Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1058 | 1059 | (Page 1060) | 1061 | 1062 | .... | 1898 | newer

  0 0

   Wananchi wa kijiji cha Nyatanga kilichopo Kata ya Panzuo Tarafa ya Mkamba mkoani Pwani wakimsikiliza Mbunge wa Jimbo la Mkuranga,Abdallah Ulega alipokuwa akizungumza nao na kupanga nao mikakati ya kujikwamua na umaskini kwa namna moja ama nyingine.
   Mbunge wa Jimbo la Mkuranga,Abdallah Ulega akikagua jengo la Zahanati ya Nyatanga iliyojengwa kwa fedha za wananchi wa kijiji cha Nyatanga kilichopo Kata ya Panzuo Tarafa ya Mkamba mkoani Pwani. 
   Mbunge wa Jimbo la Mkuranga,Abdallah Ulega akizungumza na wananchi wa wa kijiji cha Nyatanga kilichopo Kata ya Panzuo ,Tarafa ya Mkamba ambapo yupo katika ziara za kikazi katika  jimbo lake hilo la Mkuranga mkoani Pwani.Mh.Ulege ameendelea na ziara yake ya kusikiliza na kutatua kero mbalimbali za wananchi wake,ikiwemo pia na kukagua miradi mbalimbali ya Maendeleo
   Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya  Mkuranga mkoani Pwani,Mhandisi Mshamu Munde akifafanua jambo katika mkutano uliofanyika kwenye  kijiji cha Nyatanga kilichopo Kata ya Panzuo ,Tarafa ya Mkamba mkoani Pwani.
   Mbunge wa Jimbo la Mkuranga,Abdallah Ulega akisalimiana na wananchi wa Kata ya Panzuo Tarafa ya Mkamba.picha zote na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.

  0 0

   Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angelina Mabula akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi (hawapo pichani) wakati alipowasili wilayani humo kufuatilia utendaji kazi na utoaji huduma wa sekta ya ardhi kwa wananchi. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Bw. Said Mtanda.
   Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Bw. Said Mtanda akitoa ufanunuzi kwa wananchi mbele ya Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angelina Mabula kuhusu masuala mbalimbali ya ardhi  yanayotakiwa kufuatwa na wananchi pindi wanapofuatilia huduma za ardhi.
  Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angelina Mabula akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Kanondo kilichopo wilayani Nkasi mkoani Rukwa  mara baada ya kuwasikiliza kuhusu matatizo wanayokutana nayo katika sekta ya ardhi.

  0 0

  Chama cha Wamiliki/Waendeshaji wa Mitandao ya Kijamii nchini 'Tanzania Bloggers Network' (TBN) kilichosajiliwa rasmi na Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani, mwezi Aprili, 2015 na kupewa namba ya usajili, S. A 20008.  Kinapenda kuwataarifu kuwa kinatarajia kuanza mkutano wake mkuu na mafunzo kwa Bloggers kesho Jumatatu tarehe 5 -6 mwezi wa 12/2016.

  Mkutano huo na mafunzo kwa wanachama utafunguliwa rasmi na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Dk. Hassan Abbas katika Ukumbi wa Mikutano wa Jengo la Golden Jubilee Tower jijini Dar es Salaam. Mkutano huo uliodhaminiwa na Benki ya NMB na wadhamini wengine unatarajia kuanza majira ya saa mbili na nusu asubuhi na kufanyika kwa siku mbili mfululizo.

  Katika mkutano huu wanatasnia watapewa semina juu ya uendeshaji mitandao ya jamii kwa manufaa, upashaji habari kwa kutumia mitandao yao kwa kuziangatia maadili na namna ya kunufaika na mitandao hiyo kwa waendeshaji (kujipatia kipato) hasa ukizingatia kuwa wapo baadhi yetu tunaifanya kazi hii kama ajira nyingine.

  Aidha katika mkusanyiko huu mbali na washiriki kupata mafunzo pia watapata muda wa kujadili masuala mbalimbali ya umoja wao na kutoka na mkakati wa kuijenga zaidi TBN kwa mafanikio ya wana Blogu.
  Mkutano huu ni matokeo mazuri ya ushirikiano kati ya TBN na wataalam wa masuala ya habari na mitandao ya kijamii, ambao kwa pamoja tumeandaa semina hii kwa wanahabari wa mitandao ya kijamii hasa 'Bloggers' kwa lengo la kujifunza zaidi na kujadili masuala mbalimbali ya chama na tasnia nzima.

  TBN inaendelea kuishukuru Serikali kupitia taasisi zake ikiwemo Mamlaka ya Udhibiti Mawasiliano nchini (TCRA) kwa kutoa ushirikiano mkubwa hadi kuwezesha chama hiki cha wamiliki/waendeshaji mitandao ya jamii kukamilisha mchakato wa usajili wake.

  Lakini kwa namna ya pekee nayapongeza pia makampuni mengine yakiwemo PSPF, NHIF, SBL, na Coca Cola kwa kuungana nasi katika kufanikisha tukio hili la kuwaleta pamoja bloggers kwa lengo la kuwanoa zaidi juu ya shughuli wanazozifanya.

  Kimsingi lazima tukubali kuwa mitandao hii imekuwa tegemeo kubwa la vyanzo vya habari na kusambaza taarifa mbalimbali tena kwa muda mfupi, hivyo kuna kila sababu ya kuendelea kuwanoa wanaoiendesha ili kupunguza matumizi mabaya ya mitandao hii.

  TBN inaamini njia pekee ya kupambana na matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii ni kuendelea kutoa elimu kwa waendeshaji na watumiaji ili mwisho wa siku wasikubali kutumika vibaya au kuitumia vibaya mitandao hii katika kutoa taarifa. Kwa dunia ya sasa hakuna atakayepinga kuwa mitandao hii imekuwa ikielimisha umma, ikikosoa jamii na kiburudisha juu ya masuala anuai ya kijamii.


  Imetolewa na; Mwenyekiti wa Muda wa TBN
  Joachim E. Mushi
  0756469470

  0 0

   Makamu Mwenyekiti wa CCM-Bara, Philip Mangula akisaini kitabu cha maombolezo ya kifo cha Rais Mstaafu wa Cuba, Fidel Castro, nyumbani kwa Balozi wa Chuba hapa nchini, Jorge Luis Lopez Tormo (aliyesimama), Mtaa wa Alli Bin Said, Oysterbay jijini Dar es Salaam.
   Makamu Mwenyekiti wa CCM-Bara, Philip Mangula akimpa pole  Balozi wa Chuba hapa nchini, Jorge Luis Lopez Tormo baada ya kusaini kitabu cha maombolezo ya kifo cha Rais Mstaafu wa Cuba, Fidel Castro, nyumbani kwa balozi huyo,, Mtaa wa Alli Bin Said, Oysterbay jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Waziri wa zamani Adamu Malima ambaye naye alifika kusaini kitabu hicho
    Makamu Mwenyekiti wa CCM-Bara, Philip Mangula akimpa pole  Balozi wa Chuba hapa nchini, Jorge Luis Lopez Tormo baada ya kusaini kitabu cha maombolezo ya kifo cha Rais Mstaafu wa Cuba, Fidel Castro, nyumbani kwa balozi huyo,, Mtaa wa Alli Bin Said, Oysterbay jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Waziri wa zamani Adamu Malima ambaye naye alifika kusaini kitabu hicho
    Makamu Mwenyekiti wa CCM-Bara, Philip Mangula akimpa pole  Balozi wa Chuba hapa nchini, Jorge Luis Lopez Tormo baada ya kusaini kitabu cha maombolezo ya kifo cha Rais Mstaafu wa Cuba, Fidel Castro, nyumbani kwa balozi huyo,, Mtaa wa Alli Bin Said, Oysterbay jijini Dar es Salaam. 
   Makamu Mwenyekiti wa CCM-Bara, Philip Mangula akizungumza na Balozi wa Chuba hapa nchini, Jorge Luis Lopez Tormo baada ya kusaini kitabu cha maombolezo ya kifo cha Rais Mstaafu wa Cuba, Fidel Castro, nyumbani kwa balozi huyo,, Mtaa wa Alli Bin Said, Oysterbay jijini Dar es Salaam. 
  Msaidizi wa Balozi wa Chuba hapa nchini Sultan Hamud Said akimkaribsha Makamu Mwenyekiti wa CCM, Bara, Philip Mangula alipowasili kwenye ubalozi huo kusaini kitabu cha maombolezo ya kifo cha Rais mstaafu wa Cuba Fidel Castro. Picha na Bashir Nkoromo

  0 0

  Katika siku za karibuni baadhi ya vyombo vya habari na mitandao ya kijamii imechapisha taarifa zinazomhusisha Mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Mhe. Mama Salma Kikwete na Taasisi anayoiongoza ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) kwamba imeshindwa kulipia kodi mizigo mikubwa iliyoiingiza nchini na hivyo kuwa hatarini kupigwa mnada.

  Taarifa hizo zimemhusisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kuwa anahusika kuzuia mizigo hiyo bandarini mpaka hapo itakapolipiwa kodi.

  Tunapenda kuutarifu umma kuwa taarifa hizo sio kweli na ni uzushi, kwani Rais Magufuli hajawahi kuzuia wala kuagiza kuzuiwa kwa mizigo ya Mama Salma Kikwete.

  Rais Magufuli amesikitishwa sana na uzushi huo unaofanywa kwa lengo la kumchafua Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na familia yake na amewataka waandishi wa habari na vyombo vya habari nchini kuacha kuandika na kuchapisha taarifa za uzushi na badala yake vizingatie weledi na kufuata sheria.

  “Nimesikitishwa sana na uzushi unaofanywa dhidi ya Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na Mke wake Mama Salma Kikwete, tafadhali wale mnaotengeneza uzushi huu acheni mara moja na muacheni Rais Mstaafu Kikwete apumzike.

  “Rais Mstaafu Kikwete amefanya kazi kubwa ya kulitumikia Taifa hili, amestaafu anapumzika, narudia muacheni apumzike, Serikali haitaendelea kuvumilia uzushi na uchonganishi huu unaofanywa kwa makusudi ili kuwachafua viongozi wastaafu”ameonya Rais Magufuli.


  Gerson Msigwa
  Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
  Dar es Salaam
  04 Desemba, 2016

  0 0

  Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe,Riziki Pembe Juma (wa pili kulia) akimkabidhi cheti mmoja wa wanafunzi wa Darasa la saba katika sherehe za Mahfali ya Skuli ya Feza Zanzibar (Private) kwa wanafunzi wa Kidato cha 4,6 na 7 mwaka 2016,iliyofanyika juzi Skulini hapo Chukwani Wilaya ya Magharibi,(kulia) Mwalimu Mkuu Ally Yussuf Nungu.
  Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe,Riziki Pembe Juma (kushoto) akimkabidhi cheti mmoja wa wanafunzi wa Kidato cha Nne katika sherehe za  Mahfali ya Skuli ya Feza Zanzibar (Private) kwa wanafunzi wa Kidato cha 4,6 na 7 mwaka 2016,iliyofanyika juzi Skulini hapo Chukwani Wilaya ya Magharibi,(katikati) Mwalimu Mkuu Ally Yussuf Nungu.
  Wahitimu wa Kidato cha Nne katika Skuli ya Feza Zanzibar (Private) ya Chukwani Wilaya ya Magharibi Unguja wakiwa katika mahfali wanafunzi wa Kidato cha 4,6 na 7 iliyofanyika juzi,ambapo mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe,Riziki Pembe Juma,
  Wanafunzi wa Darasa la Sita na Saba katika Skuli ya Feza Zanzibar (Private) wakiimba wimbo maalum wakati wa Mahafali ya wanafunzi wa Kidato cha 4 ,6 na 7 Mwaka 2016 iliyofanyika katika Skuli hiyo iliyopo Chukwani Wilaya ya Magharibi juzi.
  Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe,Riziki Pembe Juma akimpongeza Mtoto wa darasa la 5 Zahra Zahir aliyesoma Utenzi katika sherehe za Mahfali ya Skuli ya Feza Zanzibar (Private) kwa wanafunzi wa Kidato cha 4,6 na 7 mwaka 2016,iliyofanyika juzi Skulini hapo Chukwani Wilaya ya Magharibi.
  Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe,Riziki Pembe Juma akimpongeza Mtoto wa darasa la 4 Latifah Mohamed Abdulrahman aliyeimba Wimbo wa Kizungu (ENGLISH SONG) katika sherehe za Mahfali ya Skuli ya Feza Zanzibar (Private) kwa wanafunzi wa Kidato cha 4,6 na 7 mwaka 2016,iliyofanyika juzi Skulini hapo Chukwani Wilaya ya Magharibi.
  Baadhi ya Wahitimu wa darasa la Sita katika Feza Zanzibar (Private) wakiwa katika sherehe za Mahfali ya Skuli ya Feza Zanzibar (Private) kwa wanafunzi wa Kidato cha 4,6 na 7 mwaka 2016,iliyofanyika juzi Skulini hapo Chukwani Wilaya ya Magharibi.
  Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe,Riziki Pembe Juma alipokuwa akitoa hutuba yake wakati wa sherehe za Mahfali ya Skuli ya Feza Zanzibar (Private) kwa wanafunzi wa Kidato cha 4,6 na 7 mwaka 2016,iliyofanyika juzi Skulini hapo Chukwani Wilaya ya Magharibi.
  Baadhi ya waalimu waliopewa zawadi katika sherehe za Mahfali ya Skuli ya Feza Zanzibar (Private) kwa wanafunzi wa Kidato cha 4,6 na 7 mwaka 2016,iliyofanyika juzi Skulini hapo Chukwani Wilaya ya Magharibi,ambapo mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe,Riziki Pembe Juma.
   

  0 0

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na  Napono Sokoine (wapili kulia) na  Nekiteto Sokoine (kulia) ambao ni  wajane wa aliyekuwa Waziri Mkuu, Marehemu Edward Sokoine wakati aipokwenda nyumbani kwa marehemu, Monduli Juu kuisalimia familia akiwa katika ziara ya wialaya ya Monduli Desemba 4, 2016.
  soko-1
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiweka shada la maua kwenye kaburi la aliekuwa Waziri Mkuu, Edward Sokoine wakati alipokwenda nyumbani kwa marehemu, Monduli Juu akiwa katika ziara ya wialya ya Monduli Desemba 4, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  soko-2
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipokwenda nyumbani kwa  aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Sokoine, Monduli Juu kuisalimia familia akiwa aktika ziara ya wialya ya Monduli Desemba 4, 20, 16.  Kushoto kwake  wajane wa marehemu, Napono Sokoine (w pili kulia) na kulia ni  Nekiteto Sokoine . Kulia kwake  ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo.(Picha na Ofisi ya Wziri Mkuu)

  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akipata maelezo kutoka kwa Kamishana wa Kikoso cha Zima Moto Zanzibar Abdalla Malimosi wakati alipokuwa akiaangalia picha za magari mapya ya kikosi hicho yanayotarajiwa kuwasili hivi karibuni,wakati alipotembelea ujenzi wa majengo mapya ya kikkosi hicho leo huko katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Wilaya ya Magharibi “A”Unguja.


  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) alipokuwa akizungumza na Viongozi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Zanzibar na Uongozi wa Kikosi cha Zima Moto na Uokozi, wakati alipofika kutembelea ujenzi wa majengo mapya ya kikosi hicho leo.

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) alipokuwa akipata maelezo kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Viwanja wa Ndege Zanzibar Abdulghani Himid Msoma wakati alipowasili katika Ofisi za Mamlaka hiyo akiwa katika ziara ya kutembelea majengo mapya ya kikosi Zima Moto na Uokozi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume huko Kisauni Wilaya ya Magharibi “A”Unguja leo.

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) alipokuwa akizungumza na Uongozi Mamlaka ya Viwanja wa Ndege Zanzibar na Uongozi wa Zima Moto na Uokozi mara alipowasili katika Ofisi za Mamlaka hiyo akiwa katika ziara ya kutembelea majengo mapya ya kikosi Zima Moto na Uokozi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume huko Kisauni Wilaya ya Magharibi “A”Unguja.

  Jengo hili kama linavyoonekwanwa baada ya kumalizika katika hatua za Ujenzi wake Kikosi cha Zimamoto na Uokozi itakuwa ni Ofisi ya Kikosi hicho, mbapo leo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) alitembelea kuangalia ujenzi unaoendelea.

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kushoto) akiangalia baadhi ya Vyumba vya Ofisi mpya ya Kikosi cha Zimamoto na Uokozi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume huko Kisauni Wilaya ya Magharibi “A”Unguja leo,(wa pili kulia)Kamishna wa Kikosi hicho Abdalla Malimosi na SACF Simai Haji Simai.


  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akiangalia Njia za kupitishia Umeme katika jengo jipya la Kikosi cha Zimamoto na Uokozi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume huko Kisauni Wilaya ya Magharibi “A”Unguja alipotembelea leo alipofanya ziara maalum.

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kushoto) akitoa maelekezo kwa Uongozi wa Kikosi cha Zimamoto na Uokozi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume alipotembelea kituo kidogo kinachofayiwa matengenezo akiwa katika ziara maalum leo,(kushoto)Kamishna wa Kikosi hicho Abdalla Malimosi na SACF Simai Haji Simai (wa pili kulia).
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akipata maelezo kutoka kwa Kamishna wa Kikosi cha Zimamoto na Uokozi Abdalla Malimosi wakati alipotembelea kituo kidogo kinachofayiwa matengenezo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume akiwa katika ziara maalum leo,(kushoto) Naibu Waziri wa Ujenzi,Mawasiliano na Usafirishaji Mhe,Mohamed Ahmed Salum,(wa pili kushoto) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa,Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ Mhe,Haji Omar Kheri.
  Picha na Ikulu, 04/12/2016.

  0 0

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwafariji wanawake waliolazwa kwenye wodi ya wazazi katika hospitali ya mkoa wa Arusha ya Mount Meru wakati alipotembelea wodi hiyo na kukuta wakiwa wamelala watatu kwenye kitanda kimoja Desemba 4, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waganga na Wauguzi wa hospitali ya mkoa wa Arusha ya Mount Meru wakati al;ipoitembelea Desemba 4, 2016.

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na viongozi wa wilaya ya Monduli baada ya kuwasili kwenye Ofisi ya Mkuu wa wilaya hiyo kuanza ziara ya siku moja ya kazi wilayani humo Desemba 4, 2016.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akielekea kwenye wodi ya wazazi katika hospitali ya mkoa wa Arusha ya Mount Meru wakati alipoitembelea Desemba 4, 2016. Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


  Mmoja wa wauguzi katika hospitali ya mkoa wa Arusha ya Mount Meru akideki katika wodi ya wazazi wakati Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipotembelea wodi hiyo akiwa katika ziara ya mkoa wa Arusha Desemba 4, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  Waziri Mkuu, Kasssim Majaliwa akiwapungia wananchi wa Monduli baada ya kuwasili kwenye Ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Monduli kuanza ziara ya kazi wilayani humo Desemba 4, 2016

  Waziri Mkuu, Kasssim Majaliwa akiwapungia wananchi wa Monduli baada ya kuwasili kwenye Ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Monduli kuanza ziara ya kazi wilayani humo Desemba 4, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
   

  0 0

  Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angelina Mabula akifafanuliwa jambo na mmoja wa viongozi wa Kitongoji cha Ilimba wilayani Kalombo mkoani Rukwa kuhusu mgogoro wa ardhi uliopo kati ya wananchi Zaidi ya 200 na mwekezaji wakati alipozuru shamba hilo.
  Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angelina Mabula akipokea zawadi kutoka kwa wananchi waKitongoji cha Ilimba wilayani Kalombo mkoani Rukwa mara baada ya kukaribishwa kwa burudani ya ngoma za asili za kabila la wafipa.

  Sehemu ya wakazi wa Kitongoji cha Ilimba katika Wilaya ya Kalambo wakicheza ngoma ya asili ya kabila la wafipa kama ishara ya furaha kwa kutembelewa na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angelina Mabula aliyekuwa ziarani mkoani Rukwa kutembelea utendaji wa sekta ya ardhi.
  Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angelina Mabula akizungumza na wananchi wa Kitongoji cha Ilimba katika Wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa (hawapo pichani) mara baada ya kusikiliza kero zao kuhusu sekta ya ardhi.

  Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angelina Mabula akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi (hawapo pichani) wakati alipowasili wilayani humo kufuatilia utendaji kazi na utoaji huduma wa sekta ya ardhi kwa wananchi. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Bw. Said Mtanda.
  Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Bw. Said Mtanda akitoa ufanunuzi kwa wananchi mbele ya Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angelina Mabula kuhusu masuala mbalimbali ya ardhi yanayotakiwa kufuatwa na wananchi pindi wanapofuatilia huduma za ardhi.
  Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angelina Mabula akizungumza na wananchi wa Kitongoji cha Ilimba katika Wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa (hawapo pichani) mara baada ya kusikiliza kero zao kuhusu sekta ya ardhi.
  Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angelina Mabula akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukagua mradi wa ujenzi wa nyumba za makazi zilizojengwa katika eneo la Sumbawanga Mjini mkoani Rukwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC). Kulia kwake ni Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Bw. Said Mtanda.
  Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo wakimlaki Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angelina Mabula wakati alipowatembelea kukagua utendaji wa sekta ya ardhi mkoani Rukwa. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya hiyo Bibi Julieth Binyura.

  0 0  Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imejipanga kurekebisha Sera na Sheria za kodi ili kuwasaidia wafanyabiashara na wajasiliamali kupata thamani ya shughuli wanazozifanya.

  Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu ametoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam alipokuwa akizindua Mkutano wa Chama cha Wasindikaji wa Vyakula nchini (TAFOPA) uliofanyika katika ukumbi wa Mwl. Nyerere uliopo Jijini humo.

  Mama Samia amesema kuwa wafanyabiashara na wajasiliamali nchini wamekuwa wakilalamikia ongezeko la kodi katika bidhaa mbalimbali wanazozizalisha hadi kupelekea kushindwa kuona faida ya shughuli hizo hivyo ni muhimu kwa Serikali kusikiliza kilio chao kwa kutafuta namna bora itakayomaliza tatizo hilo.

  “Serikali ya Awamu ya Tano imeliona tatizo hilo na imeahidi kulifanyia kazi kwa kuzipitia upya sheria hizo na kuzifanyia marekebisho ili kila mwananchi atoe kodi bila kinyongo na apate faida ya shughuli anayoifanya,”alisema Mama Samia.

  Amezitaja changamoto zingine ambazo Serikali itazifanyia kazi ni kujenga miundombinu katika maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya wajasiliamali, kupunguza muda wa upatikanaji wa leseni za biashara pamoja na kuhakikisha Mamlaka ya Serikali za Mitaa inatenga maeneo kwa ajili ya wajasiliamali hao.

  Kwa upande wake Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage amesema kuwa jambo analojivunia katika uongozi wake ni kuweza kuwahamasisha Watanzania kuelewa ujenzi wa uchumi wa viwanda ambapo kwa sasa nchi nzima wanazungumzia habari hiyo.

  “Asilimia kubwa ya wananchi wanazungumzia namna ya kuanzisha viwanda kama sehemu ya kujipatia kipato na ndio maana mikutano ya wajasiliamali imekua ikiongezeka siku hadi siku, hii inaonyesha dhahiri kuwa watanzania wameamua kushirikiana na Serikali katika kuinua uchumi wa nchi kupitia viwanda,”alisema Mwijage.

  Naye Mwenyekiti wa Chama cha TAFOPA, Susan Laizer amefafanua kuwa maeneo yatakapotengwa yatasaidia kupunguza uharibifu wa mazao ya chakula yanayovunwa wakati wa msimu husika pia yatatoa ajira nyingi kwa wananchi watakaokuwa wakifanya shughuli za uzalishaji katika maeneo hayo.

  “Tunaiomba Serikali yetu itusaidie kutenga maeneo kwa ajili ya shughuli zetu hadi kwenye sehemu za vijiji ili wakulima wapate soko la bidhaa zao kwa urahisi pamoja na kuepuka madalali wanaozorotesha vipato vyao,”alisema Bi. Susan.

  Aidha, Bi Susan amempongeza Mama Samia kwa kuteuliwa na Umoja wa Mataifa kuwa mjumbe wa nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika kwenye jopo la kuwawezesha wanawake kiuchumi kwani ni sifa kwa Taifa na fursa kwa wasindikaji wote nchini.

  Chama hicho kimeanzishwa rasmi mwaka 1977 baada ya wanawake kupata mafunzo ya usindikaji wa vyakula yaliyotolewa na Shirika la Maendeleo ya Viwanda Vidogo Tanzania (SIDO) ikishirikiana na Shirika la Maendeleo ya Viwanda Vidogo Duniani (UNIDO).

  0 0

  Na Ismail Ngayonga-MAELEZO
  Dar es Salaam
  MKUU wa Mkoa wa Simiyu, Antony Mtaka amewata Viongozi wa Dini na Watanzania kuendelea kumuombea Rais John Pombe Magufuli katika jitihada zake za kurejesha misingi ya maadili, nidhamu na uwajibikaji katika utumishi wa umma iliyoachwa na Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
  Anasema katika kipindi cha mwaka mmoja wa Utawala wa Rais John Pombe Magufuli, Serikali ya Awamu ya tano imejipambanua kwa vitendo katika kupiga vita rushwa, ufisadi na kusimamia nidhamu na miiko ya Uongozi katika utumishi wa Umma.
  Hayo yameelezwa leo Jijini Dar es Salaam na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Antony Mtaka wakati wa mahojiano maalum na mwandishi wa habari hizi kuelekea katika maadhimisho ya miaka 55 ya uhuru wa Tanzania Bara.
  “Ndani ya Rais Magufuli anaonekana, Mwalimu Nyerere ambaye alikuwa mstari wa mbele katika kukemea hadharani vitendo vya uvunjifu wa maadili ya mtumishi wa umma ikiwemo rushwa na ufisadi” anasema Mtaka.
  Kwa mujibu wa Mtaka anasema hatua zinazoendelea kuchuliwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika kurejesha nidhamu katika utumishi wa umma ikiwemo mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi ni jambo la kupongezwa, kwa kuwa limelenga katika kuwakumbusha watendaji kuwa Uongozi ni dhamana.
  Alisema kuwa hatua zinazochuliwa na Rais John Pombe Magufuli, zinaendelea kuongeza heshima ya Viongozi wa Tanzania katika medani ya kimataifa ya kusimamia nidhamu, maadili na miiko ya Uongozi ambayo imetekelezwa katika kipindi chote cha miaka 55 ya uhuru.
  Anaongeza kuwa, hatua hizo zilizofikiwa na Viongozi hao ni changamoto kwa Viongozi Vijana waliopo nchini kuendelea kuheshimu misingi iliyoachwa na waasisi wa taifa, na hivyo kuiwezesha Tanzania kuendelea kupiga hatua kubwa za maendeleo katika siku za usoni.
  Mtaka alisema Kiongozi wa Umma ni kioo na kiunganishi katika jamii anayoiongoza, hivyo ni wajibu wa kila kiongozi wa umma kujenga taswira chanya ya kiutawala katika kuwahudumia wananchi kwa kutambua kuwa dhamana ya kiongozi ndio tumaini la watawaliwa.
  “Katika siku za hivi karibuni tumeshudia sekta binafsi zikichukua watumishi waaandamizi kutoka Serikalini, hiki ni kiashiria kuwa nidhamu na maadili ya kazi yameimarika kwa kiasi kikubwa sana Serikalini” alisema Mtaka.
  Akifafanua zaidi Mtaka alisema katika kipindi cha mwaka mmoja wa Serikali ya Awamu ya Awamu ya tano pamekuwepo na mageuzi makubwa katika utendaji na uwazi wa shughuli mbalimbali za Serikali, hatua iliyosaidia kuokoa kiasi kikubwa cha fedha kilichokuwa kikipotea katika miaka ya nyuma.

  0 0

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemwagiza Mganga Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Dk. Frida Mokiti  kubadilisha uongozi wa  Kituo cha afya cha Levolosi baada ya kulalamikiwa na wananchi kuwa kinatoa huduma mbovu kwa wagonjwa hususan ni kwa wajawazito. 

  Pia amewataka wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini kujenga hospitali za wilaya ili kupunguza msongamano wa wagonjwa kwenye hospitali za rufaa.Waziri Mkuu ametoa maagizo hayo leo (Jumapili, Desemba 4, 2016)  wakati alipotembelea  Hospitali ya mkoa ya Mount  Meru, ambapo alisema tatizo la msongamano wa wagonjwa hospitali za rufaa na hospitali nyingine ni lazima lipatiwe ufunguzi.

  "Hatuhitaji kuwa na madaktari ambao wanasumbua wagonjwa. Daktari wa Mkoa hakikisha kile kinacholalamikiwa kule Levolosi kinatafutiwa ufumbuzi. Hapa Mount Meru hakikisheni mnaboresha mazingira ya vyoo kwenye wadi  za wazazi pamoja na kujenga sehemu ya kuoshea vyombo kwa wagonjwa, " alisema.

  Awali alipotembelea wodi ya kinamama wanaosubiri kujifungua, mmoja wa wagonjwa, Glory Paul Mkazi wa Olasiti alimweleza Waziri Mkuu kuwa mtoto wake alifia tumboni baada ya wauguzi na  madaktari wa kituo cha Afya cha Levolosi  kuchelewa kumpatia matibabu.

  "Wakati nahudhuria kliniki nishaambiwa na daktari kuwa natakiwa kujifungua kwa njia ya upasuaji na siwezi kujifungua kwa njia ya kawaida nilimwambia nesi kuwa  natakiwa kufanyiwa upasuaji wakanikatalia na kunilazimisha nijifungue kwa njia ya kawaida ambapo ilishindikana na baada ya muda waliniambia kuwa mtoto amekufa na wananifanyia upasuaji ili kuokoa maisha yangu," amesema.
  .
  Kwa upande wake Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, Athumani Kihamia alisema amepokea maagizo ya Waziri Mkuu, ambayo yanalenga kuboresha utoaji wa huduma bora kwa wananchi na kusisitiza kuwa awali alichukua hatua za kinidhamu kwa watoa huduma za afya kituoni hapo na ataendelea kusimamia nidhamu ya kazi ili kuondoa malalamiko kwa wananchi juu ya huduma za afya.
                                                             


  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU
  JUMAPILI, DESEMBA 4, 2016.

  0 0

   Naibu Mkurugenzi wa Idara ya Fedha (TRA) Bi. Anna Mndeme kulia akipokea tuzo ya utunzaji bora wa mahesabu kwa taasisi za umma  kutoka kwa Mwakilishi wa Mhasibu Mkuu wa Serikali  Bw .Shogolo Msangi katikati  wakati wa sherehe za kukabidhi tuzo hizo kwa  wawasilishaji bora wa mapato kwa mwaka 2015 yaliyofanyika nje kidogo ya jiji la Dar es salaam wa kwana kushoto ni Mwenyekiti wa NBAA Prof. Isaya Jairo.
   Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) Dkt.Ayoub Rioba kulia akipokea tuzo ya utunzaji bora wa mahesabu kwa taasisi za umma baada kuwa mshindi wa pili  kutoka kwa kwa Mwakilishi wa Mhasibu Mkuu wa Serikali  Bw .Shogolo Msangi kushoto  wakati wa sherehe za kukabidhi tuzo hizo kwa  wawasilishaji bora wa mapato kwa mwaka 2015 yaliyofanyika nje kidogo ya jiji la Dar es salaam.
   Afisa Mkuu wa Mapato kutoka kampuni ya kutengeneza sementi (Tanga Cement Plc) Bw. Pieter De Jager wa pili kulia akiwa ameshika tuzo ya washindi wa jumla kwenye masindano ya wawasilishaji bora wa mapato kwa mwaka 2015 yaliyofanyika nje kidogo ya jiji la Dar es salaam.

   Mwakilishi wa Mhasibu Mkuu wa Serikali  Bw .Shogolo Msangi katikati waliokaa  akiwa katika picha ya pamoja na washindi wa uwasilishaji bora wa mapato  wakati wa sherehe za kukabidhi tuzo hizo kwa mwaka 2015 iliyofanyika nje kidogo ya jiji la Dar es salaam.Picha Na Ally Daud-Maelezo

  Na Ally Daud-MAELEZO
  MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imeshinda tuzo ya utunzaji bora wa mahesabu kwa taasisi za umma  zilizoandaliwa na   Bodi ya Ukaguzi na Wahasibu (NBAA) kwa mwaka 2015. 

  Akipokea tuzo hiyo Naibu Mkurugenzi wa Idara ya Fedha (TRA) Bi. Anna Mndeme amesema kuwa wamepata tuzo hiyo kutokana na  kuwasilisha vizuri mahesabu ya mwaka wa fedha yaliyowasilishwa kufuatana na viwango vya uwasilishwaji  vinavyozingatiwa na Bodi ya Ukaguzi na Wahasibu (NBAA).

  “Tumefanya vizuri na tumepata tuzo kwa kushika nafasi ya kwanza kutokana na  kuwasilisha vizuri mahesabu ya mwaka wa fedha yaliyowasilishwa kufuatana na viwango vya uwasilishwaji  vinavyozingatiwa na Bodi ya Ukaguzi na Wahasibu (NBAA)” alisema Bi. Mndeme.

  Aidha Bi. Mndeme amesema kuwa tuzo hiyo ni chachu kwa TRA itayofanya waendelee kujituma zaidi katika ukusanyaji na utunzaji wa mapato ili kusaidia nchi kupata huduma bora za jamii kwa maendeleo ya taifa.

  Kwa upande wake Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi TRA Bw. Richard Kayombo amesema kuwa huo ni uthibitisho kwamba TRA inafanya kazi  kwa ueledi na uwazi kupelekea kupata tuzo ya heshima.
  Katika mashindano hayo Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) wameibuka washindi wa pili huku kampuni inayotengeneza Sementi  (Tanga Cement Plc) wakiibuka kuwa washindi wa jumla kwenye tuzo hizo .


  0 0

   Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Ardhi, Prof. Idrissa Mshoro akiwasili katika viwanja vya chuo hicho kwa ajili ya kuhudhuria katika mahafali ya 10 ya chuo hicho yaliyofanyika jana Jijini Dar es Salaam.
  tanga-1
  Mkuu wa Chuo Kikuu Ardhi, Mhe. Cleopa Msuya akimtunuku mmoja wa wanafunzi wa shahada ya Udaktari wa Falsafa (PhD) aliyoipata katika chuo hicho. Mahafali hayo yamefanyika jana Jijini Dar es Salaam katika viwanja vya chuo hicho.
  tanga-2
  Mkuu wa Chuo Kikuu Ardhi, Mhe. Cleopa Msuya (kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wengine waliohudhuria kwenye mahafali ya 10 ya chuo hicho akiwemo Kaimu Mwenyekiti wa Baraza la chuo hicho, Prof, Evelyne Ambede (wa pili kushoto), wa tatu kulia ni Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhandisi Stella Manyanya. Mahafali hayo yamefanyika jana Jijini Dar es Salaam katika viwanja vya chuo hicho.
  tanga-3Baadhi ya wanafunzi wa shahada na stashahada waliohitimu katika chuo hicho wakiwa katika viwanja vya chuo. Mahafali hayo yamefanyika jana jijini Dar es Salaam.
  …………………..
             Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO.
  Chuo Kikuu Ardhi kimekamilisha ujenzi na uwekaji wa vifaa katika Bandari ya Tanga ikiwa ni moja ya miradi ya kiutafiti inayofanywa chuoni hapo kwa ajili ya kupima hali halisi ya bahari.
  Makamu wa Mkuu wa Chuo hicho, Prof. Idrissa Mshoro ameyasema hayo alipokuwa akisoma hotuba wakati wa mahafali ya 10 ya chuo hicho yaliyofanyika jana chuoni hapo jijini Dar es Salaam.
  Prof. Mshoro amesema kuwa pamoja na jukumu la kutoa wahitimu katika fani mbalimbali kwa maendeleo ya nchi pia chuo hicho kina majukumu ya kufanya utafiti na kutoa ushauri wa kitaalam hivyo kupitia Mradi wa Utafiti wa Mabadiliko ya Tabia Nchi uliofadhiliwa na Serikali ya Norway kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania umeweza kufanikisha ujenzi huo.
  “Madhumuni ya Mradi huu ni kusaidia kuboresha mawasiliano kati ya Bandari na watumiaji wake kwani taarifa sahihi zitakazotolewa kuhusu hali halisi ya bahari zitasaidia kufanya maamuzi sahihi ya kutumia Bandari hiyo pia, taarifa hizo zitakuwa msaada mkubwa kwa wadau wengine kama wavuvi, watalii pamoja na watafiti mbalimbali,” alisema Prof. Mshoro.
  Ameongeza kuwa katika kutoa ushauri na huduma za kitaalam, chuo kimetekeleza miradi mbalimbali ya Serikali, taasisi za Umma na Binafsi katika fani zote zinazofundishwa chuoni hapo hivyo kusaidia katika kuongeza kipato cha chuo kwa ajili ya miradi, kutoa motisha kwa wafanyakazi pamoja na kutoa fursa kwa wana taaluma kupata uzoefu kwa vitendo katika fani mbalimbali walizosomea.
  Aidha, Prof. Mshoro ameishukuru Serikali ya Awamu ya Tano kwa kuendelea kukipatia chuo fedha na misaada mingine kwa ajili ya kuendeshea shughuli za chuo ambapo kwa mwaka wa fedha 2016/2017 Serikali imetengea jumla ya shilingi bilioni 5 kwa ajili ya bajeti ya maendeleo ya chuo hicho.
  Akiongelea kuhusu wahitimu, Prof.  Mshoro amefafanua kuwa jumla ya wanafunzi 968 watatunukiwa shahada na stashahada mbalimbali ambapo wanafunzi 868 watatunukiwa shahada za awali, 80 shahada za uzamili, 14 watatunukiwa stashahada pamoja na shahada za uzamivu kwa wanafunzi 6.
  Kwa upande wake Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhandisi Stella Manyanya amesema kuwa bado kuna changamoto kubwa kwa wasichana kujiunga na masomo ya sayansi kwani idadi imeonyesha kuwa wahitimu wa kike ni 320 ambayo ni sawa na asilimia 33 ya wanafunzi wote hivyo ametoa rai kwa wasichana kutumia fursa za kusomea masomo hayo bila kuogopa.
  Mhandisi Manyanya amewashauri vijana kujikita kusoma masomo yatakayowapelekea kujiajiri wenyewe kuliko yale yanayohitaji kuajiriwa kwani njia hiyo itasaidia kujikwamua kiuchumi kwa haraka na kuchangia katika maendeleo ya taifa.

  0 0

   Mchezaji wa Mbao U-20,  Ismail Mrisho Halfan akifanyiwa huduma ya kwanza ndani ya uwanja mara baada ya kuanguka kwa mara ya pili.

  Mshambuliaji wa timu ya vijana ya Mbao Fc U20  Ismail Mrisho Khalfan anayevalia jezi nambari 4 amefariki  Dunia jioni hii baada ya kuanguka Uwanjani Kaitaba wakati wa Mtanange wao dhidi ya timu ya vijana wa Mwadui ikiwa ni mechi ya mwisho ya kumaliza duru la kwanza la ligi ya Vijana.

  Ismail Khalfan  amefariki baada ya kufikishwa Hospitali ya Government ya mjini Bukoba.

  Ismail Khalfan kabla ya kufikiwa na umauti aliweza kuifungia timu yake bao la kwanza na bao la pili lilifungwa kwa mkwaju wa Penati hivyo mtanange kumalizika kwa 2-0.

  Kabla ya kuanguka Ismail aligongana na beki wa Mwadui Fc  na baadae akiwa peke yake alianguka chini lakini akainuka halafu akaanguka tena na kutokana na ukosefu wa huduma ya kwanza na gari la wagonjwa Katika Uwanja wa Kaitaba kulipelekea marehemu kupandishwa kwenye gari la zima moto na kupelekwa hospital ambapo mauti yalimkuta.


  Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi. 
  Mchezaji  Ismail Mrisho Halfan wa timu ya Mbao U-20 akitolewa uwanjani na watu wa msalaba Mwekundu baada ya kuanguka uwanjani wakati wa mchezo wao  uliokuwa ukichezwa katika uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba
   Mchezajiwa Mbao U- 20,  Ismail Mrisho Halfan akipandishwa kwenye gari la Zimamoto baada ya kutokuwepo gari la kubebea wagonjwa kwenye uwanja Kaitaba mjini Bukoba
   Gari la zimamoto klikiondoka uwanjani Kaitaba ikiwa imebeba mchezaji Ismail kuelekea hospitali ya Mkoa wa Kagera. (Picha na Faustine Ruta)
  ⁠⁠⁠⁠

  0 0

   Jeneza lililokuwa na mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Kundi la Yanga Asili, marehemu Yusuf Mzimba nyumbani kwa mtoto wake Magomeni jijini Dar es Salaam, kabla ya kusafirishwa kwa mazishi katika kijiji cha Msoga, Chalinze mkoani Pwani. (Picha na Francis Dande).
   Mchezaji wa zamani wa timu ya Yanga na  Taifa Stars,  Abeid Mziba (kushoto), akimfariji Ramadhan Yusuf 'Kampira' ambaye ni mtoto wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Kundi la Yanga Asili, marehemu Yusuf  Mzimba jijini Dar es Salaam jana, kabla ya mwili wake kusafirishwa kwa mazishi Msoga, Chalinze Mkoa wa Pwani. 

  Mzee Ibrahim Akilimali (kushoto), akifurahia jambo na wazee wenzake katika msiba wa mzee Yusuf Mzimba. Katikati ni Said Motisha.
   Kisomo kikisomwa.
   Mzee Ibrahim Akilimali akisoma wasifu wa marehemu Yusuf Mzimba.
   Wakiombea Dua mwili wa marehemu.
   Safari ya kuelekea Msoga ikianza.


  NA FRANCIS DANDE
  MAMIA ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam, jana walijitokeza kwa wingi kuaga mwili aliyekuwa Mwenyekiti wa Kundi la Yanga Asili, marehemu Yusuf Mzimba, uliosafirishwa kutoka nyumbani kwa mtoto wake, Ramadhan Yusuf ‘Kampira’, Magomeni jijini Dar es Salaam leo.

  Marehemu alifariki juzi na amezikwa jana katika makaburi ya familia yaliyopo kijijini kwake, Msoga, Chalinze, mkoani Pwani.

  Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, mtoto wa marehemu mzee Mzimba, Kampira alisema kuwa baba yake  alikuwa anasumbuliwa na maradhi kwa muda mrefu na kwamba ameacha watoto sita.

  Kampira aliongeza kuwa, Rais mstaafu wa awamu ya nne Jakaya Kikwete ataongoza waombolezaji katika maziko hayo, yatakayofanyika katika makaburi ya familia yaliyopo kijijini Msoga.

  Akisoma wasifu wa marehemu, Mzee Ibrahim Akilimani alisema kwamba marehemu alikuwa mwanachama wa siku nyingi wa Yanga na amewahi kushika nyadhifa mbalimbali katika klabu ya Yanga ikiwemo nafasi ya umeneja.

  Alibainisha ya kuwa, Mzee Mzimba aliwahi pia kuwa Katibu Mwenezi wa Yanga na mtu ambaye alikuwa na misimamo katika kuipenda Yanga na hakubadilika katika kuitetea klabu yake ya Yanga. 

  Pia alitoa mchango mkubwa ndani ya Yanga na hasa ulipotokea mgawanyiko mkubwa uliodumu kwa miaka 7 na kuibuka makundi ya Yanga Asili na Yanga Kampuni. 

  Mzee Akilimali aliongeza kwamba, licha ya kuibuka kwa migogolo ndani ya klabu hiyo, lakini Mzee Mzimba alibaki na msimamo wake mpaka leo na kuwa Yanga kitu kimoja.

  “Mtu kama Yusuf Mzimba alivyokuwa maarufu kwa Yanga leo hebu nitazamieni hao viongozi wa Yanga wako wapi, tumeondokewa na wapenzi wa Yanga kama Ismail Idrissa, Bilal Hemed Chakupewa hakuonekana hata kiongozi hata mmoja, naamini hata Ibrahim Akilimali akifa, hatoonekana kiongozi yeyote wa Yanga,” alisema.

  Mzee akilimali alisema kuwa Yanga ilianzishwa na wazee mwaka 1935 ikiwa na lengo la kujuana, kuzikana, kusaidiana kufurahi pamoja, lakini leo imekuwa hawajuani.
  Aidha amewasihi wana Yanga kutopoteza adhima ya kuanzishwa kwa klabu hiyo.

  Naye mchezaji wa zamani wa Taifa Stars na Yanga, Abeid Mziba alisema kuwa: “Katika miaka ya 80 wakati najiunga na Yanga, Mzee Mzimba ni miongoni mwa wazee walionipokea, kwa kweli tumepoteza nguzo muhimu sana ndani ya Yanga na katika familia ya mpira kwa ujumla.”

  Naye Mzee wa Yanga, Hashim Mhika alisema kuwa alimfahamu siku nyingi mzee Mzimba kutokana na misimamo yake pia alisema kuwa katika serikali ya Kikoloni, Mzee Mzimba aliwahi kuwa Mkuu wa Wilaya (DC), lakini, ameshangazwa kuona hata viongozi wa serikali hawakuonekana katika msiba huo.

  0 0

  Mwandishi wa habari na mchambuzi wa masuala ya siasa nchini Tanzania Ndg Mathias Canal mwenye shuka la kimasai shingoni akiwaelekeza watoto wa mitaani Jijini Mwanza kula kwa ufasaha pasina vurugu kama walivyozoea
   Binti Leah Mathias mtoto wa Mwandishi Mathias akiwa ameshiriki katika hafla hiyo
  Mke wa Mwandishi Mathias Canal Bi Zakati Chagamba akifurahi na Mwanae Leah Mathias wakati wa hafla hiyo, Pembeni ni Teddy Fransis Mpwa wa Mathias Canal
   Maelekezo ni muhimu ili kuwa na nidhamu katika kula
   Watoto wakifurahia chakula cha jioni pasina vurugu na kadhia yoyote
   Mlo unaendelea mpaka kushiba atakaye na aje
  Moja wa binti aliyetelekezwa akiwa na watoto wake kushiriki mlo wa chakula cha jioni ulioandaliwa na Mwandishi Mathias Canal
   Picha ya pamoja mara baada ya kushiriki Hafla ya chakula cha jioni

  Wengine ni wakubwa kabisa lakini wapo mitaani walikuwa watoto wadogo na sasa wamekua watu wazima

  Na Mwandishi Wetu, Mwanza

  Mwandishi wa habari na mchambuzi wa masuala ya siasa nchini Tanzania Ndg Mathias Canal tarehe nne ya kila Mwezi wa kumi na mbili huadhimisha kumbukizi ya kuzaliwa kwake ambapo hii leo ameadhimisha kumbukizi hiyo kwa kula chakula cha jioni na familia yake sambamba na watoto wa Mitaani (Street Children) wa JIjini Mwanza waliojitokeza kwenye hafla hiyo ya chakula cha jioni.

  Canal ameamua kufanya hivyo kutokana na watoto wa mitaani hujitokeza kwa wingi kuomba msaada wa kupatiwa hela ili wanunue chakula katika eneo maarufu Jijini Mwanza la Salma Cone ndipo mwandishi huyo kwa kushirikiana na Asasi isiyokuwa ya kiserikali ya METDO Tanzania walipoamua kushiriki chakula cha jioni kwa kula na watoto hao.

  Akizungumzia maamuzi hayo ya kukacha kwenda Beach ama maeneo ya kuvinjari kama ambavyo waadhimishaji wengine hufanya Mathias Canal alisema kuwa ni jambo la thawabu sana kwa Mungu na kwenye jamii kwa ujumla kushiriki chakula cha jioni na watotot wa mitaani kwani asilimia kubwa wapo katika mazingira ya kuomba kutokana na hali ngumu za maisha zinazozikabili familia zao, lakini pia wapo watoto wengine ambao walitelekezwa na wazazi wao jambo ambalo limesababisha kuwa katika maeneo yasiyo rasmi na kujihusisha na tabia ovu.

  ”Serikali inapaswa kuwa na mkakati mathubuti wa kuwasaidia watoto hawa kwani kuwaacha waendelee kuwa mitaani ni njia mojawapo ya kuzalisha Wezi na Majambazi, Malaya na Mashoga hii ni kutokana na vitendo ovu wanavyofanyiana wenyewe kwa wenyewe watoto hawa au kufanyiwa na watu wengine kwa kubakwa na kulawitiwa” Alisema Canal

  Serikali kupitia wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto inapaswa kulitaza jambo hili kwa umakini  kwani Tanzania inaendelea kuwa na watoto wengi wa mitaani hususani katika majiji na maeneo ya mikoa mbalimbali ili kunusuru Taifa lenye vijana wengi wa badae wasiokuwa na elimu na hatari kwa wananchi wengine kuna kila sababu ya kuweka mikakati ya kukabiliana na kadhia hiyo.

  Kuna taarifa kuwa idadi ya watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi nchini imezidi kuongezeka kwa kasi ya kutisha. Hii inatokana na idadi hiyo kufikia watoto 897,913, ambao wote wamekuwa wakikabiliwa na hali ngumu ya maisha inayoambatana na vitendo vya ukatili kila uchao.
  Kwa mujibu wa Takwimu zilizotolewa mwanzoni mwa mwaka jana zinazoonyesha kuwa watoto milioni 2.5 wamekuwa yatima baada ya wazazi wao kufariki dunia kutokana na ugonjwa wa Ukimwi na wakati huohuo, watoto wa kike watatu kati ya 10 wamebainika kufanyiwa ukatili wa kingono kabla ya kufikisha miaka 18.

  Hakika, idadi hii ya watoto wanaoishi katika mazingira magumu inatisha. Sisi tunaona kwamba sasa kuna kila sababu kwa serikali na jamii nzima kutafuta namna bora ya kuwasaidia watoto hawa kwani vinginevyo, athari zake zinaweza kuwa kubwa kwa taifa kuliko inavyoweza kudhaniwa.

  "Maisha ya mjini ni magumu sana. Mtu kulala nje, kwenye baridi na mara nyingine unanyeshewa mvua. Kuna wakati unaweza kuamka asubuhi na kukuta mwenzenu amekufa," Anasema mmoja ya watoto hao, msichana mwenye umri wa miaka 16, anasema wengine huishia kuuza miili yao ili kupata fedha za kununua chakula kabla ya kuanza kutafakari namna ya mahala pa kulala na usalama wao kimwili na kiakili.

  Naye Mkurugenzi wa Asasi isiyokuwa ya kiserikali yenye usajiri No. ooNGO/08317 inayojishughulisha na kutoa Elimu ya Mazingira kwa wananchi wanaozunguka migodi pamoja na wafanyakazi wa migodini Bw Ashraf Omary  amekiri kuwa  athari za kuwapo kwa watoto wanaoshi katika mazingira hatarishi ni kubwa kwa taifa na hivyo, wakati jitihada za kukabiliana na visababishi vya kuwapo kwa watoto hao zikiendelea kufanywa, upo ulazima pia wa kuhakikisha kwamba watoto hawa waliopo mitaani wanapatiwa upendo na huduma zote kama ilivyo watoto wengine.

  ”Ikumbukwe kuwa, ikiwa watoto wa mitaani wataendelea kuachwa wajitafutie wenyewe maisha yao, ni dhahiri kwamba nao hawatakuwa na upendo kwa jamii inayowazunguka pindi watakapokuwa watu wazima na hatimaye kuishia kuwa wakabaji pasina kuwa na huruma maana hawakupata upendo na huruma kwa jamii wangali wadogo” Alisisitiza Ashraf Omary

  Akizungumza na watoto hao mara baada ya kumaliza kula chakula cha jioni Mathias Canal alisema kuwa Katika kukabiliana na swala hili ni muhimu serikali kukabiliana na changamoto ya umasikini uliokithiri nchini Tanzania ndio njia pekee ya kunususru Taifa kuwa na tegemezi wengi tena wenye chuki na hasira na jamii yao kwa kukosekana upendo wa dhati.

  MWISHO

  0 0


  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Arusha Bw. Mrisho Gambo kufanya uchunguzi na kumpelekea taarifa ya watendaji waliohusika katika ubadhirifu wa fedha za ujenzi wa mradi wa hospitali ya wilaya ya Monduli uliogharimu sh. bilioni 2.7.


  Ametoa agizo hilo leo (Jumapili, Desemba 4, 2016) wakati akizindua hospitali ya wilaya ya Monduli ambayo katika ujenzi wake kulitakiwa kuwe na jengo la maabara ambalo halipo na fedha zimeisha.


  "Mkuu wa Mkoa shirikiana na Sekretarieti yako kufanya uchunguzi na atakayebainika kuhusika kwenye ubadhirifu huu achukuliwe hatua za kisheria kwa sababu ujenzi huu ulihusisha na jengo la maabara lakini tayari mradi umekamilika na hakuna jengo la maabara," amesema.


  Naye Mkuu wa mkoa huo Bw. Gambo amesema tayari wameanza kufanya uchunguzi wa ujenzi wa mradi huo baada ya kubaini kuwa umetumia kiasi cha fedha kilichotumika hakilingani na thamani ya mradi huo.


  Mkuu huyo wa Mkoa ameahidi kufuatilia suala hilo na uchunguzi utakapokamilika taarifa hiyo itapelekwa kwa Waziri Mkuu.


  Awali, Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo, Zaveri Benela akisoma taarifa ya hospitali hiyo inakabiliwa na changamoto ya jengo la upasuaji karibu na wodi ya wazazi hali inayowalazimu kuwasafirisha wagonjwa umbali wa zaidi ya mita 300 hadi kwenye jengo la upasuaji lililopo katika majengo ya zamani.


  Pia kukosekana kwa jengo la wagonjwa wa nje na jengo la maabara kwenye majengo hayo mapya hali inayochangia huduma kutolewa kwenye maeneo miwili tofauti kwa wakati mmoja yaani katika wodi mpya na majengo ya zamani na hali hivyo inaleta usumbufu kwa wagonjwa.

  Katika hatua nyingine Waziri Mkuu  ametoa siku saba kwa Mkuu wa Wilaya ya Monduli, Bw. Idd Kimanta kumaliza tatizo la  mgogoro wa ardhi katika kijiji cha Emairete kilichopo Monduli juu mkoni hapa  baada ya kudumu kwa miaka 20.


  Mgogoro huo ni wa shamba kubwa ambalo awali lilikuwa linamilikiwa na kampuni ya bia ya Breweries na kisha  kurejeshwa kwa kijiji hicho ambapo viongozi wa viongozi wa zamani wa  Kijiji hicho walijimilikisha kinyemela.


  Waziri Mkuu alitoa agizo hilo baada ya kusimamishwa na wanakijiji hao waliokuwa  wamebeba mabango ya kumuomba  msaada wa kutatuliwa kwa mgogoro huo wakati anatoka kudhuru kaburi la Waziri Mkuu wa zamani Hayati Moringe  Sokoine.


  Waziri Mkuu alimtaka mkuu huyo wa wilaya kueleza sababu za kwa ya nini uongozi wa wilaya umeshindwa kutekeleza maagizo yaliyotolewa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,  William Lukuvi ambaye alifika kijijini hapo na kutoa maelekezo.


  Baada ya maelekezo hayo Waziri Mkuu aliwataka wananchi hao kuendelea kuwa na imani ya Serikali ya awamu ya tano  inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dk. John Magufuli ambayo ipo kwa ajili ya kuwasaidia wananchi hasa wanyonge.


  Kwa upande wake Mkuu wa wilaya hiyo amekiri kuwepo kwa mgogoro huo kwa miaka 20 na kwamba Waziri Lukuvi alitoa maelekezo ambayo halmshauri inayafanyia kazi na imeshindwa kuleta majibu kwa wananchi hao kutokana na ziara ya Waziri Mkuu ambaye aliwataka watekeleze majukumu yao na wasitumie ziara yake kama kisingizio.


  Katika hatua nyingine Waziri Mkuu amesema Serikali na Watanzania wote wanatambua  na kuiheshimu kazi nzuri iliyofanywa na hayati Sokoine kwa Taifa kipindi cha uhai wake na itaendelea kuienzi. Pia  Serikali itaendelea kushirikiana na familia katika mambo mbalimbali.


  IMETOLEWA NA:

  OFISI YA WAZIRI MKUU

  JUMAPILI, DESEMBA 4, 2016.

  0 0


   Mkurugenzi wa Fedha wa Mfuko wa LAPF, John Kida (katikati mwenye tuzo), akiwa na wafanyakazi wenzake baada ya kutunukiwa tuzo ya Utunzaji Bora wa Mahesabu Dar es Salaam juzi. Kushoto ni Meneja Masoko na Mawasiliano wa LAPF, James Mlowe.
   Mgeni rasmi katika hafla hiyo akisoma hutuba kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA), Profesa Isaya Jairo na katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa NBAA, Pius Maneno.
   Mkurugenzi Mkuu wa NBAA, Pius Maneno (kushoto), akimpongeza Mkurugenzi wa Fedha wa Mfuko wa LAPF, John Kida baada ya kukabidhiwa tuzo hiyo. Katikati ni Mwenyekiti wa Bodi NBAA. Profesa Isaya Jairo.
   Wafanyakazi wa Mfuko wa LAPF wakipita meza kuu baada ya kutunukiwa tuzo hiyo.
  Washindi wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi na viongozi wa NBAA.

  Na Dotto Mwaibale

  MFUKO wa Pensheni wa LAPF, umetunukiwa tuzo ya kuwa kinara katika utunzaji  wa mahesabu dhidi ya mifuko mingine ya hifadhi ya jamii nchini.

  Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam juzi kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa mfuko huo, Elyudi Sanga baada ya kupokea tuzo hiyo, Mkurugenzi wa Fedha wa mfuko huo, John Kida, alisema kwao ni mafanikio makubwa kwa kupata tuzo hiyo.

  "Tunatumia njia za kisasa ya utunzaji wa mahesabu huku tukifunga mahesabu yetu kwa wakati jambo linalotupa fursa ya kuweka sawa mambo yetu ya mahesabu" alisema Kida.Alisema wamekuwa wakifunga mahesabu yao kwa kiwango cha kimataifa ndio maana wamekuwa wakiibuka washindi mara nyingi.

  Kida alisema kuwa ushindi huo ni wa mara ya nane tangu kuanzishwa kwa utoaji wa tuzo hizo mwaka 2008.Meneja Masoko na Mawasiliano wa LAPF, James Mlowe, alisema kuwa wanachama wao wanatakiwa kuendelea kuwa na imani na mfuko wao na kuwa fedha zao zipo kwenye mikono salama.

  Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA), Pius Maneno, alisema makampuni na taasisi 56 zilishiriki katika mashindano hayo kwa  mwaka huu ambapo waligawanywa katika makundi 12 kulingana na huduma wanazozitoa.

  Alisema tuzo hizo zina lengo la kuongeza uwazi na uwajibikaji katika suala zima la mahesabu na kuhakikisha viwanago vya kimataifa vinazingatiwa katika utunzaji wa mahesabu.Aliwataka wahasibu nchini kuandaa taarifa bora za fedha ili kuboresha hesabu za mashirika na makampuni na kuongeza uwazi katika shughuli zao.

  Tuzo hizo ziliandaliwa na Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (NBAA) na zilitolewa juzi katika Kituo cha Taaluma ya Uhasibu (ACP) kilichopo Bunju nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.

older | 1 | .... | 1058 | 1059 | (Page 1060) | 1061 | 1062 | .... | 1898 | newer