Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live

UN yawapiga msasa wanafunzi wa Chuo cha Tumaini Makumira juu ya SDGs

$
0
0
Mtaalamu wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) nchini, Hoyce Temu akitoa semina juu ya malengo ya maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa (SDGs) katika Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira kilichopo mkoani Arusha.(Picha na Ferdinand Shayo).

Maafisa kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa (UN) wamefanya ziara ya kutembelea Chuo cha Tumaini tawi la Arusha ikiwa ni pamoja na kutoa semina juu ya Malengo ya maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa ikiwemo kufuta umasikini, kuondoa njaa na kuhakikisha upatikanaji wa maji.

Mtaalam wa Programu kutoka Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Amon Manyama amesema kuwa wasomi na wanafunzi walioko vyuoni wanapaswa kuelewa vizuri malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) ya Umoja wa Mataifa ili waweze kuyatimiza katika ngazi zao hasa ukizingatia kuwa wanachuo ni wataalamu watarajiwa,na viongozi wa kesho.

Manyama amesema kuwa taasisi,mashirika na jamii pamoja na serikali ina jukumu kubwa la kutekeleza malengo hayo ili kuondoa umasikini, kujenga uchumi endelevu,kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi.

Mtaalam wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) nchini, Hoyce Temu amesema kuwa vijana hususan wanavyuoni wanapaswa kuwa mambalozi wazuri wa kuyatangaza malengo ya maendeleo endelevu ya UN ili yaweze kutimia na dunia iwe ni sehemu bora zaidi ya kuishi kwa kila mtu.

Temu amesema kuwa UN ina mpango wa kuwafikia vijana walioko vyuoni na mitaani ili waweze kuelewa vizuri juu ya malengo 17 ya maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa na kujua jukumu walilonalo ndani ya malengo hayo.

Na Ferdinand Shayo, Arusha
Mtaalam wa Programu kutoka Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Amon Manyama akiwapiga msasa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira juu ya malengo ya maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa (SDGs) katika ukumbi wa chuo hicho jijini Arusha.Mtaalamu wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa Hoyce Temu (katikati) naRaisi wa Chuo hicho John Maembe (kushoto).
Baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira wakifuatilia semina ya malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) iliyoandaliwa na ofisi ya Mkuu wa Umoja wa Mataifa jijini Arusha.


Baadhi ya wanafunzi wa Chuo cha Tumaini Makumira jijini Arusha katika picha ya pamoja na wakufunzi huku wakiwa wameshikilia mabango ya SDGs.
Picha ya pamoja na serikali ya wanafunzi.

MUSWADA WA SHERIA YA HUDUMA ZA HABARI WASOMWA MARA YA PILI

$
0
0
Na Eleuteri Mangi- MAELEZO

Muwada wa Sheria ya Huduma za Habari wa mwaka 2016 umesomwa mara ya pili Bungeni mjini Dodoma ukiwa na lengo la kuifanya tasnia ya habari nchini kuwa taaluma kamili.

Wiziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye amesema hay oleo Bungeni Dodoma alipokuwa akiwasilisha Muswada huo, huku akisisitiza kuwa una sehemu kuu nane ambazo zinaufanya kuleta mageuzi katika tasnia ya habari nchini na kuifanya kuwa taaluma kamili itayowaletea heshima wanahabari na tasnia hiyo kwa ujumla. 

“Hatuwezi kwa na vyombo vya habari makini kama hatutakuwa na wanahabari wenye taaluma ya habari nchini” alisema Nape.

Katika kuonesha ushirikishwaji wa wadau katika kutoa maoni yaliyolenga kuboresha Muswada huo, Waziri Nape amesema kuwa kumekuwa na ushirikishwaji mkubwa wenye wigo mpana kutoka kwa mwananchi mmoja mmoja, wanataaluma wa habari, wanasheria kupitia Chama cha Mawakili Tanzania (TLS), Baraza la Habari Tanzania (MCT), Umoja wa Wamiliki wa vyombo vya habari (MOAT) na Taasisi ya Wanahabari Kusini mwa Afrika, tawi la Tanzania (MISA-TAN).

Wadau wengine walitoa maoni yao ni Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Sikika, Wabunge kupitia Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii pamoja na michango ya Wabunge kupitia Kamati nyingine ambao umesaidia katika kuboresha Muswada huo wenye dhamira ya kuleta ufanisi katika sekta ya habari. 

Miongoni mwa maeneo ambayo wadau hao wameyafanyia maboresho ili Muswada uwe na tija ni pamoja na kuainisha haki na wajibu wa wananhabari ikiwemo uhuru wa kukusanya, kuhariri na kuchapisha au kutangaza habari pamoja na kuainisha haki ya chombo cha habari kukata rufaa kwa kuzingatia mfumo wa wazi na wa kidemokrasia kupitia vyombo vya kutoa haki ikiwemo mahakama huku Jaji Mkuu akiweka utaratibu wa kusikilizwa haraka kwa kesi za masuala ya kihabari.

Maboresho mengine yaliyofanya ni uwakilishi wa wanahabari katika Bodi ya Ithibati kwa kuzingatia uwiano wa wajumbe kutoka sekta ya habari ya umma na ya binafsi, kuviondolea adhabu vyombo vya habari au wamiliki baadhi ya makosa ya mwandishi ambapo atawajibishwa na Bodi ya Ithibati akiwa yeye ni mwanataaluma kamili kukutenda makosa ya kimaadili na vyombo vya dola kukamata mitambo na vifaa vya wanahabari maboresho yanaonesha kazi hiyo sasa itafanywa na Jeshi la Polisi kwa sheria ya Mwenendo wa Mkosa ya Jinai badala ya kazi hiyo kufanywa na Mkurugenzi wa Idara ya Habari. 

Zaidi ya maboresho hayo, Waziri Nape ameongeza kuwa maboresho mengine ni kuhusu mitambo kutohusika moja kwa moja kwa kosa la gazeti ambalo limechapisha habari yenye makosa ya kisheria dhidi ya watu au taasisi mbalimbali.

Waziri Nape amefafanua kuwa chimbuko, muktadha na mchakato wa kuandaa Muswada huo unatokana na baadhi ya vipengele vya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya kufanyiwa marekebisho mwaka 1984 ambapo haki ya kikatiba ya kutafuta, kupokea na kutoa habari imeainishwa kwenye Ibara ya 18 (b) pamoja na mikataba mbalimbali ya kimataifa ya inayoainisha haki na wajibu wa sekta ya habari. 

Mkatabahiyo ya Kimataifa ni ule wa Haki za Kisiasa na Kiraia wa mwaka 1966 ambao Tanzania iliuridhia Juni 11, 1984 pamoja na Mkataba wa Afrika wa Haki za Binadamu na Watu 1981 ambao nao uliridhiwa Februari 18, 1984.

Akinukuu maneno mbalimbali ya watu maarufu duniani juu ya masuala ya habari akiwemo Rais wa Marekani Thomas Jefferson Januari 16, 1789, Rais wa zamani wa Afrika Kusini Nelson Mandela, Muasisi wa Taifa la India Mahatma Ghandhi, Baba wa Uhuru wa Habari John Stuart Mill (1806-1873) pamoja na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere, Waziri Nape akinukuu maneno ya mmoja wa viongozi hao Mahatma Ghandhi aliamini kuwa uhuru wa kweli wa kujieleza ni ule unaoweka mbele heshima ya watu wengine na kuwalinda dhidi ya dhara, kebehi, kejeli na madhara mengine huku Baba wa Uhuru wa Habari John Stuart Mill akibainisha dhima ya uhuru wa vyombo vya habari na umuhimu wa kuwa huriu unapaswa kuzingatia ukomo wa haki ya kupata habari kuwa unakoma pale haki za watu wengine zinapoanzia.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii Peter Serukamba amesema kuwa kamati yake imeufanyia kazi Muswada huo kupitia maoni ya wadau na watu mbalimbali nchini ambayo ndio yamakuwa msingi wa kuuboresha muswada huo.



Serukamba aliongeza kuwa kati ya miswada ambayo wananchi wengi wameisoma na kusikilizwa ni Muswada habari ambao umejadiliwa kwa njia mbalimbali ikiwemo vyombo vya habari; kwenye magazeti, kwenye radio na Televisheni kupitia vipindi maalum vya kujadili Muswada huu na maoni yao mengi yameingizwa kwenye Muswada huu” alisema Serukamba.

RC NDIKILO ATEMBELEA HIFADHI YA UZIGUA

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo akitembelea hifadhi ya msitu wa Uzigua akiwa ameambatana na kamanda wa polisi mkoani Pwani Boniventure Mushongi, mkuu wa wilaya ya Bagamoyo alhaj Majid Mwanga na viongozi wengine kutoka mkoa,wilaya na wakala wa misitu (TFS)kanda ya Mashariki.
  
Mkuu wa mkoa wa Pwani mhandisi Evarist Ndikilo akizungumza jambo wakati ilipokwenda kutembelea hifadhi ya msitu wa Uzigua na kutoa agizo kwa waliwavamia waondoke Mara moja.

WANAFUNZI ELIMU YA JUU WATENGEWA BILIONI 483 ZA MIKOPO

$
0
0
Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO, Dodoma.

Jumla ya wanafunzi 119,012 wa Elimu ya Juu nchini wametengewa kiasi cha shilingi bilioni 483 Katika mwaka wa fedha 2016/2017 kwa ajili ya kupewa mikopo itakayowasaidia kujikimu pindi watakapokuwa vyuoni.

Kiasi hicho cha fedha kimetajwa leo Bungeni mjini Dodoma na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako alipokuwa akitoa kauli ya Serikali kuhusu utoaji wa mikopo ya wanafunzi wa Elimu ya Juu kwa mwaka wa masomo 2016/2017.

Prof. Ndalichako amesema kuwa mikopo hiyo inatolewa kwa kuzingatia malengo ya Mfuko wa Mikopo kwa Wanafunzi wa Elimu ya Juu ambapo kigezo kikuu kimekuwa ni uhitaji wa mwanafunzi pamoja na fani za kipaumbele anayosoma mwanafunzi.

Fani za kipaumbele kwa mujibu wa Wizara hiyo ni pamoja na Sayansi za Tiba na Afya, Ualimu wa Sayansi na Hisabati, Mafuta na Gesi Asilia, Sayansi Asilia na Mifugo, Uhandisi wa Viwanda pamoja na Kilimo na Umwagiliaji.

Prof. Ndalichako ameongeza kuwa kuna baadhi ya wanafunzi ambao wamedahiliwa kwenye fani za kipaumbele lakini hawana vigezo vya kupewa mikopo kutokana na tathmini ya uhitaji kuonesha kuwa wanaweza kusomeshwa na wazazi au walezi wao. 

“Kwa mwaka huu wa fedha, Serikali imeongeza kiasi cha fedha zinazotakiwa kwa ajili ya mikopo ya wanafunzi wa Elimu ya Juu waliochaguliwa na wanaondelea na masomo katika vyuo mbalimbali nchini kutoka shilingi bilioni 473 hadi bilioni 483 ambayo itaweza kugharamia wanafunzi wanaoanza 25,717 na wanaoendelea na masomo 93, 295”, alisema Prof. Ndalichako.

Ameongeza kuwa kumekuwa na changamoto mbalimbali za utoaji mikopo ambazo pamoja na mambo mengine zinachangiwa na mfumo wa udahili wa wanafunzi katika Vyuo vya Elimu ya Juu ambapo kwa sasa kuna mgongano kati ya Tume ya Vyuo Vikuu na Taasisi za Elimu ya Juu pia kutokuwa na tarehe moja ya Taasisi zote za Elimu juu ya kufungua vyuo kunaleta mkanganyiko.

Akiongelea kuhusu wanafunzi wanaoanza chuo mwaka huu, Prof. Ndalichako amesema kuwa jumla ya wanafunzi 58,010 wamedahiliwa na Tume ya Vyuo Vikuu na orodha yao tayari ilishawasilishwa katika Bodi ya Mikopo na hadi kufikia Novemba 2 mwaka huu jumla ya wanafunzi 21,190 wameshapewa fedha hizo.

Waziri amefafanua idadi ya wanafunzi hao waliopata mikopo kuwa 4,321 ni yatima,118 wana ulemavu na wanafunzi 87 ni wale waliosoma shule za Sekondari kwa ufadhili wa watu binafsi au Taasisi mbalimbali.Aidha, Prof. Ndalichako amesisitiza kuwa jumla ya wanafunzi 25,717 wanaoendelea na masomo waliokuwa na mikopo wataendelea kupatiwa mikopo hiyo kama ilivyokuwa katika mwaka wa masomo uliopita.

“Napenda kuwatoa hofu wanafunzi wanaoendelea kuwa Serikali haijafuta mkopo kwa mwanafunzi yoyote anayeendelea na masomo, kwa wanafunzi ambao vyuo vyao vimewasilisha taarifa za matokeo ya wanafunzi wao Bodi imekwishawatumia fedha zao za mkopo”, alisema Prof Ndalichako.

Katika taarifa hiyo, Prof, Ndalichako ameelezea kuwa taratibu za kuwabaini wanafunzi wasio na sifa stahiki zinaendelea na zitakapokamilika wanafunzi hao hawatopewa mkopo, ameahidi kufanya mapitio ya udahili wa wanafunzi vyuoni pamoja na utaratibu mzima wa utoaji na urejeshwaji wa mikopo kwa lengo la kuwa na mfumo bora zaidi.

TBS WATOA ZAWADI KWA WAANDISHI BORA WA INSHA ZA MAZINGIRA KWA WANAFUNZI SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
SHIRIKA la Viwango Nchini (TBS) limewatangaza washindi wa shindano la uandikaji wa insha lililoandaliwa na Shirika la Mazingira Duniani (UNEP) lililoshirikisha shule za msingi na sekondari Tanzania nzima.

Akizungumza kabla ya utoaji tuzo hizo,Kaimu mkurugenzi mkuu wa TBS Egid Mubofu amesema hatua hii itasaidia sana kuweza kutoa elimu kwa wananchi hasa baada ya wanafunzi hawa kuonesha jitihada kubwa za kuondokana na suala zima la uchafuzi wa mazingira.

Katika shindano hilo lililoshirikisha takribani wanafunzi 75 kutoka sehemu mbalimbali nchini lilianza rasmi mwezi Septemba na kumalizika mwishoni mwa mwezi Oktoba na kufanikiwa kupatikana kwa washiriki nane kwa shule za Msingi na 10 kutoka shule za Sekondari.

Mshindi wa kwanza kwa upande wa shule ya msingi ilichukuliwa na Nairath Ngururu kutoka shule ya Wasichana Almutanzir huku nafasi ya pili ikiendelea Eldred Medard kutoka shule ya Valentine na nafasi ya tatu kwenda kwa Shiluni Laizer kutoka shule ya Havard zote za Jijini Dar es salaam.

kwa upande wa sekondari,wasichana waliendelea kutamba baada ya Zainab Kambi kutoka Academic Internaational kushika nafasi ya kwanza, Frank Kapinga kutoka Kibaha Sekondari kushika nafasi ya pili na nafasi ya tau kuchukuliwa na Pius Mollel kutoka St Jude
 ya Jijini Dar es salaam.

Mwenyekiti wa mradi huo, Mary Meela amesema kuwa washiriki wote ni washindi kwani waliweza kuingia kwenye hatua ya mwisho ya mchujo na wanatakiwa kuja kuwa mabalozi wakubwa katika suala zima la mazingira.

Afisa mwakilishi wa UNEP, Clara Nakenya amesema kuwa hatua hii ni moja ya malengo 12 yaliyofikiwa kwa ajili ya kupambana na masuala ya mazingira kwani insha hizi zina elimu ya kutosha kwa rika zote husuani watoto, vijana na wazee katika kufanya maamuzi kuhusiana na mazingira.
Kaimu mkurugenzi mkuu wa TBS Egid Mubofu akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa shindano hilo walioingia fainali pamoja na majaji wa shindano hilo.
Kaimu mkurugenzi mkuu wa Shirika la Viwango Nchini (TBS) Egid Mubofu akizungumza wakati wa utoaji wa zawadi kwa washindi wa shindano uandishi wa insha wa mazingira lililoratibiwa na Shirika la Mazingira Duniani (UNEP) kushirikiana na shirika hilo.
Afisa mwakilishi wa Shirika la Mazingira Duniani (UNEP), Clara Nakenya akizungumza wakati wa utoaji wa zawadi kwa washindi wa shindano uandishi wa insha wa mazingira lililoratibiwa na Shirika la Mazingira Duniani (UNEP) kushirikiana na shirika hilo.
Jaji mkuu wa shindano hilo, Jumanne Mpinga akitolea ufafanuzi namna washiriki walivyoonyesha juhudi kubwa kwa kuandika insha nzuri zenye kuleta elimu kwa jamii kuhusiana na mazingira.
Mshindi wa kwanza kwa upande wa shule ya Msingi Nairath Ngururu kutoka shule ya Wasichana Almutanzir(kushoto) na Mshindi wa kwanza upande wa shule ya sekondari Zainab Kambi kutoka Academic Internationa wakiwa katika picha ya pamoja na Kaimu mkurugenzi wa Shirika la Vwiango Nchini (TBS) Egid Mubofu pamoja na Afisa mwakilishi wa Shirika la Mazingira Duniani (UNEP), Clara Nakenya.
Mwenyekiti wa mradi , Mary Meela akizungumza wakati wa utoaji wa zawadi kwa washindi wa shindano uandishi wa insha wa mazingira lililoratibiwa na Shirika la Mazingira Duniani (UNEP) kushirikiana na shirika la Viwango Nchini TBS.
Kaimu mkurugenzi mkuu wa Shirika la Viwango Nchini (TBS) Egid Mubofu akimkabdhi cheti cha heshima kwa jaji mkuu wa shindano hilo wakati wa iutoaji zawadi kwa washindi na washiriki wengine.



Kaimu mkurugenzi mkuu wa Shirika la Viwango Nchini (TBS) Egid Mubofu akikabidhi vyeti kwa washiriki mbalimbali wa Shindano la uandishi wa Insha inayihusiana na mazingira iliyoratibiwa na Shirika la Mazingira Duniani (UNEP) kushirikiana na shirika LA viwango nchini TBS.
Wazazi na washiriki wa Shindano wakiwa makini kusikiliza kabla ya utoaji wa zawadi.

WAMAMA WAWILI WAKAMATWA LEO JIJINI ARUSHA WAKIDAIWA KUIBA KATIKA DUKA LA NGUO

$
0
0
picha ikionyesha wamama wawili ambao wanatuhumiwa kwa wizi waliokamatwa katika mtaa wa koni eletronic uliopo jijini Arusha wakidaiwa kuiba katika duka moja la mfanyabiashara wa nguo ambaye hakutaka kutajwa jina lake,wakiwa wamezingirwa na wananchi mara baada ya kukutwa wakijidai kutaka kununua nguo kumbe wanachagua nguo na kuziweka katika mapochi yao  makubwa waliobeba ,wamama hao waliambulia kipigo nusu wachomwe moto lakini walibahatika kusaidiwa na polisi mara baada ya polisi kufika eneo latukio na kuwachukuwa kisha kuwapeleka katika kituo cha polisi


Na Woinde Shizza,Arusha

kumekuwepo na tabia ya baadhi ya  akina Mama,wadada kuwa na tabia ya kuingia madukani na kuibia wafanya biashara wa nguo pamoja na vipodozi vitu mbalimbali 

hapa nyuma kumekuwepo na malalamiko mengi sana wanayotoa wafanyabiashara hawa kuwa wanakuwa wanaibiwa wengine ambao wamefunga kamera madukani mwao wamekuwa wakirusha picha zinazoonyesha video za wadada hao wakiwa wanaiba 

hivi leo kuna kina mama wawili wamekamatwa katika mtaa wa koni eltronic ulipo ndani ya jijini Arusha wakiwa wanaiba katika duka la dada mmoja mfanyabiashara wanguo ,na inasemekana hao wamama walikuwa wamezoea kuiba katika duka hilo naweza kusema kuwa walipafanya kama shamba la bibi sasa leo hii wamekamatwa nusu wachomwe

Mmiliki wa libeneke la kaskazini aliweza kuwashuhudia wamama hao wakiwa wamewekwa chini ya ulinzi huku wakiwa wamezingirwa na wananchi wakiwa wanapigwa vibao na kuaambiwa wanazalilisha wanawake kwa kuwa wezi 

Wadada hao mara baada ya kukamatwa awali walisema wametokea nchini kenya lakini baadae walibadilika na kusema wametokea mkoani hapa hapa Arusha 

Wananchi wanye asira kali waliwapiga huku wengine wakitaka wachomwe moto ili kukomesha tabia hiyo lakini kabla ya tukio la uchomaji moto kutokea ndipo askari polisi walitokea na kuwachukuwa kisha kuwapeleka kituo cha polisi

RAIS MAGUFULI AWATAKA WATANZANIA KUTUMIA FURSA ZILIZOPO

$
0
0
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli amewataka watanzania kutumia fursa zilizopo katika Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) kwa ajili ya kuliletea maendeleo ya taifa.

Aliyasema hayo leo Jijini Dar es Saalam wakati wa mkutano wake na Wahariri wa vyombo vya habari nchini katika kuadhimisha mwaka mmoja wa Utawala wake, ambapo alisema kuwa ipo haja ya kuzungumza na kuelimisha watanzania juu ya fursa zilizopo katika taasisi hizo.

“Katika Jumuiya hizo zipo fursa nyingi kwa ajili ya maendeleo ingawa inahitajika elimu ya kutosha kwa watanzania kuona fursa zilizopo ikiwemo ufundishaji wa lugha ya Kiswahili nchi za nje” alisema Rais Magufuli.

Mbali na hayo, akizungumza kuhusu suala la kupambana na Rushwa nchini Rais Magufuli ametoa wito kwa vyombo vinavyohusika na kupambana na rushwa kufichua watu wotw wanaojihusisha na vitendo hivyo.

Rais Magufuli alisema kuwa vita ya Rushwa ni ya kila mwananchi, ambapo alitoa wito kwa watanzania wote kwa ujumla kujiepisha na masuala ya rushwa kwani rushwa ni kansa ya maendeleo nchini.

“Taifa litakwama tukiacha suala la rushwa liendelee, tumeumia kweli kweli katika hili hivyo nitoe wito kwa watanzania wote kwa ujumla kujiepusha na masuala haya kwa ajili ya maendeleo ya nchi kwani kesi ya rushwa ni yetu sote” alifafanua Rais Magufuli.

“SHERIA YA MUSWADA WA HUDUMA ZA HABARI IMECHELEWA” RAIS MAGUFULI

$
0
0
Rais Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akizungumza na wahariri pamoja na waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari leo, Ikulu jijini Dar es Salaam 


Na. Immaculate Makilika - MAELEZO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Magufuli amesema kuwa huu ni wakati mwafaka kwa muswada wa sheria ya huduma za vyombo vya habari kukubaliwa na kuwa sheria kwa vile tasnia ya habari inakumbwa na changamoto nyingi zitakazotatuliwa na sheria hiyo.

Akizungumza na wahariri pamoja na waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari leo, Ikulu jijini Dar es Salaam Rais Magufuli alisema kuwa muswada huo ni wa muda mrefu na sasa ni wakati mwafaka kwa vile tansia ya habari inakumbwa na changamoto nyingi zinazoweza kutatuliwa na muswada huo.

“Hii sheria ya huduma za vyombo vya habari imechelewa kwa vile mchakato wake ulianza tangu mwaka 2011 hadi sasa mwaka 2016 wadau walikuwa na muda wa kutosha wa kujiandaa na kutoa maoni yao ambayo yangeweza kuboresha muswada huo” alisema Rais Magufuli

Ameongeza kuwa, Sheria hii italeta mabadiliko katika tasnia ya habari kwa vile kutakuwepo na Bodi ambayo itashughulikia masuala ya taaluma ya habari, pamoja na mambo mengine yaliyoanishwa katika muswada huo ambayo ni maslahi ya waandishi wa habari nchini.

Muswada huu unatazamiwa kuwajengea uwezo waandishi wa habari ili waweze kufanyakazi kitaalamu kwa kuandika na kutangaza habari zenye ukweli zitakazochangia katika harakati za kuleta maendeleo kwa nia ya kuwasaidia watanzania na serikali kwa ujumla katika kufikia malengo yake. 

Muswada wa Sheria ya huduma za habari umesomwa leo Novemba 4, 2016 katika kikao cha tano cha Bunge na mkutano wa 11, ambapo utajadiliwa na kufuata taratibu zingine kabla ya kuwa sheria.

ISRAEL YAZINDUA KITUO CHA VIZA

$
0
0
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Prof. Jumanne Maghembe (Mb) ambaye alikuwa Mgeni Rasmi kwenye sherehe za kufungua Kituo cha Kutoa viza za kwenda nchini Israel akiwasilisha hotuba katika ufunguzi huo. Prof. Maghembe alipongeza uamuzi wa Israel kufungua kituo hicho hapa nchini kwa kuwa kitarahisisha ziara za kwenda Israel kwa Watanzania. Aidha, alirejea kauli ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhusu dhamira ya Serikali ya kufungua Ubalozi nchini Israel. 

Prof. Maghembe alieleza kuwa idadi ya watalii kutoka Israel kuja Tanzania inaendelea kuongezeka na jana alikutana na wakala wa usafirishaji kutoka nchi hiyo ambao wana nia ya kuanza safari za ndege za kila wiki kutoka Israel hadi mkoani Katavi (charter flights) kutembelea maoeneo ya utalii. Ndege aina kama hiyo inafanya safari za kuja Tanzania katika mikoa ya kaskazini mara mbili kwa mwaka. Prof. Maghembe alisisitiza umuhimu wa Tanzania kushirikiana na Israel katika sekta ya teknolojia hususan mbinu za kitaalamu za kukabiliana na ujangili wa wanayamapori nchini.Kituo cha viza kitakuwa na ofisi za muda kwenye Hoteli ya Hyatt Regency, Kilimanjaro jijini Dar es Salaam. 
Balozi wa Israel nchini Tanzania mwenye makazi yake Nairobi, Kenya, Mhe. Yahel Vilan akitoa neno la ukaribisho wakati wa sherehe za ufunguzi. Alisema anashukuru Mungu ametimiza ombi alilotoa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alipokutana naye Ikuku, Dar es Salaam. Mhe. Rais aliomba Serikali ya Israel ifungue Kituo cha Viza hapa nchini jambo ambalo limetia leo hii. Aliongeza kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi maarufu nchini Israel, hivyo anatarajia ahadi ya kufungua Ubalozi wa Tanzania nchini humo litatekelezwa hivi karibuni. 
Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Abdallah Kilima (kushoto) akifuatilia hotuba za sherehe za ufunguzi wa kituo cha viza cha Israel .
Balozi wa Israel akihutubia washiriki wa sherehe za ufunguzi wa kituo cha viza. 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Prof. Jumanne Maghembe na Balozi wa Israel nchini mwenye makazi yake Nairobi, Kenya, Mhe. Yahel Vilan wakikata utepe kuashiria kituo cha kutoa viza cha Israel kimefunguliwa rasmi. 
Ofisi ya Kituo cha Kutoa Viza cha Israel ambacho kwa sasa kipo katika Hoteli ya Hyatt Regency, Kilimanjaro. 
Picha ya pamoja.

RAIS DKT MAGUFULI AFANYA MAHOJIANO NA WAHARIRI WA VYOMBO VYA HABARI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM LEO

$
0
0



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akijibu maswali
kutoka kwa wahariri wa vyombo mbalimbali aliokutana nao kwa mahojiano leo Ijumaa Oktoba 4, 2016 katika ukumbi wa mikutano wa Ikulu jijini Dar es salaam

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akijibu maswali
kutoka kwa wahariri wa vyombo mbalimbali aliokutana nao kwa mahojiano leo Ijumaa Oktoba 4, 2016 katika ukumbi wa mikutano wa Ikulu jijini Dar es salaam

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akijibu maswali
kutoka kwa wahariri wa vyombo mbalimbali aliokutana nao kwa mahojiano leo Ijumaa Oktoba 4, 2016 katika ukumbi wa mikutano wa Ikulu jijini Dar es salaam

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) Dkt. Ayoub Rioba wakati wa kupokea  maswali kutoka kwa wahariri wa vyombo mbalimbali aliokutana nao kwa mahojiano leo Ijumaa Oktoba 4, 2016 katika ukumbi wa mikutano wa Ikulu jijini Dar es salaam




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimsikiliza mwanahabari Sammy Awami wa BBC wakati akiuliza maswali kutoka kwa wahariri wa vyombo mbalimbali aliokutana nao kwa mahojiano leo Ijumaa Oktoba 4, 2016 katika ukumbi w3a mikutano wa Ikulu jijini Dar es salaam


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimsikiliza Mhariri Mtendaji wa magazeti ya Serikali (TSN) Dkt. Jim Yonazi wakati akiuliza maswali
kutoka kwa wahariri wa vyombo mbalimbali aliokutana nao kwa mahojiano leo Ijumaa Oktoba 4, 2016 katika ukumbi w3a mikutano wa Ikulu jijini Dar es salaam.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimsikiliza Mtangazaji Tido Mhando wakati akiuliza maswali kutoka kwa wahariri wa vyombo mbalimbali aliokutana nao kwa mahojiano leo Ijumaa Oktoba 4, 2016 katika ukumbi w3a mikutano wa Ikulu jijini Dar es salaam.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimsikiliza Msanii Mrisho Mpoto akiimbwa wimbo wa "SIJONZE" wakati alipokutana na wahariri kwa mahojiano leo Ijumaa Oktoba 4, 2016 katika ukumbi w3a mikutano wa Ikulu jijini Dar es salaam.PICHA NA IKULU

PICHA ZA MATUKIO YA MAJADILIANO YA MUSWADA WA HABARI BUNGENI DODOMA

$
0
0
 Mwenyekiti wa Jukwaa la Habari Tanzania (TEF), Theothil Makunga (kulia), akiwa na wajumbe wa jukwaa hilo, Jane Mihanji (katikati) baada ya kutoka bungeni Dodoma jana, kusikiliza mwenendo wa majadiliano ya Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari.
 Mwenyekiti wa Bunge, Andrew Chenge akiongoza majadiliano hayo
 Waziri
 Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Medard Kalemani (kulia) akiwa na wapiga kura wake waliotembelea Bunge jana.
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye akiwasilisha bungeni Dodoma, Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye akipongezana na naibu wake, Anastazia Wambura baada ya kuwasilisha muswada huo

 Mbunge wa Tunduma, Mwakajoka akisalimiana na Mbunge wa Busanda, Leonecia Butimbaa
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye (katikati) akijadiliana jambo na Mjumbe wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEA), Jane Mihanji (kulia) na Saedy Kubenea kwenye viwanja vya Bunge, Dodoma, baada ya kuwasilisha Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari.
 Waziri Kivuli wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Joseph Mbilinyi akiwasilisha bungeni, Dodoma jana, maoni ya Kambi rasmi ya Upinzani kuhusu Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari ya Mwaka 2016
 Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini, Zitto Kabwe akichangia hoja bungeni Dodoma,  kuhusu Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari ya Mwaka 2016, ambapo alisema kuwa muswada huo hauwatendei haki wanahabari.
Mbunge wa Jimbo la Ubungo, Saedy Kubenea akichangia muswada huo


KAMBI YA UPINZANI YAUKUBALI MUSWADA WA HABARI KWA KUWEKA BIMA YA AFYA KWA WANAHABARI

$
0
0
Msemaji Mkuu wa Kambi Bungeni katika Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Joseph Mbilinyi akiwasilisha hotuba ya kambi hiyo kuhusu Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari wa 2016.

Na Mwandishi wetu, Dodoma

Kambi Rasmi ya upinzani Bungeni yaikubali Bodi ya Ithibati, Baraza Huru la Habari pamoja na Bima ya Afya kwa waandishi wa habari nchini.

Akiwasilisha maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni mjini Dodoma, Msemaji Mkuu wa Kambi hiyo katika Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Joseph Mbilinyi amesema kuwa Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari wa 2016 unamaufaa kwa wanahabari nchini

“Kifungu cha 58 kinatoa jukumu na kuwataka waajiri wa waandishi wa habarikuhakikisha kuwa waandishi wa habari wanakuwa na bima ya afya pamoja na kuhakikisha kuwa wanachangia katika mifuko ya hifadhi za jamii” alisema Mbilimnyi.Msemaji huyo aliendelea kusema “Jambo hili ni jema sana na Kambi Rasmi ya Upinzani inaliunga mkono”.

Kuanzishwa kwa Bodi ya Ithibati pamoja na Baraza Huru la Habari ni jambo jema vitu ambavyo vitalinda maslahi ya mwandishi wa habari kwa kuzingatia kuwa moja ya kazi Baraza na Bodi ni kuweka viwango vya uangalizi pamoja na utaratibu wa kitaaluma katika kuratibu tasnia ya habari nchini.

Mbilinyi ametoa rai kwa Wabunge wote bila kujali itikadi za vyama kutambua kuwa jukumu la kutunga sheria ni wajibu wao wa kikatiba ambayo wanawajibika wakiwa sehemu ya Bunge kufanya kazi kwa maslahi mapana ya taifa.

Aidha, Mbilinyi amesisitiza kuwa katika Mkutano wa Nne wa Bunge la 11 Septemba 15 mwaka huu, Serikali ilileta Muswada wa Huduma za Habari na kusomwa mara ya kwanza kwa lengo la kuwapa nafasi Wabunge pamoja na wadau mbalimbali wa habari kupitia na kuufanyia tafakuri ya kina na hatimaye kutoa ushauri kwa Serikali kuhusu Muswada huo.

Naye Wiziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye amesema kuwa mageuzi katika tasnia ya habari nchini yataifanya kuwa taaluma kamili itakayowaletea heshima wanahabari na taifa kwa ujumla.

Kupitishwa kwa Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari itatoa wigo mpana kwa wanahabari kutekeleza majukumu yao kw uhuru ya kukusanya, kuhariri na kuchapisha au kutangaza habari.

Waziri Nape ameongeza kuwa pamoja na maboresho mengi ya Muswada huo pia unzingatia suala la mitambo ya kuchapisha magazeti na majarida nalo limepewa uzito unaostahili kwa kutohusika moja kwa moja kwa kosa la gazeti ambalo limechapisha habari yenye makosa ya kisheria dhidi ya watu au taasisi mbalimbali.

Akinukuu maneno mbalimbali ya watu maarufu duniani juu ya masuala ya habari akiwemo Rais wa Marekani Thomas Jefferson Januari 16, 1789, Rais wa zamani wa Afrika Kusini Nelson Mandela, Muasisi wa Taifa la India Mahatma Ghandhi, Baba wa Uhuru wa Habari John Stuart Mill (1806-1873) pamoja na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere, Waziri Nape alimesma kuwa mmoja wa viongozi hao Mahatma Ghandhi aliamini kuwa uhuru wa kweli wa kujieleza ni ule unaoweka mbele heshima ya watu wengine na kuwalinda dhidi ya dhara, kebehi, kejeli na madhara mengine huku Baba wa Uhuru wa Habari John Stuart Mill akibainisha dhima ya uhuru wa vyombo vya habari na umuhimu wa kuwa huriu unapaswa kuzingatia ukomo wa haki ya kupata habari kuwa unakoma pale haki za watu wengine zinapoanzia.

Akichangia katika mjadala wa Muswada huo wakati, Mbunge Sixtus Mapunda amesema kuwa kwa muda mrefu tasnia ya habari haikuwahi kupata hadhi inayostahili ndani ya nchi pamoja na kazi nzuri ya kuhabarisha, kufundisha, kukosoa na kuwasaidia watu watu wenye matatizo wenye changamoto mbalimbali hata kufikia hadhi ya kuitwa muhimili wan ne wa dola.

“Tasnia hii haikuwahi kulindwa, tasnia hii haikuwahi kuenziwa, tasnia hii haikuwahi kuheshimiwa inayostahili, kwa mwandishi wa habari mwenyewe, kwa chombo cha habari na wamiliki wa chombo cha habari tofauti na tasnia nyingine nyingine, kwa mara ya kwanza ndani ya nchi hii, heshima ya tasnia inapatikana” alisema Mapunda.

Mapunda ameitaja tasni hizo kuwa ni za Madaktari, Wahasibu na Wahandisi ambao wanachombo chao kinacholinda maslahi yao, maadili yao na kinachowalinda ili kuendelea kulinda taaluma yao.

Aidha, Mapunda amesema kuwa kwa miaka miaka zaidi ya 23, Muswada utasaidia kutatua matatizo yote yaliyokuwa yanatokana na mapungufu ya Sheria ya Magazeti ya mwaka 1976 kwa kuwa na Bodi ya Ithibati, Baraza Huru la Habari, Bodi ya Ithibati Mfuko wa Mafunzo ambayo ni mambo mapya.

Zaidi ya hayo, Mapunda aliongeza kuwa watu wenye vipaji vya kuandika habari kulingana na taaluma zao ikiwemo uchumi hawajazuiliwa na Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari wa mwaka 2016.

Chimbuko la Muswada huo linatokana na baadhi ya vipengele vya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya kufanyiwa marekebisho mwaka 1984 ambapo haki ya kikatiba ya kutafuta, kupokea na kutoa habari imeainishwa kwenye Ibara ya 18 (b) pamoja na mikataba mbalimbali ya kimataifa ya inayoainisha haki na wajibu wa sekta ya habari.

Mkataba huo wa Kimataifa ni ule wa Haki za Kisiasa na Kiraia wa mwaka 1966 ambao Tanzania iliuridhia Juni 11, 1984 pamoja na Mkataba wa Afrika wa Haki za Binadamu na Watu 1981 ambao nao uliridhiwa Februari 18, 1984.

VIJUSO VYA MAGAZETI YA LEO NOVEMBA 5

AGA KHAN YAWAPIGA MSASA WABUNGE, WADAU UBORESHAJI ELIMU NCHINI

$
0
0
 Mhadhili wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Kitilya Mkumbo akielezea kwenye mkutano wa wadau wa elimu mjini Dodoma, mambo mbalimbali yanayokwamisha maendeloeo ya elimu na jinsi ya kuiboresha. Mkutano huo ambao pia walishirikisha wabunge umeandaliwa na  Chuo Kikuu cha Aga khan (AKU).PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG.

 Mwenyekiti wa Bunge ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Ilala, Mussa Zungu na Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi wakisikiliza kwa makini mada kuhusu uboreshaji wa elimu nchini.
 Washiriki wakiwa katika mkutano huo wa kujadili changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya elimu nchini na jinsi ya kuziboresha






KUMBUKUMBU YA SHEREHE ZA KUAPISHWA KWA RAIS WA AWAMU YA TANO DKT JOHN POMBE MAGUFULI UWANJA WA UHURU

$
0
0
Rais wa awamu ya Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akila kiapo.
Rais wa awamu ya Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akila kiapo.
 
Rais wa awamu ya Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akikagua gwaride rasmi likiwa katika muundo wa Alpha kuashiria kushika madaraka ya Amiri Jeshi Mkuu.
Rais wa awamu ya Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akikagua gwaride rasmi likiwa katika muundo wa Alpha kuashiria kushika madaraka ya Amiri Jeshi Mkuu.


JARIDA LA WIZARA YA HABARI

$
0
0

Attachments area

PINDA ATEMBELEA MAKAO MAKUU YA CCM, LUMUMBA

$
0
0
 Wazuri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda akizungumza na Naibu
Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi alipotembelea Ofisi Ndogo ya
Makao Makuu ya CCM, mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam, jana.
Kushoto ni Msemaji wa CCM, Christopher Ole Sendeka.
 Wazuri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda akisisitiza jambo wakati akizungumza na Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara,
Rajab Luhwavi alipotembelea Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, mtaa wa
Lumumba jijini Dar es Salaam
Wazuri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda akizungumza na Naibu Katibu
Mkuu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi alipotembelea Ofisi Ndogo ya Makao
Makuu ya CCM, mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam, Kushoto ni Msemaji
wa CCM, Christopher Ole Sendeka, na kulia ni Katibu wa NEC, Siasa na
Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Pindi Chana.
(Picha zote na Bashir Nkoromo).

Mwanahabari wa Clouds Tv / Clouds Fm, NTIBASHIMA EDWARD AUGA UKAPERA

$
0
0
Bwana Harusi Ntibashima Edward ambae ni Mwajiriwa wa Kampuni ya Clouds Media Group inayomiliki Kituo cha Runinga cha Clouds pamoja na Clouds Fm, akimvisha Pete mke wake Bi Zitha Kannonyele, wakati wa Ibada ya ndoa yao iliyofungwa leo Katika Kanisa la Morovian lililoko Kimara Stop Over Jijini Dar es Salaam na Kuhudhuriwa na Wageni mbalimbali walioalikwa kushuhudia tukio hilo muhimu kwa Wawili hao.
Bi Harusi Zitha Kannonyele akisoma mistari mitakatifu iliyoandikwa ndani ya Biblia, huku Bwana Harusi Ntibashima Edward, aliyevaa suti akisikiliza kwa makini maandiko hayo, tukio hilo limefanyika leo Jijini Dar es Salaam wakati wa Ibada ya ndoa yao, ambayo imefanyika katika Kanisa la Morovian lililoko Kimara Stop Over. 
Maharusi hao wawili wakisoma mistari mitakatifu iliyoandikwa ndani ya Biblia, wakati wa Ibada ya ndoa yao iliyofanyika leo katika Kanisa la Morovian lililoko Kimara Stop Over Jijini Dar es Salaam na Kuhudhuriwa na wageni mbalimbali walioalikwa Kushuhudia tukio hilo Muhimu kwa wanadoa hao. 
Sophia Kessy na James Lyatuu ambao Wafanyakazi wenzake na Bwana Harusi Ntibashima Edward , wakiwa wamepozi mbele ya kamera ya habari360.com, kwa ajili ya kupata picha ya Kumbukumbu. 
Hapa wakiwa wamepozi na Bi Harusi Zitha Kannonyele kwa ajili ya Kupata Picha ya Kumbukumbu.

EU YAWEKEZA EURO MILIONI 1.7 KITUO CHA UTAMADUNI MAKUMIRA

$
0
0
Umoja wa Ulaya (EU) umewekeza zaidi ya Euro milioni 1 na laki 7 katika kituo cha Utamaduni cha Makumira kitengo kilichoko ndani ya Chuo Kikuu cha Makumira ambapo chuo kikubwa cha sanaa kinajengwa pamoja na kumbi ya burudani itakayogharimu kiasi hicho.

Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) kwa nchi za Afrika Mashariki Roeland Van De Geer amefanya ziara chuoni hapo ambapo amejionea shughuli za ujenzi zinazoendelea katika chuo hicho na kusema kuwa kupitia chuo hicho cha utamaduni wa Tanzania na makabila yake utaendelezwa ili kuleta manufaa kwa vijana na jamii nzima.

Akizungumza na wanahabari mara baada ya ziara hiyo amesema kuwa wataendelea kuunga mkono juhudi za kutunza utamaduni kwani vijana wataweza kutengeneza fursa za ajira kupitia sanaa za utamaduni.
Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) kwa nchi za Afrika Mashariki Roeland Van De Geer akizungumza katika kituo cha Utamaduni cha Makumira kilichopo mkoani Arusha,mara baada ya kutembelea kituo hicho.(Picha na Ferdinand Shayo).

Meneja mradi huo Randall Stubbs amesema kuwa kwa sasa wanatoa mafunzo ya ngoma za utamaduni wa makabila ya wamasai, wameru na wachaga ikiwa ni pamoja na kufanya maonyesho ya utamaduni katika maeneo mbalimbali.

“Ujenzi utakapokamilika kutakua na ukumbi wa kisasa, jengo maalumu la mafunzo kwa utamaduni wa bara la Afrika, Asia na Ulaya ili utamaduni uweze kuwa endelevu na kurithishwa vizazi na vizazi” alisema Randall.
Meneja Mradi wa Kituo cha Utamaduni cha Makumira, Randall Stubbs akitoa maelekezo kwa Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) kwa nchi za Afrika Mashariki Roeland Van De Geer alipotembelea kituoni hapo.
Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) kwa nchi za Afrika Mashariki Roeland Van De Geer akiwa katika kituo cha Utamaduni cha Makumira kilichopo mkoani Arusha, mara baada ya kutembelea kituo hicho.
Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) kwa nchi za Afrika Mashariki Roeland Van De Geer akiwa kwenye picha ya pamoja na watumishi wa kituo cha utamaduni cha Makumira jijini Arusha.
Meneja Mradi wa Kituo cha Utamaduni cha Makumira, Randall Stubbs akitoa maelezo kwa Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) kwa nchi za Afrika Mashariki Roeland Van De Geer (kushoto) aliyeambatana na Mwakilishi wa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Amon Manyama (kulia).

BUNGE LAPITISHA RASMI MUSWADA WA SHERIA YA HUDUMA ZA HABARI WA 2016.

$
0
0
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye alipokuwa akitoa hoja kabla Kamati ya Bunge zima kujadili Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari wa 2016 ambao umepitishwa leo mjini Dodoma.
Mwenyekiti wa Bunge Andrew Chenge akitoa maelekezo wakati wa mjadala wa Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari wa 2016 ili mjadala uwe na tija kwa maendeleo ya tasnia ya habari, wanahabari na taifa kwa ujumla.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Aannastasia Wambura akichangia hoja juu ya Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari wa 2016 leo mjini Dodoma.
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Watu wenye Walemavu Dkt. Possi Abdallah akichangia hoja juu ya Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari wa 2016 leo mjini Dodoma.
Mhe. Saada Mkuya Salum akichangia hoja juu ya Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari wa 2016 leo mjini Dodoma.
Wabunge wakiwa kwenye mjadala wa Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari wa 2016 leo mjini Dodoma.
Baadhi ya Watendaji wa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wakiongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof. Elisante Ole Gabriel (wa pili kushoto) wakifuatilia mjadala wa Wabunge wakati wa Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari wa 2016 leo mjini Dodoma.
Baadhi ya Watendaji wa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wakiongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof. Elisante Ole Gabriel (wa pili kushoto) wakifuatilia mjadala wa Wabunge wakati wa Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari wa 2016 leo mjini Dodoma.
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia mjadala wa Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari wa 2016 leo mjini Dodoma.
Baadhi ya wageni wakifuatilia mjadala wa Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari wa 2016 leo mjini Dodoma.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye (wa nne kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Baadhi ya watendaji wa Wizara hiyo mara baada ya kupitishwa Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari wa 2016 leo mjini Dodoma. Wa nne kulia Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof. Elisante Ole Gabriel.(Picha na Eleuteri Mangi-MAELEZO, Dodoma)
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live




Latest Images