Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1034 | 1035 | (Page 1036) | 1037 | 1038 | .... | 1898 | newer

  0 0
 • 11/07/16--23:17: VIWANJA VINAUZWA
 • Mahali Vilipo - Mbweni Jijini Dar es Salaam Sifa:- - Vimepimwa, Vina Hati ya Umiliki -Viko sehemu nzuri - Vinafaa kwa matumizi ya Makazi -Kimoja kina Sqmt 1400, Kingine Sqmt 700 Bei- Maelewano Mawasiliano - 0653 917000

  0 0

  Mwenyekiti wa UWASMA,Peter Thadeo akiongea na wana Kikundi kuhusiana na swala zima la kujikwamua katika lindi la  umaskini jijini Dar jana.
  Katibu mkuu ,Aron Kashaija akiongea na wanakikundi kuhusu maswala mbalimbali yanayoweza kusaidia katika swala zima la kupambana na Umasikini.
  Baadhi ya Wanakikundi cha UWASMA Wakiwasikiliza viongozi kujadili maswala mbalimbali ya kimaendeleo jijini Dar es salaam.
  Wanakikundi cha UWASMA wakiwa katika picha ya Pamoja


  Jamii imetakiwa kufanya kazi kwa ushirikiano ili kutatua changamoto zinazowazunguka ili kuweza kunyanyuka kiuchumi na kunyanyua pato la Taifa.

  Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa chama cha Umoja wa wanafunzi wa St. Matthew UWASMA,Peter Thadeo na kueleza kuwa changamoto kubwa iliyopo ni suala la umaskini ambalo linapelekea jamii kubwa kutofikia malengo yao na kushindwa kupata mahitaji muhimu.

  Thadeo ameongeza kuwa lengo kubwa la kuanzisha chama hicho ni kusaidiana na kunyanyua vipato vyao kupitia uwekezaji kwenye kilimo kwa kuunganisha elimu na nguvu walizonazo.Uwekezaji katika kilimo ni njia bora ya kunyanyua na muhimili mkuu wa kupambana na umaskini.alisema thadeo.

  UWASMA ni chama kilichoanzishwa na wanafunzi waliomaliza kidato cha sita katika shule ya sekondari ya st.matthew iliyoko jijini dar es salaam lengo likiwa ni kusaidiana katika masuala mbalimbali ya kiuchumi kwa kupitia uwekezaji.

  0 0

  Mwenyekiti wa Tanzania Yemen Professional Foundation (TYPF), Dr Ameir Binzoo (kushoto) akimpatia zawadi Balozi wa Kuwait nchini Tanzania, Mheshimiwa Jasem Al Najem kwa udhamini wa siku ya afya ya mwanamke iliyoandaliwa na taasisi hiyo nchini na kudhaminiwa na Ubalozi wa Kuwait kwa ajili ya kuboresha afya ya mwanamke jijini Dar es Salaam.

  Taasisi ya Tanzania Yemeni Professional Foundation (TYPF),
  Jumamosi ya Novemba 5 mwaka huu iliendesha huduma ya upimaji wa afya kwa akina 
  mama wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa udhamini wa Ofisi ya Ubalozi wa Kuwait nchini 
  Tanzania.

  Shughuli iliyopewa jina la Women’s Health Day, ilikuwa na lengo la taasisi hiyo kutoa huduma bora kwa akina mama kama sehemu ya kuangalia namna ya kusogeza huduma karibu na wananchi sambamba na kuhamasisha suala zima la upimaji wa afya ya akina mama.

  Akizungumza katika shughuli hiyo ya upimaji afya kwa wanawake, Mwenyekiti wa Tanzania Yemen Professional Foundation (TYPF), Dr Ameir Binzoo, alisema huduma hiyo ya upimaji afya ilikuwa na dhamira ya kuwasaidia akina mama kufahamu afya zao.
  Balozi wa Kuwait akipata picha ya pamoja na wadau wa taasisi hiyo baada ya kumalizika shughuli ya upimaji afya kwa akina mama.

  Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Jasem Al Najem akipewa maelekezo aliposhiriki katika shughuli ya upimaji afya kwa wanawake jijini Dar es Salaam iliyoandaliwa na Tanzania Yemen Professional Foundation (TYPF).

  Alisema Siku hiyo ya afya ya wanawake ilidhaminiwa na Ubalozi wa
  Kuwait, ikiwa ni hatua bora ya kushirikiana na wadau wa afya kuwasaidia
  wanawake wote wa jijini Dar es Salaam, wakiwamo wale waliohudhuria katika  upimaji huo.

  “Tunashukuru kwa kufanikiwa kumaliza salama tukio letu kwa sababu
  limefanyika vizuri na kusudio letu tulilotaka limefika kwa wahusika, wakiwamo akina mama wa jijini Dar es Salaam ambao ndio walengwa haswa.

  “Tunawapongeza pia wenzetu wa Ubalozi wa Kuwait kwa kuguswa kwenye
  suala la afya ya wanawake hali iliyowasukuma kuingia kwenye tukio letu la kutoa huduma ya bure ya afya ya wanawake,” alisema Dr Binzoo.
  Kwa mujibu wa Dr Binzoo, mbali na kuwapima wanawake hao
  waliohudhuria, pia walikuwa wakitoa elimu na mbinu ya kukabiliana na magonjwa ikiwamo kujiwekea utaratibu wa kupima afya zao mara kwa mara.

  0 0

  Mkurugenzi wa Idara ya Elimu na Daktari Mkuu wa Hospitali ya Nanjing Dkt. Zhou Yujie akimkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Mnazi mmoja vitabu vitakavyotumika kuendesha mafunzo ya madaktari na wauguzi wa Zanzibar.
  Dkt. Zhou Yujie ambae ni Mkurugenzi na Daktari Mkuu wa Hospitali ya Nanjing akizungumza na madaktari na wauguzi watakaoshiriki mafunzo ya miaka mitatu nchini China na Zanzibar wakati wa uzinduzi wa mafunzo hayo uliofanyika Hospitali ya Mnazi mmoja. 
  Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Mnazi mmoja Dkt. Ali Salum Ali akizindua mafunzo ya madaktari na wauguzi yatakayofanyika katika Hospitali ya Nanjing na Hospitali kuu ya Mnazi mmoja Mjini Zanzibar, (kushoto) ni Mkurugenzi wa Idara ya Elimu na Daktari Mkuu wa Hospitali kuu ya Jimbo la Nanjing

  Picha na Makame Mshenga/Maelezo Zanzibar

  …………………………………………………………………………….

  Jimbo la Nanjing Nchini China limeongeza ushirikiano mpya na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuanzisha mpango maalumu wa mafunzo ya miaka mitatu kwa madaktari na wauguzi wa Hospitali kuu ya Mnazi mmoja.

  Mafunzo hayo yatakayofanyika kwa zamu katika Hospitali ya Mnazi mmoja na Hospitali ya Nanjing yatawashirikisha madaktari sita na wauguzi sita kutoka sehemu ya wazazi.

  Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Mnazi mmoja Dkt. Ali Salum Ali ameyazindua rasmi mafunzo hayo na kueleza kuwa wamejiandaa vizuri ili kuhakikisha mafunzo hayo yanafanyika kwa ufanisi.

  Amesema mafunzo hayo yanatarajiwa kuwaongezea uwezo madaktari wazalendo na wauguzi katika kukabiliana na vifo vya mama wajawazito wakati wa kujifungua na watoto wachanga.

  Dkt. Ali Salum amesema katika mpango huo, madaktari bingwa kutoka Hospitali ya Nanjing watakaoendesha mafunzo hayo wataambatana na wanafunzi wao kwa awamu katika hospitali ya Jimbo hilo na Hospitali ya Mnazi mmoja.

  Ameongeza lengo la kuendesha mafunzo hayo katika vituo viwili tofauti, China na Zanzibar, ni kuwapa fursa madaktari na wauguzi kujifunza kwa kutumia mazingira ya nyumbani na mazingira ya kigeni ambapo yatakuwa na ufanisi zaidi.

  “Mara nyingi vijana wetu wanapokwenda nje ya nchi kwa mafunzo hutumia teknolojia ya huko na wanaporudi wanatumia teknolojia ya kwetu hivyo baadhi ya wakati wanajikuta wapo njia panda,” aliongeza Mkurugenzi Mtendaji.

  Amesisitiza kwamba mpango huo mpya wa mafunzo utatoa fursa kwa madaktari na wauguzi wengi kutoka Zanzibar kupata mafunzo kwa wakati mmoja na utapunguza gharama za kuwasafirisha watu wachache kwa gharama kubwa.

  Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Mnazi mmoja alisema baada ya madaktari na wauguzi hao kumaliza mafunzo yao watasaidia kutoa huduma katika Hospitali na vituo vyengine vya afya vya Zanzibar.

  Mkurugenzi wa Idara ya Elimu ambae pia ni daktari mkuu wa Hospitali ya Nanjing Dkt. Zhou Yujie amesema tayari wameandaa mtaala na kufanya uteuzi wa madaktari 20 watakaosimamia mafunzo hayo.

  Katika uzinduzi wa mafunzo hayo uliofanyika Hospitali ya Mnazi mmoja, Dkt. Zhou alimkabidhi Mkurugenzi Mtendaji vitabu vitakavyotumika katika kuendesha mafunzo hayo.

  Alisema katika mafunzo hayo wakufunzi kutoka Hospitali ya Nanjing watashirikiana na wanafunzi wao kuwafanyia matibabu ya kawaida na upasua wagonjwa ikiwa ni miongoni mwa mafunzo yao.

  Amekumbusha kuwa uhusiano wa sekta ya afya kati ya Jimbo la Nanjing na Zanzibar ulianza tokea mwaka 1964 kwa kuleta madaktari katika Hospitali ya Mnazi mmoja na Hospitali ya Abdalla Mzee Mkoani na mpango wa sasa wa mafunzo ya miaka mitatu ni muendelezo wa historia hiyo.

  0 0

  Hospitali ya Kairuki katika kuboresha huduma zake kwa wagonjwa imeanza kutumia kitengo kipya kwa ajili ya kuwahudumia wagonjwa wa kutwa  hususani wale wanachama wa mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF).

  Kitengo hicho kipya (OPD 3)  kilichopo nyuma ya Jengo kuu la hospital mkabala na kitengo cha magonjwa ya viungo (Physiotherapy Unit) kina sehemu kubwa ya mapokezi, vyumba  mbalimbali  vikiwemo  vyumba 10 via madaktari, maabara,Duma la dawa,sehemu ya sindano na kufunga vidonda,chumba cha ultrasound,mapokezi , huduma za chanjo ya watoto (RCH),chumba cha wauguzi na duka dogo la vinywaji na vitafunwa nk.

  Kitengo hicho kipya kitaiwezesha hospitali hiyo kutoa huduma kwa haraka na ufanisi zaidi kwa wagonjwa wasiopungua 120,000 kwa mwaka hivyo kupunguza kero ya  foleni na msongamano iliokuwepo siku za nyuma.


  Imetolewa na Afisa Mahusiano, Arafa Mohamed
  Wagonjwa wakisubiri kupata matibabu.
  Wagonjwa wakisubiri kupata matibabu.
  Vyumba vya madaktari.

  0 0  koj

  0 0  VIONGOZI mbalimbali wakionekana kushirikiana na wananchi wa kijiji cha Kibindu Chalinze wilayani Bagamoyo,katika ujenzi wa madarasa mawili ya shule ya msingi Kibindu ,akiwemo mkuu wa mkoa wa Pwani mhandisi Evarist Ndikilo,mkuu wa wilaya ya Bagamoyo alhaj Majid Mwanga na kamanda wa polisi mkoani Pwani Boniventure Mushongi.
  (Picha zote na Mwamvua Mwinyi) 

  …………………
  Na Mwamvua Mwinyi, Bagamoyo


  SERIKALI wilayani Bagamoyo,mkoani Pwani,imeanza kuelekeza nguvu zake katika kukabiliana na uhaba wa vyumba vya madarasa kwenye shule za msingi na sekondari wilayani humo baada ya kukamilisha zoezi la madawati.

  Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo,alhaj Majid Mwanga ,aliyasema hayo wakati baadhi ya viongozi wa wilaya walipoweka kambi katika shule ya msingi Kibindu ,jimbo la Chalinze,kushirikiana na wananchi kwenye ujenzi wa madarasa mawili.Alisema zoezi hilo ni la kata zote zilizopo wilayani Bagamoyo lengo ni kuhakikisha wanamaliza tatizo la upungufu wa madarasa lililopo kwasasa.

  Alhaj Mwanga alisema lengo jingine ni kuhakikisha wanafunzi wanaofaulu kujiunga na kidato cha kwanza na wanaoandikishwa darasa la kwanza mwakani wasikose madarasa ya kusomea.Aidha alieleza kuwa kila kata sasa hivi ina siku yake maalum ya kujitolea kufanya shughuli za serikali nje ya siku ya kufanya usafi.

  “Tunachokifanya kwasasa ni kuhakikisha tunamaliza tatizo la madarasa wilayani Bagamoyo,haiwezekani wanafunzi wakasoma kwenye mazingira yasiyo bora hata kidogo,kwa pamoja tutaweza kuboresha sekta ya elimu”alisema alhaj Mwanga.

  Alhaj Mwanga aliomba wananchi wawaunge mkono kumaliza adha ya uhaba wa majengo hasa ya madarasa na vyoo katika shule za msingi na sekondari.Nae mkuu wa mkoa wa Pwani mhandisi Evarist Ndikilo,alifika katika shule hiyo kutembelea kujua namna ujenzi unavyoendelea na kushirikiana na wananchi katika ujenzi huo.

  Mkuu huyo wa mkoa alimpongeza mkuu wa wilaya hiyo kwa hatua ya kuhamasisha ujenzi wa kuongeza majengo ya madarasa wilayani humo kwani ni jitihada nzuri na ya kuigwa katika wilaya nyingine.Mhandisi Ndikilo alisema tatizo la upungufu wa madarasa wilayani hapo limebaki historia hivyo ni wakati wa kuunga mkono jitihada za mkuu wa wilaya kuelekeza nguvu katika kutatua changamoto ya uhaba wa madarasa .

  Alisema viongozi wanapaswa kujitoa,kuwa wabunifu badala ya kujibweteka wakisubiria kufuatwa na wananchi maofisini hali ambayo inapaswa ibadilike.Mhandisi Ndikilo aliiomba jamii kujenga tabia ya kushirikiana na serikali kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo pasipo kuiachia serikali pekee.

  Aliahidi kuendelea kutafuta wadau watakaoweza kuwezesha vifaa vya ujenzi vitakavyosaidia kumaliza ujenzi uliobakia na kukarabati baadhi ya shule zilizo kwenye zoezi lililoanzishwa na wilaya hiyo.Diwani wa kata ya Kibindu ,Ramadhani Mkufya alisema shule ya msingi Kibindu inakabiliwa na changamoto ya madarasa lakini wanashukuru wananchi wamejitolea nguvu kazi ili kukamilisha ujenzi huo.

  Mkufya alisema kwa kushirikiana na mbunge wa jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete,amesaidia mifuko ya saruji 200 na mabati 120 ambayo ndio wameanzia kazi ya ujenzi hivyo wanamshukuru kwa msaada huo.“Shule hiI itakapomalizika itakuwa na madarasa saba ,na anaomba wadau wa elimu waweze kujitolea misaada mbalimbali ikiwemo nondo,mbao ili kumaliza tatizo la majengo katika shule zilizopo kata ya Kibindu “alielezea Mkufya.

  Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Kibindu ,Furaha Funga ,alisema mwaka 2014 baadhi ya madarasa katika shule hiyo yaliezuliwa na mvua zilizonyesha kipindi hicho.Alisema msaada alioutoa mbunge wa jimbo la Chalinze umesaidia kuanza kwa ujenzi wa madarasa hayo ili yaweze kusaidia kuondoa adha iliyopo.Mwalimu Funga alibainisha kwamba hivi karibuni Ridhiwani pia alitoa mabati 800 na mifuko ya saruji 1,110 vyenye thamani ya sh.26 kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa madarasa ya shule za msingi za Machala,Malivundo na Kwaikonje ikiwemo Kibindu.

  Alimshukuru mkuu wa wilaya alhaj Mwanga, mbunge Ridhiwani na mkuu wa mkoa wa Pwani mhandisi Ndikilo kwa kuonyesha moyo wao wa kuhamasisha nguvu kazi na wadau.

  0 0

   Baadhi ya wapanda boda boda kati ya 250 waliojiunga na Mfuko wa Pensheni wa PPF kupitia mpango wa "Wote Scheme wilayani Temeke jijini Dar es Salaam, wakionyesha mfano wa kadi za kujiunga na mpango huo baada ya kukabidhiwa na Mkuu wa wilaya ya Temeke, Bw. Felix Jackson Lyaviva, wakati wa uzinduzi wa wiki ya nenda kwa usalama mkoani Dar es Salaam, Novemba 7, 2016.
   Bw. Lyaviva, akimkabidhi mfano wa kadi ya uanachama wa PPF, mpanda bodaboda, Mkemwa William Faustin.

  NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID.

  MFUKO wa Pensheni wa PPF umeendelea na kampeni yake ya kuandikisha wanachama wapya kupitia mpango wa “Wote Scheme”, unaohusisha wafanyakazi walio katika sekta rasmi na wale waliojiajiri wenyewe ambapo katika uzinduzi wa wiki ya nenda kwa usalama mkoani Dar es Salaam, zaidi ya waendesha bodaboda 250, kutoka wilaya ya Temeke, walijiunga na mpango huo.

  Katika uzinduzi huo uliofanyika viwanja vya Mwembe-Yanga, wilayani humo Novemba 7, 2016, Mkuu wa wilaya ya Temeke, Bw. Felix Jackson Lyaviva, ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, aliwakabidhi kadi za uanachama wa Mfuko huo baadhi ya waendesha bodaboda hao.

  Akizungumza baada ya zoezi hilo la kuwakabidhi kadi hizo, Meneja Uhusiano wa PPF, Bi. Lulu Mengele alisema, zoezi la kuandikisha wanachama wapya wakiwemo hao wa bodaboda, litakwenda sambamba na maadhimisho ya Wiki ya nenda kwa usalama ambayo itafanyika kwenye wilaya za Ilala, na Kionondoni pia.

  “Tunatoa wito kwa, wananchi wote, wakiwemo wajasiriamali, mama lishe, bodaboda, machinga, kujiunga na mpango huo ambao una faida nyingi ikiwemo kujipatia bima ya afya, mikopo ya elimu na mafao mengine mengi.” Alifafanua.
   Bw. Lyaviva, akimkabidhi mfano wa kadi ya uanachama wa PPF, mpanda bodaboda, Lowowa Emmanuel Julius
   Bw. Lyaviva, akimkabidhi mfano wa kadi ya uanachama wa PPF, mpanda bodaboda, Rubamande Ratifa Ally
   Bw. Lyaviva, akimkabidhi mfano wa kadi ya PPF, Bw. Shinne Gustaph Patrick
   Mkuu wa wilaya ya Temeke, Felix Jackson Lyaviva, akimpongeza mwanachama mpya wa PPF, ambaye ni dereva wa Bodaboda, Bw.
  Mkemwa William Faustin
  Mkuu wa wilaya ya Temeke, Felix Jackson Lyaviva, akisalimiana na Kamanda wa Polisi Kanda  ya Temeke, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, (SACP), Gilles Mroto wakati akiwasili. Kulia ni Kamanda wa Polisi Kanda ya Ilala, Salum Hamduni
   Kamanda wa polisi wa Kikosi cha Usalama Barabarani wilaya ya Temeke, Mrakibu Msaidizi wa Polisi, (ASP), Solomon Mwangamilo, akizungumza jambo na Meneja Uhusino wa PPF, Bi. Lulu Mengele. Kushoto ni Afisa Uhusiano wa Shirika la Nyumba la Taifa, (NHC), Bw. Yahya Charahani
   Mkuu wa wilaya ya Temeke, Felix Jackson Lyaviva, akisalimiana na Kamanda wa Polisi Kanda ya Ilala, Salum Hamduni
   Mkuu wa wilaya ya Temeke, Bw. Felix Jackson Lyaviva, akisalimiana na Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani, Wilaya ya Temeke, ASP, Solomon Mwangamilo
   Meneja Uhusino wa PPF, Bi. Lulu Mengele, akisalimiana na Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani wilaya ya Kinondoni, Kamishna Msaidizi wa Polisi, (ACP_, Theopista Malya
   Meneja Uhusino wa PPF, Bi. Lulu Mengele, akisalimiana na Mkuu wa Kituo cha Polisi, (OCS), cha Mabasi ya Mkoa, Ubungo Bus Terminal, Mrakibu Msaidizi wa Polisi, (ASP), Sarah Bundala
   Polisi wa usalama barabarani wakiingia kwa maandamano kwenye viwanja vya Mwembe-Yanga
   Askari wa usalama barabarani akiyaelekeza magari yaliyoshiriki kwenye maanadamano siku ya uzinduzi wa wiki ya nenda kwa usalama mkoa wa Dar es Salaam, viwanja vya Mwembe-Yanga
   Waendesha Bodaboda wakiwasili kwa maandamano kwenye viwanja hivyo
   Mwanachama mpya wa PPF, ambaye ni mwendesha bodaboda, Ratifa Ally, (kushoto), akibadilishana mawazo na Maafisa wa PPF Kanda ya Temeke, Elizabeth Chambiri, (kulia) na Donald Maeda
   Brass Band ya polisi ikiongoza maandamano
   Mkuu wa wilaya ya Temeke, Bw. Felix Jackson Lyaviva, (kulia), akipatiwa malezo ya shughuli za Mfuko wa Pensehni wa PPF, kutoka kwa Msimamizi wa Kanda ya Temeke, Sospeter Lyimo, (wapili kushoto). Kulia ni Bi. Elizabeth Chambiri
  Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PPF, Bi. Jannet Ezekiel, akimpatia maelezo Afisa huyu wa polisi kuhusu mpango wa Wote Scheme, ambao Polisi nao wanaweza kujiunga nao
  Mwanachama mpya akisajiliwa kujiunga na Wote Scheme

  0 0


  0 0

    Askari wa usalama barabarani koplo Atilio Choga akiwa anatoa maelezo mafupi ya barabara zilizopo mkoani Arusha na jinsi magari yanavyoingia na kutoka  katika siku ya uzinduzi wa wiki ya usalama barabarani ilianza Jana katika viwanja vya sheikh Amri Abeid ,mbele ni mkuu wa wawilaya ya Arusha Fabian Daqarro ambapo alikuwa mgeni rasmi
   askari polisi wa kikosi cha usalama barabarani akimuonyesha mgeni rasmi ambaye ni mkuu wa wilaya ya Arusha jinsi kifaa chakupimia ulevi kwa madereva kinavyo fanya kazi

   kabla ya sherehe kuanza kulikuwa na maaandamano  apa askari wa kikosi cha usalama barabarani wakiwasili katika viwanja vya sheikh Amri Abeid kwa maandamano
   kikundi cha walemavu wao pia walijitokeza katika sherehe hizi za uzinduzi wa siku ya usalama barabarani 
   kikundi cha ngoma cha wanafunzi   nacho kilikuwepo katika sherehe hizi za siku ya usalama barabarani

   wageni waalikwa wakiwa wanafatilia uzinduzi huo leo katika viwanja vya kumbukumbu ya Sheikh Amri Abeid
   kamanda wa kikosi cha usalama barabarani Nuru Selemani  akiwa anasoma risala
  mkuu wa wilaya ya Arusha Fabian Daqaro katikati akiwa anaandika baadhi ya changamoto alizotajiwa 
  Habari Picha na Woinde Shizza,Arusha

  Ajali za pikipiki kwa mkoa wa Arusha zimeongezeka mwaka hadi mwaka ambapo mpaka kufikia mwaka 2015 zilifika ajali 836 huku upande ajali za magari zikipungua kwa asilimia 11

  Hata ivyo ajali hizo za pikipiki kwa mwaka 2010 zilikuwa 709 ukilinganisha na ajali 277 za pikipiki mwaka 2009 ajali hizo za pikipiki bado zinaendelea kuongezeka.

  Hayo yamebainishwa na kamanda wa kikosi cha usalama barabarani Nuru Selemani wakati akielezea hali ya usalama wa barabarani kwenye uzinduzi wa maazimisho ya wiki ya usalama barabarani  mapema leo 

  Selemani alisema kuwa takwimu zinaonesha mkoa wa Arusha bado unakabiliwa na ajali za barabarani ambapo kwa kipindi cha mwaka 2007 ajali zimekuwa zikiongezeka na kulikuwa na ajali 1807na kufikiakiwango cha juu mwaka 2010 ambapo ajali 2658 huku kwa kipindi cha mwaka 2012 ajali zilianza kupungua hadi kufikia ajali 2011

  Alifafanua kuwa baada ya jeshi kutumia nguvu kubwa sana katika kupunguza ajali zinazotokana na magari zilipungua sana ingawaje kwa sasa bado wimbi kubwa la ajali linatokana na ajali za pikipiki.

  Katika hatua nyingine alisema kuwa ajali zinasababishwa na sababu za kibinadamu kwa asilimia 75,madereva kulewa huku wakiwa wanaendesha vyombo vya moto,pia ubovu wa vyombo vya usafiri kwa asilimia 15,miundombinu ya barabara kwa asilimia10.

  Awali mgeni rasmi katika uzinduzi huo mkuu wa wilaya ya Arusha Fabian Daqaro alisema jukumu la usalama wa barabarani sio la polisi wenyewe wala kamati ya kikosi cha usalama barabarani pekee bali ni ulinzi wa kila mtu.

  Fabian alisema kuwa endapo kama kila mtu atafuata sheria na kanuni za barabarani basi ajali zitakuwepo kwa kiwango cha asilimia 0.0 kwani ajali zinachangia kudidimiza mlengo wa taifa.

  Hataivyo katika uzinduzi huo baadhi ya askari wa usalama barabarani walifanikiwa kupewa vyeti vya ufanyakazi bora ambapo mmoja wa askari hao Silas Konga alisema kuwa maadili yao bora kazini yamechangia wao kutambulika na jeshi hilo.

  0 0

  MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akisalimiana na Viongozi wa Dini wakati akiwasili katika ukumbi wa Chuo cha Amali Vitongoji Pemba, kuzungumza na Waumini wa Dini na kuzindua Albam la Kwaya ya R.G.C, ya chakechake.9Picha na Othman Maulid) 7-11-2016
  MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akiangalia bidhaa zinazotengenezwa na Kikundi cha Wawanawake cha Nia Njema cha Wete Pemba wakati wa mkutano huo na Viongozi wa Dini Kisiwani Pemba uliofanyika katika Ukumbi wa Chuo cha Amali Vitongoji.(Picha na Othman Maulid)
  MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akizungumza na Waumini madhehebu mbalimbali ya dini ya Kikristo kisiwani Pemba wakati wa mkutano wake wa kutoa shukrani kwa ushirikiano wao katika shughuli na maendeleo na kudumisha amali Zanzibar na hafla ya uzindua Albam ya Kwanya ya Kikundi cha Kanisa la R.G.C, Chakechake Pemba iliozinduliwa katika ukumbi wa Chuo cha Amali Vitongoji Pemba leo.(Picha na Othman Maulid)
  MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akizungumza na Waumini wa Dini wa madhehebu mbalimbali ya Kikristo kisiwani Pemba wakati wa mkutano wake wa kuwashukuru kwa ushirikiano katika shughuli za maendeleo na kudumisha amani na kuwazinduliwa Albam ya Kwaya ya Kanisa la R.G.C Chakechake, uliofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Amali Vitongoji Pemba. kulia Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman na Mchungaji wa Kanisha la Anglikana Zanzibar Emanuel Masoud.(Picha na Othman Maulid) 
  BAADHI ya Waumini wa madhehebu mbalimbali wa Dini ya Kikristo kisiwani Pemba wakimsikiliza Mke wa Rais wa Zanzibar akitowa nasaha zake kwa waumini hao katika ukumbi wa Chuo cha Mafunzo ya Amali Vitongoji Pemba.(Picha na Othman Maulid)
  MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akizindua Albam ya Kwaya ya Kanisa la T.G.C ya Nyimbo za kuitakia Amani Zanzibar uzinduzi huo umefanyika kastika Ukumbi wa Chuo cha Mafunzo ya Amali Vitongoji Pemba kulia Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman na Mchungaji wa Kanisa la Anglikana Zanzibar Emanuel Masoud.(Picha na Othman Maulid)
  MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akionesha Albam ya Kwaya ya R.G.C ya Chakechake baada ya kuinduwa ikiwa na nyimbo za kuitakia Amani Zanzibar uzinduzi huo umefanyika katika ukumbi wa Chuo cha Mafunzo ya Amali Vitongoji Pemba.(Picha na Othman Maulid)

  0 0

  Mkurugenzi wa Idara ya Habari, MAELEZO Bw. Hassan Abbas akiwaonyesha waandishi wa habari mwongozo wa utengenezaji wa Tovuti za Serikali wakati wa mkutano wake na waandishi hao hivi karibuni Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Meneja wa Habari, Elimu na Mawasiliano wa Wakala ya Serikali Mtandao Bibi. Susan Mshakangoto.

  Picha na MAELEZO

   Mkurugenzi wa Idara ya Habari, MAELEZO Bw. Hassan Abbas akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu taasisi za Serikali kutekeleza agizo la kuhuisha taarifa na huduma katika Tovuti zao mapema kabla ya mwisho wa mwezi huu katika mkutano uliofanyika Ofisi za Wakala ya Serikali Mtandao (EGA) hivi karibuni Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Meneja wa Habari, Elimu na Mawasiliano wa Wakala ya Serikali Mtandao Bibi. Susan Mshakangoto. 

   Meneja wa Habari, Elimu na Mawasiliano wa Wakala ya Serikali Mtandao Bibi. Susan Mshakangoto akifafanua jambo kwa waandishi wa habari wakati wa mkutano na waandishi hao hivi karibuni jijini Dar es Salaam, kuhusu taasisi za umma kuhuisha taarifa katika Tovuti zao. Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari, MAELEZO Bw. Hassan Abbas.

  Na Ismail Ngayonga-MAELEZO,Dar es Salaam.

  SERA ya Taifa ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ya mwaka 2003, pamoja na mambo mengine inasisitiza umuhimu wa Serikali kutumia fursa za TEHAMA katika utendaji kazi wa kila siku na utoaji huduma kwa wananchi.

  Katika kutekeleza sera hiyo, mwaka 2004 Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma (OR-MUU) ilianza kuchukua hatua mbalimbali kuongeza matumizi ya TEHAMA katika kuimarisha mifumo ya utoaji habari na huduma kwa wananchi. 

  Moja ya maeneo ya TEHAMA ambayo Serikali imewekeza na kupata mafanikio makubwa ni pamoja na eneo la tovuti ambapo hadi kufikia mwaka 2010 takribani Taasisi zote za Serikali zilikuwa na tovuti.

  Katika kipindi cha mwaka mmoja wa Serikali ya Awamu ya Tano, kumekuwepo na mapinduzi makubwa katika mfumo wa upashanaji wa habari na utoaji wa huduma kwa umma kupitia tovuti. 

  Mtendaji Mkuu wa Serikali Mtandao, Dkt. Jabiri Bakari anasema taasisi za umma zinapaswa kuwa na tovuti zitakazosaidia wananchi kupata kwa urahisi taarifa zinazohusu shughuli na huduma mbalimbali zinazotolewa na taasisi hizo.

  “Tovuti za Serikali zinatakiwa kuwa kwa lugha ya Kiswahili na Kiingereza na mwananchi anapofungua tovuti hizo lugha itakayoonekana kwanza iwe ni Kiswahili na muda wowote mwananchi huyo anaweza kubadili kwenda kwenye lugha ya Kiingereza”.

  Dkt. Bakari amesema kuwa Wakala imetoa miongozo ya kusimamia na kuendesha tovuti hizo na unapatikana kwenye tovuti ya Wakala www.ega.go.tz sehemu ya Miongozo na Viwango.

  Akizungumzia mafanikio ya Wakala hiyo, Dkt. Jabiri anasema Wakala imetengeneza mifumo mbalimbali na kuweka miundombinu ya kuwezesha taasisi za umma kutumia Tehama katika utoaji wa huduma kwa wananchi. 

  “Tovuti Kuu ya Serikali ni zao la kwanza la Wakala na ilibuniwa na kusanifiwa na wataalam wa ndani. Katika tovuti hiyo ambayo pia ni mfumo, ina taarifa za baadhi ya taasisi za umma, sekta mbalimbali na huduma zake pamoja na balozi zilizoko nchini na zile za kwetu zilizoko nje ya nchi”, anasema Dkt. Bakari. 

  Anaongeza kuwa mfumo mwingine uliotengenezwa na Wakala hiyo ni Tovuti Kuu ya Ajira ambayo humwezesha mwananchi kuona ajira mbalimbali zinazotangazwa na Serikali ambapo muombaji wa ajira anaweza kutuma wasifu wake kwa njia ya mtandao na nafasi zinapotangazwa zenye kuhitaji mtu mwenye sifa hizo.

  Kwa mujibu wa Dkt Jabiri anasema jitihada mbalimbali zinatekelezwa na Wakala ili kuwezesha taasisi za umma kutoa huduma zao kwa njia ya mtandao kwa kuongeza uwezo wa wataalam wa Tehama kwa kuwapa maarifa na ustadi wa kubuni.

  Dkt. Jabiri anasema Wakala imetoa mafunzo kuhusu usimamizi na Ujenzi wa Mtandao wa Mawasiliano Serikalini kwa taasisi za umma 149 wakiwemo Maofisa TEHAMA 226, Mafunzo ya uendeshaji wa Vituo vya data kwa Taasisi za umma 91 wakiwemo Maofisa TEHAMA 162.

  Aidha Mafunzo ya Usimamizi wa Mfumo wa Barua Pepe Serikalini yametolewa kwa taasisi 157 pamoja na Mafunzo ya usimamizi wa taarifa tovuti za serikali yametolewa kwa taasisi 71.“Mafunzo ya uwekaji taarifa katika tovuti kuu yametolewa kwa taasisi 86 na Mafunzo hayo yanaendelea kutolewa kwa kila taasisi ambayo inatengenezewa Tovuti na Wakala” anasema Dkt. Jabiri.

  Kwa upande wake Meneja Habari, Elimu na Mawasiliano wa Wakala wa Serikali Mtandao, Suzan Mshakangoto anasema mbali na kuanzisha mtandao huo Serikali imeziagiza taasisi zote za umma kuhuisha taarifa katika tovuti zake na Tovuti Kuu ya Serikali (www.tanzania.go.tz). 

  Anaongeza kuwa tangu kuanzishwa kwa tovuti hizo kumesaidia kuongeza kasi ya utendaji, uwazi, ufanisi, uwajibikaji na tija katika utoaji wa taarifa na huduma kwa wananchi, pamoja na changamoto kadhaa zilizojitokeza katika usimamizi wa tovuti hizo. Akifafanua zaidi anasema miongoni mwa changamoto hizo ni pamoja na tovuti za taasisi za umma kutokuwa na taarifa mpya na za mara kwa mara, na kutofuatwa kwa mwongozo uliowekwa unaosisitiza usanifu wa tovuti hizo.

  Naye Mkurugenzi wa Habari, Hassan Abbas anasema ofisi yake kwa kushirikiana na e-GA tayari imezisaidia Halmashauri 93 kuhuisha taarifa zilizopo katika tovuti zao ili kuwawezesha wananchi kufahamu huduma mbalimbali zinazotolewa na Serikali katika maeneo yao.

  Abbas anasema tovuti ni mojawapo ya nyenzo na njia rahisi na ya haraka ya kutoa taarifa na kufikisha huduma kwa umma kwani miaka ya nyuma taarifa na huduma za Serikali zilitolewa kwa njia ya kutembelea ofisi husika au kwa kupitia vyombo vya habari. 

  Anasema Serikali imetoa mafunzo kwa Maafisa Habari katika Wizara, Idara, Wakala na Taasisi mbalimbali jinsi ya kuboresha taarifa katika tovuti zao, na kuanzia sasa ofisi yake itaanza kufanya tathimini ili kufahamu Wizara ambazo hazijaanza kuhuisha taarifa zake.

  Kwa mujibu wa Abbas anasema Serikali imekusudia kupanua wigo wa mawasiliano katika Wizara, Idara, na Taasisi zake kwa kuwahimiza Maafisa Habari kutumia zaidi mitandao ya kijamii kwa ajili ya kujibu na kutoa ufafanuzi wa hoja mbalimbali zinazoelekezwa kwa Serikali.Katika kuboresha mfumo wa mawasiliano Serikalini, ofisi yake imeanzisha akaunti ya twitter ya; msemaji wa Serikali@TZ_Msemaji Mkuu ambayo mwananchi anaweza kuifuata akaunti hiyo kwa kutafuta Msemaji Mkuu wa Serikali on Twitter.

  Anasema wananchi wengi kwa sasa wamekuwa wakitumia mitandao ya kijamii kwa ajili ya kuendesha mijadala mbalimbali ambayo baadhi yao imekuwa ikipotosha ukweli kuhusu utelekezaji wa sera mbalimbali za Serikali.Abbas anasema jukumu la kuboresha mawasiliano kati ya Serikali na Wananchi ni suala mtambuka, na hivyo ni wajibu wa Maafisa Habari wa Wizara, Idara, Taasisi, Wakala za Serikali kutoogopa kutoa taarifa muhimu kwa waandishi wa habari.

  “Waandishi wa habari wasitoe taarifa zisizofanyiwa utafiti wa kutosha kwa wananchi, ni vyema sote tushirikiane katika kutoa taarifa sahihi kwa wananchi kuhusu sera na mikakati ya serikali ili kuleta maisha bora kwa watanzania wote” anasema Abbas.

  Kwa kutambua umuhimu wa tovuti kama nyenzo kuu ya mawasiliano, Serikali kupitia Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Umma (PS3) unaofadhiliwa na shirika la misaada la Marekani iliunda kikosi kazi kwa ajili ya uhuishaji wa tovuti za Mamlaka ya Serikali za Mitaa (TAMISEMI).

  Kikosi kazi hicho kinahusisha Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Ofisi ya Rais- Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), na Wakala wa Serikali Mtandao (E-GA).Msimamizi wa Mifumo ya Taarifa wa PS3, Bunto Mbozi anasema tovuti nyingi za TAMISEMI zimetengenezwa, zinasimamiwa na kuendeshwa bila kuwepo na utaratibu unaofanana, hali hiyo inasababisha uwepo wa tovuti zisizokidhi viwango na ubora kufuatana na mahitaji ya watumiaji.

  Anaongeza kupitia mradi, PSE3 imekusudia kuhuisha taarifa zote za tovuti za Serikali, ambapo kwa sasa wataanza na Halmashauri 93 nchini na baadae katika Wizara, Idara, Taasisi nyingine za Umma.Bunto anasema mradi huo ulizinduliwa mapema mwaka huu mkoani Iringa ambapo hadi kufikia mwezi Agosti mwaka huu, jumla ya mikoa 13 ilifikiwa na taasisi hiyo na kuendesha mahojiano na Watendaji Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Idara na vitengo mbalimbali.

  Anaitaja mikoa hiyo kuwa ni Iringa, Shinyanga, Dodoma, Mbeya, Mwanza, Kagera, Mara, Rukwa, Kigoma, Lindi, Mtwara na Morogoro.Akifafanua zaidi anasema katika utafiti uliofanyika ulibaini kuwa mikoa mingi ilianza kutengezeza tovuti zao lakini hazikikuwa na taarifa muhimu zinazohitajika na wananchi wa kawaida.

  “Tovuti ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inatembelewa na watu zaidi ya 500,000 kwa siku, hii inatokana na mahitaji ya huduma inazotoa TRA kwa wananchi, hivyo mradi huu pia umekusudia kuzifanya tovuti za Mikoa na Halmashauri kutembelewa na wananchi wengi zaidi” anasema Bunto. 

  Kwa mujibu wa Bunto anasema, mradi huo uliichagua TAMISEMI kutokana na Ofisi hiyo kutoa huduma muhimu zinazomgusa wananchi wa kawaida ikiwemo afya, maji, elimu, mazingira, uvuvi, ufugaji na kadhalika, ambapo wananchi wengi wanapenda kufuatilia taarifa na huduma hizo katika ofisi za umma.

  Anaongeza uhuishaji wa taarifa za tovuti utasaidia kutangaza fursa na rasilimali za kiuchumi zilizopo katika mikoa, hatua itayoziwezesha halmashauri nyingi kuibua vivutio vya uwekezaji sambamba na kuboresha utoaji huduma kwa wananchi.

  0 0

  MKURUGENZI Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Mhandisi Felchesmi Mramba, (mbele kulia), akikagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa kufua umeme wa gesi wa Kinyerezi II jijini Dar es Salaam.
  NA K-VIS BLOG/KAHLFAN SAID
  MKURUGENZI Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Mhandisi Felchesmi Mramba, (anayezungumza pichani), amesema ameridhishwa na kasi ya ujenzi wa mradi wa umeme wa gesi wa Kinyerezi II utakaozalisha umeme wa Megawati 240 unaotekelezwa na shirika hilo jijini Dares Salaam.

  Mradi huo ulizinduliwa Machi 2016 kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dkt. John Pombe Magufuli, kuweka jiwe la msingi  ambapo eneo hilo lilikuwa pori tu kazi ya kusafisha eneo ili kuanza ujenzi ilianza mieziminane iliyopita.

  “Kwa wale waliokuwepo siku Mheshimiwa Rais anaweka jiwe la msingi la ujenzi wa mradi huu, mtakumbuka kuwa eneo lote hili lilikuwa pori, napenda niwapongeze wahandisina mafundiwote mnaotekeleza ujenzi huu kwa kazi nzuri nakasi ya kuridhisha.” Alipongeza Mhandisi Mramba, ambaye alitembelea eneo hilo mwishoni mwa wiki kukagua maendeleoyaujenzi wake.

  Wahandisi wa TANESCO wakishirikiana na wenzao kutoka SUMITOMO CORPORATION NA TOSHIBA za Japan na washauri wa mradi Lahmeyer International ya Humburg nchini Ujerumani, ndio wanaojenga mitambo hiyo kwa ambapo unatekelezwa kwa fedha za walipa kodi wa Tanzania na Japan.

  Akitoa taarifa ya maendeleo ya ujenzi huo, Meneja Mradi, Mhandisi Stephen Manda alisema ni pamoja na ujenzi wa msingi wa kitalu namba moja (Foundation Works Block I na ujenzi wa msingi watenki la kuhifadhia maji (raw water tank).

  “Kazi inaendelea vizuri napenda kukujulisha kuwa baadhi ya vifaa muhimu vimekwisha wasili na tunachosubiri pengine kufikia mwezi Januari ni kuwasili kwa mashine zenyewe (Turbines), hivi sasa tuko kwenye mazungumzo na watu wa TANROAD na mamlaka nyingine kuhusu utaratibu wa kusafirisha mitambo hiyo kutoka bandarini kuiletahapa.” Alifafanua Mhandisi Manda.

  Akielezea zaidi kuhusu manufaa ya mradi huo pindi utakapokamilika, Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhanidis Felchesmi Mramba alisema, TANESCO iliwaahidi watanzania kuwa kwa kushirikiana na serikali itaendelea kuboresha miundombinu ya umeme ikiwa ni pamoja na kuzalisha umeme mwingi zaidi ili hatimaye uende sambamba na malengo ya serikali yaawamu ya Tano ambayo imedhamiria kujenga nchi ya viwanda.
  “Nia yan Mheshimiwa rais ya kujenga nchi ya viwanda itafanikiwa kwa vile sasa umeme mwingi na wa uhakika utapatikana ili kuhudumia viwanda vilivyopo na vipyavinavyoendelea kujengwa.”Alihitimisha Mhandisi Mramba.
   Mhandisi Mramba, (kulia), akiongozana na Meneja Mradi wa ujenzi wa Kinyerezi II, Mhandisi Stephen Manda
   Ujenzi wa msingi wa tenki la kuhifadhia maji (raw water tank)
   Ujenziwa msingi wa moja ya sakafu ya kufunga mashine za kufua umeme, (Foundation work block).

   Mhandisi Manda, (kulia), akifafanua masuala mbalimbali yahusuyo maendeleo ya ujenzi huo
   Mhandisi Manda akiwasilisha taarifa ya hatua mbalimbali za ujenzi wa mradi huo
   Jengo la muda la utawala
   Kazi ya kuhamisha kifusi ikiendelea
   Mhandisi Manda aakionyesha kitu
   Meneja Mwandamizi wa TANESCO anayeshughulikia miradi ya usafirishaji na usambazaji umeme, Mhandisi Gregory Chegere (kulia), akizungumza jambo na mmoja wa Wahandisi viongozi kutoka kampuni ya TOSHIBA ya Japan
   "Mambo swafi" ndivyo anavyoonekana akisema, Mhandisi Mramba, wakati akianza ukaguzi wa mradi huo akifuatana na Meenja Mradi, Mhandisi Manda (kushoto)
   Mameneja na maafisa wa TANESCO waliofuatana na Mkurugenzi Mtendaji kutembelea eneo hilo
   Mhandisi kiongozi wa kampuni ya TOSHIBA
  Mameneja na maafisa wa TANESCO


  0 0

  Ujumbe kutoka kutoka jimbo la Eastern Cape kutoka nchini Afrika ya Kusini uko Nchini kwa ajili ya kujifunza kutoka Tanzania namna bora ya fursa za kiuchumi kwa wanawake nchini, uwezeshaji wa wanawake na uendeshaji wa Benki ya Wanawake Nchini. 

  Akiongea na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga kiongozi wa Msafara wa ujumbe toka Afrika Kusini Mhe. Nancy Sihiwaji Mbunge wa Jimbo la Eastern Cape amesema ziara yaoa inatokana na utekelezaji wa maazimio ya mkutano wa Wanawake Afrika uliofanyika Nchini Afrika ya kusikini kuhusu uwezeshaji wanawake kiuchumi. 

  Aidha ujumbe huu umetambelea Wizara hii ili kujifunza na kupata uzoefu kutoka Nchini ni kuona ni jinsi gani Tanzania kwa kushirikiana na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Njinsia, Wazee na Watoto wameweza kuanzisha na kufungua Benki inayolenga kuwainua wanawake kiuchumi.
  Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Njinsia, Wazee na Watoto akiongea na wajumbe wa ujumbe wa jimbo la Eastern Cape hawapo pichani kutoka Afrika Kusini leo ofisini kwake.
  Mhe. Nancy Sihiwaji Mbunge wa Jimbo la Eastern Cape akimkabidhi Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga zawadi ya sikafu yenye ujumbe kutoka Jimbo la Eastern Cape leo ofisini kwake jijini Dar es Salaam kutoka kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Jinsia kutoka Wizara hiyo Bw. Timoth Mgonja. 
  Mhe. Nancy Sihiwaji Mbunge wa Jimbo la Eastern Cape akimkabidhi Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga zawadi ya sikafu yenye ujumbe kutoka Jimbo la Eastern Cape leo ofisini kwake jijini Dar es Salaam kutoka kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Jinsia kutoka Wizara hiyo Bw. Timoth Mgonja.
  Mhe. Nancy Sihiwaji Mbunge wa Jimbo la Eastern Cape na ujumbe wake pamoja na Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga wote katikati wakiwa katika picha ya pamoja leo walipomtembelea kwa ziara ya mafunzo ya siku moja kupata uzoefu wa uwezeshaji wanawake kiuchumi hapa Nchini.

  PICHA ZOTE NA ANTHONY ISHENGOMA

  0 0

   Aliyewahi kuwa Waziri wa elimu na Utamaduni katika Serikali ya awamu ya tatu  Mhe. Joseph Mungai (pichani), amefariki dunia leo majira ya saa 11 jioni. 
  Msemaji wa Hospitali hiyo, Aminiel Eligaesha amesema kuwa marehemu Mungai amefikishwa katika hospitali hiyo akiwa tayari amekwisha fariki na kwamba kwa upande wao hawajatoa matibabu yoyote zaidi ya huduma ya chumba cha kuhifadhia maiti (Mochwari)

  "Ni kweli tumempokea Mungai, lakini alikuwa tayari amekwisha fariki, tunachosaidia sisi ni mochwari tu, kwahiyo kusema kuwa amefia Muhimbili siyo sahihi" Amesema Eligaesha.


  Kuhusu chanzo cha kifo chake, Eligaesha amesema hadi sasa bado hakijafahamika, hadi uchunguzi utakapofanyika kwa kuwa hakufia katika hospitali hiyo. "Hatuwezi kusema nini chanzo hilo ni jukumu la familia, na pia kwa kuwa hajafia hapa hatuwezi kujua hadi postmoterm ifanyike, kwa sasa amehifadhiwa hapa" Alimalizia Eligaisha.


   Mungu ilaze roho ya Marehemu mahala pema peponi, Amina
  0 0

  Katibu Tawala wa Mko wa Dar es Salaam, Theresia Mbando, akizungumza wakati akifungua rasmi Mafunzo ya Kampeni ya awamu ya tatu ya 'TUNAWEZA' lenye lengo la kuondoa aina zote za Ukatili wa kijinsia dhidi ya Wanawake, yaliyofanyika leo Nov 8, 2016 kwenye Hoteli ya Jamirex iliyopo Mwenge jijini Dar es Salaam,leo.  Kushoto ni Mratibu wa Mafunzo hayo, Rehema Msami, kutoka Kituo cha Msaada wa Sheria kwa Wanawake (WLAC).
   Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wakiwa bize kunakili kile anachokiwasilisha Katibu Tawala wakati wa ufunguzi huo.

   Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wakiwa katika mafunzo hayo.
   Katibu Tawala wa Mko wa Dar es Salaam, Theresia Mbando, akizungumza wakati akifungua rasmi Mafunzo ya Kampeni ya awamu ya tatu ya 'TUNAWEZA' lenye lengo la kuondoa aina zote za Ukatili wa kijinsia dhidi ya Wanawake, yaliyofanyika leo Nov 8, 2016 kwenye Hoteli ya Jamirex iliyopo Mwenge jijini Dar es Salaam,leo.  Kushoto ni Mratibu wa Mafunzo hayo, Rehema Msami, kutoka Kituo cha Msaada wa Sheria kwa Wanawake (WLAC).
   Mratibu wa Mafunzo hayo, kutoka Kituo cha Msaada wa sheria kwa Wanawake (WLAC) Rehema Msami, akifafanua jambo kuhusu mafunzo hayo wakati wa ufunguzi huo.
   Mwanasheria wa Kituo cha Msaada wa Sheria kwa Wanawake, Karilo Karilo, akizungumza kabla ya mgeni rasmi kufungua mafunzo hayo.

  Sehemu ya washiriki wa mafunzo hayo.

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimpa pole mke wa aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM Zanzibar, Marehemu Ferouz Bi. Shara Ferouz nyumbani kwake Mtaa wa Mbweni Zanzibar.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa amejumuika kwenye  na ndugu na jamaa msibani kwa aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM Zanzibar, Marehemu Salehe Ramadhan Ferouz  nyumbani kwake Mtaa wa Mbweni Zanzibar.
   Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM Zanzibar, Marehemu Salehe Ramadhan Ferouz likitolewa nyumbani kwake Mtaa wa Mbweni Zanzibar tayari kwenda kuswaliwa.

  0 0

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Balozi wa Uingereza nchini, Mheshimiwa Sarah Cooke, ofisini kwake bungeni mjini Dodoma Novemba 8, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  …………………………………………

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameiomba Serikali ya Uingereza ihamasishe wawekezaji zaidi kutoka nchini humo ili waje kuwekeza kwenye sekta ya viwanda.

  Ametoa kauli hiyo leo (Jumanne, Novemba 8, 2016) wakati akizungumza na Balozi wa Uingereza hapa nchini, Bibi Sarah Cooke alipokutana naye ofisini kwake Bungeni, mjini Dodoma.

  “Mheshimiwa Balozi utusaidie kualika wawekezaji wengi zaidi kwenye maeneo ya kilimo, viwanda vya usindikaji mazao ya wakulima, wavuvi na wafugaji, sekta ya mafuta na gesi, nishati na ujenzi wa makazi hasa kwa mkoa wa Dodoma ambako hivi sasa ni Makao Makuu ya Serikali,” amesema.

  Amemweleza Balozi huyo kwamba Tanzania imedhamiria kuwa nchi ya uchumi wa kati na hivyo imejipanga kuwa na viwanda vya kutosha ili iweze kusindika mazao yake hapa nchini na itoe ajira kwa wananchi wake.

  Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo pia kuishukuru Serikali ya Uingereza kwa msaada wake mkubwa wa ujenzi wa nyumba za walimu na shule mkoani Kagera zilizoathiriwa na tetemeko la ardhi lilitokea Septemba 10, mwaka huu.

  Kwa upande wake, Balozi Cooke ambaye alifika kujitambulisha rasmi, amesema ameguswa na juhudi zinazofanywa na Serikali katika kukabiliana na masuala ya ufisadi na rushwa. “Kaulimbiu yenu kwamba rushwa haikubaliki (zero tolerance on corruption) inaonyesha jinsi mlivyodhamiria kupambana na baa hili,” amesema.

  Amesema Uingereza inaongoza miongoni mwa nchi zenye wawekezaji wengi hapa nchini na kwamba inaendeleza mpango wake wa uwekezaji ambao unalenga maeneo makuu manne ambayo ni gesi na mafuta; kilimo; nishati jadidifu na uimarishwaji wa mazingira ya kufanya biashara.

  Balozi Cooke alitumia fursa hiyo kutoa pole kwa Serikali kutokana na msiba wa Spika Mstaafu wa Bunge la Tisa na Mbunge Mstaafu wa Jimbo la Urambo, Tabora, Mheshimiwa Samwel Sitta kilichotokea usiku wa kuamkia Novemba 7, mwaka huu katika hospitali ya Technical University of Munich nchini Ujerumani alikokuwa akipatiwa matibabu.

  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO), Mhandisi Felchesmi Mramba

  0 0

  Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe.Suleiman Jafo akijibu hoja mbalimbali kutoka kwa wabunge wakati wa kikao cha sita cha mkutano wa tano wa Bunge la 11 linaloendelea Mjini Dodoma Novemba 8, 2016.

  …………………………………………………………………….

  Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO, Dodoma.

  Jumla ya madereva 62 wanaoendesha mabasi yaendayo haraka (UDART) wamechukuliwa hatua za kinidhamu kwa sababu ya kukiuka Sheria za barabarani.

  Idadi hiyo ya madereva imetajwa leo na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Mhe Suleimani Jafo alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Kiembe Samaki Mhe. Ibrahim Mohammed lililohoji kuhusu hatua zinazochukuliwa na Serikali juu ya madereva hao ambao hawafuati sheria za barabarani.

  Mhe. Jafo amekiri kuwa madereva hao wamekuwa wakiendesha mabasi hayo kwa kasi kubwa kiasi cha kuhatarisha maisha ya watu waendao kwa miguu lakini madereva hao wanapaswa kuzingatia Sheria za usalama barabarani kama ilivyo kwa madereva wanaoendesha aina nyingine ya magari.

  “Tangu mabasi haya yaanze kutoa huduma, tumeshawachukulia hatua za kinidhamu madereva 62 ambapo kati ya hao, madereva 20 wamepewa onyo kwa makosa ya usalama barabarani, wawili wamefukuzwa kazi na madereva 40 wamekatwa mishahara yao kwa makosa mbalimbali ya barabarani”, alisema Mhe. Jafo.

  Naibu Waziri huyo ameongeza kuwa kwa sasa mabasi hayo yamefungwa vifaa maalum kwa ajili ya kutoa ishara ya dereva anayezidisha mwendo wa zaidi ya Kilomita 50 kwa saa moja ili kudhibiti mwendo mbaya wa mabasi hayo.

  Aidha, ili kuwakumbusha taratibu na maadili ya kazi ya udereva Mhe. Jafo ameeleza kuwa Serikali imeweka utaratibu wa kuwajengea uwezo madereva hao kupitia semina zinazoendeshwa na wataalam kutoka Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Chuo cha Elimu na Mafunzo ya Ufundi (VETA) pamoja na Askari wa Usalama Barabarani.

  Amefafanua kuwa watoa huduma wanatakiwa kuzingatia muda katika kutoa huduma mkataba baina ya DART na mtoa huduma ambaye ni U- DART unaoainisha kuwa huduma ya mabasi yaendayo haraka itaanza kuanzia saa 11:00 alfajiri hadi sa 06:00 usiku.

older | 1 | .... | 1034 | 1035 | (Page 1036) | 1037 | 1038 | .... | 1898 | newer