WANANCHI wa halmashauri ya Mufindi wameombwa kuhamasika kununua hisa zaidi katika benki ya wananchi Mufindi (MuCoBa) ili kuiwezesha benki kufungua matawi katika mikoa mingine.
Akizungumza katika uzinduzi wa huduma ya fedha kwa mashine maalum(ATM) Mkurugenzi Mtendaji wa umoja swich Daniford Milinyi amesema kuwa ili kuiendeleza benki ya mufindi wanahitaji kuwahamasisha wananchi wanunue hisa katika benki hii.
Mbilinyi alisema kuwa Mtandao huu wa umoja haushindani na benki ila unaunganisha benki lengo ni kuwa na mtandao mmoja wa mabenki nchi nzima ili kurahisisha gharama.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya mufindi Evarista Kalulu ambaye pia alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo amesema kuwa huduma za kifedha hasa vijijini pia imekuwa ni changamoto kutokana na uelewa mdogo wa mambo ya kifedha ,miundombinu duni na uwezo mdogo wa benki zinazowasaidia katika vijiji kukosa mtaji.
Kalulu alisema kuwa Napenda kuchukua nafasi hii kuwahamasisha wananchi wote kununua hisa katika benki yetu ili kuongeza mtaji na hivyo kuiwezesha benki kutanua huduma zake zaidi na wadau kusiriki kuongeza huduma za kifedha vijijini na kuboresha miundombinu mbalimbal ili kuongeza idadi a wananchi watakao pata huduma kamili za kifedha
Naye Meneja mkuu wa benki ya MuCoBa Danny Mpogole amesema kuwa lengo kuu la kuanzisha mfumo huu wa kifedha kwa kushirikiana na wa mabenki nchini na kuwawezesha wateja wa MuCoBa kupata huduma za kifedha katika maeneo mengine nje ya mafinga bila usumbufu kwa kutumia kadi ya umoja swich.
Sambamba na hayo Amezitaja sababu zingine ni pamoja ni kutanua wigo wa huduma za kifedha katika nchi yetu,pia mteja wa MuCoBa mwenyekadi ya ATM aatapata kuduma za kifedha kwa kutumia simu ya mkononi.
Pia amebainisha kuwa ATM imekubwa na changamoto ya wizi wa fedha ,hasa kutokana na kukua kwa teknolojia Tunapenda kukuhakikishia kuwa benki tayari imeshaweka tahadhari mbalimbali katika kupambana na changamoto hii” alisema Mpogole