Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1075 | 1076 | (Page 1077) | 1078 | 1079 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Bi. Lilian Liundi (kulia) akifungua Warsha ya Wasanii Juu ya Masuala ya Ukombozi wa Mwanamke Kimapinduzi hasa kwa kuangalia vipaumbele vya TGNP katika sekta ya Afya, Maji, Elimu, Kilimo na Viwanda. Warsha hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam iliandaliwa na TGNP Mtandao. Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Bi. Lilian Liundi (kulia) akifungua Warsha ya Wasanii Juu ya Masuala ya Ukombozi wa Mwanamke Kimapinduzi hasa kwa kuangalia vipaumbele vya TGNP katika sekta ya Afya, Maji, Elimu, Kilimo na Viwanda. Warsha hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam iliandaliwa na TGNP MtandaoMkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Bi. Lilian Liundi (kulia) akifungua Warsha ya Wasanii Juu ya Masuala ya Ukombozi wa Mwanamke Kimapinduzi hasa kwa kuangalia vipaumbele vya TGNP katika sekta ya Afya, Maji, Elimu, Kilimo na Viwanda. Warsha hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam iliandaliwa na TGNP Mtandao. Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Bi. Lilian Liundi (kulia) akifungua Warsha ya Wasanii Juu ya Masuala ya Ukombozi wa Mwanamke Kimapinduzi hasa kwa kuangalia vipaumbele vya TGNP katika sekta ya Afya, Maji, Elimu, Kilimo na Viwanda. Warsha hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam iliandaliwa na TGNP MtandaoMajadiliano katika warsha hiyo yakiendelea. Majadiliano katika warsha hiyo yakiendelea.Baadhi ya maofisa wa TGNP Mtandao wakiwa katika warsha hiyo. Baadhi ya maofisa wa TGNP Mtandao wakiwa katika warsha hiyo.Baadhi ya washiriki wa washa ya Wasanii Juu ya Masuala ya Ukombozi wa Mwanamke Kimapinduzi hasa kwa kuangalia vipaumbele vya TGNP katika sekta ya Afya, Maji, Elimu, Kilimo na Viwanda. Warsha hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam iliandaliwa na TGNP Mtandao. Baadhi ya washiriki wa washa ya Wasanii Juu ya Masuala ya Ukombozi wa Mwanamke Kimapinduzi hasa kwa kuangalia vipaumbele vya TGNP katika sekta ya Afya, Maji, Elimu, Kilimo na Viwanda. Warsha hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam iliandaliwa na TGNP Mtandao.Baadhi ya washiriki wa washa ya Wasanii Juu ya Masuala ya Ukombozi wa Mwanamke Kimapinduzi hasa kwa kuangalia vipaumbele vya TGNP katika sekta ya Afya, Maji, Elimu, Kilimo na Viwanda. Warsha hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam iliandaliwa na TGNP Mtandao. Baadhi ya washiriki wa washa ya Wasanii Juu ya Masuala ya Ukombozi wa Mwanamke Kimapinduzi hasa kwa kuangalia vipaumbele vya TGNP katika sekta ya Afya, Maji, Elimu, Kilimo na Viwanda. Warsha hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam iliandaliwa na TGNP Mtandao

  0 0

   Waziri wa  Katiba na Sheria Dkt.Harrison Mwakyembe akizungumza na waandishi wa habari juu ya amempongeza Makonda kwa  kutafuta vijana wanasheria na kuwapeleka katika kila Wilaya ya Dar es salaam ilikuweza kuwaidia  wananchi wanyonge katika masuala ya kisheria, leo jijini  Dar es Salaam. Kukia ni Mkuu wa Mkoa Wa Dar es salaam Paul Makonda. Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.
   Mkuu wa Mkoa Wa Dar es salaam Paul Makonda akizungumza na waandishi wa habari juu ya ujenzi  wa Mahakama utapunguza mzigo mkubwa kwa Serikali na itasaidi wakazi Nje ya Dar es salaam na Ndani katika  kupata Haki Zao za kisheria kwa haraka leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Waziri wa  Katiba na Sheria Dkt.Harrison Mwakyembe
   Waziri wa  Katiba na Sheria Dkt.Harrison Mwakyembe akisanikitambu cha wageni katika ofisi ya mkuu wa mkoa leo jijini Dar es Salaam.
   Waziri wa Katiba na Sheria, Dk. Harrison Mwakyembe akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda Katibu Mkuu wa Sheria na Katiba,  Profesa Sifuni Mchome,  Naibu Katibu Mkuu wa Sheria na Katika, Amon Mpanju
   MKUU wa Mkoa Wa Dar es salaam Paul Makonda ameahidi kuanza Ujenzi wa Mahakama 20 za Mwanzo katika Mkoa wa Dar es salaam ili kupunguza msongamano wa mahabusu katika vituo vya polisi na Magereza.

  Hayo ameyasema leo Makonda wakati alipotembelewa na Waziri wa Katiba na Sheria, Harrison Mwakyembe,  ofisini kwake, amesema ujenzi huo wa Mahakama utapunguza mzigo kwa Serikali na itasaidia wakazi  walio nje kidogo jiji la Dar es salaam kuweza kupata haki kwa wakati.

  Makonda alitoa wito kwa badhi ya Wadau mbalimbali kujitokeza ili kusaidia ujenzi wa Mahakama hizo, Amesema mtu yeyote atakaye kwenda kinyume na sheria hatakama alisaidia kujenga Mahakama,  sheria itafata mkondo wake.

  Nae Waziri wa Katiba na Sheria Dkt.Harrison Mwakyembe amempongeza Makonda kwa  kutafuta vijana wanasheria na kuwapeleka katika kila Wilaya katika  jiji la Dar es salaam ilikuweza kuwaidia  wananchi  kuwanyonge kupata haki katika masuala ya kisheria.

  " Sisi kama Wizara tunampongeza Mkuu wa Mkoa  kwa kuwatafuta vijana mbambali wanasheria na kuwapeleka katika kila Wilaya ilikuweza kuwasaidia wananchi hawa kupata msaada wa kisheria ilikupunguza uonevu kwa baadhi ya watu".amesema Mwakyembe.

  Amesema katika ujenzi huo wa Mahakama za mwanzo kutawasaidia wakazi mbalimbali wa jiji la  Dar es salaam kuwa na uhakika wa kupata haki kwa wakati mwafaka na kupunguza baadhi ya migogoro katika jamii na serikali..

  0 0

  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amewatahadharisha watanzania kuepuka vitendo vya uharibifu wa miundombinu ya barabara husasan katika kipindi hiki cha sikukuu za mwisho wa mwaka.

  Ameyasema hayo wakati akikagua mradi wa ujenzi wa barabara ya Dodoma-Babati yenye urefu wa KM 188.1, sehemu ya Mela-bonga ambapo imeripotiwa kuwepo vitendo vya uharibifu wa miundombinu kwa muda mrefu.

  'Napenda kutoa wito kwa watanzania kusherehekea sikukuu za mwisho wa mwaka kwa kuacha vitendo vya kuchoma matairi barabarani, kwani hali hii hupelekea kuharibu barabara kwa kiasi kikubwa ambazo Serikali imekuwa ikitumia fedha nyingi kuzijenga", amesema Prof.Mbarawa.

  Aidha, amekemea vitendo vya baadhi ya madereva kumwaga mafuta barabarani na baadhi ya wananchi kupitisha mifugo kwenye barabara ambapo vyote kwa pamoja vinaharibu miundombinu ya barabara.
  Amewataka wananchi kutoa ushirikiano kwa Serikali ikiwemo kuwaripoti wale wote wanaohujumu miundombinu ya barabara nchini.

  Sambamba na hilo, amewaasa madereva wa vyombo vya moto kuwa makini barabarani kwa kuzingatia sheria za alama za barabara ikiwemo kuendesha vyombo hivyo kwa mwendo unaotakiwa ili kudhibiti ajali za barabarani zinazoweza kuepukika.

  Kuhusu mradi wa ujenzi wa barabara ya Dodoma- Babati yenye urefu wa KM 188.1, Waziri Prof. Mbarawa amesema kuwa barabara hiyo inatarajiwa kukamilika mwakani kwani kwa sasa ipo katika hatua za mwisho za ujenzi wake.

  "Kazi inaenda kwa kasi kubwa, matumaini yangu ni kwamba ifikapo mwishoni mwa mwaka 2017, barabara hii itakamilika kwa viwango bora tulivyokubaliana kwenye mkataba", amesisitiza Profesa Mbarawa.
  Amefafanua kuwa kukamilika kwa barabara hiyo kutapunguza umbali wa masaa kwa abiria wanaosafiri kupitia njia ya Singida wanaotoka Dodoma na mikoa ya jirani kuelekea Manyara, Moshi na Arusha.

  Ameongeza kuwa barabara hiyo itasaidia kuiunganisha Tanzania na Nchi za kutoka Kusini na Kaskazini mwa bara la Afrika, hivyo kufungua fursa za kibiashara kwa wananchi na kuongeza pato la Taifa kupitia sekta ya utalii.
  Kwa upande wake, Meneja wa Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS) mkoa wa Dodoma, Eng. Leonard Chimagu, amemhakikishia Waziri Prof. Mbarawa kusimamia ujenzi wa barabara hiyo kwa viwago vinavyostahili na kuahidi kukamilika kwa wakati.

  Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
   Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akitoa maelekezo kwa Mhandisi Mshauri wa Kampuni ya H.P Gauff, Eng. Kini C. Kuyonza (wa tatu kulia), inayosimamia mradi wa ujenzi wa barabara ya Mela-Bonga yenye urefu wa KM 88.8. wakati alipokagua barabara hiyo, wilayani Babati.
   Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akiongea na mmoja wa madereva wa Basi linalofanya safari zake katika mikoa ya Dodoma-Babati, wakati alipokagua ujenzi wa barabara ya Mela-Bonga yenye urefu wa KM 88.8.
   Ujenzi wa barabara ya Mela-Bonga yenye urefu wa KM 88.8 inayojengwa kwa kiwango cha lami ukiendelea. Mradi huo unajengwa na Mkandarasi wa Kampuni ya M/s China Railway Seventh Group na unatajiwa kukamilika mwezi Agosti mwakani.
   Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akishindilia nondo kwenye moja ya ujenzi wa barabara ya Mela-Bonga yenye urefu wa KM 88.8, inayojengwa kwa kiwango cha lami, alipokuwa akikagua mradi huo.
   Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akikaza nondo katika ujenzi wa barabara ya Mela-Bonga yenye urefu wa KM 88.8, alipokuwa akikagua barabara hiyo.
   Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akishiriki kucheza ngoma za asili ya Kirangi katika kijiji cha Bicha, wilaya ya Kondoa mara baada ya kuongea na wakazi hao katika ziara yake ya ukaguzi wa mradi wa barabara ya Dodoma-Babati.
   Muonekano wa Daraja la Kelema ambalo ni moja ya madaraja makubwa 4 yanayojengwa katika barabara ya Mayamaya-Mela KM 99.35. Daraja hilo lenye urefu wa mita 205, lina uwezo wa kubeba tani 100.
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akikagua tabaka la lami katika barabara ya Mayamaya-Meya KM 99.35, alipokagua barabara hiyo.

  0 0  Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara Rodrick Mpogolo akikabidhiwa madawati 200 na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Morogoro, Karogeris. Madawati hayo yametolewa na CCM mkoa huo kwa ajili ya kuiunga mkono serikali katika suala la upatikanaji madawati
  Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara Rodrick Mpogolo akimpongeza Mkuu wa mkoa wa Morogoro Dk. Steven Kebwe wakiwa wamekalia madawati hayo bada ya makabidhiano.
  Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara Rodrick akizungumza na wanachama wa CCM na wananchi kwa jumla nye ya Ofisi ya CCM mkoa wa Morogoro leo
  Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Rodrick Mpogolo akiwasili ukumbini kufungua semina ya Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM mkoa wa Morogoro leo. Kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Morogoro Dk Steven Kebwe na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Morogoro, Steve Karogeris na Watatu kulia ni Kaimu Katibu wa CCM mkoa wa Morogoro Kulwa Milonge
  Mwandishi wa Magazeti ya Uhuru, Mzalendo na Burudani Latifa Ganzel akisalimia kwa niaba ya waandishi waliohudhuria kuandika habari za semina hiyo leo
  Kaimu Katibu wa CCM mkoa wa Morogoro Kulwa Milonge akizungumza kabla ya Naibu Katibu Mkuu kufungua semina hiyo.  Washiriki wakiwa kwenye semina hiyo


  Washiriki kwenye semina hiyo

  Washiriki kwenye semina hiyo


  Karogeris akimkaribisha Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara kufungua semina hiyo
  Washiriki wakiwa kwenye semina hiyo
  Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rodrick Mpogolo akifungua semina ya wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCm mkoa wa Morogoro, mjini Morogoro leo. Picha zote na Bashir Nkoromo.

  Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rodrick Mpogolo akimsalimia Mkuu wa mkoa wa Morogoro Dk Steven Kebwe alipowasili kwenye Ofisi ya CCM ya mkoa huo, akiwa katika ziara ya kikazi leo. Katika ziara hiyo alimkabidhi mkuu huyo wa mkoa madawati 200 yaliyotolewa na CCM mkoa huo na baadaye alifungua semina ya Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM mkoa wa Morogoro. Katikati ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Morogo Innocent Kalogeris
  Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rodrick Mpogolo akimsalimia Mkuu wa wilaya ya Morogoro Regina Chonjo alipowasili kwenye Ofisi ya CCM ya mkoa huo, akiwa katika ziara ya kikazi leo.
  Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rodrick Mpogolo akimsalimia Katibu Mwenezi wa mkoa wa Dorothy Mwamsiku alipowasili kwenye Ofisi ya CCM ya mkoa huo, akiwa katika ziara ya kikazi leo.
  Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rodrick Mpogolo akielekea kwenye Ofisi ya CCM mkoa wa Morogoro baada ya mapokezi
  Vijana wa Umoja wa Vijana wa CCM wakiwa kikakamavu wakati wakimpokea Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rodrick Mpogolo, alipowasili Ofisi ya CCm mkoa wa Morogoro akiwa katika ziara ya kikazi leo.
  Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rodrick Mpogolo akivishwa skavu na Kijana wa Umoja wa Vijana wa CCM, baada ya kuwasili Ofisi ya CCM mkoa wa Morogoro leo. Kushoto ni Kaimu Katibu wa CCM wa mkoa huo, Kulwa Milonge.
  Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara akimsalimia Chifu Kingalu Mwanabanzi wa 15, alipowasili Ofisi ya CCM mkoa wa Morogoro akiwa katika ziara ya kikazi leo.
  Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara Rodrick Mpogolo akimsalimia Mweka Hazina wa mkoa wa Morogoro, alipowasili Ofisi ya CCM mkoa huo leo
  Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara Rodrick Mpogolo akimsalimia Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Morogoro Mecky Mdaki alipowasili Ofisi ya CCM ya mkoa huo leo
  Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rodrick Mpogolo alimsalimia Mkuu wa mkoa waMorogoro mstaafu, Steven Mashishanga, alipowasili ofis ya CCM ya mkoa huo leo
  Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rodrick Mpogolo akisalimia Wazee maarufu, alipowasili Ofisi ya CCM ya mkoa wa Morogoro leo
  Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara Rodrick Mpogolo akiwa katika Ofisi ya Katibu wa CCM mkoa wa Morogoro, wakati akisubiri ratiba ya shughuli zake ianze, alipowasili Ofisi ya CCM ya mkoa huo leo. Aliyesimama ni Kaimu Katibu wa CCM mkoa wa Morogoro, Kulwa Milonge.
  Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rodrick Mpogolo akisalimiana na Ofisa Mwandamizi wa Makao Makuu ya CCM, Steven Kazidi walipokuwa katika Ofisi ya Katibu wa CCM mkoa wa Morogoro, leo. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO
  Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara akiingia ukumbini kuzungumza na viongozi wa ngazi ya mkoa, alipowasili Ofisi ya CCM ya mkoa wa Morogoro leo


  Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rodrick Mpogolo, akisaini Kitabu cha wageni kabla ya kuzungumza na viongozi hao leo. Kulia ni Kulwa Milonge
  Katibu wa UWT mkoa wa Morogoro Mecky Mdaki akijitambulisha ukumbini
  Kaimu Katibu wa CCM mkoa wa Morogoro Kulwa Milonge akizungumza wakati wa kikao cha Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara Rodrck Mpogolo (wapili kulia) na viongozi wa CCM ngazi ya mkoa leo
  Kulwa Milonge akisoma taarifa ya mkoa
  Milonge akipongezwa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara baada ya kusoma taarifa ya mkoa
  Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Morogoro, Karogeris akimkaribisha Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara Rodrick Mpogolo kuzungumza na viongozi hao
  Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rodrick Mpogolo akizungumza na viongozi wa ngazi ya mkoa alipokuwa katika ziara ya kikazimkoani humo leo

  Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Rodrick Mpogolo akiwasili kuzungumzana wananchi na wanachama wa CCM, nje ya Ofisi ya CCM mkoa wa Morogoro leo. Kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Dk. Steven Kebwe na Mwenyekiti wa CCM mkoa huo Karogeris
  Wana-CCM wakimshangilia Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara alipowasili kuzungumza nao nje ya Ofisi ya CCM mkoa wa Morogoro leo
  Viongozi wakiwa tayarikwenye meza kuu
  Mkuu wa mkoa wa Morogoro Dk. Steven Kwebwe akimtuza kiongozi wa kwaya ya CCM baada ya kukunwa na wimbo uliokuwa ukiimbwa na kwaya hiyo mbele ya Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara kabla ya kuzungumza na wanachama wa CCM na wananchi nje ya Ofisi ya CCM mkoa wa Morogoro
  Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rodrick Mpogolo akishangilia baada ya kumtuza kiongozi wa kikundicha kwaya ya CCM, ambaye naye pia alimkuna kwa wimbo uliokuwa ukiimbwa na wanakwaya hao
  Baadhi ya viongozi wa CCM mkoa wa Morogoro wakiwa kwenye mkutano huo

  Kada wa CCM, Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu ya Tanzania, ambaye pia amewahi kuwa Naibu Waziri Edward Mweisumo, akisalimia wakati wa mkutano huo.
  Baadhi ya wanachama na viongozi wa CCM wakiwa kwenye mkutano huo
  Chifu Kingalu Mwanabanzi wa 15 akimuombea dua ya kimila Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rodrick Mpogolo baada ya kumvalisha kofia, shuka na fimbo, kabla ya kuzungumza na wanachama wa CCM na wananchi kwa jumla nje ya Ofisi ya CCM mkoa wa Morogoro leo.
  Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Rodrick Mpogolo akinyoosha juu fimbo baada ya kukabidhiwa na Chifu Kingalu

  0 0

  Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) (kushoto) akipeana mkono na aliyekuwa Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Tonia Kandiero (kulia), baada ya kuagwa rasmi, katika Makao Makuu ya Wizara hiyo jijini Dar es salaam.
  Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) (kushoto) akimkabidhi zawadi ya shukrani aliyekuwa Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Tonia Kandiero (kulia) wakati akiagwa rasmi baada ya kupewa majukumu mengine ya Ukurugenzi Mkuu wa Benki ya AfDB kusini mwa Afrika, Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es salaam. 
  Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) akizungumza na baadhi ya viongozi wa Serikali wakati wa kumuaga aliyekuwa Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Tonia Kandiero, ambapo alimshukuru kwa jitihada zake katika kusaidia upatokanaji wa mikopo kwa ajili ya kutekeleza miradi ya Barabara, nishati, kilimo na elimu, Makao Makuu ya Wizara, Jijini Dar es salaam.
  Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) (kushoto) na aliyekuwa Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Tonia Kandiero wakifurahia uhusiano mzuri uliopo kati ya Benki ya AfDB na Tanzania ambapo mpaka sasa miradi inayofadhiliwa na Benki hiyo inafikia thamani ya Dola za Marekani Bilioni 2, wakati wa kuagwa kwa Dkt. Kandiero, Makao Makuu ya Wizara, Jijini Dar es salaam.


  0 0

  NA EVELYN MKOKOI – DAR ES SALAAM

  Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mzingira Mhe. Luhaga Mpina amefanya ziara ya kushtukiza katika bandari ya Dar es salaam ili kujionea utaratibu wa Bandari hiyo wa kuondosha taka zitokanazo na shughuli zake.

  Ziara ya Naibu Waziri Mpina imetokana na Malalamiko ya wananchi yaliyodai kuwa uchafuzi mwingi umekuwa ukifanyika katika Bahari na sehemu kubwa ya fukwe ya bandari imekuwa ikijaa taka za aina mbali mbali.

  Kutokana na malalamiko hayo ya wakazi wa jiji la Dar es Saalam, Naibu Waziri kabla ya kukagua maeneo ya kutoa na kukusanya taka za aina mbali mbali katika bandari hiyo zikiwemo taka za mafuta ghafi, alipokea taarifa kutoka kwa uongozi wa Bandari ambapo ameshangazwa na kile kilicholezwa na Afisa Mazingira wa bandari Bwana Thobias Sonda kuwa Bandani hiyo kubwa katika kanda ya Afrika Mashariki haina sehemu ya kupokea taka yaani waste reception facility na haina takwimu za taka zinazoingia na kutoka Bandarini Hapo.

  Akishindwa kujibu Baadhi ya Maswali yaliyoulizwa na Naibu Waziri Mpina Afisa mazingira huyo alieleza kuwa, Bandari hiyo inazalisha aina mbili kubwa za taka ikiwa ni taka za aina mbali mbali na taka za maji taka, alisema kuwa taka hizo zinaondoshwa na wakala ambao wanasajiliwa na Sumatra lakini haikueleweka wazi kuwa, taka hizo zinatupwa wapi na aliongeza kwa kusema kuwa, taka nyingi na hali ya uchafu inayoonekana pembezoni mwa Bandari ya Dar es Salaam inatokana na shughuli za kibinadamu kiwandani hapo, na kusema kuwa, kuna utaratibu wa kufanya usafi na kuziondosha na kukanusha kuwepo kwa taarifa za boat na meli zinazofanya safari za kuanzia bandarini hapo kuchafua mazingira ya bandari na Bahari.

  Afisa Mazingira huyo, liongeza kwa kusema kuwa taka za maji taka pamoja na kukosekana kwa takwimu za uondoshwani na umwagaji, zimekuwa zikikuswanywa a magari yao maalumu na kumwagwa katika mabwawa yao yaliyopo Kurasini jijini Dar es Salaam.

  Kwa kushangwazwa na hali hiyo, Mpina kupitia Baraza la taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC ameutaka uongozi wa Bandari hiyo kujenga mfumo mzuri wa kuhifadhi taka kwa muda wa miezi sita na kuripoti kwa Baraza za Mazingira kwa miezi mitatu Mfulizo kuonyesha namna ambavyo uondoshaji wa taka hizo unafanyika, Pamoja na kuwasilisha ripoti kwa Baraza ya Namna ambavyo mawakala hao walipatikana.

  Aidha Naibu waziri Mpina ameliagiza baraza kumpelekea ripoti ndani ya siku saba, inayoonyesha kama hao mawakala wa kukusanya taka bandarini wapo kisheria.

  Kwa Upande wake Kaimu Meneja wa Mamlaka ya Bandari Nchini Bw. Nelson Mlele amesema kuwa amepokea maagizo ya Mhe kupitia NEMC kwani yanawakumbusha utekelezaji wa majukumu yao na kwa upande wa Bandari ni changamoto itakayofanyiwa kazi haraka.;
   Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. Luhaga Mpina akizungumza na Viongozi wa Bandari ya Dar es salaam mara baada ya kuwasili Bandarini hapo kwaajiri ya kufanya ziara.

  0 0

  Waziri wa Habari,Utamaduni, Wasanii na Michezo Nape Nnauye akizungumza na mmoja wa viongzoi wa Chama Cha Kuogelea nchini (TSA), Imani Dominic kabla ya kuwazawadia waogeleaji wa Dar Swim Club, Marin de Villard, Emmanuel Moroni, Maia Tumiotto na Chichi Zengeni baada ya kushinda katika mashindano ya vijana ya Dar Junior.
  Muogeleaji chipukizi akishindana katika mashindano ya vijana


  Waogeleaji wakipozi baada ya kushinda medali katika mashindano ya vijana
  Waogeleaji chipukizi wakishindana katika mashindano ya vijana
  Mkurugenzi wa ufundi wa Chama Chama Cha Kuogelea Tanzania (TSA), Amina Mfaume akiteta jambo na makocha wa klabu ya Dar Swim Club, Michael Livingstone, (wa kwanza kushoto), Ferick Kalengela na Kanisi Mabena (kulia) wakati wa mashindano ya vijana yaliyomalizika hivi karibuni.

  ………………

  Na Mwandishi wetu

  Klabu ya kuogelea ya Dar Swim Club (DSC) imeibua katika nafasi ya kwanza kwa upande wa waogeleaji mmoja mmoja ya umri chini ya miaka 13 yaliyomalizika hivi karibuni.

  Klabu hiyo imeshinda imeibuka ya kwanza katika vipengele saba vya umri kati ya 16 za mashindano hayo na kuendelea kutamba nchini katika mchezo huo.

  Katika mashindano hayo yaliyoshirikisha timu saba, waogeleaji wa timu hiyo, Ellie Mramba alikuwa wa kwanza kwa upande wa miaka chini ya sita (U-6 wasichana) kwa kupata pointi 75 huku Sebastian Carpintero alikuwa wa kwanza kwa wavulana wa miaka 7 kwa kupata pointi 112.

  Riona Muriithi naye alikuwa wa kwanza kwa upande wa wasichana wa miaka 8 kwa kupata pointi 150, huku Maia Tumiotto akiongoza kwa waogeleaji wenye umri wa miaka 11 wasichana kwa kupata pointi 200 katika mashindano hayo yaliyodhaminiwa na Spice 4G Communication Unlimited, benki ya CRDB, Dow Elef International, Davis & Shirtliff, Sea Cliff Hotel, DSTV, American Garde na Sports Arena.

  Wadhamini wengine ni Maurel & Orom Tanzania, Warere, Best Western, Makini Studios, Food Lovers Market, UTT AMIS, Renault, CMC Formula, Print Galore, Branoz Collection, Codesh, Coca Cola, Pesi, Emmanuel Edward, The Slip Way Bookshop, Moments by Design, Olive, The Cooking Club, Nzito Shop, Ngozi,Moyo, Coletta na Mothi Mahal.

  Marin DE Villard wa klabu hiyo pia alishika nafasi ya kwanza kwa watoto wenye umri wa miaka 11 wavulana na Celina Itatiro huku akiwa wa kwanza upande wa wasichana wenye umri wa miaka 13 kwa kupata pointi 200 na Joshua Bruns alishinda kwa wavulana wa miaka hiyo kwa kupata pointi 185.

  Klabu ya Taliss imeshika nafasi ya pili baada ya kushinda vipengele vinne kupitia Natalia Ladha aliyeshinda kwa wasichana wenye umri wa miaka 9, Daniella Lamont aliyeshinda kupitia wasichana wenye umri wa miaka 10, Amani Doggart (wasichana miaka 12) na Oliver Mclntosh aliyeshinda kwa wasichana wenye umri wa miaka 12.

  Nafasi ya tatu ilichukuliwa na klabu inayokuja juu katika mchezo huo hapa nchini, Bluefins kwa kushinda vipengele vitatu. Waogeleaji walioipaisha klabu hiyo ni Aminaz Kachra aliyeshinda kwa wasichana wenye umri wa miaka 7 kwa kupata pointi 140, Ralph Sereki (wavulana miaka 8, pointi 165) na Aravid Raghavendran aliyejikusanyia pointi 176 kwa wavulana wa miaka 10.

  Klabu ya Wahoo ya Zanzibar alishika nafasi ya nne kupitia kwa Ellis Anderson aliyepata pointi 165 kwa waogeleaji wa miaka 9 wavulana huku klabu ya Champions Rise ikishika nafasi ya tano kwa kushinda kipengele kimoja cha wavulana chini ya miaka 6 kupitia William Sereki aliyepata pointi 75.

  Mwanza Swim Club na Kennedy House hazikuweza kushinda vipengele vyovyote vya jumla kwa waogeaji mmoja mmoja.

  Katibu Mkuu wa klabu hiyo, Inviolata Itatiro alisema kuwa siri ya mafanikio yao imetokana na moyo wa kujituma na ushirikiano baina ya wazazi, makocha na uongozi wa klabu.

  “Ni faraja kwetu, kwa sasa tunafurahia matunda ya mafanikio, tumepitia misuko suko kibao, kama si moyo wa uvumilivu, leo tusingekuwa hapa, wachezaji wetu wengi walihama, tuaanza upya na kufikia matunda haya,” alisema Inviolata.

  0 0

  Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (katikati), hii leo akizungumza na wanahabari baada ya kikao baina yake na viongozi wa Tanesco pamoja na wawakilishi wa kampuni zilizohusika na utengenezaji na ufungaji wa mitambo katika kituo cha kuzalisha umeme kwa kutumia mafuta mazito cha Nyakato Jijini Mwanza.

  Kushoto ni balozi wa Norway nchini Tanzania, Hanne-Marie Kaarstad na kulia ni balozi wa Denimark hapa nchini, Einar Jensen. Mabalozi hao wamehudhuria kikao hicho ikiwa ni sehemu ya kusaidia kutatua mvutano baina ya kampuni zinazotoka katika nchi zao na Tanesco kutokana na baadhi ya mitambo iliyofungwa na kampuni hizo katika kituo cha Tanesco Nyakato Jijini Mwanza kuharibika. Mradi huo uligharibu shilingi bilioni 129 hadi kukamilika kwake na una uwezo wa kuzalisha Megawati 60 za umeme.
  #BMGHabari
  Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (katikati), balozi wa Norway nchini Tanzania, Hanne-Marie Kaarstad (kushoto) pamoja na kulia ni balozi wa Denimark hapa nchini, Einar Jensen (kulia)
  Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo, ameliagiza Shirika la Umeme nchini Tanesco kufanya matengenezo kwenye mitambo yake minne ya kuzalisha umeme iliyoharibika katika Kituo cha Nyakato Jijini Mwanza kabla ya kufikia Februari 28 mwakani.

  Profesa Muhongo ametoa agizo hilo hii leo Jijini Mwanza, baada ya kukutana na viongozi wa Tanesco pamoja na wawakilishi wa kampuni zilizohusika na utengenezaji na ufungaji wa mitambo hiyo kutoka nchi za Norway na Denmark ambapo pia mabalozi wa nchi hizo wamehudhuria kikao hicho.

  Aidha Profesa Muhongo ameiagiza Tanesco kuhakikisha mitambo sita iliyosalia haiharibiki tena na kwamba inamaliza kazi ya kusafisha mitambo yote katika kituo hicho kabla ya kufikia mwezi Februari 28 mwakani ambapo imeelezwa kwamba baadhi ya mapungufu katika mitambo hiyo yalitokana na kutosafishwa kwa wakati. Kampuni zote mbili zimekubali kushirikiana na Tanesco katika kutekeleza makubaliano hayo.

  Awali kulikuwa na mvutano baina ya Tanesco na Kampuni ya Rolls Royce ya nchini Norway iliyotengeneza mitambo hiyo pamoja na kampuni ya Semco ya nchini Denmark iliyofunga mitambo hiyo, baada ya mitambo minne kati ya 10 kuharibika ndani ya kipindi cha miaka miwili na hivyo kusababisha uzalishaji wa megawati 18 kati ya 60 zilizopaswa kuzalishwa kupungua.

  Hata hivyo pande zote zinazolalamikiana zimeonekana kuwa na hoja ambapo Profesa Muhongo ameitaka Tanesco kuandika malalamiko yake na kuyawasilisha kwa kampuni Rolls Royce iliyotengeneza mitambo hiyo kabla ya februari 28 mwakani, malalamiko ambayo yanapaswa kujibiwa hadi kufikia tarehe 30 mwezi Machi mwakani ili kujua maamuz yatayofuata.

  Mabalozi wa pande zote mbili, ambao ni Hanne-Marie Kaarstad kutoka nchini Norway pamoja na Einar Jensen wa Denmark, wameeleza kuridhishwa na makubaliano ya kikao hicho wakiamini kwamba mwafaka huo utasaidia uzalishaji wa umeme kama ilivyokusudiwa ili kufikisha huduma ya umeme kwa wananchi.

  0 0

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (kushoto) na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Tonia Kandiero wakisaini mikataba miwili ya mikopo yenye masharti nafuu yenye thamani ya shilingi Bilioni 360 kwa ajili ya kuongeza Ufanisi wa Tanesco na kuiongezea mtaji Benki ya Maendeleo ya Wakulima nchini-TADB, Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es salaam.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (kushoto) na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Tonia Kandiero(kulia), wakibadilishana mikataba ya Mkopo wa Sh. Bilioni 360, zitakazo kwenda katika Sekta ya Nishati ya Umeme na Benki ya Maendeleo ya Kilimo nchini-TADB, tukio lililofanyika makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dare salaam.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (wa tatu kulia) na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Tonia Kandiero(wa pili kulia), wakisaini mikataba miwili yenye thamani ya Sh. Bilioni 360 kwa ajili ya kutunisha mfuko wa bajeti Kuu ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2016/17 na kuendeleza kilimo kupitia Benki ya Maendeleo ya Kilimo-AFDB, huku wakishuhudiwa na Mafisa wa pande zote mbili. Kushoto ni Kaimu Kamishna wa Fedha za Nje Mamelta Mutagwaba na wa pili kushoto ni Naibu Kaibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Amina Hamis Shaban, Makao Makuu ya Wizara hiyo Jijini Dar es salaam.
  Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Tonia Kandiero (kulia), akizungumza baada ya kusaini Mikataba miwili ya Mikopo yenye masharti nafuu yenye thamani ya shilingi Bilioni 360, ambapo ameshauri fedha hizo zitumike kikamilifu katika maeneo husika ambayo ni Bajeti na kuendeleza kilimo. kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James, Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango, jijini Dar es salaam.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (kushoto) akipiga makofi baada ya Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Tonia Kandiero (kulia), kuipongeza Serikali ya Tanzania kwa juhudi zake za maendeleo ya Uchumi hasa katika viwanda, baada ya kusaini mikataba miwili ya Sh. Bilioni 360, Makao Makuu ya Wizara hiyo Jijini Dar es salaam. (Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-WFM)

  0 0


   Rais wa TCCIA Ndibalema Mayanja akibadilishana nyaraka na Mkurugenzi Mkuu wa NMB Bi Eneker wakati Rais wa TCCIA na ujumbe wake ulipofanya ziara kwenye bank ya NMB. Ziara hiyo yenye lengo la kukuza uhusiano na fursa za biashara kati ya NMB na TCCIA iliwashirikisha pia Makamu wa Rais wa TCCIA Viwanda Octavian Mshiu, Kaimu Mkurugenzi wa TCCIA Bw Muganda na Mshauri wa TCCIA Masoko na Biashara Imani Kajula.


  0 0


   Takriban watu watano wamejeruhiwa baada ya basi kugonga nyumba moja.Basi hilo liligonga nyumba hiyo iliopo huko Homer Green karibu na mji wa Wycombe nchini Uingereza.Abiria watatu walijeruhiwa huku mwanamume na mwanamke waliokuwa ndani ya nyumba hiyo pia wakijeruhiwa.

  chanzo BBC

  0 0

  Wafanyakazi wa Aggrey&Clifford wakiwasili katika kituo cha Sadeline
  Mkurugenzi wa Uendeshaji wa kampuni ya Aggrey&Clifford,Cobus van Zly (kulia) na Mkurugenzi wa huduma za Matangazo,Oliver Mutere (katikati) wakikabidhi baadhi ya zawadi kwa watoto wenye mazingira magumu kwenye kituo cha Sadeline kilichopo Mbezi Juu wilayani Kinondoni kwa Msimamizi wa kituo hicho,Sarah Kitainda wakati wafanyakazi wa kampuni hiyo walipotembelea kituo hicho na kutoa zawadi na kucheza na watoto hao mwishoni mwa wiki.
  Mmoja wa watoto wanaolelewa katika kituo cha watoto wenye mazingira magumu cha Sadeline kilichopo Mbezi Juu wilayani Kinondoni,Benedicto Mutayoba akipokea zawadi kutoka kwa mfanyakazi wa kampuni ya Aggrey&Clifford,Martin Kirangu wakati wafanyakazi wa kampuni hiyo walipotembelea kituo hicho na kutoa zawadi kwa watoto na kucheza nao mwishoni mwa wiki,aliyembeba ni mama wa mtoto huyo,Grace Thomas.

  Mmoja wa watoto wanaolelewa katika kituo cha watoto wenye mazingira magumu cha Sadeline kilichopo Mbezi Juu wilayani Kinondoni,Maulid Rajab akipokea zawadi kutoka kwa mfanyakazi wa kampuni ya Aggrey&Clifford,Ndeshi Rajab
  Mfanyakazi wa kampuni ya Aggrey&Clifford,Nia van Aswegen (kulia) akiwapatia zawadi watoto Mmoja wa watoto wanaolelewa katika kituo cha watoto wenye mazingira magumu cha Sadeline
  Mfanyakazi wa kampuni ya Aggrey& Clifford, John Alexander akimkabidhi msaada wa mfuko wa vyakula mmoja wa watoto wanaolelewa katika kituo cha Sadeline.

  Wafanyakazi wa Aggrey&Clifford wakiwa wamewabeba baadhi ya watoto wanaolelewa katika kituo cha Sadeline
  Mfanyakazi wa Aggrey&Clifford,Nadah Dhiyebi akicheza na watoto wa kituo cha Sadeline
  Aggrey&Clifford yasaidia watoto wenye mazingira magumu

  Kampuni ya matangazo na ukuzaji wa masoko ya Aggrey&Clifford mwishoni mwa wiki imetoa msaada wa vitu mbalimbali kwa watoto wenye mazingira magumu kituo cha Sadeline kata ya Mbezi Juu ambapo pia baadhi ya wafanyakazi wake walishiriki kucheza na watoto hao kwa ajili ya kuwapatia faraja katika msimu huu wa sikukuu.
  Akiongea wakati wa hafla hiyo Mkurugenzi wa kitengo cha Matangazo ya Biashara wa Aggrey&Clifford,Oliver Mutere, alisema kuwa msaada huo wa nguo na chakula na vifaa vya kusomea ni kwa ajili ya kuwapatia faraja watoto hao wanaoishi katika mazingira magumu.
  “Moja ya sera ya kampuni yetu ni kusaidia shughuli za kijamii ikiwemo kuunga mkono jitihada za serikali za kukabiliana na changamoto mbalimbali zilizopo kwenye jamii ndio maana katika kipindi hiki tumeonelea kuna umuhimu wa kusaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu katika kata hii ya Mbezi Juu”.Alisema.
  Mutere alisema mbali na kutoa msaada wafanyakazi wa Aggrey&Clifford wamekuwa na utaratibu wa kujitoa na kutoa muda wao kwa ajili ya kusaidia kazi za kijamii “Kutokana na sera hii baadhi ya zawadi hizi zilizotolewa zimetokana na michango ya wafanyakazi”.
  Mratibu wa kituo cha watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu cha Sadeline ,Sarah Kitainda,alishukuru kwa msaada huo ambao alidai kuwa umeleta faraja kwa watoto hao hususani katika kipindi hiki cha msimu wa sikukuu ya Krismas na mwaka mpya.
  “Kwa niaba ya kituo hiki natoa shukrani kwa kampuni ya Aggrey&Clifford kwa kuwakumbuka watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu wa kata hii ya Mbezi na ni matumaini yangu kuwa mtazidi kushirikiana nasi kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazotukabili kuwalea watoto hawa katika siku za usoni.

  0 0

  Na.Vero Ignatus Arusha.

  Mabalozi wa usalama wa usalama barabarani kwa kushirikiana na jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani wamefanya zowezi la kutoa elimu kwa abiria pamoja na madereva huku jeshi la polisi wakiwapima madereva ulevi na kukagua ubora wa magari hayo kabla ya kuanza safari kuelekea mikoani

  Zowezi hilo limeongozwa na mkuu wa kikosi cha usalama barabarani SSP Nuru Suleiman na katika stendi kuu ya mabasi yaendendayo mikoani na nchini jirani Jijini Arusha huku zowezi hilo likiwa na lengo la kuelimisha,kukemea na kuripoti mwenendo mzima unaokiuka sheria za usalama barabarani.

  Kwa upande wake Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani Nuru Suleiman amesema kuwa kampeni hiyo inamafanikio makubwa tangia ianze kwenye wiki ya nenda kwa usalama kwani tangia mwanzoni mwa mwaka 2016 hakuna ajali ya basi iliyotokea na kuleta madhara kwa jamii kwa ujumla.

  "Kwakweli tunamshukuru sana Mungu kwani tangia mwaka huu uanze hatujapata ajali ya basi inaonyesha madereva wamepata elimu na wanaitendea kazi na tunawaomba waendelee kuwa makini ili ajali ikiwezekana zisitokee kabisa "alisisitiza kamanda Nuru.Aidha amesema kuwa wamekuwa wakiwapima madereva ulevi na madereva ambao wanakiuka sheria za usalama barabarani na pale wanapogundulika na makosa wapo wengine wanalipishwa faini na wengine wanapelekwa mahakamanikufutiwa leseni na kuzuiliwa kuendesha chombo cha moto kabisa.

  Kwa upande wake makamu mwenyekiti wa mabalozi wa usalama barabarani Bakari Msangi amesema kuwa lengo kubwa la oparesheni abiria paza sauti ni abiria kutambua wajibu na haki yake awapo ndani ya chombo cha usafiri ikiwemo kutokukaa kimya pale anapomuona dereva anakwenda kinyume na sheria za usalama barabarani,ulevi,kuyapita magari mengine mahali ambapo hapastahili,kutoa lugha zenye utata kwa abiria,dereva kuongea na simu wakati anaendesha,yote haya anatakiwa kutoa taarifa kwa jeshi la polisi.

  Aidha amesema kuwa abiria anatakiwakutoa taarifa pale dereva anapokuwa kwenye mwendo kasi, kufunga mkanda awapo ndani ya gari ili kwamba kama imetokea dharura yeyote asiweze kuhamishwa kwenye kiti alichokaa,pia wawapatie jeshi la polishi ushirikiano kwaajili ya usalama zaidi.

  "Unajua abiria wengine ni chanzo cha ajali kwani wanakuwa wanamchochea dereva kuendesha kwa mwendo kasi,wanapoulizwa na askari hawasemi kama kuna tatiuzo hilo ni kosa hebu wapeni ushirikiano jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani ni kwaajili ya faida yenu jamani."alisisitiza Bakari

  Naye mwenyekiti wa usalama barabarani Jijini Arusha bi.Stella Rutaguza amesema kuwa kazi kubwa abiria kutokukaa kimya pale anapomuona dereva anakiuka sheria za usalama barabarani ili kuweza kuepuka ajali ambazo zinaepukika.Amesema zowezi hili la Operesheni Abiria Paza Sauti litaendelea hadi April 2017.
  Mkuu wa kikosi cha Usalama barabarani SSP Nuru Suleiman akiwa katika kituo cha kikuu cha mabasi yaendayo mkoania na nchi jirani ,mkoani Arusha tayari kwa kutoa elimu kwa abiria na madereva leo 19Desemba 2016.Picha pamoja na habari na Vero Ignatus Blog.

  Kamanda wa Usalama barabarani akiwa anatoa maelekezo kwa Mabalozi wa usalama barabarani( RSA)Katika stendi kuu ya mabasi yaendayo mikoani na nchi jiarani mkoani Arusha leo 19Desemba2016.Picha na habari na Vero Ignatus Blog.
  Mabalozi wa Usalama barabarani( RSA)wakiwa tayari kuanza kazi ya kutoa elimu kwa Abiria namna ya kuutambua wajibu wao na haki zao wakiwa katika chombo cha usafiri.Picha na habari na Vero Ignatus Blog.

  Kutoka kushoto ni mwenyekiti wa Usalama barabarani mkoa wa Arusha bi.Stella Ruraguza akizungumza na mwenyekiti wa wakata tiketi stendi kuu ya mabasi yaendayo mkoani na nchi jirani Babuu Jumanne .Picha pamoja na habari na Vero Ignatus Blog
  Wa kwanza kushosto ni WP 6905 Neema Tesha pamoja na WP 5048 Coplo Mwajuma wakiwa kazini katika kukagua magari kabla hayajaanza safari kama inavyoonekana pichani nyuma yao kuna basi linaloonekana tayri wameshalikagua.Picha na habari na Vero Ignatus Blog
  Wa kwanza kushoto ni koplo Athilio Choga aliyepo katikati ni Vehicle Inspector Koplo Songoi na wa

  0 0

  FLAVANITE is bacK 24th of December @MzaLendO pUb, miLLenNium tOwerz, X Mass eVe, Come anD enjOy gOOd Musik from the Most respected Dj @boniluv ,ventUre & @dj_mackaytz
  #HatariHatariHatari
  #Flavanite
   

  0 0

  Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Susan Mlawi akizungumza na Wataalam wa kujitolea kutoka Japani waliomaliza muda wao wa kutoa huduma nchini, wakati wa hafla fupi ya kuwaaga wataalam hao iliyofanyika Ofisi ya Rais-Utumishi leo.
  Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Susan Mlawi akiwa katika mazungumzo na Wataalam wa kujitolea kutoka Japani waliomaliza muda wao wa kutoa huduma nchini, wakati wa hafla fupi ya kuwaaga wataalam hao iliyofanyika Ofisi ya Rais-Utumishi leo.
  Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Susan Mlawi akimkabidhi zawadi Mtaalam wa kujitolea kutoka Japani aliyemaliza muda wake wa kutoa huduma nchini, Bw. Hiroshi Mikuni, wakati wa hafla fupi ya kuwaaga wataalam hao iliyofanyika Ofisi ya Rais-Utumishi leo.
  Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Susan Mlawi akiwa katika picha ya pamoja na Wataalam wa kujitolea kutoka Japani waliomaliza muda wao wa kutoa huduma nchini, baada ya hafla fupi ya kuwaaga wataalam hao iliyofanyika Ofisi ya Rais-Utumishi leo.
  Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Susan Mlawi akiagana na Wataalam wa kujitolea kutoka Japani waliomaliza muda wao wa kutoa huduma nchini, mara baada ya hafla fupi ya kuwaaga wataalam hao iliyofanyika Ofisi ya Rais-Utumishi leo.

  0 0


  Meneja wa Tawi la TFA, Arusha wa Benki ya KCB Tanzania, Bi. Hogla Laizer (kulia), akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi 48,064,958 kwa Mkurugenzi mkuu wa Taasisi ya Ereto East Africa Foundation Mch. Godsave Ole Megiroo (kushoto), ikiwa ni msaada wa fedha zilizotolewa na benki hiyo kusaidia uboreshaji wa mazingira ya shule ya Mairowa Integrity katika ujenzi wa vyoo na eneo la kufulia. Wapili kushoto ni Mwalimu Mkuu Msaidizi wa shule ya Mairowa Integrity Bi. Elizabeth Mollel na mwalimu wa shule hiyo BiNancy Mseli (watatu kushoto).
  Meneja wa Tawi la TFA, Arusha wa Benki ya KCB Tanzania, Bi. Hogla Laizer (kulia), akikabidhi mfano wa hundi yenye thamni ya shilingi 48,064,958 kwa Mkurugenzi mkuu wa Taasisi ya Ereto East Africa Foundation Mch. Godsave Ole Megiroo (kushoto). Pamoja nao kwenye picha ni wafanyakazi wa benki ya KCB Tawi la TFA, Arusha.


  Meneja wa Tawi la TFA, Arusha wa Benki ya KCB Tanzania, Bi. Hogla Laizer (kulia), akizungumza na waandishi wa habari (hawamo pichani) wakati wa hafla ya makabidhiano ya Shilingi Milioni 48,064,958 kwa Taasisi ya Ereto East Africa Foundation. Katikati ni Mwalimu Mkuu Msaidizi wa shule ya Mairowa Integrity Bi. Elizabeth Mollel na mwalimu wa shule hiyo Bi Nancy Mseli.


  Afisa Biashara wa benki ya KCB Tawi la TFA, Arusha, Amedeus Tumaini akitambulisha meza kuu wakati wa hafla ya makabidhiano ya Shilingi Milioni 48,064,958 kwa Taasisi ya Ereto East Africa Foundation.

  · Mchango huo kuwezesha ujenzi wa vyoo na eneo la kufulia katika shule ya Mairowa Integrity.

  Dar es Salaam, 19 December, 2016 – Benki ya KCB Tanzania imekabidhi rasmi mchango wa shilingi 48,064,958 kwa Taasisi ya Ereto East Africa Foundation ikiwa ni mwitiko kwa ombi la Taasisi hiyo kwa ajili ya ujenzi wa vyoo 16 vya kuflashi na eneo la kufulia katika shule ya Mairowa Integrity iliyo chini ya uongozi wa taasisi hiyo. Benki ya KCB ilikua imeshawasilisha mchango huo tokea mwezi wa tatu mwaka huu.

  Akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano, Meneja wa Tawi la TFA, Arusha wa Benki ya KCB, Hogla Laizer alisema kuwa mchango huo upo ndani ya vipaumbele vya benki katika uwekezaji jamii kwa ajili ya kusaidia jamii zilizo na uhitaji.

  “Benki ya KCB Tanzania inadhamini uwajibikaji kwa jamii ambayo kwa kiwango kikubwa inalenga maeneo ya vipaumbele vya Elimu, Afya, Mazingira, Ujasiriamali na malengo yake hasa ni kujikita katika masuala ya ubinadamu”, Bi. Laizer alisema na kubainisha kwamba tangu ilipofunguliwa hapa Tanzania mwaka 1997, benki hiyo imekuwa ikijikita katika kuisadia jamii.

  Akitolea mfano wa michango iliyotolewa na benki hiyo katika kuboresha huduma za elimu nchini, Bi. Lazier alisema: “Kupitia miradi hiyo benki ya KCB Tanzania imeshatumia shilingi milioni miatatu kusaidia shule zaidi ya 20 kwa kuzipatia madawati pamoja na vifaa vingine vya kuboresha huduma na mazingira ya shule.”

  Alimaliza kwa kusema benki ya KCB ina kawaida ya kutembelea shule zote ambazo imepeleka misaada kila baada ya mwaka mmoja ili kuona manufaa yanayotokana na msaada husika. Hivyo aliieleza taasisi hiyo kuwa matunzo na matumizi mazuri ya mchango uliotolewa, ndo itaifanya benki ya KCB iongeze msaada katika shule ya Mairowa Integrity iliyo chini ya uongozi wa Ereto East Africa Foundation.

  0 0


  0 0

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mama Margart Sitta, mjane wa Spika mstaafu,  Sumuel Sitta wakati alipoitembelea familia ya marehemu jijini Dar es salaam Desemba 19, 2016. Kulia ni mkewe Mary. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
     Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary (kushoto  kwake) wakiwa katika picha ya pamoja na familia ya aliyekuwa Spika Mstaafu, Samuel Sitta wakati walipoitembelea familia hiyo, nyumbani kwa marehemu jijini Dar es salaam Desemba 19, 2016. Kulia kwake ni mjane wa marehemu, Margareth Sitta. Wengine pichani kutoka kushoto ni watoto wa marehemu, Benjamin Sitta, John Sitta na Sam Junior.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  na mkewe Mary wakisalimiana na mama Margaret Sitta, mjane wa alieyekuwa Spika mstaafu, Samuel Sitta wakati walipoitembelea familia ya Spika huyo jijini Dar es salaam Desemba 19, 2016. Wengine pichani ni watoto wa marehemu, kutoka kushoto ni  Benjamin Sitta, Sam Junior na John Sitta. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

   Kikosi cha Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, kilipoanza mazoezi leo asubuhi kujiandaa na mchezo ujao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) dhidi ya Majimaji utakaofanyika Uwanja wa Majimaji, mjini Songea, Jumamosi hii.
   Wachezaji wa Azam FC wakifanya mazoezi tofauti ya viungo
   Beki wa kati wa Azam FC, Aggrey Morris, akiruka juu kwenye mazoezi ya viungo ya kuruka koni.
   Beki wa kati wa Azam FC, Yakubu Mohammed, akimzuia winga Enock Atta Agyei
    Kiungo wa Azam FC, Salum Abubakar ‘Sure Boy’, akijaribu kumtoka winga Enock Atta Agyei
  Kipa wa Azam FC, Mwadini Ally, akiruka juu wakati wa mazoezi ya magolipa chini ya Kocha wa Makipa, Jose Garcia

  0 0


  Ofisa Mtendaji Mkuu wa Zantel Tanzania, Benoit Janin (kulia), akikata utepe kuashiria uzinduzi wa duka na kituo cha huduma kwa wateja cha kampuni hiyo katika jengo la China Plaza, Kariakoo, Dar es Salaam leo. Kushoto kwake ni wakala wa huduma kwa wateja, Asengo Adam na Meneja wa duka hilo, Yasmeen Ismail.
  Ofisa Mtendaji Mkuu wa Zantel Tanzania, Benoit Janin (katikati), akiangalia wakati wakala wa huduma kwa wateja katika duka la kampuni lililopo katika jengo la China Plaza, Magdalena Mbayuwayu (kulia), akihudumia wateja wakati wa uzinduzi rasmi wa duka na kituo hicho, Kariakoo, Dar es Salaam leo. Kulia kwake ni Meneja wa duka hilo, Yasmeen Ismail.
  Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa Zantel Tanzania, Gabriel Magambo (katikati), akizungumza na waandishi wa habari katika hafla ya uzinduzi wa duka na kituo cha huduma kwa wateja cha kampuni hiyo katika jengo la China Plaza Kariakoo, Dar es Salaam leo.
  Ofisa Mtendaji Mkuu wa Zantel Tanzania, Benoit Janin (katikati), akimsikiliza meneja wa duka na kituo cha huduma kwa wateja cha kampuni hiyo katika jengo la China Plaza, Yasmeen Ismail wakati mhudumu katika duka hilo Magdalena Mbayuwayu (kulia), akihudumia wateja mara baada ya hafla ya uzinduzi rasmi wa duka na kituo hicho, Kariakoo, Dar es Salaam leo.

older | 1 | .... | 1075 | 1076 | (Page 1077) | 1078 | 1079 | .... | 1897 | newer