Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46401 articles
Browse latest View live

BUNGE LAPITISHA MUSWADA WA SHERIA YA HUDUMA ZA HABARI

$
0
0

Na Jacquiline Mrisho na Eleuteri Mangi – MAELEZO, Dodoma.

Mkutano wa Tano wa Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania umepitisha rasmi Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari wa mwaka 2016 ambapo hatua inayofuata ni kuridhiwa na kusainiwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli ili uwe Sheria kamili ya nchi.

Muswada huo umepitishwa leo Bungeni mjini Dodoma ambapo mkutano huo uliongozwa na Mwenyekiti wa Bunge hilo, Mhe. Andrew Chenge.Wabunge walijadili Muswada huo kifungu kwa kifungu na kuunga mkono upitishwaji wake baada ya Waziri mwenye dhamana na habari kutoa hoja ili Muswada huo uweze kujadiliwa.

Akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kupitishwa Muswada huo, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye amewashukuru wadau wote walioshiriki katika kutoa maoni juu ya Muswada huo kwani ndiyo yamepelekea kukamilisha mchakato mzima wa Muswada huo.

“Kwa niaba ya Serikali napenda kuwashukuru wadau wote walioshiriki kwa namna moja au nyingine katika kuhakikisha tunatimiza malengo ya takribani miaka 20 iliyopita ya kuifanya taaluma hii ya habari kuheshimika kama zilivyo taaluma zingine”, alisema Waziri Nape.

Waziri Nape ameongeza kuwa kwa sasa Muswada huo umeshapitishwa hivyo kilichobaki ni utungaji wa Kanuni ambapo ameomba wadau wa tasnia ya habari kujitokeza kwa wingi kwa ajili ya kutoa maoni yatakayopelekea kuwa na kanuni zenye tija kwa wanahabari na taifa kwa ujumla.

Aidha, Mhe. Nape amewaasa wadau wa habari kuunganisha nguvu kwa pamoja hasa katika kipindi hiki ambacho Muswada huo umepitishwa pia amewataka wadau hao wasiruhusu mgawanyiko utokee kati yao bali washirikiane na Serikali katika kutekeleza wajibu wao wa kihabari kwa jamii.

Kwa upande wake Mwanasheria Mkuu wa Serikali George Masaju amesema kuwa Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari wa mwaka 2016 ni mwanzo mpya wa tasnia ya habari nchini ambapo amewaasa wadau wa habari wakiwemo waandishi wa habari kutambua kuwa haki mara zote huendana na wajibu, hivyo hakuna haki isiyo na wajibu.

Muswada huo uliopitishwa leo umejadiliwa na Bunge hilo kwa siku mbili ambapo kwa mara ya pili ulisomwa mbele ya Kamati ya Bunge zima na hatimaye kusomwa kwa mara ya tatu ili kukidhi hatua za utungwaji wa Sheria nchini.

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AMEONGOZA MATEMBEZI YA HISANI KWA AJILI YA KUSOMESHA WAUGUZI WAKUNGA

$
0
0

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akishiriki mazoezi ya viungo kabla ya kuanza kwa Matembezi ya Hisani kwa ajili ya kuchangia fedha za Mafunzo ya Wauguzi Wakunga kwenye viwanja vya Green Ground ,Oysterbay jijini Dar es Salaam
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akishiriki mazoezi ya viungo pamoja na umati uliojitokeza kabla ya kuanza kwa Matembezi ya Hisani kwa ajili ya kuchangia fedha za Mafunzo ya Wauguzi Wakunga kwenye viwanja vya Green Ground ,Oysterbay jijini Dar es Salaam
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (katikati) akiongoza Matembezi ya Hisani kwa ajili ya kuchangia fedha za Mafunzo ya Wauguzi Wakunga ambapo alitembea kwa kilometa 4.3 kuanzia viwanja vya Green Ground na kupitia barabara ya Toure na kurejea na barabara ya Msasani ,Oysterbay jijini Dar es Salaam wengine pichani ni Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (kushoto) na Mkurugenzi Shirika la AMREF Health Africa Dkt. Florence Temu (kulia). Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakazi wa jiji la Dar es salaam waliojitokeza kwenye Matembezi ya Hisani kwa ajili ya kuchangia fedha za Mafunzo ya Wauguzi Wakunga kwenye viwanja vya Green Ground ,Oysterbay jijini Dar es Salaam
Sehemu ya Umati uliohudhuria na kushiriki Matembezi ya Hisani ya Kusomesha Wauguzi Wakunga kwenye viwanja vya Green Ground.

..................................................................

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameongoza mamia ya wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam katika matembezi ya hisani ya kilomita 4.3 ya kuchangia fedha kiasi cha shilingi milioni 500 kwa ajili ya mafunzo ya wauguzi, wakunga 400 katika ngazi mbalimbali kupitia mafunzo ya kimtandao yaani e-learning nchini.

Akihutubia mamia ya wananchi waliojitokeza katika matembezi hayo katika viwanja vya Green Ground, Oysterbay Jijini Dar es Salaam, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amewahakikishia wananchi kuwa Serikali ya awamu ya Tano imeweka mikakati madhubuti ya kukabiliana na changamoto mbalimbali katika sekta ya Afya ikiwemo kupunguza vifo vya wanawake wajawazito na watoto kwa kuongeza idadi ya wataalamu wa Afya na kuimarisha miundombinu pamoja na upatikanaji wa dawa na vifaa tiba kote nchini.

Amesisitiza kuwa ili kuhakikisha huduma za Afya zinazotolewa kwa wananchi zinakuwa na ubora unaotakiwa Serikali itaendelea kusimamia uwajibikaji kwa watumishi na watoa huduma za Afya mpango utaenda pamoja na kuongeza vitanda kwenye wodi za wazazi na utoaji wa huduma ya Afya bure kwa makundi maalum.

Makamu wa Rais pia amehimiza wadau wa sekta binafsi waendelee kushirikiana na Serikali katika utoaji wa huduma za Afya kwa wananchi nchini ili kufikia malengo ya kupunguza vifo vya wanawake wajawazito na watoto.

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ametumia sehemu ya hotuba yake kwa kulipongeza Shirika la AMREF Health Africa Tanzania kwa mipango yake ya kusaidia jamii ya Kitanzania kupitia miradi mbalimbali inayotekelezwa na shirika hilo ukiwemo mpango wa kugharamia masomo kwa njia ya ufadhili kwa wanafunzi wanaotoka kwenye familia duni kwa lengo la kuwawezesha kusomea cheti ya uuguzi ukunga.

Kwa upande wake, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amesema kuwa mipango na mikakati ya Serikali ya awamu ya Tano ni kuhakikisha vifo vya wanawake wajawazito na watoto nchini vinapunguzwa kwa kiwango kikubwa kutokana na Serikali kuendelea kutenga bajeti ya kutosha kwa Wizara ya Afya kwa ajili ya kununua vifaa tiba na kuongeza idadi ya wataalamu.

Katika harambee hiyo, Jumla ya shilingi milioni 290 zimechangwa na wadau wa maendeleo na lengo ni kukusanya shilingi milioni 500 fedha ambazo zitatumika kusomesha wauguzi 400 wakiwemo 50 kwa ngazi ya cheti na 350 kwa ngazi ya diploma kupitia mafunzo ya kimtandao yaani e-learning.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

MKURUGENZI MTENDAJI WA TANESCO MHANDISI FELCHESMI MRAMBA, ATEMBELEA VITUO VIPYA VYA KUPOOZA NA KUSAMBAZA UMEME VYA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme nchini, (TANESCO), Mhandisi Felchesmi Mramba, (katikati), akizungumza wakati alipotembelea kituo kipya cha kupooza na kusambaza umeme cha City Centre jijini Dares Salaam, Novemba 5, 2016. Kushoto ni Meneja Mwandamizi wa Miradi ya Usafirishaji na Usambazaji Umeme wa Shirika hilo, Mhandisi Gregory Chegere, na kushoto ni Meneja Mwandamizi wa Shirika hilo kanda ya Dar es Salaam na Pwani Mhandisi, Mahende Mgaya.
Mhandisi Mramba, akizungumza na waandishi wa habari kwenye kituo cha Kupoozea na kusambaza umeme cha Ilala Mchikichini jijini Dar es Salaam .


NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID


MKURUGENZI Mtendaji wa Shirika la Umeme Nchini, (TANESCO), Mhandisi Felchesmi Mramba, ametembelea vituo vitatu vipya vya kupooza na kusambaza umeme vilivyo kwenye mradi wa uboreshaji wa huduma za umeme jijini Dar es Salaam leo Novemba 5, 2016.

Vituo alivyotembelea ni pamoja na kile cha katikati yajiji, (City Centre), kilicho jirani na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Kituo cha Kurasini na kituo cha Ilala Mchikichini.

Kwa takriban mwezi mmoja sasa, TANESCO kwa kushirikiana na wahandisi kutoka kampuni za Kijapani, Yachiyo Engineering Co Limited, Sumitomo, Takaoka na National Construction Limited, wamekuwa wakifanya kazi kubwa ya kubadilisha laini kutoka umeme mdogo kwenda umeme mkubwa, lakini pia kubadilisha vifaa vingine muhimu ili kuwezesha usafirishaji umeme uweze kuwafikia watumiaji katika ubora wa hali ya juu.

“Nimeridhishwa na hatua iliyofikiwa ya kubadilisha miundombinu yetu ya umeme, wakazi wa jiji la Dar es Salaam, sasa watapata umeme wa uhakika na ulio na ubora wa hali ya juu, jambo la kufurahisha sana ni kwamba mabadiliko haya yamekwenda sambamba na mipango ya Serikali ya awamu ya Tano ya kuifanya nchi yetu kuwa nchi ya viwanda, bila shaka umeme huu utawezesha kufikia azma hiyo ya serikali.” Alisema Mhandisi Mramba, baada ya kukagua kituo cha kupooza na kusambaza umeme cha katikati ya jiji.
Mhandisi Mramba alisema, nia ya TANESCO ni kuhakikisha wananchi wanaondokana na adha ya kukatika umeme mara kwa mara au kupata umeme hafifu usio na nguvu. “Mmeona mitambo hii nimipya kabisa nay a kisasa inayotumia teknolojia ya kisasa.” Alitoa hakikisho.

Maboresgho hayoyalihusisha ujenzi wa mfumo wa njia ya usafirishaji umeme chini ya ardhi, (Underground Transmission Lines) , kutoka shule ya sekondari ya wasichana ya Jangwani jijini Dar es Salaam na kutoka kituo cha umeme cha Makumbusho kwenda kituo kipya cha kupoozea umeme kilichoko katikati ya jiji cha City Centre cha ukubwa wa 100MVA (2X50MVA), 132/33KV, Kaimu Meneja wa Mradi huo, Mhandisi Iddi Rashidi, alisema,

Alisema, ujenzi wa mfumo huo wa njia ya umeme wa ardhini (Underground Distribution Lines), wa kilomita 4.3 wa msongo wa kilovolti 33 ni kwa ajili ya kuunganisha kituo cha City.Faida kubwa ambayo wakazi wa jiji la Dar es Salaam watarajie ni kupata umeme wa uhakika ulio kwenye viwango stahiki,

Naye Meneja Mwandamizi wa Miradi yausafirishaji na usambazaji umeme wa Shirika hilo, Mhandisi Geirge Chegere, alimueleza Mhandisi Mramba kuwa kituo cha City Centre cha 100MVA, kunafanya jiji la Dar es Salaam pekee kuwa na jumla ya vituo 9 vya aina hiyo.

Mradi huo unatarajiwa kuzinduliwa rasmi na Rais wa Jamhuriya Muunganowa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, baadaye mwezi huu wa Novemba.


Meneja Mwandamizi wa Usambazaji Umeme wa Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO), ambaye pia ndiye Meneja wa Mradi wa kuimarisha miundombinu ya Umeme, Injinia Theodory Bayona.akielezea hatuailiyofikiwa hadi sasa ya uboreshaji miundombinu ya umeme jijini Dar es Salaam
Meneja Mwandamizi wa Miradi ya Usafirishaji na Usambazaji Umeme wa Shirika hilo, Mhandisi Gregory Chegere, akielezea teknolojia ya kisasa ya mashine ndogo yenye kufanya kazi kubwa
Kituo cha City Centre
Mhandisi Mramba, akitembelea mitamboya kituo cha City Centre
Fundi mitambo ya umeme akiwa kazini kituo cha Ilala Mchikichini
Mhandisi Mramba, (kushoto), akizungumza wakati alipotembelea kituo cha Kupooza na kusambaza umeme cha Kurasini kujionea maendeleo yaujenzi wa kituo hicho
Mitambo ya kituo cha kupoozea na kusambaza umeme cha Kurasini
Mhandisi Chegere (wapili kulia), akipatiwa maelezo ya mitambo ya kituo cha City Centre
Jengojipya la kituo cha Ilala Mchikichini
moja ya mashine mpya kituo cha Ilala Mchikichini
Chumba cha mitambo mipya ya umeme kituo cha Ilala Mchikichini
Mhandisi Mramba, akiwa na wahandisiwenzake, Chegere (kulia) na Mgaya, kwenye kituo cha City Centre
Mitambomipya kituo cha Kurasini

WATAALAM WA AFYA KUTOKA NCHI TISA AFRIKA WAPATIWA VYETI

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru akizungumza katika mkutano wa wadau wa afya waliokutana Jijini Dar es Salaam Leo kwa ajili ya mafunzo ya kupima masikio na kuongea. Mafunzo hayo yamewawezesha washiriki kutoa huduma ya matibabu kwa watu wenye matatizo ya usikivu. Mafunzo hayo yameshirikisha wadau wa afya kutoka Nigeria Zambia, Ethiopia, Kenya, Malawi, Zimbabwe na Rwanda.
Baadhi ya washiriki kutoka nchi mbalimbali barani Afrika wakimsikiliza Profesa Museru Leo.
Daktari Bingwa wa magonjwa ya Koo, Sikio na Pua kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dr. Edwin Kayombo akifuatilia mkutano huo Leo.
Mtaalamu wa magonjwa ya Koo, Sikio na Pua akitoa mada kwenye mkutano huo Leo jijini Dar es Salam.
 
Mkurugenzi Mtendaji, Profesa Museru akikabidhi cheti kwa mmoja wa washiriki kutoka Muhimbili, JohnBosco Kambanga.
Mshiriki kutoka Rwanda, Fidel Munezero akipongezwa baada ya kukabidhiwa cheti Leo.
 
Wadau wa Afya wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumalizika kwa mafunzo ya kupima masikio na kuongea yalioanza Oktoba 29, mwaka huu na kufungwa leo Novemba 5, 2016 jijini Dar es Salaam.Picha na John Stephen, Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH)

Watalaam 25 wa afya kutoka nchi tisa za Afrika leo wametunukiwa vyeti vya kuhitimu mafunzo ya kupima masikio na kufundisha kuongea kwa watu wenye matatizo ya usikivu.

Mafunzo hayo yamewezeshwa na Kampuni ya MEDAL ya nchini Australia na kuhusisha washiriki kutoka nchi za Rwanda, Uganda ,Kenya , Zambia , Zimbabwe, Nigeria , Ghana, Malawi na Tanzania . Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) ni mwenyeji wa mafunzo hayo.

Akikabidhi vyeti hivyo Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru ameishukuru Kampuni ya MEDAL kwa kuwezesha kutolewa kwa mafunzo hayo ambayo yanaisaidia Hospitali kupiga hatua katika mipango yake hususani katika suala la kutoa huduma kwa wale wenye matatizo ya usikivu.

Awali, Meneja wa Maendeleo Kanda ya Afrika Mohamed El Disouky amesema MEDEL wataendelea kushirikiana na wataalam mbalimbali wakiwemo wa Muhimbili ili kuhakikisha wanapata ujuzi wa kutosha katika kutoa huduma hiyo.

Mafunzo hayo yalianza Oktoba 29 mwaka huu jijini Dar es salaam na kumalizika Novemba 5, mwaka huu.

RC IRINGA AMPONGEZA SALIM ABRI ASAS KUSAIDIA KUOKOA MAISHA YA MAJERUHI WA AJALI

$
0
0

Mwenyekiti wa kamati ya usalama barabarani mkoa wa Iringa Salim Abri Asas (kushoto) akimkabidhi mgeni rasmi katika maadhimisho ya wiki ya nenda kwausalama kwa mkoa wa Iringa leo , mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Juma Masenza zawadi maalum ya kamati ya usalama barabarani mkoa kutokana na mchango wake mkubwa kwa kamati hiyo

Kitengo cha usalama barabarani mkoa wa Iringa wakijiandaa kutoa elimu katika viwanja vya maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani
Baadhi ya wananchi na watu wenye ulemavu wakiwa katika viwanja vya maadhimisho hayo



Mwakilishi wa wakala wa barabara mkoa wa Iringa akitoa maelezo kwa mkuu wa mkoa wa Iringa na watu mbali mbali waliotembelea banda hilo kuona shughuli zinazofanywa



Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Juma Masenza akitoa hotuba yake leo wakati wa maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani ,kulia kwake ni mwenyekiti wa kamati ya usalama barabarani mkoa wa Iringa Salim Abri Asas na katibu wake RTO Leopold Fungu wakifuatilia hotuba hiyo



Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Juma Masenza akihamasisha upimaji afya na uchangiaji damu katika banda la HOspitali ya Rufaa mkoa wa Iringa ambao walishiriki maadhimisho hayo ya wiki ya nenda kwa usalama mkoa wa Iringa leo kwenye viwanja vya stendi kuu ya mkoa



Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Juma Masenza (wa tatu kushoto waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na wadau na kamati ya usalama barabarani mkoa wa Iringa mara baada ya kumalizika kwa maadhimisho hayo katika viwanja vya Stendi kuu , kushoto kwake ni katibu tawala wa mkoa wa Iringa Wamoja Ayubu ,Kaimu RPC , DC Iringa Richard Kasesela ,Naibu meya wa Manispaa ya Iringa Mh. Lyata na kutoka kushoto wa kwanza ni katibu wa kamati ya usalama barabarani mkoa Leopold Fungu na mwenyekiti wake wa kamati Salim Abri Asas



Dc Iringa Richard Kasesela akipata maelezo katika banda la zima moto



Afisa habari mkoa wa Iringa Denis Gondwe akipokea maelekezo toka kikosi cha usalama barabarani .
Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Juma Masenza akiwa akishirikiana na mwanafunzi wenye ulemavu wa ngozi toka Lugalo sekondari Semeny Sadick kuzima moto uliowashwa na kikosi cha zimamoto na uokoaji ili kutoa elimu kwa wananchi juu ya uzimaji moto baada ya kikosi hicho kutoa elimu katika shule zote za Manispaa ya Iringa



Mwanafunzi Semeny akizima moto



Wasanii toka Mkwawa Magic Site Iringa wakionyesha ujuzi wa kucheza na nyoka aina ya chatu



Askari wa usalama barabarani mkoa wa Iringa maarufu kwa jina la bibi akimpa pesa msanii wa Mkwawa Magic Site



Msanii toka kikundi cha Mkwawa Magic Site akicheza mbele ya mgeni rasmi

NYALANDU MGENI RASMI MAHAFALI YA 12 CHUO KIKUU CHA MOUNT MERU MKOANI ARUSHA

$
0
0

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mount Meru,Profesa Harrison Olang(kushoto)akizungumza na Mbunge wa Singida Kaskazini ambaye alikua mgeni rasmi katika mahafali ya 12.

Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini.Lazaro Nyalandu(kulia)akifurahia jambo na familia ya Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mount Meru,Profesa Harrison Olang

Picha ya pamoja na wahitimu


Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini.Lazaro Nyalandu(kushoto)akizungumza na Pastor Earl Pirkle(kulia) na Mkuu wa Chuo cha Mount Meru Profesa Elijah Wanje. 

Afisa Habari na Uhusiano wa Chuo cha Ufundi Arusha(ATC)Gasto Leseiyo akitunukiwa Shahada ya Uzamili wa Uongozi wa Biashara katika Chuo Kikuu cha Mount Meru mkoani Arusha.

Mdau Gasto Leseiyo ambaye ni Afisa Habari na Uhusiano wa Chuo cha Ufundi Arusha(ATC) akifurahia baada ya kutunukiwa Shahada ya Uzamili wa Uongozi wa Biashara katika Chuo Kikuu cha Mount Meru mkoani Arusha.

Mdau Goodluck Kimaro ambaye ni Afisa Rasilimali Watu wa TBL Arusha Plant akifurahia baada ya kutukiwa Shahada ya Uzamili katika Uongozi wa Biashara katika Chuo Kikuu cha Mount Meru mkoani Arusha 

PROF. MUHONGO AKUTANA NA BODI NA MENEJIMENTI YA TPDC

$
0
0
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo leo amekutana na Bodi na Menejimenti ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), katika kikao kilichochadili maendeleo ya utekelezaji wa miradi inayosimamiwa na shirika hilo ikiwemo Mradi wa Kusindika Gesi Asilia, (LNG) na Mradi wa Bomba la Kusafirisha Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) kutoka Hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga.

Katika kikao hicho Prof. Muhongo ameitaka Bodi na Menejimenti hiyo kuongeza kasi katika utekelezaji wa miradi husika kutokana na manufaa ya miradi hiyo kwa Maendeleo ya Taifa.

Mbali na Bodi na Menejimenti ya TPDC, kikao hicho pia kimehudhuriwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Prof. Justin Ntalikwa, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, anayeshughulikia Madini, Prof. James Mdoe na baadhi ya Watendaji kutoka Wizara ya Nishati na Madini.

Aidha, wakati huo huo, Waziri Muhongo pia amekutana na Balozi wa Uingereza nchini Sarah Cooke ambapo wamejadili masuala kadhaa kuhusu sekta ya nishati ikiwemo chanzo cha Nishati Jadidifu.Pia, Waziri Muhongo amekutana na Naibu Balozi wa Marekani nchini Virginia Blaser ambapo wamejadili masuala kadhaa kuhusu Sekta ya Nishati.
 Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo akisisitiza Jambo wakati wa Kikao chake na Bodi na Menejimenti ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC).
Sehemu ya Menejimenti ya TPDC wakifuatilia kikao baina yao na Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo (hayupo pichani).
Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Uingereza nchini Sarah Cooke (wa pili kushoto) na ujumbe uliofuatana na Balozi huo.
Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo (katikati) akizungumza na Balozi wa Uingereza nchini Sarah Cooken (wa kwanza kushoto) na ujumbe wake walipomtembelea leo ofisini kwake Jijijini Dar es Salaam. Kulia ni Kamishna Msaidizi wa Nishati anayeshughulikia umeme, Mhandisi Innocent Luoga.
Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo katika picha ya pamoja na Naibu Balozi wa Marekani nchini Virginia Blaser mara baada ya kumaliza mazungumzo yao wakati Naibu Balozi huyo alipomtembelea ofisini kwake jijini Dar es Salaam.

RAIS DKT SHEIN AFUNGUA MIRADI YA MAENDELEO PEMBA

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akifuatana na Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe,Omar Othman Makungu,(wa pili kushoto) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe,Issa Haji Ussi (wa pili kulia) na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Katiba,Utumishi wa Umma na Utawala Bora mara baada ya  kulifungua jengo la Mahkama kuu ya Chake chake Pemba leo akiwa katika ziara ya siku tano kisiwani humo,
z5
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akifuatana na Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe,Omar Othman Makungu,(wa pili kushoto) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe,Issa Haji Ussi (wa pili kulia) na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Katiba,Utumishi wa Umma na Utawala Bora mara baada ya  kulifungua jengo la Mahkama kuu ya Chake chake Pemba leo akiwa katika ziara ya siku tano kisiwani humo,
z6
Baadhi ya wananchi kutoka shehia mbali mbali katika Wilaya ya Chake chake Pemba wakiwa katika sherehe za Ufunguzi wa Jengo la Mahakama kuu ya Chake chake lililofunguliwa leo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akiwa katika ziara ya siku tano kisiwani humo.
z7
Viongozi wa Idara ya Mahakama wakiwa katika sherehe ya Ufunguzi wa Jengo la Mahakama kuu ya Chake chake lililofunguliwa leo Chakechake Pemba na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akiwa katika ziara ya siku tano kisiwani humo.
z8
Majaji wa Mahkama Kuu na Wananchi pamoja na Wafanyakazi wa Idara hiyo wakiwa katika sherehe ya Ufunguzi wa Jengo la Mahakama kuu ya Chake chake lililofunguliwa leo Chakechake Pemba na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akiwa katika ziara ya siku tano kisiwani humo
z9
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiwa na  Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe,Omar Othman Makungu,(kushoto) wakiwa katika sherehe ya Ufunguzi wa Jengo la Mahakama kuu ya Chake chake zilizofanyika leo Viwanja vya Mchezo wa Tenis Chakechake Pemba,
z10z11
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akitoa hutuba yake katika sherehe ya Ufunguzi wa Jengo la Mahakama kuu ya Chake chake zilizofanyika leo Viwanja vya Mchezo wa Tenis Chakechake Pemba, [Picha na Ikulu.] 05 Nov 2016.
z1
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiteremka katika Ndege ya Shirika la Ndege la AIR Tanzania mada baada ya kutua katika Uwanja wa Ndege wa Karume Pemba leo,Rais akiwa kisiwani humo atafungua miradi mbali mbali ya Maendeleo,
z2
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akipata maelezo kutoka kwa wakati alipotembelea sehemu mbali mbali baada ya kulifungua jengo la Mahkama kuu ya Chake chake Pemba leo akiwa katika ziara ya siku tano kisiwani humo,(kushoto) Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe,Omar Othman Makungu.


KAMPENI YA BINTI WA KITAA YAFIKA WILAYA YA TEMEKE JIJINI DAR, WAKAZI WAPATA ELIMU JUU YA KUZUIA MIMBA NA NDOA ZA UTOTONI.

$
0
0
 Afisa Mtendaji wa Wilaya ya Tandika Hija Kipeleka akizindua Rasmi kampeni ya Binti wa kitaa katika Wilaya ya Temeke, ambapo aliwashukuru wanaoendesha kampeni hiyo na kuahidi kushirikiana nao katika kupinga mimba na ndoa za utotoni.
 Mkurugenzi Mtendaji wa CVIF George David  Maarufu kwa jina la Ambassador Angelo akielezea kwa kina kampeni ya Binti wa kitaa ilivyo wasaidia mabinti wengi na kutoa ufafanuzi wa kina juu ya kampeni hiyo ambapo kwa sasa inaendelea kuzinduliwa katika Wilaya zilizopo jijini Dar.
 Mkazi wa Mtaa wa Mvomero Tandika Bi. Rauva Maulid akieleza namna akina baba walivyo na tabia ya kuwarubuni mabinti wenye chini ya umri wa miaka 18 na kuwababishia Mimba,na kuongeza kuwa kwa tandika watoto wengi wanapata mimba wakiwa na miaka kuanzia miaka 12.
 Mkazi wa Mtaa wa Mvomero Said Mgeni akisisitiza kuwa wazazi wanatakiwa kuwa jirani na watoto wao ili waweze kuwa rafiki na kuwaeleza matatizo wanayoyapata kwa sababu kwa kufanya hivyo mabinti watakuwa huru kueleza matatizo mbalimbali ikiwa ni pamoja na tatizo la mimba.
 Aisha mkazi wa Tandika akieleza namna vijana wanavyowarubuni na kuwasumbua ili waweze kushiriki nao katika ngono uzembe.
 Mkazi wa Mtaa wa Sheraton Tandika Fatuma akieleza namna baadhi ya mabinti wenye umri chini ya Miaka 18 wanavyopata mimba kutokana na kurubuniwa kufanya ngono uzembe na kuwapelekea kupata Mimba, na kuwasihi wasiwe wepesi kudanganyika na vijana.
 Binti huyu aliyetambulika kwa jina moja tuu Mwajuma akieleza alivyo achishwa Shule akiwa kidato cha pili kutokana na kukosa fedha za masomo hivyo timu ya Binti wa kitaa kwa kushirikiana na Serikali ya Mtaa wa Tandika kwa pamoja wameungana kumsomesha Binti huyo SIDO kwa kuwa anapenda kuja kuwa mfanyabiashara.
 Anaitwa Amani Muuza Juice ya Miwa maarufu mtaa wa sokoni akielezea jinsi Mimba za utotoni zinavyowaharibia maisha mambinti wenye  umri chini ya Miaka 18, na kuwasihi wananchi wote kuipa sapoti kampeni ya Binti wa kitaa
Muwezeshaji katika uzinduzi wa kampeni ya Binti wa Kitaa Zero akitoa elimu juu ya kuzuia mimba na ndoa za utotoni
 Kampeni ya Binti wa Kitaa huwakutanisha Mabinti pamoja na watu wa rika zote, hapa Msema chochote Steven Mfuko  maarufu kwa Jina la Zero akiwa na Bibi Zakia Seif akiwafunda mabinti wenye umri chini ya Miaka 18 kutokuwa na papara ya kukimbilia katika ngono.
 Mmoja ya wageni waliofika katika kampeni ya Binti wa Kitaa Jesca Kitomary alishauri kuwa wazazi wanatakiwa kuwaelimisha mabinti wao juu ya athari za mimba za utotoni  na kuolewa mapema, kwa kufanya hivyo itawasaidia kupata mimba na kuolewa kwa muda.
 Meneja wa Kampeni ya Binti wa Kitaa Mhandisi Eliwanjeria James kutoka kikundi cha wanawake Ma Injinia Tanzania akitoa shukurani kwa wote waliofika katika kufanikisha uzinduzi wa Kampeni ya Binti wa kitaa katika  Wilaya ya Temeke
 Mwakilishi wa Sunshine Group Fatuma akizungumza jambo wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Binti wa kitaa Temeke
 Wakiendelea kufuatilia kwa makini masomo mbalimbali wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Binti wa kitaa
Baadhi ya watu zaidi wakiwa katika pande mbalimbali wakifuatilia uzinduzi wa kampeni ya Binti wa Kitaa 
Baadhi timu ya Binti wa kitaa pamoja na wakazi wa Tandika wakiwa katika picha ya pamoja
Picha na Fredy Njeje/Blogs za Mikoa

Kutoka VOA Swahili: Zulia Jekundu S1 Ep 99: Hillary Duff, Drake, Taylor Swift, Kim Kardashian and Ciara

$
0
0
Zulia Jekundu ni kipindi cha televisheni cha kila wiki ambacho hukuletea habari mbalimbali za burudani zinazotamba. Humu utapata kujua juu ya habari za mastaa zinazogonga vichwa vya habari, kujua baadhi ya wanaosherehekea siku zao za kuzaliwa wiki husika na hata filamu 5 zilizoongoza kwa mauzo katika wiki hiyo.
KARIBU


Attachments area Preview YouTube video Zulia Jekundu S1 Ep 99: Hillary Duff, Drake, Taylor Swift, Kim Kardashian and Ciara

ROCKSTAR4000 SIGN LEGENDARY ZAMBIAN SINGER-SONGWRITER MAUREEN LILANDA TO A GLOBAL DEAL

$
0
0

JOHANNESBURG, Monday, 31st October 2016 – ROCKSTAR4000 have signed multiple award-winning Zambian singer-songwriter-musician Maureen Lilanda to a global agreement. Zambia’s leading lady of music, Maureen Lilanda and the ROCKSTAR4000 Zambia team inked the deal during an exclusive signing session in Lusaka and will see the accomplished Zambian recording artist release both her back catalog and highly anticipated future master recordings exclusively through ROCKSTAR4000 worldwide.

"I’m really excited in the future of music from Zambia as its now the time for the amazing music and sounds from Zambia to take over Africa and the world, and I’m thrilled on where this amazing partnership will be able to take my music now without borders or restrictions to fans anywhere on the planet. " Maureen commented.

"As the leading full service Pan African music entertainment network we are truly excited to now welcome the Queen of Zambian music to our family and cant wait to embark on this new Pan African and global journey with Maureen!" noted Jandre Louw, Founder & CEO of ROCKSTAR4000

"Maureen Lilanda is a highly accomplished Zambian singer-songwriter and the signing aligns strategically in sync with our highly accomplished successes and growth strategy as a group in taking the best of music entertainment from the continent to the rest of the world and are thrilled to welcome the Queen of Zambia to our royal family of Rockstars!" says Seven, Head of Talent and Music Pan African, ROCKSTAR4000

Maureen Lupo Lilanda’s distinctive voice, unique talent and generous spirit have secured her a place as one of Zambias top musicians and best female artists. With a range of musical styles from jazz to pop, Maureen blends African rhythms and flavours with sophisticated, contemporary rhythms and influences. For the past 20 years Maureen has traveled extensively, performing across Europe and Japan as well as regionally and has shared the stage with ‘Black Voices’ from the UK, Zimbabwe’s ‘Oliver Mutukudzi’, ‘Jonathan Butler’ from South Africa, ‘Fra Fra’ from the Netherlands, ‘Magic System’ from West Africa and ‘Baba Maal’ from Senegal, to name a few. Maureen has also been a regular leading feature at the annual Livingstone Festival.

Maureen has released four albums to date, ‘Nandayeye’, ‘Coming Home’, ‘Evolution’ and her latest album ‘Tetwe’. She is also lead vocalist of her European band, ‘Le Banquets de Nomads’ whose album ‘Afora’ combines Senegalese, Zambian and Belgian fusions. Maureen was lead singer of the famous Zambian Acapela group ‘Amashiwe’, which performed at the 1999 Livingstone Festival. Maureen has been awarded ‘Best female artiste by the National Arts Council for an historic four times and winner of the South African CEO Awards for the Most Influential Woman In The Arts in Zambia and the Southern Region. Maureen is also the First female President of Zambia Association of Musicians.

"If there's anyone the deserves such a huge opportunity it's definitely Maureen. Through Rockstar4000, she will finally reach every corner of the Africa and the world. We at Sling Beats are very happy to be a part of this great synergy that will advance Zambian music. I personally can't wait to begin work on the album."

"Maureen Lilanda is a Zambian superstar already as evident by all her accolades and successes and the extent of her huge ever growing fanbase. Maureen joining our family and groups further signifies our significant focus on Zambia and the region and our strategic commitment to Zambia’s best in music entertainment." noted Munya Daka, ROCKSTAR4000 Zambia & Uganda

HUDUMA YA UPANDIKIZWAJI WA VIFAA VYA USIKIVU YAANZA RASMI NCHINI.

$
0
0
Na Ally Daud-MAELEZO
HUDUMA ya upandikizwaji wa vifaa vya usikivu kwa watoto imeanza kutolewa rasmi nchini  katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili  baada ya wataalamu wa huduma hiyo kurejea wakitokea mafunzoni nchini India ili kuweza kusaidia watanznia hususani watoto wenye matatizo ya kusikia .
Akizindua huduma hiyo kwenye hafla fupi iliyofanyika jijini Dar es salaam Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Uisubisya amesema kuwa  Huduma hiyo imekua hadimu nchini hivyo kufanya kugharamia kiasi kikubwa cha fedha kwenda kuwatibia nje ya nchi.
“Kwakweli huduma hii ya kupandikiza watoto vifaa vya usikivu italeta msaada mkubwa kwa watanzania na kuokoa gharama takribani shilingi milioni 80 kwa kila mtoto ambaye alitakiwa kwenda kutibiwa nje ya nchi” alisema Dkt. Ulisubisya.
Aidha Dkt. Ullisubsya amesema kuwa wazazi wanatakiwa kuwa mstari wa mbele kugundua mapema matatizo ya watoto na kuwaleta katika Hospitali ya Muhimbili ili wapate taratibu za kupata huduma hiyo bila ya kuchelewa na kpata madhara makubwa.
Kwa upande wa Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Muhimbili Prof. Lawrence Museru amesema kuwa Huduma hiyo ambayo ilikua inafuatwa nje ya nchi sasa inafanyika nchini ikiwa ni jitihada za serikali katika kuokoa gharma za matibabu ya nje ya nchi.
Aidha Prof. Museru amesema kuwa hadi kufikia Januari 2017 MNH itaanza kufanya upasuaji na kupandikiza vifaa vya usikivu ikiwa ni huduma iliyokamilika bila ya kwenda nje ya nchi hivyo kupelekea kupunguza gharama zaidi na kusogeza huduma karibu.
“Hapa tulipofikia sio mwisho wa kutoa hudum hii , tunataka kufikia Januari 2017 tuwe tunafanya upasuaji kabla ya kupandikiza vifaa vya usikivu ikiwa ni huduma kamili na tutakuwa tumefikia baadhi ya malengo tuliyojiweka mpaka kufikia muda huo” alisema Prof. Museru
Aidha Prof. Museru amesema kuwa Serikali ilianza jitihada  za kuileta huduma hii nchini miaka mitatu iliyopita kwa kushirikiana na kampuni ya kuuza vifaa vya kupandikiza vifaa vya usikivu ya Medel kutoka nchini Misri.
Kwa upande wa Mzazi wa mtoto aliyepandikizwa kifaa cha usikivu Angel Ibrahimu (4) mkazi wa Mbeya amesema kuwa anaishukuru Serikali kwa jitihada zake za kufanikisha huduma hiyo kwa mtoto wake kwani lilikua tatizo ambalo hakuweeza kulitatua kwa uwezo wake.
Katika ufunguzi wa huduma hiyo ambayo itakua endelevu nchini imepandikiza vifaa vya usikivu kwa watoto 16 ambao wapepunguza gharama ya kwenda nje ya nchi takribani shilingi milioni 300 ambazo zitaenda kwenye huduma nyingine za maendeleo ya jamii. 
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya akiongea na waandishi wa habari hawapo pichani wakati wa uzinduzi wa huduma ya upandikizwaji wa vifaa vya usikivu kwa watoto uliofanyika leo jijini  Dar es salaam, kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Muhimbili Prof. Lawrence Museru.
 Mkurugenzi wa kampuni inayotoa huduma na kuuza vifaa vya usikivu ya Medel Bw. Mohamed Disouky wa kwanza kushoto akimpa maelezo Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya wa pili kulia jinsi huduma hiyo inavyotolewa wakati wa uzinduzi wa huduma ya upandikizwaji wa vifaa vya usikivu kwa watoto uliofanyika leo jijini Dar es salaam, wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Muhimbili Prof. Lawrence 
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Muhimbili Prof. Lawrence Museru akiongea na waandishi wa habari hawapo pichani wakati wa uzinduzi wa huduma ya upandikizwaji wa vifaa vya usikivu kwa watoto uliofanyika jijini Dar es salaam, kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya.
 Baadhi ya wazazi wa watoto wenye matatizo ya usikivu wakiwa katika foleni ya kusubiri huduma ya upandikizwaji wa vifaa vya usikivu wakati wa uzinduzi wa huduma ya upandikizwaji wa vifaa vya usikivu kwa watoto uliofanyika jijini Dar es salaam. Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jami

TANZANIA MWENYEJI WA MKUTANO WA KIMATAIFA WA BIASHARA

$
0
0
Na Amina Kibwana, Globu ya Jamii 

TANZANIA  kufikia  uchumi wa viwanda  mwaka 2020  kunahitajika kuwa na mazingira yatakayoweza kuwavutia wawekezaji  watakaoweza kuwekeza viwanda ikiwa ni pamoja na kuimarisha viwanda vidogo  vidogo katika kuzalisha bidhaa kwa wingi 

Akizungumza na Waandishi wa habari leo jijini Dar,Mkurugenzi Mtendaji wa  Mfuko wa Sekta Binafsi Nchini (TPSF),Godfrey Simbeye ameyasema hayo wakati  akitangaza mkutano wa Kimataifa  uunaotarajiwa kufanyika Desemba 5 hadi 7 katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere  jijini Dar es Salaam.

Simbeye amesema kuwa mkutano  huo utazishirikisha nchi mbalimbali Duniani ambazo zimepiga hatua  katika sekta ya viwanda,ambapo wawekezaji watapata fursa za kuwekeza katika sekta ya  viwanda nchini.

Mkutano huo ambao umeandaliwa na TPSF kwa kushiriana na  tasisi mbalimbali za Serikali ikiwemo Wizara ya Viwanda,Biashara, Arusha ya International Conference Centre, Shirika la Viwanda Vidogo, Vido IDO,TIC,EPZA,ZIPA,TTB pamoja na TANTRADE ambapo kwa pamoja wataingaza Tanzania katika  sekta ya viwanda nchini ili iweze kuleta matunda kwa watanzania pamoja kukuza uchumi.

Simbeye amesema mkutano kama huo  ulishafanyika mara mbili  katika nchi za Afrika ikiwepo  Misri na Afrika Kusini  na Tanzania imepata nafasi ya tatu katika kufanyika mkutano huo  ambapo ni fursa ya Tanzania katika  kuelekea uchumi wa viwanda kufikia 2020.

Amesema kampuni ya Biashara  nchini yatafaidika katika kutanua  uwigo wa mitandao ya kibiashara na kubadilishana uzoefu, taaluma  za kuweza kufanya fursa za uwekezaji, kuonyesha uwepo wa nchi katika jukwaa la kimataifa pamoja na kuongeza ushawishi na kuchochea maendeleo ya kiuchumi kutokana na kuongezeka mzunguko wa fedha za kigeni nchini  kutokana na ujio wa wageni wataoshiriki mkutano huo.

"Tanzania tunajivunia kuwa nchi ya tatu katika kufanyika mkutano huu, hii ni fahari sana kwetu, kwani tunaanza kuonekana kuwa nchi yetu ina hadhi” amesema Simbeye.

Sembeye  amesema mikutano kama hii inapokuja katika Nchi yetu inawapa watu fursa ya kuhudhuria na kufaidika pia inasaidia kukuza uchumi kwani tunategeme kupata wageni  400 ambapo wageni 200 watatoka nje ya nchi." 

Aidha ameongeza kuwa mkutano huo utakuwa sambamba na maonesho ya viwanda  yatakayoanza Desemba 7 hadi 11 mwaka huu ambapo washiriki wa mkutano watapata fursa ya kutembelea maonesho hayo. Simbeye amesema Tanzania ina jumla ya viwanda 49000, lakini viwanda vikubwa vipo 2000 tu hivyo hii ni fursa kwetu kutangaza bidhaa zetu.

TEA YAHAMASISHA UAZISHWAJI WA MIFUKO YA ELIMU

$
0
0
 Meneja Tathmini na  Ufuatiliaji Miradi wa Mamlaka ya Elimu Tanzania, Wendo Chiduo (kushoto) akihamasisha uanzishwaji wa Mifuko ya Elimu kwa uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza Mkoa wa Kigoma.
 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania, Joel Laurent akihamasisha uanzilishwaji wa Mifuko ya Elimu kwa Uongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Kasulu, Mkoa wa Kigoma.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania Joel Laurent na mwanafunzi wa Shule ya Msingi Nengo iliyopo Kibondo yenye wanafunzi wenye mahitaji maaluum. Elimu maalum ni moja kati ya miradi inayaotekelezwa na Mamlaka ya Elimu Tanzania.
Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa Mamlaka ya Elimu Tanzania, Bi Sylvia Lupembe (kushoto) akihamasisha uanzishwaji wa Mifuko ya Elimu kwa Uongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Singida. 
Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa Mamlaka ya Elimu Tanzania Bi. Sylvia Lupembe akikagua mradi wa ujenzi wa Nyumba ya walimu katika shule ya Sekondari Isanzu iliyopo Wilaya ya Mkalama,Singida. Mradi huu unafadhiliwa na Mamlaka ya Elimu Tanzania na ukitekelezwa na Watumishi Housing Company.

DC WA KASULU KANALI MKISI AKERWA NA TABIA YA WAKULIMA NA WAFUGAJI WANAOVAMIA HIFADHI YA ZA MISITU

$
0
0

Na Rhoda Ezekiel Kigoma,


MKUU wa Wilaya ya Kasulu Kanali Martine Mkisi ameeleza kukerwa na tabia ya wakulima na wafugaji wanaovamia hifadhi ya Msitu wa Kagerankanda na kufanya shughuli za ufugaji na kilimo katika msitu huo wenye sifa pekee ya Uoto wa Asili Mkoani Kigoma.

Kauli hiyo aliitoa mwishoni mwa wiki katika kikao cha Baraza la madiwani kilichokuwa kikiwasilisha taarifa mbalimbali za utendaji kazi wa kamati husika katika kipindi cha Julai-Septemba 2016, ambapo mkuu huyo wa Wilaya alitumia nafasi hiyo kuwaasa madiwani wahamasishe wananchi wapishe hifadhi hiyo kabla ya kutumika nguvu ya ziada.

Kanali Mkisi alisema changamoto ya uvamizi katika msitu huo ni ya muda mrefu na kueleza kusikitiswa na vitendo hivyo kutokana na kuwa vitendo hivyo ni janga kwa kizazi cha kijacho, kutokana na makundi ya wakulima na wafugaji kuendelea kujazana katika msituni huo kwa shughuli za kilimo na ufugaji wakati kuna maeneo makubwa yapo wazi na yana rutuba kwa uzalishaji wa bidhaa zao.

“mimi ni kanali siendeshi wilaya kiraia ,nataka sheria,kanuni na taratibu zitumike katika kurasimisha makazi si kuvamia misitu ya asili yenye hadhi ya uoto wa asili na mimi niseme ukweli, nashangzwa na baadhi ya viongozi wanalifumbia macho wakati rasilimali inatumiwa hovyo kwa maslahi yenu binafsi” alisema

Aidha Mkisi alisema, hatojali zengwe kwa kuwa amechaguliwa na serikali hivyo nitasimamia sheria, kanuni na taratibu husika, na kusema kuwa aliondolewa katika nafasi yake huku akiwa anasimamia sheria na kanuni hatosita kuendelea na shughuli nyingine.

Akizungumzia kero ya uvamizi wa hifadhi hiyo Diwani wa kata ya Kagerankanda Ezekieli Mshingo, alikiri wananchi kutumia msitu huo kwa zaidi ya miaka 12 kama kichaka cha wahamiaji haramu,ufichwaji wa silaha haramu za moto pamoja na makundi ya wafugaji na wakulima kuongezeka kila kukicha.

Mshingo alisema uvamizi unatokana na usimamizi mbovu kuanzia ngazi ya juu hadi ya chini na kitendo cha kuwaondoa makundi hayo katika msitu wa kagerankanda ni changamoto kwa kuwa, wavamizi wengi wanasaidiwa na watu wakubwa hali inayochangia mauwaji kila mwaka na kutolea mfano wa  Novemba 3, 2016 kuna mfugaji mmoja Majigwa Magesa ameuwawa na mwishoni na kwamba hakuna hatua zilizochukuliwa dhidi ya waharifu.

Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu vijijini Yohana Mshita alisema taifa lilipofikia linahitaji kiongozi muwazi, mkweli mwenye moyo wa dhati katika kuondoa kero za wananchi kwa uadilifu huku akifuata sheria zilizopo lengo lkiwa ni kutimiza malengo yake na kusema kuwa katika utendaji huo baadhi ya watendaji wa halmashauri za wilaya wamekua na taba ya majungu ya kukwamisha utekelezaji wa shughuli mbalimbali hivyo kumuomba mkuu huyo kutosikiliza maneno yao.

DC Kibondo amwamuru Mkurugenzi kuwasimamisha watumishi watatu kwa ubadhirifu wa shilingi milioni 109 za mradi wa ujenzi wa madarasa

$
0
0
Na Rhoda Ezekiel globu ya Jamii,Kigoma,

MKUU wa Wilaya ya Kibondo Mkoa wa Kigoma Luice Bura amemtaka  Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kibondo kuwasimamisha kazi watumishi watatu katika kitengo cha ujenzi kwa tuhumaa za ubadhirifu wa fedha kiasi cha Sh.Milioni 109 kati ya sh.milioni 264 zilizotakiwa kumaliza mradi wa vyumba vitatu vya madarasa na nyumba ya walimu yenye uwezo wa kuishi familia za watu sita na matundu matano ya vyoo katika Sekondari ya Itaba katani humo.

Maagizo hayo aliyatoa Jana katika kikao cha ulinzi Na usalama ambacho yeye ndiye Mwenyekiti wa kamati hiyo baada ya kufika eneo la Ujenzi wa vyumba vya madarasa Na vyoo katika shule za sekondar tank Na Nyumba za walimu Na kukuta vyoo havija sakafiwa Na vyumba vingine havijajengwa.

Bura aliwataja watumishi watakao simamishwa ni pamoja na Salehe Mbogoye, Felix Ngomano na Haruni Mbapaye kutoka idara ya ujenzi , ambao ndio waliokuwa wakisimamia ujenzi wa majengo hayo na kuchangia upotevu wa sh.milioni 109, ilihali kiasi cha sh.milioni 46 zimelipwa bila kufanyiwa kazi na ujenzi uliofanyika upo chini ya kiwango huku ujenzi upo chini ya asilimia 50% na kuidhinisha malipo hewa

" baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wananchi kutokana na mradi huo niliamua kuituma Kamati ya ulinzi na usalama ,walifika katika eneo la ujenzi na kukuta ujenzi haujakamilika ambapo matundu ya choo ni mashimo tu, madirisha hayapo sakafu haijawekwa na ninakuomba Mkurugenzi uwasimamishe kwa muda watumishi hao hadI uchunguzi utakapo kamilika kutokana Na tuhuma hizo",alisema Bura.

Hata hivyo Bura alisema cha kushangaza Madiwani wa kamati ya ujenzi waliomba posho ya kufanya ukaguzi wa ujenzi na wakapewa posho ya siku tano ,kumbe hata kwenye eneo la ujenzi hawajafika hali iliyowapelekea watumishi wengine kuangukiwa na barua za maadili ni pamoja na Ofisa Elimu Sekondari Wilaya Honolata Kabundugulu, Fedy Eliasafu Ofisa Maliasili na Ofisa kilimo wilaya Said Shemahonge ambao wataitajika kujibu tuhuma hizo. 

Akitoa ufafanuzi juu ya mradi huo Mjumbe wa kamati ya maendeleo ya kata husika Bosco Ngomagi alisema serikali ihakikishe inashirikisha wananchi wa eneno husika,ili kuondoa uhujumu uchumi wa jamii ambapo kamati husika watasimamia mradi husika Na wannchi wtafuatilia kwa ukaribu ilikujua no kiasi gani kimetengwa ilikuweza kukamilisha mradi Na mradi ukamilike kwa wakati.

Nao baadhi yaVibarua kutoka kampuni iliyochukua zabuni ya ujenzi ya Mangalazi Engenearing ya Kigoma Mjini Paschal Leonardi walimuomba mkuu huyo awasaidie malipo yao kwa kuwa fedha nyingi zimeshatumika Na wao hawajapata malipomyao mpakasasa wanaendelea Na kazi lakini mpakaka sasa kunabaadhi wamechukua fedha hizo bado hawajawalipa.

LIGI YA WANAWAKE KUENDELEA KESHO

$
0
0
 Zainab Nyamka,Globu ya Jamii
 
Raundi ya Pili ya Duru la Kwanza ya Ligi Kuu ya Taifa ya Wanawake itaendela kesho Jumanne kwa mchezo mmoja tu, wa Panama ya Iringa kuwa wageni wa timu ya Marsh Academy kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Lakini, wakati mchezo huo Na. 5 wa Kundi B, ukifanyika michezo mingine mitano ya raundi ya pili ikiwamo mitatu ya Kundi A, imebidi iahirishwe na itapangiwa tarehe nyingine. Sababu kubwa ya kuahirishwa kwa michezo hiyo ni uwingi wa wachezaji kutoka timu zinazoshiriki ligi hiyo kujumuishwa kwenye timu ya taifa ya Wanawake – Twiga Stars.

Kwa mujibu wa ratiba ya ligi hiyo, michezo ya Kundi B iliyoahirishwa ni kati ya Majengo Women ya Singida iliyokuwa icheza na Baobab ya Dpdoma kwenye Uwanja wa Namfua mjini Singida wakati mechi nyingine ni kati ya Victoria Queens ya Kegera iliyokuwa icheze na Sisters ya Kigoma – mchezo ulipangwa kufanyika Uwanja wa Katiba mjini Bukoba.

Michezo ya Kundi A iliyoahirishwa ni kati ya Fair Play ya Tanga iliyokuwa iikaribishe Mburahati Queens ya Dar es Salaam kesho Novemba 8, 2016 kwenye Uwanja wa Mkwakwani ilihali michezo mingine iliyoahirishwa ni ya Novemba 9, ambako JKT Queens ya Dar es Salaam ilikuwa icheze na Viva Queens kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam wakati Evergreen Queens na Mlandizi zilikuwa zitumie Uwanja wa Karume, Ilala kucheza mechi yao hiyo.

MKUU WA MKOA WA MWANZA AZINDUA KITUO CHA HUDUMA SHIRIKISHI DHIDI YA UKATILI WA KIJINSIA NA WATOTO

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella, akikata utepe kuashiria uzinduzi wa kituo cha One Stop Centre katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mwanza, Sekour Toure, hii leo.

Na BMG

Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella, akikata utepe kuashiria uzinduzi wa kituo cha One Stop Centre katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mwanza, Sekour Toure
Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella, akizindua jengo la kituo cha One Stop Centre katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mwanza, Sekour Toure
Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella, akizindua jengo la kituo cha One Stop Centre katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mwanza, Sekour Toure
Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella, akizungumza wakati wa ufunguzi wa kituo cha One Stop Centre katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mwanza, Sekour Toure
Antony Binamungu ambaye ni mlinzi wa mtoto na ukatili wa kijinsia kutoka shirika la PACT Tanzania, akizungumza wakati wa uzinduzi huo
Mwakilishi kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Notigela Ngaponda, akizungumza kwenye uzinduzi wa Kituo cha Pact Tanzania
Viongozi mbalimbali
Mwakilishi kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Notigela Ngaponda, akizungumza na wanahabari ambapo amesema kituo hicho kitarahisisha upatikanaji wa huduma kwa wahanga wa ukatili wa kijinsia.
Baadhi ya watumishi wa hospitali ya Sekour Toure

Na George Binagi-GB Pazzo


Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella amewataka maafisa ustawi wa jamii kwa kushirikiana na askari polisi kitengo cha dawati la jinsia, kufikisha elimu ya kupambana na ukatili wa kijinsia kwa wananchi ili kusaidia mapambano dhidi ya vitendo hivyo.

Mongella ametoa agizo hilo wakati akifungua kituo cha huduma Shirikishi dhidi ya Ukatili wa kijinsia na watoto cha One Stop Centre kilichojengwa na taasisi ya Pact Tanzania kwa ufadhiri wa watu wa Marekani, katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mwanza Sekour Toure.

Amesema hatua za kukabiliana na ukatili wa kijinsia zinapaswa kuchukuliwa mapema badala ya kusubiri utokee katika jamii ambapo amesema watakaokuwa wakipatikana na hatia za kujihusisha na ukatili wa aina hiyo watachukuliwa hatua za kisheria mara moja.

Mganga Mkuu wa Hospitali ya Sekour Toure, Dkt.Leonard Subi, amesema kituo hicho kitajumuisha watumishi mbalimbali ikiwemo polisi, maafisa ustawi wa jamii pamoja na wataalamu wa afya kwa ajili ya kuwahudumia wahanga wa vitendo vya ukatili wa kinjinsia ambavyo bado vimeshamiri mkoani Mwanza.

Amebainisha kwamba kwa kipindi cha mwezi julai hadi septemba, wananchi 238 mkoani Mwanza wamepatiwa huduma za ukatili wa kijinsia katika hospitali na vituo mbalimbali vya afya na kati ya hao 77 ni ukatili wa watoto. Kituo hicho tayari kimehudumia watu wazima 30 waliolengwa na ukatili wa kijinsia huku watoto wakiwa ni 67.

Naye Antony Binamungu ambaye ni mlinzi wa mtoto na ukatili wa kijinsia kutoka shirika la PACT Tanzania, amesema ujenzi wa kituo hicho umegharimu shilingi milioni 80 ikiwa ni pamoja na gharama za vifaa na mafunzo ambapo kinakuwa kituo cha nane nchini miongoni mwa vituo vya One Stop Centre.

BODI YA PAMBA KUHAMIA MWANZA.

$
0
0
 Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na UvuviMhe.  William Ole Nasha akijibu hoja mbalimbali za wabunge katika Bunge la 11 Mjini Dodoma.

Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO, Dodoma

Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi imejipanga kuhamishia Bodi ya Pamba katika Mkoa wa Mwanza kabla ya Novemba 10 mwaka huu ili kuhakikisha wakulima wa pamba waliopo katika mkoa huo wanapata huduma zilizo bora kwa ukaribu na haraka.

Hayo yamesemwa leo mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhe.  William Ole Nasha alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Bukombe Mhe. Doto Biteko lililohoji juu ya hatua ya Serikali kwa wakulima walioathirika na pembejeo zilizotolewa ambazo hazikuwa na ubora pamoja na kuhamishia Bodi ya Pamba katika mkoa huo.

”ili kuwafikia kirahisi wakulima wa pamba waliopo mkoani Mwanza, Wizara imeamua kuhamishia Bodi hiyo katika mkoa huo na kwa taarifa zilizopo Bodi hiyo inatakiwa kuhama haraka iwezekanavyo kabla ya Novemba 10 mwaka huu”, alisema Mhe.Ole Nasha.

Kwa upande wa matatizo ya pembejeo, Mhe. Ole Nasha amesema kuwa Serikali tayari ina taarifa kuhusu tatizo lililowapata wakulima wa pamba katika maeneo mbalimbali kwa kusambaziwa viuatilifu pamoja na mbegu ambazo hazikuwa na ubora unaotakiwa hivyo kuathiri wakulima nchini.

“Serikali iliiagiza Tropical Pesticides Research Institute (TPRI) kufanya uchunguzi wa malalamiko ya wakulima ambao ulibaini kuwa viuatilifu hivyo vilikuwa na utendaji hafifu hivyo Serikali itaanza kuzalisha mbegu bora za pamba za UK08 ili kuhakikisha tatizo hili halijirudii tena”, alisema Mhe. Ole Nasha.

Naibu Waziri huyo amefafanua kuwa kufuatia changamoto hizo za uotaji wa mbegu, Serikali iliamua kufanya majaribio ya utoaji wa mbegu ambazo zilikuwa zikisambazwa hapo awali bila kujua ufanisi katika uotaji wake.

Amethibitisha kuwa, matokeo ya jaribio hilo yamewezesha kutoa maelekezo kuhusu aina za mbegu za pamba zenye sifa za msingi ambazo zitasambazwa kwa wakulima katika msimu wa kilimo wa mwaka 2016/2017.

Halmashauri tatu za Mkoa wa Mara zimevuka lengo la BRN Matokeo ya Darasa la 7

$
0
0
Na. Lilian Lundo – MAELEZO - Mara

Halmashauri tatu za Mkoa wa Mara zimevuka Lengo la Matokeo Makubwa Sasa (Big Results Now – BRN) la asilimia 80 katika matokeo ya darasa la saba ya mwaka 2016.

Hayo yamesemwa leo, Wilayani Tarime na Afisa Elimu wa Mkoa wa Mara Mwalimu  Hamis Lissu alipokuwa akifungua semina ya Mawasiliano na kushirikishana jitihada zenye mafanikio kwenye Elimu kwa maafisa wa Elimu wa Mkoa wa huo.

“Halmashauri za Tarime Mji, Tarime Manispaa na Musoma Manispaa ni halmashauri ambazo zimevuka lengo la BRN katika Mkoa wa Mara, Halmashauri hizo kila moja zimepata wastani wa asilimia 82 katika matokeo ya darasa la Saba ya mwaka, 2016,” alifafanua Lissu.

Aliendelea kwa kusema kuwa, ufaulu wa darasa la saba katika Mkoa wa Mara umekuwa ukipanda mwaka hadi mwaka kuanzia mwaka 2014, ambapo kwa mwaka 2014 Mkoa wa Mara ulikuwa Mkoa wa 25 kati ya Mikoa 25, mwaka 2015 Mkoa ulishika nafasi ya 17 kati ya Mikoa 25 na mwaka huu 2016 umeshika nafasi ya 13 kati ya Mikoa 26.

Lissu amesema kuwa Halmashauri zote za Mkoa wa Mara zimeongeza ufaulu katika matokeo ya mwaka huu ukilinganisha na matokeo ya mwaka 2015 na 2014.Vile vile amesema kuwa ongezeko hilo la ufaulu limefanikishwa kwa kiwango kikubwa na Mpango wa Kuinua Ubora wa Elimu Tanzania (Education Quality Improvement Programme -Tanzania) EQUIP-T  unaosimamiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kushirikiana na Serikali ya Uingereza.

Mpango huo umekuwa ukitoa mafunzo ya kuboresha utendaji wa walimu darasani pamoja na kutoa pikipiki kwa waratibu elimu kata wote ambao ndio wafuatiliaji wakubwa wa ufundishaji wa walimu na maendeleo ya taaluma ya mwanafunzi katika ngazi ya kata.

Aidha Lissu amesema kuwa kuna asilimia kubwa ya Mkoa huo kushika nafasi ya kumi bora kitaifa katika matokeo ya mwaka 2017.
Viewing all 46401 articles
Browse latest View live




Latest Images