Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46395 articles
Browse latest View live

SHIRIKA LA BIMA LA TAIFA (NIC) LANG'ARA MAONYESHO YA WADAU WA BIMA DAR

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) Sam Kamanga (kushoto) akisisitiza jambo wakati wa maonyesho ya wadau wa bima yaliyoandaliwa na Taasisi ya Bima Tanzania (IIT) yanayofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam, wa pili kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya bima ya Mgen Charles Sumbwe , Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Bima ya G A Tanzania, Amit Srivastavr na Mkurugenzi Mtendaji wa kamapuni ya Bima ya Maxinsure, Bhaskar Nair. 
Mmoja wa wananchi aliyefika kwenye manesho ya wadau wa bima Gudumo Gaironga(kushoto) akimsikiliza kwa makini Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) Sam Kamanga (kulia) alipokuwa akimfafanulia jambo wakati wa maonyesho ya wadau wa bima yaliyoandaliwa na Taasisi ya Bima Tanzania (IIT) yanayofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. 
Kamishina wa wa Bima Tanzania Ezraell Kamuzora (kulia) akiwapongeza wafanyakazi wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wao Sam Kamanga (kushoto) wakati alipotembelea banda lao lililopo kwenye maonyesho ya wadau wa bima yaliyoandaliwa na Taasisi ya Bima Tanzania (IIT) yanayofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) Sam Kamanga akimpongeza mwanafunzi wa mwaka wa tatu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) anayesoma kozi ya maswala ya bima Baraka Dinis kwa kujitolea kutoa damu kwa ajili ya kuchangaia Mpango wa Taifa wa Damu salama kwenye maonyesho ya wadau wa bima yaliyoandaliwa na Taasisi ya Bima Tanzania (IIT) yanayofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Masoko na Huduma kwa Wateja wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) Elisante Maleko.

TAASISI YA DORIS MOLELL FOUNDATION YAANDAA MATEMBEZI KUKABILIANA NA VIFO VYA WATOTO NJITI

$
0
0
Na Bakari Madjeshi,Globu ya Jamii

Katika kuhakikisha kuwa vifo vya Watoto Njiti vinapungua hapa nchini,Taasisi ya Doris Mollel Foundation imeandaa Matembezi ya Hisani ili kukabiliana na vifo vya watoto hao kupungua.

Matembezi hayo yenye kauli mbiu ya "Okoa Maisha ya Mtoto Njiti" yatafanyika Visiwani Zanzibar kutokana na Wanawake wengi visiwani humo kukabiliwa kwa asilimia kubwa na suala hilo la Watoto kuzaliwa Njiti.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, Mwanzilishi wa Taasisi hiyo, Doris Mollel amesema kuwa Watoto wengi wanakufa kutokana na kushindwa kupumua wenyewe, hivyo wao kama Taasisi imewasukuma kusaidia suala hilo.

Dorice ametoa  shukrani kwa Wadhamini waliojitolea kuasaidia kukabiliana na suala hilo ikiwa ikiwa ni Vodacom Foundation Tanzania, GSM Foundation, Clouds Media Group na UTT AIMS, Michuzi Media Group na wengine wengi.

Pia ametoa shukrani kwa Viongozi wa Serikali kama Mhe. Angela Kairuki, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda pamoja na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Wizara za Afya Tanzania Bara na Visiwani.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Vodacom Tanzania, kupitia kwa Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano na Mwasiliano, Jacquiline Materu amesema wameamua kudhamini Kampeni hiyo ikiwa ni fursa nzuri kuondoa vifo vya Mama na Mtoto.

Naye Afisa Mwandamizi Masoko na Uhusiano wa UTT AMIS amesema wanashirikiana Doris Mollel Foundation toka mwaka Jana amesema watasaidia Kampeni hiyo ya Okoa Mtoto Njiti kuhakikisha wanapunguza vifo vya akina mama na Mtoto.
 Muanzilishi wa Taasisi ya Dorice Mollel, Dorice Mollel akizungumza na waandishi wa habari kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Serena jijini Dar es salaam leo Novemba 16, 2016 juu ya matembezi ya hisani ya kuadhimisha Kilele cha Siku ya Mtoto Njiti Duniani, yanayotarajiwa kufanyika Novemba 19, 2016 Mjini Unguja Visiwani Zanzibar, ambapo Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mama Asha Balozi ndie anaetarajiwa kuyaongoza matezi hayo. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Jacqueline Materu na kushoto ni Afisa Mwandamizi wa Masoko na Uhusiano - UTT AMIS, Martha Mashiku.
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Jacqueline Materu akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) katika mkutano uliofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Serena jijini Dar es salaam leo Novemba 16, 2016, juu ya matembezi ya hiari yaliyodhaminiwa na Vodacom Tanzania Foundation kwa ajili ya watoto njiti yanayotarajiwa kufanyika Mjini Unguja, Zanzibar mwishoni mwa wiki hii. Kulia ni Muanzilishi wa Taasisi ya Dorice Mollel, Dorice Mollel.
Afisa Mwandamizi wa Masoko na Uhusiano - UTT AMIS, Martha Mashiku (kulia) akielezea namna walivyoshirikiana na Taasisi ya Dorice Mollel Foundation katika kufanikisha matembezi hayo.

RC Galawa ahimiza wafanyabiashara kusajili biashara

$
0
0
Na Mwandishi Wetu,Songwe

SERIKALI Mkoani Songwe imewataka wafanyabiashara mkoani humo, kubadilika kimtazamo kwa kuachana na biashara za uchuuzi ili kuingia katika ushindani wa kweli utakaoleta tija na kukuza uchumi wa mkoa na mtu mmoja mmoja.

Mkuu wa mkoa wa Songwe Captain Mstaafu Chiku Galawa alitoa changamoto hiyo jana wakati akifungua mafunzo ya siku tano, yanayotolewa na Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni ( BRELA), mafunzo yanayolenga kuwajengea uwezo wafanya biashara namna ya kurasimisha na kusajili biashara zao.

“Mafunzo haya ni fursa kubwa, naomba itumieni na kuichukulia kama changamoto ya kubadilika,” alisema Captain Galawa.Alisema ujio wa Brela katika mkoa wake ni njia mojawapo ya mwanzo wa kuibua fursa na kuwajenga kifikra na kimtazamo wafanyabiashara hao ambao wamekuwa wakifanya bishara kimazoea.“Naomba mbadilike, Brela wametuletea kitu kipya kwetu ni lazima tuamke,” alisema,

Bi.Galawa, alisisitiza kua biashara nyingi zimekua zikifanywa kwa uchuuzi na kuongeza kua bila kua na mtazamo wa mbele ni vigumu kuendelea.“Sajili biashara yako irasimishe uanze kushindana, mmezoea vibiashara vidogo vidogo, havina tija kwenu,” alisisitiza.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni ( BRELA) Frank Kanyus amemshukuru Mkuu wa Mkoa wa Songwe kwa jitihada zake za kuhamasisha wafanyabiashara wake ambao walijitokeza kwa wingi na kupewa elimu ya namna ya kusajili na kurasimisha majina ya biashara na kampuni zao.“Namshukuru kwa namna ya pekee mheshimiwa mkuu wa mkoa mama Galawa, ameleta hamasa kubwa,"alisema Kanyus.

Alisema namna wafanyabiashara wa Mkoa wa Songwe walivyojitokeza, imeonyesha ni namna gani Mkuu wa mkoa huyo alivyo na mwamko wa kuufanya mkoa wake ukue kimaendeleo kwa haraka kupitia wafanyabiashara na wawekezaji.“ Huu ni mfano wa kuigwa, wafanyabiashara wamekuja kwa wingi mbali na kupata mafunzo lakini wamesajili majina ya biashara zao,” aliongeza

Aidha Kanyus aliwashukuru wakuu wa Mikoa yote waliyopita na kutoa mafunzo, ikiwa ni pamoja na kusajili majina ya biashara, kuwa wameonyesha ushirikiano wa hali ya juu kwa Wakala huyo.“ Kwa kweli nawapongeza sana, wakuu wa mikoa ya Mwanza, Geita, Simiyu, Mara na Mbeya, kwa kutupokea vizuri,” aliongeza.

Kwa upande wake Afisa Mtendaji wa TCCIA Mkoani Songwe, Bw. Ditrick Mapunda amesema ujio wa Brela katika mkoa wake umesaidia kurahisisha zoezi ambalo lilikua likiwagharimu wafanyabiashara kwa kiasi kikubwa kwa kutumia muda mwingi.“ Hii ni neema kwetu, wafanyabiashara wamekua wakitumia muda mwingi na gharama kubwa kwenda Dar es Salaam kusajili majina ya Biashara,” alisema Mapunda.

BRELA ipo katika zoezi endelevu la kuhamasisha wafanyabiashara kurasimisha na kusajili majina ya biashara zao nchini nzima.
Mkuu wa Mkoa wa Songwe Captain Mstaafu Chiku Galawa ( kushoto) akisisitiza jambo wakati akizungumza na wafanyabiashara na watendaji wa Mkoa wa Songwe wakati wa mafunzo ya siku tano, yanayotolewa na Wakala wa Usajili wa leseni na Biashara ( BRELA), mafunzo yanayolenga kuwajengea uwezo wa namna ya kurasimisha na kusajili biashara zao, (katikati) ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Brela Frank Kanyus (kulia) ,Msajili Msaidizi Mwandamizi wa Mampuni Bw. Noel Chani, mafunzo hayo yanakwenda sambamba na zoezi la usajili wa papo kwa papo wa majina ya biashara.
Baadhi ya wafanyabiashara na Watendaji wa Mkoa wa Songwe, wakimfuatilia kwa makini mtoa mada kutoka wakala wa usajili wa biashara na Leseni ( BRELA) hayupo pichani, wakati wa mafunzo ya siku tano yaliyoandaliwa na Brela, mafunzo yanayolenga kuwajengea uwezo wa namna ya kurasimisha na kusajili biashara zao, mafunzo hayo yanakwenda sambamba na zoezi la usajili wa papo kwa papo wa majina ya biashara.
Mkuu wa Mkoa wa Songwe Captain Mstaafu Chiku Galawa ( kulia) akiwa katiaka akizungumza jambo na Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni ( BRELA) Frank Kanyus ( kushoto) muda mfupi mara baada ya kufungua mafunzo ya siku tano, yanayotolewa na Wakala wa Usajili wa leseni na Biashara ( BRELA), mafunzo yanayolenga kuwajengea uwezo wa namna ya kurasimisha na kusajili biashara zao, ( katikati) ni Mtendaji wa TCCIA Mkoa wa Songwe Bw. Ditrick Mapunda

UMOJA wa waandishi habari wanawake Tanzania(WJT) wafanya ziara ya utalii wa ndani hifadhi ya taifa ya Saadan

$
0
0
Na Editha Karlo,Globu ya Jamii -Saadani

UMOJA wa waandishi habari wanawake Tanzania(WJT)wameanza ziara ya utalii wa ndani na ya kazi katika hifadhi ya Taifa ya Saadani.

Ziara hiyo ya siku kumi iliyofadhiliwa na SHIRIKA la hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA)ambayo imehusisha wanahabari wanawake kutoka mikoa mbalimbali nchini wa vyombo mbalimbali wanavyofanyia kazi.

Akiongea na mtandao huu mwenyekiti wa umoja huo wa wanahabari wanawake Ester Macha mwandishi wa gazeti la majira kutoka Mkoa wa Mbeya alisema kuwa ziara hiyo itawapa fursa ya kujifunza na kuona kwa vitendo vivutio mbalimbali vilivyopo katika hifadhi za Taifa watakazo tembelea.

"Tumefurahi sana ka wanahabari kupata fursa hii ya kutembelea hifadhi zetu ikiwa ni sambamba na kuzitangaza kupitia kalamu zetu"alisema Ester.Aliwataka wananchi wote kujenga tabia ya kutembelea hifadhi zetu nasi kuwaachia wageni kutoka nje peke yao kuja kutembelea hifadhi na kufanya utalii.

Naye Mhifadhi utalii wa hifadhi ya Taifa ya Saadani Hapaikunda Mungure alisema hifadhi ya saadani ina utalii wa kuangalia wanyama kwa kutembea na magari,fukwe nzuri za bahari,utalii wa boti kwenye mto wami,matembezi ya miguu.
Mhifadhi utalii wa hifadhi ya Taifa ya Saadani Apaikunda Mungure akitoa maelezo mafupi kwa waandishi wa habari wanawake kuhusu utalii wa boti unaofanywa ndani ya mto wa wami katika hifadhi ya saadani.

Mwandishi wa habari wa blog hii Editha Karlo(kushoto)kutoka Kigoma na mwandishi wa gazeti la mwananchi Joyce Joliga kutoka Mkoa wa Ruvuma wakifanya utalii wa boti ndani ya mto wami uliopo hifadhi ya Taifa ya saadani.
Waandishi wa habari wanawake kutoka mikoa na vyombo mbalimbali wakifanya utalii wa ndani wa boti kati mto wami ndani ya hifadhi ya Saadani

WAZIRI MWAKYEMBE AKUTANA NA MWAKILISHI MKAZI WA UPR AFRIKA

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria Dkt Harrison Mwakyembe amekutana na mwakilishi wa Taasisi Isiyo ya Kiserikali ya Kupitia Hali ya Haki za Binadamu kanda ya Afrika Bw, Gilbert Onyango na kuzungumza jinsi ya kusaidia utekelezaji wa mapendekezo 130 ambayo Serikali iliyakubali mbele ya Baraza la Haki za Binadamu wakati wa kupitia Ripoti ya Tathmini ya Hali ya Haki za Binadamu
 
.Mhe. Waziri Mwakyembe amesema Serikali kama ambavyo ilivyoridhia mapendekezo hayo itasimama imara kuhakikisha yanatekelezwa kikamilifu na hivyo kuimarisha hali ya haki za binadamu nchini.

Amesema nia ya Serikali ni kuona haki za bindamu nchini zinaheshimiwa bila ya kuingilia au kukiuka mila, tamaduni , desturi na imani za kidini ambazo Tanzania imekuwa ikizifuata au kuziamini tangu enzi.

Nae bw. Onyango alisema kwamba wao kama taasisi isiyo ya kiserikali wanafanya kazi na serikali mbalimbali duniani, taasisi zisizo za serikali na Umoja wa Mataifa katika kuhakikisha haki za binadamu zinaimarishwa na kuthaminiwa na kuongeza kuwa lengo hasa la kukutana kwake ni kujitambulisha na kuomba kufanya kazi na serikali katika kuhakikisha mapendekezo yaliyokubaliwa yanatekelezwa kikamailifu.

Pia aliomba kupatiwa nafasi ya kutoa mafunzo jinsi ya utekelezaji huo kwa taasisi na watumishi wa umma wanaohusika na utekelezaji wa mapendekezo hayo ili kufanikisha mpango wa utekelezaji wa mapendekezo hayo.

Alisema kwamba lengo lao kuu ni kuunganisha mpango wa tathmini ya hali ya haki za binadamu nchini ili uendane na mpango wa malengo ya milenia ili kuweza kufikia maendeleo ya kweli huku haki za binadamu zikiimarishwa na nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa.

Mwezi Septemba 2016, Serikali iliyakataa mapendekezo 94, kuyaangalia upya mapendekezo 25 na kukubali 130 kati ya 227 yaliyotolewa na mataifa wanachama wa Umoja wa Mataifa, likiwemo suala la hali ya kisiasa Zanzibar. Tamko hilo lilitolewa kwenye mkutano wa Baraza la Haki za Binadamu wakati wa kupitisha Ripoti ya Tathmini ya Dunia (UPR) mbele ya Baraza la Haki za Binadamu wakati wa kupitia Ripoti ya Tathmini ya Hali ya Haki za Binadamu kwa nchi wanachama uliofanyika mjini Geneva nchini 





Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria Dkt Harrison Mwakyembe (katikati) akiongea na mwakilishi wa Taasisi Isiyo ya Kiserikali ya Kupitia Hali ya Haki za Binadamu kanda ya Afrika Bw, Gilbert Onyango (kulia) alipomtembelea leo (16/11/2016) ofisini kwake jijini Dar Es Salaam. Wengine pichani ni Mkurugenzi wa Idara ya Katiba na Ufuatiliaji haki Wizara ya Mambo ya Katiba na Sheria Bw. Patience Ntwina (kushoto) na Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Katiba Bw. Stanley Kamana.


Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria Dkt Harrison Mwakyembe (kushoto) akiongea na mwakilishi wa Taasisi Isiyo ya Kiserikali ya Kupitia Hali ya Haki za Binadamu kanda ya Afrika Bw, Gilbert Onyango alipomtembelea leo (16/11/2016) ofisini kwake jijini Dar Es Salaam.

Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria Dkt Harrison Mwakyembe (kushoto) akiongea na mwakilishi wa Taasisi Isiyo ya Kiserikali ya Kupitia Hali ya Haki za Binadamu kanda ya Afrika Bw, Gilbert Onyango alipomtembelea leo (16/11/2016) ofisini kwake jijini Dar Es Salaam.

DKT KIGWANGALLA NA KAMATA KAMATA YA KUFUNGIA VIWANDA MBALIMBALI VINAVYOKIKUKA TARATIBU

Mchakato wa ndege za Saudi Arabia na Tanzania waanza kusukwa

$
0
0


Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, H.E Balozi Hemedi Mgaza kulia, akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ndege la Saudi Arabian Airlines, Mh Saleh Bin Nasser Al Jasser, katika kikao chao maalum cha kujadili namna ya ndege za shirika hilo kuanza safari za kutoka Saudi Arabia hadi nchini Tanzania. Picha zote kwa Hisani ya Ofisi ya Balozi wa Tanzania Saudi Arabia.

Na Mwandishi Wetu, Saudi Arabia

WATALII, wafanyabiashara, mahujaji wa Watanzania pamoja na watu kutoka nchi za Kiarabu hususan Saudi Arabia, huenda wakapata fursa ya kuwasili Tanzania kwa urahisi endapo mchakato Shirika la Ndege la Saudi Arabian Airlines wa kutoa ndege za kutoka Saudi Arabia hadi nchini Tanzania utakapofanikiwa kama ulivyoanza kushughulikiwa.



Mapema wiki hii Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, H.E Balozi Hemedi Mgaza alifanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ndege la Saudi Arabian Airlines, Mh Saleh Bin Nasser Al Jasser, ambapo shughuli mbalimbali za utalii na vivutio vya Tanzania vilijadiliwa, kama njia ya kuangalia namna bora ya ndege hizo kufanya safari zake vizuri kwa kuzingatia mkataba wa ushirikiano wa mambo ya anga baina ya Tanzania na Saudi Arabia Bilateral Air Service Agreement (BASA).

Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, H.E Balozi Hemedi Mgaza kulia akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ndege la Saudi Arabian Airlines, Mh Saleh Bin Nasser Al Jasser kushoto.
Kikao kinaendelea kati ya balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, H.E Balozi Hemedi Mgaza na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ndege la Saudi Arabian Airlines, Mh Saleh Bin Nasser Al Jasser kushoto.



*Ni matokeo ya kikao kati ya balozi Mgaza na Mkurugenzi Mkuu Saudi Arabian Airline.
*Vivutio vingi vya utalii nchini Tanzania vyatajwa kwenye kikao hicho cha aina yake
 
Akizungumza katika kikao hicho, Balozi Mgaza alisema kuwa Tanzania ni nchi yenye vivutio vingi vya Utalii kama mbuga nzuri za wanyama pamoja na Mlima wa Kilimanjaro ambao ni alama bora za utalii nchini humo inayochochea wageni wengi kuingia na kutoka katika nchi hiyo yenye amani na upendo.

Alisema endapo kutakuwa na ndege za moja kwa moja kutoka Saudi Arabia hadi nchini Tanzania, Shirika linaweza kutoa huduma bora bora kwa kupitia sekta ya utalii pamoja na ile ya mahujaji.


“Unapozungumzia sekta ya utalii, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuna vivutio vingi vinavyosisimua, hivyo naamini kuna kila sababu ya Shirika hili la Ndege kuangalia jinsi ya kuanzisha safari za moja kwa moja.


“Nchi yetu imepiga hatua katika sekta mbalimbali na viwanja bora vya ndege vipo katika hali nzuri, huku tukiamini kuwa endapo wazo hili litafanikiwa nchi yetu Tanzania itapiga hatua kubwa kwa sababu watu wengi watahamasika kufika kutalii bila kusahau watakaotaka kuwekeza kwenye mbio za serikali za kuifanya nchi yetu kuwa nchi ya viwanda,” Alisema Balozi Mgaza.


Kwa sasa mashirika makubwa yanafanya safari zake kama vile Emirates, Oman Air, Etihad Airways, Fly Dubai, Qatar Airways, Egypt Air na Turkish Airlines jambo linalochochea kiu kubwa kwa abiria wa Saudi Arabia na Tanzania wanaopenda kuingia na kutoka kwenye nchi hizi mbili.

JIKO: TIBA YENYE NGUVU ZA AJABU!

$
0
0
Tiba hii inaitwa JIKO. Kila mwanaume anae itumia, INAMPONYESHA KABISA tatizo la UKOSEFU na UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME. Imethibitishwa na MKEMIA MKUU WA SERIKALI YA TANZANIA

Kufahamu jinsi tiba hii inavyo fanya kazi, bofya link hii hapa chini :


Kwa mahitaji yako ya tiba hii, wasiliana na duka la NEEMA HERBALIST & NUTRITIONAL FOODS CLINIC kwa simu namba 0766 53 83 84.

Tunapatikana UBUNGO jijini DAR ES SALAAM, jirani na SHULE YA MSINGI UBUNGO NATIONAL HOUSING nyuma ya jengo la UBUNGO PLAZA. · Kwa wateja waliopo DAR ES SALAAM, wasio na nafasi ya kufika ofisini kwetu, watapelekewa dawa mahali walipo ( HOME & OFFICE DELIVERY ).

· Kwa wateja waliopo mikoani, watatumiwa dawa kwa njia ya mabasi mbalimbali.

· Kwa wateja waliopo Zanzibar, watatumiwa dawa kwa njia ya usafiri wa boti.

· Kwa wateja wa Mombasa, watatumiwa dawa kwa basi la TAHMEED COACH.

· Kwa wateja wa NAIROBI watatumiwa dawa kwa basi la DAR EXPRESS.

· Na kwa wateja wa UGHAIBUNI ( DIASPORA), watatumiwa dawa kwa njia ya POSTA au DHL.

· Kwa taarifa zaidi kuhusu huduma zetu, tembelea kila siku website yetu www.neemaherbalist.com


KUMBUKUMBU YA MHE. JACKSON MVANGILA MAKWETTA

$
0
0
Ni miaka minne toka tumpoteze baba yetu mpendwa Mhe. Jackson Mvangilwa Makwetta, Leo tunakukumbuka ukiwa Baba kwa kutufundisha mengi yaliyo Mema Duniani.

Pia ulikuwa ni kiongozi wa muda mrefu katika nchi yetu na ulie
pendwa na wengi kutokana na Uwazi, Ukweli,Uwajibikaji, hekima juhudi katika kazi ukiwa katika wizara tofauti ulizohudumu ikiwamo Elimu, kilimo,Nishati na Madini,Mawasiliano,Ulinzi na Utumishi.
Watoto wako na watanzania bado tunadhamini mchango wako na tutakukumbuka daima.
Upumzike kwa Amani

TANAPA YAPANIA KUDHIBITI UGONJWA WA KIMETA USIINGIE KWENYE HIFADHI ZA TAIFA

$
0
0

Maafisa wa idara ya wanyapori wakiangalia mmoja wa mizoga iliyokufa kutokana na ugonjwa wa Kimeta katika Shoroba ya Selela wilayani Monduli mkoa wa Arusha.
Daktari wa Mifugo wa halmashauri ya wilaya ya Monduli,Yandu Marmo akimkagua mnyama aliyekufa kwa ugonjwa wa Kimeta.
Mzoga wa Swala
Ndege wakiwa wamejikusanya kula mizoga iliyokufa kwa ugonjwa wa Kimeta.
Mzoga wa mnyama aina ya Nyumbu.


Maafisa wa Shirika la Hifadhi za Taifa(Tanapa) na Idara ya Wanyamapori wakiwa kwenye Shoroba ya Selela kudhibiti ugonjwa wa Kimeta,katikati ni Meneja Uhusiano wa Tanapa,Pascal Shelutete na Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara,Noelia Myonga kulia kwake wajidaliana jambo.

Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara,Noelia Myonga(kushoto) akizungumza wakati wa kupanga mikakati ya kudhibiti ugonjwa wa Kimeta ambao unahusisha watumishi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro na Idara ya wanyamapori.

Zantel yanogesha sherehe za Full Moon Party mjini Zanzibar

$
0
0
Wasanii wa kikundi cha sanaa cha Bagamoyo African Culture wakionyesha uhamiri wao wakati wa sherehe ya Kendwa Rocks Full Moon iliyofanyika mjini Zanzibar hivi karibunii. Full Moon Party hudhaminiwa na Zantel na hujumuisha watanzania na watalii kutoka nchi mbali mbali duniani.
Wasanii wa kikundi cha sanaa cha Bagamoyo African Culture wakitumbuiza wakati wa sherehe ya Kendwa Rocks Full Moon iliyofanyika mjini Zanzibar hivi karibunii. Full Moon Party hudhaminiwa na Zantel na hujumuisha watanzania na watalii kutoka nchi mbali mbali duniani.
Wasanii wa Karafuu Band wakitoa burudani wakati wa sherehe ya Kendwa Rocks Full Moon iliyofanyika mjini Zanzibar hivi karibunii. Full Moon Party hudhaminiwa na Zantel na hujumuisha watanzania na watalii kutoka nchi mbali mbali duniani. 
Maofisa mauzo wa Zantel Tanzania wakijiandaa kutoa huduma katika sherehe ya Kendwa Rocks Full Moon inayofanyika kila mwezi wakati wa mbalamwezi kamili mjini Zanzibar. 

VIWANDA VINAJENGWA KWA KASI MKOA WA PWANI-MWIJAGE

$
0
0
Na Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii.

Waziri wa Viwanda Biashaa na Uwekezaji, Charle’s Mwijage  amefanya ziara kutembelea viwanda vilivyopo Mkoa wa Pwani na kuangalia maendeleo ya mkoa huo katika sekta ya viwanda.Katika ziara hiyo Waziri Mwijage alipotembelea kiwanda cha Viuadudu cha kibaha, Sayona Fruits, Global Packaging kiwanda cha kuunganisha matrekta pamoja na kiwanda cha Eveline.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumaliza ziara hiyo, Mwijage  amesema ujenzi wa viwanda katika mkoa wa Pwani unakua kwa kasi na kuonngeza ajira kwa watanzania.

Amesema kitendo cha mmiliki  wa kiwanda cha Sayona kuwapa  wanakikjiji  fursa ya kupata elimu mpaka ngazi ya chuo kikuu na kisha kuajiliwa katika kiwanda hicho ni uungwana ambao watafanya kazi ya kufundisha wafanyakazi wenzao.

“Wafanyakazi wa Sayona kupatiwa fursa ya kwenda chuo kikuu kujifunza ili kuja kuwafundisha wenzao, kasi hiyo imenifurahisha sana” amesema Waziri Mwijage.
 Waziri  wa Viwanda Biashaa na Uwekezaji Charle’s Mwijage akizungumza na Mkuu wa mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo mara baada ya kuwasili mkoani pwani kwaajili ya ziara ya siku moja.
 .Waziri wa Viwanda Biashaa na Uwekezaji Charle’s akizungumza na meneimenti ya kiwanda cha viua vidudu kilichopo kibaha, mkoani Pwani Kulia ni Kaimu Meneja Mkuu wa Kiwada hicho,Samwel Mziray mkoani Pwani. 
 Waziri wa Viwanda Biashaa na Uwekezaji Charle’s Mwijage akipata maelezo kwa Kaimu Meneja Mkuu wa Kiwanda Viua Vidudu hicho,Samwel Mziray katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Assumpter Mshama. 
 Waziri  wa Viwanda Biashaa na Uwekezaji Charle’s Mwijage akizungumza na wafanyakazi wa kiwanda cha viua vidudu, Kibaha.
 Waziri  wa Viwanda Biashaa na Uwekezaji Charle’s Mwijage akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Global Packaging, Wasonga Otieno mkoani Pwani.
 Waziri wa Viwanda Biashaa na Uwekezaji Charle’s Mwijage akisalimia wafanyakazi wa  kiwanda cha Sayona mbele mwenye miwani ni  Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Alhaj Majjid Mwanga  

Waziri wa Viwanda Biashaa na Uwekezaji Charle’s Mwijage akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Chama  cha Mapinduzi  wa mkoa wa Pwani. Picha na  Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii.

Zantel yanogesha sherehe za Full Moon Party mjini Zanzibar

$
0
0
Wasanii wa kikundi cha sanaa cha Bagamoyo African Culture wakionyesha uhamiri wao wakati wa sherehe ya Kendwa Rocks Full Moon iliyofanyika mjini Zanzibar hivi karibunii. Full Moon Party hudhaminiwa na Zantel na hujumuisha watanzania na watalii kutoka nchi mbali mbali duniani.
Wasanii wa kikundi cha sanaa cha Bagamoyo African Culture wakitumbuiza wakati wa sherehe ya Kendwa Rocks Full Moon iliyofanyika mjini Zanzibar hivi karibunii. Full Moon Party hudhaminiwa na Zantel na hujumuisha watanzania na watalii kutoka nchi mbali mbali duniani.
Wasanii wa Karafuu Band wakitoa burudani wakati wa sherehe ya Kendwa Rocks Full Moon iliyofanyika mjini Zanzibar hivi karibunii. Full Moon Party hudhaminiwa na Zantel na hujumuisha watanzania na watalii kutoka nchi mbali mbali duniani. 
Maofisa mauzo wa Zantel Tanzania wakijiandaa kutoa huduma katika sherehe ya Kendwa Rocks Full Moon inayofanyika kila mwezi wakati wa mbalamwezi kamili mjini Zanzibar. 

MAKALA YA HIFADHI YA TAIFA YA KATAVI

$
0
0
Mmoja wa Simba akiwa katika Hifadhi ya Taifa ya Katavi 
Baadhi ya Mamba wakiwa wamepumzika katika hifadhi ya Taifa ya Katavi
Hawa ni Punda milia wakiwa katika Hifadhi ya Taifa ya Katavi
Kama kibao kinavyo onekana hili ni Eneo la Tambiko ambapo watu huja kusali na kutoa sadaka mbalimbali 
Simba akiwa na mzoga wa Kiboko 
Twiga akiwa katika hifadhi ya Taifa ya Katavi


Na Walter Mguluchuma wa Katavi yetu Blog

Hifadhi ya Taifa ya Katavi inapatikana kusini Magharibi mwa Tanzania karibu na Ziwa Tanganyika katika Wilaya za Mpanda ,Tanganyika na Mlele Mkoa wa Katavi inapatikana katika latitude 6.63.7.34 kusini na na longitude 3.74.31.84 Mashariki.

Hifadhi hii ilitangazwa kuwa Hifadhi ya Taifa mwaka 1974 ikiwa na ukubwa wa kilometa za mraba 2253 iliongezwa ukubwa mwaka 1996 na kufikia ukubwa wa kilometa za mraba 4471 na kuifanya kuwa Hifadhi ya tatu kwa ukubwa Tanzania baada ya Ruaha na Serengeti .

Ilipata jina lake kutokana na mzimu wa kabila la Wabende aliyejulikana kwa  jina la Katabi ambapo mpaka leo watu mbalimbali wamekuwa wakifika ndani ya Hifadhi ya Katavi na kwenda kwenye mti ulioko kwenye Ziwa Katavi wakiamini kuwa mzimu Katabi alikuwa akiishi hapo zamani kabla ya kuwepo Hifadhi ya Taifa ya Katavi .

Jina la Hifadhi hii lilijulikana kama Katabi kutokana na imani ya jamii hizo kwa mzimu Katabi inaaminika kwamba mzimu Katabi una uwezo wa kufanya miujiza ikiwemo kufanya mvua inyeshe , kuzuia magonjwa ya mlipuko kama vile ndui na kutatua shida za watu mbalimbali .

Hifadhi hii inafikika mwaka mzima kwa kupitia Mikoa ya Dares,salaam,Mwanza , Kigoma Arusha hadi Mpanda kupitia Tabora kwa kutumia usafiri wa ndege za kukodi Chartered planes au kwa njia ya barabara kwa kupitia Mbeya na Sumbawanga pia kwa kutumia usafiri wa Treni kutokea Tabora .

Katavi 'National Park' inawanyama wengi na adimu na wakubwa kuliko wanyama wanaopatikana kwenye Hifadhi nyingine hapa Nchini kutoka na hari ya uoto wa asili uliopo kwenye Hifadhi hii ambayo kwa sasa imeanza kupata watalii tofauti na hapo awali .

Mbali ya kuwepo kwa wanyama wengi madhari yake ni pana kuanzia uwanda tambarare wa nyasi katika mkondo wa bonde la ufa hadi kwenye miteremko mikali ambayo ni matawi mawili sambamba na bonde la ufa la Mashariki maarufu kama bonde la ufa la Rukwa .

Uoto uliopo unavutia unavutia sana kuanzia kuanzia Misitu iliyofunga mpaka misitu ya wazi ,vichaka uwanda wa nyasi maziwa ya msimu ya Chada na Katavi mabwawa na uoto kando ya mito .Wakati wa kipindi cha mvua kuna aina nyingi za maua aina ya 'species' mbalimbali za miti na majani aina za 'species' 226 za miti zimeisha tambuliwa zikiwemo aina tatu zenye mvuto wa kisayansi .

Uhai wa Hifadhi ya Katavi unategemea mto Katuma ambao humwaga maji yake ziwa Katavi upande wa kaskazini ,Ziwa Chada na mbuga yenye eneo la kilometa za mraba 425 ambayo hutuamisha maji Floodplain katikati ya Hifadhi ziwa Chada hupokea pia maji kutoka mto Kapapa ambao mkondo wake hutokea Kaskazini mwa Hifadhi ya Taifa Katavi .

Kuna aina mbalimbali za wanyama pori ,idadi kubwa ya vipepeo na ndege wa aina mbalimbali katika Hifadhi ya Katavi ni kivutio vikubwa kwa wageni idadi ya watalii na shughuli za maendeleo ndani ya Hifadhi bado ni ndogo hivyo kufanya mazingira kuwa asilia zaidi .

Baadhi ya wanyama wanaopatikana kwenye Hifadhi ya Katavi ni makundi makubwa ya Tembo , Nyati, Simba , Pundamilia , Mbwa mwitu , kongoni Swala pala , Nyemela na wanyama wengineo .Pia kwenye eneo la mto Stalike  na Iku utakuta kuna makundi makubwa sana ya viboko na mamba ambapo kumekuwa na mapigano ya mara kwa mara na kufanya eneo hilo kuwa kivutio kikubwa kwa watalii.

Upande wa Hotel hifadhi hiyo inayo hotel nzuri za kufikia wagani ndani ya Hifadhi iiingawa bado ni chache pia hotel nyingine zinapatikana katika Kijiji cha Stalike ambacho kipo jirani na Hifadhi na pia katika Mji wa Mpanda makao makuu ya Mkoa wa Katavi uliopo umbali wa kilometa 40 kutoka Hifadhi ya Katavi .

Hivi karibuni kaimu Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Katavi Elias Manase aliwaambia wandishi wa Habari wa vyombo mbalimbali wa Mkoa wa Katavi  kwamba Hifadhi hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali .

Baadhi ya changamoto hizo ni ujangili wa wanyama hasa Tembo ambao unasababishwa na kuwepo kwa kambi za wakimbizi za Mishamo na Katumba ambazo wanaishi Raia wa Burundi na Kongo .

Ilidai kuwa watu wanao ishi kwenye makazi hayo wamekuwa wakiingiza silaha za kivita na kuziingiza nchini kisha wamekuwa wakifanya ujangili wa kuuwa Tembo na kisha wanachukua meno ya Tembo na kuyasafirisha kwenye soko la nchi jirani.Changamoto nyinginei ni uhaba wa miundo mbinu  ndani ya Hifadhi kwani bado haiku mizuri sana ingawa barabara zake zinapitika karibu mwaka mzima .

Manase alitowa wito kwa watanzania kujenga utamaduni wa kutembelea Hifadhi za Taifa kwani gharama ya kutembelea Hifadhi za Taifa ni ndogo kuliko gharama ya mtu anayoitumia kwenye Bar kunywa pombe . 

Askari wa Hifadhi ya Katavi Joseph Mhina aliielezea Hifadhi ya Katavi kuwa   ni hifadhi ambayo ipo tofauti kabisa na Hifadhi nyingine kwani watalii wanaotembelea Hifadhi hiyo huwa wanawaona wanyama kiurahisi kabisa kwani watalii huwa ni wachache hivyo huwa hakuna kugombania kuwaona wanyama kama Hifadhi nyingine .

Imeandaliwa na Blogs za Mikoa kupitia Katavi yetu Blog

VIWANJA VYA MICHEZO KUJENGWA KATA YA ENGUTOTO

$
0
0

mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo(kwanza kulia) akizungumza na wadau wa maendeleo Bw. Hans Paul(pili kulia) ambaye amehaidi kujenga viwanja vya michezo ndani ya kata ya Engutoto na Bw. Jagjit Aggarwal


Na Woinde Shizza,Arusha

WANANCHI kutoka kata ya Engutoto jijini hapa,wanatarajiwa kutimiza ndoto zao za muda mrefu juu ya ukosefu wa viwanja baada ya mfadhili kujitokeza kuwajengea.

Mfadhili huyo Hans Paul kupitia kampuni ya Dharam Singh Hanspaul & son ltd alisema hayo mbele ya mkuu wa mkoa Arusha kuwa katika kutimiza adhma ya serikali kusaidia maendeleo ya michezo kwa vijana amejitolea kujenga viwanja viwili vya michezo.

“Viwanja tutakavyojenga ni kwa mpira wa miguu na mpira wa Netiboli na vinatarajiwa kugharimu kiasi cha shilingi milioni 30 fedha za kitanzania na tunatarajia kuanza ujenzi huo ifikapo mwanzoni mwa mwaka 2017,”Alisema Paul.

Alisema kuwa lengo kuu la kujenga viwanja ni katika kuwawezesha vijana wapate muda wa kujihusiha na michezo ili kuepukana na tabia hatarishi ambazo zingeharibu ndoto za maisha yao.

Baahi ya wakazi wa kata hiyo wakizungumzia neema watakayoipata kutoka kwa mfadhili huyo walisema “Ni jambo la kupongeza kwani vijana wengi wamekuwa hawana mahali pa kufanya mazoezi na kwa hali hii itasidia sasa kuanza kuona vipaji vya michezo katika kata hii.” Alisema mmoja wa wakazi hao.

Kwa upande wake mkuu wa mkoa Arusha Mrisho Gambo alisema juhudi alizozifanya mfadhili huyo katika sekta ya michezo ni jambo la heri ambalo linatakiwa liwe mfano kwa wadau wengine katika kusaidia kuinua michezio katika jamii sambamba na kuwa michezo ni moja ya ajira kwa Vijana .

WAZIRI WA FEDHA DK.PHILIP MPANGO MGENI RASMI MAADHIMISHO YA SIKU YA TAKWIMU AFRIKA

$
0
0
 Meneja wa Idara ya Pato la Taifa kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Daniel Masolwa (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika yatakayofanyika kesho Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa mkabala na Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM). Kulia ni Ofisa Habari wa Idara Habari Maelezo, Beatrice Lyimo.
Mkutano na wanahabari ukiendelea.

Na Dotto Mwaibale

WAZIRI wa Fedha Dk. Philip Mpango anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika yatakayofanyika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa mkabala na Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM)

Maadhimisho hayo yatafanyika kesho kuanzia saa tatu asubuhi ambapo wadau mbalimbali wa masuala ya takwimu na wananchi watahudhuria.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi Meneja wa Idara ya Pato la Taifa kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Daniel Masolwa alisema maadhimisho hayo ni muhimu sana na kuwa kauli mbiu yake ya mwaka huu ni " Kuimarisha Takwimu za Kiuchumi kwa Mtangamano wa Kikanda, Mabadiliko ya Miundo na Maendeleo Endelevu"

Masolwa alisema lengo kuu la  kuadhimisha siku hiyo ni kuongeza uelewa mpana kwa watumiaji wote wa Takwimu Afrika kuhusu umuhimu wa takwimu katika kupanga mipango ya maendeleo katika sekta zote za kijamii na kiuchumi katika Bara la Afrika.

Aidha alisema ni siku ambayo hutoa fursa kwa nchi kutathmini na kufuatilia malengo yaliyofikiwa katika Mipango ya Maendeleo ya ndani na nje ya Nchi.

Alisema Maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika huwa yanaandaliwa na kauli mbiu mbalimbali kila mwaka zinahusiana na umuhimu wa takwimu katika kupanga maendeleo na kutunga sera katika Bara la Afrika.

Masolwa alisema umuhimu wa kuboresha na kuimarisha takwimu za kiuchumi na zenye ubora kwa utangamano wa kikanda barani Afrika utasaidia kuleta mabadiliko ya kiuchumi na kufanikisha malengo endelevu, Agenda 2063 ya Afrika na mipango ya kitaifa ya kukuza uchumi.

DC HAPI AAINISHA MAENEO YA MAGULIO WILAYANI KINONDONI

$
0
0
Na Bashir Nkoromo

Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, imeainisha maeneo ya magulio kwa ajili ya wafanyabiashara ndogo ndogo, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa agizo la Rais John Magufuli kuzitaka mamlaka zinazohusika kutenga maeneo ya wafanyabiashara hao kabla ya kuwatimua katika maeneo yasiyoruhisiwa.Akizungumza na waandishi wa habari leo Ofisini kwake, Mkuu wa Wilaya hiyo, Salum Hapi, ameyataja maeneo hayo kuwa yapo katika kata za Kinondoni, Bunju, Msasani, Mabwepande, Kunduchi na Kata ya Wazo.

Hapi amesema, vitu vitakavyoruhiswa kuuzwa kwenye magulio hayo ni bihaa za sokoni, vyombo vya nyumbani, nguo mpya na mitumba, viatu, urembo, na kwamba kwa ujumla ni bidhaa ambazo hutumiwa na watu katika maisha ya kila siku. Ametaja mpangilo unaotakiwa kwenye magulio hayo kuwa ni, kupangwa eneo moja bidha zinazofanana, viwepo vyoo vya muda, na usafi wa eneo la gulio ambao utasimamiwa na Mtendaji Mwenyewe wa eneo husika.

MPANGILIO NA RATIBA KAMILI YA MAGULIO HAYO


MAKAMU WA PILI RAIS ZANZIBAR BALOZI SEIF ALI IDDI AZINDUA JENGO LA MAABARA YA SKULI YA KITOPE

$
0
0
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akikata utepe kuashiria kuzindua pamoja na kukabidhi Jengo la Maabara la Skuli ya Sekondari ya Kitope aliloligharamia yeye pamoja na ufadhili wa Ubalozi China Nchini Tanzania na Kampuni ya simu za mkononi yaTigo.
Mwalimu wa Masomo ya Sayansi wa skuli ya Sekondari Kitope Mwalimu Ali Mohamed aliyeshika kifaa cha Maabara akimuelezea Balozi Seif  urahisi wa kazi yao ya ufundishaji kwa sasa baada ya kupata  Maabara yenye kukidhi kiwango kinachokubalika kwa skuli za Sekondari.
Mwalimu Ali Mohamed akiendelea kutoa maelezo kwa Balozi Seif  jinsi wanafunzi wa masomo ya sayansi katika skuli yao walivyofarajika kutokana na kujengewa maabara iliyokamilika kwa kazi zao za vitendo.
 Mwalimu Wanu Ndende Juma akiwasilisha Risala ya walimu na wanafunzi wa skuli ya Sekondari ya Kistope kwenye hafla ya uzinduzi na kukabidhiwa rasmi jengo la Maabara ya skuli hiyo lililomalizika kujengwa pamoja na kuwekwa vifaa vyake.
Baadhi ya Wanafunzi wa skuli ya sekondari ya Kitope wakifuatilia matukio mbali mbali yaliyojiri kwenye uzinduzi wa maabara ya skuli yao.
Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini “B” Ndugu Issa Juma akitoa salamu katika hafla ya uzinduzi wa jengo jipya la maabara ya skuli ya sekondari ya kitope.
 Waziri wa Elimu Mh. Riziki Pemba Juma akimshukuru Mwakilishi wa Jimbo la Mahonda Balozi Seif  kwa uzalendo wake wa kuunga mkono sekta ya Elimu wakati wa hafla ya uzinduzi wa Maabara ya skuli ya Kitope.

Picha na – OMPR – ZNZ.
                             
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliitahadharisha Jamii  kuelewa kwamba maendeleo kwa wana Taaluma wa Fani ya Sayansi iwe Maskulini au vyuoni  yataendelea kuwa ndoto iwapo  hakutakuwa na mipango imara ya  kuimarisha miundombinu kwenye Majengo ya Maabara katika maeneo husika.

Alisema Wazazi kwa kushirikiana na Kamati za Maskuli na vyuo kupitia usimamizi wa Wizara inayosimamia masuala ya Elimu bado wana jukumu la kuhakikisha vilio vya Wanafunzi kutokana na kukabiliwa na ukosefu wa Maabara kwenye Taasisi zao vinamalizika.

Balozi Seif Ali Iddi ambae pia ni Mwakilishi wa Jimbo la Mahonda alitoa tahadhari hiyo wakati wa hafla fupi ya kukabidhi pamoja na kulizindua rasmi Jengo la Maabara ya Skuli ya Sekondari ya Kitope iliyomo ndani ya Wilaya ya Kaskazini “B”.

Jengo hilo aliloligharamia yeye pamoja na kupata msaada wa nguvu za ufadhili wa baadhi ya vifaa kutoka Ubalozi wa Jamuhuri ya Watu wa China na Kampuni ya mitandao ya simu za mkononi ya Tigo limegharimu jumla ya shilingi za Kitanzania Milioni 38,780,000/-.

Balozi Seif  alisema wanafunzi wa Skuli ya Sekondari ya Kitope kwa sasa hawana sababu ya kufanya vibaya katika mitihani yao ya Kitaifa kutokana na kumalizika kwa Jengo hilo la Maabara ambalo lilikuwa kilio kwao na walimu wao kwa karibu miaka Kumi sasa.

Aliwaasa Wanafunzi hao kuhakikisha kwamba Vifaa walivyopatiwa kwenye Maabara ya Skuli yao wataendelea kuvitunza kwa tahadhari  ili viweze kudumu kwa kipindi kirefu na kutumiwa pia na wanafunzi wenzao watakaofuatia baada ya wao.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif aliupongeza na kuushukuru Uongozi wa Ubalozi wa Jamuhuri ya Watu wa China hapa Nchini pamoja na ule wa Kampuni ya Mitandao ya Simu za mkononi wa Tigo kwa upendo wao wa kuunga mkono Sekta ya Elimu hapa Zanzibar.


Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
17/11/2016.

WAJASIRIAMALI KIGOMA WANUFAIKA NA MAFUNZO YA TPSF

$
0
0
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji Yuda Thadeus Mboya (katikati) akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina ya wajasiriamali iliyoandaliwa na Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (Tanzania Private Sector Foundation),(Kulia) Meneja wa SIDO mkoa Kigoma, Gervas Ntahamba na (wa pili kushoto) Mwenyekiti wa chama cha Wafanyabiashara na wenye viwanda mkoa Kigoma (TCCIA), Ramadhani Gange. 
Mwenyekiti wa chama cha Wafanyabiashara na wenye viwanda mkoa Kigoma (TCCIA), Ramadhani Gange (wa pili kushoto aliyesimama) akitoa neno la shukrani kwa mgeni Rasmi wakati wa ufunguzi wa semina kwa wajasiliamali iliyotayarishwa na taasisi ya sekta binafasi Tanzania (TPSF) .

Baadhi ya wajasiliamali wa Manispaa ya Kigoma Ujiji wakijadiliana mada mbalimbali zilizotolewa na wawezeshaji wakati wa semina ya wajasiriamali iliyoandaliwa na taasisi ya sekta binafasi Tanzania (TPSF).

Wajasiriamali waliopo mkoani Kigoma wametakiwa kutumia raslimali mbalimbali zilizopo mkoani humo na fursa zinazojitokeza kwa sasa kuibua miradi ya biashara na kuendesha biashara yao kitaalamu wakiwa na malengo ya kujikwamua kutoka katika hali ya umaskini. Ushauri huo umetolewa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji , Yuda Thadeus Mboya, wakati wa ufunguzi wa mafunzo maalumu ya mbinu za kuendeleza wajasiriamali yaliyoandaliwa na taasisi ya Tanzania Private Sector Foundation (TPSF) na kufanyika katika ukumbi wa St.Martha mjini Kigoma. 

Alisema serikali imefungua milango ya kuwasaidia wafanyabiashara wadogo kwa kutumia fursa zilizopo hivyo aliwataka kushiriki mafunzo mbalimbali ya mbinu za biashara na kuibua miradi ya biashara na kuwa na utayari wa kukabiliana na changamoto mbalimbali zilizopo katika biashara kwa kipindi hiki mojawapo ikiwa ni ushindani mkubwa na kufanya biashara kwa kufuata njia halali zinazotakiwa ikiwemo kulipa kodi za serikali kwa mujibu wa sheria. 

Hivi sasa biashara zinafanyika katika mazingira ya ushindani na wateja wanahitaji bidhaa zenye ubora hivyo haitakiwi ubabaishaji wa aina yoyote kwa mfanyabiashara anayetaka mafanikio”.Alisema Mboya. Aliipongeza taasisi ya TPSF kwa kuendesha miradi ya mafunzo kwa wajasiariamali sehemu mbalimbali nchini “Nawapongeza kwa kuwafikishia mafunzo wajasiriamali wa ngazi za chini katika ngazi ya mikoa na wilaya kwa kuwa wafanyabiashara wakipata mafunzo kama haya kwa vyovyote wataweza kupata mafanikio katika shughuli zao”.Alisema . 

Kwa upande wake Meneja Mradi wa Mafunzo kutoka taasisi ya TPSF,Celestine Mkama alisema kuwa taasisi hiyo inaendesha mradi wa kuwapatia mafunzo wajasiriamali kuhusiana na mbinu mbalimbali za kufanya biashara kwa lengo la kupata mafanikio.

 “Mafunzo haya yamelenga kuwapatia maarifa wafanyabiashara wadogo ili yawajengee uwezo wa kukabiliana na changamoto zilizopo katika biashara “Tafiti nyingi zinaonyesha kuwa wafanyabiashara wengi wadogo wamekuwa wakikosa mbinu za kufanya biashara kutokana na kukosa elimu ya biashara ndio maana tumeona tuwasaidie katika eneo hili la kuwajengea uwezo kupitia kuwapatia elimu ya ujasiriamali”.Alisema Bw.Mkama. 

Mkama alisema baadhi ya masuala yanayofundishwa kupitia mafunzo haya ni utunzaji wa mahesabu ya biashara,nidhamu katika matumizi ya fedha,utunzaji wa kumbukumbu za biashara na jinsi ya kupanga miradi. Alisema mafunzo haya tayari yameishafanyika katika mikoa mbalimbali na kuwafikia wajasiriamali wengi na tathmini ya awali inaonyesha kuwa waliopata mafunzo haya wameanza kuendesha biashara zao kwa ufanisi na kutoa mchango katika pato la taifa kupitia kulipa kodi.

WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO DKT. PHILIP MPANGO AKUTANA NA WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA FINLAND KAI MYKKANEN

$
0
0
 Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) (kulia), akifafanua jambo kwa wajumbe kutoka Serikali ya Finland (hawapo pichani), Kushoto ni Kamishna Msaidizi wa Ushirikiano wa Kikanda kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Judica Omary.
 Waziri wa Mambo ya Nje, Biashara na Maendeleo wa Finland, Kai Mykkanen (kulia), akizungumza katika Mkutano kuhusu Ushirikiano wa Maendeleo katika Sekta mbalimbali ikiwemo  Kilimo, Biashara, Mawasiliano na Nishati, kati ya Tanzania na Finland . Kushoto ni Balozi wa Finland nchini Tanzania Pekka Hukka, Mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
 Wajumbe kutoka Serikali ya Finland (kushoto) na wenyeji wao kutoka Tanzania (kulia) wakiwa katika mkutano wa pamoja wakijadili kuhusu masuala ya Ushirikiano wa Maendeleo katika Sekta mbalimbali ikiwemo Kilimo na Nishati, kati ya pande hizo mbili, Mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) (katikati), akipeana mkono na Balozi wa Finland nchini Tanzania Pekka Hukka (kulia),  baada ya kumalizika kwa Mkutano kati ya Tanzania na Finland kuhusu Ushirikiano wa Maendeleo katika Sekta ya Nishati, Biashara, Kilimo na Mawasiliano. Kushoto ni Waziri wa Mambo ya Nje, Biashara na Maendeleo wa Finland Kai Mykkanen, Mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango, jijini Dar es Salaam.

Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano, Wizara ya Fedha na Mipango
Viewing all 46395 articles
Browse latest View live




Latest Images