Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46202 articles
Browse latest View live

MREMBO JULITHA KABETE AAHIDI MAKUBWA MISS AFRIKA

0
0
MWAKILISHI wa Tanzania katika mashindano ya Miss Afrika, Julitha Kabete ameondoka leo kuelekea nchini Nigeria katika fainali ya michuano hiyo inayofanyika Novemba 26 mwaka huu huku akiwaahidi watanzania kwua  ataipeperusha vyema bendera ya Tanzania .

Akizungumza kabla ya kuondoka kwenye  Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Kabete amesema kuwa lengo lake ni kuwa mmoja wa wawakilishi bora katika shindano hilo na kuitangaza vyema nchini  pamoja na kurudi taji hilo na kwa kupitia kampuni ya Millen Magese Group chini ya Mkurugenzi wake ,Happiness 'Millen' Magese ameshukuru kwa kuingia nae mkataba ili aweze kushiriki michuano hiyo na kufanya Kazi nyingine za urembo. 

"Mimi kama mwakilishi wa Tanzania nitahalikisha anafanya vizuri katika shindano hilo, ambalo nimepata nafasi ya kuwa mpeperusha bendera wa nchini yangu Tanzania " amesema. Kabete alikabidhiwa bendera ya taifa na Waziri wa Habari Sanaa Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye ambaye alimshihi kwenda kujituma zaidi kwani wana imani na uwezo wake na pia ni moja ya warembo watakaowakilisha vyema nchi yetu na kurudi na taji hilo.

“Lengo la Serikali ni kuhakikisha washiriki wa shindano la Miss Tanzania wanapata fursa nyingine si tu akishapatikana mshinda wengine wanaachwa, hivyo tunaamini mrembo huyo anavigezo vyote na atakwenda kufanya vizuri,” amesema Nape.

Shindano hilo litafanyika nchini humo katika jimbo la Cross River, mji wa Calabar,ambapo Gavana wa jimbo hilo la Cross River Profesa Ben Ayade, atatoa zawadi ya gari na zaidi ya sh.million 52 ya Tanzania hiyo itakuwa kwa ushindi wa kwanza, mshindi wa pili atapata zawadi ya Sh.milioni 32 na ushindi wa Tatu ni Sh.million 22. 

Shindano hilo la Miss Afrika 2016 ambalo limebeba kauli
mbiu ya Kutunza, Kujali na Kuthamini Uchumi wenye kutoa kipaumbele kwa Mazingira kama nyenzo kwa ajili ya Maendeleo endelevu.

Julietha alichaguliwa katika shindano lililoendeshwa na kampuni ya Millen Magese (MMG), inayoshughulika na kusaka vipaji vya warembo pamoja na 
Mmratibu wa MMG, Matukio Chuma, amesema kuwa wanamitindo kutoka kwenye shindano hilo wameweza kuendelea kufanya vizuri kupitia Swahili Fashion Week.

Taasisi hiyo imekuwa ikifanya shughuli zake ndani na nje ya bara la Afrika, ikiwemo nchini Marekani, Millen Magese amekuwa Kinara, Balozi wa kuheshimika na aliye mfano ndani na nje ya Bara la Afrika. mwisho

MREMA AMWANDIKIA WAZIRI MKUU BARUA KULALAMIKIA JESHI LA MAGEREZA KUKWAMISHA MPANGO WAKE WA KUWATOA WAFUNGWA

0
0
Mwenyekiti wa Taifa wa Bodi ya Parole,Dkt. Augustine Mrema  amemwandikia barua Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Kasim Majaliwa kulalamikia jeshi la Magereza kukwamisha mpango wake wa kuwatoa wafungwa ambao tayari wameshalipiwa fedha na wasamalia wema baada ya kukidhi vigezo.

Dkt. Mrema ameyasema hayo mchana huu wakati wa kutoa taarifa yake hiyo kwa waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam kuzungumzia suala lake hilo la Maafisa wa Magereza kusitisha hatua ya kukatisha mpango wake licha ya kuwalipia wafungwa waliokidhi vigezo.

“Mimi nimeona nisinyamaze. Napaza sauti nataka Rais aone, ajue kama magereza yetu yanashida na tunalotatizo kwa nini mpango huu umesimamishwa na umesitishwa tumekosea wapi?. 

Nimesha muandikia barua Waziri Mkuu kulalamikia jeshi la Magereza kukwamisha mpango huu na watu 43 tayari tumesha walipia faini hiyo lakini bado wapo magerezani wanasota. Mrema amefanya kosa lipi? Ama Mama Mchungaji Getrude Rwakatare amekosa nini? Mpaka wamesitisha zoezi hili” amesema Mrema kwa waandishi wa habari.

Dkt. Mrema ameweza kuonyesha nyaraka ikiwemo risiti mbalimbali walizofanya malipo kwa ajili ya kuwatoa wafungwa hao ambapo amesema haki ya kuzuia mpango huo imeweza kumuumiza vibaya kwani wasamalia wema walioweza kujitolea fedha za mpango huo imewagusa pia.

Pia ameongeza kuwa,  mpaka sasa magereza mbalimbali kuna msongamano wa wafungwa ambao wanahitaji msaada wa kutoka ila hawajapata fedha za kulipiwa hivyo pindi wasamalia wema kama Mchungaji Mama Rwakatare wanapojitokeza wanatakiwa kupongeza na wala si kupinda kona kona.Hivi karibuni Jeshi la Magereza lilisitisha shughuli iliyokuwa ikiendeshwa na Mchungaji Getrude Lwakatare ya kuwalipia faini wafungwa walioko magerezani hadi hapo utaratibu mwingine utakapotolewa.

Awali ilidaiwa kuwa Mpango huo unaofanywa na Lwakatare kwa kushirikiana na Mwenyekiti wa Taifa wa Bodi ya Parole, Augustine Mrema tayari umewezesha wafungwa 78 kutoka magerezani baada ya kuwalipia faini inayofikia Sh25 milioni. 

Kwa mujibu taarifa zilizonukuliwa katika moja ya vyombo vya habari hapa mchini vilieleza kuwa, Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dodoma, Antonio Kilumbi alisema amepata maelekezo ya kusitishwa kwa mpango huo kutoka ngazi ya juu ya jeshi hilo na  kuongeza kuwa, wananchi wengine bado wanaweza kuwalipia faini hiyo ndugu zao. 

Hata hivyo Mrema alisema  mpango huo ulilenga kupunguza msongamano magerezani na kuipunguzia Serikali gharama za kuwahudumia wafungwa hivyo kusitisha unarudisha nyuma juhudi za Bodi hiyo ya Parole katika kuwasaidia wafungwa waliokizi vigezo

PROF. MBARAWA AHIMIZA SEKTA BINAFSI KUWEKEZA NCHINI

0
0
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa akiteta na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Bi. Tonia Kandiero, wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 10 wa Mashauriano wa wadau wa Sekta ya Uchukuzi, jijini Dar es Salaam.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi), Dkt. Leonard Chamuriho akitoa hotuba wakati wa Ufunguzi wa mkutano wa 10 wa Mashauriano wa wadau wa Sekta ya Uchukuzi, jijini Dar es Salaam.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Eng. Joseph Nyamhanga akitoa hotuba wakati wa Ufunguzi wa mkutano wa 10 wa Mashauriano wa wadau wa Sekta ya Uchukuzi, jijini Dar es Salaam.
 Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB), Bi.  Tonia Kandiero, akitoa hotuba wakati wa Ufunguzi wa mkutano wa 10 wa Mashauriano wa wadau wa Sekta ya Uchukuzi, jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa akifungua mkutano wa 10 wa Mashauriano wa wadau wa Sekta ya Uchukuzi, jijini Dar es Salaam.
 Washiriki wa Mkutano wa 10 wa  Mashauriano  wa wadau wa Sekta ya Uchukuzi wakimsikiliza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa  mkutano huo, jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa akiwa katika picha ya pamoja na wadau wa maendeleo alipofungua mkutano Mkutano wa 10 wa  Mashauriano  wa Sekta ya Uchukuzi, jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amewataka wadau wa Sekta binafsi kujitokeza na kushirikiana na Serikali katika uwekezaji wa ujenzi wa miradi ya usafirishaji nchini.

Aidha amewataka wadau hao kuendelea kufadhili utekelezaji wa miradi ya maendeleo iliyo chini ya sekta hiyo ili kuchochea fursa za maendeleo.
Hayo ameyasema wakati akifungua mkutano wa 10 wa mashauriano wa wadau wa Sekta ya Uchukuzi na usafirishaji uliofanyika jijini Dar es Salaam. 
“Michango ya Sekta binafsi inahitajika kwa kiasi kikubwa pamoja na Serikali kuendelea kutenga fedha za utekelezaji wa miradi ya maendeleo”, amesema Prof. Mbarawa.

Prof. Mbarawa amesema kuwa mafanikio ya malengo ya mwaka jana ya mkutano huo yamepelekea Serikali kupitia sekta hiyo kuboresha usafiri wa anga kwa kununua ndege mbili za Bombadier Q400 mwaka huu.
Ameongeza kuwa kwa sasa Serikali ipo katika hatua za awali za ununuzi wa ndege nyingine tatu ambazo ndege ya kwanza itawasili Mwezi Julai mwakani na nyingine mbili zitawasili mwezi Mei na Septemba 2018.

“Mapitio ya mkutano wa 9 ni matunda ya upatikanaji wa ndege za Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), hivyo mikutano kama hii ina tija kwani inaisaidia kuboresha hali ya miundombinu nchini”, amefafanua Waziri Prof. Mbarawa.
Amesisitiza wadau kutumia mkutano huo kama chachu ya kupata maoni na mawazo mapya ambayo yatasaidia katika kufanikisha uboreshaji wa Sera, Sheria  na kanuni za sekta ya usafarishaji nchini.“Tumieni mkutano huu kujadili na kushauriana ili kupata majawabu yatakayosaidia kutatua changamoto zilizopo katika Sekta hii”, amesema Prof. Mbarawa.

Naye, Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Bi. Tonia Kandiero ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo katika uboreshaji na ukuzaji wa Sekta ya Usafirishaji ambayo ni kiungo kikubwa katika kukuza pato la Taifa.
Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo (Sekta ya Uchukuzi), Dr. Leonard Chamuriho amesema kuwa anaimani mkutano huo utasaidia kutatua changamoto za miradi mbalimbali iliyokuwa ikisuasua katika Sekta yake.

Katibu Mkuu wa Wizara hiyo (Sekta ya Ujenzi), Eng. Joseph Nyamhanga amesema kuwa sekta yake imefanikiwa kuunganisha kwa kiwango cha lami barabara zote ndani ya mikoa na nchi jirani ambapo kwa sasa sehemu iliyobaki ni kuunganisha ukanda wa Magharibi.

Amezitaja barabara ambazo zipo katika ukanda huo kuwa ni Manyoni-Tabora-kigoma, Kigoma-Kidahwe-Kasulu, Kibondo-Nyakanazi, Sumbawanga-Mpanda-Uvinza-Kasulu, Tabora-Koga-Mpanda, Mbeya-Chunya-Makongorosi-Rungwe na Itigi mpaka Mkiwa.Mkutano huo wa siku moja umewashirikisha wadau wa Sekta ya Uchukuzi na wafadhili mbalimbali katika kujadili miradi na utekelezaji wake pamoja na kutafuta suluhu za changamoto zinazoikabili sekta.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

SERIKALI YAOMBWA BAJETI KUSAIDIA PASADA NA WENGINE

0
0
SERIKALI imeombwa kutengeneza bajeti ya kusaidia taasisi mbalimbali zinazojishughulisha na kusaidia watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI ikiwa ndio njia ya kuhakikisha huduma kwa waathirika hao zinaendelea kuimarika.

Imeelezwa kuwa ingawa serikali ndiyo inayotoa dawa za kufubaza makali ya UKIMWI ARVs, haitengenezi bajeti kwa ajili ya wafanyakazi wanaohudumia waathirika kisaikolojia na kitiba.

Hoja hiyo imetolewa na Meneja mradi wa Pastoral Activities and Services for People with AIDS Dar es Salaam Archdiocese (PASADA) Jovin Riziki wakati akijibu maswali katika mkutano na ujumbe wa nchi za jumuiya ya NORDIC waliotembelea makao makuu ya PASADA yaliyopo Chang’ombe, Temeke Dare s salaam kuangalia miradi mbalimbali ya kijamii inayofadhiliwa na UNICEF.

Nchi za Jumuiya ya Nordic ni wafadhili wakubwa wa miradi inayoendeshwa na Mashirika ya Umoja wa Mataifa hapa nchini.
Meneja mradi wa Pastoral Activities and Services for People with AIDS Dar es Salaam Archdiocese (PASADA) Jovin Riziki (kushoto) akitoa maelezo kwa sehemu ya ujumbe kutoka nchi za Nordic ulioambatana mwenyeji wao Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (wa pili kulia) katika chumba cha kuhifadhia kumbukumbu za wagonjwa ulipotembelea kwenye kituo hicho cha PASADA jijini Dar es Salaam. Kulia ni kiongozi wa ushirikiano wa kimataifa wa Shirika la Misaada la Sweden (SIDA), Anders Rönquist.(Habari picha na Zainul Mzige wa Modewjiblog)

Akijibu swali nini ambacho atataka kumweleza Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akikutana naye, Riziki alisema kwamba angelipenda kuona serikali inawajibika kusaidia huduma katika taasisi mbalimbali zinazoigusa jamii zinaendelea kutolewa.

Alisema asasi zinazosaidia waathirika wa UKIMWI kama hiyo ya PASADA hutegemea asilimia 100 misaada ya nchi na wafadhili wa kigeni ambapo miradi ikimalizika mara nyingi waliokuwa wanahudumiwa hukosa mahali pa kupata misaada iliyokuwa inawawezesha kuendelea kuishi kiutu kwa kuwa na siha njema na kufanya shughuli za kiuchumi.
Meneja mradi wa Pastoral Activities and Services for People with AIDS Dar es Salaam Archdiocese (PASADA), Jovin Riziki (kushoto) na ujumbe kutoka nchi za Nordic ulioambatana mwenyeji wao Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (kulia) wakipata maelezo kutoka kwa mtoa huduma katika kitengo cha dawa za kupunguza makali ya Virusi vya UKIMWI ARV's ulipotembelea kwenye kituo hicho cha PASADA jijini Dar es Salaam.

Alisema kuna changamoto kubwa kuhudumia wagonjwa zaidi ya elfu 21 wengine wakiwa kufani majumbani bila kuwa na mtaji wa kutosha hasa malipo kwa watoa huduma ambao ni wataalamu.

“Ipo haja ya serikali kuchangia kazi hii ya kibinadamu hasa fedha kwa ajili ya kulipa wataalamu na kuendeleza miradi ambayo inasaidia jamii moja kwa moja” alisema huku akiongeza kwamba kwa sasa mathalani wanaendelea kufanya mazungumzo na watu mbalimbali kuendeleza mradi uliokuwa ukisaidiwa na USAID.

Alisema Septemba mwaka huu USAID wamemaliza mchango wao wa mradi muhimu ambao ndani yake ulikuwa unawasaidia waathirika katika elimu, tiba na pia kiuchumi.
Ujumbe huo ukiwa kwenye mazungumzo na vijana wanaoishi na VVU ambao wamepata mafunzo ya ujasiriamali yaliyowawezesha kujiajiri kwa kufanya biashara ndogo ndogo zinazowapatia kipato cha kusaidia familia zao na mahitaji yao madogo madogo.

Alisema mara nyingi kunapoendeshwa mradi ambao ndani yake watu wanawezeshwa kiuchumi hujitokeza kwa wingi na hivyo kama serikali ikitenga bajeti maana yake watu hao watafika kupata elimu na pia kufufua matumaini ya maisha kwa kuwezeshwa kiuchumi.

PASADA iliyoanza Agosti 1992 wakati kundi dogo la watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI kujikusanya ili kupata msaada wa pamoja sasa hivi ina wateja 36,000, ikitoa huduma za upimaji kwa watu 10,000 kila mwezi.

Aidha PASADA ambayo imekuwa ikikua ikitegemea fedha za wahisani imekuwa ikiwafikia watu walio majumbani ambao hawawezi na waliokufani kuwapatia huduma za kibinadamu.
Ujumbe kutoka nchi za Nordic ulioambatana mwenyeji wao Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (hayupo pichani) wakipata maelezo nje ya eneo la vipimo katika kituo cha PASADA.

Ingawa PASADA ipo chini ya kanisa katoliki huduma zake hupatikana kwa kila mwananchi bila ubaguzi na huendesha pia huduma za elimu kuhusu afya ya uzazi, ujana na maradhi ya UKIMWI.

Sehemu kubwa ya elimu ni kuondoa unyanyapaa na kuhimiza wananchi kupima afya zao. Aidha elimu imelenga watu kubadilika tabia.

Ikiwa na watu wazima 3000 wanaotumia dawa na watoto 600, PASADA imesema kwamba bado inakabiliwa na changamoto kubwa hasa pale ambapo wahisani wanapojitoa kusaidia miradi iliyopo ya elimu na kiuchumi.

Aidha PASADA imekuwa ikipambana kwa kusaidiana na wadau wengine kuhakikisha kwamba haki za msingi za wenye virusi vya UKIMWI hazikiukwi.
Meneja mradi wa Pastoral Activities and Services for People with AIDS Dar es Salaam Archdiocese (PASADA), Jovin Riziki akiongoza ujumbe kutoka nchi za Nordic ulioambatana watalaam kutoka mashirika ya Umoja wa Mataifa pamoja na mwenyeji wao Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (wa pili kulia) kutembelea vitengo mbalimbali vinavyotoa huduma kituo cha PASADA jijini Dar es Salaam.

Ikiwa imefanikiwa kupunguza maambukizi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto kwa asilimia 97, huku ikiwa imefikia asilimia 4 ya waathirika nchini na kwa mikoa ya Dar es salaam na Pwani asilimia 30, PASADA ikiwa na wafanyakazi 140 inahitaji sana uhakika wa bajeti na serikali ndiyo inayoweza kutoa kwa kuwa kazi inayofanywa na serikali kupitia vituo vya umma ndiyo inafanywa na PASADA.

Ujumbe huo wa NORDIC ambao ulikujwa na wenyeji wao Mashirika ya Umoja wa Mataifa ulielezea kuridhishwa kwake na kazi inayofanywa na PASADA na kusema ipo haja kwa wadau kushirikiana kurejesha heshima ya binadamu na kufanya serikali kuwajibika kwa watu wake.

Naye Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa ambaye ndiye mwenyeji wa ujumbe huo unaopita katika miradi mbalimbali serikalini na hata katika taasisi binafsi, Alvaro Rodriguez, alisema kuna changamoto nyingi katika kusaidia wananchi katika maradhi yanawasibu kwa sababu ni kazi ya kibinadamu zaidi na wala si ya kimaendeleo.
Ziara ya ujumbe kutoka nchi za Nordic ulioambatana watalaam kutoka mashirika ya Umoja wa Mataifa ikiendelea kutembelea vitengo mbalimbali vinavyotoa huduma za afya kwa watu wanaoishi na VVU kituo cha PASADA jijini Dar es Salaam.

Alisema hata hivyo ili kuwa na haki sawa mashirika ya Umoja wa Mataifa yamekuwa yakisaidia kupatikana kwa haki za maisha kwa kusaidia mambo kadhaa ambayo hayana uhusiano wa moja kwa moja na wagonjwa lakini yakiwa na mchango mkubwa katika afya na shughuli za uzalishaji mali.

Alisema amefurahishwa na ziara ya ujumbe huo wa Nordic ambao ni wafadhili wakubwa wa miradi mbalimbali yenye lengo la kuwezesha uwajibikaji na utawala bora nchini ikiwemo misaada ya kibinadamu.

Alisema ni kazi ya mashirika ya Umoja wa Mataifa kushawishi mabadiliko ya kitamaduni ili kujiweka sawa katika shughuli za maendeleo.
Ujumbe kutoka nchi za Nordic ulioambatana watalaam kutoka mashirika ya Umoja wa Mataifa ukiwa katika eneo maalum lililotengwa na kituo cha PASADA kwa ajili ya watoto kufanya michezo mbalimbali walipofanya ziara kituoni hapo. 
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (kulia) akibadilishana mawazo na kiongozi wa ushirikiano wa kimataifa wa Shirika la Misaada la Sweden (SIDA), Anders Rönquist wakati wa ziara ya kutembelea vitengo mbalimbali katika kituo kinachohudumia watu wanaoishi na VVU, PASADA jijini Dar es Salaam.
Meneja mradi wa Pastoral Activities and Services for People with AIDS Dar es Salaam Archdiocese (PASADA), Jovin Riziki akitoa historia fupi ya kituo hicho pamoja na changamoto zinazowakabili katika kuhudumia watu wanaoishi na VVU nchini kwa ujumbe kutoka nchi za Nordic ulioambatana watalaam kutoka mashirika ya Umoja wa Mataifa ulipotembelea kituo hicho.
Sehemu ya ujumbe huo ukimsikiliza Bwana Jovin Riziki.
Kiongozi wa ushirikiano wa kimataifa wa Shirika la Misaada la Sweden (SIDA), Anders Rönquist akifafanua jambo wakati wa kutoa mrejesho baada ya ziara ya kutembelea vitengo mbalimbali katika kituo cha PASADA jijini Dar es Salaam.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akitoa neno la shukrani kwa uongozi wa PASADA baada ya ziara ya kutembelea kituo hicho na kujionea changamoto zinazowakabili.

Rais magufuli atia saini sheria ya huduma za habari ya mwaka 2016

0
0

VIJANA WA KITANZANIA KUPEWA ELIMU YA UJASIRIAMALI KUTOKA THUD YA NCHINI AFRIKA KUSINI

0
0
                                  Na Zainab Naymka, Globu ya Jamii.

THE Africa Entrepreneurship Compass (AEC) kutoka nchini Tanzania kwa kushirikiana na The Hook Up Dinner (THUD) kutoka Afrika Kusini wamedhamiria kutoa elimu wa vijana kuhusiana na ujasiriamli pamoja na kukutana nao kwa pamoja ili kufahamu changamoto wanazokutana nazo.

Ujio huo unakuwa ni kwa mara ya kwanza kuja hapa Tanzania na tayari wameshawasili nchini wakiwa viijana kumi na mbili kutoka Afrika Kusini na wanatarajia kufanya uzinduzi wa THUD nchini kesho huku Mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Waziri wa Viwanda na Uwekezaji Charles Mwijage pamoja na Mkurugenzi wa makampuni ya Mohamed Enterprises, Mohamed Dewji.

THUD ni jumuiko kubwa la wajasiriamali kwa lengo la kuunganisha wajasiriamali wasiopungua milioni moja duniani hususani barani Afrika na  ilianzishwa mwaka 2012  Kijana Selebogo Molefe na mpaka sasa imeshajikita katika nchi kadhaa ambzo ni Afrika Kusini, Zimbabwe, Botswana, Lesotho, Kenya, Israel, Australia, Msumbiji, Hull City Uingereza, Zambia na Mauritius. 

AEC iko chini ya mtanzania Fay Nicholaus Shao imelenga zaidi kuwaunganisha wajasiriamali na kuunganisha nchi kulingana na mahitaji mara ya kwanza sasa Tanzania na  inatarajia kuwaunganisha wajasiriamali na fursa zilizopo kwenye uwekezaji Afrika na Dunia ikiwa inalenga na kutegemea kuwaleta pamoja wajasiriamali wasiopungua milioni moja.
siriamali wasiopungua milioni moja.

Safari hii isingewezekana kama si kwa ushirikiano wa hali ya juu na wa kipekee wa Ubalozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini, Naibu Balozi Mama Rosemary Chambe Jairo, Wizara ya Mambo ya Nje na idara ya Diaspora Uratibu na Habari inayosimamiwa Matukio Chuma

Naye Moja ya wawakilishi wa THUD Tanzania ambaye ni mtanzania anayeishi Afrika Kusini Baraka Mtavangu amesema kuwa THUD  iko tayari na wamewasili  na uzinduzi rasmi utakuwa Novemba 18 mwaka huu na  wajasiriamali wote wanakaribishwa kwani hakuwatuwa na kiingilio chochote  pia anawshukuru sana  SAB South Africa Kickstart kwa kusaidia ujio huu nchini Tanzania.
 Muanzilishi wa The Hook Up Dinner (THUD)Selebogo Molefe (Kulia) akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kuhusiana na uzinduzi wa THUD nchini Tanzania unaotarajiwa kufanyika kesho. Kushoto ni mwakilishi wa THUD Tanzania Baraka Mtavangu.
 Mratibu wa habari wa Wizara ya Mambo ya Nje na idara ya Diaspora Matukio Chuma akizungumza na waandishi wa habari juu ya ujio huo ambao utakuja kuwa na mafufaa kwa vijana hususani wajasiriamali wa hapa nchini.

Sikinde yawaandalia mashabiki onyesho maalumu Novemba 27,litafanyika DDC Kariakoo

0
0
BENDI ya muziki wa dansi ya Mlimani Park Orchestra, imewaandalia mashabiki wake onyesho maalumu litakalojulikana kwa jina la 'Usiku wa

Sikinde'.

Onyesho hilo, ambalo limelenga kuwakumbusha mashabiki nyimbo za zamani za bendi hiyo na mpya, linatarajiwa kufanyika Novemba 27, mwaka huu, kwenye ukumbi wa DDC Kariakoo, Dar es Salaam.

Akizungumza mjini Dar es Salaam, jana, Mratibu wa onyesho hilo, Rashid Zahor, alisema maandalizi yote muhimu yanakwenda vizuri, ikiwa ni pamoja na bendi hiyo kuzifanyia mazoezi ya nguvu baadhi ya nyimbo za zamani.

"Hili ni onyesho maalumu kwa watu maalumu, ndio sababu tumelipa jina la 'Usiku wa Sikinde', kwa sababu tunataka kuwakumbusha mashabiki, zile enzi bendi ilipokuwa ikitamba kwa miondoko hiyo,"alisema Zahor.

Alizitaja baadhi ya nyimbo adimu zitakazopigwa kuwa ni pamoja na Celina, Maudhi, Taraka rejea, Clara, Christina Bundala, Hiba, Barua kutoka kwa mama, Chenga ya mwili, Dua la kuku, Sitokubali kuwa mtumwa, Mtoto akililia wembe, Cenjesta, Epuka jambo lisilokuhusu na nyinginezo.

Aidha, Zahor alisema bendi hiyo pia itatumia fursa hiyo kutambulisha baadhi ya nyimbo zake mpya na zile zilizorekodiwa katika albamu ya hivi karibuni, inayojulikana kwa jina la Jinamizi la talaka.

Nyimbo hizo ni Jinamizi la Talaka, Za mkwezi mbili, Nikipata nitalipa,
Kibogoyo, Dole gumba, Ng'ombe haelemewi, Nundu, Tabasamu, Supu umeitia nazi na Wali nazi.Kwa mujibu wa Zahor, wakati wa onyesho hilo, mashabiki wataruhusiwa kuomba nyimbo watakazotaka kupigiwa na pia kutatolewa zawadi mbalimbali kwa watakaovutia kwa mavazi na kujimwayamwaya vizuri. 

Mratibu huyo alisema onyesho hilo limedhaminiwa na Kampuni ya Isere Sports, inayojihusisha na uuzaji wa vifaa mbalimbali vya michezo, gazeti la Burudani na kituo cha Redio Uhuru.Kwa upande wake, kiongozi wa bendi hiyo, Abdalla Hemba, aliwahakikishia mashabiki kwamba, watapata burudani murua na adimu, ambayo hawataisahau katika maisha yao.

Alisema wameshaanza kuzifanyia mazoezi baadhi ya nyimbo za zamani ili kuwapa mashabiki ladha halisi na kwamba, hakutakuwa na tofauti 
licha ya wanamuziki wengi wa zamani kutokuwepo kwenye bendi hiyo kwa sasa. Hemba amewataka mashabiki kujitokeza kwa wingi kwenye onyesho hilo ili kuiunga mkono bendi yao, ambayo imekuwa mstari wa mbele kukuza na kuendeleza muziki wa dansi wa miondoko ya asili. 

Aidha, kiongozi huyo wa Sikinde alisema watalitumia onyesho hilo kumkaribisha tena jukwaani mwimbaji nyota nchini, Hassan Bicthuka, ambaye alipumzika kutokana na kuwa mgonjwa.

Mlimani Park Orchestra ilianzishwa 1978 na lililokuwa Shirika la Usafiri na Huduma za Taksi (TTTS), kwa lengo la kutoa burudani kwa mashabiki. Shirika hili lilikuwa mali ya serikali.TTTS iliacha kuiendesha bendi hiyo mwaka 1982, ikachukuliwa na Shirika la Uchumi na Maendeleo la Mkoa wa Dar es Salaam (DDC). Kuanzia wakati huo, bendi ilibadilishwa jina la kuitwa DDC Mlimani Park Orchestra.

Mwaka 2010, uongozi wa DDC uliamua kujitoa kuiendesha bendi hii na kukabidhi vyombo kwa wanamuziki ili waweze kujiendesha. Tangu wakati huo, bendi hii imekuwa ikiendeshwa na wanamuziki wenyewe na kuchagua viongozi kila baada ya miaka miwili.

Baadhi ya wanamuziki waliowahi kuiongoza bendi hii ni marehemu Michael Enock, Muhidin Gurumo, Bennovilla Anthony, marehemu Nasir Lubua, Shabani Dede, Hussein Jumbe, Habibu Abbas 'Jeff' na Hemba.

TAHADHARI YA UGONJWA WA KIPINDUPINDU

0
0


Mkuu wa Wilaya ya Arusha ametoa angalizo kwa wananchi wote kuhusu tahadhari ya mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu ambao umeripotiwa kuwepo katika Mikoa mbalimbali na maeneo ya jirani na Wilaya hii.

Akizungumza kwenye kikao maalumu na watendaji wa Kata, Maafisa Afya pamoja na wadau wa Afya Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe. Alexander Mnyeti ameelezea hatua ambazo Serikali ya Wilaya imechukua hadi hivi sasa kudhibiti mlipuko wa ugonjwa kuwa ni:

-         Kuandaa kambi maalumu kwa ajili ya wagonjwa watakaojitokeza –ipo katika Kituo cha Afya Levolosi
-         Kuagiza dawa na vifaa tiba kwa ajili ya tahadhari ya ugonjwa 
-         Kusambaza  mabango, vipeperushi na miongozo  katika vituo vua kutolea huduma za afya, Ofisi za Kata na mitaa pamoja na maeneo ya mikusanyiko
-         Kufanya kikao na wadau wote na kuunda timu ya usimamizi wa mlipuko wa kipindupindu.

Kupitia kikao hiki kwa kauli moja wajumbe walikubaliana hatua za kuchukua ili kupambana na mlipuko:
-         Kuhakikisha upatikanaji wa maji safi  kwenye maeneo yote yenye uhaba wa maji
-         Kuchukua Sampuli za maji katika Kata za pembezoni
-         Kupiga marufuku uuzaji wa matunda yaliyomenywa,vyakula barabarani na pombe za kienyeji
-         Kutembelea kaya na kukagua uwepo wa vyoo na matumizi yake
-         Kugawa vidonge vya Kutibu maji kwenye kila  Kaya
-         Kuwachukulia hatua wote watakaokiuka wa kanuni za Afya 

Pia wananchi walishauriwa kujikinga na ugonjwa huu kwa njia zifuatazo;
-         Kunywa maji yaliyochemchwa au yaliyowekewa dawa ya kuua vimelea 
-         Kula chakula cha moto kilichotayarishwa katika hali ya Usafi. 
-         Kunawa mikono kwa sabuni na maji ya kutitirika (usinawe ndani ya chombo).
-         Kuhakikisha matumizi bora ya choo na kinyesi cha watoto wadogo  kitupwe chooni
-         Kuepuka kula matunda bila kuyaosha na kunywa juisi na vyakula vinavyouzwa kiholela. 
IMETOLEWA NA                            
Nteghenjwa Hosseah
Afisa Habari, Halmashauri ya Jiji
Arusha.
17  Novemba ,2016

BANK OF AFRICA - TANZANIA (BOA) YAZINDUA PROGRAMU MPYA YA MIKOPO YA UJENZI WA NYUMBA ‘WEZESHA’

0
0
Kutoka kushoto ni Ibrahim Samuel- Meneja Uhusiano- Mikopo ya Nyumba, Wasia Mushi- Naibu Mkurugenzi Benki ya Afrika Tanzania (BOA), na Muganyizi Bisheko- Meneja Masoko Utafiti na Maendeleo wakiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani).
Kutoka kushoto ni Beatrice Mirigo- Marketing executive, Ibrahim Samuel- Meneja Uhusiano- Mikopo ya Nyumba, na Wasia Mushi- Naibu Mkurugenzi Benki ya Afrika Tanzania (BOA) wakiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani).

BANK OF AFRICA- TANZANIA leo imezindua aina mpya ya mkopo wa ujenzi wa nyumba unaoitwa ‘WEZESHA’ ambapo mtu anaweza kukopa kiasi cha shilingi milioni 40 hadi 500 kwa mrejesho wa miaka hadi 25 bila utaratibu wa kutoa malipo yoyote ya awali.

Akizungumzia progamu hiyo, Naibu Mkurugenzi wa BANK OF AFRICA- TANZANIA bwana Wasia Mushi alisema, ‘programu hii ya mkopo wa ujenzi wa makazi mapya unawapa uwezo wateja wetu kubuni nyumba zao kadiri wanavyopenda, kulingana na mahitaji yao na ndani ya bajeti zao. Kwa kiwango kidogo kabisa cha riba na katika viwango vya punguzo, Bank ya Afrika pia imetengeneza mazingira rafiki na kuondoa usumbufu kwa mteja pindi anapohitaji mkopo huu’

Aidha, huduma ya mkopo ya ‘Wezesha’ inapatikana kwa watu wote wenye mishahara katika sekta za umma na binafsi, na kwa kutoa muda wa miaka 25 ya kulipa deni, mkopaji atapata uhuru zaidi pindi atakapochukua mkopo.

Mpango wa huu wa ‘Wezesha’ kujenga makazi unalenga kutoa suluhu kwa changamoto za makazi zinazowakabili watanzania wengi ambao kwa mazingira ya kawaida hutumia zaidi ya miaka 10-15 kujenga nyumba ya kawaida ya kuishi.

Fursa hii ya kutatua changamoto ya makazi kwa watanzania wengi, inaendana na ongezeko kubwa la watu kupata ardhi iliyopimwa, hivyo kuwapa watu nafasi ya kujenga nyumba wanazozitaka kwa masharti nafuu na rahisi ambapo kwa kuanzia mteja atatakiwa kuwa na kiwanja ambacho nyumba hiyo itajengwa.

Kwa mujibu wa takwimu, Tanzania ina uhaba wa nyumba kwa ajili ya makazi zaidi ya 3,000,000. Huku kukiwa na ongezeko la uhitaji huo kwa zaidi ya asilimia 1 kila mwezi.

Muganyizi Bisheko, Meneja Masoko Utafiti na Maendeleo wa BANK OF AFRICA-TANZANIA aliongeza kuwa, ‘Benki inatoa asilimia 100 ya ufadhili wa ujenzi ili watu wengi waweze kuumudu mkopo. Mara nyingi, hasa kwa mtu anayeanza maisha, kujiwekea akiba na kupata kiwango cha kulipia gharama za ujenzi wa makazi ni jambo gumu sana. Jambo hilo liliwezekana kwa wale wenye kipato kikubwa na endelevu, lakini kwa sasa, na kwa uwepo wa WEZESHA, si jambo gumu tena la kuchelewesha ndoto zako za kumiliki makazi ya kuishi, kwa kuweka akiba kwa miaka 2-5’

Aliongeza kuwa, ‘Mara mteja wetu anapopata mkopo wa makazi, yeye ndiye atachagua mkandarasi wa kujenga nyumba yake miongoni mwa makandarasi waliochaguliwa na BANK OF AFRICA- TANZANIA. Mkopo utatolewa kulingana na hatua za ujenzi, kama vile msingi, boma, paa, na umaliziaji. Na fedha hizo zitapelekwa kwenye akaunti ya Kandarasi anayejenga iliyofunguliwa kwenye Benki ya Afrika.Baada ya kukamilisha ujenzi, ripoti ya mkaguzi wa ubora itakabidhiwa kabla ya fedha za hatua nyingine ya mkopo kutolewa’

Kwa mara ya kwanza BANK OF AFRICA- TANZANIA ilizindua mkopo wa nyumba mwaka 2011 ambao ulikuwa unajumuisha mkopo wa ununuzi wa nyumba pamoja na uboreshaji wa nyumba. Toka mkopo ulipoanza kutolewa zaidi ya shilingi bilioni 10 zimeshatolewa.

Pamoja na mikopo ya nyumba, BANK OF AFRICA- TANZANIA pia imekuwa ikitoa mikopo kwa wakandarasi wa ujenzi ili kuongeza upatikanaji wa nyumba bora za makazi na wakati huo huo wakiwezesha watu wa kawaida kuzinunua nyumba hizo.

Taasisi ya Vijana ya TYVA na IRI Zatoa mafunzo kwa vijana kuhusu Mchakato wa mabadiliko ya katiba katika wilaya nne

0
0

Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba Tanzania Bw, Deus Kibamba akitoa elimu kuhusu mchakato wa mabadiliko ya Katiba pamoja na historia ya mchakato huo kwa vijana wa wilaya ya Chamwino mkoani  Dodoma.
Afisa wa IRI, Tony Alfred akizungumza jambo wakakati wa mafunzo ya mchakato wa mabadiliko ya Katiba kwa vijana wa wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma.
Makamu mwenyekiti wa TYVA, Kamala Dickson akizungumza jambo kwenye mkutano huo
Baadhi ya Vijana wa wilaya ya Chamwino wakiwa kwenye mafunzo kuhusu mchakato wa mabadiliko ya Katiba.

Katibu Mtendaji wa TYVA Saddam Khalfan akitoa ufafanuzi kuhusu shirika hilo wakati wa mafunzo hayo.
Baadhi ya Vijana wa wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam wakiwa kwenye mafunzo kuhusu mchakato wa mabadiliko ya Katiba
Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba Tanzania Bw, Deus Kibamba akitoa elimu kuhusu mchakato wa mabadiliko ya Katiba pamoja na changamoto zake kwa vijana wa wilaya ya Tanga Mjini mkoani  Tanga.

Mmoja wa washiriki akichangia mada
Kijana mwenye ulemavu wa ngozi akisoma katiba ya Tanzania kwa makini sana wakati wa  mafunzo kuhusu mchakato wa mabadiliko ya Katiba yaliyofanyika Mjini Tanga.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo yaliyofanyika Tanga wakifuatilia mada

Na Mwandishi Wetu
Asasi Ya Vijana, Tanzania Youth Vision Association kwa Kushirikiana Na International Republican Institute zimetoa mafunzo ya kuboresha Uwezo wa Vijana kuhusu mchakato wa mabadiliko ya Katiba nchini katika Mikoa mitatu ilijumuisha Wilaya Nne, ikiwemo Kinondoni, Dodoma Mjini, Chamwino Na Tanga Mjini.

Mafunzo hayo yameweza kufikia vijana 500 kwa njia ya Warsha na Vijana aa wananchi zaidi ya 100,000 kupitia mitandao ya kijamii.

Lengo kuu la Mafunzo hayo ni kuongeza uelewa na ushiriki wa Vijana katika mchakato wa Mabadiliko ya Katiba. Katika ufunguzi wa mafunzo hayo, Katibu Mtendaji wa TYVA ndugu Saddam Khalfan alisema, TYVA inaamini Katiba ni Sheria mama na mwongozo ambao una uhusiano wa moja kwa moja na maisha yetu ya kila siku.

Alibainisha watu wengi wamekua wakisoma au kuisikia Katiba, na wengine wakidhani Katiba ni maalumu kwa ajili ya wanasheria au wasomi tu. Kuna uhusiano mkubwa kati ya Katiba bora ya Nchi, Demokrasia na Maendeleo ya Jamii.

Mwanaharakati Na Mtetezi wa HAKI za Binadamu ndugu Deus Kibamba alipata kuwaelezea washiriki wa mafunzo hayo historia ya mchakato wa mabadiliko ya Katiba, Ushiriki wa wananchi katika mchakato wa Katiba, hatua muhimu katika Mchakato wa utengenezaji Katiba, Mambo ya Msingi yaliyomo katika Katiba inayopendekezwa na Mambo muhimu kuelekea kura ya Maoni ya Katiba Inayopendekezwa.

Alidokeza pia, katika mchakato wa Katiba, hasa katika hatua ya Bunge la Katiba ulikosa maridhiano ya Kitaifa. kuna haja ya kuwepo mkutano wa kitaifa utajaowaleta wadau na jopo la wataalamu mbalimbali kwa ajili ya kunyambua yale mambo yanayoendelea kuleta ukakasi linapaswa kufanyika.

Ndugu Dickson Kamala ambaye ni Mtetezi wa HAKI za vijana na Makamu Mwenyekiti Wa TYVA aliwasilisha mada ya umuhimu wa Vijana kushiriki na kushirikiana katika mchakato wa mabadiliko ya Katiba ili kupata Katiba itayojali maslahi yao na ya Taifa kwa ujumla.

Afisa kutoka IRI, Tony Alfred aliwatarifu Vijana washiriki kusoma kuhusu Katiba na wanaweza kupata habari na taarifa zaidi kuhusu Katiba kwa kupitia ujumbe mfupi wa maandishi kwa kutuma Neno "Katiba yetu" Kwenda 0684996494.

NHC YAZINDUA TAASISI YA MAFUNZO YA UONGOZI KWA WATENDAJI WAKE

0
0
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu akizungumza na Mameneja wa Shirika ambao wapo katika mafuzo ya Uongozi yanayoendeshwa na Taasisi ya Uongozi ya NHC yanayotarajiwa kuchukua miaka mitatu yenye lengo la kuboresha utendaji na utekelezaji wa malengo ya Shirika kwa ufanisi unaopaswa.
Mshauri Mwelekezi wa Mafunzo ya Rasilimaliwatu, Zuhura Sinare Muro akizungumza na Mameneja wa Shirika ambao wapo katika mafuzo ya Uongozi yanayoendeshwa na Taasisi ya Uongozi ya NHC yanayotarajiwa kuchukua miaka mitatu yenye lengo la kuboresha utendaji na utekelezaji wa malengo ya Shirika kwa ufanisi unaopaswa.
Picha ya pamoja ya Mameneja wa Shirika ambao wapo katika mafuzo ya Uongozi yanayoendeshwa na Taasisi ya Uongozi ya NHC yanayotarajiwa kuchukua miaka mitatu yenye lengo la kuboresha utendaji na utekelezaji wa malengo ya Shirika kwa ufanisi unaopaswa.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu akizungumza na Mameneja wa Shirika ambao wapo katika mafuzo ya Uongozi yanayoendeshwa na Taasisi ya Uongozi ya NHC yanayotarajiwa kuchukua miaka mitatu yenye lengo la kuboresha utendaji na utekelezaji wa malengo ya Shirika kwa ufanisi unaopaswa.
Baadhi ya Mameneja wa Shirika la Nyumba la Taifa ambao wapo katika mafuzo ya Uongozi yanayoendeshwa na Taasisi ya Uongozi ya NHC yanayotarajiwa kuchukua miaka mitatu yenye lengo la kuboresha utendaji na utekelezaji wa malengo ya Shirika kwa ufanisi unaopaswa.

Baadhi ya Mameneja wa Shirika la Nyumba la Taifa ambao wapo katika mafuzo ya Uongozi yanayoendeshwa na Taasisi ya Uongozi ya NHC yanayotarajiwa kuchukua miaka mitatu yenye lengo la kuboresha utendaji na utekelezaji wa malengo ya Shirika kwa ufanisi unaopaswa.
Baadhi ya Mameneja wa Shirika la Nyumba la Taifa ambao wapo katika mafuzo ya Uongozi yanayoendeshwa na Taasisi ya Uongozi ya NHC yanayotarajiwa kuchukua miaka mitatu yenye lengo la kuboresha utendaji na utekelezaji wa malengo ya Shirika kwa ufanisi unaopaswa.
Baadhi ya Mameneja wa Shirika la Nyumba la Taifa ambao wapo katika mafuzo ya Uongozi yanayoendeshwa na Taasisi ya Uongozi ya NHC yanayotarajiwa kuchukua miaka mitatu yenye lengo la kuboresha utendaji na utekelezaji wa malengo ya Shirika kwa ufanisi unaopaswa.
Baadhi ya Mameneja wa Shirika la Nyumba la Taifa ambao wapo katika mafuzo ya Uongozi yanayoendeshwa na Taasisi ya Uongozi ya NHC yanayotarajiwa kuchukua miaka mitatu yenye lengo la kuboresha utendaji na utekelezaji wa malengo ya Shirika kwa ufanisi unaopaswa.
Baadhi ya Wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa ambao walifika kushuhudia mafuzo ya Uongozi yanayoendeshwa na Taasisi ya Uongozi ya NHC yanayotarajiwa kuchukua miaka mitatu yenye lengo la kuboresha utendaji na utekelezaji wa malengo ya Shirika kwa ufanisi unaopaswa.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu akizungumza na Mameneja wa Shirika ambao wapo katika mafuzo ya Uongozi yanayoendeshwa na Taasisi ya Uongozi ya NHC yanayotarajiwa kuchukua miaka mitatu yenye lengo la kuboresha utendaji na utekelezaji wa malengo ya Shirika kwa ufanisi unaopaswa.
Mshauri Mwelekezi wa Mafunzo ya Rasilimaliwatu, Zuhura Sinare Muro akizungumza na Mameneja wa Shirika ambao wapo katika mafuzo ya Uongozi yanayoendeshwa na Taasisi ya Uongozi ya NHC yanayotarajiwa kuchukua miaka mitatu yenye lengo la kuboresha utendaji na utekelezaji wa malengo ya Shirika kwa ufanisi unaopaswa.
Mshauri Mwelekezi wa Mafunzo ya Rasilimaliwatu, Profesa Kumbwaeli Salewi akizungumza na Mameneja wa Shirika ambao wapo katika mafuzo ya Uongozi yanayoendeshwa na Taasisi ya Uongozi ya NHC yanayotarajiwa kuchukua miaka mitatu yenye lengo la kuboresha utendaji na utekelezaji wa malengo ya Shirika kwa ufanisi unaopaswa.

TRA YAONGEZA MUDA WA KUBORESHA TAARIFA ZA WALIPAKODI HADI JANUARI 2017

0
0
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inapenda kuwashukuru wakazi wa Dar es Salaam kwa  kushiriki katika zoezi la kuhakiki Namba ya Utambulisho Mlipakodi (TIN).

Kutokana na mwitikio mkubwa wa wananchi kutaka kuhakiki taarifa zao, Mamlaka imeamua kuongeza muda wa uhakiki hadi tarehe 31 Januari, 2017. Pamoja na kuongeza muda wa uhakiki, Mamlaka pia imeongeza vituo vya kuhakiki

TRA pia inawakumbusha wananchi kuwa wale wenye TIN za biashara wanatakiwa kuhakiki katika ofisi za kodi Mkoa husika na wenye TIN zisizo za biashara (yaani TIN iliyotokana na maombi ya leseni ya udereva au ya kuingiza mzigo bandarini) wanaweza kuhakiki katika kituo chochote hapa Dar es Salaam.

Vituo vya uhakiki vilivyopo ni kama  ifuatavyo:
Pamoja na vituo hivyo, Mamlaka imeanzisha kituo kinachohama (Mobile Office) ambacho kinatoa huduma sehemu mbalimbali.  Ili kuongeza ufanisi, Mamlaka itaendelea kuboresha huduma zake kwa kuongeza vitendea kazi na vituo vingine vya kuhakiki.

Mwisho, Mamlaka inawasihi  wananchi kuepuka kutumia  Matapeli (Vishoka) kwani zoezi hili linamtaka mlengwa kufika mwenyewe kwenye kituo husika.

Kwa ufafanuzi zaidi tafadhali wasiliana na kituo cha huduma kwa walipakodi kwa kupiga simu za bure: 0800 780078 / 0800 750075 barua pepe: huduma@tra.go.tz

Pamoja Tunajenga Taifa Letu

Limetolewa na:
Idara ya Huduma na Elimu kwa Mlipakodi
TRA- Makao Makuu

TAMASHA LA TANO LA SIKU MBILI LA WATU WENYE ULEMAVU LAFUNGWA LEO JIJINI DAR.

0
0
 Afisa Mradi, Kitengo cha Kujenga Uwezo kutoka shirika lisilo la Kiserikali la  ‘The Foundation For Civil Society’ Nasim Losai, akitoa mada wakati wa ufungaji wa Tamasha la Tano la Watu wenye Ulemavu lililoanza jana Nov 16, 2016 kwenye Hoteli ya Blue Pearl Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam. Tamasha hilo limefungwa hii leo hayo. 
 Mkufunzi Mwelekezi, Salma Maoulid, akisimamia zoezi la maswali na majibu wakati wa kufunga Tamasha la Tano la Watu wenye Ulemavu lililoanza jana kwenye Hoteli ya Blue Pearl Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam.
 Afisa Uchumi Mwandamizi, Mchambuzi na Mipango, Andrea Aloyce, akitoa mada kwa washiriki wakati wa kufunga Tamasha la Tano la Watu wenye Ulemabu lililoanza jana Nov 16, 2016 kwenye Hoteli ya Blue Pearl – Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam.
 Mshereheshaji akiendelea kuongoza Tamasha hilo
 Mkurugenzi wa Kampuni ya Governance & Economic Policy Centre, Moses Kulaba, akitoa mada kwa washiriki wakati wa kufunga Tamasha la Tano la Watu wenye Ulemabu lililoanza jana Nov 16, 2016 kwenye Hoteli ya Blue Pearl – Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam. 
 Mkarimani akiwatafsiria walemavu Viziwi kila kilichokuwa kikizungumzwa ukumbini hapo
 Mshereheshaji akiendelea kuwachangamsha washiriki, ''Abunuasi aliwauliza Je mnajua lichowaitia?? wakajibu hapana, akwaambia basi kama hamjui basi rudini nyumbani, wakaru, Siku yapili Je mnajua nilichowaitia?? wakajibu Ndiyooo,akawaambi basi kama mnajua basi rudini nyumbani kwa sababu mnajua ninachotaka kuzungumza nanyi, ikabidi waondoke, Siku ya Tatu wakaja tena alipo wauliza Je mnajua nilichowaitia??? siku hiyo wakakubaliana kujigawa wengine wakasema Ndiyoooo, na wengine wakajibu Hapanaaaa, akawaambia basi sasa itabidi nyie mnaojua muwaambie hao wasiojua kile ninachotaka kuzungumza, kisha mrudi nyumbani'' kila mmoja akaguna na kuondoka mahala hapo kwa hasira....
 Mshiriki akiongozwa kuingia ukumbini.
 Waratibu wa Tamasha hilo wakiwa bize kuratibu yaliyokuwa yakiendelea ukumbini hapo wakati wa kufunga Tamasha hilo. 
 Mshiriki akiuliza swali.
 Sehemu ya washiriki wa Tamasha hilo wakifuatilia kilichokuwa kikiendelea ukumbini hapo.

INTRODUCING GALAXY CERTIFIED NEW SONG-TOP IN MY HEART

0
0

SHIRIKA LA NDEGE LA ETIHAD LAPANUA HUDUMA ZAKE ULAYA

0
0
                     Idara ya Usafirishaji Mizigo ya Shirika la Ndege la Etihad,  imeanzisha ndege tatu kwa ajili ya kuimarisha sekta ya usafirishaji bidhaa barani Ulaya.

Mwezi uliopita kitengo hicho kilianzisha ndege ya boing 777 kutoka East Midlands na Uwanja wa Ndege wa Stansted nchini Uingereza na kutokea Copenhagen nchini Denmark.

Makamu wa Rais, wa Idara ya Usafirishaji Mizigo ya Etihad, David Kerry alisema, ”Tumetekeleza mahitaji ya wateja wetu kulingana na umuhimu wa usafirishaji nje ya Ulaya, pia ndege zetu zina uwezo wa kutoa huduma kulingana na mazingira yaliyopo pindi inapohitajika.”

Alisema, “Huduma hizi mpya zitawaunganisha wazalishaji na wateja karibu ulimwenguni kote. Wazalishaji nchini Uingereza na Denmark sasa wanaweza kukutana na wateja wao waliopo Mashariki ya Kati kwa haraka zaidi ndani ya masaa 24.”
Mwendeshaji Mkuu wa uwanja wa Copenhagen Airport, Peter Krogsgaard alisema,” Tunayofuraha kwa Kitengo cha Usafirishaji cha Etihad Cargo kuanzisha shughuli zake katika Uwanja wa Ndege wa Copenhagen. Usafirishaji mizigo kwa njia ya anga ni muhimu zaidi kwa ukuaji wa haraka kibiashara kwa Wadenmak. Asilimia kubwa ya Wadenmark hutumia zaidi huduma za usafirishaji kwa njia ya anga ambao pia wengi wao ni ndege.

Copenhagen ni kitovu muhimu cha biashara kwa Ukanda wa Ulaya Kaskazini kwa usafirishaji wa mizigo kwa anjia ya anga na kimataifa kutokana na uwekezaji uliofanywa na shirika la ndege la etihad katika kuimarisha soko la kimaraifa.”

Safari hizi mpya zimewezesha kufikia tisa kwa ndege zinazofanya safari zake Ulaya. Tayari Kitengo cha Usafririshaji cha Etihad kimeifikia miji mingine Ulaya kama vile Amsterdam, Frankfurt (Frankfurt Main na Frankfurt-Hahn), Milan, Brussels pamoja na Zaragoza ikiwamo na huduma za usafiri wa anga kwa abiria katika maeneo mbalimbali barani Ulaya.

Umoja wa Ulaya ni miongoni mwa washirika muhimu wa kibiashara na Umoja wa Falme za Nchi za Kiarabu ambapo inakadiriwa biashara ya mafuta ya zaidi ya dola 65 za marekani ilifanyika mwaka 2015. Kwa mwaka huo huo Nchi za Falme za Kiarabu ilikuwa miongoni mwa nchi kubwa ikishika nafasi ya nane  inayofanya biashara na Ulaya huku Umoja wa Ulaya ikiwa ya 13 kwa kufanya biashara kimataifa kwa ujumla.

NEWS ALERT: RAIS AMTEUA DIWANI ATHUMANI KUWA RAS KAGERA NA ATEUA WENYEVITI WA BODI ZA TAASISI TANO AKIWEMO JAJI WARIOBA

0
0

NG’OMBE TATU NA MBUZI TATU ZATOLEWA KWA MABINGWA WA KATA ZOTE ZA TARAFA YA SADAN KWENYE MASHINDANO YA MGIMWA CUP

0
0

Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahamood Mgimwa na katibu wa chama cha mapinduzi (CCM) mkoani iringa Hassan Mtenga wakifuatila mchezo wa fainali katika kata ya Ikwea ambapo mshindi alipata ng'ombe mmoja na mshindi wa pili akipokea zawdi ya mbuzi mmoja ambapo zawadi zote hizo zimetolewa na mbunge huyo.
katibu wa chama cha mapinduzi (CCM) mkoani iringa Hassan Mtenga akikabidhi ng'ombe kwa mshindi wa kwanza katika kata ya Ikwea ambapo mshindi wa kwanza ilikuwa timu ya Ugenza FC walipata Ng’ombe mkubwa na mpira mmoja.

Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahamood Mgimwa na katibu wa chama cha mapinduzi (CCM) mkoani iringa Hassan Mtenga walipomkabidhi zawadi mshindi wa pili Ikwea FC mbuzi mmoja na mpira mmoja


Na Fredy Mgunda,Mafinga


MASHINDANO ya Mpira wa miguu yaliyodhaminiwa na Mbunge wa jimbo la mufindi kaskazini Mahamood Mgimwa yanayojulikana kama Mgimwa Cup yamefika tamati katika tarafa ya Sadan yenye kata tatu ambazo Ikwea,Sadan na Igombavanu na fainali zote zilifanyika katika kata husika ambapo kila mshindi wa kata alipata ng’ombe mmoja na mshindi wa pili alipata mbuzi moja,hivyo jumla ya ng’ombe tatu na mbuzi tatu zimetolewa katika tarafa ya Sada.

Katika fainali ya kwanza ilichezwa katika viwanja vya kijiji cha Ugenza iliyopo katika kata ya Ikwea ilishuhudiwa timu ya Ugenza FC wakiibamiza timu ya Ikwea FC kwa goli 1-0 katika mchezo wa vuta nikuvute.

Baada ya mchezo huo katibu wa chama cha mapinduzi mkoa wa Iringa Hassani Mtenga alikabidhi zawadi mbalimbali kwa washiriki wa michuano hiyo ambapo mshindi wa tatu ambaye ilikuwa timu ya Victoria FC alizawadiwa mipira miwili, mshindi wa pili Ikwea FC walipata mbuzi mmoja na mpira mmoja na mshindi wa kwanza ambaye ni Ugenza FC walipata Ng’ombe mkubwa na mpira mmoja.

Mtenga aliwaasa wachezaji kuithamini michezo kwa kuwa sasa ni ajira hivyo wanajukumu la kujituma na kuipa kipaumbe michezo na kuacha tabia za kukaa kwenye vijiwe na vilabu ambako wanapoteza muda kwa kujadili mambo yasiyo ya msingi.Akifunga mashindano hayo mbunge wa jimbo la Mufindi kaskazini Mahamood Mgimwa aliwaomba vijana hao wajiunge katika vikundi ili waweze kupata fedha kwa ajili ya kuanzisha miradi ya maendeleo ambapo itawasaidia kukuza uchumi wao na wa Taifa.

"Mimi kama Mbunge ambaye nimetokea katika kata hii nimevutiwa sana na ninaguswa na matatizo yanayowakabili vijana hasa katika ajira na michezo hii imefungua ukurasa mpya kwenu nawaomba vijana wote mjiunge katika vikundi ili tuweze kuwasaidia kwa kuwapatia fedha kwa ajili ya miradi mbalimbali,"alisema makilagi.

Mgimwa alisema kuwa ligi hiyo itakuwa ikichezwa kila mwaka huku shughuli za maendeleo kwa vijana hao zikiendelea kama alivyowaahidi kuwa atawatafutia fedha kwa ajili ya maombi yao waliyotoa kwa mbunge huyo.

Naye mgeni rasmi katika fainali ya kata ya Sadan Yohanies Kaguo ambaye ni mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (CCM) alishuhudia timu ya Kibada fc ikiibuka mshindi kwa kuifunga timu ya Ihanzutwa fc goli moja kwa bila na kuwakabidhi washindi ng’ombe mmoja na mshindi wa pili alikabidhiwa mbuzi mmoja.

Kaguo aliwataka wachezaji wa timu zote za kata ya Sadan kutunza vipaji vyao kwa kuwa ndio ajira yao na kuongeza kuwa serikali ya awamu ya tano chini ya Rais DR John Pombe Magufuli wamedhamili kuvithamini vipaji vyote nchini na kuvigeuza kuwa ajira kwao.

“Angalia wakina Thomas Ulimwengu,Mbwana Samatta na wachezaji wengi wanavyonufaika na vipaji vyao vya michezo hivyo na nyinyi mnatakiwa kujituma ili kufikia mafanikio waliofika baadhi ya hao wachezaji” alisema kaguo.

Kwa upande wa kata ya Igombavanu mgeni rasmi alikuwa katibu wa chama cha mapinduzi wilaya ya Mufindi (CCM) Jimson Mhagama naye alishudia timu ya Lugoda fc ikiibuka mshindi na aliikabidhi timu hiyo zawadi ya ng’ombe mmoja na mshindi wa pili alipewa mbuzi mmoja.

Mhagama alimpongeza mbunge wa jimbo la Mufindi Mahamood mgimwa kwa jitihada za kuinua na kuibua vipaji vipya kutoka kwenye jimbo lake."Kutoa ng’ombe mmoja na mbuzi mmoja kila kata sio jambo dogo linahitaji kujipanga sana hivyo mnapoona mashindano kama haya mnapaswa kuyakimbilia na kushiriki kikamili ili kuibuka washindi na kuweka historia kwa kuwa mabingwa" alisema mhagama

Mashindano ya Mgimwa cup yatafanyika katika tarafa zote za jimbo la Mufindi kaskazi na jumla ya ng’ombe kumi na moja na mbuzi kumi na moja zitatolewa kwenye jimbo la Mufindi kaskazini.

WAZIRI MWIGULU NCHEMBA AFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA UHOLANZI NA UMOJA WA FALME ZA KIARABU, JIJINI DAR ES SALAAM

0
0
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba akimfafanulia jambo Balozi wa Uholanzi nchini, Jaap Frederiks (katikati) wakati Balozi huyo alipomtembelea ofisini kwake, jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kujadiliana masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na Uholanzi. Kulia ni Eugene Gies ambaye ni Katibu wa Uchumi na Sera za Biashara wa Ubalozi huo nchini. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (katikati) akimsikiliza Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Balozi Simba Yahya alipokuwa anamfafanulia jambo Balozi wa Umoja wa Falme za Kiarabu, Abdulla Ibrahim Alsuwaidi (kulia) alipomtembelea Waziri Mwigulu ofisini kwake, jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kujadiliana masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya nchi hizo mbili. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (katikati) akimsikiliza Balozi wa Uholanzi nchini, Jaap Frederiks alipokuwa anamfafanulia jambo Waziri huyo ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo, walipokuwa wanajadiliana masuala mbalimbali ua ushirikiano kati ya Tanzania na Uholanzi. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Balozi Simba Yahya. Kulia ni Katibu wa Uchumi na Sera za Biashara wa Ubalozi huo nchini, Eugene Gies.  Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (kushoto)akimsindikiza Balozi wa Umoja wa Falme za Kiarabu, Abdulla Ibrahim Alsuwaidi mara baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliyofanyika katika ofisi ya Waziri Mwigulu, jijini Dar es Salaam leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (kulia) akimkaribisha ofisini kwake Balozi wa Uholanzi nchini, Jaap Frederiks kwa ajili ya kufanya mazungumzo naye kuhusu masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Uholanzi na Tanzania. Mazungumzo hayo yalifanyika katika ofisi ya Waziri huyo, jijini Dar es Salaam leo. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

MSAKO WA AZAM U-17 KUHAMIA MBEYA JUMAMOSI IJAYO

0
0
KLABU Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, inatarajia kuendelea na mpango wake wa kitaifa wa kusaka wachezaji wenye umri chini ya miaka 17 (U-17) Jumamosi Ijayo Novemba 19, mwaka huu (kesho) katika Uwanja wa Sokoine, jijini Mbeya kuanzia saa 1.00 asubuhi hadi saa 8.00 mchana.

Azam FC wikiendi iliyopita iliendesha zoezi hilo Dar es Salaam lililohudhuriwa na vijana 433 na kuchaguliwa saba pekee, na hivyo kufanya idadi kamili ya waliochaguliwa kwenye mchujo wa kwanza kufikia 50 miongoni mwa vijana 2,593 walisailiwa mpaka sasa katika maeneo manne ambayo Azam FC imeendesha zoezi hilo (Dar es Salaam, Tanga, Morogoro & Dodoma na Visiwani Zanzibar).

Mara baada ya zoezi hilo kukamilika kwenye maeneo yote, vijana wote watafanyiwa mchujo wa mwisho mwezi ujao katika Uwanja wa Azam Complex kabla ya timu hiyo kuundwa rasmi kwa vijana bora watakaofanya vizuri kuchukuliwa.

Vijana wanaotakiwa kuhudhiriwa zoezi hilo na wale walizaliwa kuanzia mwaka 2000, 2001, 2002, 2003 au 2004, ambapo uhakiki wa vyeti utafanyika kwa wale watakaochaguliwa.

Kwa majaribio mengine ya wazi katika maeneo mengine kuzunguka Tanzania yatatangazwa hivi karibuni.

WAZIRI MUHONGO AFANYA MAZUNGUMZO NA JICA

0
0
Na Veronica Simba.

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo amekutana na Ujumbe kutoka Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japani (JICA) na kufanya mazungumzo kuhusu maendeleo ya miradi mbalimbali ya sekta ya nishati nchini inayofadhiliwa na shirika hilo.

Kikao hicho kilifanyika Novemba 17 mwaka huu katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara na kuhudhuriwa na viongozi waandamizi kutoka sekta ya nishati ambao ni pamoja na Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Sekta ya Nishati, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo, Kaimu Kamishna wa Nishati na Masuala ya Petroli - James Andilile, Kaimu Kamishna Msaidizi wa Nishati Sehemu ya Petroli – Mwanamani Kidaya na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Mhandisi Kapuulya Musomba.
Ujumbe wa JICA uliongozwa na Mwakilishi wake Mkuu hapa nchini, Toshio Nagase.
 Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kushoto), akisisitiza jambo katika kikao baina yake na Ujumbe kutoka JICA. Kushoto kwake ni Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Nishati - Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo, Kaimu Kamishna wa Nishati na Maendeleo ya Petroli - James Andilile, Kaimu Kamishna Msaidizi wa Nishati Sehemu ya Petroli – Mwanamani Kidaya na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Mhandisi Kapuulya Musomba. 
 Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (Kulia), akiwasikiliza baadhi ya Maofisa kutoka JICA, wakati wakisaini Kitabu cha Wageni ofisini kwake baada ya kikao baina yao kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara hivi karibuni.
 Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Ujumbe kutoka JICA, walipomtembelea ofisini kwake hivi karibuni na kufanya mazungumzo kuhusu maendeleo ya miradi mbalimbali ya Sekta ya Nishati inayofadhiliwa na Shirika hilo hapa nchini.
 Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Digital Grid kutoka Japan, inayojishughulisha na usambazaji wa vifaa vya umeme wa jua hapa nchini, Bwana Akita (kulia), akielezea kuhusu utendaji kazi wa kampuni yake kwa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, watendaji mbalimbali wa Wizara na Taasisi zilizo chini ya Wizara pamoja na Ujumbe kutoka JICA.
Kaimu Kamishna wa Nishati na Masuala ya Petroli, James Andilile (mwenye tai nyekundu-kulia), akifafanua jambo kwa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, wakati wa kikao baina ya Waziri na Ujumbe kutoka JICA. Kulia kwa Waziri ni Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Sekta ya Nishati, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo.
Viewing all 46202 articles
Browse latest View live




Latest Images