Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1048 | 1049 | (Page 1050) | 1051 | 1052 | .... | 1903 | newer

  0 0


   Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mkuu wa Chuo Kikuu Huria Tanzania, Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda wakati wakielekea kwenye Viwanja vya Chuo hicho, Bungo Kibaha Mkoani Pwani, katika Mahafali ya 31 ya Chuo hicho. 
   
  Sehemu ya Wahitimu wa Kozi mbalimbali wa Chuo Kikuu Huria wakiwa katika Mahafali hayo.

  0 0

  Na Humphrey Shao,Globu ya Jamii

  Katibu mkuu wa Wizara ya habari  Sanaa na michezo Profesa Elisante Ole Gabriel amesema kuwa tatizo la ukosefu  wa ajira Afrika ni matokeo na sio tatizo kama watu wanavyosema ama dhania.

  Profesa Gabriel amesema hayo katika Mdahalo wa wanazuoni  kutoka Afrika Mashariki uliofanyika katika ukumbi wa mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam leo.

  "Tatizo kubwa la Afrika ni soko na kubadilisha fikra za vijana katika bara letu kwa  kupata ellimu juu ya namna   Watakavyoweza kujikwamua kiuchumi  hali itakayosadia kuondokana na umaskini uliokithiri hivyo ifike hatua watu wasiwe wanahitaji kupewa pesa pindi inapohitaji kupewa elimu "amesema Profesa Gabriel

  Amewataka wakufunzi wa vyuo kurudi vyuoni na kubadilisha mawazo ya vijana kurudi katika mtazamo chanya wa kujipatia maendeleo kuliko kusubiri kusukumwa na watu juu ya kupata ajira.
   Profesa Elisante Ole Gabriel akizungumza katika Mjadala huo
  washiriki wakimsikiliza Profesa Ole Gabriel

  0 0

    Mratibu Msaidizi na Katibu mwenezi,Habari na Mawasiliano wa Muungano wa wapiga kura Tanzania Berrynice Mayunga akizungumza na waandishi wa habari, kulia ni Mshauri wa Muungano wa wapiga Kura Tanzania Mchungaji Donald Mathew.

  Na Amina Kibwana,Glabu ya Jamii

    Muungano wa wapiga kura Tanzania (TANVU) umeandaa matembezi ya Hiayari ya upandaji mti kwa lengo la kuunga mkono  Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ya Awamu ya tano.

    Matembezi hayo yanatarajiwa kuanza rasmi Novemba 26 hadi 30,2016, ambayo yataanzia Mkoani Singida wilaya ya Ikungi hadi Mkoa wa Dodoma ambapo zaidi ya wazalendo 600 wnatarajiwa kuhudhuria katika matembezi hayo.

    Akizungumza na waandishi wa habari Mratibu Msaidizi na Katibu mwenezi,Habari na Mawasiliano Barrynice Mayunga amesema kuwa katika matembezi hayo kutakuwa na upandaji wa miti ipatayo 12,500 (Elfu kumi na mbili na miatano)  kwa ajili ya utunzaji wa mazingira na misingi endelevu kwa viwanda.

    Amesema Mayunga, kwa kufanya hivyo pia itasaidia kujenga na kudumisha uzalendo ndani ya mioyo ya watanzania pamoja na kufanya kazi kwa kutumia kauli mbiu ya Rais Dkt John Pombe Magufuli wa Hapa kazi tu.

    "Sisi kama wazalendo tumeamua kujitoa kwa kufanya mate mbezi ya hiyari ili tuweze kukamilisha shughuli za upandaji miti kwa kuisaidia serikali ya awamu ya tano katika kuzisimamia rasilimali za nchi yetu."

    Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mipango na Uwezeshaji John Meena amesema kuwa miti ni pamoja na mikakati ya utunzaji wa mazingira kwani bila kuwa na miti kunaweza kusababisha madhara mbalimbali katika nchi ikiwemo, kuharibika kwa mifugo, kusababisha ukame nchini, Kupotea kwa mazao ya asili kama mbao,asali na matunda pamoja na kushuka kwa uzalishaji wa mazao na kuharibika kwa miundombinu ya hali ya hewa.
   
    Hata hivyo Muungano wa wapiga kura Tanzania (TANVU) umetoa wito kwa wanachi wote kujiandikisha na kuungana nao katika matembezi haya ili waweze kufikia lengo kwa pamoja kama wazalendo, Pia wameipomgeza serikali  yaawamu ya tano kwa jitihada inayoionesha katika kusimamia masuala mazima ya uwajibikaji kwa wanachi wake.

  0 0

  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
  WIZARA YA MALIASILI NA UTALII

  TAARIFA KWA UMMA

  MAADHIMISHO KITAIFA YA SIKU YA UTALII DUNIANI NA MAONESHO YA ‘’KARIBU KUSINI’’ 2016


  Wizara ya Maliasili na Utalii  kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa  Mkoa wa Iringa, Mradi wa kuboresha Mtandao wa Hifadhi za Kusini mwa Tanzania (SPANEST)  pamoja na Wadau wa Sekta ya Utalii nchini watashiriki  katika Maadhimisho ya Siku ya Utalii Duniani   kwa mwaka 2016 sambamba na Sherehe za maadhimisho ya ‘’Karibu Kusini ‘’ Karibu Tanzania Southern Circuit’’  ambayo  Kitaifa yataadhimishwa   Mkoani Iringa kwenye viwanja vya  Kichangani  kuanzia tarehe 25 hadi 29 Novemba, 2016.
  Lengo la maadhimisho hayo ni  kuweka uelewa kwa Jamii kuhusu umuhimu wa utalii na thamani yake ikiwa pamoja na  kuutangaza Utalii kwa kuihamasisha jamii kutumia fursa za utalii zilizopo katika kuinua uchumi wa wakazi wa Ukanda wa Kusini mwa Tanzania na Taifa kwa ujumla
  Kauli Mbiu ya maadhimisho ya Siku ya Utalii Duniani kwa mwaka  2016  ni “Utalii kwa wote – wote wawezeshe’’ (Tourism for All – Promoting Universal Accessilibity). Kwa kuzingatia Kauli Mbiu hii, Serikali inatambua kuwa kuna watu wenye mahitaji maalumu kama vile walemavu, wazee na watoto ikisisitiza miundombinu rafiki, gharama nafuu kutembelea  vivutio vya utalii na gharama nafuu za usafiri ili kuhakikisha kwamba, utalii unawahusisha watu wengi zaidi kunufaika nao.
  Katika Maadhimisho hayo, Wizara itakuwa na washiriki ambao ni Idara pamoja na Taasisi zake mbalimbali. Idara zitakazoshiriki ni Utalii, Wanyamapori, Mambo ya Kale na Misitu na Nyuki.
  Kwa upande wa Taasisi zitakazoshiriki  ni Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Chuo cha Taifa cha Utalii, Makumbusho ya Taifa, Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, Mamlaka ya Usimamizi ya Wanyamapori (TAWA) Mfuko wa Misitu Tanzania  (TaFF) Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, (TFS)  Taasisi ya Utafiti wa Misitu na Wadau wa Wizara ya Maliasili na Utalii.
  Wadau wa Sekta ya Utalii kutoka mikoa  ya Nyanda za Juu Kusini watashiriki kuonesha bidhaa na huduma zao muhimu. Mikoa hiyo ni pamoja na Iringa, Njombe, Ruvuma, Mbeya na Songwe
  Aidha, Wizara itatoa punguzo kwa watanzania kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Ruaha pamoja na vivutio vya utalii vilivyokaribu na mji wa Iringa ambavyo ni Ismila,Kalenga na Boma la Mkuu wa Wilaya  kwa gharama nafuu.
  Kupitia Maadhimisho hayo wito unatolewa kwa kuwaalika wadau wote wa utalii na jamii husika kwa pamoja na kuadhimisha siku hii kama ishara ya jitihada za pamoja za kuufanya utalii nguzo ya kweli ya maendeleo ya jamii na maendeleo ya jamii ni chanzo cha sekta ya utalii endelevu zaidi.
   Imetolewa na:
  Kitengo cha Habari na  Mawasiliano Serikalini
  Wizara ya Maliasili na Utalii.


  0 0

           Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema Serikali inajipanga kuondoa utitiri wa kodi mbalimbali zinatozwa kwenye viwanda kama hatua ya kuviwezesha viwanda vingi nchini kuongeza uzalishaji na kutoa ajira nyingi kwa watanzania.

  Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo leo Jijini Arusha baada ya kutembelea kiwanda cha kutengeneza mafuta ya kupikia cha Mount Meru Millers ili kujua changamoto zinazokikabili kiwanda hicho ili Serikali iweze kuzifanyia kazi katika kuleta unafuu kwenye uzalishaji wa mafuta ya kupikia nchini.

  Makamu wa Rais amesema mlolongo wa kodi zinazotozwa kwa wamiliki wa viwanda hazina uratibu mzuri hivyo mkakati ya Serikali wa awamu ya Tano inataka kuweka utaratibu mzuri wa ulipaji wa kodi hizo ikiwemo kuondoa kodi ambazo ni kero kwenye viwanda.

  Amesisitiza kuwa Serikali ya awamu ya Tano imedhamiria kuhakikisha viwanda vingi vinajengwa nchini ambavyo vitatumia malighafi zinazozalishwa hapa nchini hali ambayo itasaidia uuzaji wa bidhaa zinazozalishwa ndani ya nchi kuuzwa kwenye masoko ya nje ya nchi na kuliingizia taifa mapato na kuongeza ajira kwa makundi mbalimbali ya wananchi.

  Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amesema ziara ambazo anafanya kwenye viwanda mkoani Arusha ni kujionea jinsi viwanda hivyo vinavyofanya kazi za uzalishaji na pale kwenye changamoto zinazokwamisha viwanda hivyo kufanya kazi vizuri ziweze kufanyia kazi na Serikali.

  Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Mount Meru Millers Atul Mittal amesema kama Serikali itafuta au kuondoa utitiri wa kodi wanazotozwa kwenye Viwanda hivyo watakuwa na uwezo wa kuongeza maradufu uzalishaji na kutoa ajira nyingi kwa Watanzania.

  Amesema kwa sasa Kampuni hiyo inafanya kazi kwenye nchi 10 barani Afrika na kwa Tanzania pekee imeajiri wafanyakazi zaidi ya 1000 ambao wanafanyakazi katika maeneo mbalimbali nchini.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na uongozi wa kiwanda cha Mt. Meru Millers mara baada ya kufanya ziara kiwandani hapo.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Mt. Meru Bw. Atul Mittal akitoa taarifa kwa Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan juu ya maendeleo ya kiwanda pamoja na changamoto wanazokutananazo wafanyabiashara wazawa.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia malighafi zinazotumika kuzalishia mafuta ya kupikia kutoka kiwanda cha Mt. Meru Miller kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Mt. Meru Bw. Atul Mittal akitoa ufafanuzi juu ya malighafi hizo.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia malighafi zinazotumika kuzalishia mafuta ya kupikia kutoka kiwanda cha Mt. Meru Miller mjini Arusha.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akingalia ndoo za plastiki zinazotengenezwa na kampuni ya Mt. Meru Millers kwa ajili ya kuhifadhia mafuta ya kula ,kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Mt. Meru Bw. Atul Mittal.

  0 0

   Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme nchini, (TANESCO), Mhandisi Felchesmi Mramba, (katikati), akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, leo Novemba 24, 2016. Alikuwa akitoa ufafanuazi kuhusu masuala muhimu ya TANESCO. Wengine pichani, kulia ni Meneja wa Vyuo vya TANESCO, Mhandisi Said Msemo na kushoto ni Kaimu Meneja Uhisano wa Shirika hilo, Leila Muhaji.
  NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID

  SERIKALI kupitia Shirika lake la umeme nchini TANESCO limefanya uwekezaji mkubwa kwenye miradi mbalimbali ya umeme yenye thamani ya Shilingi Trilioni 5.35, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo, Mhandisi Felchesmi Mramba amewaambia waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, leo Novemba 24, 2016.

  Akitoa ufafanuzi juu ya masuala mbalimbali muhimu ya Shirika hilo, Mhandisi Mramba alisema, “Katika historia ya sekta ya umeme, haijawahi kutokea uwekezaji mkubwa kufanyika kwa wakati mmoja kama ilivyo sasa, Miradi yote ya umeme inayoendelea na ambayo tayari iemtengewa fedha ina thamani ya Shilingi Trilioni 3.85, na majadiliano kati ya Serikali na Exim Bank ya mradi wa Dar es Salaam-Arusha wa Shilingi Trilioni 1.5 yakiwa katika hatua za mwisho.” Alifafanua Mhandisi Mramba.

  “ Uwekezaji huu unathibitisha kwamba nia ya Serikali ya awamau ya tano ya kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda sio ya maneno matupu bali inaambatana na vitendo kwa uwekezaji madhubuti kwenye umeme.” Alisema.

  Mhandisi Mramba alitaja Miradi hiyo mikubwa ya umeme kuwa ni pamoja na ule wa upanuzi wa Kinyerezi I, Kinyerezi II, mradi wa Backbone, Kenya-Tanzania, TEDAP, Makambako-Songea, Uboreshaji umeme jijini Dar es Salaam, City Centre-Dar es Salaam, Electricity V, Bulyanhulu-Geita, Geita Nyakanazi na Rusumo Power Plant (T), miradi yote hii ikiwa na jumla ya thamani ya Shilingi Trilioni 3.85.

  Akifafanua zaidi kuhusu uwekezji huo, Mhandisi Mramba alisema, Miradi yote ambayo thamani yake imetajwa haihusishi Miradi ya usambazaji umeme Vijijini chini ya mpango wa REA.Akizungumzia utaratibu mpya wa manunuzi,(Procumbent), Mhandisi Mramba alisema, TANESCO imechukua hatua kadhaa ili kuboresha manunuzi ambapo kuanzia sasa makampuni yanayomilikiwa na mtu mmoja kuhodhi manunuzi ya Shirika hilo, na kwamba zabuni zote zilizotangazwa kuanzia mwaka huu wa fedha, haitaruhusiwa kampuni moja kuwa na mikataba miwili kwa wakati mmoja.

  Akifafanua zaidi alisema, Katika zabuni moja haitaruhusiwa kampuni moja kupewa zaidi ya Lot 1, “Hii imeanza kusaidia kuondoa ukiritimba katika manunuzi na kuwapa Watanzania wengi zaidi nafasi pana ya kushiriki katika zabuni za kusambaza vifaa vya umeme.” Alifafanua Mhandisi Mramba.

  Aidha Mhandisi Mramba alisema, ili kuwezesha Watanzania wengi kushiriki katika uchumi wa nchi, TANESCO itanunua vifaa vya umeme vinavyozalishwa hapa nchini na kuachana na mtindo wa kuagiza kutoka nje.

  “Mfano kwa nguzo za umeme tumewapa Sao Hill, ambao watatuuzia nguzo 96,500, na new Forest watatuuzia nguzo za umeme 9,668, na kwa upande wa Transfoma za umeme, kandarasi hiyo imepewa kampuni ya TANELEC itakayotuuzia transfoma 1,500” Alifafanua.

  Akieleza zaidi kuhusu ununuzi wa vifaa, Mhandisi Mramba alisema, kampuni ya East Africa Cables, intarajiwa kupewa kazi ya kusambaza waya na kuongeza kuwa utaratibu huo pia utatumika kwenye huduma nyingine kama vile Bima, ambapo alisema Shirika linatarajia kulitumia Shirika la Bima la Taifa, (NIC), kutoa huduma hiyo.

  Akizungumzia kuhusu hali ya umeme, Mhandisi Mramba aliwahakikishia Watanzania kuwa kutokana na uwekezaji mkubwa uliofanywa na Shirika hilo katika kuboresha miundombinu ya umeme, hakutakuwa na mgao wa umeme nchini na ndio maana kwa muda mrefu sasa hakuna mgao wa umeme.“Mwaka 2015 nchi ilikuwa na mgao wa umeme wa jumla ya MW300, na maeneo mengine yalikuwa na hali mbaya hususan Mwanza, Arusha na Kilimanjarolakini kwa sasa hali ya umeme katika mikoa yote na mingine ni nzuri hakuna mgao na kama ikitokea umeme umekatika ni matatizo ya kiufundi katika eneo dogo na kwa muda mfupi.” Alisema.

  Hata hivyo alisema Shirika lake linaongeza juhudi za kusambaza umeme kwa watanzania wengi zaidi kote nchini, kutokana na uwekezaji wa miundombinu unaoendela kila kona ya nchi.Mhandisi Mramba aliwaondoa wasiwasi wananchi kuhusu ombi la Shirika hilo la kuongeza asilimia 18.9 ya bei ya umeme kuanzia Januari mwakani, kwa kusema ongezeko hilo halitaathiri watumiji wa kawaida majumbani.

   “Tunachoomba kutoka kwa Msimamizi (Regulator), ni kufanya mabadiliko ya kutenganisha watumiaji umeme wa majumbani na wale wanaotumia kibiashara kama vile mabango ya matangazo, kwani hivi sasa wote wanalipa gharama sawa na hili si sawa.” Alisema.

  Aliwaasa wananchi kuridhia ongezeko hilo kwani Shirika limo katika jitihada kubwa za kuhakikisha Wananchi wengi zaidi wanapatiwa umeme kwa kufikisha miundombinu ya umeme kwenye maeneo mbalimbali ya nchi, ambapo gharama za kufanya hivyo zimeongezeka.
   Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria mkutano huo
    Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria mkutano huo
   Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO, Leila Muhaji, (kushoto), akizunguzma jambo

  0 0

   Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Profesa Shadrack Mwakalila (kushoto), akihutubia wakati akifungua Baraza la Wahitimu wa chuo hicho, Dar es Salaam leo.
   Katibu wa Baraza la Wahitimu wa chuo hicho, Jumanne Muruga (kushoto), akihutubia katika baraza hilo.
   Mwenyekiti wa Baraza hilo, Simon Simalenga (katikati), akiongoza baraza hilo. Kulia ni Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Profesa Shadrack Mwakalila na kushoto ni Katibu wa baraza hilo, Jumanne Muruga.

   Diwani wa Kata ya Mbezi, Humphrey Sambo ambaye aliwahi kuwa Rais wa Serikali ya chuo hicho (MASO), akichokoza mada katika baraza hilo.
   Wimbo wa Taifa ukiimbwa.
   Meza kuu ikimba wimbo wa taifa.
   Wanachuo wakiimba wimbo wa taifa.
   Taswira ya mkutano huo.
   Baraza likiendelea.
  Majadiliano yakiendelea.
   Wanafunzi wakisikiliza mada kwa makini.
   Taswira ya ukumbi.
  Mwanahabari Suleiman Msuya ambaye ni muhitimu wa chuo hicho, akichangia mada katika baraza hilo.
  Wanafunzi wakisikiliza mijadala.
  Vyeti vikitolewa
  Picha ya pamoja.  Na Dotto Mwaibale

  MKUU wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Profesa Shadrack Mwakalila amesema chuo hicho kipo katika mpango wa kujenga miundombinu mizuri ili wanafunzi wapate elimu katika mazingira bora.

  Profesa Mwakalila ameyasema hayo wakati akifunga Baraza la Wahitimu wa chuo hicho lililofanyika chuoni hapo Dar es Salaam leo kutokana na maombi ya wahitimu wa chuo hicho wanaounda baraza hilo kulalamikia miundombinu katika shule hiyo.

  "Ni kweli tunachangamoto kubwa ya miundombinu hapa chuoni lakini tupo katika mpango wa kuijenga kwani tayari Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) wameanza kuandaa michoro ya majengo na fedha tunategemea kupata kutoka kwa mifuko ya hifadhi ya jamii kwa ajili ya ujenzi na sasa tupo katika mazungumzo nao" alisema Mwakalila.

  Alisema miundombinu  hasa madarasa na hosteli ni changamoto kubwa kwani kutokana na sifa ya chuo hicho wanafunzi wamekuwa wakiongezeka kila mwaka hivyo kusababisha changamoto hiyo ambayoitakwisha muda si mrefu.

  Akizungumzia kuhusu la Baraza la Wahitimu alisema lilianzishwa kwa mujibu wa sheria ya chuo na lipo chini yake na lengo kubwa ni kupata na kutunza orodha ya wahitimu pamoja na anuani zao, kuandaa mikutano na makongamano yenye mada zinazohusu maendeleo ya chuo pamoja na serikali na jamii kwa ujumla na kutafuta vyanzo vya mapato ya kusaidia maendeleo ya chuo.

  Katibu wa baraza hilo John Muruga alisema kamati yao imebaini kuwa udahili wa wanafunzi umekuwa ukiongezeka mwaka hadi mwaka ambapo kwa mwaka 2016/ 2017 ni wanafunzi 2363 walidailiwa wanafunzi 553 wakiwa wa programu ya Astashahada, wanafunzi 471 wa programu ya Stashahada na wanafunzi 1339 wakiwa ni wa programu ya shahada ya kwanza.

  "Idadi hii ya udahili inajumuisha pia wanafunzi waliodahiliwa katika Tawi la chuo cha Zanzibar ambao ni 354 " alisema Muruga.

  0 0

   Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Profesa Makame Mbarawa (kulia) akiongea na baadhi ya wajumbe wa menejimenti ya Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) alipotembelea wakala huo mapema jana. KushOto ni Mtendaji Mkuu wa TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu. 
   Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Profesa Makame Mbarawa (kulia) akisikiliza maelezo ya dereva wa serikali aliepeleka gari lake katika karakana ya Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) MT. Depot iliyoko Dar es Salaam kuhusu ubora wa huduma pamoja zinazotolewa alipotembelea na kukagua karakana hiyo jana.
   Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Profesa Makame Mbarawa (kushoto) akiongea na Mafundi wa karakana ya  Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) MT. Depot iliyoko Dar es Salaam alipotembelea  na kukagua karakana hiyo jana.
   Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Profesa Makame Mbarawa(kushoto) akiangalia vifaa vilivyopo katika stoo ya vifaa vya matengenezo ya magari katika karakana ya Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) MT. Depot iliyoko Dar es Salaam kulia ni Mtendaji Mkuu wa TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu .
  Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Profesa Makame Mbarawa (aliye simama) akiongea na baadhi ya watumishi wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) katika ukumbi wa karakana ya MT. Depot alipotembelea wakala huyo mapema jana.

  Picha na Theresia Mwami – TEMESA

  0 0

   Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Bi.Halima Dendegu akizungumza jambo wakati wa ufunguzi wa semina ya siku moja ya mafunzo kwa viongozi wa mikoa ya Mtwara na Lindi kuhusuUratibu,usimamizi na ufuatiliaji wa utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Uwezeshaji wananchi kiuchumi ya mwaka 2004.  Mafunzo hayo yamefanyika mkoani Mtwara na kuratibiwa na Baraza la Taifa la Uwezeshaji wananchi kiuchumi (NEEC).
   Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) Bi.Beng’i Issa akifafanua jambo kwenye semina elekezi kwa viongozi wa mikoa ya Mtwara na Lindi kuhusu uratibu, usimamizi na ufatiliaji wa utekelezaji wa sera ya Taifa ya Uwezeshaji wananchi kiuchumi ya mwaka 2004. Kushoto kwake ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Lindi, Bw .Ramadhani Kaswa.  Mkutano huo umefanyika mkoani Mtwara jana na kuratibiwa na NEEC.
  Viongozi wa mikoa ya Mtwara na Lindi wakifatilia mada katika semina ya mafunzo juu ya uratibu, usimamizi na ufatiliaji wa utekelezaji wa sera ya Taifa ya Uwezeshaji wananchi kiuchumi ya mwaka 2004.  Mkutano huo ulifanyika jana Mkoani Mtwara na kushirikia Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri wa mikoa hiyo na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC)

  Na mwandishi wetu, Mtwara
   Viongozi wa Mikoa ya Mtwara na Lindi wametakiwa kutafsiri katika vitendo mafunzo kuhusu uratibu, usimamizi na ufuatiliaji wa utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi ya Mwaka 2004 kwa kuwajengea uwezo wananchi katika kuibua fursa zitakazowaletea  maendeleo.


   Akishiriki katika mafunzo ya siku moja mjini hapa jana  juu ya utekelezaji wa sera ya uwezeshaji  iliyoratibiwa na Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi(NEEC), Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Bi Halima Dendegu, aliwambia viongozi kwamba mkoa hiyo miwili imejaliwa mambo mengi na kwa hiyo wananchi wanayo fursa ya kushinda umaskini iwapo wataongozwa vizuri.

  “Tukatekeleze kwa vitendo elimu tunayoipata kutoka kwa wezeshaji wetu na ikawe na tafsiri halisi kwa wananchi katika maendeleo,” alisema Bi.Dendegu aliyefungua mkutano huo.


  Amesema wajibu wa viongozi hao  ni  kuwachachua  kifikra wananchi katika maeneo yao  ili wawe wabunifu katika kuibua fursa na kuzifanyia kazi na wajipatie  maendeleo.


  “Mafunzo haya yatajenga uelewa wa pamoja kwa viongozi na utekelezaji uwe wa pamoja katika mikoa yetu,” alisema  na kuongezea kuwa  mafunzo haya hayatakuwa na maana kama tafsiri yake haitaonekana kwenye ngazi ya jamii.


  Bi.Dendegu alizitaja fursa zilizopo Mkoani Mtwara ambazo wananchi waongozwe kuzifaidi kuwa ni zao la korosho, gesi asilia, ardhi kwa kilimo, fukwe za Bahari ya Hindi, bandari na kiwanda cha cement cha Dangote , na kusema haya  ni maeneo ambayo wananchi wanaweza kubuni miradi itakayoendana na fursa hizo.


  Alisema serikali itahakikisha kuchagua masoko ya bidhaa zitakazozalishwa na wananchi zinauzika kwa bei nzuri kama ilivyo katika zao la korosho kwa mwaka msimu huu.


  Alishukuru NEEC kwa mikoa ya Mtwara na Lindi  na kuahidi kutoa ushirikiano ili kutimiza azma ya serikali ya kufikia uchumi wa kati.


   Katibu Mtendfaji wa NEEC, Bi.Beng’i Issa,  amesema madhumuni ya mafunzo haya ni kuwajengea uwezo Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri za mikoa hiyo miwili   juu ya sera ya uwezeshaji wananchi kiuchumi.


  ”Viongozi wengi ni wageni katika nyadhifa zao; hivyo  imetulazimu kutoa mafunzo haya ili kuwe na ushirikiano na waratibu wa madawati ya uwezeshaji katika ngazi za halmashauri,” amesema Bi.Issa


  Amesifia  mwitiko wa wajumbe katika mafunzo haya  kwa kuwa viongozi wote wamehudhuria.

  Mawazo ya wajumbe katika kuchangia mada yameboresha mikakati ya kuwawezesha wananchi kiuchumi, amesema na kuongeza kuwa  ushirikiano wa viongozi na wananchi ndio njia pekee ya kufika malengo ya kumuinua mwananchi kutoka  kipato cha chini na kufikia kipato cha kati.

   Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea,  Bi.Rukia Muwango, amesema mafunzo yatawasaidia viongozi  kuwajengea uwezo wananchi  juu ya dhana ya uwezeshaji.

  Ameonyesha  na kusisitiza  umuhimu wa wananchi  kutunza fedha na kujiwekea akiba na kuwekeza katika fursa mbalimbali ili kukuza vipato vyao.


  NEEC itaendelea kufanya mafunzo haya kwa kanda tano nchini ili viongozi wote wawe  na fafsiri moja katika dhana ya uezeshaji wananchi kiuchumi.

  0 0    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na baadhi ya wahitimu wa  Shahada ya Uzamivu ya Udaktari wa Falsafa  wakati wa mahafali ya 31 ya  Chuo Kikuu Huria cha Tanzania yaliyofanyika kwenye kampasi ya chuo hicho huko huko Bungo, Kibaha,  mkoa wa Pwani leo Novemba 24, 2016.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na  baadhi ya wahadhiri wakati wa mahafali ya 31 ya  Chuo Kikuu Huria cha Tanzania yaliyofanyika kwenye kampasi ya chuo hicho huko huko Bungo, Kibaha,  mkoa wa Pwani leo Novemba 24, 2016
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipiga makofi wakati Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) na Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Mizengo Pinda akimtunuku Shahada ya Uzamivu ya Udaktari wa Falsafa mhitimu Hebson Opiyo Andala kutoka Rwanda wakati wa mahafali ya 31 ya chuo hicho yaliyofanyika kwenye kampasi ya OUT huko Bungo, Kibaha,  mkoa wa Pwani leo Novemba 24, 2016
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akihutubia wakati wa mahafali ya 31 ya  Chuo Kikuu Huria cha Tanzania yaliyofanyika kwenye kampasi ya chuo hicho huko huko Bungo, Kibaha,  mkoa wa Pwani leo Novemba 24, 2016
   Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Profesa, Joyce  Ndalichako  akihutubia wakati wa mahafali ya 31 ya  Chuo Kikuu Huria cha Tanzania yaliyofanyika kwenye kampasi ya chuo hicho huko huko Bungo, Kibaha,  mkoa wa Pwani leo Novemba 24, 2016.
  Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) na Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Mizengo Pinda akimtunuku Shahada ya Uzamivu ya Udaktari wa Falsafa mhitimu Philip Filikunjombe wakati wa mahafali ya 31 ya chuo hicho yaliyofanyika kwenye kampasi ya OUT huko Bungo, Kibaha,  mkoa wa Pwani leo Novemba 24, 2016
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Profesa, Joyce Ndalichako,    Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) na Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Mizengo Pinda,  Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu Huria cha Tanzania Profesa Samuel Wangwe Makamu Mkuu wa Chuo hicho  Prof. Elifas Bisanda  wakiondoka jukwaa kuu baada ya kuhitimisha mahafali ya 31 ya chuo hicho yaliyofanyika kwenye kampasi ya OUT huko Bungo, Kibaha,  mkoa wa Pwani leo Novemba 24, 2016.

  PICHA NA IKULU
    Serikali itaendelea kusimamia ubora wa elimu kwa kuhakikisha shule na taasisi zinadahili wanafunzi wenye sifa stahiki za kujiunga na kozi wanazoomba.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametoa kauli hiyo leo tarehe 24 Novemba, 2016 katika sherehe za mahafali ya 31 ya Chuo Kikuu Huria Tanzania zilizofanyika Bungo, Kibaha Mkoani Pwani.

  Kabla ya Rais Magufuli kutoa kauli hiyo, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria Prof. Elifas Tozo Bisanda alieleza kuwa chuo hicho kimeshindwa kudahili idadi kubwa ya wanafunzi baada ya Tume ya Vyuo Vikuu (TCU) kuzuia udahili wa wanafunzi wanaotaka kujiunga na masomo ya elimu ya juu kwa kutumia sifa ya kupatiwa kozi ya awali (Foundation Course) ambayo imekuwa ikitumiwa na wanafunzi wasio na sifa za kujiunga vyuo vikuu kwa vigezo vya TCU.

  "Kwa vile mnachukuliwa sawa na vyuo vingine ni lazima mzingatie vigezo vya mtu kuitwa mhitimu wa Chuo Kikuu, kwa hiyo nasema kwa dhati nakubaliana sana tena kwa asilimia 100 na yale yaliyozungumzwa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Ufundi Prof. Joyce Ndalichako.

  "Kwa hiyo ni lazima hili suala la kuweka viwango vya ubora wa elimu yetu tulizingatie, ni mara kumi tuwe na wanafunzi hata 10 wanaohitimu elimu ya juu kuliko kuwa na wanafunzi 20,000 wakati hawana sifa, kwa sababu tutakapokwenda kwenye ajira hatutauliza kama huyu ametoka Chuo Kikuu Huria, huyu ametoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ama huyu ametoka Chuo Kikuu cha Dodoma, wote tutawaangalia kwa usawa.

  "Tusitafute njia ya mkato, njia ya mkato ni mbaya, kwa hiyo kwa hili kwa kweli Mhe. Prof. Ndalichako nakubaliana na wewe, nafikiri ndio maana umekuwa Waziri wa Elimu, tunataka kulinda hadhi ya elimu yetu"amesema Dkt. Magufuli.

  Hata hivyo, Rais Magufuli amekipongeza Chuo Kikuu Huria kwa kazi nzuri ya kutoa elimu ya juu kwa Watanzania wengi na kuanzisha matawi katika nchi mbalimbali za Afrika na ameahidi kuwa Serikali yake itaendelea kuunga mkono juhudi hizo ikiwa ni pamoja na kukabiliana na changamoto za miundombinu na mahitaji mengine.

  Aidha, Rais Magufuli amewaonya viongozi na watendaji wa taasisi mbalimbali za Serikali ambao wamekuwa wakitumia vibaya fedha za umma ikiwemo kuweka fedha nyingi za Serikali katika akaunti za muda maalum (Fixed Deposit Account) kwenye benki za biashara ambako hujipatia fedha kupitia faida ya akiba bila kujali kuwa vitendo hivyo husababisha Serikali kukosa fedha na kulazimika kukopa kutoka benki za biashara ambako hutozwa riba kubwa.

  "Sasa sifahamu kama Chuo Kikuu Huria na nyinyi mmekuwa mkiweka fedha za maendeleo katika Fixed Deposit Account, lakini huo ndio umekuwa ni mchezo, juzi hapa tumekuta fedha kiasi cha Shilingi Bilioni 26 zilizokuwa zimetolewa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa ajili ya matumizi ya TRA, zikapelekwa kwenye benki tatu kama Fixed Deposit Account na Bodi ya TRA ikapitisha, ndio maana nilipozipata hizo taarifa, fedha nikachukua na Bodi kwa heri.

  "Hata kwa sasa hivi Waziri upo hapa, Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) ambayo ilianzishwa kwa sababu maalum, inachangiwa fedha wakati kuna fedha zao wameziweka kwenye Fixed Deposit Account, Waziri hiyo ni message sent and Delivered"amesisitiza Rais Magufuli.

  Katika Mahafali hayo, Mkuu wa Chuo Kikuu Huria na Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Mizengo Kayanza Peter Pinda amewatunuku shahada na vyeti jumla ya wahitimu 4038, wakiwemo wahitimu 8 wa shahada ya Uzamivu, 217 wa shahada ya Uzamili, 111 wa Stashahada ya Uzamili, 1,186 wa Shahada ya Kwanza, 484 wa Stashahada na 1,421 wa vyeti mbalimbali.


  Gerson Msigwa
  Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
  Dar es Salaam
  24 Novemba, 2016.
  0 0

   Mkurugenzi wa Idara ya Uchambuzi na Ushauri wa Kazi wa Ofisi ya Rais-Utumishi, Bw. Mick Kiliba akitoa maelezo kuhusu Mafunzo ya siku mbili ya Ufuatiliaji na Tathmini kwa Wizara mbalimbali yanayofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Rais-Utumishi.
   Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bi Susan Mlawi, akifungua Mafunzo ya siku mbili ya Ufuatiliaji na Tathmini kwa Wizara mbalimbali yanayofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Rais-Utumishi.
   Baadhi ya washiriki kutoka Wizara Mbalimbali wakifuatilia mada wakati wa Mafunzo ya Ufuatiliaji na Tathmini yanayofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Rais-Utumishi.
   Mshiriki wa Mafunzo ya Ufuatiliaji na Tathmini kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Bi Mariam Silim akitoa neno la shukrani kwenye Mafunzo ya Ufuatiliaji na Tathminiyanayofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Rais-Utumishi.
  Mkurugenzi Msaidizi, Sehemu ya Ufuatiliaji na Tathmini ya Utendaji Kazi kutoka Ofisi ya Rais - Utumishi, Bi Sakina Mwinyimkuu akiwasilisha mada kwenye mafunzo ya Ufuatiliaji na Tathminiyanayofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Rais-Utumishi.

  Serikali imesema itahakikisha inaimarisha uwezo wa kitaasisi ili kumudu vyema kazi za ufuatiliaji na tathmini ikiwa ni pamoja na kutoa miongozo mbalimbali itakayosaidia kuboresha utendaji kazi za Ufuatiliaji na tathmini serikalini. 

  Hayo yamesemwa leo na Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bi. Susan Mlawi alipokuwa akifungua Mafunzo ya siku mbili ya Ufuatiliaji na Tathmini kwa Wizara mbalimbali yanayofanyika Ofisi ya Rais-Utumishi. 

  Mlawi alisema Mkakati wa Serikali wa kuimarisha Mfumo wa Ufuatiliaji na Tathmini kwa taasisi hizo kunatonakana na kukosekana kwa mfumo madhubuti wa Ufuatiliaji na Tathmini ambao ungetoa suluhisho la changamoto mbalimbali zinazozikabili Taasisi za Umma nchini. 

  “Kukosekana kwa mfumo madhubuti wa Ufuatiliaji na Tathmini katika taasisi za umma nchini umesababisha kukwama kwa utekelezaji wa majukumu ya kila siku na utoaji maamuzi sahihi,” 

  Bi. Mlawi aliongeza. Alidha, Kaimu Katibu Mkuu huyo alizitaja baadhi ya changamoto zinazoikabili Serikali kuwa ni pamoja na baadhi ya taasisi zake kulalamikiwa na wananchi kwa kutoa huduma zisizoridhisha, utendaji ambao haulingani na thamani halisi ya uwekezaji wa fedha za Umma katika taasisi hizo, mchango mdogo wa baadhi ya Taasisi za Umma katika kuchangia mapato katika Mfuko Mkuu wa Serikali, ongezeko la utegemezi kwa Serikali kuu, uzalishaji na tija ndogo na ukosefu wa vipaumbele katika taasisi hizo.

  Akitoa maelezo juu ya mafunzo hayo, Mkurugenzi wa Idara ya Uchambuzi na Ushauri wa Kazi wa Ofisi ya Rais-Utumishi, Bw. Mick Kiliba alitaja lengo hasa la mafunzo hayo ni kubadilishana uzoefu katika eneo la Ufuatiliaji na Tathmini ambayo washiriki wanayafanyia kazi, kujenga uwezo wa Wataalam wa Ufuatiliaji na Tathmini kwenye Wizara zao pamoja na kuona namna bora ya kuimarisha utendaji kazi katika taasisi za Serikali.

  “Eneo la Ufuatiliaji na Tathmini limekuwa likilega leg asana katika taasisi nyingi za Serikali hivyo tumeona ni vema tukakaa pamoja kuona namna bora ya kuliimarisha,” Bw. Kiliba aliongeza.

  Mafunzo hayo yameanza leo na yanahudhuriwa na wajumbe kutoka Wizara 12 ambazo ni Ofisi ya Waziri Mkuu, Ofisi ya Rais –Menejimenti ya utumishi wa Umma, Wizara ya Fedha na Mipango, Wizara ya Ardhi, Nyumba na maendeleo ya Makazi, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Wizara ya Maliasili na Utalii, Wizara ya Katiba na Sheria na Tume ya Mipango.

  Imetolewa na:
  Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,
  Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora)
  24 Novemba, 2016

  0 0

  Picha ikionyesha wa kwanza kushoto mwimbaji wa zamani wa bendi ya FM academia Kingombe Mohamed (kingblez) akisaini mkataba wa miaka mitano wa kufanyakazi katika bendi mpya ya East African Gwasuma music band ilipo jijini Arusha anayefata wa kwanza kulia ni wakili wa bendi hiyo Vivianus Rugakingira wanyuma wa kwanza ni mkurugenzi wa bendi hiyo Muktar Abdu Bolydo (Obama) na wafanyakazi wake wakishuhudia king blez akisaini mkataba wa kufanyakazi katika bendi hiyo kwa miaka mitano .
  Mkurugenzi wa bendi hiyo ya East African Ngwasuma Music bendi Mukhtar Abdul Bolydo (Obama) akisaini mkataba wa kumuajiri kingblez kwa muda wa mika mitano ambapo alisema amemchukuwa fm Academia kwa kiasi cha shilingi milioni 20 
   Afisa utamaduni wa jiji la Arusha Benson Maneno akimkabidhi KIng blez mkatabawake mara baada ya kusaini 
  meneja wa bandi akifatilia kwa makini mkataba wa wasanii hao
   Mkurugenzi wa bendi hiyo ya East African Ngwasuma Music bendi Mukhtar Abdul Bolydo (Obama) akitoa neno
  baadhi ya wasanii wa bendi ya East African gwasuma music band   Na Woinde Shizza,Arusha

  WASANII mbalimbali jijini hapa wanatarajiwa kuanza kupata neema ya kukuza vipaji vyao baada ya bendi mpya ya muziki kuanzishwa.

  Bendi hiyo mpya 'East African ngwasuma music band itakuwa ikifanya kazi zake jijini hapa.Mkurugenzi wa bendi hiyo ya East African Ngwasuma Music bendi Mukhtar Abdul Bolydo (Obama) alisema ni fursa kwa vijana wenye vipaji vya sanaa ya muziki katika uimbaji kujitokeza ili kuwania nafasi katika bendi hiyo.

  "Hivi sasa tumeanzisha bendi hii bado tunauhitaji wa vijana wasiopungua 20 kwani malengo yetu ni kuwa na bendi mbili hapo baadaye na ni wakati wa Arusha kupata burudani ya aina yake",alisema Abdul.

  Alisema bendi hiyo itaongozwa na msanii nguli wa muziki kutoka Fm Academia ambaye amehama na kujiunga na bendi hiyo mpya kwa kiasi cha shilingi Milioni 20 na amesaini mkataba wa miaka mitano wa utoaji wa huduma ya muziki.

  Msanii huyo 'King of the king'king'(mzee wa mujini) Kingombe Mohammed alisema ataitumikia bandi hiyo kwa ajili ya kutoa burudani."Nimekuwa FM Academia kwa miaka mingi hivi sasa nimehama na tumeamua kuanzisha bendi mpya itakayokuwa moto wa burudani,".alisema Mohammed.

  Bendi hiyo mpya ya East African Ngwasuma Music bendi yenye makao yake makuu jijini hapa, ina jumla ya wasanii 12 kati yao wawili wanawake na kila msanii ana mkataba wa miaka miwili na baada ya hapo kama atafanya vizuri ataendelea kutumikia kulingana na uwezo wake.

  0 0

  Secretary General of the EAC, Amb. Liberat Mfumukeko and Ambassador of the Federal Republic of Germany His Excellency Egon Kochanke signs the agreement as Ms Lena Thiede, Counsellor / Head of Regional Cooperation at the German Embassy in Dar es Salaam; Director of KfW Development Bank Dr. Helmut Schon and EAC Deputy Secretary General (Productive and Social Sector) Hon Bazivamo looks on
  Amb. Liberat Mfumukeko and Ambassador of the Federal Republic of Germany pose for a picture after initialled Financing Agreement
  Secretary General of EAC , Amb. Liberat Mfumukeko signs the second agreement with KfW Development Bank Director, Dr. Helmut Schon
  Amb. Liberat Mfumukeko and KfW Development Bank Director, Dr. Helmut Schon displays the Financing Agreement document .


  The Secretary General of the East African Community, Amb. Liberat Mfumukeko having a chat with His Excellency Egon Kochanke, Ambassador of the Federal Republic of Germany to the United Republic of Tanzania and Accredited to the EAC
  ……………………………………………………………

  The Federal Republic of Germany, KfW Development Bank and the East African Community (EAC) today signed Financing Agreement of 40 million euros in total, to support regional immunization programme and establishment and operations of the Regional Laboratory Network for Communicable Diseases.

  The Secretary General of the East African Community, Amb. Liberat Mfumukeko signed on behalf of the Community while His Excellency Egon Kochanke, Ambassador of the Federal Republic of Germany to the United Republic of Tanzania and also accredited to the East African Community initialled on behalf the Germany Government and Dr. Helmut Schon, on behalf of KfW. 

  30 million euros in financial assistance will be invested in Immunization programmes in the EAC in collaboration with GAVI
  Another 10 million euros in financial assistance will be used in the operation of the Regional Laboratory Network for Communicable Diseases consisting of mobile laboratory units located at national reference laboratories.

  This new commitment will bring Germany’s contribution to fight child mortality through immunisation programmes to 90 million euros since 2013. So far about 50 million of Rota Virus Vaccines, Pneumococcal Vaccines and Pentavalent Vaccines have been financed in the EAC Partner States. Implicitly, an equal number of children have been vaccinated against the biggest killers of children, namely diarrhea and pneumonia.

  Speaking during the signing ceremony, the EAC Secretary General, Amb. Liberat Mfumukeko, thanked the Government of the Federal Republic of Germany for its support to the EAC. ‘’We have truly benefited from the German support which has catalysed other development Partners to support our projects and programmes.

  Amb. Liberat Mfumukeko underscored the assistance for the health sector in the EAC reaffirms Germany’s status as a true friend of the people of East Africa. H.E. Egon Kochanke, Ambassador said: “The new commitments underline that Germany continues to be a strong partner for the EAC, contributing to an integration process that puts the people in the centre”.

  On his part, the Director of KfW Development Bank, Dar es Salaam Office, Dr. Helmut Schon said ‘’the support from KfW underlines the importance we give to the East African Community’’ a regional approach under the EAC coordination makes very much sense to address communicable diseases.

  Accompanying Amb. Kochanke was Ms Lena Thiede, Counsellor/Head of Regional Cooperation at the German Embassy in Dar es Salaam, and Director of KfW Development Bank, Dr. Helmut Schon.

  Others at the function were EAC Deputy Secretaries General (Finance and Administration), Hon Jesca Eriyo; (Productive and Social Sector), Hon. Christophe Bavizamo and (Political Federation), Mr. Charles Njoroge.

  0 0


  0 0


  Na Mwandishi Wetu- Tanga.

  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye amekemea vikali baadhi ya tabia ya viongozi wa timu zinazoshiriki michezo mbalimbali kutumia wachezaji wasiostahili kutumika katika mashindano husika.

  Ameyasema hayo wakati akizindua mashindano ya michezo mbalimbali yanayoandaliwa na Shirikisho la Michezo ya mashirika ya Umma na Binafsi (SHIMMUTA) yanayoendelea Jijini Tanga ambayo yameshirikisha timu mbalimbali kutoka mashirika ya Umma na Binafsi Tanzania.

  Mhe. Nnauye amewataka viongozi wa SHIMMUTA kufanya uhakiki upya wa wachezaji wa timu shiriki ili kuondoa lawama zinazoweza kutokea na kupata mshindi anayestahili kwa kufata Sheria na taratibu zote za mashindano.“Nawaomba viongozi muangalie na kupitia upya wachezaji wa timu shiriki ili kusiwe na zengwe lolote katika mashindano haya na mshindi katika kila mchezo apatikane kihalali” alisisitiza Mhe. Nnauye.

  Aidha ametoa wito kwa mashirika kutenga muda na fedha ili kuwezesha timu zao kushiriki katika michezo ikiwa ni moja ya kujenga mshikamano na amani kwa watanzania na pia kujenga afya ya mwili na akili.Mashindano ya SHIMMUTA yameshirikisha mashirika ya Umma na Binafsi katika michezo 12 ikiwemo Mpira wa Miguu(Football), Mpira wa Pete(Netball),kuvuta kamba, Riadha, Mchezo wa vishale(Darts),Mchezo wa Pooltable, mchezo wa bao, Karata,kukimbia na magunia.
   Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza na washiriki wa mashindano ya SHIMMUTA wakati wa uzinduzi wa mashindano hayo Novemba 24, 2016 yanayofanyika Jijini Tanga.
  Baadhi ya Timu zikiwasili katika katika Uwanja wa Mkwakwani kwa ajili ya mashindano ya SHIMMUTA yanayofanyika Jijini Tanga.
  Baadhi ya Timu zikiwasili katika katika Uwanja wa Mkwakwani kwa ajili ya mashindano ya SHIMMUTA yanayofanyika Jijini Tanga.
  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye na Mwenyekiti wa SHIMMUTA Bw. Hamis Mkalachi wakipokea maandamano ya timu shiriki zilizopokuwa zikiwasili katika Uwanja wa Mkwakwani kwa ajili ya mashindano ya SHIMMUTA yanayofanyika Jijini Tanga.
  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akicheza muziki aina ya kwaito pamoja na wachezaji na viongozi wa timu shiriki wakati wa sherehe za uzinduzi wa mashindano ya SHIMMUTA yanayofanyika Jijini Tanga.
  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akikagua timu mbalimbali kabla ya kuanza kwa michezo mbalimbali wakati wa uzinduzi wa mashindano ya SHIMMUTA yanayofanyika Jijini Tanga.
  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akikagua timu mbalimbali kabla ya kuanza kwa michezo mbalimbali wakati wa uzinduzi wa mashindano ya SHIMMUTA yanayofanyika Jijini Tanga.
  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akipiga mpira kuashiria uzinduzi rasmi wa mashindano ya SHIMMUTA yanayofanyika Jijini Tanga.
  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akionesha ufundi wa kupiga danadana wakati wa uzinduzi rasmi wa wa mashindano ya SHIMMUTA yanayofanyika Jijini Tanga, akimshuhudia akipiga danadana hizo ni Mbunge wa Tanga Mjini Mhe.Musa Mbaruk.Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WHUSM.

   

  0 0

  -Usalama wa Wanawake kufuatia Mabadiliko ya Tabia Nchi

  Ukatili dhidi ya wanawake ni uvunjaji mkubwa wa haki za msingi za binadamu na tishio kwa mamilioni ya wasichana na wanawake duniani kote. Takribani mwanamke mmoja kati ya wanawake watatu duniani amekuwa akipigwa, kulazimishwa kufanya ngono, au kunyanyaswa vinginevyo katika maisha yake. 
   
  Jamii nzima imeathiriwa na ukatili ambao unaweza kuwa wa kimwili, kingono (unyanyasaji, kulazimishwa au kubaguliwa) na kisaikolojia (kunyanyaswa kwa maneno au kwa hisia, kama vile kuonewa au kutengwa).

  Katika siku hii ya Kimataifa ya Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake, UNESCO inaangazia mabadiliko ya tabia nchi na uhaba wa rasilimali kama sababu za kuchochea ukatili dhidi ya wanawake – nyumbani, mitaani, wakati wa majanga asilia yanayosababishwa na tabia nchi.

  Mabadiliko ya tabia nchi yanazidisha tishio - yanaweza kuongeza uhamaji na kukosa makazi kwa watu na kuchangia katika kutokuzalishwa kwa mazao au mafuriko, kuongeza msukumo nyumbani na katika utafutaji wa riziki. Utafiti unaonyesha kwamba wanawake wanawajibika kwa asilimia 65 ya uzalishaji wa chakula katika kaya huko Asia, kwa asilimia 75 katika nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara na kwa asilimia 45 huko Amerika ya Kusini. 
   
  Mara nyingi, ni wajibu wa kiutamaduni wa wanawake unaowaweka katika hatari kubwa dhidi ya madhara ya mabadiliko ya tabia nchi – na kwa hiyo kujikuta wakiwa katika mazingira yenye uwezekano wa kufanyiwa ukatili wanavyotembea maili nyingi kila siku kutafuta chakula, maji na kuni au baada ya kukosa makazi au kupata umasikini kutokana na majanga. 
   
  Kukosa njia za kujitafutia riziki na umasikini kunaweza pia kusababisha ukatili nyumbani kutokana na msukumo wa kiuchumi, pamoja na kuendelea kwa muda mrefu kwa mienendo ya ukeketaji wa wanawake na ndoa za utotoni.

  UNESCO inashiriki kikamilifu katika kuimarisha ujasiri wa kukabili mabadiliko ya tabia nchi, ujumuishaji wa mkabala wa kijinsia katika utendaji wake wote. Kwa kutumia ushirikiano na mipango ya kibunifu, UNESCO inaendeleza fikra inayodai kuwa wanawake na wasichana ni muhimu katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi, hasa, kwa mfano, mipango ya kusimamia maji na utayari wa kukabiliana na majanga. 

  Tunafahamu kwamba uzalishaji wa gesi ukaa unaiathiri sayari ya dunia. Tunapaswa pia tutambue kwamba mabadiliko ya tabia nchi yanaathiri maisha ya wasichana na wanawake duniani kote. 
   
  Tunapokuwa tupo tayari kuanza kutekeleza Mkataba wa Tabia Nchi wa Paris na kujiandaa kwa ajili ya mafanikio ya COP22 huko Marrekech, tusiisahau nusu ya idadi ya watu wetu na uwezo wao mkubwa wanaouwakilisha. Wanawake lazima wawe katika kiini cha utatuzi wote wa mabadiliko ya tabia nchi.

  0 0

  -Usalama wa Wanawake kufuatia Mabadiliko ya Tabia Nchi 

  Ukatili dhidi ya wanawake ni uvunjaji mkubwa wa haki za msingi za binadamu na tishio kwa mamilioni ya wasichana na wanawake duniani kote. 

  Takribani mwanamke mmoja kati ya wanawake watatu duniani amekuwa akipigwa, kulazimishwa kufanya ngono, au kunyanyaswa vinginevyo katika maisha yake. 
   
  Jamii nzima imeathiriwa na ukatili ambao unaweza kuwa wa kimwili, kingono (unyanyasaji, kulazimishwa au kubaguliwa) na kisaikolojia (kunyanyaswa kwa maneno au kwa hisia, kama vile kuonewa au kutengwa). 

  Katika siku hii ya Kimataifa ya Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake, UNESCO inaangazia mabadiliko ya tabia nchi na uhaba wa rasilimali kama sababu za kuchochea ukatili dhidi ya wanawake – nyumbani, mitaani, wakati wa majanga asilia yanayosababishwa na tabia nchi. 

  Mabadiliko ya tabia nchi yanazidisha tishio - yanaweza kuongeza uhamaji na kukosa makazi kwa watu na kuchangia katika kutokuzalishwa kwa mazao au mafuriko, kuongeza msukumo nyumbani na katika utafutaji wa riziki. Utafiti unaonyesha kwamba wanawake wanawajibika kwa asilimia 65 ya uzalishaji wa chakula katika kaya huko Asia, kwa asilimia 75 katika nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara na kwa asilimia 45 huko Amerika ya Kusini. 
   
  Mara nyingi, ni wajibu wa kiutamaduni wa wanawake unaowaweka katika hatari kubwa dhidi ya madhara ya mabadiliko ya tabia nchi – na kwa hiyo kujikuta wakiwa katika mazingira yenye uwezekano wa kufanyiwa ukatili wanavyotembea maili nyingi kila siku kutafuta chakula, maji na kuni au baada ya kukosa makazi au kupata umasikini kutokana na majanga. 
   
  Kukosa njia za kujitafutia riziki na umasikini kunaweza pia kusababisha ukatili nyumbani kutokana na msukumo wa kiuchumi, pamoja na kuendelea kwa muda mrefu kwa mienendo ya ukeketaji wa wanawake na ndoa za utotoni. 

  UNESCO inashiriki kikamilifu katika kuimarisha ujasiri wa kukabili mabadiliko ya tabia nchi, ujumuishaji wa mkabala wa kijinsia katika utendaji wake wote. Kwa kutumia ushirikiano na mipango ya kibunifu, UNESCO inaendeleza fikra inayodai kuwa wanawake na wasichana ni muhimu katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi, hasa, kwa mfano, mipango ya kusimamia maji na utayari wa kukabiliana na majanga. 

  Tunafahamu kwamba uzalishaji wa gesi ukaa unaiathiri sayari ya dunia. Tunapaswa pia tutambue kwamba mabadiliko ya tabia nchi yanaathiri maisha ya wasichana na wanawake duniani kote. 
   
  Tunapokuwa tupo tayari kuanza kutekeleza Mkataba wa Tabia Nchi wa Paris na kujiandaa kwa ajili ya mafanikio ya COP22 huko Marrekech, tusiisahau nusu ya idadi ya watu wetu na uwezo wao mkubwa wanaouwakilisha. Wanawake lazima wawe katika kiini cha utatuzi wote wa mabadiliko ya tabia nchi.

  0 0


   Katibu wa mbunge wa Mkuranga Bw Omar Kisatu akipeana mikono na baadhi ya wachezaji wa timu shiriki mashindano ya Ulega Cup yanayoendelea kutimua vumbi Wilayani Mkuranga.
   Diwani wa Kata ya Panzua Bw Juma Magaila akiongea na waandishi wa habari kuhusu ligi ya Ulega Cup  inayoendelea  Wilayani Mkuranga.
  Katibu wa mbunge wa mkuranga Bw Omar Kisatu Akiongea na waandishi wa habari kuhusu mashindano hayo ya Ulega Cup yanayoendelea kutimua vumbi Wilayani Mkuranga.

   Diwani wa Kata ya Mkamba Wilayani Mkuranga Bw Hassan Dunda Akiongea na waandishi wa habari kuhusiana na Mtiririko mzima wa ligi ya Ulega Cup unaondelea huko Wilayani Mkuranga.
  VIJANA wa Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani wamesema kuwa kitendo cha Mbunge wa Jimbo hilo Abdallah Ulega kupiga marufuku kukodi wachezaji Kutoka Nje ya Wilaya hiyo imeleta changamoto kwao kuonesha vipaji vyao Kwenye ligi ya mbunge inayoendelea.

  Wamesema kuwa wao kama vijana ndio wakati muafaka kwao kuonesha vipaji vyao na uwezo ili mwisho wa siku wapate nafasi ya kushiriki Kwenye ligi mbalimbali.Mbunge Ulega ameazisha Ligi ya mbunge ambapo hivi sasa timu Kutoka kila kijiji zinapambana na baadae zitatoa timu moja ya Kata ambayo itakwenda kushindana na Kata zingine zilizopo ndani ya Wilaya ya Mkuranga.

  Akizungumzia ligi hiyo jana wilayani humo Kijana khatibu Dadi alisema kuwa mbunge Ulega amedhamiria kuinua vipaji vya vijana wa Mkuranga na hiyo nikutokana na wito wake wakutaka ligi hiyo ishirikishe vijana wa maeneo husika tofauti na wanavyofanya kungineko."Kwa kifupi kila mtu anampongeza Mh.Mbunge Kwa uamuzi wake kwani lazima ifike wakati sisi kama vijana wa Mkuranga tuoneshe wenyewe uwezo na vipaji vyetu na tunaamini kupitia ligi hii ya Mbunge tutapata timu kabambe ya Wilaya."alisema Dadi

  Akizungumzia mwendelezo wa Ligi hiyo Katibu wa Mbunge Omar Kisatu alisema kuwa Mashindano yanaendeleo vizuri na mwitikio ni mkubwa na vijana wako kwenye morali ya hali ya juu.Alisema kuwa hatua inayoendelea sasa ni ya timu za vijiji kupambana na kuna kamati maalumu ambayo Kazi yake nikuangalia vijana wenye uwezo watakao tengeneza timu ya Kata.

  Aliongeza kuwa ligi hiyo Kwa sasa ipo chini ya u simamizi wa Madiwani na ikishafika kwenye hatua ya kushindana kata Kwa Kata hapo Mbunge ataingiza nguvu zake moja Kwa moja."Kama mnavyoona ligi inaendelea vizuri na hapa katika ngazi hii Madiwani ndio wanasimamia lakini ikishafika Kwenye ngazi ya Kata na kuendelea Mh.Mbunge atakuwa ndio mfadhili mkubwa."alisema Kisatu.

  Ligi hiyo imeshirikisha timu 125kutoka katika vijiji vyote 125 vilivyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga na itarajiwa kupatikana timu 25 zitakazo cheza ngazi ya Kata.

  0 0

  Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda akizungumza na watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya na Manispaa Ubungo leo jijini Dar es Salaam kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Humphrey Polepole. Mhe Makonda yupo katika ziara ya siku 10 jijini Dar es Salaam kwaajili ya kusikiliza kero za wananchi.
  Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Humphrey akimkaribisha Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda kuzungumza na watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya na Manispaa Ubungo leo jijini Dar es Salaam
  Watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya na Manispaa Ubungo wakimsikiliza Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda.Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.

  0 0


older | 1 | .... | 1048 | 1049 | (Page 1050) | 1051 | 1052 | .... | 1903 | newer