Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1057 | 1058 | (Page 1059) | 1060 | 1061 | .... | 1897 | newer

  0 0
  0 0

  Every year, International Day of Persons with Disabilities is an opportunity for the world to stand together against the discrimination of women and men with disabilities and to raise the flag for inclusion and empowerment through education, the sciences, culture and communication and information. 
    The 2030 Agenda for Sustainable Development connects inclusion and development – this is vital, because persons with disabilities continue to face discrimination, violence, stigma, and exclusion. This is particularly true for the most vulnerable groups in society, such as migrants, refugees and indigenous people with disabilities.
   Women and girls also shoulder heavy burdens, lacking opportunities, at greater risk from abuse, violence and exclusion. These challenges throw a shadow over societies as a whole.In this year of action to take forward the 2030 Agenda, our message is clear -- sustainable development will not be possible without the full inclusion of persons with disabilities at every level, without their roles and voices built into all decision-making and policies. 
    UNESCO is pulling out all the stops to support implementation of the 2006 United Nations Convention on the Rights of Persons with Disabilities and to take forward the new Sustainable Development Goals. We need redoubled efforts to ensure that all women and men with disabilities around the world are integrated fully into all aspects of social, political, cultural and economic life, to build a world that is pluralistic, open, participatory and knowledge-based. 
  This is how our societies will become truly inclusive.This must begin with education. UNESCO is leading support to its Member States to implement SDG4-Education 2030, which commits all countries to ensure equal access to all levels of education and vocational training, regardless of disability status.We must raise visibility for stronger advocacy. 
  This is the importance of the UNESCO/Emir Jaber al-Ahmad al-Jaber al-Sabah Prize for Digital Empowerment of Persons with Disabilities, which will recognize this year the outstanding contribution of individuals and organizations in promoting the inclusion and accessibility, and enhancing the lives of persons with disabilities through application of digital solutions, resources and technologies. 
  UNESCO has also revised the International Charter of Physical Education, Physical Activity and Sport, to reinforce physical education, physical activity and sport around the world, and the Organisation is accompanying Member States in reviewing national physical education policies to become child-centered, flexible, sensitive, and inclusive, independently of abilities. 
    In this spirit, we dedicate the 2016 International Day of Persons with Disabilities to promoting the 17 Sustainable Development Goals, to build together a more inclusive and equitable world for all.

  0 0

  WANAWAKE NA MAENDELEO FOUNDATION
  D A R ES SALAAM | IJUMAA |DESEMBA 2, 2016
  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

  Katika gazeti la Raia Mwema toleo No 486 la Tarehe 30 Novemba, 2016 kumeandikwa habari yenye kichwa kilichosomeka “Mali za Salma Kikwete kuuzwa kwa mnada?”.  Katika habari hiyo kumetolewa madai ati kwamba taasisi ya WAMA inayoongozwa na Mheshimiwa Mama Salma Kikwete inao mzigo mkubwa bandarini ambao haujalipiwa ushuru na kodi. Na kwa sababu hiyo, Mamlaka ya Mapato Tanzania imepanga kuuza mali hizo.

  Kwa niaba ya Taasisi ya WAMA napenda kutoa masikitiko yetu kwamba habari hizo ni za uongo na hazina ukweli wowote. Kwa maoni yetu gazeti hilo lina dhamira mbaya dhidi ya Taasisi ya WAMA na Mwenyekiti wake, Mheshimiwa Mama Salma Kikwete. Nia yao ni kupaka matope na kuchafua majina na sifa ya taasisi yetu na kiongozi wake.

  Ukweli kuhusu jambo hili ni kwamba, WAMA ilitumiwa maboksi Kumi na Moja (11) ya vitabu vikiwa ni zawadi (grant) kutoka Nakayama Foundation ya Japani ambayo ndiyo iliyofadhili ujenzi wa Shule ya Sekondari ya WAMA-Nakayama iliyopo Nyamisati, Kibiti. Maboksi hayo yaliyotumwa kupitia BL 243016002211 yaliwasili bandarini tarehe 27/06/2016. Yalitolewa tarehe 10/8/2016 baada ya WAMA kulipia kodi zote na ushuru wote unaotahili tarehe 26/07/2016.

  Vitabu hivyo vimekwishapelekwa shuleni na wanafunzi wanavitumia. Hakuna mzigo wowote wa Taasisi ya WAMA uliopo bandarini unaosubiri kutolewa wala kuuzwa na TRA. Hivyo basi, gazeti hilo kuandika kuwepo kwa mzigo mkubwa wa WAMA bandarini ni jambo la kughushi ambalo limefanywa kwa dhamira mbaya na kwa sababu wanazozijua wao.

  Tumelitaka gazeti la Raia Mwema limuombe radhi Mwenyekiti wa WAMA Mheshimiwa Mama Salma Kikwete na kuiomba radhi WAMA Foundation kwa kuandika taarifa za uongo. Gazeti hilo limechafua sifa ya Mwenyekiti wa WAMA na WAMA Foundation kiasi ambacho wanao wajibu wa kuomba radhi na kusafisha majina na heshima zetu mbele ya jamii. 

  Ikiwa hawatatekeleza haya ndani ya kipindi cha siku Saba, yaani kabla ya tarehe 07 Desemba, 2016, tutalazimika kuchukua hatua zipasazo za kisheria.

  Daudi Nasib,
  Katibu Mtendaji,
  Dar es Salaam,
  Tel: +255 22 2781287 

  info@wamafoundation.or.tz

  0 0


  Tarehe 1 Desemba kila mwaka ni siku ya maadhimisho ya Ukimwi Duniani,mwaka huu 2016 Kampuni ya Uchimbaji Madini ya dhahabu ya Acacia kupitia mgodi wa Buzwagi uliopo wilayani Kahama mkoani Shinyanga imeadhimisha siku hiyo kwa kuzindua Mashindano ya mpira wa miguu na pete “Mahusiano Cup” ili kuhamasisha jamii inayozunguka mgodi huo kupima virusi vya Ukimwi.
  Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mashindano ya Mahusiano yaliyoenda sambamba na zoezi la upimaji wa VVU katika uwanja wa taifa mjini Kahama , Meneja mkuu wa mgodi wa Buzwagi Mhandisi Asa Mwaipopo alisema kampuni yao inazidi kufarijika kuona namna mahusiano baina ya mgodi na wananchi wanaozunguka mgodi huo.


  “Mahusiano na jamii yamekuwa yakiimarika siku hadi siku,awali tulipoanza mashindano haya mwaka 2009 ni kata ya Mwendakulima pekee ndiyo ilikuwa ikinufaika kwa kuzikutanisha timu zinazounda mitaa yake ambayo ni Mwime,Chapulwa,Busalala na Mwendakulima”,alisema Mhandisi Mwaipopo. 

   Mhandisi Mwaipopo alisema mashindano hayo yataendelea hadi Desemba 8 mwaka huu yakikutanisha timu 14 za mpira wa miguu na timu 6 za mpira wa pete. "Timu zote 20 zimekabidhiwa jezi na mipira vyote vikiwa na gharama ya shilingi 20,355,000/=,kwa timu ya mpira wa miguu na pete  mshindi wa kwanza atapewa zawadi ya shilingi 400,000/= na kombe,mshindi wa pili 300,000/= na mshindi na kwa upande wa kampeni ya utoaji elimu ya Ukimwi jumla ya shilingi 25,600,000/= zimetumika kununulia vifaa vya upimaji na uendeshaji wa zoezi lenyewe",aliongeza Mhandisi Mwaipopo.

   Alisema kwa kubadilisha mtazamo wa uendeshaji wa michezo ya mahusiano Cup awamu hii wamezihusisha kata nyingi zaidi za tarafa ya Kahama Mji na itakuwa fursa muhimu kwa wadau wa michezo kuweza kuona vipaji vya wanamichezo na kutafuta namna nzuri ya kuviendeleza.
  Alizitaja timu za mpira wa miguu zitakazoshiriki kuwa ni Nyihogo,Nyahanga,Busoka,Kahama mjini,Zongomela,Malunga,Majengo,Mwendakulima,Ngogwa,Nyasubi,Mhongolo,Wendele na timu ya mgodi wa Buzwagi na timu za mpira wa pete kuwa ni Kahama mjini,Mhungula,Mwendakulima,Mhongolo,Ngogwa na Zongomela.
  Katika hatua nyingine mhandisi Mwaipopo alisema kiwango cha maambukizi ya virusi vya Ukimwi vimeshuka katika mgodi wa dhahabu wa Acacia Buzwagi wilayani Kahama mkoani Shinyanga kutoka asilimia 2.6 mwaka hadi kufikia asilimia 0.4 mwaka 2016 baada ya kuwahamasisha kupima afya zao.
  Mwaipopo alisema pamoja na kiwango cha ndani ya mgodi kuridhisha maeneo yanayozunguka mgodi wa Buzwagi yana kiwango cha juu cha maambikizi ya VVU ambapo takwimu zinaonesha kuwa kiwango cha maambukizi kwa wilaya ya Kahama kwa takwimu za kitaifa ni asilimia 9.6,mkoa wa Shinyanga asilimia 7.4.
  Naye mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu aliupongeza mgodi huo kwa kuchukua hatua ya kuhamasisha jamii kupima VVU kupitia michezo kwani takwimu za maambukizi zinatisha wilayani humo ambapo asilimia 70 ya vijana wenye umri kati ya miaka 20 hadi 49 wamepata maambukizi ya VVU,ambao ndiyo nguvu kazi ha taifa.
  Nkurlu aliupongeza mgodi huo kwa kuwa mdau mkubwa wa michezo wilayani humo kwa kudhamini timu kadhaa na kuziwezesha kushiriki katika mashindano mbalimbali ndani nan je ya mkoa wa Shinyanga.
  Tazama picha hapa chini Matukio yaliyojiri wakati wa uzinduzi wa Mahusiano Cup-Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog

  Mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu (katikati) akisindikizwa na meneja mkuu wa mgodi wa Buzwagi Mhandisi Asa Mwaipopo kwenda kukagua  timu zinazoshiriki Mahusiano Cup mara baada ya kuwasili katika uwanja wa taifa wa Kahama.Kulia ni Meneja Uendelevu mgodi wa Buzwagi George Mkanza na wa kwanza kushoto ni mwenyekiti wa chama cha mpira wa miguu wilaya ya Kahama Ibrahim Khan akifuatiwa na mkuu wa polisi wilaya ya Kahama Kulia ni afisa mawasiliano na habari wa mgodi wa Buzwagi bwana Magesa Magesa (mwenye shati la bluu) akiongozana na maafisa wa serikali walipowasili uwanjani. Kushoto kwake ni katibu tawala wilaya ya Kahama Timoth Ndanya ,Mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Kahama Anderson Msumba pamoja na maafisa wengine wa serikali


  Washiriki wa Mahusiano Cup wakiwa uwanjani wakisubiri kukaguliwa na mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu
  Mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu akisalimiana na wachezaji wa timu ya mpira wa miguu ya Nyihogo
  Mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu alikagua timu ya mpira wa pete ya Mhungula
  Meneja mkuu wa mgodi wa Buzwagi mhandisi Asa Mwaipopo akisalimiana na wachezaji wa Mhungula
  Kushoto ni mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Kahama Anderson Msumba akiteta jambo na mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu na meneja wa mkuu wa mgodi wa Buzwagi Mhandisi Asa Mwaipopo
  Katibu tawala wa wilaya ya Kahama Timoth Ndanya akisalimia wananchi na wanamichezo wakati wa uzinduzi wa Mahusiano Cup


  Meneja mkuu wa mgodi wa Buzwagi Mhandisi Asa Mwaipopo akizungumza wakat wa uzinduzi wa Mahusiano Cup siku ya Ukimwi Duniani 


  Mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mahusiano Cup

  Wachezaji wa timu ya Nyihogo wakiwa katika picha ya pamojaWachezaji wa timu ya Buzwagi wakijiandaa na mchezo Mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu akisikiliza maelezo kutoka kwa mwamuzi mkuu wa mchezo wa ufunguzi kati ya timu ya Nyihogo na timu ya mpira wa miguu ya mgodi wa Buzwagi


  Wachezaji wa timu ya Buzwagi wakitakiana mchezo salama na wachezaji wa timu ya Nyihogo
  Mkuu wa wilaya Kahama Fadhili Nkurlu akijiandaa kupiga mpira kuashiria ufunguzi rasmi wa Mahusiano Cup
  Mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu akiachia shuti
  Mchezaji wa timu ya Buzwagi  Felix Mwakisunga akikimbilia mpira uliopigwa na mkuu wa wilaya Mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu akifungua mchezo kati ya Kahama mjini na Mhungula Wachezaji wa timu ya mpira wa pete ya Kahama mjini wakiwa tayari kuanza mchezo kati yao na Mhungula katika mchezo wa mechi ya ufunguzi wa Mahusiano Cup Wachezaji wa timu ya mpira wa pete ya Mhungula wakiwa uwanjani Mchezo kati ya Kahama mjini na Mhungula ukiwa umeanza Mchezo unaendelea ambapo Kahama mjini waliibuka washindi kwa kuwafunga Mhungula goli 33 kwa 7 Mwenyekiti wa chama cha mpira wa miguu wilaya ya Kahama Ibrahim Khan akisisitiza jambo wakati wa mchezo kati ya Buzwagi na Nyihogo ambapo Buzwagi waliibuka washindi kwa kuibamiza Nyihogo bao 2-0 Moja ya heka heka katika lango la timu ya Buzwagi
  Dawati la ufundi la timu ya Buzwagi
  Dawati la ufundi timu ya Nyihogo Mchezo unaendelea Mashabiki wa mpira wa miguu wakiwa uwanjani


  Mchezo kati ya Nyihogo na Buzwagi unaendelea ambapo mpaka filimbi ya mwisho inapulizwa Buzwagi walikuwa wanaongoza kwa goli 2-0
  Wakati mashindano yakiendelea wananchi pia walikuwa wakimiminika kwa wingi katika banda la kupima VVU
  Mmoja wa wananchi waliojitokeza kupima VVU akipokea zawadi ya simu ya kisasa kutoka kwa mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu baada ya kuibuka mshindi wa mchezo wa bahati nasibu uliowahusisha wananchi waliojitokeza kupima afya zao kwa hiari
  Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog

  0 0  0 0

   Mhandisi wa umeme wa Shirika la Umeme nchuini Tanzania TANESCO, akiwa kazini jijini Dar es Salaam

  SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO) linawatangazia wateja wake wa Mikoa ya Dodoma, Singida, Shinyanga, Tabora, Mwanza,  Geita, Mara, Simiyu na na baadhi ya maeneo ya Mikoa ya  Arusha, Manyara, Kilimanjaro  na Tanga na baadhi ya maeneo ya Mkoa wa Dar es Salaam (Tazara, Mlimani City, Mandela Road, Ubungo na Kimara, Sinza, Mabibo) kuwa yatakosa Umeme siku ya Jumapili DESEMBA 04, 2016 kuanzia saa 02:00 Asubuhi hadi saa 11.00 Jioni.

  SABABU: Kuruhusu Mkandarasi anayejenga Njia Kuu ya Kusafirisha Umeme ya Msongo Mkubwa ya Kilovolti 400 maarufu kama (Backbone Transmission Line 400 kV) kutoka Iringa hadi Shinyanga.
  SABABU: Kuzimwa kwa njia ya Umeme ya Msongo wa Kilovolti 33 Kituo cha Ubungo Dar es Salaam ilikumruhusu Mkandarasi kufanya matengenezo.

  Matengenezo hayo yanalenga kuboresha na kuimarisha hali ya upatikanaji wa Umeme Nchini.
    
  Uongozi unaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.
  Imetolewa na; Ofisi ya Uhusiano
  TANESCO Makao Makuu  0 0

   Vijana 43 wa kihadzabe wakipanda mabasi kuelekea katika kambi ya JKT Makutopora kikosi cha KJ 834 kujiunga na kikosi hicho kwa hiyari kwa mkataba wa miaka ya miwili mara baada ya kuagwa na mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Singida. Jamii ya kihadzabe huendesha maisha yao kwa kuwinda na kula nyama pori, matunda ya porini, asali na mizizi.
   Mmoja wa kijana wa kihadzabe Zuhura Ramadhani Longa ambaye alikuwa akiwasindikiza vijana wenzake wanawinda na kurina asali, amesema ameamua kujiunga na jeshi ili aweze kuisaidia familia yake lakini pia aweze kulitumikia taifa.
   Vijana 43 wa kihadzabe wakipunga mikono kuonyesha utayari wa kujiunga na kambi ya JKT Makutopora kikosi cha KJ 834 kwa hiyari kwa mkataba wa miaka ya miwili mara baada ya kuagwa na mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Singida. Jamii ya kihadzabe huendesha maisha yao kwa kuwinda na kula nyama pori, matunda ya porini, asali na mizizi.
  Vijana wa kihadzabe ambao walikuwa wanawinda na kurina asali, wamesema wameamua kujiunga na jeshi ili waweze kusaidia familia yake lakini pia waweze kulitumikia taifa.

   Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Singida Bw. Buhacha Baltazar Kichinda ambaye ni Katibu Tawala Msaidizi sehemu ya utawala na rasilimali watu akiwaaga Vijana 43 wanaojiunga na kambi ya JKT Makutopora kikosi cha KJ 834 kwa hiyari kwa mkataba wa miaka ya miwili. Bw. Kichinda amesema wakiwa jeshini watafundishwa uzalendo, ukakamavu, stadi za jamii na nidhamu, amewaasa wazazi kuwapeleka shule wanafunzi na kupokea fursa kama za jeshi.
   Afisa Tawala ofisi ya Mshauri wa Mgambo Rhinocerus Magembesoni akiwaasa vijana 43 wa kihadzabe wakipanda mabasi kuelekea katika kambi ya JKT Makutopora kikosi cha KJ 834 kujiunga na kikosi hicho kwa hiyari kwa mkataba wa miaka ya miwili mara baada ya kuagwa na mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Singida. Jamii ya kihadzabe huendesha maisha yao kwa kuwinda na kula nyama pori, matunda ya porini, asali na mizizi.

  0 0


  MJIENDELEZE MSIISHIE HAPO  MLIPOFIKIA-MWAKYEMBE.

  Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria Dkt Harrison Mwakyembe amewataka wahitimu wa astashada na stashada za Sheria wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto kujiendeleza zaidi kielimu ili waweze kwenda na wakati hasa ikizingatiwa kuwa dunia ya sasa inataka kujiendeleza kila siku vinginevyo wataachwa nyuma.

  Mhe. DKT Mwakyembe ametoa rai hiyo alipowatunuku vyeti vya Astashahada na Stashahada wahitimu hao katika ukumbi wa Jaji Nyalali uliopo chuoni hapo mjini Lushoto.Amewataka wahitimu hao kuwa tayari kulihudumia taifa kwa kufanya kazi kwa moyo na kuepuka kujihusisha na vitendo vya rushwa kwa kuwa rushwa ni adui mkubwa wa haki duniani Amewataka wahitimu hao kuwa tayari kuwahudumia wananchi katika eneo hilo hasa ikizingatiwa kuwa serikali iko mbioni kutunga sheria ya ahuduma ya msaada wa kisheria ambayo itawawezesha wananchi wenye uhitaji kupata huduma za kisheria kupitia wasaidizi wa kisheria.

  "Niwaambie ninyi mliohitimu hapa leo mna bahati sana, Serikali sasa inatunga Sheria ya Msaada wa huduma za kisheria , umeshasomwa Bungeni kwa mara ya kwanza na Bunge likiupitisha na kuwa Sheria mtaweza kufanya kazi kama wasaidizi wa sheria na hivyo kuwahudumia wananchi wengi wenye uhitaji na kusaidia harakati za utoaji haki nchini," alisema Dkt Mwakyembe.Amesema kutungwa kwa sheria hiyo kutawawezesha wahitimu hao kuwa na uwezo wa kuwahudumia wananchi kwa kuwapa msaada wa kisheria wananchi hasa wale wasio na uwezo wa kumudu gharama za mawakili.

  Dkt Mwakyembe ametunuku vyeti vya astashahada kwa wahitimu 135 na stashahada kwa wahitimu 208 katika Mahafali ya 16 ya Chuo cha Uongozi wa Mahakama kilichopo Lushoto mkoani Tanga.

  Wakati huo huo Chuo hicho cha IJA kimezindua NEMBO yake , Tovuti mpya ya Chuo na mfumo wa mawasiliano kwa barua pepe kutumia mtandao wa Serikali.Akizungumza wakati wa uzinduzi wa vitu hivyo Mkuu wa Chuo hicho Mhe. Jaji Dkt Paul Kihwelo alisema  sio kwamba Chuo hakikuwa na Nembo na Tovuti ila yanefanyika marekebisho makubwa katika vitu hivyo ili kwenda na wakati.

  Alisema kwamba  Chuo ndio kimeanza  kutumia barua pepe kwa kutumia mtandao wa Serikali ambapo kwa sasa utawahusu watumishi wa chuo hicho kama ilivyo kwa taasisi nyingine za Serikali na wanatarajia pia kuwaunganisha wanafunzi hapo baadae.
   
   

   


  0 0

  Na Henry Mdimu.

  Mtangazaji machachari wa vipindi vya TV aliyevunja rekodi katika ukosoaji uliotukuka, Salama Jabir ametajwa kuta ndiye atakayeendesha tunzo za EATV Jumamosi ijayo zitakazofanyika katika ukumbi wa Mlimani City.

  Roy Mbowe, Mratibu Mkuu wa tunzo hizo amable pia ni mkuu wa Masoko wa EATV amemtaja mwanadada huyo jana usiku saa nne kwamba ndiye atakayekuwa Mc kwa masaa matatu mfululizo akiongoza shughuli hiyo ambayo itarushwa live na kituo cha EATV pekee.

  Jumla ya tunzo tisa zitatolewa kwa wasanii wa muziki na filamuwaliofanya vyema kwenye tasnia hiyo huku tunzo moja ya heshima ikitolewa kwamdau mwenye mchango uliotukuka katika tasnia ya sanaa kwa mwaka 2015/16.
  0 0

  Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Ardhi, Prof. Idrissa Mshoro (katikati kulia) akiteta jambo na Kaimu Naibu Makamu Mkuu wa Chuo hicho (Taaluma), Prof. Gabriel Kassenga(katikati kushoto), pembeni kulia ni Kaimu Naibu Makamu Mkuu wa chuo hicho (Mipango, Fedha na Utawala),Prof. Robert Kiunsi, pembeni kushoto ni Maafisa Waandamizi wa chuo hicho. Shughuli hizo zimefanyika leo Jijini Dar es Salaam katika viwanja vya chuo hicho.
  Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Ardhi, Prof. Idrissa Mshoro akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa chuo na wanafunzi waliofanya vizuri kitaaluma wakati wa shughuli za ugawaji wa vyeti na zawadi kwa wanafunzi waliofaulu masomo mbalimbali uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam katika viwanja vya chuo hicho.
  Mmoja kati ya washindi wa jumla wenye alama za juu, Anyighwile Lwijiso akipokea zawadi kutoka kwa mmoja wa wafadhili ambao ni Kampuni ya Hightech System mara baada ya kutangazwa kuwa mshindi. Shughuli hizo zimefanyika leo Jijini Dar es Salaam katika viwanja vya chuo hicho.  Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO.

  Chuo Kikuu cha Ardhi kimetoa zawadi na tuzo kwa wanafunzi 104 waliofanya vizuri kitaaluma ili kutoa hamasa kwa wanafunzi wengine kuweka juhudi katika masomo.

  Zawadi hizo zimetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Prof. Idrissa Mshoro ambaye ametangaza kuwa jumla ya wanafunzi wanne kati ya waliofanya vizuri wamepata alama sawa hivyo kuibuka washindi wa jumla kwa mwaka 2016. 

  Akisoma hotuba wakati wa sherehe hizo, Kaimu Naibu Makamu Mkuu wa Chuo hicho (Taaluma), Prof. Gabriel Kassenga amesema kuwa sherehe hizo zimekuwa zikiwezeshwa na wadau mbalimbali waliojitoa kwa hali na mali kutoa zawadi na tuzo kwa wanafunzi waliofaulu vizuri kwenye vipengele mbalimbali vya taaluma hivyo amewasihi wadau hao kuendelee kuunga mkono jitihada zinazofanywa na wanafunzi hao ili kuwashawishi wanafunzi wengine kufanya vizuri.

  “Zawadi mbalimbali zinazotolewa na wafadhili zimekua zikiwasaidia wanafunzi hawa kuongeza tija kwenye maisha yao ya kielimu na kiuchumi kwani wengi wao wamekuwa wakizitumia fedha hizo kama mitaji ya kufanyia biashara pindi wamalizapo masomo yao,”alisema Prof. Kassenga.

  Amefafanua kuwa mwaka huu umekuwa wa tofauti kwani idadi ya wanafunzi wanawake na wanaume waliopata tuzo hizo iko sawa tofauti na miaka mitatu iliyopita ambapo wanawake walikua wakiongoza kwa asilimia 3.7 kwa kupata tuzo nyingi wakati wanaume wakiwa ni asilimia 2.2. 

  Prof. Kassenga ametaja baadhi ya zawadi zilizotolewa na wafadhili walioshiriki katika shughuli hiyo kuwa ni vyeti, Kompyuta mpakato (laptop),vifaa vinavyotumika katika kupimaji wa ardhi pamoja na fedha taslimu.Aidha, Prof. Kassenga ametoa rai kwa kwa wanafunzi wote waliomaliza chuoni hapo kuwa juhudi walizokuwa wakizionyesha wakati wa masomo waende wakaziendeleze katika jamii zinazowazunguka pamoja na kwenye shughuli mbalimbali za ujenzi wa Taifa ili wakawe mfano bora kwa vizazi vijavyo.

  Kwa upande wake Emily Elandogo ambaye ni mmoja kati ya wanafunzi waliopewa zawadi hizo amewashukuru walimu wa chuo hicho kwa elimu wanayoitoa ambayo itakua ni chanzo cha kuwaletea maendeleo sehemu yoyote watakapokuwa pia ametoa ushauri kwa wanafunzi wenzake kuitumia vizuri elimu waliyoipata ili iweze kuwasaidia katika maisha yao. 

  Mahafali ya Kumi ya chuo hicho yanategemewa kufanyika Disemba 3 mwaka huu katika viwanja va chuo hicho ambapo wahitimu wa shahada mbalimbali watatunukiwa stahili pamoja na vyeti vyao. 

  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati ufunguzi wa mkutano wa Wadau wa kuendeleza maeneo Tengefu ya Viwanda vya Usindikaji Vyakula uliofanyika kwenye ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati ufunguzi wa mkutano wa Wadau wa kuendeleza maeneo Tengefu ya Viwanda vya Usindikaji Vyakula uliofanyika kwenye ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam ambapo aliwapongeza TAFOPA kwa kazi nzuri wanayoifanya lakini pia aliwataka Wasindikaji kuongeza ushirikiano ili kufikia maendeleo na mafanikio ya juu.
  Wadau waliohudhuria na kushiriki wakimsikiliza kwa makini Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati ufunguzi wa mkutano wa Wadau wa kuendeleza maeneo Tengefu ya Viwanda vya Usindikaji Vyakula uliofanyika kwenye ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
   Mwenyekiti wa TAFOPA Bi. Suzy Laizer akihutubia wakati ufunguzi wa mkutano wa Wadau wa kuendeleza maeneo Tengefu ya Viwanda vya Usindikaji Vyakula uliofanyika kwenye ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam, mgeni rasmi kwenye mkutano huu alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia bidhaa mbalimbali za vyakula vilivyosindikwa zinazotengenezwa na wajasiriamali   muda mfupi kabla ya kufungua wa mkutano wa Wadau wa kuendeleza maeneo Tengefu ya Viwanda vya Usindikaji Vyakula uliofanyika kwenye ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam. 

                                         ................................................................. 


  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema Serikali ipo mbioni kupunguza muda wa utoaji wa leseni za biashara nchini ili kutoa fursa kwa wananchi wengi zaidi kupata leseni hizo kwa ajili ya shughuli za kibiashara.


  Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere wakati anafungua mkutano wa wadau wa kuendeleza maeneo tengefu ya viwanda vya usindikaji wa vyakula nchini.

  Makamu wa Rais amesema mpango utaenda pamoja na kupunguza baadhi ya kodi na tozo ambazo ni kero kwa wananchi hasa wenye viwanda kama hatua ya kukuza biashara na uwekezaji katika sekta ya viwanda nchini.


  Amesisitiza kuwa Serikali inaendelea na mazungumzo na wenye mabenki hususani benki ya TIB ili kutoa mikopo yenye riba nafuu kwa wawekezaji wenye nia ya  kuanzisha viwanda.

  Kuhusu usindikaji wa bidhaa nchini, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ambaye pia ni Mjumbe katika jopo la Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa la kumuwezesha mwanamke kiuchumi akiwakilisha nchi za ukanda wa Kusini na Mashariki mwa Afrika amepongeza jitihada zinazofanywa na wasindikaji wadogo nchini katika utengenezaji wa bidhaa mbalimbali ambazo zitakidhi katika masoko ya ndani na nje ya nchi.


  “Serikali inafarijika sana kuona kuwa wasindikaji wadogo nchini wamethubutu na wana uwezo wa ushindani katika biashara ya ndani na hata nje, hivyo tunayohaki ya kujigamba kwa kuthubutu, Tumeweza na Tuendelea Kusonga mbele  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema umefika wakati kwa Wizara na taasisi za Serikali na wadau wa maendeleo kuona umuhimu wa kuhakikisha viwanda vinajengwa vijijini ili mkulima mdogo anapolima awe na uhakika wa kupata soko katika viwanda hivyo.

  Amesema kuwa hali hiyo itaondoa changamoto ya kusafirisha bidhaa nyingi ambazo zinaharibika njiani au zinapofika sokoni na hivyo kukosesha jamii kipato kilichotarajiwa.

  Makamu wa Rais pia amehimiza watafiti nchini wajielekeza katika kufanya tafiti ambazo zitasaidia sekta binafsi na serikali kwa ujumla kuhusu namna bora ya kukuza sekta ya viwanda nchini.
  Kwa upande wake, Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage amekiri kuwa bado kuna changamoto kubwa ya maeneo ya yatakayojengwa  viwanda na kwamba Serikali imeliona tatizo hilo na inalifanyia kazi ambapo tayari  imeshaziagiza Halmashauri zote nchini kujenga maeneo kwa ajili ya viwanda.

  0 0  0 0

  Wasanii wanaowania  tunzo za EATVleo walifanya semina na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ilikuwapa uthubutu wa kutambua vipaji vyao na kuvifanyia kazi ili kuweza kukabiliana na soko la ajira pindi watakapomaliza masomo yao.
   
  Semina hiyo iliyoendeshwa na benki ya Barclays chini ya pango wake wa ready to Work ilifanyikakatika ukumbi wa Nyerere uliopo katika eneo la Chuo Kikuu Mlimani ambapo jumla ya wasanii 45 waliochaguliwa kuwania tunzo za EATV walihudhuria.
   
  PICHANI JUU: Mwakilishi kutoka Barclays Bank,  Joe Bendera akiongea na wanahabari waliohudhuria seminaya wasanii kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam yenye lengo la kuelimisha wanavyuo kuhusiana na kugundua vipaji vyao na kuvifanyia maamuzi baada ya masomo ilikukwepa adha ya ukwasi wa ajira inayolikabili Taifa
  Hapa ni Kajala Masanja anayewania tunzo ya muigizaji bora wa Kike akiongea na wanahabari
  Baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha dar es Salaam wakisikiliza shuhuda za wasanii mbali mbali wanaowania tunzo za EATV katika semina ya ushawishi wa kugundua vipaji vyao na kuvifanya kazi iitwayo Ready to Work inayosimamiwa na benki ya Barclays
   Mjadala ukiendelea
   Lady Jaydee amble anawania tunes ya msanii Bora wa kike akijibu maswali ya wanafunzi
  Mmoja kati ya wasanii wanaowania tunzo ya Msangi Bora wa kiume Daudi Tairo a.k.a Duma akijibu hoja za wanafunzi
   Khadija Ally anayewania tunzo ya muigizaji bora wa kike akiongea wakati wa semina ya Ready to Work inayoshirikisha wasanii wanaowania tunzo za EATV
  Mwakilishi wa Benki ya Barclays akijibu hoja za wanafunzi kuhusiana na mpangowa Ready to Work unaoendeshwa na benki hiyo
   Mwanafunzi akiuliza swali
  Kahala Masanja akijibu hoja

  0 0

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizindua kiwanda cha Lodhia Plastic Industries Limited kabala ya kukitembelea kiwanda hicho Desemba 3, 2016.   Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho  Gambo na kulia kwa Waziri Mkuu ni Mwenyekiti wa Kampuni ya Nodhia Group, Haroon Nodhia.
  1
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kitazama matangi yanayotengenezwa katika kwanda cha Lodhia Plastic Industries wakati alipokitembelea kiwanda hicho Desemba 3, 2016
  2
  Waziri Mkuu,Kasim Majaliwa akitazama gari linalotengenezewa bodi maalum kwa ajili ya shughuli za utalii wakati alipotembelea kiwanda cha kutengeneza mabodi ya magari cha HansPaul cha jijini Atusha Desemba 3, 2016.
  3 
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda cha Fibreboards cha Arusha, Tosky Hans (wapili kulia) kuhusu bidhaa zinazozalishwa na kiwanda hicho wakati alipokitembelea Desemba 3, 2016. Watatu kulia ni Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo.
  5
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Mwenyekiti wa Kiwanda cha Lodhia Plastic Industries Limited cha jijini Arusha, Haroon Lodhia (kushoto ) kuhusu utengenezaji wa mabomba ya plastic wakati alipotembelea kiwanda hicho,Desemba 3, 2016.
  7
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua shehena ya ungwa uliosindikwa wakati alipotembelea kwanda cha unga cha MOBAN cha jijiniArusha Desemba 3, 2016.
  8 
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama mfuko wenye unga wakati alipotembelea kiwanda cha unga cha MONABAN jijini Arusha Desemba 3, 2016.
  9
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha unga cha MONABAN cha Arusha wakati alipokitembelea  Desemba 3, 2016.

  (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0


  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akizindua Kongamano la Wajasiriamali katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi la Zamani Mnazi Mmoja Mjini Unguja leo

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimkabidhi zawadi Meneja wa Tawi la DTB hapa Zanzibar Mbarouk Ramadhan Mbarouk katika hafla ya uzinduzi wa Kongamano la Wajasiriamali Zanzibar katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi la Zamani Mnazi Mmoja Mjini Unguja leo

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimkabidhi zawadi Ofisa wa Taasisi ya ‘Mchele Z’bar Foundation’ hapa Zanzibar Eshe Haji Ramadhan katika hafla ya uzinduzi wa Kongamano la Wajasiriamali Zanzibar katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi la Zamani Mnazi Mmoja Mjini Unguja leo.

  Mratibu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia Dkt.Afwa Mohamed akitoa hutuba fupi kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia katika hafla ya uzinduzi wa Kongamano la Wajasiriamali Zanzibar katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi la Zamani Mnazi Mmoja Mjini Unguja leo,ambalo lilizinduliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,
  Baadhi ya Wajasiriamali wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akizindua Kongamano la Wajasiriamali hao lililofanyika katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi la Zamani Mnazi Mmoja Mjini Unguja leo,

  Baadhi ya Wajasiriamali wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akizindua Kongamano la Wajasiriamali hao lililofanyika katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi la Zamani Mnazi Mmoja Mjini Unguja leo.

  [Picha na Ikulu.]

  0 0

   Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Jengo la pili la Taaluma lenye ghorofa 7 la Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini Kampasi Kuu ya Dodoma, lililogharimu shilingi Bilioni  10.3. Kulia kwake ni Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa Chuo hicho Prof. Razack Lokina na kushoto kwake ni Mkuu wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini Dkt. Frank Hawassi wakifurahi kwa pamoja mara baada ya uzinduzi huo.
    Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango, akiangalia viatu vya ngozi vilivyotengenezwa na mjasiliamali mdogo Bw. Stephano Chifwaguzi (nayeonesha bidhaa ya ngozi kiunoni) baada ya kuwezeshwa kiutaalamu na Chuo cha Mipango na Maendeleo Vijijini, kwa ufadhili wa Jumuiya ya Ulaya, wakati wa mahafali ya 30 ya Chuo hicho Kampasi Kuu ya Dodoma.
   Meza Kuu ikiongozwa na Mgeni Rasmi, Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) akifurahia mahafali ya 30 ya Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini, yaliyofanyika Kampasi Kuu ya Dodoma katika eneo la Miyuji-mkoani humo.
   Wajumbe wa Baraza la kumi na la tisa la uongozi wa  Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini wakiimba wimbo wa Taifa wakati wa Mahafali ya 30 ya Chuo cha Mipango na Maendeleo Vijijini Kampasi ya Dodoma, iliyoko katika eneo la Miyuji, mkoani humo.
  Wahitimu wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini pamoja na wageni waalikwa, wakiimba wimbo wa Taifa wakati wa Mahafali ya 30 ya Chuo hicho yaliyofanyika katika eneo la Miyuji, mkoani Dodoma.


  0 0  0 0

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Charles Tizeba kufanya uchunguzi kwa nini mbolea ya minjingu inayozalishwa nchini haitumiki na badala yake inaagizwa mbolea kutoka nje ya nchi.

  Ametoa agizo hilo jana (Jumamosi, Desemba 3, 2016) wakati alipotembelea kiwanda cha Fibre Board 2000 Limited ambacho kinatengeneza bidhaa mbalimbali ikiwemo mbolea ya Minjingu, wakati akiwa katika siku ya pili ya ziara yake ya kikazi mkoani Arusha.Alisema mbolea hiyo licha ya kuwa na viwango vya ubora vinavyohitajika, haitumiki nchini kwa sababu ya kuingiliwa na masuala ya kisiasa dhidi ya matumizi yake.

  “Nchi jirani ya Kenya inaiona mbolea hii bora kuliko sisi wa ndani? Mheshimiwa Waziri wa Kilimo are we serious? Tunazalisha mbolea hapa tunasema haina kiwango lakini Kenya wanaitaka na wameagiza tani 300,000,” alisema.

  Waziri Mkuu aliongeza kuwa “Jambo hili lazima liangaliwe ndani ya Wizara kwa nini mnaagiza mbolea kutoka nje wakati ndani tunazalisha hii ni mianya ya rushwa, rushwa ulaji ulaji tu. Waziri lichukulie maanani jambo hili hatutaki siasa katika sekta ya kilimo,”.Alisema kumekuwa na mijadala mingi kuhusu mbolea ya minjingu kumbe baadhi ya watendaji wanatengeneza mianya ya kwenda kununua mbolea nje ambako hutumia fedha nyingi ambazo zingeweza kutumika katika miradi mingine ya maendeleo.

  Kwa upande wake Mkurugenzi wa kiwanda cha Fibre Board 2000 Limited, Tosk Hansi  amesema kampuni hiyo inayozalisha bidhaa mbalimbali ikiwemo mbolea ya minjingu, imetoa ajira kwa watu zaidi ya 1,800 wengi wao wakiwa ni vijana ila inakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo ya urasimu wakati wanapoomba vibali vya uvunaji mazao ya misitu.
  Awali, kampuni hiyo ya Fibre Board 2000 limited imemkabidhi Waziri Mkuu mchango wa madawati 1,000 kwa ajili ya shule mbalimbali za mkoani Arusha ili kuwawezesha wanafunzi kusoma katika mazingira mazuri.


  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU
  JUMAPILI, DESEMBA 4, 2016.

  0 0


  0 0

   Mwenyekiti wa Kampuni ya Lodhia Group  Bw. Arun Lodhia akimpokea Waziri Mkuu wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania  Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa ili kuzindua kiwanda cha Lodhia Plastic kinachotengeneza Mabomba ya Maji ,kilichopo Njiro jijini Arusha Leo, 3 Disemba 2016.
  Mwenyekiti wa Kampuni ya Lodhia Group Bw. Arun Lodhia akitoa maelezo kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania  Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa wakati alipofika kuzindua kiwanda cha Lodhia Plastic kinachotengeneza Mabomba ya Maji ,kilichopo Njiro jijini Arusha Leo, 3 Disemba 2016.
   Mwenyekiti wa Kampuni ya Lodhia Group  Bw. Arun Lodhia (wa kwanza kushoto waliokaa) akiteta jambo na Waziri Mkuu wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania  Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa akifuatiwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo na Naibu waziri wa kilimo ,Mifugo na Uvuvi Mhe. William Ole Nasha wakati walipofika kuzindua kiwanda cha Lodhia Plastic kinachotengeneza Mabomba ya Maji ,kilichopo Njiro jijini Arusha Leo, 3 Disemba 2016.
  Waziri Mkuu wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania  Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa akikata utepe tayari kwa uzinduzi wa  kiwanda cha Lodhia Plastic kinachotengeneza Mabomba ya Maji ,kilichopo Njiro jijini Arusha Leo, 3 Disemba 2016.
   Kutoka Kushoto (mwenye suti bluu) ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Lodhia Group  Bw. Sailesh Pandit,  Mwenyekiti wa kampuni ya Lodhia Group Bw. Arun Lodhia wakiongozana na  Waziri Mkuu wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania  Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa ndani ya kiwanda cha Lodhia Plastic kinachotengeneza Mabomba ya Maji ,kilichopo Njiro jijini Arusha Leo, 3 Disemba 2016.
  Waziri Mkuu wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania  Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuzindua kiwanda cha Lodhia Plastic kinachotengeneza Mabomba ya Maji ,kilichopo Njiro jijini Arusha Leo, 3 Disemba 2016.
   Mwenyekiti wa Kampuni ya Lodhia Group  Bw. Arun Lodhia akimkaribisha Waziri Mkuu wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania  Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa ili kuongea na hadhara iliyopo kwenye kiwanda hicho mara baada ya kuzindua kiwanda kinachotengeneza Mabomba ya Maji ,kilichopo Njiro jijini Arusha Leo, 3 Disemba 2016.
  Waziri Mkuu wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania  Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa akiongea machache mara baada ya kuzindua kiwanda cha Lodhia Plastic kinachotengeneza Mabomba ya Maji ,kilichopo Njiro jijini Arusha Leo, 3 Disemba 2016.
   Waziri Mkuu wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania  Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa akizindua jiwe la msingi katika kiwanda cha Lodhia Plastic kinachotengeneza Mabomba ya Maji ,kilichopo Njiro jijini Arusha Leo, 3 Disemba 2016.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Lodhia Group  Bw. Sailesh Pandit akiagana na  Waziri Mkuu wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania  Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa mara baada ya kuzindua kiwanda cha Lodhia Plastic kinachotengeneza Mabomba ya Maji ,kilichopo Njiro jijini Arusha Leo, 3 Disemba 2016.
  Mwenyekiti wa kampuni ya Lodhia Group Bw. Arun Lodhia akiagana na  Waziri Mkuu wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania  Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa mara baada ya kuzindua kiwanda cha Lodhia Plastic kinachotengeneza Mabomba ya Maji ,kilichopo Njiro jijini Arusha Leo, 3 Disemba 2016.


  Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Lodhia Group  Bw. Sailesh Pandit akisoma risala mbele ya Mgeni rasmi ambaye niWaziri Mkuu wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania  Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa ndani ya kiwanda cha Lodhia Plastic kinachotengeneza Mabomba ya Maji ,kilichopo Njiro jijini Arusha Leo, 3 Disemba 2016. Picha zote Gadiola Emanuel

  habari na  Woinde Shizza Globu ya jamii Arusha.

   Halmashauri za majiji, manispaa na miji wametakiwa kutumia mabomba ya maji yanayozalishwa nchini badala ya kuagiza bidhaa hiyo toka nje ili kuweza kuvinufaisha  viwanda vya ndani.

                 

  Hayo yamebainishwa na waziri mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa wakati akizindua kiwanda cha   kutengeneza mabomba ya Plastic ya maji yenye  ukubwa wa aina mbalimbali  (Lodhia Plastics ) kilichopo njiro jijini hapa.Alisema kuwa haiana haja ya halmashauri  au majiji kuagiza bidhaa mbalimbali nje ya nchi  wakati  nchi yetu inaviwanda vya kutosha vya kutengeneza bidhaa hizo.  “Sioni sababu ya wahandisi wa Halmashauri na washauri elekezi halmashauri kushinikiza wakandarasi wa hapa Arusha kwenda kununua mabomba ya maji nje ya mkoa wakati hapa kuna kiwanda kama Lodhia ambacho kinatengeneza hizo bidhaa kwakweli hii labda iwe   ni chuki tu”alisema Majaliwa ambaye ameanza ziara ya siku nane mkoani Arusha.  Alisema ni muhimu kwa halmashauri kununua mabomba hayo kwa matumizi ya miradi ya maji na kuunga mkono juhudi zinazofanywa na wawekezaji wa ndani.  “Washauri wa miradi mbalimbali acheni chuki …waache wakandarasi wanunue bidhaa bora zilizothibitishwa na Shirika la Viwango la Taifa (TBS) na Shirika la Viwango la Kimataifa (ISO),” alisema.Aidha alitoa mfano, kwa upande wa Mkoa wa Arusha kuna mpango wa kujenga mradi mkubwa wa maji utakaogharimu dola za Marekani milioni 200, na katika utekelezaji wake ni lazima watoe kipaumbele cha kutumia mabomba yanayozalishwa na kiwanda hicho.Mradi huo ukikamilika unatarajiwa kumaliza kero ya maji kwa wakazi wa jijini hapa.

  Alisisiza haoni umuhimu wa halmashauri na wakandarasi kununua mabomba kutoka nje ya Arusha au nje ya nchi wakati kuna mabomba yanayozalishwa na wawekezaji wazawa na yanakidhi viwango.

  “Serikali  yetu itaendelea kuwaenzi na kuwalinda wawekezaji wote wa ndani ambao wamekuwa msaada mkubwa wa kutoa ajira ambayo ni janga kwa taifa na dunia kwa ujumla”alisema Majaliwa.

  Awali Mwenyekiti wa Bodi ya Lodhia Group, Arun Lodhia, alisema serikali ichukue nafasi ya kuzungumza na wenye viwanda mara kwa mara ili kujua matatizo yao na kuyatafutia ufumbuzi.Alisema viwanda chini ya kampuni hiyo, vinazalisha bidhaa nyingi zenye ubora lakini makampuni yanashindwa kununua na kupenda zaidi kununua bidhaa za nje.

  Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda hicho, Sailesh Pandit, alisema  kwamba wanashindwa kuuza mabomba ya maji na malighafi nyingine katika miradi mikubwa ya maji iliyopo mkoani Arusha.

  Alisema wanashindwa kufanya hivyo licha ya bidhaa zao kuwa na TBS na ISO kutokana na hujuma wanazofanyiwa na baadhi ya wahandisi na washauri elekezi wa miradi.“Imeshatokea mara kadhaa kwa wakandarasi wanaotekeleza miradi kuzuiwa kununua mabomba ya maji kutoka Lodhia Plastics na badala yake hulazimishwa kununua mabomba kutoka nje ya mkoa hivyo kuwasababishia gharama za ziada,” alisema.

  Kuhusu ajira, alisema kiwanda hicho kimetoajiri  Watanzania kati ya 1, 200 hadi 1, 300 lakini pia Watanzania zaidi ya 500 wananufaika kutokana na kushiriki katika utoaji wa huduma mbalimbali kiwandani hapo.

  Alisema mtandao wa viwanda vinne vinavyomilikiwa na kampuni ya Lodhia Group wanalipa kodi wastani wa Sh. bilioni 20 kwa mwaka.Kwa upande wao, baadhi ya makandarasi, Samuel Lugemalila wa Kampuni ya Vest Tanzania Ltd na Kastuli Mandange kutoka Fraju Group Ltd  na Maxmilian Iranghay  wa kampuni Wining Spirit Construction Ltd, walitoa ushuhuda kuhusu namna washauri waelekezi na watumishi wengine wanavyowakataza kununua bidhaa za Lodhia Plastics na kuwataka wanunue zinazotengenezwa nje ya mkoa.

  Walisema kitendo hicho kinawashababisha kushindwa  kukamilisha miradi yao kwa wakati na kuwaongezea gharama kubwa.
  Aidha waliiomba serikali kuondoa urasimu kwa wahasibu kulipa malipo kwa wakati licha ya miradi kukaguliwa na kupata cheti cha uhakiki wa kazi.

older | 1 | .... | 1057 | 1058 | (Page 1059) | 1060 | 1061 | .... | 1897 | newer