Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live

UJENZI WA BARARABARA ZA JUU (FLYOVERS) WAFIKIA ASILIMIA 19

$
0
0
 Mhandisi Mkazi kutoka Kampuni ya ujenzi ya Sumitomo Mitsui, Bw.Kiyokazu Tsuji (wa kwanza kulia) akionesha hatua zilizofikiwa katika mradi wa ujenzi wa Barabara za juu (Flyovers) eneo la Tazara Jijini Dar es Salaam. Pembeni yake ni kiongozi wa timu ya ukaguzi wa Miradi kutoka Tume ya Mipango, Mhandisi Omari Athuman.
  Kiongozi wa timu ya ukaguzi wa Miradi kutoka Tume ya Mipango, Mhandisi Omari Athuman (mwenye shati ya mikono mifupi) akitoa ushauri kwa wahandari wanaotekeleza mradi wa ujenzi wa bararabara za juu jijini Dar es Salaam.
  Shughuli za ujenzi wa barabara za juu (Flyovers) zikiendelea katika eneo la Tazara jijini Dar es Salaam.
    Mhandisi Omari Athuman (kulia) akiongea na Ofisa Mshauri wa masuala ya usalama kazini,  Bw. Richard Barwan wakati wa ziara ya Timu ya Mipango katika mradi wa ujenzi wa Barabara za juu eneo la Tazara jijini Dar es Salaam.  
  Shughuli za ujenzi wa barabara za juu (Flyovers) zikiendelea katika eneo la Tazara jijini Dar es Salaam.

Na Adili Mhina, Dar.

Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Tume ya Mipango imefanya ziara katika Mradi wa ujenzi wa Barabara za juu (Flyovers) unaoendelea katika makutano ya barabara za Nyerere/Mandela Jijini Dar es salaam na kuelezwa kuwa utekelezaji wake umefikia asilimia 19.2.

Ziara hiyo iliyofanyika hivi karibuni kwa lengo la kuangalia maendeleo ya mradi huo ilitoa fursa kwa Bw. Kiyokazu Tsuji, Mhandisi Mkazi kutoka Kampuni ya ujenzi ya Sumitomo Mitsui ambayo ndiyo inayotekeleza ujenzi huo kueleza maendeleo ya ujenzi kwa wataalam kutoka Tume ya Mipango. 

Mhandisi huyo alieleza kuwa malengo ya awali yalielekeza kuwa hadi kufikia mwishoni mwa mwezi Novemba 2016, utekelezaji uwe umefikia asilimia 21.2 lakini lengo hilo halikufikiwa kutokana na moja ya mashine kupata hitilafu na kulazimika kuagiza wataalam kutoka nje ya nchi kuja kuifanyia matengenezo. 

Hata hivyo Mkandarasi huyo alieleza kuwa tayari wamejipanga vizuri katika kuhakikisha wanafidia muda uliopotea wakati mashine hiyo ilipokuwa haifanyi kazi ili ujenzi wa barabara hizo ukamilike ndani ya muda uliopangwa. 

Nao walaalam kutoka Tume ya Mipango walieleza kuwa Serikali na Wananchi kwa ujumla wanatarajia kuwa ujenzi huo utakamilika kwa muda uliopangwa hivyo Mkandarasi huyo ana wajibu wa kufanya kila linalowezekana ili mradi huo ukamilike kwa wakati. 

Wataalamu hao pia walimshauri Mkandarasi huyo kuwa ni vyema akawapeleka nje wataalam wanaoziendesha mashine hizo ili waweze kupata ujuzi na uwezo wa kutengeneza mitambo pale inapohitajika badala ya kusubiri watu kutoka nje kuja kufanya kazi hiyo. 

Walieleza kuwa kuwepo kwa wataalam wa ndani wenye uwezo wa kutatua hitilafu zinazojitokeza katika mitambo itasaidia kupunguza gharama na kuokoa muda ili kufanya mradi uende bila kusimama.

Ujenzi huo unaotekelezwa kwa miezi 35 kauanzia Disemba 1, 2015 hadi Oktoba 31, 2018 unalenga kupunguza tatizo la msongamano wa magari na kuboresha huduma za usafiri katika Jiji la Dar es Salaam

WAZIRI MKUU AZINDUA MRADI WA MAJI MADABA

$
0
0
*Wagharimu sh. bilioni 1.092, unahudumia wakazi 5,300

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amezindua mradi wa maji safi na tenki lenye uwezo wa kuhifadhi lita 200,000 ambao utahudumia vijiji viwili vya Mkongotema na Magingo katika kata ya Mkongotema, wilayani Songea, mkoani Ruvuma.

Akisoma taarifa ya mradi huo kwa Waziri Mkuu jana (Alhamisi, Januari 5, 2017), Mkurugenzi wa Halmashauri ya Madaba, Bw. Shafi Mpenda alisema mradi huo ulioanza kujengwa mwaka 2013, umegharimu sh. bilioni 1.09.

“Hadi kukamilika kwake, mradi huu umegharimu sh. 1,092,439,812 ambapo kati ya hizo sh. 1,069,647,312 zimetolewa na Serikali kuu na sh. 22,792,500 zimechangwa na wananchi,” alisema.

Bw. Mpenda alisema mpaka sasa kaya 915 zenye watu 5,300 zinahudumiwa na mradi huo wenye vituo 57 vya kutolea huduma za maji kwa jamii. Alisema lengo lao ni kufikisha vituo 71 ifikapo mwishoni mwa mwaka huu.

Akifafanua zaidi, Bw. Mpenda alisema kukamilika kwa mradi huo kumesaidia kuwapunguzia wananchi gharama za kununua maji ambapo pipa moja liligharimu sh. 3,000. “Pia kutasaidia kupunguza adha ya kufuata maji umbali mrefu; kupunguza magonjwa yanayotokana na mlipuko na kuwapa wananchi muda wa kutosha kufanya shughuli nyingine za maendeleo,” alisema.

Akizungumza na wananchi waliohudhuria uzinduzi wa mradi huo, Waziri Mkuu aliwapongeza wakazi hao kuwa kukubali kuchangia ujenzi wa mradi huo kwani katika baadhi ya maeneo miradi kama hiyo imekwama kukamilika kwa sababu wananchi waligomea kuchangia.

Aliwataka wakazi wa vijiji hivyo wasiharibu mazingira na watunze vyanzo vya maji ili mradi huo uweze kuwa endelevu. “Mradi huu ni lazima tuutunze kwani hali ya hewa imebadilika sana hivi sasa, sababu ni sisi wenyewe wananchi ambao tumekata miti sana ili kupanua maeneo ya kilimo.”

“Changamoto inayotupata hivi sasa ni kwama tumebakia kuwa na eneo kubwa la kilimo lakini mazao yanayopatikana ni kidogo. Mtazamo wetu katika Serikali hivi sasa ni kulima kwenye eneo dogo lakini mavuno yawe mengi,” alisema.

“Mtu asilime chochote karibu na chanzo hiki ili tuweze kukitunza chanzo chetu. Na wenyeviti wa Serikali za vijiji vyote viwili, wekeni utaratibu wa wananchi kwenda kupanda miti ili eneo hili libaki kuwa na unyevunyevu kwa muda mrefu,” alisisitiza.

“Sera ya Serikali ni kuhakikisha kuwa kila mwananchi anapata maji katika umbali usiozidi mita 400, na hili tutaweza kulitimiza kama tu mtatunza vyanzo vya maji vilivyopo,” alisema.

Alitumia fursa hiyo kuwaomba wakazi wa vijiji hivyo watunze akiba ya chakula walichonachi kwa sababu hali ya hewa imebadilika na hakuna anayejua mvua itaanza kunyesha lini. “Hatujui mvua itakuja lini na kwa kiasi gani; mara zitakapoanza kunyesha kila mmoja katika familia ahakikishe analima mazao mbadala kama kunde, maharage na mihogo ambayo yanastahimili ukame,” alisema.

Waziri Mkuu pia alikagua utoaji huduma kwenye kituo cha afya cha madaba na ujenzi wa kituo cha kupozea umeme cha Madaba.


IMETOLEWA NA
OFISI YA WAZIRI MKUU
IJUMAA, JANUARI 6, 2017.

Makala Maalum Mkutano wa Uendeshaji wa Serikali kwa Uwazi (OGP), Paris Ufaransa

Mbowe apingwa kila kona,Ni kuhusu kubeza juhudi za Serikali Kagera

$
0
0
*Wasomi wamshukia, wamtaka aache siasa

WADAU mbalimbali wamempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuwa muwazi kwa wananchi wake wakati wanapohitaji misaada mbalimbali wakati wa majanga.

Wametoa kauli hiyo leo jijini Dar es salaam wakati wa mahojiano na mwandishi wa habari hizi kueleza kauli ya hivi karibuni ya Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema, Freeman Mbowe ambaye amekaririwa akidai kuwa kauli za Rais mkoani Kagera ni za hatari.

Wamesema kuwa baadhi ya Watanzania wamezoea kupewa ahadi ambazo kwa wakati mwingine ni vigumu kutekelezeka na sasa watu kama Mbowe bado wako kwenye mtazamo huo.

Wameongeza kuwa Rais Magufuli amekuwa siku zote mkweli, jambo ambalo baadhi ya watu wasiopenda ukweli wanapotosha kauli zake kwa kutaka kuwachonganisha wananchi na Rais wao ambaye amekusudia kuwaletea wananchi maendeleo.

Rais Magufuli akiwa Kagera hivi karibuni alisisitizia msimamo ambao si mpya, umekuwa msimamo wake na wa Serikali tangu yalipotokea maafa ya tetemeko la ardhi mkoani humo kwamba Serikali itasaidia lakini haitaweza kumjengea nyumba kila mtu.“Baadhi ya wanasiasa na viongozi wamekuwa wakitoa kauli zenye kupotosha na kubeza hotuba ya Rais Magufuli mkoani Kagera jambo ambalo sio zuri na sio ukomavu wa kiasa” walisema.

Mhadhiri Mwandamizi Chuo Kikuu cvha Dar es Salaam, Dkt Bashiru Ally amesema kuwa katika mfumo wa siasa huru kuna kutofautiana mitazamo kati ya wananchi ,Serikali na viongozi wa siasa lakini ni wazi kuwa Rais alisimama katika msimamo wa Serikali yake na uwezo wa kutekeleza ahadi zake.

Alisema kuwa Rais Magufuli alikuwa na maana nzuri ya kukabiliana na majanga nchini inategemea uwezo wa nchi na mshikamano wa wananchi na huo ni ukweli ambao wengi hawakupenda kuusikia.

Dkt. Bashiru Ally alisema kuwa kwa janga la Kagera kulikuwepo mshikamano wa Serikali katika ngazi zote, wananchi na wadau mbalimbali walishiriki kwa namna moja ama nyingine kukabiliana na janga hilo.

“Wito wangu ni kuwataka wanasisa kujifunza kutokana na majanga badala ya kutoa kauli tatanishi na zenye kubomoa mshikamano wa wananchi, bali wanatakiwa kukosoa bila kubeza, kupotosha kwa namna ni ya kungwana,” alisema Dkt Bashiru

Kwa upande wake Dkt. Benson Bana kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam amesema kuwa watu wanatafsiri vibaya maneno ya Mhe. Rais aliyoyaongea Mkoani Kagera hivi juzi.

“Mheshimiwa ameongea ukweli kwa sababu ni sahihi kuwasaidia watu wengi kwa pamoja kuliko kumsaidia mtu mmoja mmoja,” alisema.

Aliongeza kuwa hakuna haja ya kuwa na wasiwasi juu ya lugha za Mhe. Rais kwani lugha zake hazina ubabaishaji ni za kweli na ziko moja kwa moja, hao wanaomuongelea vibaya ni wale wenye lengo la upinzani tu na sio maendeleo ya Taifa.

Ameongeza kuwa kwa upande wake pamoja na wananchi wenye mapenzi ya kweli wamemuelewa Mhe. Rais na ndio maana walikuwa wakimpigia makofi wakati akiongea kule Kagera.

”Mimi nilikuwepo mkoani Kagera na hotuba za mheshimiwa zote nilizisikiliza kwa makini ndio maana nasema wanye nia mbaya na Rais ndio wanaoongea mabaya juu yake kwani mbona alivyoongelea suala la kupunguza umeme hawakusema chochote?” alihoji Dkt. Bana.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Chama cha United Democratic Party (UDP) John cheyo amewataka Watanzania kutotegemea serikali kwa kila kitu pindi wanapopatwa na majanga.

Alisema kuwa lengo la Mheshimiwa Rais Magufuli ni kutaka Watanzania kujenga utamaduni wa kujitegemea pindi wanapofikwa na majanga mbalimbali na ndio maana alitaka kujua juhudi zao kabla ya kuomba msaada wa Serikali.

Profesa Haji Semboja alisema kuwa kauli ya Rais ilikuwa ni kuwahimiza watu wa Kagera ambao anajua wana uwezo wa mambo mengi ya kulima mazao mbalimbali kama vile mazao ya chakula na biashara ikiwemo ndizi na kahawa ambayo yanaweza kuwapatia chakula cha kutosha wananchi wa mkoa huo.

Naye Kaimu Mkuu wa Chuo cha Diplomasia nchini Dkt. Bernad Achiula amesema kuwa baadhi ya wananchi wamepokea hotuba ya Rais John Magufuli kwa mtazamo tofauti, lakini ni dhahiri hakuna nchi yeyote duniani ambayo inahudumia kila mwananchi katika majanga ya kiasili yanayotokea.

“Wajibu wa Serikali katika nchi yeyote ni kujenga na kuboresha miundombinu mbalimbali iliyotokea ikiwemo barabara, hospitali, shule, malazi ya muda kwa waadhirika, madawa, miundombinu ya umeme, maji kwa waathirika hatua inayolenga kuwapa pole waathirika hao.

Alisema kuwa hatua hizo zinalenga kutoa huduma kwa wananchi wengi kuliko kutoa msaada kwa mtu mmoja mmoja. Alisema wanaotaka kumlaumu Rais basi wangemlaumu kama angekuwa Serikali yake haijatoa huduma hizo muhimu.

Alipoulizwa kuhusu kauli hizo za Mbowe, Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO ambaye pia ndiye Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi alisema lugha ya Rais na Serikali kwa ujumla kuhusu maafa ya Kagera na mengine yaliyotokea nchini haijawahi kubadilika wala kutetereka.

“Rais na Serikali yake kwa ujumla wamekuwa wazi katika hili na itaendelea kuwa wazi kwamba kama Taifa hatuna raslimali za kumsaidia kila mwathirika wa tetemeko la Kagera kwa kumfanyia kila kitu.

Serikali ilitibu majeruhi wote bure, ilisaidia kifuta machozi kwa familia zote zilizopoteza ndugu zao, ilisaidia waathirika kupata huduma za kibinadamu kama dawa, ushauri wa kisaikolojia, vyakula na mavazi na maturubai kwa makazi ya muda na inaendelea kujenga miundombinu kama shule, zahanati na barabara,” alisema.

Dkt Abbas akasisitiza: “Mbowe atafute tu ajenda nyingine. Nilikwenda Kagera na kukaa kwa wiki mbili baada ya tetemeko kutokea ambapo nilibahatika kuzungumza na waathirika mijini na vijijini; hakuna kati yao popote aliyekuwa anasema Serikali itamjengea nyumba au kumsaidia kila kitu. Kwa hiyo ujumbe wa Rais ulieleweka tangu mwanzo na hata sasa.”

Ameongeza kuwa Serikali imesaidia kaya maskini kwa kuwapatia sajuri na mabati kwa ajili ya ujenzi wa nyumba.

UZINDUZI WA AWAMU YA KWANZA YA BRANDING YA KARAFUU YA ZANZIBAR

$
0
0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) alipokuwa akiwaangalia wafanyakazi wa Shirika la ZSTC wakitoa uchafu katika Karafuu zinazotayarishwa kwa mauzo  ambazo huingizwa  katika chupa na kuwekewa alama maalum kwa ajili ya mauzo  wakati alipotembelea kazi hizo leo katika  uzinduzi Awamu ya kwanza ya Branding  ya Karafuu ya Zanzibar,ikiwa ni shamra shamra za maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,(wa pili kushoto) Mkurugenzi Mwendeshaji Dkt.Said Seif Mzee
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) alipokuwa akipata maelezo kwa Asmahani Abdulkadir alipotembelea Karafuu zinazotiwa katika chupa kuwekewa alama maalum kwa ajili ya mauzo  wakati alipowasili Saateni Mjini Unguja kuzindua Awamu ya kwanza ya Branding  ya Karafuu ya Zanzibar  leo,ikiwa ni shamra shamra za miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,(kushoto) Mkurugenzi Mwendeshaji Dkt.Said Seif Mzee.
 Baadhi ya Wafanyakazi wa Shirika la ZSTC na Wananchi waliohudhuria katika  uzinduzi wa Awamu ya kwanza ya Branding  ya Karafuu ya Zanzibar huko Saateni Mjin Unguja leo,wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipotoa hutuba yake katika hafla hiyo ikiwa ni shamra shamra za maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
 Waziri wa Biashara Viwanda na Masoko Mhe,Amina Salum Ali alipokuwa akimkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa tatu kushoto) kuzungumza na Wananchi na Viongozi waliohudhuria katika uzinduzi wa Awamu ya kwanza ya Branding  ya Karafuu ya Zanzibar huko Saateni Mjini Unguja leo,ikiwa ni shamra shamra za miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
  Baadhi ya Viongozi waliohudhuria nkatika hafla ya Uzinduzi wa Awamu ya kwanza ya Branding  ya Karafuu ya Zanzibar  huko Saateni Mjini Unguja leo,wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipotoa hutuba yake katika hafla hiyo ikiwa ni shamra shamra za maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akizungumza na Viongozi,Wafanyakazi na Wananchi  katika hafla ya Uzinduzi wa Awamu ya kwanza ya Branding  ya Karafuu ya Zanzibar huko Saateni Mjini Unguja leo,ikiwa ni shamra shamra za maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,(kulia) Waziri wa Biashara Viwanda na Masoko Mhe,Amina Salum Ali,
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akizungumza na Viongozi,Wafanyakazi na Wananchi  katika hafla ya Uzinduzi wa Awamu ya kwanza ya Branding  ya Karafuu Zanzibar huko Saateni Mjini Unguja leo,ikiwa ni shamra shamra za maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,(kulia) Waziri wa Biashara Viwanda na Masoko Mhe,Amina Salum Ali na (kushoto) Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la ZSTC Maalim Kassim Suleiman.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein(kulia) akinyanyua Nembo ya KARAFUU kama ishara ya Uzinduzi wa  Awamu ya kwanza ya Branding  ya Karafuu ya Zanzibar,uliofanyika leo  huko Saateni Mjini Unguja,ikiwa ni shamra shamra za maadhimisho ya  miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,(kulia) Waziri wa Biashara Viwanda na Masoko Mhe,Amina Salum Ali,(kushoto) Mwenyekiti wa Bodi ya ZSTC Maalim Kassim Suleiman.  
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akiagana na Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la ZSTC Maalim Kassim Suleiman (katikati) baada ya kumalizika hafla ya Uzinduzi wa   Awamu ya kwanza ya Branding  ya Karafuu Zanzibar huko Saateni Mjini Unguja leo,ikiwa ni shamra shamra za maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,(kushoto) Waziri wa Biashara Viwanda na Masoko Mhe,Amina Salum Ali.

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akisalimiana na Makamu wa Pili wa Rais Mhe Balozi Seif Ali Iddi wakati alipowasili Saateni Mjini Unguja kuzindua Awamu ya kwanza ya Branding  ya Karafuu ya Zanzibar  leo,ikiwa ni shamra shamra za miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,(katikati) Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Mhe,Ayoub Mohamed Mahamoud.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akisalimiana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa,Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ Mhe, Haji Omar Kheri wakati alipowasili Saateni Mjini Unguja kuzindua Awamu ya kwanza ya Branding  ya Karafuu  ya Zanzibar leo,ikiwa ni shamra shamra za maadhimishio ya miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
(Picha na Ikulu)

KATIBU MKUU OFISI YA MAKAMU WA RAIS AFNYA MKUTANO NA VIONGOZI ILI KUTENGENEZA MKAKATI WA KUDHIBITI UVUVI HARAMU WA KUTUMIA MABOMU

$
0
0
 Kaimu Mkurugenzi Idara ya Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Richard Muyungi akiwasilisha mada iliyohusu mapendekezo ya mkakati wa pamoja wa kudhibiti uvuvi haramu wa kutumia mabomu, katika mkutano wa Makatibu wakuu na wadau wa sekata ya mazingira ulohusu mkakati wa kudhibiti uvuvi haramu wa kutumia mabomu.
Kushoto Katibu Mkuu ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Profesa Faustin Kamuzora akizungumza katika kikao cha Makatibu wakuu na wadau wa sekta husika za masuala ya mazingira, katika mkutano ulohusu mkakati wa kudhibiti uvuvi haramu wa kutumia mabomu. Mkutano huo wa ndani ulifanyika katika ukumbi wa mkutano wa Ofisi ya Makamu wa Rais jijini Dar es Salaam. (Picha na Evelyn Mkokoi). Sehemu ya washiriki katika mkutano wa Makatibu Wakuu wa Wizara na wadau wa  sekta husika za masuala ya mazingira uliohusuhusu mkakati wa kudhibiti uvuvi haramu wa kutumia mabomu.

BILIONI 251 ZATENGWA KUIMARISHA HUDUMA ZA DAWA KATIKA VITUO VYA AFYA.

$
0
0
SERIKALI kupitia Wizarya afya , maendele ya jamii , Jinsia Wazee na Watoto imetenga bilioni 251 ili kuimarisha upatikanaji wa dawa katika vituo vya afya na zahanati zote nchini .

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu Wizara Ya Afya, Maendeleo Ya Jamii, Jinsia, Wazee Na Watoto Dokta Mpoki wakati wa mahojiano katika kipindi cha Tunatekeleza kinachoendeshwa na kituo cha matangazo TBC1 jijini Dar es salaam.

“Kutokana na taarifa zinazozagaa juu ya upungufu wa dawa katika zahanati hapa nchini ,taarifa hizo si za kweli napenda kuwatoa hofu wananchi na bajeti yetu ya mwaka huu ni shilingi Bil. 251 kwa ajili ya dawa tu” alisema Dkt. Ulisubisya

Aidha Dkt. Ulisubisya alisisitiza kuwa kuna dawa zitapewa kipaumbele kutokana na mahitaji yake kuwa makubwa nchini ukilinganisha na mahitaji ya dawa nyingine hivyo dawa zote zitaendelea kuwepo ili kuwasaidia wananchi wote wenye uhitaji. 

Dkt. Ulisubisya aliweka wazi juu ya mipango ya serikali katika kuimarisha huduma za afya katika maeneo mbali mbali nchini ili kujenga taifa lenye watu imara kiafya.Kwa mujibu wa Dkt. Ulisubisya amesema kuwa vituo vya serikali na vya watu binafsi ni vyema viendelea kufuata sera, taratibu na sheria ikiwemo bei elekezi katika kuwahudumia wananchi huduma bora kwa gharama ndogo.

Dkt. Ulisubisya amesisitiza kuwa Kufikia mwezi wa tano mwaka huu asilimia 90 ya dawa zote zitakua zimepatikana na kusambazwa kwenye vituo vya afya na zahanati zote nchini ili kuimarisha sekta ya afya na mpaka sasa chanjo zote zipo za kutosha.

“Tunataka kila kituo cha afya kinachojengwa sasa hivi kitoe huduma za upasuaji ili kupunguza mlundikano wa wagonjwa wanahoitaji huduma hiyo na kuokoa maisha ya mtanzania kwa haraka zaidi alisema Dkt. Ulisubisya.

Aidha Dkt Ulisubisya alisema kuwa Serikali ina mkakati wa kuimarisha huduma zote za vipimo ili zipatikane katika hospitali za wilaya na kikanda mpaka kufikia 2020 ili kuwezesha taifa kupiga hatua katika sekta ya afya.

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA “NITASHUGHULIKIA MLIPWE FEDHA HARAKA ILI MTAMBO WA KUPOOZEA UMEME WA GRIDI YA TAIFA KUTOKA MAKAMBAKO MKOANI NJOMBE KWENDA SONGEA MKOANI RUVUMA UKAMILIKE KWA WAKATI”

$
0
0

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, KASSIM MAJALIWA katika ziara yake ya Siku ya Pili mkoani Ruvuma ametembelea na kukagua eneo litakalojengwa mtambo wa kupoozea umeme wa Gridi ya Taifa kutoka Makambako mkoani Njombe kwenda Songea mkoani Ruvuma . Habari kamili hii hapa video yake.Ruvuma Tv


SERIKALI MKOANI SIMIYU YADHAMIRIA KUMALIZA MIGOGORO YA ARDHI

$
0
0
 Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,Mhe.Anthony Mtaka (kushoto) akiwa na Mbunge wa Viti Maalum wa Mkoa wa Simiyu kupitia CCM, Mhe. Leah Komanya wakizungumza na wananchi wa Wilaya ya Meatu katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kituo cha Mabasi cha Mjini Mwanhuzi kwa lengo la kusikiliza na kutatua kero mbalimbali za wananchi wilayani humo.
 Baadhi ya Viongozi wa Mkoa wa Simiyu na Wilaya ya Meatu wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka wakati alipokuwa akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Meatu kwenye  mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kituo cha Mabasi cha Mjini Mwanhuzi kwa lengo la kusikiliza na kutatua kero mbalimbali za wananchi wilayani humo.
 Baadhi ya Viongozi wa Mkoa wa Simiyu na Wilaya ya Meatu wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka wakati alipokuwa akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Meatu kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kituo cha Mabasi cha Mjini Mwanhuzi kwa lengo la kusikiliza na kutatua kero mbalimbali za wananchi wilayani humo.
 Ndg. Ngodongo Maganga mkazi wa kijiji cha Cambala wilayani Meatu akimweleza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (hayupo pichani) kero yake ya kuporwa eneo wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kituo cha Mabasi cha Mjini Mwanhuzi kwa lengo la kusikiliza na kutatua kero mbalimbali za wananchi wilayani humo.
 Kutoka kushoto Mkuu wa Wilaya ya Meatu, Mhe. Dkt. Joseph Chilonga, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Meatu, Fabian Manoza, Mbunge Viti Maalum, Mhe. Leah Komanya, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka na Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Ndg.Jumanne Sagini wakimkabidhi mabati Bibi Yunge Masanja yaliyotolewa na Mhe.Mbunge Komanya ili kumsaidia katika ujenzi wa nyumba yake.
 Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (kulia) na Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Simiyu, Mhe. Leaah Komanya wakizungumza na Bibi Yunge Masanja mara baada ya kumkabidhi mabati yaliyotolewa na Mbunge huyo kwa lengo la kumsaidia kujenga nyumba.
Baadhi ya wananchi wa Wilaya ya Meatu wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (hayupo pichani) kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kituo cha Mabasi cha Mjini Mwanhuzi kwa lengo la kusikiliza na kutatua kero mbalimbali za wananchi.

Na Stella Kalinga, Simiyu
Serikali  Mkoani  Simiyu imedhamiria kwa mwaka 2017 kutatua na kuondoa migogoro yote  ya  ardhi ambayo imekuwa ikijitokeza mara kwa mara kwa wananchi wa mkoa huo.

Akitoa ufafanuzi wa namna ya  kutatua kero hiyo wakati wa mkutano wake na wananchi wa jimbo la  Meatu ,Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka alisema kuwa amechoshwa kusikia na kuona migogoro ya ardhi  inayojitokeza ndani ya mkoa wake, hivyo mwaka 2017 ndio utakuwa mwisho wa kero hizo.

Mtaka amesema kuwa kamwe hawezi kukubali kuona migogoro  hiyo inaendelea hivyo wananchi na watendaji wa idara ya ardhi wanapaswa kila mmoja ajue utaratibu sahihi wa utoaji na ununuaji wa ardhi ili kuepusha sintofahamu zinazojitokeza.

“ mwaka huu  wa 2017 ni mwaka ambao mimi mkuu wa Mkoa wa Simiyu nimeamua kusimamia ,kusikiliza na kutatua kero zote za ardhi…nataka ndani ya kipindi hichi ifikie mahali migogoro ya ardhi kwa mkoa wa Simiyu inakuwa sio kipaumbele chetu…Mtaka.

Aidha, Mtaka alieleza kuwa anataka watendaji wa idara ya ardhi kuhakikisha wanafanya kazi zao kwa umakini na kuweka kumbukumbu za kimaandishi katika  kila mgogoro unaotatuliwa kwani kuna baadhi ya wananchi wamekuwa wakiibua mgogoro hiyo upya pindi kunapotokea mabadiliko ya viongozi  katika maeneo yao.

Sambamba na hilo pia amewataka wananchi wote wa mkoa wa Simiyu kutovamia maeneo ya Taasisi za Serikali na endapo wapo ambao wako ndani ya maeneo hayo waondoke mara moja kabla serikali haijawachukulia hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kubomolewa kwa nyumba zao.

Hata hivyo katika kikao hicho kulibainika  kuwepo na tatizo la watendaji wa ardhi kutoa umiliki wa kiwanja kimoja kwa zaidi watu wawili hali ambayo inasababisha mgongano mkubwa baina ya wananchi hao, ambapo wananchi wote walioonekana kupata tatizo hilo waliahidiwa kupewa viwanja mbadala na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu.

Michael Stephano mkazi wa Meatu amesema kuwa amefurahishwa sana na mfumo wa mkuu wa Mkoa kusikiliza kero za wananchi , kwani kwa kufanya hivyo wananchi watapata haki zao stahiki ambazo hapo awali walikuwa hawazipati.

“tunamshukuru sana mkuu wa Mkoa wetu…kitendo anachokifanya kwa kweli kimetupa nguvu ya kujua wapi tunapata haki zetu pale tunapoona tumeibiwa haki hiyo…sambamba na hilo ametusaidia mwongozo na kutatua kero za ardhi na ninaamini mpaka kuisha mwaka huu kero nyingi zitakuwa zimeisha…Alisema Stephano.

Kwa upande wake Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Simiyu, Mhe.Leah Komanya amewataka Watumishi wa Idara ya ardhi kuzingatia sheria na taratibu kila wanapotwaa, kuuza, kuthamini au kupima ardhi kwa  sababu kitendo cha kutofuata sheria na taratibu kwa watumishi hao kimekuwa chanzo cha migogoro mingi ya ardhi.
Wakti huo huo Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,Mhe.Anthony Mtaka amemtaka Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu, Ndg.Fabian Manoza kuchunguza tuhuma zilizotolewa na wananchi dhidi ya viongozi wa Vijiji na Vitongoji juu ya kutumia maeneo ya misitu yaliyohifadhiwa yajulikanayo kama HASHI (Hifadhi Ardhi Shinyanga) kwa manufaa yao, na watakaobainika wachukuliwe hatua.
Mtaka amesema kwa kuwa wilaya hiyo inatarajia kuanzisha mradi wa ufuagaji bora wa ng’ombe wa kisasa, maeneo yote ya HASHI yatumike kupanda majani ya malisho kwa ajili ya kuwasaidia wafugaji kupata malisho hasa wakati wa kiangazi.

KIJANA WA KITANZANIA DENNIS MHINA ASHIKA NAFASI YA NNE KWA UBORA DUNIANI MASHINDANO YA KUOGELEA CANADA

$
0
0

Mchezaji wa timu ya Taifa ya kuogelea,Dennis Khamis Mhina akipokea shada la maua kutoka kwa baba yake mzazi mzee Khamis Hussein Mhina wakati alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa JK Nyerere leo alasili akitokea nchini Canada ambako alishinda na kushika nafasi ya nne katika mashindano ya vijana ya Dunia ya kuogelea yaliyofanyika nchini humo hivi karibuni.
Mchezaji wa timu ya taifa ya kuogelea ya vijana Kijana Dennis Khamis Mhina akipokewa na ndugu jamaa na marafiki wakati alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa JK Nyerere leo alasili akitokea nchini Canada ambako alishinda na kushika nafasi ya nne katika mashindano ya vijana ya dunia ya kuogelea yaliyofanyika nchini humo hivi karibuni.
Mchezaji wa timu ya taifa ya vijana ya kuogelea Kijana Dennis Khamis Mhina akitoka nje na mama yake mzazi Bhoke Mukoji Mhina kulia wakati alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa
Kimataifa wa JK Nyerere leo arasili akitokea nchini Canada ambako alishinda na kushika nafasi ya nne katika mashindano ya vijana ya dunia ya kuogelea yaliyofanyika nchini humo hivi karibuni.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Kuogelea nchini, Ramadhan Namkoveka akizungumza wakati walipompokea mchezaji wa timu ya taifa ya vijana ya kuogelea Kijana Dennis Khamis Mhina wakati alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa
Kimataifa wa JK Nyerere leo alasili akitokea nchini Canada ambako alishinda na kushika nafasi ya nne katika mashindano ya vijana ya dunia yaliyofanyika nchini humo hivi karibuni, Kulia ni mama mzazi wa kijana Dennis Mhina Bi Bhoke Mukoji Mhina.
Mchezaji wa timu ya taifa ya vijana ya kuogelea Mchezaji wa timu ya taifa ya vijana ya kuogelea Kijana Dennis Khamis Mhina akizungumza mara baada ya kuwasili nchini kwenye uwanja wa ndege wa
Kimataifa wa JK Nyerere leo alasili akitokea nchini Canada ambako alishinda na kushika nafasi ya nne katika mashindano ya vijana ya dunia yaliyofanyika nchini humo hivi karibuni kulia ni mama mzazi Dennis Mhina Bi. Bhoke Mukoji Mhina, kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa Chama Cha Kuogelea nchini, Ramadhan Namkoveka na baba yake Khamis Hussein Mhina
Mama mzazi Dennis Mhina Bi. Bhoke Mukoji Mhina akizungumza kwenye uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa JK Nyerere, kulia ni Dennis Mhina na kushoto ni Baba yake Bw. Khamis Hussein Mhina.
Baba yake Dennis Mhina Bw. Khamis Hussein Mhina akizungumza na waandishi wa habari kwenye uwanja wa ndege wa
Kimataifa wa JK Nyerere,kulia ni Bi. Bhoke Mukoji Mhina Mama wa Dennis Mhina aliyesimama katikati.

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA ATEMBELEA MGODI WA MAKAA YA MAWE YA NGAKA WILAYA YA MBINGA MKONI RUVUMA

$
0
0
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiangalia shughuli za uchimbaji wa makaa ya mawe unavyofanywa nakampuni ya Tancoul katika mgodi wa Ngaka uliopo wilayani Mbinga  kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la maendeleo la taifa NDC Dr Samuel Nyantahe.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiangalia mkaa wa mawe ulivyo
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa ameongozana na mkuu wa mkoa wa Ruvama Mhandisi Mahenge pamoja naviongozi mbalimbali walipokuwa wanatemmbelea mgodi wa Ngaka

 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na mkurugenzi mkuu wa Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) Mlingi Mkucha wakati alipotembelea mgodi wa makaa ya mawe wa Ngaka unaomilikiwa na kampuni ya Tancoul uliopo wilayani Mbinga  kushoto kwa waziri mkuu ni Mwenyekiti wa bodi ya NDC Dr Samuel Nyantahe
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Tancoul Bwana Mark McAnderew  wakati alipotembelea mgodi wa makaa ya mawe ya Ngaka unaomilikiwa na kampuni ya Tancoul uliopo wilayani Mbinga  kushoto kwa waziri mkuu ni Mwenyekiti wa bodi ya NDC Dr Samuel Nyantahe
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Ofisa Rasilimali watu wa kampuni ya Tancoul Ms  Pendo Mweli wakati alipotembelea mgodi wa makaa ya mawe unaomilikiwa na kampuni ya Tancoul uliopo Ngaka wilayani Mbinga  Mkoani Ruvuma
Picha na Chris Mfinanga

UZINDUZI WA KIWANDA CHA AZAM DAIRY PRODUCTS LIMITED FUMBA

$
0
0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) na Mwenyekiti wa Kampuni ya Azam Group Bw.Said Salim Bakhresa wakikata utepe kuashiria Uzinduzi wa Mradi wa kiwanda cha uzalishaji wa Maziwa (Azam Dairy Products Ltd.) huko Fumba wilaya ya Magharibi "A" Unguja, ikiwa ni katika shamra shamra za maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,(kushoto)
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akifungua pazia kuashiria Uzinduzi wa Mradi wa kiwanda cha uzalishaji wa Maziwa (Azam Dairy Products Ltd.) huko Fumba wilaya ya Magharibi "A" Unguja, ikiwa ni katika shamra shamra za maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,(kushoto) Mwenyekiti wa Kampuni ya Azam Group Bw.Said Salim Bakhresa
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akisalimiana na Mwenyekiti wa Kampuni ya Azam Group Bw.Said Salim Bakhresa mara alipowasili katika Viwanja vya Kiwanda cha Maziwa cha (Azam Dairy Products Ltd.) huko Fumba Kororo Wilaya ya Magharibi "A" Unguja leo kukizindua rasmi,ikiwa ni katika shamra shamra za maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,(kulia) Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Mhe,Ayoub Mohamed Mahmoud
 Wafanyakazi wa Kiwanda cha Maziwa cha (Azam Dairy Products Ltd.) wakiendelea na shuhuli zao za kuhakikisha maziwa yanapangwa vizuri katika  sehemu zinazohusika wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipotembelea baada ya kukizindua kiwanda hicho leo huko Fumba Kororo Wilaya ya Magharibi "A" Unguja,ikiwa ni katika shamra shamra za maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akipata maelezo kutoka kwa Meneja Uzalishaji katika Kiwanda cha Maziwa cha AZAM DAIRY PRODUCTS LTD ADILSON FAGUNDES (kushoto) wakati alipotembelea Kiwanda hicho huko Fumba Kororo Wilaya ya Magharibi "A" Unguja kuona harakati za uzalishaji baada ya kukizindua leo,ikiwa ni katika shamra shamra za maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akipata maelezo kutoka kwa Meneja Uzalishaji katika Kiwanda cha Maziwa cha AZAM DAIRY PRODUCTS LTD ADILSON FAGUNDES (kushoto) wakati alipotembelea Kiwanda hicho huko Fumba Kororo Wilaya ya Magharibi "A" Unguja kuona harakati za uzalishaji baada ya kukizindua leo,ikiwa ni katika shamra shamra za maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akipata maelezo kutoka kwa Meneja Uzalishaji katika Kiwanda cha Maziwa cha AZAM DAIRY PRODUCTS LTD ADILSON FAGUNDES (kushoto) wakati alipotembelea Kiwanda hicho huko Fumba Kororo Wilaya ya Magharibi "A" Unguja kuona harakati za uzalishaji baada ya kukizindua leo,ikiwa ni katika shamra shamra za maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar
 Baadhi ya wafanyakazi wa Kiwanda cha Maziwa cha (Azam Dairy Products Ltd.) wakiendelea na shuhuli zao za kuhakikisha maziwa yanapangwa vizuri katika maboksi katika hatua za mwisho kuelekea  sokoni,wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipotembelea baada ya kukizindua kiwanda hicho leo huko Fumba Kororo Wilaya ya Magharibi "A" Unguja,ikiwa ni katika shamra shamra za maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) na Mwenyekiti wa Kampuni ya Azam Group Bw.Said Salim Bakhresa wakikata utepe kuashiria Uzinduzi wa Mradi wa kiwanda cha uzalishaji wa Maziwa (Azam Dairy Products Ltd.) huko Fumba wilaya ya Magharibi "A" Unguja, ikiwa ni katika shamra shamra za maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,(kushoto) 
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akifungua pazia kuashiria Uzinduzi wa Mradi wa kiwanda cha uzalishaji wa Maziwa (Azam Dairy Products Ltd.) huko Fumba wilaya ya Magharibi "A" Unguja, ikiwa ni katika shamra shamra za maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,(kushoto) Mwenyekiti wa Kampuni ya Azam Group Bw.Said Salim Bakhresa
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akifungua pazia kuashiria Uzinduzi wa Mradi wa kiwanda cha uzalishaji wa Maziwa (Azam Dairy Products Ltd.) huko Fumba wilaya ya Magharibi "A" Unguja, ikiwa ni katika shamra shamra za maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,(kushoto) Mwenyekiti wa Kampuni ya Azam Group Bw.Said Salim Bakhresa
 Baadhi ya Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi na Viongozi wengine waliohudhuria katika hafla ya Uzinduzi wa Mradi wa kiwanda cha uzalishaji wa Maziwa (Azam DairyProducts Ltd.) huko Fumba wilaya ya Magharibi "A" Unguja,wakishuhudia  na kusikiliza maelezo yaliyotolewa kuhusu Kiwanda hicho,ikiwa ni katika shamra shamra za maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar
 Baadhi ya wananchi mbali mbali waliohudhuria katika hafla ya Uzinduzi wa Mradi wa kiwanda cha uzalishaji wa Maziwa (Azam Dairy Products Ltd.) huko Fumba wilaya ya Magharibi "A" Unguja,wakishuhudia  na kusikiliza maelezo yaliyotolewa kuhusu Kiwanda hicho,ikiwa ni katika shamra shamra za maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar
Mwakilishi wa Kampuni ya Azam Diary Bw.Salim Aziz akitoa maelezo kuhusu mradi wa uzalishaji wa maziwa katika uzinduzi wa Kiwanda cha Maziwa  cha (Azam Dairy Products Ltd.) leo huko Fumba Kororo wilaya ya Magharibi A" Unguja,katika shamra shamra za maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar. Picha na IKULU

VIJUSO VYA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI JANUARI 7, 2017

WAZIRI MKUU ANUSA MADUDU MRADI WA NGAKA,AAHIDI KUTUMA GAVANA ,CAG,MSAJILI WA HAZINA KUFANYA UKAGUZI

$
0
0
*Asema Serikali haitaruhusu uagizaji wa makaa hayo kutoka nje ya nchi
*Autaka uongozi wa kampuni uimarishe teknolojia ili kuongeza uzalushaji

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa atamtuma mara moja Msajili wa Hazina aende kufanya uchunguzi wa kina na wa kijinai (forensic investigation) ili kijiridhisha kama mapato na matumizi ya kampuni ya TANCOAL ni halali.

Ametoa kauli hiyo leo mchana (Ijumaa, Januari 6, 2017) mara baada baada ya kupokea taarfa na kutembelea mgodi huo ili kuona shughuli za uzalishaji zikoje.

Waziri Mkuu amesema atamwagiza pia mdhibiti na mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ili apitie mahesabu ya kampuni tangu mwaka 2011 walipoanza uzalishaji. “Mbali CAG, itabidi Gavana wa Benki Kuu naye aangalie utumaji wa fedha uliokuwa ukifanywa kama ulifanyika kwa halali,” amesema.

Katika maswali aliyoyauliza Waziri Mkuu, alitaka kujua ni kwa nini kampuni hiyo haijalipa gawio kwa Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) ambao ni mbia (asilimia 30) na kampuni ya Intra Energy Limited (asilimia 70) licha ya kuwa imekuwa ikifanya uzalishaji wa makaa ya mawe na kuyasafirisha kwenye viwanda hapa nchini na nje ya nchi.

“Taarifa zenu zinaonyesha kuwa mmepata kila mwaka lakini rekodi nilizonazo zinanionyesha kuwa mwaka 2013 mlipanga kuzalisha tani 50,000 na mkauza zaidi ya hapo. Mkagzi wa hesabu anasema kampuni imepata, hii itawezekanaje?” alisema wakati akimhoji Mkurugenzi Mtendaji wa NDC, Bw. Mlingi Mkucha.

“Desemba 2013 mliuza tani 39,000 kwa wamiliki wa viwanda vya nguo, pia mliuza tani 2,000 kwa kampuni ya saruji ya Zambia, Novemba 2013 mliingia makubaliano ya kuuza tani 165,000 kwa kampuni ya saruji ya Kitanzania na ziliuzwa. Mbona financial statement zenu zinasema mwaka huo nao mlipata hasara?”

“Mnasema gawio (dividend) hutolewa baada ya mtu kutangaza faida. Mbona mlivuka lengo lakini mkatangaza kuwa kamouni imepata hasara katika mwaka huo wa fedha?”

Waziri Mkuu alimbana Bw. Mkucha aeleze ni kwa nini akiwa mwanasheria wa NDC aliruhusu kuwepo kwa mkataba unaotoa mwanya kwa kampuni ya TANCOAL kulipia gharama za menejimenti kwa wakurugenzi ambao wako Australia wakati hawahusiki na utendaji wa kila siku wa TANCOAL hapa nchini.

Pia alihoji ni kwa nini aliyekuwa Mkurugenzi wa NDC, Bw. Gideon Nassari alikuwa ni mjumbe wa Bodi ya TANCOAL na mjumbe wa Bodi ya Intra Energy Corporation ya Australia huku akiwa ni Mtendaji Mkuu wa NDC. “Wewe ulikuwa mwanasheria wa NDC na ulilijua hilo lakini hukuona taabu ya kiutendaji katika hilo? Au ulishindwa kusema kwa sababu alikuwa ni bosi wako?”

Waziri Mkuu amemtaka Bw. Mkucha aupeleke mikataba huo kwa MwanasheriA Mkuu wa Serikali ili aupitie upya na hasa kipendgele cha kufungua akaunti za NDC kwa kutumia kanuni za Australia na suala la utaratibu wa gawio kwa wanahisa ambapo kifungu kilichopo kinaipa Bodi ya TANCOAL mamlaka ya kuamua kutoa au kutokutoa kwa wanahisa.

“Kipengele kama hiki kwenye mikataba kinazuia ninyi kupata gawio, na ndiyo maana hesabu zao kila mwaka zimekuwa zinasoma hasara na ninyi mnaona sawa tu huku Serikali ikiendelea kukosa mapato yake,” amesema.

Waziri Mkuu ameutaka uongozi wa kampuni ya TANCOAL uongeze uzalishaji ili iweze kukidhi mahitaji ya ndani kwani makampuni mengi yamebaini gharama kubwa iliyopo kwenye matumizi ya mafuta ya dizeli na sasa yanahitaji makaa ya mawe kwa uzalishaji.

“Nimetembelea mgodi na kujiridhisha kuwa makaa ya mawe yapo ya kutosha. Uongozi wa kampuni mmesema mashine ziko bandarini Mtwara, lipieni mkamilishe taratibu ili mashine na mitambo yenu vije kusaidia kuongeza uzalishaji,” amesema.

“Nirudie wito wa Serikali kuwa hatutaruhusu uagizaji wa makaa ya mawe kutoka nje ya nchi na kwa maana nyingine tumewaongezea wigo wa soko lakini ninyi mnakosa teknolojia ya uchimbaji makaa kwa wingi. Fanyeni haraka kuleta hivyo vifaa vilivyoko bandarini,” alisisitiza.

Akiwa kwenye mgodi huo, Waziri Mkuu alielezwa kuwa kampuni hiyo imepanga kuongeza uzalishaji na kufikia tani 60,000 kutoka tani 2,500 za sasa. Hivi sasa, uchimbaji kwenye mgodi wa Ngaka unafanyika kwenye eneo la Mbalawala na Mbuyura ambayo yana mashapo (deposits) ya tani milioni 423.

(mwisho)

IMETOLEWA NA
OFISI YA WAZIRI MKUU
IJUMAA, JANUARI 6, 2017.

HOSPITALI ZOTE ZA MIKOA KUWA NA WATAALAM WA MIFUPA

$
0
0


Na: Frank shija - MAELEZO

WATAALAM wa mifupa wamepelekwa katika Hospitali zote za Kanda na mataraji ya baadaye ni kuwapeleka katika Hospitali za Mikoa ikiwa ni kusogeza huduma za tiba ya mifupa karibu zaidi na wananchi.

Hayo yamebainishwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya katika kipindi cha TUNATEKELEZA kinachorushwa na kituo cha luninga cha TBC1 kwa kushirikiana na Idara ya Habari MAELEZO jana jijini Dar es Salaam.

Dkt. Ulisubisya amesema kuwa wataalamu hao wamepelekwa katika Hospitali hizo ili kutatua changamoto ya matibabu ya magonjwa ya mifupo yaliyoongezeka kwa wingi kutokana na ajali hasa zitokanazo na Bodaboda.

“Serikali imepeleka Wataalamu wa mifupa katika Hospitali za Kanda ikiwa ni njia ya kusogeza huduma za matibabu ya mifupa karibuzaidi na wananchi kwani kumekuwa naongezeko la wagonjwa kutokana na ajali hasa za Bodaboda” alisema Dkt. Ulisubisya.

Aidha Katibu Mkuu huyo amesema kuwa pamoja na kupeleka wataalamu wa mifupa katika Hospitali za Kanda na mikoa, mikakati ya Serikali ni kuhakikisha huduma za Afya zinakuwa bora na zinawafikia wananchi kwa urahisi ndiyo maana Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli imekuja na dhana ya kuwa na Zahanati kila Kijiji ambazo zitapatia dawa na vifaa tiba muhimu.

Aliongeza kuwa katika kuhakikisha dhana hiyo inatekelezeka Wizara ya Afya imekuwa ikishirikiana na TAMISEMI ambayo ndiyo yenye jukumu la kusimamia huduma, kuhakikisha huduma za msingi zinapatikana ikiwemo miundombinu ya Zahanati, Vituo vya Afya na Hospitali pamoja na Dawa na Vifaa Tiba.

“Pamoja na kuwa mambo mengine yanasimamiwa na TAMISEMI lakini ninapokuwa katika ziara nikikutana na changamoto zinazowahusu nashughulikia kisha nawapa taarifa ili wachukue hatua stahiki, hivyo ndivyo tunavyoshirikiana katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za Afya.”Alifafanua

Kuhusu upatikanaji wa dawa Dkt. Ulisubisya amesema kuwa hadi kufikia mwezi wa tano upatikanaji wa dawa utakuwa umefikia asilimia 90% kutoka 70% za sasa na kuongeza kuwa suala la dawa limepewa kipaumbele katika bajeti ya mwaka wa fedha wa 2016/2017 ambapo takribani shilingi 251 bilioni zimetengwa kwa ajili ya dawa na vifaa tiba.
Mwisho.

MJUMBE WA HALIMASHAURI KUU CCM NA MNEC WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA(MB) AKUTANA NA VIONGOZI WA CCM MKOA WA RUVUMA KATIKA OFISI CCM MKOA WA RUVUMA

$
0
0
Mjumbe wa Halimashauri Kuu ya CCM na MNEC Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (MB) akingalia burudani ya ngoma ya Mganda ambayo ilikuwa imeandaliwa kwa ajili ya kumkaribisha katika ofisi ya CCM Mkoa wa Ruvuma kwa ajili ya kuzungumza na Viongozi wa CCM Mkoa wa Ruvuma
Mjumbe wa Halimashauri Kuu ya CCMna MNEC Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (MB)amemkabidhi kadi ya CCM Bwana Musa Ndomba ambaye amerudi CCM mwanzo alikuwa mwana chama wa Chadema na Diwani wa Kata ya Tanga manispa ya songea na mwenyekiti wa wawanafunzi katika chuo kikuu cha mtakatifu John kilichopo Songea shughuli hiyo imefanyika katika ukumbi wa ccm mkoa wa Ruvuma
Mjumbe wa Halimashauri Kuu ya CCMna MNEC Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (MB)akisaini kitabu cha wageni katika ofisi ya CCM Mkoa wa Ruvuma wakatialipofika hapo kwa ajili ya kuongea na viongozi wa ccm mkoa wa Ruvuma kushoto ni Mwenyekiti CCM mkoa wa Ruvuma Bwana Oddo Mwisho na anaye fuatia ni katibu wa CCM Mkoa wa Ruvuma Verena Shumbusho
Mjumbe wa Halimashauri Kuu ya CCM na MNEC Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (MB)akizungzumza na viongozi wa CCM mkoa wa Ruvuma katika ukumbi wa CCM Mkoani Ruvuma
Waziri Mkuu yupo mkoani Ruvuma kwa ziara ya kikazi

Picha na Chris Mfinanga

MAKAMU WA RAIS AFUNGUA MKUTANO WA NANE WA CHAMA CHA MAJAJI NA MAHAKIMU WANAWAKE TANZANIA

$
0
0

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akihutubia wakati wa ufunguzi wa mkutano wa nane wa Majaji Wanawake ulioandaliwa na Chama Cha Majaji Wanawake Tanzania (TAWJA) unaofanyika kila baada ya miaka miwili na mkutano wa mwaka huu ulikuwa na kauli mbiu isemayo Kuongoza njia kufikia hitajio la upatikanaji wa haki kwa wote na kwa wakati.

Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman akihutubia wakati wa mkutano wa nane wa chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake Tanzania uliofanyika kwenye ukumbi wa PSPF Golden Jubilee jijini Dar es Salaam.

Mhe. Othman Makungu, Jaji Mkuu wa Mahakama Kuu ya Zanzibar,Mhe. Othman Makungu,akitoa nasaha zake wakati wa uzinduzi wa mkutano wa nane wa chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake Tanzania (TAWJA)

Mwenyekiti wa Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake Tanzania Jaji Imani Aboud akitoa salaam za ufunguzi wa mkutano wa nane wa chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake Tanzania (TAWJA)

Sehemu ya waliohudhuria wakiwa makini katika kuchukua yale yaliosemwa na Mhe. Makamu wa Rais wakati wa uzinduzi wa mkutano wa nane wa Chama Cha Majaji na Mahakimu Wanawake Tanzania (TAWJA).

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewaagiza Majaji na Mahakimu wanawake kote nchini kupambana ipasavyo katika kukabiliana vitendo vya rushwa,unyanyasaji kijinsia na rushwa ya ngono ili kusaidia wanawake kupata haki zao za msingi bila kubaguliwa katika jamii. 

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa agizo hilo jijini Dar es Salaam wakati anafungua Mkutano Mkuu wa NANE wa Chama cha Majaji na Mahakimu wanawake Tanzania (TAWJA).

Makamu wa Rais pia ameonya kuhusu vitendo vya rushwa ya ngono inayofanywa na baadhi ya watendaji wenye madaraka na kusema tabia hiyo  ni mbaya na lazima ikomeshwa mara moja katika jamii.

Amesema kuwa vitendo hivyo vya rushwa ya ngono huzuia na kukwamisha juhudi za wanawake kufikia huduma za kijamii na za kiserikali ipasavyo ikiwemo elimu, ajira na haki kwa ajili ya ustawi wa wanawake.

Aidha Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amekishukuru Chama cha Dunia cha Majaji Wanawake (IAWJ) kwa mchango na msaada wake kwa TAWJA katika programu ya miaka mitatu ya kupambana na matumizi mabaya ya madaraka na rushwa ya ngono.

Makamu wa Rais pia ameipongeza Wizara ya Katiba na Sheria, Shirika la UN Women na wadau wengine wa TAWJA kwa kuunga mkono mapambano ya aina zote za ubaguzi na ukatili dhidi ya wanawake na watoto nchini. 

Amesema elimu ya haki za Binadamu iliyotolewa na Chama hicho imeleta badiliko kwa wengi kwa njia ya mafunzo na machapisho na jitihada hivyo lazima ziongezwe ili huduma hiyo iweze kuwafikia wananchi wengi zaidi kote nchini.

Amesisitiza wanachama wa Chama cha TAWJA waendelee kutoa msaada katika kuwasaidia wanawake na watoto ambao wanakandamizwa kwa kunyimwa haki zao katika jamii ili waweze kupata haki zao nchini.

Kwa upande wake, Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mohamed Chande Othman amemhakikishia Makamu wa Rais kuwa mkakati wa uimarishaji wa shughuli za mahakama nchini unaendelea vyema lengo likiwa ni kutenda haki kwa wananchi kote nchini bila ubaguzi.Kauli mbiu ya Mkutano Mkuu wa NANE wa Chama cha Majaji na Mahakimu Tanzania (TAWJA) “Kuongoza njia kufikia hitajio la upatikanaji wa haki kwa wote na kwa wakati”.

ANNE MAKINDA AONGOZA WAOMBOLEZAJI MSIBA WA ANNA SENKORO

$
0
0

Picha ya marehemu Anna Senkoro enzi za uhai wake.

 Spika mstaafu wa Bunge la Tanzania, Anne Makinda akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lililokuwa na mwili wa aliyekuwa mgombea wa Urais wa Kwanza Mwanamke marehemu Anna Senkoro katika Kanisa la Wninner Chapels International jijini Dar es Salaam jana, Marehemu alizikwa katika makaburi ya Kinondoni.
Spika mstaafu wa Bunge la Tanzania, Anne Makinda akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lililokuwa na mwili wa aliyekuwa mgombea wa Urais wa Kwanza Mwanamke marehemu Anna Senkoro katika Kanisa la Wninner Chapels International jijini Dar es Salaam jana, Marehemu alizikwa katika makaburi ya Kinondoni. 
 Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza la marehemu Anna Senkoro.
Kada wa Chadema akitoa heshima za mwisho.

 Mwili wa aliyekuwa mgombea wa Urais wa Kwanza Mwanamke mwaka 2005, marehemu Anna Senkoro ukiwasili  leo katika Kanisa la Wninner Chapels International lililopo Banana jijini Dar es Salaam. (Picha na Francis Dande).
 Mwili ukiwasili kanisani.
 Humphrey Polepole akitoa salama za Chama na Serikali wakati wa ibada ya mazishi ya marehemu Anna Senkoro.
 Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Ilala, Makongoro Mahanga akitoa salamu za Chama chake wakati wa ibada ya mazishi ya aliyekuwa mgombea wa urais wa kwanza mwanamke katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2005.
Spika mstaafu wa Bunge la Tanzania, Anne Makinda ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), akitoa salamu za rambirambi wakati wa ibada ya mazishi ya marehemu, Anna Senkoro.

Mwili ukiwasili kanisani.  
 Wafiwa.
 Ndugu wa marehemu.
Spika mstaafu, Anne Makinda na Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM, Humphrey Polepole.
 Kutoka kulia ni Spika mstaafu, Anne Makinda, Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM, Humphrey Polepole na Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Ilala, Makongoro Mahanga.
 Jeneza.
 Wafiwa.
 Wafiwa. 
Poleni sana. 





Dk. Senkoro aliyegombea urais mwaka 2005 kupitia Chama cha TPP –Maendeleo alifariki dunia ghafla Januari 4, mwaka huu wakati akipelekwa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa ajili ya matibabu.

Shughuli ya kumuaga Dk. Senkoro ilianzia leo nyumbani kwake, Tabata Segerea, kisha mwili wake ulihamishiwa katika Kanisa la Winners Chapel International, Banana, Ukonga kwa ibada fupi, ambapo viongozi walitoa salamu za rambirambi. 

Mbali na Makinda, viongozi wengine waliohudhuria ni; Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM,  Humphrey Polepole na Mwnyekiti wa Chadema Wilaya ya Ilala, Dk. Makongoro Mahanga.

Akizungumza baada ya ibada hiyo, Makinda ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), alisema alipokea kwa mshtuko mkubwa kifo cha rafiki yake na mdogo wake huyo katika siasa.

Alisema Dk. Senkoro alijaribu kuwa rais mwaka 2005, lakini Mungu akamwambia anaweza kuwatumikia wananchi kwa njia nyingine kama alivyofanya.

“Tumemuamini Kristo hivyo hatuwezi kufika kwake bila kulala na Anna amefariki dunia katika Ukristo, swali, jiulize wewe kama ungekuwa Senkoro ungekwenda wapi?” alihoji Makinda.

Alisema familia yake ikae kwa amani na kwamba waamini Anna yuko kwa Mungu amekwenda kutuandalia makao.
Naye Dk. Mahanga akitoa salamu za Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na rafiki yake, Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, alisema wamesikitishwa na kifo hicho na kuwapa pole ndugu, jamaa na marafiki walioondokewa na kipenzi chao.

"Sisi kama chama tumempoteza kamanda mwenzetu na mpambanaji toka alipojiunga na chama mwaka juzi Julai, yote ni mapenzi ya Mungu," alisema Dk. Mahanga.
Kwa upande wake, Polepole akitoa salamu kwa niaba ya Mwenyekiti wa chama hicho, Rais John Magufuli pamoja na Katibu Mkuu, Abdulrahman Kinana alisema:

"Tuishi maisha mema na yenye kutenda haki kwa sababu Biblia inasema taifa linalotenda haki Mungu uliinua pamoja na kuwa waaminifu kwa uajibikaji na kutenda haki."
Dk. Senkoro wakati wa uhai wake aliwahi kufanya kazi katika Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi katika Gereza la Ukonga, ameacha watoto watu na wajukuu wawili.

Msemaji wa Taasisi ya JKCI, Maulid Kikondo, alisema mara ya mwisho kabla ya kufikwa na mauti, Dk. Senkoro alifika hospitalini hapo kwa ajili ya matibabu na kufanyiwa vipimo kadhaa ambavyo madaktari waligundua tatizo lililokuwa likimsumbua.

Alisema jopo la madaktari bingwa wa taasisi hiyo walikuwa na nafasi ya kuokoa maisha ya Senkoro iwapo angekubali kulazwa kwa ajili ya matibabu katika kitengo hicho.
Alisema baada ya vipimo alishauriwa kulazwa kutokana na hali yake, lakini Dk. Senkoro alikataa na kutaka kurudi nyumbani. 

HAPI AKIPIGA JEKI KITUO CHA POLISI MSIMBAZI KWA KUKIPATIA MIFUKO 100 YA SARUJI KUFANYIA UKARABATI

$
0
0

Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Ally Hapi leo ametembelea kituo cha Polisi cha Msimbazi jijini Dar es salaam ambacho kilipatwa na ajali ya moto siku za hivi karibuni na kutoa msaada wa mifuko 100 ya saruji sawa na tani 5.
Katika ziara yake kwenye kituo hicho, Hapi ametembelea kambi ya makazi ya askari na familia zao iliyoko nyuma ya kituo hicho ambapo amekabidhi mifuko hiyo ya Saruji kwa Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Ilala Ernest Matiku na kuagiza kuwa saruji hiyo itumike kwa ukarabati wa jengo zima la kambi hiyo ambayo inakaliwa na familia 72 za askari.

Kaimu Mkuu wa Mkoa ameeleza kuwa Polisi wanafanya kazi kubwa ya kulinda amani na usalama na hivyo jamii haina budi kuwaunga mkono.
Kwa upande wake Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa kipolisi Ilala Ernest Matiku ameeleza kuwa wanamshukuru Kaimu Mkuu wa Mkoa kwa msaada huo kwani jengo lao limechakaa sana hali inayohatarisha usalama wa askari na familia zao.Hivyo wataanza ukarabati mara moja vifaa vitakapo kamilika na kila kitu kitafanyika kama ilivyo kusudiwa.

Mawaziri 7 Wakutana leo Kuweka Mikakati ya kupambana na Uvuvi Haramu.

$
0
0



dar-1
Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (MAZINGIRA) na mwenyekiti wa kikao hicho   Januari Makamba akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) kuhusu mkakati wa Serikali katika kupambana na uvuvi haramu nchini mara baada ya kumalizika kwa kikao kilichohusisha Wizara Saba kushoto ni  Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Charels Tizeba.dar-2
Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Charels Tizeba akiwaeleza waandishi wa habari (Hawapo Pichani) athari za  uvuvi haramu na jinsi unavyoathiri uchumi wa nchi kushoto ni Naibu Waziri aOfisi ya Rais TAMISEMI Suleiman Jaffo.dar-2
Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Suleiman Jaffo akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) na kutoa maagizo ya Serikali kwa wakurugenzi nchini hasa kwenye maeneo wanayojishughulisha na uvuvi kuwachukulia hatua maafisa uvuvi wanaoshindwa kutimiza wajibu wao wa kupambana na uvuvi haramu, kushoto ni Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na mwenyekiti wa kamati hiyo.
PICHA NA BEATRICE LYIMO-MAELEZO.
………….
Na Beatrice Lyimo-MAELEZO
Serikali imewaagiza wakurugenzi nchini hasa kwenye maeneo wanayojishughulisha na uvuvi kuwachukulia hatua maafisa uvuvi wanaoshindwa kutimiza wajibu kwa kushindwa kuzuia uvuvi haramu.
Akizungumza baada ya kikao cha kamati kilichohusisha Wizara saba za Maliasili, Ulinzi, Nishati na Madini Tamisemi, Kilimo, Mifugo na Uvivi pamoja na Mambo ya Ndani Naibu Waziri TAMISEMI Suleiman Jaffo aliwataka watendaji hao kutumia agenda ya kupambana na uvuvi haramu kuwa agenda ya kudumu  katika vikao vyao.
Alisema kuwa maafisa uvuvi hao wanatakiwa kupimwa wajibu na utendaji kazi kwa kuangalia ni kiasi gani wanajihusisha na masuala mazima ya kupambana na uvuvi wa kutumia mabomu.
“Kuna baadhi ya mafisa uvuvi wanahusika na vitendo vya uvuvi haramu nchini hivyo kuanzia kesho wataanza kupimwa wajibu wao na kwa atakayeshindwa kutimiza wajibu atatolewa katika nyazifa hiyo”.
Kwa upande wake Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Januari Makamba alisema kuwa nchi yetu inaeneo kubwa la bahari na kwa miaka kadhaa nchi yetu imekuwa na changamoto ya uvuvi haramu, hivyo tumeona kuna haja ya kuchukua hatua ya haraka katika kupambana na uharamia huo.
Akifafanua zaidi kuhusu hilo Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Charels Tizeba alisema kuwa jambo la uvuvi haramu lisipochukuliwa kwa umakini litapelekea kuathiri uchumi wa nchi hivyo lengo la Serikali ni kukomesha uharibifu unaojitokeza sasa.
Alisema ni aibu kwa taifa letu la Tanzania kuendelea kuvua kwa njia haramu kwani nchi nyingi kwa sasa zimeondoka katika uvuvi wa namna hiyo.Naye Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mwigulu Nchemba alitoa wito kwa watanzania wote kushirikiana na Serikali katika kufichuwa wale wanaohusika na uvuvi haramu.Mwigulu Nchemba alisisitiza kuwa “kila mtanzania anawajibu wa kuwa makini katika kulinda rasilimali za majini tulizo nazo”.
Kikao hicho ni utekelezaji wa agizo la Makamu wa Rais la kupambana na uvuvi haramu ambapo maazimio hayo yatafanyiwa kazi na kuahidi kukutana baada ya miezi sita kwa ajili ya kutafakari hatua zilizochukuliwa pamoja na kurekebisha pale patakapoonekana pana changamoto
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live




Latest Images