Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46343 articles
Browse latest View live

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AKUTANA NA KATIBU MKUU WA CCM ,NDUGU KINANA JIJINI DAR LEO

$
0
0



Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikarishwa na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana alipofika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba Dar es Salaam, kwa ajili ya mazungumzo na Katibu mkuu huyo wa CCM, leo.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongozwa na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana kwenda eneo la kufanyia mazungumzo, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam.


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisaini kitabu cha wageni baada ya kuwasili Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba Dar es Salaam, kwa ajili ya mazungumzo na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungmza na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, leo katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO- theNkoromo Blog

VIJANA WAJASILIAMALI KUTOKA MIKOA MBALIMBALI YA TANZANIA WATEMBELEA SIDO DAR KUJIFUNZA UZALISHAJI

$
0
0
 Mbunifu wa Shirika la kuhudumia Viwanda vidogo Sido, Zacharia Maziku, akiwaonyesha baadhi ya vijana wajasiliamali jinsi ya kuandaa na kutengeneza Jora la Kitambaa wakati Vijana hao walipotembelea kujionea kazi na uzalishaji wa Shirika hilo jana Nov 24, 2016, wakiwa katika zaiara ya mafuzo yaliyoandaliwa na Shirika lisilo la Kiserikali la The Foundation for Civil Cociety kwa kushirikiana na Tanzania Women Chambers of Commerce (TWCC). Mafunzo hayo yanamalizika rasmi hii leo kwenye Hoteli ya Blue Pearl Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam.  Picha na Mafoto Blog
 Mbunifu wa Shirika la kuhudumia Viwanda vidogo Sido, Zacharia Maziku, akiwaonyesha baadhi ya vijana wajasiliamali jinsi ya kuandaa na kutengeneza Jora la Kitambaa wakati Vijana hao walipotembelea kujionea kazi na uzalishaji wa Shirika hilo jana Nov 24, 2016, wakiwa katika zaiara ya mafuzo yaliyoandaliwa na Shirika lisilo la Kiserikali la The Foundation for Civil Cociety kwa kushirikiana na Tanzania Women Chambers of Commerce (TWCC). Mafunzo hayo yanamalizika rasmi hii leo kwenye Hoteli ya Blue Pearl Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam. 
 Baadhi ya vijana wakiangalia jinsi Jora linavyotengenezwa.....
 Meneja Uzalishaji wa Shirika la kuhudumia Viwanda vidogo Sido, Laurent Mwaisamila, akiwaonyesha baadhi ya vijana wajasiliamali jinsi ya kuandaa na kutengeneza Jora la Kitambaa wakati Vijana hao walipotembelea kujionea kazi na uzalishaji wa Shirika hilo jana Nov 24, 2016, wakiwa katika zaiara ya mafuzo yaliyoandaliwa na Shirika lisilo la Kiserikali la The Foundation for Civil Cociety kwa kushirikiana na Tanzania Women Chambers of Commerce (TWCC). Mafunzo hayo yanamalizika rasmi hii leo kwenye Hoteli ya Blue Pearl Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam. 
 Meneja Uzalishaji wa Shirika la kuhudumia Viwanda vidogo Sido, Laurent Mwaisamila, akiwaonyesha baadhi ya vijana wajasiliamali jinsi ya kuandaa na kutengeneza Jora la Kitambaa wakati Vijana hao walipotembelea kujionea kazi na uzalishaji wa Shirika hilo jana Nov 24, 2016, wakiwa katika zaiara ya mafuzo yaliyoandaliwa na Shirika lisilo la Kiserikali la The Foundation for Civil Cociety kwa kushirikiana na Tanzania Women Chambers of Commerce (TWCC). Mafunzo hayo yanamalizika rasmi hii leo kwenye Hoteli ya Blue Pearl Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam. 
 Meneja Uzalishaji wa Shirika la kuhudumia Viwanda vidogo Sido, Laurent Mwaisamila, akiwaonyesha baadhi ya vijana wajasiliamali jinsi ya kuandaa na kutengeneza Jora la Kitambaa wakati Vijana hao walipotembelea kujionea kazi na uzalishaji wa Shirika hilo jana Nov 24, 2016, wakiwa katika zaiara ya mafuzo yaliyoandaliwa na Shirika lisilo la Kiserikali la The Foundation for Civil Cociety kwa kushirikiana na Tanzania Women Chambers of Commerce (TWCC). Mafunzo hayo yanamalizika rasmi hii leo kwenye Hoteli ya Blue Pearl Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam. 
 Meneja Uzalishaji wa Shirika la kuhudumia Viwanda vidogo Sido, Laurent Mwaisamila, akiwaonyesha baadhi ya vijana wajasiliamali jinsi ya kuandaa na kutengeneza Jora la Kitambaa wakati Vijana hao walipotembelea kujionea kazi na uzalishaji wa Shirika hilo jana Nov 24, 2016, wakiwa katika zaiara ya mafuzo yaliyoandaliwa na Shirika lisilo la Kiserikali la The Foundation for Civil Cociety kwa kushirikiana na Tanzania Women Chambers of Commerce (TWCC). Mafunzo hayo yanamalizika rasmi hii leo kwenye Hoteli ya Blue Pearl Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam. 
 Meneja Uzalishaji wa Shirika la kuhudumia Viwanda vidogo Sido, Laurent Mwaisamila, akiwaonyesha baadhi ya vijana wajasiliamali jinsi ya kuandaa na kutengeneza Jora la Kitambaa wakati Vijana hao walipotembelea kujionea kazi na uzalishaji wa Shirika hilo jana Nov 24, 2016, wakiwa katika zaiara ya mafuzo yaliyoandaliwa na Shirika lisilo la Kiserikali la The Foundation for Civil Cociety kwa kushirikiana na Tanzania Women Chambers of Commerce (TWCC). Mafunzo hayo yanamalizika rasmi hii leo kwenye Hoteli ya Blue Pearl Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam. 

 Vijana hao wakiwa katika Viwanja vya Sido baada ya kuwasili
 Baadhi ya Vijana wakiangalia moja ya bidhaa zinazozalishwa katika Shirika hilo na Mwalimu wao, 
 Vijana hao wakiwa katika kiwanda cha kuzalisha Majora kwa mafunzo
 Mafunzo na maelekezo ya kutumia mashine kuzalisha Majora yakiendelea
 Maelekezo yakiendelea.......
 Wengine wakijiselfie kiwandani hapo kwa kumbukumbu....
 Msimamizi wa Mashine za Shirika hilo, Mlagani Keneth, akitoa maelekezo kwa vijana hao.
 Vijana wakiwa bize kufuatilia maelekezo ya kutumia mashine hizo
 Vujana wakimsikiliza Mkurugenzi wa Kampuni ya EFA Production Solutions Ombeni Selestine, wakati wakilitembelea Ofisi yake jana.
 Mkufunzi Mwajuma Hamza, akitoa maelekezo kwa vijana hao kabla ya kuanza ziara hiyo katika kiwanda cha Mjasiliamali Ombeni Selestine.
 Vujana wakimsikiliza Mkurugenzi wa Kampuni ya EFA Production Solutions Ombeni Selestine, wakati wakilitembelea Ofisi yake jana.
 Vujana wakimsikiliza Mkurugenzi wa Kampuni ya EFA Production Solutions Ombeni Selestine, wakati wakilitembelea Ofisi yake jana.
 Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya EFA Production wakijaza Lotion katika makopo kwa kutumia mikono tayari kwa kupaki katika maboksi na kuuzwa.
  Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya EFA Production wakipanga bidhaa katika maboksi baada ya kujazwa.
 Vijana wakiwa kiwandani hapo
  Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya EFA Production wakijaza Lotion katika makopo kwa kutumia mikono tayari kwa kupaki katika maboksi na kuuzwa.
 Vijana Wajasiliamali wakiangalia jinsi mfanyakazi wa EFA Production anavyobandika lebo lakitika kifungashio.
 Mmoja kati ya vijana wajasiliamali akijaribu kwa vitendo kubandika Lebo baada ya kuelekezwa.
 Wakiangalia vifungashio.
 Selfiepia zilihusika pande hizo....
 Wakiangalia Viti vinavyotengenezwa kwa Mkeka.....
 Wakiangalia Kikapu kilichotengenezwa kiwandani hapo
Fundi wa Mshine za kukamua miwa, Marry Gerald, akitoa maelezo kwa Vijana hao kuhusu utengezaji na ufanyaji kazi wa Mashine hizo.
 Mfanyakazi wa Sido, Jonathan akizungumza na Vijana hao wakati walipotembelea Shirika hilo kwa mafunzo.
 Vijana wakizungumza na mafundi wa Daria Disgn walipotembelea Ofisi hiyo iliyopo Upanga jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa Daria Disgn, Daria Makaramba akizungumza na vijana hao walipotembelea Ofisi yake kwa mafunzo jana.
 Vijana wakipiga picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Daria Disgn baada ya mafunzo.
Picha ya kumbukumbu.

TATIZO LA UMEME DAR KUTATULIWA.

$
0
0
Na Beatrice Lyimo-MAELEZO.

SERIKALI imedhamiria kuimarisha mtandao wa usafirishaji na usambazaji umeme nchini ili kufikia malengo ya taifa ya asilimia 75 ya watanzania wanaonufaika na huduma ya umeme ifikapo 2025.

Katika kutimiza azma hiyo, hivi karibuni Serikali kupitia Shirika la ugavi la umeme Tanzania (TANESCO) imezindua mradi wa uboreshaji wa huduma za umeme jijini Dar es salaamu uliobuniwa kwa lengo la kuboresha Miundombunu ya Usafirishaji na usambazaji umeme katika jiji la Dar es salaam.

Mradi huo umetokana na ongezeko la wahitaji wa huduma ya umeme katika Jiji la Dar es Salaam ambapo mradi huo utasaidia katika kuimarisha upatikanaji wa umeme wa uhakika na hivyo ku0vutia wawekezaji wapya katyika sekta za viwanda.

Akizindua Mradi huo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alisema kuwa Serikali kupitia Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) imekuwa katika jitihada mbalimbali za kuboresha miundombinu yake ili iweze kuwafikia wananchi wengi na katika ubora unaohitajika.

“Mradi huu wa kuboresha miundombinu ya umeme unalenga kuimarisha upatikanaji wa huduma ya umeme wa uhakika katika jiji la Dar es Salaam” anasema Majaliwa.Anasema mradi huo utafungua fursa nyingi za uzalishaji na kupelekea upatikanaji wa fursa za ajira za uhakika kwa wananchi.

Aidha, Waziri Mkuu anasema kuwa upatikanaji wa Umeme wa uhakika utaiwezesha nchi kufikia uchumi wa kati kupitia viwanda ikiwa ni lengo la Serikali ya Awamu ya Tano.Naye Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO Mhandisi. Felchesmi Mramba alisema kuwa Mradi huo umetumia jumla ya Shilingi bilioni 74.6, ikiwa ni fedha kutoka Serikali ya Finland kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania.

“mradi huu unafadhiliwa na Serikali ya Finland ambapo wametoka kiasi cha Tsh. Bilioni 63.56 sawa na asilimia 94.3 pamoja na Serikali imetoa kiasi cha Tsh. Bilioni 11.03 ikiwa ni asilimia 5.7.Mhandisi Mramba anaongeza kuwa mradi huo utasaidia kuvutia wawekezaji wapya katika sekta za viwanda na biashara nchini ili kuchochea ukuaji wa Sekta ya Viwanda vilivyopo kutokana na uwepo wa nishati hiyo inayokidhi mahitaji ya jamii.

Katika hatua hiyo, Mhandisi Mramba alibainisha baadhi ya miradi iliyohusisha Mradi huo ikiwa ni pamoja na ujenzi wa kituo kipya cha kupoza umeme cha kV 132/33/2x50MVA cha City Center, ujenzi wa kituo cha udhibiti mifumo ya usambazaji umeme katika msongo wa kV 33 na kV 11.

Akifafanua zaidi anasema miradi mingine ni pamoja na ujenzi wa njia ya umeme chini ya ardhi kwa ajili ya kuunganisha vituo vya Kariakoo, Railway na Sokoine mpaka kituo cha zamani cha city center.

Sambamba na hilo anasema kuwa, miradi mingine ya uboreshaji umeme inayoendelea jijini Dar es salaam ni mradi wa TEDAP unauhusisha uboreshaji wa miundombinu ya usafirishaji na usambazaji umeme katika maeneo mbalimbali ya jiji hilo na Mikoani, ikiwemo maeneo ya Gongolamboto, Kipawa, Kurasini, Chang’ombe, Mbagala, Ubungo, Mburahati, eneo la uwanja wa ndege KIA, pamoja na Mikoa ya Kilimanjaro na Arusha.

Aidha alisema kuwa mradi wa ukarabati na uboreshaji miundombinu ya umeme jijini Dar es salaam katika maeneo ya Ilala, Jangwani Beach, Kunduchi, Mwananyamala, Muhimbili na Msasani unatekelezwa na Serikali ya Tanzania kupitia TANESCO kwa kushirikiana na Serikali ya Japan kupitia JICA unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi Februali mwaka 2017.

Mhandisi Mramba alisema kuwa Miradi hiyo ya usafirishaji umeme na usambazi umeme inatekelezwa sambamba na miradi mikubwa ya ufuaji wa umeme wa Megawat 425 ya Kinyerezi II na upanuzi wa Kinyerezi I ambayo kwa sasa iko katika hatua mbalimbali za utekelezaji.

Mbali na hayo Mhandisi Mramba alisema kuwa tatizo la kukatika kwa umeme kumepungua ikilinganishwa na awali pia upotevu wa umeme umepungua kutoka asilimia 18 hadi asilimia 17 kwa mwaka 2016.

Kwa upande wake Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo ameutaka uongozi wa TANESCO kushughulikia na kumaliza changamoto ya kukatika kwa umeme nchini kwani kufikia uchumi wa kati kupitia viwanda itahitaji umeme wa uhakika.
Pia Waziri wa Biashara na Maendeleo wa Finland Bw. Kai Mykkanen, alisema kuwa Serikali ya Finland itaendelea kushirikiana na Tanzania katika masuala ya maendeleo hususani katika sekta ya Nishati.

LAPF YATOA MSAADA BUIGIRI,MKOANI DODOMA

$
0
0
Mfuko wa Pensheni wa LAPF wakabidhi vifaa vya umwagiliaji maji kwa kikundi cha watu wenye Ulemavu cha Buigiri, Dodoma. Pichani ni Afisa Masoko Mwandamizi wa LAPF Rehema Mkamba akikabidhi baadhi ya vifaa hivyo kwa viongozi wa kikundi hicho. Vifaa hivyo vitawasaidia kuendesha shughuli za kilimo cha mboga mboga cha umwagiliaji ili kujipatia kipato.

PLUIJM, LWANDAMINA KIROHO SAFI WATAMBULISHWA RASMI LEO

$
0
0

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

MAKAMU Mwenyekiti wa klabu ya Yanga Clement Sanga amemtambulisha rasmi kocha mkuu wa timu hiyo Mzambia George Lwandamina, aliyechukua nafasi ya Mholanzi  Hans Van De Pluijm aliyevikwa viatu vya Mkurugenzi wa ufundi wa timu hiyo.

Lwandamina anachukua mikoba ya Mholanzi Hans Van De Pluijm aliyebadilishiwa majukumu na kuwa mkurugenzi wa ufundi ili kumsaidia Mzambia huyo katika masuala mbali mbali ya maendeleo ya klabu hiyo, na moja kwa moja Mzambia huyo huku mzambia huyo akafunguka juu ya kikosi atakachoingia nacho vitani.

Sanga ameweka wazi kuwa ujio wa kocha huyo sasa ni rasmi na wamempa kandarasi ya miaka miwili,lengo kubwa ikiwa ni kuongeza nguvu kwenye kikosi cha wanajangwani hao katika kutetea Ubingwa wa ligi kuu ya Vodacom na michuano ya kimataifa. 

"Uongozi wa Yanga leo hii unayo furaha kuwatambulisha kocha mkuu George Lwandamina na Mkurugenzi wa ufundi Hans Van De Pluijm, tunaamini kwa pamoja wataweza kuipa mafanikio zaidi timu yetu kutoka hapa ilipo na kusonga mbele zaidi" amesema Sanga.

Baada ya utambulisho huo, Kocha mkuu Lwandamina akafunguka na kusema kuwa ni changamoto mpya kwake kwani anajua Yanga ni klabu kubwa na amepewa nafasi hiyo na kwa kushirikiana na benchi la ufundi kwa ujumla na wachezaji kwa pamoja atahakikisha anatumia kila kinachowezekana kuhakikisha Yanga inafanya vizuri kuanzia kwenye ligi ya nyumbani hadi klabu Bingwa Afrika. 

Akaeleza kuwa kuna habari zinazoenea kuwa anakuja na wachezaji wapya kutoka Zesco, akasisitiza zaidi kuwa "Nasikia tetesi kuhusu wachezaji wapya kutoka Zesco kusajiliwa Yanga mimi kama kocha mkuu sijui chochote labda michakato hiyo inafanyika bila mimi kushirikishwa kikosi kilichopo ndicho nitaendelea nacho". 

Mkurugenzi wa ufundi wa klabu hiyo Pluijm akawa na yake ya kusema na kueleza kuwa hana shida na kubadilishiwa majukumu na zaidi ataendelea kushirikiana na benchi la ufundi kwa ujumla katika kuhakikisha wanaendelea kutetea ubingwa wao na kufanya vizuri kwenye kombe la Klabu Bingwa Afrika.
Makamu Mwenyekiti wa klabu ya Yanga Clement Sanga akimkabidhi jezi ya timu hiyo Kocha Mkuu George Lwandamina leo Jijini Dar es salaam.
Kocha Mkuu George Lwandamina akisalimiana Mkurugenzi wa benchi la Ufundi Hans Van De Pluijm ambaye awali alikuwa ndiye kocha Mkuu.
Makamu Mwenyekiti wa klabu ya Yanga Clement Sanga akizungumza na waandishi wa habari wakati wa utambulisho wa kocha mkuu  Mzambia George Lwandamina (kulia) pamoja na nafasi ya Mholanzi Hans Van De Pluijm aliyechukua nafasi ya mkurugenzi wa ufundi. 

ATCL YAKILI KUKABILIANA NA CHANGAMOTO BAADA YA KUPOKEA NDEGE MPYA AINA YA BOMBARDIER Q400

$
0
0

Mwenyekiti wa Bodi ya ATCL,Mhandisi Emmanuel Korosso(katikati) akizungumza na Waandishi wa Habari leo katika Ofisi za Shirika hilo,Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika,Ladislaus Matindi,kulia ni Mjumbe wa Bodi,Dkt. Mussa Mgwata.
 
 Na Bakari Madjeshi,Globu ya Jamii

Baada ya kuanza safari zake Octoba 14 2016,Shirika la Ndege la ATCL limekili kuwepo kwa changamoto mbalimbali zikiwemo ucheleweshaji wa ndege na kutoa huduma katika maeneo ambayo yalipaswa kuhudumiwa.

Akitoa changamoto hizo,Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika hilo,Mhandisi Emmanuel Korosso amekili kuwepo kwa changamoto ya Marubani katika Shirika hilo ikizingatiwa mpaka sasa Shirika hilo linatarajiwa kumaliza mafunzo ya Marubani 13 katikati ya mwezi Desemba.

Amesema kuhusu Wafanyakazi Bodi yake imeagiza Menejimenti ya Shirika kusimamisha kwa muda mkataba wa hiari ambao unatoa mwanya kwa wafanyakazi kutumia vibaya ruhusa za matumizi ya tiketi za bure.

"Katokana na haja ya kuboresha Utendaji, ATCL iliamuliwa Wakurugenzi wote katika Menejimenti ya ATCL isipokuwa Mkurugenzi Mtendaji,na baadhi ya Menejimenti waondolewe katika nafasi zao Mara moja kutokana na Utendaji dhaifu na viwango vya Elimu visivyokidhi matakwa ya nafasi zao",amesema Mhandisi Korosso

"Tumeamua wakurugenzi wanaokaimu nafasi zao warudishwe katika nafasi zao za chini ambazo siyo za Menejimenti au wahamishiwe katika vituo vya mikoani",ameeleza Mhandisi Korosso

Aidha,Wakurugenzi na Menejimenti waliokuwa wamethibitishwa tumeagiza waondolewe ATCL ili wapangiwe majukumu mengine kulingana na sifa zao.

Aidha Bodi imemuagiza Mtendaji Mkuu kutangaza mara moja nafasi zote za Wakurugenzi na pia nafasi za Mameneja zilizo wazi kwa kufuata muundo wa muda uliopitishwa na Bodi (Interim Organization Structure).

Pia Mtendaji Mkuu ameagizwa kutangaza nafasi zozote ambazo anaona kuna umuhimu wa kuajiri watu wengine kutokana na utendaji usioridhisha wa wafanyakazi wanaoshikiria nafasi hizo kwa sasa.

SERIKALI KUFANYIA KAZI MAPENDEKEZO YA WASAFIRISHAJI

$
0
0
Na Humphrey Shao,Globu ya Jamii

Serikali imejipanga kufanyia kazi mapendekezo yaliyotolewa na jukwaa la usafirishaji nchini ,ili kuboresha hali ya usafiri hapa nchini kutoka bandarini kutoka nchini jirani.

Hayo yamesemwa na Katibu mkuu wa Wizara ya Mawasiliano na uchukuzi,Profesa Faustine Kamuzora alipokuwa akifungua jukwaa hilo lililoasisiwa na tasisi ya Trade Mark East Afrika.

"Hivyo serikali imejipanga na kuakikisha kuwa bandari ya Dar es Salaam inakuwa sehemu rafiki kwa wafanyabiashara kutoka nchi zinazotunguka kwa kupunguza urasimu unaochangia kuchelewa kwa kutoa mzigo bandarini"amesema Prof Kamuzora

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jukwaa hilo la usafirishaji ,Angelina Ngalula , amesema kuwa serikali inatakiwa kuanza kuandaa mazingira ya upatikanaji wa mzigo wa tani milioni 10 katika reli ya Standard Geji inayo taraji kujengwa hapa nchini .

Amesema kuwa wazo la serikali la kujenga reli ya kisasa ni zuri hivyo tunaiomba serikali inahakikisha  inaandaa mazingira ya upatikanaji wa mizigo hili tusije tukaiona reli hiyo kama pambo tu.
  Mkurugenzi mkazi wa Trademark East Afrika,John Ulanga akizungumza na wadau wa usafirishaji wakati uzinduzi wa jukwaa lamusafirishaji.
 Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF ,Godfrey Simbeye  akito maelezo jinsi tasisi yake inavyofanya kazi bega kwa bega na wawekezaji ususani katika swala la usafirishaji.
 Mwenyekiti wa Jukwaa la Usafirishaji ,Angelina Ngalula akizungumza na wadau wa usafirishaji wakati uzinduzi wa jukwaaa hilo.
 Katibu mkuu wa wizara ya Uchukuzi,Prof Faustine Kamuzora akitoa hotuba ya ufunguzi wa jukwaa la usafirishaji jijini Dar es Salaam
Wadau wa usafirishaji wakisikiliza kwa makini wakati wa uzinduzi wa jukwaa hilo.
 Picha ya pamoja ya wadau wa usafirishaji na mgeni rasmi.

Serikali yawataka maafisa elimu kupanga muda wa kusikiliza kero za walimu na kuzitafutia ufumbuzi kuongeza morali ya walimu kufundisha.

$
0
0

Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Selemani Said Jafo akisaini kitabu cha wageni shule ya sekondari Segera, kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Bw. Wiliam Makufwe na kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mh. Godwin Gondwe.
Picha ya pamoja ya Mhe. Selemani Said Jafo na waalimu wa shule ya sekondari ya Segera.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni akitoa utambulisho mfupi kwenye ukumbi wa Halmashauri.
Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mh. Godwin Gondwe akitoa taarifa fupi ya Wilaya kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya Handeni.
Naibu waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Mh. Selemani Said Jafo akizungumza ma watumishi wa Wilaya ya handeni.
Baadhi ya Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni.
Viongozi wakisikiliza kwa makini maagizo ya Naibu Waziri ikiwa ni pamoja na kuwa na usimamizi bora wa rasilimali fedha.


Serikali imewataka maafisa elimu kupanga muda wa kusikiliza kero za walimu na kuzitafutia ufumbuzi ili kuongeza morali ya walimu kufundisha. Agizo hilo lilitolewa na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe.Seleman Said Jafo alipokuwa akiongea na walimu wa shule ya sekondari Segera iliyopo wilayani Handeni, wakati wa ziara ya kiserikali Wilayani Handeni na Mkoa wa Tanga.

Mhe.Jafo alisema kuwa wapo baadhi ya Maafisa elimu ambao wanajifanya kuwa ni Miungu watu linapokuja suala la kusikiliza na kutatua kero za walimu. Waziri Jafo alisema “Wapo walimu wanaotembea umbali mrefu kufuata huduma makao makuu ya Halmashauri kwa wakubwa wao mara nyingi wameshindwa kutatuliwa kero zao hali inayopelekea usumbufu, Kuanzia leo 24/11/2016 napiga marufuku tabia hiyo”. 
 
Aliongeza msisitizo kuwa Maafisa elimu wapo kwa lengo la kuwasikiliza walimu na kuwasaidia kutatua kero zao ili waweze kujikita katika ufundishaji wa wanafunzi. Alisema kuwa walimu ni watu muhimu sana nchini ila wamekuwa wakikatishwa tamaa na utendaji wa baadhi ya maafisa elimu. Aliongeza kuwa kero kubwa ya walimu ni kutokupanda madaraja kwa wakati na kutopata stahiki zao ikiwa ni pamoja na posho za likizo,uhamisho na madai mengine.

Wakati huohuo, Naibu Waziri aliiagiza Halmashauri ya Wilaya ya Handeni kukamilisha miradi yote ya SEDP-II ambayo haijakamilika kuhakikisha inakamilika kabla au ifikapo tarehe 20/12/2016. Alisema kuwa katika kusimamia miradi hiyo na miradi ya maendeleo kwa ujumla kila mtu lazima atimize wajibu wake na kuhakikisha fedha iliyotengwa na kutolewa inatumika vizuri na thamani yake kuonekana kwa muda mrefu (value for money).

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI aliwataka Maafisa utumishi pia kusimamia vizuri haki za watumishi ili kuwawezesha watumishi wote kufanya kazi kwa moyo na kuwaondolea msongo wa mawazo usio wa lazima. 
 
“Maafisa utumishi wakifanya kazi zao kwa weledi na kutimiza wajibu wao, Halmashauri haitakuwa na malalamiko kutoka kwa watumishi kitu ambacho kitaongeza ufanisi katika utendaji wao”. Vilevile, aliwataka kutambua michango ya watumishi bora na wanaojituma kufanya kazi wanapotimiza wajibu wao kwa juhudi na maalifa kuwepo na utaratibu wa kuwapa pongezi na motisha ( acknowledgement).

Aidha amewaeleza waweka hazina kuhakikisha wanatimiza wajibu wao kwa kufuat sheria taratibu na kanuni zilizopo za Halmashauri kwani kufanikiwa au kutofanikiwa kwa malengo ya Halmashauri kunachangiwa kwa kiasi kikubwa kwa utendaji kazi wa waweka hazina wa Halmashauri.”Mwekahazina atayeshindwa kutimiza wajibu wake atapisha nafasi hiyo kwa mtu mwingine ambaye ataweza kusimamia kwa ufanisi”alisema.

Pia aliwaagiza wakurugenzi wa Mjini Bw. Kenned Haule na Bw. William Makufwe Mkurugenzi wa Handeni Vijijini kuweka malengo ya utendaji kazi kwa kutumia mfumo wa Opras kwa kila mkuu wa Idara na kitengo na kuhakikisha wanafuatilia kwa karibu utendaji kazi wa watumishi hao, ili kutambua kwa kiasi gani malengo hayo yamekamilishwa. Wametakiwa kuhakikisha pia wanakuza vipaji vya watumishi kwa kutumia elimu na taaluma walizonazo ipasavyo ili kuendeleza Halmashauri.

Wakurugenzi wametakiwa kuhakikisha pia watumishi wa idara ya maendeleo ya jamii wanatumika ipasavyo katika kuhudumia jamii ikiwa ni pamoja na kuhakikisha fedha za miradi ya vikundi vya vijana na kinamama zinatolewa na kutumiwa kama ilivyokusudiwa.

Mwisho Naibu Waziri aliwashukuru watumishi na kuwaomba wapendane kwani upendo baina ya watumishi ni chachu ya maendeleo na kwamba kila mtumishi afanye majukumu yake kwa kukuza thamamani ya kazi yake na kutoa ushirikiano kwa viongozi wetu hasa wabunge. Aliwakumbusha watumizi kufanya kazi kama ajira kwani wanapata mishahara, kuacha alama ( legacy) na kufanya kazi kama ibada kwa kuwatumikia wananchi.

Aidha Aliwataka Waheshimiwa Madiwani kufanya maamuzi sahihi pindi linapofika suala la kufanya maamuzi kwa manufaa ya wananchi na sio kunufaisha Viongozi wachache au kikundi cha watu. Hasa upatikanaji wa eneo la kujenga ofisi za Halmashauri zilizo gawanywa ili kuondoa gharama zisizo za lazima za ulipaji fidia wa maeneo.

Mkuu wa wilaya ya Handeni Mh. Godwin Gondwe aliahidi kusimamia utekelezaji wa maagizo yote yaliyotolewa na Naibu Waziri kwa karibu na ukamilifu wake kwa dhati .

Nae Mbunge wa Jimbo la Handeni Mjini, Mhe. Omary Kigoda pamoja na kutoa shukrani kwa ziara ya Naibu Waziri, alichukua fulsa hiyo kumuomba Naibu Waziri kusaidia upatikanaji wa watumishi wa sekta ya afya kutokana na uhaba mkubwa wa watumishi wa kada hiyo hali inayofifisha huduma kwa jamii. Alisema kwamba watumishi waliopo ni 25% ya watumishi wanaohitajika hivyo upungufu ni mkubwa.

Naibu Waziri Jafo alifanya ziara ya siku moja Wilayani Handeni ambapo pamoja na mambo mengine aliongea na watumishi wa wilaya hiyo.

Alda Sadango

Afisa Habari

Halmashauri ya Wilaya ya Handeni

25/11/2016


SERIKALI imepanga kununua ndege za kisasa ili kuimarisha ulinzi katika Hifadhi za Taifa nchini.

$
0
0

Hayo yamesemwa jana na Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Meja Jenerali Gaudence Milanzi wakati akihojiwa na kipindi maalumu cha TUNATEKELEZA kinachorushwa hewani na kituo cha Televisheni ya Taifa (TBC1).

Meja Jenerali Milanzi anasema Serikali imeweka mfumo maalumkatika kulinda hifadhi zilizopo na ili kuweza kukabiliana na ujangili unaojitokeza katika hifadhi mbalimbali nchini.

“Sekta ya Utalii nchini inachangia pato la taifa kwa takribani asilimia 17.5 na kutoa ajira kwa zaidi ya watumishi milioni 3 katika sekta mbali mbali ya utalii nchini, hivyo ni vyema tukaweka mikakati madhubuti katika kulinda vyanzo vilivyopo” alisema Meja Milanzi.

Aidha, alisema kuwa Serikali itaendelea kuwachukulia hatua kali za kisheria watu wote watakaobainika kujihusisha na ujangili pamoja na biashara ya magogo ili kulinda hifadhi za Taifa na kuweza kuvutia watalii nchini.Aidha Meja Jenerali Milanzi aliitaka jamii kwa ujumla kuona umuhimu wa kutumia nishati mbadala ili kulinda misitu iliyopo kwa kutunza mazingira na hifadhi za taifa.

Mbali na hayo Meja Jenerali Milanzi alisema Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazovutia watalii wengi kutoka Marekani na Uingereza hivyo kuwataka wananchi kuzingatia sheria na kanuni zinazosimamimia Hifadhi za Taifa ili kuzudi kuvutia watalii nchini.

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AMJULIA HALI MKUU WA MKOA WA TANGA- SHIGELA

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimjulia hali Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigela  ambaye amelazwa kwenye hospitali ya taifa ya Muhimbili, Novemba 25, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Barabara ya mabatini yazidi kuwa kero kwa wakazi wa Jijiji

$
0
0
Sehemu ya barabara ya Mabatini ambayo imekuwa korofi kwa muda mrefu sana huku uongozi wa Halmashauri na mkoa kuendelea kuitazama licha ya kuwa ni kiungo muhimu kati ya Kijitonyama na Sinza Afrika sana.

WAFANYABIASHARA MKOANI SINGIDA WAJIPATIA BILIONI 1.8 KWA MAUZO YA KUKU.

$
0
0
Mwenyekiti wa Kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa na Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Mathew John Mtigumwe akiongoza kikao hicho, kushoto kwake ni Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dokta Angelina Mageni Lutambi, wa kwanza kulia ni Waziri wa Mambo ya ndani Mwigulu Lameck Nchemba na anayefuata ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida Mhe. Martha Mlata.
Mbunge wa Viti maalum CCM Singida Aisharose Matembe akichangia hoja katika kikao cha kamati ya ushauri ya Mkoa wa Singida (RCC). 
Meneja wa SIDO Mkoa wa Singida Shoma Kibende akichangia hoja katika kikao cha kamati ya ushauri ya Mkoa wa Singida (RCC).

Na Nathaniel Limu-Singida
Wafanyabiashara wa kuku wa asili/kienyeji mkoani Singida wamejipatia mapato ya zaidi ya shilingi bilioni 1.8, baada ya kuuza kuku 151,242 katika kipindi cha mwaka jana hadi sasa.

Hayo yamesemwa juzi na kaimu Katibu Tawala Msaidizi Uchumi na Uzalishaji Beatus Choaji wakati akitoa taarifa ya uendelezaji wa kuku wa asili, kwenye kikao cha kamati ya ushauri mkoa (RCC) kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano uliopo kwenye jengo la ofisi ya mkuu wa mkoa mjini hapa.

Chowaji amesema mapato hayo yamepatikana baada ya kuku hao 151,242 kusafirishwa  na kuuzwa nje ya mkoa ikiwemo jijini Dar-es-salaam.

“Kuku wa asili wakifungwa vizuri kwa kudhibiti ugonjwa wa mdondo na kuzingatia kanuni za ufugaji bora wanaweza kuleta mabadiliko makubwa na ya haraka ya kipato. Kuku wa asili pia ni lishe bora hususani kwa watoto na akina mama”, ameongeza Choaji.

Ili kuimarisha ufugaji kuku wa asili amesema imependekezwa halmashauri zote zitekeleze mkakati wa kuchanja kuku kwa wakati moja mara tatu kwa mwaka kwa kutumia watoa chanjo wasiokuwa wataalam wa mifugo.

Akisisitiza amesema “Mkakati huu unatarajiwa kuanza mara halmashauri zitakazokamilisha utoaji wa mafunzo kwa watoa chanjo hao. Halmashauri zimesisitizwa kushiriki kikamilifu kutekeleza mkakati huo ili kuinua kipato cha wananchi kwa haraka zaidi”.

Mapema Mkuu wa Mkoa wa Singida na mwenyekiti wa kikao hicho, Mhandisi Mathew John Mtigumwe, akifungua kikao hicho ameagiza kuwa wananchi wahamasishwe, ili wasiendelee kuuza chakula walichovuna msimu uliopita kiweze kuwafikisha msimu ujao wa mavuno.

Mhandisi Mitugumwe amesema kwa mujibu wa mamlaka ya hali ya hewa nchini (TMA) mvua za msimu huu zinatarajiwa kunyesha kwa kiwango cha chini ya wastani.

“Hivyo ni jukumu letu sote kuhimiza na kushauri wananchi kufuata kanuni bora za kilimo na kupanda mazo ya kipaumbele yanayostahimili ukame, na yanayokomaa mwa muda mfupi.

Wakati huo huo Mkuu huyo wa mkoa, ametumia fursa hiyo kutoa shukrani zake za dhati kwa wananchi wadau wa elimu, wafanyabiashara, kampuni za simu za viganjani na mashirika ya umma na binafsi, kwa kushiriki kutekeleza agizo la rais Magufuli la kumaliza uhaba wa madawati mashuleni.

MTANZANIA VICTORIA MWANZIVA ASHIRIKI KOZI MAALUM YA WANAWAKE KWA AJILI YA KUDUMISHA AMANI BARANI AFRIKA, ADDIS ABABA ETHIOPIA.

$
0
0
Bi. Victoria Mwanziva (kulia) akitoa mchango wake katika kozi maalum kwa wanawake  kwa ajili ya kudumisha Amani Barani Afrika.
Baadhi ya washiriki kutoka Nchi mbalimbali Barani Afrika wakiwa na Profesa Juan Sainz Borgo (wa tano kutoka kulia) aliyetoa somo juu ya amani na ambaye ni mmoja wa viongozi wa chuo cha Amani Umoja wa Mataifa
Baadhi ya washiriki wa Mafunzo hayo maalum wakiwa katika picha ya pamoja.
Bi. Victoria Mwanziva alipotembelea Ubalozi wa Tanzania Nchini Ethiopia 
 Bi. Victoria Mwanziva alipotembelea Makao Makuu ya Umoja wa Afrika walipofanya ziara ya mafunzo.

WAZIRI WA AFYA UMMY APOKEA VIFAA VYA MACHO VYENYE THAMANI YA MILIONI 320

$
0
0
Na Amina Kibwana, Globu ya Jamii.

WIZARA ya Afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto imepokea vifaa vya huduma za macho vyenye thamani ya milioni 321, 234,002 kutoka kwa Shirika la Christian Blind Blind Mission kupitia benki ya Standard Chartered kupitia mradi wa "Seeing is Believing, Child Eye Health" leo jijini Dar es salaam. 

Akipokea misaada hiyo, Waziri wa Afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto Ummy Mwalimu ameshukuru kwa msaada huo kwani kupata vifaa hivyo vitasaidia katika uboreshaji wa afya ya macho hususani kwa watoto ambapo vitazuia ulemavu wa kutokuona. 

Ummy amesema kuwa, vifaa hivyo vitaboresha huduma za macho na jamii nzima itanufaika kwa uwepo wa vifaa hivi kwani matumizi yake hayataishia kwa watoto tu bali hata watu wazima wanaokabiliwa na matatizo ya macho. 

"vifaa hivi vitasambazwa katika sehemu tofauti nchini na vitawalenga watu wote sio watoto tu, hii ni kutokana na kutaka kupunguza athari za magonjwa ya macho kwani hupelekea kuleta ulemavu kwani kulingana na mahitaji kuwa mengi husuani kwa watoto huduma hizi hazijafikia kiwango kinachoshauriwa na Shirika la Afya duniani,"amesema Ummy. 

Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered Sanjay Rughani amesema kuwa wametoa vifaa hivyo kwa ajili ya kuwasaidia watu wote wenye matatizo ya macho wakiwemo watoto kwani wanaamini kuwa macho ni kiungo muhimu sana kwa binadamu. 

Vifaa hivyo ambavyo vitagawanywa sehemu mbalimbali ikiwemo hospitali na Mikoani kama Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Hospitali ya Rufaa ya kanda Bungando,Hospitali ya Rufaa ya kanda Mbeya,Hospitali za Rufaa za mikoa ya ilala,Kinondoni,temeke,Mbeya,Rukwa,manyara,Tabora,Mwanza na Halmashauri za miji ya mbeya na babati pamoja na Halmashauri za wilaya za babati, Mbulu, Simanjiro,Kiteto,Igunga,Sikoine na Nzega. 
Waziri wa Afya, MaendeleoyaJamii, Jinsia na Watoto Ummy Mwalimu wa pili kulia akipokea Dubini ya kufanyia operesheni ya macho kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya Standard Chartered Bw. Sanjay Rughani watatu kushoto wakati wa kukabidhi vifaa vya uchunguzi wa macho vyenye thamani ya shilingi milioni 320 leojijini Dar es salaam, wa kwa kulia ni Kaimu Mganga Mkuu wa Wizara Dkt. Mohammed Mohammed. 
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Ummy Mwalimu akimkabidhi Kifaa cha uchunguziwa macho Kaimu Mganga Mkuu wa mkoa Dkt. Daisy Majamba kulia wakati wa kukabidhiana vifaa vya uchunguzi wa macho vyenye thamani ya shilingi milioni 320 leo jijini Dar es salaam.
Waziri waAfya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Ummy Mwalimu kulia akiongea na waandishi wa habari hawapo pichani wakati wa kukabidhiana vifaa vya uchunguzi wa macho vyenye thamani ya shilingi milioni 320 leo jijini Dar es salaam.

Baraza la Madiwani Lamfukuza Kazi Mtumishi.

$
0
0

Na. Immaculate Makilika - MAELEZO

BARAZA la Madiwani ya Halmashauri ya Mji wa Bunda limemfukuza  kazi  Bw. Eliud Haonga aliyekuwa mtumishi wa Idara ya Ardhi na Mipango  na Mthamini  daraja la pili mapema wiki hii, baada ya kughushi nyaraka ili kujipatia fedha za malipo ya pango.

Bw. Haonga alipokea fedha za malipo ya pango kiasi cha shilingi milioni saba kutoka kiwanda cha OLAM Tanzania mwezi Juni mwaka huu.

Akizungumza kwa njia ya simu,  Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Bunda, Mkoa wa Mara, Bi. Janeth Mayanja alisema kuwa Bw. Haonga amekiuka Sheria za Utumishi wa Umma, kanuni ya 42 na uamuzi uliotolewa na baraza la madiwani  ni sahihi.

Bi. Janeth alisema “Bw. Eliud Haonga alihifadhi shilingi milioni mbili tu katika akaunti ya Halmashauri ya Mji wa Bunda  na kutumia shilingi milioni tano kwa matumizi yake binafsi”.“Maamuzi haya yamechukuliwa baada ya Kamati ya Uchunguzi  kumaliza kazi yake kwa mujibu wa  Sheria, kanuni na taratibu za Utumishi wa Umma.” alisema  Bi. Mayanja.

Aidha,  Bi. Mayanja amewaasa watumishi wa Halmashauri  Bunda  kujiepusha na vitendo vinavyoashiria wizi na ubadhirifu,  na hatua kali  zitachukuliwa kwa yeyote atakayekiuka maadili ya utumishi wa umma.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Bunda, mkoa wa Mara Bi. Janeth
Mayanja akiwa Ofisini kwake.

WAZIRI MKUU AHOJI TANZANIA KUTOKAMILISHA MKATABA WA MAWAKILI

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametoa wiki moja kwa Waziri wa Katiba na Sheria, Dk. Harrison Mwakyembe kumpa maelezo kuhusu sababu za Tanzania kutokukamilisha mkataba wa Mawakili wa Afrika Mashariki kutambuana katika utendaji wao.

Ametoa agizo hilo leo (Ijumaa, Novemba 25, 2016) wakati akimuwakilisha Rais Dk. John Magufuli katika ufunguzi wa mkutano wa 21 wa mwaka wa Chama cha Wanasheria wa Afrika Mashariki kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.

“Nimeshtushwa kidogo kusikia kwenye taarifa yenu kuwa mkataba huo uliolenga nchi zote za Afrika Mashariki hautaihusisha Tanzania kutokana na kutokukamilisha sehemu yao ya kuufanyia kazi, nitahitaji maelezo,”
“Nitapenda kupata maoni yako wewe mwenyewe Mheshimiwa Waziri wa Katiba na Sheria wa Tanzania kwa vile wewe ni Mwanasheria mwandamizi na siyo Mwanasheria  wa Tanganyika Law Society peke yake kwa nini Tanzania haijakamilisha mkataba huu,” amesisitiza.

Waziri Mkuu amesema kwa mujibu wa maelezo ya awali aliyopewa kuhusu mkataba huo, utakuwa na umuhimu mkubwa kwenye ukanda wa Afrika Mashariki kama ilivyo kwenye sekta nyingine zinazoshirikiana ikiwemo uhandisi, uhasibu, uthamini na uchoraji wa majengo.

Katika hatua nyingine Waziri Mkuu amewataka Wanasheria hao kuzisaidia nchi zao ili ziondokane na umaskini uliokithiri na Serikali zipate muda wa kushirikisha watu wake katika kufanya kazi kwa lengo la kuwapatia maendeleo.

Amesema nchi zilizoendelea na zinazoendelea, baada ya chaguzi hufanya shughuli za ujenzi wa taifa lao na maendeleo ya watu wake. Ili kudumisha demokrasia wana muda wa mikutano na maandamano na kazi.

“Hawaandamani tu bila kupata kibali cha Polisi, hawaruhusiwi kuzuia magari yasipite, kuzuia kazi isifanyike. Mfano kifungu cha 115 cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, kinataka kesi zinazotokana na uchaguzi ziwe zimefunguliwa mahakamani ndani ya siku thelathini tangu kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi na ziwe zimesikilizwa na kutolewa maamuzi ndani ya miezi kumi na miwili tangu tarehe ya kufunguliwa mahakamani,” amesema..

Amesema “kwa uelewa wa kawaida, Kifungu hiki ni kuwa jamii inataka masuala ya siasa za uchaguzi yawe na muda wake wenye ukomo maalum ili baada ya hapo wananchi waelekeze muda, nguvu na rasilimali zao nyingine katika kazi au shughuli nyingine za maendeleo na ujenzi wa Taifa lao”.

Aidha, Waziri Mkuu amesema eneo jingine ambalo ni muhimu kulitupia jicho ili kukuza ushindani wa kibiashara katika Jumuia ya Afrika Mashariki ni la uendeshaji wa mashauri mahakamani hasa kwa mashauri ya madai.

“Wote tunakubaliana kuhusu misingi na haki za kidemokrasia kuwa kila mtu anayo haki kikatiba na kisheria kusikilizwa madai yake na kutetea haki zake; na kuwa chombo chenye mamlaka ya kutoa haki ni Mahakama”. Amesema.

Amesema kuna taarifa za kuwepo kwa kesi zenye kuhusisha mali za thamani kubwa zinazochukua muda mrefu sana kumalizika mahakamani huku baadhi ya sababu za kuchelewa kwa kesi hizo ni utoaji wa maombi ya kuziahirisha mara kwa mara kwa sababu binafsi jambo linalosababisha uendeshaji wa kesi kuwa mgumu na kuchukua muda mrefu.

Waziri Mkuu amesema wakati mwingine hata kesi zilizosikilizwa huendelea kubaki mahakamani muda mrefu kutokana na maombi na rufaa za hapa na pale zinazoishia kumnyima mwenye haki fursa ya kutekelezewa haki yake.

“Ni wazi kesi kama hizi zinapohusisha mahusiano ya kibiashara na au mitaji mikubwa ya biashara, matokeo yake ni kudumaza na hata kuua biashara, achilia mbali ushindani wa kibiashara. Ni wajibu wenu Wanasheria kupata ufumbuzi wa tatizo hili lenye athari hasi kibiashara,’ amesema.

Amesema haki ya wadaiwa kusikilizwa kikamilifu na Mahakama, haki na uhuru mlionao Mawakili kuwawakilisha wadaiwa wao bila hofu au shinikizo lolote, viwe chachu ya maendeleo ya ushindani wa kibiashara na visiwe kikwazo.


 IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
2 MTAA WA MAGOGONI,
S.  L. P. 3021,
11410 DAR ES SALAAM.
IJUMAA, NOVEMBA 25, 2016.

WAZIRI UMMY AZINDUA KAMPENI YA SIKU 16 ZA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA LEO JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0

 Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akiongea katika uzinduzi wa kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia  uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.Kushoto kwake ni  Mkurugenzi wa  WiLDAF Dkt.Judith Odunga ,Balozi wa Ireland nchini Bw.Paul Sherlock(wa tatu kushoto), na Kamanda wa Polisi kanda maalum ACP Lucas Mkondya.
  Mkurugenzi wa WiLDAF Dkt.Judith Odunga akitoa neno la ufunguzi katika  uzinduzi wa kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia  uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.Kulia kwake ni Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu na ni  Mratibu Mkazi kutoka Umoja wa Mataifa nchini Bi.Maria Karadenizli 
 Picha na Daudi Manongi
 Balozi wa Ireland nchini Bw.Paul Sherlock akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia  uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.kulia kwake ni  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,  Wazee na  Watoto Mhe.Ummy Mwalimu, Mkurugenzi wa WiLDAF Dkt.Judith Odunga, Kamanda wa Polisi kanda maalum ACP Lucas Mkondya na Mkuu wa Dawati la Jinsia,ACP Mary Nzoki.
  Mwakilishi kutoka Umoja wa nchi za Ulaya Bw.Roeland Van Geer akizungumza juu ya ukatili wa kijinsia na athari zake katika uzinduzi wa kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.Kulia kwake ni Mratibu Mkazi kutoka Umoja wa Mataifa nchini Bi.Maria Karadenizli, Mkurugenzi wa WiLDAF Dkt.Judith Odunga, Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu
 Mwanamziki wa Bongo Fleva nchini Bi.Mwasiti Almasi akitumbuiza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia  uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akiongea jambo na Balozi wa Ireland nchini Bw.Paul Sherlock mara baada ya uzinduzi wa kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia  uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
 Waandamaji kutoka Taasisi na Asasi mbalibali  wakionyesha ujumbe mbalimbali unaopinga ukatili wa kijinsia wakati wa uzinduzi wa kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia  uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akisaini katika ubao wenye kauli mbiu katika uzinduzi wa kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia  uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.

DK. KIGWANGALLA ATUNUKU VYETI WAITIMU SEKTA YA MAENDELEO YA JAMII TENGERU

$
0
0

 Na Anthony Ishengoma

Serikali inajipanga kuajili wataalamu wa maendeleo ya jamii 5,554 kwa kipindi cha miaka mitano ili waweze kutoa huduma za maendeleo ya jamii kuanzia  ngazi ya Serikali kuu hadi kijiji kama ilivyokuwa kwa utawala wa amu ya kwanza nchini.

Akihutubia wakati wa Mahafari ya sita ya Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tenguru nje kidogo ya jiji  la Arusha Naibu Waziri Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Hamis Kigwangalla amesema serikali ya awamu ya kwanza ilikuwa na idadi kubwa ya mabibi na mabwana maendeleo ya jamii kila kata.
 Aliongeza kuwa kwasasa wataalamu katika sekta ya maendeleo ya jamii  wameanza kupungua sana na kukitaka chuo kuongeza udaili wa wanafunzi ili kuendana na azima ya serikali ya kuwa na wataalamu awa kila wilaya na kata.

Aidha aliitaka Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru kuendela kutoa taaluma yenye viwango na  bora na uzingatiwe katika mchakato wote wa utoaji mafunzo kuanzia kwenye udahili wa wanafunzi wenye sifa na vigezo ili kujenga jamii ya wasomi wenye tija katika Taifa letu.
  Alisema Nchi itabadilika sana na kuwa na maendeleo ikiwa wanataaluma wa Nchi hii wataipenda Nchi yao kama ambavyo kila mtu ampendavyo mama yake nakujituma sana katika utendaji kazi utaendana na falsafa ya hapa kazi tu.

Naye Mkuu wa Tasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru Anatory Bunduki wakati akuhutubia Mahafari hayo amesema kuwa pamoja na mikakati iliyopo ya kuboresha chuo hicho kwasasa chuo kimeanzisha kituo cha taifa cha utafiti na uhifadhi wa machapisho ya wanawake Nchini kituo ambacho kimeanzishwa kwa ushirikiano wa UNESCO na UNFPA pamoja na Wizara ya Afya, Maendeleo jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.
Mkuu wa chuo alienedelea kusema lengo la kuanzishwa kwa kutuo hicho ni kufanya tafiti za kina kwa masuala ya wanawake, jinsia, watoto wa kike ili kuwainua kiuchumi, kisiasa,kiutamaduni na kijamii na kuzitumia tafiti hizi kujadili katika kuandaa sera na kutoa maamuzi yanayojumuisha amsuala ya kijinsia katika kutekeleza sera mbalimbali hapa Nchini.

Mahafaria ya sita ya Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru yametoa wahitimu katika fani za astashahada, shahada ya kwanza na stashahada ya uzamili ya maendeleo ya jamii.

RAIS DKT MAGUFULI AMPIGIA SIMU RC MAKONDA NA KUMPONGEZA KWA KAZI ANAYOIFANYA

$
0
0
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii. 

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli amempongeza mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam , Paul Makonda kwa juhudi anazofanya katika ziara yake kwa kusikiliza kero za Wananchi wa mkoa wa Dar es Salaam. 

Rais Magufuli ambaye alimpigia mkuu huyo wa mkoa wakati alipokuwa akisikiliza kero za Wananchi katika Kata ya Mbezi Luis eneo la Malamba Mawili ambako aliweza kumsisitiza kuwa aendelee kutumbua watu huko huko aliko. 

 “Endelea hivyo kutembelea wananchi na kutoa ufafanuzi kwa sababu nyingine ufafanuzi huu kama ungetolewa mapema wala wananchi wasingekuwa na sababu ya kuja kuuliza maswali kui kwa hiyo endeleeni hivyo hivyo na juhudi za Dar es Salaam na wakuu wa Wilaya yako na watendaji wote kwa kazi nzuri mnazozifanya kwa kusikiliza kero zao bila kujali vyama vyao bila kujali makabila yao na uendelee kutumbua huko huko” Amesema Rais Magufuli. 

 Amemtaka pia kuendelea kupiga kazi na kumwabia kuwa yeye yupo nyuma yake kwani amevunja mwiko wa viongozi waliokuwa wanapendelea kukaa ndani. Kwa upande wake mkuu huyo wa mkoa aliendelea kuwa mtiifu huku akimsikiliza Rais Magufuli kwa Makini juu ya pongezi anazopewa mbele ya watu kwani ameweza kurudisha imani kwa viongozi wa serikali ambayo iliondoka kwa watu kutokana na ujinga wa watu wa chache. Mhe. Makonda.

NGONYANI AZINDUA SAFARI ZA NDEGE YA ATCL KIGOMA

$
0
0
 Mkuu wa Bandari ya Kigoma Bw. Athuman Mwaibamba akijadiliana jambo na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani alipoitembelea bandari ya Kigoma kukagua utendaji kazi wa bandari hiyo.
 Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani akifafanua jambo kwa wafanyakazi wanaopakia na kushusha mizigo katika bandari ya Kigoma.
 Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani akisikiliza changamoto zinazowakabili abiria wanaotumia treni ya reli ya kati katika stesheni ya Kigoma.
 Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani akipata ufafanuzi kutoka kwa Kaimu mkuu wa Shirika la Posta Mkoa wa Kigoma Bw.Juma Kaungenge wakati alipokagua huduma za posta katika mkoa huo.
 Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani akitoa maelekezo kwa viongozi wa uwanja wa ndege na Mamlaka ya anga Mkoani Kigoma namna ya kuhudumia ndege ili kuvutia idadi ya abiria.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani akiwaaga viongozi na watendaji wa taasisi zilizo chini ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano  Mkoani Kigoma mara baada ya kuzindua safari za ndege Bombadier Q400 toka Kigoma kwenda Dar es salaam. Picha na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano -WUUM


Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani amewataka wakazi wa mikoa ya Kigoma, Katavi na Rukwa kuwekeza katika biashara na vivutio vya utalii ili kunufaika na fursa ya ujio wa Ndege mpya za Shirika la ndege Tanzania (ATCL) katika kanda hiyo.

Akizungumza wakati wa kuzindua usafiri wa ndege ya ATCL kutoka Kigoma kwenda Dar es salaam Eng.Ngonyani amesema Serikali itahakikisha inaufufua ukanda wa magharibi mwa Tanzania kwa kuimarisha barabara za lami na kuwa na safari za ndege za uhakika ili kuvutia watalii kutembelea vivutio hivyo na hivyo kukuza uchumi wa mikoa hiyo.


“Kwa kuanza ATCL itakuwa na safari nne kwa wiki kuja Kigoma na idadi ya abiria ikiwa ya kutosha tutaziongeza ili kuwawezesha wasafiri na wadau wengine wa utalii kufika Kigoma kwa urahisi”, Amesema Eng. Ngonyani.

Amewataka wafanyakazi wa ATCL na viwanja vya ndege nchini (TAA), kuwa wabunifu ili kuvutia abiria wengi na hivyo juhudi za Serikali za kuiunganisha nchi kwa usafiri wa  anga zifanikiwe katika muda mfupi.


“Serikali tutaendelea kuongeza ukubwa wa uwanja wa ndege wa Kigoma na Mpanda na kutoza gharama nafuu ili kuwezesha ndege nyingi kutua katika ukanda wa Ziwa Tanganyika na kuwezesha abiria na watalii wengi kunufaika na usafiri wa anga,”. Amesisitiza  Eng. Ngonyani.

Katika hatua nyingine Naibu Waziri Ngonyani amemuagiza Mkuu wa Stesheni ya reli Kigoma Bw. Ally Shamte na Mkuu wa Bandari ya Kigoma Bw. Athumani Mwaibamba kutengeneza mkakati wa pamoja utakaowezesha bandari ya Kigoma kupata mizigo mingi kutoka katika nchi za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Burundi na hivyo kuwezesha biashara ya uhakika kufanyika katika bandari hiyo.

“Angalieni soko lilivyo na jinsi  soko linavyobadilika, hakikisheni mnaongeza wateja na kuongeza ubunifu ili watu wavutike kutumia bandari yetu”. Amesisitiza Eng. Ngonyani.Naibu Waziri huyo amesema Serikali itaendelea na jitihada za kuboresha miundombinu ya reli na bandari hivyo kazi ya watendaji iwe ubunifu wa kibiashara ili kuiwezesha Serikali kupata faida.

Mwenyekiti wa taasisi zilizo chini ya wizara ya ujenzi,uchukuzi na mawasiliano ambae pia ni Meneja wa Wakala wa Barabara mkoa wa Kigoma (TANROADS) eng. Narcis Choma amemhakikishi Naibu Waziri Ngonyani kuwa wamejipanga kuhakikisha wanaboresha miundombinu ya mkoa wa Kigoma ili kukuza uchumi wa watu wa  kanda ya magharibi.


Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.



Viewing all 46343 articles
Browse latest View live




Latest Images