Akizungumza na waandishi wa habari  katika mahojiano maalumu kuhusina na utekelezaji wa maagizo hayo ya naibu Waziri Mkurugenzi mtendaji wa  halmashauri ya Wilaya ya Kibiti Alvera Ndabagoyo alisema kuwa kwa sasa tayari wameshaanza kununua vifaa mbali mbali katika zahanati  ili kuweza kuboresha huduma kwa wagonjwa wanaokwenda kupatiwa matibabu.

Alvera alisema kwamba hapo awali katika sekta ya afya hasa kwa upande wa wananchi waliokuwa wanaishi  maeneo ya visiwani (Delta) walikuwa wanakabiliwa na changamoto  ya upatikanaji wa huduma ya afya kwa kipindi kirefu kutoka na sehemu zenyewe ufikaji wake kuwa ni  mgumu kutokana na kutumia usafiri wa majini.

“ Ni kweli hivi karibuni Naibu Waziri ofisi ya Rais Seleman Jafo alifanya katika Wilaya yetu mpya ya Kibiti, na kuweza kukagua miradi mbali mbali ya maendeleo na kujionea changamoto zinazowakabii wananchi,hivyo alituagiza sisi kama watendaji tujipange na kuweza kuzitafutia ufumbuzi wa kudumu changamoto hizo,hasa katika sekta ya afya na kimsingi tumefanikiwa kwa kiasi kikubwa kununua mambo muhimu ambayo yanahitajika kwa wananchi wetu,”alisema Mkurugenzi huyo.

Alibainisha kuwa licha ya Wilaya hiyo ya Kibiti kuwa ni mpya lakini uongozi wa halmashauri hiyo wameshaanza kuweka mikakati kabambe kwa ajili ya kuweza kuleta mabadiliko chanya ya kimaendeleo kwa wananchi wao katika maeneo mbali mbai ikiwemo  sekta ya afya, elimu, miundombinu pamoja na maji  ili kuweza kuwasogezea huduma kwa ukaribu.

Pia Mkurugenzi huyo alisema moja ya jitihada ambazo wamekwisha zifanya ni pamoja na kupeleka nishati ya umeme wa Solar power katika zahanati ya Salale,kupeleka kitanda maalumu kwa ajii ya kujifungulia kinamama wajawazito katika zahanati ya Mchinga ikiwa sambamba na kupeleka Solar Power nyingine katika zahanati ya Mfisini.

Kadhalika alisema nia na madhumuni yao makubwa ni kuhakikisha wanatekeleza maagizo yote yaliyotolewa na Naibu waziri hasa kwa kuwaangalia zaidi wananchi wa maeneo ya vijijini na wale wanaoshi sehemu za Delta katika kuwafikishia huduma mabli mbali wanazostahili.

HIVI karibuni Naibu Waziri ofisi ya Rais Seleman Jafo alifanya ziara yake ya kikazi katika Wilaya mpya ya Kibiti na ambapo aliweza kubaini kuwepo kwa changamoto mbali mbali katika sekta ya afya, elimu, maji, miundombinu, usafiri, hivyo aliagiza uongozi wa halmashauri hiyo kuweza kuzitatua haraka iwezekanavyo  ili kuweza kuwapa fursa wananchi waweze kufanya shughuli za maendeleo bila ya kuwa na vikwazo.




Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI) Seleman Jafo kushoto akiteta jambo na Mbunge wa Jimbo la Kibiti Ally Ungando wakati alipofanya ziara yake ya kikazi kwa ajili ya kukagua miradi mbali mbali ya maendeleo ikiwa sambamba na kubaini changamoto mbali mbali zinazowakabili.
Naibu Waziri ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI) Seleman Jafo kulia akizungumza na Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Kibiti Alvera Ndabagoyo wakati alipofanya ziara yake ya kikazi kwa ajili ya kukagua shughuli za kimaendeleo pamoja na kubaini changamoto zinazowakabili wananchi(PICHA NA VICTOR MASANGU)

kilichokuwa kiota cha maraha kati kati ya jiji la Dar,Bilicanas Club imebaki stori tu kwa sasa

$
0
0
 Pichani kati ni kile kilichokuwa kiota maarufu cha maraha katikati ya jiji la Dar,kilichojulikana kwa jina la  Billicanas Club,tayari kwa asilimia kubwa kimeishabomolewa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC),kama uonavyo pichani,baada ya kunaswa na Camera ya Globu ya Jamii.
Shirika  la Nyumba la Taifa (NHC) linaendelea kwa kasi kubomoa jengo la iliyokuwa Klabu Bilicanas.

SERIKALI YAMALIZANA NA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA.

$
0
0
Na Anthony John Glob jamii.

Baada ya mvutano wa muda mrefu baina ya Serikali na Wenyeviti wa Serikali za mitaa,Serikali imesitisha muongozo wake wa kuzuia kutumia mihuri kwa wenyekiti wa serikali.

Akizungumza leo hii Jijini Dar es salaam na wawakilishi kutoka serikali za mitaa, Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tamisemi, George Simba Chawene amesema amesitisha muongozo uliotolewa juu ya utumiaji wa mihuri kwa Wenyeviti wa serikali za mitaa mpaka mpaka hapo baadae itakapojadiliwa tena.

''Hakukuwa na dhamira yeyote ya kupunguza mamlaka ya heshima yenu Wenyeviti, lakini kama muhuri inaweza kupunguza heshima yenu nimeona kufuta muongozo huu Mpaka pale tutakapo jadili tene upya swala hili" amesema

Sanjari na hayo Waziri Simbachawene amefafanua kuwa kulikuwa na sababu za msingi za kutoa muongozo huo wa kutokutumia mihuri kutokana na matumizi mabaya ya mihuri kwa Wenyeviti wa serikali za mitaa na kupelekea kuigawa ardhi bila utaratibu maalumu.

Hata hivyo Katibu wa Wenyeviti Mkoa wa Dar es salaam Mariam Machicha ameishukuru Serikali kwa kuona tatizo hilo na kuahidi kulifanyioa kazi. 

Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tamisemi, George Simba Chawene akizungumza na wawakilishi kutoka serikali za mitaa leo jijini Dar es Salaam kuhusiana na kusitisha muongozo wa kuzuia kutumia mihuri kwa wenyekiti wa serikali.
Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tamisemi, George Simba Chawene akizungumza akizungumza na waandishi wa habari.
Baadhi ya wawakilishi kutoka serikali za mitaa wakimsikiliza Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tamisemi, George Simba Chawene wakati akisitisha muongozo wa kuzuia kutumia mihuri kwa wenyekiti wa serika.
Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tamisemi, George Simba Chawene akizunguimza akizungumza na waandishi wa habari.
Wawakilishi kutoka serikali za mitaa wakisikiliza jambo kwa Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tamisemi, George Simba Chawene wakati.
Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tamisemi, George Simba chawene akiwa katika picha ya pamoja na Wawakilishi kutoka serikali za mitaa.

CCM YAWAASA WANANCHI KUWAPUUZA WANASIASA WANAOGEUZA MATATIZO YAO KAMA MTAJI WA KISIASA

$
0
0
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii 
 
Chama cha Mapinduzi (CCM) kimesema ni vyema wananchi wakaanza kuwapuuza wanasiasa wa vyama vya upinzani ambao wamekuwa wakigeuza matatizo ya wananchi kama mtaji wa kisiasa. 
 
Hayo yamesemwa na katibu wa Siasa itikadi na uenezi wa CCM, Humphrey Polepole alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo juu ya mambo mbalimbali yanayoendelea hapa nchini. 
 
“CCM haitashiriki malumbano yasiyo kuwa na tija kwa lengo la kuleta uchochezi kwa wananchi kama ilivyo kwa viongozi wa vyama vya upinzani nchini, ambao wamekuwa wakitoa matamko kuwa Taifa limekumbwa na baa la njaa kama sehemu yao ya mtaji wa kisiasa, jambo ambalo Chama cha Mapinduzi kinaona hiyo ni siasa chafu” amesema Polepole. 
 
Amesema kuwa kwanza tuwapuuze na maneno yao, kwani mwenye mamlaka ya kutangaza baa la njaa nchini ni Rais peke yake, hivyo ni vema wakajua kuwa Tanzania hatujafikia kiwango hicho, ambao wao wanakiomba, bali wanatakiwa kujua kuwa mpaka sasa tuna kiasi cha Tani Milioni 1 na nusu ambacho kitasambazwa katika maeneo mbalimbali ambayo yana upungufu wa chakula. 
 
Ameongeza kuwa sera ya CCM ni kujitegemea, hivyo kama ndicho chama ambacho kinaongoza dola,hatujafikia hatua ya kukosa chakula katika nchi yetu. 
 
Pole Pole Ametoa wito kwa viongozi mbalimbali nchini kuacha kubweteka na kuwalaghai na kuwafarakanisha Wananchi,bali wanapaswa kuwaambia ukweli wananchi ili waweze kutunza nafaka na kuacha kutumia kwa matumizi mabaya kama kupikia pombe na masuala mengine yasiyokuwa ya lazima.

POLISI YANG’OA TAA 665 ZA MAGARI ZISIZO SAHIHI

$
0
0
Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO.


Jeshi la Polisi Tanzania limeondoa taa za ziada (spot light) 665 zilizokuwa zimewekwa kwenye baadhi ya magari bila kupata kibali na utaratibu wa mtengenezaji wa chombo husika.

Hatua hiyo inalenga kupunguza ajali za barabarani zinazosababishwa na matumizi ya taa hizo zisizo sahihi.

Takwimu hizo zimetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani, DCP Mohamed Mpinga alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu matumizi ya taa za gari.

DCP Mpinga alisema kuwa marekebisho yoyote katika gari yanahitaji kibali cha mtengenezaji , kinyume cha hapo ni uvunjaji wa sheria.Aliongeza kuwa taa hizo hutumika vibaya hasa nyakati za usiku na kuwa chanzo cha ajali kwa sababu zinapotumika hupoteza uwezo wa mtumiaji kuzitawala kwa maana ya kubadilisha uwakaji wake.

Kamanda Mpinga aliwashukuru baadhi ya watumiaji wa barabara kwa kuunga mkono usimamizi wa sheria kwa kuziondoa taa hizo kwa hiari na kuwasisitiza kuwa zoezi hilo ni endelevu hivyo waendelee kuzitoa taa hizo wenyewe.

Aidha, Kamanda huyo alitaja ajali za barabarani zilizotokana na matumizi mabaya ya taa kwa mwaka 2015 zilikuwa 104 na mwaka 2016 zilikuwa 123.

Wanawake wanaoshiriki katika mradi wa Wanawake Kwenye Usukani (WOW) wapewa mafunzo ya haki za wanawake

$
0
0
1
Martin Gabone-Mkurugenzi Mkuu Mradi wa Wanawake Kwenye Usukani (WOW) akifungua semina ya mafunzo ya haki za wanawake wanaoshiriki katika mradi huo iliyofanyika mwishoni mkwa wiki Kinondoni jijini Dar es salaam.
23
Martin Gabone-Mkurugenzi Mkuu Mradi wa Wanawake Kwenye Usukani (WOW) akimtambulisha WIGAYI KISSANDU-Mwanasheria Kituo cha Msaada wa Sheria kwa Wanawake (WLAC) mkufunzi wa mafunzo hayo yaliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam.
4
WIGAYI KISSANDU-Mwanasheria Kituo cha Msaada wa Sheria kwa Wanawake (WLAC) akitoa mafunzo katika semina hiyo.
56
WIGAYI KISSANDU-Mwanasheria Kituo cha Msaada wa Sheria kwa Wanawake (WLAC) akifafanua jambo wakati alipokuwa akitoa mafunzo katika semina hiyo.
7
Baadhi ya washiriki wakiwa katika semina hiyo.
89
Martin Gabone-Mkurugenzi Mkuu Mradi wa Wanawake Kwenye Usukani (WOW) na Victor Francis-Meneja Mafunzo wa Mradi wa Wanawake Kwenye Usukani (WOW) wakiwa katika semina hiyo.
................................................................................
Wanawake wanaoshiriki katika mradi wa Wanawake Kwenye Usukani (WOW) unaoendeshwa na Kampuni ya AFREXA International Ltd, wametakiwa kufahamu haki mbalimbali za binadamu zinamwongoza mwanadamu kushiriki vyema katika shughuli za kimaendeleo.

Akizungumza Jijini DSM, wakati wa semina ya siku moja ya wanawake kuelekea katika mafunzo ya kuendesha vyombo vya moto vya biashara, mwanasheria kutoka Kituo cha Msaada wa Sheria kwa Wanawake (WLAC) WIGAYI KISSANDU amesema ni muhimu kwa wanawake kufahamu haki hizo kwa kuwa zinatoa mwongozo kufikia malengo.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu Mradi wa Wanawake Kwenye Usukani (WOW) MARTIN GABONE amesema semina hiyo ni moja ya hatua za mwanzo za mafunzo ya udereva kwa wanawake kwa ajili ya kuendesha vyombo vya moto vya biashara na kusisitiza wanawa wajibu wa kuhakikisha wanawake hao wanaingia rasmi katika sekta ya usafirishaji kwa kuajiriwa au kujiajiri.

Mradi wa Wanawake Kwenye Usukani (WOW) hadi sasa umesajili zaidi ya wanawake 200 kutoka maeneo mbalimbali nchini, ili waweze kuwapatia bure mafunzo ya udereva wa vyombo vya moto vya biashara ambapo baada ya mafunzo hayo watatafutiwa ajira na wengine watawezeshwa ili waweze kujiajiri.

NAIBU WAZIRI ANGELLINA MABULA " IUNDWE KAMATI YA UCHUNGUZI JUU YA UPIMAJI WA VIWANJA KATIKA HALMASHURI MPYA YA PERAMIHO"

$
0
0

Naibu Waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi, DOKTA. ANGELLINA MABULA , ameagiza kuundwa kwa kamati ya uchunguzi wa viwanja vinavyopimwa katika halmashauri mpya ya peramiho, iliyopo wilaya ya songea mkoani mkoani Ruvuma, baada ya kuonekana kuwepo na ujanjaujanja katika upimaji huo ikiwemo kufanya uchunguzi wa utunzaji wa kumbukumbu ya ardhi katika halmashauri hiyo.

MAKAMU WA RAIS MAMA SAMIA MGENI RASMI MAADHIMISHO YA MWAKA MPYA WA KICHINA.

$
0
0
NA Daudi Manongi – MAELEZO.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Hassan Suluhu anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya mwaka mpya wa kichina yatakayofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja tarehe 21 na 22 January 2017 kuanzia saa tatu asubuhi mpaka saa 11 Jioni.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Mkuu wa Kituo cha Utamaduni wa China nchini Bw.Gao Wei alipokuwa akizungumza na waandishi wa Habari.

Amesema mwaka huu utafahamika kama mwaka wa Jogoo wenye kuweka mtazamo mkubwa Afrika huku yakiambatana na burudani nyingi kutoka kwa vikundi mbalimbali vya sanaa kutoka China na nchini,maonyesho ya picha,vyakula vya kichina na maonyesho mbalimbali ya kibiashara.

Katika maadhimisho hayo makampuni 60 yatashiriki katika kuonyesha bidhaa mbalimbali,pia nchi 150 na majiji 400 yatasherehekea maadhimisho haya ya mwaka mpya.

Akizungumzia mahudhurio ya siku hiyo Bw.Wei amesema kuwa wanategemea ushiriki wa watu zaidi ya 6000 katika maadhimisho hayo ya siku mbili ambayo yanasisitiza zaidi urafiki na mshikamano.

Katika kufanikisha maadhimisho hayo Kampuni za HUAWEI na CRDB Benki zimejitokeza kudhamini maadhimisho ya mwaka huu.
Mkuu wa Kituo cha Utamaduni wa China nchini Tanzania Gao Wei akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam kuhusu maadhimisho ya mwaka mpya wa Kichina unaotarajiwa kuadhimishwa tarehe 21 na 22 mwezi huu katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. Maadhimisho hayo yataambatana na maonyesho ya utamaduni wa Kichina. Kushoto ni Meneja Uhusiano wa Kampuni ya HUAWEI Jimmy Liguo Jin na kulia ni Ofisa wa Ubalozi wa China, LIU Yun.
Meneja Uhusiano wa Kampuni ya HUAWEI Jimmy Liguo Jin akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa mkutano wao na waandishi hao kuhusu maadhimisho ya mwaka mpya wa Kichina unaotarajiwa kuadhimishwa tarehe 21 na 22 mwezi huu katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.Picha na: Frank Shija – MAELEZO.

KATIBU MKUU WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI ATEMBELEA MRADI WA UJENZI NYUMBA ZA ASKARI MAGEREZA, UKONGA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (aliyevaa Kaunda suti), akiteta jambo na Kaimu Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, Dk. Juma Malewa wakati alipotembelea kukagua maendeleo ya Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za Makazi ya Askari wa Jeshi la Magereza, ambao unakadiriwa kuhifadhi watumishi zaidi ya 300 ukikamilika katika eneo la Ukonga, jijini Dar es Salaam. (Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi).

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (kushoto), akisalimiana na Mshauri wa Kitengo cha Utafiti wa Udongo kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (BICO,UDSM), Dk. Dalmas Nyaoro, baada ya kuwasili eneo la Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za Makazi ya Askari Magereza ambao unakadiriwa kuhifadhi watumishi zaidi ya 300 ukikamilika katika eneo la Ukonga, jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira, akisaini dafrari la wageni baada ya kuwasili kwenye Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za Makazi ya Askari Magereza unaoendelea katika eneo la Ukonga, jijini Dar es Salaam. Mradi huo unakadiriwa kuhifadhi watumishi zaidi ya 300 ukikamilika.
Mratibu wa Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za Makazi ya Askari wa Jeshi la Magereza kutoka Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Julius Chego (kulia), akimpa maelekezo Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira alipotembelea kukagua maendeleo ya mradi huo katika eneo la Ukonga, jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Kaimu Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, Dk. Juma Malewa. Mradi huo unakadiriwa kuhifadhi watumishi zaidi ya 300 ukikamilika.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (katikati), akimpa maelekezo Mratibu wa Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za Makazi ya Askari wa Jeshi la Magereza, Julius Chego (kulia) wakati alipotembelea kukagua maendeleo ya mradi huo ambao unakadiriwa kuhifadhi watumishi zaidi ya 300 ukikamilika katika eneo la Ukonga, jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Kaimu Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, Dk. Juma Malewa.
Kaimu Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, Dk. Juma Malewa, akifafanua jambo kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (katikati), wakati Katibu Mkuu alipotembelea kukagua maendeleo ya Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za Makazi ya Askari wa Jeshi la Magereza, ambao unakadiriwa kuhifadhi watumishi zaidi ya 300 ukikamilika katika eneo la Ukonga jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mratibu Mkuu wa mradi huo kutoka Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Julius Chego.
IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI

WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA UJUMBE KUTOKA KINGDOM LEADERSHIP NETWORKS

$
0
0

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mwenyekiti wa Taasisi ya Kingdom Leadership Network Tanzania Ibrahimu Kaduma aliyemtembelea Makamu wa Rais na kumuelezea mikakati ya kuanzisha Chuo cha Joseph Business School.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (kulia) akizungumza na Mwenyekiti wa Taasisi ya Kingdom Leadership Network Tanzania Ibrahimu Kaduma aliyemtembelea Makamu wa Rais na kumuelezea mikakati ya kuanzisha Chuo cha Joseph Business School kushoto ni Meneja Mradi Dkt Charles Sokile.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na ujumbe wa Taasisi ya Kingdom Leadership Network Tanzania uliomtembelea ofisini kwake, Ikulu jijini Dar es Salaam.


..............................................................

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameuhimiza uongozi wa Taasisi ya Kingdom Leadership Network Tanzania kuharakisha mchakato wa kuanzisha Chuo cha Joseph Business School hapa nchini chuo ambacho kitatoa mafunzo mbalimbali ya biashara, maadili ya uongozi na ugunduzi wa mawazo ya biashara ili kusaidia mamia ya Watanzania kuimarisha shughuli zao za kiuchumi.

Makamu wa Rais ametoa kauli ofisini kwake Ikulu Jijini Dar es Salaam leo alipokutana na kufanya mazungumzo na Viongozi wa Taasisi ya Kingdom Leadership Network Tanzania ambao walimtembelea Makamu wa Rais kumweleza hatua ambazo wamefikia katika uanzishaji wa Chuo hicho.

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amesema wazo la uanzishaji wa Chuo hicho ulitolewa na Dkt Bill Winston ambaye ni Mwanzilishi wa Winston Ministries mwaka jana katika Maombezi ya Taifa ambaye yeye alikuwa mgeni rasmi katika maombi hayo, anasema aliupokea kwa furaha mpango huo kwa sababu chuo hicho kitasaidia watanzania wengi kupata elimu na ujuzi wa kuimarisha biashara zao wakati taifa likielekea kwenye uchumi wa Viwanda.

Amesema hatua za uanzishwaji wa Chuo hicho hapa nchini ni fursa pekee na nzuri kwa Watanzania kujifunza ubunifu na ugunduzi katika biashara, maadili ya uongozi katika biashara ili kuongeza ufanisi katika biashara zao kwa ajili ya manufaa yao na taifa kwa ujumla hasa katika ulipaji wa kodi.

Kwa Upande wake, Mwenyekiti wa Taasisi ya Kingdom Leadership Network Tanzania Ibrahimu Kaduma na Meneja Mradi Dkt Charles Sokile wamemhakikishia Makamu wa Rais kuwa hatua ambazo wamefikia kwa sasa katika uanzishaji wa Chuo hicho ni nzuri ambapo mpaka sasa wamepata majengo kwa ajili ya ofisi na maeneo ya kufundishia na hatua za usajili wa chuo hicho zipo katika hatua za mwisho.

Wamesisitiza kuwa wanataka kushirikiana ipasavyo na Serikali katika uanzishaji wa chuo hicho ambacho kitatoa elimu ya biashara hasa ugunduzi wa mawazo ya biashara nchini kama hatua ya kutekeleza kwa vitendo dhana ya kuelekea kwenye uchumi wa viwanda nchini.

Kliniki ya Airtel Rising Stars yaanza Dar, Vijana waanza kujifua

$
0
0
Mkurugenzi wa Ufundi wa Soka la vijana TFF, Kim Paulsen akitoa maelekezo kwa wachezaji wa timu ya vijana U-17 wakati wa ufunguzi wa kliniki ya Airtel Rising Stars katika uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam jana.

Kliniki ya Soka ya Airtel Rising Stars imeanza leo kwenye Uwanja wa Karume kwa kuwakutanisha wavulana 40 na huku ya wasichana ikifanyika kwenye uwanja wa JK Park zamani kidongo chekundu.

Akizungumza wakati wa kliniki hiyo, Kocha Mkuu wa Timu ya Serengeti Boys, Bakari Shime alisema, ‘kwanza tutakuwa tukiangalia ufundi binafsi wa mchezaji’. Hii ni mara ya kwanza kukutana na wachezaji hawa na kuangalia vitu binfasi ambavyo mchezaji anatakiwa kuwa navyo hii itatusaidia kujua ni sehemu ipi ya kutilia mkazo.

 Juhudi binafsi za Mchezaji, Ufundi na stamina (ukakamavu) ni vitu muhimu kwa mchezaji kuwa navyo katika kiliniki hii, hiyo ndio sababu leo kwa siku ya kwanza wachezaji tumewapa nafasi ya kuchezea mpira ili kuangalia vitu hivyo,’ alisema Shime.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Kampuni ya Airtel Tanzania, Beatrice Singano akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ufunguzi wa kliniki ya Airtel Rising Stars kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam jana.

Lakini pia tutapata nafasi ya kuingalia timu yetu ye Serengeti Boys kama ina mapungufu yoyote na kama kutakuwa na wachezaji wenye umri mkubwa basi hauwaruhusiwa  kuendelea kuchezea timu ya vijana.

 Hapa ndipo tutapa fursa ya wachezaji wa kuweza kuziba nafasi zilizoachwa wazi katika timu hiyo,  Kwa wiki hii yote tutakuwa na kazi ya kushirikiana na Makocha wengine  kuikamilisha zoezi hili, aliongeza Shime.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Maendeleo ya Soka la vijana TF,  Ayoub Nyenzi alisema, ‘klikini ya Airtel Rising Stars inatoa fursa pana kwa vijana chipukizi kuonyesha uwezo wao mbele ya makocha wenye uzoefu wa mpira wa miguu nchini’. 
Katibu Mkuu TFF, Selestine Mwesigwa akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ufunguzi wa kliniki ya Airtel Rising Stars kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam jana.
Hii ni nafasi adhimu kwa  vijana wetu kuendelea kuonyesha uwezo wao na kuzidi kuendeleza vipaji vyao. Sio lazima wachezaji wote hawa hawawezi kuchanguliwa kuchezea timu ya vijana ya Serengeti Boys, lakini kuna klabu zetu ambazo zinaitahitaji wachezaji kwenye timu zao za vijana. Hii ndio nafasi kwao kujitokeza na kuangalia wachezaji wenye uwezo wa kuchezea timu zao,  Ayoub aliyasema hayo jana.

Naye Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania, Beatrice Singano Mallya alisema, ‘kufanyika kwa kliniki ya Airtel Rising Stars kunahitimisha awamu ya sita ya michuano ya Airtel Rising Stars’  ambayo ilifanyika kwa Mikoa tisa nchini kwa mafanikio makubwa sana. 
‘Nachukua fursa hii kuwashukuru TFF pamoja na wadau wote wa mpira wa miguu nchini ambao tumeshirikiana kwenye 2016 Airtel Rising Stars. Michuano hii lifanyika kwa mafanikio makubwa sana na leo tunapaonza kliniki hii inayojumuisha wachezaji bora naomba tuendelea tushirikiana kwa pamoja ili vijana wetu waweze kutimiza ndoto zao za kuwa wachezaji bora katika maisha yao’ alisema Mallya

Things to note after resuming work from the holidays

$
0
0
By Jumia Travel Tanzania

If you are a regular user of the roads in the City Dar es Salaam, then you must have noticed that they have started to form queues comparing to the past few weeks of the festive season. The main reason is because most people are back from the holidays to proceed with their daily office routines following the end of festivities.

Honestly, many people find the month of January very difficult to work with the same pace as before following the holidays. Most of them are lamenting of the fatigue, boredom, and that not-to-work-feeling due to too much time spent away from the office. The following are the few things to note that Jumia Travel (www.travel.jumia.com) thinks would be helpful to you in combating that situation.

Set the alarm to wake you up early

It’s obvious that nobody bothers to set the alarm during the holidays because there are no reasons to. But if you did so, now it is the time to reset it again otherwise you will be late for work during the first few days.

Start by tackling the unfinished tasks

Not all people do finish their tasks before leaving for holidays, you can’t finish them all by the way. Therefore, the first thing when you get back to the office is to make sure you complete all the unfinished tasks so as to get back on track with your colleagues.

Ask your colleagues what went down when you were not around

It does not mean that things are not proceeding when you are not around. It's better to be proactive by asking your co-workers the projects on board, and what your responsibilities are.

Do exercise

Exercises are good for your mental and body health because they will help you to recover to your normal condition. You can either do exercises in the morning or evening after work on your way back home. Also, you can decide to join the nearby gym or jogging alongside the road, that depends on your own preferences.

Evaluate yourself

The moment when you get back to the office after the holidays, is the perfect time to do a self evaluation to contemplate on what you have achieved over the past year. This will help you to understand what you attained and what went wrong so as to formulate effective strategies towards this new year.

Seek for advice

Sometimes it is not possible to overcome the transitions our minds and bodies go through. Hence, we are advised to seek for advice from people who have been in the same condition and who understand what we are going through. Moreover, seeking professional help from therapists is widely advised more oftenly.

There are a lot of several techniques to help someone from escaping that feeling of not to work or boredom in the early few days after the holidays. Jumia Travel (www.travel.jumia.com) hopes these tips will help you recover your momentum.

WAZIRI MKUU AONGOZA KUZINDUA DUKA LA BOHARI YA DAWA (MSD), MPANDA, MKOANI KATAVI

$
0
0


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (katikati), akikata utepe kuashiria uzinduzi wa  duka la Dawa la Bohari ya Dawa (MSD), Mpanda mkoani Katavi. Kutoka shoto mwenye shati la kijani ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa  Katavi, Peter Mselemu, Mkurugenzi wa MSD, Laurean Bwanakunu, Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Kanali mstaafu Raphael Muhuga. Wa tatu kulia ni Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo.

Jiwe la Msingi.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkurugenzi wa MSD, Laurean Bwanakunu wakifurahi wakiwa ndani ya duka hilo.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkurugenzi wa MSD, Laurean Bwanakunu na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo wakiwa meza kuu wakati wa uzinduzi wa duka hilo.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa MSD.
Mwonekano wa duka hilo la MSD, mkoani Katavi.


WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema utaratibu wa MSD wa kununua dawa moja kwa moja kutoka kwa wazalishaji litaboresha upatikanaji wa dawa na kupunguza gharama za kununua dawa kutoka nje ya nchi.

Amesema hayo wakati wa uzinduzi wa duka la dawa la MSD,  Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda, mkoani Katavi, ambalo linaifanya MSD kuwa na jumla ya maduka 7 ya dawa nchini.

Waziri Mkuu pia amesema kwa mwaka huu wa fedha shilingi Bilioni 251 zimetengwa kwa ajili ya ununuzi wa dawa na vifaa tiba ili kupunguza changamoto za uhaba wa dawa na kueleza kuwa shabaha ya serikali ni kufikia asilimia 95-100 ya upatikanaji wa dawa hadi itakapofika mwezi Juni, 2017.

Kwa upande wake,Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Bwana Laurean Bwanakunu ameeleza kuwa duka hilo wataliendesha kwa mwaka mmoja tu,na kisha kulikabidhi kwa Halmashauri ili iliendeshe na kuongeza mapatao yao.

Kwa upande wa upatikanaji wa dawa, Bwanakunu amesema kuwa kwa sasa fedha sio tatizo,na dawa zinaendelea kuagizwa kulingana na mahitaji.
Viewing all 46379 articles
Browse latest View live




Latest Images