Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46395 articles
Browse latest View live

WAZIRI SIMBACHAWENE AFUNGA MAFUNZO YA UONGOZI NA MAADILI YA VIJANA WAZALENDO 47 KIVUKONI JIJINI DAR ES ESALAAM

$
0
0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Tamisemi) George Simbachawene, akisalimiana na Katibu Mkuu mstaafu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilson Mukama, baada ya kuwasili Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kufunga mafunzo ya uongozi na maadili ya vijana wazalendo 47 yalifungwa chuoni hapo Dar es Salaam leo. Kulia ni Samuel Kasori, aliyekuwa Msaidizi wa Hayati Baba wa Taifa ambaye alipata fursa ya kuzungumza katika hafla hiyo kuhusu suala zima la maadili ya uongozi na uzalendo.
Kikao kifupi kikifanyika ofisini kwa mkuu wa chuo hicho 
kabla ya kwenda ukumbini.
Wanafunzi wa chuo hicho wakiwa ukumbini kwenye hafla hiyo.

 
 
Mgeni rasmi Waziri Simbachawene (wa pili kushoto) na viongozi wengine wakielekea ukumbini. Kutoka kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Filbert Sanga, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhan Madabida, Katibu Mkuu mstaafu wa CCM, Wilson Mukama na Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Profesa Shadrack Mwakalila.
Wimbo wa Taifa ukiimbwa.
Wimbo wa Taifa ukiimbwa.
Taswira ya ukumbi wakati wa hafla hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Filbert Sanga akizungumza kwenye hafla hiyo.
Mbunge wa Kigamboni, Dk. Faustine Ndungulile akizungumza.
Mzee Samuel Kasori, aliyekuwa Msaidizi wa Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere akizungumza kwenye hafla hiyo.
Wahitimu hao 47 wakiwa kwenye sherehe hiyo.
Wahitimu hao 47 wakiimba wimbo maalumu.
Waziri Simbachawene akihutubia.
Muhitimu, Ebeneza Emmanuel akipokea cheti kutoka kwa 
mgeni rasmi.
Petro Magoti akikabidhiwa cheti.
Mhitimu Happiness Agathon akipokea cheti.
Mzalendo Theodora Malata akipokea cheti.
Mgeni rasmi katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali.
Picha ya pamoja na wahitimu hao.
Na Dotto Mwaibale
 
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais (Tamisemi) George Simbachawene amesema ili kusimamia mabadiliko na maendeleo ya nchi na maadili inatakiwa kuwa na kiongozi mbabe na mtemi.
 
Simbachawene aliyasema hayo wakati akifunga mafunzo ya uongozi na maadili kwa wahitimu 47 wazalendo waliyoyapata Chuo cha Kumbukumbu cha Mwalimu Nyerere Kivukoni Kigamboni jijini Dar es Salaam baada ya kumaliza kazi ya ujenzi ya kujitolea ya mwezi mmoja wilayani Mkuranga mkoani Pwani.
 
Alisema ili kusimamia mabadiliko na maendeleo nchi inatakiwa kuwa na mtu mbabe na mtemi na si kutegemea kundi fulani la watu kwani kwa kufanya hivyo kila kundi litahitaji kupendelewa baada ya kujiona bora kuliko jingine.
 
Alisema bila kuwa na viongozi wenye maadili nchi haiwezi kusonga mbele kwani tangu kuachwa kwa vijana kujiunga na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) ambako kulikuwa kukitolewa mafunzo ya maadili athari zake zilijitokeza na ndipo kwa kipindi cha miaka 20 Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilijikuta kikivamiwa na matajiri wakitaka nafasi mbalimbali za uongozi katika ngazi za ubunge, urais na kuingia katika ujumbe wa mkutano mkuu wa chama kwa njia ya fedha.
 
“Napenda kusema kuwa tunahitaji mabadiliko makubwa ya kukifumua chama chetu hasa katika mfumo mzima wa kupata viongozi kwani uliopo umetufanya tupoteze baadhi ya nafasi katika majimbo na hata katika uchaguzi ndogo kutokana na mfumo mbaya tulishindwa vibaya baada ya wanachama wetu kumpigia kura mtu mwingine kwa hasira huko vikao vyote vikiendeshwa kwa misingi ya fedha” alisema Simbachawene.
 
Alisema ilifika kila jambo lilikuwa haliwezi kufanyika bila ya kuomba ufadhili kutoka kwa matajiri ambao wengi wao ndio hao walikuwa wakwepa kodi.
 
Aliongeza kuwa watumishi wa umma wamekuwa wakilalamika kuwa hali ya maisha imekuwa ngumu huku wengine wakisema hazina hakuna fedha wakati hakuna hata mwezi mmoja ambao mtumishi amekosa kupewa mshahara wake.
 
Alisema pengine hali hiyo inatokea kwa kuwa watumishi hao walikuwa wakitegemea kitu kingine mbali ya mshahara baada ya mianya hiyo kufungwa ndio maana wameanza kulalamika.
 
Simbachawene alisema awali bandarini kulikuwa na pilika pilika nyingi mlundikano wa mankotenta na magari lakini makusanyo yalikuwa hayafiki hata bilioni moja kwa mwezi lakini hivi sasa pilika pilika hizo hazipo tena makusanyo yanafikia trioni  moja hii inaonesha pamoja na kuwepo kwa pilika pilika hizo kodi ilikuwa hailipwi ipasavyo.
 
Alisema nchi ilifikia pabaya kwani kila sehemu kulikuwa na madalali iwe hospitali, ofisi za serikali, mahakamani na hata kupata cheo lakini hivi sasa mambo hayo yamebanwa.
 
 Alisema anachokifanya Rais John Magufuli ni mabadiliko ili watu waache kuishi kwa mazoea badala yake wafanye kazi ili nchi ipige hatua katika masuala yote.
 
Simbachawene alisema changamoto kubwa iliyopo ni kuchanganya sera za siasa na za uongozi jambo linalosabisha mambo mengine kushindindwa kusonga mbele.

Waziri Simbachawene aliwapongeza wahitimu hao kwa kuwa na uzalendo kwa nchi yao ambapo aliahidi majina yao kuyapeleka kwa Rais Dk. John Magufuli kuona jinsi ya kuwasaidia ukizingatia kuwa wote ni wasomi wa shahada ya kwanza katika ngazi ya taaluma mbalimbali na akawaomba vijana wengine kuiaga mfano wa vijana hao.
Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Profesa Shadrack Mwakalila alisema baada ya kuona mmomonyoko wa maadili miongoni mwa jamii ya watanzania hasa kwa baadhi ya viongozi chuo hicho kimeona ni vyema kurejesha tena mafunzo ya uongozi na maadili ili kupitia mafunzo hayo waweze kupunguza kama si kumaliza kabisa kasi ya mmomonyoko wa maadili iliyopo kwa sasa.

NEC YAZIONYA ASASI ZINAZOTAKA KUTOA ELIMU YA MPIGA KURA

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhe. Dkt. Binilith Mahenge (kushoto) akimkaribisha ofisini kwake Kamishna wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Mhe. Jaji Mstaafu Mary Longway (wa pili kushoto) wakati kabla ya kutoa elimu ya mpiga kura kwenye mkutano wa kamati ya Ushauri ya mkoa wa Ruvuma uliofanyika kwenye halmashauri ya manispaa ya Songea mkoani Ruvuma.Wa pili kulia ni Katibu Tawala wa mkoa huo Bw. Hassan Bendeyeko na kulia ni Mkurugenzi wa Huduma za Kisheria wa NEC Bw. Emmanuel Kawishe.
Kamishna wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Mhe. Jaji Mstaafu Mary Longway (kulia) akisaini kitabu cha wageni kwenye ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhe. Dkt. Binilith Mahenge (kushoto) kabla ya kutoa elimu ya mpiga kura kura kwenye mkutano wa kamati ya Ushauri ya mkoa wa Ruvuma uliofanyika kwenye halmashauri ya manispaa ya Songea mkoani Ruvuma.
Kamishna wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Mhe. Jaji Mstaafu Mary Longway (kulia) akieleza jambo wakati akitoa elimu ya mpiga kura kwenye mkutano wa kamati ya Ushauri ya mkoa wa Ruvuma uliofanyika kwenye halmashauri ya manispaa ya Songea mkoani Ruvuma.Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhe. Dkt. Binilith Mahenge na katikati ni Katibu Tawala wa mkoa huo Bw. Hassan Bendeyeko.
Mkurugenzi wa Huduma za Kisheria wa NEC Bw. Emmanuel Kawishe, akitoa elimu ya mpiga kura kwenye mkutano wa kamati ya Ushauri ya mkoa wa Ruvuma uliofanyika kwenye halmashauri ya manispaa ya Songea mkoani Ruvuma.
Kamishna wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Mhe. Jaji Mstaafu Mary Longway (kulia) akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhe. Dkt. Binilith Mahenge vitabu vya Taarifa ya Tathmini Baada ya Uchgauzi wa Rais,Wabunge na Madiwani baada ya kutoa elimu ya mpiga kura kwenye mkutano wa kamati ya Ushauri ya mkoa wa Ruvuma uliofanyika kwenye halmashauri ya manispaa ya Songea mkoani Ruvuma.
Baadhi ya wajumbe wa mkutano wa kamati ya Ushauri ya mkoa wa Ruvuma uliofanyika kwenye halmashauri ya manispaa ya Songea mkoani Ruvuma wakifuatilia elimu ya mpiga kura.

Hussein Makame, NEC

TUME ya Taifa ya Uchaguzi imesema haitasita kuifutia kibali cha kutoa Elimu ya Mpiga Kura Asasi yoyote itakayotoa maneno ya kuleta uchochezi au kupigia debe sera za chama fulani cha siasa kwani kufanya hivyo kukiuka matakwa ya Kisheria.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Huduma za Kisheria wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Emmanuel Kawishe wakati akijibu swali la mmoja wa wajumbe wa mkutano wa kamati ya Ushauri ya mkoa wa Ruvuma kwenye mkutano huo uliofanyika kwenye halmashauri ya manispaa ya Songea mkoani Ruvuma leo.

Mjumbe huyo ambaye pia ni Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Mhandisi Stela Manyanya alitaka kufahamu Tume ina utaratibu gani kuhakikisha baadhi ya Asasi zinazofadhiliwa kutoa elimu ya mpiga kura kutumia nafasi hiyo kuhasisha sera za chama fulani.

Bw. Kawishe alisema Kifungu cha 4 (C) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi kimeipa mamlaka Tume kuzipa kibali Asasi na kuzisimamia na kuratibu Elimu ya Mpiga Kura na haitasita kufuta kibali hicho iwapo masharti yatakiukwa.

“Tume ikishatoa kibali inafanya ufuatiliaji na tathmini.Tumekwambia nenda katoe elimu ya mpiga kura..lazima tutafuatilia ili kuona kwamba unachotakiwa kusema ndicho.Lakini kwa sababu tu umetoa uchochezi Tume ndiyo imekupa kibali na Tume ndiyo yenye mamlaka ya kukunyima icho kibali” alisema Bw. Kawishe na kuongeza:

“Kwa hiyo kwa kuwa Tume haina uwezo wa kifedha inaruhusu Asasi zijitegemee lakini zikishaenda kwenye siasa tutazinyia icho kibali na kibali kitafutwa kwa sababu Tume ina mamalaka hayo Sheria inaturuhusu Kifungu cha 4 (C) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi kimeipa mamlaka Tume kuzipa kibali Asasi na kuzisimamia na kuratibu Elimu ya Mpiga Kura na haitasita kufuta kibali hicho iwapo masharti yatakiukwa”

Kwa uapnde wake Kamishna wa Tume hiyo Jaji Mstaafu Mary Longway amewataka wajumbe wa mkutano wa kamati ya Ushauri ya mkoa wa Ruvuma kufikisha elimu ya mpiga kura kwa wananchi wao ili wafahamu mambo mbalimbali yanayohusu uchaguzi mkuu.

Jaji Mst. Longway aliyasema hayo wakati akitoa elimu ya mpiga kura kwa wajumbe wa mkutano huo kwenye uliofanyika ukumbi wa mikutano wa halmashauri ya manispaa ya Songea mkoani Ruvuma.

Alisema kwa sasa Tume ya Taifa ya Uchaguzi inatekeleza matakwa ya Katiba, Sheria na Kanuni ya kutoa elimu ya mpiga kura katika kipindi chote cha mwaka leongo ni kuwahamasisha wananchi kutumia haki yao ya kikatiba na kujitokeza kushiriki kuchagua viongozi wao.

“Elimu hii inawajengea wananchi ufahamu na ulelewa kuhusu haki na wajibu wao katika kushiriki katika na wawezesha wananchi na wadau wa uchaguzi kupata taarifa sahihi kuhusu mchakato wa uchaguzi wa Rais, wabunge na madiwani” alisema Jaji Mst. Longway na kuongeza:

“Tunawaomba wajumbe wa mkutano huu muende mkafikishe elimu hii ya mpiga kura kwa wananchi mnaowaongoza ili wafahamu mambo mbalimbali yanayohusu uchaguzi mkuu na kutekeleza haki na wajibu wao kikamilifu”

Katika mkutano huo wajumbe kutoka halmashauri nane za mkoa wa Ruvuma walipata elimu ya mpiga kura na kuuliza maswali ambayo yalijibiwa.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi inatoa elimu ya moiga kura kupitia njia mbalimbali ili kutekeleza matakwa ya Katiba, Sheria na Kanuni zinazoongoza majukumu ya Tume ambapo mbali na kutoa elimu katika mkutano huo ilitarajiwa kutoa elimu kwenye Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Sengea.



Picha zote na Hussein Makame, NEC

KAMILISHENI UJENZI WA MAGOMENI KOTA KWA WAKATI - WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA

NAIBU WAZIRI MPINA ALITOZA FAINI YA SHILINGI MILIONI THELATHINI GEREZA LA KEKO NA MILIONI ISHIRINI, KIWADA CHA MADAWA CHA KEKO, KWA KOSA LA UCHAFUZI WA MAZINGIRA

$
0
0
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Luhaga Mpina akifanya akipita pembezoni mwa mfereji wa maji taka, ambapo uko karibu na makazi ya watu
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Luhaga Mpina akikakagua uchafuzi wa mazingira unaofanywa na gereza la keko lililopo temeke jijini Dar es salaam.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Luhaga Mpina akizungumza na waandishi wa habari mapema hii jana mara baada ya kufanya ziara ya ukaguzi wa mazingira jijini Dar es salaam.

Kupitia Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Naibu Waziri Ofisi ya makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina (Mb.) Amelitoza faini ya shilingi milioni thelathini Gereza la keko kwa kosa la kutiririsha maji taka yanayozalishwa gerezani hapo hivyo kuhatarisha maisha ya Binadamu na viumbe hai wengine.

Akiwa katika ziara nyingine ya ukaguzi wa mazingira jijini Dar es Salaam, Naibu Waziri Mpina Alilitaka Baraza hilo kutoa agizo kwa mkuu wa gereza hilo litakalokuwa na maelekezo ya kujenga miundombinu ya majitaka ambayo ni rafiki kwa mazingira sambamba na kulipa faini hiyo kwa muda uliyotajwa.

“Taasisi za Serikali zinapaswa kuwa mfano kwa kutii sheria za nchi hususani sheria ya mazingira nimeshasema mara nyingi na ninarudia hapa tena taasisi za serikali haziruhusiwi kuchafua mazingira kwa namna yoyote ile kwa mujibu wa sheria. “ alisisitiza Mpina.

Aidha Mpina ameitaka Manispaa ya Temeke kusimamia kuwa makini na zoezi la usafi wa mazingira katika maeneo ya Keko na kuwachukulia hatua wananchi wote wanaotiririsha maji taka katika mifereji ya maji ya mvua.

Akitoa ufafanuzi wa adhabu hiyo mwanasheria wa Baraza la mazingira, Suguta Heche, amesema kuwa Tasisi za serikali na mashirika ya umma yana wajibu wa kufuata sheria za nchi hususani sheria za mazingira na ukiukwaji wa sheria hizo utaambatana na adhabu kama zinatolewa kwa mashirika na makampuni binafsi.

Awali Naibu Waziri Mpina alitembelea kiwanda cha kutengeneza dawa cha Keko Pharmaceutical limited na kutoridhishwa na uharibifu wa mazingira unaofanywa na kiwanda hicho wa kutiririsha maji taka katika makazi bila kutibiwa, na kutokuwa na kibali cha utiririshaji kutoka kwa bonde na kuwatoza faini ya shilingi milioni ishirini inayopaswa kulipwa ndani ya wiki mbili, na kuelekeza usafi wa mazingira kufanyika katika mifereji ya maji ya mvua na kuwaasa wakazi wa maeneo jirani kutokutupa takataka katika maeneo hayo.

Kwa upande wake Bwana Selemani Ndugwana, Meneja uthibiti na Ubora wa kiwanda hicho cha dawa alipokea adhabu hiyo, na kusema kwamba ni kubwa sana wanaomba serikali iwapunguzie adhabu hiyo, kwa kuwa ni kosa la mara ya kwanza. Akiwakilisha wakazi wa eneo la keko mtendaji wa kata hiyo Bwana Samweli Magali alisema kero ya uchafuzi wa mazingira unaotoka kwenye kiwanda hicho cha madawa ni kubwa na ni hatarishi kwa afya za wakazi wa eneo hilo.

WAZIRI MWIJAGE AZINDUA RASMI KAMATI YA KUBORESHA MAZINGIRA YA BIASHARA NCHINI

$
0
0
Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji, Mh Charles Mwijage amezindua rasmi Kamati ya Kuboresha Mazingira ya Biashara Tanzania,Kamati yenye lengo la kufanya uchambuzi wa kina wa  kufanya biashara nchini.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kamati hiyo jijini Dar es Salaam,Waziri Mwijage amesema utashi wa Serikali ya Awamu ya Tano ni kuifanya Tanzania kuwa nchi ya uchumi  unaoongozwa na viwanda kama inavyoelekezwa katika Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025.

Amesema kuwa “Uwekezaji wa mazingira bora ni zoezi endelevu hivyo kazi yetu Sekta ya Umma na Sekta binafsi ni kujipima katika maboresho”.

Katibu Mkuu-Sera,Ofisi ya Waziri Mkuu(PMO),Dkt.Hamisi Mwinyimvua amezungumzia Jitihada za Serikali kuhusu Maboresho ya Mazingira ya Biashara zilizokwisha fanyika na kuahidi kuendelea kufanyika.
 Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mh. Charles Mwijage akizungumza na Wadau mbalimbali wa Sekta ya Biashara wakati wa uzinduzi wa Kamati ya Kuboresha Mazingira ya Biashara jijini Dar es Salaam.
   Katibu Mkuu-Sera,Ofisi ya Waziri Mkuu(PMO), Dkt.Hamisi Mwinyimvua akizungumzia Jitihada za Serikali kuhusu Maboresho ya Mazingira ya Biashara zilizokwisha fanyika jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mh. Charles Mwijage akiwa katika picha ya pamoja na ziongozi mbalimbali jijini Dar es Salaam. Picha na Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii.


TAASISI YA DORIS MOLLEL YA YATOA MSAADAWA LEO JIJINI DAR ES SALAAM.

$
0
0
Katika kuadhimisha Siku ya Watoto Njiti duniani,Taasisi ya Doris Mollel inayojihusisha na maswala ya watoto wanaozaliwa kabla ya wakati wameamua kuadhimisha siku hii kwa kumpelekea wheel chair, vyakula pamoja na box la sabuni kwa mama aliyejulikana kwa jina la Zainab Rashidi ambae ni mlemavu,mwenye watoto wawili waliozaliwa kabla ya wakati.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam,Msaidizi wa Kitengo cha Elimu-Taasisi ya Doris Mollel Rahma Amood amesema “Tumeamua kufanya hivi kwa lengo la kuhamasisha Taasisi nyingne na watu wengne waweze kuwakumbuka watoto hawa na kuweza kuwasaidia”. 

Doris Mollel Foundation kesho itaadhimisha siku hii kwa kutembea kilometa 3 visiwani Zanzibar kwa matembezi yatakayolenga kupunguza Watoto Njiti wanaozaliwa kote nchini. 

Kwa upande wake Mama huyo mwenye Watoto wawili waliozaliwa kabla ya wakati,Bi.Zainabu Rashid ameishukuru Taasisi hiyo kwa kumpa msaada huo kwa kumkumbuka.
Msaidizi wa Kitengo cha Elimu-Taasisi ya Doris Mollel, Rahma Amood akikabidhi msaawa wa wheel chair, vyakula pamoja na box la sabuni kwa mama aliyejulikana kwa jina la Zainab Rashidi leo jijini Dar es Salaam.
Msaidizi wa Kitengo cha Elimu-Taasisi ya Doris Mollel, Rahma Amood akimwelekeza, Zainab Rashidi njisi ya kutumia wheel chair leo jijini Dar es Salaam.
Msaidizi wa Kitengo cha Elimu-Taasisi ya Doris Mollel, Rahma Amood akiwa katika picha ya pamoja na Zainab Rashidi.
Msaidizi wa Kitengo cha Elimu-Taasisi ya Doris Mollel, Rahma Amood akiwa katika picha ya pamoja na familia ya Zainab Rashidi.picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.

WAZIRI MKUU ATOA SIKU 18 UMEME UKAMILIKE MLANDIZI

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametoa siku 18 kwa Mkandarasi wa umeme kwenye kiwanda cha Kiluwa Steel Group awe amemaliza kazi ya kuweka ume mkubwa ili kiwanda hicho kianze kazi.

Ametoa agizo hilo leo (Jumamosi, Novemba 19, 2016) wakati akizungumza na wananchi na viongozi mbalimbali wa Serikali na wa Mkoa wa Pwani waliofika kiwandani hapo eneo la Mlandizi wakati akikagua utekelezaji wa maagizo aliyoyatoa Julai 12, mwaka huu alipozuru kiwanda kwa mara ya kwanza.

“Nilipokuwa hapa mara ya kwanza niliagiza itengenezwe njia ya reli kutoka njia panda ya reli ya kati, lakini pia niliagiwa uwekwe umeme wa msongo mkubwa ili kiwanda kiweze kuanza uzalishaji mapema mwakani. Nimefarijika kukuta maagizo haya yametekelezwa kwa kiasi kikubwa isipokuwa hili la umeme,” amesema.

“Mkandarasi ameomba siku 14, nimempa hadi tarehe 7 Desemba ahakikishe umeme unafanya kazi kwa kiwango kinachotakiwa. Sasa hivi wameanza test lakini muda ili transforma iweze kuhimili mzigo mkubwa… hili ni suala la kitaalamu kwa hiyo tuwape muda.”

Waziri Mkuu pia amesema amefarijika kusikia kwa orodha ya watu wanaodai fidia sababu ya kuoisha njia ya reli ijengwe, imeshawasilishwa kwa Mkuu wa Mkoa na mwenye kiwanda yuko tayari kuwalipa maa taratibu zitakapokamilika.

Mapema, akiwasilisha taarifa fupi, Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Eng. Evarist Ndikilo alisema haelewi ni kwa nini mkandarasi huyo anazidi kuomba siku 14 ili kukamilisha wakati aliahidi kuwa 14 za awali zingetosha kukamilisha kazi hiyo.

Kuhusu fidia kwa wananchi na Halmashauri ya Wilaya hiyo, Mkuu huyo wa Mkoa alisema wananchi waliopisha njia wanadai fidia ya sh. milioni 95.76 na Halmashauri inadai sh. milioni 307.26 na kwamba jumla yote inafikia sh. milioni 403.

Alipopewa nafasi na Mkuu wa Mkoa huo ajieleze mbele ya Waziri Mkuu, Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Dekan Group Ltd, Eng. Desderius Luhaga ambaye amepewa kazi ya kuweka umeme na transforma Mlandizi alisema anahitaji apewe siku 14 ili aweze kukamilisha kazi hiyo.

“Kazi kubwa ya umeme tumeshaifanya na hii ni ya umeme wa msongo wa kilovoti 132, na tumeanza kutest umeme katika baadhi ya mitambo hapa kiwandani, lakini tunahitaji siku karibu tano ili transforma ipoe tangu tulipoifunga ndipo iweze kupokea mzigo mkubwa. Kisha tutaanza kuunganisha katika maeneo mengine madogo madogo humu ndani,” amesema.

Katika hatua nyingine, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Reli Tanzania (TRL), Bw. Masanja Kadogosa  amesema shirika hilo limetumia sh. milioni 863 kukamilisha ujenzi wa reli ya km.5 kutoka njia panda hadi kwenye kiwanda hicho ambapo kati ya hizo km.1.5 zimo ndani ya kiwanda.

Amesema hadi sasa wameshaweka njia nne za reli, moja ikiwa ni mahsusi kwa ajili ya kubeba makaa ya mawe. “Tulilazimika pia kujenga culvert katika eneo moja kwa sababu pailikuwa na shimo kubwa. Tumetumia fedha kidogo kwa sababu tumetumia mafundi wetu badala ya wakandarasi,” ameongeza.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Kiluwa Steel Group, Bw. Mohammed Kiluwa alimweleza Waziri Mkuu kuwa anatarajia kuanza uzalishaji Januari, mwakani na kwamba ataajiri wafanyakazi wapatao 200.

“Tunataraji kuanza uzalishaji Janruari, mwakani na uzalishaji utakuwa tani 2,000 kwa siku. Ila tumekubaliana na wawekezaji wenzangu tuweke pia viwanda vingine vitatu kwa sababu kutakuwa na umeme wa kutosha.”

“Tunatarajia kufungua viwanda vine vya kutengeneza gypsum powder, pikipiki, nguzo na vifaa vya kufungia nyaya za umeme mkubwa pamoja na tissue. Tuna eneo lingine Mkuranga lakini kule hakuna umeme, kwa hiyo tumepanga kuweka hivyo viwanda hapa kwa sababu tuna eneo la kutosha.”

Hata hivyo, Bw. Kiluwa alitumia fursa hiyo kumweleza Waziri Mkuu kwamba wanapata taabu ya makaa ya mawe kwa sababu wanaletewa makaa yenye ukubwa wa milimita 10 hadi 15 badala ya milimita 35 – 40 ambazo wanahitaji kwa ajili ya kiwanda chao.

“Tukiagiza tani 30, tunachambua mawe ya saizi inayotufaa na kujikuta tunabakia na tani saba tu. Kiasi kilichobakia ni vumbi tupu,” alisema.

Waziri Mkuu alimwagiza Naibu Katibu Mkuu wa Viwanda na Biashara, Eng. John Malongo awasiliane na Wizara ya Nishati na Madini ili afuatilie ni kwa nini watengenezaji wa makaa ya mawe hawafuati vipimo halisi vinavyotolewa na wawekezaji.


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMAMOSI, NOVEMBA 19, 2016.

MCHEZAJI LANGA LESSE BERCY WA JAMHURI YA CONGO

$
0
0
Kama ilivyoripotiwa hapo awali, Shiikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) baada ya kutoridhika na kujiridhisha kuwa mmoja wa wachezaji wa Jamhuri ya Congo-Brazzaville, alikiuka kanuni za mashindano ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 17, mwaka huu  lilimkatia rufaa mchezaji Langa-Lesse Bercy katika Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF).
Kutokana na rufaa hiyo dhidi ya mchezaji huyo wa Congo, Langa Lesse Bercy, CAF liliagiza apelekwe Makao Makuu ya Shirikisho hilo, lililoko Cairo, Misri  kwa ajili ya kurudia na kuthibitisha umri wake kwa kipimo cha MRI (Magnetic Imaging Resonance).
TFF iliagizwa na CAF igharimie zoezi zima ikiwa ni pamoja na kulipia gharama za usafiri wa mchezaji husika na daktari wake  pamoja na kulipia gharama za vipimo. TFF ilikubaliana na matakwa hayo ya CAF na kulipia.
Kipimo ilikuwa kifanyike leo Novemba 19, 2016 saa 5.00 asubuhi mjini Cairo, Misri. Ujumbe wa TFF wa watu wanne ukiambatana na madaktari wawili uliwasili mjini Cairo tangu Novemba 17, 2016 ili  kuwa shuhuda wa zoezi la kipimo hicho.
Jana usiku saa 5.00 TFF ilipokea ujumbe kutoka CAF kuwa mchezaji Langa Bercy ameshindwa kusafiri kwenda Cairo kwa kuwa yuko katika eneo lililoko "vitani",eneo hilo halikutajwa.
TFF inaendelea kufuatia kwa karibu jambo hili ili kuhakikisha haki inatendeka .
Kadhalika Aidha TFF inaomba wadau wa mpira wa miguu wawe na subira katika kipindi hiki.

TaWaSaNet yawakutanisha wadau mbalimbali wa mazingira nchini

$
0
0

Mtandao wa asasi za kiraia unaojihusisha na masuala ya Maji na mazingira Nchini (TaWaSaNet) umeandaa mkutano  uliowakutanisha wadau Mbalimbali wa Mazingira Nchini, ili kuadhimisha  wiki ya usafi wa Mazingira inayoenda sambamba na siku ya choo na kunawa mikono Duniani inayo adhimishwa novemba 19 ya kila mwaka.

Akizungumza katika mkutano huo mgeni rasmi Naibu waziri wa Afya Jinsia wazee na Watoto Dkt Khamisi Kigwangala amesema, wizara yake imejipanga kusimamia kwa ukaribu  utekelezaji wa mikakati mbalimbali ya  kitaifa na kimataifa inayolenga upatikanaji wa vyoo bora mashuleni na kwenye vituo vya Afya.

Dkt Kigwangala ameipongeza Taasisi ya TaWaSaNet kwa kufanikisha na kuandaa mkutano huo kwa kuwa wadau wazuri wa mazingira na kuzitaka asasi nyingine za kiraia kuunga mkono jitihada za serikali ya Awamu ya Tano katika kuendeleza kampeni mbalimbali za usafi  hapa Nchini.

Katika mkutano huo Kigwangala ametoa Tuzo kwa wanahabari mahiri kwenye uandishi wa makala usafi na mazingira ambapo  Bw.Gervas Hubile amepata tuzo ya makala bora ya usafi wa mazingira kwa upande wa radio na Bi Salome Gregory ametwaa tuzo ya Makala bora ya usafi wa mazingira kwa upande wa magazeti.

 Naibu waziri wa Afya Jinsia wazee na Watoto Dkt Khamisi Kigwangala akizungumza na wadau mbalimbali wa mazingira juu ya kutoa tuzo kwa wanahabari mahiri kwenye uandishi wa makala usafi na mazingira leo jijini Dar es Salaam.  
 .Afisa Sera wa Taasisi ya Tanzania Water and Sanitation Network (TAWASANET), Darius Mhawi wa (kwanza kushoto) akizungumza machache  kwenye utoaji wa tuzo kwa wanahabari mahiri kwenye uandishi wa makala usafi na mazingira leo jijini Dar es Salaam.
 Naibu waziri wa Afya Jinsia wazee na Watoto Dkt Khamisi Kigwangala akiwa katika picha ya pamoja na wadau mbalimbali  leo jijini Dar es Salaam.picha na Yasir Adam wa Globu ya jamii.

KLABU YA ROTARY YA OYSTER BAY YASHIRIKIANA NA WADAU KUTOA UFADHILI WA ELIMU KWA WANAFUNZI WA VYUO

$
0
0
Wanafunzi 20 kutoka vyuo mbalimbali hapa nchini wamepata ufadhili wa elimu unaofikia jumla ya Tshs Milioni 70 kutoka Klabu ya Rotary ya Oyster Bay, fedha zilizokusanywa kutokana na michango ya makampuni na watu binafsi.

Lengo la mradi huu ni kutoa msaada wa kifedha kwa wanafunzi wa Kitanzania wenye alama za juu kimasomo na waliopata nafasi za kujiunga na vyuo lakini wakakosa fedha za kulipia masomo.

Wanafunzi hao walikabidhiwa hundi za malipo katika tafrija fupi iliyofanyika tarehe 18 November katika mgahawa wa Waterfront uliopo Slipway jijini Dar es Salaam. Tafrija hiyo iliandaliwa kwa lengo la kuadhimisha miaka 100 ya mfuko wa Rotary ambapo fedha zilizochangishwa katika hafla hiyo zitawekwa kwenye mfuko huo wa Rotary ujulikanao kama Rotary Foundation.

Rotary Foundation iliyoanzishwa miaka 100 iliyopita ina lengo la kuwawezesha wanachama wa Rotary duniani kote kukuza amani kwa kuboresha afya, kusaidia elimu na kutokomeza umasikini. Mradi wa Klabu ya Rotary Oyster Bay wa ufadhili wa masomo unaenda sambamba na juhudi za Rotary International za kusaidia elimu.

Mradi wa ufadhili wa masomo katika Klaby ya Rotary ya Oyster Bay ulianza mwaka 2010 na wanafunzi wawili kwa msaada wa mfadhili mmoja. Katika kipindi cha miaka mitano, mradi huu umefanikiwa kuwa mradi mkubwa zaidi ukilinganisha na miradi mingine inayofanywa na klabu hiyo. Mwaka huu, klabu ya Rotary ya Oyster Bay imetoa ufadhili kwa wanafunzi 20 kwenye aina mbalimbali za masomo ikiwemo uhasibu, uhandisi, udaktari na sheria na inajivunia kuanza kuona matunda yake ambapo mmoja wa wanafunzi hao amehitimu na kuanza kazi ya udaktari.

Wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali nchini Tanzania hutuma maombi ya ufadhili na mchakato wa kina hufanyika ili kuchagua wanafunzi wanaokidhi vigezo. Maendeleo ya wanafunzi wanaochaguliwa kupata ufadhili huangalia kwa ukaribi ili kubaini kama wanastahili kuendelea kupata ufadhili wa masomo katika mwaka unaofuata.

Mradi huu wa ufadhili Kwa wanafunzi unawezeshwa na michango kutoka kwa makampuni na watu binafsi ambapo mwaka huu michango imetoka Karimjee Scholarships, Karimjee Jivanjee Scholarships, D.B Shapriya Scholarships, R Sheth Scholarships, K Shah Scholarships, Nasim Manji, JDC Scholarships, Eleanor and Paul Best, Diamond Trust Bank, S Rhemtullah, pamoja na Gajjar Autoworks and Premium Finishes Limited.

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA ATEMBELEA KIWANDA CHA CHUMA NA KIWANDA CHA KUUNGANISHA MAGARI NA TREKTA MKOANI PWANI

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameliegiza Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha lifanye maamuzi ya kupima ardhi haraka na kutenga maeneo kwa ajili makazi na viwanda ili kujiandaa na uwekezaji mkubwa.

Ametoa agizo hilo leo mchana (Jumamosi, Novemba 19, 2016) wakati akizungumza na wananchi na viongozi mbalimbali wa Serikali na wa Mkoa wa Pwani mara baada ya kukagua kiwanda cha kutengeneza magari ya zimamoto na matrekta cha Equator SUMA JKT Limited kilichopo Ruvu JKT, wilayani Kibaha mkoani Pwani.  

“Jiji la Dar es Salaam limejaa, na Kibaha mjini pia hawana ardhi ya kutosha kwa kimbilio pekee hivi sasa ni Kibaha Vijijini. Baraza la Madiwani fanyeni maamuzi, pimeni ardhi na mtenge maeneo ya makazi, viwanda na taasisi za elimu ili mkipata wawekezaji iwe rahisi kuwapa maeneo,” amesema.

Waziri Mkuu amesema ujenzi wa kiwanda hicho utakuwa mkombozi kwa taasisi nyingi na halmashauri nyingi nchini kwani zilikuwa zinashindwa kumudu bei ya kununua magari ya zimamoto. “Baadhi ya Halmashauri nyingi zilikuwa zinanunua gari moja kwa sh. milioni 500 na hiki ni kiasi kikubwa mno… kwa hiyo kiwanda hiki kitakuwa mkombozi kwa taasisi nyingi na halmashauri zetu,” amesema.

Amesema maeneo mengi nchini yanahitaji magari ya zimamoto lakini yalikuwa yanashndwa kumudu bei za magari hayo. Aliyataja maeneo hayo kuwa ni viwanja vya ndege, bandari, taasisi zilizo chini ya TAMISEMI kama vile shule za sekondari za bweni, Majiji, miji mikuu, Manispaa na Halmashauri za Wilaya.

Amesema ameguswa kukuta kiwanda hicho pia kina uwezo wa kutengeneza matreka na zana za kilimo (farm implements) kwani asilimia kubwa ya Watanzania ni wakulima na wanategemea jembe la mkono. “Kupitia kiwanda hiki, matrekta mengi yataunganishwa na nina imani bei itakuwa ya chini ili wananchi waweze kumudu.”

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Equator SUMA JKT Ltd, Eng. Robert Mangazini alimweleza Waziri Mkuu kwamba asilimia 80 ya ujenzi wa kiwanda hicho imekamilika na kwamba hivi sasa wako kwenhye hatua ya kufunga mitambo. Hata hivyo, alisema wanaisubiri iwasili kutoka India.

Alisema kiwanda hicho kikikamilika kitaweza kuunganisha matrekta 3,000 kwa mwaka na magari ya zimamoto 100 na kubainisha kuwa faida za kuunganisha magari hayo hapa nchini ni kuwa na uwezo wa kuzalisha vipuri ndani ya nchi.“Tukiweza kuzalisha vipuri hapa nchini kwa asilimia 60, umiliki wa magari haya na matrekta utakuwa ni wa Tanzania na siyo wa kampuni za nje tena. Pia tutakuwa tumefaulu kuhamisha teknolojia kwa vijana wetu,” alisema.

Alisema hadi sasa vijana 60 wamekwishapatiwa mafunzo ona wako tayari kuanza kazi mara uzalishaji utakapoanza Machi, 2017.Kuhusu teknolojia ya utengenezaji wa magari ya zimamoto, Eng. Mangazini alisema kiwanda hicho ni cha pili kujengwa barani Afrika cha kwanza kikiwa huko Bassa, Afrika Kusini.

Mapema, akisoma risala mbele ya Waziri Mkuu, mwakilishi wa Equator SUMA JKT Ltd. Kapteni Farijala Mkojera alisema kiwanda hicho kinamilikiwa kwa pamoja na kampuni ya Equator Automech Ltd ambao wana hisa asimilia 70 na SUMA JKT inamiliki asilimia 30 ya hisa za kiwanda hicho.

Akizungumzia ujenzi wa kiwanda hicho, alisema hadi sasa wamekwishatumia sh. bilioni 1.5 na kwamba hadi ujenzi utakapokamilika, wanatajia kuwa wametumia sh. bilioni mbili. “Ujenzi ukikamilika, tunatarajia kuajiri wafanyakazi 200 katika fani mbalimbali,” alisema.

Alisema wakianza uzalishaji, mbali ya magari ya zimamoto na matrekta, wataweza pia kuunganisha mabasi na zana za kilimo kama vile combine harvesters. “Tutakuwa tumefanikiwa kuhamisha teknolojia kutoka Russia (magari za zimamoto) na India na Poland (matrekta). Tuna uhakika wa soko hapa nchini katika Jumuiaya za EAC na SADC,” alisema.

Waziri Mkuu amerejea Dodoma mchana huu.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMAMOSI, NOVEMBA 19, 2016.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli nchini TRL, Masanja Kadogosa (kulia) kuhusu ujenzi  wa reli  inayounganisha  reli ya kati na  kiwanda cha Kiluwa Still Group cha Mlandizi Pwani Novemba 19, 2016  . Kulia kwake ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua mitambo ya kiwanda cha chuma cha Kiluwa Still Group kilichopo Mlandizi Pwani Novemba 19,2016 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 
 Waziri Mkuu, Kassim  Majaliwa akizungumza baada ya kukagua  maendeleo ya ujenzi wa kiwanda cha Kiluwa Still Group cha Mlandizi mkoani Pwani  Novemba 19, 2016.  Kushoto ni  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa 
 Waziri  Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua kiwanda cha kuunganisha magari ya zimamoto na matrekta cha Equator SUMMA kilichopo Mlandizi mkoani Pwani Novemba 19,2016(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu), 

DC WA HANDENI,MH GONDWE AFANYA ZIARA YA KUSULUHUSHA MGOGORO WA WAFUGAJI NA WAKULIMA MSITU WA HIFADHI YA LUGALA KIJIJI CHA KITUMBI WILAYANI HANDENI

$
0
0

Pichani wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni,Bw. William Makufwe akifuatiwa na Mkuu wa Wilaya walipokuwa wakisikiliza kero za wanakijiji cha Kitumbi
Mkuu wa Wialaya ya Handeni,Mh Godwin Gondwe akizungumza na wanakijiji wa kijiji cha Kitumbi .

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni, Bw. William Makufweakizungumza na wanakijiji wa kijiji cha kitumbi.
Afisa ardhi wa Halmashauri ya wilaya ya Handeni Bw. Sixtus Akiwaelewesha wanakijiji wa kijiji cha kitumbi kuhusu ardhi.
Baadhi ya wanakijiji wa kijiji cha kitumbi wakitoa kero zao kwa Viongozi

WANATASNIA WA FILAMU MKOANI GEITA WAPEWA MTIHANI WA KUANDAA TAMASHA LA FILAMU.

$
0
0
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania, Bi.Joyce Fesso (kushoto), akizungumza kwenye kikao cha Wanatasnia ya Filamu mkoani Geita hii leo kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Geita.

Mgeni Rasmi alikuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nhauye, aliyewakilishwa na Waziri wa Afya Zanzibar, Mhe.Mahmood Thabith Kombo (wa piAli kushoto).

Wa kwanza kulia ni Mwenyekiti Chama cha Waigizaji mkoani Geita, Rosemary Michael na anayefuata ni Herman Matemu ambaye ni Kaimu Afisa Tawala mkoa wa Geita.
Na BMG
Baadhi ya wanatasnia ya Filamu mkoani Geita waliohudhuria kikao baina yao na Bodi ya Filamu mkoani humo, wakimsikiliza Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania, Bi.Joyce Fesso, ambapo amewasisitiza kuungana pamoja na kutengeneza filamu moja iliyo bora kwa ajili ya kuwatambulisha kwenye soko la filamu na pia kuutambulisha mkoa wa Geita badala ya kuwa na filamu nyingi zisizo na ubora.
Kutoka kulia ni mgeni rasmi, Waziri wa Afya Zanzibar, Mhe.Mahmood Thabith Kombo ambaye amemwakilisha Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nhauye.

Wanaofuata ni Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu nchini, Bi.Joyce Fessoo, Mwakilishi wa balozi wa Tanzania nchini Denmark, Dotto Kahindi pamoja na Mratibu wa Tamasha la Kimataifa la Filamu Zanzibar (Zanzibar International Film Festival), Robert Manondolo.
Mgeni rasmi kwenye kikao baina ya Bodi ya Filamu nchini na Wanatasnia ya Filamu mkoani Geita, Waziri wa Afya Zanzibar, Mhe.Mahmood Thabith Kombo (katikati) ambaye amemwakilisha Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nhauye, akisisitiza wasanii mkoani Geita kushikamana na kushirikiana na viongozi wao pamoja na Serikali na kuandaa Tamasha la Filamu kwa kuwa fursa hiyo wanayo.
Mgeni rasmi kwenye kikao baina ya Bodi ya Filamu nchini na Wanatasnia ya Filamu mkoani Geita, Waziri wa Afya Zanzibar, Mhe.Mahmood Thabith Kombo (katikati) ambaye amemwakilisha Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nhauye,
Herman Matemu (aliyesimama) ambaye ni Kaimu Afisa Tawala mkoa wa Geita amesema viongozi wa serikali mkoani Geita wakiwemo Maafisa Utamaduni wako tayari kutoa ushirikiano wao ili kuboresha tasnia ya filamu mkoani humo.

Amewapa chachu wanatasnia ya Filamu mkoani Geita kuungana pamoja na kutengeneza kazi bora kwani sanaa hiyo inaweza kubadilisha maisha yao na kuwa mabilionea ikiwa watafanya kazi bora.
Mwenyekiti wa Chama cha Waigizaji mkoani Geita, Rosemary Michael, amebainisha kwamba chama hicho kimeweka mikakati ya kuboresha soko la filamu mkoani Geita huku matamanio yao ni kuwa na Tamasha la Filamu ili fursa kwa wasanii kuonesha kazi zao.
Mmoja wa wanatasnia ya filamu mkoani Geita akisoma risala kwa niaba ya wasanii wengine ambapo amebainisha kwamba wanasanii wa filamu mkoani Geita wanahitaji kupewa mafunzo zaidi namna ya kuboresha kazi zao pamoja na upatikanaji wa stemp/stika kwa ajili ya ulinzi wa kazi zao hivyo bodi ya filamu nchini iwasaidie katika hilo ambapo Katibu Mtendaji wa bodi hiyo, Joyce Fesso, amekubalina na maombi yao.
Wanatasnia ya filamu mkoani Geita wanasema bado hawanufaiki na uuzaji wa kazi zao kwa kuwa zinaoneshwa bure kwenye baadhi ya visimbuzi nchini pamoja na kudurufiwa (kunakiliwa) kwa wingi mitaani hivyo bodi ya filamu iwasaidie namna ya kuzisajili ili kulinda maslahi yao.
Wanatasnia ya filamu mkoani Geita wameshauri kiundwe kikosi kazi kwa ajili ya kukomesha udurufishaji (kunakiliwa) wa kazi zao mitaani kwa kuwa zinasababisha kukosa stahiki zao.
Wanatasnia ya filamu mkoani Mwanza wameomba mazingira ya ukaguzi wa filamu yaboreshwe zaidi ili kuwapa fursa ya filamu zao kukaguliwa.
Waigizaji, waongozaji wa filamu na watunzi wa hadithi za filamu na tamthilia ni miongoni mwa makundi yanayokamilisha wanatasnia ya filamu.
Kikao baina ya Wasanii wa Filamu/Tamthilia mkoani Geita na Bodi ya Filamu nchini.
Picha ya pamoja katika viongozi mbalimbali akiwemo mgeni rasmi Waziri wa Afya Zanzibar, Mhe.Mahmood Thabith Kombo (wa nne kulia) na wanatasnia ya filamu mkoani Geita
Na George Binagi-GB Pazzo
Wanatasinia ya Filamu mkoani Geita wamepewa mtihami ambao hata hivyo ni mwepesi ikiwa watakuwa na dhamira ya dhati ya kuikuza tasnia hiyo. 

Mtihani huo umetolewa hii leo na Waziri wa Afya Zanziar, Mahmood Kombo, aliyekuwa mgeni rasmi kwa niaba ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, kwenye kikao baina ya wasanii wa filamu mkoani Geita na Bodi ya Filamu nchini.

Mtihani wenyewe ni wanatasnia hao kwa kushirikiana na chama cha Waigizaji mkoa wa Geita, kuandaa Tamasha la Filamu mkoani Geita ambalo litasaidia kuinua tasnia hiyo mkoani humo, Kanda ya Ziwa na hata nchini kwa ujumla.

"Mkitayarisha Tamasha lenu, mimi mwakani nitakuja pamoja na familia yangu". Amesisitiza Waziri Kombo akitolea mfano Tamasha la Kimataifa la Filamu Zanzibar namna linavyofana na kuwatangaza wasanii pamoja na kuwaongezea kipato.

Hata hivyo wanatasnia ya filamu mkoani Geita kwenye risala yao wamesema wanahitaji kupewa mafunzo zaidi juu ya namna ya kuboresha filamu zao pamoja na upatikanaji wa stemp/stika kwa ajili ya ulinzi wa kazi hizo hivyo bodi ya filamu nchini iwasaidie katika hilo ambapo Katibu Mtendaji wa bodi hiyo, Joyce Fesso, amekubalina na maombi yao na kuahidi kufikisha mafunzo ya filamu mkoani Geita kama ilivyokuwa hivi karibuni mkoani Mwanza.

Tazama HAPA Mafunzo kwa Wanatasnia ya Filamu mkoani Mwanza.

TAASISI YA DORIS MOLLEL YAADHIMISHA SIKU YA MTOTO NJITI KWA MATEMBEZI, VISIWANI ZANZIBAR

$
0
0
Washiriki wa Matembezi ya hisani ya kuadhimisha Siku ya Mtoto Njiti Duniani yaliyotaribiwa na Taasisi ya Doris Mollel wakiwa na bango lenye ujumbe wa kuadhimisha siku hiyo, iliyoadhimishwa kitaifa Mjini Unguja, Zanzibar Novemba 19, 2016. Matembezi hayo yalianzia katika Uwanja wa Amani kupitia Uwanja wa Tumbaku na kuishia Viwanja vya Maisara.
 Baadhi ya viongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wakijumuika pamoja Wadhamini na Waratibu wa Matembezi ya hisani ya kuadhimisha Siku ya Mtoto Njiti Duniani, wakishiriki Matembezi hayo, yalianzia katika Uwanja wa Amani kupitia Uwanja wa Tumbaku na kuishia Viwanja vya Maisara, Mjini Unguja, Zanzibar.
Brass Band ya Chuo cha Mafunzo, Zanzibar ikiongoza Matembezi ya hisani ya kuadhimisha Siku ya Mtoto Njiti Dunian,  iliyoadhimishwa kitaifa Mjini Unguja, Zanzibar Novemba 19, 2016. Matembezi hayo yalianzia katika Uwanja wa Amani kupitia Uwanja wa Tumbaku na kuishia Viwanja vya Maisara.

Mkuu wa Kitengo ya Uhusiano na Mawasiliano wa Kampuni ya Vodacom Tanzania, Jacqueline Materu akiwa pamoja na Muanzilishi wa Taasisi ya Doris Mollel, Doris Mollel pamoja na washiriki wengine katika Matembezi ya hisani ya kuadhimisha Siku ya Mtoto Njiti Duniani, yaliyoadhimishwa kitaifa Mjini Unguja, Zanzibar Novemba 19, 2016.
Mgeni Rasmi katika hafla ya Matembezi ya hisani ya kuadhimisha Siku ya Mtoto Njiti Duniani, Naibu Waziri wa Afya wa Zanzibar, Harusi Said Suleiman akitoa hotuba yake, katika hafla ya Kilele cha siku ya Mtoto Njiti Duniani, iliyoadhimishwa kitaifa Mjini Unguja, Zanzibar Novemba 19, 2016. Vodacom ndio Wadhamini wakuu walioeza kufanyikisha shughuli hiyo. Kulia ni Muanzilishi wa Taasisi ya Doris Mollel na Mratibu wa Matembezi hayo, Doris Mollel na kushoto ni Mkuu wa Kitengo ya Uhusiano na Mawasiliano wa Kampuni ya Vodacom Tanzania, Jacqueline Materu.
Mkuu wa Kitengo ya Uhusiano na Mawasiliano wa Kampuni ya Vodacom Tanzania, Jacqueline Materu akizungumza katika hafla ya Kilele cha siku ya Mtoto Njiti Duniani, iliyoadhimishwa kitaifa Mjini Unguja, Zanzibar Novemba 19, 2016. Vodacom ndio Wadhamini wakuu walioeza kufanyikisha shughuli hiyo.

Baadhi ya Vikundi vya Jogging kutoka maeneo mbalimbali Visiwani Zanzibar, wakipasha moto misuli mara baada ya kumalizika kwa Matembezi ya hisani ya kuadhimisha Siku ya Mtoto Njiti Duniani, yaliyoadhimishwa kitaifa Mjini Unguja, Zanzibar Novemba 19, 2016.






Mshehereshaji wa hafla hiyo, Mishy Bomba akiweka sawa mambo.






Mkuu wa Kitengo ya Uhusiano na Mawasiliano wa Kampuni ya Vodacom Tanzania, Jacqueline Materu akipokea



MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA ATUNUKU SHAHADA NA STASHAHADA KATIKA MAHAFALI YA PILI YA CHUO CHA TAKWIMU MASHARIKI MWA AFRIKA

$
0
0

Mgeni Rasmi katika Mahafali ya Pili ya Kutunuku Shahada na Stashahada za Chuo cha Takwimu Mashariki ya Afrika Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongozana na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe.Dkt. Philip Mpango (kushoto) pamoja na mkuu wa chuo hicho Prof. Innocent Ngalinda (kulia) kuingia ukumbini pamoja na wahitimu tayari kwa mahafali.
 Mgeni Rasmi katika Mahafali ya Pili ya Kutunuku Shahada na Stashahada za Chuo cha Takwimu Mashariki ya Afrika Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akifungua mahafali ya pili yaliofanyika chuoni hapo.
 Sehemu ya Wahitimu wa Chuo cha Takwimu Mashariki Mwa Afrika.
Mgeni Rasmi katika Mahafali ya Pili ya Kutunuku Shahada na Stashahada za Chuo cha Takwimu Mashariki ya Afrika Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimtunuku mmoja wa wahitimu kati ya wahitimu 133 waliohitimu leo na kutunukiwa Shahada na Stashahada.
 Mgeni Rasmi katika Mahafali ya Pili ya Kutunuku Shahada na Stashahada za Chuo cha Takwimu Mashariki ya Afrika Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Balozi wa Sudan Mhe.Mahgoub Ahmed Sharfi , ambapo mabalozi mbali mbali walihudhuria.
 Mgeni Rasmi katika Mahafali ya Pili ya Kutunuku Shahada na Stashahada za Chuo cha Takwimu Mashariki ya Afrika Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja Mabalozi wa nchi mbali mbali waliohudhuria  mahafali hayo.


..............................................................

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amekiri kuwa Wizara, Idara na taasisi za Serikali zina matumizi madogo ya takwimu sahihi zinazotolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu nchini  hali ambayo inachangia kurudisha nyuma shughuli za upangaji wa maendeleo za wananchi.

Makamu wa Rais wa Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo leo trh 19-Nov-2016 katika hotuba yake kwenye mahafali ya Pili ya Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika (EASTC)Jijini Dar es Salaam.


Kutokana na hali hiyo, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameziagiza wizara, Idara na taasisi za Serikali kuimarisha matumizi ya takwimu sahihi kwa ajili ya kupanga na kuweka mikakati ya kuwaletea wananchi maendeleo endelevu.


Makamu wa Rais ameutaka uongozi wa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika   uimarishe ushirikiano na Wakuu wa Takwimu wa Afrika kwa kuhakikisha watakwimu wanaoingia katika soko la ajira wanafanya kazi zao kwa kufuata misingi ya kisheria na kanuni zake katika ukokotoaji wa takwimu zinazokubalika kitaifa na kimataifa ambazo zitawezesha Afrika kupanga maendeleo ya wananchi kwa ufanisi mkubwa.


Amewahimiza wahitimu wa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika pindi watakapoanza kufanya kazi zao wafanye kazi kwa ufanisi na kwa umakini wa hali ya juu ili kutimiza azma ya kutokomeza kabisa umaskini uliokithiri ifikapo mwaka 2030 katika bara la Afrika.

“Wito wangu kwa Wizara, Idara na Taasisi za Serikali kuhakikisha zinaimarisha vitengo vya takwimu kwa kuwaruhusu maofisa waliopo katika vitengo vyao vya sera na mipango wapate fursa ya kupatiwa mafunzo elekezi na ya muda mfupi kwa ajili ya kuongeza ujuzi wao wa kuchambua na kukokotoa takwimu rasmi”

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amesisitiza kuwa hategemei kuona wahitimu walio maliza masomo yao katika ngazi mbalimbali katika Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika wamalize soli za viatu kusaka ajira na kwamba Serikali itawawekea mazingira bora ya kupata ajira haraka.


Kwa upande wake, Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Philip Mpango amesema Serikali itaendelea kushirikiana kikamilifu na Ofisi ya Taifa ya Takwimu katika kutumia takwimu sahihi ambazo zimetolewa na ofisi hiyo katika kupanga shughuli za maendeleo za taifa.
Katika mahafali hiyo ya Pili ya Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewatunuku vyeti wahitimu 133 katika ngazi za Shahada ya Uzamili ya Takwimu, Shahada ya awali ya takiwmu na Stashahada ya takwimu kwa wahitimu kutoka nchi Kumi za Afrika ambazo ni Nigeria,Ghana,Sierra Leon, Ethiopia,Somalia, Uganda, Swaziland, Liberia, Rwanda na mwenyeji Tanzania.

Rais Magufuli afanya uteuzi wa wenyeviti watatu

NDEREMO,VIFIJO VYATAWALA MAHAFALI YA CHUO KIKUU CHA TUMAINI DAR

$
0
0
 Wanafunzi waliohitimu na kutunukiwa Shahada ya Uzamili ya Uongozi wa Biashara wakishangilia wakati wa Mahafali ya 10 ya  Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira tawi la Dar es Salaam Tudarco yaliyofanyika leo Mwenge, Dar es Salaam.

Mkuu wa Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira, Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk Frederick  Shoo, alitunuku  jumla ya wahitimu 733. (PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG}
 Mkuu wa Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira, Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk Frederick  Shoo,akimtunuku Evelyn Wallace Shundi Shahada ya Uzamili ya Uongozi wa Biashara wakati wa Mahafali ya 10 ya  Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira tawi la Dar es Salaam Tudarco yaliyofanyika leo Mwenge, Dar es Salaam.
 Wahitimu Agnes Nsokolo (kulia) na Asha Kidendei wakiwa na furaha baada ya  kuwa miongoni mwa wahitimu 43 waliotunukiwa  Shahada ya Uzamili ya Uongozi wa Biashara wakati wa Mahafali ya 10 ya  Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira tawi la Dar es Salaam Tudarco yaliyofanyika leo Mwenge, Dar es Salaam.
 Evelyn Shundi ambaye ni mfanyakazi wa Ewura akiwa na furaha wakati wa mahafali hayo.
 Wahitimu wakivaa kofia baada ya kutukiwa
 Mmoja wa wanafunzi akipatiwa cheti wakati wa mahafali hayo
 Wakivaa kofia ikiwa ni ishara ya kunukiwa
 Wahitimu wakiwa wamekaa baada ya kutunukiwa
 Wahitimu wakiwa wamesimama mbele ya Mkuu wa Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira wakisubiri kutunukiwa Shahada ya Uzamili
 Domina Rwemanyila (kushoto) na Diana Tengia wakiwa na furaha baada ya kutunukiwa Sahada ya Sanaa ya  Mawasiliano ya Umma
 Ni furaha iliyoje kutunukiwa Shahada ya Uzamili
 Mkuu wa Chuo Kikuu hicho, Dk Frederick Shoo na viongozi wengine wakiwa katika picha ya pamoja na wahitimu waliotunukiwa Sahada ya Uzamili ya Uongozi wa Biashara
 Wapigapicha wakiwa kazini wakati wa mahafali hayo
 Brass Band ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) wakipiga wimbo wa Taifa wakati wa kuhitimisha mahafali hayo
 Julieth (katikati) akiwa na ndugu zake baada ya kuhitimu katika chuo hicho.


RC PAUL MAKONDA AANZA ZIARA YAKE YA SIKU 10 NDANI YA JIJI LA DAR ES SALAAM.

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda ameanza ziara yake ya siku 10 ndani ya jiji la Dar es salaam kwa ajili ya kusikiliza kero za wananchi pamoja na kuzitafutia ufumbuzi.

Ziara hiyo imeanzia katika wilaya ya Kigamboni ambapo kabla ya kwenda kusikiliza kero za wananchi mtaani, Mkuu huyo alizungumza na viongozi wa wilaya hiyo pamoja na kuzindua mpango mkakati wa mkuu wa wilaya ya Kigamboni 

Akiongea na viongozi hao wa wilaya ya Kigamboni, Makonda amesema anafanya ziara hiyo ili kugundua kero za wananachi pamoja kuwahamasisha wafanyakazi wa serikali kuwajibika."Nataka wafanyakazi wafanyekazi kwa bidii ili kuendana na kasi ya Rais wetu, nimegundua asilimia 80 ya wafanyakazi wa serikali hawafanyi kazi, asilimia 80 ya  watumishi umma hawafanyi kazi, ni wapiga majungu, wasoma magazeti, niwambea. Kilichobaki ni kusubiri mwisho wa mwezi kwa ajili ya mshahara," alisema Mkonda.

Pia Makonda alisema hataki kuona wananchi wanakimbilia kwa mkuu wa mkoa kuomba msaada wa utatuzi wa changamoto zao wakati serikali inawafanya kazi kuanzia ngazi ya  vitongoji.Aidha mkuu huyo alitembelea pia mtaa wa Maweni, Mjimwema ambapo alishuhuda uharibifu mkubwa wa mazingira na kumtaka mkuu wa wilaya hiyo pamoja na vyombo vya ulinzi kuwashghulikia wote watakaoendelea kuchimba kokoto eneo hilo.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda akizindua mpango kazi wa manispaa ya Kigamboni leo jijini Dar es Salaam.   Katika ni Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni,Hashim Mgandilwa na kulia ni Mkurungenzi wa manispaa ya Kigamboni,Stepheni Katembe.
 Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandilwa  akizungumza machache katika   uzindunzi wa mpango kazi wa manispaa ya Kigamboni leo jijini Dar es Salaam.
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda na Kamisha wa Polisi Simon Sirro, wakimuangalia mmoja wa vijana wa kituo cha kuwasaidia vijana waliothirika na dawa za kulevya cha PEDEREF Sober,Kigamboni  ambaye alikuwa akitia ushahidi wa jinsi alivyoathiriwa na dawa hizo kwa kubeba dawa tumboni, wakati wa ziara ya mkuu huyo wa mkoa, wilayani humo,leo. 
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda akikagua uharibifu wa mazingira machimbo ya kokoto Mjimwema jijini Dar  es Salaam. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni,Hashim Mgandilwa.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda akikagua machimbo ya kokoto yalipo Mjimwema jijini Dar  es Salaam.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda akizungumza na vijana wa Sober House  iliyopo  Vijibweni leo jijini Dar es Salaam.
 amanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina Simon Sirro  akiwa katika picha ya pamoja na vijana kutoka asasi mbalimbali zisizo za kiserikali zinazo jitolea  kusikiliza  changamoto na kero za wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda akipokea zawadi kutoka kwa  Mmiliki wa Kituo cha  vijana wa Sober House,Nuru Saleh leo jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandilwa  akipokea zawadi kutoka kwa  Mmiliki wa Kituo cha  vijana wa Sober House,   Nuru Saleh leo jijini Dar es Salaam.picha zote na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.







Rais Magufuli amjulia hali mkuu wa mkoa wa Tanga katika hosipitali ya Muhimbili

VIJUSO VYA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI NOV 20

Viewing all 46395 articles
Browse latest View live




Latest Images