Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1046 | 1047 | (Page 1048) | 1049 | 1050 | .... | 1897 | newer

  0 0


  Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani amewataka wananchi waliowekewa alama za kubomoa nyumba zao zilizopo pembezoni mwa barabara ya Njombe-Makete hadi Mbeya KM 205 waanze kuhama kwenye nyumba hizo ili kupisha zoezi la ujenzi wa barabara hiyo kwa kiwango cha lami.

  Akizungumza mara baada ya kukagua barabara hiyo Eng. Ngonyani amesema awamu ya kwanza ya ujenzi wake itaanza wakati wowote kuanzia sasa mara baada ya kupatikana mkandarasi na mkandarasi mshauri ambayo itahusisha sehemu ya Njombe hadi Makete KM 109.4.

  “Kuweni waadilifu waliowekewa alama za kijani kwenye nyumba zao watalipwa fidia lakini wenye alama nyekundu hawatalipwa hivyo ni vizuri wote kutafuta maeneo mengine ya makazi ili kuepuka usumbufu mara zoezi la ujenzi litakapoanza”. Amesema Eng. Ngonyani.

  Eng. Ngonyani amesema kwa kuwa kazi ya ujenzi na ulipaji fidia zinagharamiwa na Serikali ni vema zoezi la ujenzi wa barabara likaanza wakati Serikali ikitafuta fedha kwa ajili ya fidia.“Ili tuweze kufanikiwa katika mambo yote tumeona tuanze na zoezi lenye gharama kubwa ambalo ni ujenzi wa barabara kisha zoezi la fidia litaendelea wakati ujenzi wa barabara unaendelea”. amesisitiza Eng. Ngonyani.

  Naye Mkuu wa Mkoa wa Njombe Dkt. Rehema Nchimbi ameishukuru Serikali kwa jitihada za ujenzi wa daraja la Ruhuhu linalounganisha Mkoa wa Njombe na Ruvuma na ameiomba Serikali kuangalia namna ya kuweka lami barabara inayokwenda kwenye hospitali ya Mkoa wa Njombe na ile inayoenda hospitali ya misheni ya Ikonda wilayani Makete ili kuwezesha barabara hizo kupitika kwa urahisi wakati wote wa mwaka.

  Katika hatua nyingine Mbunge wa Makete Profesa, Norman Sigara amemuomba Naibu Waziri Eng. Ngonyani kuhakikisha Mkandarasi anayejenga barabara ya Njombe –Makete na Makete –Mbeya kupitia Kitulo anaanza kazi iyo kwa wakati ili kuongeza kasi ya wananchi kubomoa nyumba zao katika maeneo ya hifadhi ya barabara na hivyo kuunganisha kirahisi mkoa wa Njombe na Mbeya kwa barabara ya lami.

  Naibu Waziri Ngonyani yupo katika ziara ya kukagua Miundombinu ya Barabara, Bandari na Mawasiliano katika mikoa ya Nyanda za juu Kusini ambapo tayari amekamilisha ziara yake katika Mikoa ya Pwani, Lindi na Ruvuma.

  Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
   
  Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani akifafanua jambo kwa wananchi wa kijiji cha Mang’oto Wilayani Makete ambapo aliwataka walioko kwenye hifadhi ya barabara wabomoe nyumba zao na kutafuta nyumba mbadala ili kuwezesha zoezi la ujenzi wa barabara kuanza na zoezi la fidia lifuate baadaye.
  Mbunge wa Makete Profesa, Norman Sigala akifafanua jambo kwa wananchi wa Jimbo hilo kuhusu umuhimu wa kutafuta nyumba mbadala ili kupisha ujenzi wa barabara ya Njombe –Makete KM 109 utakaoanza hivi karibuni.
  Mkuu wa Mkoa wa Njombe Dkt. Rehema Nchimbi (kulia), akimshukuru Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani kufuatia hatua ya ujenzi wa daraja la Ruhuhu linalounganisha mkoa wa Njombe na Ruvuma.
  Wanananchi wa kijiji cha Mang’oto Wilayani Makete wakimsikiliza Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani (Hayupo pichani).

  0 0  0 0

  Waziri wa Afya katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Tamasha la Kimataifa la Filamu Zanzibar ZIFF, Mhe.Mahmood Thabith Kombo, akizungumza kwenye Uzinduzi wa Tamasha la Uoneshaji wa Filamu kwa njia ya Sinema mkoani Geita, kwa niaba ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe.Nape Nhauye.

  Uzinduzi huo ulifanyika jana katika Ukumbi wa Desire Park Geita ambapo Taasisi ya Sanaa Na Mazingira ya Kijani Consult Tanzania imeanzisha kampeni ya kuonesha bure Filamu mbalimbali kwa ajili ya kufikisha elimu kwa umma ikiwemo elimu ya Utunzaji wa Mazingira (Mabadiliko ya Tabianchi), Ufugaji wa kuku wa kienyeji, Usalama barabarani, Madawa ya kulevya, Madhara ya ndoa za utotoni miongoni mwa mambo mengi ya kijamii. Mradi huo umefadhiriwa na ZIFF.

  Kutokana na Mwitikio wa wanatasnia ya Filamu mkoani Geita kuonesha shauku ya kuwa na Maonesho hayo ya Filamu, Mhe.Kombo alisema mwakani Tamasha la Kimataifa Zanzibar pia litafanyika mkoani Geita ikiwa ni sehemu ya ZIFF ni sehemu ya kusherehekea miaka 20 tangu kuanzishwa ZIFF.
  Na BMG
  Mhe.Kombo alisema mwakani Tamasha la Kimataifa Zanzibar pia litafanyika mkoani Geita ikiwa ni sehemu ya ZIFF ni sehemu ya kusherehekea miaka 20 tangu kuanzishwa ZIFF.
  Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania, Bi.Joyce Fessoo, akizungumza kwa niaba ya Serikali kwenye uzinduzi huo ambapo aliwahakikishia Wanatasnia ya Filamu mkoani Geita na nchini kwa ujumla kwamba Serikali itahakikisha inaboresha zaidi sanaa ya filamu ikiwemo kuendelea kutoa mafunzo ya filamu kwa wanatasnia hiyo ili filamu zinazozalishwa ziwe na ubora.

  Aidha alidokeza kwamba Serikali inatoa baraka zote kuhusiana na Tamasha la Kimataifa la Filamu Zanzibar, pia kufanyika mkoani Geita hapo mwakani.
  Mkuu wa Mkoa wa Geita, Meja Jenerali Mstaafu, Ezekiel Kyunga, akizungumza kwenye Uzinduzi wa Uoneshaji wa Filamu mkoani Geita, ambapo alisisitiza kwamba sanaa ni ajira hivyo wanatasnia hiyo watumie fursa mbalimbali ikiwemo mafunzo yanayotolewa na serikali ili kuboresha zaidi kazi zao.
  Katibu wa Tamasha la Kimataifa la Filamu Zanzibar ZIFF, Robert Manondolo, akizungumza kwenye uzinduzi huo ambapo alibainisha kwamba ZIFF imekuwa ikitoa ufadhiri kwa taasisi mbalimbali nchini ikiwemo Taasisi ya Kijani Consult kwa lengo la kuziwezesha kufikisha elimu kwa umma kwa njia ya kuonesha filamu bure na kufikisha elimu iliyokusudiwa.
  Katibu Tawala Wilayani Geita, Thomas Dimme, akizungumza kwenye uzinduzi wa Tamasha la Uoneshaji wa Filamu bure mkoani Geita ili kufikisha elimu mbalimbali ikiwemo Ufugaji na utunzaji wa Mazingira.
  Herman Matemu (aliyesimama) ambaye ni Kaimu Afisa Tawala mkoa wa Geita, akisalimia kwenye uzinduzi huo.
  Kulia ni Kuka Kahindi ambaye ni Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Sanaa na Mazingira ya Kijani Consult ya mkoani Geita, akisoma risala kuhusiana na Mradi wa Uoneshaji Filamu Bure mkoani Geita.

  Alisema mradi huo umelenga kutoa chachu kwa wanajamii kutumia fursa mbalimbali ikiwemo ufugaji kujipatia kipato badala ya kutegemea shughuli moja kama vile madini. Pia kuwahimiza kujiepusha na uharibifu wa mazingira. Yote hayo pamoja na mengine yanafikishwa kwa wananchi kwa njia ya filamu.
  Mgeni Rasmi, Waziri wa Afya katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Tamasha la Kimataifa la Filamu Zanzibar ZIFF, Mhe.Mahmood Thabith Kombo (kulia) akipokea taarifa ya mradi wa uoneshaji wa filamu bure mkoani Geita kutoka kwa Kuka Kahindi ambaye ni Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Sanaa na Mazingira ya Kijani Consult ya mkoani Geita (kushoto).
  Mkuu wa idara ya Habari, Kijani Consult Tanzania, Rose Mweko, akitoa salamu zake kwenye uzinduzi wa mradi wa kuonesha filamu bure katika maeneo ya wazi mkoani Geita.
  Kutoka Kushoto ni Mwakilishi wa Balozi wa Denimark nchini Tanzania, Dotto Kahindi, Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania, Bi.Joyce Fessoo na Mgeni Rasmi, Waziri wa Afya katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Tamasha la Kimataifa la Filamu Zanzibar ZIFF, Mhe.Mahmood Thabith Kombo, wakifuatilia kwa makini zoezi la uzinduzi wa mradi wa Kuonesha Filamu bure mkoani Geita ili kufikisha elimu kuhusu masuala mbalimbali kwa wanajamii.
  Meza kuu wakifuatilia matukio mbalimbali kwenye uzinduzi wa mradi wa Kuonesha Filamu bure mkoani Geita
  Wageni mbalimbali waliohudhuria uzinduzi huo
  Maafisa Habari mkoani Geita wakifuatilia uzinduzi wa mradi wa kuonesha filamu bure mkoani Geita
  Wageni mbalimbali wakifuatilia uzinduzi wa mradi wa kuonesha filamu bure mkoani Geita
  Wanahabari mkoani Geita wakifuatilia uzinduzi wa mradi wa kuonesha filamu bure mkoani Geita
  Wanatasnia wa Filamu mkoani Geita
  Burudani za asili mkoani Geita
  Burudani za asili zikiendelea
  Baadhi ya wakazi wa mkoa wa Geita wakifuatilia Uzinduzi wa Mradi wa Uoneshaji wa Filamu bure mkoani humo ili kufikisha elimu ya masuala mabalimbali ikiwemo uharibifu wa mazingira pamoja na ufugaji kwa njia ya filamu
  Mgeni Rasmi, Waziri wa Afya katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Tamasha la Kimataifa la Filamu Zanzibar ZIFF, Mhe.Mahmood Thabith Kombo (mwenye kofia) pamoja na viongozi wengine, wakiwa kwenye picha ya pamoja na watoto walioshiriki shindano fupi la kucheza muziki kwenye Uzinduzi wa Mradi wa kuonesha Filamu bure mkoani Geita.
  Mgeni Rasmi Mhe.Kombo (mwenye kofia) pamoja na viongozi wengine, wakiwa kwenye picha ya pamoja na watoto, Maisala Ibrahimu anayesoma kidato cha pili shule ya Sekondari Kangalala (ke) na Joshua Tito anayesoma darasa la kwanza shule ya msingi Kivukoni Geita (Me) ambao walioonesha vipaji vya hali ya juu katika kucheza muziki. 

  ZIFF imetoa fursa ya kuwanunulia mavazi ya shule watoto hao huku pia wakipata fursa ya Kuhudhuria Tamasha la Kimataifa la Filamu katika Visiwa vya Zanzibar hapo mwakani.

  Bonyeza HAPA Kutazama picha za kikao cha Wanatasnia ya Filamu mkoani Geita na Bodi ya Filamu Tanzania.

  0 0

   Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Mohammed Kiganja akiongoza Wachezaji wa timu ya Taifa ya mchezo wa kabadi walipowasili jijini Dar es salaam wakitokea nchini India kwenye mashindano ya mchezo huo uliofanyika hivi karibu nchini humo .
   Wachezaji wa timu ya Taifa ya mchezo wa kabadi wakiwasili jijini Dar es salaam wakitokea India kwenye mashindano ya mchezo huo uliofanyika hivi karibu nchini humo ambapo Tanzania imetolewa kwenye mashindano hayo .
  Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Mohammed Kiganja akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam wakitokea nchini India kwenye mashindano ya mchezo wa kabadi uliofanyika hivi karibu nchini humo.
   

  0 0
 • 11/20/16--21:02: TIBA YENYE NGUVU ZA AJABU!
 • Tiba hii inaitwa JIKO. Kila mwanaume anae itumia, INAMPONYESHA KABISA tatizo la UKOSEFU na UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME. Imethibitishwa na MKEMIA MKUU WA SERIKALI YA TANZANIA

  Kufahamu jinsi tiba hii inavyo fanya kazi, bofya link hii hapa chini :


  Kwa mahitaji yako ya tiba hii, wasiliana na duka la NEEMA HERBALIST & NUTRITIONAL FOODS CLINIC kwa simu namba 0766 53 83 84.

  Tunapatikana UBUNGO jijini DAR ES SALAAM, jirani na SHULE YA MSINGI UBUNGO NATIONAL HOUSING nyuma ya jengo la UBUNGO PLAZA. · Kwa wateja waliopo DAR ES SALAAM, wasio na nafasi ya kufika ofisini kwetu, watapelekewa dawa mahali walipo ( HOME & OFFICE DELIVERY ).

  · Kwa wateja waliopo mikoani, watatumiwa dawa kwa njia ya mabasi mbalimbali.

  · Kwa wateja waliopo Zanzibar, watatumiwa dawa kwa njia ya usafiri wa boti.

  · Kwa wateja wa Mombasa, watatumiwa dawa kwa basi la TAHMEED COACH.

  · Kwa wateja wa NAIROBI watatumiwa dawa kwa basi la DAR EXPRESS.

  · Na kwa wateja wa UGHAIBUNI ( DIASPORA), watatumiwa dawa kwa njia ya POSTA au DHL.

  · Kwa taarifa zaidi kuhusu huduma zetu, tembelea kila siku website yetu www.neemaherbalist.com


  0 0

  Msafara wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ukiwa eneo la Kisarawe II.
  15
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe: Paul Makonda akisalimiana na Mkurugenzi wa Kiwanda cha maji na maziwa (MILKCOM), Said Nahdi (mwenye kanzu), alipotembele kukagua shughuli za kiwanda hicho wakati wa ziara yake.
  16
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe: Paul Makonda (katikati), akiwa amefuatana na Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandilwa, na   Mkurugenzi wa Kiwanda cha maji na maziwa (MILKCOM), Said Nahdi  (mwenye kanzu) wakiwa ndani ya kiwanda hicho wakikagua shughuli za kiwanda hicho.
  17
  Mkurugenzi wa Kiwanda cha Maziwa na Maji (MILKCOM), Yusuph  Said akizungumza na waandishi wa habari wakati wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe: Paul Makonda alipotembelea kukagua kiwanda.
  18
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe: Paul Makonda akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa shule ya msingi Tunduwi Songani.
  19
  Wananchi wa Tunduwi Songani wakishuhudia uwekaji jiwe la msingi la ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa shule ya msingi .
  20
  Wanafunzi wa shule ya msingi Tunduwi Songani.
  21
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe: Paul Makonda  akimsikiliza Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Bakari Mbwana kuhusiana na kero wanazozipata zalugha chafu wanapokwenda katika zahanati .

  MKUU wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amesema Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Bakari Mbwana hawezi kupandishwa cheo kuwa Mganga Mkuu wa Wilaya hiyo mpaka hapo atakapotatua changamoto za zahanati ya Tundu Songani Kata ya Pemba Mnazi.

  Makonda aliyasema hayo mwisho wa  ziara yake ya siku ya pili Wilayani Kigamboni Novemba 20, 2016 wakati alipokwenda kuzindua madarasa ya Shule ya Msingi Tundu Songani,ambapo  mara baada kuzindua madarasa hayo aliongea na wananchi na kusikiliza kero.

  “Kwa mamlaka uliopewa na Rais wewe ndio mwakilishi wake katika upande wa afya wilaya ya Kigamboni  uwezi kupandisha cheo kuwa Mganga wa Wilaya hii mpaka hapo utakaponiakikishia kupeleka gari la wagonjwa na kutoa lugha nzuri kwa wateja”alisema Makonda.

  Makonda alisema awezi kumtumbua jipu Mganga huyo kwa kuwa ameteuliwa muda mfupi mpaka sasa ana mwezi mmoja  hivyo amempa muda kwa ajili ya kumwangalia katika utendaji wake kama kaimu Mganga mkuu wa Wilaya hiyo.

  Hatua hiyo ya Makonda kutoa agizo la kumchunguza Mganga huyo linafuatia wananchi wa Tundu Songani kulalamika mbele ya Serikali ya Mkoa  kuwa mganga huyo ajawai kufika eneo hilo na wananchi kupewa lugha chafu wanapokwenda katika zahanati .

  Kwa upande wake Kaimu Mganga Mkuu huyo,alipoulizwa kuhusiana na malalamiko ya wananchi alisema  yeye kama mganga mkuu anachofahamu changamoto iliyokuwepo katika zahanati hiyo gari la wagonjwa akuna.
  Naye Mwananchi Asha Abadalah alisema mwanamke Mjamzito akienda katika kituo hicho anambiwa aende katika hospitali ya Wilaya ya Temeke  na Mgaga huyo ajawai kufika katika Kata hiyo ya Pemba Mnazi ni mara yake ya kwanza.

  Wakati huohuo katika kusogeza huduma za jamii kwa wanachi Makonda alisema kuhusu kusogeza huduma ya umeme kwa wananchi mradi wa umeme vijijini utawafikia kila mwananchi atapata umeme huo kwa gharama y ash,27,000 na kila mmoja atavuta.Alisema utaratibu wa kupata fomu watatangaziwa wote na Watendaji wao wa Mitaa husika
  Hivyo wananchi wawe wavumilivu kwa muda wasubilie mradi huo ufike ili wote waweze kupata umeme wa bei raisi .
  22
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe: Paul Makonda akisikiliza kero za wanachi katika mkutano wa hadhara ulifanyika katika uwanja wa shule ya msingi Buyuni ikiwa mwisho wa ziara siku ya pili katika Wilaya ya Kigamboni jijini Dar es Salaam.
  23
  Mkazi wa Buyuni akielezea kero zake.
  2425
  Wananchi wa Buyuni wakiwa katika mkutano wa hadhara.
  1
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe: Paul Makonda (katikati) akisaini kitabu cha wageni alipotembelea daraja la Nyerere lililopo Wilaya ya Kigamboni jijini Dar es Salaam wakati wa ziara yake ya kuangalia na kutatua changamoto za wananchi ikiwa ni mwisho wa ziara siku ya pili kwenye Wilaya hiyo (kulia), Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Profesa Godius Kahyrara, Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandilwa.
  PICHA ZOTE NA PHILEMON SOLOMON-FULLSHANGWEBLOG
  01
  Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandilwa akimuelezea Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kuhusiana na tozo  ya magari  kuvuka katika daraja la Nyerere wilayani.
   
   Mgandilwa, amelitaka Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF) kuangalia upya  tozo  ya magari  kuvuka katika daraja la Nyerere wilayani humo  ikiwa ni pamija  na kutaka magari yote ya  serikali na watumishi wa umma wanaofanya kazi katika halmshauri hiyo kutokulipa tozo hiyo.
  Mkuu huyo wa wilaya alitoa kilio hicho  mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul akonda, wakati wa ziara  ya mkuu huyo wa mkoa ya kusikiliza na kutatua kero za wananchi  mkoani humo.

  Mgandilwa alisema, kitendo cha  magari  ya halmshauri hiyo na watumishi wa umma wanaoishi nje ya halmshauri kutozwa fedha kuvuka katika daraja hilo   kinaleta changamoto kubwa  na kukwamisha ufanisi.
  Alimuomba Makonda kuingilia kati suala la gharama hizo  na kuitaka NSSF kuziondoa kwa magari yote ya halmshauri na  watumishi.

  “Kila gari  ya halmashari inayopita katika daraja hili inatozwa fedha. Hasa ikizingatiwa kuwa halmashauri hii ni mpya hivyo  watumishi wengi wanatokea nje  ya halmashauri,”alisema Mgandilwa.

  Alielezea changamoto nyingine kuwa ni  kipande cha Kilometa 1.5  cha barabara ya vumbi kutoka katika daraja  hilo upande wa Kigamboni.
  “Hii barabara licha ya kutumiwa na magari mengi  yanayopita katika daraja hili, lakini  haijajengwa kwa kiwango cha lami hivyo wananchi kupata kero kubwa   kutokana na vumbi ,”alisema Mgandilwa.
  2
  Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Profesa Godius Kahyrara  akitoa ufafanuzi kuhusu suala la tozo la daraja daraja la Nyerere lililopo Wilaya ya Kigamboni jijini Dar es Salaam.
  Akitoa ufafanuzi kuhusu suala  la tozo  ya daraja hilo, Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Profesa  Godius Kahyrara, alikiri kupokea malalamiko ya watu wengi kutaka kupunguziwa au kuondolewa tozo hiyo.
  “Ni kweli tumekuwa tukipokea malalamiko hayo kutoka kwa wananchi mbalimbali, lakini suala ni kwamba sisi kama NSSF huwa hatupangi viwango vya tozo za kuvuka daraja bali tunapokea maelekezo kutoka  wizara husika (Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi),”alisema Profesa Kahyaraa.
  Alisema atawasilisha suala hilo katika wizara  husika ili kuona uwezekano  wa kuondoa tozo hiyo ama kupunguza.
  Mbali na hayo, Profesa Kahyarara, alitaja changamoto zingine kuwa ni  vijana kuligeuza daraja hiyo kuwa kijiwe na wengine kuwa na nia ovu ya kulihujumu kwa kuharibu miundombinu, ingawa ulinzi umeendelea kuimarishwa.
  3
   Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akifafanua.
  Kwa upande wa Makonda, alisema, suala la tozo ya magari ya halmashauri na watumishi  kuvuka katika daraja hilo atazungumza na waziri mwenyedhamana.
  4
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Mhe: Paul Makonda (kushoto), akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandilwa wakielekea kugagua miundombinu ya daraja hilo.
  5
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe: Paul Makonda (kushoto), akiangalia mti uliopandwa na  Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandilwa.
  6
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe: Paul Makonda akiwa na kamati ya ulinzi na usalama pamoja na viongozi wengine wakiangali mtaro wa wakupitishia maji katika daraja la Nyerere lililopo Wilaya ya Kigamboni jijini Dar es Salaam.
  7
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Mhe: Paul Makonda akiwa na kamati ya ulinzi na usalama pamoja na viongozi wengine wakikagua miundombinu ya daraja hilo.
  8
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Mhe: Paul Makonda akizungumza na wananchi   wanaoshi eneo la daraja Nyerere lililopo Wilaya ya Kigamboni jijini Dar es Salaam ilipoishia barabara ya kiwango cha lami aliposimama na msafara wake ili kusikiliza kero na changamoto wanazozipata katika eneo hilo.
  Akihutubia wananchi wanaoishi jirani na daraja hilo,Makonda alisema, tayari mkandarasi wa ujenzi  wa kipande cha barabara cha kilometa 1.5 inayounganisha daraja la Nyerere  atanza kujenga kipande hicho kwa kiwango cha lami.
  “Mkandarasi aliyejenga daraja  hili ndiyo ataendelea na ujenzi  wa kipande  hiki kilichobakia.Pesa zipo na ndani ya wiki mbili kuanzia sasa  ujenzi utaanza,”alisema.
  9
  Wananchi wanaoishi karibu na mradi wa daraja hilo wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Mhe:   Paul Makonda (hayupo pichani) alipo simama na msafara wake.
  10
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe: Paul Makonda akisikiliza kero za wananchi aliposimama na msafara wake eneo la Kibada Wilaya ya Kigamboni jijini Dar es Salaam.
  11
  Mkazi wa Kibada, Bi Siwazuri Abdalah akimuelezea Makonda kero anazozipata katika Hospital ya kibada.
  12
  Mkuu wa Idara ya Uifadhi wa Mazingira na Usimamizi wa Taka Ngumu, Fanuel Kibera akimuonyesha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda (katikati), mchoro wa dampo la kisasa  litakalojengwa eneo la Kisarawe II Kigamboni.
  13
  Muonekano wa eneo litakalojengwa dampo la kisasa  Kisarawe II Kigamboni.
  26
  Vikosi vya ulinzi na usalama wakisaidia kulisukuma gari la  Clouds Media liliponasa katika mchanga ene la Kisarawe II wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kukagua eneo litakalojengwa dampo la taka la kisasa.


  0 0
  0 0

   Muonekano wa Meli za Mv. Njombe na Mv.Ruvuma ambazo ujenzi wake umekamilika kwa asilimia 99, meli hizo zipo katika hatua za majaribio kabla ya kuanza kutoa huduma.

   Mkurugenzi wa Kampuni ya Songoro Marine Transport Bw. Salehe Songoro akimuonesha Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani (katikati) ripoti ya ukaguzi wa ujenzi wa meli mbili za mizigo katika bandari ya Itungi ziwa Nyasa.
   Kaimu Meneja  wa bandari ya Itungi na Kiwira Eng. Juma Kisavara (wa kwanza kushoto) akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani (katikati) kuhusu namna ya kuondoa mchanga katika kingo za ziwa Nyasa ili kuwezesha meli zinazotengenezwa kuingizwa katika maji kwa urahisi.
   Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani akikagua Meli ya Mv. Njombe ambayo ujenzi wake umekamilika kwa asilimia 99.
   Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani akipanda juu ya Meli ya Mv. Ruvuma ambayo ujenzi wake umekamilika kwa asilimia 99 ili kuona mfumo wa injini unavyofanya kazi.
   Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani akikagua mfumo wa uendeshaji wa Meli ya Mv. Njombe ambao ujenzi wake umekamilika kwa asilimia 99.

  Meneja wa Wakala wa barabara Mkoa wa Mbeya Eng. Paul Lyakurwa akifafanua jambo kwa  Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani alipokagua ujenzi wa barabara ya Kikusya-Ipinda hadi Matema KM 34.6 ambayo inajengwa kwa kiwango cha lami.Picha na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano


  Imeelezwa kuwa uchumi wa wananchi wa Mikoa ya Njombe, Mbeya na Ruvuma utaimarika kwa kasi kama watatumia vizuri fursa ya uwepo wa meli za mizigo na abiria katika ziwa Nyasa.

  Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani amesema kukamilika kwa meli mbili za mizigo za Mv. Njombe na Mv. Ruvuma na ujenzi wa meli ya abiria ya Mv. Mbeya ni fursa mpya ya kiuchumi kwa wakazi wa mikoa hiyo.

  “Tumejipanga kuhakikisha tunafungua ukanda huu wa nyanda za juu kusini kiuchumi hivyo ni jukumu la wananchi kuchangamkia fursa za kibiashara zinazoweza kusafirishwa ndani na nje ya nchi ili kukuza uchumi”.amesema Eng. Ngonyani.

  Naibu Waziri Ngonyani ameelezea kuridhishwa kwake na hatua ya ujenzi wa meli za Mv.Njombe na Ruvuma ambao umefikia asilimia tisini na tisa na kusisitiza kuwa Serikali itaendelea kuwaamini makandarasi wazawa wanaofanya kazi kwa ubunifu, uadilifu na uaminifu ili kutoa fursa nyingi za ajira kwa watanzania.

  Kaimu Meneja wa bandari ya Itungi na Kiwira Eng. Juma Kisavara amemhakikishia Naibu Waziri Ngonyani kuwa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) imejipanga kuhaikikisha bandari zote kumi na tano zilizopo katika ziwa Nyasa kwa upande wa Tanzania zinafufuliwa na kutumika kupakia na kushusha mizigi ikiwemo vifaa vya ujenzi, makaa ya mawe,mbolea na mazao ambayo yana soko ndani na nchi za jirani.

  Eng. Kisavara amemhakishia Naibu wa Ujenzi kuwa tayari wametafuta soko la kutosha la kusafirisha mizigo hivyo kuiomba Serikali kuendelea na kasi ya ujenzi wa meli nyingine zitakazotumika katika ziwa Nyasa.

  Zaidi ya shilingi bilioni 11 zimetumika kwa ajili ya ujenzi wa Meli ya Mv.Ruvuma na Mv. Njombe zinazojengwa na kampuni ya Songoro Marine Transport ya hapa nchini na meli hizo zinatarajiwa kukabidhiwa kwa Serikali mwezi Januari mwakani.

  Katika hatua nyingine Naibu Waziri Ngonyani amekagua ujenzi wa barabara ya Kikusya-Ipinda hadi Matema KM 34.6 wilayani Kyela inayojengwa kwa kiwango cha lami na kusisitiza kuwa Serikali italipa fedha kwa mkandarasi anayejenga barabara hiyo ili kuiwezesha kukamilika kwa muda uliopangwa.

  Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.  0 0

   Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu)Mhe. Dkt. Abdallah Possi akipokea mafuta maalumu ya ngozi kwa watu wenye ualbino kutoka kwa Mkuu wa Kituo cha kuhudumia watoto wenye Ualbino cha Lamadi Bi. Hellen Ntambulwa ikiwa ni sehemu ya zawadi kwa ziara yake kituoni hapo. Novemba 20, 2016

   Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi  akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watoto wenye ualbino wanaolelewa na Kituo cha Lamadi Wilayani Busega Mkoa wa Simiyu.
  Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi akimsikiliza Mwandishi wa habari wa ITV Bw. Berensi China wakati wa ziara yake Kituo cha kulelea watoto wenye Ualbino cha Lamadi Simiyu.  (PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU).
   Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi  akisalimiana na baadhi ya Watendaji wa Serikali katika Wilaya ya Busega Mkoani Simiyu wakati wa ziara yake ya kutembelea vituo na shule za watu wenye Ulemavu tarehe 20 Novemba, 2016.
   Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi  akizungumza na baadhi ya watendaji wa Serikali (hawapo pichani) katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega Mkoani Simiyu alipofanya ziara ya kikazi.

   Mkuu wa Wilaya ya Busega Mhe. Tano S. Mwera akizungumza na watendaji wa Kituo cha kulelea watoto wenye ualbino cha Lamadi (hawapo pichani) wakati wa ziara ya Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi Novemba 20, 2016 Mkoani Simiyu.


  0 0


  Meneja Mawasiliano wa Barclays Tanzania, Hellen Siria, akihojiwa na waandishi kutoka vyombo mbalimbali vya habari, wakati wa uzinduzi rasmi wa maabara ya kompyuta inayotembea itakayohudumia shule nne za sekondari katika wilaya hiyo. Mradi wa kompyuta unawezeshwa kwa kushirikiana na asasi ya PEN Tanzania. Hafla hiyo ilifanyika katika Shule ya Sekondari Kijitonyama, Dar es Salaam .
  Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Barclays Tanzania, Aron Luhanga (wa tatu kulia), Meneja Teknolojia wa benki hiyo, Dakshit Pandya (katikati mwenye miwani), na Mkurugenzi wa asasi ya PEN Tanzania, Sharnel Deo (wa nne kulia), wakikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa maabara ya kompyuta inayotembea itakayohudumia shule nne za sekondari katika wilaya hiyo. Mradi wa kompyuta unawezeshwa kwa kushirikiana na asasi ya PEN Tanzania. Hafla hiyo ilifanyika katika Shule ya Sekondari Kijitonyama, Dar es Salaam .
  Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Barclays Tanzania, Aron Luhanga (wa pili kulia) akikabidhi pedi za kike kwa baadhi ya wanafunzi wa shule za sekondari za Wilaya ya Kinondoni mara baada ya uzinduzi wa maabara ya kompyuta inayotembea itakayohudumia shule nne za sekondari katika wilaya hiyo. Mradi wa kompyuta unawezeshwa kwa kushirikiana na asasi ya PEN Tanzania. Hafla hiyo ilifanyika katika Shule ya Sekondari Kijitonyama, Dar es Salaam. Kulia ni Meneja Teknolojia wa benki hiyo, Dakshit Pandya.
  Mtaalamu wa Mifumo ya Kompyuta wa Benki ya Barclays, Goodhope Mongi (wa tatu kulia) akikabidhi pedi za kike kwa baadhi ya wanafunzi wa shule za sekondari za Wilaya ya Kinondoni mara baada ya uzinduzi wa maabara ya kompyuta inayotembea itakayohudumia shule nne za sekondari katika wilaya hiyo. Mradi wa kompyuta unawezeshwa kwa kushirikiana na asasi ya PEN Tanzania. Hafla hiyo ilifanyika katika Shule ya Sekondari Kijitonyama, Dar es Salaam. Kulia ni Meneja Teknolojia wa benki hiyo, Dakshit Pandya na Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa benki hiyo, Aron Luhanga.
  Mkuu wa Kitengo cha Mifumo ya Teknolojia wa Benki ya Barclays, Gustasv Mphosu (wa pili kulia) akikabidhi pedi za kike kwa baadhi ya wanafunzi wa shule za sekondari za Wilaya ya Kinondoni mara baada ya uzinduzi wa maabara ya kompyuta inayotembea itakayohudumia shule nne za sekondari katika wilaya hiyo. Mradi wa kompyuta unawezeshwa kwa kushirikiana na asasi ya PEN Tanzania. Hafla hiyo ilifanyika katika Shule ya Sekondari Kijitonyama, Dar es Salaam. Kulia ni Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa benki hiyo, Aron Luhanga.
  Ofisa Masoko wa Benki ya Barclays, Nasikiwa Berya (wa tano kushoto), akitoa maelekezo kwa baadhi ya wanafunzi waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa maabara ya kompyuta inayotembea itakayohudumia shule nne za sekondari katika wilaya ya Kinondoni. Mradi wa kompyuta unawezeshwa kwa kushirikiana na asasi ya PEN Tanzania. Hafla hiyo ilifanyika katika Shule ya Sekondari Kijitonyama, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Wengine kutoka kushoto ni Meneja Mawasiliano wa PEN Tanzania, Nancy Kataraihya, Meneja Mawasliano wa Barclays, Hellen Siria na Meneja Teknolojia wa benki hiyo, Dakshit Pandya.

  Wawakilishi kutoka Benki ya Barclays, asasi ya PEN Tanzania na baadhi ya wahudhuriaji wengine wakipozi kwa picha ya kumbukumbu mara baada ya hafla hiyo.

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo akiwasalimiana na viongozi wa Wilaya katika eneo la mapokezi wakati wa ziara yake Wilayani hapo.

  Nteghenjwa Hosseah , Monduli.

  Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo ameuagiza uongozi wa wilaya ya Monduli Mkoani Arusha pamoja na baraza la madiwani la wilaya hiyo kuhakikisha wanabadilisha umiliki wa shamba la Manyara ranch lenye ukubwa wa ekari 44,930 kutoka kwa taasisi ya Tanzania Land Conservation Trust{TLCT} kwenda kwa wananchi wa vijiji viwili kama Rais wa awamu ya tatu Mhe. Benjamini William Mkapa alivyoagiza.

  Rc Gambo alitoa agizo hilo katika mikutano ya hadhara iliyofanyika katika kata ya Elesilalei na Makuyuni baada ya kutembelea miradi  ya mamilioni ya fedha iliyopo ndani ya shamba hilo inayofadhiliwa na African Wildlife Foundation{AWF} na kuelezwa kero na changamoto zilizopo juu ya umiliki wa shamba hilo kwa taasisi ya TLCT.
  Mkuu wa Mkoa wa Arusha akitoa maelekezo ya kubadilisha Hati ya Umiliki wa shamba kutoka kwa TLCT kwenda kwa wananchi wa vijiji vya Elesilalei na Ortukai.

  Alisema nyaraka zinaonyesha wazi kuwa Shamba hilo lilitolewa kwa wananchi wa vijiji vya Elesilalei na Ortukai na Rais Mstaafu wa awamu ya tatu  mwaka 1999   kwa ajili ya kilimo na ufugaji lakini hilo halikufanyika badala yake  taasisi ya TLCT ikajimilikisha shamba hilo kinyume na maagizo.

  Mkuu huyo wa Mkoa  alisema kutokana na hali hiyo ninawaagiza viongozi wote wa wilaya ya Monduli wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya hiyo pamoja na baraza la madiwani kuhakikisha ndani ya muda mfupi wanabadilisha umilikiwa wa shamba hilo kutoka taasisi hiyo kwenda katika vijiji hivyo.

  Gambo alisema serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt John  Magufuli iko madarakani kwa ajili ya kuwahudumia wanyonge na watu wa hali ya chini na kamwe haiwezi kuona baadhi ya watu fulani wananufaika na rasilimali ya nchi kwa manufaa yao.
  Meneja wa Ranch hiyo Ndg. Fidelis Ole Kashe akiwasilisha taarifa ya Shamba hilo kwenye Kikao maalum na Mkuu wa Mkoa wa Arusha pamoja na viongozi wa Wilaya.

  Alisema TLCT inamiliki shamba hilo kinyume na maagizo kwani shamba hilo lilipaswa kumilikiwa na vijiji hivyo kwa faida yao lakini walijitokeza wataalamu wakabadilisha maelekezo hayo  na kujimilikisha kitu ambacho Serikali ya Awamu ya Tano haiwezi kulivumilia kamwe.

  ‘’Nimeagiza umiliki wa shamba hili unapaswa kubadilishwa haraka kwa kushirikisha vikao na kufuata taratibu zote za kisheria ikiwemo kupitishwa na baraza la madiwani ili wananchi waweze kunufaika na ardhi yao na sio watu wachache wanaolipwa mamilioni ya fedha bila ya sababu za msingi’’alisema Gambo.

  Naye Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mhe. Julius Kalanga na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Mhe. Isack Joseph wote kwa pamoja waliunga mkono wazo la Mkuu wa Mkoa na kusema kuwa watatoa ushirikiano wa dhati kuhakikisha umiliki wa shamba hilo unabadilishwa na kwenda kwa vijiji hivyo.
  Mkurugenzi wa TLCT Ndg. Boniface Ngimojiro akielezea muundo wa Taasisi hiyo yenye umiliki wa Shamba la Manyara Ranch.

  Mkurugenzi wa TLCT Bonfance Ngimojiro alipopewa nafasi ya kujieleza katika mikutano hiyo miwili alisema kuwa taasisi hiyo inaongozwa na bodi ya wadhamini yenye wajumbe nane wakiongozwa na Mbunge wa zamani wa Mondul, Mhe. Edward Lowassa kama mwenyekiti wa Bodi hiyo.

  Ngimonjiro alikiri kupata amri ya kubadilishwa umiliki wa shamba hilo kutoka katika taasisi hiyo kwenda kwa wananchi wa vijiji hivyo viwili lakini yeye hawezi kujuwa ni kwa nini amri hiyo hadi jana haikutekelezwa.

  Mkurugenzi huyo alisema yeye ni mwajiriwa tu ambaye hajalipwa mishahara kwa miaka zaidi ya minne sasa katika taasisi hiyo hivyo hawezi kujuwa kwa undani zaidi kushindikana kutekelezwa kwa amri hiyo kwani wakitafutwa wahusika wanaweza kuwa na majibu sahihi.
  Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo akikagua Boma la Ngombe lililopo katika shamba la Manyara Ranch.

  Naye Meneja wa AWF, Fidelis Ole Kashe yeye alisema kuwa wamekuwa wakifanya kazi katika mazingira magumu sana ndani ya shamba hilo pamoja na kufadhili miradi mbalimbali ya maendeleo katika shamba hilo ikiwemo shule,zahanati ,ufugaji wa kisasa na machinjio.

  Kashe alisema utulivu ndio njia pekee itayofanya miradi iliyopo katika shamba hilo kuendelea vinginevyo wafadhili hao wanaweza kusikitisha kila kitu.

  Alisema AWF imekuwa mstari wa mbele kufadhili miradi mbalimbali katika wilaya ya Monduli na nchini kwa ujumla na inapenda kuona fedha inazotoa zinafanya kazi iliyokusudiwa na sio vinginevyo.
  Mbunge wa LongIDO Mhe. Julius Kalanga(kulia) akiwa na viongozi wa Chama cha Mapinduzi katika ziara ya Mkuu wa Mkoa.
  Eneo la malisho kwa ajili ya Ngombe 780 waliopo katika shamba hilo na Kondoo 300.

  0 0

  Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya 
  Taifa ya Uchaguzi (NEC) 
  Bw. Kailima Ramadhani
  Na Margareth Chambiri – Dar es salaam.

  Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Bw. Kailima Ramadhani amesema jambo kubwa ambalo watanzania wanapaswa kujifunza kutokana na Uchaguzi wa Marekani uliomalizika hivi karibuni ni kwa wananchi kuheshimi mifumo ya Uchaguzi.

   Mkurugenzi Kailima ametoa kauli hiyo ikiwa ni tathimi yake kuhusu uchaguzi huo wa Marekani na namna ambavyo baadhi ya watu wamekuwa wakihoji kuhusu ucheleweshaji wa kutangaza matokeo ya uchaguzi unaofanywa na Tume ikilinganishwa na ilivyofanyika nchini Marekani.

  Akizungumza mwishoni mwa wiki katika kipindi cha Power Breakfast kinachorushwa na Kituo cha Redio cha Clouds FM, Kailima amesema siyo sahihi kulinganisha uchaguzi wa Marekani na Tanzania, akitolea mfano sekta ya mawasiliano ambayo ni muhimu katika kusafirisha vifaa na taarifa mbalimbali za uchaguzi inavyokabiliwa na changamoto.

  Amesema watanzania na hasa Wapiga kura wengi wanaishi maeneo ya vijijini ambayo baadhi yake hayafikiki kwa urahisi na kwamba haiwezekani Tume ikatangaza matokeo bila kuhakikisha kuwa kila kura imehesabiwa ikiwemo ya yule mwananchi wa kijijini.

  Amebainisha kuwa yapo mambo ya msingi ambayo watanzania wanapaswa kujifunza kutokana na Uchaguzi wa Marekani, kubwa ikiwa ni hatua ya kuheshimu mifumo ya Uchaguzi sambamba na Mamlaka zinazosimamia chaguzi hizo.

  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), Bi. Eda Sanga na msomaji wa taarifa ya pamoja ya Mtandao wa wadau kutoka asasi za kiraia unaotetea marekebisho ya sheria na sera ihusuyo usalama barabarani Tanzania akizungumza katika Siku ya Kimataifa Kuwakumbuka Wahanga wa Ajali za Barabarani inayoadhimishwa kila Novemba 20, 2016 Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), Bi. Eda Sanga (katikati) na msomaji wa taarifa ya pamoja ya Mtandao wa wadau kutoka asasi za kiraia unaotetea marekebisho ya sheria na sera ihusuyo usalama barabarani Tanzania akizungumza katika Siku ya Kimataifa Kuwakumbuka Wahanga wa Ajali za Barabarani inayoadhimishwa kila Novemba 20, 2016. Kulia ni Jones John kutoka Taasisi ya Jukwaa la Haki za Watoto Tanzania na Mwakilishi kutoka TAWLA, Nasieku Kisamby (kushoto). Taasisi ya Jukwaa la Haki za Watoto Tanzania, Jones John (katikati) akizungumza katika Siku ya Kimataifa Kuwakumbuka Wahanga wa Ajali za Barabarani inayoadhimishwa kila Novemba 20, 2016 iliyofanyika Ofisi za TAMWA jijini Dar es Salaam. Kulia ni Bi. Gladness Munuo kutoka TAMWA


  MTANDAO WA WADAU KUTOKA ASASI ZA KIRAIA UNAOTETEA MAREKEBISHO YA SHERIA NA SERA IHUSUYO USALAMA BARABARANI TANZANIA. SIKU YA KIMATAIFA KUWAKUMBUKA WAHANGA WA AJALI ZA BARABARANI 20 NOVEMBA, 2016.

  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI Matukio ya ajali za barabarani yamekuwa na athari nyingi hapa nchini kiuchumi na kijamii. Vilevile matukio haya ya ajali za barabarani yamekuwa yakiwasababishia wananchi madhara makubwa yakiwemo kupoteza maisha, majeraha makubwa, ulemavu wa kudumu, mali kuharibika ikiwa ni pamoja na kuacha familia nyingi zikiwa tegemezi baada ya kuondokewa na watu wanaowategemea. 
   
  Takwimu zinaonyesha kuwa takribani watu milioni 1.24 duniani hufariki kila mwaka kutokana na ajali za barabarani, aidha, watu milioni 20 mpaka 50 hupata ulemavu. (Hii ni kutokana na takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO). Kadhalika sehemu kubwa ya vifo na madhara ya ajali hizi zimetokea Kusini mwa Jangwa la Sahara , Tanzania ikiwa moja ya nchi hizo. 
   
  Takwimu pia zinaonyesha kuwa ajali nyingi zinatokea kwa sababu ya makosa ya kibinadamu hasa uzembe wa madereva kutokutii sheria na kanuni za barabarani, ambapo kwa mujibu wa taarifa za jeshi la polisi nchini Tanzania, asilimia 76% ya ajali barabarani husababishwa na uzembe wa madereva, asilimia 8% husababishwa na ubovu wa barabara. Aidha ubovu wa vyombo vya moto husababisha ajali kwa asilimia 16%. 
   
  Hata hivyo ajali nyingi zinaepukika kama madereva na watumiaji wengine wa barabara watazitii sheria na kanuni za Usalama barabarani. Kutokana na ajali hizo kuongezeka ndio maana ikatengwa siku maalum ya kimataifa ya kuwakumbuka waathirika wa ajali za barabarani kila mwaka ambayo huadhimishwa kila ifikapo tarehe 20 Novemba ya kila mwaka. Siku hii inatambulika kama siku rasmi ya kimataifa ya kuwakumbuka waathrika wa ajali hizo na familia zao na kuzitaka nchi wanachama pamoja na jumuiya za kimataifa kuitambua siku hiyo. 
   
  Pia siku hiyo hutoa fursa kwa jamii nzima kukutana na kuwakumbuka wahanga wa ajali za barabarani ,kutafakari madhara, gharama, na hatua zinazoweza kuchukuliwa katika kuzuia ajali zisitokee. Vilevile siku ya kuwakumbuka wahanga wa ajali za barabarani inatoa nafasi kwa wadau kuikumbusha serikali wajibu wake na jamii nzima katika suala la kuzifanya barabara kuwa sehemu salama kwa kila mmoja. 
   
  Hivyo basi mtandao wa wadau kutoka asasi za kiraia unaotetea marekebisho ya sheria na sera ihusuyo usalama barabarani Tanzania kama ambavyo unaratibiwa na Chama cha Wanawake Wanasheria (TAWLA) pamoja na mambo mengine katika kuadhimisha siku hii tunaisihi serikali na watunga sheria kuifanyia maboresho sheria ya Usalama barabarabi ya mwaka 1973 ili iweze kukabiliana ipasavyo na suala la ajali za barabarani pamoja na athari zinazotokana na ajali hizo Maeneo ndani ya sheria ambayo mtandao huu utajielekeza kuona sheria inafanyiwa mabadiliko/maboresho ni pamoja na;
   
  Matumizi ya mikanda; Sheria ya sasa ya Usalama barabarani inasema ni kosa kisheria kwa dereva na abiria anayekaa kiti cha mbele kutokufunga mkanda wakati wa safari lakini sheria hiyo hiyo haisemi chochote kwa abiria wanaokaa kiti cha nyuma.

  Utafiti uliofanywa na Shirika la Afya Duniani (WHO) unasema kuwa iwapo ajali ikitokea madhara/athari kwa abiria wa kiti cha mbele itapungua kwa 50% na kwa abiria wa nyuma madhara yatapungua kwa 70%. Kanuni zilizotungwa na SUMATRA zinataka abiria wote wafunge mkanda ila kwa vile sheria mama (Road Traffic Act of 1973) ipo kimya katika eneo hili utekelezaji wa kanuni unakuwa mgumu. Hivyo basi ni rai yetu sheria hiyo ibadilishwe na kuwataka abiria wote wanaokuwa katika chombo cha usafiri wa kibiashara au binafsi kufunga mkanda wakati wote wa safari. 

  Matumizi sahihi ya kofia ngumu; Sheria ya sasa ya usalama barabarani inasema kuwa ni kosa kwa muendesha pikipiki kutokuvaa kofia ngumu wakati wa kuendesha chombo hicho. Lakini sheria hiyohiyo haisemii chochote kwa abiria anayepanda katika chombo hicho.

  Vilevile pamoja na kuanishisha kosa kwa dereva wa pikipiki kutovaa kofia ngumu lakini pia sheria haielezi ni jinsi gani kofia inatakiwa kuvaliwa na aina maalum ya kofia inayotakiwa kuvaliwa. Kwa mujibu wa Utafiti wa Shirika la Afya Duniani (WHO) unaonyesha kuwa iwapo ajali itatokea madhara yanayotokea kwa kutovaa kofia maalum na kwa usahihi ni makubwa sana ukilinganisha na kofia hiyo ikivaliwa na kwa usahihi.
   
   Hivyo basi ukizingatia kuwa sasa hivi usafiri wa pikipiki umekuwa unatumika kwa kiasi kikubwa (public transport) hivyo ni rai yetu sheria hiyo ifanyiwe maboresho na kuweka kuwa ni sheria kwa mtu yoyote anayepanda pikipiki kuvaa kofia ngumu na kwa usahihi. 

  Matumizi ya vilevi na uendeshaji vyombo vya usafiri: Sheria ya sasa ya usalama barabarani inasema kuwa itakuwa kosa kwa mtu yoyote kuendesha chombo cha moto akiwa na kiwango cha kilevi katika damu yake kinachozidi asilimia 0.08% katika mfumo wa mwili. 
   
  Kiwango hiki ni kikubwa sana kikilinganishwa na tafiti zilizofanywa na Shirika la afya duniani na kupendekeza kiwango asilimia 0.05% kwa dereva aliyebobea (experienced driver) na asilimia 0.02% kwa dereva mchanga (young driver). Hivyo basi ni rai yetu kuwa sheria ifanyiwe marekebisho ili iendane na kiwango cha sasa cha kimataifa kilichofanyiwa utafiti. 

  Mwendo kasi (Speeding): Mwendokasi umeendelea kuwa sababu kubwa ya ajali zinazogharimu uhai wa watu wengi. Sheria yetu inayo mapungufu kadhaa pamoja na juhudi nyingi za Jeshi la Polisi na wadau wengine kutaka kudhibiti jambo hili lemeendelea kuwa tatizo. Adhabu zisiszokidhi wala kuleta hofu kwa maderava wasiotaka kutii zimeendelea kufifisha juhudi za kudhibiti tatizo hili.

  Tunatoa wito kwa watunga sera kutaka kujihulisha zaidi na wadu kuuelimisha umma zaidi katika eneo la uhusiano wa adhabu zitokanazo na makosa ya usalama barabarani na ongezeko la ajali. Pia sheria kufanyiwa maboresho na kuangalia kwa upya mianya iliyopo. Mwakilishi kutoka Chama cha wake Wanasheria Tanzania (TAWLA), Nasieku Kisamby (wa kwanza kushoto) akizungumza katika Siku ya Kimataifa Kuwakumbuka Wahanga wa Ajali za Barabarani inayoadhimishwa kila Novemba 20, 2016. Kutoka kulia ni Gladness Munuo, Jones John na Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), Bi. Eda Sanga. Ofisa Mradi Msaidizi kutoka Tanganyika Law Society (TLS), Mabhezya Rehani akizungumza katika Siku ya Kimataifa Kuwakumbuka Wahanga wa Ajali za Barabarani inayoadhimishwa kila Novemba 20, 2016. Meza kuu ikiwa imesimama kwa dakika mbili kuwakumbuka watu waliopoteza maisha kutokana na ajali katika Siku ya Kimataifa Kuwakumbuka Wahanga wa Ajali za Barabarani inayoadhimishwa kila Novemba 20, 2016. Christina Thomas mkazi wa Kibaha na mmoja wa waathiriwa wa ajali za barabarani akizungumza katika Siku ya Kimataifa Kuwakumbuka Wahanga wa Ajali za Barabarani inayoadhimishwa kila Novemba 20, 2016 iliyofanyika Ofisi za TAMWA jijini Dar es Salaam. Salum Juma Haji (kulia) makazi wa Buguruni jijini Dar es Salaam akizungumza jambo katika Siku ya Kimataifa Kuwakumbuka Wahanga wa Ajali za Barabarani inayoadhimishwa kila Novemba 20, 2016. Mkutano kati ya wanahabari kutoka vyombo mbalimbali vya habari pamoja ya Mtandao wa wadau kutoka asasi za kiraia unaotetea marekebisho ya sheria na sera ihusuyo ukiendelea.

  0 0

  Waziri wa Viwanda na biashara Mhesimiwa Charles Mwijage amewapongeza watengenezaji wa vifaa vya kuhifadhia maji kwa kuendelea kuyaunga mkono malengo ya serikali ya kuanzisha viwanda nchini. 

  Hayo aliyasema katika hafla ya kuitimisha kampeni ya miezi mitatu ya uza SIMTANK na ushinde na kutoa zawadi kwa mawakala wauzaji wa SIMTANK Bi. Fatina Said na Bw. Rama Jurijs ambao walijishia gari kila mmoja iliyofanyika jijini Dar es Salaam. 

  “Nawaomba SILAFRICA waendelee kuibua na kufikia masoko mapya na kutengeneza bidhaa zinazokidhi mahitaji ya wateja wao ikiwa ni pamoja na matumizi ya viwandani na majumbani” alisema Mh. Mwijage. 

  Viwanda vingi vitakavyoanzishwa nchini vitahitaji kwa kiasi kikubwa vifungashio vya bidhaa zake hivyo pamoja na SILAFRICA kuzalisha matangi ya kuhifadhia maji kuna fursa kubwa ya kiwanda hiki kutumia plastiki kuzalisha hivyo vifungashio. Pia Mh. Mwijage aliwataka mawakala wa SIMTANK kuhakikisha wakaazi wa vijijini wanafikiwa na huduma hii ya vifaa vya kutunzia maji vilivyobora ukilinganisha na vile vya asili yaani mitungi inayowezavunjika wakati wowote. 

  Pamoja na hayo waziri aliwaomba SIALFRICA kuanzisha mpango wa elimu ya kukusanya na kuhifadhi maji wakati wa mvua ili kuwaepusha wananchi na usumbufu wa kukosa maji kipindi cha kiangazi. 

  Mkurugenzi mkuu wa SILAFRICA TANZANIA LTD, Bw. Alpesh Patel alimuhakikishia waziri kuwa wako tayari kutoa elimu kwa wananchi juu ya uhifadhi wa maji na kusema kuwa kampeni ya mwaka huu imekuwa na vipengele saba vilivyoshindaniwa hii yote ni kuonyesha jinsi kampuni inavyowajali mawakala wake na wateje wake kwa ujumla. 

  Leo SILAFRICA, tunafurahi kuzawadia magari mawili kwa mawakala wetu walifanya mauzo vizuri katika mwaka huu. Zawadi hizi ni ishara tosha kuwa bidhaa zetu zinaamika kwa watanzania na pia tumetoa zawadi kwa mawakale wengine waliofanya vizui katika mauzo yao” alisema Bw. Alpesh. 

  Ningependa kuwapongeza washindi wa kwanza mwaka huu Bi. Fatina Said na Bw. Jurijs kwa kupata zawadi katika kampeni ya uza SIMUTANK na ushinde ya huu wa 2016. Pia pongezi hizi ziende kwa washinde wengine wote katika siku ya leo na niwatie moyo kuwa tayari kupambana kwaajili ya kampeni ya mwaka kesho. 

  Baadaya kupewa zawadi hiyo Bi. Fatina Said aliishukuru SILAFRICA kwa kutambua mchango wa mawakala wao na kutoa motisha ili kuendelza jitihada zao. Hafla hii imeenda sambamba na udhati wao katika kuwasaidia mamilioni ya watanzania katika lindi zima la ukosefu wa maji. 

  “Kwangu mimi ushindi si muhimu sana bali kuendelea kuwauzi wateja wangu bidhaa ninazoamini ni borana zinazokidhi mahitaji yao. Hivyo SIMTANK ni bidhaa ambayo wateja wetu huamini” alisema Bi. Fatina. 

  Naye Bw. Said” alisema wateja wake wengi huuhitaji huduma ya SIMTANK na hii humfanya ajisikie vizuri na ndiyo sababu toka aanze biashara hajasita  kuuza matanki haya. Ni bidhaa bora na yenye kupendwa hata katika nchi jirani. 

  Chapa ya SIMTANK ilizinduliwa nchini Tanzania miaka 20 iliyopita kwa lengo la kuzalisha bidhaa safi, imara, na salama za kutunzia maji. Kwa sasa imekuwa ikiaminika katika soko kwa sababu ya ubora wa teknolojia na malighafi zinazotumika katika utengenezaji wake. 
  Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage wa pili kulia akimkabidhi funguo za gari mmiliki wa duka la vifaa vya ujenzi la FMJ, Fatima Said baada ya kuibuka mshindi wa mauzo ya bidhaa za tangi la maji aina ya Simtank, kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Simtank, Alpesh Patel na kulia ni mshindi mwengine wa shindano hilo Ramadhani Sakalani
  Mh. Mwijage akisalimiana na mshindi wa gari katika kampeni ya uza SIMTANK na ushinde Bw. Ramadhani Sakalani. Wakitazama kushoto ni Bw. Alpesh Patel na Bi. Fatina Said.
  Bw. Ramadhani Sakalani akionyesha ufunguo wa gari aliloshinda baada ya kukabidhiwa na Mh. waziri.
  Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage wa nne kulia akifafanua jambo mara baada ya kukabidhi funguo za gari kwa mmiliki wa duka la vifaa vya ujenzi la FMJ, Fatima Said baada ya kuibuka mshindi wa mauzo ya bidhaa za tangi la maji aina ya Simtank.
  Picha ya pamoja
  Bi Fatina Said akiongea na waandishi wa habari baada ya kukabidhiwa zawadi ya gari aliyopata kwa kuvuka malengo ya mauzo ya SIMTANK kupitia kampeni ya uzxa na ushinde.
  Waziri wa Viwanda na Biashara Mh. Charles Mwijage akisalimiana na wafanyakazi wa kiwanda cha SILAFRICA baada ya kuwasili katika hafla ya utoaji tuzo kwa washindi wa Uza SIMTANK na ushinde.

  0 0

   Meya wa jiji la Arusha Kalisti Lazaro akizungumza katika Mahafali ya Chuo cha Uandishi wa Habari na Utangazaji  Arusha (AJTC) ,Kulia ni Mkurugenzi wa Mafunzo katika Chuo hicho Joseph Mayagila, kushoto ni Diwani wa kata ya Themi, Melans Kinabo. 
  Wahitimu wa Chuo cha Uandishi wa Habari na Utangazaji  Arusha (AJTC) wakirusha kofia juu ishara ya kuonyesha kutunukiwa vyeti vya Shahada na Stashahada. Picha na Mahmoud Ahmad, Arusha

  0 0

  Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Juma Assad.
  Soko la Mwanjelwa jijini Mbeya 


  Na JamiiMojaBlog,Mbeya 

  MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesanu za serikali(CAG), anatarajia kuanza kufanya kazi ya ukaguzi maalum katika halmashauri ya Jiji la Mbeya baada ya kudaiwa kuwepo kwa viashiria vya ubadhilifu wa fedha zilizotumika kukamilisha ujenzi wa soko la Mwanjelwa.

  Awali, Agosti 9 mwaka huu, Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa akiwa katika ziara yake Mkoani Mbeya, alifanikiwa kutembelea mradi huo wa soko ambao inasemekana umetumia kiasi cha shilingi Bilioni 26, tofauti na matarajio ya serikali.

  Serikali, ilikuwa ikiamini mradi huo utagharimu kiasi cha shilingi bilioni 16 lakini kutokana na utendaji kazi wa hovyo unaodaiwa kufanywa na baadhi ya watendaji tena kwa maslahi yao binafsi ulisababisha soko hilo kutumia kiasi cha shilingi bilioni 26.

  Hatua hiyo ndio iliyomfanya waziri Mkuu, kumuagiza Mkaguzi Mkuu wa Hsabu za serikali kwenda Mbeya na kufanya ukaguzi wa mradi huo ili kuondoa utata uliopo juu ya kiasi sahihi cha fedha kilichotumika kwenye mradi huo.
  Mstahiki Meya wa Jiji la Mbeya, David Mwashilindi 

  Akizungumzia hilo, Mstahiki Meya wa Jiji la Mbeya, David Mwashilindi amesema kuwa baada ya agizo la waziri mkuu kutolewa, halmashauri ilianza mchakato wa kumuita mkaguzi huyo ili kufika kufanya ukaguzi.

  Amesema, kinachofanyika sasa ni kamati ya fedha kuketi kwa ajili ya kupitisha matumizi hayo ya fedha na kazi kuanza kufanyika ikiwa na kutekeleza agizo la Waziri Mkuu. Amesema Kamati ya fedha inataraji kukaa November 22 mwaka huu, na kutoa maamuzi na kupitisha kiasi hicho cha fedha kwa ajili ya kutumika kwa kazi ya mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali ya kufanya ukaguzi wa fedha katika soko la Mwanjelwa.

  Aidha, Meya huyo aliwaomba wafanya biashara wote ambao tayari waliingia mikataba na halmashauri ya Jiji, kuanza kuendesha biashara zao kama makubaliano ya mkataba yanavyoelekeza.Hata hivyo, aliongeza kuwa tayari halmashauri imeingia mkataba na wakala atakayendesha zoezi la kuwaondoa wafanyabiashara wote ambao wamekiuka makubaliano ya mkataba kwa kushindwa kuendesha biashara kwa kipindi husika.

  0 0


  Napenda kuutaarifu umma wa Watanzania kupitia kwenu waandishi wa habari kwamba ni jambo la ajabu na aibu kwa watu makini na wenye kuhitaji mabadiliko ya kweli Kuacha kuunga Mkono juhudi zinazofanywa na serikali ya awamu ya tano chini Uongozi wa Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli bila kusahau utendaji makini wa Waziri Mkuu wake Mhe. Majaliwa Kasim Majaliwa (Mb) pamoja na mawaziri mbalimbali wameonesha kutaka kufuata mwenendo wa Rais Magufuli na Waziri Mkuu wake.

  Mimi Moses Joseph Machali niliyefanya sana siasa za Upinzani hapa nchini na niliyepiga kelele na kupinga siasa za kifisadi zilizoitawala nchi hii; niliyepinga pia ufisadi uliokuwa umeitawala serikali huko nyuma kwa nguvu na uwezo wangu wote nikishirikiana na wapinzani wenzangu, ninaamua kujiunga na watu wanaonesha dhamira safi ya kuiendeleza nchi yetu Tanzania. Watu wenye mwelekeo na dhamira ya kuijenga nchi yetu kwa maendeleo enedelevu ni jamii ya akina Magufuli, Kasim Majaliwa, nk.

  Mwaka mmoja wa Uongozi wa Rais Magufuli na baadhi ya wasaidizi wake kupitia hatua mbalimbali zilizochukuliwa dhidi ya ufisadi uliokuwa umeigubika nchi yetu, inatosha kabisa kwa mtu yeyote makini kufanya uamuzi wa kumuunga mkono au kutokumuunga mkono Rais Magufuli.

  Mimi nimechagua kumuunga Mkono Rais kwa vitendo, kwa sababu ninaposoma Rekodi yangu ya enzi nikiwa Mbunge (Hansard) na kabla ya kuwa mbunge ni kwamba nilipinga mnoo wizi na ufisadi wa kila aina; Nilipinga Matumizi ya fedha serikalini yasiyo ya lazima na yasiyo na tija kwa taifa (Rejeeni hotuba yangu ya Bajeti ya Wizara ya Uchukuzi, nikiwa Waziri Kivuli wa wizara hiyo ya mwaka 2014/2015 na 2015/2016), vilevile bila kusahau hotuba zangu mbalimbali Bungeni na nje ya Bunge.

  Kwa kushirikiana na wapinzania wenzangu enzi hizo tulishauri na kupinga ufisadi wa kila aina, tuliitaka serikali kufanya mambo yenye tija kwa taifa na sasa kila mwenye macho anaona hatua zinazochukuliwa na serikali ya awamu ya tano. Miradi kama ya Ujenzi wa Reli, Ununuzi wa ndege mbili na mipango ya kununua ndege zaidi kama namna ya kulifufua shirikia la ATCL ni mambo tuliyoyahitaji kuyaona wapinzani; sasa yanafanyika. Wale wenye dhamira ya dhati ya kuona nchi yetu ikipiga hatua, kamwe hatuwezi kubeza mambo hayo bali kuyaunga mkono.

  Wale tuliosema na kupiga kelele kwamba Serikali ni dhaifu ktk kuwachukulia hatua watu mbalimbali wenye dhamana serikalini walioonekana kufanya vibaya serikalini ktk nafasi zao, leo tunaona kumekuwepo na kasi nzuri ktk kuwachukulia hatua watu hao. Hata hivyo leo hii upinzani umepiteza mwelekeo kwa sababu unapingana na kile ulichokihubiri nchini.

  Agenda ya kupinga ufisadi siyo ya upinzani tena bali ya JPM na CCM yake au yao. Wapinzani wamegeuka kuwa watu wanaokataa yale waliyoyasimamia na kuyahubiri huko nyuma. Hakika huo siyo uungwana bali aina mpya ya ufisadi nchini na usaliti kwa agenda zao.

  Kama kweli sisi tumekuwa wapinzani na tulioonesha kupinga kwa nguvu zote ufisadi ulioiumiza nchi hii tulimaanisha yale tuliyoyahubiri na kuwaaminisha watu basi tunao wajibu wa kuacha tabia ya kuwa vigeugeu kwa mambo tuliyoyaamini na kuyahubiri. Kutofanya hivyo basi ni mwendelezo wa ufisadi kwa maslahi binafsi.

  Ni nani asiyeona kwamba serikali ya awamu ya tano inafanyia kazi mambo mengi tuliyoyapigia kelele? Au tunajifanya kutokukubali ukweli unaoishi kwa ule msingi wa upinzani wa Tanzania kwamba Tukimuunga mkono Mtawala kamwe hatutapata kuaminiwa na wapiga kura nchini na hivyo tupinge tu hata kama ni ukweli? Nadhani kinachofanyika ni mwendelezo wa kupinga hata mazuri ili kutafuta fursa ya wapinzani kukubalika kisiasa zaidi hata kwa njia na mbinu haramu kama kawaida ya siasa zilizo zoeleka hapa nchini kwa miaka mingi.

  Taifa hili haliwezi kuendelea kwa kuwa na siasa za kutokukubaliana na ukweli unaoishi. Kama dhamira ya kila mtanzania ikiwemo wapinzani ni kuona nchi ina move basi hatuhitaji kuwa watu wa kupingapinga hata yaliyo mema bali kuyaunga mkono yale yaliyo mema bila kujali yanafanywa na nani bali msingi mzuri unapaswa kuwa ukweli kwa kila jambo.

  Serikali ya awamu ya tano imeonesha njia ktk mambo mengi na inastahili kuungwa mkono. Safari ni hatua na ninaamini kwamba hata yale yanayoonekana kutokufanyiwa kazi ndani ya mwaka mmoja uliopita na ambayo yalishindikana huko nyuma, bado yanaweza kuja kufanyiwa kazi huko mbeleni. Serikali ya JPM imejitahidi sana tukilinganisha na huko tuliko toka. Uongozi huu unafanana sana na ule wa akina Hayati EDAWARD MORINGE SOKOINE chini ya hayati Baba wa Taifa Mwl Julius Kambarage Nyerere.

  Daima ninaamini ktk yale ninayoyaamini pasipo kufungwa na ukada bali kuangalia ukweli ni upi. Hata kelele wanazopiga baadhi ya watu kwamba maisha yamekuwa magumu kwa sababu ya Magufuli ni propaganda tu kwa sababu hakuna uhusiano wa maisha magumu na suala la KUDHIBITI wapiga dili wa fedha na mali za umma bali tukubali kwamba wapiga dili waliozoea kupiga dili na kuziingiza fedha walizopiga ktk mzunguko kwamba siyo jambo la msingi ktk kujenga uchumi imara.

  Uchumi imara hauwezi kujengwa kwa kuruhusu ubadhirifu wa fedha na mali za umma au hata za mtu mmoja mmoja. Kinachoonekana hivi sasa ni kama nchi inasukwa upya na hivyo tuwaunge mkono viongozi wa serikali ya awamu ya tano kwa mema wanayoyafanya na kuwashauri kurekebisha ktk yale ambayo hayajakaa vizuri. Tuachane na siasa nyepesi za kutaka kuona kwamba mazuri ni yale yanayofanywa na wapinzani huku mambo hayohayo yakifanywa na CCM yaonekane hayafai na kutajwa kuwa ni ya hovyo. CCM ya JPM siyo ile ya 2015 kurudi nyuma kidogo. Hii ni tofauti na ninaiunga mkono.

  Hivyo basi leo Tarehe 21/11/2016 ninatangaza rasmi kwamba ninajiunga na timu JPM kwa maslahi ya taifa kwa kuwa sioni sababu ya kupingana na yale niliyoyapigania na itakuwa ni sawa na mtu kupigana na kivuli chake mwenyewe. Kwaherini Upinzani nimeamua kuanza siasa mpya za masuala yale niliyoyaamini na ninayoyaamini. Imani ni Matendo Na Matendo ni imani. Piga vita ufisadi kwa imani na Matendo.

  Moses Joseph Machali

  X-mbunge, Kasulu Mjini 2010-2015,

  0 0

  Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) limeziagiza Kampuni ya simu nchini kutekeleza Sheria ya Fedha ya mwaka 2016 inavyotaka kuanza uandikishaji wa umikilikishaji wa asilimia 25 ya hisa zake kwa umma kwa kujiunga na soko la hisa la Dar es Salaam.

  Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mtendaji Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) Bi.Beng’i Issa leo Jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano na waandishi wa habari.Amesema kuwa lengo la mabadiliko hayo ya kisheria katika sekta ya mawasiliano ni kuongeza uwazi katika usimamizi wa Kampuni hizo na kuongeza makusanyo ya kodi kwa Serikali.Bi. Beng’i ameongeza kuwa hatua hiyo itatoa fursa ya kuwawezesha watanzania kiuchumi kuwa wamiliki wa Kampuni hizo kupitia ununuaji wa hisa katika soko la hisa la Dar es Salaam.

  “Kampuni za simu za mikononi hapa nchini zitakiwa kutekeleza mabadiliko haya ya kisheria ndani ya muda wa miezi sita kuanzia Julai Mosi mwaka huu kukamilisha taratibu za kisheria za masoko ya mitaji na hisa kwa kutoa asilimia 25 ya hisa zao na kujiunga na soko la hisa la Dar es salaam ili wananchi waweze kununua hisa kwa ajili ya kuwa sehemu ya wamiliki wa Kampuni hizo hapa nchini” alisisitiza Katibu Mtendaji huyo.

  Aidha Katibu Mtendaji huyo ametoa wito kwa watanzania wote kujiandaa kushiriki kikamilifu katika ununuzi wa hisa za Kampuni hizo za simu mara zitakapokamilisha taratibu za kujiunga na soko la hisa la Dar es Salaam.

  Mbali na hayo Baraza litatoa elimu kwa umma kwa muda wa mwezi mmoja kupitia vyombo mbalimbali vya habari katika kuelimisha na kuhamasisha umma kuhusu fursa hii muhimu kiuchumi na pia wananchi wataelimishwa namna ya kununua hisa,faida za kununua hisa pamoja na athari zake.

  Baraza la Taifa la Uwezeshaji linatoa rai kwa Mashirika ya Hifadhi ya Jamii Nchini kuandaa utaratibu mzuri utakaowawezesha wanachama wao kuweza kushirika katika kununua hisa za Kampuni za si Aidha linafuatilia kwa karibu maendeleo ya utekelezaji wa mabadiliko haya ya kisheria na kuhakikisha utekelezaji wake unafanyika kwa wakati kama ilivyoainishwa katika sheria ya Fedha ya Mwaka 2016.

  Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilipitisha mswada wa Sheria ya Fedha ya Mwaka 2016(The Finance Act, 2016) Juni, 23 mwaka huu ambapo pamoja na mambo mengine lilifanyia mabadiliko sheria ya electroniki na mawasiliano ya posta(Electronic and Postal Communication Act,Cap 306).

  0 0  Wananchi wakimsikiliza Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alipozungumza nao, kusikiliza na kutatua kero zao katika eneo la Keko Dar es Salaam leo, akiwa katika ziara ya kikazi wlayani Temeke. Mh.Paul Makonda yuko kwenye ziara ya siku kumi ya kuijenda upya Dar Es Salaam.PICHA NA BASHIR NKOROMO

  0 0


  Na Humphrey Shao,Globu ya Jamii

  Mwanamuziki mkongwe wa muziki wa Dansi hapa nchini , Ally Choki, anataraji kufanya Tamasha kubwa la kutimiza miaka 30 ya muziki na kuzindua kitabu chake katika ukumbi wa Mango Garden Kinondoni Novemba 26.

  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo,Choki amesema kuwa siku ya Onesho hilo watu watapata fursa ya kujinunulia kitabu hicho kinachozungumzia maisha yake yote ya muziki .

  "Siku hiyo  tutakuwa na wanamuziki wakongwe wengi kama mzee Zahir Ally Zoro , Hamza Kalala na wengine wengi,ambao ni moja ya watu ninao ingia nao kambini kwa ajili ya shoo hii ya aina yake ambayo inandika historia katika muziki wa Dansi hapa nchini"amesema Ally Choki.

  Amemaliza kwa kusema kuwa anawaomba watu watu wajitokeze kwa wingi kwani kingilio ni shilingi 15'000/- kwa kila mmoja .
   Mwanamuziki wa muziki wa Dansi nchini Ally Choki, akionyesha mfano wa kava la kitabu kinachozungumzia maisha yake ya Muziki.
   Mwanamuziki mkongwe Komandoo Hamza Kalala ,akizungumza na waandishi wa habari juu ya maisha ya choki alipokuwa Bantu Group.
   Msemaji wa mwanamuziki,Ally Choki na Mwandishi wa kitabu cha Maisha ya Ally Choki,Juma Kasesa akizungumzia kwa kifupi juu ya kitabu hicho.
  Msemaji wa kinywaji cha Windhoek Lager,Andrea Missana akizungumza na wanahabri juu ya kinywaji hicho kudhamini tamasha hilo la miaka 30 ya Ally Choki.

older | 1 | .... | 1046 | 1047 | (Page 1048) | 1049 | 1050 | .... | 1897 | newer