Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1056 | 1057 | (Page 1058) | 1059 | 1060 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makala amelishukuru Shirika la Umoja wa Mataifa kwa misaada na ushirikiano kwa serikali ya Tanzania ikiwemo huduma kwa kambi za wakimbizi, Mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana yenye kauli mbiu ya Vijana - Fursa na misaada mingi katika shughuli za maendeleo Hayo ameyasema wakati wa mazungumzo na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez aliyemtembelea Mkuu huyo wa mkoa ofisini kwake. RC Makalla amewahakikishia ushirikiano zaidi kwa mradi wa Vijana kutambua fursa na kuzitumia utakaotekelezwa Mkoa wa Mbeya mwakani. 
  Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla (kushoto) akisalimiana na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez aliyemtembelea ofisini kwake na kufanya mazungumzo ya kuboresha ushirikiano baina ya Serikali na Umoja wa Mataifa jijini Mbeya.(Picha na Zainul Mzige wa Modewjiblog)
  Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akisaini kitabu cha wageni ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla alipomtembelea ofisini kwake na kufanya mazungumzo ya kuimarisha ushirikiano baina ya Serikali na Umoja wa Mataifa jijini Mbeya.
  Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akielezea dhumuni la safari yake mkoani Mbeya kwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla wakati alipomtembelea Mkuu huyo wa mkoa na kufanya naye mazungumzo kwa lengo la kuimarisha ushirikiano baina Umoja wa Mataifa na Serikali.
  Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makala akielezea mipango aliyonayo ya kuinua uchumi wa mkoa wake na kutatua tatizo la ajira kwa vijana ambalo limekua changamoto kubwa nchini kwa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (katikati) aliyemtembelea ofisini kwake akiwa ameambatana na Mtalaam wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa nchini, Hoyce Temu (kushoto).
  Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez akitoa taarifa zilizomo kwenye Ripoti ya Umoja wa Mataifa ya Mpango wa misaada ya Maendeleo UNDAP II 2016-2021 kwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla alipomtembelea ofisini kwake na kufanya naye mazungumzo kwa lengo la kuimarisha ushirikiano baina ya Umoja wa Mataifa na Serikali.
  Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez akimkabidhi rasmi Ripoti ya Umoja wa Mataifa ya Mpango wa misaada ya Maendeleo UNDAP II 2016-2021 Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla alipomtembelea ofisini kwake jijini Mbeya.
  Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makala katika picha ya pamoja na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez aliyeambatana na Mtalaam wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa nchini, Hoyce Temu (kulia) nje ya jengo la ofisi za mkuu huyo wa mkoa.
  Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez na Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Amos Makalla katika picha ya pamoja na "Orange car" ikiwa ni wiki ya maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia: 'Elimu kwa wote" nje ya ofisi za mkuu huyo wa mkoa.
  Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Amos Makala akiagana na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez aliyemtembelea ofisini kwake na kufanya naye mazungumzo jijini Mbeya.

  0 0

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

  TIMU ya JKT Ruvu imefanikiwa kunasa saini ya kocha wa timu ya Vijana Chini ya miaka 17 Serengeti Boys Bakari Shime na kumpatia kandarasi ya miaka miwili ili kuweza kukinoa kikosi hicho cha maafande.

  Shime amechukua nafasi ya Mzanzibar Malale Hamsini aliyekuwa anakinoa kikosi hicho raundi ya kwanza lakini akishindwa kuipatia matokeo timu hiyo.

  Mkurugenzi wa Ufundi wa JKT Ruvu Kocha mwandamizi Abdalla Kibadeni amesema kuwa uamuzi huo umekuja baada ya uongozi wa juu kuona kuwa Kocha Malale Hamsini ameshindwa kuipatia matokeo timu yake na kama raundi ya pili ikiendelea hivyo basi inaweza ikashuka daraja.

  Kibadeni amesema kuwa, kwa sasa Shime amepewa nafasi ya kuangalia wachezaji wa timu ya vijana kuangalia kama anaweza kuwatumia kwani hawana malengo ya kufanya usajili wowote kwa wachezaji kutoka timu zingine.A

  Shime ameweza kufanikiwa kufanya vizuri na timu ya vijana ya Serengeti Boys kwahiyo wana imani naye kuweza kuisaidia timu ya JKT Ruvu katika duru la pili ambapo kwa sasa ipo nafasi ya tatu kutoka Chini.

  0 0

  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Willam Lukuvi akiwa katika ziara ya Utatuzi wa Migogoro ya Ardhi Mkoani Kigoma amerudisha ardhi iliyokuwa ikimilikiwa na Mzee Shaban Hussein mkazi wa Machinjioni Kigoma Mjini, ambaye alinyng’anywa na Raia wa Kongo Bwana Mwenge Muyombi.

  0 0

   picha wa kwanza  kushoto ni meneja  Utalii na masoko wa Tanapa Ibrahimu Musa katikati ni Mkurugenzi wa Tanapa Allen Kijazi  wa kwanza kushoto ni mkurugenzi wa kampuni ya Zara  Zainabu  Ansell wakati wa mkutano wao na waandisi wa habari juu ya   maandalizi ya miaka 55 ya uhuru ambayo yanatarajiwa kufanyika december 9

   Mkurugenzi wa Kampuni ya  Zara Tours Zainabu Anselm  akiongea juu ya kampuni yake ambapo aliwataka wananchi wajitokeze kwa wingi kutembelea vivutio vilivyopo ndani ya nchi yetu na sio kuendelea kuviona kwa mbali tu na kuvisikia


   Mkurugenzi wa mamlaka ya hifadhi za taifa (Tanapa) Allen Kijazi akiongea na waandishi wa habari
  meneja  Utalii na masoko wa Tanapa Ibrahimu Musa katikati ni Mkurugenzi wa Tanapa Allen Kijazi  wa kwanza kushoto ni Afisa uhusiano wa Tanapa Paschal Shelutete

   Habari  Picha na Woinde Shizza,Arusha
  Aliyekuwa mkuu wa majeshi na mwenyekiti wa bodi ya tanapa Jenerali Mstaafu George Waitara anatarajiwa kuongoza  msafara wa zoezi la kupanda mlima kilimanjaro desemba 5 hadi kumi ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 55 ya  uhuru wa tanzania,
  Aidha katika msafara huo wa kupanda mlima kilimanjaro watakuwepo pia wanajeshi kutoka jeshi la wananchi tanzania pamoja na wanahabari ambao watakuwa wanahabarisha jamii kuhusiana na tukio hilo.
  Akizungumza na vyombo vya habari mkurugenzi mkuu wa tanapa allan kijazi alisema kuwa mwaka huu tanzania itaadhimisha miaka 55 ya uhuru na hivyo shrikia hilo imeshirikiana na kampuni ya utalii ya zara pamoja na bodi ya utalii (ttb) kuandaa zoezi la kupanda mlima kilimnajro ili kuweza kuhamasisha  watanzania kuvifahamu vifutio vya utalii.
  Alisema kuwa zoezi hilo la upandaji mlima litahusissha baadhi ya viongozi mashuhuri  wa jeshi awastaafu akiwemo aliyekuwa mkuu wa majeshi ili kuhamasisha watanzania waweze kupanda mlima ambapo tukio hilo litajulikana kama Uhuru Epedition .
  Kijazi alifafanua kuwa pamoja na kuadhimisha uhuru wa nchi ,lakini madhumuni mengine ya zoezi hilo ni kuhamasisha utalii na kuhimiza uhifadhi wa mazingira kwani bado watanzania wengi hawana muamko wa kutembelea vufutio vya utalii hivyo kujikuta asilimia kubwa ya watalii ni kutoka nje ya nchi.
  "Katika maadhimisho haya tuna malengo ya kuhamasisha watanzania ili wajitokoze kupanda mlima kilimanajaro pamoja na kutembela hifadhi mbali mbaki kwani tunavyo vivutio 16 ambavyo vipo ndani ya tanzania na vinahitaji watanzania wote wanufaike navyo sio tu wageni kutoka nje ya nchi bali hata wa hapa wajue wanazo fursa "aliongeza kijazi.
  Kwa upande wake mkurugenzi wa zara Zainabu Ansell alisema kuwa watanzania wanapaswa kujitokeza kwa wingi katika zoezi hilo la kihistoria kwani  wengi wao wamekuwa na mawazo potofu ya kufikiria wanaopaswa kupanda mlima na kutembelea hifadhi ni wazungu tu na wageni kutoka nje ya nchi hali inayowafanya watanzania kupoteza haki yao.Kauli mbiu ya zoezi la kupanda mlima kilimanjaro mwaka huu ni endelea kuweka mazingira safi na salama ya fahari ya afrika.

  0 0

  NEW MUSIC FROM SPICY (GROUP MEMBER OF 2NITE ENTERTAINMENT)  
  Spicy is Mr. Flavour's pianist 
  Enjoy the good music

  0 0

  Na Rhoda Ezekiel Globu ya Jamii-Kigoma.

  WILAYA ya Kakonko Mkoa wa Kigoma imeelezwa kuendelea kuporomoka kiuchumi kutokana na mzunguko mdogo wa fursa za kibiashara kupelekwa wilaya ya jiran na watumishi wa idara  inayohudumia  wakimbizi katika kambi ya mtendeli kuishi Wilayani Kibondo, hali inayo pelekea shughuli zao zote kufanyika Wilayani humo.

  Kufuatia hali hiyo mkuu wa Wilaya Kanali Hosea Ndagala  alitoa  wito kwa watumishi  hao kutoa fursa za kiuchumi kwa wafanya biashara wa Wilaya ya Kakonko wakati wa ujenzi wa nyumba za kudumu za wakimbizi, lengo likiwa ni kuongeza mzunguko  wa kibiashara kwa Wananchi wanao izunguka kambi hiyo na kuacha tabia ya kutoa tenda zote za ujenzi kwa wafanya biashara wa Wilaya ya Kibondo.

  Akizungumza na waandishi wa habari jana Wilayani humo, Ndagala alisema watumishi wengi wa Kambi ya mtendeli wamekuwa wakifanya biashara na wafanya biashara wa Kibondo,wakati kambi hiyo inahudumia wakimbizi katika Wilaya ya Kakonko hali inayo pelekea uchumi wa wananchi wa Kakonko waliotegemea kuupata kupitia kambi hiyo kuanzishwa kukosekana na kuhamia wilya nyingine ya Kibondo.

  Ndagala alisema halmashauri ya Wilaya ya Kakonko ni halmashauri ambayo uchumi wake bado upo chini,unahitaji kuinuliwa hivyo akawaomba wafanyakazi wa kambi ya Mtendeli pamoja na shirika la kuhudumia wakimbizi UNHCR kutoa vipaumbele kwa  Wananchi wa Wilaya ya Kakonko ili kuinua uchumi wa Wilaya hiyo kwa kuwapatia ajira za ujenzi na ununuzi wa vifaa vya ujenzi kwa wafanya biashara wa Kakonko.

  Hata hivyo Mkuu huyo aliwaomba watumishi wote  wa Kambi hiyo na mashirika yanayo hudumka wakimbizi kurudi kuishi Kakonko kwakuwa sababu iliyo kuwa ikiwapelekea waishi Kibondo ya kukosekana kwa Nyumba za kupanga Wilayani humo limekwisha Wananchi wamejitahidi kujenga nyumba zenue ubora ambazo wanaweza kupanga na kufanya kazi zao za kuhudumia wakimbizi wakiwa wilayani humo.

  "Tenda nyingi za ujenzi wa Nyumba za kudumu za Wakimbizi zimekuwa zikitolewa kwa wafanya biashara wa kibondo jambo ambalo sio zuri ukizingatia Wilaya yetu inakambi yenye wakimbizi wengi shughuli zao za Kijamii zinategemea wilaya yetu ni lazima Wananchi wetu na Wilaya kwa ujumla tunufaike na ujio wa wakimbizi sio wilaya yetu inaadhirikana Wilaya nyingine inanufaika",alisema Ndagala

  Aidha mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kakonko ,Juma Maganga  alisema Mpaka sasa Kambi ya Mtendeli ina jumla ya wakimbizi 50,000 ambapo kambi hiyo imejaa na inatarajiwa kuanzishwa kambi nyingine kufuatia hali hiyo Wilaya yetu inawahudumia wote hao na wanategemea huduma nyingine kama vile ukataji wa kuni uchotaji wa maji kutoka kwa Wanakijiji wanao xunguka kambi,endapo fursa za kiuchumi zinapo pelekwa kibondo haileti picha nzuri kwa wanNchi wetu.

  alisema kwa sasa ni fursa mojawapo kwa wilaya  ya kakonko kunufaika na ujio wa wakimbizi  kupitia mradi wa uanzishwaji wa majengo ya kudumu kwa wafanya biashara kupata tenda za kuhudumia vifaa vya ujenzi,vyakula kwa Mafundi na wakimbizi mara watakapo kurejea  nchini kwao baada ya kuridhika uwepo wa amani.

  Pia tungependa watumishi wote warudi Kakonko kambi haiwezi kuwa katika Wilaya yetu na watumishi wanaishi Wilaya nyingine jambo hilo sio zuri linaweza kupelekea uharibifu Mkubwa ukizingatia wakombizi hao baadhi hutoroka nyakati za usiku  na kufanya vitendo vya kiuhalifu kwa Wananchi wanao izunguka kambi.

  Kwa upande wake Mkuu wa kambi ya Mtendeli Inocent Mwaka alisema Suala hilo atalifanyia kazi atazungumza na wahusika iliwaweze kufanya mambo hayo yaliyo pendekezwa na Mkuu wa Wilaya kwa kuwashawishi kuwahamishia watumishi wote wa kambi katika Wilaya ya kakonko na kutoa fursa kwa Wananchi wa Kakonko kunufaika na ujio wa wakimbizi hao.

  0 0
  Mkuu wa wilaya ya Njombe Ruth Msafuri akizungumza na wananchi wa Mjini Njombe katika mkutano wake wa Hadhara


  Baadhi ya wakazi mjini njombe wakisikiliza mkutano wa mkuu wa wilaya ambapo walipata nafasi ya kutoa maoni yao

  WANANCHI halmashauri ya Mji wa Njombe wamemuomba mkuu wa wilaya hiyo Ruth Msafiri kuiamuru halmashauri hiyo kuwagawia wananchi viwanja vilivyopimwa ambapo katika halmashauri hiyo tangu mwaka 2012 hakujapimwa tena viwanja.

  Wananchi wanatoa kero zao wakati wa mkutano wa kwanza wa mkuu wa wilaya na wananchi ambapo ni kitu cha kwanza kufanyika wilayani hapo.Nestori Kigae akitoa kero yake kwa mkuu wa Wilaya ya Njombe alisema kuwa halmashauri hiyo haigawi viwanja kwa vijana na kuwa sasa ni muda mrefu viwanja havijagawiwa na kusasabisha wananchi kukosa maeneo ya kujenga.

  Alisema kuwa vijana wapo tayari kujenga makazi yao lakini halmashauri hiyo haipimi viwanja na kuvigawa kwa wananchi.Mkuu wa wilaya alitoa nafasi kwa afisa wa Ardhi kujibu masuala yanayo husu ardhi yaliyo ulizwa na wananchi.

  Afisa ardhi Taday Kabonge alisema kuwa halmashauri yake ilipima viwanja mwaka 2012 lakini mpaka sasa haijawahi kupima na kuwa kuna viwanja ambavyo mpaka leo bado vipo havijachukuliwa.

  Alisema kuwa viwanja vinavyo gawiwa na halmashauri vinauzwa na havigawiwi bure kwa wananchi na kuwa vinatolewa kwa wananchi wote wa halmashauri hiyo.Katika hotuba ya mkuu wa wilaya ya Njombe ya lisaa limoja kwa wananchi anasema kuwa serikali itahakikisha kero kwa wananchi zinaondoka na kuishi kwa amani bila bughuza.

  Hata hivyo aliitaka halmashauri hiyo kuhakikisha kuwa inapima viwanja mara kwa mara ili wananchi wake kuendelea kupata maeneo ya kujenga na kuachana na kujenga maeneo ambayo hayahusiki.Alisema kuwa haiwezekani halmashauri ikapima viwanja kila mara na sio baada ya miaka minne, na kuwa wananchi wanajenga kila wakati.

  Hata hivyo diwani wa kata ya Njombe Mjini, Agrey Mtambo alilalamika viwanja vinavyo pimwa na halamshauri kuuzwa bei ghari na kusababisha wananchi kushindwa kuvimiliki.

  Na Furaha Eliabu wa Habari Online na Elimtaa

  0 0

   Mwenyekiti Mteule wa Chama cha Afya ya Jamii Tanzania (TPHA), Shaibu Mashombo (wa nne kushoto), akiwa na viongozi wenzake wateule waliochaguliwa katika mkutano mkuu wa chama hicho 2016 jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Dismas Vyagusa, Violeth Shirima, Dk. Godfrey Swai, Dk.Nderineia Swai, Dk. Feliciana Mmasi,  Dk. Mwanahamisi Hassan na Dk.Elihuruma Nangawe ambaye alikuwa Mwenyekiti wa chama hicho aliyemaliza muda wake.
  Mwenyekiti wa Chama cha Afya ya Jamii Tanzania (TPHA), aliyemaliza muda wake Dk.Elihuruma Mangawe (katikati), akiongoza kikao cha mkutano mkuu wa chama hicho. Kushoto ni Katibu Mkuu wa TPHA, Fabian Magoma na kulia ni Ofisa Utawala wa chama hicho, Erick Goodluck.
   Mwenyekiti Mteule wa Chama cha Afya ya Jamii Tanzania (TPHA), Shaibu Mashombo (kulia) akiwaelekeza jambo wajumbe kabla ya kufanyika kwa uchaguzi uliompa nafasi hiyo.
  Wajumbe wakiwa kwenye mkutano huo.
  Mkutano ukiendelea.
  Wajumbe wa mkutano huo.
  Usikivu katika mkutano huo.
  Mkutano ukiendelea.


  Na Dotto Mwaibale

  CHAMA cha Afya ya Jamii (TPHA) kimepata viongozi wapya ambapo kimemchagua Dk. Shaibu Mashombo kuwa Mwenyekiti.

  Mashombo alishinda nafasi hiyo kwa kupata kura 35 na kumbwaga Feliciana Mmassy aliyepata kura 10 na kura moja ikiharibika.

  Katika nafasi ya Mhariri Mkuu Dk.Godfrey Swai aliibuka kidedea dhidi ya Ndeniria Swai aliyepata kura 15 na kura tisa zilikataa ambapo katika nafasi ya Katibu Mwenezi wagombea walikuwa wawili Elizabeth Nchimbi aliyepata kura 15 na Ndeniria Swai ambaye aliibuka mshindi kwa kupata kura 29 huku kukiwa hakuna kura iliyopotea.

  Katika nafasi ya Mtunza Fedha licha ya kuwepo na ushindani makali aliyeibuka mshindi ni Mwanahamisi Hassan ambaye alipata kura kura 20 dhidi ya mgombea mwenzake Violeth Shirima aliyepata kura 24.

  Nafasi ya Katibu wa Mipango ilikwenda kwa Dk. Mwanahamisi Hassan aliyepata kura 38 dhidi ya Othman Shem aliyeambulia kura tano huku Feliciana Mmasi na Dismas Vyagusa wakishinda nafasi ya wajumbe wa kamati ya utendaji.

  0 0

  Shirikisho la Shirikisho la Vyuo vya Elimu ya Juu-CCM, limefanya semina ya utendaji kwa makatibu wake wote wa matawi katika mkoa wa Dar es Salaam, kwa lengo la kuwajengea uwezo katika kazi zao ili kuliimarisha Shirikisho na Chama Cha Mapinduzi.

  Katibu Msaidizi wa CCM, Daniel Zenda alisema, katika semina hiyo iliyofanyia Novemba 30, mwaka huu, jumla ya Makatibu 32 walihudhuria na kuondoka wakiwa wameongeza upeo wao katika kazi zao za chama.

  Alisema, moja ya mambo ambayo walifundwa Makatibu hao ni namna nzuri ya kuwezesha Chama Cha Mapinduzi kupata wanachama wapya miongoni mwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza katika vyuo vikuu, kwa kuwa tegemeo na uhai wa Shirikisho hilo ni wanafunzi wa aina hiyo.

  "Unajua Shirikisho linatilia mkazo sana katika kuhakikisha Makatibu wa Matawi wanashughulika kwa juhudi kubwa kuhakikisha kila wakati tunapata wanachama wapya hasa hawa wanaokuwa wanajiunga katika vyuo katika mwaka wa kwanza kwa kuwa hawa wanakuwa bado wabichi na wenye nguvu kutumikia Shirikisho na Chama kwa jumla", alisema Zenda na kuongeza..

  "Shirikisho linalipa kipaumbele suala la kuingiza wanachama kutoka wale wa mwaka wa kwanza kwa sababu kuingia kwa wanavyuo wapya vyuoni kuna kuwa na maana pia kuwa wapo wanaondoka kutokana na kuhitimu masomo yao, ambao baada ya kuhitimu wanaweze kushindwa kuendelea kuwa wanachama wazuri wa shirikisho kutokana na kubanwa na shughuli nyingine".

  Alisema, katika semina hiyo iliyofanyika Ukumbi wa Sekretarieti, Makao Makuu ya Umoja wa Vijana wa CCM, jijini Dar es Salaam, Makatibu wa matawi walihimizwa juu ya Wajibu wao, Muundo na wajibu wa kazi zao, Umuhimu wa Vikao na kujua tathmini ya  Wanachama Wapya.

  Zenda alisema pia katika semina hiyo, makatibu walielimishwa namna bora ya utunzaji wa kumbukumbu na Taarifa za Vikao, Ufanyikaji wa Madarasa ya itikadi, Uzalendo na Maadili katika  ngazi ya Matawi na namna ya kufuatilia na kuwa tayari kusimamia vema chaguzi ndogo za kuziba nafasi zilizo wazi ndani ya Shirikisho.

  Alisema, waliwataka Makatibu kufuatilia na kujua kwa undani changamoto zilizopo miongoni wa wanafunzi kuhusu mikopo, pia amesema walitakiwa kuhakikisha kila tawi kuwa na vitabu vya Katiba na Ilani ya CCM, na Kanuni za Shirikisho la Elimu ya Vyuo vya Elimu ya Juu-CCM.

  Zenda alisema, pia waliwaelekeza Makatibu kujenga utaratibu wa kupokea maoni, Ushauri na Changamoto wanazokabiliana nazo wanafunzi na wanachama waliopo vyuoni kulingana na mazingira yaliyopo.
   Katibu Msaidizi wa CCM, Daniel Zenda akiongoza semina hiyo
  Washiriki wakiwa kwenye semina hiyo katika Ukumbi wa Sekretarieti, Makao Makuu ya Umoja wa Vijana wa CCM, jijini Dar es Salaam.

  0 0

  Mkuu wa mkoa wa Simiyu Mh Anthony Mtaka (wa pili kulia) akiwa pamoja na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT), Profesa Elifas Bisanda (katikati mwenye tai),  Katibu Tawala wilaya ya Ilala (DAS) Edward Mpogolo (wa pili kulia) Bw Hume wa OUT na Derek Murusuri (kushoto) baada ya majadiliano ya muda mfupi kuhusu mchango wa OUT kwenye maendeleo ya elimu nchini Tanzania jijini leo.

  0 0

  Na.Anthony John blog jamii.

  Naibu Waziri wa nchi ofisi ya Rais tawala za mikoa na serikali  za mitaa  (TAMISEMI) Mh Suleiman Jaffo amewataka watumishi wa umma kufanya kazi kwa kujiamini  katika kutekeleza majukumu yao ili kuleta mabadiliko  ya  kimaendeleo katika Taifa.

  Mh Jaffo ameyasema hayo  leo wakati akizungumza na watumishi wa umma  wa manispaa ya Ilala na jiji la Dar es slaam,  watendaji ,wabunge pamoja na madiwani  na kuwaelekeza wakuu wa idara kufanya kazi na kuwapa ushirikiano watumishi wa ngazi  za chini  katika idara zao na kuacha kuwanyanyasa .

  ‘’Nawaagiza wakuu wa idara  muache kuwa nyanyasa watumishi walio  chini yenu kwakuwa  wengi wanafanya kazi kwa hofu ya kuogopa kutumbuliwa  nakupelekea kutokuwa na amani katika maeneo yao ya kazi.’’ Alisema  Jaffo.

  Aidha amesema  wizara yake itatoa ushirikiano kwa  watumishi wote wanaotekeleza majukumu yao kwa moyo na bidii na amewaagiza wakuu wa idara kuwa na utaratibu wa kutambua kazi za watumishi wanao jituma na kuvuka malengo ya kazi walio wekewa  hatakama hakuna pesa za kuwapa  angalau waandikiwe barua ama kupewa vyeti vya kutambua michango yao mahala pakazi.

  Hata hivyo amempongeza  mkuu wa mkoa wa Dar es salaam , mkurugenzi wa jiji pamoja na madiwani  kwa kusimamia  suala  la usafi wa jiji kuwa nzuri  kwakuwa kipindi cha nyuma jiji lilikuwa halitamaniki.‘’Zamani jiji la Dar es salaam  lilikuwa chafu  lakini kwa sasa  hali imekuwa nzuri ukilinganisha na kabla ya kampeni ya usafi haijaanza.hayo amesema Jaffo.

  Pamoja na hayo mh Jaffo ameuagiza uongozi  wa manispaa ya ilala kwa kushirikiana na katibu tawala  mkoa wa  Dar es salaam  kupitia upya mkataba alio pewa mpangaji katika eneo lilotolewa na Dawasco kwa ajili ya kujenga shule ya kata ya secondary  Buguruni   kutembelea eneo hilo na kisha kufanya maamuzi ili eneo hilo liweze kujengwa shule.

  0 0

   Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati akizundua Bodi ya Udhamini ya Mfuko wa Udhibiti Ukimwi (ATF)  Hoteli ya Hyatt Regency Dar es Salaam jana.
   Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS), Dk.Leonard Maboko akizungumza kwenye uzinduzi huo.
   Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu) Jenista Mhagama akihutubia kwenye uzinduzi wa mfuko huo.
   Wadau wakiwa kwenye uzinduzi huo.

   Meza kuu.
   Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaa, Alhad Salum Mussa (kulia), akishiriki uzinduzi wa mfuko huo na wadau wengine.
   Uzinduzi ukiendelea.
   Mkutano ukiendelea.
   Wadau wakiwa kwenye uzinduzi huo.
   Wadau wakiwa kwenye uzinduzi huo.

   Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan (katikati), akimkabidhi cheti Mkurugenzi wa Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF), Godfrey Simbeye kwa ushiriki wake katika kuchangia mfuko huo. Kutoka kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu), Jenista Mhagama na Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS), Dk.Leonard Maboko. 
   Mwakilishi wa Kampuni ya GGM (Geita), Tenga Tenga akizungumza kwenye uzinduzi huo. Kampuni hiyo ilichangia sh.milioni 100.
   Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akipokea mfano wa hundi yenye thamani ya sh.milioni 100 kutoka kwa Mwakilishi wa Kampuni ya GGM (Geita), Tenga Tenga kwa ajili ya kuchangia mfuko wa ukimwi Dar es Salaam juzi. Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS), Dk.Leonard Maboko.

  Makamu wa Rais akipeana mkono na mdau aliyeshiriki uzinduzi huo. 

  Meneja Mawasiliano Msaidizi  wa Mamlaka ya MawasilianoTanzania (TCRA), Semu Mwakyanjala akizungumza baada ya kutoa mchango wa sh. milioni tano.


  Na Dotto Mwaibale

  MAKAMU wa Rais Samia Suluhu Hassan ameendesha harambee ya sh. bilioni 1,036, 050,000 ahadi ikiwa ni sh. bilioni 5, 913,650,000 pamoja na ahadi ya serikali kwa ajili ya  Mfuko wa Ukimwi Tanzania.

  Akizungumza katika uzinduzi wa Bodi ya Udhamini ya Mfuko wa Ukimwi (ATF) ulioenda sanjari na Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi  Duniani jijini Dar es Salaam juzi,  aliwaomba wadau mbalimbali  kuchangia mfuko huo ili kukabiliana na changamoto ya ukimwi nchini.

  "Tunaomba wadau mbalimbali kusaidia mfuko huo kwani bado tunachangamoto kubwa ya ugonjwa wa ukimwi" alisema Makamu wa Rais mama Samia.

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu) Jenista Mhagama Sera ya ukimwi ya mwaka 2001 imeelekeza kuanzishwa kwa mfuko wa ukimwi ambapo serikali ilianza mchakato wa kuanzisha mfuko huo mwaka 2008.

  Alisema mfuko huo umeanzishwa kwa kupitia marekebisho ya Sheria ya Tume ya Kudhibiti Ukimwi namba 6 ya mwaka 2015.

  "Madhumuni makubwa ya mfuko wa Ukimwi ni kuhakikisha uwepo wa rasilimali za kutosha na za uhakika katika kupambana na ukimwi zilizotokana na mapato ya ndani" alisema Mhagama.

  Alisema kulingana na Mkakati wa Tatu wa Taifa wa Kudhibiti Ukimwi uliothaminishwa, mahitaji ya Taifa kugharamia Ukimwi katika kutekeleza makakati huo kwa kipindi cha miaka mitano 2013/14 na 2017/18 yanakadiriwa kufika 6 Trilioni (USD 2.975 bilioni).

  Alisema asilimia 93 ya fedha hizo zinatarajiwa kutoka kwa wafadhili na asilimia 7 kutoka vipato vyandani na kuwa sehemu kubwa ya asilimia 56 ya fedha zote katika miaka hiyo mitano ni kwa ajili ya manunuzi ya dawa za kufubaza VVU (ARV drugs)

  Alisema mahitaji ya fedha katika kipindi cha mwaka 2016/17 ni Trilioni 1.258, fedha ambazo zimeahidiwa na wafadhili ni Tsh. Bilioni 833 na hivyo kuwa na upungufu wa Bilioni 425.

  Alisema katika kipindi cha mwaka 2017/18 mahitaji ya fedha ni Tsh. Trilioni 1.260, fedha ambazo zimeahidiwa na wafadhili ni Tsh. Bilioni 740 na hivyo kuwa na upungufu wa Bilioni 520.

  Mhagama alisema licha ya kupungua kwa ahadi ya wafadhili bado hakuna uhakika kama fedha zilizoahidiwa zitapatikana zote kwa mantiki hiyo hivyo kuongeza fedha zinazotoka ndani ya nchi ni suala la muhimu sana.
  0 0

   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza  na watumishi wa serikali na halmashauri wa mkoa wa Arusha kwenye ukumbi wa Simba wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha, Desemba 2, 2016.
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea  taarifa ya mkoa wa Arusha kutoka kwa Mkuu wa Mkoa huo, Mrisho Gambo baada ya kusomewa taarifa hiyo katika mkutano wake na watumishi wa serikali na halmashari kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) Desemba 2, 2016.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea bahasha yenye nyaraka mbalimbali zinazoonyesha ubadhirifu  unaofanyika katika halmashauri ya Wilaya ya Arusha kutoka kwa  Benard Mtei wa Idara ya Afya katika halmashauri hiyo wakati alipozungumza  na watumishi wa serikali na halmashauri mjini Arusha Desemba 2, 2016. 
  Baadhi ya watumishi wa serikali na halmashauri wakimsikiliza  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza  nao kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC), Desemba 2, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

   Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (katikati) akisaini Mkataba kwa niaba ya Serikali na Klabu ya Yanga ya jijini Dar es salaam ambayo iliwakilishwa na Kaimu Katibu Mkuu wa Klabu hiyo Baraka Deusdedit (kulia) leo jijini Dar es salaam. Mkataba huo unahusu Klabu ya Yanga kutumia Uwanja Mkuu wa Taifa na Uwanja wa Uhuru katika mechi za Kimataifa na Ligi Kuu. Wa kwanza kushoto ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Sheria Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Evordy Kyando. 
   Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akibadilishana Mkataba waliosaini na Kaimu Katibu Mkuu wa Klabu ya Yanga Baraka Deusdedit leo jijini Dar es salaam.  Mkataba huo unahusu Kalabu ya Yanga kutumia Uwanja Mkuu wa Taifa na Uwanja wa Uhuru, Wa kwanza kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Alex Nkenyenge.
  Picha ya pamoja ya Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (wa pili kushoto) mara baada ya kusaini Mkataba na Klabu ya Yanga leo jijini Dar es salaam. Wa pili kulia ni Kaimu Katibu Mkuu wa Klabu ya Yanga Baraka Deusdedit.


  Na Eleuteri Mangi – WHUSM.

  Serikali imesaini Mkataba na Klabu ya Yanga kutumia Uwanja Mkuu wa Taifa pamoja na Uwanja wa Uhuru kwa ajili ya michezo yote ya Kimataifa pamoja na michezo ya Ligi Kuu ya ndani. 

  Mkataba huo umesainiwa leo jijini Dar es salaam na Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel kwa niaba ya Serikali na Kaimu Katibu Mkuu wa Klabu ya Yanga Baraka Deusdedit kwa niaba ya Klabu ya Yanga.

  Katika Mkataba huo, Klabu ya Yanga imeruhusiwa kutumia viwanja hivyo kama viwanja vyake vya nyumbani kwa sharti la kuvitunza viwanja hivyo wakati wote wanapovitumia.

  Miongoni mwa masharti hayo ni kutunza viwanja, mali na vifaa vyote vilivyopo katika viwanja hivyo, na endapo kutatokea uharibifu wowote utakaofanywa na wachezaji ama mashabiki, Klabu hiyo itawajibika kubeba gharama za matengenezo yote yatakayotokana na uharibifu huo.

  Aidha, Klabu ya Yanga inaweza kutumia viwanja hivyo kwa mazoezi ya kujianadaa na mechi zinazowakabili.

  0 0

  Mwenyekiti wa muda wa mitandao ya Kijamii Tanzania Bloggers Network (TBN), Joachim Mushi (wa pili kulia) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mkutano mkuu wa chama cha Bloggers Tanzania (TBN) utakaofanyika kwa siku mbili katika ukumbi wa PSPF jijini Dar es Salaam.Kulia ni Katibu wa TBN,Khadija Khalili na Mwisho kushoto ni Meneja wa Mitandao wa NMB,Joyce Nsekela.

  Akizungumza  mbele ya Wanahabari  mapema leo (hawapo pichani) ndani ya Ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO,Mwenyekiti wa Tanzania Bloggers Network (TBN),Joachim Mushi amesema kuwa mkutano huo unatarajiwa kufanyika kuanzia Desemba 5 na 6 ,2016 hapa hapa jijini Dar,ambao utawashirikisha wanachama wapatao 150 kutoka Tanzania Bara na Visiwani.Mushi alisema kuwa katika mkutano huo Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Habari,Michezo,Utamaduni na Sanaa Mh Nape Mosses Nnauye,

  "Mgeni rasmi anaetarajiwa kufungua mkutano huo ni  Waziri Nape Nnauye,lengo kuu la mkutano huo likiwa ni kupeana elimu na kubadilishana mawazo  juu ya uendeshaji wa Mitandao ya Kijamii kwa manufaa,upashaji habari kwa kutumia mitandao yao kwa kuzingatia maadili  na namna ya kunufaika na mitandao hiyo kwa waendeshaji",alisema Mushi.

  Alisema kuwa uendeshaji wa Mitandao baadhi yao wanaifanya ni kama ajira nyingine,hivyo kimsingi lazima wakubali kuwa mitandao hii imekuwa tegemeo kubwa la kusambaza habari mbalimbali tena kwa muda mfupi tangu kutokea kwa tukio fulani,hivyo kuna kila sababu ya kuendelea kuwapiga msasa wanaoiendesha ili kupunguza matumizi mabaya  ya mitandao hii,

   Mkutano huo utakaokuwa wa aina yake na kuiandika historia tangu kuanza kwa mitandano ya Kijamii hapa nchini,umedhaminiwa na Benki ya NMB ambaye ni mdhamini mkuu ,NHIF, SBL, PSPF na Coca Cola
  Ofisa Uhusiano wa NMB, Doris Kilale akizungumzia udhamini wa benki ya NMB katika mkutano mkuu wa Chama cha Bloggers Tanzania (TBN) utakaofanyika kwa siku mbili na kuwakutanisha blogger kutoka Tanzania Bara na Visiwani.   
  Mwenyekiti wa muda wa Chama cha Bloggers Tanzania (TBN), Joachim Mushi(wa pili kutoka kulia) akipokea hundi ya shilingi milioni 10 kutoka kwa Ofisa Uhusiano wa NMB, Doris Kilale kwa ajili y kudhamini mkutano huo.

  0 0


  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisaini kitabu cha kumbukumbu cha maombelezo ya aliyekuwa Rais wa nchi hiyo na mpigania ukombozi Fidel Castro aliyefariki dunia novemba 25,2016 mjini Havana, aliyesimama kushoto ni Balozi wa Cuba nchini Balozi Jorge Luis Lopez Tormo.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisaini kitabu cha kumbukumbu cha maombelezo ya aliyekuwa Rais wa nchi hiyo na mpigania ukombozi Fidel Castro aliyefariki dunia novemba 25,2016 mjini Havana.


  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Munngano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikata utepe katika vitendea kazi kama ishara ya Uzinduzi wa Bodi ya Udhamini dhidi ya Ukimwi uliofanyika tarehe 1 Desemba kwenye hotel ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Munngano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akionyesha vitendea kazi atakavyovikabidhi kwa bodi mara baadaya ya kuizindua  Bodi ya Udhamini dhidi ya Ukimwi uliofanyika tarehe 1 Desemba kwenye hotel ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Munngano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Mwenyekiti wa Bodi ya Udhamini dhidi ya Ukimwi Bw. Godfrey Simbeye vitendea kazi vya bodi hiyo mpya katika hafla ya uzinduzi wa bodi hiyo uliofanyika tarehe 1 desemba kwenye hotel ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Munngano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia kwenye Uzinduzi wa Bodi ya Udhamini dhidi ya Ukimwi uliofanyika tarehe 1 Desemba kwenye hotel ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.

                    ................................................................................................... 

  Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan amezindua Bodi ya Udhamini dhidi ya UKIMWI na kuwagawia vitendea kazi sambamba na uzinduzi wa mpango wa hiari wa familia kuchangia mfuko wa UKIMWI, shughuli iliyokwenda sambamba na maadhimisho ya siku ya Ukimwi duniani ambayo huadhimishwa duniani kote desemba mosi.


  Madhumuni ya Bodi hiyo ni kujenga nguvu ya ndani ya kifedha pamoja na kuhakikisha uwepo wa rasilimali za kutosha katika kupambana na ugonjwa wa Ukimwi ambao bado ni tishio huku tafiti za mwaka 2015 zikionesha kuwa takribani watu 48,000 huambukizwa VVU kila mwaka nchini, huku watu milioni 1.5 wakiishi na VVU kati yao wastani wa laki nane wanatumia dawa za kufubaza virusi vinavyosababisha UKIMWI.

  Akizungumza katika uzinduzi huo, Makamu wa Rais amesema kazi kubwa ya kutafuta kutunisha mfuko itakuwa ni chachu katika kupambana na ugonjwa huo na kuitaka bodi hiyo kubuni mbinu za kutunisha mfuko huo kufuatia ukweli kwamba uhisani una mwisho na uhisani una vipaumbele vyake kutokana na wakati husika.

  Katika harambee iliyofanyika jana usiku wakati wa uzinduzi wa bodi hiyo,zaidi ya milioni 340 zilipatikana.

  0 0

   Naibu Waziri Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura (wa pili kulia) akisalimiana na Bw. Kishor Thakrar kutoka  Kampuni ya Shree All World Gayarti Pariwar inayohamasisha jamii huru  isiyotumia Dawa za Kulevya, kutunza na kuhifadhi mazingira pamoja na kuwa na mazoezi ya afya kwa jamii walipomtembelea ofisini kwake kwa ajili ya kumpatia vitabu vinavyohamasisha jamii iliyo huru, leo jijini Dar es Salaam. 
   Bw. Kishor Thakrar kutoka Kampuni ya Shree All World Gayarti Pariwar inayohamasisha jamii huru  isiyotumia Dawa za Kulevya, kutunza na kuhifadhi mazingira pamoja na kuwa na mazoezi ya afya kwa jamii (kulia) akizungumza na Naibu Waziri Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura alipomtembelea ofisini kwake kwa ajili ya kumkabidhi vitabu vinavyotoa elimu kwa jamii juu ya madhara ya Dawa za  Kulevya pamoja na uharibifu wa mazingira leo jijini Dar es Salaam.
   Naibu Waziri Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura (wapili kulia) akizungumza na ujumbe kutoka Kampuni ya Shree All World Gayarti Pariwar inayohamasisha jamii huru isiyotumia Dawa za Kulevya, kutunza na kuhifadhi mazingira pamoja na kuwa na mazoezi ya afya kwa jamii walipomtembelea ofisini kwake kwa ajili ya kuwasilisha vitabu wanavyovitumia kutoa elimu hiyo kwa jamii hasa katika shule za msingi na sekondari leo jijini Dar es Salaam. 
   Naibu Waziri Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura (wapili kulia) akipokea vitabu vinavyotumika kuhamasisha jamii hasa wanafunzi wa Shule za Msingi na Sekondari kujiepusha na matumizi ya Dawa ya Kulevya pamoja na kuhifadhi mazingira kutoka kwa ujumbe kutoka Kampuni ya Shree All World Gayarti Pariwar inayohamasisha jamii huru isiyotumia Dawa ya Kulevya, kutunza na kuhifadhi mazingira pamoja na kuwa na mazoezi ya afya kwa jamii walipomtembelea ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam. 
     Bibi. Sarla Thakrar kutoka Kampuni ya Shree All World Gayarti Pariwar inayohamasisha jamii huru isiyotumia Dawa ya Kulevya, kutunza na kuhifadhi mazingira pamoja na kuwa na mazoezi ya afya kwa jamii (katikati) akimuonyesha Naibu Waziri Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura (kulia) moja ya vitabu vinavyotumika kuwaongoza vijana kuwa huru na kuacha kutumia madawa ya kulevya walipomtembelea ofisini kwake kwa ajili ya kuwasilisha vitabu hivyo ili viweze kutumiwa na jamii leo jijini Dar es Salaam.
   Naibu Waziri Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura (wapili kulia) akiangalia picha za matukio mbalimbali yanayofanywa na Kampuni ya Shree All World Gayarti Pariwar inayohamasisha jamii huru isiyotumia madawa ya kulevya, kutunza na kuhifadhi mazingira pamoja na kuwa na mazoezi ya afya kwa jamii walipomtembelea ofisini kwake leo Jijini Dar es Salaam.
  Picha na: Genofeva Matemu - WHUSM

  0 0  0 0

  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akisalimiana na Balozi wa Umoja wa Falme za Kiarabu nchini Mhe.Abdulla Ibrahim Ghanim Alsuwaidi alipowasili katika ofisi za ubalozi huo kushiriki sherehe ya madhimisho ya miaka 45 ya muungano.Tanzania na UAE zimepiga hatua kubwa za ushirikiano hususan ya kiuchumi ambapo kwa takwimu za Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC) hadi Juni, 2015 makampuni 67 ya uwekezaji kutoka UAE yamewekeza hapa nchini katika sekta mbalimbali wenye thamani ya USD 497.12 Millioni na kuajiri Watanzania 9,044. Taifa la Umoja wa Falme za Kiarabu unaundwa na falme saba ambazo ni Abu Dhabi, Dubai, Sharjah, Ras Al Khaimah, Fujairah, Ajman na Umm al-Quwain .
  Rais Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya nne ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Taifa la Umoja wa Falme za Kiarabu Mhe.Abdulla Ibrahim Ghanim Alsuwaidi wakati wa sherehe ya maadhimisho ya miaka 45 ya muungano wa falme hizo .
  Mhe.Waziri Balozi Dkt.Mahiga akivalishwa skafu maalum
  Mhe.Waziri Balozi Dkt. Mahiga akiwa katika picha ya pamoja na Balozi Mhe.Abdulla Ibrahim Ghanim Alsuwaidi
  Wageni waalikwa wakifuatilia jambo
  Balozi wa Taifa la Umoja wa Falme za Kiarabu Mhe.Abdulla Ibrahim Ghanim Alsuwaidi akizungumza wakati wa maadhimisho
  Mhe. Waziri Balozi Dkt. Mahiga akitoa hutuba fupi wakati wa maadhimisho ya sherehe hizo
  Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati Balozi Abdalla Kilima akisalimiana na Mhe. Balozi wakati wa sherehe za maadhimisho 

  ----------------------------------------------------------- 

  Tanzania na Umoja wa Nchi za Kiarabu (UAE) zimepiga hatua kubwa za ushirikiano hususan wa kiuchumi ambapo kwa takwimu za Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) hadi Juni, 2015 Makampuni 67 kutoka UAE yamewekeza hapa nchini katika sekta mbalimbali kwa mtaji wa thamani ya Dola za Marekani milioni 497.12 na kuajiri Watanzania zaidi ya 9,044. 

  Hayo yalibainishwa jana katika sherehe za kuadhimisha Siku ya Kitaifa ya UAE zilizofanyika jijini Dar Es Salaam ambapo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga alikuwa Mgeni Rasmi. 

  Tanzania na UAE zinatarajiwa kufanya Mkutano wa Kwanza wa Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano (JPC) ambao utakuwa chachu ya kuimarisha mahusiano baina ya nchi hizi mbili hususan ya kiuchumi.

  Akiongea katika hafla hiyo, Mhe. Waziri alilipongeza taifa hilo kwa kuadhimisha siku yake ya Kitaifa ikiwa imepiga hatua kubwa ya kimaendeleo ya kichumi, kijamii na kisiasa. Mhe. Waziri alisema kuwa siku hiyo ni inatoa fursa pia ya kutathmini mahusiano mazuri yaliyopo baina ya Tanzania na UAE. 

  Kwa upande wake, Balozi wa UAE hapa nchini, Mhe. Abdulla Ibrahim Ghanim Alsuwaidi aliishukuru Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano mkubwa inayotoa kwa Ubalozi huo ambao unamwezesha kutekeleza majukumu yake kwa wepesi ikiwa ni pamoja na kuimarisha mahusiano ya nchi hizi mbili. Mhe. Balozi aliahidi kuendeleza ushirikiano huo hususan katika kutimiza azma ya Serikali ya Awamu ya Tano ya Kuifanya Tanzania kuwa nchi ya Viwanda. 

  Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) unajumusha falme saba ambazo ni Abu Dhabi, Dubai, Sharjah, Ras Al Khaimah, Fujairah, Ajman na Umm al-Quwain huadhimisha siku yake ya Kitaifa tarehe 02 Disemba ya kila mwaka tokea mwaka 1971.

older | 1 | .... | 1056 | 1057 | (Page 1058) | 1059 | 1060 | .... | 1897 | newer