Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 100 | 101 | (Page 102) | 103 | 104 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Mkurugenzi wa huduma za kibenki kwa wateja wakubwa wa Benki ya KCB Tanzania Frank Nyamundege akitoa mada juu ya huduma za benki hiyo wakati wa hafla ya chakula cha jioni kilichoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya wateja wake jijini Dar es Salaam juzi.
  Mkurugenzi mtendaji wa Benki ya KCB Tanzania Moezz Mir akiwahutubia wageni waalikwa wakati wa hafla ya chakula cha jioni kilichoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya wateja wake jijini Dar es Salaam juzi.
  Mwenyekiti wa bodi ya Benki ya KCB Tanzania Dk Edmund Mndolwa (kushoto) akibadilishana mawazo na mjumbe wa bodi Nehemiah Mchechu (katikati) pamoja na mkuu wa kitengo cha sheria na katibu wa benki hiyo Edward Lyimo, muda mfupi kabla ya chakula cha jioni kilichoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya wateja wake jijini Dar es Salaam juzi.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akipokea ujumbe maalumu toka kwa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt Donald Kaberuka ulioletwa kwake na mwakilishi mkazi wa Benki hiyo nchini Mhe Tonia Kandiero leo Juni 13, 2013 katika Ikulu Ndogo Dodoma.
  Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na mwakilishi mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) hiyo nchini Mhe Tonia Kandiero leo Juni 13, 2013 katika Ikulu Ndogo Dodoma baada ya kupkkea ujumbe maalumu toka kwa Rais wa Benki ya hiyo Dkt Donald Kaberuka. PICHA NA IKULU

  0 0

  TAARIFA ILIYOKIA CHUMBA CHA HABARI CHA GLOBU YA JAMII,INAELEZA KUWA MSANII WA MUZIKI WA KIZAZI KIPYA AITWAYE LANGA KILEO A.K.A LANGA AMEFARIKI DUNIA MAPEME LEO JIONI KATIKA HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI ALIKOKUWA AMELAZWA.

  LANGA AMBAYE INADAIWA KUWA ALIPATWA NA MALARIA KALI KIASI HATA KUPELEKEA KUKIMBIZWA HOSPITALI SIKU YA JANA.

  MUNGU AILAZE ROHO YA MAREMU MAHALI PEMA PEPONI-AMEN.

  0 0

   Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Bw. Nyirembe Munasa, akisisitiza jambo katika ufunguzi wa Mafunzo ya usimamizi wa Sheria ya Mazingira na Udhibiti wa biashara haramu ya bidhaa zinazoharibu tabaka la Ozoni. Mafunzo haya ya siku mbili nayafanyika katika Chuo cha Utalii Arusha na yanahusisha washiriki kutoka mikoa ya Arusha, Tanga na Kilimanjaro. Wa kwanza kulia na Kaimu Mkurugenzi Msaidizi Ofisi ya Makamu wa Rais, Bi. Rogathe Kisanga na Bw. Japhet Kanizius Afisa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais.  
   Sehemu ya washiriki wa Mafunzo hayo kutoka Sekta za mbalimbali wakiwemo Maafisa Forodha, Maafisa Biashara, Polisi, Mahakama, Waendesha Mashtaka, Uhamiaji, Wataalamu wa Mazingira na Vyombo vya Habari wakifuatilia hotuba ya ufunguzi katika kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Bw. Nyirembe Munasa. 
  Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Bw. Nyirembe Munasa (Kulia) akiongea na mmoja wa washiriki wa mafunzo ya usimamizi wa Sheria ya Mazingira na Udhibiti wa biashara haramu ya bidhaa zinazoharibu tabaka la Ozoni. Katikati ni Kaimu Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Mazingira Bi. Rogathe Kisanga. (Picha Na Lulu Mussa). 
   =======  ===========  =============
  Imeelezwa kuwa zaidi ya asilimia 90 ya Kemikali zinazoharibu tabaka la Ozoni hutumika katika vipoozi (refrigerants) kama majokofu na viyoyozi na matumizi ya kemikali hizi yapo kwa wingi katika nchi zilizoendelea na zinazoendelea kama Tanzania.


  Hayo yamesemwa leo na Mkuu wa Mkoa wa Arusha katika Hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Bw. Nyirembe Munasa katika ufunguzi wa Mafunzo ya Siku mbili kwa washiriki  kutoka Sekta mbalimbali wakiwemo Maafisa Forodha, Maafisa Biashara, Polisi, Mahakama, Waendesha Mashtaka, Uhamiaji, Wataalamu wa Mazingira na Vyombo vya Habari.


  Amesema, tafiti mbalimbali duniani zinaonyesha kuwa mionzi ya kikiukaurujuani (Ultraviolent-B radiation) husababisha kuongezeka kwa magonjwa ya saratani ya ngozi, uharibifu wa macho na upungufu wa uwezo wa mwili kujikinga na maradhi.


  Hata hivyo, katika kukabiliana na changamoto za mionzi hiyo mwaka 1993 Serikali  ya Tanzania iliridhia mkataba wa Vienna na Montreal kwa lengo la kudhibiti na kusitisha utengenezaji na matumizi ya kemikali zinazoharibu tabaka hilo kwa awamu kwa kuzingatia upatikanaji mbadala na rafiki kwa Tabaka la Ozoni.


  Japokuwa juhudi za kuhamasisha wadau kuhusu faida za kutumia kemikali mbadala na teknolojia mpya katika vifaa na mitambo mbalimbali zimeendeleshwa kwa kipindi kirefu, matumizi ya kemikali haribifu bado yapo. 


  Changamoto hii imetokana na kupungua kwa uingizaji wa vifaa hasa majokofu na viyoyozi vilivyotumika na vinavyotumia kemikali zisizo rafiki wa tabaka la Ozoni, uhaba wa mitambo ya kunasa na kurejereza vipoozi katika soko na ongezeko la mafundi wasiokuwa na taaluma na vifaa sahihi vya kuhudumia majokofu na viyoyozi.


  Mafunzo haya ya siku mbili yanafanyika katika Chuo cha Utalii Arusha na yanahusisha washiriki kutoka mikoa ya Arusha, Tanga na Kilimanjaro.


  Na Lulu Mussa

  Afisa Habari

  Ofisi ya Makamu wa Rais – Arusha  0 0

  Pata majibu na maelezo ya maswali yafuatayo na matibabu ya njia rahisi kutoka blog ya Afya Njema Na Mafanikio (www.mtsimbe.blogspot.com). Kwa sasa katika blog kuna maelezo ya:

  ·        Je Una Maumivi Ya Gouts (Viungo)?
  ·        Je Una Maumivu Ya Uti Wa Mgongo?
  ·        Je Una Tatizo la Kisukari?
  ·        Je Una Upara?
  ·        Je Ungependa Kuondoa Mabaka Mabaka Kwenye Ngozi?
  ·        Je, Nywele Zako Zinanyonyoka?
  ·        Je Una Fibroids Au Uvimbe Katika Kizazi?
  ·        Je Una Matatizo Ya Kushika Mimba?
  ·        Je Una Matatizo Na Siku Za Hedhi Au Maumivu?
  ·        Jinsi Ya Kupunguza Unene
  ·        Jinsi Ya Kuzuia Kumaliza Mapema
  ·        Je Jogoo Wako Hapandi Mtungi?
  ·        Je, Unapoteza Kumbukumbu?
  ·        Je, Ungependa Kuondoa Michirizi Katika Ngozi?
  ·        Jinsi Ya Kufanya Meno Yawe Meupe
  ·        Jinsi Ya Kuondoa Makunyanzi Ya Ngozi
  ·        Jinsi Ya Kufanya Matiti Yasimame (Yasilale)
  ·        Jinsi Ya Kuondoa Nywele Usoni
  ·        Je, Ungependa Kuwa Na Matiti Makubwa?
  ·        Je Macho Yako Hayaoni Vizuri?
  ·        Je, Una High Blood Pressure?
  ·        Je Una Allergies Na Kitu Chochote?
  ·        Jinsi Ya Kuondoa Vipele Vya Kunyoa Ndevu
  ·        Jinsi Ya Kuondoa Chunusi Usoni
  ·        Je Wewe Unakoroma Usiku Na Ungependa Uache?

  Kwa maoni tuandikie: mtsimbe@gmail.com

  0 0

   Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa kata ya Themi na kuwaambia wasirudie kosa la kudharauliwa kwa kuchagua watu wasiotambua thamani ya kura zao.
   Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwahakikishia wana Themi kuwa wakati huu ni wa kuirudisha heshima ya Arusha na kwa kumchagua mgombea wa CCM kutasaidia sana kuleta mabadiliko ya kimaendeleo katika mji huo.
  Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akimtambulisha mgombea wa kiti cha udiwani kata ya Themi, Victor G. Mkolwe, Juni, 13,2013 .
   Mgombea wa kiti cha udiwani kata ya Themi, Victor G. Mkolwe akihutubia wakazi wa kata hiyo na kuwaelezea moja ya mikakati yake ya kuleta maendeleo kwa wakazi hao,ambpo pia aliwaambia yeye hatangulizi siasa bali maendeleo na anatambua wakazi wake vizuri na changamoto zao na namna ya kuwasaidia.
   Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Arusha, Catherine Magige akihutubia wakazi wa kata ya Themi ambapo pamoja na kuwaomba kumpigia kura mgombea wa udiwani kwa tiketi ya CCM pia aliahidi kuwasaidia wakina mama Wajane ambao walitelekezwa na ahadi za uongo za vyama upinzani.
   Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisalimiana na baadhi ya wakina mama Wajane ambao walidanganywa na vyama vya upinzani na sasa wamerejea CCM.
  Wajane wa kata ya Themi wakisalimiana na mbunge wa viti maalum wa mkoa wa Arusha ,Catherine Magige. 
   Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisalimiana na vijana wa Arusha mjini waliokuwa wakijiburudisha na mchezo wa karata.
   Meya wa Jiji la Arusha, Ndugu Gaudence Lyimo akihutubia wakazi wa kata ya Themi na kuwataka wasifanye makosa katika uchaguzi huu.
  Rehema Mohamed maarufu kama Iron Lady akihutubia wakazi wa kata ya Themi ambapo aliwataka wakazi hao kuwa makini sana na wanasiasa wasiokuwa na mipango ya maendeleo.
   Kikundi cha ngoma cha Kambarage kikiburudisha wakazi wa kata ya Themi wakati wa mkutano wa kampeni za udiwani kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi.
   Kijana anayefahamika kwa jina la Mboya ambaye alikuwa mstari wa mbele katika harakati za Chadema,akihutubia wakazi wa kata ya Themi wilaya ya Arusha mjini na kuwaambia wasirudie kuchagua vyama ambavyo kura yao itapotea kwa matapeli wa kimataifa.
   Nico ambaye naye alikuwa mstari wa mbele kuongoza mipango michafu ya kuvuruga amani ya Arusha, amekiri kuwa chama pekee cha kisiasa Tanzania kwa sasa ni CCM na ameomba wakazi wa kata ya Themi kuungana na kumchagua diwani anayetokana na CCM ili kuleta maendeleo na si migomo.
   MNEC wa wilaya ya Arusha mjini Godfrey Mwalusamba akihutubia wakazi wa kata ya Themi,ambapo aliwaambia kuna uhumu wa kufanyia kazi maendeleo yao zaidi kuliko kushabikia vitu visivyo na tija.

  0 0

  0 0
 • 06/14/13--03:20: GARI INAUZWA BEI POA KABISA
 • DSC03335DSC03336DSC03340
  Make:Daihatsu
  Model:VS100P
  Body type:Station Wagon
  Colour:Silver
  Year:2001
  CC:659
  Fuel:Petrol
  Price: 7.8 Milion
  Contact :+255 754 940992.

  0 0

  Mratibu wa shindano la Redd's Miss Kinondoni 2013, Deniss Ssebo akiongea na waandishi wa habari kuhusiana na shindano hilo, alisema kuwa mwaka huu imeleta mapinduzi Makubwa katika sekta ya Afya, Elimu pamoja na Ajira.

  Ambapo mshindi wa kwanza atapata udhamini wa masomo (Scholarship) kwa muda wa mika miwili katika kuendeleza masomo yake na kama amemaliza kusoma basi atapa ajira kwenye hoteli ya kimataifa ya JB Belmonte kulingana na elimu aliyonayo. 

  Pia atapata shopping vocha kutoka Oriflame ya tshs. 300,000 pamoja na fedha taslimu tshs. 500,000. Mshindi wa pili;  atapata udhamini wa masomo (Scholarship) ya mwaka mmoja, fedha taslimu 300,000 na shopping vocha kutoka Oriflame ya tshs. 200,000.
  Mshindi wa tatu;  atapata udhamini wa masomo (Scholarship) ya mwaka mmoja, fedha taslimu 200,000 na shopping vocha kutoka Oriflame ya tshs. 100,000.
  Mshindi wa 4 na tano; watapata uthamini wa masomo ya kompyuta ya miezi sita. Mshindi wa nne atapata pia pesa taslimu laki mbili  na nusu na wa 5 laki moja na nusu.Washiriki wengine wote watapata kifuta jasho cha shilingi laki mbili kwa kila mmoja.

  Mashindano ya Redd's Miss Kinondoni 2013 yanatarajia kufanyika kwenye ukumbi wa hoteli ya Golden Tulip siku ya Ijumaa 21 June 2013. Viingilio katika onyesho hilo ni shs. 60,000 VIP, shs. 25,000 kwa tiketi za kawaida na meza ya watu ukitazama zawadi.

  Mashindano ya Redd's Miss Kinondoni yanatarajiwa kufanyika June 21, huku walowa yamedhaminiwa na Redd's Original, Chilly Willy Energy Drink, Oriflame Natural Beauty Products, Times Fm, JB Belmonte Hotel, Michuzi Media Group, Michuzijr Blog, Mtaa Kwa Mtaa Blog, Fullshangwe Blog, Mrokim Blog, SufianMafoto Blog, Global Publisher, Mdimuz Blog, Lukaza Blog, MO Blog, DjChoka Blog na Kajunason Blog.


   Muonekano wa warembo wa Redd's Miss Kinondoni 2013
   Kila mmoja akiwa na furaha na bashasha.
   Baada ya mkutano na waandishi wa habari warembo walipata nafasi ya kutembelea ofisi za wadhamini wao ambao ni Oriflame Natural Beauty Products zilizopo jengo la Mkapa jijini Dar es Salaam, na hapo waliweza kupata semina ya kuelezewa jinsi vipodozi vyao vinavyofanya kazi kama pichani unavyoona mwezeshaji akitoa somo kwa warembo.
   Mmoja ya warembo wa Redd's Miss Kinondoni 2013 akiuliza swali kwa mwezeshaji.
  Kila mrembo akijaribu kuweka kumbu kumbu kwa yale waliyokuwa wakifundishwa.

  0 0  0 0


  ZIFF today announced a list of all selected participants to the 3 main
  Workshops on film to be held during ZIFF 2013.

  We congratulate the selected participants and further information will
  be communicated to then in due time.


  Script Writing Workshop: (SPONSORED)

  1.      Philbert Aime Mbabazi – Rwanda

  2.      Jean Kwezi – Rwanda

  3.      Denis Kimathi – Kenya

  4.      Gabriel Kami – Tanzania

  5.      Christine Awor – Uganda

  (TO SELF SPONSOR)

  6.      Joan Kabugu – Kenya

  7.      Zaka Riwa – Tanzania

  8.      Haidary Yahaya – Tanzania/Zanzibar

  9.      Irene Sanga – Tanzania

  10.  Fadhili Mfate - Tanzania

  Film Production Workshop: (TO SELF SPONSOR)

  1.      John Kallage – Tanzania

  2.      Abdallah Mambia – Tanzania

  3.      Protas Pius Rubaba – Tanzania

  4.      Joseph Mpangala – Tanzania

  5.      Ally Othman – Tanzania/Zanzibar

  6.      Iddi Haji – Tanzania/Zanzibar

  7.      Yusuph Kisoki – Tanzania/Zanzibar

  The Assistant Director Workshop: (TANZANIANS-SELF SPONSOR)

  1.      Edwin Mallya

  2.      Amir Shivji

  3.      Nasser Mkugwa

  4.      Issa Mohamed

  5.      Biubwa Kombo

  6.      Elly Omukubi (Kenya)

  7.      Grace Cleti

  8.      Richard Magumba

  9.      Daniel Manege

  10.  Walter Elia

  0 0

  1

  Mkurugenzi wa shirika la hifadhi za Taifa (TANAPA),Ndu.Allan Kijazi akikagua gwaride la kikosi maalum cha kupambana na ujangili katika hifadhi za Taifa wakati wa ufungaji wa mafunzo hayo yaliyofanyika katika mbuga ya Ruaha kando kando ya Mto Ruaha, wakipewa mafunzo hayo na Wakufunzi,Martin Mthembu 
  kutoka taasisi ya African Field Ranger Training Services ya Afrika Kusini  na Genes Shayo ambaye ni mhifadhi Mkufunzi wa TANAPA

  Kikosi hicho Maalum cha TANAPA kilikuwa na askari wapatao 20 ambao walihitimu mafunzo hayo ya askari,lakini mmoja kati ya hao kwa bahati mbaya hakumaliza mafunzo kwa sababu za kiafya.Aidha kivutio kikubwa kilikuwa ni kwa askari Mwanamke pekee katika kikosi hicho,aitwaye Aikandaeli Lema ambaye aliweza kufanya mafunzo kwa kiwango cha juu bila kuwa na tofauti yoyote kiutendaji ya kijinsia,amemaliza mafunzo yote magumu na kulenga shabaha kwa kiwango cha juu kabisa,alimwelezea mkufunzi wa mafunzo hayo Martin Mthembu kutoka nchini Afrika Kusini na kummwagia sifa za pongezi nyingi kwa uwezo wake kama Mwanamke.
  3
  Mkurugenzi wa shirika la hifadhi za Taifa (TANAPA),Ndu.Allan Kijazi akirejea kwenye meza kuu mara baada ya kukagua gwaride hilo katika ufungaji wa mafunzo hayo yaliyofana kwa kiasi kikubwa.
  4
  Kikosi hicho kikitembea kwa ukakamavu kabisa kusonga mbele tayari kwa kutoa heshima zao kwa wageni rasmi.
  6
  Mkurugenzi wa shirika la hifadhi za Taifa (TANAPA),Ndu.Allan Kijazi  akipokea heshima kutoka kwa kikosi hicho wakati alipofunga mafunzo rasmi ya kukabiliana na ujangili katika hifadhi za Taifa,kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa bwa.Adam Swai na kushoto ni Mkurugenzi wa Uhifadhi wa TANAPA,Bwa.Martin Loiboki.
  10
  Mkurugenzi wa shirika la hifadhi za Taifa (TANAPA),Ndu.Allan Kijazi   akimkabidhi cheti cha kuhitimu mafunzo hayo ya Uaskari,Frank Anthon Malema,pichani kulai ni Mkurugenzi wa Uhifadhi TANAPA,Bwa.Martin Loiboki na kushoto ni Mkufunzi wa Mafunzo hayo na Mhifadhi wa TANAPA,Bwa.Genes Shayo.


   7Askari wahitimu wa kikosi hicho kushoto ni Frank Anthon Malema na Mwanamke pekee katika kikosi hicho Aikandaeli Lema wakisoma risala mbele ya mgeni rasmi wakati wa ufungaji wa mafunzo hayo 
  .

  8Wageni waalikwa mbalimbali wakiwa katika hafla ya ufungaji wa mafunzo hayo12Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la hifadhi za taifa TANAPA Ndugu Allan Kijazi akimpongeza John Kijazi baada ya kupokea cheti cha kuhitimu mafunzo hayo 13Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la hifadhi za taifa TANAPA Ndugu Allan Kijazi akizungumza na wahitimu wa mafunzo hayo.14Martin Mthembu Mkufunzi wa mafunzo hayo kutoka nchini Afrika Kusini akitoa maelezo kwa Allan Kijazi Mkurugenzi wa Shirika la hifadhi za taifa TANAPA wakati akikagua eneo maalum la kulenga shabaha katika ufungaji wa mafunzo hayo kulia ni Dr. Christopher Timbuka mhifadhi mkuu wa Ruaha Nation Park.15Askari maalum wa kikosi hicho cha kupambana na ujangili katika hifadhi za taifa wakionyesha moja ya kazi zao wakati wakitafuta majangili katika hifadhi hizo16Mmoja wa Askari wa kikosi hicho akilenga shabaha 17Mkufunzi wa Mafunzo hayo Martin Mthembu akielezea mafanikio ya kikosi hicho katika kulenga shabaha kwa mkurugenzi wa hifadhi za taifa TANAPA Ndugu Allan Kijazi wa pili kutoka kushoto wa pili kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Uhifadhi Martin Loiboki na wa kwanza kushoto ni Dr. Christopher Timbuka Mhifadhi Mkuu Ruaha Nation Park20Mkufunzi Martin Mthembu akielezea jinsi askari hao wanavyotakiwa kuwatafuta majangili huku wakiwa na maamuzi ya haraka bila kuchelewa na kutoua jangili ambaye hana madhara askari wa anatakiwa kufanya kazi yake kwa ufanisi lakini pia kulinda usalama wake yaani fanya kazi yako lakini rudi salama21Askari mwanamke pekee Aikande Lema akilenga shabaha huku mkufunzi huyo akiangalia22Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA Allan Kijazi naye akimshuhudia askari huyo23Askari Aikande Lema akirejea mara baada ya kumaliza kazi aliyotumwa na mwalimu wake kwa mafanikio katika kulenga shabaha. 

  0 0


  Airtel yawaomba Watanzania kuendelea kuwaokoa wawakilishi wa Tanzania BBA

  ·         Wateja wa Airtel Lipieni DSTV kwa Airtel Money mambo mazuri yaja

  Watanzani wametakiwa kuwapigia kura nyingi kadri wawezavyo,
  wawakilishi wao katika shindano la Big Brother Africa ‘The Chase’
  linaloendelea nchini Afrika Kusini ili kuhakikisha wanaendelea kubaki
  ‘mjengoni’ wakipeperusha bendera ya taifa.

  Wito huo, umetolewa na Meneja Uhusiano wa Kampuni ya simu ya Airtel
  Tanzania, inayodhamini shindano hilo,Jackson Mmbando, huku akiwataja
  wawakilishi hao wa Tanzania kuwa ni Feza Kessy  na Ammy Nando.

  Mmbando alisema kuwa, ili kuendelea kumbakisha Feza katika
  kinyang’anyiro cha BBA ‘The Chase,’ Watanzania wanapaswa kutuma ujumbe  wenye jina ‘FEZA’ kwenda namba 15456,  ili kumuokoa mshiriki huyo aliyeingia mara mbili kikaangoni, tofauti
  na Nando(22), ambaye anafanya vizuri.

  “Watanzania tuna kila sababu za kuwapigia kura wawakilishi wetu, ili
  waweze kuwakilisha vema na kipaumbele zaidi kiwe kwa kumpigia Feza kwa
  kuandika jina lake kwa herufi kubwa “FEZA” kisha kwenda kwa namba
  15456,” alisema Mmbando.

  Mshindi wa mwaka huu, atajinyakulia kitita cha Dola za 300,000 za
  Marekani.Tangu shindano hilo lianze ni Mtanzania Richard, ndiye pekee
  aliyewahi kushinda shindano hilo.

  Mashindanohayo yanayofanyika kwa mara ya nane, yanashirikisha
  washiriki 24 kutoka nchi 14za Afrika na watakaa ndani ya nyumba hiyo
  kwa siku 90, ambako kusalia kwao mjengoni kunategemea kura za
  watazamaji wa shindano hilo.

  Katikahatua nyingine, Mmbando aliwataka Watanzania kuendelea kulipia
  huduma zao zaDSTV kupitia Airtel money, kwani kuna kuna kitu cha ziada
  kinakuja kwa ajili yao.

  “Airtel ili kuleta burudani zaidi kwa wale wanaolipia huduma na
  vifurushi vya kila mwezi vya DSTV kupitia huduma ya Airtel Money kuna
  mambo mazuri yenye kuvutia yanakuja yatakayowafanya waendeleee
  kutosheka zaidi kupitia huduma zetu zote” alimaliza kwa kusema bw,
  Mmbando

  0 0


  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Moh’d
  Shein  amewataka wananchi wa  Mangapwani  kulinda, kuenzi na 
  kuendeleza  Utamaduni wa asili wa Zanzibar ili kuweka historia kwa 
  kizazi cha baadae.

   Dk. Shein  ameyasemahayo leo huko Mangapwani Mkoa wa Kaskazini Wilaya   
  ya kaskazini B Unguja, wakati alipokuwa  akizinduwa  Tamasha la Urithi  
  la  wana kijiji cha Mangapwani linalohamasisha kuinua hali za maisha 
  ya kijiji na kutunza historia ya kijiji hicho.

  Amesema historia ni kitu muhimu sana kwa mwanadamu kufahamu yale 
  yaliopita  ambayo yalikuwa muhimu na kutoa mchango mkubwa kwa wana
  kijiji hivyo kuitunza historia watu wa Mangapwani ni jambo muhimu kwao
  na Taifa kwani litapelekea kupata kipato kutokana na wageni (watalii )
  wanaoingia kijijini hapo .

  “Mambo ya asili yasitupwe yaendelezwe, leo vijana wanapoteza muelekreo
  kusahau ya zamamani walio kuwa wakiyafanya wazee  ambayo yaliwaongezea  
  afya kujenga miili yao kwa kula vya kula vya asili lakini leo chipsi  
  zimetawala na vijana kuwa na matatizo ya kiafya kwa kula mafuta kuzidi  
  kipimo.” alisema Dkt Ali Mohamed Shein.

  Aidha Dkt. Shein alisema njia nzuri ya kuutunza na kuendeleza
  utamaduni ni kutunga vitabu na kuviuza vitakavyoelezea Historia,
  Tamaduni na Silka za  kijiji hicho ili wakija wageni kutoka nchi
  mbalimbali wavikute na kujisomea.

  Aidha Rais wa Zanzibar na Mwenyeki wa Baraza la Mapindunzi Dkt Ali
  Muhamed Shein alisema kua matamasha kama hayo ni mazuri na ni muhimu
  sana  kufanyika katika maeneo ya historia kwani hueleza hali halisi ya
  sehemu kama hizo ambazo zilikaliwa na wakoloni kwa kufanya shughulizao
  mbalimbali kama vile ulinzi na usalama.

  “ Ngome sehemu ya Mangapwani ilitumika katika masuala kama vile ulinzi
  na usalama kwa kujenga ghala la silaha ili kujilinda na
  maaduwi”alisema Dkt Shein.

  Hata hivyo Dkt Shein alimpongeza Rais mstaafu  Mzee Ali Hsani Mwinyi
  kuwa mlenzi wa tamasha hilo na kusema kua anamshukuru kwa ujasiri wake  kukubali kuwa mstari wa mbele na kuona tamasha hilo linafanikiwa .  Akijibu risala ya wana kijiji wa hapo juu ya kupatiwa eneo la ujenzi
  wa chuo cha uvuvi na utengenezaji wa magari alisema jambo hilo ni zuri
  na atamuagiza Waziri wa Ardhi Ramadhali Abdalla Shabani kuangalia
  uwezekano wa kuwapatia wana kijijihicho eneo la kutimiza azma yao .

  Nae Rais Mstahafu Ali Hassani Mwinyi alisema kua kuna haja kurejesha
  hadhi ya Mangapwani  pamoja na mambo ya asili ambayo yamepotea kwa
  siku nyingi .   Amesema manga pani ya zamani siile yaleo ambayo vivutio vyake vina   potea jambaambalo kuna haja kubwa kutunzwa na wannchi kufaidika navyo.

  “Irudishwe hadhi ya mangapwani kwani  mcheza kwao hutuzwa,” alisema Mzee Ali.   
   Aidha alisema  kua tamasha hilo ni kutafuta nia ya kuwawezesha
  wanakijiji wa ukunda huo wa mangapwani na jirani zao kuwawezesha
  kiutalii na utamaduni pamoja na kuwakumbuka wasanii marufu wataarabu
  hapa Zanzibar.

  Nae mwenyekiti wa Tamasha hilo  Mwinyi Jamal Nasib akisoma Risala
  kwaiaba ya wanakijiji cha manga pwani kwenyetamasha hilo  alisema
  malengo makuu ya Tamasha ni kurejesha utamaduni ulio potea
  ,asilizawatu wa hapo,kutafuta dawa ya kujikwamua na umasikini,
  kuendeleza utalii na kujenga chuo cha kumuenzi Rais Mstaafu  Mzee Ali
  Hssan Mwinyi ambae ni mlenzi wa Chuo hicho.

  Ali Issa na Miza Othuman maelezo Zanzibar .     

  IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR

  0 0
 • 06/14/13--13:34: Mnuso wa iringa na bei yake

 • 0 0

   Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Mama Salma Kikwete akipokea tuzo ya Millenium Development Goals, Women Progress Awards 2013, kutoka kwa Ms Jennie Yeung , Rais wa Shirika la Sun Zhong Shan Foundation lililo chini ya United Nations Education, Science, Cultural and Health Advancement  Foundation la nchini Marekani.  Mama Salma alipokea tuzo hiyo baada ya kutimiza baadhi ya malengo ya Millenia katika masuala ya ukimwi, elimu kwa watoto waliokosa fursa  na kuwawezesha wanawake kiuchumi nchini Tanzania. Kulia ni Katibu wa WAMA, Ndugu Daud Nassib na kushoto ni Dr. Judy Kuriansky, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Columbia nchini Marekani.
   Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo Mama Salma Kikwete akimkabidhi tuzo hiyo Katibu wa WAMA Foundation , Ndugu Daud Nassib  wakati wa kupokea   tuzo hiyo huko New York nchini Marekani tarehe 13.6.2013.
   Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipongezwa na Dr. Judy Kuriansky, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Columbia mara tu baada ya kukabidhiwa tuzo yake.
   Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwahutubia  waalikwa waliohudhuria sherehe za utoaji tuzo kwa wake wa Marais wa Bara la afrika zilizofanyika huko New York nchini Marekani. Picha na John Lukuwi
  Mama Salma Kikwete akiongea baada ya kutunukiwa tuzo hiyo 
  ========  ========   ===========  ======
  Na Anna Nkinda – New York 
  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete ametunukiwa tuzo ya Malengo ya Maendeleo ya Milinia ya mwaka 2013 kwa wanawake na Shirika la Voices of African Mothers (VAM) la nchini Marekani kutokana na kazi kubwa anayoifanya ya kusaidia jamii wakiwemo wanawake na watoto. 

   Sherehe ya kukabidhi tuzo hizo zimefanyika jana katika ukumbi wa mikutano uliopo makao makuu ya Umoja wa Mataifa (UN) mjini New York. Mama Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) amekabidiwa tuzo hiyo kutokana na uongozi wake madhubuti, mafanikio na mchango wake na kujitoa kwake kuwasaidia wanawake na watoto wa Tanzania. 

   Akikabidhi tuzo hizo Nana – Fosu Randall ambaye ni Rais na mwanzilishi wa shirika hilo alisema kuwa tathimini ilitofanyika kwa mwaka 2012 juu ya Malengo ya Maendeleo ya Milenia wametambua kwamba malengo matatu yamefikiwa nchini Tanzania kabla ya muda uliowekwa wa kikomo wa mwaka 2015. Alisema kuwa wake wa Marais wa Afrika wanamajukumu mbalimbali katika nchi zao ili kufikia Malengo hayo, Taasisi ya VAM imekuwa ikifanya tathimini juu ya hatua zilizofikiwa na Taasisi za wake wa Marais kupitia taarifa za mwaka na zingine zinazowasilishwa.

   “Wanawake hawa wanastahili kutuzwa kwani wamefanya kazi kubwa pamoja na kufanya shughuli zao katika mazingira yenye changamoto nyingi ukilinganisha na wenzao katika nchi zingine. Hafla ya tuzo hizi siyo tu inasherehekea mafanikio ya wake wa marais wa Afrika bali pia inawahamasisha na kuwatia moyo wakati huu ambapo mwaka 2015 unakaribia”, alisema . 


   Alimalizia kwa kusema kuwa mara nyingi vyombo vya habari vimekuwa vikiandika habari zisizokuwa sahihi kutokana na kazi zinazofanywa na wake wa marais lakini vinasahau kuandika mambo mazuri na kazi kubwa wanayoifanya ya kuwasaidia wananchi na kuviomba vyombo hivyo kubadilika na kuthamini kazi kubwa wanayoifanya. 

   Akiongea mara baada ya kukabidhiwa tuzo hiyo Mama Kikwete alishukuru kwa tuzo aliyopewa na kusema kuwa Tanzania ni moja ya nchi ambazo zimepiga hatua kubwa sana katika kufikia malengo ya milinia kwani vifo vya watoto vimepungua kwa asilimia 45 na 49 kwa watoto wachanga. 

   Alisema kuwa haya ni mafanikio makubwa sana japokuwa lengo ni kuondoa kabisa vifo ambavyo vinatokana na sababu ambazo zinazuilika na katika malengo mengine maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (VVU) yanaendelea kupungua kutoka asilimia 5.7 kwa mwaka 2004 hadi asilimia 5.1 kwa mwaka 2011. Mama Kikwete alisema;

   “Elimu ya msingi inatolewa bure kwa watoto wote walio na umri unaostahili na hatua kubwa imepigwa katika kupunguza ugonjwa wa maralia na vifo vya akina mama vinavyotokana na tatizo la uzazi” Kwa upande wa harakati za kumkomboa mtoto wa kike alisema kuwa ni lazima ziendelee na zizingatie changamoto mpya za mazingira mapya kwani unapompatia elimu unampunguzia changamoto za ujinsia na kumpatia huduma ya afya ikiwemo uzazi wa mpango, unamuwezesha kushiriki zaidi shughuli za maendeleo ya kiuchumi, unasaidia familia yake na jamii kuweza kuendelea. 

   Kwa upande wake Dk. Judy Kuriansky ambaye ni mwakilishi wa Asasi zisizo za Kiserikali zilizo chini ya UN alisema kuwa wake wa marais wanafanya kazi kubwa ya kuisaidia jamii hivyo basi ni jukumu la kila mmoja kuwaunga mkono na kushirikiana kwa pamoja ili kuweza kutimiza malengo ya maendeleo ya milinia. Dk. Kuriansky alisema kuwa ili kufikia malengo ya milinia inatakiwa kuimarisha miundombinu iliyopo jambo ambalo litasababisha kuifikia jamii kwa ukaribu zaidi na kuweza kutatua changamoto zinazowakabili. 

   Tuzo hizo zimetolewa kwa mara ya kwanza na shirika hilo kwa kushirikiana na Taasisi ya The reed for Hope (RFHF) na Bethesda Counsel kwa wake wa marais wa Afrika akiwemo Mke wa Rais wa Burundi Mama Dk. Denice Nkurunziza, Mke wa Rais wa Equatorial Guinea Mama Constancia Mangue de Obiang na Mke wa Rais wa Mali Mama Mintou Doucoure Epse Traore.

  0 0

  image
  Kufuatia kifo cha ndugu yetu, JEROME MPEFO, kilichotokea juzi tarehe 12, June,2013-,Houston, Texas, mipango ya kusafirisha mwili wa marehemu kwenda nyumbani Tanzania kwa mizishi inafanyika.

  Tunawaomba ndugu,jamaa, marafiki, watanzania na yeyote aliyeguswa na msiba huu kusaidia kwa michango ya hali na mali ili tuweze kufanikisha kuupeleka mwili wa marehemu nyumbani.

  Kwa wale ambao hawawezi kuleta michango katika pesa taslimu, tunapokea michango kupitia;

  Name of The Bank : Bank Of America
  Account Number: 586033522448
  Routing Number: 113000023
  Name On The Account: STELLA LIMING

  Pia tutakuwa na fundraising siku ya Jumamosi (tarehe 15, June,2013) kuanzia Saa 10 Jioni. Anuani ya mahali Fundraising itakapofanyika ni
  5800, Westheimer Road,
  Houston, Texas, 77057

  Misa ya kumuaga ndugu yetu JEROME MPEFO, itafanyika siku ya Jumanne wiki ijayo. Tutawataarifu juu ya muda na mahali.
  Kwa upande wa nyumbani Tanzania, wasiliana na wafuatao kuhusu msiba na maelekezo yoyote ya jinsi ya kufika nyumbani kwa wafiwa;
  GRACE MPEFO: +255 717 400808
  RAYMOND: +255 714 644964
  Asanteni sana. Bwana Alitoa na Bwana Ametwaa. Jina lake lihimidiwe.Amen.

  0 0

  President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete meets and hold talks with Sir. Richard Branson in London this evening . Sir.Richard is a British business magnate best known as the founder and chairman of Virgin Group of more than 400 companies. President Kikwete is in London UK for a three days working visit in which, among other things, he will attend the G8 summit.
  President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete and his delegation in conversation with The Chairman of Virgin Group of Companies Sir. Richard Branson in London this evening. Others in the picture are from left are Minister for Transport Dr. Harrison Mwakyembe, Tanzania Tourist Board Managing Director Dr.Aloyce Nzuki, President’s advisor Economic Affairs Dr.Hamis Mwinyimvua and Tanzanian High Commissioner to the United Kingdom Peter Kallaghe. (photos by Freddy Maro)

  0 0


  Mshindi wa Redds Miss Iringa,Neema Mality akiwapungia mkono washabiki mbalimbali wa onesho hilo waliofika ukumbini humo hapa jana kwenye ukumbi wa Highland hall.
  kutoka kulia ni mshindi no 2 Lucy  George, kushoto ni mshindi no 3 Lilian Samson na katikati ni kinara wa Redds Miss Iringa 2013,Neema Mality akitoa tabasamu la nguvu.
  Pichani ni washiriki wa Redds Miss Iringa waliongia tano bora safi kabisa.Picha zote kwa hisani ya Francis Godwin wa mtandao wa MatukioDaima-Iringa.

  0 0
 • 06/14/13--21:20: Article 1


older | 1 | .... | 100 | 101 | (Page 102) | 103 | 104 | .... | 1897 | newer