Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1050 | 1051 | (Page 1052) | 1053 | 1054 | .... | 1903 | newer

  0 0

   Mwenyekiti wa Jukwaa la  Wastaafu wa Taaluma ya Elimu, Profesa Herme Joseph Mosha akizungumza na waandishi wa habari kuhusu wakati wa kukitambulisha rasmi Jukwaa hilo katika Ukumbi wa Idara ya Habari –MAELEZO leo jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni wajumbe wa Sekretarieti ya chama hicho Bibi. Khadija Mchatta Maggid na Muhwela Kalinga.
   Katibu Mtendaji wa Jukwaa la Wastaafu wa Taaluma ya Elimu, Bibi. Marystella Maufi Wassena akifafanua jambo wakati wa mkutano wa kukitambulisha Jukwaa hilo leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mwenyekiti wa Jukwaa hilo Profesa. Herme Joseph Mosha
   Mjumbe wa Sektretarieti ya Jukwaa la  Wastaafu wa Taaluma ya Elimu Bw. Muhwela Kalinga akielezea jambo wakati wa mkutano wa kukitambulisha chama hicho leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa Jukwaa hilo Profesa Herme Joseph Mosha.
   Baadhi ya Sekretarieti ya Jukwaa la  Wastaafu wa Taaluma ya Elimu wakiwa katika mkutano na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam. Picha zote na: Frank Shija

  WALIMU wastaafu nchini wameanzisha jukwaa maalum litakalotumika kwa ajili ya kushauriana na kubadiliana uzoefu baina yao na serikali kuhusu mfumo na utaratibu utoaji bora wa elimu nchini.
  Hayo yamesemwa leo, Jijini Dar es Salaam na mwenyekiti wa jukwaa hilo Prof. Herme Mosha alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari juu ya lengo la uanzishwaji wa jukwaa hilo.

  Prof. Mosha alisema walimu wastaafu wana uzoefu mkubwa katika sekta ya elimu hivyo kupitia jukwaa hilo watakuwa wakitafakari maeneo ambayo sekta ya elimu  haitoweza kufanya vizuri na hivyo kuishauri hatua zinazopaswa kuchuliwa na Serikali.

  “Unapokuwa mtumishi wa Umma unaona kila kitu kinaenda sawa, lakini unapokuwa nje unaona kuna mambo mengi ambayo yalikuwa hayaendi sawasawa,” alifafanua Prof. Mosha.

  Kwa mujibu wa Prof. Mosha alisema alipokuwa katika utumishi Umma walikuwa wakiandikisha wanafunzi wa darasa la kwanza  kwa asilimia 95, lakini baada ya tamko la elimu bila ada idadi ya wanafunzi iliongezeka zaidi.

  Prof. Mosha alisema kitendo hicho kinaonyesha kuwa n kwamba  asilimia kubwa ya watoto walikuwa hawaandikishwi kuanza elimu ya msingi kutokana na vikwazo vya ada.

  Aidha aliipongeza serikali Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuboresha sekta ya elimu ambapo kwa sasa kila mwanafunzi anakaa katika dawati tofauti na miaka ya nyuma.

  Kwa upande wake Katibu wa Jukwaa hilo Bi. Marystella Wassena alisema jukwaa hilo litakuwa likijishughulisha pia na kufanya tafiti  mbalimbali za kuboresha sekta ya elimu.


  Bi. Wassena aliwataka walimu waastaafu nchini kujiunga na jukwaa hilo na kutumia uzoefu walioupata ili kuishauri Serikali na kuhakikisha kuwa elimu bora inatolewa katika ngazi zote za elimu. 


  0 0

  Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania, Dk. Haruni Kondo (katikati), akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam jana, kuhusu kuipitia upya mikataba iliyoingia shirika hilo na Taasisi mbalimbali na watu binafsi kutokana na baadhi yake kugundulika ikiwa na utata wa maslahi ya shirika hilo. Kushoto ni Kaimu Postamasta Mkuu, Fortunatus Kapinga na Kulia ni Katibu wa Shirika, Rochus Assenga. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
  Baadhi ya wakuu wa vitengo vya Shirika la Posta na waandishi wa habari, wakifuatilia masuala mbalimbali yaliyokuwa yakielezwa na Mwenyekiti wa Bodi ya shirika hilo, Dk. Haruni Kondo katika mkutano huo.  
  Baadhi ya wakuu wa vitengo vya Shirika la Posta wakifuatilia maelezo yaliyokuwa yakitolewa na Mwenyekiti wa bodi ya shirika hilo, Dk. Haruni Kondo kwa waandishi wa habari, jijini Dar es Salaam jana.
  Baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya Shirika la Posta wakimsikiliza Mwenyekiti wa bodi hiyo, Dk. Haruni Kondo, wakati alipokuwa akielezea kuhusu kuipitia upya mikataba yenye utata, iliyoingia shirika hilo na taasisi mbalimbali pamoja na watu binafsi. 
  Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania, Dk. Haruni Kondo, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam jana, kuhusu kuipitia upya mikataba iliyoingia shirika hilo na Taasisi mbalimbali na watu binafsi kutokana na baadhi yake kugundulika ikiwa na utata wa maslahi ya shirika hilo.
  Baadhi ya waandishi wa habari na baadhi ya wakuu wa vitengo vya Shirika la Posta, wakifuatilia masuala mbalimbali yaliyokuwa yakielezwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania, Dk. Haruni Kondo katika mkutano huo. 
  Baadhi ya wakuu wa vitengo vya Shirika la Posta na waandishi wa habari, wakiwa katika mkutano huo.
  Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta, Fortunatus Kapinga, akitoa ufafanuazi kwa waandishi wa habari na pia kuitaja baadhi ya miradi hiyo na sehemu ilipo, wakati wa mkutano huo. Katikati ni Mwenyekiti wa Bodi ya shirika, Dk. Haruni Kondo na kulia ni Katibu wa shirika hilo, Rochus Assenga. 
  Baadhi ya wapiga picha wa vyombo vya habari, wakichukua maelezo yaliyokuwa yakitolewa na Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania, Dk. Haruni Kondo, wakati akizungumza na waandishi wa habari. 
  Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta, Fortunatus Kapinga, akitoa ufafanuazi kwa waandishi wa habari walipotaka ufafanuazi wa masuala mbalimbali kuhusu miradi hiyo. Katikati ni Mwenyekiti wa Bodi ya shirika, Dk. Haruni Kondo na kulia ni Katibu wa shirika hilo, Rochus Assenga. 
  Baadhi ya wakuu wa vitengo vya Shirika la Posta wakiwa katika mkutano huo na waandishi wa habari. 
  Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania, Dk. Haruni Kondo (katikati), akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari, wakati akijibu maswali kuhusu masuala mbalimbali ya utekelezaji na hatua zitakazo chukuliwa kwa wahusika wa mikataba hiyo, isiyo na tija kwa shirika hilo.

  0 0


  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia nguo zinazotengenezwa na Kiwanda cha A to Z,kulia ni Mkurugenzi wa kiwanda hicho Bw.Kalpesh Shah.Makamu wa Rais amefanya ziara kwenye kiwanda hicho ikiwa sehemu yakutambua mchango wa wawekezaji wa ndani na changamoto wanazokutana nazo ili kupata majibu ya kurahisisha kufanikisha Tanzania mpya ya Viwanda.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia namna nguo zinazotengenezwa na Kiwanda cha A to Z kilichopo Kisongo mkoani Arusha,kulia ni Mkurugenzi wa kiwanda hicho Bw.Kalpesh Shah.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo ya namna kiwanda cha A to Z kinavyofanya utafiti wa kupambana na wadudu wanaoharibu Mahindi kutoka kwa Mkurugenzi wa kituo cha utafiti cha Africa Technical Research Centre Dkt.Johson Ouma Odera.


  .......................................................................................

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema serikali itaendelea kuviimarisha vyuo vya ufundi stadi nchini –VETA- ili viweze kutoa wahitimu bora ambao watakidhi katika soko la ajira hasa kwenye viwanda vilivyopo na vitajengwa nchini.

  Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo leo wakati anazungumza na uongozi wa kiwanda cha A to Z kilichopo mkoani Arusha katika ziara yake ambayo imeingia siku ya Pili ya kutembelea viwanda mbalimbali mkoani humo ili kujua changamoto zinazokabili viwanda hivyo na serikali kuzitafutia ufumbuzi.

  Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amesema serikali imetenga fedha za kutosha zitakazotumika kuviimarisha vyuo vya Veta ili viweze kutoa mafunzo bora yatakayosidia vijana kufanya kazi zao kwa ufanisi wa hali ya juu pindi watakapoajiriwa au kujiajiri wenyewe.

  Kuhusu maslahi kwa wafanyakazi wa Kiwanda cha A to Z,Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ameutaka uongozi wa kiwanda hicho kulinda na kutetea haki za wafanyakazi kwa kutoa maslahi mazuri ambayo yatawezesha wafanyakazi hao kufanya kazi kwa bidii.

  Makamu wa Rais pia amesisitiza usawa katika ulipaji wa mishahara kwa wafanyakazi wa ndani na wa nje ya nchi walioajiriwa kwenye kiwanda hicho ili kuondoa tofauti za mishahara hali ambayo ijenga motisha kwa wafanyakazi.Kiwanda cha A to Z kilichopo eneo la Kisongo mkoani Arusha ambacho kinatengeneza vyandarua, nguo na mifuko mbalimbali ikiwemo ya saruji kimeajiri zaidi ya wafanyakazi 7500 ambapo asilimia 80 ya wafanyakazi wote ni wanawake.

  Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amewahimiza wawekezaji kote nchi walipe kodi za serikali mapema kodi ambazo zitatumika kuimarisha utoaji wa huduma bora kwa wananchi.

  Amewahakikishia wawekezaji kuwa Tanzania itaendelea kujenga na kuimarisha mazingira bora kwa wawekezaji ili kuhakikisha wawekezaji wanafanyakazi zao vizuri kwa ajili ya manufaa ya taifa na ya wawekezaji.

  0 0


  Na Dotto Mwaibale

  SHILINGI milioni 10 zinazodaiwa kutolewa na Halmshauri ya Manisaa ya Temeke kwa ajili ya ujenzi wa choo katika  Soko la Madenge hazijulikani zilipo hivyo kuzua tafrani kwa wananchi.

  Wananchi hao wamelalamikia kukosa choo katika soko hilo kwa zaidi ya miaka mitano licha ya kutengwa kiasi hicho cha fedha kwa ajili ya ujenzi wa choo hicho.

  Wakizungumza kwa nyakati tofauti na mtandao wa www.habari za jamii.com wananchi hao walisema wanalazimika kutumia choo cha kulipia baada ya choo cha soko hilo kilichoanza kujengwa kushindwa kumalizika.

  Mmoja wa wafanyabiashara wa soko hilo ambaye aliomba jina lake lihifadhiwe alisema Manispaa ya Temeke ilitenga  fedha hizo kwa ajili ya ujenzi wa choo hicho lakini kwa muda wa miaka mitano ujenzi wake haujakamilika.Hali hiyo inaleta adha kwa wafanyabiashara kwa kuendelea kulipia huduma za choo kilichopo sokoni hapo kinyume cha matarajio yao.

  " Hii ni hujuma au matumizi mabaya ya fedha  kwa nini ujenzi wa choo umeishia njiani licha ya fedha kutolewa na Manispaa na kibaya zaidi baadhi  ya miundombinu kama milango imeng'olewa hivyo kubaki kama gofu" alihoji.

  Akitoa ufafanuzi wa malalamiko hayo Ofisa Masoko wa Wilaya ya Temeke, Johnson Makalanga alikiri kuwepo kwa jambo hilo na kuwa limetokana na mkandarasi aliyepewa tenda ya ujenzi wa choo hicho kukomea njiani kwa kuwa fedha zake hakumaliziwa."Ninachofahamu mimi Changamoto kubwa iliyosababisha kutokamilika kwa ujenzi huo ni mkandarasi kucheleweshewa fedha zake kwani anadai sh.milioni 4" alisema Makalanga.

  Makalanga aliongeza kuwa ujenzi wa vyoo hivyo ilikuwa ni kwa baadhi ya masoko ya wilaya hiyo ambapo yeye alisimamia kujenga choo kilichopo kwa Urasa Kigamboni ambacho kinatoa huduma na kuingiza mapato yanayotokana na wananchi kuchangia fedha baada ya kupata huduma za choo hicho.

  Makalanga alisema hawezi kulizungumzia suala hilo kwa mapana kwa vile ni hayupo kwa muda mrefu katika kata hiyo badala yake aliomba atafutwe ofisa Mtendaji au Diwani wa Kata ya Temeke kwa ufafanuzi zaidi.

  Jitihada za gazeti hili kumpata mtendaji wa kata hiyo ziligonga mwamba baada ya kufika ofisini kwake jana na kuambiwa alikuwa kwenye kikao na watendaji wake.
   Choo cha Soko la Madenge katika Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam kikiwa kimeng'olewa milango kutokana na kutokamilika ujenzi wake licha ya manispaa hiyo kutenga sh.milioni 10 za ujenzi. 
   Mkazi wa Temeke akipita mbele ya choo hicho.
  Mwonekano wa moja ya tundu la choo hicho ambacho hakina miundombinu ya mifereji.

  0 0


   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipofungua Mkutano wa Mwaka wa 21 wa Chama cha Wanasheria Afika ya Mashariki   kwenye ​ Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam Novemba 25, 2016.
  Waziri wa Katiba na Sheria Dkt.  Harrison Mwakyembe akizungumza katika mkutano wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam Novemba 25, 2016.
   Baadhi ya washiriki wa Mkutano   wa 21 wa mwaka wa Chama cha Wanansheria Afrika Mashariki wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  wakati alipofungua mkutano huo  kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam Novemba 25, 2016.
   aziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Rais wa Chama cha Wanansheria Afrika  Mashariki Wakili Nassor Hamis Mohmmed (kushoto) na Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt.Harrison Mwakyembe (kulia)  baada ya kufungua ​Mkutano wa Mwaka wa 21 wa Chama cha Wanasheria Afrika ya Mashariki  kwenye ​ Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam Novemba 25, 2016. 

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0


  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa sherehe fupi za ufunguzi wa jengo la ofisi za Umoja wa Mataifa litakalotumika kutunza kumbukumbu mbalimbali za Mahakama ya Umoja wa Mataifa Kuhusu Mauaji ya Rwanda (MICT) katika eneo la Laki Laki nje kidogo ya mji wa Arusha.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka jiwe la msingi la ufunguzi wa jengo la ofisi za Umoja wa Mataifa litakalotumika kutunza kumbukumbu mbalimbali za Mahakama ya Umoja wa Mataifa Kuhusu Mauaji ya Rwanda (MICT) katika eneo la Laki Laki nje kidogo ya mji wa Arusha.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa Mahakama hiyo wakati ufunguzi wa jengo la ofisi za Umoja wa Mataifa litakalotumika kutunza kumbukumbu mbalimbali za Mahakama ya Umoja wa Mataifa Kuhusu Mauaji ya Rwanda (MICT) katika eneo la Laki Laki nje kidogo ya mji wa Arusha, kutoka kushoto ni John Hocking (Msajili MICT ), Theodor Meron (Rais wa MICT ) , Miguel de Serpa Suares (Msaidizi wa katibu mkuu wa Umoja wa Taifa katika masuala ya kisheria ) ,kulia ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga, Mkuu wa mkoa wa Arusha mhe. Mrisho Gambo,Serge Brammertz (Mwendesha Mashitaka wa MICT ) na Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Mohamed Chande Othman (kulia)

  .......................................................................

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan amezindua majengo ya ofisi za Umoja wa Mataifa zitakazotumika kutunza kumbukumbu mbalimbali za Mahakama ya Umoja wa Mataifa Kuhusu Mauaji ya Rwanda (MICT) katika eneo la Laki Laki nje kidogo ya mji wa Arusha.

  Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amezindua majengo hayo kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dakta John Pombe Magufuli na kusisitiza kuwa Tanzania itaendelea kudumisha mahusiano

  Majengo hayo yamejengwa katika eneo la Laki laki mkoani Arusha baada ya Serikali ya Tanzania kuipatia Umoja wa Mataifa eneo lenye ukubwa wa ekari 16.17 bure kwa ajili ya kujenga hayo ya kihistoria hapa nchini.

  Tanzania inaomba nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kusaidia kupatikana kwa wote waliohusika na mauaji hayo ya kimbari ili kuhakikisha haki inapatikana kwa wahanga wa mauaji hayo.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI  0 0

   Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akikata utepe kuzindua vyumba vya madarasa katika shule ya Sekondari ya Urafiki wilayani Ubungo mkoani humo, leo akiwa katika ziara kukagua utekelezaji wa Ilani ya Chama, kusikiliza kero za wananchi na kujadili nao namna ya kuzitatua. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Humphrey Polepole.
   Makonda akiondoka baada ya kuzindua vymba hivyo vya madarasa katika shule ya sekondari ya Urafiki
   Makonda akimtania mwanafunzi wa shule ya sekondari ya Urafiki Rajabu Fadhili, baada ya kuzindua vyumba vya madarasa kwenye shule hiyo leo
   Makonda akimtania mwanafunzi wa shule ya sekondari ya Urafiki Rajabu Fadhili, baada ya kuzindua vyumba vya madarasa kwenye shule hiyo leo
   Makonda akimtania mwanafunzi wa shule ya sekondari ya Urafiki Rajabu Fadhili, baada ya kuzindua vyumba vya madarasa kwenye shule hiyo leo
   Makonda akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Ubingo Humphrey Polepole, baada ya kuzindua vyumba vya madarasa kwenye shule hiyo leo

   Wananfunzi wakisubiri kumsikiliza Makonda baada ya kuzindua vyumba vya madarasa ya shule hiyo leo
  Mkuu wa wilaya ya Ubungo Polepole akizungumza maneno ya utangulizi kumkaribisha makonda kuzungumza.

  MAKONDA AKIFURAHIWA NA WANANFUNZI WAKATI AKIONDOKA BAADA YA KUZINDUA VYUMBA VYA MADARASA
  ??

  MKUTANO WA HADHARA MARAMBA MAWILI
  ??
  Wananchi wa King'zanzi, Malamba mawili, wakiwa na bango lenye ujumbe waliokusudia aupate Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alipohutubia mkutano wa hadhara kusikiliza kero za wananchi katika eneo hilo leo
  Mwananchi akiluiza swali kuhusu kero ya vijiwe vya wavutabangi na vibaka ambao alidai wamekuwa wakikamatwa na polisi na kisha kuachwa.
  Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akijibu baadhi ya maswali kwa kuwaita wahusika kutoka katika maofisa kadhaa alipofuatana nao katika msafara wake akiwemo kutoka sekta mbalimbali ili kujibu hoja za wananchi. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida
  Mwananchi akiluiza swali kuhusu mgogoro wa ardhi katika eneo la Malamba Mawili, wilayani Ubungo. Mkuu wa mkoa Paul Makonda pamoja na kutoa majibu kwa kuwataka wahusika kutoa maelezo, pia alimwalika Rais Dk John Magufuli kuzungumzoa masuala ya migogoro ya ardhi hasa kwa wanaopakana na barabara kuu katika eneo la Ubungo. Kulia ni Ofisa kutoka TANROADS ambaye hata hovyo hakuweza kutoa majibu kama ilivyotarajiwa na badala yake muulizaji alipewa ufafanuzi wa kina na Mkuu wa wilaya ya Ubungo Humphrey Polepole.
  Wananchi wakiwa wametulia wakati Rais Dk John Magufuli alipokuwa akitoa majibu kwa njia ya simu, kuhusu migogoro ya ardhi kwa wanaopakana na barabara kuu katika eneo la Ubungo
  Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Humphrey Polepole akifunga mkutano. Kushoto ni Mkuu wa Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam. Paul Makonda. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO- theNkoromo Blog

  0 0

  SHIRIKA lisilo la kiserikali la Culture and Development East Africa (CDEA) leo limezindua rasmi mradi wa Atamishi ya kazi za sanaa (IIDEA) ambapo utakuwa nguzo muhimu kwa nchi za Umoja Wa Afrika Mashariki ikiwemo Tanzania na Uganda.

  Akizungumza wakati wa uzinduzi huo mgeni rasmi, Kaimu Mkurugenzi wa Sanaa Bw.Habibu Msammy aliyemwakilisha Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye, ameeleza kuwa sanaa ni ajira hivyo mpango huo utasaidia kuinua ajira kwa wasanii watakaofikiwa na kukuza soko la Afrika Mashariki kupitia Sanaa zao.

  “Sanaa ni kazi ya kujikimu na kazi ni hutu hivyo ni wajibu wa kila msanii kujiheshimu na kufuata taratibu ili kuwa njia kwa jamii na kuheshimika zaidi hasa katika sanaa yake. Nawapongeza sana CDEA kwa mpango huu kwani utaendelea kudumisha umoja wa Afrika Mashariki, utasaidia Wasanii wetu kupanua mawazo yao zaidi na kujiongezea maarifa ya juu katika taaluma yao ya Sanaa.” Alieleza Bw. Habibu Msammy.

  Pia alisisitiza kuwa mafunzo watakayoyapata wayatumie kujiimalisha kiuchumi huku akisisitiza kuwa bado wanayo nafasi ya kujifunza zaidi katika kuweza kubuni vazi la Taifa.
  “Kwa kuwa mradi huu unagusa sanaa za Ubunifu wa mavazi, Urembo na filamu. Wabunifu wa Tanzania ni wasaha wa kuendelea kubuni vazi la Taifa, Wasanii wanaangaliwa na wengi hivyo kuanzia mavazi na mawazo yao ya ubunifu na tunawategemea pia katika kubuni vazi letu la Taifa” alieleza Habibu Msammy.

  Mradi huo wa mwaka mmoja unatarajia kuanza kutoa mafunzo kwa wabunifu wa mavazi na urembo, Wanamuziki na wasanii wa filamu.

  Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa CDEA, Bi. Ayeta Anne Wangusa amebainisha kuwa, baada ya mwezi mmoja kuanzia sasa wataanza mchakato wa kupata washiriki ambapo wahusika watatakiwa kutuma maombi ya ushiriki baada ya kuona matangazo mbalimbali yatakayotolewa na CDEA kupitia mitandao ya kijamii na sehemu zingine za Utamaduni.

  Katika uzinduzi huo, watu mbalimbali wameshiriki wakiwemo wasanii wa filamu, maigizo, wabunifu wa mavazi, wanahabari, wanamuziki na wasanii wa kazi za sanaa ikiwemo za mikono na ubunifu.
  dsc_1296
  Afisa wa Mradi wa IIDEA, Bi. Angela Kilusungu wa CDEA, akisoma taarifa fupi juu ya mradi huo mpya wa utakaosaidia sanaa kwa Afrika Mashariki
  dsc_1306
  Wajumbe wa Bodi ya Ushauri ya CDEA, wakiwa katika mkutano huo
  dsc_1316dsc_1333
  Allen Enjewele wa CDEA akifanya mahojiano katika tukio hilo
  dsc_1354
  Msanii Remigius Sostenes wa CDEA akitoa burudani katika tukio hilo
  dsc_1337
  Mwenyekiti wa Bodi wa CDEA, Mzee Madaraka Nyerere akijadiliana jambo na Mjumbe wa bodi hiyo ambaye anatokea Burundi, Bw. Gilbert Hagabimana wakati wa uzinduzo huo.
  dsc_1341
  Baadhi ya wadau wa Sanaa nchini wakijadiliana katika uzinduzi huo
  dsc_1342dsc_1346
  Mkurugenzi Mtendaji wa CDEA, Bi. Ayeta Anne Wangusa (kushoto) akijadiliana jambo na wadau wa sanaa
  dsc_1348dsc_1357
  Msanii Nick wa Pili akielezea namna sanaa inavyohitaji ubunifu wakati wa tukio hilo
  dsc_1369
  Baadhi ya wadau wa sanaa na wanahabari wakipata kujadiliana jambo
  dsc_1406
  Wadau wa sanaa wakifuatilia makala fupi ya CDEA iliyokuwa maalum wakati wa uzinduzi huo
  dsc_1408
  Uzinduzi huo ukiendelea
  dsc_1427
  Mkurugenzi Mtendaji wa CDEA, Bi. Ayeta Anne Wangusa akielezea jambo katika tukio hilo
  dsc_1433
  Mwenyekiti wa Bodi wa CDEA, Mzee Madaraka Nyerere akitoa neno na kumkaribisha mgeni rasmi
  dsc_1440
  Mgeni rasmi, Kaimu Mkurugenzi wa Sanaa Bw.Habibu Msammy aliyemwakilisha Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye akizindua rasmi mradi huo
  dsc_1434
  Mzee Kitime mmoja wa wadau wa Sanaa nchini akifuatilia kwa makini tukio hilo la uzinduzi
  dsc_1438
  Wadau wa kifuatilia uzinduzi huo
  dsc_1455dsc_1461
  dsc_1471
  cdea
  Wajumbe wa Bodi wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi mara baada ya uzinduzi wa mradi huo wa IIDEA, mapema leo Novemba 25.2016.
  PICHA ZOTE NA ANDREW CHALE</

  0 0


  Katikati Bwana Jamal Baruti Mratibu wa Baraza la Taifa na Usimamizi wa Mazingira NEMC kanda ya ziwa, akitoa adhabu kwa wamiliki wa leseni za uchimbaji mdogo wa madini wa kampuni ya Jushua Mine na Sekenke one Mine wa Sekenke, mkoani Singida, kwa kosa la uharibifu wa mazingira kwa kutumia vibaya madini aina ya zebaki katika uchimbaji wao, pembeni yake ni Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina akimsikiliza Bwana Baruti.
  Naibu Waziri ofisi ya Makamu wa Rais Mungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina akinyooshea kidole sehemu inayoonekana kuwa na maji katika ziwa Kitangiri Wilayani Iramba wakati kwa hali halisi ziwa hilo limepotea kabisa, hii ni kutokana na athari za mabadiliko ya tabia nchi.
  Sehemu ya viongozi wa Mkoa wa Singida Pamoja na wadau , Wakimsikiliza Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina hayupo Pichani katika kikao cha pamoja cha kupokea ripoti ya Mazingira ya Mkoa na kutolea ufafanunuzi baadhi ya masuala ya swala zima la usimamizi wa mazingira nchini. (Picha na Evelyn Mkokoi OMR)

  Na Evelyn Mkokoi-Singida

  Wamilki wa Leseni za uchimaji mdogo wa madini wa Joshua Mine na Sekeknke one mine wa Sekenke Mkoani Singida, wametozwa faini ya shilingi milioni 10 kila moja kwa kosa la uchafuzi wa mazingira wa kutumia vibaya madini ya zebaki, hivyo kuhatarisha maisha ya viumbe hai.

  Baraza la taifa la Hifadhi na usimamizi wa Mazingira limeitoza faini hiyo kupitia mratibuwa wa Barazakanda a Ziwa Bw. Jamali Baruti na kiwataka wamiliki hao kulipa faini hiyo ndani ya siku 14.

  Adhabu hiyo inatokana na makelele katika eneo la uchimbaji, kusambaa kwa vumbi lisilovumilika, kukosekana kwa vyoo pia na matumizi mabaya ya miti katika uchimbaji wao ambao huenda sambamba na uharifu wa misitu.Aidha Baraza limewataka wachimbaji hao kuwa na vyeti vya tathmini ya athari ya mazingira pamoja na leseni ya uchimbaji.

  Kwa Upande wake Mkuu wa Wiaya ya Mkalama Injinia Joakim Masakala akimuwaklisha mkuu wawiaya ya Iramba, alisema kuwa ni vizuri wakazi wa maeneo hayo wanavyojibidisha katika kazi lakini ni muhimu sana kuzingatia afya kwani uchimbaji wa kutumia madini aina ya zebaki bila vifaa salama kazini unaweza kuleta maradhi hususan ya saratani kwani madini hayo upenya kirahisi katika mwili wa binadamu.

  Awali Katika Kikao na uongozi wa Mkoa pamoja na wadau wa Mazingira Naibu Waziri Mpina alitolea ufafanuzi masuala mbalimbali ya Mazingira ikiwemo matumizi ya Mifuko ya plastic na kuwashauri wakazi wa singida kutunza mazingira akitolea mfano wa ziwa Kitangiri lililoo Hatarini kutoweka kabisa.

  0 0

  Uzinduzi wa siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia kanda ya kaskazini ulitanguliwa na maandamano yaliyopita katika barabara mbalimbali za mji wa Moshi na kuhitimishwa katika viwanja vya kituo kikuu cha mabasi mjini Moshi.
  Washiriki kutoka Asasi mbalimbali wakipita mbele na mabango yakiwa na ujumbe mbalimbali katika uzinduzi wa siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia kanda ya kaskazini.
  Baadhi ya viongozi wa taasisi mablimbali wakiwa wameketi meza kuu na mgeni rasmi wa uzinduzi wa siku 16 za kupinga ukatili kanda ya kaskazini Said Mecky Sadiki.
  Mwenyekiti wa Kamati ya Siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia,Elizabeth Mushi akisoma taarifa mbele ya mgeni rasmi (hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa siku 16 za kupinga ukatli wa kijinsia.
  Mwenyekiti wa Kamati ya Siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia Elizabeth Mushi akipeana mkono na Mgeni rasmi katika unzinduzi huo,Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Said Mecky Sadiki mara baada ya kutoa taarifa juu ya ukatili.
  Mkuu wa Wilaya ya Moshi Kippi Warioba akizungumza kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Said Mecky Sadiki kutoa hotuba yake wakati wa uzinduzi wa siku 16 za kupina ukatili wa kijinsia.
  Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Said Mecky Sadiki akizungumza wakati wa uzinduzi wa siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia ,uzinduzi iliofanyika katika viwanja wa vya kituo kikuu cha mabasi mjini Moshi.
  Baadhi ya washiriki katika uzinduzi huo wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi.
  Mwenyekiti wa Mtandao wa Polisi katika Shule ya Polisi Theresia Nyangasa  akisoma taarifa juu ya vitendo vya kuutali na njia zilizoanza kuchukuliwa katika kukabiliana navyo wakati wa uzinduzi wa siku 16 za kupinga ukatili kanda ya Kaskazini .
  Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Said Mecky Sadiki pamoja na Mkuu wa wilaya ya Moshi Kippi Warioba wakifuatilia taarifa juu ya ukatili wa kijinsia iliyokuwa ikitolewa na viongozi wa Asasi mbalimbali .
  Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro akitoa cheti kwa Kaimu Kamnada wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro Koka Moita cha kutambua mchango wa jeshi la Polisi katika kupamban vita dhidi ya ukatili wa kijinsia.
  Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Said Mecky Sadiki akipena mkono kabla ya kumkabidhi cheti Mwenyekiti wa Mtandao wa Polisi Wanawake (TPF Network) Grace Lyimo ,kutambua mchango wake katika vita dhidi ya ukatili wa kijinsia.
  Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Said Mecky Sadiki akipeana mkono na Mwenyekiti wa Dawati la Jinsia la Jeshi la Polisi wilaya ya Moshi,Elina Maro kabla ya kumkabidhi cheti kutambua mchango wake katika vita dhidi ya ukatili wa kijinsia.
  Mkuu wa wilaya ya Moshi,Kippi Warioba akipata maelezo kutoka kwa baadhi ya washiriki alipopita kugagua mabanda ya maonesho ya shughuli zinazofanywa na taaisisi zinazopambana na ukatili wa kijinsia.
  Mwenyekiti wa TAWREF ,Dafrosa Itemba akitoa taarifa juu ya vitendo vya ukatili wa kijinsia wakati wa uzinduzi wa siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia kwa kanda ya kaskazini uliofanyika katika viwanja vya kituo kikuu cha mabasi mjini Moshi.

  Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

  0 0

  MKUU wa wilaya ya Tunduru JUMA HOMELA akizungumza na mwandishi wa RUVUMA TV on line ambaye hayupo pichani mafanikio ya kupambana na utoro mashuleni pamoja na kutokomeza mimba mashuleni. Kwa undani wa habari hii bonyeza hiyo video.

  0 0

  Tanga, KIWANDA Cha Saruji Cha Simba Cement kimeijengea shule ya Msingi ya Kange vyumba viwili vya madara na madawati 50 pamoja na matundu mawili vya vyoo vyote vikiwa na thamani zaidi ya shilingi milioni 76.
  Msaada huo umekuja kupunguza kero ya wanafunzi kurundikana darasa moja na wengine kukaa chini jambo ambalo hupunguza ufahamu wa wanafunzi darasani.
   
  Akizungumza katika hafla fupi ya makabidhiano, Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Thobias Mwailapwa, alisema msaada huo uwe mfano kwa makampuni mengine na wadau wa elimu lengo likiwa ni kuondokana na changamoto ya  baadhi ya shule inazokabiliana nazo.
   
  Kwa upande wake, Mkuu wa Rasilimali watu kiwanda cha Saruji cha Simba Cment, Anna Malambugi, alisema kiwanda hicho moja ya sera zake ni kusaidia  jamii ikiwemo, Elimu, Afya na Mazingira.
   
  Nae Mwalimu mkuu wa Shule hiyo, Debora Danniel, alisema awali walikuwa wakiwaweka wanafunzi 120 darasa moja kufuatia uhaba wa madarasa.
  Alisema kwa msaada huo utaondosha kero ya wanafunzi kurundikana darasa moja na kuwaomba wadau wa elimu kuisaidia shule hiyo katika Nyanja mbalimbali ikiwemo miundombinu yamaji na uchakavu wa majengo.
   Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Thobias  Mwailapwa akifungua moja milango ya vyumba viwili ya madarasa shule ya msingi Kange Tanga, anaemtazama ni Afisa Fedha Pitter De Jagger na kulia ni Mkurugenzi wa jiji la Tanga, Daudi Mayeji.
   Afisa Uhusiano kiwanda cha Saruji cha Simba Cement cha Tanga, Noor Mtanga, akiwakabidhi madawati 50 wanafunzi wa shule ya msingi ya Kange pamoja na majengo mawili na vyoo vyenye matundu mawili vyote vikiwa na thamani zaidi ya shilingi milioni 76, nyuma kulia ni Mwenyekiti wa mtaa wa Kasera, Aidan Munis na kulia ni mwalimu mkuu wa shule hiyo, Debora Mzava.
  Mkuu Rasiliwamali watu kiwanda cha Saruji cha Simba Cement cha Tanga,  Anna Mwalambuji akiwakabidhi madawati 50 wanafunzi wa shule ya msingi ya Kange kufuatia uhaba wa madawati shule hiyo pompja na kuwakabidhi jengo la vyumba viwili na vyoo vyenye matundu mawili vyote vikiwa na thamani zaidi ya shilingi milioni 76.

  0 0

   Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina Pamoja na wananchi wa Mji wa Singida wakikusanya uchafu katika siku ya Usafi Kitaifa Mjini Singida.
   Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muugano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina akipeleka uchafu katika kizimba cha uchafu cha soko  kuu la Singida lililoko katika Mtaa wa Ipembe.
   Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina akiandaa mche wa mti kitalam kabla ya kuupanda katika zoezi la usafi na upandaji miti mjini Singida leo.
  Naibu Wazir Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe Luhaga Mpina Akipanda Mti aina ya Mparachichi katika eneo la Misuna Stand Mpya Mjini Singida leo katika Zezi la usafi wa mazingira Kitaifa. (Picha na Evelyn Mkokoi wa OMR)  Na Evelyn Mkokoi – Singida.

  Katika kutekeleza agizo la Serikali la usafi wa mazingira kila Jumamosi ya Mwisho wa Mwezi, wananchi wa Mkoa wa Singida wamejitokeza kwa kwingi katika zoezi hilo lililofanyika kitaifa mwezi huu mkoani humo.

  Akishiriki zoezi hilo  Mkoani Singida kitaifa, Naibu waziri Ofisi ya Makamu w Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina, ameupongeza uongozi wa Mkoa wa Singida na wana  singida kwa ujumla kwa jitihada walizoonyesha kwani kila eneo la Singida Jumamosi ya leo Limeonekana kuwa nadhifu kabla hata ya muda wa kuanza kufanya usafi tofauti na mikoa mingine ambayo amewahi kushiriki zoeZi hilo.

  Akiongea na Hadhara iliyojitokeza katika siku ya usafi Mjini Singida Leo, Mpina alisema kuwa usafi wa mazingira  unapunguza magonjwa yatokanayo na uchafu akitolea mfano ugonjwa wa kipindu pindu na hivyo taifa likiwa safi litaweza kuokoa ngumukazi yake, na kupunguza gharama ambazo zingetumika kutibu maradhi hayo.

  “Ukiona Msichana mzuri barabarani ujue kagharamiwa ukiona kijana mtanashati vilevile ujue kagharamiwa Mkiona taifa zuri na safi ujue limegharamiwa na wananchi wake wamejipanga vizuri, hivyo wana singida Muendelee kujitahidi katika suala zima la usafiwa mazingira.” Alisisitiza Mpina.

  Zoezi la usafi wa Mazingira Mkoani Singida lilienda sambamba na zoezi la upandaji miti ambapo, Naibu Waziri Mpina Pia alishiriki  na wananchi katika zoezi la kupanda miti mkoani Singida ambapo alipanda mti aina ya mpararachichi katika eneo la stand mpya ya Misuna.

  0 0

  Mkurugenzi wa Mifumo Ofisi ya Rais (TAMISEMI), Henry Katabwa ametaka Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDG’s) kuhusishwa kwenye michakato ya maendeleo ya serikali za mitaa, hasa kwenye programu zinazotekelezwa kwenye ngazi za chini kabisa ambapo ndiko wananchi wenye hali duni kimaendeleo wanapatikana. 
   
  Kauli hiyo aliitoa wakati akifunga warsha ya malengo ya maendeleo endelevu kwa Maafisa Maendeleo ya Jamii na Mipango kutoka mikoa saba ya kanda ya ziwa. Alisema malengo 17 ya maendeleo endelevu (SDGs) yamehusishwa kwenye mpango wa maendeleo wa miaka mitano hivyo ni vyema kuhakikisha hata katika ngazi za chini utekelezaji wa program unazingatia malengo hayo.
   
   “Kuna haja ya kuhakikisha kwamba, shabaha ya malengo haya inahusishwa kwenye michakato ya maendeleo ya serikali za mitaa na hasa kwenye miradi ya program zinazotekelezwa kwenye ngazi za chini kabisa, ambako ndiko wananchi wenye hali duni ya kimaendeleo wanapatikana” alisema .
  Mwenyekiti wa warsha ya siku tatu ya Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) kwa Maafisa Maendeleo ya Jamii na Mipango nchini ambaye pia ni Katibu Tawala Msaidizi idara ya Mipango na Uratibu mkoa wa Mara, Eldom Anyosisye akitoa neno la ukaribisho wakati wa kufunga warsha ya siku tatu ya Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) kwa Maafisa Maendeleo ya Jamii na Mipango nchini iliyomalizika mwishoni wa juma mjini Dodoma chini ya ufadhili wa Shirika UNDP.

  Pia alisema serikali kupitia Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa kushirikiana na mradi wa uimarishaji wa wa sekta ya umma inaendelea kuboresha mfumo wa ukusanyaji takwimu ili uweze kukusanya takwimu katika ngazi zote za serikali za mitaa ili zitumike kuandaa mipango ya maendeleo. 
   
  Akisoma maazimio kwa niaba ya washiriki wa warsha hiyo, Afisa Mipango wa wilaya ya Kyerwa mkoani Kagera, Innocent Maduhu alisema sheria ya Bajeti ya mwaka 2015 izingatiwe na kila mhusika atekeleze wajibu na majukumu yake. Pia yafanyike mapitio ya mgawanyo na matumizi ya fedha za mapato ya ndani kwa lengo la kupata uhalisia sambamba na kuweka mkazo katika kutafuta rasilimali kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya Maendeleo.
  Mkurugenzi wa Kupunguza Umaskini na Kuinua Uchumi kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Anna Mwasha akizungumza jambo kabla ya mgeni rasmi kufunga warsha hiyo iliyomalizika mwishoni mwa wiki mjini Dodoma.

  Aidha wajumbe hao waliazimia kila sekta iwezeshwe vitendea kazi na rasilimali muhimu ili ziweze kutimiza majukumu yake pia mifumo ya upangaji mipango na utoaji taarifa ihuishwe ili iendane na Malengo ya Maendeleo Endelevu. Pia wametaka yafanyike mafunzo rejea ya mifumo kwa watumishi na kwa wakati na rasilimali katika sekta ya Kilimo ziongezwe kwa lengo la kuongeza na kuboresha uzalishaji na kupata malighafi kwa ajili ya viwanda. 
   
  Sambamba na halmashauri zote kuboresha mifumo ya ukusanyaji mapato na kubuni vyanzo vipya pamoja na kudhibiti mapato na matumizi, uwepo mpango au mkakati maalumu wa kuendeleza Mikoa na Halmashauri zilizopo nyuma kimaendeleo. “Mbinu za uibuaji na upangaji wa miradi ya maendeleo kutoka ngazi ya chini ufanyike upya katika halmashauri zote” alisema Maduhu.
  Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Mifumo Ofisi ya Rais (TAMISEMI), Henry Katabwa akitoa hotuba ya kufunga warsha ya siku tatu ya Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) kwa Maafisa Maendeleo ya Jamii na Mipango nchini iliyomalizika mwishoni wa juma mjini Dodoma chini ya ufadhili wa Shirika UNDP.
  Afisa Mipango wa wilaya ya Kyerwa, mkoani Kagera, Innocent Maduhu akiwasilisha maazimio ya warsha ya SDGs yaliyoandaliwa na Maafisa Maendeleo ya Jamii na Mipango nchini mbele ya mgeni rasmi (hayupo)wakati wa hafla ya kufunga warsha ya siku tatu iliyomalizika mwishoni mwa wiki mjini Dodoma chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP)
  Meza kuu ikifuatilia kwa makini maazimo ya SDGs yaliyoazimiwa na Maafisa Maendeleo ya Jamii na Mipango nchini wakati wa hafla fupi ya kufunga warsha hiyo ya siku tatu iliyomalizika mwishoni mwa juma mjini Dodoma, kutoka kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi OR-TAMISEMI, Injinia Enock Nyanda, mgeni rasmi Mkurugenzi wa Mifumo Ofisi ya Rais (TAMISEMI), Henry Katabwa na Mkurugenzi wa Kupunguza Umaskini na Kuinua Uchumi kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Anna Mwasha.

  Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Mifumo Ofisi ya Rais (TAMISEMI), Henry Katabwa akizungumza na Maafisa Maendeleo ya Jamii na Mipango nchini walioshiriki warsha ya siku tatu ya SDGs wakati wa hafla fupi ya kufunga warsha hiyo iliyomalizika mjini Dodoma mwishoni mwa juma.
  Mkurugenzi Msaidizi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Shomari Maknandi akiwasilisha mada kuhusu Ugatuzi wa madaraka (D by D) na utoaji wa huduma kwa wananchi kwenye warsha ya siku tatu ya Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) kwa Maafisa Maendeleo ya Jamii na Mipango nchini iliyomalizika mwishoni wa juma mjini Dodoma chini ya ufadhili wa UNDP.
  Afisa Mipango wa Halmashauri ya Kibondo mkoani Kigoma, Anganile Mwasongwe akiwasilisha maoni wakati wa hafla fupi ya kufunga warsha ya kufunga warsha ya siku tatu ya Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) kwa Maafisa Maendeleo ya Jamii na Mipango nchini iliyomazika mjini Dodoma mwishoni mwa wiki chini ya ufadhili wa Shirika la UNDP.
  Afisa Maendeleo ya Jamii Mwandamizi Manispaa ya Bukoba, Richard Salu akichangia maoni wakati wa kuwasilisha maazimio ya SDGs kwa mgeni rasmi (hayupo pichani) wakati wa hafla fupi ya kufunga warsha ya siku tatu ya Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) kwa Maafisa Maendeleo ya Jamii na Mipango nchini iliyomazika mjini Dodoma mwishoni mwa wiki iliyofadhiliwa na Shirika la UNDP.
  Pichani juu na chini ni Maafisa Maendeleo ya Jamii na Mipango nchini walishiriki warsha ya siku tatu ya Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) iliyomalizika miwshoni mwa juma mjini Dodoma.  Baadhi ya wafanyakazi wa Wizara ya Fedha na Mipango ambao ndio waratibu wa warsha hiyo.
  Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Mifumo Ofisi ya Rais (TAMISEMI), Henry Katabwa akiondoka katika ukumbi wa mikutano wa Hazina ndogo baada ya kufunga warsha hiyo

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akizungumza na wananchi wa Kata ya Msigani mtaa wa Temboni juu ya watendaji wote wa Kata kuwa na taarifa zote za miradi ya maendeleo vinginevyo atawachukulia hatua stahiki leo jijini Dar es salaam.
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akimsikila Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Humphrey Polepole  alipokuwa akitolea ufafanuzi kuhusu mradi wa maji huo
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akikangua mradi wa maji ambao ulikuwa ukiratibiwa na kamati ya maji ya Mtaa ambapo ulionesha mapungufu na kwasasa mradi huo unasimamiwa na Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka DAWASCO
  Mkazi wa Mtaa wa Temboni, Moroen Goube akifafanua jambo katika ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda leo jijini Dar es Salaam. Picha na Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii.
  Wananchi wa Mtaa wa Temboni wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda leo jijini Dar es Salaam.

  Ikiwa ni muendelezo wa ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ambapo leo ni siku ya nane tangu aanze ziara hiyo, akiwa katika ziara yake ndani ya Wilaya ya Ubungo Kata ya Msigani mtaa wa Temboni RC Makonda ametoa agizo kwa Watendaji Kata wote katika Mkoa wake.

  RC Makonda amewataka watendaji wote wa Kata kuwa na taarifa zote za miradi ya maendeleo vinginevyo atawachukulia hatua stahiki.
  "Sitaki Kumkuta Mtendaji yeyote wa Kata ambaye hajui jambo lolote kwenye kata yake" Alisema RC Makonda. 

  Ambapo amemtolea mfano mzuri Mkuu wa Wilaya hiyo Humphrey Polepole kwa kuwa na taarifa mbalimbali kuhusu miradi ya maendeo na kuwaomba waige kutoka kwake.

  Pia RC Makonda amemuagiza RPC Mkoa wa kipolisi Kinondoni Suzan Kaganda kwa kushirikiana na TAKUKURU kumshikilia na kumfanyia uchunguzi aliyekuwa Mtendaji wa Kata hiyo Neema Kalumbe ambaye kwa sasa ni Mtendaji wa Kata ya Makongo kujibu tuhuma za ubadhirifu wa fedha za mradi wa Barabara ya kutokea Msuguri na Msingwa ambao ulitengewa milioni 17 na hakuna barabara iliyojengwa. 

  Katika hatua nyingine RC Makonda amemtaka mwenyekiti wa wa Mtaa huo wa Msigani Israel Mushi kutofanya kazi kwa upendeleo kwani kuna Mkazi aliyefahamika kwa jina la Maureen Gomba ambaye amelalamikia kuwa mwenyekiti huyo amekuwa akigawa vizimba kwa watu anaowafahamu. 

  RC Makonda amewatoa hofu wakazi hao kuhusu huduma ya maji na kwani kwasasa mradi huo upo chini ya Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka DAWASCO, huku Mkuu wa Wilaya hiyo akihaidi kukutana na wananchi hao ili kumaliza kero hiyo kabisa ifikapo Desemba 21.

  0 0

   Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Angella Kairuki akimkabidhi cheti cha kuhitimu mafunzo ya uchunguzi Afisa Uchunguzi wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa umma Edson Kamugisha. Hafla hiyo ilifanyika katika Chuo cha maafisa wa Jeshi la Polisi Kidatu, Mkoani Morogoro jana.
   Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Angella Kairuki akimkabidhi cheti cha kuhitimu mafunzo ya uchunguzi Katibu Msaidizi  wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa umma Evodia Pangani. Hafla hiyo ilifanyika katika Chuo cha maafisa wa Jeshi la Polisi Kidatu, Mkoani Morogoro jana. 
   Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Angella Kairuki akimkabidhi cheti cha kuhitimu mafunzo ya uchunguzi Katibu Msaidizi  Kanda ya Mashariki wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa umma Eritrudi Cyliacus Ishengoma. Hafla hiyo ilifanyika katika Chuo cha maafisa wa Jeshi la Polisi Kidatu, Mkoani Morogoro jana.
   
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Angella Kairuki akimkabidhi cheti cha kuhitimu mafunzo ya uchunguzi Katibu Msaidizi  Kanda ya Mashariki wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa umma Eritrudi Cyliacus Ishengoma. Hafla hiyo ilifanyika katika Chuo cha maafisa wa Jeshi la Polisi Kidatu, Mkoani Morogoro jana.

  0 0

  Wachezaji wa timu ya soka ya Vodacom Tanzania, Voda Stars, Mbisso Ephram (kushoto), Gabby Magori na Astrid Mapunda (kulia),wakimbana mchezaji wa timu ya  Jipange Venture,Rajabu Juma ( wa pili kulia) kwenye mechi ya kirafiki katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam leo Novemba 26, 2016. Voda Stars ilishinda 1-0.
   Mshambuliaji wa Jipange Venture, Rajabu Juma ( kulia) akijaribu kuiwatoka wachezaji wa timu ya soka ya Vodacoma Tanzania, Voda Stars, Mbisso Ephram (kushoto) na Gabby Magori kwenye mechi ya kirafiki katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam leo Novemba 26, 2016. Voda Stars ilishinda 1-0.
   Mchezaji wa timu ya soka ya Vodacom Tanzania, Voda Stars,  Gabby Magori (kushoto)  akichuana na Shaaban  Abdi wa  timu ya  Jipange Venture, kwenye mechi ya kirafiki katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam leo Novemba 26, 2016. Voda Stars ilishinda 1-0. 
   Mfungaji wa goli pekee la timu ya soka ya Vodacom Tanzania, Voda Stars, Astrid  Mapunda akishangilia bao lake wakati timu yake ilipocheza na timu  Jipange Venture, kwenye mechi ya kirafiki katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam leo Novemba 26, 2016. Voda Stars ilishinda 1-0.
  Wakiwa katika picha ya pamoja ni kikosi cha timu ya soka ya Vodacom Tanzania, Voda Stars iliyocheza kwenye mechi za kirafiki katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam leo Novemba 26, 2016.

  0 0   Mkuu wa Chuo UDOM ambaye ni Rais Mstaafu Benjamin Mkapa akitunuku Shahada ya Uzamivu(PHD)Ombeni Msuya katika mahafali ya saba ya chuo hicho.
   Mkuu wa Chuo UDOM ambaye ni Rais Mstaafu Benjamin Mkapa akitunuku Shahada mbalimbali katika mahafali ya saba ya chuo hicho.
   Wahitimu wa Mahafali ya saba ya Chuo cha Udom.
  Wahitimu wa Shahada ya Uzamili katika Chuo cha Udom wakiwa katika nyuso za furaha baada ya kuhitimu.


  RAIS mstaafu katika serikali ya Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa, amempongeza Rais wa Awamu iliyopita, Jakaya Kikwete, kwa kuthubutu na kuwezesha ujenzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom).

  Akizungumza katika mahafali ya saba ya chuo hicho, alisema Maono ya chuo hicho yalianza na serikali zote tatu ikiwamo aliyoiongoza lakini hakuweza kuthubutu.

  “Nampongeza mzee Kikwete kwa kuweza kuthubutu na kufanikisha ujenzi wake na leo tupo hapa.Mradi wa ujenzi wa chuo hichi, uliafikiwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) tangu utawala wa Rais wa Awamu ya Kwanza, Hayati Julius Nyerere, Ali Hassan Mwinyi (awamu ya pili) na kisha mimi lakini wote hatukuweza kuthubutu,”alisema Mkapa.

  Kadhalika, Rais Mkapa alishauri Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ikutane na kufanya mazungumzo na Vyuo Vikuu vinavyomilikiwa na Serikali ili kuchambua matatizo yanayotokea mara kwa mara. Alisema ni vyema uwepo mkutano wa wenyeviti wa vyuo hivyo ili kufahamu gharama wanzotumia kwa ajili ya uendeshaji wake.

  Hata hivyo alibainisha idadi ya wanachuo kila kukicha inaongezeka na nakusababisha vyuo hivyo kushindwa kujiendesha, hivyo jambo bora ni kukutana kwa wenyeviti hao na kujadiliana kuhusu gharama za uendeshaji wake.

  Hata hivyo alisema kutoa amri na maagizo kwa wanachuo kila wakati, si suluhisho la kumaliza migogoro vyuoni, lakini pale wenyeviti wa Vyuo Vikuu vyote wakikutana pamoja na kufahamu gharama zao za uendeshaji, kuna uwezekano wa kutatua kero zote.

  Naye makamu Mkuu wa Chuo hicho, Prof, Idris Kikula, alisema wahitimu hao wanakabiliwa na changamoto ya upatikanaji ajira ambayo kwa sasa imekuwa tishio duniani huku akiwashauri kujiajiri na kuacha kutegemea ajira serikalini kutokana na tatizo hilo kuwa la kidunia.

  0 0
  Baadhi ya akinamama waliofika Hospitali ya Mnazimmoja kufanyiwa uchunguzi wa saratani ya matiti wakipata maelekezo kutoka kwa mhudumu wa hospitali hiyo.
  Mkurugenzi wa Ilala Afya Centre ya Dar es salaam Jaffer Dharsee (kulia) akibadilishana mawazo na viongozi wa Jumuiya ya watu wanaoishi na saratani Zanzibar (ZCA) ambapo taasisi hizo mbili kwa kushirikiana na Wizara ya Afya zimeandaa kampeni hiyo.
  Dak. Nalvis Dominguez Torres akimfanyia uchunguzi wa maradhi ya saratani ya matiti mmoja wa akinamama waliofika Hospitali ya Mnazimmoja kwa ajili ya uchunguzi wa maradhi hayo.
  Daktari bingwa wa uchunguzi wa maradhi ya saratani Zanzibar Msafiri Marijani akichukua sampuli kutoka kwa mmoja wa akinamama waliofika Hospitalini hapo kwa ajili ya uchunguzi wa saratani.
  Mkurugenzi wa Ilala Afya Centre ya Dar es salaam Jaffer Dharsee akitoa maelekezo kwa akinamama waliofanyiwa uchunguzi wa saratani ya matiti katika kampeni iliyoandaliwa kwa ushirikiano wa kituo hicho, Wizara ya Afya na ZCA. icha na Makame Mshenga/Maelezo Zanzibar.  Na Ramadhani Ali/Maelezo Zanzibar

  26.11.2016

  Zaidi ya wanawake 500 wamefanyiwa uchunguzi wa saratani ya matiti iliyoandaliwa kwa ushirikiano wa Jumuiya ya watu wanaoishi na maradhi hayo (ZCA), Ilala Afya Centre ya Dar es salaam na Wizara ya Afya Zanzibar.

  Kampeni hiyo ya siku moja iliyofanyika Hospitali kuu ya Mnazimmoja iliwashirikisha akinamama wenye umri kuanzia miaka 25 ilikuwa na lengo la kuweza kuwagundua mapema akinamama wenye tatizo la maradhi hayo ambayo dalili zake zinachelewa kujitokeza.

  Daktari bingwa wa uchunguzi wa maradhi ya saratani Zanzibar ambae pia ni Mwenyekiti wa ZCA Dkt. Msafiri Marijani amesema kampeni hiyo ilihusisha uchunguzi wa Utrasound na uchunguzi wa sindano na waliopatikana na dalili watafanyiwa vipimo ili kujua kama ni saratani ama matatizo mengine.

  Dkt. Marijani amekumbusha kuwa saratani hadi hivi sasa haina tiba na kitu muhimu ni kuigundua mapema ili kuidhibiti kabla haijaleta athari kubwa hivyo amewashauri wananchi kupima afya zao mara kwa mara.

  “Saratani ni maradhi yanayouwa watu wengi duniani kutokana na kuchelewa kugundulika mapema, kitu muhimu ni wananchi kujenga utamaduni wa kuchunguza afya zao,” alisisiti Dkt. Marijani.Amesema Hosipitali zote za Wiala na vituo vingi vya Afya vya vijijini vinatoa huduma ya uchunguzi wa saratani hivyo amewashauri wananchi kuvitumia.

  Kiongozi wa Jumuiya ya watu wanaoishi na maradhi ya saratani Zanzibar Bi. Zakia Mohd amesema kufuatia uchunguzi huo ambapo zaidi ya wanawake 100 wamebainika kuwa na dalili za saratani, wamegundua kuwa tatizo ni kubwa kinyume na walivyo fikiria awali.Amesema kutokana na hali hiyo ZCA itafikiria kununua chombo maalumu cha uchunguzi ‘mamography’ ambacho kinauwezo wa kugundua dalili za awali kabisa za maradhi hayo.

  Ameongeza kuwa Jumuiya imeazimia kufanya uchunguzi mwengine wa saratani ya shingo ya kizazi na saratani ya tenzi dume katika siku zijazo kwa vile ni miongoni mwa maradhi yanayowasumbuwa wananchi wengi wa Zanzibar. Mwisho

  IMETOLEWA NA MAELEZO ZANZIBAR.

  0 0

   Rais mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi akiwatunuku wahitimu wa kozi mbalimbali katika mahafali ya Chuo Kikuu cha Kampala cha jijini Dar es Salaam kwenye sherehe za mahafali.
   Baadhi ya waadhiri wa chuo hicho wakiwa kwenye mahafali hayo.
   Rais mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi (kushoto) na mgeni rasmi katika mahafali ya Chuo Kikuu cha Kampala cha jijini Dar es Salaam akiteta jambo na Makamu Mkuu wa chuo hicho, Profesa Muhammad Ndaula katika mahafali hayo yaliyofanyika jana.
   Baadhi  ya wahitimu wa ngazi ya digree kozi ya afya wakila kiapo cha kuhitimu fani hiyo.
   Sehemu ya wahitimu wakiwa katika mahafali hayo.
   Sehemu ya wahitimu wakiwa katika mahafali hayo.
   Sehemu ya wakufunzi na wahitimu wa Chuo Kikuu cha Kampala wakiwa kwenye mahafali.

  Mahafali yakiendelea


  Msafara wa mahafali ukiongozwa na Rais msaafu wa Awamu ya Pili, Mwinyi mara baada ya sherehe za mahafali ya nne ya Chuo Kikuu cha Kampala (KIU) cha jijini Dar es Salaam.kumalizika.

  RAIS mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi amewataka wahitimu wa vyuo vikuu nchini kuacha tabia ya kuchagua kazi za kufanya mara baada ya kuhitimu elimu yao. Mwinyi alisema tabia hiyo imepitwa cha wakati hasa katika dunia ya sasa yenye changamoto kubwa ya ajira.

  Rais Mwinyi alitoa kauli hiyo juzi wakati akizungumza na wahitimu wa kozi mbalimbali kwenye sherehe za mahafali ya nne ya Chuo Kikuu cha Kampala (KIU) cha jijini Dar es Salaam.

  Alisema kitendo cha baadhi ya wahitimu hasa wa vyuo vikuu kupendelea kuchagua kazi za kufanya kimekuwa kikiwapotezea muda na fursa anuai, hivyo kuwataka kuacha tabia hiyo ambayo kwa kipindi hiki imepitwa na wakati.Alisema wahitimu hawana budi kuanza kufanya kazi zozote zinazojitokeza mbele yao na kutumia fursa hiyo kuelekea kwenye mafanikio kadri walivyojipangia katika  maisha yao. 

  "...Nawapongeza wahitimu kwa hatua hii, sasa mnaingia katika maisha mapya na ya vitendo msiende kuchagua kazi za kufanya, anza na kazi yoyote inayojitokeza mbele  yako kisha uitumie kutimiza ndoto zako," alisema katika hotuba yake kwa wahitimu hao.

  Aidha Rais huyo mstaafu aliwataka wahitimu hao kuwa wachapakazi, wabunifu na kutumia ipasavyo ujuzi na elimu waliopewa katika ngazi mbalimbali ili  kuweza kuisaidia jamii na taifa kwa ujumla. 

  Alisema kuwa Serikali ya Tanzania imejipanga kuhakikisha wanafunzi wote wenye sifa na vigezo vya kujiunga na chuo wanapata nafasi hiyo bila vikwazo kupitia  Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu nchini (HESLB). 

  Akihimiza matumizi ya lugha ya Kiswahili hasa kufundisha programu katika vyuo vikuu, Mwinyi alivitaka vyuo vikuu kuanza kufundisha programu za lugha hiyo ili kuchochea matumizi yake kama yanavyofanya mataifa mengine kwenye vyuo vyao iwemo China, Urusi, USA, Iran na mengineyo.

  Alisema Afrika lazima iwe na lugha moja ya kuwaunganisha watu wake na lugha pekee inayozungumzwa na mataifa mengi ya Afrika ni Kiswahili hivyo kuna kila sababu ya kujivunia lugha hiyo na kuitumia ipasavyo. "...Naahidi katika mahafali yajayo nitatoa hotuba yangu kwa lugha ya Kiswahili na salamu zangu zote nitazitoa kwa kiswahili," alisema Mwinyi.

  Awali akizungumza katika mahafali hayo, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kampala (KIU), Profesa Ndaula Muhammad alisema jumla ya wahitimu 1079 wamehitimu masomo yao katika ngazi ya Shahada, Stashahada na Asatashahada katika fani mbalimbali.

older | 1 | .... | 1050 | 1051 | (Page 1052) | 1053 | 1054 | .... | 1903 | newer