Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1077 | 1078 | (Page 1079) | 1080 | 1081 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii imetoa ufafanuzi wa uamuzi wake wa kuzuia biashara ya usafirishaji wa wanyamahai nje ya nchi kwa kipindi cha miaka mitatu mfululizo na kusema kuwa uamuzi huo ulitolewa kwa lengo la kupanga vizuri biashara hiyo kwa faida ya serikali na wafanyabiashara wenyewe.

  Ufafanuzi huo umetolewa jana na Waziri wa Wizara hiyo, Prof. Jumanne Maghembe katika kikao alichokiitisha wizarani hapo na wafanyabiashara wa wanyamahai wa makundi ya wadudu, vyura, mijusi, ndege, nyani na tumbili ambao walitaka kupata ufafanuzi wa hatima ya biashara yao kutoka serikalini.

  Katika risala iliyosomwa na kiongozi wa wafanyabiashara hao, Adam Rashid Warioba kwa Waziri Maghembe, aliiomba Serikali kutoa ufafanuzi wa hatma ya biashara yao iliyofungiwa ambayo imekuwa tegemeo pekee katika kuendesha maisha yao huku wakitaka kujua hatma ya wanyamahai waliohifadhiwa na gharama zao walizolipia Serikalini.

  Akitoa ufafanuzi wa uamuzi wa Serikali kufungia biashara hiyo kwa wafanyabiashara hao, Prof. Maghembe amesema wanyamahai wengi kutoka nchini Tanzania wamekuwa wakisafirishwa nje ya nchi bila ya kufuata utaratibu maalum ikiwemo vibali vya kukamata na kuwasafirisha wanyama hao jambo ambalo limekuwa likiikosesha serikali mapato mengi.

  “Wapo kati yenu ambao walikuwa wanasafirisha wanyamahai kinyume cha sheria, bila vibali vyovyote, na wanyama wa Tanzania walikuwa wakimatwa kwenye bandari na viwanja vya ndege, ambao wanasafirishwa kinyume cha sheria, wengi tu, na ndio maana Serikali ikasema hii biashara tusimamae kwanza tuwekwe utaratibu ambao kila mtu ataufuata, na ambao hautaweza kututia aibu huko nje” alisema.

  Alisema sababu nyingine iliyopelekea serikali kufunga biashara hiyo kwa muda ni bei ndogo inayouzwa wanyama hao nje ya nchi ambayo haiwanufaishi wafanyabiashara na Serikali ukilinganisha na thamani yake kwa kile wanachoenda kufanyiwa, alitolea mfano tumbili ambao hufanyiwa utafiti wa madawa mbali mbali na baadae kuuzwa mabilioni ya fedha huku tumbili huyo akiuzwa kwa dola 25 tu.

  “Nimefurahi yule bwana aliyesema tumbili mmoja ni dola 25, lakini akasema hao ndio wanafanyamedical research (utafiti wa madawa) yote duniani, sasa sisi tunapata dola 25 na wenzetu wanafanya research (utafiti) wanatuuzia madawa yote billions of dollars (mabilioni ya dola za kimarekani), tuweke utaratibu na ninyi mtakapokuwa mnafanya hii biashara mpate sio lazima serikali ndio lazma ipate, mpate kilicho sawa na thamani ya wanyama mnaowauza”, alisema Prof. Maghembe.

  Aliwahakikishia wafanyabiashara hao kuwa Serikali ya awamu ya tano ni sikivu hivyo kuahidi kushuulikia changamoto walizoziwasilisha hadi kufikia Januari 10, mwakani (2017), aliwaeleza kuwa hatma ya wanyamahai ambao wamewahifadhi pamoja gharama za vibali walizowalipia serikalini zitashuulikiwa.

  “Ambacho ninaweza kuwaambia hapa leo, kwamba tumepata hii taarifa, tunayo ile idadi ambayo imepitiwa na wataalamu huko kwenye mazizi, tunazo zile permit (vibali) za serikali ambazo mmepewa na leseni, vyote vile mlivyonavyo na sisi tunavyo, tutavipitia vyooote kabisa, alafu tutaona ni namna gani tutawainua kwa kuwafuta jasho”, alisema.

  Aliongeza kuwa “Tutaangalia kila mfanyabiashara ameilipa nini serikali, kwa wanyama hawa ambao wapo, ambao katazo lilipofanywa walikuwa nao kwenye mazizi yao na wanyama hao tunawafanyia tathmini tukishakamilisha tutaamua sasa wanyama hao wanapelekwa wapi, na maeneo yenyewe ni machache tu, ama kwenye mazoo, ili waweze kutunzwa na kuendelezwa kwa vile ni vigumu kuwarudisha tena maporini.

  “Na kutokana na vibali na risiti mbalimbali ambazo wameilipa serikali katika kuwapata hao wanyama basi tutaviangalia na kuangalia utaratibu wa kuwarudishia wale wafanyabiashara hela zao”.

  Akizungumzia lalamiko la wafanyabiashara hao kuwa wao wamezuiliwa kufanya biashara hiyo huku mfanyabiashara mmoja kutoka nje akiruhusiwa kufanya biashara hiyo kwa tangazo la serikali, Prof. Maghembe anasema “Na hilo tangazo mnalosema lina mtu amebebwa hamna ruhusa ya mtu kubebwa hapa, na mtu atayempa huyo mtu kibali mnafahamu kitakachotokea, hakuna ruhusu, ndivyo serikali ilivyosema”.

  Mei 26, mwaka huu, akifanya majumuisho ya hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya wizara yake kwa mwaka 2016/17, Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe, alitangaza kuwa ni marufuku kusafirisha wanyamahai wote nje ya nchi kwa miaka mitatu mfululizo.

  “Kuanzia sasa (saa moja na dakika tano usiku) kwa miaka mitatu serikali imepiga marufuku usafirishaji wa wanyamahai wote kwenda nje ya nchi, hata chawa wa Tanzania hawataruhusiwa kusafirishwa nje, Na katika kipindi hiki cha miaka mitatu, idara ya wanyamapori itafanya kazi ya kuishauri serikali namna gani biashara hiyo itakavyoendeshwa”, alisema Prof. Maghembe.

  Imetolewa na;
  Hamza Temba
  Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  Wizara ya Maliasili na Utalii

  0 0

    Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) (kushoto) akizungumza na ujumbe kutoka Mfuko wa Maendeleo wa Kuwait, kuhusu miradi ya miundombinu itakayofadhiliwa na Mfuko huo, ukiwemo mradi wa barabara kwa kiwango cha lami kutoka Chaya kwenda Nyahua mkoani Tabora. Kulia ni mwakilishi wa Balozi wa Kuwait hapa nchini Bw. Mohammad Rashid Alamiri, Makao Makuu ya Wizara, Jijini Dar es salaam.
  Maafisa waandamizi wa Wizara ya Fedha na Mipango wakimsikiliza Mwakilishi wa Balozi wa Kuwait Nchini Tanzania Bw. Mohammad Rashid Alamiri (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza katika Kikao kati yake na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), katika Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es salaam.
  Wataalamu toka Mfuko wa Maendeleo wa Kuwait (kushoto) na wataalamu kutoka Tanzania (kulia) wakijadili kuhusu mkopo wa masharti nafuu kutoka Serikali ya Kuwait, utakao saidia kujenga barabara Mkoani Tabora, Mazungumzo yaliyofanyika katika ukumbi wa Wizara hiyo, Jijini Dar es salaam.
   Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) (kushoto) akipeana mkono na Mwakilishi wa Balozi wa Kuwait Bw. Mohammad Rashid Alamiri huku wakifurahia jambo baada ya kumalizika kwa mkunano kati yao uliojikita katika mikopo yenye masharti nafuu kwa ajili ya ujenzi wa miradi mbalimbali ikiwemo barabara na sekta ya afya, Mkutano huo umefanyikaatika Makao makuu ya Wizara, Jijini Dar es salaam.
   Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) (kulia), akisalimiana na Mshauri wa masuala ya ufundi kutoka Kuwait Bw. Mohammad Alhadidi, baada ya kumalizika kwa kikao kati ya Waziri huyo na Wajumbe kutoka Mfuko wa Maendeleo wa Kuwait, katika ukumbi wa Wizara hiyo Jijini Dar es salaam.
   Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe toka Mfuko wa Maendeleo wa Kuwait (Kuwait Fund) baada ya kumalizika kwa kikao kati yake na wajumbe hao ambapo mbali na kutoa mkopo wa ujenzi wa barabara kutoka Chaya kwenda Nyahua mkoani Tabora, walionesha nia ya kutoa mikopo mingine yenye masharti nafuu katika miradi mbalimbali ya maendeleo nchini Tanzania. Kikao hicho kimefanyika Makao Makuu ya Wizara hiyo, Jijini Dar es salaam. (Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-WFM)

  Na Benny Mwaipaja, WFM, Dar es salaam
  Serikali ya Kuwait imeahidi kuipatia Tanzania mkopo wenye riba nafuu wa dola za Kimarekani Milioni 34 kwa ajili ya ujenzi wa barabara yenye urefu wa Kilometa 85 kwa kiwango cha lami kutoka eneo la Chaya hadi Nyahua mkoani Tabora.

  Hayo yamesemwa Jijini Dar es salaam na mwakilishi wa Balozi wa Kuwait hapa nchini, Bw. Mohammad Rashid Alamiri, aliyeongoza ujumbe kutoka Mfuko wa Maendeleo wa Kuwait, ulipomtembelea na kufanya mazungumzo na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, kuhusu masuala mbalimbali ya ushirikiano wa kiuchumi na kijamii kati ya Tanzania na Kuwait.

  Dkt. Mpango ameushukuru Mfuko wa Maendeleo wa Kuwait (Kuwait Fund) kwa kuipatia Tanzania mkopo wenye masharti nafuu utakaochochea maendeleo kwa Watanzania hususani wanaoishi maeneo hayo kutokana na umuhimu wa barabara katika kukuza uchumi wa Taifa.

  Amesema kuwa kipande hicho cha barabara kutoka Chaya hadi Nyahua, ambacho kiko Barabara Kuu itokayo Dar es salaam kwenda katika mikoa ya Tabora na Kigoma, licha ya umuhimu wake katika kukuza biashara na usafiri na usafirishaji wa abiria na mizigo ikiwemo inayokwenda nchi jirani, ilikuwa haijapata fedha kwa ajili ya ujenzi wake.

  “Riba waliyoiweka mezani kwa mazungumzo ni asilimia 2 lakini nimewaomba waangalie uwezekano wa kuiteremsha walau ifikie asilimia 1.5 na wamependekeza kipindi cha kuanza kulipa mkopo kiwe miaka ishirini ijayo lakini nimewaomba wasogeze hadi kufikia miaka 25 kama ilivyo kwa mradi wa Hospitali ya Mnazimmoja” aliongeza Dkt. Mpango

  Dkt. Mpango amesema Serikali ya Kuwait kupitia Mfuko wake huo wa Maendeleo wameonesha nia ya kutoa mkopo wenye masharti nafuu kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa Hospitali ya Mnazi Mmoja iliyoko Visiwani Zanzibar.

  “Nawahakikishia kuwa baada ya muda si mrefu wananchi wa mikoa ya Tabora na Kigoma watarajie kuona mkandarasi akiingia kazini ili kujenga barabara hii muhimu sana kwao na kwa uchumi wa Taifa kwa ujumla” Alisisitiza Dkt. Mpango.

  Ameeleza kuwa ujenzi wa kipande cha barabara hiyo kutoka Chaya hadi Nyahua unatarajia kugharimu shilingi Bilioni 61 lakini Kuwait haitatoa fedha zote hivyo ameuomba Mfuko huo uangalie uwezekano wa kutoa kiasi hicho chote cha fedha ili uweze kukamilika mapema.

  0 0

  Mbunge waArusha mjini Godbless Lema na mkewe Neema Lema

  Na,Vero Ignatus.Arusha.

  Kesi iliyokuwa isikilizwe leo 22 disemba 2016 inayomkabili mbunge wa Arusha mjini Godbless Leman na mkewe Neema Lema ya kumtukana mkuu wa mkoa Mrisho Gambo imeahirishwa kutokana na hali ya lema kuwa mbaya gerezani.

  Taarifa za Lema kushindwa kufika mahakamani zimetolewa na wakili wa serikali Elizabeth Swai leo asubuhi kwa hakimu mfawidhi katika mahakama ya hakimu mkazi Augustino Rwezile ,alisema alipata taarifa kutoka kwa Afisa Magereza mshatakiwa kwanza anumwa hivyo siku ya leo alipewa mapumziko pamoja na hayo taarifa hizo hazijaeleza kwa undani ni tatizo gani linamsumbua mbunge huyo.

  Pia alisema alipewa cheti cha mgonjwa cha zahanati ambacho kilionyesha mahudhurio ya mgonjwa kwenye zahanati hiyo kutokana na kuwepo na taarifa za kuumwa za mbunge huyo na kushindwa kufika mahakamani,aliiomba mahakama ipange tarehe nyingine .

  Leo ilikuwa ni siku ya kusomewa hoja za awali kwa mbunge huyo na mkewe Neema Lema , ambapo pia shahidi wa kwanza kutoka jamhuri alikuwa Georgr Katabazi alikuwa anatoa ushahidi.

  Hata hivyo hakimu mfawidhi
  Augustino Rwezile amesema kuwa kesi hiyo imeahirishwa hadi tarehe 18 Januari 2017

  Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema na mkewe Neema Lema wanakabiliwa na kesi ya mkumtukana mkuu wa mkoa Mrisho Gambo.

  0 0

  Anna Sangai (mbele) programu programu kutoka TGNP Mtandao akiwasilisha mada katika mkutano na wananchi wa Kata za Kipunguni, Kivule na Mzinga zote za jijini Dar es Salaam kutoa elimu juu ya namna ya kukabiliana na vitendo vya ukatili wa kijinsia ikiwemo vile vya ukeketaji ambavyo vimekuwa vikifanywa na baadhi ya jamii maeneo hayo. Anna Sangai (mbele) programu programu kutoka TGNP Mtandao akiwasilisha mada katika mkutano na wananchi wa Kata za Kipunguni, Kivule na Mzinga zote za jijini Dar es Salaam kutoa elimu juu ya namna ya kukabiliana na vitendo vya ukatili wa kijinsia ikiwemo vile vya ukeketaji ambavyo vimekuwa vikifanywa na baadhi ya jamii maeneo hayoAnna Sangai (kulia) programu programu kutoka TGNP Mtandao akiwasilisha mada katika mkutano na wananchi wa Kata za Kipunguni, Kivule na Mzinga zote za jijini Dar es Salaam kutoa elimu juu ya namna ya kukabiliana na vitendo vya ukatili wa kijinsia ikiwemo vile vya ukeketaji ambavyo vimekuwa vikifanywa na baadhi ya jamii maeneo hayo. Anna Sangai (kulia) programu programu kutoka TGNP Mtandao akiwasilisha mada katika mkutano na wananchi wa Kata za Kipunguni, Kivule na Mzinga zote za jijini Dar es Salaam kutoa elimu juu ya namna ya kukabiliana na vitendo vya ukatili wa kijinsia ikiwemo vile vya ukeketaji ambavyo vimekuwa vikifanywa na baadhi ya jamii maeneo hayoAnna Sangai (kulia) programu programu kutoka TGNP Mtandao akiwasilisha mada katika mkutano na wananchi wa Kata za Kipunguni, Kivule na Mzinga zote za jijini Dar es Salaam kutoa elimu juu ya namna ya kukabiliana na vitendo vya ukatili wa kijinsia ikiwemo vile vya ukeketaji ambavyo vimekuwa vikifanywa na baadhi ya jamii maeneo hayo. Anna Sangai (kulia) programu programu kutoka TGNP Mtandao akiwasilisha mada katika mkutano na wananchi wa Kata za Kipunguni, Kivule na Mzinga zote za jijini Dar es Salaam kutoa elimu juu ya namna ya kukabiliana na vitendo vya ukatili wa kijinsia ikiwemo vile vya ukeketaji ambavyo vimekuwa vikifanywa na baadhi ya jamii maeneo hayo.Muwasilishaji wa mada, Bi. Agnes Lukanga (kulia mbele) kutoka TGNP Mtandao akizungumza katika mkutano wa wananchi wa Kata za Kipunguni, Kivule na Mzinga zote za jijini Dar es Salaam kutoa elimu juu ya namna ya kukabiliana na vitendo vya ukatili wa kijinsia ikiwemo vile vya ukeketaji ambavyo vimekuwa vikifanywa na baadhi ya jamii maeneo hayo. Muwasilishaji wa mada, Bi. Agnes Lukanga (kulia mbele) kutoka TGNP Mtandao akizungumza katika mkutano wa wananchi wa Kata za Kipunguni, Kivule na Mzinga zote za jijini Dar es Salaam kutoa elimu juu ya namna ya kukabiliana na vitendo vya ukatili wa kijinsia ikiwemo vile vya ukeketaji ambavyo vimekuwa vikifanywa na baadhi ya jamii maeneo hayo.Mmoja wa viongozi wa Dini, Issa Abdullah (mbele) akijadili jambo katika mkutano wa kutoa elimu kwa wananchi kukabiliana na vitendo vya ukatili wa kijinsia vikiwemo vile vya ukeketaji. Mkutano huo ulifanyika katika Kata za Kipunguni, Kivule na Mzinga zote za jijini Dar es Salaam. Mmoja wa viongozi wa Dini, Issa Abdullah (mbele) akijadili jambo katika mkutano wa kutoa elimu kwa wananchi kukabiliana na vitendo vya ukatili wa kijinsia vikiwemo vile vya ukeketaji. Mkutano huo ulifanyika katika Kata za Kipunguni, Kivule na Mzinga zote za jijini Dar es SalaamMjumbe wa Serikali ya Mtaa wa Kipunguni, Hija Mzome (mbele-kulia) akiwasisitisha washiriki wa mkutano huo kukubali kubadilika na kuachana na vitendo vya kikatili vilivyopitwa na wakati hasa ukeketaji. Mjumbe wa Serikali ya Mtaa wa Kipunguni, Hija Mzome (mbele-kulia) akiwasisitisha washiriki wa mkutano huo kukubali kubadilika na kuachana na vitendo vya kikatili vilivyopitwa na wakati hasa ukeketaji.Baadhi ya washiriki wakiwa katika mkutano wa kutoa elimu kwa wananchi kukabiliana na vitendo vya ukatili wa kijinsia vikiwemo vile vya ukeketaji. Mkutano huo ulifanyika katika Kata za Kipunguni, Kivule na Mzinga zote za jijini Dar es Salaam. Baadhi ya washiriki wakiwa katika mkutano wa kutoa elimu kwa wananchi kukabiliana na vitendo vya ukatili wa kijinsia vikiwemo vile vya ukeketaji. Mkutano huo ulifanyika katika Kata za Kipunguni, Kivule na Mzinga zote za jijini Dar es Salaam.Mjumbe wa Shina namba Saba Majohe, Mohamed Kassim (mbele) akichangia jambo katika mkutano huo wa kutoa elimu kwa wananchi kukabiliana na vitendo vya ukatili wa kijinsia vikiwemo vile vya ukeketaji. Mkutano huo ulifanyika katika Kata za Kipunguni, Kivule na Mzinga zote za jijini Dar es Salaam. Mjumbe wa Shina namba Saba Majohe, Mohamed Kassim (mbele) akichangia jambo katika mkutano huo wa kutoa elimu kwa wananchi kukabiliana na vitendo vya ukatili wa kijinsia vikiwemo vile vya ukeketaji. Mkutano huo ulifanyika katika Kata za Kipunguni, Kivule na Mzinga zote za jijini Dar es SalaamMmoja wa washiriki wa mkutano huo akichangia katika mkutano wa kutoa elimu kwa wananchi kukabiliana na vitendo vya ukatili wa kijinsia vikiwemo vile vya ukeketaji. Mkutano huo ulifanyika katika Kata za Kipunguni, Kivule na Mzinga zote za jijini Dar es Salaam. Mmoja wa washiriki wa mkutano huo akichangia katika mkutano wa kutoa elimu kwa wananchi kukabiliana na vitendo vya ukatili wa kijinsia vikiwemo vile vya ukeketaji. Mkutano huo ulifanyika katika Kata za Kipunguni, Kivule na Mzinga zote za jijini Dar es Salaam.Mmoja wa washiriki wa mkutano huo akichangia katika mkutano wa kutoa elimu kwa wananchi kukabiliana na vitendo vya ukatili wa kijinsia vikiwemo vile vya ukeketaji. Mkutano huo ulifanyika katika Kata za Kipunguni, Kivule na Mzinga zote za jijini Dar es Salaam. Mmoja wa washiriki wa mkutano huo akichangia katika mkutano wa kutoa elimu kwa wananchi kukabiliana na vitendo vya ukatili wa kijinsia vikiwemo vile vya ukeketaji. Mkutano huo ulifanyika katika Kata za Kipunguni, Kivule na Mzinga zote za jijini Dar es Salaam.

  0 0  0 0

  Rais wa gambia Yahya Jammeh ameonya kuwa atakataa jaribio lolote la viongozi wa kieneo kumlazimisha kuondoka madarakani licha ya kushindwa katika uchaguzi na mfanyibiashara Adama Barrow.

  Akihutubia wanachama wa muungano wa Bar Afrika nchini humo Bw Jammeh alisema: ''Waje wajaribu kuniondoa.wanasubiri nini? mimi ni mtu mpenda amani lakini haimaanishi kwamba sitalitetea taifa langu, kwa ujasiri na uzalendo na kuibuka mshindi''.

  Amesema kuwa alikataa wito wa muungano wa viongozi wa mataifa ya Magharibi ECOWAS akiwemo rais Muhammadu Buhari wa Nigeria na Ellen Johnson Sirleaf wa Liberia kuondoka nchini Gambia.

  Akiongezea: ''Wao ni kina nani wa kuniambia mimi niondoke nchini mwangu.

  Amewashtumu viongozi hao kwa kuingilia a ya ndani ya Gambia.

  ECOWAS tayari imesema kuwa inamtambua bw Barrow kama rais wa taifa hilo na kwamba litachukua hatua zozote kuhakikisha kuwa matokeo ya uchaguzi yanaheshimiwa.

  Viongozi wa kieneo watahudhuria kuapishwa kwa Bw Barrow mnamo mwezi Januari 18 kulingana na taarifa ya Ecowas.

  Rais Jammeh awali alikuwa amekubali matokeo ya uchaguzi huo manamo tarehe mosi mwezi Disemba ,lakini baadaye akaitisha uchaguzi mpya utakaoandaliwa na tume ya uchaguzi inayomcha mungu.

  Alisema kwamba matokeo hayo uchaguzi yaligubikwa na dosari.
   

  0 0

  Na Ripota wa globu ya Jamii Ileje.

  Upepo na mvua kubwa vimesababisha uharibifu wa mali na miundo mbinu katika kata ya Mbebe Wilayani Ileje mkoani Songwe na kusababisha majeruhi wengi na kifo cha mtu mmoja katika kata hiyo.

  kwa mujibu wa ripota wa globu ya jamii aliyepo wilayani humo amesema kuwa mvua za mwaka hu katika Wilaya hiyo ni chache lakini ni hatari sana kwani tukio hilo la na Mvua za upepo mkali ni lapili hali inayotishia usalama wa wakazi wa eneo hilo.

  kwa upande wake mkuu wa Wilaya hiyo Joseph Mkude amesema kuwa ameshafika katika eneo la tukio lilitokea janga hilo la upepo na kuzungumza na wananchi namna ya kuchukua thadhari.

  "Nimewaambia wananchi wawe waungwana kwa kusaidia siku ya leo, kwani kuanzia kesho halmashauri itatoa utaratibu hata hivyo katika ajali hiyo ni mtu mmoja tu ambaye amefariki huku wengine wakiwa wamekimbizwa katika hospitali ya Itumba kwa ajili ya matibabu zaidi"amesema Dc Mkude
   Baadhi ya nyumba zilizoharibiwa na Mvua kubwa ilionyesha wilayani humo
   Mkuu Wa Wilaya ya Ileje Joseph Mkude akikagua barabara
   Mkuu Wa Wilaya ya Ileje Joseph Mkude akiongea na Wananchi
   

  0 0

  Pichani kulia ni mrembo wa Taifa Miss Tanzania 2016 Diana Edward akizungumza na baadhi ya waandishi wa habari mara baada ya kuwasili  leo (21 Desemba 2016) akitokea Washington DC Marekani, ambapo alikwenda kushindana katika mashindano ya urembo ya Dunia. Miss World Beauty Contest 2016.
  Miss Tanzania 2016 Diana Edward aliwasili nchini muda wa saa 10 alasiri na Shirika la ndege la Emirates, na kulakiwa na Waandishi wa Habari, Wazazi wake, baba na mama mzazi, wadau, pamoja na wajumbe wa Kamati ya Miss Tanzania.

  Uongozi wa Kampuni ya Lino International Agency Limited utatoa ratiba ya shughuli zake za kijamii hapo baadae, baada ya mapumziko ya mwisho wa mwaka.

  Tunawatakia Heri na Baraka za Sikukuu ya X Mass pamoja na Mwaka mpya wa 2017.
  Mrembo wa Taifa Miss Tanzania 2016 Diana Edward akilakiwa na wazazi wake mara baada ya kuwasili  leo (21 Desemba 2016) akitokea Washington DC Marekani, ambapo alikwenda kushindana katika mashindano ya urembo ya Dunia. Miss World Beauty Contest 2016.

  0 0


  Mkurugenzi wa Kampuni ya Global Education Link akifafanua jambo kwenye maonyesho ya vyuo vya nje yanayoendelea katika viwanja vya kumbukumbu ya Azimio la Arusha, Jijini Arusha.
  Meneja wa Global Education Link tawi la Arusha, Regina Lema (wa pili kutoka kushoto) akimsikiliza kwa umakini mmoja wa watu waliofika kwenye maonyesho ya vyuo vya nje yanayoendelea katika viwanja vya kumbukumbu ya Azimio la Arusha, Jijini Arusha

  HAKUNA Ubishi kwamba Tanzania ni nchi inayohitaji teknolojia nyingi mpya ili iweze kukua haraka kiuchumi kwa kuendana na kauli ya Serikali inayotaka kuona Tanzania inakuwa nchi ya viwanda.

  Mojawapo ya njia inayoweza kusaidia kukuza haraka teknolojia nchini ni kwa Watanzania kwenda nje ya nchi kusoma kisha kurudi na ujuzi kuliendeleza taifa. Hivi ndivyo ilivyofanya nchi nyingi Duniani, hatimaye leo nchi hizo zimevuka kwenye lindi la umaskini.

  Kwa wale ambao wanafuatilia historia ya Tanzania watakubaliana na ukweli kwamba nchi hii ilikotoka haikuwa na teknolojia nyingi muhimu, zikiwamo zile zilizosaidia kuharakisha maendeleo.

  Kwamba, mambo mengi nchini yamekuwa yakifanyika kwa staili za kijadi, kwa mfano hata kupata mchele, mtu alilazimika kutumia nguvu kubwa kutwanga mpunga au ilikuwa ni lazima kutumia kinu kutwanga mahindi ili kupata unga, lakini ni kupitia teknolojia mpya, leo kuna mashine nyingi za kufanya kazi hizo katika maeneo mbalimbali nchini.  Kwa sasa kuna teknolojia nyingi nchini, nyingi zikitokea nje ya nchi. Nyingi za teknolojia hizi zililetwa na wafanyabiashara au wasomi wachache waliokwenda nje, kwani sio wengi ambao wamekuwa na ufahamu kuhusu vyuo vya nje.

  Ukilinganisha na mataifa mengine kama Kenya, Nigeria na mengineyo ya Afrika Mashariki, Tanzania imekuwa na idadi ndogo ya watu wanaokwenda kusoma nje, sababu kubwa pamoja na mambo mengine ni kutokuwa na ufahamu kuhusu vyuo vya nje.

  Aidha wapo wengine wana imani isiyo sahihi kwamba kusoma nje inamuhitaji mtu kuwa na fedha nyingi, imani ambayo sio kweli, kuna vyuo nchini ni gharama zaidi kuliko vya nje.

  Kwa mfano baadhi ya kozi nje unaweza kusoma Shahada kwa maana ya ada na gharama za malazi kwa mwaka ni kati ya dola 3100 hadi 5000, sawa na Shilingi milioni sita hadi kumi. Hapa nchini kuna shule hutoza ada ya dola 5000 (zaidi ya milioni kumi za Kitanzania) kwa mwaka kwa elimu ya msingi au sekondari.  Mkakati wa kuielimisha jamii kuhusu vyuo vya nje

  Ni kutokana na kuonekana kwamba Watanzania wengi wanahitaji ufahamu zaidi kuhusu vyuo vya nje, Kampuni ya Global Education Link (GEL) ilianzishwa, lengo kubwa likiwa ni kuhakikisha inawasaidia Watanzania kuwapa maelezo sahihi kuhusu vyuo vya nje na mwongozo mzima kuhusiana na uchaguzi sahihi wa masomo.

  “Nimesoma nje na nimekuwa nikiona tofauti iliyoko ya kwenda nje kati ya vijana wa Kitanzania na wenzetu wa mataifa mengine ya Afrika Mashariki, ndipo mwaka 2006 nikalazimika kuanzisha GEL, na sasa nimekuwa nikiendesha maonyesho katika mikoa mbalimbali ili kutoa fursa ya watu kupata ufahamu zaidi kuhusu uchaguzi sahihi wa kozi za kusoma pamoja na namna gani mtu anaweza kusoma nje,” alisema Abdulmalik Mollel katika mahojiano na mwandishi wa makala hii.

  Kwa mujibu Mollel, nje ya kuanzisha kampuni ambayo ina makao yake makuu Dar es Salaam, pia imefungua matawi katika mikoa ya Mbeya, Dodoma, Mwanza na Zanzibar. Lakini pia imeanzisha mkakati wa kufanya maonyesho mikoani.

  “Tumekuwa na maonyesho ya vyuo vikuu vya nje katika mikoa tofauti mfululizo, tulianza na Dodoma, Mbeya na kisha jana tulianza hapa Arusha, na tunatarajia maonyesho haya yatamaliza leo,” alisema Mollel na kuongeza kuwa mwitikio umekuwa mzuri kwa Watanzania wengi kufurika kwenye maonyesho.

  Maonyesho kama hayo pia yanatarajiwa kufanyika Zanzibar na Mwanza mapema mwakani, azma kubwa ikiwa ni kuwa ni kutumia maonyesho hayo kama jukwaa la kuelezana kuhusu mwongozo wa kusoma nje ya nchi, uchaguzi sahihi wa kozi za kusoma na kila kitu kinachohusu namna gani mtu anaweza kusoma nje.

  Baadhi ya Watanzania waliofurika kwenye maonyesho hayo wameelezea kufurahishwa kwao huku wakisema kama mpango kama huo ungekuwepo miaka mingi ya nyuma, huenda sasa Tanzania ingekuwa na maendeleo makubwa kiviwanda na uchumi kwa ujumla.

  “Mimi nimesoma nje, nafahamu kwa kina umuhimu wa kusoma nje ya nchi. Ukweli wenzetu wako juu sana katika teknolojia, wana vifaa vya kufundishia na wanafundisha zaidi kwa vitendo kuliko sisi, haya ni baadhi ya mambo yaliyosababisha wazazi wangu walinipeleka nje kusoma na sasa nimerudi nchini, ni kati ya maofisa katika taasisi fulani,” alisema Othman Mohammed akiwa katika viwanja vya Kumbukumbu ya Azimio la Arusha ambako maonyesho ya vyuo vya nje yanaendelea.  Kuhusu Maonyesho ya Arusha

  Maonyesho hayo makubwa ya vyuo vya nje yalianza jana tarehe 21 Disemba na yatamalizika jioni ya leo tarehe Disemba 22 katika uwanja wa Makumbusho ya Azimio la Arusha.

  Kwa mujibu wa Meneja wa Global Education Link (GEL) tawi la Arusha, Regina P. Lema uwanja huo ambao maonyesho yatafanyika unatazamana na Mnara wa Mwenge.

  “GEL ndio tunaoendesha maonyesho haya kwa kushirikiana na vyuo vya nje ambavyo baadhi yao tayari vimeshatuma wawakilisha wao. Maana yake ni kwamba watu watapata fursa ya kuzungumza na wafanyakazi wa GEL au hao wawakilishi waliotoka nje ili kupata ufahamu mpana zaidi kuhusiana na suala la kusoma nje,” alisema.

  Regina alifafanua kuwa baadhi ya vyuo ambavyo vimetuma wawakilishi watakaoshiriki maonyesho hayo ni Lovely Professional University, Sharda University, Chandigarh University na Maharishi Markandeshwar University vyote vya nchini India.

  “Nawakaribisha watu wa Arusha na vitongoji vyake kuja kujionea masuala ya namna ya kusoma nje ya nchi, pamoja na uchaguzi wa kozi za kusoma,” aliongeza Mkurugenzi Mkuu wa GEL, Abdulmalik Mollel na kufafanua kuwa lengo la maonyesho hayo ni kufahamishana kozi mbalimbali zinazotolewa nje ya nchi.

  “Kuna kozi za kila aina zikiwamo za injinia katika masuala mengi tofauti yakiwamo ya petroli na gesi. Pia kozi za biashara, masoko, afya, udaktari, madini, uchumi na nyingine nyingi,” aliongeza na kufafanua kuwa vyuo ambavyo mtu anaweza kupatiwa maelezo katika maonyesho hayo ni vya nchi nyingi tofauti duniani vikiwamo vya China, Malaysia, India, Canada, Marekani, Australia, Uingereza, Afrika Kusini na Ukraine.  Kulingana na Mollel katika maonyesho hayo wanaotaka kusoma nje wanaweza kujaza fomu hapohapo kwenye maonyesho kwa ajili ya kuanza masomo Mwaka 2017 ikiwamo mwezi Januari, Februari, Machi na kuendelea kulingana na matakwa ya mwombaji.

  “Wengi wamekuwa wakitaka kusoma nje, lakini baadhi wamekuwa wakishindwa kuwa na uchaguzi sahihi za nini cha kwenda kusoma, kwa hiyo kupitia maonyesho haya tutakuwa tunatoa ufafanuzi wa kozi mbalimbali,” alisema Mollel.

  Waliomaliza kidato cha nne, sita na vyuo mbalimbali ni baadhi ya wale ambao wanaweza kuunganishwa na GEL kusoma vyuo vya nje ya nchi.

  GEL ni kampuni iliyosajiliwa Mwaka 2006 kwa lengo la kufanya shughuli za uwakala wa vyuo vya nje. Hadi sasa imeweza kuwaunganisha Watanzania zaidi ya 5400 na vyuo mbalimbali Duniani vikiwamo vya Marekani, Canada, Uingereza, Ukraine, China na India.

  Serikali yathamini mchango wa Global Education Link, yaitunuku nishani ya uzalendo

  Mchango wa Global Education Link (GEL) umekuwa ukithaminiwa na wadau mbalimbali wa maendeleo pamoja na Serikali.

  Wiki iliyopita Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Stadi, Profesa Joyce Ndalichako ameitunuku nishani ya uzalendo kampuni ya Global Education Link (GEL) kutokana na mchango inaotoa katika maendeleo ya elimu nchini.

  Nishani hiyo aliitoa wakati akizindua mkutano mkuu wa 11 wa Umoja wa Wakuu wa Shule za Sekondari nchini (TAHOSSA) mkoani Dodoma.

  Rais wa TAHOSSA, Bonus Nyimbo alisema GEL imekuwa mdau mkubwa katika kusaidia shughuli za TAHOSSA na masuala mengine muhimu katika maendeleo kwa ujumla nchini.

  “Tunaipongeza sana Global Education Link, kwani wamekuwa karibu na jamii, wamekuwa karibu na sekta ya elimu na maendeleo ya nchi kwa ujumla,” alisema Katibu Mkuu wa TAHOSSA Diana Matemu.

  Global Education Link ni kampuni iliyoanzishwa Mwaka 2006 kwa lengo la kuwaunganisha watu na vyuo vya nje. Tangu imeanza hadi sasa imewaunganisha Watanzania 5400 na vyuo mbalimbali vilivyoko Marekani, Canada, India, Malaysia na China.

  0 0

  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

  JESHI la Polisi limesema linaendelea kufanya upelelezi kupotea kwa raia, Benard Focus 'Ben Saanane', (pichani) na kutaka wananchi kutoa taarifa zinazohusiana na huyo mtu kupotea.

  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Makao Makuu ya Jeshi la Polisi,Kaimu Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI), Kamishina wa Jeshi la Polisi, Robert Boaz, amesema jeshi la polisi lilipopata taarifa walianza kufanyia kazi kwa upelelezi kwa kupotea raia huyo.

  Amesema taarifa za kupotea zililipotiwa kituo cha polisi na mtu aliyejitambulishwa kuwa ni rafiki yake na baada ya kuokea taarifa hizo jalada la uchunguzi lilifunguliwa na taratibu zote za kiupelelezi zinazohuusu mtu aliyepotea zilifuatwa na bado upelelezi na suala hilo unaendelea.

  Boaz amesema wananchi wamekuwa pamoja wakitoa taarifa mbalimbali na kuahidi kwamba taarifa zote zitafanyiwa kazi na pindi wanavyopata wawasilishe katika vituo vya Polisi.

  Aidha amesema wakati upelelezi wa matukio hayo ukiendelea ,tunawaomba wananchi kuendelea kuwa watulivu , Jeshi la Polisi litaendelea kutoa taarifa kadri ya upelelezi utavyokuwa unaendelea.

  Wakati huo huo, Kamishina Boazi, amesema maiti saba iliyokutwa katika Mto Ruvu kati ya Desemba 9/12 miili sita ilizikwa kutokana na hali zake kuwa mbaya.

  Amesema mwili mmoja waliuchukua na kupeleka katika hospitali ya Bagamoyo kwa ajili ya utambuzi lakini haukuweza kutambuliwa na kuamua kuzika na upelelezi unaendelea.

  0 0  0 0  0 0

  NA K-VIS BLOG/Khalfan Said, Singida.

  WANAKIJIJI wa vijiji 126 wanaopitiwa na mradi mkubwa wa umeme, Backbone wa ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme wa msongo wa Kilovolti 400, kutoka mkoani Iringa hadi Shinyanga kupitia mikoa ya Singida na Dodoma, wataunganishiwa umeme kwa kulipia kiasi kidogo cha fedha shilingi elfu 27,000/-, tu, Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO, Bi. Leila Muhaji, (pichani juu) amesema.

  Bi Leila ameyasema hayo kwenye kijiji cha Igurubya, mkoani Shinyanga, wakati wa ziara ya wahariri wa vyombo vya habari kutembelea mradi huo, Desemba 22, 2016.

  “Nia ya Serikali, kupitia Shirika lake la Umeme nchini TANESCO, ni kuwapatia wananchi wote huduma ya umeme, ambayo ni muhimu katika kuinua uchumi wa mwananchi mmoja mmoja na taifa kwa ujumla, kwa kawaida gharama ya kuunganishiwa umeme kwa vijijini ni shilingi 177,000/- pamoja na kodi ya ongezeko la thamani VAT.” Alisema.

  Alisema, kwa kuzingatia hilo, kumekuwepo na juhudi mbalimbali za Shirika la Umeme, TANESCO, kufikisha huduma ya umeme vijijini chini ya mradi wa Wakala wa Usamabzaji Umeme Vijijini (REA), lakini kukamilika kwa mradi huu wa Backbone kutaongeza kasi ya kuwapatia wananchi huduma hii muhimu ya umeme na kwa bei nafuu.” Aliongeza.

   Alisema, Serikali kupitia TANESCO imepiga hatua kubwa ya kuwafikishia umeme wananchi ambapo tayari karibu asilimia 45 ya wananchi wa Tanzania wamepatiwa huduma ya umeme.

  Akizungumzia kukamilika kwa mradi huo wa Backbone uliojikita katika kujenga minara na njia za kusafirisha umeme pamona na upanuzi wa vituo vine vya kupoza na kusambaza umeme, Meneja wa Mradi huo anayesimamia usafirishaji umeme, Mhandisi Oscar Kanyama, alisema, mradi huo wa Backbone wa kusafirisha umeme wa msongo wa Kilovolti 400, na urefu wa Kilomita 670, kutoka mkoani Iringa hadi Shinyanga kupitia mikoa ya Singida na Dodoma, umekamilika rasmi Desemba 22, 2016 kwa kuwasha kipande kilichokuwa hakijakamilika cha kutoka Dodoma kwenda Singida.
  Mradi huo ulianza kutekelezwa mwishoni mwa mwezi Novemba mwaka 2013 na unafadhiliwa na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo umegharimu karibu shilingi Trilioni 1.

  Kazi iliyokuwa ikifanywa ni pamoja na ujenzi wa minara mikubwa yenye uwezo wa kubeba nyaya 6, tatu kila upande tofauti na ile ya awali iliyokuwa na uwezo wa kubeba nyaya 2 tu moja kila upande. “Lakini pia kazi nyingine iliyokuwa ikifanyika chini ya mradi huu, ni upanuzi wa vituo vinne vya kupoza na kusambaza umeme, vituo hivyo ni kile cha Iringa, Zuzu, mkoani Dodoma, Kibaoni mkoani Singida, na Ibadakuli mkoani Shinyanga Shinyanga.” Alifafanua.
   Meneja wa Mradi huo anayesimamia usafirishaji umeme, Mhandisi Oscar Kanyama, akizungumza kwenye kituo cha Kibaoni Singida
   Mkuu wa kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Kibaoni mkoani Singida, akitoa maelezo kwa wahariri.
   Mhariri wa Star TV, Jenifer Sumi
   Mhariri wa Clouds Media, Joyce Shebe, akinakili maelezo ya kiufundi kuhusiana na kituo cha umeme cha Kibaoni mkoani Singida.
   Picha ya pamoja ya wahariri na wafanyakazi wa TANESCO mkoani Singida
   Kituo cha Kibaoni mkoani Singida ambacho kilifanyiwa upanuzi chini ya mradi wa Backbone
   Mdhibiti mifumo ya umeme kituo cha Kibaoni Mkoani Singida, aimuonyesha kitu Mhariri Mtendaji wa Tanzania Daima, na Katibu Mkuu wa Jukwaa la Wahariri Tanzania, (TEF), Neville Meena
   Minara ya kubeba nyaya za kusafirisha umeme, upande wa kulia ni minara mipya na kushoto ni ile ya zamani

  0 0

   Wanafamilia   wakiwa   wamelizungika kaburi la marehemu Ngaga  aliyezikwa kaburi  moja na kondoo pamoja na  kuku mweusi  leo kwenye  kitongoji cha Mkawaganga kijiji  cha Mbigili  wilaya ya  Kilolo mkoani Iringa 
    Mganga  wa  kienyeji  Galasiano  Nyenza (kulia)  akiwa na mtoto wa marehemu  Andrea Ngaga  ,Kurugenzi Ngaga  kushoto  baada ya  kufanyika kwa mazishi ya kimila  katika  kijiji  cha Mbigili Kilolo kwa marehemu kuzikwa kaburi moja na kondoo na kuku  mweusi 
   Mganga  Nyenza aliyeongoza mazishi hayo katikati  akiwa na baadhi ya ndugu kando ya kaburi 
   Waombolezaji  wakitoka kuzika 
                                                        Marehemu  enzi  za uhai  wake 
  Nyumbani kwa marehemu   waombolezaji  wakiwa  kwenye  foleni 
  ....................................................................................................
                                Na MatukiodaimaBlog
  MAMIA  ya  wakazi  wa kijiji  cha  Mbigili na  mji  wa Ilula  katika  wilaya ya  Kilolo  wamefurika katika mazishi  ya aina  yake  yaliyofanyika katika kitongoji  cha Mkawaganga  kijiji  cha Mbigili  wilaya ya  kilolo mkoani Iringa  kushuhudia mazishi hayo ya  kihistoria baada ya mzee mmoja aliyefariki  dunia ghafla  kuzikwa kaburi  moja na kondoo pamoja na   kuku mweusi.

  Tukio   hilo  limetokea  leo  wakati  wa mazishi ya mzee Andrea Ngaga (90) mkazi wa kitongoji  cha Mkawaganga  aliyekuwa  akijishughulisha na kazi  za uganga  wa kienyeji kijijini  hapo enzi  za  uhai  wake .

  Baadhi ya  wananchi  waliofika katika mazishi  hayo  walisema  kuwa  walilazimika  kusitisha   shughuli  zao za  shamba na biashara na  kufika  kushuhudia  mazishi hayo ambayo ni mara ya kwanza  kufanyika katika  kijiji  hicho  alisema  John  Mfaligoha  kuwa  kabla ya  kifo marehemu  huyo  alipata  kuwaeleza  aina ya mazishi yake  yatakavyokuwa .

  Hivyo alisema  wananchi   waliowengi   walifika  kutaka  kushuhudia tukio  hilo la mazishi  na  ndio  sababu  iliyopelekea  wananchi kusukumana msibani  wakati wa mazishi  kwa  kila mmoja kutaka  kushuhudia  tukio  hilo la kihistoria katika kijiji   hicho.

  Mwenyekiti  wa  serikali ya  kijiji  cha Mbigili  Ibrahim  Rashid (46)  alisema  amezaliwa katika  kijiji  hicho  tukio hilo ni la kwanza  kufanyika hajapata  kushuhudia mazishi ya  aina  hiyo   zaidi ya  kusikia katika vyombo  vya habari  kutoka nje ya  kijiji  chake na  kuwa  mazishi hayo  yamefanyika kimila  zaidi na kimsingi  huwa marehemu anachagua mtu  wa  kuzikwa nae  kabla ya  kifo .

  Ila hakuweza  kuacha maagizo zaidi ya  kuomba pindi atakapokufa kuzikwa kimila na ndio  sababu  aliyeongoza  mazishi hayo ni mganga  wa kienyeji  kutoka Ifunda  wilaya ya  Iringa  Galasiano Mfaume Nyeza  ambae  ni baba mdogo  na marehemu  huyo .


  Mtendaji  wa serikali ya  kijij  hicho cha Mbigili Thabith  Kalolo  alisema  kuwa kimsingi  hakuna  kosa  lolote  familia ambalo  wamelifanya kwa  kufanya mazishi ya  aina  hiyo  kwani serikali haiingilii uhuru wa  wananchi  wake kuamini masuala ya  mila na kuwa   iwapo mazishi hayo yangekiuka haki  za  binadamu mwingine mfano  kama wangekata  kumzika  marehemu na  binadamu mwingine aliyehai hapa isingewezekana  ila  kwa kumzika na kondoo na kuku  mweusi hakuna  shida .

  Hata   hivyo  alisema tofauti  ya  rekodi ya misiba iliyopata  kutokea  katika  kijiji  hicho ,msiba wa mganga  huyo  umevunja rekodi kwa  kuhudhuriwa na idadi kubwa ya  watu  na kuwa   msiba uliovunja rekodi kwa michango ni huo pekee  kwani  misiba mingine fedha za rambi rambi   huwa ni kati ya Tsh 300000 hadi 500000 mwisho  ila msiba  huo rambi rambi ni  zaidi ya Tsh milioni 1.3

  Mtoto  wa marehemu  Kurugenzi Ngaga  alisema  kuwa babake  alifariki  dunia juzi  Desemba 20 majira ya  saa 6 usiku mwakla huu kuwa  alikuwa  akisumbuliwa na tatizo ya chembe  ya Moyo  na kuwa ameacha   wajane   wawili na watoto 19.

  Kurugenzi alisema  kimila kama  ingekuwa  zamani  marehemu  angezikwa na mjukuu wake  aliyemteua kushika mikoba yake  ila  kutokana na mambo  ya mila kwa  sasa kupewa kisogo waliona ni  vema wakamzika na kondoo na kuku  huyu  mweusi .

  0 0  Yesterday, DAC handed-over 10 refurbished children's bicycles to PASADA which formed part of the assistance the club provided the organisation from the proceeds of the World Aids Day 2016 Charity Ride that was held on Saturday, 3rd December 2016. In addition to the bike donation, DAC paid for the repair and maintenance of 15 of the centre's old bikes and has committed to provide maintenance of the bicycles for the next 3 months.

  PASADA is a social service agency striving to provide holistic care and support to those living with HIV. To find out more about the centre and it's activities, please go to www.pasada.or.tz.

  We thank each and everyone who joined us on the fundraising drive.

  0 0


  Hapa ni katika ukumbi wa mikutano hotel ya Empire mjini Shinyanga ambapo leo Jumatano Desemba 21,2016 waandishi wa habari mkoani Shinyanga wamepewa mafunzo kuhusu masuala ya watu wenye ualbino.

  Mafunzo hayo yameandaliwa na Chama cha watu wenye Ualbino nchini (TAS) kupitia programu ya Elimu kwa Jamii kuhusu mambo ya Ualbino 'Community Awareness Raising Program' inayofadhiliwa na shirika la Open Society Foundations.

  Aliyesimama ni katibu wa Chama cha Watu wenye Ualbino mkoa wa Shinyanga Lazaro Anael akizungumza katika semina hiyo ambapo alisema lengo la semina hiyo ni kuwajengea uwezo waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga ili waweze kuandika habari sahihi zaidi kuhusu masuala ya watu wenye ualbino.

  Katibu wa Chama cha Watu wenye Ualbino mkoa wa Shinyanga Lazaro Anael akizungumza.Kulia ni Afisa Mahusiano na Habari Chama Cha Watu Wenye Ualbino nchini Tanzania Josephat Torner
  Mgeni rasmi Mkuu wa polisi wilaya ya Shinyanga George Mdoe aliyemwakilisha kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga akifungua semina hiyo ambapo aliwasisitiza waandishi wa habari kuendelea kushirikiana na jeshi la polisi katika kutoa taarifa mbalimbali kuhusu masuala yanayohusu watu wenye ualbino.
  Hata hivyo aliitaka jamii kuacha uoga katika kutoa ushahidi katika kesi za watu wanaojihusisha na mauaji ya watu wenye ualbino
  Alisema hivi sasa serikali inahitaji watu wenye ualbino wajumuike katika jamii ndiyo maana baadhi yao wameondolewa katika kambi zao mfano Buhangija katika manispaa ya Shinyanga na kurudishwa katika jamii yao ili kuondoa tofauti yao na watu wengine katika jamii
  Afisa Mahusiano na Habari Chama Cha Watu Wenye Ualbino nchini Tanzania Josephat Torner akiteta jambo na mwezeshaji katika semina iliyolenga kuwajengea uelewa zaidi waandishi wa habari kuhusu masuala ya watu wenye ualbino, bwana Kadama Malunde,ambaye pia ni mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga

  Waandishi wa habari wakiwa ukumbini

  Waandishi wa habari wakiandika dondoo muhimu


  Semina inaendelea

  Afisa Mahusiano na Habari Chama Cha Watu Wenye Ualbino nchini Tanzania Josephat Torner, akizungumza ukumbini akielezea kuhusu changamoto zinazowakabilia watu wenye ualbino ambazo ni pamoja na kukumbwa na saratani ya ngozi hali ambayo inafanya maisha ya watu wenye ualbino kuwa mafupi
  Bi Nabaggala Edith ambaye ni Mkurugenzi wa shirika linalojihusisha na masuala ya watu wenye ualbino nchini Uganda (Albinism Support Association Uganda ASAU) akifuatilia kilichokuwa kinaendelea ukumbini Mwezeshaji katika semina hiyo Kadama Malunde akiwasilisha mada kuhusu mchango wa vyombo wa habari katika vita dhidi ya mauaji ya watu wenye ualbino nchini Tanzania. Malunde alisema vyombo vya habari vimekuwa na mchango mkubwa sana katika kuongeza ufahamu wa jamii juu ya masuala ya watu wenye ualbino kitaifa na kimataifa,kupunguza matukio ya ukataji viungo vya watu wenye ualbino na mauaji, kuelezea juhudi mbalimbali za TAS kwa kushirikiana na wadau mbalimbali.

  Malunde alisema ni kupitia vyombo vya habari hata wadau wamefika nchini na kuchangia kuboresha hali na maisha ya watu wenye ualbino na kufanikisha kuanzishwa kwa siku ya watu wenye ualbino duniani ambayo hufanyika kila mwaka tarehe 13 kila mwezi Juni
  Hata hivyo Malunde alisema bado kuna unyanyasaji wa kijinsia ambapo akina mama waliozaa watoto wenye ualbino wengi wao wamekimbiwa na waume zao,wameachika,wametelekezewa watoto na pia watoto wenye ualbino nao wametekelezwa na kwamba bado kuna mkazo hafifu katika sera na sheria kuhusu masuala ya mauaji ya albino.

  Afisa Mahusiano na Habari Chama Cha Watu Wenye Ualbino nchini Tanzania Josephat Torner akizungumza katika semina hiyo ambapo alisema ipo haja ya kuondoa majina yanayodhalilisha na badala yake itumike "Watu Wenye Ualbino" na siyo maneno mengine.
  Afisa programu kutoka Chama Cha Watu wenye ualbino Tanzania,Severin Edward akifuatilia kilichokuwa kinaendelea ukumbini
  Afisa Mahusiano na Habari Chama Cha Watu Wenye Ualbino nchini Tanzania Josephat Torner akisikiliza hoja kutoka kwa mwandishi wa habari gazeti la Jamboleo Stephen Kidoyayi

  Afisa Mahusiano na Habari Chama Cha Watu Wenye Ualbino nchini Tanzania Josephat Torner akielezea jambo

  Picha ya pamoja washiriki wa semina hiyo


  Picha ya pamoja
  Picha zote na Shinyanga Press Club


  0 0

  Its a nice beach view house 8 Bedrooms, Large space for dining, Nice modern Kitchen, Large Green Garden, fully Air Condition.

  The house is located Mbezi beach Shoppers.

  Contact 0713 882 800.

  0 0


   Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Christopher ole Sendeka akisalimiana na Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Mji Njombe Dkt Samwel Ndalio Thomas mara baada ya kuwasili Halmashauri hapo. Kulia kwake ni Mkuu wa Kitengo cha manunuzi na mweka hazina wa Halmashauri.
   Mhe. Ole sendeka akisalimiana na Karani wa Fedha “Cashier” wa Halmashauri Neema Kalundwa  
   Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Njombe Illuminatha Mwenda akisoma taarifa ya utekelezaji wa shughuli mbalimbali za Halmashauri zilizofanyika.
  Mhe. Ole sendeka akionesha nakala ya kitabu cha Ilani ya uchaguzi ambapo amewataka watumishi kuisoma na kila mmoja kuwajibika  kwenye eneo lake la utekelezaji  kutekeleza ilani ya uchaguzi ya chama Cha Mapinduzi.Kushoto kwake ni  Katibu Tawala Mkoa wa Njombe Jackson Saitabahu akifuatiwa na Mkuu wa Wilaya ya Njombe Mhe. Ruth Msafiri.


  Hyasinta Kissima –Njombe

  Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Christopher Ole Sendeka amekutana na kufanya mazungumzo na watumishi wa ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Mji Njombe ikiwa ni ziara yake ya kwanza ya kujitambulisha mara baada ya kuteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa huo.

  Akiwasilisha salamu za shukrani kwa mapokezi mazuri aliyopatiwa toka alipowasili Mkuu huyo wa Mkoa amesema kuwa, Mkoa wa Njombe ni miongoni mwa Mikoa ambayo alipendelea sana kufanya kazi kutokana na uwepo wa fursa nzuri za maendeleo, mandhari nzuri na hali nzuri ya hewa.

  ”Nimefurahi sana kuwa katika Mkoa huu kwani kwa kipindi chote nilitamani sana kufanya kazi katika MKoa wa Njombe na nilitamani sana kama nafasi hii niliyoipata ningeipata kipindi nilipokua kijana lakini bado nafuraha kubwa kwani ndoto yangu ya kuitumikia na kuifanya Njombe ya maendeleo imeanza kutimia kupitia uteuzi wa Mhe. Rais na ninawahakikishia kuwapatia ushirikiano wa kutosha katika yale yote mtakayoona yanahitaji uwepo wangu.”alisema Mhe.Ole Sendeka.

  Awali akiwasilisha taarifa fupi ya utekelezaji wa shughuli mbalimbali za Halmashauri mbele ya Mkuu wa Mkoa Mkurugenzi wa Halmashauri Illuminatha Mwenda amesema kuwa, Halmashauri imejitahidi kufanya shughuli mbalimbali za maendeleo ikiwa ni pamoja na ujenzi wa zahanati katika kila kijiji, ujenzi wa nyumba za waalimu katika shule mbalimbali za sekondari, utoaji wa mikopo ya vijana na wanawake ambapo katika robo ya kwanza jumla ya Tsh. milioni 52 zilitolewa kutoka mapato ya ndani huku shughuli za ukusanyaji mapato mpaka kufikia sasa halmashauri imefikia asilimia 40% ya ukusanyaji wa mapato kupitia mashine za ukusanyaji mapato(POS) 97 zilizopo katika maeneo yote ya ukusanyaji ushuru wa Halmashauri.

  Mara baada ya kuipokea taarifa hiyo Mkuu huyo wa Mkoa amesema kuwa kwa sasa Chama Kilichopo Madarakani ni Chama Cha Mapinduzi chini ya Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli, na hivyo watumishi wote hawana budi kuhakikisha kuwa wanaipitia Ilani ya Chama Cha Mapinduzi na kuhakikisha kuwa kila mtu anasoma katika eneo lake na atambue kwamba ni kwa namna gani anahusika katika utekelezaji wa ilani hiyo. Ameendelea kusema hatakuwa na huruma kwa watendaji watakaoshindwa kukiri mapungufu na kukubali kusahihishwa katika kutekeleza majukumu yao ipasavyo na yeye hatakuwa na matatizo na mtumishi ambaye atatekeleza majukumu yake ipasavyo na amewaonya wanasiasa wanaochochea migogoro na kukwamisha shughuli za maendeleo kwani yeye hatakua na mswalia mtume kwa chama cha aina yeyote ile.

  “Mkurugenzi Mhe. Rais amekuamini na amekuteua kuisimamia Halmashauri hii hakikisha kuwa unasimamia watendaji wako wote mpaka wale watendaji wa ngazi za chini Kabisa kama watendaji wa Vijiji, usiwaonee huruma kwani ukiwaonea huruma wale wa juu hawatakuonea huruma wewe na mimi pia sitakuonea huruma. Lengo letu ni kuhakikisha kuwa Halmashauri za Mkoa wetu zinakuwa za mfano kwa kuwa na watendaji wenye weledi na wachapakazi kama kauli ya Mhe. Rais inavyosema Hapa kazi tu.”ameendelea kusema

  “Naipongeza Halmashauri kupitia taarifa yako Mkurugenzi kwa kuhakikisha kuwa kwa vipindi vyote Halmashauri ya Mji Njombe haijawahi kupata mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu na msibweteke kwa kulewa sifa hizo bali hakikisheni Mji unaendelea kuwa msafi.

  Mhe. Sendeka ameiagiza Halmashauri kuhakikisha kuwa inatenga maeneo ya upandaji miti kwa kadri halmashauri itakavyoshirikiana na wakala wa barabara (TANROAD ) na idara ya misitu na mazingira ili kuhakikisha kuwa wanapata aina nzuri ya miti itakayopandwa pembezoni mwa barabara za watembea kwa miguu, maeneo ya taasisi na kila mwananchi ahamasishwe kupanda mti nje ya eneo lake la makazi.

  Awali kabla ya kukutana na watumishi wa Halmashauri ya Mji Njombe Mkuu huyo wa Mkoa alipata nafasi ya kutembelea mradi wa maji uliopo Kambarage na Ujenzi wa standi mpya ya Mabasi mradi unaofadhiliwa na Benki ya Dunia na amemtaka Mwandisi wa Ujenzi kumfikishia taarifa mapema hii leo ya sababu zilizopelekea mkandarasi wa mradi huo kuongezewa muda wa umaliziaji wa awamu ya pili ya ujenzi wa stand hiyo kinyume na mkataba.


  0 0

   Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akimkabidhi Hati ya Kumiliki Ardhi Bibi Ester Lukondo mkazi wa Bunda Mkoani Mara, ambaye ni miongoni mwa wakazi 154 waliopelekewa Hati hizo na Waziri wa Ardhi Wilayani Bunda badala ya wakazi hao kuzifuata Mkoani Mwanza.
       Wananchi wa Musoma mjini wakikwasilisha Kero zao za migogoro ya ardhi kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi ili aweze kuzipatia ufumbuzi.
     Wananchi wa Bunda wakikwasilisha Kero zao za migogoro ya ardhi kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi ili aweze kuzipatia ufumbuzi.
    Waziri Lukuvi akikagua nyumba za gharama nafuu zilizojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) eneo la Buhare wilayani Musoma lenye jumla ya nyumba 50 zinazokaribia kukamilika.
      Waziri Lukuvi akikagua nyumba za gharama nafuu zilizojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) eneo la Buhare wilayani Musoma lenye jumla ya nyumba 50 zinazokaribia kukamilika.
   Jengo la Biashara la Musoma Mjini lililojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) ambalo Waziri Lukuvi alifika kuangalia maendeleo yake.
   Jengo la Biashara la Musoma Mjini lililojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) ambalo Waziri Lukuvi alifika kuangalia maendeleo yake.
   Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akiwa ndani ya jengo hilo.
    Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akiwa ndani ya jengo hilo.


  Na. Hassan Mabuye (Kitengo cha Mawasiliano - Wizara ya Ardhi)
  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akimkabidhi Hati 154 za Kumiliki Ardhi kwa wakazi wa wilaya ya Bunda Mkoani Mara wakati alipofanya ziara ya siku mbili ya utatuzi wa Migogoro ya Ardhi mkoani humo. 

  Lukuvi alitoa hati hizo kwa wananchi wa Wilaya ya Bunda ili kuwarahisishia wakazi hao utaratibu wa kupata hati zao pale walipo badala ya kuzifuata Mkoani Mwanza katika ofisi za Kamishana Msaidizi wa Ardhi Kanda ya Ziwawa.

  Aidha, Katika ziara hiyo Waziri Lukuvi ametatua migogoro ya Ardhi ya wananchi wa Musoma mjini na wananchi wa Bunda walio na kero za migogoro ya ardhi na kuzipatia ufumbuzi pamoja na kupokea vielelezo vya kero za wananchi zaidi 300 walizoziwasilisha kwa Waziri ili azitolee maamuzi.

  Waziri Lukuvi alikagua nyumba za gharama nafuu zilizojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) eneo la Buhare wilayani Musoma lenye jumla ya nyumba 50 zinazokaribia kukamilika, ambapo alimtaka Meneja wa Mradi wa NHC mkoa wa Mara Frank Mambo kukamilisha mradi huo ndani ya miezi mitatu.

  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi anaendelea na Ziara zake za utatuzi wa Migogoro ya Ardhi nchini, ambayo imejikita zaidi katika kutatua migogoro ya ardhi ya Mikoa ya kanda ya Magharibi, Kaskazini na ile ya Kanda ya Ziwa hapa nchini.

  Aidha, Mhe. Lukuvi baada ya ziara hiyo anatarajiwa kuwasili mkoani Arusha ambapo pia atatua migogoro ya ardhi inayoukabili mkoa huo katika wilaya za Arumeru na Karatu.

  Hadi sasa Mhe. Lukuvi ndani ya mwezi huu wa Desesmba ameishatatua migogoro ya ardhi ya Mkoa wa Kigoma na wilaya zake za Kigoma mjini, Kasulu na Kibondo na katika Mkoa wa Shinyanga na wilaya zake za Kishapu na Shinyanga mjini na katika mkoa wa Geita amefanya ziara katika wilayani Chato

  0 0

  KATIKA hatua za kuhakikisha inayafikia maeneo mengi Afrika Mashariki, Shirika la Etihad la Umoja wa Falme za nchi za Kiarabu limeingia makubaliano na Shirika la ndege la hapa nchini Precision Air ambayo yamelenga kupanua huduma zaidi ndani na nje ya Tanzania.

  Makubaliano hayo yanatoa fursa kwa, Shirika la Ndege la ‘Precision Air’ ambalo linaongoza kwa utoaji huduma hapa nchini kuweza kutoa huduma za moja kwa moja katika nchi za Umoja wa Falme za Kiarabu na zaidi.

  Kupitia makubaliano hayo, Shirika la Ndege la Etihad litaweka alama yake ya kibali EY kwenye ndege za ‘Precision Air’ zinatoa huduma kati ya Dar es Salaam, Kilimanjaro, Mwanza, Mtwara, Nairobi, Zanzibar na Pemba, Vilevile kwenye ndege zinazotoa huduma kati ya Nairobi, Kilimanjaro na Zanzibar.

  Aidha, Precision Air pia itaweka alama yake ya PW kwenye Ndege za Etihad zinazotoa huduma zake za kila siku kati ya Dar es Salaam na Abu Dhabi ikiwa ni hatua ya kuhimarisha uhusiano kati ya Afrika Mashariki na Falme za Kiarabu.

  Kwa mujibu wa Ofisa Mkuu wa Mipango na Mikakati wa Shirika la ndege la Etihad, Kevin Knight, ‘Precision Air’ ni shirika lenye ubunifu wa hali ya juu ambalo limeweza kuibuka na tuzo mbalimbali katika utoaji wa huduma bora za anga. 

  Makubaliano yetu leo yanadhihirisha kuwa ndoto ya Shirika la Ndege la Etihad ya kuhimarisha huduma katika Ukanda wa Afrika Mashariki inazidi kukua.

  “Huu ni mfano mzuri zaidi katika kuifikia mipango mikakati yetu ya kufanya kazi na wadau ili kutimiza dhamira yetu na kutoa huduma bora za kibiashara na usafiri wenye raha kwa chaguo bora zaidi,” aliongeza Ofisa huyo.

  Naye Sauda Rajabu ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji na Ofisa Mkuu wa Precision Air Services PLC, alisema, “Hii ni hatua muhimu na mpya kwa Precision Air, na tunafurahi sana kufanya kazi na Shirika la Ndege la Etihad katika ushiriiano huu. Tunatazamia kuwakaribisha abiria wengi zaidi wa Shirika la ndege la Etihad kwenye ndege zetu na ni furaha yetu kuendelea kuzifikia fursa nyingi zaidi katika hatua ambayo itasaidia kuhimarisha uhusiano wetu kwa mipango ya muda mrefu.

  “Kwa kupitia ushirikiano huu, tunawasaidia wateja wetu wa safari za ndani kujipatia fursa zaidi ya kwenda Abudhabi, na kusafiri maeneo zaidi ya 100 duniani kupitia mtandao mpana wa Shirika la ndege la Etihad ambao ni Afrika Mashariki ya Kati, Afrika, Ulaya, Asia, Australia na Marekani,”
  Tangu jana abiria wameanza kukata tiketi za safari kutoka kwa mawakala au katika ofisi za mashirika haya kwa ajili ya safari za Januari 11, mwakani na kuendelea.

  Shirika la Ndege la Etihad kwa sasa linatoa huduma katika nchi kumi barani Afrika 10 Afrika ikiwemo Johannesburg, Nairobi, Entebbe, Dar es Salaam, Khartoum, Casablanca, Rabat, Lagos, Cairo na Mahé, Seychelles.

older | 1 | .... | 1077 | 1078 | (Page 1079) | 1080 | 1081 | .... | 1897 | newer