Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1091 | 1092 | (Page 1093) | 1094 | 1095 | .... | 1896 | newer

  0 0

  Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella, akizungumza hii leo, kabla ya kukabidhi msaada wa vitanda 20, magodoro 20, vyandarua 20 pamoja na mashuka 100, uliotolewa na mbunge wa Viti Maalumu kupitia Chama cha Mapinduzi CCM mkoani Mwanza, Kemirembe Lwota.

  Ameonya juu ya suala la uchafu kukithiri kwenye wodi za wagonjwa katika vituo vya kutolea huduma za afya ikiwemo hospitali ya rufaa ya Sekour Toure.

  Na BMG

  Mganga Mkuu mkoani Mwanza, Dkt.Leonard Subi, akizungumza kwenye utoaji wa msaada huo
  Mbunge wa Viti Maalumu CCM mkoani Mwanza, Kemirembe Lwota, akizungumza wakati wa utoaji wa msaada huo
  Mkuu wa Taasisi ya Mo Dewji, Barbara Gonzales, akizungumza wakati wa utoaji wa msaada huo
  Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella (kushoto), akimpongeza Mbunge wa Viti Maalumu CCM mkoani Mwanza, Kemirembe Lwota, baada ya kufanikisha upatikanaji wa msaada 


  LakeFmHabari

  Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella, ameonya juu ya suala la uchafu kukithiri kwenye wodi za wagonjwa katika vituo vya kutolea huduma za afya ikiwemo hospitali ya rufaa ya Sekour Toure.

  Mongella ametoa onyo hilo hii leo wakati akikabidhi msaada wa vitanda, magodoro, mashuka pamoja na vyandarua, uliotolewa na mbunge wa Viti maalumu kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Mkoani Mwanza, Kemirembe Lwota.

  Ameeleza kusikitishwa na hali ya uchafu katika wodi za wagonjwa hususani akina mama katika Vituo vya Afya, Zahanati pamoja na Hospitali huku akikuta mashuka mpya yamehifadhiwa stoo kwenye baadhi ya vituo hivyo.

  “Na siyo hapa Sekour Toure tu, hata maeneo mengine, huwa nasikitika sana ninapokuta shuka chafu kitandani. Bahati mbaya nimewahi kwenda mahali nikakuta shuka mpya stoo, mimi nasema hizi shuka zitumike, zichakae, tutafute zingine”. Amesisitiza Mongella na kutaka suala la usafi kupewa kipaumbele zaidi.

  Mganga Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Dkt.Leonard Subi, amesema huduma za afya zinaendelea kuboreshwa licha ya kuwepo uhitaji mkubwa wa vitendea kazi ambapo kwa siku yanahitajika mashuka manane kwa kila kitanda.

  Mbunge wa Viti Maalumu CCM Mkoani Mwanza, Kemirembe Lwota, amewahimiza wadau wengine kujitokeza ili kusaidia kutatua kero za huduma za afya, huku akiishukuru taasisi ya Mo Dewji kwa kusaidia upatikanaji wa msaada huo ambao ni mashuka 100, vitanda 20, magodoro 20 pamoja na vyandarua 20 wenye thamani ya shilingi Milioni 25.

  Mkuu wa Taasisi ya Mo Dewji, Barbara Gonzales, amesema taasisi hiyo imedhamiria kusaidia uboreshaji wa huduma mbalimbali katika nyanza za elimu, afya pamoja na maendeleo ya jamii ili kuboresha zaidi maisha ya wananchi.


  0 0

  Na Jacquiline Mrisho - MAELEZO

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (anayeshughulikia Muungano na Mazingira) Mhe. January Makamba ameteua wajumbe wa Bodi ya wadhamini ya Mfuko wa Taifa wa Dhamana ya Hifadhi ya Mazingira Nchini (National Environmental Trust Fund - NETFUND).

  Waziri huyo amefanya uteuzi huo leo jijini Dar es salaam kufuatia uamuzi wa Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kumteua Ali Mafuruki kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Mfuko huo.

  Mh. Waziri Makamba amefanya uteuzi huo kwa mujibu wa Sheria ya mazingira Sura ya 191 ya mwaka 2004, kifungu cha 215 (2).

  Uteuzi huo ni kufuatia mabadiliko madogo yaliyofanyika hivi karibuni kwenye Sheria ya mazingira ambapo Bodi itakuwa na uwezo na mamlaka ya kualika mtu yeyote ambaye siyo mjumbe kushiriki katika maamuzi pale inapoona inafaa

  Amewataja wajumbe walioteuliwa kuwa ni Mwajuma Mbogoyo, Emelda Teikwa, Profesa Razak Bakari Lokina na Hatibu Senkoro.Wengine ni Alesia Mbuya, Baraka Juma Kalangahe,Dkt. Andrew Komba na Profesa Yunus Mgaya.

  Mhe. Makamba amesema kuwa uteuzi huo unaanza mara moja na kuwatakia kila la heri wajumbe wapya wa Bodi hiyo katika kutekeleza majukumu yao kama yalivyoainishwa katika Sheria.

  0 0

  *Ataka Wakuu wa Idara watoe ushauri wa kitaalamu bila woga   

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka Wakuu wa Idara kwenye Halmashauri za Wilaya na Manispaa wasaidie kutoa utaalamu badala ya kupingana na madiwani ili wawezeshe kuleta maendeleo kwa wananchi.

  Pia amewataka madiwani wasikilize ushauri wa kitaalamu unaotolewa na Wakuu wa Idara katika utekelezaji wa miradi iliyotengwa na Halmashauri.

  Ametoa wito huo leo mchana (Alhamisi, Januari 5, 2017) wakati akizungumza na watumishi mbalimbali wa Halmashauri ya Wilaya ya Mabada na viongozi na watendaji wa mkoa wa Ruvuma akiwa katika siku ya pili ya ziara yake mkoani humo.

  “Wakuu wa Idara nyie ni washauri. Tumieni taaluma zenu kutoa ushauri, semeni bila woga pale inapodidi. Ninawasihi waheshimiwa madiwani wasitumie fursa yao ya ‘kuazimia’ pale inapotokea kuna watumishi wenye msimamo,” amesema.

  Akizungumzia kuhsu ukusanyaji wa mapato, Waziri Mkuu amesema Serikali iko makini kwenye matumizi kwa kila senti inayokusanywa na akawataka watumishi hao kila mmoja aongeze mapato ya Serikali kupitia sekta aliyopo. Pia amepiga marufuku matumizi holela ya fedha za umma.

  “Kuanzia leo, marufuku kwa fedha iliyokusanya kwa mapato ya ndani kutumika bila utaratibu. Serikali hii haina mzaha na miradi inayotekelezwa chini ya viwango. Mtumishi ukiharibu hapa Madaba, usidhani utahamishwa, tunamalizana na wewe hapahapa. Wala usiombe ndugu yako akuombee uhamisho, tutakufuata hukohuko,” amesisitiza.

  Amewataka watumishi wa umma wote watumie Ilani ya Chaguzi ya CCM katika kutekeleza majukumu kwani inaeleza kila kitu ambacho Serikali inatakiwa kukifanya katika kipindi ca miaka mitano.

  “Zaidi ya hayo, ninawasihi kila Mkurugenzi atoe nakala ya hotuba ya Mheshimiwa Rais ambayo aliitoa Novemba 20, 2015 wakati akizindua Bunge la 11, awape watendaji wake waisome na kufanyia kazi maeneo yote aliyoyaainisha kwani ilitoa dira ya nini anataka kufanya katika Serikali hii,” amesema.

  Waziri Mkuu amesema Serikali kwa upande wake inaendelea kuboresha maslahi ya watumishi na imeanza kulipa madeni yaliyokuwa yamelimbikizwa. “Serikali imedhamiria kupunguza madeni ya watumishi na hadi kufikia Novemba 30, 2015 jumala ya sh. bilioni 28.9 zilikuwa zimekwishlipwa kwa watumishi 31,032 wenye madai katika sekta mbalimbali. Zoezi hili linaendelea.”

  Alitumia fursa hiyo kuwakumbusha watumishi wa wilaya hiyo wajibu wao wa kuwahudumia Watanzania bila kujali dini, itikadi, kabila au hali zao na akasisitiza kuwa Serikali haitamuonea mtumishi yeyote ambaye anatimiza wajibu wake.

  Akifafanua kuhusu upandishaji madaraja ya watumishi, Waziri Mkuu amesema Serikali imeondoa utaratibu wa mtumishi kulazimika kuandika barua ya kukiri kupandishwa daraja/cheo ndipo aanze kupata stahili zake mpya.

  "Hii imeondoa ucheleweshaji wa kufanyika marekebisho ya mshahara na pili imeondoa tofauti za mishahara kwa watumishi wenye ngazi moja (sifa sawa za kitaaluma, tarehe moja ya kuajiriwa) ambao walikuwa wakilipwa tofauti kwa sababu mmoja aliwahi kuandika barua ya kukiri na mwingine alichelewa kuandika barua kama hiyo hiyo, " amesema.

   IMETOLEWA NA
  OFISI YA WAZIRI MKUU
  ALHAMISI, JANUARI 5, 2017.

  0 0

    Katibu Mkuu wa CCM,Andulrahman Kinana akimnadi Mgombea wa Ubunge jimbo la Dimani Juma Ali Juma, katika uzinduzi wa kampeni za Uchaguzi mdogo wa Ubunge katika jimbo hilo, mjini Zanzibar, leo, Januari 5, 2017. (Picha na Bashir Nkoromo).
   Katibu Mkuu wa CCM akihutubia wananchi katika mkutano wa uzinduzi wa kampeni za CCM za uchaguzi mdogo jimbo la Dimani, Zanzibar, uliofanyika leo. (Picha na Bashir Nkoromo)
   Katibu wa NEC Itikadi na Uenez, Humphrey Polepole, akisalimia wananchi alipotambulishwa naKatibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, katika mkutano wa uzinduzi wa kampeni za CCM za uchaguzi mdogo wa Ubunge Jimbo la Dimani, Zanzibar, leo. (Picha na Bashir Nkoromo). 

   Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rodrick Mpogolo, akisalimia wananchi alipotambulishwa naKatibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, katika mkutano wa uzinduzi wa kampeni za CCM za uchaguzi mdogo wa Ubunge Jimbo la Dimani, Zanzibar, leo. (Picha na Bashir Nkoromo).
   Wananchi wakishangilia wakati wa mkutano wa uzinduzi wa kampeni za CCM za uchaguzi mdogo wa Ubunge jimbo la Dimani, Zanzibar leo.
   .Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Kanali Mstaafu, Ngemela Lubinga, akisalimia wananchi alipotambulishwa naKatibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, katika mkutano wa uzinduzi wa kampeni za CCM za uchaguzi mdogo wa Ubunge Jimbo la Dimani, Zanzibar, leo.
   Naibu Katibu Mkuu wa CCM VuaiAli Vuai akimkaribisha Katibu Mkuu wa CCM, Kinana
   Shamra shamra zikiendelea


  0 0
  0 0  Mkuu wa wilaya ya Tanga,Thobias Mwilapwa akizungumza wakati wa mkutano wa wananchi wa Kijiji cha Marungu ambao ni sehemu ya waathirka na mgogoro huo sambamba na muwekezaji wa shamba hilo na kusema kuwa makubaliano yaliyofikiwa baina ya serikali na wafugaji hao lazima yatekelezwe kwa wakati ili kuepusha vurugu za uvunjifu wa amani uliokuwa ukijitokeza mara kwa mara.
  Katibu Tawala wa wilaya ya Tanga(DAS),Faidha Salim akizungumza katika mkutano huo

  Diwani wa Kata ya Marungu (CCM) Mohamed Mambea akizungumza wakati wa mkutano huo
  Mkuu wa wilaya ya Tanga,Thobias Mwilapwa katikati akiandika baadhi ya maswali ya wananchi ambao walikuwa wakiuliza kwenye mkutano huo.


  Wananchi wakifuatilia mkutano wa hadhara wa Mkuu huyo wa wilaya.


  MKUU wa Wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa ameingilia kati mgogoro wa wafugaji na mwekezaji wa shamba la mkonge la Marungu Mkoani Tanga na kutoa miezi mitatu kwa wafugaji hao kuhakikisha wanaondoka katika shamba hilo kabla ya serikali haijatumia nguvu ya kuwahamisha.


  Akizungumza katika kikao cha wananchi wa Kijiji cha Marungu ambao ni sehemu ya waathirka na mgogoro huo sambamba na muwekezaji wa shamba hilo na kusema kuwa makubaliano yaliyofikiwa baina ya serikali na wafugaji hao lazima yatekelezwe kwa wakati ili kuepusha vurugu za uvunjifu wa amani uliokuwa ukijitokeza mara kwa mara.

  Maamuzi hayo yamekuja ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa agizo lililotolewa siku chache zilizopita na Mh;WAziri MKuu la kuwataka Wakuu wote wa Wilaya nchi nzima kuhakikisha wanamaliza migogoro ya ardhi iliyondani ya uwezo wao ili kutoa fursa kwa wananchi kuendelea na shughuli zao.

  Mwilapwa alisema kumekuwepo na madhara mengi yanayojiketokeza kutokana na kuwepo kwa migogoro ya wakulima na wafugaji hadi kufikia kutokea mapigano yanayohatarisha amani iliyopo baina ya makundi hayo mawili jambo ambalo serikali imejidhatiti kumaliza migogoro hiyo kwa makubaliano ya mazungumzo.

  “Kumekuwepo na mapigano ya mara kwa mara baina ya wakulima,mwekezaji na wafugaji jambo linalovunja amani na hata kuhatarisha maisha ya watu nisema ikiwa makubaliano haya hayatatekelezwa basi Serikali itaingilia kati na itawahamisha wafugaji hao kwa nguvu”Alisema Mwilapa.

  Kwa upande wa Diwani wa kata ya Marungu Mohamed Mwambea alisema kuwepo kwa wafugaji hao katika shamba hilo ndani Kijiji hicho kumeleta madhara makubwa kutokana na kutokea mapigano kwa pande hizo mbili na kutokea uharibifu wa mazao ya wananchi wanaojishughulisha na kilimo Kijijini hapo.

  Mwambea alisema imekuwa kawaida kwa wafugaji kushinda katika kesi zao dhidi ya wakulima jambo linaloshangaza wanapata wapi haki ya kuweza kushinda kila aina ya kesi zinazojitokeza baina ya wakulima na wafugaji.

  “Ifike wakati kwa Serikali iwe inatenda haki kwa wakulima dhidi ya wafugaji ili kujenga usawa kwa jamii hizo mbili ambazo zinaingia katika migogoro inayohatarisha maisha yao na hata jamii inayotuzunguka”Aalisema Mwambea.

  Nae Meneja wa shamba la mkonge la Marungu Casmir Joackim alisema wameshindwa kuendelea na uzalishaji katika shamba hilo kwa zaidi ya miaka miwili kutokana kuingiliwa na wafugaji hao waliohamishia shughuli zao za kifugaji na makazi katika shamba hilo.

  Joackim alisema dhamira ya muwekezaji wa shamba hilo ni kutekeleza agizo la Serikali ya awamu ya tano ya kuwataka wawekezaji wote nchini wayaendeleze mashamba yao kiuzalishaji na hata kutoa ajira kwa wananchi ili kukwepa mkono wa Serikali unaoweza kufuta hati ya umili wa shamba hilo na kurudishwa serikalini kwa ajili ya kugawiwa upya wananchi.

  “Ikiwa ndani ya shamba letu wapo wafugaji wanaendelea na shughuli zao za ufugaji pamoja na maisha kwa ujumla tangu mwaka 2014 ni namna gani tunaweza kundeleza shughuli zetu,huoni mkono wa Serikali unaweza kutukumba lazima tutendewe haki kwa hawa watu ambao ni wavamizi”Alisema Joackim.

  Habari kwa hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha

  0 0

  Katika kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya tano ya kuboresha hudumza za afya kwa mama na mtoto, Taasisi ya MO Dewji imetoa msaada wa vitanda 20, magodoro 20 na mashuka 100 kwa Hospitali ya SekouToure iliyopo mkoani Mwanza. Akizungumza katika hafla ya kukabidhi msaada huo, Mkuu wa Taasisi ya MO Dewji, Barbara Gonzalez amesema msaada huo ni sehemu ya malengo ya taasisi hiyo ya kuhakikisha inasaidia sehemu zenye uhitaji katika sekta ya afya, elimu na ustawi wa jamii. Amesema msaada huo unalenga kusaidia kupunguza vifo vya wanawake na watoto kwani kwa sasa idadi ni kubwa hivyo msaada huo utawezesha mkoa wa Mwanza kuongeza kasi ya mapambano ili kumaliza kabisa vifo vya wanawake na watoto. 
  Mkuu wa Taasisi ya MO Dewji, Barbara Gonzalez akizungumza kuhusu juhudi ambazo zinafanywa na taasisi hiyo kwa ajili ya kusaidia jamii na malengo ya kutoa msaada katika Hospitali ya Sekou Toure.

  "Tunafahamu kwamba asilimia 32 ya vifo vya watoto chini ya miaka mitano vinatokea katika siku 28 za mwanzo lakini pia tunaelezwa kuwa kila mwaka cha wanawake 8,000 hufariki dunia wakati wa ujauzito na wakati wa kujifungua kwa sababu ambazo zinaweza kuzuilika na sisi kitu cha kwanza tunachotaka ni kusaidia mapambano ya kupunguza vifo vya watoto na wanawake," amesema Barbara. Nae mgeni rasmi katika hafla hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella ameitaja Taasisi ya MO Dewji kuwa mfano wa kuigwa kwa msaada ambao wameutoa kwa hospitali ya mkoa huo na kuwaomba kuendelea kuwasaidia pindi wanapohitaji msaada zaidi.
  Mgeni rasmi katika hafla hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella akizungumzia mipango ya Serikali kuboresha huduma za afya lakini pia kuishukuru Taasisi ya MO Dewji kwa msaada ambao wamewapatia.

  "Ukimpa mama afya bora, umesaidia jamii nzima, jambo lililofanywa na Taasisi ya MO Dewji ni kubwa sana, hospitali zetu zinamahitaji makubwa sana na kwa hili ambalo wamefanya ni mfano wa kuigwa na watu wengine, tunawashukuru sana na tunawaomba muwe tayari kutusaidia kwa muda mwingine," amesema Mongella. Kwa upande wa Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Kemirembe Lwota amesema aliomba Taasisi ya MO Dewji kuwasaidia baada ya kuona changaoto nyingi ambazo zinawakabili wanawake ambao wanakwenda kujifungua katika Hospitali ya Sekou Toure na watoto ambao wanazaliwa.

  Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Kemirembe Lwota akieleza sababu ya kuiomba msaada Taasisi ya MO Dewji ili iwasaidie vitanda, magodoro na mashuka kwa ajili ya wodi ya wazazi.

  "Rais Magufuli alikuja hapa na hata yeye aliona changamoto ambazo zinatukabili na mimi kama mbunge niliamua kwenda kuzungumza na watu wa MO Dewji Foundation na napenda kuwashukuru kwa kukubali kutusaidia na naamini msaada huu utasaidia kupunguza baadhi ya changamoto ambazo zilikuwa zinatukabili," alisema Lwota.

  Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Dk. Leonard Subi akitoa taarifa ya Hospitali ya Sekou Toure.

  Nae Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Dk. Leonard Subi amesema hospitali hiyo licha ya changamoto ambazo zinawakabili inahudumia wagonjwa 500 kwa siku na kwa wanawake ambao wanafika kujifungua kwa siku wanakadiriwa kuwa kati ya 30 na 40.
  Mgeni rasmi katika hafla hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella akipokea msaada wa vitanda 20, magodoro 20 na mashuka 100 kutoka Taasisi ya MO Dewji.
  Mgeni rasmi katika hafla hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella akimshukuru Mkuu wa Taasisi ya MO Dewji, Barbara Gonzalez kwa msaada ambao wamewapatia.
  Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Sekou Toure Dk. Rweyendela Onesmo akitoa neno la shukrani.Mmoja wa wanawake ambao wamejifungua katika Hospitali ya Sekou Toure, Eveline Francis akiishukuru MO Dewji Foundation kwa msaada ambao wametoa kwenye hospitali hiyo.
  Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Kemirembe Lwota na Mkuu wa Taasisi ya MO Dewji, Barbara Gonzalez wakimjulia hali Zuwena Mohammed baada ya hafla ya kukabidhi msaada.
  Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Kemirembe Lwota, Mkuu wa Taasisi ya MO Dewji, Barbara Gonzalez, Mwenyekiti wa UWT Mwanza, Ellen Bagohe na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Dk. Leonard Subi wakiwa katika picha ya pamoja.Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Kemirembe Lwota, Mkuu wa Taasisi ya MO Dewji, Barbara Gonzalez, Mwenyekiti wa UWT Mwanza, Ellen Bagohe na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Dk. Leonard Subi wakiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Hospitali ya Sekou Toure.
  Mkuu wa Taasisi ya MO Dewji, Barbara Gonzalez akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella. Kulia ni Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Kemirembe Lwota.
  Mkuu wa Taasisi ya MO Dewji, Barbara Gonzalez akiagana na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella.

  0 0

  Kaimu Meenja Uhusiano TANESCO, Bi.Leila Muhaji


  NA K-VIS BLOG.
  SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO) limesema, kwa sasa linafanya mabadiliko ya uongozi wa ndani ya Shirika kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu za Shirika kwa lengo la kuongeza ufanisi zaidi na kazi hiyo ambayo tayari imeanza itakapokamilika, Umma wa Watanzania utahafahimshwa kupitia vyombo vya habari.

  Taarifa fupi iliyotolewa na Ofisi ya Uhusiano Makao Makuu TANESCO leo Januari 5, 2017 imeviomba vyombo vya habari vitoe fursa fursa kwa Mamlaka husika kuendelea kukamilisha zoezi hili muhimu kwa maendeleo ya Shirika na Taifa kwa ujumla na taarifa rasmi itatolewa baada ya zoezi kukamilika.


  0 0

  Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

  Meneja wa mwanamuziki wa anayefanya vizuri katika soko la muziki wa bongo fleva nje na ndani ya nchi, Naseeb Abdul ‘Diamond’ , Hamisi Taletale ‘Babu tale’ amekanusha taarifa zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii na vyombo vya habari kuwa msanii Q Chief Kajiunga na kundi la wasafi.

  Babu tale amesema hayo alipokuwa akizungumza na ripota wa globu ya jamii juu ya taharifa za msanii huyo kujiunga na WCB.

  “Ninachokwambia mimi kama Meneja kuwa Q Chief kaja kutembea tu kama wanavyokuja kutembea wasaniii wengine, hivyo kuonekana pale sio ndio tunataka kumsajili tuwe nae,wasafi kama wasafi itabaki na watu wale wale” amesema Babu tale.

  WCB ni kundi la muziki liliasisiwa na Msanii wa Bongofleva almaarufu kwa jina la Diamond, liomeonesha kuwa na mafanikio makubwa katika kipindi kifupi kwa kuwezesha wasanii wa hapa nchini kufanya kazi kimataifa kuliko ilivyozoeleka awali.

  Katika kipindi cha mwaka 2016 kundi hilo limefanikiwa kuwasajili wasanii wengine kadhaa akiwemo msanii Rich Mavoko pamoja na Harmonize ambaye kwa sasa wote wanafanya vizuri.

  0 0

  Mkuu wa mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo akizungumza katika mkutano wa Wadau wa Afya uliofanyika kwenye ukumbi wa halmashauri ya Meru,kushoto ni Mganga Mkuu wa mkoa,Dk frida Mokiti.

  Nteghenjwa Hosseah, Arusha

  Mganga Mkuu wa Mkoa wa Arusha Dokta Frida Mokiti amesema kuwa uhaba wa vituo vya afya katika maeneo ya pembezoni mwa miji umekua ukichangia vifo vya mama wajawazito na watoto kutokana na kutembea umbali mrefu kutafuta huduma hiyo.

   Akizungumza katika Kikao kazi cha Mkoa kinachojadili hali ya afya ya mkoa, Dr. Mokiti amesema kuwa juhudi za makusudi zinahitajika kuhakikisha kuwa huduma za afya kwa mama na mtoto zinapatikana kwa urahisi ili kupunguza tatizo hilo ambalo limekua likirudisha nyuma afya ya wakina mama pamoja na kukatisha maisha yao.

   Akizungumza katika Kikao hicho Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo amewaagiza Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi kuhakikisha kuwa wanajenga Kituo cha Afya katika kila tarafa ili kusogeza karibu huduma za afya kwa wananchi pia amewataka viongozi kuweka mipaka katika maeneo ya zahanati ili kuepuka uvamizi wa maeneo hayo yanayowahudumia watu.

  “Wakati sasa umefika wa kuhakikisha tunatokomeza kabisa changamoto hii ya vifo vya mama na mtoto, inasikitisha sana kuona mama anafariki wakati wa kujifungua kwa sababu tu amekosa huduma ya afya karibu na makazi yake,lazima tuwalinde na kuwajali wananwake, kwa sababu bila ya wao kujifungua hata sisi tusingekuwepo” Alisema Gambo.

  Aliongeza kuwa Kila Halmashauri ihakikishe inatenga Fedha kwenye mapato yake ya ndani halkadhalika Ruzuku toka Serikali Kuu ielekezwe kwenye Miradi ya Afya na tuendelee kutafuta wadau watakaotusaidia katika utekelezaji wa miradi hii bila kusahau uhamasishaji wa nguvu za wananchi kwa Pamoja tutatokomeza tatizo hili.

   Kwa upande wake Mkazi wa Arusha   Hussein Igunge na Mkuu wa Wilaya ya  Longido Mhe. Daniel Chongolo  wameitaka serikali iboreshe huduma za afya ikiwemo upatikanaji wa madawa kwa wale waliokata bima ili waweze kunufaika na bima zao pamoja na uhaba wa watumishi katika sekta ya afya.
  Mganga Mkuu wa mkoa wa Arusha,Dk Frida Mokiti akizungumza katika mkutano wa Wadau wa Afya uliofanyika kwenye ukumbi wa halmashauri ya Meru,kulia ni Mkuu wa mkoa,Mrisho Gambo akimsikiliza kwa makini,kushoto ni Katibu Tawala wa wilaya ya Karatu na Katibu Tawala mkoa wa Arusha,Richard Kwitega.
  Baadhi ya Watalaam wa sekta ya afya wakiwa kwenye mkutano huo uliofanyika kwenye ukumbi wa halmashauri ya Meru mkoa wa Arusha.
  Baadhi ya viongozi wa dini walioshiriki mkutano huo wakisikiliza kwa makini pia waliahidi kushirikiana na mfuko wa Bima ya Afya(NHIF)kuhamasisha waumini wao kujiunga na mfuko wa CHF.
  Wakuu wa wilaya za mkoa wa Arusha wakiwa kwenye mkutano huo uliojadili kwa kina mikakati ya kuinua sekta ya Afya kutoka kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Arusha,Gabriel Daqarro,Mkuu wa wilaya ya Monduli,Idd Kimanta na Mkuu wa wilaya ya Karatu,Theresia Mahongo.

  0 0

   Naibu Waziri ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI) Seleman Jafo wa kati kati akiwa katika boti maeneo ya nyamisati mto Rufiji kwa ajili ya kujiandaa na safari ya kwenda kuwatembelea wananchi wa Wilaya ya Rufiji hususan wale wanaoishi katika maeneo ya Delta ikiwa ni ziara yake ya kikazi Mkoani Pwani ya kukagua miradi  mbali mbali ya maendeleo(PICHA NA VICTOR MASANGU)
  Naibu Wazari Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI) Seleman Jafo wa kati kati akiwa kwenye boti katika ziara yake ya kikazi katika Wilaya ya Kibiti na viongozi wengine wa serikali,na wa kwanza kulia  kwake ni Mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Kibiti Khatibu Chaurembo kwa ajili ya safari ya kwenda kuwatembelea wananchi wa maeneo ya Delta kwa ajili ya kukagua miradi ya  mbali mbali maendeleo.(PICHA NA VICTOR MASANGU)  


  NA VICTOR MASANGU, KIBITI

  LICHA ya serikali ya awamu ya tano kuongeza juhudi za kuboresha sekta ya afya katika maeneo mbali mbali hapa nchini bado sehemu nyingine utoaji wa huduma hali bado ni tete kutokana na kukabiliwa na changamoto mbali mbali ikiwemo ukosefu wa wauguzi,madaktari, madawa, magari ya kubebea wagonjwa,vitanda pamoja na vifaa tiba hivyo kusababisha wagonjwa kupata shida kubwa pindi wanapokwenda kupatiwa matibabu.

  Changamoto hizo ambazo zinadaiwa ni sugu na hazijafanyiwa utekelezaji wowote zimeweza kubainika baada ya Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Japo kufanya ziara yake ya kikaz ya siku mbili kwa wananchi wa Wilaya ya Kibiti Mkoa wa Pwani hususan katika maeneo ya wananchi wanaoishi katika maeneo ya Delta kwa ajili ya kukagua miradi mbali mbali ya maendeleo pamoja na kubaini changamoto za muda mrefu zilizokuwa zinawakabili ili kuweza kuzitafutia ufumbuzi.

  Kutokana na kuwepo kwa hali hiyo Mwandishi wa habari hizi aliweza kuzungumza na baadhi ya wakinamama ambao ndio wameonekana kuguswa zaidi katika afya akiwemo Fatma Mbashilu na Hafiswa Hamada wametoa kilio chao kwa Naibu Waziri huyo na kuweka bayana changamoto zinazowakabili wakati wa kujifungua kwani wanapandishwa katika kitanda cha kamba ambacho sio salama na kinawaumiza sambamba na kijifungulia kwa kutumia mwanga wa kibatali kutokana na eneo hilo la visiwani kutokuwa na nishati ya umeme.

  “Sisi katika kijiji chetu hususan kinamama wajawazito kwa sasa tunakabiliwa na changamoto nyingi hasa katika upatikanaji wa kupewa huduma, kwani kwa sasa tunajifungulia katika kitanda cha kamba kwa hiyo tunajikuta wakati wa kujifungua tunapata maumivu mara mbili, kwa hiyo tunamwomba Waziri Jafo kwa kuwa ameamua kuja kututembelea huku visiwani atusaidie sisi wakinamama,”walisema kwa uchungu wakinamama hao.

  Aidha walisema mbali na kukabiliwa na changamoto hiyo ya kitanda pia kero yao nyingine kubwa ni kutokana na kutumia mwanga wa kibatari katika kujifungulia na wakati mwingine wanakosa kabisa hela ya kununulia mafua ya taa, hivyo wanajikuta wanapata shida sana hasa katika nyakati za muda wa usiku wanakuwa katika hali ya sintofahamu.

  Pia wakinamama hao walimpongeza Jafo kwa kuamua kwenda kuwatembelea katika maeneo ya delta wanayoishi kwani kwa kipindi kirefu hawajawahi kuona kiongozi mkubwa wa kitaifa wa serikali ambaye amekwenda kuwajulia hali, hivyo ujio wa waziri huo utaweza kuleta mabadiliko chanya katika kuleta maendeleo kwa wakazi wanaoishi maeneo hayo.

  Naye Mganga mfawidhi wa zahanati ya Mchinga Kuluthumu Zuberi amekiri kuwepo kwa tatizo la kipindi cha muda mrefu kwa wakinamma hao kujifungulia katika mazingira amabayo sio rafiki kwa upande wao kwa kutumia kitanda kilichojengwa kwa miti na kamba ambapo amedai kiafya sio nzuri hivyo serikali inapaswa kuwasaidia ili kuboresha utoaji wa huduma kwa wagonjwa.

  Akijibu malalamiko ya hayo ya wananchi Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Seleman Jafo ambaye alionekana kuchukizwa na kuwepo kwa hali hiyo aliamua kuchukua maamuzi magumu na kwa kupiga marufuku kabisa tabia ya kuona wauguzi au madaktari kuwalaza wakinamama wajawazito katika vitanda vya kamba pindi wanapokwenda kujifungua kwani kufanya hivyo kuna hatarisha usalama wa uhai wa mama na mtoto anayezaliwa.

  Jafo alisema kuwa serikali ya awamu ya tano lengo lake kubwa ni kihakikisha kwamba wanaboresha sekta ya afya kuanzia ngazi za vijijini hivyo wamejipanga vilivyo katika kuzitatua changamoto zinazowakabili wananachi ili kuweza kuwapatia huduma nzuri, na kuongeza kuwa ameshamwagiza mkurugenzi wa halmashauri ya Kibiti kupeleka kitanda katika zahanati ya kijiji cha Mchinga ili wakinamama waondokana na kero hiyo ya kujifungulia katika kitanda cha kamba.

  “Ninaagiza kuanzia sasa sitaki kuona wakinamama wajawazito wanajifungulia wakiwa katika kitanda cha miti, hii kwa upande wangu sipapendezwa nayo hata kidogo kwani inahatarisha maisha ya mama pamoja na mtoto wake kwa hivyo viongozi wa Wilaya ya Kibaiti kwa hili naomba mlifanyie kazi kwa haraka kupeleka kitanda kingine,”alisema Jafo.

  Aidha katika hatua nyingine Jafo amewaagiza viongozi wa halmashauri ya Kibiti kuachana na tabia ya kufanya kazi kwa mazoea na badala yake wajikite zaidi kuwahudumia wananchi wao ikiwa sambamba na kuweka kipaumbele zaidi katika kutenga bajeti kwa ajili ya ununuzi wa madawa ya kuwatibu wagonjwa wakati wote hasa katika zahanati zote zilizopo katika maeneo yote yaliyozungukwa na maji Delta.

  Naibu Wazari huyo kwa sasa yupo anaendelea na ziara yake ya kikazi katika  Mkoani Pwani ikiwa ni moja kukagua miradi mbali mbali ya maendeleo pamoja na kuweza kuibaini changamoto mbali mbali zinazowakabili wananchi hasa wale hasa wale wanaoishi vijijini ambao wamekuwa wakisahaulika na viongozi wao na kujikuta wanakosa mahitaji na huduma mbali mbali za msingi ikiwemo, afya, elimu, maji hivyo kuwafanya waishi katika mazingira magumu na kushindwa kufanya shughuli za kimaendeleo.

  0 0

   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimjulia hali Sophia Mgeni ambaye ametoka kujifungua mtoto wa kike, Waziri mkuu alitembelea Zahanati ya Madaba iliyopo wilaya ya Songea ili kuwasikiliza wagonjwa katika zahanati hiyo Waziri mkuu yupo Mkoani Ruvuma kwa ziara ya kukagua shughuli za maendeleo 
   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na wauguzi wa zahanati ya Madaba huku akiwataka waendelee na moyo waliokuwa nao wa kuwapenda wagonjwa na kuwahudumia, kwani serekali inatambua mchango wao wanaoutoa kwa taifa
  Waziri Mkuu Kassim  Majaliwa akiwahutubia wananchi wa madaba waliojitokeza kwa wingi kumsikiliza,Waziri Mkuu alitumia nafasi hiyo kuwaelezaa  Wananchi hao juhudi za serekali za kuwasaidia katika sekta mbali mbali ikiwemo Huduma ya bima ya afya.  Waziri mkuu yupo mkoani Ruvuma kwa ziara ya kikazi.Picha na Chris Mfinanga

  0 0


  Mkuu wa Wilaya ya Makete Veronica Kessy

  HERI YA MWAKA MPYA!

  Ndugu wananchi wa Makete na Watanzania wote kwa ujumla,wananchi wa kijiji cha Isapulano katika kata ya Isapulano hapa Wilayani Makete wamepatwa na maafa mnamo tarehe 02/01/2017

  Maafa hayo yalisababishwa na mvua kubwa iliyoambatana na upepo,jumla ya nyumba 16 zenye jumla ya watu 37 ziliathirika kwa viwango tofauti.Katika tukio hilo waliumia watu wawili,wakapatiwa matibabu katika Zahanati ya Isapulano na kwa bahati nzuri wanaendelea vizuri,Aidha tunamshukuru Mungu hakuna mwananchi aliyefariki

  Ndugu wananchi nyumba hizo zinahitaji vifaa vya ujenzi yaani matofali, saruji, mbao, misumari, mabati n.k, pia wananchi walioathirika wanahitaji kusaidiwa mahitaji ya kibinadamu kwa hiyo nawaomba wananchi na wadau wote wa ndani na nje ya Wilaya ya Makete tuguswe kwa namna moja ama nyingine kuchangia fedha au vitu ili kuwasaidia wananchi hao

  Kwa sasa wananchi hao wamehifadhiwa na majirani na ndugu zao,Aidha wananchi wa kijiji hicho wameanza kujitolea kusaidia ujenzi huo .Ninawashukuru na kuwapongeza kwa jitihada hizo,nawasihi tuwaunge mkono kwa kutoa misaada ya hali na mali,michango ya fedha iingizwe kwenye Akaunti ifuatayo iliyopo NMB MAKETE

  Jina la Akaunti:Kijiji cha Isapulano
  Namba ya Akaunti:60410004408

  Na msaada wa vitu au vifaa uwasilishwe kwa Mtendaji wa kata ya Isapulano Bi.Tabu Mohamed mwenye namba 0745571046

  Ahsanteni sana 
  Ni mimi Veronica Kessy 
  Mkuu wa Wilaya ya Makete

  0 0

  Usikose kufuatilia maombezi na ibada ya neno la Mungu kutoka kwa Mchungaji Dkt.Daniel Moses Kulola wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya lililopo Sabasaba Jijini Mwanza, mubashara (live) kupitia ukurasa wake wa facebook.

  Ni kila siku ya alhamisi kuanzia saa nane kamili mchana kupitia ukurasa wake wa facebook wa DANIEL KULOLA ambapo mahubiri na maombezi yatarushwa moja kwa moja (mubashara) kwa njia ya video.

  0 0

  Waziri wa Maliasili na Utalii,Prof,Jumanne Maghembe akitoa hotuba yake wakati wa hafla ya uzinduzi wa Bodi ya Wadhamini ya Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) iliyofanyika katika ukumbi wa Mahakama ya Afrika jijini Arusha.
  Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Maliasili na Utalii,Prof ,Jumanne Maghembe .
  Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Mkuu wa Majeshi Mstaafu ,Jenerali George Waitara akifuatilia hotuba ya uzinduzi wa Bodi hiyo iliyotolewa na Waziri wa Maliasili na Utalii ,Prof,Jumanne Maghembe.
  Waziri wa Maliasili na Utalii,Prof Jumanne Maghembe akimkabidhi vitendea kazi Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Allan Kijazi ambaye pia ni mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Tanapa .
  Waziri wa Maliasili na Utalii,Prof Jumanne Maghembe akimkabidhi vitendea kazi Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Tanapa Dkt Chanasa Mpelumbe Ngeleja.
  Waziri wa Maliasili na Utalii,Prof Jumanne Maghembe akimkabidhi vitendea kazi Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Tanapa Prof Wineaster Anderson
  Waziri wa Maliasili na Utalii,Prof Jumanne Maghembe akimkabidhi vitendea kazi Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Tanapa Prof,Alexander Songorwa.
  Waziri wa Maliasili na Utalii,Prof Jumanne Maghembe akikabidhi vitendea kazi Devota Mdachi mjumbe wa bodi ya Wadhamini wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) .
  Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Mkuu wa Majeshi Mstaafu ,Jenerali George Waitara akitoa salam zake wakati wa uzinduzi wa Bodi hiyo uliofanika katika ukumbi wa Mhakama ya Afrika jijini Arusha.
  Waziri wa Maliasili na Utalii,Prof Jumanne Maghembe akifurahia jambo na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini iliyomaliza muda wake Modestus Lilungulu walpkutana katika hafla fupi ya uzinduzi wa bodi mpya .
  Mkurugenzi wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Allan Kijazi ambaye pia ni mjumbe wa Bodi hiyo akifanya utamburisho wa wajumbe wa bodi ya Wadhamini wa shirika hilo.
  Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya TANAPA,Prof,Wineaster Anderson ambaye pia ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Taasisi ya Maliasili na Utalii endelevu Afrika (NARESTi Africa) akitamburishwa kwa wafanyakazi wa Shirika hilo.
    Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya TANAPA, Dkt Lucy Lugwisa kutoka Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira akitamburishwa kwa wafanyakazi wa Shirika hilo.
    Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya TANAPA,Prof,Alexander Songorwa ambaye pia ni Mkurugenzi wa Wanyamapori kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii akitamburishwa kwa wafanyakazi wa shirika hilo.
    Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya TANAPA,Kamishna Marijani Nsato ambaye pia ni Mkuu wa Operesheni na Mafunzo Makao Makuu ya jeshi la Polisi akitamburishwa kwa wafanyakazi wa shirika hilo.
    Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya TANAPA,Dkt Chanasa Mpalumbe Ngeleja ambaye pia ni Daktari Mkuu wa Mifugo ,Wizara ya Kilimo ,Mifugo na Uvuvi akitamburishwa kwa wafanyakazi wa shirika hilo.
    Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya TANAPA,George Fumbuka ambaye pia ni Mtendaji Mkuu na Mwenyekiti wa Kampuni ya Core Securities akitamburishwa kwa wafanyakazi wa shirika hilo.
  Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya TANAPA,Devota  Mdachi ambaye pia ni Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii nchini akitamburishwa kwa wafanyakazi wa Shirika hilo.
  Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) iliyomaliza muda wake ,Modestus Lilungulu akitoa salam zake wakati wa uzinduzi rasmi wa Bodi mpya ya Wadhamini ya TANAPA.
  Baadhi ya wafanyakazi wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) wakifuatilia uzinduzi huo uliofanyika katika ukumbi wa Mahakama ya Afrika jijini Arusha.
  Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA),Mkuu wa Majeshi Mstaafu,Jenerali George Waitara (kushoto) akizungumza jambo na Waziri wa Maliasili na Utalii,Prof ,Jumanne Maghembe mara baada ya kuzinduliwa kwa Bodi hiyo.katikati ni Mkurugenzi wa TANAPA,Allan Kijazi.
   Waziri wa Maliasili na Utalii,Prof Jumanne Maghembe akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) muda mfupi baada ya bodi hiyo kuzinduliwa.
   Waziri wa Maliasili na Utalii,Prof Jumanne Maghembe pamoja na Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) wakiwa katika picha ya pamoja na Wakurugenzi wa idara mbalimbali katika shirika hilo.
  Waziri wa Maliasili na Utalii,Prof Jumanne Maghembe pamoja na Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) wakiwa katika picha ya pamoja na mameneja katika shirika hilo. 

  Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kasazini.

  0 0

   Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaji Mussa Mbaruku kushoto akimkabidhi rangi Ustadhi wa Madrasat Ikhilaswi ,Ibrahim Hassani Mtaa wa Mwarongo Kata ya Marungu kwa ajili ujenzi wa msikiti huo
   Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaji Mussa Mbaruku akisoma risala ya Madrasat Ikhilaswi mara baada ya kukabidhiwa baada ya kwenda kuwatembelea na kukabidhi msaada wa makopo ya rangi kwa ajili ya ujenzi unaoendelea
  Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaji Mussa Mbaruku akuzungumza na wanafunzi wa Madrasat Ikhilaswi wakati alipotembelea kuona changamoto wanazokabiliana nazo ikiwa ni ziara yake lakini pia aliwakabidhi makopo ya rangi
  Hili ni Jengo la Madrasat Ikhilaswi lililopo mtaa wa Mwarongo Kata ya Marungu Jijini Tanga muonekano wake.habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha

  0 0


  By Jumia Travel Tanzania

  2016 is over, and has been substituted by 2017 towards a long-run of 12 months to come. The tourism sector is still a strong foreign exchange earner, generating US $ 2.2 billion during the previous year.

  According to a report by the Tanzania Minister of Finance and Planning, Dr. Phillip Mpango, about 1,020,816 tourists entered the country in the duration between January and October 2016.

  The hotel business involves several categories of customers such as business and leisure travelers. These two types of travelers have got their preferences and in order to win them, hoteliers must make sure they meet their needs and wants. Jumia Travel (www.travel.jumia.com) shares the differences between business and leisure travelers.


  Business travelers

  Location is key to them: Business travelers are very selective with the location where they will stay due to their tight schedules. For example, being at a hotel just a few meters away from a conference center is an advantage to them. Therefore, this is a key point to be noted by hotel managers when they market their hotels.

  To be connected all the time: Business travelers like to stay in a place where there is a guaranteed electricity, and internet connection. This will guarantee a full-time connection for their devices such as laptops or smartphones as well as be assured to get in touch with their clients and colleagues.

  Loyalty: Hotel managers should invest in winning their customers’ loyalty. For instance, business travelers have a tendency to stay in the same hotel regularly once offered the best services. Most importantly, they rarely find enough time to look for other alternatives due to their fixed schedules.

  Collective services at one point: Business travelers prefer a place with all their necessary services available, to simplify their routines. For example, services such as breakfast, coffee maker or ironing in the morning. Hence, a hotel with such amenities has got a chance to fit this kind of travelers.


  Leisure travelers

  Cost sensitive: Since they are traveling for leisure, this group usually is searching for best hotel deals to cater their needs. To win leisure travelers, hotel managers must be clever in offering best price deals to beat others in the market.

  Consider reviews and recommendations: Most of the time leisure travelers seek advice from their family, friends and colleagues before making decisions. Recommendations from their closest people do matter a lot and play a great role towards their decision making. From this point, hoteliers must consider following and working on reviews left by their customers on different platforms.

  Attracted to special offers: There is nobody who doesn’t like an offer, and since this group’s top priority is to have leisure, they consider much hotels which offering the best offers to them. Hoteliers are advised to be very creative in designing special treatment to their customers.

  Exceptional services: Exceptionality in business must be highly considered so as to differentiate your business among others in the same field. Leisure travelers like to go to places having unique amenities such as fitness gym, spa services, water sports, a boat trip to an island and so forth.


  In order to have a successful business, one must be aware of the needs and preferences of the customers for both business and leisure categories.


  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wenyeviti wa TPSF,CTi,TCCIA na ZNCCIA juu ya mpango wa kibiashara unaojulikana kama China One Belt, One Road ulio asisiwa na serikali ya China na unajumuisha bara la Asia, Mashariki ya Kati,Ulaya na Afrika, Ikulu jijini Dar es Salaam.
   
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Wenyeviti wa TPSF,CTi,TCCIA na ZNCCIA juu ya mpango wa kibiashara unaojulikana kama China One Belt, One Road ulio asisiwa na serikali ya China na unajumuisha bara la Asia, Mashariki ya Kati,Ulaya na Afrika.
                                 .......................................................................
  Jitihada za Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan za kuiingiza Tanzania katika mpango mkubwa wa Biashara kwenye bara la Asia, Mashariki ya kati,Ulaya na Afrika  umefanikiwa baada ya Tanzania kuchaguliwa kuwa miongoni mwa nchi Saba kuingizwa katika mpango unaojulikana kama China One Belt, One Road Stratergy.


  Nchi nyingine ambazo zimechanguliwa kuingizwa kwenye mpango huo ni Malaysia,Sri lanka, Nepal, Bangladesh,Pakistan na Thailand.

  Baada ya Tanzania kuingizwa rasmi katika mpango huo, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ambaye pia Mjumbe katika jopo la Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa la kumuwezesha mwanamke kiuchumi akiwakilisha nchi za ukanda wa Kusini na Mashariki mwa Afrika amekutana na Watendaji kutoka Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF),Chama cha Wafanyabiashara wenye Viwanda na Biashara (TCCIA) na Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI) kuwaeleza kuhusu muhimu wa Tanzania kuingizwa kwenye mpango huo.


  Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amesema Tanzania imepata uanachama wa mpango huo baada ya kukutana na kufanya mazungumzo na Mfanyabiashara wa Madini na Vito kutoka China Dkt Helen Lau kuhusu manufaa ya mpango huo na Makamu wa Rais alimwomba Mfanyabiashara huyo kuisaidia Tanzania kuingia kwenye mpango huo China One Belt, One Road Stratergy jambo ambalo limefanikiwa.

  Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ameeleza kuwa Mwezi Septemba mwaka 2016 ulifanyika mkutano Guangdong nchini China kujadili maombi ya kujiunga na mpango huo ambapo Makamu wa Rais alimwomba Dkt Helen kuiwakilisha Tanzania katika kuwasilisha maombi na kwa bahati nzuri ombi la Tanzania lilikubaliwa na kupata uanachama katika mpango huo mkubwa wa China One Belt, One Road.  Makamu wa Rais amesema kuwa moja ya fursa zinazotolewa na Serikali ya China katika mpango huo ni kila nchi Mwanachama kupewa vyumba vya ofisi katika jengo linaloitwa 21stCentury Maritime Silk Road Expo bila kulipa kodi ya pango kwa miaka Mitatu na baadhi ya vyumba vya jengo hilo vitatumiwa na nchi husika kuonyesha na kutangaza bidhaa zao.

  Kufutia Tanzania kuingizwa kwenye mpango, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amewaagiza watendaji wa sekta binafsi alikutana nao ikulu jijini Dar es Salaam wajipange na kuweka mikakati ya namna ya kunufaika na mpango huo haraka iwezekanavyo.

  Amesisitiza kuwa mpango huo wa China One Belt, One Road Stratergy uliobuniwa na serikali ya China kwa dhamira ya kuzikutanisha Jumuiya za Wafanyabiashara za  Mashariki mwa bara Asia, Mashariki ya kati, Ulaya na Afrika kwa ajili ya kubadilishana mawazo,kuonesha njia na kupeana ushauri wa jinsi ya kukuza biashara kati ya nchi wanachama wa mpango huo kwa lengo la kuiwezesha sekta ya biashara kuchangia nyema kwenye uchumi wa mataifa yao.
   
  Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amesema Tanzania baada ya kuingia kwenye mpango huo itanufaika na fedha za mfuko kwa ajili ya maendeleo ya miundombinu ambazo zinatolewa kwa nchi zilizojiunga na mpango huo.

  Kwa upande wake, Mweyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania Godfrey Simbeye na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Wenye Viwanda na Wakulima Zanzibar Taufik Turki wamemuahidi Makamu wa Rais kuwa watatumia fursa hiyo ipasavyo ili kukuza biashara kati ya Tanzaniana Nchi wanachama wa mpango huo.

  0 0

  Kutoka kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Mwanza, mbunge viti maalumu CCM Mkoani Mwanza, Mkuu wa Mo Dewji Foundation, Mwenyekiti wa UWT mkoani Mwanza pamoja na wadau wengine, wakiwa kwenye wodi ya akina mama hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mwanza, kujionea hali ya wodi hiyo.

  LakeFmHabari
  Baadhi ya akina mama waliojifungulia katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mwanza Sekou Toure, wameishukuru serikali pamoja na wadau wengine wa afya kwa kuendelea kuboresha huduma za afya katika hospitali hiyo.

  Akina mama hao wameyasema hayo jana baada ya mbunge wa viti maalumu kupitia Chama cha Mapinduzi mkoani Mwanza, kukabidhi msaada wa vitanda, magodoro, mashuka na vyandarua katika hospitali hiyo.

  Wamesema hivi sasa huduma za afya hususani kwa mama na mtoto zimeboreshwa katika hospitali hiyo ikilinganishwa na kipindi kilichopita ambapo wameomba maboresho zaidi yaendelelee ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za afya.

  Mganga Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Dkt.Leonard Subi amesema huduma za afya zinaendelea kuboreshwa katika halmashauri mbalimbali mkoani Mwanza huku msisitizo ukiwa ni kuwahamasisha akina mama kujifungulia kwenye vituo vya afya.

  Mbunge wa viti maalumu kupitia Chama cha Mapinduzi mkoani Mwanza, Kemirembe Lwota kwa kushirikiana na taasisi ya Mo Dewji amesaidia upatikanaji wa mashuka 100 pamoja na vitanda 20 vilivyoambana na magodoro pamoja na vyandarua.

  0 0

   Mkuu wa wilaya ya Mbulu, Chelestino Mofuga  akizungumza na wananchi wa kijiji cha Gidmadoy baada ya kusikiliza mgogoro wa mapato na matumizi uliodumu tangu 2014 hadi 2016. Mkuu wa wilaya aliagiza kukamatwa mtendaji wa kijiji ambaye alihamishwa kinyume cha utaratibu kukimbia madeni na kumweka ndani masaa 48.

   Pia mkurugenzi aliagizwa kukagua taarifa ndani ya siku saba na kuleta taarifa kwa wananchi. Pia mkurugenzi aliagizwa kutuma watalaam wa ardhi kukagua maeneo yaliyopimwa na kulalamikiwa na wananchi. Wananchi walikiri hawajawahi kutembelewa na Mkuu wa wilaya au kiongozi wa wilaya tangu kuanzishwa kwa kijiji hicho kwake
  Baadhi ya wananchi wakimsikiliza mkuu wa wilaya Mbulu


older | 1 | .... | 1091 | 1092 | (Page 1093) | 1094 | 1095 | .... | 1896 | newer