Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46316 articles
Browse latest View live

HIFADHI YA TAIFA YA MIKUMI YAHOFU KUTOWEKA KWA BAADHI YA WANYAMA ADIMU KUFUATIA WANYAMA WENGI KUGONGWA NA MAGARI

$
0
0
 Waandishi wa habari  wanawake kutoka Mikoa mbalimbali wakimsikiliza Ofisa wa Tanapa Abdallah Choma akiwapa maelezo juu ya hifadhi ya Mikumi
 Mkuu wa hifadhi ya Mikumi Donat Mnyagatwa akiongea na waandishi wa habari wanawake waliofanya ziara katika hifadhi ya mikumi
Baadhi ya vivutio vilivyopo katika hifadhi ya Mikumi

Na Editha Karlo wa blog ya jamii,Mikumi.

HIFADHI ya Taifa ya Mikumi imeelezea hofu yake ya kutoweka kwa baadhi ya wanyama adimu katika hifadhi hiyo kutokana na kasi ya kuuwawa kwa kugongwa na magari ya abiria, binafsi, mizigo yanayopita bara bara ya kutoka dar es salaam na kwenda nyanda za juu kusini iliyopo ndani ya hifadhi hiyo.

Uwepo wa barabara ya lami inayopita katikati hifadhi hiyo na kuongeza kasi ya kugongwa wanyama kila mwaka huku na kutia hofu ya kutoweka kwa baadhi ya wanyama adimu iwapo hatua za haraka hazitachukuliwa.

Hofu hiyo inatokana na takwimu zinazoonyesha kuwa wastani wa mnyama mmoja anagongwa kila siku huku pia zikionyesha kuwa kwa kipindi cha miaka 25 iliyopita hadi kufikia mwaka 2015 wanyama wa aina mbalimbali zaidi ya 3,435 walikufa kwa kugongwa na magari.

Mhifadhi mkuu wa hifadhi ya mikumi , Donat Mnyagatwa wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa habari wanawake waliotembelea hifadhi hiyo kwa lengo la kuitangaza zaidi ikiwa ni sehemu ya ziara ya siku kumi katika hifadhi za taifa za Saadan, Mikumi, Udzungwa na Ruaha mkoani Iringa.

Alisema kuwa kwa mujibu wa takwimu zilizopo wanyama waliogongwa kuazia mwaka 1992 walikuwa 72 idadi ambayo imekuwa ikingezeka kwa kasi kila mwaka ambapo kwa kipindi cha mwaka jana 2015 wanyama wa aina mbalimbali waliogongwa na kufa ni 237.

Hata hivyo Mnyagatwa alitaja takwimu za miaka tisa iliyopita ikianzia na mwaka 2007 waliokufa kwa kugongwa ni wanyama 43, 2008 wanyama 82, 2009 wanyama 45, 2010 wanyama 19, 2011 wanyama 125, 2012 wanyama 111, 2013 132 na mwaka 2014 wanyama 351.

“Hifadhi hii ina ukubwa wa Kilomita za mraba 3230 lakini barabara imepita Km 50 ndani ya hifadhi inaweza kukadiriwa ama kuonekana ni jambo dogo lakini lina athari kubwa mno kwani tunaweza kupoteza baadhi ya aina ya wanyama kutokana na ongezeko la kasi la kufa kwao kutolingana na kasi ya kuzaliana”alisema.

Aidha mhifadhi Mnyagatwa alitaja changamoto nyingine za uwepo barabara hiyo kuwa ni pamoja na hifadhi hiyo kupoteza mamilioni ya fedha kwa kufa wanyama, uchafuzi wa mazingira pamoja na kufanyika utalii wa bure ambao unapoteza mapato mengi ya serikali .

"Ndugu zangu waandishi wa habari tunaomba sana mtusaidie hili suala la changamoto ya barabara hili ni tatizo kubwa hivyo tunaamini kuwa mtasaidia katika hili "alisema Mhifadhi Mkuu huyo.

Alitaja chanagamoto nyingine ni pamoja na ujangili, kuzuka kwa moto, kubadili tabia za wanyama kwani baadhi ya watu wamekuwa wakiwarushia wanyama matunda na vyakula vya binadamu na kuota kwa mazao ya biashara yanayosafirishwa kupitia barabara hiyo yanapomwagika ndani ya hifadhi hiyo.

Alisema kuwa baadhi ya madereva nyakati za usiku wamekuwa wakigiiza kuharibika kwa magari katikati ya hifadhi ili waweze kufanya ujangili .

Akizungumzia kuhusu kutoweka kwa wanyama kipindi cha masika Mhifadhi utalii wa hifadhi ya Mikumi ,Abdalah choma alisema kuwa kipindi kizuri cha kutembelea hifadhi hiyo ni kipindi cha masika ambacho wanyama wengi hujikusanya sehemu moja katika hifadhi hiyo hivyo kutoa fursa kwa watalii kuona wanyama wengi hasa nyakati za asubuhi na jioni.

TANZANIA KUENDELEA KUENDELEA KUSHIRIKIANA NA AFRIKA YA KUSINI KATIKA SEKTA YA UTAMADUNI NA SANAA.

WAZIRI MAHIGA ASAINI MKATABA NA SERIKALI YA CHINA

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga na Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China nchini Tanzania Mhe. Dkt. Lu Youqing wakisaini Mkatababa wa makubaliano ya uwekwaji wa thamani katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam. Tukio hili limefanyika mapema leo Wizarani Jijini Dar es Salaam 
Mazungumzo yakiendelea kabla ya kusaini mkataba 
Mhe. Waziri Mahiga akifafanua jambo kwa Balozi wa China nchini Tanzania Balozi Dkt. Youqing walipokutana Wizarani Jijini Dar es Salaam

NAIBU WAZIRI WA KILIMO, MIFUGO ATEMBELEA MNADA WA MHUNZE WILAYANI KISHAPU

$
0
0
Wafugaji wametakiwa kufuga kwa njia za kisasa kulingana na malisho badala ya kuwa na mifugo mingi huku wakikosa mahali pa kulishia.
Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi, William Tate Ole Nasha alipotembelea mnada uliopo mjini Mhunze wilayani Kishapu mkoani Shinyanga.

Ole Nasha alisema si vyema wafugaji kuwa na mifugo mingi wakati hakuna rasilimali za kufugia kama nyasi ambazo katika maeneo mengi zipo chache hivyo kushindwa kukidhi mahitaji.Alisema pamoja na changamoto hizo Serikali kwa upande wake inaendelea na jitihada za kutatua changamoto hizo zinazowakabili wafugaji hapa nchini.

Aidha, Naibu waziri aliwataka wafanyabishara wa mifugo katika mnada wa Mhunze kujenga utamaduni wa kulipa ushuru wa Serikali badala ya kukwepa.Alisema kitengo cha kutorosha ng’ombe kukwepa kulipa ushuru wa mnada kunaikosesha Serikali mapato hivyo kushindwa kuwapa huduma.     
 Naibu Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi, William Tate Ole Nasha (mwenye Kaunda suti ya bluu) akikagua ng’ombe ndani ya mnada wa Mhunze alipofanya ziara katika wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga.
 Naibu Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi, William Tate Ole Nasha akizungumza na wananchi katika viwanja vya mnadani alipozuru mnada mji mdogo wa mhunzewilayani Kishapu.
 Naibu Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi, William Tate Ole Nasha (wa pili kulia) akifurahia jambo wakati mkutano wa hadhara katika viwanja vya mnadani. Wengine pichani kuanzia kushoto ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Boniphace Butondo, Katibu Tawala Wilaya, Shadrack Kangese na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Stephen Magoiga.
 Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi akiwasikiliza wafugaji na wafanyabiashara wa mifugo katika mnada wa Mhunze.
 Sehemu ya umati wa wananchi wakimsikiliza Naibu Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi, William Tate Ole Nasha (hayupo pichani) wakati akiwahutubia viwanja vya mnadani.
 Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Boniphace Butondo akizungumza katika mkutano huo wa hadhara.
Mkuu wa Idara ya Mifugo Wilaya ya Kishapu, Dk. Alphonce Bagambabyaki (kushoto) akitoa maelezo kuhusu mnada huo kwa ujumbe wa Naibu Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi, William Tate Ole (wa pili kulia). Wengine pichani ni Leonard Basil kutoka Idara ya Uzalishaji na Masoko wizarani na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri, Stephen Magoiga (kulia).

REMEMBRANCE

$
0
0

THE LATE DONAT SAMIKE MASHIKU
Baba, God saw you struggling and no cure in this world was there to make you stay, he then decided to call you that day of 20th November 2013. They were days, weeks, months and now 2 years without you. It is true that you are gone.
Our hearts were hurt but we had no choice, we had to let you go. We miss your smile, your words, and many more that we cannot express .We continue praying for you papa that your heart continue to rest in Eternal Peace.
There will be a holy mass at Changanyikeni Catholic Church on 20th November 2016  and later on we will gather at your home Mapinga for remembrance of your great life teachings.

Our friends and family please join us when commemorating the life of a beloved HUSBAND,DAD,BABU,UNCLE and a BROTHER. 
Blessed are the pure in heart for they will see God."Mathew 5:8"

May your gorgeous soul continue to Rest In eternal Peace. Amen.

JARIDA LA WIZARA YA NISHATI NA MADINI TOLEO NA 146

VODACOM TANZANIA FOUNDATION YAPIGA JEKI HOSPITALI KUU YA MNAZI MMOJA ZANZIBAR LEO

$
0
0
 Baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania,wakiongozana kutoa msaada wa nguo na vyakula mbalimbali kwa wodi ya watoto Njiti kwenye hospitali kuu ya Mnazi Mmoja Zanzibar jana kuelekea matembezi ya kesho kuadhimisha siku ya mtoto njiti duniani yatakayofanyika mjini Zanzibar.
 Muuguzi Mkuu wa hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar, Magreth Sylvester(kushoto)akipokea baadhi ya vyakula mbalimbali  na nguo kwa ajili ya wodi ya watoto njiti hospitalini hapo jana toka kwa Mkuu wa Vodacom Tanzania kanda ya Zanzibar, Mansour Mansour(kulia)wapili kushoto ni Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa kampuni hiyo,Jacquiline Materu na Mwanzilishi wa Mfuko wa kusaidia watoto njiti,Doris Mollel.
 Muuguzi dhamana wa wodi ya watoto njiti katika hospitali kuu ya Mnazi Mmoja Zanzibar,Khadija Mgeni(kushoto)akitoa maelezo kwa Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Jacquiline Materu na Mwanzilishi wa Mfuko wa kusaidia watoto njiti,Doris Mollel ,walipotembelea hospitali hiyo kutoa misaada ya vyakula mbalimbali na nguo jana katika hospitali hiyo. 
aadhi ya wahudumu wa wodi ya watoto njiti wa hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja pamoja na wafanyakazi wa Vodacom Tanzania na Dorris Mollel Foundation wakiwa wamewabeba baadhi ya watoto hao waliopo katika wodi hiyo,wakati walitembelea hospitalini hapo kutoa misaada mbalimbali ya vyakula na nguo.

MJUE MNYAMA TEMBO NA SIFA ZAKE

$
0
0
Tembo wa Asia
Na Pamela Mollel,Mikumi

Tembo ni mnyama kubwa kuliko wote lakini sio mrefu kama twiga,kuna aina mbili ya tembo.tembo w a bara la Afrika na  bara la Asia 

Ukitaka kujua tofauti zao wa bara la Afrika ni wakubwa ,na maskio yao yanamuonekano wa ramani ya bara la afrika lakini tembo bara la Asia wanamasikio madogo na pia wanaweza kufundishwa kulima na michezo mbalimbali

 Akizungumza na waandishi wa habri kuhusu mnyama huyo (Tembo)Afisa wa shirika la Tanapa katika hifadhi ya Mikumi Abdalla Choma alisema kuwa Tembo hao wa  wa bara la Afrika wapo katika makundi mawili,1.     Tembo wa msituni wanameno ambayo  yamenyooka kwaajili ya kuwawezesha kupita katika msitu
2.       Tembo wa Savana, meno yao yamepindapinda wanapenda kuishi katika familia moja wanaweza kuishi kwanzia wawili hadi 45 kwa familia
Alisema Tembo wauwezo mkubwa wa kusikia na wanakumbukumbu ya kutosha
 
Akizungumzia kuhusu uzazi wa tembo mzee Chuma alisema kuwa tembo wanauwezo wa kubeba mimba na kuzaa kwa miezi 18-20
 
Tembo wa bara la Afrika
Tembo huyo hunyonyesha motto wake kwa takribani miaka miwili hadi mitatu na motto wa tembo huyo akishafikisha miaka 15 huesabika ameshakuwa na kutakiwa kuondoka katika familia hiyo na kwenda kujitegemea
 
Tembo huishi kwa miaka 60-75 kwa sasa lakini miaka ya nyumba walikuwa na uwezo wa kuishi miaka 80-120 .“Sababu za kuishi miaka michache kwa miaka hii ni kutokana na mabadiliko ya tabia nchi “alisema mzee Mchoma
 
CHAKULA CHA TEMBO
 
Hupendelea kula matawi ya miti na nyasi za chini,pia hupenda kula kwa masaa 16 kati ya masaa 24,Kiasi cha chakula anachokula ni kati ya 150-300 kg kwa tembo mkubwa na hunywa maji kati ya lita 200 hadi 250

SERIKALI, KAMPUNI YA UJERUMANI WAJADILI ZAIDI UJENZI KIWANDA CHA MBOLEA

$
0
0
 Naibu katibu Mkuu anayeshughulikia Nishati, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo (mbele) akielezea jinsi Serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini ilivyojipanga kutekeleza ujenzi wa Mradi wa Kiwanda cha Mbolea wilayani kilwa. Balozi wa Denmark Nchini, Einar H. Jensen (kulia kwa Dkt. Pallangyo), Ujumbe kutoka Kampuni ya Ferrostaal Industrial GmbH Ujerumani, Viongozi Waandamizi kutoka Wizarani pamoja na Mwakilishi kutoka Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) wakimsikiliza Dkt. Pallangyo.
 Naibu katibu Mkuu anayeshughulikia Nishati, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo (mbele) akiwakilisha kabrasha ya kanuni za bei ya Gesi asilia kwa Balozi wa Denmark Nchini, Einar H. Jensen (mbele) wanaoshuhudia katika picha ni wajumbe kutoka Taasisi za Serikali pamoja na Ujumbe kutoka Kampuni ya Ferrostaal Industrial GmbH kutoka Ujerumani.
 Balozi wa Denmark Nchini, Einar H. Jensen (aliyenyanyua mikono) akielezea mpango wao wa kujenga kiwanda cha mbolea wilayani Kilwa kwa washiriki kutoka upande wa Serikalini (hawapo pichani) wanaoonekana pichani ni Ujumbe kutoka kampuni ya Ferrostaal Industrial GmbH kutoka Ujerumani.
Viongozi Waandamizi kutoka Serikalini wakimsikiliza Meneja wa Biashara ya Gesi (Downstream) kutoka Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Emmanuel Gilbert Simon wakati akielezea jambo katika kikao hicho.

Na Rhoda James.

Serikali ya Tanzania na kampuni ya Ferrostaal Industrial GmbH kutoka Ujerumani wamekutana kwa mara nyingine na kujadili mambo mbalimbali ikiwemo namna ya kutatua changamoto zilizopo katika ujenzi wa Mradi wa kiwanda cha Mbolea wilayani Kilwa Mkoa wa Lindi.

Katika kikao hicho ambacho kimefanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam, na ni mwendelezo wa vikao vya aina hiyo vilivyotangulia, Naibu katibu Mkuu anayeshughulikia Nishati, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo alizitaja changamoto hizo kuwa ni pamoja na upatikanaji wa ardhi na utambuzi wa bei ya kuuza  gesi kwa kiwanda hicho. 

Dkt. Pallangyo alifafanua kuwa, utaratibu wa kupata ardhi kwa ajili ya Mradi huo unaendelea vizuri kwani tayari Wananchi wamepata fidia ili kupisha Mradi huo na kufikia Januari, 2017 Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) watakuwa na hati mpya itakayoruhusu Kampuni ya Ferrostaal kuanza maandalizi ya ujenzi wa kiwanda hicho.

Pamoja na hilo pia Dkt. Pallangyo alisema kuwa bei ya gesi inajadiliwa na wadau mbalimbali ikiwemo Wizara ya Nishati na Madini, Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Mdhibiti wa Mkondo wa Juu wa Shughuli za Mafuta (PURA), Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), wazalishaji wa gesi (Upstreamer) na watumiaji wa gesi (Downstreamer) ili kujua bei halisi ya kuuza gesi hiyo kwa kampuni ya Ferrostaal kwa kuwa inatarajia kutumia gesi katika uzalishaji wa mbolea hiyo.

Kwa upande wake Balozi wa Denmark Nchini , Einar H. Jensen alisema kuwa, ni vema Bodi ya TPDC ikakamilisha utaratibu wa makubaliano ya ubia (Joint Venture Agreement) kati yao na TPDC ili kuharakisha uanzishwaji wa utekelezaji wa mradi huo.

Ujenzi wa Mradi huo wa mbolea utashirikisha Kampuni tatu ambazo ni Ferrostaal Industrial GmbH ya Ujerumani, Fauji Fertilizer ya Pakistani na Haldor Topsoe ya Denmark pamoja na TPDC. Kikao hicho kilishirikisha wawakilishi kutoka Kampuni ya Ferrostaal Industrial GmbH, Viongozi waandamizi kutoka Wizara ya Nishati na Madini pamoja na TPDC.

MAKAMU WA RAIS AMALIZA ZIARA YA SIKU 5 MKOANI MWANZA

$
0
0

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka jiwe la msingi la ufunguzi wa Jengo la Utawala Manispaa ya Ilemela .
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikikabidhi madawati kwa Mbunge wa Nyamagana Mhe. Stanslaus Mabula ambayo yalitolewa na Ofisi ya Bunge ambapo zaidi ya madawati 1074 yalikabidhiwa kwa wilaya ya Nyamagana na Ilemela.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipanda mti wa kumbukumbu mara baada ya kufungua jengo la Manispaa ya Ilemela.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wananchi wa Nyamagana kabla ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa machinjio ya Nyakato.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo ya ujenzi wa machinjio ya Nyamagana kutoka kwa Mhandisi wa jiji la Mwanza Ndugu Ezekiel Kunyalanyala (kushoto) kabla ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa machinjio ya Nyakato.
..............................................................................................


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ametoa muda wa mwezi Mwezi Moja kuanzia leo tarehe 18-Nov-2016 kwa watendaji na viongozi waandamizi wa wilaya ya Ilemela wahamie kwenye wilaya hiyo haraka iwezekanavyo na waache tabia ya kukaa kwenye wilaya nyingine kwa kisingizio cha kukosa nyumba za serikali.

Makamu wa Rais ametoa agizo hilo katika hotuba yake kwa wananachi na watendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela waliojitokeza katika hafla ya uzinduzi jengo la utawala la Manispaa hiyo na kukabidhi madawati 1,074 yaliyotolewa na ofisi ya Bunge.

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ameonyesha kukerwa na tabia hiyo na amewataka viongozi hao wahamie karibu na maeneo yao ya kazi kabla ya muda aliotoa kwisha ili waweze kuwa karibu na wananchi katika kuwasaidia kutatua kero na matatizo yanayowakabili kwa haraka.
Akiwa katika wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza wakati anaweka jiwe la msingi katika mradi wa ukarabati wa mchinjio ya Nyakato jijini Mwanza, Makamu wa Rais ameuagiza uongozi jiji la Mwanza kusimamia kikamilifu mradi wa ukarabati wa machinjio ya Nyakato na watendaji watakaobainika kuhujumu mradi ambao utagharimu zaidi ya shilingi bilioni Tatu wachukuliwe hatua kali za kisheria.

Makamu wa Rais ametoa kauli hiyo katika hotuba yake kwa wananchi na watendaji wa jiji la Mwanza waliohudhuria hafla ya uwekaji jiwe la msingi katika mradi wa ukarabati wa machinjio ya Nyakato unaohusisha uboreshaji wa jengo la machinjio,tanki la kuhifadhi maji,ujenzi wa vyumba vya baridi vya kuhifadhi nyama na ujenzi wa mtambo wa kutibu majitaka yanayotoka kwenye machinjio hiyo.

Makamu wa Rais katika hotuba yake, amesema hategemei hata kidogo ukarabati wa machinjio hiyo ufanyike chini ya kiwango kwa sababu ni mradi wa kibiashara ambao ukikamilika na kuanza kufanya kazi utasaidia jiji la Mwanza kupata mapato yatakayosaidia utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya wananchi.

Makamu wa Rais pia amemwagiza Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella ahakikishe anasimamia uundaji wa menejimenti ya machinjio hiyo ambayo itafanya kazi vizuri na sio kuingiza watu ambao hawana uwezo ambao watakwamisha utendaji kazi wa machinjio hiyo.

Kuhusu ukusanyaji wa kodi, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amewahimiza watendaji wa Halmashauri zote za mkoa wa Mwanza waongeze kasi ya ukusanyaji wa mapato ya serikali kwa njia ya kielekroniki kutoka kwenye vyanzo mbalimbali fedha ambazo zitasaidia utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya wananchi mkoani humo.

Makamu wa Rais pia ametoa wito maalum kwa wananchi nchini wahakikishe wanadai risiti wanaponunua bidhaa mbalimbali kwani kufanya hiyo watasaidia kuongeza mapato yake ambao yataelekezwa kwenye miradi ya maendeleo.

Katika Mkutano wake wa Majumuisho ya ziara yake ya kikazi ya Siku Tano mkoani Mwanza na viongozi wa mkoa wa Mwanza, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amewasisitiza viongozi na watendaji wa mkoa wa Mwanza wafanye kazi kwa bidii katika kuwatumikia wananchi kwa kuzingatia kanuni na taratibu za umma.

Ameonya kuwa serikali ya awamu ya Tano haitasika kuwachukulia hatua kali viongozi na watendaji ambao watakwenda kinyume na maadili ya utumishi wa umma kwenye maeneo yao ya kazi.Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amewataka viongozi wa mkoa wa Mwanza kusimamia kikamilifu katika kulinda hali ya amani na Utulivu na wachukue hatua kali kwa watu wanaotaka kuharibu amani ya nchi.

Makamu wa Rais amehitimisha ziara yake ya kikazi ya siku Tano mkoani Mwanza kwa kukagua,kuzindua na kuweka mawe ya msingi katika miradi ya mbalimbali ya maendeleo katika wilaya za Ilemela,Misungwi, Kwimba, Magu na Nyamagana.
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

MAJALIWA ASALI SALA YA IJUMAA MSIKITI WA KICHANGANI MAGOMENI NA KUZUNGUMZA

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza baada ya sala ya Ijumaa kwenye Msikiti wa Kichangani, Magomeni jijini Dar es salaam Novemba 18, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

TANZANIA KUENDELEA KUSIMAMIA HISTORIA YA UKOMBOZI WA BARA LA AFRIKA

$
0
0
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Moses Nnauye (kulia) akieleza jambo kwa Waziri wa Sanaa na Utamaduni wa   Afrika ya Kusini Ndg. Nathi Mthehwa(kushoto) ambaye yupo nchini kwa ziara ya kikazi kwa siku tatu yenye lengo la kuimarisha ushirikiano baina ya nchi hizo kupitia Sanaa na Utamaduni ikiwemo kuhifadhi historia ya ukombozi wa Afrika ya Kusini leo Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Prof.Elisante Ole Gabriel (kulia) akisalimiana na Waziri wa Sanaa na Utamaduni wa Afrika ya Kusini Ndg.Nathi Mthehwa (Kushoto) leo Jijini Dar es Salaam alipotembelea Wizara hiyo kwa ajili ya mazungumzo ya kuimarisha uhusiano baina ya nchi hizo katika sekta za Sanaa na Utamaduni, katikati ni Balozi wa Afrika ya Kusini Nchini  Thamsanga Dennis Mseleku.
Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Nape Moses Nnauye  akiongea na waandishi wa habari (hawapo katika Picha) leo Jijini Dar es Salaam kuhusu ziara ya Waziri wa Sanaa na Utamaduni wa Afrika ya Kusini Ndg. Nathi Mthehwa  ambaye yupo nchini kwa siku tatu kwa lengo la kuimarisha ushirikiano baina ya nchi hizo kupitia sekta ya Sanaa na Utamaduni ikiwemo kuhifadhi historia ya ukombozi wa Afrika ya Kusini.
Waziri wa Sanaa na Utamaduni wa   Afrika ya Kusini Ndg. Nathi Mthehwa (kulia) akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu ziara yake ya siku tatu nchini leo Jijini Dar es Salaam (kushoto) ni Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Moses Nnauye . 
Mshauri Mtaalamu wa Urithi wa Utamaduni Dkt.Daniel Ndagala akichangia hoja  wakati wa kikao baina ya Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Moses Nnauye na Waziri wa Sanaa na Utamaduni wa   Afrika ya Kusini Ndg. Nathi Mthehwa leo Jijini Dar es Salaam.
Wajumbe kutoka Tanzania na Afrika ya Kusini wakifuatilia kwa makini mazungumzo baina ya Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Moses Nnauye na Waziri wa Sanaa na Utamaduni wa   Afrika ya Kusini Ndg. Nathi Mthehwa  katika mkutano wao na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam katika Ukumbi wa Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo.
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Moses Nnauye (wanne kushoto)na Waziri wa Sanaa na Utamaduni wa Afrika ya Kusini Ndg.Nathi Mthehwa(wa tatu kutoka kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe kutoka Tanzania na Afrika ya Kusini baada ya kumaliza kwa kikao leo Jijini Dar es Salaam.Picha Na Lorietha Laurence – WHSUM


Na Genofeva Matemu - WHSUM.

Serikali ya Tanzania itaendelea kuweka historia ya Ukombozi wa Bara la Afrika kwa kuhifadhi kumbukumbu zote huku ikitunza na kuweka alama maeneo ambayo yalitumika wakati wa kupigania Uhuru wa Bara la Afrika na kutunza makaburi ya wapigania uhuru hao pamoja na kuyafanya kuwa ya kihistoria.

Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye alipokutana na Waziri wa Utamaduni na Sanaa wa Afrika ya Kusini Mhe.Nathi Mthehwa aliyeko nchini kwa ziara ya siku tatu kwa lengo la kuimarisha uhusiano wa nchi hizo mbili katika sekta ya Utamaduni na Sanaa.

 “Tumeanza kuandika historia ya Ukombozi wa Bara la Afrika kwa kuhoji baadhi ya wanaharakati walioshiriki katika kuwasaidia wapigania uhuru kuanzisha vyama vyao vya ukombozi ambapo historia hii itahifadhiwa kwa njia ya sauti na picha lakini pia tutaendelea kutunza kumbukumbu zote tutakazozipata na kuwekea alama maeneo ambayo yalitumika wakati wa kupigania uhuru” amesema Mhe. Nnauye

Aidha, Mhe. Nnauye amesema kuwa makubaliano yaliyosainiwa mwaka 2011 kati ya Tanzania na Afrika ya Kusini kufuta Visa ya kusafiria kati ya nchi hizo mbili yameleta  mabadiliko makubwa katika eneo la Sanaa nchini kwani wasanii wamekua wakitumia fursa hiyo kwenda Afrika ya Kusini kuandaa kazi zao na kuzifanya kuwa na ubora zaidi.

Kwa upande wake Waziri wa Utamaduni na Sanaa wa Afrika Kusini Mhe. Nathi Mthehwa ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa kuendeleza ushirikiano uliopo baina ya nchi hizo mbili na kuthamini mchango uliofanywa na Tanzania katika kukomboa nchi ya Afrika ya Kusini.

Pamoja na hayo Mhe. Mthethwa ameahidi kuendeleza ushirikiano ulipo na kuthamini maendeleo yaliyopo kwenye maeneo ya Utamaduni na Sanaa kwa kuhakikisha kuwa mafanikio ya Sekta za Ubunifu ndani ya Afrika ya Kusini yanakua sehemu ya mafanikio ndani ya nchi ya Tanzania.

Ziara hii inaangalia namna nchi hizi mbili zinaweza kuimarisha makubaliano ya mwaka 2011, katika maeneo mengine ya mashirikiano kama vile upande wa tasnia ya filamu ambapo Afrika ya Kusini imekua ikifanya vizuri ikiwemo kusimamia haki za wasanii kwa kutengeneza mifumo ya kisheria ya kulinda haki za ubunifu na kuongeza mahusiano ya  nchi hizo mbili.

Waziri huyo  atatembelea Mkoa wa Morogoro kwenye kambi ya wapigania Uhuru wa Afrika ya Kusini Mazimbu, Dakawa pamoja na Bagamoyo ambapo kulikua na kambi yao,pamoja na baadhi ya maeneo Jijini Dar es Salaam.

MAJALIWA ATEMBELEA MRADI WA UJENZI WA NYUMBA MAGOMENI KOTA

$
0
0
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mshauri wa Wakala ya Majengo Tanzania (TBA), Edwin Nnuduma  kuhusu Mradi wa Ujenzi wa Nyumba, Magomeni Kota jijini Dar es salaam wakati alipotembelea mradi huo Novemba 18, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mshauri wa Wakala ya Majengo Tanzania (TBA), Edwin Nnuduma  kuhusu Mradi wa Ujenzi wa Nyumba, Magomeni Kota jijini Dar es salaam wakati alipotembelea mradi huo Novemba 18, 2016. Wapili kulia ni Mkuu wa wilaya ya Kinondoni, Ally  Happy.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipokagua Mradi wa Ujenzi wa Nyumba, Magomeni Kota jijini Dar es salaam Novemba 18, 2016.  Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Happy. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na wajenzi wakati alipotembelea Mradi wa Ujenzi wa Nyumba, Magomeni Kota jijini Dar es salaam kukagua mendeleo ya mradi huo Novemba 18, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

WAKAZI WA MWENGE MSHINDO WA MUOMBA RAIS AWASAIDIE WAWEZE KULIPWA STAHIKI ZAO

$
0
0
Baadhi ya wananchi wa kata ya MWENGEMSHINDO Manispaa ya SONGEA mkoani RUVUMA ambao maeneo yao yamechukuliwa na MAMLAKA ya Ukanda Maalumu wa Uwekezaji nchini (EPZA) kwa kipindi cha miaka tisa iliyopita bila kuwalipa fidia yoyote, wamemuomba rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania DOKTA JOHN POMBE MAGUFULI kuingilia kati suala hilo ili waweze kupata haki yao.story kamili bonyeza hiyo video. 

TAARIFA KUTOKA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF

$
0
0
YAHYA HAMAD KAIMU MWENYEKITI KAMATI YA SAA 72 YA TFF 

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), kunashukuru wanafamilia wa soka kwa salamu mbalimbali za rambirambi kutokana na msiba wa Mwenyekiti wa Azam FC na Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Kuu, Sheikh Said Muhammad aliyefariki dunia Novemba 7, 2016 katika Hospitali ya Aga Khan, Dar es Salaam.

Hayati Sheikh Said Muhammad kualikuwa hazina katika mpira wa miguu nchini kutokana na uwezo wake mkubwa wa kutoa mchango ya mawazo na miongozo katika Kamati ya Utendaji ya TFF. 

Itakumbukwa kwamba Sheikh Muhammad aliongoza Klabu ya Azam kwa mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kubeba ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara na Kombe la Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kagame Cup) kwa mara ya kwanza tangu klabu hiyo ianzishwe.

Kutokana na kufariki kwa Sheikh Muhammed, Rais wa TFF, Jamal Malinzi amempendekeza Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi, Bwana Yahya Hamad - kukaimu nafasi ya Mwenyekiti wa Kamati ya Uendeshaji Ligi (Kamati ya Saa 72) ili kushughulia masuala yote ya mechi zilizochezwa tangu mwanzo wa Novemba, 2016 baada ya kifo cha Sheikh Muhammad.

Tunachukua nafasi hii kutoa wito kwa klabu kumpa ushirikiano Bwana Hamad katika majukumu yake mapya akiongoza kamati hiyo yenye wajumbe ambao ni Baruan Muhuza (Azam Tv), Boniface Wambura (Mtendaji Mkuu Bodi ya Ligi), Jonas Kiwia (Kaimu Mkurugenzi wa Mashindano TFF), Philemon Ntahilaja (Mdau wa Mpira wa Miguu), Charles Ndagala (Katibu Kamati ya Waamuzi ya TFF), Kanali Mstaafu wa JWTZ, Isaron Chacha na Steven Mnguto ambaye ni Mjumbe wa Bodi ya ligi. 


KUMEKUCHA AZAM SPORTS FEDERATION CUP

Azam Sports Federation Cup (ASFC) itakayoshirikisha timu 86 msimu huu, itaanza rasmi kesho Novemba 19, 2016 kwa uzinduzi rasmi utakaofanyika mkoani Tanga kwa kuzikutanisha Bingwa wa Mkoa wa Tanga, Muheza United na Sifa Politan ya Temeke, Dar es Salaam kwenye  Uwanja wa Mkwakwani jijini humo.

Siku hiyo kabla ya mchezo kutakuwa na shamrashamra kupamba michuano hiyo ambako wachezaji wa zamani wa Coastal Union na African Sports za Tanga zitachuana kabla ya kuanza kwa mchezo huo wa uzinduzi. Timu hizo za maveterani, zitachezwa kuanzia saa 8.00 mchana.

Pia kutakuwa na shamrashamra za wasanii walioandaliwa na Wadhamini Azam Tv ambayo kwa msimu wa 2016/17 zimeongezwa timu 22 kutoka mabingwa wa mikoa-- Muheza na Sifa Politan ni miongoni mwa timu hizo. Ongezeko hilo tofauti na msimu uliopita ambako kulikuwa na timu 64.

Mwaka huu kuna timu 16 za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL); timu zote 24 za Ligi Daraja la Kwanza (FDL), timu zote 24 za Daraja la Pili (SDL) na timu 22 za mabingwa wa mikoa. Mashindano hayo yatakuwa ni ya mtoani na yataendeshwa kwa raundi tisa (9).

Raundi ya Kwanza itashirikisha timu zote 22 za Mabingwa wa Mikoa katika makundi manne ya timu sita na timu tano ambako timu mbili za juu zitaingia raundi ya pili.Raundi ya Pili itashirikisha timu nane zilizofuzu za RCL katika raundi ya kwanza na kujumlisha timu 24 za Daraja la Pili (SDL) kufanya jumla ya timu zote kuwa 32 kwa hatua ya pili.

Raundi ya Tatu itashirikisha timu 16 zilizofuzu hatua ya pili kushindana ili kupata timu nane zitakazoingia hatua ya nne.Raundi ya Nne itashirikisha timu zote za Daraja la Kwanza (24) na kumulisha timu nane (8) zilizoshinda Raundi ya Tatu (3) kufanya timu zote kuwa 32.

Raundi ya Tano, itashirikisha timu 16 zilizofuzu Raundi ya Nne (4) na kumuisha timu zote 16 zinazoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara na kufanya timu zote katika raundi hii kuwa 32.Raundi ya Sita itashirikisha timu zote 16 zilizofuzu katika Raundi ya Tano na mzunguko huo utaitwa Hatua ya 16 Bora.

Raundi ya Saba (7) itashirikisha timu nane zilizofuzu katika raundi ya sita na mzunguko huo kutambuliwa kuwa Nane Bora au Hatua ya Robo fainali .Raundi ya Nane ambayo itashirikisha timu nne zilizofuzu Raundi ya Saba (Robo Fainali) na mzunguko huo utatambuliwa kuwa ni Nusu Fainali.

Raundi ya Tisa itashirikisha timu mbili zilizofuzu Raundi ya Nane na washindi hao wa Nusu Fainali na kumpata Bingwa wa Azam Sport Federation Cup kwa msimu wa 2016/2017.

………………..…………………………………………………………………………….
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA

KIKAO CHA USHIRIKIANO NA MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI BAINA YA WIZARA YA AFYA MAENDELEO YA JAMII JINSIA WAZEE NA WATOTO

$
0
0
Wakili Nyinula Watson Mwakyusa kushoto toka TAWLA na Msajili wa NGOs kutoka Wizara ya Afya, Mendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wakiendesha kikao cha ushirikiano baina ya NGOs na Wizara hiyo.
Wadau mbalimbali kutoka Mashirika yasiyo ya Kiserikali wakipitia nyaraka mbalimbali wakati wa Mkutano wa Ushirikiano baina ya Wizara ya Afya, Jinsia, Wazee na Watoto na Mashirika yasiyo ya kiserikali leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Washiriki kutoka moja ya Mashirika yasiyo ya Kiserikali wakifuatilia jambo kwa makini wakati wa Mkutano wa Ushirikiano baina ya Wizara ya Afya, Jinsia, Wazee na Watoto na Mashirika yasiyo ya kiserikali leo jijini Dar es Salaam.

MAKAMBA AONGOZA UJUMBE WA TANZANIA KATIKA MKUTANO WA 22 WA DUNIA WA MABADILIKO YA TABIANCHI,

$
0
0
 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. January Makamba (Kulia) akiongoza ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa 22 wa Dunia wa Mabadiliko ya Tabianchi, huko Maracckech - Morocco. Kushoto ni Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Mbarak Abdulwakil.


UFUNDI WA VETA WAHITAJIKA KATIKA UCHUMI WA VIWANDA –SABUNI

$
0
0
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa VETA , Geoffrey Sabuni akizungumza katika mahafali ya 46 katika Chuo cha VETA, Chang’ombe  leo jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Chuo cha VETA, Chang’ombe, Douglas Kipokola  akitoa maelezo katika mahafali ya 46 ya chuo hicho leo jijni Dar es Salaam.
 Wahitimu wakiimba shairi kwa mgeni rasmi (hayupo pichani) katika Mahafali ya 46 ya Chuo cha VETA, Chang’ombe leo jijini Dar es Salaam.
 Sehemu ya wahitimu wakati wa Mahafali ya 46 ya Chuo cha VETA, Chang’ombe leo jijini Dar es Salaam.
 Sehemu ya wazazi  katika Mahafali ya 46 ya Chuo cha VETA, Chang’ombe leo jijini Dar es Salaam.
 Kaimu Mkurugenzi Mkuu VETA , Geoffrey Sabuni akitoa cheti kwa mmoja wa wahitimu katika Mahafali ya 46 ya Chuo cha VETA, Chang’ombe leo jijini Dar es Salaam


Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.

NCHI inakwenda katika uchumi wa viwanda ambavyo vinahitaji wataalam  mbalimbali  katika kuweza kufikia  uchumi huo kwa kuhitaji wataalam wanaozalishwa nchini wakiwemo wahitimu wa mafunzo stadi yanayotolewa  na vyuo vya VETA.

Hayo ameyasema leo Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mafunzo na Ufundi Stadi (VETA), Geoffrey Sabuni wakati wa mahafali ya 46 katika Chuo cha VETA,  Changombe Dar es Salaam, amesema VETA inazalisha wataalam ambao wamebobea kwa ujuzi.

Amesema wahitimu wa VETA hawatafuti ajira kutokana na kuwa ujuzi wanaoupata  unawawezesha  kujiajiri au kuajiriwa kwa kutafutwa na wamekuwa wakifanya vizuri katika maeneo walioajiriwa na kujiajiri.

Sabuni amesema wanaosoma VETA  wapo waliohitimu kidato nne hadi  waliopata shahada ya kwanza hivyo jamii iondoe dhana  ya kwamba wanaosoma VETA ni wale walioshindwa kufanya vizuri katika shule za sekondari na msingi.

Aidha amewataka wahitimu wanaozalishwa na vyuo hivyo kuwa na  weledi  katika kufanya kazi na kuondokana kuwaibia waajiri hali ambayo itafanya baadhi yao kupoteza sifa ya kujiajiri au kuajiliwa.

Nae Mkuu wa Chuo cha  VETA Changombe, Douglas Kipokola amesema kuwa wahitimu mwaka huu  wako 423 katika fani mbalimbali na kwamba wapo tayari katika soko la ajira kutokana na mafunzo walioyapata.

Amesema kuna changamoto za  walimu ambapo wameshaanza kulifanyia kazi kutokana na mitaala inahitaji mafunzo yenye tija  kwa uwiano wa mwalimu mmoja  kwa wanafunzi wasiozidi 20.

PRIDE Tanzania Yatoa Misaada kwa Wateja Wake Walioathirika na Tetemeko la Ardhi Bukoba

$
0
0
PRIDE (Promotion of Rural Initiative and Development Enterprise)ni shirika lisilo la kiserikali (NGO) linalotoa huduma za kifedha kwa masharti nafuu kwa wafanyabiashara ndogondogo na wa kati. Huduma hizo zina lengo la kuchangia pato la taifa na kuondoa umasikini nchini. 

PRIDE ilisajiliwa mnamo Mei 1993 chini ya wadhamini wasio na hisa (Company Limited by guarantee, not Having Share Capital) kulingana na Sheria ya Makampuni Cap, 212 ya mwaka 2012.na kuanza rasmi shughuli zake mwaka 1994 mjini Arusha.Kwa sasa Shirika lina matawi 85 yalioenea nchi nzima.

Tangu kuanzishwa, PRIDE imeweza kukopesha wajasiliamali mbalimbali nchini wapatao 1,700,000 nakutoa mikopo yenye thamani ya shilingi bilioni miatisa (bil. 900.0).

Katika kuungana naWatanzania, PRIDE Tanzania walitoa misaada mbalimbali moja kwa moja kwa wateja wao wa tawi la Bukoba ambao waliathirika na tetemeko la ardhi lililotokea Mkoani Kagera.Msaada huu ulilenga kuwawezesha wateja wa PRIDE kukarabati makazi yao. 

Vilevile PRIDE ilichangia katika mfuko wa maafa wa serikali kwa kutoa mifuko ya saruji na mabati.

Mtejawa PRIDE Tanzania,Tawi la Bukoba, Bw. Revocatus Siliden akifurahia msaada wa mifuko ya saruji aliyopewa kwa ajili ya kumsaidia katika ujenzi wa nyumba ya ke iliyoharibika baada ya kutokea tetemeko la ardhi Mkoani Kagera.
pr2
Mteja wa PRIDE Tanzania, tawi la Bukoba, Bw. Revocatus Siliden akionyesha madhara aliyoyapata kwenye nyumba yake baada ya kutokea tetemeko la ardhi huko Mkoani Kagera.
pr3
Afisa wa PRIDE Tanzania, Ndugu Samson Tenga akimkabidhi Mteja wa PRIDE Tanzania, Tawi la Bukoba mifuko ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa nyumba yake ambayo ilibomoka kutokana na janga la tetemeko la ardhi lililotokea Mkoani Kagera.
pr4
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Mstaafu Salum Kijuu akifurahia jambo na mmoja wa wawakilishi wa wateja wa PRIDE Tanzania, tawi la BukobaBi. Mariam Seleman ambae pia ni muathirika wa tetemeko la ardhi lililotokea Mkoani Kagera.
pr5
Diwani wa Kata ya Miembeni, Manispaa ya Bukoba, Mkoa wa Kagera (Shati la Kijani) Bw. Richard Gaspar pamoja na maafisa wa PRIDE Tanzania wakimkabidhi mifuko ya saruji mteja wa PRIDE, ambaye nyumba yake iliathirika na tetemeko la ardhi lililotokea Bukoba.
pr6
Meneja wa Kanda ya Ziwa, Bi. Hilda Nsombo akikabidhi kwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Mstaafu SalumKijuu msaada wa mabati na mifuko ya saruji kwa ajili ya waathirika wa tetemeko la ardhi lililotokea Mkoani Kagera.
pr7
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Mstaafu SalumKijuu akimshukuru Meneja wa PRIDE Tanzania, tawi la Bukoba Bi. Digna Tarimo baada ya kupokea msaada wa mabati na mifuko ya saruji kwa ajili ya waathirika wa tetemeko la ardhi lililotokea Mkoani Kagera.
pr8
Mmoja wa wateja wa PRIDE Tanzania, tawi la Bukoba, Bw. Audax John akionyesha nyumba yake jinsi ilivyoathirika na tetemeko la ardhi lililotokea Mkoani Kagera.
pr9
Nyumba ya Bi.Dorosta Pastory mmoja wa wateja wa PRIDE Tanzania walionufaika na msaada wa saruji uliotolewa na PRIDE ikionekana upande wa nyuma baada ya ukuta wake kuanguka kutokana na tetemeko la ardhi lililotokea Mkoani Kagera.
pr10
Moja ya nyumba za wateja wa PRIDE Tanzania, tawi la Bukoba walionufaika na msaada wa saruji uliotolewa na PRIDE ikionekana upande wa mbele baada ya ukuta kuanguka kutokana natetemeko la ardhi lililotokea Mkoani Kagera.
pr11
Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Brigedia Mstaafu Salum Kijuu akimshukuru Meneja wa PRIDE Tanzania, Kanda ya Ziwa, Bi. Hilda Nsombo baada ya zoezi la upokeaji wa misaada ya waathirika wa tetemeko la ardhi lililotokea Mkoani Kagera. Wengine ni Meneja wa PRIDEtawi la Bukoba, Afisa wa PRIDEtawi la Bukoba pamoja na viongozi wa wateja wa PRIDE tawi la Bukoba.

VIJUSO VYA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI NOV 19

Viewing all 46316 articles
Browse latest View live




Latest Images