Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46334 articles
Browse latest View live

GLOBAL EDUCATION LINK YAPELEKA WANAFUNZI KATIKA VYO VYA NCHINI CHINA.

$
0
0
GLOBAL Education Link (GEL) imepeleka wanafunzi 50 ikiwa ni awamu ya tatu kwa mwaka huu hiyo inatokana na uhitaji wa wataalam katika udaktari na uhandisi.

Akizungumza wakati wa safari hiyo ya wanafunzi hao, Mkurugenzi Mtendaji wa GEL, Abdulmalik Mollel amesema nafasi ya udahili nchini ni chache hivyo kama wakala wa vyuo vya nje kuchukua nafasi kwa wanafunzi wanaokosa udahili.Amesema mwitikio wanafunzi kusoma nje ni mkubwa ikilinganishwa na miaka ya nyuma.

Mollel amesema kutokana na nchi kuingia katika sekta ya Viwanda wanafunzi wengi wamekwenda kusoma uhandisi wa Viwanda ili waweze kuja kuleta utaalam huo na nchi iweze kupata maendeleo

Amesema GEL inachofanya ni kuhakikisha wanafunzi wanaosoma vyuo vya nje kuwa wazazi wanaweza kumudu gharama za vyuo sawa na vya ndani.Hata hivyo amesema bado wanafunzi wanasajili hivyo wazazi wenye nia ya kutimiza ndoto za watoto wawasiliane na ofisi za GEL.
Mkurugenzi Mtendaji wa GEL, Abdulmaliki Mollel akiwa na wafanyakazi katika uwanja wa ndege wa Kimataifa Mwalimu Julius Nyerere.
Wanafunzi wakiingia katika chumba cha ukaguzi katika uwanja wa ndege wa Kimataifa Mwalimu Julius Nyerere.


Mkurugenzi Mtendaji Global Education Link (GEL), Abdulmaliki Mollel akizungumza na wazazi waliowasindiza wanafunzi wanaokwenda kusoma vyuo vya China.

CHAKALE DHAHABU TAMASHA LA UTAMADUNI LITAKALO KUTANISHA MAKABILA ZAIDI ZAIDI YA 100 NA MACHIFU

$
0
0
Mtaribu wa tamasha la 'Kale ni Dhahabu' ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Seree, Sabina ​Kaphipa akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana kuhusiana na tamasha la utamaduni litakalowahusisha machifu zaidi ya 100 wa Tanzania. Pamoja nae ni Afisa Masoko, Anael Masasi
Mtaribu wa tamasha la 'Kale ni Dhahabu' ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Seree, Sabina ​Kaphipa akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana kuhusiana na tamasha la utamaduni litakalowahusisha machifu zaidi ya 100 wa Tanzania. Pamoja nae ni Afisa Masoko, Anael Masasi (kushoto) na Msemaji wa Tamasha hilo, Juma Mwajacho (kulia) pamoja na Mke wa Chief.
Mtaribu wa tamasha la Kale ni Dhahabu ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Seree, Sabina Maro akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana kuhusu tamasha la utamaduni litakalowahusisha machifu zaidi ya 100 wa Tanzania.
 Logo ya tamasha
Kampuni inayoandaa tamasha.
 Sabina Kaphipa akicheza ngoma na wasanii wa Kundi la sanaa Makumbusho. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.

Mtaribu wa tamasha la 'Kale ni Dhahabu' ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Seree, Sabina ​Kaphipa akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana kuhusiana na tamasha la utamaduni litakalowahusisha machifu zaidi ya 100 wa Tanzania. Pamoja nae ni Afisa Masoko, Anael Masasi (kushoto) na Msemaji wa Tamasha hilo, Juma Mwajacho (kulia).
 Juma Mwajasho ambaye ni msemaji wa tamasha hilo (kulia) akizungumza.


Mtaribu wa tamasha la 'Kale ni Dhahabu' ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Seree, Sabina ​Kaphipa akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana kuhusiana na tamasha la utamaduni litakalowahusisha machifu zaidi ya 100 wa Tanzania. Pamoja nae ni Afisa Masoko, Anael Masasi.
 ***************
SEREEE Company Inayo furaha kuandaaa Tamamsha la kiutamaduni wa Mtanzania linaloitwa CHAKALE DHAHABU, kwa lengo  kuu la kudumisha tamaduni zetu na kufanya jamii ya Kitanzania kuishi kwa kufurahia utamaduni wake.

SEREEE Company  inaandaa tamasha la kwanza la CHAKALE DHAHABU ambalo litafanyika  katika jiji la Dar es salaam, litakua ni tamasha la siku nzima ambalo litafanyka katika viwanya vya Uhuru( Uwanja wa Taifa  tarehe 3 December na kufuatiwa na tukio jingine siku ya tarehe 4 december ambapo kutakua na chakula cha jioni katika hoteli ya Golden Tulip Dar es salaam.

CHAKALE DHAHABU inalengo la kuwa ni tamasha ambalo litakua likifanyika kila mwaka likizunguka katika mikoa tofauti ndani ya nchi ya Tanzania.

CHAKALE DHAHABU ni Tamasha lililo beba utamaduni wa kitanzania ambapo makabila yoye yatashiriki pamoja na machifu wao, Tamamsha litalinda na kuendeleza utamaduni wa mtanzania na Africa kwa ujumla.

Tamasha limegawanyika katika burudani na shughuli mbalimbali za kiasili kama muziki,Ngoma,Chakula,Vinywaji,Mashairi,Hadithi,Matambiko pamoja na maonyesho ya bidhaa mbalimbali za kiasili. Zinazotengenezwa hapa Tanzania.

Seree Company ni kampuni ya Kitanzania inayokua haraka katika nyanja  ya juandaa na kusimamia  burudani na Matamasha kwa mfano, Harusi,Sherehe za kifamilia,Sherehe za makampuni, na sherehe za Kiserikali. Dira yetu ni kuwaunganisha pamoja wazee,vijana na wazazi katika nyanja ya sanaa na utamaduni wetu ambao kwa namna moja au nyingine unaendelea kufifia.

Tamasha litafanyika kwa monyesho kama ifuatavyo

MACHIFU
Machifu hawa ni viongozi wa kimila ambao ndio chimbuko la utamaduni wa Mtanzania  walikuwepo kabla tawaza za kiserikali kuwepo  walisimamia na kuziendesha koo pamoja makabila, nafasi ya machifu katika tamasha la CHAKALE DHAHABU ni kutoa elimu kwa jamii kuacha kabisa tabia ya kuwauwa vikongwe na maalbino pia watatuonyesha jinsi matambiko yalivyokua yakifanyka kwa lengo la kukumbuka na kuielimisha jamii nzima ya watanzania.

BURUDANI
Patakua na Burudani ya muziki wa asili  pamoja na ngoma toka katika makabila tofauti ya Tanzania, pia patakua na hadithi toka kwa wasimulizi mahiri toka hapa Tanzania  pamoja ma mashaishi toka kwa malenga wetu.

VYAKULA
Kutakua na vyakula vya aina tofauti kutoka katika makabila tofauti ya Tanzania.

Sereee campany inatoa shukrani za dhati kwa waandishi wa habari  kwakua  kupitia nyie Tamasha hili litakua na mafanikio .

ZAIDI YA SH. BILIONI 177 ZIMEPELEKWA HALMASHAURI-MAJALIWA-WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema hadi kufikia Oktoba mwaka huu, Serikali imekwishapeleka zaidi ya sh. bilioni 177 kwenye halmashauri mbalimbali nchini ili kutekeleza miradi ya maendeleo.

Ametoa kauli hiyo leo (Alhamisi, Novemba 3, 2016) Bungeni mjini Dodoma wakati akijibu swali lililoulizwa na Mbunge wa Viti Maalumu, Bibi Munde Tambwe aliyetaka kupata kauli ya Serikali kuhusu ucheleweshwaji wa fedha za bajeti ya maendeleo katika halmashauri mbalimbali nchini.

“Kwa kuwa Serikali ina mifumo, miongozo, sheria na taratibu za kupeleka fedha kwenye halmashauri mara baada ya kikao cha bajeti. Mheshimiwa Waziri Mkuu unatoa kauli gani kuhusu ucheleweshwaji wa fedha hizo katika halmashauri nchini zikiwemo za mkoa wa Tabora? Alihoji Mheshimiwa Munde.

Akijibu swali hilo, Waziri Mkuu amesema: “Baada ya Bunge kuridhia na kutoa mamlaka ya matumizi ya fedha, Serikali ilianza kujiridhisha uwepo wa mfumo sahihi ya makusanyo na mapato na matumizi yake. Ni kweli kwamba Serikali yetu baada ya kikao cha bajeti inawajibika kutekeleza maamuzi ya Bunge kwa kupeleka fedha zilizopangwa.”

Waziri Mkuu amesema Serikali ilianza kupeleka watumishi watakaosimamia ukusanyaji mapato katika halmashauri zote nchini. Kutathmini miradi yote iliyoanza ambayo haijaendelezwa pamoja na mipya ili kutambua thamani na kisha kupeleka fedha.

Amesema Serikali itaendelea na upelekaji wa fedha kwenye halmashauri kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli za maendeleo. Amezisisitiza halmashauri hizo kuendelea kukusanya mapato ndani ili kuongezea bajeti kwa fedha wanazopelekewa na watumie mfumo wa kielektroniki ili kudhibiti mapato hayo.

Aidha, Waziri Mkuu amezitaka halmashauri zote nchini zihakikishe fedha zinazopelekwa katika maeneo yao zinatumika kama ilivyokusudiwa kwa miradi husuka. Amewasihi Wabunge wafuatilie na wasimamie matumizi ya fedha hizo ili miradi iliyopangwa iweze kukamilika.

Wakati huo huo; Waziri Mkuu amesema Serikali haijafilisika na kuhusu suala la mfuko wa jimbo bado unatambulika na fedha zitapelekwa kwenye majimbo na wabunge watajulishwa kiasi kilichopelekwa ili waweze kuratibu miradi yao ya maedndeleo.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo wakati akijibu swali la mbunge wa jimbo la Ukonga Mheshimiwa Mwita Waitara aliyetaka kupatiwa kauli ya Serikali kuhusu kutopelekwa kwa fedha za mfuko wa jimbo.

Pia Mheshimiwa Waitara alilalamikia kitendo cha jimbo lake kutengewa fedha kidogo katika mgawo wa mfuko wa jimbo ambazo ni sh. milioni 16 licha ya kuwa na wananchi wengi huku jimbo la Segerea alilosemma lina watu wachache likitengewa sh. milioni 33. Ameiomba Serikali ingalie upya ugawaji huo kulingana na mazingira ya jimbo husika.

Waziri Mkuu amesema kumejitokeza matatizo kwenye halmashauri zenye majimbo zaidi ya moja na Serikali inaendelea kufanya sensa kutambua idadi ya wananchi kwenye majimbo hayo ili itakapopeleka fedha iweze kuzingatia idadi hiyo na kuwawezesha wabunge kupanga miradi ya maendeleo.


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 980,
DODOMA.
ALHAMISI, OKTOBA 3, 2016.

SEKTA YA DAWA ZA BINADAMU NCHINI YAPATA WAWEKEZAJI

$
0
0

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage akijibu swali leo Bungeni mjini Dodoma


Na Jacquiline Mrisho, Dodoma.

Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji pamoja na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) wamefanikiwa kuhamasisha baadhi ya wawekezaji kuwekeza katika sekta ya dawa za binadamu na vifaa tiba ili kupunguza uagizaji wa dawa kutoka nje ya nchi.

Hayo yamesemwa leo mjini Dodoma na Waziri wa wizara hiyo, Mhe. Charles Mwijage alipokuwa akijibu swali la Mhe. Khadija Ali (Viti Maalum) aliyehitaji kufahamu mpango wa Serikali wa kutumia malighafi zilizopo kuzalisha baadhi ya dawa na vifaa tiba.

Waziri Mwijage amesema kuwa Serikali inaendelea na Mkakati Unganishi wa Maendeleo ya Viwanda (IIDS) pamoja na Mpango wa Pili wa Maendeleo ya Miaka Mitano ambayo yote inalenga kuondoa changamoto ya kununua dawa na vifaa tiba kutoka nje ya nchi.

“Serikali kupitia mashirika yake ya MSD, TIRDO, NHIF, TIB na TFDA wamepewa jukumu la kuandaa mazingira wezeshi kwa sekta binafsi kuwekeza katika sekta ya dawa za binadamu pamoja na vifaa tiba kwa hiyo kupitia wizara yangu na TIC tayari tumefanikiwa kuwahamasisha wawekezaji kutoka nchi mbalimbali duniani”, alisema Mwijage.

Baadhi ya wawekezaji hao ni JSN Solution ambao watajenga kiwanda cha kuzalisha IV Fluid, China Dalian International Economic Development Group Co. Ltd ambao watajenga kiwanda cha kutengeneza vifaa tiba, Zinga Pharmaceuticals Ltd pamoja na Hainan Hualon ambao watatengeneza madawa mbalimbali ya binadamu.

Waziri Mwijage amesema kuwa kupitia Ubalozi wa Korea nchini, Kampuni ya Boryung Pharmaceuticals Co. Ltd itatengeneza madawa ya Penicilin Orals Solids Antibiotics, wakati Agakhan Foundation Network watazalisha dawa mbalimbali.

Waziri Mwijage ameongeza kuwa kujengwa kwa viwanda vya dawa za binadamu na vifaa tiba kutakuwa na fursa pana ya kuwahakikishia Watanzania nafasi za ajira kwa vijana nchini kipindi kifupi kijacho.

SPIKA WA KWANZA WA BUNGE LA AFRIKA MASHARIKI, KATIBU MKUU WA CCM, ABDULRAHMAN KINANA AKUTANA NA WABUNGE WA BUNGE HILO LEO

$
0
0

Spika wa kwanza wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA), Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akizungunguza na wabunge wa Bunge hilo, walipomtembelea ofisini kwake jijini Dar es Salaam, ili umsalimia na kupata mawazo kutokana na uzoefu wake hasa alipokuwa Spika wa Bunge hilo la Afrika Mashariki. Wa Kwanza kulia upande wa mstari wa kushoto, ni Mwenyekiti wa Wabunge hao, Makongoro Nyerere, Shayrose Bhaji, Yves Nsabimana, Maryam Ussi, Twaha Tasilima, Wilime Asheri ambaye ni mratibu EALA, na kutoka kulia, mstari wa kulia ni, Katibu wa NEC Oganaizesheni, Mohammed Seif Khatib, na Wabunge wa EALA, Adam Kimbisa, Bernard Murunya, Abdulla Mwinyi,Angela Kizigha na mwisho Msemaji wa CCM, Christopher Sendeka.
Mwenyekiti wa Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Makongoro Nyerere, akiwasili Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, kuongoza msafara wa wabunge hao kumsalimia Spika wa kwanza wa Bunge hilo, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, leo
Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Shy-rose Bhanji, akiwasili Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, wakati msafara wa wabunge yeye na wabunge wenzake wa Bunge hilo, walipofika kumsalimia Spika wa kwanza wa Bunge hilo, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, leo
Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Shy-rose Bhanji, akiwasili Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, wakati msafara wa wabunge yeye na wabunge wenzake wa Bunge hilo, walipofika kumsalimia Spika wa kwanza wa Bunge hilo, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, leo. Kulia ni Mbunge Bunge hilo, Yves Nsabimana.
Mwenyekiti wa Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Makongoro Nyerere, akiteta jambo na Mbunge wa Bunge hilo, wakati wakimsubiri kuingia ukumbini, Spika wa kwanza wa Bunge hilo, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, leo
Katibu wa NEC, Oganaizesheni, Mohammed Seif Khatib akisalimiana na Mbunge wa Bunge la Afika Mashariki Bernard Murunya, alipowasili wakati Wabunge wa Bunge hilo, walipofika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumbai Dar es Salaam, kumsalimia Spika wa kwanza wa Bunge hilo, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, leo. Katikati ni Adam Kimbisa.


Katibu wa NEC, Oganaizesheni, Mohammed Seif Khatib akifurahia jambo na Makongro Nyerere wakati wakisalimiana ukumbini, kabla ya Kinana kuwasili
Katibu wa NEC, Oganaizesheni, Mohammed Seif Khatib akisalimiana na Mbunge wa Bunge la Afika Mashariki Shy-Rose Bhanji, alipowasili wakati Wabunge wa Bunge hilo, walipofika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumbai Dar es Salaam, kumsalimia Spika wa kwanza wa Bunge hilo, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, leo.
Katibu wa NEC, Oganaizesheni, Mohammed Seif Khatib (kulia), akiwa na Wabunge wa Bunge la Afika Mashariki, Adam Kimbisa, Bernard Murunya, na Abdulla Mwinyi, wakati wakimsubiri Kinana kuingia ukumbini
Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki Yves Nsabimana na Maryam Ussi, wakibadilishana mawazo ukumbini
Mbunge wa Afrika Mashariki Angela Kizigha akimsalimia Mbunge mwenzake wa Bunge hilo, Bernard Murunya alipowasili ukumbini

Spika wa kwanza wa Bunge la Afrika Mashariki, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimsalimia Mweneyekiti wa Wabunge wa Bunge hilo, Makongoro Nyerere alipowasili ukumbini
Kinana akimsalimia Shy-Rose Bhanji
Spika wa kwanza wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA), Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akizungunguza na wabunge wa Bunge hilo, walipomtembelea ofisini kwake jijini Dar es Salaam, ili umsalimia na kupata mawazo kutokana na uzoefu wake hasa alipokuwa Spika wa Bunge hilo la Afrika Mashariki.
Spika wa kwanza wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA), Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akizungunguza na wabunge wa Bunge hilo, walipomtembelea ofisini kwake jijini Dar es Salaam, ili umsalimia na kupata mawazo kutokana na uzoefu wake hasa alipokuwa Spika wa Bunge hilo la Afrika Mashariki.
ukumbini
Spika wa kwanza wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA), Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akiwa katika picha ya pamoja baada ya kuzungunguza na wabunge wa Bunge hilo, walipomtembelea ofisini kwake jijini Dar es Salaam, ili umsalimia na kupata mawazo kutokana na uzoefu wake hasa alipokuwa Spika wa Bunge hilo la Afrika Mashariki.
Shy-Rose Bhanji akimshukuru Kinana.
Kisha akapozi naye kwa picha ya kumbukumbu
Halafu akapozi na Msemaji wa CCM, Ole Sendeka
Baadaye tena akajipiga selfie, akiwa na Katibu wa NEC, Uchumi na Fedha Zakia Meghji
Spika wa kwanza wa Bunge la Afrika Mashariki, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiagana na Makongoro Nyerere
Spika wa kwanza wa Bunge la Afrika Mashariki, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiagana na Twaha Tasilima. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO-theNkoromo Blog

RAIS DKT.MAGUFULI AKUTANA NA MWAKILISHI WA BENKI YA DUNIA KWA NCHI ZA TANZANIA, BURUNDI, MALAWI NA SOMALIA BI. BELLA BIRD IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akisalimiana na Mwakilishi wa Benki ya Dunia kwa nchi za Tanzania, Burundi, Malawi na Somalia Bi. Bella Bird Ikulu jijini Dar es Salaam 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akiagana na Mwakilishi wa Benki ya Dunia kwa nchi za Tanzania, Burundi, Malawi na Somalia Bi. Bella Bird mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU.




Ikulu, Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 03 Novemba, 2016 amekutana na Mwakilishi wa Benki ya Dunia katika nchi za Tanzania, Burundi, Malawi na Somalia Bi. Bella Bird na kuzungumzia utekelezaji wa miradi ya maendeleo nchini Tanzania yenye thamani ya jumla ya Dola za Marekani Bilioni 1.6 zikiwa ni mkopo kutoka benki hiyo.



Akizungumza baada ya kumaliza mazungumzo yake na Rais Magufuli, Bi. Bella Bird amesema mikopo hiyo inalenga kusaidia juhudi za maendeleo nchini Tanzania na itatolewa katika sekta mbalimbali zikiwemo nishati, usafirishaji, elimu na maji.

"Miradi hii yote imelenga zaidi kuharakisha maendeleo na kuleta matokeo katika maisha ya Watanzania, ni miradi ambayo inahitaji uongozi na msukumo mzuri kutoka Serikalini na tunafurahi kwamba Rais Magufuli ni kiongozi ambaye ana dhamira ya dhati ya kusimamia maendeleo" amesema Bi. Bella Bird.


Kwa upande wake Rais Magufuli ameishukuru Benki ya Dunia kwa kuendelea kushirikiana na Tanzania katika maendeleo na ametoa wito kwa Benki hiyo kuharakisha utoaji wa mikopo kwa ajili ya kutekeleza miradi.


"Tunataka kuona mambo yanatokea badala ya kutumia muda mwingi kuzungumza, miradi hii ina manufaa makubwa kwa watanzania na tungependa utekelezaji wake ufanyike haraka, na ili ufanyike haraka Benki ya Dunia inapaswa kutupatia mikopo kwa wakati unaofaa" amesisitiza Rais Magufuli.


Aidha, Rais Magufuli amemhakikishia Bi. Bella Bird kuwa Serikali yake ya Awamu ya Tano imejipanga kusimamia utekelezaji wa miradi yote inayotekelezwa sasa na itakayoanza kutekelezwa katika siku zijazo kwa mkopo kutoka Benki ya Dunia.

Kwa hivi sasa miradi 26 yenye thamani ya Jumla ya Dola za Marekani Bilioni 4.5 inatekelezwa hapa nchini kwa mkopo kutoka Benki ya Dunia.



Gerson Msigwa

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

Dar es Salaam

03 Novemba, 2016

DKT MGWATU: SIJARIDHISHWA NA UKUSANYAJI MAPATO NA MADENI.

$
0
0
Kivuko cha MV. Kilambo kinachotoa huduma ya uvushaji katika Mto Ruvuma, unaozitenganisha nchi za Msumbiji na Tanzania katika eneo la KIlambo (TANZANIA) na Namoto (Msumbiji). . Kivuko hiki kinasimamiwa na Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA)
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme ( TEMESA) Dkt Mussa Mgwatu akikagua kitabu kinachoonyesha taarifa za safari zinazofanywa na kivuko pamoja na hali ya kivuko kinapokuwa safarini.Picha zote na Theresia Mwami TEMESA Mtwara.
 
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA Dkt Mussa Mgwatu (kushoto) akiongea na Meneja wa TEMESA Mtwara Mhandisi Said Mongomongo alipotembelea ofisi hiyo, ili kujionea hali halisi ya kituo hicho pamoja na utendaji kazi wake.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA Dkt Mussa Mgwatu (kulia) akisikiliza malalamiko ya abiria wa MV. Mafanikioalifanya ziara Mkoani Mtwara.
 
 
Na Theresia Mwami TEMESA Mtwara.

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dkt. Mussa Mgwatu amesema kuwa hajaridhishwa na ukusanyaji wa mapato na madeni katika kituo cha Mtwara katika robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2016/2017 ambapo karakana imekusanya asilimia 20% tu ya kiasi cha pesa ilichozalisha.

Dkt Mgwatu amesema kuwa hatovumilia uzembe wowote utakaojitokeza katika suala la ukusanyaji wa mapato na madeni katika vituo vyote vya TEMESA nchini.“Hatuwezi kuendesha vituo na karakana zetu kwa mwendo huu hivyo inatupasa kuongeza juhudi katika kufuatilia madeni” alisema Dkt. Mgwatu.

Kwa upande wake Meneja wa TEMESA Mtwara Mhandisi Said Mongomongo amesema kuwa kuna changamoto za Taasisi nyingi kutolipa kwa wakati gharama za matengenezo ya magari na mashine mbalimbali katika karakana yake.Mhandisi Mongomongo amewataja baadhi ya wadaiwa sugu kuwa ni pamoja na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na Ofisi ya Katibu Tawala mkoani Mtwara.

Akiwa mkoani Mtwara, Dkt Mgwatu ametembelea Kivuko cha MV. Mafanikio kinachotoa huduma ya usafiri kati ya Msangamkuu na Msemo pamoja na Kivuko cha MV. Kilambo kinachotoa huduma kati ya Kilambo (upande wa Tanzania) na Namoto (upande wa Msumbiji).

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dkt. Mussa Mgwatu yupo katika ziara ya kikazi katika mikoa ya Lindi na Mtwara kuangalia utendaji kazi wa vituo hivyo.

NYUKI WAZUA KIZAA ZAA KATIKA MCHEZO WA RUVU SHOOTING NA AFRICAN LYON

$
0
0
 Wachezaji wa timu za Ruvu Shooting wenye jezi rangi ya bluu na wa African Lyon wakiwa wamelala chini ikiwa ni kujihami na makundi ya nyuki ambayo yalikuwa yanapita uwanjani hapo hivyo wachezaji, waamuzi na mabenchi ya wachezaji wa akiba wote walilazimika kulala chini ikiwa ni kujinusuru kutokana na hali hiyo. Katika mchezo huo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara. Shooting iliibuka na ushndi wa bao 1-0 lililofungwa na mshambuliaji mwenye nguvu za miguu Issa Kanduru kunako dakika ya 19.
 'Ni kama wanasema 'Nyuki hao bado wapo tuendelee kujificha chini ya viti"

 Watu wazima chini ya viti 'Chezea nyuki wewe'

VIJUZO VYA MAGAZETI YA LEO IJUMAA NOVEMBA 4

MAHOJIANO YA KWANZA YA RAIS MAGUFULI NA WAHARIRI IKULU

OFISI YA MTAKWIMU MKUU YATOA TAARIFA YA MFUMKO WA BEI ZANZIBAR.

$
0
0
Baadhi ya Waandishi wa Habari waliohudhuria katika Mkutano kuhusiana na Mfumuko wa bei katika Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali Mwanakwerekwe Zanzibar wakifuatilia maelezo kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha bei Khamis Ahmada Shauri.
Mkuu wa Kitengo cha Bei Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali Khamis Ahmada Shauri akielezea kuhusu Mfumuko wa Bei kutoka Sept 2016 ambapo ulifika asilimia 4.0 na kufikia asilimia 4.1 Oct 2016.
Meneja Msaidizi Idara ya Uchumi Benki Kuu Tawi la Zanzibar Evarist Mgangaluma akifafanua jambo kuhusiana na Mfumuko wa Bei kutoka Sept 2016 ambapo ulifika asilimia 4.0 na kufikia asilimia 4.1 Oct 2016.
Mwandishi mwandamizi kutoka ITV Farouk Karim akiuliza maswali katika mkutano wa kuelezea Mfumuko wa Bei kutoka Sept 2016 ambapo ulifika asilimia 4.0 na kufikia asilimia 4.1 Oct 2016.PICHA NA YUSSUF SIMAI-MAELEZO ZANZIBAR.

KUTOKA BUNGENI MJINI DODOMA

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mfunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Novemba 3, 2016. Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

SERIKALI YAANZA MCHAKATO WA UJENZI WA RELI YA KATI KWA KIWANGO CHA KIMATAIFA (STANDARD GAUGE)

$
0
0
 
Na Frank Shija, MAELEZO.
 
Serikali ya Awamu ya Tano ndani ya mwaka mmoja imeanza mipango ya kuboresha usafiri wa reli ya Kati kwa kuijenga kwa kiwango cha kimataifa yaani Standard Gauge. Usafiri huu utaongeza fursa za kiuchumi kwani mazao ya chakula na biashara toka mikoa ya Kigoma, Kagera, Mwanza, Shinyanga, Simiyu, Tabora na Singida kuelekea Dar es Salaam yatasafirishwa kwa haraka.

Reli hii itarahisisha pia usafiri wa abiria wa mikoa ya Kanda ya Ziwa, Kati na Magharibi. Usafiri wa treni kwa kiwango kikubwa huwa ni wa uhakika na wa gharama nafuu. Hivyo ujenzi wa reli kwa Standard Gauge uteleta ukombozi mkubwa wa kiuchumi kwa watu wa maeneo hayo na Taifa kwa ujumla.

Kwa kipindi kirefu huduma ya usafiri wa treni kupitia Reli ya Kati (Central Line Railway) imekuwa msaada mkubwa kwa wananchi wa mkoa wa Kigoma na maeneo ya Kanda ya ziwa na nchi za jirani zikiwemo Burundi, Rwanda, Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.Historia inaonesha kuwa Reli ya Kati kama inavyojulikana sasa ilijengwa kati ya mwaka 1905 hadi 1914 wakati huo ikiitwa Reli ya Tanganyika kwa kuwa ilikuwa ikielekea Mkoani Kigoma ambako Ziwa Tanganyika linapatikana.

Kutokana na umuhimu wake katika kukuza uchumi kupitia usafirishaji bidhaa na huduma mbalimbali ndani na nje ya Tanzania, Katika mwaka wa fedha 2016/2017 Serikali imeamua kuja na mpango kabambe wa kuifanyia maboresho miundombinu ya  reli hiyo ili iweze kwenda na wakati na kasi ya ukuaji wa uchumi.Mpango huo unahusisha ujenzi wa mtandao wa Reli mpya ya Kati katika Viwango vya Kimataifa (Standard Gauge 80’) ili kuendana na kasi ya ongezeko la mizigo.

Msemaji wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Bw. William Budoya anaeleza kuwa gharama iliyokaidiriwa kutumika kukamilisha mradi huo ni Dola za Kimarekani Bilioni 7.6 ambazo ni sawa na shilingi za Kitanzania Trilioni 16.Fedha hizo zitatumika kugharamia ujenzi wa Kilomita 2,561 za reli kwa kiwango cha Kimataifa . Ili kufanikisha mradi huo Serikali imepata ufadhili kutoka Benki ya Exim ya China ambayo imekubali kutoa mkopo wenye masharti nafuu.

Aidha, katika kuhakikisha kuwa ujenzi huo unafanikiwa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli anakutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Benki ya Exim ya China Bw. Liu Liang Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Katika mazungumzo yao Rais wa benki hiyo anamuhakikishia Rais Dkt. John Magufuli kuwa Benki hiyo iko tayari kutoa kiasi hicho cha fedha ili kufanikisha ujenzi wa kilometa 2,190 za reli. Pia anamuhakikishia Rais kuwa Benki hiyo itashirikiana na Tanzania katika kubadilishana uzoefu na utaalamu katika ujenzi na uendeshaji wa reli hiyo.Akiuzungumzia ujenzi wa Reli hiyo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli anabainisha kuwa kukamilika kwa mradi huo kutasaidia kuinua uchumi wa Tanzania na nchi jirani zisizopakana na bahari zikiwemo Uganda, Rwanda, Burundi, na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Anasema reli hiyo mpya itakua tofauti na inayotumika sasa kutokana na uwezo  wake wa kuhimili usafirishaji wa mizigo mingi kwa kuwa inajengwa kwa kiwango cha Kimataifa "Standard Gauge railway " na itaanzia Dar es Salaam Mpaka Kigoma, kupitia Tabora, Mwanza,Isaka hadi Rusumo; Kaliua -Mpanda -Karema na Uvinza -Musongati nchini Burundi.

Katika ufafanuzi alioutoa hivi karibuni kuhusu ujenzi wa reli hiyo wakati wa Mkutano Mkuu Maalum wa Chama cha Mapinduzi mjini Dodoma hivi karibuni, Rais John Pombe Magufuli alisema tayari mchakato wa ujenzi wa reli hiyo umeanza kwa kutangaza zabuni ili kumpata mkandarasi atakaye jenga Reli hiyo.

Anasema sambamba na kazi hiyo Serikali itakarabati matawi ya reli ya kati sehemu ya Kaliua-Mpanda ili kuboresha ufanisi wake, kwa kutenga Sh. bilioni 5.5 za ajili ya usanifu.Aidha, Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa miaka mitano uliowasilishwa bungeni Dodoma na Waziri wa Fedha na Mipango ,Dk. Philip Mpango unaeleza kuwa Serikali imejipanga kufanya usanifu na ujenzi wa madaraja 16 kati ya 28 yaliyochakaa kati ya Dar es Salaam na Tabora.

Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Servaciaus Likwelile akizungumza mara baada ya utiaji saini wa makubaliano wa ujenzi wa reli hiyo kwa niaba ya Serikali ya Tanzania na Naibu Meneja Mikopo Nafuu wa Benki ya Exim ya China Bw. Zhu Ying anasema kuwa Dola za Kimarekani bilioni 7.6 ambazo ni sawa na Shilingi Trilioni 16 zitatumika kutekeleza mradi huo.
 
Dkt. Likwelile anasema hatua hiyo inawezesha kuanza kwa kazi ya upembuzi yakinifu, usanifu na uundwaji wa timu za pamoja kuanza kuainisha mahitaji halisi ya ujenzi wa mradi huo.Anasema mradi huu umekuja wakati muafaka kutokana na kwamba reli iliyopo sasa ambayo ni ya Kiwango cha "meter gauge” haina uwezo mkubwa katika ubebaji wake wa mizigo, hata baada ya kufanyiwa ukarabati.Kwa mwaka ni tani Milioni 5 za mizigo ndizo zinaweza kupitishwa na reli ya sasa, ambazo haziwezi kukabili mahitaji ya mizigo ya Kanda hii ambayo itafikia tani Milioni 30 ifikapo mwaka 2025.

Kutokana na uhitaji huo wa kukabiliana na uongezaji wa mizigo kwa kujenga uwezo wa kuihudumia kwa kuwa na reli ambayo pamoja na kuwa na uwezo wa kubeba mizigo hiyo itakuwa na uwezo wa kubeba abiria wengi zaidi na kwa starehe lakini pia kwa kasi ya spidi ya wastani wa kilometa 100 kwa saa hivyo kuwezesha abiria kufika haraka zaidi sehemu wanazokwenda.

Pia wakati wa ujenzi wa reli hiyo watanzania takribani 300,000 watapata ajira kutokana na kushiriki katika ujenzi wa reli hiyo.

WIZARA YA ELIMU YAKABIDHIWA RASMI VYUO VYA MAENDELEO YA WANANCHI

$
0
0

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo, Jinsia , Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga wa kwanza kulia akimkabidhi Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia Bi. Maimuna Tarish katikati hati za makubaliano ya kuhamishia Vyuo vya maendeleo ya Wananchi wakati wa hafla fupi ya makabidhiano hayo yaliyofanyika jijini Dar es salaam. 
 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo, Jinsia , Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga aliyesimama akiongea na watendaji wa Wizara hiyo na Wizara ya Elimu hawapo pichani wakati wa makabidhiano ya nyaraka za makubaliano ya kuhamishia Vyuo vya maendeleo ya Wananchi Wizara ya Elimu yaliyofanyika jijini Dar es salaam. Aliyekaa ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia Bi. Maimuna Tarish.Picha Na Ally Daud- MAELEZO.


Na Ally Daud-MAELEZO.

WIZARA ya Elimu,Sayansi na Teknolojia imekabidhiwa rasmi Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi vipatavyo 55 kutoka Wizara ya Maendeleo, Jinsia , Wazee na Watoto ikiwa ni kutekeleza agizo la Rais Magufuli alilotoa Aprili mwaka huu wakati akikabidhi hati idhini kwa Wizara hiyo ili kuendeleza vyuo hivyo nchini.

Akiongea na waandishi wa habari wakati wa makabidhiano ya nyaraka za makubaliano Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo, Jinsia , Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga amesema kuwa kukabdhiwa kwa vyuo hivyo kwenye Wizara ya Elimu ni utekelezaji wa Agizo la Mhe. Rais Magufuli la kuhamishia lililotolewa Aprili mwaka huu.

“Tumekabidhi rasmi vyuo vya maendeleo ya wananchi mikononi mwa wizara ya Elimu kama alivyotuagiza Mh. Rais Aprili mwaka huu ili visimamiwe kwa utaratibu mzuri pamoja na maendeleo yake kwa ajili ya wananchi na taifa kwa ujumla” alisema Bi. Nkinga.

Aidha Bi. Nkinga amesema kuwa vyuo hivyo vitaendelea na shughuli zake za kutoa elimu kwa wananchi kama ilivyokua zamani ikiwa chini ya Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia kama ilivyoonyeshwa kwenye hati idhini iliyotolewa na Mh. Rais Magufuli.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia Bi. Maimuna Tarish amesema kuwa Vyuo hivyo vinatakiwa kuwa na ufundi stadi ambao upo kwenye viwango vya Wizara hiyo ili kufikia uchumi wa kati hususani kwenye viwanda.

“Vyuo sasa vinatakiwa kutoa mafundi na wahandisi wenye ufundi stadi ambao upo kwenye kiwango cha wizara ya Elimu ili kukidhi teknolojia na kukuza uchumi wan chi kufikia uchumi wa kati kupitia viwanda” alisema Bi.Tarish.

Naye Mkuu wa Chuo Cha Maendeleo ya Wananchi Arnautoglu Bi. Nsembia Mbwambo amesema kuwa wanaamini Wizara ya Elimu itawapa muongozo mzuri zaidi kuongeza ufundi stadi kwa wanafunzi wa vyuo hivyo.

Makabidhiano hayo yaliyofanywa na Wizara hizo mbili ni makubaliano ya utekelezaji wa agizo la Mh. Rais lililotolewa Aprili mwaka huu kuwa vyuo vyote vya maendeleo ya wananchi viratibiwe na Wizara ya Elimu, Sayansi na teknolojia.

EU YAWEKEZA EURO MILIONI 1.7 KITUO CHA UTAMADUNI MAKUMIRA

$
0
0
Umoja wa Ulaya (EU) umewekeza zaidi ya Euro milioni 1 na laki 7 katika kituo cha Utamaduni cha Makumira kitengo kilichoko ndani ya Chuo Kikuu cha Makumira ambapo chuo kikubwa cha sanaa kinajengwa pamoja na kumbi ya burudani itakayogharimu kiasi hicho.

Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) kwa nchi za Afrika Mashariki Roeland Van De Geer amefanya ziara chuoni hapo ambapo amejionea shughuli za ujenzi zinazoendelea katika chuo hicho na kusema kuwa kupitia chuo hicho cha utamaduni wa Tanzania na makabila yake utaendelezwa ili kuleta manufaa kwa vijana na jamii nzima.

Akizungumza na wanahabari mara baada ya ziara hiyo amesema kuwa wataendelea kuunga mkono juhudi za kutunza utamaduni kwani vijana wataweza kutengeneza fursa za ajira kupitia sanaa za utamaduni.Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) kwa nchi za Afrika Mashariki Roeland Van De Geer akizungumza katika kituo cha Utamaduni cha Makumira kilichopo mkoani Arusha,mara baada ya kutembelea kituo hicho.(Picha na Ferdinand Shayo).

Meneja mradi huo Randall Stubbs amesema kuwa kwa sasa wanatoa mafunzo ya ngoma za utamaduni wa makabila ya wamasai, wameru na wachaga ikiwa ni pamoja na kufanya maonyesho ya utamaduni katika maeneo mbalimbali.

“Ujenzi utakapokamilika kutakua na ukumbi wa kisasa, jengo maalumu la mafunzo kwa utamaduni wa bara la Afrika, Asia na Ulaya ili utamaduni uweze kuwa endelevu na kurithishwa vizazi na vizazi” alisema Randall.Meneja Mradi wa Kituo cha Utamaduni cha Makumira, Randall Stubbs akitoa maelekezo kwa Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) kwa nchi za Afrika Mashariki Roeland Van De Geer alipotembelea kituoni hapo.Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) kwa nchi za Afrika Mashariki Roeland Van De Geer akiwa katika kituo cha Utamaduni cha Makumira kilichopo mkoani Arusha, mara baada ya kutembelea kituo hicho.Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) kwa nchi za Afrika Mashariki Roeland Van De Geer akiwa kwenye picha ya pamoja na watumishi wa kituo cha utamaduni cha Makumira jijini Arusha.Meneja Mradi wa Kituo cha Utamaduni cha Makumira, Randall Stubbs akitoa maelezo kwa Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) kwa nchi za Afrika Mashariki Roeland Van De Geer (kushoto) aliyeambatana na Mwakilishi wa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Amon Manyama (kulia).

PICHA TANO ZA RAIS DKT MAGUFULI ALIPOFANYA MAHOJIANO NA WAHARIRI WA VYOMBO VYA HABARI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM LEO

TANZANIA CIVIL SOCETY STATEMENT TOWARDS THE UNFCCC COP22

$
0
0
ForumCC Project Officer Fazal Issa (left) and Dar es Salaam Program Manager of Oxfam Tanzania Heri Ayubu speaking to journalists during a press conference organized by ForumCC, Care Tanzania and Oxfam Tanzania to brief on the Tanzania Civil Society Statement towards the UNFCCC COP22 which will be held in Marrakesh-Morocco from 7-18th November 2016.
Journalists taking notes during a press conference organized by ForumCC, Care Tanzania and Oxfam Tanzania to brief on the Tanzania Civil Society Statement towards the UNFCCC COP22 which will be held in Marrakesh-Morocco from 7-18th November 2016

Read more in the below attached statement

MAJIBU YA SERIKALI YA HOJA ZA WABUNGE KUHUSU MPANGO WA MAENDELEO WA TAIFA NA MWONGOZO WA BAJETI YA SERIKALI KWA MWAKA 2017/2018

$
0
0

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) (Kulia wanaoshuka ngazi), akizungumza jambo na Mbunge wa Kasulu Mjini, Mhe. Daniel Nsanzugwanko, baada ya kumalizika kwa mjadala wa mchana kuhusu Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa mwaka 2017/2018 na Mwongozo wa Kuandaa Mpango wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka 2017/2018, Bungeni Mjini Dodoma
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (MB), (kushoto), akijibu hoja mbalimbali za Waheshimiwa wabunge kuhusu Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa mwaka 2017/2018 na Mwongozo wa Kuandaa Mpango wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka 2017/2018, Bungeni Mjini Dodoma

Baadhi ya Wabunge wakiwapongeza Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) (Kulia) na Naibu Waziri wake Mhe. Dkt Ashatu Kijaji (Mb) (Katikati), baada ya kujibu hoja mbalimbali za Waheshimiwa wabunge kuhusu Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka 2017/2018 na Mwongozo wa Kuandaa Mpango wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka 2017/2018, Bungeni Mjini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), akimpongeza Naibu Waziri wake, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, baada ya kuwasilisha kwa umahili mkubwa majibu ya serikali kutokana na hoja mbalimbali zilizotolewa na wabunge wakati wa kujadili Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka 2017/2018 na Mwongozo wa Kuandaa Mpango wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka 2017/2018, Bungeni Mjini Dodoma.
Naibu Waziri wa Wizara ya Fedha na Mipango, Mhe. Dkt Ashatu Kijaji (Mb), akizungumza na Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango Bibi Florence Mwanri (kulia) pamoja na maafisa wengine waandamizi wa Tume hiyo baada ya kuwasilishwa kwa majibu ya hoja mbalimbali za Waheshimiwa Wabunge kuhusu Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka 2017/2018 na Mwongozo wa Kuandaa Mpango wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka 2017/2018, Bungeni Mjini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bibi Dorothy Mwanyika, akifurahia jambo na Kamishna wa Bajeti wa Wizara hiyo, Bw. John Cheyo, baada ya kujibiwa kwa hoja mbalimbali za Waheshimiwa Wabunge kuhusu Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa mwaka 2017/2018 na Mwongozo wa Kuandaa Mpango wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka 2017/2018, Bungeni Mjini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (MB), (kushoto), akipongezwa na Mbunge wa Liwale, George Huruma Mkuchika, baada ya Waziri huyo kujibu hoja mbalimbali za Waheshimiwa wabunge kuhusu Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa mwaka 2017/2018 na Mwongozo wa Kuandaa Mpango wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka 2017/2018, Bungeni Mjini Dodoma
Baadhi ya Maafisa waandamizi wa Wizara ya Fedha na Mipango pamoja na Tume ya Mipango, wakiwa katika picha ya pamoja baada ya Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (MB), na Naibu waziri wake Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) kujibu hoja mbalimbali za Waheshimiwa Wabunge kuhusu Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa mwaka 2017/2018 na Mwongozo wa Kuandaa Mpango wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka 2017/2018, Bungeni Mjini Dodoma.
Kamisha wa Bajeti kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. John Cheyo (kulia), akibadilishana mawazo na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Profesa Joyce Ndalichako (katikati) na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Susan Kolimba, nje ya ukumbi wa Bunge baada ya Serikali kupitia Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (Mb) na Naibu Waziri wake Mhe. Dkt Ashatu Kijaji (Mb), kujibu hoja mbalimbali za Waheshimiwa wabunge kuhusu Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa mwaka 2017/2018 na Mwongozo wa Kuandaa Mpango wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka 2017/2018, Bungeni Mjini Dodoma. (Picha zote na Benny Mwaipaja-Wizara ya Fedha na Mipango)

RAIS DKT MAGUFULI AFANYA MAHOJIANO NA WAHARIRI WA VYOMBO VYA HABARI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM LEO

$
0
0



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akijibu maswali
kutoka kwa wahariri wa vyombo mbalimbali aliokutana nao kwa mahojiano leo Ijumaa Oktoba 4, 2016 katika ukumbi wa mikutano wa Ikulu jijini Dar es salaam

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akijibu maswali
kutoka kwa wahariri wa vyombo mbalimbali aliokutana nao kwa mahojiano leo Ijumaa Oktoba 4, 2016 katika ukumbi wa mikutano wa Ikulu jijini Dar es salaam

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akijibu maswali
kutoka kwa wahariri wa vyombo mbalimbali aliokutana nao kwa mahojiano leo Ijumaa Oktoba 4, 2016 katika ukumbi wa mikutano wa Ikulu jijini Dar es salaam

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) Dkt. Ayoub Rioba wakati wa kupokea  maswali kutoka kwa wahariri wa vyombo mbalimbali aliokutana nao kwa mahojiano leo Ijumaa Oktoba 4, 2016 katika ukumbi wa mikutano wa Ikulu jijini Dar es salaam




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimsikiliza mwanahabari Sammy Awami wa BBC wakati akiuliza maswali kutoka kwa wahariri wa vyombo mbalimbali aliokutana nao kwa mahojiano leo Ijumaa Oktoba 4, 2016 katika ukumbi w3a mikutano wa Ikulu jijini Dar es salaam


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimsikiliza Mhariri Mtendaji wa magazeti ya Serikali (TSN) Dkt. Jim Yonazi wakati akiuliza maswali
kutoka kwa wahariri wa vyombo mbalimbali aliokutana nao kwa mahojiano leo Ijumaa Oktoba 4, 2016 katika ukumbi w3a mikutano wa Ikulu jijini Dar es salaam.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimsikiliza Mtangazaji Tido Mhando wakati akiuliza maswali kutoka kwa wahariri wa vyombo mbalimbali aliokutana nao kwa mahojiano leo Ijumaa Oktoba 4, 2016 katika ukumbi w3a mikutano wa Ikulu jijini Dar es salaam.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimsikiliza Msanii Mrisho Mpoto akiimbwa wimbo wa "SIJONZE" wakati alipokutana na wahariri kwa mahojiano leo Ijumaa Oktoba 4, 2016 katika ukumbi w3a mikutano wa Ikulu jijini Dar es salaam.PICHA NA IKULU

MADAKTARI BINGWA WA TAASISI YA MOI WAFANYA UPASUAJI WA VICHWA MAJI NA MGONGO WAZI MNAZI MMOJA ZANZIBAR

$
0
0
Daktari bingwa wa upasuaji wa ubongo na mishipa ya fahamu ambae pia ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Taasisi ya MOI Othman Kiloloma akimueleza Waziri wa Afya Zanzibar (hayupo pichani) jinsi Taasisi hiyo inavyookoa maisha ya watoto wanaokabiliwa na maradhi hayo, (kulia) ni Afisa Habari wa GSM Foundation Khalfani Kiwamba.
Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo akizungumza na ujumbe wa Taasisi ya MOI na GSM Foundation ambao wapo Zanzibar kuwafanyia upasuaji watoto wenye vichwa vikubwa katika Hospitali ya Mnazi mmoja Mjini Zanzibar.
Dkt. Mohammed Ali Haji wa Kitengo cha upasuaji vichwa maji na mgongo wazi wa Hospitali ya Mnazimmoja akizungumzia ukubwa wa tatizo hilo katika visiwa vya Unguja na Pemba.
Dkt. Yassin Juma kutoka Kitengo cha MOI akiwa katika maandalizi ya kumfanyia upasuaji wa kichwa mmoja ya watoto waliofika Hospitali ya Mnazi mmoja kufanyiwa tiba hiyo.
Waziri wa Afya wa Zanzibar Mahmoud Thabit Kombo wa nne (kulia) akiwa na Dkt. Othman Kiloloma watatu (kulia)wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Wizara na maafisa wa GSM Foundation. Picha na Makame Mshenga/Maelezo Zanzibar.
Viewing all 46334 articles
Browse latest View live


Latest Images