Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1096 | 1097 | (Page 1098) | 1099 | 1100 | .... | 1898 | newer

  0 0

  Frank Mvungi-Maelezo

  Serikali imewahakikishia Watanzania kuwa kuna utoshelevu wa dawa kwa asilimia 86 kinyume na taarifa za upotoshaji zinazotolewa na baadhi ya watu.Akizungumza na Waandishi wa Habari Leo .

  Jijini Dar es salaam Mkurugenzi Mkuu wa Bohari kuu ya Dawa (MSD) Bw. Laurean Rugambwa amesema kuwa Serikali ya awamu ya tano imetenga bajeti yakutosha kukidhi mahitaji ya dawa hapa nchini ambapo kufikia machi 2017 upatikanaji wa Dawa utafikia asilimia 90.

  “ Serikali imetenga bilioni 250 katika bajeti ya mwaka huu na Kila mwezi Serikali inatoa zaidi ya bilioni 20 ajili ya ununuzi wa dawa hali iliyosaidia kuondoa tataizo la dawa hapa nchini kwa sasa”

  Akifafanua Rugambwa amesema kwa sasa fedha sio tatizo kwa Bohari ya dawa kutokana na hatua za makusudi zinazochukuliwa na Serikali ya awamu ya tano katika kuhakikisha kuwa Watanzania wanapata huduma bora za afya ikiwemo upatikanaji wa dawa.

  Moja ya mikakati iliyochukuliwa na Serikali katika kuimarisha hali ya upatikanaji wa dawa ni kuboresha matumizi ya mfumo wa msimbo pau (Barcode) hali itakayosaidia kuongeza ufanisi katika upokeaji,utunzaji na usambazaji wa dawa na vifaa tiba.

  Mikakati mingine ni kuanziasha mpango wa huduma maalum kwa wateja wakubwa ambao ni Hosipitali ya Taifa Muhimbili,MOI, Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, Hospitai ya Bugando,Hosipitali ya Kibongoto,Hospitali ya Mirembe,Hospitali ya Amani, Hospitali ya Temeke, Mwanenyemala,Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Mbeya,KCMC, Hosipitali ya Benjamin Mkapa na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete.

  Pia kununua dawa moja kwa moja kutoka kwa wazalishaji na kuanzisha mchakoto wa ujenzi wa viwanda vya kuzalisha dawa na vifaa tiba nchini ili kupunguza gharama.

  Katika kipindi cha mwaka 2016 MSD imefungua maduka ya dawa sehemu mbalimbali nchini lengo likiwa ni kuwezesha Hospitali ambazo ndio wateja wakubwa wa MSD,Maduka ambayo mpaka sasa yameshafunguliwa ni pamoja na lile lililopo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili,Sekou Toure Mwanza,Hospitali ya rufaa Mbeya,Mount Meru Hospitali ,Chato Halmashauri ya Mji wa Geita na Ruangwa Mkoani Lindi.
  Mkurugenzi wa Bohari ya Dawa (MSD) Laurean Bwanakunu (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, wakati akitoa taarifa ya kuimarika kwa upatikanaji wa dawa nchini. Kulia ni Ofisa Mwandamizi wa Idara Habari Maelezo, Zamaradi Kawawa.

  0 0

  Frank Mvungi- MAELEZO

  Watanzania wameaswa kupunguza unywaji wa pombe ili waweze kushiriki katika ujenzi wa uchumi wa viwanda na kulifikisha taifa kwenye uchumi wa kati ifikapo 2020.

  Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Msaidizi Magonjwa yasiyopewa Kipaumbele kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Prof. Ayoub Maghimba amesema kuwa ni vyema watu wakapunguza unywaji wa Pombe ili kutumia muda mwingi katika uzalishaji na kuepuka magonjwa yasiyo ya kuambukiza.

  “Magonjwa yasiyo ya kuambukiza ni pamoja na Saratani,magonjwa ya moyo,magonjwa sugu ya njia ya hewa,seli mundu,magonjwa ya akili na dawa za kulevya,magonjwa ya figo,kisukari,ajali, na magonjwa ya macho yasiyo ya kuambukiza” Alisisitiza Prof. Maghimba.
  Akifafanua Prof. Maghimba alisema kuwa utafiti uliofanyika ulionyesha asilimia 15.9 ya wananchi wanavuta sigara, asilimia 29.3 wanakunywa pombe, asilimia 97.2 wanakula mbogamboga na matunda chini ya mara tano kwa siku hali inayowaweka katika hatari ya kupata magonjwa yasiyo ya kuambukiza.

  Alisema kuwa unywaji wa pombe uliokithiri unasababisha magonjwa kama saratani ambayo inachangia vifo na wastani wa wagonjwa 109 hugundulika na saratani kila siku hapa nchini.

  “Magonjwa yasiyo ya kuambukiza au magonjwa sugu ni magonjwa ambayo mtu akiyapata hawezi kuambukiza wengine na ataishi nayo hadi siku ya kufa.” Alisisitiza Prof.Maghimba.

  Magonjwa haya yamekuwa yakiongezeka duniani kote, hasa kwenye nchi zilizo chini ya Jangwa la Sahara,Tanzania ikiwemo. Magonjwa yasiyo ya kuambukiza yanachangia asilimia 27 ya vifo vyote duniani.

  0 0

  Ajali ya Jahazi ambayo ilitokea usiku wa kuamkia leo iliyosababisha vifo vya abiria 12 na wengine 25 kujeruhi kwenye tukio hilo.

  Jahazi hilo lenye namba za usajili Z5512 MV Burudani maarufu kama Sayari lilikuwa likitokea eneo la Bandari Bubu ya Sahare kuelekea Visiwani Pemba ambapo lilipofika eneo la Jambe chombo hicho kilipigwa na dhoruba kali na hivyo kumshinda nahodha wake Badru Saidi na kuzama

  Akizungumza na MTANDAO huu,Mbunge Mussa alisema amepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za ajali hiyo na kuwataka ndugu na jamaa kuwa na uvumilifu na kuhaidi kuwa nao bega kwa bega.

  Licha ya hivyo lakini pia mbunge huyo alikabidhi sanda 12 kwa ajili ya maziko ambayo yanatarajiwa kufanyika leo na kesho kwenye maeneo mbalimbali hapa nchini.Ajali hiyo ambayo ilitokea usiku wa kuamia leo kwenye eneo la kisiwa cha Jambe kandokando ya bandari ya Tanga imeacha simamanzi kubwa kwa wakazi wa mji huu na viunga vyake.

  Alisema kuwa yeye kama mbunge wa Jimbo la Tanga yupo nao bega kwa bega na kuwaombea mwenyezi mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi.“Ajali sio jambo ambalo tunalipanga bali ni mipango ya mwenyezi mungu lakini pia nivitake vyombo vya usafiri majini kuhakikisha havipakii mizigo mingi zaidi ya uwezo wao kwani hali hiyo inaweza kusababisha ajali “Alisema.

  Kamanda wa Polisi Mkoani Tanga,Benedict Wakulyamba alithibitisha kutokea tukio hilo na kueleza hivi sasa vyombo vya ulinzi na usalama wapo kwenye mchakato wa kutafuta watu wengine kwenye bahari ya hindi.

  Alisema kati ya miili hiyo iliyopatikana mpaka sasa wanaume watano na wanawake 7 wameweza kuokolewa katika tukio hilo.Aidha alisema mpaka sasa chanzo cha ajali hiyo bado hakijajulikana hivyo wanashirikiana na vyombo vyengine ili kubaini ingawa kwa mujibu wa mashuhuda chanzo chake kinatokana na chombo hicho kupigwa na wimbi eneo la nyuma na kukosa mwelekeo na kuzama baharini.

  Kwa upande wake,Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Bombo,Dkt Goodluck Mbwilo alithibitisha kupokea maiti 12 pamoja na majeruhi 25.Alisema kati ya majeruhi hao 18 ni watu wazima huko watoto wadogo wakiwa ni saba ambao waliweza kupewa huduma ya kwanza na kuendelea na matibabu mengine.
  MBUNGE wa Jimbo la Tanga (CUF) Mussa Mbaruku ametoa pole kwa ndugu na jamaa waliopoteza ndugu zao kwenye ajali ya kuzama kwa Jahazi kwenye kisiwa cha Jambe kandokando ya Bahari ya Hindi jijini Tanga na kuwataka kuwa na moyo wa uvumilifu katika kipindi hiki kigumu.

  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati ) alipokuwa akitoa hutuba yake ya Ufunguzi wa Tamasha la Tatu (3) la Biashara Zanzibar  katika viwanja vya Maisara wilaya ya Mjini Unguja leo ikiwa ni katika shamra shamra za miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,(kulia) Waziri wa Biashara,Viwanda na Masoko Mhe, Amina Salum Ali , na Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara,Viwanda na Masoko Bakari Hassan Bakari (kushoto).
  Waziri wa Biashara,Viwanda na Masoko Mhe, Amina Salum Ali ,(kulia) alipo
  kuwa akimkaribisha  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein ( katikati )  kufungua Tamasha la Tatu (3) la Biashara Zanzibar  katika viwanja vya Maisara wilaya ya Mjini Unguja leo ikiwa ni katika shamra shamra za miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
  Baadhi ya Watendaji na wageni mbali mbali waliohudhuria katika sherehe za Ufunguzi wa maonesho ya Tamasha la tatu la Biashara Zanzibar wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) alipokuwa kitoa hutuba yake ya ufunguzi katika viwanja vya Maisara Wilaya ya Mjini Unguja leo baada kufungua rasmi maonesho hayo
  ikiwa ni katika shamra shamra za miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
  Wafanyakazi kutoka Taasisi za Serikali na Binafsi waliohudhuria katika Ufunguzi wa maonesho ya Tamasha la tatu la Biashara Zanzibar wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) alipokuwa kitoa hutuba yake ya ufunguzi katika viwanja vya Maisara Wilaya ya Mjini Unguja leo baada kufungua rasmi maonesho hayo ikiwa ni katika shamra shamra za miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
  Wafanyakazi kutoka Taasisi za Serikali na Binafsi waliohudhuria katika Ufunguzi wa maonesho ya Tamasha la tatu la Biashara Zanzibar wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) alipokuwa kitoa hutuba yake ya ufunguzi katika viwanja vya Maisara Wilaya ya Mjini Unguja leo baada kufungua rasmi maonesho hayo ikiwa ni katika shamra shamra za miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,.
  Kikundi cha wasanii wa ngoma ya kibati wakiburudisha kwa Viongozi na Wananchi wakati wa Ufunguzi wa maonesho ya Tamasha la tatu la Biashara Zanzibar lililofunguliwa leo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) katika viwanja vya Maisara Wilaya ya Mjini Unguja leo,ikiwa ni katika shamra shamra za miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
  Viongozi mbali mbali waliohudhuria katika Ufunguzi wa  Tamasha la tatu la Biashara Zanzibar  lililofunguliwa leo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) sambamba na maonesho katika viwanja vya Maisara Wilaya ya Mjini Unguja leo,ikiwa ni katika shamra shamra za miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Waziri wa Biashara,Viwanda na Masoko Mhe, Amina Salum Ali alipowasili katika viwanja vya Maisara wilaya ya Mjini Unguja leo kufungua Tamasha la tatu la Maonesho ya Biasahara Zanzibar ikiwa ni katika shamra shamra za miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tantrade Dar es Salaam Edwin N.Rutageruka, mara alipowasili katika viwanja vya Maisara wilaya ya Mjini Unguja leo kufungua Tamasha la tatu la Maonesho ya Biasahara Zanzibar ikiwa ni katika shamra shamra za miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifuatana na Waziri wa Biashara,Viwanda na Masoko Mhe, Amina Salum Ali alipowasili katika viwanja vya Maisara wilaya ya Mjini Unguja leo kufungua Tamasha la tatu la Maonesho ya Biasahara Zanzibar ikiwa ni katika shamra shamra za miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
  [Picha na Ikulu.] 10/01/2017.

  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Dhow Financial Prof Mohamed Warsame akiwasilisha mada wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji wa Umma (PIC) juu ya uwekezaji katika mashirika ya Umaa.
  Waheshimiwa Wabunge ambao ni Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji wa Umma (PIC) wakifuatilia mafunzo ya kuwajengea uwezo juu ya uwekezaji katika mashirika ya Umma.
  Msajili wa Hazina Dkt Oswald Mashindano akizungumza na Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji wa Umma (PIC) wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo Wabunge hao juu ya uwekezaji katika mashirika ya umaa. Kulia kwake ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe Albert Obama.Mafunzo hayo ya siku mbili yamefanyika Jijini Dar es Salaam.
  (Picha na Ofisi ya Bunge)

  0 0

  Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO.

  MAAFISA Maendeleo ya Jamii nchini wametakiwa kuacha kutumia muda mwingi kukaa maofisini na badala yake kutembelea jamii inayowazunguka ili kubaini fursa zitakazoleta mabadiliko ya haraka katika jamii.

  Kauli hiyo imetolewa jana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Bi. Sihaba Nkinga wakati wa mahojiano Maalum ya kipindi cha TUNATEKELEZA kinachoratibiwa na Idara ya Habari (MAELEZO) na kurushwa hewani na Shirika la Utangazaji Nchini (TBC).

  Bi. Sihaba amesema kuwa Serikali imefanya juhudi kubwa ya kuanzisha Vyuo vya Maendeleo ya Jamii kwa ajili ya kuzalisha maafisa wengi wa kada hiyo watakaotumika kuisaidia Serikali katika kuibua fursa mbalimbali zilizopo kwenye jamii ambazo zitasaidia kuleta maendeleo ya nchi.

  “Afisa Maendeleo ya Jamii ni chachu ya maendeleo ya jamii na Taifa kwa ujumla kwani wao ndio wana jukumu la kubaini fursa na kuwaongoza wananchi katika kutumia fursa hizo,” alisema Bi. Sihaba.

  Ameongeza kuwa jukumu kubwa la maafisa maendeleo ni kuwahamasisha, kuwashirikisha na kuwajengea uwezo wanajamii kutumia rasilimali walizonazo kujiletea maendeleo yatakayopelekea kukua kwa uchumi wa nchi.

  Aidha, Bi. Sihaba amewataka wananchi kuacha dhana potofu ya kuitegemea Serikali na badala yake washirikiane na Serikali kuleta maendeleo kwa kufanya kazi kwa bidii kwa kutumia rasilimali zinazowazunguka katika maeneo wanayoishi.

  Akiongelea kuhusu makazi ya wazee, Bi. Sihaba amesema kuwa kwa sasa kuna vituo 17 nchi nzima vyenye jumla ya wazee 460 wanaopatiwa huduma mbalimbali zikiwemo za malazi, mavazi na chakula.

  “Tunatoa rai kwa vijana kufanya kazi kwa bidii ili waweze kujitegemea na sio kwenda kukaa kwenye nyumba za wazee ili wapatiwe huduma, makazi ya wazee ni kwa ajili ya wazee wasiojiweza tu,” alimalizia Bi. Sihaba.

  0 0

    Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mjane wa Rais wa Kwanza wa Serikali ya Mpinduzi ya Zanzibar, Mama  Fatma Karume wakati alipomtembelea nyumbani kwake  eneo la    Maisara Zanzibar Januari 10, 2017.    (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakizungumza na mjane wa Rais wa kwanza wa serikali ya  Mapinduzi ya Zanzibar, Mama Fatma Karume  (katikati wakati walipomtembelea nyumbani kwake eneo la Maisara mjini Zanzibar Januari 10, 2016.
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akizungumza na mjane wa Rais wa kwanza wa Serikali ya Mapinduzi   ya  Zanzibar, Mama Fatma Karume wakati alipomtembelea nyumbani kwake, eneo la  Maisara, Zanzibar, Januari 10, 2017.
    Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa  akisalimiana na  Mjane wa Rais wa Kwanza wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mama Fatma Karume wakati yeye na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa walipomtembelea nyumbani kwake   ENEO LA  Maisara Zanzibar  Januari 10, 2017.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkewe Mary  wakiongozana na Mjane wa Rais wa Kwanza wa  Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mama Fatma Karume  kutoka  ndani  wakati walipomtembelea  mama huyo nyumbani kwake eneo la Maisara mjini Zanzibara, Januari 10, 2017. 
  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akikata utepe kuashiria ufunguzi wa Tamasha la tatu la Biashara Zanzibar sherehe zilizofanyika leo huko katika viwanja vya Maisara Wilaya ya Mjini Unguja ikiwa ni katika shamra shamra za miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,(kushoto) Waziri wa Biashara,Viwanda na Masoko Mhe Amina Salum Ali.

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akitia saini kitabu cha wageni mara baada ya kufungua Tamasha la tatu la Biashara Zanzibar leo katika viwanja vya Maisara Wilaya ya Mjini Unguja ikiwa ni katika shamra shamra za miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,(kulia) Waziri wa Biashara,Viwanda na Masoko Mhe Amina Salum Ali.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein ( wa pili kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Najma Hussein (katikati) alipotembelea banda la maonesho ya Biashara la Bakhresa Group Companies mara baada ya kufungua Tamasha la tatu la Biashara Zanzibar leo katika viwanja vya Maisara Wilaya ya Mjini Unguja ikiwa ni katika shamra shamra za miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Injinia Hamis Lusanda (kulia) kutoka Vigor Tp Company Ltd wakati alipotembelea mabanda ya maonesho ya Biashara mbali mbali mara baada ya kufungua Tamasha la tatu la Biashara Zanzibar katika viwanja vya Maisara Wilaya ya Mjini Unguja leo ikiwa ni katika shamra shamra za miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akipata maelezo kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tantrade Dar es Salaam Edwin N.Rutageruka wakati alipotembelea mabanda ya maonesho ya Biashara mbali mbali mara baada ya kufungua Tamasha la tatu la Biashara Zanzibar katika viwanja vya Maisara Wilaya ya Mjini Unguja leo ikiwa ni katika shamra shamra za miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akipata maelezo kutoka kwa Ndg.Mohamed Suleiman wa Kiwanda cha Uchapaji cha Serikali wakati alipotembelea mabanda ya maonesho ya Biashara mbali mbali alipofungua Tamasha la tatu la Biashara Zanzibar leo katika viwanja vya Maisara Wilaya ya Mjini Unguja leo ikiwa ni katika shamra shamra za miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa kituo cha tiba,ushauri nasaha na Utafiti wa magonjwa Sugu na Ukimwi Dr.John A.Kidua (kulia) wakati alipotembelea mabanda ya maonesho ya Biashara mbali mbali alipofungua Tamasha la tatu la Biashara Zanzibar katika viwanja vya Maisara Wilaya ya Mjini Unguja leo ikiwa ni katika shamra shamra za miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,(kushoto) Waziri wa Biashara,Viwanda na Masoko Mhe Amina Salum Ali.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) alipokuwa akisalimiana na Wajasiriamali kutoka Mkoa wa Mwanza,ambao wanafanya bishara ya mikoba na dawa asilia wakati alipotembelea mabanda ya maonesho ya Biashara mbali mbali alipofungua Tamasha la tatu la Biashara Zanzibar katika viwanja vya Maisara Wilaya ya Mjini Unguja leo ikiwa ni katika shamra shamra za miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,(kushoto) Waziri wa Biashara,Viwanda na Masoko Mhe, Amina Salum Ali,[Picha na Ikulu.] 10/01/2017.

  0 0


  0 0

   Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angelina Mabula akikagua mfumo wa kielektroniki wa ukadiriaji na ulipaji kodi ya ardhi  Wilayani Kilolo mkoani Iringa mara baada ya kuwasili wilayani humo mapema wiki hii kufuatilia utendaji wa sekta ya ardhi. Dkt. Mabula pia alikagua kumbukumbu za majalada za ulipaji kodi.Anayetoa maelezo ya ufanyaji kazi wa mfumo huo ni Afisa Ardhi wa Halmashairi ya Wilaya hiyo Bw. Elinaza Kiswaga.
  Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angelina Mabula akikagua mfumo wa kielektroniki wa ukadiriaji na ulipaji kodi ya ardhi  Wilayani Kilolo mkoani Iringa mara baada ya kuwasili wilayani humo mapema wiki hii kufuatilia utendaji wa sekta ya ardhi. Dkt. Mabula pia alikagua kumbukumbu za majalada za ulipaji kodi.Anayetoa maelezo ya ufanyaji kazi wa mfumo huo ni Afisa Ardhi wa Halmashairi ya Wilaya hiyo Bw. Elinaza Kiswaga.

  0 0

  Na George Binagi @BMG
  Jimmy Gospo (pichani) ni mwanamziki mpya kwenye muziki wa injili nchini Tanzania. Kabla ya mwaka 2014 alikuwa akifanya muziki wa Bongo Fleva, akiwakilisha mkoa wa Geita na Kanda ya Ziwa kwa ujumla.

  Baada ya mwaka 2014, Jimmy Gospo aliamua kugeuza uelekeo na kuanza kuimba nyimbo za injili kwenye matamasha mbalimbali ya injili hususani Kanda ya Ziwa. Baada ya hapo alianza kurekodi albamu yake ambayo hadi sasa jina liko kampuni.

  Mwaka huu 2017 ameanza kuachia rasmi baadhi ya nyimbo zilizo kwenye albamu hiyo. Ameanza na wimbo uitwao "Nakujua Bwana" ambao hakika ni wimbo bora kusikiliza na hata mafundisho yake.

  "Ni nyimbo nzuri kwa watu wengi hasa wale ambao tunatamani kuisikia faraja ya Bwana ikitenda na sisi. Niwakaribisheni watanzania wote tuisikilize Ninakujua Bwana, ni nyimbo nzuri na natumaini utaifurahia na kuipenda". Amesisitiza Jimmy.
  Mwimbaji wa muziki wa injili, Jimmy Gospo (kulia), akizungumza na George Binagi-GB Pazzo wa BMG (kushoto), kuhusiana na ujio wake kwenye muziki huo, baada ya kuachana na muziki wa kidunia.

  Sikiliza Mahojiano Hapa kusikiliza mahojiano.

  0 0

  Na George Binagi-GB Pazzo
  Taasisi ya lugha ya International Language Traing Centre iliyopo Isamilo Jijini Mwanza, imeiomba serikali kuzisaidia taasisi binafsi za kelimu nchini ili kutimiza vyema wajibu wake.

  Mkurugenzi wa taasisi hiyo, Mwalimu Charles Mombeki (pichani), ameyasema hayo wakati akizungumza na Lake Fm ya Mwanza na kuomgeza kwamba ikiwa serikali itafanya hiyo, itazisaidia taasisi hizo kutekeleza vyema wajibu wa kutoa elimu bora kwa wananchi.

  Amesema si vyema serikali kuzifungia taasisi binafsi za kielimu ikiwemo shule na vyuo pindi zinapokabiriwa na changamoto za kielimu badala yake inaweza kuzisaidia katika kuondokana na changamoto hizo.

  Taasisi ya International Language Training Centre inajihusisha na uendelezaji wa lugha mbalimbali ikiwemo lugha za asili, Kiswahili, kiingereza, kifaransa na nyinginezo.
  Bonyeza hapa kusoma zaidi

  0 0


  Nteghenjwa Hosseah, Arusha 

  Serikali Mkoani Arusha imesema busara ilipaswa kutumika zaidi katika Utekelezaji wa Agizo la Waziri Mkuu Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa alilotoa wakati wa ziara yake Wilayani Karatu katika Bonde la Eyasi kuhusu kusogezwa kwa Mashine za kuvuta maji Umbali wa Mita 500 kutoka chanzo cha Maji. 

  Katika Agizo lake Mhe. Waziri Mkuu aliagiza kusogezwa kwa mashine za za kuvuta maji kutoka chanzo cha maji cha bonde la Eyasi ambapo akati mchakato wa utekelezaji ukiendelea baadhi ya wakazi wa eneo hilo walizichoma moto mashine hizo ambazo kwa wakati huo zilikuwa zimesogezwa umbali wa mita 60 ambazo zinaruhusiwa kisheria. 

  Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo kiwa katika ziara ya Kikazi Wilayani Karatu amesema kutokana na umuhimu wa bonde la Eyasi katika uzalishaji wa Chakula haikuwa busara kwa wananchikuchoma mashine hizo bila kujali mazao ambayo tayari yameshaoteshwa katika eneo hilo na gharama zilizotumika kununua mashine hizo. 

  Aliongeza kuwa wananchi hao walienda mbali zaidi kwa kujichukulia sheria mikononi na kuharibu mali mbalimbali ikiwemo nyumba za wamiliki wa mashine hizo hali iliyopeleka kuleta hofu, usumbufu na sintofahamu kwa wananchi wa maeneo hayo. 

  “Vyombo vya ulizni na usalama vupo kwanini wananchi hawa wasiende kuripoti tatizo hilo kwenye vyombo vinavyohusika na badala yake wanaamua kujichukulia sheria Mkononi, Kisheria hairuhusiwi kwa mtu yeyeote kuharibu mali ya mwananchi ilikua ni lazima tuwachukulie hatua wote waliofaya uharibifu ule” Alisema Gambo. 

  Mhe. Gambo aliongeza kuwa haikuwa rahisi kwa wananchi wa Mang’ola kuamua kufanya zoezi lile pekeyao inaonekana kuna viongozi wa Kisiasa ambao wako nyuma ya vurugu zile na sisi kama Serikali tunaamini jukumu la kiongozi ni kuleta Amani na sio uvunjifu wa Amani na ukienda kinyume sheria inafuata mkondo wake. 

  “Hivyo katika kudhibiti vurugu zile wananchi wote na viongozi wao waliohusika kwa namna moja ama nyingine kufanya uharibifu wa mashine na mali za wananchi tuliwakamata na kuwapeleka Mahakama ili iwe fundisho katika maeneo mengine” Alisem Gambo. 

  Kwa kuwa sasa wahusika wamekwisha tambua makosa yao tunaweza kukaa pamoja na kuangalia namna gani bora ya kutumia maji ya bodne hili bila kusababisha vurugu za aina yeyote ili kila mtuamiji aweze kunufaika na maji ya bonde hilo. 

  Bonde hilo linatumiwa na wananchi zaidi ya elf 20 wanaojishughulisha na shughuli za Kilimo cha mazao mbalimbali kwa njia ya umwagiliaji hutegemea maji yanayotoka katika Bonde la Eyasi . 
  Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo akizungumza na walimu wa Wilaya ya Karatu wakati wa ziara yake ya Kikazi Wilayani humo.
  Katika Kikao kingine Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo(aliyesimama mbele) akizungumza na Wazee wa Karatu pamoja na Viongozi wa Dini.
  Mtaalamu wa Halmashauri ya Karatu(kwanza kulia) akiwaandikisha Wananchi wa Kijiji cha Oldeani waliojiunga na Mfuko wa afya ya Jamii wakati wa Mkutano wa hadhara na Mkuu wa Mkoa wa Arusha.
  Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo(kwanza kulia) akichangia Fedha kwa ajili ya wazee 10 kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii.
  Kutoka kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Karatu Theresia Mahongo akifuatiwa na Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe. Mrisho Gambo wakati wa kikao cha viongozi wa dini pamoja na wazee wa Karatu.

  0 0

  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa Mhandisi Lili-Ang kutoka kampuni ya Beijing Construction Engineering Group (BCEG) inayakarabati na kujenga uwanja wa ndege wa Mwanza.
  Mhandisi Mshauri anayesimamia ukarabati na ujenzi wa uwanja wa ndege wa Mwanza akimuonesha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa Mnara wa jengo la kuongozea ndege alipokagua ujenzi wa uwanja huo.
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa viongozi wa uwanja wa ndege wa Mwanza namna ya kushirikiana na Mkandarasi Beijing Construction Engineering Group (BCEG) anayekarabati na kujenga uwanja huo.
  Muonekano wa jengo jipya la kuongozea ndege linalojengwa na kampuni ya Beijing Construction Engineering Group (BCEG) katika uwanja wa ndege wa Mwanza.

  …………

  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amemtaka Mkandarasi anayejenga na kukarabati uwanja wa ndege wa Mwanza Beijing Construction Engineering Group (BCEG), kuhakikisha ujenzi huo unakamilika ifikapo Novemba mwaka huu.

  Akizungumza mara baada ya kukagua ujenzi wa mnara wa kuongozea ndege, jengo la kuhifadhia mizigo, eneo la kuegeshea ndege na jengo la umeme litakalotoa huduma katika uwanja huo, Profesa Mbarawa amesema tayari Serikali imeshamlipa mkandarasi huyo kiasi cha shilingi bilioni saba kwa ajili ya ujenzi huo.

  “Sisi tumeshamlipa pesa yake yote na hivyo tunachotaka kwake ni kukakamilisha kazi yetu kwa wakati ili kuupa hadhi inayostahili uwanja wa ndege wa Mwanza amboa ni kiungo muhimu katika kanda ya Ziwa”, Amesema Profesa Mbarawa.

  Prof. Mbarawa amemuagiza Meneja wa uwanja wa ndege wa Mwanza Bi .Easter Madale kuhakikisha vikwazo vyote vinavyomkabili mkandarasi vinaondolewa ili kumuwezesha kufanya kazi kubwa kabla ya kipindi cha mvua za masika zinazotarajiwa kuanza mwezi machi.

  Kwa upande wake Mhandisi Lili Ang aneyesimamia ujenzi huo kutoka kampuni ya BCEG amemhakikishia Prof. Mbarawa kuwa baada ya kupokea malipo wamejipanga kukamilisha kazi hiyo kwa wakati na viwango ili waweze kupata fursa nyingine za ujenzi hapa nchini.

  Naye Meneja wa Uwanja wa ndege wa Mwanza Bi .Easter Madale ameyataka mashirika ya ndege kuongeza safari za ndege kwenye uwanja wa Mwanza kwa kuwa sasa utakuwa na hadhi ya kimataifa na kusisitiza umuhimu wa wawekezaji wa hoteli, vituo vya mafuta na maduka makubwa kuwekeza karibu na uwanja huo ambao ndio lango la uchumi wa kanda ya ziwa.

  Katika hatua nyingine Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano ameelekea mkoani Simiyu kuanza ziara ya siku mbili mkoani humo amabapo pamoja na mambo mengine anatarajiwa kushiriki katika ufunguzi wa barabara ya Bariadi- Lamadi iliyojengwa kwa kiwango cha lami.

  Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawssiliano

  0 0

  Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Prof. Faustin Kamuzora akisalimiana na baadhi ya Wafanyakazi wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) mara baada ya kutemebelea Ofisi za Taasisi hiyo zilizopo Mikocheni jijini Dar es Salaam. NEMC ni Taasisi iliyopo chini ya Ofisi ya Makamu wa Rais.
  Katibu Mkuu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Prof. Faustin Kamuzora (kulia) akiongea na Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira Bw. Bonaventure Baya (Kushoto) mara baada ya kuetembelea Ofisi za Baraza hilo zilizopo Mikocheni Jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha ni sehemu ya wajumbe wa Menejimenti katika Ofisi hiyo.
  Katibu Mkuu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Prof. Faustin Kamuzora (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Menejimenti ya Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC). Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira Bw. Bonaventure Baya na Bi. Magdalena Mtenga Mkurugenzi Msaidizi Ofisi ya Makamu wa Rais.

  Picha zote na SIGLINDA CHIPUNGAUPI

  0 0

   Mfanyabiashara maarufu, Mustafa Jaffar Sabodo
   Baba wa Taifa, Hayati Julius Kambarage Nyerere
  Aliyekuwa Kiongozi wa Taifa la Iran, Ayatolah Khomein 


  HAKIKA ukitaja jina la Mustafa Jaffer Sabodo, siyo geni masikioni mwa Watazania wengi.


  Hii ni kutokana na mchango wake kwa jamii katika kuliondoa taifa kutoka sehemu moja ya chini kwenda juu, yaani maendeleo.


  Sabodo mfanyabiashara maarufu ambaye ni Mtanzania mwenye asili ya Asia amekuwa akitoa mchango kwa maendeleo ya Taifa katika nyanja mbalimbali kuanzia za uchumi, siasa, elimu, afya na maji.


  Mfanyabiashara huyo ambaye ni mzaliwa wa mkoani Lindi takriban miaka 73 iliyopita amejitolea kujenga shule mbalimbali nchini, hospitali, visima vya maji hata kufadhili shughuli za kisiasa na kiuchumi.


  Michango yake hiyo kwa jamii ya Watanzania, imefanya jina lake kuandikwa katika mioyo ya wananchi wengi kwani alidhirisha tabia yake isiyojificha ya uzalendo kwa Taifa lake Tanzania.


  Sabodo anatajwa kuwahi kuvifadhili vyama vya siasa vya CCM na Chadema kwa nyakati tofauti.


  Pia anatajwa kwamba alikuwa rafiki wa karibu wa Mwalimu Julius Nyerere na wanasiasa mbalimbali nchini hata kuwahi kutumwa kwenda nchini Iran kukutana na kuomba mafuta kwa aliyekuwa kiongozi wa taifa hilo la Kiislamu, Ayatolah Khomein katika miaka ya 1970 baada ya taifa kukumbwa na uhaba wa mafuta uliochagizwa na sababu mbalimbali ikiwamo ukosefu wa fedha za kigeni.


  Hali hiyo ilitokea kipindi hicho wakati dunia ilikuwa bado ikishuhudia mgawanyiko kwa baadhi ya nchi kuegemea Marekani kisiasa na kimfumo, nyingine zikifuata mfumo wa iliyokuwa Muungano wa nchi za Kisovieti za Urusi (USSR).


  Si hivyo tu kwa kusoma alama za nyakati, baadhi ya nchi zilikaa kando na utengano huo na kuanzisha Jumuia ya Nchi Zisizofungamana na Upande Wowote.


  Miungoni mwa mataifa yaliyofuata siasa za kutofungamana na upande wowote, Tanzania wakati huo chini ya uongozi wa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere ilikuwa mojawapo.


  Tofauti hizo za kisiasa hata kidini kati ya mataifa zilisababisha athari zilizozaa tofauti ya hali hasa kiuchumi na kisiasa hata baadhi ya nchi kuingia kwenye mahangaiko ikiwamo Tanzania iliyokumbwa na uhaba wa mafuta ya Petroli na fedha za kigeni.


  Sabodo anasimulia kwamba kufuatia hali hiyo iliyoilazimu Serikali kuzuia magari yake kutembea Jumapili huku Jumamosi yakitembea hadi saa nane mchana, alipata nafasi ya kukutana na Rais Nyerere.


  Anasimulia kwamba katika mazungumzo hayo alimwabia Rais Nyerere haja yake ya kutaka kwenda Iran kuomba mafuta.


  “Nikamwambia wacha niende Iran. Nilifanya hivyo nikiamini Khomein atanisikiliza. Nakumbuka nilikwenda na Chifu Adam Sapi Mkwawa,” anasema.


  Anasimulia: “Mimi ni Khoja, Mwislamu wa dhehebu la Shia na Khomein pia, nilipokutana naye, nikamwambia wanaoteseka Tanzania kwa shida ya mafuta wamo piaWaislamu wa Shia wengi tu.”


  “Nilimwambia Tanzania ni nchi nzuri haina ubaguzi na Rais Nyerere ni mtu mwema, hata Waziri Mkuu wake ni Rashid Kawawa na Waziri wa Madini na Mafuta ni Anoor Kassam, nikamwangukia miguuni nikiliaa kuomba aipe nchi yetu mafuta, akakubali” anakumbuka Sabodo.


  Hata hivyo, anasema licha ya kukubali, Khomein  akasema hawezi kumpa mafuta yeye Sabodo hadi watu wa Serikali ya Tanzania watakapofika Iran kuthibitisha ombi hilo.


  “Nikarudi Tanzania na kumpa taarifa baba wa Taifa naye alimwambia Kawawa na John Malicela ikakubalika tukaenda tena Iran safari hii nikiwa na mawaziri wa Fedha, Cleopa Msuya, Anoor Kassam wa Mafuta na Usafirishaji pia alikuwepo Peter Noni kwa niaba ya Benki Kuu na Adam Sapi Mkwawa,” anasema.


  Sabodo anakumbuka kuwa safari hiyo ilizaa matunda kwani Khomein aliipa Tanzania mafuta yenye thamani ya Dola za Kimarekani 80,000.


  “Nakumbuka hapo urafiki wangu na Nyerere uliniwezesha kuliokoa Taifa kwa kupata mafuta baada ya kunituma kwenda Iran nilipomshauri,” anasema Sabodo ambaye wazazi wake alizaliwa Lindi.


  Anakumbuka kuwa pia katika safari hiyo alimshauri Khomein kufungua ofisi ya Ubalozi wa Iran nchini naye alikubali na alifanya hiyo pia kwa Zambia, Tanzania nayo ikafungua ubalozi Iran.  Don’t forget to read my book; CORRUPTION IS CRUCIFICATION OF TANZANIA, which is in process


  0 0


  Rais Barack Obama ametoa hotuba yake ya mwisho akiwa kama rais wa Marekani, huko Chicago hotuba ambayo ilijaa hisia kali na kupelekea kutokwa na machozi yeye pamoja na baadhi ya watu.
  Rais wa Marekani Barack Obama amewahimiza Wamarekani kuitetea demokrasia, kwenye hotuba yake ya mwisho kama rais wa Marekani mjini Chicago.
  "Kwa kila kipimo, Marekani sasa ni bora zaidi, na ina nguvu zaidi" kuliko ilivyokuwa miaka minane iliyopita alipochukua madaraka, amewaambia maelfu ya wafuasi wake waliokusanyika mjini humo.
  Hata hivyo, "demokrasia inatishiwa kila inapokosa kutiliwa maanani".
  Amewaomba Wamarekani wa kila asili kuangazia mambo kutoka kwa msimamo wa wengine, na kusema kwamba "lazima tuwategee sikio wengine na kusikia".
  Rais Obama ndiye rais wa kwanza nchini Marekani wa asili ya Afrika na alichaguliwa mwaka 2008 akiahidi kurejesha matumaini na kutekeleza mabadiliko.

  Mrithi wake Donald Trump ameahidi kubatilisha baadhi ya sera kuu alizofanikisha Bw Obama, 55.
  Michelle Obama akimliwaza binti yake Milia ambaye alijikuta akitokwa na machozi wakati akisikiliza hotuba ya baba yake Rais Barack Obama
  Makamu wa rais wa Marekani Joe Biden naye alijikuta akishindwa kujizuia na kutokwa na machozi
   Rais wa Marekani, Barack Obama akikumbatiana na Makamu wa rais wa Marekani Joe Biden baada ya kumaliza hotuba yake.
  Michelle Obama akimkumbatia mumewe rais Barack Obama baada ya kumaliza hotuba yake. 
  Rais wa Marekani Barack Obama akimkumbatia binti yake Milia baada ya kumaliza hotuba yake.

  0 0

   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Makamu  wa Rais Mstaafu, Dkt.  Mohammed Gharib Bilal  wakati alipomtembelea  nyumbani kwake eneo la Mbweni, Zanzibar Januari 10, 2017.
   Waziri Mkuu, Kassim  Majaliwa na Mkewe Mary  wakisalimiana na Rais Mstaafu wa Zanzibar, Dkt. Salmin  Amour wakati walipomtembelea nyumbani kwake eneo la Kilimani, Zanzibar Januari 10, 2017. 
   Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa (kulia) akizungumza na  Mama Azza Salmin, Mke wa Rais Mstaafu wa Zanzibar, Dkt. Salmin Amour wakati yeye na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa walipoitembelea familia hiyo eneo la Kilimani Zanzibar Januari  10, 2017.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akizungumza na  Rais Mstaafu wa Zanzibar, Dkt. Salmin Amour wakati alipomtembelea nyumbani kwake eneo la Kilimani, Zanzibar Januari 10, 2017.
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkewe Mary (kulia) wakizungumza na watoto wa Rais Mstaafu wa Zanzibar, Dkt Salmin Amour wakati walipoitembelea familia ya Rais huyo eneo la  Kilimani mjini Zanzibar, Januari 10, 2017.
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Rais Mstaafu wa Zanzibar, Dkt. Salmin  Amour wakati alipomtembelea nyumbani kwake eneo la Kilimani, Zanzibar Januari 10, 2017.
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akizungumza na  Rais Mstaafu wa Zanzibar, Dkt. Salmin Amour wakati alipomtembelea nyumbani kwake eneo la Kilimani, Zanzibar Januari 10, 2017.
   Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary  Majaliwa  akizungumza na  wake za  Makamu wa Rais Mstaafu, Dkt. Mohammed Gharib  Bilal, Zakia  (kushoto na Asha (katikati)  wakati yeye na  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa walipoitembelea familia ya  Dkt. Bilal , eneo la Mbweni Zanzibar, Januari 10, 2017.
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  na mkewe Mary  (watatu kushoto)  wakizungumza na Makamu wa Rais Mstafu, Dkt. Mohammed Gharib Bilal  na wake zake, Mama Zakia Biala (kushoto) na  Mama  Asha Bilal wakati walipowatembelea  nyumbani kwao eneo la  Mbweni, Zanzibar Januari 10, 2017.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  na mkewe Mary  (wapili kulia)  wakiagana  na Makamu wa Rais Mstaafu, Dkt. Mohammed Gharib Bilal  na wake zake, Mama Zakia Biala (wapili kushoto) na  Asha Bilal  (watatu kulia) wakati walipowatembelea  nyumbani kwao eneo la  Mbweni, Zanzibar Januari 10, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

  Uoto wa asili wa aina mbalimbali unavyoonekana wakati unapoanza safari ya kuelekea kituo cha Kibo ukitokea kituo cha Horombo.
  Mawe yenye michoro mithili ya mistari ya Pundamilia yanaonekana katika eneo lijulikanalo kama Zebra Rocks.
  Kwa mbali ni muonekano wa vibanda viwili maalumu kwa ajili ya kujisaidia ambavyo viko njiani wakati unaelekea Kibo Hut ,eneo hili linajulikana kama Last woter Point ni eneo la mwisho linaloonekana kuwa na maji.
  Ndege wakubwa aina ya Kunguru mwenye baka jeupe shingoni wanaonekana katika maeneo haya wakisubiri mabaki ya chakula kutoka kwa wageni wanaopanda Mlima Kilimanjaro.
  Maeneo mengine yanaonekana kuwa na mabonde makubwa huku ukungu ukifunika uoto wa asili katika maeneo hayo.
  Uoto wa asili hupotea kabisa na kubaki nyasi fupi hasa maeneo ambayo yamefunikwa na mchanga ,eneo hili ni maarufu kwa jina la Saddle .
  Ukiwa njiani katika eneo hili unapata nafasi ya kupita katikati ya vilele viwili vya mlima Kilimanjaro yaani Kibo na Mawenzi na hiki ni kilele cha Kibo ilipo Uhuru Peak.
  Hii ni sehemu tu ya vilima vilivyo njiani na eneo hili hutumika kwa ajili ya kupata chakula kabla ya kuendelea na safari ya kuelekea Kibo Hut.
  Haya ni maeneo tofauti yanavyoonekana wakati wa safari ya kuelekea Kiboo Hut.
  Ukipata bahati ya kuamka mapema ,hii ndio hali unayokutana nayo pindi uwapo katika safari ya kuelekea Kibo Hut.
  Na huu ndio muonekano wa kituo kimojawapo majira ya asubuhi pindi kunapokuchwa.
  Kwa mbaali taswira ya kilele cha Kibo ndivyo kinaonekana.
  Upande wa pili kilele cha Mawenzi hivi ndivyo huonekana.
  Njiwa pori pia wanaonekana katika maeneo haya.
  Hii ni sehemu ya juu ya mlima ambayo hujulikana kama Jamaica ,sehemu ya mwisho kabla ya kufika Gilmans point.
  Safari inayoendelea ni ya kupita eneo ambalo limezingirwa na barafu kuelekea kituo cha Stella.
  Vilima vya barafu ni sehemu ya maumbile yanaoonekana katika eneo la jirani kabisa na kilele cha Uhuru.
  Maeneo mengine licha ya kuwa juu ,yanaonekana kuwa makavu .
  Na hapa ndio Kilele cha Uhuru ambako safari ya siku nne inakufikisha na kuandika historia kuwa miongoni mwa watu waliowahi kufika eneo la juu kabisa Afrika na la pili Duniani.

  N Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii ,Kanda ya Kaskazini.

  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto)  akisalimiana na Makamo wa Rais wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Korea  KOICA Bw.Wooyong Chung   akiwa na ujumbe aliofuatana nao walipofika Ikulu Mjini  Zanzibar jana
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein (kulia) alipokuwa  akizungumza na  Ujumbe wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Korea  KOICA unaoongozwa na Makamo wa Rais wa Shirika hilo Bw.Wooyong Chung (wa pili kulia) mara  walipofika Ikulu Mjini Zanzibar jana.

older | 1 | .... | 1096 | 1097 | (Page 1098) | 1099 | 1100 | .... | 1898 | newer