Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46397 articles
Browse latest View live

NAPE AFUNGA KAMPENI ZA UDIWANI ELERAI-JIJINI ARUSHA

$
0
0
Wakazi wa kata ya Elerai ,Arusha mjini wakiwa kwenye picha ya pamoja na Katibu wa NEC Itikdi na Uenezi Nape Nnauye maraa baada ya kufungwa kwa kampeni za uchaguzi wa Diwani, juni 14.2013.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akisalimiana na wanachama wa CCM kata ya Elerai mara tu baada ya kuwasili kwenye kata hiyo.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akibadilishana jambo na mmoja wa wanachama wakongwe wa kata ya Elerai kabla ya kuanza kwa mkutano wa kufunga kampeni za uchaguzi wa Udiwani ya kata hiyo.
 Mbunge wa Vijana mkoani Arusha , Ndugu Catherine Magige akihutubia wakazi wa kata ya Elerai na kuwataka wakazi wa kata hiyo kutambua thamani ya kura kwa kuichagua CCM.
 Naibu Waziri wa Ardhi, Mhe. Goodluck Olemadeye akihutubia wakazi wa kata ya Elerai na kuwaambia CCM inatekeleza ilani yake ya uchaguzi kwa wakati na kila kilichoahidiwa Arusha kitafanyika.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akimnadi mgombea wa kiti cha udiwani kata ya Elerai, Mwl.Emmanuel Laizer,na kuwaambia wana Arusha muda wa kufanya maendeleo ni huu na CCM haina kazi nyingine zaidi ya kuleta maendeleo Arusha.
 Mgombea wa kiti cha Udiwani kwa tiketi ya CCM, Mwalimu Emmanuel Laizer akihutubia wakazi wa kata ya Elerai  kwenye mkutano wa kufunga kampeni.


 Bibi na mjukuu wake wakifuatilia kwa makini yale yanayosemwa na viongozi wa CCM wakati wa kufunga kampeni za udiwani kata ya Elerai.
Mbunge wa Vijana Arusha ,Ndugu Catherine Magige akisikiliza kwa makini sera za mgombea wa udiwani wa kata ya Elerai ,Mwl. Emmanuel Laizer.

 Mboya akihutubia wakazi wa kata ya Elerai na kuwaelezea kuwa alipotea sana kuishabikia Chadema na amewasihi wakazi wa kata hiyo kutofanya makosa kama kweli wanataka maendeleo.

SEMINA KWA VIJANA -LIKIZO NA MAFANIKIO.

HAPPYNESS WATIMANYWA NDIE MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI

$
0
0

Mshindi wa taji la Redds Miss Kanda ya Kati Happiness Watimanywa (Katikati) akiwa na nyuso ya furaha mara baada ya kamati ya majaji kumtangaza mshindi katika kinyanganyiro kilichoshirikisha walimbwendwe 12 kutoka Mikoa ya Dodoma, Singida, Tabora na Kigoma Wa Kwa Kwanza kulia Ni Mshindi wa Tatu Jackline huku Mshindi wa Pili ni  ( Wa kwanza Kushoto) Sabrina Juma Kutoka Mkoani Tabora


Jaji Mkuu wa Shindano ya Kumsaka Mloimbwende wa Kanda ya Kati Mh Hashim Lundenga Akipungia mikono watanzania waliofika kushuhudia mlimbwende wa Kanda ya kati anapatikana
Mshiriki wa Kinyanganyiro Cha Redds Miss Kanda ya Kati Hawa Nyange akijitambulisha
 Mmoja wa Washiriki wa Kinyanganyiro Cha Kumtafuta Mlimbwende wa Kanda ya kati akijitambulisha mbele ya hadhara
 Muda wa Kuonyesha Vipaji ukawadia
 Mavazi ya Ubunifu
 Walimbwende walioingia hatua Ya Tano Bora
 Wadau wa Miss Tabora wakifuatilia shindano kwa ukaribu kabisa
Mratibu na mwandaaji wa Redds Miss Kanda ya Kati akitoa Maneno huku pembeni yake ni Mgeni Rasmi (katikati) Mh John Komba akiwa na baadhi ya wabunge wenzake kutoka Zanzibar
Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya Amin akicheza na mmoja wa mashabiki wake ambaye alikua akiigiza kama Linah jana wakati wa shindano la kumtafuta Redds Miss Kanda ya Kati
Mmoja wa mashabiki wakimtunza Mwanamziki wa Kizazi kipya Amin wakati alipokuwa akitoa Burudani Jana katika Kinyanganyiro Cha Kumtafuta Mlimbwende wa Kanda ya Kati
Baadhi ya wadau waliojitokeza kwenye kushuhudia Shindano la Redds Miss Kanda ya Kati lililofanyika Usiku wa Kuamkia Leo Katika Ukumbi wa Kilimani Mkoani Dodoma.Picha Na Josephat Lukaza Wa Lukaza Blog

hafla ya Washindi wa Mashindano ya Guinness Football Challenge 2013

$
0
0

 Washindi wa Mashindano ya Guinness Football Challenge 2013 wakiwa kjatika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) Epraimu Mafuru naMeneja wa bia ya Guinnes Davis Kambi wakati wa tafrija hiyo.
 Mkurugenzi wa Masoko wa SBL, Ephaim Mafuru nae akionesha kipaji chake mbele ya vijana hao.
 Meneja wa bia ya Guinness Davis Kambi (kushoto) na Mkurugenzi wa Masoko wa SBL, Ephraim Mafuru wakiwa katika picha na wadau wengine wa Guinness na wafanyakazi wa SBL.
 Ilikuwa ni furaha tu kwa kila mtu.
Wadau wa Guinness wakibadilishana mawili matatu wakati wa tafrija hiyo.
 Regina Gwae kutoka kampuni ya R & R Associate akizungumza jambo na mmoja wa washiriki wa mashindano ya Guinness Football Challenge
 Meneja wa bia ya Guinness Davis Kambi akilamba picha na mabalozi wa kinywaji hicho.
Baada ya kumalizika kwa mashindano ya Guinness Football Challenge yaliyokuwa yakiendeshwa na Kupitia kipindi maarufu cha  Guinness Football Challenge TV Show, hatimaye wawakilishi wa Tanzania katika mashindano hayo jana wamefanyiwa sherehe fupi katika Ukumbi wa Savannah Lounge Jijini Dar es Salaam na waandaji  na wadhamini wa shindano hilo Kampuni ya Bia ya Serengeti kwa kuwapongeza kwa hatua waliyofikia.



Yaliyokuwa yakifanyika Afrika Kusini hatimaye yalimalizika hivi karibuni huku timu ya Tanzania ikiishia katika hatua ya nusu fainali kwa nchi kadhaa za Afrika ikiwemo Ghana, Cameroon, Kenya na Uganda zilizoshiriki mashindano hayo ukiwa ni msimu wa tatu.



Katika hafla hiyo ambayo pia ilihudhuriwa na wanahabari iliwashuhudia vijana walioshiriki mashindano hayo wakiwa na nyuso za furaha na kulakiwa kwa shangwe na uongozi wa Kampuni ya Bia ya Serengeti.



Akizungumza katika hafla fupi iliyofanyika katika Ukumbi wa Savannah Lounge Meneja Masoko wa Kampuni ya bia ya Serengeti,Moses Kebba ameipongeza timu hiyo kwa kufikia hatua nzuri ya mashindano hayo ambayo yalishirikisha timu mbalimbali za nchi zingine  za Afrika.



Alisema kwamba katika hatua hiyo ya nusu fainali waliofikia ni dhahiri vijana hao wamefanya kazi nzuri huku akivishukuru vyombo vya habari kwa kuwatangaza vyema wakati wa ushiriki wao kati mashindano hayo ya Guinnes Football Challenge.



Amesema kwamba katika mashindano hayo nchi kadhaa zilishiriki kama vile  Ghana, Cameroun, Kenya & Uganda, ambapo amekiri kwamba katika mashindano hayo kumekuwapo na ushindani mkubwa licha ya Tanzania kutoibuka na ushindi ilifanikiwa kufikia katika hatua ya nusu fainali.

Kwa upende wake Meneja wa bia ya Guinnes Davis kambi amesema kwamba  wataendelea kusaidia zaidi kuibua vipaji vya soka kupitia ushiriki huo ambao utaleta tija katika soka la Tanzania kwa kutangazika hatimaye kufanya vyema katika mashindano hayo ambayo yamekuwa na umaarufu mkubwa Afrika na sasa wataendelea kutafuta zaidi vipaji vitakavyoshiriki katika msimu ujao.




“Kila mmoja katika kampuni yetu ya SBL na watanzania wanayofuraha na nakuwapongeza Daniel Msekwa na  Mwalimu Akida,  kwa kufanya vizuri licha ya kushindwa kufika hatua ya fainali lakini kazi mlioifanya imeonekana na mmeweza kuiwakilisha vyem Tanzania katika mashindano ya Guinness Football Challenge”, Alisema Kambi



Katika fainali ya mashinado hayo yaliyoshirikisha pia timu za Uganda na Kenya timu ya Tanzania ya  GUINNESS® FOOTBALL CHALLENGE iliwakilishwa na Daniel Msekwa, Mwalimu Akida, Mohamed Kobembe, Gullam Sosha, Hamza Rashid,Lukwesa Kanakamfumu, Abubakari Mohamed, Kherry Sadallah, Simon Chimbo na Emmanuel Temu. 



Akizungumzia mashindano hayo Daniel Msekwa amesema: “Tumepata uzoefu mkubwa katika mashindano lakini kubwa ni kuhakikisha tunafanya mambo kulingana na mawasiliano ya kupata vipaji zaidi ambapo timu za Kenya na Uganda zilifanikiwa kufikia malengo mazuri lakini hayo yote ni changamoto kwetu.”



 “Tunaishukuru Kampuni ya Bia ya Serengeti kwa sababu walifanya kila jitihada kipindi tupo Afrika Kusini kwenye mashindano na kuona utofauti wa nchi zingine kama Ghana na Cameroon,

hafla ya Washindi wa Mashindano ya Guinness Football Challenge 2013

$
0
0

 Washindi wa Mashindano ya Guinness Football Challenge 2013 wakiwa kjatika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) Epraimu Mafuru naMeneja wa bia ya Guinnes Davis Kambi wakati wa tafrija hiyo.
 Mkurugenzi wa Masoko wa SBL, Ephaim Mafuru nae akionesha kipaji chake mbele ya vijana hao.
 Meneja wa bia ya Guinness Davis Kambi (kushoto) na Mkurugenzi wa Masoko wa SBL, Ephraim Mafuru wakiwa katika picha na wadau wengine wa Guinness na wafanyakazi wa SBL.
 Ilikuwa ni furaha tu kwa kila mtu.
Wadau wa Guinness wakibadilishana mawili matatu wakati wa tafrija hiyo.
 Regina Gwae kutoka kampuni ya R & R Associate akizungumza jambo na mmoja wa washiriki wa mashindano ya Guinness Football Challenge
 Meneja wa bia ya Guinness Davis Kambi akilamba picha na mabalozi wa kinywaji hicho.
Baada ya kumalizika kwa mashindano ya Guinness Football Challenge yaliyokuwa yakiendeshwa na Kupitia kipindi maarufu cha  Guinness Football Challenge TV Show, hatimaye wawakilishi wa Tanzania katika mashindano hayo jana wamefanyiwa sherehe fupi katika Ukumbi wa Savannah Lounge Jijini Dar es Salaam na waandaji  na wadhamini wa shindano hilo Kampuni ya Bia ya Serengeti kwa kuwapongeza kwa hatua waliyofikia.



Yaliyokuwa yakifanyika Afrika Kusini hatimaye yalimalizika hivi karibuni huku timu ya Tanzania ikiishia katika hatua ya nusu fainali kwa nchi kadhaa za Afrika ikiwemo Ghana, Cameroon, Kenya na Uganda zilizoshiriki mashindano hayo ukiwa ni msimu wa tatu.



Katika hafla hiyo ambayo pia ilihudhuriwa na wanahabari iliwashuhudia vijana walioshiriki mashindano hayo wakiwa na nyuso za furaha na kulakiwa kwa shangwe na uongozi wa Kampuni ya Bia ya Serengeti.



Akizungumza katika hafla fupi iliyofanyika katika Ukumbi wa Savannah Lounge Meneja Masoko wa Kampuni ya bia ya Serengeti,Moses Kebba ameipongeza timu hiyo kwa kufikia hatua nzuri ya mashindano hayo ambayo yalishirikisha timu mbalimbali za nchi zingine  za Afrika.



Alisema kwamba katika hatua hiyo ya nusu fainali waliofikia ni dhahiri vijana hao wamefanya kazi nzuri huku akivishukuru vyombo vya habari kwa kuwatangaza vyema wakati wa ushiriki wao kati mashindano hayo ya Guinnes Football Challenge.



Amesema kwamba katika mashindano hayo nchi kadhaa zilishiriki kama vile  Ghana, Cameroun, Kenya & Uganda, ambapo amekiri kwamba katika mashindano hayo kumekuwapo na ushindani mkubwa licha ya Tanzania kutoibuka na ushindi ilifanikiwa kufikia katika hatua ya nusu fainali.

Kwa upende wake Meneja wa bia ya Guinnes Davis kambi amesema kwamba  wataendelea kusaidia zaidi kuibua vipaji vya soka kupitia ushiriki huo ambao utaleta tija katika soka la Tanzania kwa kutangazika hatimaye kufanya vyema katika mashindano hayo ambayo yamekuwa na umaarufu mkubwa Afrika na sasa wataendelea kutafuta zaidi vipaji vitakavyoshiriki katika msimu ujao.




“Kila mmoja katika kampuni yetu ya SBL na watanzania wanayofuraha na nakuwapongeza Daniel Msekwa na  Mwalimu Akida,  kwa kufanya vizuri licha ya kushindwa kufika hatua ya fainali lakini kazi mlioifanya imeonekana na mmeweza kuiwakilisha vyem Tanzania katika mashindano ya Guinness Football Challenge”, Alisema Kambi



Katika fainali ya mashinado hayo yaliyoshirikisha pia timu za Uganda na Kenya timu ya Tanzania ya  GUINNESS® FOOTBALL CHALLENGE iliwakilishwa na Daniel Msekwa, Mwalimu Akida, Mohamed Kobembe, Gullam Sosha, Hamza Rashid,Lukwesa Kanakamfumu, Abubakari Mohamed, Kherry Sadallah, Simon Chimbo na Emmanuel Temu. 



Akizungumzia mashindano hayo Daniel Msekwa amesema: “Tumepata uzoefu mkubwa katika mashindano lakini kubwa ni kuhakikisha tunafanya mambo kulingana na mawasiliano ya kupata vipaji zaidi ambapo timu za Kenya na Uganda zilifanikiwa kufikia malengo mazuri lakini hayo yote ni changamoto kwetu.”



 “Tunaishukuru Kampuni ya Bia ya Serengeti kwa sababu walifanya kila jitihada kipindi tupo Afrika Kusini kwenye mashindano na kuona utofauti wa nchi zingine kama Ghana na Cameroon,

WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA AZINDUA KITABU CHA SUMBAWANGA NG'ARA

$
0
0
 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mizengo Kayanza Peter pinda akikata utepe kuashiria kuzindua rasmi kitabu cha "Sumbawanga Ng'ara" kilichoandikwa na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya (wa katikati) katika ukumbi wa Dodoma Hoteli Mjini Dodoma, kulia ni Mstahiki Meya wa Manispaa ya Sumbawanga Sabas Katepa. Kitabu hicho kinaelezea na kutoa muongozo juu ya usafi na uhifadhi wa mazingira katika Manispaa ya Sumbawanga, Mkoa wa Rukwa na taifa kwa ujumla. Kitabu hicho kinauzwa Tsh. 3,500 kwa lengo la kukusanya fedha ya kuchapisha machapisho mengine zaidi. 
 Zoezi la uzinduzi likiendelea. SOMA ITABU HICHO HAPO CHINI........ 
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mizengo Kayanza Peter pinda akisoma hotuba yake wakati wa uzinduzi wa kitabu hicho alitoa wito kwa Uongozi wa Mkoa wa Rukwa kuhakikisha wanasimamia utekelezaji wa mpango waliouanzisha wa Sumbawanga Ng'ara kwa kuweka mikakati na kutengeneza sheria ndogondogo za kusimamia mpango huo. 
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya akisoma hotuba yake ya kumkaribisha Waziri Mkuu kuzindua kitabu cha Sumbawnga Ng'ara ambapo alimshuru kiongozi huyo Mkuu katika nchi kwa kutenga muda wake pamoja na waliohudhuria katika hafla hiyo fupi ya uzinduzi. Zaidi ya vitabu 175 vilinunuliwa baada ya uzinduzi huo. 
Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima akitambulisha viongozi mbalimbali walioshiriki hafla hiyo wakiwemo baadhi ya mawaziri, wabunge, madiwani kutoka Manispaa ya Sumbawanga na viongozi wengine wa chama na Serikali. 
 Mama Tunu Pinda mke wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mzengo Kayanza Peter Pinda akizungumza katika hafla hiyo ambapo alimpongeza sana Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya kwa kuanzisha mpango wa Sumbawanga Ng'ara pamoja na kuandikia kitabu. Alisema viongozi kama hawa wanaofanya mambo kwa vitendo ndio viongozi wa mfano wanaotakiwa katika taifa letu. 
 Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anaeshugulia Elimu Mhe. Kassim Majaliwa akizungumza katika hafla hiyo. Kwa upande wake alisema kama Wizara wanaipongeza Serikali na wananchi wa Mkoa wa Rukwa kwa kuanzisha mpango huo wa Sumbawanga Ng'ara na kuunga mkono. Alisema halmashauri zingine zinatakiwa zijifunze kwa kuanzisha mipango mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ya utunzaji wa mazingira. Mhe. Majaliwa aliahaidi kununua vitabu 10 vya Sumbawanga Ng'ara. 
Mhe. Pindi Chana, Mbunge Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Njombe akizungumza katika hafla hiyo. Alimsifu mwandishi wa kitabu hicho cha Sumbawanga Ng'ara ambaye pia ni muasisi wa mpango huo Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya na kusema ni mchapakazi wa kuigwa. Mhe. Chana aliahidi kununua vitabu 30 vya Sumabwanga Ng'ara kwa ajili ya kuhamasisha usafi Mkoani Njombe.



Mbunge wa Kilindi CCM Mhe. Beatrace Shelukindo akizungumza katika hafla hiyo ambaye naye alipewa fursa na Waziri Mkuu aweze kuzungumza ambapo alisema Mkoa wa Rukwa umepata kiongozi thabiti ambaye angetamani afanye kazi katika Mkoa wake wa Tanga. Mhe. Selukindo alinunua vitabu 20 kwa ajili ya madiwani wa Korogwe ili awape wivu wa kufanya kazi katika maeneo yao.

 Mama Anne wa UNDP akizungumza katika hafla hiyo ya uzinduzi wa kitabu cha Sumbawanga Ng'ara ambapo alifurahishwa na kitendo hicho na kusema yeye pia ni mdau wa mazingira na hivyo akaahidi kununua vitabu 10 kwa ajili ya kuviweka katika maktaba yake.

 Mstahiki Meya wa Manispaa ya Sumbawanga Sabas Katepa akielezea kwa kifupi Mpango wa Sumbwanga Ng'ara ambapo alisema tangu mpango huo uanzishwe na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya wananchi wengi wameupokea vizuri na tayari Mji wa Sumbawanga umeshanza kubadilika ukilinganisha na kipindi cha nyuma.

 Wajukuu wa Baba wa Taifa Mwalimu Julius K. Nyerere wanaosoma nchini Marekeani wakijitambulisha katika hafla hiyo baada ya kupewa fursa na Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda.

 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa akiendelea na hotuba yake.

 Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda akimkadhi Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima kitabu cha Sumbawanga Ng'ara mara baada ya kukizindua rasmi.

(Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa @ rukwareview.blogspot.com)

Benki ya Barclays yatoa msaada wa vitu mbalimbali wodi ya watoto hospitali ya Taifa Muhimbili.

$
0
0
 Wafanyakazi wa Benki ya Barclays wakitoa msaada wa vitu ,mbalimbali katika wodi ya watoto Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam, vikiwemo sabuni, vyandaru, miswaki, vinywaji baridi pamoja na dawa za meno, vitu hivyo vimetokana na michango ya wafanyakazi wanawake wa benki hiyo.
 Mwanasheria wa Benki ya Barclays, Farija Ghilas akimkabidhi sehemu ya msaada waliotoa kwa watoto waliolazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam, Sakina Hassani. Vitu hivyo vimetokana na michango ya wafanyakazi wanawake wanaofanyakazi katika benki hivyo. 
 Rahma Said mkazi wa Manzese jijini Dar es Salaam akipokea sehemu ya msaada uliotolewa na wafanyakazi wanawake wa benki ya Barclays wakati walipofika kuwajulia hali wagonjwa waliolazwa katika wodi ya watoto katika hospitali ta Taifa Muhimbili. Vitu vilivyokabidhiwa leo ni pamoja na sabuni, vyandaru, miswaki, vinywaji baridi pamoja na dawa za meno, vitu hivyo vimetokana na michango ya wafanyakazi wanawake wa benki hiyo.
 Mwanasheria wa Benki ya Barclays, Farija Ghilas akimkabidhi sehemu ya msaada waliotoa kwa watoto waliolazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam jana, Sakina Hassani. Vitu vimetokana na michango ya wafanyakazi wanawake wanaofanyakazi katika benki hivyo. 

 Poa zawadi ya mafuta mama.
Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Barclays, Neema Sengo akizungumza na waandishi wa habari baada kutembelea wodi ya watoto katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam na kwafariji watoto walolazwa katika wodi hiyo na kuwabidhi vitu mbalimbali vikiwemo sabuni, miswaki, vyandarua, mafuta, pamoja na vinywaji baridi kwa watoto waliolazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es salaam, leo. 

SHEREHE YA UWT KWA PLO ZAFANA DAR

$
0
0
 Mwenyekiti wa Ujoma wa Wanawake Tanzaia (UWT) Sophia Simba akiwalaki Mjumbe wa Kamati Tendaji wa Chama Cha Ukombozi wa Palestina (PLO), Jehad Abu Zead na Makamu Mwenyekiti wa POL Tayseer Khalid (mwanaume mwenye miwani) Khalid na ujumbe wake walipowasili kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, leo jioni kwa ajili ya sherehe maalum, waliyoandaliwa na UWT kwenye viwanja hivyo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu wa NEC ya CCM, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro na Wanne Kushoto ni Katibu Mkuu wa UWT, Amina Makilagi.

 Mwenyekiti wa Ujoma wa Wanawake Tanzaia (UWT) Sophia Simba (wapili kulia), akiwa na  Mjumbe wa Kamati Tendaji wa Chama Cha Ukombozi wa Palestina (PLO), Jehad Abu Zead, Makamu Mwenyekiti wa PLO Tayseer Khalid, wakati ujumbe wa chama hicho ulipowasili kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, leo jioni kwa ajili ya sherehe maalum, iliyoandaliwa na UWT kwenye viwanja hivyo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu Mkuu wa UWT, Amina Makilagi 
 Mjumbe wa Kamati Tendaji ya Chama Cha Ukombozi wa Palestina (PLO) Jihad Abu Zead akitazama bidhaa za kina mama wa UWT, ujumabe wa Makamu Mwenyekiti wa PLO, Tayseer Khali (kulia kwa Jihad), ulipowalisi. Wengine ni Mwenyeji wao, Katibu wa NEC ya CCM, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migoro na Mwenyekiti wa UWT, Sophia Simba.
 UNAONA WANAVYOWASHANGILIA! Katibu wa NEC ya CCM, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro akimwambia Mjumbe wa Kamati Tendaji ya Chama Cha Ukombozi cha Palestina (PLO), Jehad Abu Zead, wakati ujumbe wa chama hicho ulipowasili kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, leo jioni kwa ajili ya sherehe maalum, iliyoandaliwa na UWT kwenye viwanja hivyo jijini Dar es Salaam. Watatu kushoto ni, Makamu Mwenyekiti wa PLO, Tayseer Khalid na Mwenyekiti wa UWT, Sophia Simba.
 Mjumbe wa Kamati Tendaji ya Chama Cha Ukombozi cha Palestina (PLO) Jehad Abu Zead, akimpa kadi mwanachama mpya wa CCM, Mohamed Ali, katika sherehe maalum iliyoandaliwa na Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) leo kumkaribisha Makamu Mwenyekiti wa PLO, Tayseer Khalid (Wapili kulia) na ujumabe wake, kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa UWT, Sophia Simba na Wanne ni Katibu wa NEC ya CCM, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro na Wasita niBalozi wa Palestina hapa nchini, Dk. Nasri Abujaisa
 Mwenyekiti wa Ujoma wa Wanawake Tanzaia (UWT) Sophia Simba akimzadia nguo, Mjumbe wa Kamati Tendaji wa Chama Cha Ukombozi wa Palestina (PLO), Jehad Abu Zead, wakati  cha Palestina (PLO) Jehad Abu Zead, akimpa kadi mwanachama mpya wa CCM, Mohamed Ali, katika sherehe maalum iliyoandaliwa na UWT leo kumkaribisha Makamu Mwenyekiti wa PLO, Tayseer Khalid (kulia) na ujumabe wake, kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam.
 Katibu wa NEC ya CCM, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro akizungumza wakati sherehe maalum iliyoandaliwa na Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) leo kumkaribisha Makamu Mwenyekiti wa PLO, Tayseer Khalid (Wapili kulia) na ujumabe wake, kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam.
 Mamia ya wanachama wapya wa CCM ambao wengi wao ni vijana, wakiwa katika picha ya p0amoja na viongozi baada ya kupewa kadi zao katika sherehe maalum iliyoandaliwa na Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) leo kumkaribisha Makamu Mwenyekiti wa PLO, Tayseer Khalid (Wapili kulia) na ujumabe wake, kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam.
 Kinamama wakimwayamwaya wakati wa sherehe hiyo
 Wengine wakigaragara chini kwa furaha wakati wa sherehe hiyo
 Kikundi cha Vijana wa CCM cha Ilala wakionyesha umahiri wao wa kuchgeza sarakasi wakati wa sherehe hiyo
 Katibu Mkuu wa UWT, Amina Makilagi akimwekeza jambo, Mwenyekiti wake, Sophia Simba wakati wa sherehe hiyo
 Viongozi wote wa meza kuu wakiwaaga wananchi baada ya sherehe hiyo kufana
 Wana-UWT nao wakiwaaga viongozi kwa furaha
 Mjumbe wa Kamati Tandaji wa PLO, Jihad akionyesha zawadi aliyopewa na wanachama wa UWT katika sherehe hiyo. Kushoto ni Katibu wa NEC ya CCM, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro na Kulia ni Mwenyekiti wa UWT Sophia Simba na Makamu Mwenyekiti wa PLO Tayseer Khalid.
 Mwenyekiti wa UWT Sophia Simba akizungumza wakati wa sherehe hiyo
 Jihad akizungumza wakati wa sherehe hiyo
 Vijana wanaoshiriki Miss Kanga Party ya Kibaha, wakisalimiana na wageni wa heshima kwenye sherehe hiyo.
 Wana-UWT wakiwa wamemzonga Jihad na hivyo Katibu Mkuu wa UWT Amina Makilagi kulazimika kutumia msuli kuwazuia, walipokuwa wakimshangilia kiongozi wakati akiondoka Uwanjani
Mwenyekiti wa UWT, Sophia Simba akiagana na Makamu Mwenyekiti wa PLO baada ya sherehe. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO.

MLIPUKO MWENGINE ARUSHA KATIKA MKUTANO WA CHADEMA NA KUJERUHI WATU KADHAA JIONI YA LEO.

$
0
0
DAMU ZIKITAPAKAA ENEO LA TUKIO.
Watu saba wanadaiwa kujeruhiwa vibaya kufuatia kwa kile kinachodhaniwa  ni mlipuko wa bomu uliotokea  kwenye mkutano wa CHADEMA Wakati  Mwenyekiti   wa chama hicho ,Mh Freeman Mbowe alipomaliza kuhutubia kwenye uwanja wa  Soweto jijini  Arusha .Picha kwa hisani ya MWAIPAYA-BLOG.

MAJERUHI WAKIWA CHINI.

MFUKO UNAOSEMEKANA NDIYO ULIYOKUWA NA HICHO KITU KILICHOSABABISHA MLIPUKO

MAJERUHI WAKIWA HOSPITALI

MAJERUHI WAKIPATA HUDUMA

kambi ya redds miss kinondoni yazinduliwa rasmi jijini dar.

$
0
0
Naibu Mustahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Mheshimiwa Songolo ambaye alimwakilisha mgeni rasmi meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda akiongoza harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya kununua vitanda kwa ajili ya akina mama wanaojifungua (delivery beds) kwa hospitali za Mwananyamala pamoja na Sinza Palestina ambapo warembo hao walitembelea wodi za akina mama na kufanya usafi. Pamoja na harambee kulizinduliwa rasmi kambi ya Redds Miss Kinondoni 2013. Pembeni ni Mkuu wa Itifaki wa Mashindano ya Miss Tanzania, Albert Makoye na Mratibu wa shindano la Redd's Miss Kinondoni Bw. Ssebo. Harambee hiyo ilifanyika ukumbi wa Ambassador uliopo hoteli ya JB Belmont jijini Dar es Salaam. 
Jumla ya vitanda 15 vyenye thamani ya shilingi milioni 52.5 zimepatikana katika harambee iliyoandaliwa na warembo wa Redds Miss Kinondoni 2013 kwa ajili ya kununua vitanda kwa ajili ya akina mama wanaojifungua (delivery beds) kwa hospitali za Mwananyamala pamoja na Sinza Palestina iliyofanyika katika ukumbi wa Ambassador uliopo hoteli ya JB Belmont jijini Dar es Salaam. 

Akizungumza mshiriki wa shindano hilo, Sarah Paul alisema kuwa wanamshukuru Mungu kwa kuweza kuwawezesha kufanya harambee hiyo ambayo ilitokana na wao baada ya kutembelea hospitali ya Mwananyamala pamoja na Sinza Palestina wakajionea uhaba wa vitanda vya akina mama wakati wa kujifungua.

"Tulisononeshwa sana na hali tuliyoikuta hospitalini hapo ambapo baada ya kuongea na mganga mkuu wa Manispaa ya Kinondoni dokta Gunini Kamba alitueleza kuwa jumla ya akina mama wapatao 50 mpaka 80 hujifungua kwa siku moja hivyo wanauhaba wa vitanda, tukaona tukae na viongozi wetu watusaidie kuandaa harambee na tunamshukuru Mungu tumefanikiwa kupata vitanda 15 japo nia yetu ilikuwa ni kupata vitanda 20," alisema mrembo huyo.

Mashindano ya Redd's Miss Kinondoni 2013 yanatarajia kufanyika kwenye ukumbi wa hoteli ya Golden Tulip siku ya Ijumaa 21 June 2013. Viingilio katika onyesho hilo ni shs. 60,000 VIP, shs. 25,000 kwa tiketi za kawaida na meza ya watu ukitazama zawadi.
Warembo wa Redds Miss Kinondoni 2013 wakitambulishwa kwa Naibu Mustahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Mheshimiwa Songolo ambaye alimwakilisha mgeni rasmi meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda. Mgeni huyo pia alipata fulsa ya kuzinduliwa rasmi kambi ya Redds Miss Kinondoni 2013 iliyopo katika hoteli ya JB Belmont jijini Dar es Salaam. 

Warembo wa Redds Miss Kinondoni 2013 walipata fulsa ya kucheza mara baada ya harambee na ufunguzi rasmi ya kambi yao. 
Furaha zilitanda.
Kila mmoja akionyesha ufundi wake.
Mashindano ya Redd's Miss Kinondoni yamedhaminiwa na Redd's Original, Chilly Willy Energy Drink, Oriflame Natural Beauty Products, Times Fm, JB Belmonte Hotel, Michuzi Media Group, Michuzijr Blog, Mtaa Kwa Mtaa Blog, Fullshangwe Blog, HandeniKwetu Blog, Mrokim Blog, TheHabari.com, JestinaGeorge Blog, SufianMafoto Blog, Global Publisher, Mdimuz Blog, Lukaza Blog, MO Blog na Kajunason Blog.

"USIKU WA TUDD THOMAS" Juni 30, 2013 DAR LIVE

NAPE: PUUZENI VITISHO VYA CHADEMA

$
0
0

 Adai kesho ulinzi upo wa kutosha.
Awapongeza Arusha kuitosa Chadema.
. Atamba  CCM kuzoa kata zote.
. Awasihi wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura kesho.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Ndg.Nape Nnauye amewataka wananchi kwenye kata zinazofanya uchaguzi mdogo kesho kupuuza alivyoviita vitimbi vya Chadema na wafuasi wao badala yake wajitokeze kwa wingi kushiriki kwenye upigaji wa kura kwa amani na utulivu.

Nape ameyasema hayo jijini Arusha jana wakati alipokuwa anajibu maswali ya waandishi wa habari waliotaka kujua tathimini ya kampeni na jinsi CCM ilivyojipanga kwenye uchaguzi mdogo katika kata mbalimbali nchini.

Nape alisema kwa ujumla wake kampeni zimekwenda vizuri karibu katika kila kata ukiacha matukio kadhaa machache ya vurugu ambayo alidai yamekuwa yakiratibiwa na Chadema na wafuasi wao baada ya kuvuta bangi na kunywesha vijana wao viroba.

"nimekuwa Arusha kwa siku mbili tatu, hakuna mashaka kuwa Arusha wamechoshwa na vurugu za Chadema , baada ya kuhangaishwa kwa miaka mitatu na vurugu za Chadema wameamua sasa kurudisha utulivu na heshima ya jiji la Arusha, hivyo nawapongeza sana" alisema Nape.

" ni kweli hata mie nimesikia wenzetu baada ya kuona maji ya shingo wameamua kutumia vitisho kujaribu kutisha watu hasa kina mama na wazee wasiende kupiga kura, lakini nawahakikishia CCM tumejipanga kuwalinda waende kupiga kura kwa amani na utulivu. Isitoshe taarifa tulizoziapata zinaonyesha serikali imejipanga vizuri sana kulinda amani na utulivu, hivyo tunawaomba wananchi wajitokeze kwa wingi kupiga kura bila hofu" alisisitiza Nape.

Aidha Nape alidai kwa taarifa walizonazo wanamatumaini kuwa kata zote 25 zinazofanya uchaguzi mdogo CCM itashinda kwani wanaamini kuwa wananchi wana imani kubwa na CCM na kuwa vitimbi vinavyofanywa na wapinzani nchini vimewachefua sana wananchi.

Itakumbukwa kuwa chaguzi ndogo nchini zinafanyika kwenye kata 25 kufuatia kata hizo kuwa wazi kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo vifo na baadhi kuhama au kufukuzwa vyama vyao vya siasa.

Ushindani mkubwa ulitegemewa sana jijini Arusha ambapo kuna kata nne zinafanya ucahguzi mdogo kufuatia Chadema kuwafukuza madiwani wake. Hata hivyo hali jijini Arusha inaonyesha Chadema kulemewa sana kiasi cha kuwa na uwezekano wa kupoteza kata zote ambazo walikuwa wakizimiliki mwanzoni.


Nape Moses Nnauye
Chama Cha Mapinduzi
Ideology and Publicity Secretary

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AWAONGOZA VIONGOZI NA WANANCHI KUAGA MWILI WA MAREHEMU TIMOTH APIYO KARIMJEE LEO

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili wa aliyewahi kuwa Katibu Mkuu Kiongozi, marehemu, Timoth Apiyo, aliyefariki dunia nchini Afrika ya Kusini alikokuwa amelazwa kutokana na kusumbuliwa na maradhi. Shughuli hiyo ya kuaga mwili wa marehemu imefanyika leo Juni 15, 2013 kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, na baadaye mwili ulisafirishwa kuelekea Mkoani Mara kwa maziko.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwafariji wanafamilia baada ya kutoa heshima za mwisho mblele ya jeneza lenye mwili wa aliyewahi kuwa Katibu Mkuu Kiongozi, marehemu, Timoth Apiyo, aliyefariki dunia nchini Afrika ya Kusini alikokuwa amelazwa kutokana na kusumbuliwa na maradhi. Shughuli hiyo ya kuaga mwili wa marehemu imefanyika leo Juni 15, 2013 kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, na baadaye mwili ulisafirishwa kuelekea Mkoani Mara kwa maziko.

Naibu Katibu Mkuu Mstaafu wa Umoja wa Mataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro, akipita kutoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili wa aliyewahi kuwa Katibu Mkuu Kiongozi, marehemu, Timoth Apiyo, aliyefariki dunia nchini Afrika ya Kusini alikokuwa amelazwa kutokana na kusumbuliwa na maradhi. Shughuli hiyo ya kuaga mwili wa marehemu imefanyika leo Juni 15, 2013 kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, na baadaye mwili ulisafirishwa kuelekea Mkoani Mara kwa maziko.
Makamu wa Rais na Viongozi wengine mbali mbali waliokuwepo kwenye kuaga mwili wa aliyewahi kuwa Katibu Mkuu Kiongozi, marehemu, Timoth Apiyo, aliyefariki dunia nchini Afrika ya Kusini alikokuwa amelazwa kutokana na kusumbuliwa na maradhi. Shughuli hiyo ya kuaga mwili wa marehemu imefanyika leo Juni 15, 2013 kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, na baadaye mwili ulisafirishwa kuelekea Mkoani Mara kwa maziko.
Viongozi mbali mbali pia walikuwepo.
Katibu Mkuu Kiongozi,Mh. Balozi Ombeni Sefue akizungumza na waandishi wa habari.Picha na OMR.

Exim Bank supports national blood donation drive

$
0
0
 Exim Bank Tanzania staff donate blood during the bank’s annual Vein-to-Vein Campaign in a bid to raise 100 units of blood as part of the bank’s  commemoration of the World Blood Donor Day that is celebrated worldwide today.
 The Exim Bank Tanzania Assistant General Managers Shesgagiri Rao (right) and Kuldip Paliwal (centre) take part in the bank’s annual Vein-to-Vein Campaign that seeks to raise awareness on voluntary blood donation. 
The Exim Bank Tanzania Corporate Relations Manager Kinemo Kihomano (centre) briefs reporters on the bank’s annual Vein-to-Vein Campaign that seeks to raise awareness on voluntary blood donation. 
 The Exim Bank Tanzania Corporate Relations Manager Kinemo Kihomano (second left) takes a high-blood pressure test during the bank’s annual Vein-to-Vein Campaign that seeks to raise awareness on voluntary blood donation. 
A cross section of Exim Bank Tanzania staff pose for a photo shortly before the event.

Naibu Waziri Kilimo mgeni rasmi Tamasha la wasanii Mkuranga

$
0
0
   
NAIBU Waziri wa Kilimo, Adam Kighoma Malima atakuwa mgeni rasmi katika Tamasha la Wasanii Mastaa litakalofanyika Juni 29, mwaka huu kwenye kijiji cha Mwanzega, Mkuranga mkoa wa Pwani.

Akizungumza na viongozi wa Mtandao wa Wasanii (SHIWATA) mjini Dodoma katika vikao vya Bunge vinavyoendelea, Malima alisema amekubali kuwa mgeni rasmi vile vile tukio hilolinafanyika katika jimbo lake la uchaguzi la Mkuranga.

Mwenyekiti wa SHIWATA, Caasim Taalib alisema maandalizi ya tamasha hilo yanaendelea vizuri na kuongeza kuwa kutakuwa na matukio ya wanachama kukabidhiwa nyumba zao kwa wale waliomaliza michango yao akiwemo mchezaji wa zamani wa timu ya Taifa yaTanzania ‘Taifa Stars, Jellah Mtagwa atakabidhiwa nyumba yake.

Alisema Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida ambaye alikuwa mgeni rasmi tamasha lililopita Mei mwaka huu Dar es Salaam na kuahidi kukarabati barabara za kuingia kijiji cha wasanii Mkuranga atakabidhiwaq kadi piataasisi yake ya ujasiriliamali ambayo itawakopesha wasanii wa SHIWATA sh. Bil. 7 kwa ajili ya kuendeleza wasanii, itaanza kutekeleza mpango huo wa Awamu ya Kwanza siku hiyo.

Alisema mbunge wa Kinondoni Bw. Idd Azzan naye atakabidhiwa kadi ya kujiunga na SHIWATA ambako pia wabunge mbalimbali wamealikwa kuhudhuria tamasha hilo akiwemo mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu, Mbunge wa Ilala, Mussa Zungu.

Wabunge wengine wa mkoa wa Dar es Salaam walioalikwa katika tamasha hilo ni John Mnyika wa Ubungo, Mbunge wa Kawe, Halima Mdee, na Mwenyekiti wa Taifa wa NCCR- Mageuzi , James Mbatia.

Alisema mtandao wa SHIWATA ambao umekuwa ukiandaa matamasha ya wasanii kila mwezi limepeleka tamasha la Juni kwenda wilaya ya Mkuranga ambako ndiko zinakojengwa nyumba zao katika kijiji cha Mwanzega-Kimbili ambako mpaka sasa watu nane watakabidhiwa nyumba zao.

Wasanii 400 kutoka vikundi mbalimbali vikiwemo vya mkoa wa Pwani wanatarajiwa kushiriki katika tamasha hilo.

Wanachama wa SHIWATA nao wanakaribishwa kuhudhuria tamasha hilo.


Peter Mwenda
Ofisa Habari wa SHIWATA
0715/0752 222677


Rais Kikwete Mgeni rasmi mechi ya wakuu wa wilaya na wabunge

$
0
0
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mechi ya hisani itakayowakutanisha waheshimiwa wabunge na Wakuu wa wilaya, itakayopigwa Juni 29, katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

Mechi hiyo itatanguliwa na ile ya Juni 22 mjini Dodoma, ambapo huko mgeni rasmi atakuwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ambapo lengo la mechi hizo ni kuchangisha fedha za ujenzi wa shule ya albino, huku kukipangwa kuwa na burudani za kila aina, sambamba na wasanii watakaoamua kuungana na serikali juu ya uchangiaji huo.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Msemaji Mkuu wa timu hiyo ya wakuu wa wilaya, ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Muhingo Rweyemamu, alisema kuwa huku mheshimiwa rais akiwa mgeni rasmi, ila wamejipanga imara kwa ajili ya kuwaonyesha kazi wabunge, ambao baadhi yao wameanza kujigamba dhidi ya mechi hiyo ya aina yake.

Alisema kuwa Watanzania wote watakaopata fursa ya kuhudhuria kwenye mechi hizo wataaburudika kwa kiasi kikubwa, huku wakiamini kuwa licha ya wakuu wa wilaya wengi kuwa mikoani, ila wana nguvu na ari ya kushinda mbele ya wabunge. “Tupo imara na tutaanza mazoezi yetu kesho Jumatatu kwa kukutanisha wakuu wa wilaya wote waliokuwa kwenye timu hii, huku barua za kuwaombea mialiko kutoka kwa Wakuu wa Mikoa tayari zimeshafika kwa ajili ya kufanikisha zoezi hili.

“Katika mechi hizi, mwamuzi wa kati atakuwa atakuwa Reginald Mengi, ambaye ni Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, huku waamuzi wa pembeni wakiwa ni IGP Said Mwema na Stephen Wassira, ambapo wote watashiriki katika mchezo huu,” alisema.

Aliwataja Wakuu wa wilaya waliotwa kwenye uundwaji wa kikosi hicho kuwa ni pamoja na Venas Mwamoto (Kibondo), Ramadhan Maneno (Kigoma), Norman Sigara (Mbeya), Krispin Meela (Rungwe), Benson Mpesya (Kahama), Deodatus Kinanilo (Chunya), Herman Kapufyi (Same), Francis Isaac ( Chemba), Wilson Mkambaku (Kishapu), Yahya Nawanda (Iramba), Elibariki Kingu (Igunga), Festo Kiswaga (Nanyumbu), Paza Mwamlima (Mpanda), Abdallah Ulega (Kilwa), Seleman Mzee (Kwimba), John Mongela (Arusha), Konstantin Kanyasu (Ngara), Paulo Mzindakaya (Busega), Mrisho Gambo (Korogwe), uhingo rweyemamu handeni, Cristofa Magala( Newala), Erasto Sima (Bariadi), Jordan Rugimbana (Kinondoni), Joseph Mkirikiti (Songea), Ngemela Rubinga (Mpanda) nay eye mwenyewe anayotokea wwilaya ya Handeni, ambaye pia ni msemaji wa timu hiyo.

Aidha, Muhingo alitaja kikosi cha wanawake kuwa kinaongozwa na Beth Mkwasa (Bahi), Sarah Dumba (Njombe), Josephine Mapiro (Makete), Hafsa Mtasiwa (Pangani), Mboni Mgaza (Mkinga), Halima Dendegu (Tanga), Queen Mlozi (Singida), Angelina Mabula (Butiama), Merry Tesha (Ukerewe), Christina Mndeme (Hanang), Anna Magoha (Urambo) Jacqueline Liana ( Magu).

NAPE AITEKA DONGOBESH NA BASHNET

$
0
0

 Umati mkubwa wa wakazi wa Dongo besh wakimsikiliza kwa makini Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi kwenye mkutano wa kuhitimisha kampeni za udiwani zilizofanyika Dongobesh.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akihutubia wakazi wa kata ya Dongo besh na kuwaambia wakati ndio huu kwa wao kuchagua kiongozi atakaye wafaa kwa kuleta maendeleo yao.
 Mgombea wa udiwani wa Dongo besh, Joseph almaarufu Cheng Lee akihutubia wakazi wa eneo hilo.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akimsikiliza mkazi wa  Dongo besh aliyeamua kurudisha kadi ya Chadema  na kurejeaa CCM,baada ya kuelewa yale aliyokuwa akihutubia Nape.
 Mtoto huyu hakuwa nyuma kufuatilia mkutano wa kampeni za udiwani kwa tiketi ya CCM kata ya Dongo besh.
 Wakazi wa Dongo besh wakiwa juu ya mti kabisa kusikiliza sera za CCM.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi ,Nape Nnauye akipata mapokezi ya kichama alipowasili kwenye kata ya Dongo besh.
 Wazee wa kimila wakifanya ibada ya kimila kabla ya kuanza kwa mkutano wa kampeni za Udiwani Dongo besh.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akishiriki kucheza ngoma ya wenyeji wa Dongo besh mara baada ya kumaliza kuhutubia na kufunga kampeni za kugombea kiti cha udiwani.


BASHNET
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisalimiana na Waziri wa nchi ofisi ya Waziri Mkuu ( Uwekezaji na Uwewezeshaji) Dk. Marry Nagu.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akisalimiana na Mbunge wa Babati Vijijini  , ndugu JituSoni .


 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Taifa Nape Nnauye akisalimiana na mbunge wa Simanjiro Christopher Ole Sendeka.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akihutubia wakazi wa Bashnet wwakati wa kuhitimisha mikutano ya kampeni za udiwani.

 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akimtambulisha mgombea wa kiti cha udiwani kwa tiket ya CCM, Ndugu Nicodemus Gwandu.


 Mbunge wa Babati Vijijini, Jitu Soni akiwa pamoaja na wananchi wa jimbo lake wakati wa mkutano.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akimjulia hali mama mzazi wa Laurent Tara.

KAMPUNI YA STEPS YANOGESHA TUZO ZA BONGO MOVIE

$
0
0
Mkurugenzi wa Kampuni ya Steps, Diresh Solanki akimpa tuzo msanii bora wa kiume katika tasnia ya filamu nchini Jacob Stevin JB wakati wa utoaji wa tuzo hizo zilizofanyika usiku wa kuamkia leo na kuhudguliwa na wasanii wengi nchini hii ni kwa mara ya kwanza steps inaandaa tuzo hizi zitakazokuwa zikitolewa kila mwaka.
Pazia ra Tuzo za Steps Bongo Movie Awards ukiwa umefunguliwa na waziri wa Sayansi na Teknolojia Makame Mbawala
Mzee Majuto akipokea Tuzo ya msanii bora wa uchekeshaji.
Msanii Steve Nyerere akipokea Tuzo
Msanii Nice Mohamedi 'Mtunis' akipokea tuzo ya Mwaka 2012 zilizoandaliwa kwa mara ya kwanza na kampuni ya Steps Entatainment tuzo hizi zitakazokuwa zikitolewa kila mwaka.


MAMA SHILOLE AKIWA JUKWAANI
Mtoto Jenifa akichukua tuzo yake
Add caption


Msanii Niva akichukua TUZO ya msanii bora Chipkizi kulia yupo msanii mwenzake Rado
Photo: Mjumbe wa Kamati ya saidia Taifa Stars Ishinde, Ridhiwani Kikwete kushoto akimkabidhi tuzo Haji Adamu kwa niaba ya Jimmy Mponda aliyeshinda msanii bora wa Filamu za Mapigano wakati wa utoaji wa tuzo hizo zilizofanyika kwa mara ya kwanza nchini na kuandalia na kampuni ya Steps Picha na www.burudan.blogspot.com
Mjumbe wa Kamati ya saidia Taifa Stars Ishinde, Ridhiwani Kikwete kushoto akimkabidhi tuzo Haji Adamu kwa niaba ya Jimmy Mponda aliyeshinda msanii bora wa Filamu za Mapigano wakati wa utoaji wa tuzo hizo zilizofanyika kwa mara ya kwanza nchini na kuandalia na kampuni ya Steps.
Mjumbe wa Kamati ya saidia Taifa Stars Ishinde, Ridhiwani Kikwete wa tatu kushoto akiwapongeza baadhi ya wasanii wa marehemu Kanumba baada ya kuwakabizi tuzo
Mkurugenzi wa Kampuni ya Steps Dilesh Solanki akimkabizi tuzo ya mwongozaji bora wa filamu nchini kwa mwaka 2012 Vicent Kigosi 'Ray ' wakati wa utoaji wa tuzo hizo zilizofanyika usiku wa kuamkia leo na kuhudguliwa na wasanii wengi nchini hii ni kwa mara ya kwanza steps inaandaa tuzo hizi zitakazokuwa zikitolewa kila mwaka.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Steps Dilesh Solanki akifafanua jambo baada ya kumkabizi tuzo Vicent Kigos 'Ray' ya mwogozaji bora wa filamu nchini kwa mwaka 2012 wakati wa utoaji wa tuzo hizo zilizofanyika usiku wa kuamkia leo na kuhudguliwa na wasanii wengi nchini hii ni kwa mara ya kwanza steps inaandaa tuzo hizi zitakazokuwa zikitolewa kila mwaka.Picha na www.burudan.blogspot.com

Wafanyakazi wa Kampuni ya Steps wakipokea tuzo

Baazi ya wasanii wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kukabiziwa tuzo zao za kwanza kwa mwaka 2012 zilizozaminiwa na kampuni ya steps Picha na www.burudan.blogspot.com.

MPIGA PICHA mOHAMED aralakia  ZA KAVA MBALIMBALI ZA KAMPUNI YA STEPS AKIPOKEA TUZO

:KAMPUNI ya Usambazaji wa filamu ya Steps Entatainment ya jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki iliyopita ilitoa tuzo kwa wasanii bora waliofanya vizuri katika tasnia ya filamu nchini kwa mwaka 2012 ikiwa ni kwa mara ya kwanza kuanzishwa kwa tuzo hizo

Akizungumzia tuzo hizo Mkurugenzi wa Kampunu hiyo Direshi Solanki amesema kuwa tuzo hizo watakuwa wakizitoa kila mwaka kwa kuleta maendeleo ya filamu nchini kampuni hiyo iliyojikita katika kusambaza filamu za wasanii wameweka historia ya kuigwa kutokana na kuanzisha tuzo hizo

Baadhi ya washindi ambao walipatikana katika tuzo hizo wa kwanza ni Stevin Mangendela 'Stive Nyerere', Issa Mussa 'Cloud 112' Mohamed Nurdini 'Chek budi' Nice Mohamed 'Mtunisi' Iren Paul akinyakuwa msanii bora chipkizi wa kike

Wakati katika kinyanganyiro cha kumpata msanii bora wa kiume alinyakuwa Jacob Stevin 'JB' huku msanii bora wa kike ikienda kwa mwana dada Iren Uwoya

na msanii bora wa filamu za mapingano ilikwenda moja kwa moja kwa Jimmy Mponda 'Jimmy Masta'

Wakati katika kipengere cha muhongozaji bora wa filamu kilikwenda kwa vicent Kigosi' Ray' na kampuni yake ya RJ Filamu

mbali na hivyo kulikuwa na tuzo za heshima kwa wasanii waliofanya vizuri rakini kwa sasa awapo duniani moja ni kwa Stevin Kanumba,Saidi Kilowoko 'Sajuki' John Stefano,Hussein Ramadhani Mkiety,'Sharo Milionea'

Katika utoaji wa tuzo huzo kulikua na burudani nyingi zikiongozwa na Odama Bendi

MRISHO MPOTO NA BENDI YA MJOMBA BAND KUFANYA KAMPENI YA USAFI WA MAZINGIRA

$
0
0
1Msanii wa ngoma za asili na Mkurugenzi wa bendi ya Mjomba Band Mrisho Mpoto akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Kinondoni Mkwajuni wakati alipotangaza kuhusu kundi lake kuanza kampeni kubwa ya kuhamasisha wananchi kuhusu usafi wa mazingira mijini na vijijini kwa kunawa mikono na sabuni, kujenga na kutumia vyoo bora na kuboresha mzingira kwa ujumla ili kuhakikisha elimu hiyo inawafikia walengwa kwa kubadili tabia na njia mbadala za mawasiliano kuhusu elimu hiyo, Upatikanaji wa maji safi na salama na usafi wa mazingira bado ni tatizo kubwa kwa watanzania walio wengi, mwaka 2010 aslimia 9 tu ya wananchi waishio vijijini na asilimia 22 ya wananchi waishio mijini waliweza kupata huduma bora za usafi wa mazingira. kati ya sababu zingine , ni watu kutozingatia faida za usafi wa mazingira Katika k kampeni hiyo Mrisho Mpoto na kundi lake la mjomba Bandi wanashirikiana kwa pamoja na Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii, kushoto ni Mariam Mahamudu Afisa Afya, Mazingira Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii , Kampeni hiyo itaanza na mikoa ya Dodoma, Mara, Njombe, Rukwa na Tanga kabla ya kuendelea mikoa mingine2Mariam Mahamudu Afisa Afya, Mazingira Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii akizungumza katika mkutano huo kuzungumzia kuhusu kampeni hiyo, kulia ni Mrisho Mpoto Mkurugenzi wa Mjomba Band.3Kundi zima la mjomba band likiwa katika mazoezi makali katika makao makuu ya kundi hilo Kinondoni Mkwajuni.


Tumelala 4-2 dhidi ya ivory coast mnasemaje kiwango wadau..! HAYA PATA UHONDO WA MAPICHA

$
0
0
 Krosi maridadi ikitolewa na Shomary Kapombe iliyotupatia bao la pili lililotiwa kimiani na Mshambuliaji Thomas Ulimwengu.








 Shangwe zilitawala Uwanja mzima ambao leo ulijaa kuliko siku zote,maana hakukuonekana hata nafasi iliyokuwa wazi.


 Mshambuliaji wa Timu ya Ivory Coast,Yao Gerveis akiwania mpira na Beki wa Taifa Stars,Erasto Nyoni.
 Hapa ni kibega tu (hawajui kama sisi hiyo ni staili yetu).

 Vikosi vya Timu zote vikiwa vimejipanga wakati wa Wimbo wa Taifa.
 Benchi la Timu ya Ivory Cost likiongozwa na Kocha wao.
 Benchi letu.
 Wadau wa NSSF wakiwakilisha ipasavyo Uwanjani hapa.
 Jukwaa kuu likiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Mh. Said Meck Saddick,Waziri wa Ulinzi,Mh. Shamsi Vuai Nahodha na Viongozi wengine mbali mbali.
 Salamu za Wachezaji.
 Kikosi cha Taifa Stars.
Kikosi cha Ivory Cost.
 Leo ilikuwa ni burudani tupu kwani hata mashabiki wa timu za Simba na Yanga wakiungana na kuunganisha bendera zao,huku wakisema uzalendo kwanza.
 Ulinzi ni wa Uhakika maana wazee wa Feva walikuwepo kila kona.
 Ubao uonekanavyo baada ya mchezo.
 Watanzania Wenzetu wakiingia Uwanjani kuisapoti Timu yao.
 Kocha wa Taifa Stars,akisabahiana na Marefa.















Viewing all 46397 articles
Browse latest View live


Latest Images