Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46395 articles
Browse latest View live

TGN YAANDAA WARSHA YA KUCHANGIA SERA MPYA YA ARDHI KWA KUWASHIRIKISHA WADAU MBALIMBALI

$
0
0
Na Amina Kibwana,Globu ya Jamii

Mtandao wa Jinsia (TGNP) imeandaa warsha ya kuchangia sera mpya ya ardhi kwa kuwashirikisha wadau mbalimbali kupitia fursa yake iliyopata kutoka Wizara ya ardhi maendeleo na makazi ili kuweza kujua namna ambavyo jinsia imeibuka katika kuchangia sera hii.

Akizungumza na Waandishi wa habari jijini dar es Salaam, Meneja Idara ya Ujenzi wa nguvu za pamoja Grace Kisetu, amesema kuwa katika warsha hiyo wameweza kuwashirikisha wadau mbalimbali kutoka katika Halmashauri wanazofanyia kazi zikiwemo Kishapu,Morogoro,Mbeya,Mara  na Shinyanga  pamoja na asasi zisizokuwa za kiserikali na wanajamii kutoka sehemu ambazo tunafanyia kazi na baadhi ya washiriki kutoka wizra ta ardhi.

“Tumeamua kuwashirikisha wadau hao ili waweze kutusikiliza na kujua chambuzi ambazo tumeweza kuzifanya ili waweze kujua ni lipi tunaloliona kwamba kwenye rasimu walioitoa pengine linahitaji kuboreshwa zaidi hususani tukiangalia je jinsia ni ninsi gani imechukuliwa na kuweza kujitokeza kwenye hiyo sera ya ardhi ya mwaka 2016”

Kwa upande wake Muwezeshaji wa warsha hiyo Magdalena Luwevangila ameongeza kuwa katika Warsha hii tunaangalia jinsi gani sera inaweza ikakidhi mahitaji ya watu wote hususan katika masuala ya kijinsia,wanawake watoto,wanaume na watu waliopo pembezoni ili iweze kufanya kazi na kumaliza migogoro ya ardhi mara tu inapojitokeza.

” migogoro ya ardhi inayojitokeza hasa kwa upande wa rushwa ambapo serikali za vijiji zimeshindwa kusimamia tatizo hili na badala yake ubadhilifu umekuwa mwingi, hivyo sera hii ijikite katika kutatua na kuondoa migogoro hiyo”.

Nae mmoja wa wadau ambaye ni Mkulima  kutoka Mkoa wa Mara Kata ya Nyakonga, Nyangi Marwa ameiomba serikali kuwaangali wanawake na wajane  waliopo pembezoni kwani wengi wao hawajui haki zao juu ya umiliki wa ardhi ili kuepuka kunyanyasaji hasa katika kipindi cha mirasi.

TGNP ni shirika ambalo lipo mstari wa mbele katika masuala ya kijinsia na imepata nafasi ya kuweza kuchangia katika suala zima la sera mpya ya ardhi , ambapo kutokana na warsha hiyo TGNP inatarajia kutengeneza kikosi kazi cha Taifa Kitakachoundwa na wadau mbalimbali ambacho kitaongeza nguvu na ufuatiliaji wa utekelezaji wa sera hizi  ili kuongeza nguvu kwenye ushawishi na utetezi wa usawa wa kijinsia hususan utekelezaji wa sera zetu .

MAHAKAMA YAWAPA SIKU KUMI MAWAKILI WA LEMA

$
0
0
Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema akiteta jambo na mkewe Neema baada ya mahakama kumalizika leo.Picha na Vero Ignatus Blog.
 

Na.Vero Ignatus,Arusha

Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha Dkt.Modesta Opiyo amewapa siku kumi(10)mawakili wa mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema wawe wamewasilisha notisi ya kukata rufaa dhidi ya maamuzi ya mahakama ya chini iliyomnyima dhamana Lema .

Agizo hilo limekuja kutokana na Mahaka kutoridhishwa na hoja za maombi ya mapingamizi mawili yaliyowekwa na mawakili wa serikali dhidi ya taarifa ya dharura ya kusudio la kukataa rufaa ya mawakili wa Mbunge huyo. 

Jaji Dkt.Modesta Opiyo wa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha alisema katika maamuzi yake kuwa pingamizi zilizowekwa hazina msingi kwani waleta maombi walifuata taratibu zote za katika kiapo na hati ya dharua ya kuitwa mahakamani,ambapo amesema mahakama haijaona ucheleweshwaji wa lazima.

Baada ya uamuzi huo Jaji Opiyo aliwataka mawakili wa Lema ,Shekh Mfinanga na Faraji Mangula kuwasilisha notisi ndani ya siku kumi kuanzia leo,hadi hapo tar 30dec2016 shauri hilo litakaposikilizwa tena.

****TUJIKUMBUSHE****

Mbunge Godbless Lema anakabiliwa na kesi hiyo ya uchochezi aliyosomewa katika mahakama ya wilaya ya Arusha mbele ya hakimu mkazi Deusdedit Kamugisha Novemba 8 mwaka huu na aliwekewa pingamizi na mawakili wa serikali ya kutopata dhamana baada ya hakimu kusema kuwa dhamana iko wazi.

Mbunge huyo wa Arusha Mjini alikamatwa Novemba 2 mwaka huu Mkoani Dodoama kwa kosa hilo baada ya kuhutubia katika mikutano ya hadhara katika kata mbalimbali za Jiji la Arusha kuwa ameoteshwa kuwa Rais Magufuli atakufa kabla ya mwaka 2020 hali inayodaiwa kuleta uchochezi kwa wananchi waliomchagua kuwa Rais wa nchi.
 


VODACOM TANZANIA FOUNDATION YAWAKUMBUKA WAZEE WA BABATI MKOANI MANYARA

$
0
0
Baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania,wakiwa wanaelekea katika kituo cha wazee na wasiojiweza  cha Sarame Magugu, Wilayani Babati Mkoani Manyara, kutoa msaada wa shuka na vyandarua na  vyakula mbalimbali , dawa na mahitaji mengine yenye thamani ya zaidi ya sh10 milioni yaliyotolewa msaada na Vodacom Tanzania Foundation.
Meneja ruzuku na mawasiliano wa Vodacom Tanzania Foundation, Sandra Oswald, akimkabidhi, mmoja kati ya wazee wa kituo cha wazee na wasiojiweza Sarame Magugu, Wilayani Babati Mkoani Manyara, Aaron Owiso, ambapo waliwakabidhi wazee hao mashuka, vyandarua, vyakula, dawa na mahitaji mengine yenye thamani ya zaidi ya sh10 milioni.
Mzee Maalim Masaja (kushoto)anayelelewa katika kituo chawazee wasiojiweza cha Sarame Magugu, Wilayani Babati Mkoani Manyara, akipokea mfuko wenye mchele kwa niaba ya wenzake toka kwa Meneja ruzuku na mawasiliano wa Vodacom Tanzania Foundation, Sandra Oswald, ambapo msaada huo ulitolewa na Vodacom Tanzania Foundation kwa wazeeikiwa ni pamoja na mashuka, vyandarua, vyakula, dawa na mahitaji mengine yenye thamani ya zaidi ya sh10 milioni.

SERIKALI HAIJAZUIA WATUMISHI WA UMMA KUKOPA

$
0
0
Kumekuwa na taarifa inasambazwa katika mitandao ya kijamii, makundi ya ‘WhatsApp’, ‘Facebook’ na majukwaa mbalimbali ikieleza kuwa Serikali imepiga marufuku watumishi wa umma kukopa Benki,SACCOS,VICOBA na Taasisi mbalimbali za kifedha.

Taarifa iliyotolewa leo tarehe 20 Desemba 2016 na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali imeeleza kuwa taarifa inayosambazwa, ambayo imetafsiri mawasiliano ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ni ya kupotosha, hivyo watumishi wote wa umma wanaombwa kuipuuza.

Vilevile watumishi wa umma wametakiwa kuzingatia kuwa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali HAINA mamlaka ya kuzuia wala kuruhusu mtumishi yeyote wa Serikali kukopa au kutokopa katika Taasisi yoyote ya Fedha nchini.

Watumishi wa umma pia wamekumbushwa kuwa mikopo yote ya watumishi wa umma katika Taasisi za Fedha hutolewa kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na taratibu zilizopo ili mradi mtumishi awe ametimiza vigezo.

Aidha, watumishi wa umma wameaswa kuacha tabia ya kusambaza taarifa zisizo za kweli na ambazo zina mamlaka husika ya kuzitoa ikiwa ni pamoja na kuzingatia maadili ya utumishi wa umma.

Kompyuta za Bayport zatinga mkoani Morogoro

$
0
0

Meneja Masoko na Mawasiliano wa Bayport Financial Services, Ngula Cheyo, kushoto, akimkabidhi moja ya kompyuta sita zilizotolewa na Taasisi yao kwa ajili ya kuusaidia Mkoa wa Morogoro katika vifaa vya ofisini ili kurahisisha utendaji kazi. Anayepokea ni Mkuu wa Mkoa Morogoro, Mheshimiwa Dkt Stephen Kebwe, leo mkoani Morogoro. Picha zote na Mpiga Picha Wetu.

TAASISI ya Kifedha ya Bayport Financial Services inayojihusisha na mikopo imekabidhi kompyuta sita kwa uongozi wa Mkoa wa Morogoro, kwa kupitia Mkuu wake wa Mkoa, Mheshimiwa Dkt Stephen Kebwe, ili zisaidie utendaji kazi wa watumishi wa umma katika ofisi za Halmashauri ya Wilaya Mvomero, Manispaa ya Morogoro Mjini pamoja na Morogoro Vijijini.

Ugawaji wa kompyuta hizo ni mwendelezo wa taasisi hiyo kugawa vitendea kazi hivyo baada ya kumkabidhi kompyuta 125 kati ya 205 kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mheshimiwa Angellah Kairuki, huku kompyuta zote zikiwa na thamani ya Sh Milioni 500.
Meneja Masoko na Mawasiliano wa Bayport Financial Services, Ngula Cheyo mwenye miwani akifurahia jambo na Mkuu wa Mkoa Morogoro, Mheshimiwa Dkt Stephen Kebwe mwenye suti nyeusi. Kulia kwa Cheyo ni Afisa Tawala wa Mkoa Morogoro, Victor Ndiva na nyuma ni Mercy Mgongolwa, Mratibu wa Masoko na Mawasiliano wa Bayport Financial Services.
Hapa ni Meneja Masoko na Mawasiliano wa Bayport Financial Services, Ngula Cheyo mwenye miwani akipiga picha ya furaha na Mkuu wa Mkoa Morogoro, Mheshimiwa Dkt Stephen Kebwe mwenye suti nyeusi. huku akiwa ameshikana mkono na Afisa Tawala wa Mkoa Morogoro, Victor Ndiva. Nyuma kwa Cheyo ni Mercy Mgongolwa, Mratibu wa Masoko na Mawasiliano wa Bayport Financial Services.

Akizungumza katika makabidhiano hayo, Meneja Masoko na Mawasiliano wa Bayport Financial Services, Ngula Cheyo, alisema kwamba wamejisikia furaha kufikisha vitendea kazi hivyo kwa serikali ya mkoa wa Morogoro.

Alisema taasisi yao inafanya kazi ya utoaji wa mikopo ya fedha taslimu kwa watumishi wa umma na wafanyakazi wa kampuni binafsi zilizoidhinishwa pamoja na ile mikopo ya viwanja kwa Watanzania wote, wakiwamo wajasiriamali.

“Bayport tumejipanga kuhakikisha kwamba tunaboresha utendaji kazi wa watumishi wetu wa umma kwenye ofisi za mikoa na wilaya, hivyo zoezi la kutoa kompyuta litakuwa endelevu kadri tulivyoelekezwa na serikali baada ya kuwapelekea wazo letu la kununua na kusambaza msaada huu kwao.

“Pamoja na kutoa misaada mbalimbali ya kijamii, tunaahidi kuendelea kufanya kazi kwa bidii ya kutoa huduma bora ya mikopo kwa watumishi wa umma, ambapo kusudio letu ni kuona wateja wetu wanajikwamua zaidi kwa kuanzisha au kuendeleza biashara zao ili waongeze vyanzo vya kipato na kuacha kutegemea mishahara,” alisema Cheyo.

Naye Mkuu wa Mkoa Morogoro, Dkt Kebwe, aliwashukuru Bayport kwa kujitolea kwenye jamii na kuwakabidhi kompyuta sita ili ziwasaidie mkoani kwao, akiamini kuwa zitachangia utendaji uliotukuka kwa watumishi wa umma.

“Tunawashukuru Bayport kwa kuona tunastahili msaada huu mkubwa kwetu, tukiamini kuwa watumishi wetu watafanya kazi kwa moyo ili kuhakikisha kuwa kila mtu anatimiza wajibu wake ipasavyo kama wote tunavyokusudia,” alisema Dkt Kebwe na kuwasihi Bayport waendelee kujitoa kusaidia matatizo yanayoikabili jamii ya Morogoro na Tanzania kwa ujumla.

Kwa mujibu wa Kebwe, Mkoa wao upo kwenye mchakato mkubwa wa kupambana na changamoto mbalimbali zinazowakabili ili kuupatia maendeleo Mkoa wao wa Morogoro.

Mikoa na wilaya mbalimbali za Tanzania Bara zinatarajiwa kunufaika na misaada ya kompyuta kwa ofisi za umma kama dira na dhamira ya taasisi ya Bayport kurahisisha utendaji kazi utakaochangia kuleta maendeleo hapa nchini.

SHIRIKA LA TAYOA LASAIDIA KUONGEZA UELEWA KUHUSU SARATANI YA MLANGO WA KIZAZI MKOANI MWANZA

$
0
0
Mkurugenzi Msaidizi wa Shirika lisilo la kiserikali linalojihusisha na masuala ya afya pamoja na ukatili wa kijinsia kwa vijana na wanawake nchini la Tanzania Youth Alliance (TAYOA), Elizaberth Ndakidemi, akizungumza hii leo wakati wa mkutano wa kushirikishana uzoefu, changamoto pamoja na mafanikio katika utekelezaji wa awamu ya pili ya mradi wa Saratani ya shingo ya kizazi mkoani Mwanza, unaotekelezwa na shirika hilo.#BMGHabari
Wadau wa afya mkoani Mwanza, wakimsikiliza Mkurugenzi Msaidizi wa Shirika la TAYOA, Elizaberth Ndakidemi, wakati akizungumza kwenye mkutano wa kushirikishana uzoefu, changamoto pamoja na mafanikio katika utekelezaji wa awamu ya pili ya mradi wa Saratani ya shingo ya kizazi mkoani Mwanza.
Mkurugenzi Msaidizi wa Shirika la TAYOA, Elizaberth Ndakidemi, akizungumza hii leo wakati wa mkutano wa kushirikishana uzoefu, changamoto pamoja na mafanikio katika utekelezaji wa awamu ya pili ya mradi wa Saratani ya shingo ya kizazi mkoani Mwanza, unaotekelezwa na shirika hilo.
Mratibu wa Afya ya Uzazi ngazi ya jamii mkoani Mwanza, Esperance Makuza, akizungumza kwa niaba ya Mratibu wa afya ya uzazi ngazi ya mkoa wa Mwanza.
Mratibu Miradi wa Shirika la TAYOA, Isaack Ghalib, akifafanua namna mradi huo ulivyofanya kazi, mafanikio na changamoto zake.
Mratibu Miradi wa Shirika la TAYOA, Isaack Ghalib, akifafanua namna mradi huo ulivyofanya kazi, mafanikio na changamoto zake.
Baadhi ya wadau wa afya mkoani Mwanza wakifuatilia mkutano wa kushirikishana uzoefu, changamoto pamoja na mafanikio katika utekelezaji wa awamu ya pili ya mradi wa Saratani ya shingo ya kizazi 
Baadhi ya wanahabari pamoja na wadau wa afya mkoani Mwanza wakifuatilia mkutano wa kushirikishana uzoefu, changamoto pamoja na mafanikio katika utekelezaji wa awamu ya pili ya mradi wa Saratani ya shingo ya kizazi 
Mmoja wa watumishi wa afya mkoani Mwanza
Mradi huo ulifadhiriwa na Pink Ribbon Red Ribbon pamoja na washirika wengine kama wanavyoonekana katika picha. Mitandao ya simu ilisaidia kutoa nambari za bure ambazo ni 117 kwa ajili ya wananchi kupiga ili kuelimishwa kuhusu Saratani.

Uelewa kuhusu dalili za awali za maambukizi ya Saratani ya mlango wa kizazi kwa wanawake mkoani Mwanza, umeongezeka na hivyo kufanya idadi ya wanawake wanaojitokeza kupima maambukizi hayo kufikia wanawake 60 kwa mwezi.

Hatua hiyo imefikiwa kutokana na juhudi zinazofanywa na serikali kupitia wizara ya afya kwa kushirikiana na mashirika mbalimbali ikiwemo TAYOA katika kuhakikisha akina mama nchini wanafahamu umuhimu wa kufanya uchunguzi wa awali kuhusu maambukizi ya saratani kwa ujumla.

Hayo yamebainishwa Jijini Mwanza na Mkurugenzi wa Shirika la TAYOA, Elizaberth Ndakidemi, kwenye mkutano wa kushirikishana uzoefu, changamoto pamoja na mafanikio katika utekelezaji wa awamu ya pili ya mradi wa Saratani ya shingo ya kizazi mkoani Mwanza, unaotekelezwa na shirika hilo.

Katika mradi huo ulioanza kutekelezwa mwezi April mwaka 2014, zaidi ya akina mama elfu 20 mkoani Mwanza wamefikiwa na kupewa elimu kuhusiana na saratani ya shingo ya kizazi, kuwaongezea ujuzi watoa huduma za afya wapatao 70 katika ngazi za jamii pamoja na kusaidia upatikanaji wa vifaa vya uchunguzi wa dalili za awali za saratani hiyo katika vituo vya afya mkoani Mwanza ambapo tamati ya mradi huo ni Disemba 31 mwaka huu.

Aidha mradi huo umesaidia kuwasafirisha akinamama 392 mkoani Mwanza, kwenda katika hospitali za rufaa ikiwemo Bugando kwa ajili ya uchunguzi zaidi wa Saratani ya shingo ya kizazi ambapo miongoni mwao zaidi ya akina mama 70 wamepatiwa matibabu.

Awali Mratibu Miradi wa Shirika la TAYOA, Isaack Ghalib, amebainisha kwamba wakati mradi huo unaanza kulikuwa na dhana potofu kuhusiana na ugonjwa wa saratani ya shingo ya kizazi ambayo wanawake wengi walikuwa wakiamini wamerogwa na hivyo kuchelewa kufika hospitalini huku baadhi yao wakikimbiwa na waume zao.

Akizungumza kwa niaba ya Mratibu wa afya ya uzazi mkoani Mwanza, Mratibu wa Afya ya Uzazi ngazi ya jamii, Esperance Makuza, amewahimiza watoa huduma wa afya walionufaika na mafunzo yaliyotolewa katika mradi huo, kuyatumia mafunzo hayo kutoa huduma zinayostahili ili kuwanusuru akina mama na madhara yatokanayo na saratani hiyo.

Inaelezwa kwamba zaidi ya asilimia 80 ya akina mama wanaougua saratani ya shingo ya kizazi nchini hupoteza maisha kutokana na kuchelewa kufanya uchunguzi na kupatiwa tiba mapema, ikizingatiwa kwamba saratani hiyo hutibiwa ikiwa mgonjwa atawahi matibabu.

Aidha akina mama wanakumbushwa kuzingatia kanuni bora za kiafya ikiwemo kufanya mazoezi, kujiepusha na uvutaji wa sigara, ulevi pamoja na wapenzi wengi ili kuondokana na maambukizi ya saratani ya shingo ya kizazi.

BODI YA CHAKULA, DAWA NA VIPODOZI ZANZIBAR YAFANYA UKAGUZI WA KUSHTUKIZA KATIKA MADUKA YA DAWA KUANGALIA UHALALI WA MADUKA NA UTAALAMU WA WAFANYAKAZI WAKE

$
0
0
 Mkaguzi Mkuu wa Bodi ya Chakula, Dawa na Vipodozi Zanzibar Mwadini Ahmada Mwadini (kushoto) akifanya ukaguzi katika moja ya Duka la dawa kuangalia usalama wa dawa zinazouzwa na duka hilo lililopo mtaa wa kilimani.
 Mkaguzi Mkuu wa Bodi ya Chakula, Dawa na Vipodozi Zanzibar Mwadini Ahmada Mwadini (kushoto) akifanya ukaguzi katika moja ya Duka la dawa kuangalia usalama wa dawa zinazouzwa na duka hilo lililopo mtaa wa kilimani.
Maafisa ukaguzi kutoka Bodi ya Chakula, Dawa na vipodozi wakiangalia dawa zinazoendelea kuuzwa na duka la Fahud liliopo Mkunazini Mjini Zanzibar.

 Msaidizi Mfamasia Kombo Masoud Khatib akitoa maelezo kwa mkaguzi wa Bodi ya Chakula Dawa na Vipodozi  Amne Nassor Issa wakati maafisa hao walipofanya ukaguzi wa kushtukiza katika maduka ya dawa ya Mjini Zanzibar.Picha na Makame Mshenga.

MWENYEKITI WA CCM TAIFA RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA VIONGOZI WAPYA WA CHAMA ALIOWATEUA HIVI KARIBUNI NA DC MTEULE WA UBUNGO

$
0
0
Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mteule Mhe. Kisare Makori akishuhudiwa na viongozi wapya wa CCM aliowateua hivi karibuni. Kutoka kulia ni Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Humphrey Polepole, Katibu NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Kanali Ngemela Eslom Lubinga na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Ndg. Rodrick Mpogolo walipoenda kujitambulisha Ikulu jijini Dar es salaam leo Desemba 20, 2016.
Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Dkt John Pombe Magufuli akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mteule Mhe. Kisare Makori (kushoto) pamoja na viongozi wapya wa CCM aliowateua hivi karibuni. Kutoka kulia ni Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Humphrey Polepole, Katibu NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Kanali Ngemela Eslom Lubinga na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Ndg. Rodrick Mpogolo walipoenda kujitambulisha Ikulu jijini Dar es salaam leo Desemba 20, 2016.
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mteule Mhe. Kisare Makori (kushoto) akibadilishana mawasiliano na na viongozi wapya wa CCM walioteuliwa hivi karibuni. Kutoka kulia ni Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Humphrey Polepole, Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Ndg. Rodrick Mpogolo  na Katibu NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Kanali Ngemela Eslom Lubinga walipoenda kujitambulisha kwa Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam leo Desemba 20, 2016. PICHA NA IKULU

MAN FONGO WITH SINGELI DANCE AT GIRAFFE OCEAN VIEW HOTEL ON XMAS DAY

MAHAFALI YA 28 YA SEKONDARI YA AL- HARAMAIN NA YA KWANZA KWA KWA CHUO CHA UALIMU KWA WALIMU WA NGAZI YA CHETI WA SHULE ZA MSINGI

$
0
0

Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Al Haramain, Mwalimu Nuhu Jabir, akiwakaribisha wageni mbalimbali waliohuduria mahafali hayo.
Wahitimu wa Kidato cha nne, Jokha Ayoub (kushoto) na Hafsa Omar (wa pili kulia), wakisoma utenzi, wakati wa mahafali yao hayo.
Wahitimu wa Ualimu wa ngazi ya Stasha ya Ualimu wa Elimu ya Msingi, Hawa Hassan (kushoto) na Sofia Juma wakisoma risala ya wahitimu wa ngazi hiyo,wakati wa mahafali yao hayo.
Mhitimu wa Kidato cha Nne, Sada Ramadhan, akisoma risala ya wahitimu hao, katika mahafali hayo. 
Naibu Katibu Mkuu wa Baraza la Waislamu Tanzania (Bakwata), upande wa Utawala, Salim Abeid, wamiliki wa Shule na Chuo cha Al Haramain, akizungumza, wakati akiliwakilisha baraza hilo,katika mahafali hayo.
Watangazaji wa Radio Qur'an wakiwa kazini, wakirusha matangazo ya mahafali hayo, moja kwa moja.
Mkuu wa Chuo cha Ualimu cha Al Haramain, Mwaalim Suleiman Urassa, akizungumza wakati wa mahafali hayo, jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Al Haramain, Mwalimu Nuhu Jabir, akitoa taarifa ya shule hiyo, wakati wa mahafali hayo.
Mgeni rasmi katika mahafali hayo, Imam Mkuu wa Msikiti wa Al Maamur na Mjumbe wa Baraza la Ulamaa, Sheikh Issa Othman, akitoa hotuba yake, wakati wa mahafali hayo hivi karibuni.
Wazazi na wageni mbalimbali waliohudhuria mahafali hayo, wakimsikiliza mgeni rasmi, Imam Mkuu wa Msikiti wa Al Maamur na Mjumbe wa Baraza la Ulamaa, Sheikh Issa Othman, alipokuwa akitoa hotuba yake.
Mgeni rasmi katika mahafali hayo, Imam Mkuu wa Msikiti wa Al Maamur na Mjumbe wa Baraza la Ulamaa, Sheikh Issa Othman, akisisitiza jambo, wakati akitoa hotuba yake, wakati wa mahafali hayo.
Mwalimu wa Taaluma, Rashid Kassim akizungumza kabla ya mgeni rasmi kuanza kukabidhi vyeti kwa wahitimu.
Mwanafunzi bora katika nidhamu Hafsa O. Abdallah, akikabidhiwa cheti cha kuhitimu kidato cha nne na mgeni rasmi, Sheikh Issa Othman.
Mwanafunzi Bora katika usafi, Mbaraka Salmini, akiabidhiwa cheti na mgeni rasmi Sheikh Issa Othman.
Mgeni rasmi, Imamu Mkuu wa Msikiti wa Al Maamur, Upanga jijini Dar es Salaam, Sheikh Issa Othman, akimkabidhi cheti mwanafunzi bora katika mahudhurio, Ahmed Said. Wa pili kulia ni Mkuu wa shule hiyo, Mwalimu Nuhu Jabir.
Mgeni rasmi, Imamu Mkuu wa Msikiti wa Al Maamur, Upanga jijini Dar es Salaam na Mjumbe wa Baraza la Maulamaa, Sheikh Issa Othman, akimkabidhi cheti mwanafunzi bora wa somo la Fisikia (Physics), Suhaila Is-haaq.
Mwanafunzi Bora katika somo la Kiingereza, Habib Tajdin, akiabidhiwa cheti na mgeni rasmi Sheikh Issa Othman.
Mhitimu wa kidato cha nne, Faiza Wililo, akiabidhiwa cheti na mgeni rasmi Sheikh Issa Othman.
Mhitimu Zuhura Abdallah wa Ngazi ya Cheti wa Elimu ya Awali, akipokea cheti chake kutoka kwa mgeni rasmi, Sheikh Issa Othman.
Mhitimu Tabu Ramadhan wa Ngazi ya Cheti wa Elimu ya Awali, akipokea cheti chake kutoka kwa mgeni rasmi, Sheikh Issa Othman.
Mhitimu Athuman Nduli wa Ngazi ya Cheti wa Elimu ya Awali, akipokea cheti chake kutoka kwa mgeni rasmi, Sheikh Issa Othman.
Mhitimu Emmanuel Charles wa Ngazi ya Cheti wa Elimu ya Awali, akipokea cheti chake kutoka kwa mgeni rasmi, Sheikh Issa Othman.
Mhitimu Nkumi Hussein wa Ngazi ya Cheti wa Elimu ya Awali, akipokea cheti chake kutoka kwa mgeni rasmi, Sheikh Issa Othman.
Mkuu wa Chuo, Mwaalimu Suleiman Urassa (kulia) na Mkuu wa Sekondari ya Al Haramain Mwalimu Nuhu Jabir, wakijadili jambo mara baada ya kumalizika mahafali hayo.
Vijana wa Madrasat Muhajrina ya Kinondoni wakiwaongoza wahitimu kwa kaswida, kuelekea kwenye viwanja vya mahafali, Sekondari na Chuo cha Ualimu cha Al Haramain jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
Vijana wa Madrasat Muhajrina wakitumbuiza kwa kaswida, wakati wakiwaongoza wahitimu kuelekea kwenye viwanja vya mahafali.
Mgeni rasmi katika mahafali ya 28 ya Shule ya Sekondari ya Al Haramain na ya Kwanza ya ngazi ya Cheti kwa Walimu wa Shule za Msingi ya Chuo cha Al Haramain, Imam Mkuu wa Msikiti wa Al Maamur na Mjumbe wa Baraza la Ulamaa, Sheikh Issa Othman (katikati), akiongozwa na Mkuu wa Chuo, Suleiman Urassa (kushoto) na Mkuu wa Sekondari ya Al Haramain, Nuhu Jabir (kulia), wakati wa mahafali hayo jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
Wahitimu wa Ualimu Elimu ya Awali, ngazi ya Cheti, wakiingia kwenye viwanja vya mahafali hayo.
Wahitimu wa Ualimu Elimu ya Awali ngazi ya Cheti, wakielekea kwenye viwanja vya mahafali.
Wahitimu wa Kidato cha Nne wa Shule ya Sekondari ya Al Haramain, wakiwa kwenye gwaride la kuingia kwenye viwanja vya mahafali hayo.
Wahitimu wa Ualimu na wa Kidato cha Nne wakiingia kwenye viwanja vya mahafali hayo.
Wahitimu wa Ualimu, Ngazi ya Stashahada ya Ualimu wa Elimu ya Msingi, wakiwa wamekaa sehemu yao, wakati wa mahafali yao hayo hivi karibuni.
Wahitimu wa Ngazi ya Cheti, Elimu ya Awali, wakiwa katika sehemu yao.
Wahitimu ngazi ya cheti wa Ualimu wa Elimu ya Awali, wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa mahafali yao hayo.
Wahitimu ngazi ya Stashahada ya Ualimu wa Elimu ya Msingi, wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa mahafali yao hayo.
Mgeni rasmi katika mahafali ya 28 ya Shule ya Sekondari ya Al Haramain na ya Kwanza ngazi ya Cheti kwa Walimu wa Shule za Msingi ya Chuo cha Al Haramain, Imam Mkuu wa Msikiti wa Al Maamur na Mjumbe wa Baraza la Ulamaa, Sheikh Issa Othman (katikati), akiwa na Mkuu wa Chuo, Suleiman Urassa (kulia) na Mkuu wa Sekondari ya Al Haramain, Nuhu Jabir (kushoto), wakichua nafasi zao kwenye meza kuu wakati wa mahafali hayo.
Mmoja wa Walimu wa Chuo cha Dini cha Al Haramain, Ramadhan Pazi, akisoma dua ya ufunguazi wa mahafali hayo.
Baadhi ya wahitimu wa kidato cha nne wakiwa wameketi katika sehemu yao.
Mhitimu wa Kidato cha nne, akisoma Qur'an, Suratul Waatin, wakati wa ufunguzi wa mahafali hayo.
Mhitimu wa Kidato cha nne, akitoa tafsiri ya Suratu Watin, iliyosomwa katika ufunguzi wa mahafali hayo.

WAMILIKI WA VIWANDA WALIOJENGA JUU YA MITARO YA MAJITAKA KUINGIA HATIANI – MPINA

$
0
0
NA EVELYN MKOKOI -DSM

Akiwa katika siku nyingine ya ukaguzi wa mazingira jijini Dar es salaam, Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina, leo ametembelea katika Maeneo ya keko Magurumbasi na kujionea namna ambavyo wamiliki wa viwanda wanavyotiririsha maji katika mfereji maarufu kwa jina la mseleleko. 

Baada ya ukaguzi wa mazingira katika maeneo hayo, Naibu Waziri Mpina amewaasa wawekezaji wenye viwanda nchini waliojenga juu ya miundombinu ya majitaka kutafuta njia nyingine ya ujenzi sahihi ya miundombinu ya majitaka kutoka viwandani mwao kwenda kwenye mfumo wa mamlaka za maji na kuelekeza kuwa iwapo wataonekana kuziba kwa ujenzi wa majengo yao mitaro mikubwa ya miundombinu ya maji, sheria itachukua mkondo wake ikiwa ni pamoja na kubomoa majengo yao.

Akijibu swali la mwandishi wa habari wa kituo kimoja cha television hapa nchini, lilihoji kuusika kwa watumishi wa umma kwa namana moja au nyigine kiujanja ujanja katika kuruhusu vibali vya ujenzi na kupelekea uharibifu wa miundombinu ya majitaka na mazingira kwa ujumla, Mpina alisema kuwa endapo kutagundulika kuwa na ushiriki wowote wa watumishi wa umma katika suala hilo sheria pia itachukua mkono wake.

Pamoja na hilo Naibu Waziri Mpina amewaeleza wenye viwanda wanaoendelea kuchafua mazingira kuwa kutakuwa na oparesheni kubwa nchini ya ukaguzi wa mazingira itakayohusisha halmashauri za miji, mamlaka za maji, wamiliki wa mabomba ya maji taka na wananchi ili kuwajibika kwa pamoja katika kunusuru uharibifu wa mazingira.

Aidha Ameliagiza Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC kuiandikia hati ya zuwio TANROADS ya mwezi mmoja itayowataka wafumue karavati lao linalopita chini ya barabara katika eneo la kurasini BP darajani na kuliongeza ukubwa ili majitaka yaweze kupita kwa nafasi.

Naibu waziri Mpina Pia amewataka Viongozi wa Manispaa ya Ilala kusimamia kikamilifu usafi wa Mazingira na kuwataka wananchi wa eneo la keko magurumbasi wanaokaa karibu na mfereji wa mseleleko kufanya usafi katika mfereji huo na kutooutumia kama DAMPO.


Kwa upande wake mratibu wa Mazingirawa kanda ya mashariki kutoka NEMC Bw. Jaffari Chimgege amesema wao kama Baraza watakaa kwa Pamoja na wawekezaji, wenye makaravati madogo yanazoshindwa kupitisha majitaka vizuri jijini DSM na kutafuta suluhisho la kudumu kwani hali hiyo ni hatari hasa katika kipindi cha mvua, inaweza kusababisha magojwa ya milipuko kama vile kipindupindu.

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Luhaga Mpina, kulia akiwa katika ziara ya ukaguzi wa Mazingira Keko magulumbasi katika mfereji wa maji taka mseleleko Jijini Dar es salaam mara baada ya kupata malalamiko kutoka kwa wananchi wanaoishi maeneo hayo. 
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Luhaga Mpina akimsikiliza Mtaalamu wa Mazingira kutoka NEMC, Jaffar Chimgege katika ziara hiyo ya ukaguzi wa mazingira jijini Dar es salaam. 
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Luhaga Mpina, akiwa ameongozana na wananchi wanaoishi maeneo ya Keko Magulumbasi katika ziara ya ukaguzi wa Mazingira. 
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Luhaga Mpina, akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuhitimisha ziara yake ya ukaguzi wa mazingira Keko Jijini Dar es salaam.

KUKO BIZE KARIAKOO JIJINI DAR ES SALAAM KUELEKEA SIKUKUU ZA MWISHO WA MWAKA

$
0
0



Wakazi wa Dar es Salaam wakiwa katika harakati ya kupata mahitaji kuelekea sikukuu za mwisho wa mwaka katika eneo la Kariakoo jijini Dar es Salaam. Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.

MFUKO WA FIDIA KWA WAFANYAKAZI WAZINDUA HUDUMA YA UTOAJI MAFAO YA FIDIA KWA WAFANYAKAZI KATI YA MFUKO NA WATOA HUDUMA ZA AFYA

$
0
0

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira na wenye ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama, akikata utepe kuzindua mafaoya Fidia na na ubia baina ya watoa huduma za afya .Uzinduzi huo ulifanywa na Waziri Mhagama kwa niaba ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa jijini Dar es Salaam, Desemba 20, 2016. wanaoshuhudia ni Naibu Mawaziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Mh. Anthony Mavunde, (wapili kulia), Mh. Dkt. Abdallah Possi, (watatu kulia), Bw. Emmanuel Humba, Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), wanne kulia, na Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba. (watano kulia)..( PICHA NA MUHIDIN SUFIANI)

NA ANTHONY JOHN, GLOBU YA JAMII
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera,Bunge kazi ,vijana Ajira na watu wenye ulemavu, Jenista Muhagama, amewataka waajili wote kuwasilisha Michango ya wafanyakazi wao Mfuko Fidia kwa Wafanyakazi WCF kwa wakati.

Akizungumza katika Uzinduzi wa Huduma za utoaji wa Mafao ya fidia kwa wafanyakazi na ubia kati ya Mfuko na watoa Huduma za Afya amesema kuwa
kwa Mwaka huu wafedha Serikali imewasilisha Michango ya wafanyakazi wake wote ambapo alizitaka Sekta binafsi pia kuwasilisha Michango yao kwa wakati.

Sanjari  na Hayo Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo Masha Mshomba ameongeza kuwa Mpaka kufikia Novemba 30 Mwaka huu Jumla ya waajili 5945 wamechangia na wamepewa na ya usajili.

Hata Hivyo Mweketi  wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mfuko huo Emmanuel Humba amesema Mfuko Huo utachangia kwa kiwango kikubwa Sera ya Tanzania ya Viwanda  iliyoa anzishwa na Serikali ya awamu ya tano kwani wafanyakazi watakapo  kuwa na Afya njema watafanya kazi kwakujiamini na kuleta Maendeleo.
 Waziri Mhagama akihutubia
 Mwenyekiti wa bodi ya WCF, Bw. Emmanuel Humba akitoa hotuba yake
 Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw.Masha Mshomba, akitoa hotuba yake
 Mgeni rasmi, Naibu Mawaziri, viongozi wa WCF, na waliotunukiwa vyeti wakiwa kwenye picha ya pamoja

Waziri Mhagama, akimkabidhi cheti cha ubia baina ya WCF na watoa huduma za afya,  Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Bernard Konga, wakati wa hafla ya uzinduzi wa Huduma ya Utoaji wa Mafao ya Fidia kwa Wafanyakazi na Ubia kati ya Mfuko na watoa huduma za afya, WCF uliozinduliwa jijini Dar es Salaam, leo.


Waziri Mhagama, akimkabidhi cheti cha ubia baina ya WCF na watoa huduma za afya,  Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Mkifupa (MOI), Dkt. Othman Kiloloma, wakati wa hafla ya uzinduzi wa Huduma ya Utoaji wa Mafao ya Fidia kwa Wafanyakazi na Ubia kati ya Mfuko na watoa huduma za afya, WCF uliozinduliwa jijini Dar es Salaam, leo.

 Mgeni rasmi akimpongeza msanii Mrisho Mpoto kwa ujumbe wake murua kupitia sanaa
Mgeni rasmi akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa WCF na wageni wengine
Waziri akisalimiana na mameneja na maafisa wa WCF, wakati akiwasili
 Wafanyakazi wa WCF wakimsubiri mgeni rasmi
 Waziri akiongozana na  Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba, huku akisalimiana na baadhi ya wafanyakazi wa wcf
Waziri Mhagama, akisalimiana na baadhi ya wafanyakazi waWCF

NDEGE YA ATCL KUPELEKA WANAMICHEZO WA TAASISI YA LOHANA MAHAJAN KISUMU NCHINI KENYA

$
0
0
1
Mwenyekiti wa Taasisi ya Kidini ya Lohana Mahajan Bw.Navin Kanabal akitia saini katika moja ya nyaraka wakati taasisi hiyo ilipokabidhiwa tiketi za Shirika la Ndege la ATCL kwa ajili ya safari ya wachezaji wake kwenda Kisumu Nchini Kenya ambapo tarehe 23 /12/ 2016 huu jumla ya wachezaji 49 watasafiri wa kwa ndege ya shirika hilo kwa ajili kushiriki tamasha la michezo ambalo litafanyika nchini humo na kurejea tarehe 27/12/2016.

Akizungumza katika makabidhiano hayo ya tiketi Mkurugenzi wa Masoko na Maendeleo ya Biashara ATCL Bw. Edward Nkwabi ameishukuru taasisi hiyo kwa kutambua na kusafiri kwa ndege za Shirika la Ndege la ATCL kwani itakuwa njia bora na nzuri ya kuanza kujitangaza kimataifa kwa kuanzia katika nchi zetu wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Ameongeza kuwa ATCL itatoa huduma bora kabisa wakati wa safari yao ya Kwenda Kisumu Kenya na Kurudi nchini ili wakati mwingine wasafiri na ndege za ATCL Ameongeza kwamba kwa sasa Ndege za shirika hilo zinatoa huduma ya usafiri wa anga katika viwanja vya Songwe, Bukoba, Mwanza, Kilimanjaro , Zanzibar na Comoro na hapo baadaye wataongeza huduma katika viwanja vya Dodoma na Arusha, Tabora Mtwara pamoja na Mpanda.

Hafla ya makabidhiano ya tiketi hizo imefanyika kwenye Mgahawa wa AKEMI uliopo jengo la Golden Tower jijini Dar es salaam, Katika pichwa wanaoshuhudia tukio hilo ni Mkurugenzi wa Masoko na Maendeleo ya Biashara ATCL Bw. Edward Nkwabi wa pili kutoka kulia, James Mbago Meneja Mauzo na Usambazaji, na aliyesimama nyuma ni Katibu wa Taasisi ya Lohana Mahajan Bw.Sanjit Ramji.
2
Mwenyekiti wa Taasisi ya Kidini ya Lohana Mahajan Bw.Navin Kanabal akipokea tiketi kutoka kwa Mkurugenzi wa Masoko na Maendeleo ya Biashara ATCL Bw. Edward Nkwabi kwa ajili ya wanakikundi wenzake 48 kwa ajili ya safari ya kwenda na kurudi Kisumu nchini Kenya kwa ajili ya Tamasha la Michezo litakalofanyika nchini humo.
3
Mkurugenzi wa Masoko na Maendeleo ya Biashara ATCL Bw. Edward Nkwabi akimkabidhi tiketi Meneja wa timu ya Lohana Mahajan Bi. Sona Thakrar.
4
Mkurugenzi wa Masoko na Maendeleo ya Biashara ATCL Bw. Edward Nkwabi akiwa katika picha ya pamoja na maofisa wenzake kutoka shirika la ndege la ATCL baada ya kumalizika kwa hafla hiyo.

TTCL KUANZA KUTOA HUDUMA ZA KIFEDHA

$
0
0
Mhandisi wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Paul Magembe akitoa maelezo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, kuhusu mitambo ya kutolea huduma za kifedha iliyopo katika ofisi za Kampuni hiyo mkoani Dodoma.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, akitoa ufafanuzi kwa baadhi ya watendaji wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), alipokuwa akikagua mitambo ya kutolea huduma za kifedha iliyopo katika ofisi za Kampuni hiyo mkoani Dodoma.



Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, akitoa maelekezo kwa Meneja wa Shirika la Posta Nchini, kanda ya Dodoma Bw. Laurent Thobias (kulia), kuhusu utoaji wa matangazo ya huduma ya Posta mlangoni katika ofisi za Shirika hilo mkoani humo.



Meneja wa Wakala wa Ufundi na Umeme Nchini (TEMESA), Mkoa wa Dodoma, Eng. Bikulamchi Liberatus, akitoa ufafanuzi kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, kuhusu mikakati ya utengenezaji wa magari katika karakana iliyopo Mkoani humo.



Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, akizungumza na watumishi wa taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo (hawapo pichani), alipokutana nao Mkoani Dodoma.



Baadhi ya Watumishi wa Taasisi za Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, wakimsikiliza Waziri wa WIzara hiyo (hayupo pichani), alipokutana nao kuwapa mikakati ya utendaji wa Wizara hiyo, Mkoani Dodoma,

………….


Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa ameitaka Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) kujipanga na kuanza mkakati wa kutangaza huduma za fedha ambazo zitatolewa na kampuni hiyo mwanzoni mwa mwaka ujao.

Prof. Mbarawa ametoa agizo hilo baada ya kukagua mitambo itakayotumika kwa huduma hiyo ambayo itaongeza ushindani wa biashara kwenye huduma za simu nchini mkoani Dodoma.

“Lazima mjipange kwenye idara ya masoko kwa kuanza kutangaza huduma hiyo kupitia njia zote zikiwemo mitandao ya kijamii, ili wananchi warahisishiwe huduma za fedha kupitia TTCL”, amesema Waziri Prof. Mbarawa.

Aidha, ameiagiza kampuni hiyo kupitia idara ya masoko kujipanga kuona fursa zilizopo kwa kufahamu mahitaji ya wateja wao na kuhakikisha inaongeza wateja katika mkoa huo ili kuteka soko la ushindani ambapo Serikali inajipanga kuhamia huko.

Waziri Prof.Mbarawa ametaja baadhi ya maeneo ambayo TTCL inahitaji kuboresha zaidi ni upande wa Simu (Voice) na Data (video) ili kuweza kurahisisha mawasiliano kwa njia ya video conference kwa kuwa kuna baadhi ya watendaji wengine watabaki Dar es salaam.

“Mkiimarisha mawasiliano upande wa data mtarahisisha hata maamuzi na pia kazi zitaenda vizuri Serikalini hasa ukizingatia baadhi ya watumishi watakuwa hapa Dodoma na wengine Dar es Salaam”, amesisitiza Waziri Prof. Mbarawa.

Sambamba na hilo, Waziri Mbarawa ameliagiza Shirika la Posta nchini kuja na mkakati wa kuandaa matangazo ya kutambulisha huduma ya Posta mlangoni kwa jamii ili kuiwezesha huduma hiyo kutambulika kirahisi.

Amesisitiza kwa Taasisi hizo kuongeza kasi ya ukusanyaji mapato ili kufikia malengo waliojiwekea na kuendana na kasi ya utendaji wa Serikali ya Awamu ya Tano.

Akiwa mkoani humo Prof. Mbarawa amemhakikishia Mkuu wa Mkoa, Jordan Rugimbana kuboresha miundombinu nchini hususan katika mkoa huo ikiwemo kuboresha usafiri wa anga katika uwanja wa ndege wa Dodoma ili kuruhusu ndege kubwa kuweza kuruka na kutua.

Katika hatua nyingine, Waziri Mbarawa ameongea na watendaji pamoja na wafanyakazi wa Taasisi zilizo chini ya Wizara yake na kusisitiza kufanya kazi kwa kasi, uadilifu, ubunifu na kushirikiana katika utendaji wa majukumu yao ya kila siku.

Akizungumza kwa niaba ya wafanyakazi hao Meneja wa Wakala wa Majengo(TBA) mkoani humo, Arch. Masalu Bururu, amemuahidi Waziri huyo kutekeleza yale yote aliyowàagiza ili kuleta ufanisi na tija kwa Taifa.

Waziri Prof. Mbarawa amemaliza ziara yake ya siku kumi katika mikoa ya Mwanza, Mara, Arusha, Manyara na Dodoma ambapo ametembelea miradi mbalimbali ambayo inatekelezwa na Wizara hiyo.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

TANZANIA NA UAE ZAKUTANA KWA KIKAO CHA KWANZA CHA TUME YA USHIRIKIANO

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Balozi Augustine Mahiga (kushoto) kwa pamoja na Mhe. Reem Ebrahim Al Hashimy, Waziri wa Nchi anayeshughulikia Ushirikiano wa Kimataifa wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) wakisaini Mkataba wa Ushirikiano katika Sekta ya Anga. Mkataba huo ulisainiwa wakati wa kikao cha kwanza cha Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano kilichofanyika Abu Dhabi, Falme za Kiarabu tarehe 19 na 20, Desemba, 2016. 
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Masharika, Balozi Ramadhan Muombwa Mwinyi (kushoto) pamoja na Mkurugenzi wa Uchumi na Biashara wa Wizara ya Mambo ya Nje ya UAE wakiwekeana saini baadhi ya makubaliano yaliyoafikiwa. 
Mhe. Dkt. Mahiga na ujumbe alioongozana nao wakiwa katika kikao cha kwanza cha Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano na ujumbe wa UAE kilichofanyika Abu Dhabi tarehe 19 na 20, Desemba, 2016. 
Mratibu wa Mkutano kwa upande wa Serikali ya Tanzania kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Hangi Mgaka akifuatilia mkutano. 
Picha ya pamoja ya ujumbe wa Tanzania na UAE mara baada ya kukamilisha kikao cha kwanza cha Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano kilichofanyika Abu Dhabi tarehe 19 na 20, Desemba, 2016. 



TANZANIA NA UMOJA WA FALME ZA KIARABU ZAFANYA MKUTANO WA KWANZA TUME YA PAMOJA YA KUDUMU YA USHIRIKIANO HUKO ABU DHABI. 

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) zimefanya kikao cha kwanza cha Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano huko Abu Dhabi makao makuu ya Umoja wa Falme za Kiarabu. Kikao hicho kilifanyika tarehe 19 na 20, Desemba, 2016.

Mkutano huo ulioshirikisha sekta mbalimbali za Serikali zote mbili uliongozwa na Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (MP), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania na Mhe. Reem Ebrahim Al Hashimy, Waziri wa Nchi anayeshughulikia Ushirikiano wa Kimataifa wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE). 

Pamoja na mambo mengine, katika mkutano huo Tanzania na UAE zimekubaliana kushirikiana kwenye masuala ya Kidiplomasia; Uchumi; Utalii; Nishati; Kilimo; Sayansi na Teknolojia; Usafirishaji; Miundombinu; Ulinzi na Usalama; Elimu pamoja na Kazi na Ajira. 

Sambamba na mkutano huo, Tanzania na UAE zimesaini Mkataba wa Ushirikiano katika Sekta ya Anga (Bilateral Air Service Agreement-BASA) na Mkataba wa Ushirikiano katika Sekta ya Utalii. Vilevile Serikali zote mbili zimekubaliana kukamilisha na kusaini Mkataba wa Kutotoza Kodi Mara Mbili na Kuzuia Ukwepaji wa Kodi za Mapato; Mkataba wa Kuhamasisha na Kulinda Uwekezaji; pamoja na ushirikiano katika sekta ya Elimu, Afya, Ulinzi na Usalama, Ushirikiano katika Usafiri wa Majini, Kazi na Ajira pamoja ushirikiano katika masuala ya Zimamoto na Uokoaji. 

Mkutano huo umekuwa ni chachu katika mahusiano ya kihistoria ya nchi hizi mbili ambapo umeweka mazingira rasmi ya ushirikiano sio tu kwa Serikali bali pia kwa sekta binafsi. Mheshimiwa Waziri Mahiga katika hotuba yake ya ufungaji alitoa wito kwa Jumuiya za Wafanyabiashara na sekta binafsi kwa ujumla za Tanzania na Umoja wa Falme za Kiarabu kuchangamkia fursa zinazopatikana katika nchi hizi mbili kuafuatia mkutano huo.

Imetolewa na:

Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Dar es Salaam, 21 Desemba, 2016.

SHIRIKA LA TAIFA LA BIASHARA ZANZIBAR LATILIANA SAINI MAKUBALIANO YA KILIMO HAI CHA KARAFUU NA KAMPUNI YA GANEFRYD YA DENMARK

$
0
0
Na Ramadhani Ali/Maelezo.

Shirika la Biashara la Taifa Zanzibar (ZSTC) litapatiwa hati ya kuuza karafuu hai kwenye soko la Ulaya baada ya kutiliana saini na Kampuni ya Ganefryd ya Denmark makubaliano ya kuimarisha kilimo hai cha mazao tofauti (organic) kwa kuanzia na kilimo cha karafuu.

Sherehe za kutiliana saini makubaliano hayo zilifanyika katika ofisi za eneo tengefu Saateni na ZSTC iliwakilishwa na Mkurugenzi Mwendeshaji Dkt. Said Seif na Kampuni ya Genefryd iliwakilishwa na Afisa wake Bw. Pale Christeusen.

Akizungumza baada ya kutia saini makubaliano hayo, Dkt. Said amesema Zanzibar imekuwa ikifanya biashara ya karafuu kwa miaka mingi lakini hivi sasa itapanua wigo wa kuuza karafuu hai Ulaya na kupata faida kubwa.

Alisema ili Zanzibar iweze kutoa karafuu hai tahadhari kubwa inapaswa kuchukuliwa wakati wa kuotesha miche, ukuaji wake na kufikia wakati wa kuzaa bila ya kuingizwa aina yoyote ya mbolea zenye kemikali. 

Ameongeza kuwa uangalizi mkubwa pia unahitaji katika mchakato mzima wa kushughulika kilimo hicho kuanzia hatua ya kuchuma, kuanika, kuzihifadhi mpaka kuzisafirisha hivyo amewaomba wananchi kuunga mkono kuingia katika kilimo hai kwa vile karafuu ndio tegemeo lao na Taifa kwa jumla. 

Amesema sambamba na kuanzisha kilimo hai cha zao la karafuu Mkurugenzi Mwendeshaji wa ZSTC amewataka wananchi kuendeleza zao hilo katika mfumo wa kawaida kwa kuongeza upandaji miche na kuacha tabia ya kukata mikarafuu kwa ajili ya kuni, kufanyia mkaa na kujengea.

Afisa wa Kampuni ya Genefryd Bw. Pale Christeusen amesema hatua ya kutiliana saini makubaliano hayo ni kuimarisha ushirikiano kati ya taasisi hizo mbili na kuongeza kipato cha mkulima wa karafuu na kuiongezea Serikali mapato.

Bw. Christeusen amewashauri wakulima wa karafuu Zanzibar kuongeza kilimo hai cha karafuu kwa vile kinafaida kubwa katika soko la Ulaya.
 Mkurugenzi Mwendeshaji wa Shirika la Taifa la Biashara Zanzibar (ZSTC) Dkt. Said Seif akitiliana saini na mwakilishi wa Kampuni  Denmark Bw. katika ofisi za Shirika hilo ziliopo Saateni Mjini Zanzibar.

 Wafanyakazi wa  ZSTC wakisafisha karafuu hai kabla ya kuhifadhiwa kwenye mifuko maalum kwa ajili ya kuuzwa kwa wateja. 
 Afisa Masoko wa ZSTC Nassor Salum Nassor akitoa maelezo kwa waandishi wa habari kuhusu utaratibu unaotumika wa kupokea na kuzihifadhi karafuu hai kabla ya kuingizwa sokoni.
Picha na Makame Mshenga. 

SERIKALI YASIMAMISHA SHUGHULI ZA MFUKO WA UENDELEZAJI WA ZAO LA KOROSHO.

$
0
0
Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO.

Serikali imesimamisha shughuli za Mfuko wa Wakfu wa Kuendeleza Zao la Korosho ili kupisha uchunguzi wa matumizi ya fedha za mfuko huo.

Hatua hiyo imechukuliwa baada ya Mfuko huo kushindwa kutekeleza majukumu yake kikamilifu pamoja na kuwepo kwa malalamiko ya muda mrefu kuhusu utendaji wa mfuko huo.

Uamuzi huo umechukuliwa leo jijini Dar es Salaam na Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dkt. Charles Tizeba alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari juu ya mafanikio na changamoto ya zao hilo.

Dkt. Tizeba alisema kuwa lengo la uanzishwaji wa mfuko huo lililoafikiwa na Serikali pamoja na wadau wa korosho limekuwa halifanani na utekelezaji wake kwani maendeleo yote yanayoonekana kwenye zao hilo hayatokani na uwepo wa mfuko bali yanatokana na nguvu ya Serikali.

“Baada ya kutafakari utendaji wa mfuko huo tumegundua kuwa mfuko umeshindwa kutimiza malengo yaliyodhamiriwa, umeshindwa kusimamia na kutekeleza maelekezo mbalimbali yanayotolewa na Bodi ya Korosho hivyo tumeamua kusitisha shughuli za mfuko huo na kuanzia leo shughuli hizo zitatekelezwa na Bodi ya Korosho mpaka hapo tutakapotoa maelekezo mengine.”alisema Waziri huyo.

Waziri aliongeza sababu nyingine za kusitishwa kwa Mfuko huo ni kujihusisha na vitendo vinavyohujumu wakulima wa zao hilo hasa wakati wa ununuzi wa pembejeo pamoja na kununua viuatilifu vilivyo chini ya kiwango kwa bei kubwa, matumizi mabaya ya fedha kinyume cha Sheria na Kanuni za mfuko pamoja na kushindwa kutekeleza agizo la Serikali kwa kuweka fedha kwenye amana za muda maalumu katika Benki mbalimbali badala ya kupeleka Benki Kuu.

Aidha, Dkt. Tizeba alimtaka Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania anapowasilisha fedha zilizokusanywa na watu wanaosafirisha korosho nje ya nchi kuwasiliana kwanza na Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Korosho ili kufahamu usimamizi na utaratibu wa fedha hizo.

Kwa upande mwingine, Dkt. Tizeba ameizuia Menejimenti ya mfuko huo kufanya muamala wowote wa fedha za mfuko mpaka hapo maelekezo ya hatima yao yatakapotolewa na badala yake miamala yote itafanyika kwa utaratibu utakaopangwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango.

Ameiagiza Bodi ya Korosho kusimamia kwa haraka jukumu la upatikanaji wa pembejeo na viuatilifu kwa sababu msimu wa zao hilo umekaribia.

BODABODA ACHENI KUJIINGIZA KATIKA VITENDO VYA UHALIFU

$
0
0
ZAIDI ya wandesha bodaboda 500 wameweza kusajiliwa na mfuko wa Jamii wa GEPF katika fao la ‘Jikwamue Scheme’ ambapo huko wanapata huduma mbalimbali ikiwemo mkopo na siku za karibuni wataweza kufaidika na huduma za afya.

Hayo yalisemwa Jijini Dar es Salaam na Ofisa Masoko, Elivine Faini, wakati wa kufunga mafunzo ya waendesha boda Jijini Dar es Salaam yaliyokuwa yakifanyika katika maeneo mbalimbali Jijini humo, ambapo GEPF walikuwa mmoja wa watoa mada.

Faini alisema wameamua kujikita kwa kundi hilo kutokana na ukweli kwamba hakuna mfuko ambao mpaka sasa umewafikia na kuongeza kwamba nao wana mahitaji kama ilivyo kwa watu wa sekta nyingine katika mifuko ya hifadhi ya jamii.

Alisema ili kuweza kufaidika na fao hilo, mwendesha boda anatakiwa anatakiwa achangie sio chini ya miezi sita, ambapo ataweza kupata mkopo wa boda na kuondokana na adha ya kuajiriwa kwa kumiliki boda yake mwenyewe au kufungua biashara nyingine nje ya bodaboda na hivyo kujiongezea kipato.

Kuhusu fao la matibabu alisema bado wapo katika majadiliano na vyama vya boda ambapo alidai kwamba kutokana na usafiri huo kuwa mojawapo ya usafiri unaoongoza kwa matukio ya ajali kwa sasa itawasaidia kupata huduma za matibabu kwa uhakika pale inapotokea.

Awali akizungumza katika tukio hilo, Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Felix Lyaviva, alisema mpango wa GEPF kulifikia kundi hilo unapaswa kuigwa kwa kuwa ni moja ya kazi ambazo serikali imeamua kuihalalisha.

Lyaviva alisema ni wakati wa Bodaboda kuchangamkia fursa hiyo ya kujiwekea akiba kwa kuwa ukweli ni kwamba hakuna anayejua kesho yake atakuwa katika hali gani ya kukosa uwezo wa kufanya kazi.

Kuhusu mafunzo alisema angependa kuona kuwa hakuna boda anayeruhusiwa kuingia barabarani bila cheti cha mafunzo ya usalama barabarani wala leseni.

Naye Kamanda wa Polisi wa kikosi cha usalama Barabarani, Mohammed Mpinga,, alisema katika mafunzo hayo, madereva wemeweza kujifunza mambo mbalimbali ikiwemo usalama wa kujihami, namna ya kuikarabati pikipiki, muenekano wa dereva na somo la ujasirimali ambapo alidai wameshaanza kuona mabadiliko chanya kwa wahitimu hao.

Katibu wa waendesha boda, Daudi Laurian, alisema watahakikisha kampeni inayoanza Januari ya kutoruhusiwa boda wasio na mafunzo wala leseni, wanalisimamia wenyewe kwa kuwa limekuwa likiwaathiri hata ambao wanafuata taratibu.

Laurian alisema wanataka kuona wanauruka mwaka 2007 salama bila ya boda kuhusishwa na vitendo vya ujambazi wala ajali na kuongeza ni jukumu la kila mmoja kuhakikisha hayo yanatimia jambo litakalosaidiwa pia na kufuata sheria.
Mkuu wa Wilaya Temeke,Felix Lyaniva akizungumza na wamiliki na madereva pikipiki 500 juu ya kutojiingiza katika vitendo vya uhalifu ikiwemo kuwapora pochi abiria wao pamoja na kuwapakia majambazi kwa ajili ya kuenda kufanya uhalifu.leo jijini Dar es Salaam.picha zote na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii
Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohammed Mpinga akizungumza na wamiliki na madereva pikipiki 500 juu ya madereva wote wanatakiwa kutii sheria bila shuruti kwa wakati wote wanapokua barabarani ikiwa ni pamoja na kuvaa helment,kutokupakia mishikaki pamoja na kuendesha chombo wakiwa hawajalewa ili kuepusha ajali zisizokuwa za lazima leo jijini Dar es Salaam.
Afisa Masoko wa Mfuko wa Maſao ya Kustaafu-GEPF Jacob Ondara akizungumza na wamiliki na madereva pikipiki 500 juu umuhimu wa kujiungaa na Mfuko wa huo ilikuweza kupata bima ya Afya kwaajili ya kupata matibababu kwa haraka, leo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Wilaya Temeke,Felix Lyaniva akimkabidhi cheti Mwakilishi wa Darasa la Kibaha,Akas Kiruwa katika hafla ya kuwatunuku vyeti madelewa wa pikipiki leo jijini Dar es Salaam.
Viongozi wa Madara ya Mbalilmbli wa madereva wa pikipiki wakiwa katika picha ya pamoja katika hafla ya kuwatunuku vyeti madelewa wa pikipiki leo jijini Dar es Salaam.
Madereva wa pikipiki wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya Temeke,Felix Lyaniva katika hafla ya kuwatunuku vyeti madelewa wa pikipiki leo jijini Dar es Salaam.

WIZARA YA AFYA YAENDESHA MAFUNZO YA KUPAMBANA NA MAGONJWA YASIOAMBUKIZA NCHINI

$
0
0
 Mkurugenzi wa Tiba Wizara ya Afya Dkt. Margaret Mhando akipitia baadhi ya nyaraka za kufundishia kabla ya kufungua mafunzo ya kupambana na magonjwa yasioambukiza kwa watoa huduma ngazi za mikoa na wilaya yaliyofanyika Mkoani Morogoro.
 Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Magonjwa yasioambukiza Dkt. Sarah Maongezi akiongea na madaktari na watoa huduma hawapo pichani wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya kupambana na magonjwa yasioambukiza kwa watoa huduma ngazi za mikoa na wilaya yaliyofanyika Mkoani Morogoro.
 Mratibu wa Magonjwa yasioambukiza Mkoa wa Dar es salaam Dkt. Digna Riwa akitoa mafunzo kwa waganga na watoa huduma hawapo pichani wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya kupambana na magonjwa yasioambukiza kwa watoa huduma ngazi za mikoa na wilaya yaliyofanyika Mkoani Morogoro.
 Baadhi ya madaktari kutoka mikoa tofauti nchini wakifuatilia kwa makini mafunzo kutoka kwa mkufunzi hayupo pichani wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya kupambana na magonjwa yasioambukiza kwa watoa huduma ngazi za mikoa na wilaya yaliyofanyika Mkoani Morogoro.
Mkurugenzi wa Tiba Wizara ya Afya Dkt. Margaret Mhando katikati waliokaa akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya madaktari kutoka mikoa tofauti nchini wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya kupambana na magonjwa yasioambukiza kwa watoa huduma ngazi za mikoa na wilaya yaliyofanyika Mkoani Morogoro.

Na Ally Daud
WIZARA ya Afya ,Maendeleo  ya Jamii ,Jinsia ,Wazee na Watoto kupitia kitengo cha Magonjwa yasioambukiza (NCD) chini ya Kurugenzi ya Tiba inaendesha mafunzo ya kupambana na magonjwa yasioambukiza kwa watoa huduma ngazi za mikoa na wilaya.

Akifungua mafunzo hayo leo jijini Morogoro Mkurugenzi wa Tiba Wizara ya Afya Dkt. Margaret Mhando amesema kuwa wameamua kuanzisha mpango huo ili kuwapa nguvu na uwezo watoa huduma kwa ajili ya kupambana na magonjwa hayo.

“Magonjwa yasiyo ya kuambukiza yamekuwa yakiongezeka kwa kasi sana duniani na haswa nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania hivyo hatuna budi kuongeza juhudi za kupambana nayo” alisema Dkt. Mhando

Aidha Dkt. Mhando amesema kuwa pamoja na juhudi zinazofanywa na Wizara katika kupambana na magonjwa hayo kila mkoa na wilaya lazima ziangalie uwezekano wa kuifanya NCD kuwa kipaumbele katika mipango yao ya  maendeleo.

Kwa mujibu wa Dkt. Mhando amesema kuwa viashiria vya magonjwa yasiyo ya kuambukiza imeonyesha kuongezeka kwa hali ya juu ambapo  idadi ya watu wanaovuta sigara ni asilimia 15.9 wanaokunywa pombe ni asilimia 29.3, wenye uzito uliopita kiasi 34.7, shinikizo la damu ni asilimia 25.9 na wagonjwa wa kisukari ni asilimia 9.1.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Magonjwa yasioambukiza Dkt. Sarah Maongezi amesema kuwa wanatakiwa kupunguza moja ya tatu ya vifo vitokanavyo na magonjwa yasiyo ya kuambukiza kwa kukinga, kutibu na kuzingatia afya ya akili Kufikia mwaka 2030.

Aidha Dkt. Maongezi amesema kuwa  wanatarajia waganga wa ngazi za mikoa na wilaya kufanya kazi kwa nguvu na kwa ukaribu zaidi na kitengo cha magonjwa yasiyo ya kuambukiza cha Wizara ili huduma hizi ziwafikie watu wote hadi ngazi ya jamii.

Mafunzo hayo ya siku tatu yanayofanyika jijini Morogoro yanalenga kuwafundisha madaktari na watoa huduma kuhusu kupambana na ya magonjwa yasioambukiza ikiwemo kisukari, magonjwa ya moyo, shinikizo la damu, kansa, ajali za barabarani  na uzito kupita kiasi.

Viewing all 46395 articles
Browse latest View live




Latest Images