Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46362 articles
Browse latest View live

RAIS DKT. MAGUFULI AMTEUA JAJI PROF. IBRAHIM JUMA KUWA KAIMU JAJI MKUU WA TANZANIA


WAKULIMA wa wilaya ya Kilolo na Mufindi mkoani Iringa kuanza kunufaika na kilimo cha zao la pareto

$
0
0

Wananchi wa kijiji cha Madege kata ya Idete wakiwa katika mkutano wa uhamasishaji wa kilimo cha zao la Pareto

Wananchi wa Madege wakisikiliza elimu ya kilimo cha zao la Pareto .


Wananchi wakitawanyika katika mkutano wa uhamasishaji wa kilimo cha pareto uliofanyika ofisi ya kijiji Madege Kilolo

Vitalu vya miche ya Pareto kwa ajili ya kupewa bure wananchi


mwakilishi wa kiwanda cha Pareto Mafinga Bw Godfrey Mbeyela akiwaeleza wananchi wa Bomalang'ombe Kilolo faida ya kilimo cha zao la Pareto

Mwamasishaji wa zao la Pareto nchini Gerald Chuwa akiwapa maelezo wananchi wa Madege kata ya Idete juu ya faida ya kilimo cha Pareto

Wananchi wa Bomalang'ombe wakimsikiliza diwani wa viti maalum



Na MatukiodaimaBlog

WAKULIMA wa wilaya ya Kilolo na Mufindi mkoani Iringa kuanza kunufaika na kilimo cha zao la pareto baada ya kiwanda cha Pyrethrum company Tanzania Ltd (PCT) Mafinga kuanza kugawa bure ya zao la Pareto .
Akizungumza katika mkutano wa uhamasishaji wa kilimo cha zao La Pareto mwakilishi wa kiwanda cha PCT Bw. Godfrey Mbeyela jana wakati wa mkutano wa hadhara na wananchi wa kata ya Bomalang'ombe na Idete , alisema kuwa kampuni hiyo imeamua kutoa miche bure ili kuwaondolea usumbufu wananchi wa kupata mbegu.

Alisema pamoja na kugawa bure kwa wananchi waliotayari kulima zao hilo la biashara pia kwa wale watakaojiunga vikundi watapewa ajira ya kuotesha miche ya Pareto na kuiuza kwa kampuni ili kuigawa bure kwa wakulima zoezi ambalo litakuwa kwa mwakani

"Kwa mwaka huu miche ipo ya kutosha ya kuwawezesha wananchi zaidi ya 40,000 kulima Pareto ila kwa kuwa idadi ya wakulima inaweza ongezeka zaidi mwakani vikundi vitapewa kazi ya kuotesha miche na kuuza kwa kampuni….. kampuni haitaki mkulima wa zao la Pareto kununua miche"

Juu ya soko la zao hilo ambalo miaka ya nyuma Wilaya ya Kilolo ilikuwa akiongoza kwa uzalishaji alisema kwa sasa soko ni uhakika kwani kampuni imekuja kwa kasi ya kuwakomboa wakulima na sasa fedha za mazao zitatolewa papo kwa papo shambani baada ya mavuno na hakuna mpango wa kumkopa mkulima .

Pia alisema bei ya zao hilo kwa kilo kwa wananchi wa Kilolo kwa ajili ya kuhamasisha kilo itanunuliwa kati ya Tsh 20000 hadi Tsh 30000.
Mkuu wa wilaya ya Kilolo Asia Abdalah aliwataka wananchi kujiunga na kilimo hicho kwani ni moja kati ya mazao ambayo hayahitaji gharama kubwa ya kuhudumia zaidi ya palizi pekee.

Hivyo alishauri kila mwananchi kulima japo hekari moja ya Pareto japo mazao mengine waliyozoea yakiwemo mahindi kwa ajili ya Chakula kulima hekari nyingi zaidi. Mkuu huyo wa wilaya ya Kilolo alisema kilimo hicho cha Pareto ni fursa kubwa kwa wananchi ambao watachangamkia kuanza kilimo hicho.

Awali wananchi walisema kuwa waliacha kilimo hicho na mashamba ya Pareto kufyeka na kupanda viazi baada ya kuyumba kwa soko la Pareto ila kwa sasa kwa utaratibu huu mpya wapo tayari kuchangamkia kilimo hicho.

Tanzania kuanza kutumia mfumo wa Dirisha Moja la Huduma (Electronic Single Window System)

$
0
0
 
Kaimu Kamishna Mkuu TRA, Mary Maganga.

Katika kuhakikisha inaboresha huduma kwa wafanyabiashara ambao wanaingiza mizigo nchini kwa njia ya bandari, mipaka na viwanja vya ndege, Serikali kupitia Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) imeeleza mpango wa Serikali wa kuanza kutumia mfumo wa Dirisha Moja la Huduma (Electronic Single Window System) ambao kwa hakika utamaliza tatizo la mizigo kukaa muda mrefu kwa sababu ya kukosekana vibali. 
 
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumalizika mafunzo ya siku moja kuhusu mfumo wa Dirisha Moja la Huduma kwa taasisi zinazotoa vibali na wafanyabiashara, Meneja Mfumo wa Kieletroniki wa Dirisha Moja la Huduma, Tinka Felix alisema lengo la kuanza kutumia mfumo huo ni kuboresha huduma ambazo wanazitumia sasa ili wafanyabiashara wanaoingiza mizigo nchini waweze kuipata kwa haraka kuliko ilivyo sasa.

Meneja Mfumo wa Kieletroniki wa Dirisha Moja la Huduma, Tinka Felix akizungumza kuhusu mfumo wa Dirisha Moja la Huduma (Electronic Single Window System). (Picha zote na Rabi Hume - MO DEWJI BLOG)

“Ni mpango wa Serikali kuboresha huduma kwa wateja kwa kupunguza muda wa kutoa mizigo bandarini au mipakani au kwenye viwanja vya ndege, kupitia mfumo huu wateja hawatakuwa wakienda kwenye idara na taasisi za Serikali na badala yake wakiwa hukohuko kwenye ofisi zao wataweza kuomba na kupata vibali na kupata bili za malizo kwenda kulipa benki, mfumo pia utafanya kazi na benki," alisema Felix. 
 
Alisema Tanzania haitakuwa nchi ya kwanza kutumia mfumo huo na mataifa mengi yanautumia ili kurahisisha huduma kutolewa kwa haraka kwani mfumo wa sasa wa forodha (tancis system) unashindwa kufanya kazi kwa haraka jambo ambalo linasababisha mizigo kuchelewa kutolewa kutokana na muda mrefu mmiliki kutumia kutafuta vibali. Mkurugenzi wa Sera Utafiti Na Ushauri wa TPSF, Gili Teri akizungumza faida za kutumia mfumo wa Dirisha Moja la Huduma (Electronic Single Window System).

“Mfumo wa sasa ili mtu apate kibali anatakiwa atembelee hizo ofisi hata mara 10 na baadhi ya ofisi wanataka vibali zaidi ya kimoja lakini mfumo huu wa sasa muda ambao unatumika kuomba vibali utapungua na tunategemea kuokoa Dola milioni 65 kwa kutumia tu mfumo wa electronic single window system,” alisema Felix. 
 
Alisema kwa sasa kuna taasisi za Serikali 47 ambazo zinatoa vibali lakini mfumo wa Dirisha Moja la Huduma utatumiwa na taasisi 32 ambazo kwa pamoja zitakuwa zikitoa vibali 106. Aidha alisema Serikali imeagiza kuwa mfumo huo uanze kutumika baada ya mwaka mmoja hivyo wanategemea kuanzia mwakani mfumo ambao watakuwa wakitumia utakuwa ni wa Dirisha Moja la Huduma (Electronic Single Window System) ambao utawezesha wafanyabiashara ambao wanatoa mizigo kupitia bandari, mipaka au viwanja vya ndege kupata vibali kwa haraka. Na Rabi Hume, MO DEWJI BLOG Baadhi ya washiriki wa semina hiyo ya siku moja wakiuliza maswali na kutoa maoni kuhusu mfumo wa Dirisha Moja la Huduma (Electronic Single Window System).

MTWARA ICHUNGUZWE SABABU ZA KUFELI KIDATO CHA PILI-MAJALIWA

$
0
0
 WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameuagiza uongozi Wazara wa Elimu Sayansi na Telnolojia pamoja na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kwenda mkoani Mtwara kufanya uchunguzi ili kubaini sababu zilizosababisha shule tisa za mwisho katika matokeo ya kidato cha pili kutoka mkoani humo.
Pia ameziagiza halmashauri nchini kushirikiana na Idara ya Ukaguzi ili kuhakikisha wanawasimamia vizuri walimu jambo litakalowezesha kuboresha ufundishaji na hatimaye kupata matokeo mazuri.
Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Jumanne, Januari 17, 2017) wakati akizungumza na watumishi na wananchi wa mkoa wa Katavi alipowasili Ikulu ndogo ya Mpanda kwa ajili ya kufungua duka la dawa la Bohari Kuu ya Dawa (MSD) katika hospitali ya Manispaa ya Mpanda.
Kwa mujibu wa matokeo hayo kati ya shule 10 za sekondari zilizofanya vibaya kwenye mtihani huo, tisa zinatoka katika Mkoa wa Mtwara na moja Tanga. Shule za Mtwara zilizofanya vibaya ni Chingungwe, Malocho, Naputa, Chanikanguo, Mtiniko, Michiga, Msimbati, Salama na Lukodoka  huku ya Tanga ikiwa ni Nywelo.
“Viongozi wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia pamoja na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) waende Mtwara wakafuatilie kwa kina wajue kuna nini hadi shule tisa kati ya 10 zilizofanya vibaya katika matokeo ya mitihani ya kidato cha pili mwaka jana zitoke huko,” amesisitiza.
Mbali na kuuagiza huongozi wa wizara hizo kwenda mkoani Mtwara pia Waziri Mkuu amewataka wasimamie vizuri mikoa ambayo awali ilikuwa na matokeo mabaya na sasa inafanya vizuri na wahakikishe shule za mikoa hiyo hazishuki na badala yake ziendelee kupata matokeo mazuri zaidi.
Awali, akisoma taarifa ya mkoa huo, Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Meja Jenerali Mstaafu, Raphael Muhuga alisema katika matokeo ya mtihani kidato cha pili ya mwaka jana mkoa wake ulishika nafasi ya pili kitaifa ukiongozwa na mkoa wa Geita.
Alisema kwa sasa wanajipanga kuhakikisha katika mitihani ya mwaka huu wanashika nafasi ya kwanza kitaifa, hivyo alitoa wito kwa watendaji wa Idara ya Elimu, wakuu wa shule, wazazi na walezi kushirikiana kwa pamoja kuhakikisha malengo hayo yanafanikiwa.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMANNE, JANUARI 17, 2017.

RAIS DKT MAGUFULI KUMUAPISHA KAIMU JAJI MKUU WA TANZANIA IKULU JIJINI DAR LEO

CHEYO ASEMA SERIKALI NDIYO YENYE MAMLAKA YA KUTANGAZA NJAA

$
0
0
Na: Lilian lundo - MAELEZO

Serikali ndiyo yenye mamlaka ya kutangaza ikiwa nchi inakabiliwa na janga la njaa na wala si taasisi, asasi za kiraia au wanasiasa.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Chama cha UDP John Cheyo wakati wa mahojiano na mwandishi wa habari hii alipokuwa akitoa maoni yake kuhusu mijadala mbalimbali inayoendelea katika vyombo mbalimbali vya habari kwamba Tanzania imekabiliwa na tatizo la njaa.

Cheyo alisema kuwa, huwezi kusema nchi ina njaa wakati vyakula vipo katika masoko mbalimbali hapa nchini. Amewataka watanzania kutofautisha kupanda kwa bei za vyakula na janga la njaa.

Aidha, Cheyo alisema kuwa tatizo hilo tayari limetatuliwa na Serikali kwa kutoa tani milioni 1.5 za mahindi  ambazo zitasambazwa nchi nzima kwa ajili ya wananchi kununua.

Aliendelea kwa kusema kuwa kuna umuhimu mkubwa wa mahindi hayo kuuzwa kwa uangalifu kwani gharama yake itakuwa ni ya chini, hivyo kuna watu ambao watajitokeza kununua kiasi kikubwa na kwenda kukihifadhi kwa ajili ya kukiuza kwa gharama ya juu baadae.

Vile vile aliwataka watanzania kuwa na tabia ya kutunza vyakula badala ya kuuza vyakula vyote mara wanapovuna, ili vyakula hivyo viweze kuwasaidia pale ambapo mvua zinakuwa zimechelewa kama ambavyo imekuwa kwa mwaka huu.

MADIWANI WA MANISPAA YA MOSHI WATEMBELEA OFISI ZA MAMLAKA YA MAJI SAFI NA USAFI WA MAZINGIRA MJINI MOSHI (MUWSA)

$
0
0
Chanzo cha Maji cha Shiri kilichopo wilaya ya Hai.
Madiwani wakiwa katika chanzo cha maji cha Shiri walipofanya ziara kutembelea vyanzo hicho na kupata maelezo.
Madiwani wakipata maelezo kutoka kwa Meneja Ufundi wa Mamlaka hiyo ,Patrick Kibasa namna maji yanavyotibiwa.
Madiwani wakiwa katika chanzo kipya  cha maji cha Mkashiringi .
Meneja Ufundi wa MUWSA,Patrick Kibasa akitoa maelezo kwa madiwani mara baada ya kutembelea chanzo cha maji cha Njoro ya Goha.
Madiwani wakiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira mjini Moshi (MUWSA) mara baada ya kuhitimisha ziara ya kutembea ofisi hizo pamoja na vyanzo vya maji.

Mkurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) Joyce Msiru akizungumza wakati wa ukaribisho wa Madiwani wa Halmashauri ya manispaa ya Moshi walipotembelea ofisi za mamlaka hiyo.
Baadhi ya Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi wakifuatilia maelezo ya awali ya Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na  Usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) alipokuwa akitoa neno la ukaribisho.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Moshi,Raymond  Mboya akizungumza wakati wa utamburisho wa Madiwani waliotembelea ofisi za MUWSA.
Baadhi ya Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi,Michael Mwandezi aliyeongozana na Madiwani wa Halmashauri hiyo akizungumza wakati wa  ziara ya madiwani katika ofisi za MUWSA.
Baadhi ya Madiwani wakiwa katika kikao cha kupokea taarifa za Mamlaka hiyo.
Mkuu wa kitengo cha Mipango na Huduma za Biashara Mamlaka ya maji safi na usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) Tumaini Marandu akitoa taarifa ya Mamlaka hiyo kwa Madiwani waliofanya ziara katika ofsi za MUWSA.
Diwani wa kata ya Miembeni ,Mbonea Mshana akichangia jambo katika taarifa ya Mamlaka hiyo.
Diwani wa kata ya Kilimanjaro,Priscus Tarimo akichangia jambo mara baada ya kusikiliza taarifa ya Mamlaka hiyo katika utoaji wa huduma ya maji safi na maji taka kwa wakazi wa manispaa ya Moshi.
Diwani wa kata ya Mabogini,Emanuel Mzava akichangia jambo katika kikao hicho.
Diwani wa kata ya Njoro ,Jomba Khoi akichangia jambo katika kikao hicho.
Diwani wa viti maalumu ,Mama Kowelo  akichangia katika kikao hicho.
Mkurugenzi ,Joyce Msiru akitoa ufafanuzi juu ya hoja mbalimbali zilizoibuliwa na madiwani katika kikao hicho.
Meneja Ufundi wa MUWSA ,Patrick Kibasa akitoa ufafanuz juu ya hoja zilizohusu masuala ya ufundi .
Kaimu Meneja Fedha wa MUWSA ,Rehema Minja akiteleza jambo katika kikao hicho.
Kaimu Meneja rasilimali watu wa MUWSA,Laurian Kessy akichangia jambo katika kikao hicho.
Mkaguzi wa ndani wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi,(MUWSA) Benson Maro akizungumza katika kikao hicho.
Baadhi ya Madiwani wakifuatilia maelezo wakati a mjadla katika kikao hicho.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi,(MUWSA) Joyce Msiru akiteta jambo na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi,Michael Mwandezi.(kushoto).
Madiwani wakitembelea chanzo cha maji cha Shiri.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini. 

TACAIDS YAJIPANGA KUHAKIKISHA MAAMBUKIZI MAPYA YA UKIMWI KUBAKI HISTORIA IFIKAPO 2030

$
0
0
 Mkurugenzi wa Uraghabishi na Habari – TACAIDS Jumanne Issango akizungumza na waandishi wa habari kuhusu masuala ya UKIMWI kwa vijana leo jijini Dar es Salaam.Kutoka kushoto ni Mratibu wa Shughuli za Vijana TACAIDS Bibi. Grace Kessy, Mratibu Mwandamizi wa Shirika la Restless Development Bw. Oscar Kimaro na Mratibu wa Shughuli za Rufaa kwa Watoto na Walezi waishio katika mazingira magumu Dar es Salaam, Dkt. Fredy Frank.
 Mratibu Mwandamizi wa Shirika la Restless Development Bw. Oscar Kimaro akifafanua jambo wakati wa mkutano wao na waandishi wa habari kuhusu masuala ya UKIMWI kwa vijana leo jijini Dar es Salaam.Kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Uraghabishi na Habari – TACAIDS Jumanne Issango na Mratibu wa Shughuli za Rufaa kwa Watoto na Walezi waishio katika mazingira magumu Dar es Salaam kutoka Shirika la PACT, Dkt. Fredy Frank (katikatika).
  Mratibu wa Shughuli za Rufaa kwa Watoto na Walezi waishio katika mazingira magumu Dar es Salaam, Dkt. Fredy Frank akifafanua jambo wakati wa mkutano wao na waandishi wa habari kuhusu masuala ya UKIMWI kwa vijana leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia mkutano baina yao na wawakirishi kutoka Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS), Restless Development na Shirika la PACT uliofanyika leo jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO).

Picha zote na: Frank Shija – MAELEZO.


NAIBU WAZIRI WA ARDHI ATUMBUA WATUMISHI WATATU RUVUMA

$
0
0

Naibu Waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi, Dokta. ANGELLINA MABULA, amewatumbua Maafisa ardhi Watatu wa halmashauri za wilaya mkoani Ruvuma , afisa ardhi wa Halmashauri ya SONGEA ATHUMANI CHIPAKAPAKA, Mkuu wa Idara ya ardhi wilaya ya Tunduru JAPHET MNYAGALA pamoja na Afisa Ardhi mteule wa wilaya ya Tunduru EVALIST MAPUNDA kwa makosa mbalimbali,

Kongwa wapigwa marufuku kutengeneza pombe kwa kutumia nafaka

$
0
0
CHAMA Cha Wanyakazi wastaafu wilaya ya Singida kimesema kuwa idadi kubwa ya wafanyakazi waliostaafu utumishi wa serikali hawajui kuwa  wanapaswa kulipwa mafao kwa kipindi cha miaka mitatu mara baada ya mume au mke wa mnufaika wa mafao hayo atakapofariki.

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Wafanyakazi Wastaafu Mkoa wa Singida,Shabani Mwanja aliyasema hayo kwenye mkutano wa wanachama wa chama hicho uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Kituo cha walimu Nyerere,Manispaa ya Singida.

Alifafanua Mwanja kwamba  iwapo mtumishi wa serikali aliyestaafu anapokea mafao ya uzeeni,endapo atafariki mwenza wake atapaswa kulipwa mafao hayo( Survival Penshen) kwa kipindi cha miezi 36 (miaka mitatu) yeye pamoja na mtoto ambaye alikuwa bado tegemezi wa marehemu.

“Watumishi wale wanaopokea pensheni serikalini akifariki mwenza wake analipwa survaival Penshen miezi 36 au miaka mitatu yeye na mtoto wake ambaye alikuwa bado tegemezi wa marehemu,mnanielewa hapo ?”alihoji Makamu Mwenyekiti huyo.

Aidha Mwanja alibainisha pia kuwa kama mama amefariki wakati alikuwa akipokea malipo ya pensheni,baba atalipwa miezi 36 na mtoto tegemezi ambaye alikuwa bado ana umri mdogo,au mama vile vile atalipwa kwa ajili ya mume wake aliyefariki akiwa analipwa pensheni na mtoto ambaye alikuwa tegemezi.

“Hiyo mlikuwa mnaielewa sasa ikitokea nenda kwenye mfuko unaohusika utalipwa Survaival Penshen,sawa eeeh ?”aliwahoji wanachama hao wa wafanyakazi wastaafu.

Kwa upande wake Katibu wa Chama hicho Wilaya ya Singida,Hassani  Dumwala aliweka bayana kwamba lengo la kuanzishwa kwa chama hicho ni kupigania maslahi ya wafanyakazi wastaafu ili waweze kunufaika na huduma wanazotakiwa kupatiwa na serikali baada ya utumishi wao kufikia ukomo.

Aidha Katibu Dumwala alizitaja baadhi ya haki ambazo wanachama wao hawanufaiki kwa mujibu wa sheria kuwa ni huduma duni za matibabu,malipo pensheni ya shilingi laki moja yaliyopitwa na wakati, haitoshelezi chochote kile kwa wakati uliopo kwa sasa.

Kwa mujibu wa Katibu huyo kwa kuwa serikali inawaamini wastaafu hao na kikubwa zaidi kwa kuwa ilishawaona utendaji wao wa kazi,hivyo alitumia fursa hiyo kuiomba serikali kuangalia uwezekano wa kuwaongeza malipo yao ya mafao ya pensheni,ili yaweze kuwasaidia kujikimu kimaisha,kwani kiwango wanacholipwa kwa sasa ni kidogo huku hali ya maisha ikizidi kupanda.

Katibu huyo wa Chama Cha Wafanyakazi wastaafu wilaya ya Singida hata hivyo aliwahakikishia wanachama hao kwamba wanaandaa utaratibu wa kuwaita watendaji wa mifuko ya hifadhi ili wakatoe elimu juu ya haki za wastaafu hao kwa kila mfuko uliosajili wanachama hao.

Akifunga mkutano huo wa wafanyakazi waliostaafu kwa niaba ya Ofisa Tarafa ya Unyakumi,Edward Salumu alitumia fursa hiyo kuwahimiza wanachama hao kutokosa kuhudhuria kwenye mkutano wao unaotarajia kufanyika jan,31,mwaka huu kwenye ukumbi wa mikutano wa Kituo cha Walimu Nyerere,Manispaa ya Singida lengo likiwa kupata viongozi.

Mkutano huo wa wanachama wa wafanyakazi waliostaafu wilaya ya Singida ulilazimika kutofanyika na hivyo kuahirishwa hadi jan,31,mwaka huu baada ya wanachama kutoka katika kata za Mwankoko,Utemini,Uhamaka na Mandewa kutohudhuria kwenye mkutano huo. 
Baadhi ya wanachama wa chama cha wafanyakazi wastaafu wa wilaya ya Singida wakiwa kwenye ukumbi wa mikutano wa kituo cha walimu Nyerere,Manispaa ya Singida wakiwa na lengo la kuchagua viongozi wao.



 Baadhi ya wanachama wa chama cha wafanyakazi wastaafu wa wilaya ya Singida wakipiga kura za kukubaliana kuahirishwa kwa mkutano huo baada ya wajumbe wa kata nne kutohudhuria kwenye mkutano huo na nhivyo kupangwa kufanyika tena jan,31,mwaka huu.(Picha zote na Jumbe Ismailly)

TAARIFA

SHIRIKA LA UNDER THE SAME SUN LATOA ELIMU KWA WADAU KUHUSU UALIBINO JIJINI MWANZA.

$
0
0
Afisa Maendeleo ya Jamii mkoani Mwanza Isaac Ndassa, akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, kwenye ufunguzi wa semina kwa wadau wanaosaidia kutokomeza ukatili dhidi ya watu wenye ualibino, inayofanyika kwa siku nne kuanzia leo Jijini Mwanza. 

Semina hiyo imeandaliwa na Shirika la kimataifa la kutetea haki za watu wenye ualibino la Under The Same Sun ambapo imelenga kupanua uelewa kwa wanajamii/ wadau  kuhusu ualibino ili kusaidia kupambana na ukatili kwa watu wenye hali hiyo.
Binagi Media Group
Mwasisi wa Shirika la kimataifa la kutetea haki za watu wenye ualibino la Under The Same Sun, lenye makao yake makuu nchini Canada, Peter Ash, akizungumza na wanahabari kwenye semina hiyo.
Mkurugenzi wa Shirika la kimataifa la kutetea haki za watu wenye ualibino la Under The Same Sun nchini Tanzania, Bi.Vicky Ntetema, akifafanua jambo kwenye semina hiyo.
Mkufunzi Dr.George Rhoades kutoka nchini Marekani, akitoa 
 Shirika la kimataifa la kutetea haki za watu wenye ualibino duniani, Under The Same Sun, limebainisha kwamba vitendo vya ukatili dhidi ya watu wenye ualibino nchini vinaendelea kupungua.

Mkurugenzi wa shirika hilo nchini, Vicky Ntetema, ameyasema hayo leo Jijini Mwanza kwenye semna kwa wadau wanaofanya kazi kwa ukaribu na watu wenye uaribino kutoka taasisi mbalimbali ikiwemo za kijamii, elimu na afya.

Ntetema amesema elimu inayoendelea kutolewa kwa wanajamii imesaidia kupunguza ukatili kwa watu wenye ualibino ikiwemo kukatwa viungo na mauaji licha ya kwamba kumekuwepo taarifa za makaburi ya watu wenye ualibino waliofariki kufukuliwa katika mikoa ya Kagera, Mbeya na Morogoro.

Mwasisi wa shirika hilo lenye makao yake makuu nchini Canada, Peter Ash, ameeleza kufurahishwa na maendeleo ya wanafunzi zaidi ya 300 wenye ualibino wanaosomeshwa na shirika hilo katika mikoa ya Kanda ya Ziwa ambapo amewasihi wanajamii kuondokana imani potofu juu ya watu wenye ualibino ili kutokomeza ukatili dhidi yao.

Akizungumza kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Mwanza, Afisa Maendeleo ya Jamii mkoani Mwanza Isaac Ndassa, amesema serikali imelenga kuhakikisha vitendo vya ukatili kwa watu wenye ualibino vinatokomezwa ambapo amesisitiza elimu zaidi kuendelea kutolewa kwa wananchi ili kufanikisha lengo hilo.

POLISI YAWANOA WATENDAJI WA URA SACCOS

$
0
0
Kaimu kamanda wa Polisi mkoa wa Mororgoro (ACP) Leonce Rwegasila (katikati), akipokea taarifa ya washiriki wa mkutano mkuu wa nane wa chama cha ushirika cha kuweka akiba na kukopa cha Usalama wa Raia Saccos (URA SACCOS LTD), kutoka kwa (ASP) Emmanuel Katabi, kulia ni Meneja Mkuu wa URA SACCOS (SSP) Kim O. Mwemfula, na wamwisho ni (ASP) Bakari H. Mzungu.
Mwezeshaji Mkaguzi wa Polisi (INSP) Edwin B. Mkole , akiwasilisha mada kuhusiana na taratibu za utoaji wa mikopo kwa wanachama wa chama cha ushirika cha kuweka akiba na kukopa cha Usalama wa Raia Saccos (URA SACCOS LTD), wakati wa mkutano mkuu wa nane wa chama hicho unaofanyika mkoani Morogoro.
Baadhi ya watendaji wa chama cha ushirika cha kuweka akiba na kukopa cha Usalama wa Raia Saccos (URA SACCOS LTD), wakiwasili mkoani Morogoro, kuhudhuria mkutano mkuu wa nane wa chama hicho utakaofanyia kwa muda wa siku mbili na kuwashirikisha watendaji na wawakilishi kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini.
    Kaimu kamanda wa Polisi mkoa wa Mororgoro (ACP) Leonce Rwegasila (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watendaji wa chama cha ushirika cha kuweka akiba na kukopa cha Usalama wa Raia Saccos (URA SACCOS LTD), mara baada ya ufunguzi wa mkutano mkuu wa nane unaofanyika mkoani Morogoro. (Picha zote na Demetrius Njimbwi – Jeshi la Polisi).


Na Demetrius Njimbwi – Jeshi la Polisi Morogoro.

Jeshi la Polisi nchini, limeendesha mafunzo ya kuwajengea uwezo watendaji wa chama cha ushirika cha kuweka akiba na kukopa cha Usalama wa Raia Saccos (URA SACCOS LTD) ili kuboresha utoaji wa huduma kwa wanachama wao kote nchini huku ikiweka dhamira ya kutoza riba ya mkopo kwa  asilimia 10.5 kwa mwaka.

Akifungua mafunzo ya siku mbili yanayofanyika mkoani Morogoro, Kaimu kamanda wa Polisi hapa (ACP) Leonce Rwegasila, alisema kuwa, kwa kuzingatia umuhimu na uzito wa mkutano huu ni vyema kila mshiriki akazingatia mahudhui ya kile kitakachotolewa ili kuwa mjumbe mzuri kwa kupeleka elimu mahala alikotoka, alisema.

Hata hivyo, alisema, katika mafunzo haya zipo mada pamoja na mijadala mbalimbali itakayojadiliwa ili kuja na majibu mujarabu yatakayowezesha kuwa na Saccos imara na yenye kukidhi mahitaji kwa  wanachama wao ambao ni askari Polisi pamoja na familia zao.
Kwa upande wake Meneja Mkuu wa URA SACCOS LTD (SSP) Kim O. Mwemfula, alisema zipo huduma zilizoanzishwa za uhakika za ushirika wa kuweka akiba na kukopa kupitia Usalama wa Raia Saccos (URA SACCOS LTD), ambapo askari aliye mwanachama wa ushirika huo uweza kuweka na kukopa kwa riba nafuu ili kuweza kuboresha maisha yake na familia yake katika Nyanja za Kielimu, Biashara na hata Ujenzi wa nyumba.

Ameongeza kuwa, masuala ya ustawi kwa askari yamesaidia kujenga utulivu wa akili kwa askari Polisi pamoja na kuboresha suala la ustawi wa usalama wa raia na mali zao na kulifanya taifa kuwa la amani na utulivu na kukabiliana na aina zote za matishio ya kiuhalifu na wahalifu.

Lavy Workshop yaandaa semina Kwa Wote Wanaotumia Bidhaa Za Lavy

$
0
0
Jana kampuni ya bidhaa za kucha, Lavy iliandaa semina kwa ajili ya baadhi ya watengeza kucha wanaotumia bidhaa zao ili kufundishana mawili matatu kuhusu bidhaa hizo na sekta nzima inayohusu masuala ya kucha. Semina hii ilifunguliwa rasmi na Naibu Waziri wa Afya, Doctor Kigwangala.
Changamoto kwenye sekta hii ni nyingi kuanzia kwenye bidhaa, utengenezaji wa kucha, sehemu husika za kutengeneza kucha pamoja na watengeneza kucha wenyewe.Mbali na Lavy kuelimisha matumizi sahihi ya bidhaa zao pia imegusia changamoto nyingine nyingi zikiwepo usafi na usanifu na sekta hii.
 
Mh. Doctor Kigwangala akizawadiwa notebook kwa ajili yake na bidhaa za Lavy kwa ajili ya Mke wake.
Flaviana Matata akitoa somo kuhusu usafi wa vifaa na saluni kwa ujumla, huku akigusia kuhusu huduma bora kwa wateja itakayokua chachu ya kuongeza mapato ya saluni na idadi ya wateja.
 
Wakipokea vyetu vya kuhudhuria semina ya Lavy workshop.
(Certificate of participation)
 

WASICHANA WANNE WA TANZANIA WAENDA KUPATA MAFUNZO YA UONGOZI, UTAMADUNI AFRIKA MASHARIKI NA KATI

$
0
0
 Wasichana wanne wa Tanzania wakiaga  kwa kupungia mikono huku wakiwa na , Bendera ya Taifa waliyokabidhiwa na Kamishna Mkuu wa Chama cha Tanzania Girl Guids (TGGA), Symphorosa Hangi katika hafla ya kuwaaga kwenda Uganda ambako watakutana na wenzao 31 kutoka nchi za Afrika Mashariki na Kati katika mafunzo ya uongozi na utamaduni katika nchi hizo. Hafla hiyo ilifanyika Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, Dar es Salaam juzi. Kutoka kulia ni Farida Mjoge,Elizabeth Betha, Edna Chembele na Ummy Mwabondo. (PICHA, HABARI NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG)
 Kamishna Mkuu wa Chama cha Tanzania Girl Guids (TGGA), Symphorosa Hangi (kushoto) akiwakabidhi wasichana wanne, Bendera ya Taifa katika hafla ya kuwaaga kwenda Uganda ambako watakutana na wenzao 31 kutoka nchi za Afrika Mashariki na Kati katika mafunzo ya uongozi na utamaduni katika nchi hizo. Hafla hiyo ilifanyika Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, Dar es Salaam juzi. Kutoka kulia niElizabeth Betha, Edna Chembele, Farida Mjoge na Ummy Mwabondo. 

Na Richard Mwaikenda
WASICHANA wanne wameondoka kwenda Uganda  kwenye programu maalumu ya kubadilishana uzoefu wa mafunzo ya uongozi na utamaduni.

Wakifika Uganda wataungana na wenzao 31 kutoka nchi nane za Afrika Mashariki na Kati, ambapo watapigwa msasa wa mafunzo hadi Januari 25, mwaka huu watakapotawanywa kwenda nchi mbalimbali.

Wasichana hao wanachama wa Chama cha Tanzania Girl Guids (TGGA),waliondoka Uwanja wa Ndege wa Kimaitafa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam, juzi kwa Ndege  ya Kenya Airways, baada ya kukabidhiwa Bendera ya Taifa na Kamishna Mkuu wa Tgga,  Symphorosa Hangi.

Wasichana hao 35 watagawanywa katika nchi hizo nane ambapo nchini wataletwa watatu kutoka katika baadhi ya nchi hizo, kuja kujifunza masuala ya uongozi na utamaduni.

Akizungumza wakati wa kuwaaga wasichana hao, Kamishna Mkuu wa Tgga, Hangi  alisema lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo wasichana ili wawe viongozi bora wa baadaye katika nchi zao ikiwemo pia kujiamini na kujithamini.

Alitaja nchi zitakashiriki kwenye programu hiyo ambayo kwa hapa nchini  ilianza mwaka jana, kuwa ni; Tanzania, Kenya, Uganda, Zambia, Rwanda, Burundi, Zimbabwe na Afrika Kusini.

Alisema kuwa watakapokuwa kwenye nchi hizo husika, kila mmoja ataishi maisha ya kujitegemea kwa kwenda vijijini kuishi na wananchi na kuzungumza nao kuhusu mambo mbalimbali ya maisha ikiwemo uongozi, utamaduni, kujiamini na kujithamini. Gharama za kwenda katika nchi hizo hufahiliwa na Taasisi ya FK Norway ambayo huwapatia nauli, fedha za malazi, posho na masuala ya afya.

Alisema kuwa watakaporejea nchini Julai mwaka huu, watapaswa kutoa mrejesho wa waliojifunza huko, ili usaidie kuwaelimisha wasichana wengine nchini.



 Kamishna akiwakabidhi nyaraka mbalimbali za kazi

 Ni furaha iliyoje
 Wakipiga picha na baadhi ya wafanyakazi wa TGGA

 Wakipiga picha na dereva wa TGGA,Juma Rashid
Kamishna akiagana na mmoja wa wasichana hao

MSIMU WA 15 WA MASHINDANO YA KIMATAIFA YA MBIO ZA KILIMANJARO PREMIUM LAGER MARATHON 2017 WAZINDULIWA RASMI MKOANI KILIMANJARO

$
0
0
Mkuu wa wilaya ya Moshi,Kippi Warioba akizungumza wakati wa uzinduzi wa msimu wa 15 wa mbio za kimataifa za Kilimanjaro Premium Lager Marathon 2017 ,uzinduzi uliofanyika Kibo Palace Home mjini Moshi.
Baadhi ya wageni waalikwa wakifuatilia uzinduzi huo.
Meneja Mauzo wa Kampuni ya TBL mikoa ya Kilimanjaro na Tanga ,Richard Temba akizungumza wakati wa uzinduzi huo,TBL ndio wadhamini wakuu wa Mbio hizo kupitia Bia yake ya Kilimanjaro Premium Lager.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Mawasiliano ya simu za mkononi ya TIGO ,Kanda ya Kaskazini,George Lugata akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mbio za Kimataifa za Kilimanjaro Premium Lager Marathon 2017 ,Tigo wanadhamini mbio hizo kwa upande wa Mbio za Kilometa 21
Baadhi ya wageni waalikwa katika hafla fupi ya uzinduzi wa mbio hizo.
Meneja Masoko wa Kampuni ya GAPCO Tanzania ,Caroline Kakwezi akizingumza wakati wa hafla hiyo ya uzinduzi wa mbio za Kilimanjaro Premium Lager Marathon 2017,GAPCO wanadhamini mbio za Kilometa 10 kwa upande wa walemavu.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Executive Solution ,Aggrey Mareale ambao ndio waratibu wa mbio hizo akizungumza wakati wa hafla hiyo.
Mwakiishi wa Kampuni ya Sukari ya TPC,Allen Maro akizungumza wakati wa hafla hiyo,TPC pia ni wadhamini wa mashindano hayo ya kimataifa ambayo hufanyika kila mwaka.
Afisa Uhusiano na Mawasiliano wa Kampuni ya kuchimba Dhahabu ya Geita Gold Mining (GGM) Tenga B Tenga akizungumza wakati wa uzinduzi huo,GGM wakiwa ni wadhamini wapya katika mashindano hayo.
Mwenyekiti wa Chama cha Riadha mkoa wa Kilimanjaro (KAA) Liston Methacha akizungumza kwa niaba ya shirikisho la Riadha Tanzania katika uzinduzi huo.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Wildfrontiers,John Hudson ambao ndio waandaaji wa mbio hizo akizungumza wakati wa hafla hiyo.
Mkurugenzi wa Kibo Palace,Vicent Lasway akizungumza katika hafla hiyo.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,Wilbroad Mutafungwa akizungumza katika hafla hiyo.
Mgeni rasmi katika hafla hiyo Mkuu wa wilaya ya Moshi,Kippi Warioba akiwapongeza wawakilishi wa kampuni zilizojitokeza kudhamini Mbio hizo za kimataifa.
Mkuu wa wilaya ya Moshi,Kippi Warioba akiwa na wawakilishi wa kampuni zinazodhamini mbio za Kimataifa za Kilimanjaro Marathoni 2017 pamoja na jeshi la Polisi ,akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Mbio hizo.
Mgeni rasmi katika hafla fupi ya uzinduzi wa Mbio za Kimataifa za Kilimanjaro Premium Lager Marathoni 2017 akiwa katika picha ya pamoja na wadhamini wa Mbio hizo.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii kanda ya Kaskazini. 

TUME YA MIPANGO YATEMBELEA KIWANDA CHA TANGA CEMENT

$
0
0
Meneja wa Kiwanda cha Tanga Cement, Mhandisi Ben Lema (mwenye Miwani) akimwonesha Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri (mwenye koti jenkundu) eneo (halipo pichani) linalochimbwa na kiwanda hicho kwa zaidi ya miaka 30 kwa ajili ya kupata malighafi zinazotumika katika kutengeneza saruji kiwandani hapo. Wengine ni Maofisa wa Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo walioambatana na Kaimu Katibu Mtendaji katika ziara hiyo.


Eneo linalochimbwa kwa zaidi ya miaka 30 kwa ajili ya kupata mawe yanayotumika kutengenezea saruji. Baada ya kumalizika kwa shughuli za uchimbaji, Kiwanda cha Tanga Cement kitafanya eneo hilo kuwa sehem ya utalii kwa kutengeneza bwawa na kufuga wanyama mbalimbali.


Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri akiuliza namna mifumo ya komputa ya kiwanda hicho inavyoendesha shughuli za uzalishaji wa saruji katika kiwanda cha Tanga Cement.
Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri akikagua mifumo ya kisasa inayotumika kuendesha shughuli mbalimbali katika kiwanda cha Tanga Cement.
Meneja wa Kiwanda cha Tanga Cement, Mhandisi Ben Lema akionesha aina za malighafi na aina mbalimbali za saruji zinazozalishwa na kiwanda hicho.
Baadhi ya mitambo inayoendelea kufanya kazi katika kiwanda cha Tanga Cement.PICHA ZOTE NA ADILI MHINA, TUME YA MIPANGO

Na Adili Mhina, Tanga.

Timu ya ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Tume ya Mipango ikiongozwa na Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume hiyo, Bibi Florence Mwanri imefanya ziara katika Kiwanda cha Tanga Cement kilichopo Mkoani hapa kwa lengo la kukagua shughuli mbalimbali zinazofanywa na kiwanda hicho.

Katika ziara hiyo, Bibi Mwanri alipata fursa ya kukagua maeneo mbalimbali ya kiwanda hicho ikiwa ni pamoja na eneo linalotumika kuchimba malighafi za kutengenezea saruji, teknolojia ya kisasa inayotumika kuendesha mashine kiwandani hapo pamoja na kuangalia hatua mbalimbali zinazotumika katika uzalishaji wa saruji.

Akiwa katika eneo linalochimbwa mawe ya kutengenezea saruji, Mwanri alieleza kuwa kiwanda hicho kina wajibu wa kuhakikisha sheria na taratibu za utunzaji wa mazingira zinazingatiwa muda wote ili kuhakikisha mazingira yanabaki salama licha ya shughuli za uchimbaji kuendelea kufanyika.

Mwanri alipongeza uongozi wa kiwanda hicho kwa kuendelea kutekeleza majukumu yake katika kuunga mkono dhamira ya Serikali ya kuwa nchi ya Viwanda na kuharakisha malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo inayosisitiza kufikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

Naye Meneja wa Kiwanda hicho, Mhandisi Ben Lema alisema kuwa kiwanda hicho kimeendelea kutoa ajira kwa watanzania katika kada mbalimbali ambapo kwa sasa kua ajira zaidi ya 600 ambapo ajira 300 ni za moja kwa moja huku ajiara 300 zingine ambazo sio za moja kwa moja zinajumuisha wauzaji, wasambazaji, wasafirishaji na wengine walioko katika mnyororo huo.

Aliongeza kuwa bidhaa za kiwanda hicho bado zinafanya vizuri sokoni licha ya ushindani uliopo kufuatia kuanzishwa kwa viwanda vingi vinavyozalisha saruji kwa kuwa mahitaji ya saruji bado ni mwakubwa sokoni.

Lema alieleza kuwa viwanda vya saruji vinapata faraja kubwa kwa kuwa miradi mbalimbali ya ujenzi inayotekelezwa na Serikali na hata inayotekelezwa na sekta binafsi inatumia saruji inayotengenezwa na viwanda vya ndani

PROFESA MBARAWA ATAKA MFUKO WA MAWASILIANO KUKAMILISHA MAWASILIANO VIJIJINI

$
0
0
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa(Kulia), akitoa maelekezo kwa Mjumbe wa Bodi ya Mfuko wa Mawasiliano kwa wote UCSAF Bw. Godfrey Simbeye, wakati alipokagua shughuli zinazofanywa na mfuko huo jijini Dar es salaam.
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa(Kulia), akipata taarifa ya utendaji kutoka kwa Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa wote UCSAF Eng. Peter Ulanga, alipokagua shughuli zinazofanywa na mfuko huo jijini Dar es salaam.
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, akikagua kumbukumbu za wateja wanaohudumiwa  na kampuni ya simu TTCL kanda ya Kaskazini eneo la Kijitonyama jijini Dar es salaam.
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (Katikati), akisisitiza jambo kwa maofisa wa kampuni ya Simu TTCL kanda ya Kaskazini alipokagua huduma zinazotolewa na kampuni hiyo.
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa mmoja wa ofisa wa kampuni ya Simu TTCL namna ya kufanya kazi kwa ubunifu  ili kuongeza wateja katika  kampuni hiyo. Picha na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa ameitaka Menejimenti ya Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF), kuhakikisha vijiji vyote nchini ambavyo havijaunganishwa na huduma ya  mawasiliano vinaunganishwa kabla ya mwisho wa mwaka huu.
Aidha, Profesa Mbarawa amesisitiza mfuko huo kutoa kipaumbele kwa vijiji vyote vilivyomo sehemu za mipakani ili kuimarisha ulinzi na uharaka wa mawasiliano katika maeneo hayo.

Amewaagiza UCSAF kukutana na mitandao ya simu ili kukamilisha kazi  kwa mujibu wa mkataba kwa kata 121  ambazo hazijapata huduma ya mawasiliano hapa nchini.

 “Nia ya Serikali ni kuhakikisha vijiji vyote nchini vinapata huduma ya mawasiliano ifikapo mwishoni mwa mwezi Novemba ili kuwezesha mikakati mingine ya kuboresha Mifumo ya Tehama katika shule na Hospitali kuendelea na hivyo kuhuisha huduma za Tehama katika Sekta za afya na elimu”, amesema Profesa Mbarawa.

Profesa Mbarawa ameonya kampuni za simu zitakazoshindwa kupeleka mawasiliano katika maeneo waliyopangiwa kwa wakati zitapokonywa masafa katika maeneo husika ili kuzipa kampuni zilizo tayari.
Naye Mjumbe wa Bodi ya UCSAF Bw. Godfrey Simbeye, amemhakikishia Waziri Mbarawa kuwa Bodi yake imejipanga kuhakikisha inaratibu huduma zote za Tehama zinazotolewa na taasisi mbalimbali nchini ili kuweka uwiano wa huduma hizo nchini kote.

Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa UCSAF Eng Peter Ulanga, amesema kuwa mfuko huo umejipanga kupeleka mawasiliano katika maeneo yasiyo na mvuto kibiashara ili kutoa haki kwa wakazi wa maeneo hayo kunufaika na fursa za mawasiliano na kuchochea maendeleo.Takribani asilimia 94 ya Wakazi wa Tanzania wanapata huduma ya mawasiliano lengo likiwa ni kufikia asilimia 100 ifikapo mwishoni mwa mwaka huu.


Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

NAIBU WAZIRI MHANDISI MASAUNI AWASILI LEO JIJINI MBEYA KWA ZIARA YA KIKAZI

$
0
0
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto), akisindikizwa na kiongozi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe baada ya kuwasili jijini Mbeya kwa ziara ya kikazi.

Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(kushoto), akisalimiana na viongozi wa Idara za wizara yake hiyo jijini Mbeya baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe kwa ziara ya kikazi.

Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia), akiweka saini katika kitabu cha wageni baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe, jijini Mbeya kwa ziara ya kikazi.Wengine ni viongozi wa idara za wizara yake jijini hapo.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(katikati), akizungumza na aliyewahi kuwa kiongozi katika Serikali zilizopita,Profesa David Mwakyusa (kushoto), baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe, jijini Mbeya kwa ziara ya kikazi.(Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA ATATUA MGOGORO WA MPAKA WA KILINDI NA KITETO

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akizugumza na  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi   (kushoto),  Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Dkt. Joel Bendera wakiwa katika kijiji cha Lembapuli kilichopo kwenye mpaka  wa wilaya ya Kiteto na Kilindi  Januari 18, 2017.  Mheshimiwa Majaliwa alikwenda Kiteto na Kilindi kutatua mgogoro wa mpaka unaovikabili vijiji vya  Mafisa na Kijungu. Wapili kushoto ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga na Muu wa Wilaya ya Tanga mjini , Thobias Mwilapwa. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri   Mkuu, Kassim Majaliwa  akielekea kwenye moja ya  jiwe la mpaka wa  wilaya ya Kilindi na Kiteto wakati alipokwenda  kwenye kijiji cha Lembapuli kilichopo kwenye mpaka wa Kiteto na Kilindi kutatua  mgogoro wa mpaka Januari 18, 2017. Kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Dkt. Joel Bendera na kulia kwake ni  Mkuu wa wilaya na Tanga na Kaimu  Mkuu wa Mkoa wa Tanga Thobias Mwilapwa. 
 Waziri Mkuu, Kassim  Majaliwa akipata maelezo  kutoka kwa watalaam wa upimaji ardhi kuhusu jiwe la alama ya mpaka wa wilaya ya Kilindi na Kiteto katika kijiji cha  mpakani cha Lembapuli  Januari 18, 2017. . Kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Dkt. Joel Bendera na kulia kwake ni  Mkuu wa wilaya na Tanga na Kaimu  Mkuu wa Mkoa wa Tanga Thobias Mwilapwa. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akipata  maelezo kuhusu ramani inayoonyesha mpaka  wa wilaya  ya Kilindi na Kiteto katika kijiji cha mpakani cha Lembapuli wakati alipokwenda kutatua mgogoro wa mpaka kati ya wialya hizo Januari 18, 2017.  Mheshimiwa  Majaliwa apia alifuatana na Mawaziri , William Lukuvi wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya makazi na George Simbachawene  wa Ofisi ya Rais- TAMISEMI.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wananchi wa Kiteto na Kilindi  wakati  alipokwenda kwenye kijiji  cha Lembapuli  kilichopo kwenye mpaka wa wilaya hizo  kutatua mgogoro wa mpaka Januari  18, 2017.  Wapili kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Manyara, Dkt. Joel Bendera na wapili kulia ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga na Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Thobias Mwilapwa. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akihutubia  mkutanao wa hadhaa katika kijiji cha  Lembapuli kilichopo mpakani mwa wilaya za Kilindi na Kiteto alikokwenda kutatua mgogoro wa  mpaka  Januari 18, 2017. 
  Baadhi ya wananchi wa  wilaya za Kilindi na Kiteto wakimshangilia  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipohutubia mkutano wa hadhara katika kijiji  cha  Lembapuli kilichopo  mpakani mwa wilaya za Kiteto na Kilindi alikokwenda kutatua mgogoro wa mpaka Januari 18, 2017. (Picha na Ofisi ya  Waziri Mkuu)


WAZIRI MKUU AMALIZA MGOGORO WA MPAKA KILINDI NA KITETO
*Awaonya viongozi wa siasa wasiwavuruge wananchi

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameumaliza mgogoro wa mpaka wa ardhi baina ya vijiji vya wilaya za Kiteto na Kilindi uliodumu kwa muda mrefu.

Mgogoro huo ambao ulianza kusuluhishwa tangu mwaka 1997, umepata suluhu kwenye mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Waziri Mkuu na kuwajumuisha Wakuu wa Mikoa hiyo miwili, Wabunge wa Kiteto na Kilindi, wenyeviti wa Halmashauri na madiwani wa kata mbili za mpakani pamoja na wananchi wa kata hizo.

Waziri Mkuu pia amewataka wanasiasa na viongozi wengine kutowavuruga wananchi na badala yake wawaongoze vizuri na kutoa maelekezo kwa mujibu wa sheria za nchi.

Ametoa agizo hilo leo (Jumatano, Januari 18, 2017)  wakati akizungumza na wananchi wa wilaya za Kiteto na Kilindi katika kijiji cha Lembapili wilayani Kiteto, mkoani Manyara ambako ni kuna mpaka wa  wilaya hizo mbili alipokwenda kutatua mgogoro huo.

Amesema viongozi wa wilaya hizo lazima wafuate sheria na wawaelekeze wananchi umuhimu wa kuzingatia sheria za nchi ikiwa ni pamoja na kuheshimu mipaka iliyowekwa kwa mujibu wa sheria ili kuepusha migogoro.

Akizungumzia kuhusu mgogoro huo wa mpaka, Waziri Mkuu amesema nchi ilishaweka mipaka ya mikoa na wilaya zake yote tangu zamani na kumbukumbu zipo zikiwemo za mpaka wa  wilaya hizo tangu mwaka 1961 kwa  tangazo la Serikali namba 65 na hakuna mabadiliko. Hivyo, aliwasisitiza wauheshimu na kuufuata.

Amesema Serikali kupitia Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi itakwenda kuweka alama vizuri na viongozi wa wilaya hizo watashirikishwa. Alama hizo zitawekwa na kifaa maalumu, hivyo amewataka wahusika watoe ushirikiano.

Waziri Mkuu amesema katika kipindi ambacho Serikali itakuwa ikiweka alama hizo, wananchi waendelee na shughuli zao hadi hapo zoezi litakapokamilika na wala wasibughudhiwe.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu ametoa siku nane kwa watu wote wanaomiliki silaha katika wilaya za Kilindi na Kiteto wazipeleke kwenye vituo vya Polisi ili zisajiliwe upya na kisha Wakuu wa Mikoa wafanye operesheni maalum na atakayekutwa anamiliki silaha kinyume cha sheria achukuliwe hatua.

“Wakuu wa Mikoa fanyeni ukaguzi maalum na atakayekutwa anamiliki silaha kinyume na utaratibu achukuliwe hatua kwa mujibu wa sheria. Pia kuna watu wana mitambo ya kutengenezea bunduki hapa, nao pia waisalimishe haraka,” amesisitiza. 

Kwa upande wake, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Bw. William Lukuvi amesema mwanzoni mwa Februari wataalamu wake watakwenda katika mpaka huo ili kuanza kuweka alama vizuri.

Amesema baadhi ya viongozi huwa wana tabia ya kuzuia watendaji kutekeleza majukumu yao, hivyo ametumia gursa hiyo kuwaomba viongozi wa wilaya hizo watoe ushirikiano.

Amesema moja ya majukumu aliyopewa na Mheshimiwa Rais, Dk. John Pombe Magufuli ni kuhakikisha ndani ya miaka hii mitano anamaliza migogoro ya ardhi nchini ukiwemo huo wa Kilindi na Kiteto.

(mwisho)

IMETOLEWA NA
OFISI YA WAZIRI MKUU
JUMATANO, JANUARI 18, 2017.

Viewing all 46362 articles
Browse latest View live




Latest Images