Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46317 articles
Browse latest View live

WAREHOUSE GODOWN FOR RENT

$
0
0
Kimara stop over Meter 50 kutoka Morogoro Road Parking ipo kwa magari makubwa .

Mawasiliano 0713 882 800

DC wa Tanganyika,Saleh Mhando akagua shughuli mbalimbali za uvuvi ziwa Tanganyika mkoani Katavi

$
0
0

Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi,Mh.Saleh Mbwana Mhando leo amefanya ziara ya kutembelea na kukagua shughuli mbalimbali za uvuvi wa samaki aina ya Sangara na Dagaa katika mwambao wa ziwa Tanganyika mkoani humo.Dc Mhando amesema kuwa ziara hiyo imelenga kuangalia fursa mbalimbali zilizopo na kuwawezesha wavuvi hao wadogo wadogo.Pichani Dc Mhando (pili kulia) akipata maelezo mafupi kuhusiana na mradi huo wa kukausha dagaa pembezoni mwa ziwa Tanganyika,mkoani Katavi.

Samaki aina Sangala kama aonekanavyo pichani mara baada kuvuliwa kwenye ziwa Tanganyika.
Mmoja wa akina mama wanaojishughulisha na ukaushaji wa dagaa pembezoni mwa ziwa Tanganyika,akimuelezea Dc Mhando changamoto mbalimbali wazipatazo kuhusiana na suala zima la soko na usafirishaji

Let’s nurture a culture to set New Year’s resolutions

$
0
0


By Jumia Travel Tanzania


Are you still wondering why you are not impressed with the achievements attained in the previous year 2016? If the answer is YES, then this article would be of a great importance to you.

Most people don’t understand why it is very difficult to track their personal development due to not having a set of goals. Goals differ according to what one desires to achieve in a certain period of time. Jumia Travel (www.travel.jumia.com) would like to share with you the following tips as we are still at the very beginning of the New Year 2017.

First of all, we must understand that goals can be big or small, long-term or short-term that depends on somebody’s preference. Therefore, it is very important to know the kind of goals you have. For instance, a goal to build a house cannot be achieved with the same strategies and tactics as to buy furniture.

It is suggested that we should not put limit to ourselves towards the goals we set because of how big they are or based on our ability to achieve them. Set a realistic goal that you will be able to achieve in a given period of time.

Usually, human beings are guided by goals which ultimately make life meaningful. Goals may differ from one person to another such as the desire to become a prominent person within the community or to achieve something in a lifetime.

There are a lot of people who want to be renowned journalists or authors in the community but do not show any effort to become ones. For example, a goal to become a well celebrated journalist might be influenced by one you consider your best within the industry. So, have you had a chance to read or research on his or her biography? Know challenges he or she has been through? Those are key questions someone must ask himself/herself before taking a decision.

It is every student’s dream to become top of the class or school after the final exams but how many do really work hard to make that become a reality? Most of them fail to achieve that because they lack effective strategies and tactics. You might find that a student neither attend the classes nor study after class hours but still hopes to pass the exams.

Apart from those examples, there is nothing as challenging as setting and achieving a long-term goal like saving some money for future use. For instance, January is the toughest month to most people because it is the time they have spent much money on holidays, and are required to clear many bills including school fees, house rents, vehicle’s insurance, and road licences to mention a few. But believe it or not people will forget and live normal lives as if nothing has happened, and will keep on lamenting on the same situation during the next occasion.

Those are just a few examples of goals which can be set and achieved. This is the right time to set your own goals. With the New Year still young, you still have enough time to plan and execute as well as do evaluation on the past moves. We know it is a very difficult culture to adapt, especially to most Tanzanians but it is useful once you start to practice and be committed.

Tujenge utamaduni wa kujiwekea malengo kila tunapoingia mwaka mpya

$
0
0


Na Jumia Travel Tanzania

Je, bado unajiuliza ni kwanini mwaka wa 2016 umeisha lakini haujapendezwa na mafanikio uliyoyafikia? Kama ni ndiyo, basi makala haya juu ya kujiwekea malengo itakuwa yenye msaada mkubwa kwako.

Watu wengi bado wanashindwa kuelewa ni kwanini inawawia vigumu kufuatilia hatua za kimaendeleo walizopiga katika maisha yao kutokana na kutojiwekea malengo. Malengo yanatofautiana kulingana na jambo au mambo gani ambayo mtu anatamani kuyatimiza ndani ya kipindi fulani cha muda. Jumia Travel (www.travel.jumia.com) ingependa kukukumbusha haya mapema, kwani bado mwaka 2017 ni mchanga.

Malengo yanaweza kuwa makubwa au madogo, ya muda mrefu au mfupi kutegemea na mtu atakavyojiwekea. Hivyo ni muhimu kutambua kwamba malengo yako ni ya aina gani kwani itakurahisishia namna ya kuyakamilisha. Kwa mfano, lengo la kujenga nyumba ya kuishi haliwezi kufikiwa kwa mbinu au mikakati sawa na kununua samani za ndani.

Hivyo basi katika kujiwekea malengo haitakiwi kujiwekea vikwazo akilini kwamba hauwezi kulifikia lengo fulani kwa sababu ni kubwa, au hauna uwezo wa kulifanikisha. Weka lengo ambalo unaona utaweza kulifikia na kulifanikisha kulingana na uwezo ulionao ndani ya muda uliopo.

Kwa kawaida, maisha ya binadamu yanaongozwa na malengo, hivyo tunaweza kusema kwamba maisha bila ya malengo hayana maana yoyote. Malengo hayo yanaweza kuwa mtu fulani au kupata kitu fulani, inategemea na matamanio ya mtu.

Kuna watu wanatamani kuwa waandishi wazuri wa habari au vitabu na kuwa mfano wa kuigwa lakini hawaonyeshi jitihada zozote za kufikia lengo hilo. Kwa mfano, ili kuwa mwandishi wa habari kwanza kabisa lazima utakuwa umevutiwa na mwandishi mmojawapo katika tasnia hiyo. Je, unafanya jitihada gani za kumfuatilia mtu huyo alipoanza? Changamoto gani alizopitia mpaka akafanikiwa?

Ni ndoto ya kila mwanafunzi kufaulu vizuri shuleni lakini ni wangapi wanafanya bidii ya kufuatilia masomo na kusoma kwa bidii? Wengi wao wanakosa mbinu za kufikia malengo hayo kutokana na kutojiwekea mikakati thabiti, unakuta hahudhurii au kufuatilia vipindi vya darasani wala kujitengea muda wa ziada kujisomea baada ya ule wa darasani.

Hakuna jambo linalowashinda watu wengi kama kujiwekea malengo ya muda mrefu kama vile kutenga fedha kwa ajili ya matumizi ya kitu fulani. Kwa mfano, kipindi hiki cha mwanzo wa mwaka watu wengi wanalalamika kuwa fedha hakuna huku mahitaji yakiwa ni mengi. Kipindi hiki asilimia kubwa watu wanahitajika kulipia pango za nyumba, karo za shule, leseni za vyombo vya moto na kadhalika. Lakini hayo yote yatasahaulika baada ya mwezi huu kupita pasipo kujiaandaa yasijekutokea tena kipindi kijacho.

Hiyo ni mifano tu ya malengo mtu anaweza kujiwekea, na namna ya kuyafanikisha kwa sababu hiki ndicho kipindi sahihi. Ingawa ni utaratibu mgumu kwa watu wengi hususani Watanzania, ila una faida kubwa sana kama ukiuanza na kuuzingatia.

KATIBU WA ARUSHA PRESS CLUB(APC) AMIR MONGI AFUNGA NDOA NA BI MUNIRAH BAWAZIRI

$
0
0

Katibu wa Arusha Press Club Amir Mongi akiwa na mkewe siku ya ndoa yao katika ukumbi wa Mamba Complex Marangu Mkoani Kilimanjaro.
Bi Munira mke halali wa Amir Mongi akiwa na mumewe Amir Mongi siku ya sherehe ya ndoa yao jumamosi katika ukumbi wa Mamba Complex Marangu mkoani Kilimanjaro.
Amir Mongi akimvisha pete mewe Munirah Bawaziri siku ya ndoa yao ,katika sherehe iliyofayika kwenye ukumbi wa Mamba Complex Marangu Kilimanjaro januari 2017.
Katibu wa Arusha Press Club Amir Mongi akivishwa pete na mkewe Munirah Bawaziri katika sherehe ya ndoa yao ,iliyofanyika katika ukumbi nwa Mamba Complex Marangu Mkoani Kilimanjaro.
Amiri Mongi akimkumbatia mkewe Munirah Bawazir .
Maharusi wakiwa wanapata chakula pamoja na waandishi wa habari kuroka Jiji la Arusha.
Sherehe inaendelea.

Baadhi ya waandishi wa habari kutoka Jijini Arusha wakiwa wamesimama na mmoja wao aliyevaa gauni la njano Pamella Mollel akiwa anazungumza kwa niaba yao.

Wakilisakata rumba katika sherehe hiyo pamoja na maharusi .
MC Kiko akiwa anateta jambo na mmoja wa wazee wa upande wa bwana harusi katika sherehe hiyo,ambapo naye alikuwa msema chochote siku hiyo.Picha na Vero Ignatus Blog.
Pongezi mbalimbali zikiendelea kutoka kwa ndugu jamaa na marafiki.picha na vero Ignatus Blog.

Fifa kuongeza nchi zinazocheza Kombe la Dunia hadi 48

$
0
0
Rais wa Fifa Gianni Infantino ameshauri kuongezwa wa timu zinazoshiriki kombe la dunia na kufikia 48 zaidi ya ahadi yake aliyoitoa wakati akiwania nafasi hiyo kuwa atafikisha timu 40.Anashauri kuwa timu 16 kati ya zote zitatolewa katika hatua ya awali kabisa.

Kisha kubaki 32 zitakazoendelea katika makundi baada ya hatua ya mtoano kukamilika.Infantino anasema kuwa mapendekezo hayo yatapelekwa katika bodi ya Fifa Januari.''Haya ni mawazo ya kupata suluhisho la uhahika, tutayajadili mwezi huu na kufahamu nini cha kufanya mwaka 2017,'' alisema Infantino mwenye miaka 46.

Infantino aliingia madarakani kuliongoza shirikisho hilo la Fifa mwezi Februari baada ya kujiuzulu kwa Sepp Blatter.

HAFLA YA UZINDUZI USANIFU WA AWALI MRADI WA BOMBA LA MAFUTA YAFANYIKA UGANDA

$
0
0
 Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospter Muhongo (wa tatu kushoto) na Waziri wa Nishati na Maendeleo ya Madini wa Uganda Mhandisi Irene Muloni (wanne kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa   Hafla ya Uzinduzi wa Usanifu wa Awali wa michoro ya mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi kutoka Uganda Hadi Bandari ya Tanga Tanzania mjini Kampala Uganda.
Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo akisaini kitabu cha Wageni katika Ubalozi wa Tanzania nchini Uganda baada ya kuhudhuria Hafla ya Uzinduzi wa Usanifu wa Awali wa Michoro ya Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi kutoka Uganda hadi Bandari ya Tanga, Tanzania.  Wengine wanaoshuhudia kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Prof. Justin Ntalikwa, Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Mhandisi Kapuulya Musomba na Mtaalam kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Marwa Petro.

Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo tarehe 9/1/2017 aliongoza Ujumbe wa Tanzania jijini Kampala nchini Uganda katika hafla ya Uzinduzi wa Usanifu wa Awali (Front End Engineering Design -FEED) wa mradi wa Bomba la kusafirisha Mafuta Ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga, Tanzania. 

Uzinduzi huo ulifanyika Makao Makuu ya Wizara ya Nishati na Maendeleo ya Madini ya Uganda na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Mawaziri wa nchi zote mbili za Uganda na Tanzania, Makatibu Wakuu wa nchi zote mbili, Wakurugenzi wa mashirika ya mafuta na gesi, Kampuni zilizogundua mafuta nchini Uganda za Total (Ufaransa), CNOOC (China), TULLOW (Uingereza), Kampuni ya Mafuta ya Uganda National Oil Co. (UNOC), Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) na wawakilishi wa vyombo vya habari.

Wakati wa uzinduzi huo ilielezwa   kuwa, FEED ni moja ya hatua muhimu katika kuhakikisha mradi huo unatekelezwa katika viwango vinavyozingatia usalama wa kimazingira na ustawi wa jamii.

Vilevile, ilielezwa kuwa, hatua hiyo itajumuisha pia upatikanaji wa njia ya gharama nafuu ya kupitisha bomba la mafuta ambapo pia Wataalamu wa taaluma mbalimbali watahusika katika kuhakikisha mradi huo unafuata viwango na ubora wa kimataifa.

Pia , imeelezwa  kuwa bomba hilo litakuwa la kwanza kwa urefu duniani kuwa bomba linalopashwa joto muda wote kutokana na asili ya mafuta yanayosafirishwa.

Mradi huo mkubwa utatekelezwa kwa ushirikiano wa Serikali za Uganda na Tanzania na pia utahusisha kampuni za TOTAL, CNOOC na TULLOW.

Waziri Mahiga amuaga Waziri wa Mambo ya Nje wa China Mhe. Wang

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushrikiano wa Afrika Mashariki, Mhe.Balozi Dkt. Augustine Mahiga akijadili jambo na mgeni wake Waziri wa Mambo ya Nje wa China, Mhe. Wang Yi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Nyerere Jijini Dar es Salaam, wakati akijiandaa kuondoka baada ya kumaliza ziara yake ya kikazi nchini. Wa kwanza kulia ni Balozi wa China nchini Tanzania Mhe. Lu Younqing 
Waziri Mahiga akimsikiliza Waziri wa Mambo ya Nje wa China Mhe. Wang Yi 
Waziri Mahiga na Waziri Wang Yi wakifurahia jambo wakati wa mazungumzo 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe.Balozi Dkt. Augustine Mahiga akiagana na Waziri wa Mambo ya Nje wa China Mhe.Wang Yi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Nyerere wakati akiondoka nchini mara baada ya kumaliza ziara yake ya kikazi 
Waziri Mhe. Balozi Dkt. Mahiga Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia Balozi Mbelwa Kairuki (katikati kulia) na Makuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali na Msemaji wa Wizara Bi. Mindi Kasiga wakipunga mikono kumuaga Warizi Mhe. Wang wa China.

Hali ya Upatikanaji wa Dawa nchini ni ya kuridhisha MSD

ADAKWA KWA TUHUMA ZA KUGHUSHI NYARAKA ZA SERIKALI ILI KUTAPELI IDARA YA HABARI MAELEZO

$
0
0


Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo, Dkt. Hassan Abbas (Pichani kati) akizungumza na waandishi wa habari mara baada kukamatwa kwa watu wanaodaiwa kutaka kusajili gazeti kwa nyaraka za kughushi leo jijini Dar es Salaam, Kulia ni Kaimu Msajili wa Idara ya Habari Maelezo, Patrick Chipangula na kushoto ni Afisa Habari wa Idara ya Habari MAELEZO,Lilian Lundo. Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.
watuhumiwa waliotaka kusajili gazeti kwa nyaraka za kugushi wakiwa chini ya ulinzi leo jijini Dar es Salaam.
watuhumiwa waliotaka kusajili gazeti kwa nyaraka za kugushi wakiwa chini ya ulinzi leo jijini Dar es Salaam,tayari kuelekea kituo cha polisi kati.Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.

MPOGOLO AONGOZA MAZISHI YA ALIYEKUWA KATIBU WA CCM WILAYA YA KILINDI LEO JIJINI DAR

$
0
0
Na Bashir Nkoromo

Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rodrick Mpogolo, ameongoza umati wanachama wa CCM na nawananchi kwa jumla, katika mazishi ya aliyekuwa Katibu wa CCM wilaya ya Kilindi mkoani Tanga, Hawa Nangaju, yaliyofanyika leo Januari 10, 2017, Mbagala, Dar es Salaam.

Katika mazishi hayo, walihudhuria pia viongozi kadhaa akiwemo Katibu wa Halmashauri Kuu Taifa(NEC) ya CCM, Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Kanali Mstaafu Ngemela Lubinza na Waziri wa Afya, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu na baadhi ya viongozi kutoka Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba.

Akizungumza kwenye mazishi hayo, Mpogolo alisema, Chama Cha Mapinduzi kimeondokewa na kiongozi ambaye alikuwa mwadilifu, mchapakazi na anayekipenda kwa dhati Chama, hivyo kimebakiwa na majozi makubwa kutokana na kifo cha katibu wake huyo.

"Ni kutokana na Chama kilivyomfahamu na kumwamini Hawa Omari Nangajau, ndiyo sababu sisi viongozi tuliobaki pamoja na wanachama wenzetu wa CCM, tumepokea msiba huu kwa majonzi makubwa, hivyo ili kumuenzi ni sisi kufanyakazi kwa uadilifu, kujituma na kukipenda Chama kama alivyokuwa akifanya", alisema Mpogolo.

Akisoma, wasifu, Mkuu wa Utawala Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, Bakari Khamis Hamadi alisema, Marehemu Hawa Nanganjau aliyezaliwa Novemba 27, 1962 katika Kijiji cha Mkaramo Wilayani Kilwa mkoani Lindi alihitimu elimu yake ya sekondari katika shule ya Sekondari Kibasila, Temeke, Dar es Salaam mwaka 2004.

Khamis alisema, amekuwa akifanya kazi mbalimbali katika CCM tangu mwaka 1981 akiwa katibu wa Tawi na kupita katika nafasi mbalimbali za ukatibu hadi nanafasi yake ya mwisho ya Ukatibu wa CCM wilaya ya Kilindi mkoani Tanga, tangu mwaka 2013 hadi mauti yalipomfika, Januari 8, 2017, kutokana na maradhi ya tumbo.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara Rodrick Mpogolo,amkimfariji mtoto aliyekuwa Katibu wa CCM,Wilaya ya Kilindi mkoa wa Tanga,hawa Omari Nanganjau,Said Mbaraka,Wakati wa masishi ya Katibu huyo,yaliyofanyika leo,Mbagala jijini Dar.Picha na Bashir Nkoromo.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara Rodrick Mpogolo (wapili kushoto), akiwa msibani wakati wa mazishi ya aliyekuwa Katibu wa CCM wilaya ya Kilindi Hawa Omari Nanganjau, yaliyofanyika leo nyumbani kwa marehemu, Mbagala, Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Ngemela Lubinza
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Rodrick Mpogolo akisalimiana na Waziri wa Afya, Jinsia, Wazee na WatotoUmmy Mwalimu, wakati wa mazishi ya aliyekuwa Katibu wa CCM wilaya ya Kilindi Hawa Omari Nanganjau, yaliyofanyika leonyumbani kwa marehemu, Mbagala, Dar es Salaam. 
Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rodrick Mpogolo na Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Kanali Mstaafu Ngemela Lubinza wakiwapa pole waombolezaji, wakati wa mazishi ya aliyekuwa Katibu wa CCM wilaya ya Kilindi Hawa Omari Nanganjau, yaliyofanyika leo nyumbani kwa marehemu, Mbagala, Dar es Salaam.

MHE. KAIRUKI AFANYA MAZUNGUMZO YA KIKAZI NA BALOZI WA USWISI NCHINI TANZANIA

$
0
0
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akipokea kitabu kilichojikita katika Tafiti ya Kazi za Sanaa za Tanzania kutoka kwa Balozi wa Uswisi nchini Tanzania Bi. Florence Tinguely Mattli alipomtembelea  Waziri huyo ofisini kwake leo.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akimsikiliza Balozi wa Uswisi nchini Tanzania Bi. Florence Tinguely Mattli alipomtembelea ofisini kwake mapema leo.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akizungumza na Balozi wa Uswisi nchini Tanzania Bi. Florence Tinguely Mattli alipofanya ziara ya kikazi ofisini kwake leo. Kulia ni Mkuu wa Mahusiano wa ubalozi wa Uswisi nchini Bi. Romana Tadeschi.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akizungumza na Balozi wa Uswisi nchini Tanzania Bi. Florence Tinguely Mattli (hayupo pichani) alipotembelewa na Balozi  huyo ofisini kwake leo.

Siku Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip I. Mpango, alipoagana na aliyekuwa Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika-AfDB, nchini Tanzania, Dkt. Tonia Kandiero

WASTAAFU KANDA YA ZIWA WATAKIWA KUJITOKEZA KUHAKIKIWA

$
0
0
Na Benny Mwaipaja, WFM, Mwanza
Wizara ya Fedha na Mipango yawataka wastaafu wanalipwa na Hazina ambao hawajahakikiwa katika mikoa ambayo zoezi hilo limeshafanyika na wanauwezo wa kufika katika maeneo ambayo zoezi hilo linaendelea , wajitokeze kwa wingi  kwa ajili ya kuhakikiwa.
Wito huo umetolewa mkoani Mwanza na Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali, Msaidizi, Bw. Stanislaus Mpembe wakati wa uzinduzi wa zoezi la Uhakiki wa Wastaafu wanaolipwa na Wizara ya Fedha na Mipango katika Kanda ya Ziwa, mikoa ya Mwanza, Kagera, Mara, Shinyanga, Simiyu na Geita.
Mpembe alisema kuwa zoezi hilo ni muhimu kwa wastaafu na Serikali kwa ujumla kwani limelenga kuiwezesha Wizara ya Fedha na Mipango kuhuisha taarifa za Wastaafu, kupata orodha sahihi ya wastaafu wanaolipwa na Wizara hiyo ili Serikali iweze kuwalipa wale wote wanaostahili.
Alifafanua kuwa suala la uhakiki ni la lazima na kuwaomba wastaafu wajitokeze kwa wingi kwani baada ya zoezi hilo kumalizika nchi nzima wastaafu ambao hawatahakikiwa watafutwa katika mfumo wa malipo.
“Naomba wastaafu wote wajitokeze katika Halmashauri zilizotangazwa, hata wasiokuwa na nyaraka wajitokeze wataelekezwa mahali wanapoweza kupata nyaraka zote muhimu” aliongeza Bw. Mpembe.
 Alisema kuwa wagonjwa na wasiojiweza wametengewa siku ya Ijumaa ambayo ni siku ya mwisho ya uhakiki, ambapo watakuja ndugu au jamaa zao watakaotoa taarifa sehemu walipo hususani waliopo hospitalini na sehemu ambazo zinaweza kufikika kwa karibu na wahakiki ili nao wahakikiwe.
Naye Mstaafu John Msanja, pamoja na kuomba serikali iwafikirie kuwaongezea pensheni ili waweze kukabiliana na hali ngumu ya maisha inayowakabili, aliipongeza Serikali kupitia Wizara ya Fedha na Mipango pamoja na waratibu kwa kuendesha  zoezi hilo kistaarabu pamoja na kutoa kipaumbele kwa wagonjwa  na wasiojiweza ambao waliweza kufika katika eneo hilo kwa lengo la kuhakikiwa.
Alisema kuwa zoezi hilo linaonesha ni namna gani Serikali inawajali wazee waliolitumikia Taifa kwa muda mrefu kwa kuhakikisha ni namna gani wanapata stahili zao kwa wakati.
Zoezi hili lilianza Oktoba, 2016 katika Mkoa wa Pwani na kuendelea katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini, Kanda ya Kati na Kanda ya Kaskazini. Mpaka sasa wastaafu wa mikoa 13 ya Tanzania Bara wameshahakikiwa.
Baada ya uhakiki kumalizika Kanda ya Ziwa, zoezi hili litaendelea katika mikoa ya Kigoma na Tabora.
 Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali, Msaidizi, Bw. Stancilaus Mpembe, akizungumza na waandishi wa habari mkoani Mwanza wakati wa Uzinduzi wa zoezi la Uhakiki wa Wastaafu wanaolipwa na Wizara ya Fedha na Mipango Kanda ya Ziwa.
Baadhi ya wastaafu wakiwa wanahakikiwa na Wakaguzi wa ndani wa Serikali mkoani Mwanza katika uzinduzi wa zoezi la Uhakiki wa Wastaafu wanaolipwa na Hazina, huku wengine (waliosimama kulia) wakiwa katika foleni.
Picha ya pamoja ya Wakaguzi wa Ndani wakiendelea na zoezi la Uhakiki wa Wastaafu Wanaolipwa na Wizara ya Fedha na Mipango mkoani Mwanza, huku baadhi ya wastaafu wakiendelea kusubiri zamju zao katika viti.
Baadhi ya wastaafu wakiwa wamepumzika wakisubiri zamu zao za kuhakikiwa wakati wa zoezi la Uhakiki wa Wastaafu wanaolipwa na Hazina,  utakao dumu hadi mwishoni mwa juma, jijini Mwanza.

IMF Executive Board Completes the Fifth Review Under the Policy Support Instrument for Tanzania

$
0
0
On January 9, 2017, the Executive Board of the International Monetary Fund (IMF) completed the fifth review of Tanzania’s economic performance under the program supported by a three-year Policy Support Instrument (PSI). The Board’s decision was taken on a lapse of time basis.

In completing the review, the Board also granted waivers for the non-observance of the end-June 2016 assessment criteria on the overall fiscal deficit and the non-accumulation of domestic expenditure arrears on the grounds that the slippages were minor. The PSI for Tanzania was approved by the Board on July 16, 2014 (see Press Release No. 14/350).
Tanzania’s macroeconomic performance remains strong. Economic growth was robust during the first half of 2016 and is projected to remain at about 7 percent this fiscal year. Inflation came down below the authorities’ target of 5 percent and is expected to remain close to the target, while the external current account deficit was revised down on account of lower imports of capital goods. Nevertheless, there are risks that could adversely affect economic growth going forward, arising from the currently tight stance of macroeconomic policies, the slow pace of credit growth that may become protracted, slow implementation of public investment, and private sector uncertainty about the government’s new economic strategies.

Program performance was broadly satisfactory and most assessment criteria for June 2016 and all indicative targets for September 2016 were met. While progress in structural reforms identified under the program has been generally slow, the authorities have recently stepped up efforts to advance them. These include measures taken to strengthen public financial and debt management, modernize the monetary policy framework, and improve monitoring of parastatal enterprises. The authorities have committed to further reforms in these areas.

The current tight macroeconomic conditions should be addressed by loosening the short-term policy stance, in line with program targets. After recording a small fiscal surplus in July-September, the government is committed to stepping up budget implementation, particularly in public investment, including by mobilizing external financing. Monetary policy should be eased to address the tight liquidity situation and support credit to the private sector. The Bank of Tanzania’s steps in this regard are appropriate, but will need to be fine-tuned when the planned fiscal spending materializes. The increase in international reserves recorded since the beginning of the fiscal year is a welcome step to gradually rebuild buffers.

The authorities are implementing an ambitious development and reform agenda over the medium term, as described in their recently-released second Five-Year Development Plan. The strong drive against corruption and tax evasion has led to higher fiscal revenues, which, if sustained, will provide a good foundation for the envisaged scaling up of infrastructure investment, starting with the 2016/17 budget. The Plan also envisages a significant structural transformation of the economy by nurturing human development. Full involvement of all stakeholders in policy design and implementation—including importantly the private sector—will be crucial.

VYAMA AU WAGOMBEA WATAKAOKIUKA MAADILI KAMPENI ZA UCHAGUZI MDOGO KUCHUKULIWA HATUA.

$
0
0
Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC), pia na Jaji Mkuu Mstaafu wa Zanzibar Mhe. Hamid Mahamoud Hamid

Na. Aron Msigwa – NEC

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imewataka wagombea na Vyama vya Siasa vinavyoendelea na kampeni za Uchaguzi mdogo wa Ubunge na Madiwani kufanya kampeni za kistaarabu zinazozingatia maadili ya Uchaguzi ya mwaka 2015 na kwamba Chama au mgombea atakayekiuka maadili hayo atachukuliwa hatua.

Kauli hiyo imetolewa na Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Mkuu (Mst. Znz.) Hamid M. Hamid zikiwa zimebaki siku chache kabla ya kufanyika kwa Uchaguzi huo Januari 22, 2017 kufuatia baadhi Vyama na Wagombea kuanza kukiuka Maadili na taratibu za Kampeni  kwa kutoa matamko yaliyo nje ya Sera za Vyama vyao.

Amesema kipengele cha 2.1 (m) cha Maadili ya Uchaguzi kinachoeleza  Wajibu wa Vyama vya Siasa na Wagombea katika kuendesha shughuli za Siasa wakati wa Kampeni kinavitaka Vyama vya Siasa, Wagombea na Wafuasi wao kufanya kampeni kwa kuzingatia misingi inayolenga kutangaza Sera ambazo hazijengi chuki, mafarakano na kuleta mgawanyiko katika jamii.

“Katika Kampeni zinazoendelea, baadhi ya vyama vya Siasa vimeanza kukiuka taratibu za kampeni na maadili na kutumia fursa ya kampeni vibaya, vinawasema viongozi wa Kitaifa , kutoa matamko ambayo kihalisia siyo ya kumnadi mgombea na kufanya kampeni zisizo za kistaarabu,” Amesema Jaji Hamid.

Amesema kuwa vyama Vyama au Wagombea watakaoendelea kukiuka Maadili ya Uchaguzi katika Mikutano ya kampeni inayoendelea katika maeneo mbalimbali ya Tanzania pamoja na Jimbo la Dimani, Zanzibar watachukuliwa hatua.

Jaji Hamid ameeleza kuwa kipengele cha 5.3 cha Maadili ya Uchaguzi kinaeleza wazi kuwa Chama au Mgombea atakayekiuka Maadili ya uchaguzi katika jimbo au Kata yenye uchaguzi mdogo atafikishwa katika kamati ya maadili ya ngazi husika na kuchukuliwa hatua stahiki.

Aidha, kipengele cha 5.10 cha Maadili ya Uchaguzi yaliyokubaliwa na Vyama vyote vya Siasa kinafafanua kuwa Kamati za Maadili ya uchaguzi ngazi ya Taifa, Jimbo na Kata katika kushughulikia malalamiko na kutoa adhabu zinaweza kuchukua hatua mbalimbali ikiwa ni pamoja na kukitaka Chama au Mgombea kusahihisha kosa au makosa au kuomba msamaha hadharani.

Hatua nyingine ni Kukisimamisha Chama au Mgombea kuendelea kufanya kampeni za Uchaguzi, kutoza Faini, Kutangaza jina la Chama au Mgombea aliyekiuka Maadili kwa kueleza kosa au Makosa yake kupitia redio, televisheni, magazeti na njia nyingine za mawasiliano.

RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA PROF. IBRAHIM GAMBARI MJUMBE MAALUM WA RAIS WA NIGERIA, CHATO MKOANI GEITA.

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifanya mazungumzo na Profesa Ibrahim Gambari ambaye ni Mjumbe maalum wa Rais wa Nigeria Chato mkoani Geita.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea barua yenye ujumbe maalum kutoka kwa Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari uliowasilishwa na Profesa Ibrahim Gambari ambaye ni Mjumbe maalum wa Rais huyo wa Nigeria, Chato mkoani Geita.
 Profesa Ibrahim Gambari ambaye ni Mjumbe maalum wa Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari  akimshukuru Rais Dkt. John Magufuli mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Chato mkoani Geita.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza mgeni wake Profesa Ibrahim Gambari ambaye ni Mjumbe maalum wa Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Chato mkoani Geita.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na mgeni wake Profesa Ibrahim Gambari ambaye ni Mjumbe maalum wa Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Chato mkoani Geita. PICHA NA IKULU

Gambo awasihi Wizara ya Kilimo kusitisha kutoa vibali vya Kusafirisha Mahindi Nje ya Nchi

$
0
0
Nteghenjwa Hosseah, Arusha

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo ameitaka Wizara ya Mifugo, Chakula na Ushirika kuacha kutoa vibali vya kusafirisha mahindi nje ya nchi kwa wafanyabiashara wa hapa nchini kwani Serikali Mkoani Arusha ilishapiga marufuku usafirishwaji wa mahindi hayo nje ili kulinda viwanda vya hapa nchini.

Mhe. Gambo alisema hayo jana baada ya kutembelea maghala matatu ya Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula{NFRA} Kanda ya Arusha kujionea hali halisi ya uhifadhi wa mahindi katika maghala hayo na kuskiliza changamoto zake na kukuta tani 6,620 za mahindi zilizoko kwa sasa.

Alisema serikali Mkoani Arusha ilishapiga marufuku uuzwaji wa mahindi nje ya nchi lakini kuna baadhi ya wafanyabiashara wamekamatwa na vyombo vya ulizni na usalama wakiwa na vibali kutoka Wizarani vinavyowaruhusu kupeleka mahindi nchi jirani ya Kenya hali inayowafanya watendaji wa serikali kushindwa kufanya kazi kutokana na mkanganyiko huo.

Mkuu huyo alisema uamuzi wa kupiga marufuku uuzwaji mahindi nje ulitolewa na serikali kuu na Mkoa ulisimamia hilo kwa lengo la kuvilinda viwanda vya hapa nchini kwa uzalishaji wa bidhaa hivyo na kunufaika na unga na pumba za mahindi tofauti na ilivyo sasa.

Alisema kutokana na mkanganyiko huo aliwaomba watendaji wa Wizara kuacha kutoa vibali kwa wafanyabiashara kuuza mahindi nje ili kuwasaidia wenye viwanda vya nafaka kuuza unga na pumba nje wenye kiwango ili nao waweze kupata faida na nchi iweze kupata faida zaidi.

Mhe. Gambo alisema mbali ya hilo pia serikali Mkoani Arusha imefanikiwa kuziba njia zote za panya zilizokuwa zikitumika na wafanyabiashara kutorosha mahindi kwenda nchi jirani ya Kenya na kusema kuwa hilo nalo linapaswa kuungwa mkono na Wizara ili amri hiyo iweze kutekelezeka.

‘’Vibali vya Wizara kwa wafanyabiashara kuuza mahindi nje vinatuchanganya sana na vinapingana na amri yetu na nchi kwa ujumla na kutokana na hali hiyo tunaiomba wizara iache kufanya hivyo kwa maslahi ya nchi na wafanyabishara wa ndani ili waweze kuuza unga badala ya mahindi kwani watanufaika zaidi’’alisema Gambo

Naye Meneja wa NFRA Kanda ya Arusha, Abdillah Nyangasa alikitoa taarifa kwa Mkuu wa Mkoa, alisema kuwa zoezi la ununuzi lililoanza agosti 25 mwaka jana na kumalizika novemba 30 mwaka huo huo malengo yalikuwa kununuwa mahindi tani 15,000 lakini walifanikiwa kununuwa mahindi tani 5,111 tu na hiyo ni kutokana na ufinyu wa bajeti.

Nyangasa alisema changamoto iliyowakabili katika kipindi cha ununuzi kipindi hicho ilikuwa uzalishaji mdogo wa nafaka hususani mahindi ambo haukwenda sambasamba na mahitaji au matumizi ya kukidhi nchi na hali hiyo ilichangia sana bei ya mahindi au unga kupanda kwa kasi kubwa kwenye soko lake karibu nchi zima.

Alisema changamoto nyingine ni udhibiti mdogo wa soko la mahindi kwenye maeneo ya mipakani kwani kumekuwa na njia nyingi zizizo rasmi maarufu kwa njia ya panya kwa mikoa ya Arusha na Kilimanjaro na mahindi mengi yamevuka kwenda nchini Kenya kitu ambacho yangesaidia sana uhaba mkubwa wa chakula ulioko sasa endapo yangedhibitiwa.

Meneja huyo alisema kutokana na ununuzi mdogo wa mahindi Kanda ya Arusha NFRA makao makuu inaanga lia uwezekano wa kuongeza akiba hiyo kwa kuhamisha sehemu ya akiba yake kutoka katika kanda zake za Nyanda za Juu Kusini ambazo ununuzi wake ulikuwa wa kuridhika kidogo.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Mashaka Gambo (Pili kushoto) akiwasili katika Ofisi za Wakala wa Taifa wa Uhifadhi wa Chakula Kanda ya Kaskazini zilizoko Mkoani Arusha kuangalia na kukagua hali ya uhifadhi wa Chakula.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo(kwanza kushoto) pamoja na Meneja wa NFRA Kanda ya Kaskazini Ndg.Abdillah Nyangasa wakitembelea maghala ya kuhifadhia Chakula wakati wa ziara yake katika Ofisi hizo.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo(kwanza kulia) akikagua taarifa za mazao yaliyohifadhiwa katika Magahala ya NFRA wakati wa ziara yake ya kukagua hali ya Uhifadhi wa Chakula.
Kutoka kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha Ndg. Richard Kwitega akifuatiwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo na Meneja wa NFRA Ndg. Abdillah Nyangasa wakati wa kikao na wafanyakazi wa NFRA Kanda ya Kasikazini.

FMF YAWAKUMBUKA WANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI MSINUNE, BAGAMOYO MKOANI PWANI

$
0
0
Taasisi ya Flaviana Matata Foundation (FMF) leo imezindua rasmi msimu wa muhula/mwaka mpya wa masomo 2017 #BackToSchool2017 kwa kutoa msaada wa vifaa vya kujifunzia kwa wanafunzi 317 wanaosoma Shule ya Msingi Msinune iliyopo kata ya Kiwangwa wilayani Bagamoyo mkoani Pwani. Msaada huo umekabidhiwa moja kwa moja kwa wanafunzi ikiwa ni moja ya juhudi za Taasisi kuinua kiwango cha elimu kwa kuwahamasisha wanafunzi mashuleni.  Katika harakati zake za kuinua kiwango cha elimu shuleni Msinune na kurahisisha upatikanaji wake, pamoja na kugawa vifaa vya kujifunzia na kufundishia kwa wanafunzi na walimu; Taasisi ya Flaviana Matata imefanikiwa kujenga na kukarabati madarasa, kujenga vyoo kwa ajili ya walimu na wanafunzi na kutoa msaada wa madawati. 

Akizungumza wakati wa kupokea msaada Kaimu Mkuu wa Shule ya Msinune alisema kwamba tangu taasisi ya Flaviana Matata ianze kutoa misaada shuleni hapo kumekuwa na upungufu wa utoro kwa wanafunzi na pia idadi ya wanafunzi waliomaliza darasa saba imeongezeka kutoka 18 waliomaliza mwaka 2015 mpaka 46 kwa mwaka 2016. Pia ufaulu wa wanafunzi umeongezeka kwa asilimia 2.64; mwaka 2015 wanafunzi 5 walichaguliwa kujiunga na masomo ya sekondari na kwa 2016 wanafunzi 14 walichaguliwa.  Akielezea changamoto zinazowakabili, Kaimu Mkuu wa Shule amezielezea kwamba ni pamoja na Elimu kukosa kipaumbele wilayani Bagamoyo, upungufu wa vyumba vya madarasa, uhaba wa walimu (shule ina walimu 6), ukosefu wa nyumba za walimu na mila na desturi za wakazi wa eneo hilo ambao wanafanya jitihada kuzuia watoto wa kike wasiendelee na elimu ya sekondari ili waweze kuolewa, hii hupelekea wazazi wa watoto wa kike kuwalazimisha wajifelishe wakati wa mitihani ya kumaliza darasa la saba. 
 Akiongea wakati wa kukabidhi misaada hiyo, mwanzilishi wa Taasisi na Mlezi wa shule ya Msinune Flaviana Matata alisema kwamba Taasisi yake itaendelea kuisimamia na kujitahidi kuiboresha shule hiyo kwa kumalizia kujenga madarasa yaliyobaki na kuangalia namna ya kuwashirikisha wadau wengine wa elimu na serikali kushughulikia nyumba za walimu.

WATUHUMIWA WA UNYANYASAJI NA SHAMBULIO ZA KUDHURU MWILI WAKAMATWA

Viewing all 46317 articles
Browse latest View live




Latest Images