Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1023 | 1024 | (Page 1025) | 1026 | 1027 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Gombe Bw. Donatus Bayona (kulia) na Bi.Happy Kiyemi Mkuu wa Idara ya Utalii wakimuongoza Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. January Makamba kutembelea Hifadhi ya Gombe .

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. January Makamba akizungumza na Uongozi wa Shirika lilisilo la Kiserikali la Jane Goodall, mara baada ya Mhe. Waziri Makamba kutembelea Ofisi zao Kigoma Mjini. Wa kwanza kulia ni Bi. Mary Mavanza Naibu Mkurugenzi wa Mradi wa kuhifadhi mfumo wa Ikolojia Ukanda wa Magharibi mwa Tanzania. Kushoto ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Bw. Samson Anga
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. January Makamba akiwa katika boti Maalumu kuelekea Hifadhi ya Taifa ya Gombe
  ………………………………………………………

  Na Lulu Mussa- Kigoma

  Shirika lisilo la Kiserikali la Jane Goodall linalojishughulisha na Mradi wa utafiti wa sokwe na wanyamapori wengine limepongezwa kwa jitihada zake za kutunza mazingira na kusaidia jamii kuhifadhi mfumo wa ikolojia ukanda wa Magharibi mwa Tanzania.

  Pongezi hizo zimetolewa leo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. January Makamba mara baada ya kutembele Ofisi zao Mkoani Kigoma. Waziri Makamba amesema kuwa Shirikal hilo la Jane Goodall limekuwa mstari wa mbele katika kubuni miradi ambayo inagusa jamii moja kwa moja.

  Akitoa maelezo ya shughuli zinazotekelezwa na shirika hilo kwasasa, Naibu Mkurugenzi wa Bi. Mary Mavanza amesema kuwa wanatekeleza miradi mitatu ikiwa ni pamoja na Mradi wa utafiti wa sokwe na wanyamapori, Mradi wa Mizizi na chipukizi ambao unatekelezwa nchi nzima katika shule zote na mradi wa uhifadhi unatekelezwa katika Halmashauri za Wilaya za Mpanda, Nsimbo kwa Mkoa wa Katavi na Uvinza kwa Mkoa wa Kigoma.

  Aidha, Shirika hili pia limefanikiwa kuhamasisha wanajamii 42 kufanya shughuli za kukuza kipato ambazo ni rafiki kwa mazingira kupitia ufugaji nyuki na huduma za ki ikolojia. Pamoja na mafanikio hayo shirikali hili limewasilisha hoja ya kwa Waziri Makamba kusaidia kukamilika kwa Mchakato wa kupandisha hadhi ya ardhi jumla kuwa misitu ya Hifadhi ya Wilaya ili kudhibiti idadi kubwa ya sokwe waliobaki Tanzania ambao kwa sasa hawana ulinzi thabiti.

  Taasisi ya Jane Goodall liliasisiwa miaka 56 iliyopita na mtafifiti Dr. Jane Goodall kwa lengo la kufanya shughuli za kitafiti, kurejesha uoto wa asili uliopotea na kuhakikisha wanajamii wanaboresha uchumi wao kwa kutumia maliasili zinazowazunguka.

  Waziri Makamba pia ametembelea Hifadhi ya Taifa ya Gombe kwa lengo la kufuatilia changamoto za kimazingira Hifadhini hapo.

  0 0

  Wachezaji wa Timu ya Azam Fc wakiwa uwanjani Kaitaba hii leo jioni wakijifua, Tayari kwa mchezo wao na Wenyeji wao Kagera Sugar.
  Kipa wa Timu ya Azam FC "Wanalambalamba", Aeshi Manula akiwa na Mwalimu wake.  Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) msimu 2016/17, raundi ya 12 inaendelea keshokwa michezo sita ambako mabingwa watetezi Young Africans ya Dar es Salaam itakuwa mgeni wa Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Kaitaba ulioko Bukoba mkoani Kagera.
  Jijini Dar es Salaam, katika Uwanja wa Uhuru African Lyon itakuwa mwenyeji wa Mbeya City ya Mbeya ilihali Mwadui ya Shinyanga itasafiri hadi Mtwara kucheza na Ndanda Fc kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona wakati Stand United itakuwa mgeni wa Mtibwa Sugar ya Morogoro kwenye mchezo utaofanyika Uwanja wa Manungu, ulioko Turiani – Mvomero.
  Majimaji itakuwa mwenyeji wa Ruvu Shooting ya Pwani kwenye Uwanja wa Majimaji huko Songea. Michezo yote mitano hapo juu itaanza saa 10.00 jioni kwa saa za Afrika Mashariki lakini mchezo kati ya Azam FC na JKT Ruvu itaanza saa 1.00 usiku kwenye Uwanja wa Azam huko Chamazi-Mbagala Dar es Salaam.

  BEKI mahiri wa kulia wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, Shomari Kapombe Baada ya kukosa mechi kama sita alionekana kama bado anaugulia jeraha lililomfanya afanye mazoezi mepesi na akiwa peke yake katika Uwanja wa Kaitaba leo. Jumapili itakuwa ni zamu ya kinara wa ligi hiyo, Simba ambayo itaikaribisha Toto Africans ya Mwanza kwenye Uwanja wa Uhuru wakati Tanzania Prisons itapambana na Mbao FC kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.

  Michezo yote ya Dar es Salaam, mfumo wa kuingia utabaki kuwa ni uleule wa kutumia kadi za Selcom kununua tiketi za kielekroniki. Viingilio kwenye mechi za Uwanja wa Uhuru ni Sh 30,000 kwa Jukwaa Kuu (VIP-A), VIP-B na C Sh 20,000 na mzunguko ni Sh 5,000 wakati Kiingilio Uwanja wa Azam ni Sh 10,000 kwa VIP na Mzunguko ni Sh 3,000.  Kipa wa Azam Fc

  Mashabiki jukwaa kuu wakiwachabo Wachezaji wa Azam Fc kwenye Uwanja wa Kaitaba hii leo

  Wakimsikiliza kwa Makini Kocha wao  Shabiki mkubwa na Mpenzi wa Timu ya Azam Fc Ally Kulialia nae alikuwepo Uwanjani hapo  Mwalimu wa Makipa(kulia) wa Azam Fc  Kipa wa Timu ya Azam FC "Wanalambalamba", Aeshi Manula

  0 0

  Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. Luhaga Mpina (katikati) alipofanya ziara ya kukagua mazingira katika kiwanda cha kutengeneza viroba vya mifuko Unberg International kilichopo jijini Dar es salaam.
  Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. Luhaga Mpina (kushoto) mara baada ya kuwasili na kutembelea kiwanda cha kutengeneza sabuni ya unga cha Murzer kilichopo jijini Dar e s salaam.
  Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. Luhaga Mpina akikagua sehemu ya kuyeyushia viroba ya mifuko katika kiwanda cha Unberg International kilichopo jijini Dar es salaam mapema hii leo.

  ………………………………………………………………………

  EVELYN MKOKOI-DAR ES SALAAM

  Shule ya sekondari ya Almuntazir iliyopo upanga jijini Dae es salaam imetozwa faini ya shilingi milioni ishirini na tano kwa kosa la uchafuzi wa mazingira kwa kutirirsha maji taka ya chooni katika mto msimbazi ndani eneo la mikoko katika eneo la daraja la salenda na kujenga uzio wa ukuta bila kuzingatia mita sitini zinazotakiwa kisheria.

  Faini hiyo inatakiwa kulipwa ndani ya wiki moja imetokana na ziara ya Naibu waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina iliyofuatia malalamiko ya wakazi wa Upanga iliyompelekea Naibu Waziri kufanya ziara yakwenda kujionea uchafuzi huo.

  Akiongea kwa Niaba ya shule meneja wa shule hiyo Bw. Serialis Rwechungura amesema kuwa, watalipa faini hiyo kama ilivyoelekezwa na serikali na hakuwa tayari kuongelea swala la ukuta wa shule hiyo.

  Naibu Waziri Mpina amesisitiza kuwa serikali haitakuwa tayari kuwavumila wawekeajia wakiukaji wa sheria hasa ya mazingira, na kuweka rehani maisha ya watanzania.

  Aidha Naibu Waziri alitembelea maeneo ya mwenge kijijini na kuonea uchafu wa mazingira uliotokana na kuvuja kwa maji taka ya choo kutoka kwenye miundombinu ya majitaka ya DAWASCO hali inayosababibsha wakazi na wafanyabiashara wa maeneo ya mwenge kushindwa kustahimili hali hiyo na kuwa hatarini kupata magonjwa ya maambukizi kama kipindupindu na homa ya matumbo.

  Akiikemea DAWASCO kwa mara nyingine kwa kutokuonyesha uwajibikaji na utii kwa mamlaka za juu, Naibu Waziri Mpina ameita NEMC kuiandikia DAWASCO faini ya shilingi milioni ishirini na tano kwa kutelekeza miundombinu yao na kutakiwa kulipa adhabu hiyo kwa muda wa wiki mbili.

  0 0   Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Mashaka Gambo akimkabdihi Mkuu wa Shule ya Sekondari  Engaranaibo  Mwl. Petro Sabatho Tsh 500,000 kwa ajili ya  kuchangia ujenzi wa bweni la wasichana katika Shule hiyo wakati wa ziara yake inayoendelea katika Wilaya ya Longido.
    Viogozi wa Chama na Serikali Mkoa wa Arusha pamoja na wananchi wa kijiji cha Olgira Kata ya Mundarara wakielekea kwenye eneo la ujenzi wa daraja ambalo linajengwa kwa nguvu za wananchi.
     Hili ndilo daraja ambalo wananchi wa Kata ya Mundarara wamejitolea fedha na nguvu zao kuhakikisha ujenzi wa daraja unakamilika na kufanya barabara zinazounganisha vijiji vyao kupitika kipindi chote cha mwaka.
   Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo (aliyeko kwenye mtaro) akishiriki ujenzi wa daraja la chini linalojengwa na wananchi wa Mundarara.
   Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo (katikati) akihamasisha wananchi waendelee kuchangia ujenzi wa daraja la Mundarara ili liweze kukamilika kwa wakati.
   Wanawake wa Jamii ya Kimaasai maarufu kama Siangiki walijitokeza barabarani kumlaki Mkuu wa Mkoa wa Arusha wakati wa ziara yake wilayani Longido.
  1Mabinti wa jamii ya kimaasai maarufu kama Selengeni pia walishirki mapokezi ya Mkuu wa Mkoa wakati wa ziara ya kazi wilayani Longido.  Nteghenjwa Hosseah - Longido Wananchi wa Kijiji cha Orgirah Kilichopo Kata ya Mundarara Tarafa ya Engarenaibor Wilayani Longido wamelazimika kutumia nguvu zao binafsi kujenga daraja la chini kwa ajili lengo la kuunganisha mawasiliano ya barabara kati ya kata hiyo na kata ya Gelai.

  Aidha wamelalamikia kero ya maji tangu mwaka 2013 hadi leo hii hakuna maji yanayotoka kwenye mradi mkubwa wa maji unaofadhiliwa na Benki ya Dunia (WB) unaolenga kusaidia vijiji vitano kwenye kata hiyo.

  Wakiongea na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo ambaye anaendelea na ziara yake kwenye wilaya hiyo jana, Afisa Mtendaji wa kijiji cha Orgirah, Mathayo Laizer alisema mradi huo wa daraja ni muhimu kwao kwani unafungua fursa za kimaendeleo katika kata mbili za Mundarara na Gelai.

  Alisema mradi ulianza mwaka jana na walipata michango mbalimbali kutoka Ofisi ya Mkuu wa Wilaya hiyo ambayo ilitoa Sh. 400,000, Ofisi ya Mkurugenzi Sh, 640,000 na wananchi walichanga Sh, milioni 5.3 lakini ili waweze kukamilisha ujenzi wa daraja hilo wanahitaji mifuko ya saruji 135 pamoja na ndono za kuweka kingo pembeni ya daraja hilo zenye thamani ya Sh milioni 2.9

  Naye Esther Mathayo alimuomba Rc, Gambo kuwasaidia kutatua kero ya maji katika kata hiyo ambayo ipo kwenye mradi wa benki ya Dunia tangu mwaka 2013 lakini hadi leo wananchi wanatembea umbali mrefu kutafuta maji hayo kwaajili ya matumizi mbalimbali.

  Alisema awali mradi huo uliofadhiliwa na benki ya dunia ulilenga kusaidia vijiji vitano na ulijengwa katika kata hiyo zaidi ya miaka minne iliyopita lakini cha ajabu kwenye chanzo cha maji hakukuguswa na baadhi ya miundombinu imeharibika iliyokwisha wekwa awali sehemu mbalimbali na hawajui ni kwanini umekwama.

  Baada ya wananchi kutoa kero zao, Rc Gambo aliwapongeza wananchi hao kwa ujenzi wa daraja hilo la chini kwa kutumia nguvu zao wenyewe kwa kuleta maendeleo ikiwemo kufungua njia za mawasiliano kati ya sehemu moja na nyingine.

  "Nawapongeza kwa kazi hii mliyojitolea kwaajili ya kutatua changamoto ya usafiri lakini pia natoa rai kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Longido, Juma Mhina kuhakikisha wanatafuta ufumbuzi wa mradi huu wa maji kama ni fedha watenge kwenye bajeti ya halmashauri hiyo ili wananchi wanywe maji "

  Pia aliweza kuchangia mifuko ya saruji 30, pamoja na kufanya harambee na kuchangisha zaidi ya Sh, milioni 1 kutoka kwa watumishi wa sekta mbalimbali alioambatana nao ili daraja hilo liweze kukamilika,awali Gambo kwa kushirikiana na Mkuu wa wilaya hiyo, Daniel Chongolo waliingia ndani ya kingo za daraja hilo kwaajili ya kusaidiana na wananchi kuweka mawe kwenye msingi wa daraja pamoja na wananchi wa kijiji hicho.

  0 0

   Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt.Hamisi Kigwangwalla akiongea na wajumbe pamoja na watumishi wa hospitali ya Wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro  wakati wa  uzinduzi wa bodi ya hospitali hiyo inayotoa huduma ya kifua kikuu sugu
   Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt.Hamisi Kigwangwalla akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa  bodi ya hospital ya Wilaya ya Siha inayotoa huduma ya kifua kikiu sugu

  Baadhi ya wajumbe wa bodi hiyo mpya(wanne mbele) wakimsikiliza mgeni rasmi,wa kwanza  kushoto ni Dkt.Sayoki Mfinganga,Dkt.Said Egwaga(Mwenyekiti wa bodi),Dkt.Janeth Mghamba na Justice Mkita ambaye bi mwakilishi toka jamii inayotumia huduma za hospitali hiyo. 

  0 0

  Naibu Waziri Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia James Wambura (kushoto) akizungumza na Wadau wa Lugha ya Kiswahili (hawapo pichani) wakati wa kikao na wadau hao kujadili changamoto zinazokabili Tasnia ya Lugha nchini na kuzipatia ufumbuzi leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Lugha Hajjat Shani Kitogo
  Mkurugenzi Msaidizi Lugha Hajjat Shani Kitogo akifafanua jambo wakati wa kikao na wadau wa Lugha ya Kiswahili kujadili changamoto zinazokabili Tasnia ya Lugha nchini na kuzipatia ufumbuzi leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Naibu Waziri Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia James Wambura
  Mwandishi wa Vitabu vya Riwaya Bw. Adam Shafi (aliyesimama) akichangia mada wakati wa kikao na wadau wa Lugha ya Kiswahili kujadili changamoto zinazokabili Tasnia ya Lugha nchini na kuzipatia ufumbuzi leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mmiliki wa kampuni ya machapisho ya Mkuki na Nyota Bw. Walter Bgoya
  Wadau mbalimbali wa Lugha ya Kiswahili wakijadiliana wakati wa kikao na Naibu Waziri Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia James Wambura (kushoto) kujadili changamoto zinazokabili Tasnia ya Lugha nchini na kuzipatia ufumbuzi leo Jijini Dar es Salaam.
  Mshairi mama Mipango akiimba shairi la kuipongeza Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa kusimamia vizuri Lugha ya Kiswahili katika kuikuza na kuieneza wakati wa kikao na wadau wa Lugha ya Kiswahili kujadili changamoto zinazokabili Tasnia

  Naibu Waziri Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia James Wambura (katikati waliokaa) katika picha ya pamoja na Wadau wa Lugha ya Kiswahili wakati wa kikao na wadau hao kujadili changamoto zinazokabili Tasnia ya Lugha nchini na kuzipatia ufumbuzi leo Jijini Dar es Salaam. Kulia waliokaa ni Mkurugenzi Msaidizi Lugha Hajjat Shani Kitogo na kushoto waliokaa ni Mjumbe kutoka Idara ya Lugha na Fasihi Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) Bibi. Gertrude Joseph.

  Picha na: Genofeva Matemu – WHUSM

  ……………………………………………….

  Na: Genofeva Matemu – WHUSM

  Wadau wa Lugha ya Kiswahili nchini wamepongezwa kwa kazi kubwa na nzuri wanazozifanya za kukuza, kueneza, kuimarisha na kuendeleza lugha ya Kiswahili kwani wamekifanya Kiswahili kuwa lugha yenye mawasiliano mapana katika nchi za Afrika Mashariki, Afrika na Dunia nzima.

  Hayo yamesema na Naibu Waziri Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia James Wambura wakati wa kikao na wadau hao kujadili changamoto zinazokabili Tasnia ya Lugha nchini na kuzipatia ufumbuzi leo Jijini Dar es Salaa.

  “Vyama mbalimbali vya kukuza na kueneza Lugha ya Kiswahili nchini kwa kushirikiana na wadau mbalimbali mmekua kichocheo kikubwa cha kuendeleza lugha ya Kiswahili na kuisambaza kwa kasi hata kuweza kuvuka mipaka ya Tanzania” amesema Mhe. Anastazia.

  Mhe. Anastazia amewataka wadau wa Lugha ya Kiswahili kushiriki vema katika mijadala itakayokua inaandaliwa ya lugha hiyo ili waweze kutoa maoni na mapendelkezo fahafu yenye lengo la kuimarisha ushirikiano kati ya Serikali, Taasisi, Asasi na vyama mbalimbali vya wadau wa lugha ya Kiswahili nchini.

  Kwa upande wake Mkuregenzi kutoka Chama cha Kiswahili na Sanaa (KINASA) Bw. Mutalemwa Jason ameiomba serikali kuhakikisha kuwa utamaduni wa Vilabu vya Kiswahili kwa shule za msingi na sekondari unarejeshwa ili kutoa fursa nzuri kwa wanafunzi kukutana na kujadili misamihati mbalimbali ya Kiswahili.

  Naye Naibu Katibu Mkuu kutoka Umoja wa Washairi Tanzania (UWASHATA) ameviomba vyombo vya habari nchini kusaidia kurusha mashairi yanaimbwa na wadau wa lugha ya Kiswahili kwani kwa kufanya hivyo watawezesha misamihati ya lugha ya Kiswahili kuenea kwa kasi ndani na nje ya nchi.

  Tangu tulipopata uhuru mwaka 1961 masuala yahusuyo Lugha katika nchi yetu yamezingatiwa kama kipengele muhimu katika Sera ya Utamaduni ya mwaka 1997, Serikali ya awamu ya tano imezingatia umuhimu mkubwa wa kuwa na Sera ya Taifa ya Lugha ambayo ni muongozo dhabiti inayosimamia masuala yote yanayohusu Lugha nchini ambapo kwa sasa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo inaendelea na mchakato wa uandaaji wa rasimu ya Sera ya Taifa ya Lugha katika hatua ya ukusanyaji wa maoni ya wadau wa Lugha hiyo.

  0 0

  Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mst. Damian Lubuva (kushoto) akimkabidhi Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu Mhe. Jenista Mhagama, Taarifa ya Tathmini Baada ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani wa Mwaka 2015 kwenye ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Bungeni mjini Dodoma leo.
  Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Mst. Damian Lubuva (kushoto) na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu Mhe. Jenista Mhagama, wakionesha Taarifa ya Tathmini Baada ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani wa Mwaka 2015 ambayo ilikabidhiwa kwa Mhe. Waziri na NEC kwenye ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Bungeni mjini Dodoma leo.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu Mhe. Jenista Mhagama akihutubia kwenye mkutano wa kukabidhiwa Taarifa ya Tathmini Baada ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani wa Mwaka 2015, kwenye ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Bungeni mjini Dodoma leo.Kushoto ni Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Mst. Damian Lubuva na Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa NEC Jaji Mst. wa Zanzibar Hamid Mahmoud Hamid..
  Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Mst. Damian Lubuva akitoa maelezo kuhusu Taarifa ya Tathmini Baada ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani wa Mwaka 2015 ambayo aliikabidhi kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu Mhe. Jenista Mhagama kwenye ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Bungeni mjini Dodoma leo.
  Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Bw. Kailima Ramadhani akitoa maelezo ya Utangulizi kuhusu Taarifa ya Tathmini Baada ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani wa Mwaka 2015, ambayo Tume iliikabidhi kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu Mhe. Jenista Mhagama (kushoto) kwenye ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Bungeni mjini Dodoma leo.Katikati ni Makamu Mwenyekiti wa NEC Jaji Mst. wa Zanzibar Hamid Mahmoud Hamid.
  Baadhi ya washiriki wa mkutano wa makabidhiano ya Taarifa ya Tathmini Baada ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani wa Mwaka 2015 wakifuatilia hotuba ya Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mst. Damian Lubuva (aliyesimama mbele).Taarifa hiyo ilikabidhiwa kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu Mhe. Jenista Mhagama, kwenye ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Bungeni mjini Dodoma leo.

  Picha zote na Hussein Makame-NEC, Dodoma

  …………………………………………………………………….

  Christina Njovu-NEC, Dodoma

  Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imekabidhi Taarifa ya Tathmini baada ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani wa mwaka 2015 kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu , Sera, Bunge, Kazi , Ajira, Vijana na Walemavu Mh. Jenista Mhagama mjini Dodoma leo.

  Akikabidhi taarifa hiyo Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damin Lubuva alisema kuwa Tathmini hiyo imeonesha kuwa Tume hiyo imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuendesha na kusimamia uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani uliofanyika Oktoba 25 mwaka 2015.

  Alisema kwa mujibu wa tathmni hiyo Tume imebaini kuwa sheria, kanuni na zilizotumika wakati wa Uchaguzi mkuu zilikuwa chachu ya kufanikisha Uchaguzi Mkuu, Watendaji wa Uchaguzi walionesha kuwa na uelewa wa kutosha wa Shriea na Kanuni za Uchaguzi.

  Jaji Mst. Lubvuva alisema kuwa lengo la tathmini hiyo ni kupata taswira halisi ya Tume kutoka kwa Wadau kwa lengo la kujenga msingi bora wa utekelezaji wa chaguzi zijazo na kujua kwa nini baadhi ya maeneo yalikuwa na mwitikio mdogo katika kupiga kura wakati yalikuwa na mwitikio mkubwa kwenye kuandikisha wapiga kura kwenye Daftari la kudumu la Wapiga Kura.

  Alisema kuwa Tathmini hiyo ni ya kwanza kufanyika tangu kuanzishwa kwa Tume hiyo mwaka 1993 ambayo imeweza kuwapatia mrejesho juu ya utekelezaji wa Uchaguzi Mkuu kutoka kwa wadau wa Uchaguzi .

  Alibainisha kuwa wakati wa tathmini hiyo wadau wengi walionesha kuridhishwa na utendaji wa Tume katika kusimamia Uchaguzi Mkuu na kutangaza matokeo kwa kufuata sheria na kanuni zilizopo.

  Akipokea Taarifa hiyo , Waziri wa Nchi Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu Mhe. Jenista Mhagama ameipongeza Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa kuweza kufanikisha Uchaguzi Mkuu ulikuwa na changamoto nyingi na ushindani mkubwa wa kisiasa na kufanikiwa kufanya tathmini ya Uchaguzi Mkuu ambayo imekabidhia kwake kwa niaba ya Serikali.

  “Ni kweli kwamba wananchi wengi wamekuwa na mwamko wa kisiasa katika jamii yetu, hasa vijana , hivyo taarifa hii itasaidia sana wananchi kuifahamu vyema zaidi namna Tume inavyosimamia , kuendesha na kuratibu mchakato mzima wa Uchaguzi kuanzia uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura, hadi kutangaza matokeo.” Alisema Waziri Mhagama.

  Alisema Tathmini hii itawawezesha wadau mbalimbali kuitumia kama nyenzo muhimu katika kushiriki na kufanya maandalizi ya chaguzi zijazo.

  Naye Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC, Bw. Ramadhan Kailima katika maelezo ya utangulizi alieleza kuwa tathimini hiyo ilitumia njia ya mahojiano ya ana kwa ana na majadiliano na ilijumuisha makundi 192 ya wazee wenye umri wa zaidi ya miaka 60 na makundi 192 ya vijana wenye umri kati ya miaka 18 na 35.

  Alisema matokeo ya tathmini hiyo yanaonesha kuwa kati ya watendaji 1,029 walihojiwa na watendaji wengi kati wao walisema taratibu mbalimbali za uchaguzi hadi kutangaza matokeo zilizingatiwa.

  Bw. Kailima aliongeza kuwa kuhusu Elimu ya Mpiga Kura wadau wa Uchaguzi 1,915 waliohojiwa kuhusu uelewa wao juu ya Elimu ya Mpiga Kura kati yao Wadau 1,463 sawa na asilimia 76.4 walisema kuwa walikuwa na uelewa wa Elimu ya Mpiga Kura na Watu 452 sawa na asilimia 23.6 hawakuwa na uelewa.

  Kutokana na tathmini hiyo Bw. Kailima alisema kuwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi imejipanga kutoa Elimu ya MpigaKura kwa lengo la kuwafikia wananchi na wadau moja kwa moja na imeweza kushiriki katika maonyesho mbalimbali yakiwemo ya Sabasaba, Nanenane , Mkutano wa Tawala za Mitaa Tanzania na Wiki ya Vijana iliyofanyika Mkoani Simiyu.

  Sambamba na hilo, aliongeza kuwa Tume imepanga kuhudhuria na kutoa Elimu katika mikutano ya viongozi mbalimbali ikwemo viongozi wa Dini, Mabaraza ya Madiwani na mikutano mikuu ya vijiji na mitaa.

  Kutoa elimu ya Mpiga Kura kwa njia ya luninga, redio, mabango na mitandao ya kijamii, Kutoa vibali vya kutoa elimu ya Mpiga kura kwa Taasisi na Asasi.

  Kufanyika kwa tathmini Baada ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani wa mwaka 2015 ni mojawapo ya ukamilishaji wa mzunguko wa Uchaguzi huo ambao ulitanguliwa na zoezi kukabidhi ripoti ya Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani kwa Mh. Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ikulu jiji Dar es Salaam na ni mwanzo wa kuanza kwa mchakato wa Uchaguzi mwingine.

  0 0

  The GSMA today announced that it has elected Sunil Bharti Mittal, Founder and Chairman, Bharti Enterprises, as Chairman for the two-year period from January 2017 through December 2018. As GSMA Chairman, Mr. Mittal will oversee the strategic direction of the organisation, which represents nearly 800 of the world’s mobile operators, as well as more than 300 companies in the broader mobile ecosystem. Bharti Airtel was the host of the inaugural GSMA Mobile 360 – India event in New Delhi this week, as well as a meeting of the GSMA Board.

  A highlight of the week, GSMA Chair-elect Mr. Mittal led the GSMA Board delegation at a meeting with the Indian Prime Minister, Shri Narendra Modi on Wednesday afternoon. In a broad-ranging discussion, the meeting highlighted the pivotal role of mobile in delivering the government's Digital India vision of broadband as a utility for every citizen, bringing digital and financial inclusion to every corner of the country.
  The GSMA delegation led by the newly elected Chairman Mr Sunil Bharti Mittal with the Hon'ble PM of India, Shri Narendra Modi.

  The GSMA also elected the new members of the 26-member Board and re-elected Mari-Noëlle Jego-Laveissiere, Executive Vice President, Innovation, Orange Group as Deputy Chair for the two-year period.

  Mr. Sunil Bharti Mittal said, “I am delighted to be elected as Chairman of the GSMA, and look forward to working closely with the rest of the Board, the GSMA leadership team and our entire membership to address the critical issues facing our industry and our customers. In a relatively brief period of time, mobile has had a transformational impact on individuals, businesses, industries and societies, contributing significantly to local economies and improving the lives of billions around the world. I am excited about what the next chapter holds for us, as we work to connect everyone and everything to a better future.”

  “In my new global role, I am excited to support the ongoing mobile broadband revolution in India to boost the Government’s Digital India Program and its vision of broadband access for all”, added Mr. Mittal.

  The first Indian to be elected as Chairman of the prestigious global telecom industry board, Sunil Bharti Mittal took over as Chairman of the International Chamber of Commerce (ICC) early this year. He already serves on the Boards and Councils of several reputed international bodies and think-tanks like the World Economic Forum (WEF), Telecom Board of International Telecommunication Union (ITU), the Broadband Commission, Harvard University’s Global Advisory Council - Board of Dean’s Advisors at HBS, International Advisory Panel of the Monetary Authority of Singapore and Prime Minister of Singapore’s Research, Innovation and Enterprise Council. He is also a Trustee of the Carnegie Endowment for International Peace and on the Board of Qatar Foundation Endowment.

  The GSMA Board has 26 members, including 25 operator representatives from the world’s largest operator groups as well as smaller, independent operators with global representation. The GSMA’s Director General Mats Granryd also serves on the GSMA Board. The GSMA Board for the 2017-2018 term comprises:

  Juan Carlos Archila, Executive Vice President, International Relationships, América Móvil
  Bill Hague, Executive Vice President-Global Connection Management, AT&T Mobility
  Sunil Bharti Mittal, Founder and Chairman, Bharti Enterprises
  Sha Yuejia, Executive Director and Vice President, China Mobile
  Sun Kangmin, Executive Director and Executive Vice President, China Telecom
  Lu Yimin, President and Vice Chairman, China Unicom
  Wolfgang Kopf, Senior Vice President, Public and Regulatory Affairs, Deutsche Telekom
  Hatem Dowidar, CEO International, Etisalat
  Mats Granryd, Director General, GSMA
  Christian Salbaing, Deputy Chairman, Europe, Hutchison
  Takashi Tanaka, President, KDDI
  Eelco Blok, CEO, KPN
  Chang-Gyu Hwang, Chairman and CEO, KT Corporation
  Mauricio Ramos, CEO, Millicom
  Phuthuma Nhleko, Chairman and Acting CEO, MTN Group
  Andrei Dubovskov, President, MTS
  Kazuhiro Yoshizawa, President and CEO, NTT DOCOMO
  Mari-Noëlle Jego-Laveissiere, Executive Vice President, Innovation, Orange Group
  Dong-Hyun Jang, President and CEO, SK Telecom
  Julio Linares López, Vice President of the Board, Telefónica
  Sigve Brekke, President and CEO, Telenor Group
  Johan Dennelind, President and CEO, Telia Company
  Kaan Terzioğlu, CEO, Turkcell
  Roy Chestnutt, Chief Strategy Officer, Verizon
  Serpil Timuray, Group Chief Commercial Operations and Strategy Officer, Vodafone
  Scott Gegenheimer, CEO, Zain Group

  GSMA Chairman Mr. Jon Fredrik Baksaas will step down from the Board at the end of 2016, after holding this position for the past three years. Mr. Baksaas was elected as a member of the GSMA Board in 2008.

  “With nearly 4.8 billion individuals around the world subscribing to mobile services, it is the most pervasive and fast-growing platform of users ever built. It is now accessible to billions in both developing and developed markets, providing life-enhancing services and enabling new socio-economic opportunities for all,” commented Baksaas. “The mobile industry is at the very heart of the world’s digital transformation, driving efforts to make the world a better place, in support of the UN Sustainable Development Goals. It has been a true privilege to serve on the GSMA Board for eight years, the last three as Chair. I wish the new Board and Chair, Mr. Sunil Bharti Mittal, the very best of luck as the GSMA focuses on extending global platform capabilities, such as GSMA Mobile Connect, to billions of users around the globe.”

  0 0


  Meneja Mwandamizi wa Uhusiano wa Umma wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), Noves Moses katika akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Jengo la Vyoo katika shule ya msingi Pande ambavyo limegharimu kiasi cha sh.milioni 14.5 kushoto ni Afisa Kilimo na Mazingira Jiji la Tanga,Ened Mzava na kulia ni Afisa Elimu Sayansi Kimu, Rukia Magogo

  Meneja Mwandamizi wa Uhusiano wa Umma wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), Noves Moses akizundua Jengo jipya la Choo cha Shule ya Msingi Pande ambalo wamelijenga.
  Meneja Mwandamizi wa Uhusiano wa Umma wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), Noves Moses pamoja na wageni wengine wakipiga makofi mara baada ya kulizundua jengo hilo
  Meneja Mwandamizi wa Uhusiano wa Umma wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), Noves Moses kulia akipongezwa na mwalimu mkuu wa shule ya Msingi Pande,Mathias Anthony mara baada ya kuzindua Jengo la Choo

  Meneja Mwandamizi wa Uhusiano wa Umma wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), Noves Moses katikati akielekea kuzindua Jengo hilo
  Afisa Elimu Msingi wilaya ya Mkinga,Zakayo Mlenduka akizungumza kwenye halfa hiyo
  Meneja Mwandamizi wa Uhusiano wa Umma wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), Noves Moses wa tatu kutoka kushoto akionyeshwa choo za zamani ambacho kilibomoka na Afisa Kilimo na Mazingira Jiji la Tanga,Ened Mzava wa tatu kulia wakati alipotembelea eneo hilo.
  Choo cha zamani ambacho kilikuwa kinatumiwa na wanafunzi wa shule hiyo ambacho kilianguka


  Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha

  0 0
 • 10/28/16--07:46: KUMBUKUMBU
 • OMUTWALE Paschal Rutaihwa Kakiziba
  13 JULAI 1935 – 28 OKTOBA 2004

  Baba yetu mpendwa umetimiza mwaka wa 12 tangu ulipotwaliwa na Bwana. Picha yako inatukumbusha uwepo wako tulipokuwa sote hapa duniani, na hasa ukarimu, upendo, upole, uchangamfu na wingi wa busara.

  Ni vigumu kukubali kwamba haupo nasi lakini hatuna budi kuamini kwamba uko nasi kiroho kwa vile tunaye Mungu ambaye anaendelea kututia nguvu kila iitwapo leo. Busara zako na ucheshi wako vinazidi kutuimarisha kila siku na tunaendelea kuzingatia maneno yako uliyokuwa ukihimiza juu ya kuwa na upendo na umoja katika familia huku tukiendelea kumtumaini Mungu wetu ambaye amekuita kwake.

  Mke wako Mary-Hilda Kakiziba, rafiki yako Galita, watoto wako, wajukuu, wakwe zako, dada zako, kaka zako na wadogo zako, ndugu, marafiki na majirani wanakosa ucheshi na ushauri wako na wanakukumbuka daima. MISA YA KUMBUKUMBU ITAFANYIKA JUMAPILI, OKTOBA 30, 2016, SAA 3 ASUBUHI KWENYE KIGANGO CHA MT. ANTHONY WA PADUA, BOKO, DSM.

  Tumaini letu linajengwa na neno lisemalo: ”Umevipiga vita vilivyo vizuri, mwendo umeumaliza na imani umeilinda” (2Tim. 4:7) Tunakuomba Ee Bwana uendelee kuipumzisha roho yake mahali pema peponi, AMEN.

  0 0


  Mwanafunzi aliyeongoza masomo yote Rahma Mdeka akipokea cheti cha kuhitimu darasa la saba na zawadi yake wakati wa mahafali ya shule ya Southern Highlands Mafinga
  Mkurugenzi wa shule za Southern Highlands Mafinga ,Mary Mungai kulia akitambulisha watumishi wa shule hiyo.
  .........................................................................................................

  Na MatukiodaimaBlog

  UONGOZI wa shule ya Southern Highlands Mafinga wilaya ya Mufindi mkoani umeeleza kufurahishwa na matokeo ya mtihani wa darasa la saba Taifa baada ya wanafunzi wote 51 waliofanya mtihani huo kufaulu na kuifanya shule hiyo kushika nafasi ya kwanza Kiwilaya .

  Pamoja na kuongoza kiwilaya pia shule hiyo ya Southern Highlands Mafinga imekuwa shule ya 6 kati ya shule 232 katika mkoa wa Iringa na shule ya 198 kati ya shule 8109 kitaifa .Mkurugenzi mtendaji wa shule hiyo Mary Mungai akizungumza leo kufuatia matokeo hayo alisema kuwa pamoja na kuwa shule hiyo haijapata kufelisha mwanafunzi hata mmoja toka ilipoanzishwa 2001 ila bado ana imani jitihada zaidi zitaongezwa ili kuzidi kushika nafasi za juu zaidi kimkoa na kitaifa .

  “ Ni jambo la kumshukuru Mungu na tunaendelea kumshukuru Yeye Kwa kuwezesha watoto wetu wa Southern Highlands School, kufaulu vizuri, kwa kishindo kila mwaka wanafunzi wote wamekuwa wakifaulu mitihani ya kitaifa ya darasa la saba na wote kuchaguliwa na kuendelea na masomo ya Sekondari....ni matumaini yetu imani kwa wazazi inazidi kuongezeka zaidi kwa shule yetu"Alisema kuwa toka shule hiyo ilipoanzishwa mwaka 1994 kama Day Care na Pre-school na mwaka 1997 kuanza shule ya msingi imekuwa ikifanya vizuri na hakuna mtoto aliyepata kufeli .

  “Shule yetu mwaka 2001 shule ilitoa wanafunzi wa kwanza wa darasa la Saba na wanafunzi walikuwa 17, wote walifaulu vizuri na wote walichaguliwa kuendelea na masomo ya kidato cha kwanza”

  Alisema katika matokeo ya mitihani ya darasa la 7 ya mwaka 2001 Southern Highlands School ilishika nafasi ya kwanza kitaifa katika mitihani ya Somo la Kiingereza. Aidha alisema kwa mwaka huu 2016 jumla ya wanafunzi 51 walisajiliwa kufanya mtihani wa darasa la saba na wote walifanya wastani wa shule 185.3137 kundi la shule watahiniwa 40 au zaidi ambapo imeweza kuongoza kiwilaya kuwa ya kwanza na kimkoa ya 6.

  Mkurugenzi huyo alisema kuwa ajili ya kuwashukuru wazazi wanaosomesha watoto wao katika shule hiyo wameamua kutoa punguzo ya ada kwa wanafunzi hao waliofaulu mtihani wa darasa la saba ambao watajiunga na shule ya Sekondari ya Southern Highlands Mafinga ,huku akiwaomba wazazi wenye watoto wanaohitaji kujiunga na shule hiyo kuwapeleka watoto wao kwani shabaha kuu ni kuona watoto wanaendelea kupata elimu bora.

  0 0

  Na. Immaculate Makilika- MAELEZO

  Udhibiti wa huduma ya habari kwa namna ya ili kulinda usalama, utulivu amani na maslahi ya kiuchumi, maadili au afya ya jamii ni jambo jema ambalo huzingatiwa na nchi zote duniani.

  Hayo yamesemwa na Kaimu Mkuu wa Chuo cha Diplomasia, Dkt. Bernard Achiula alipokuwa akifanya mahojiano kuhusu namna muswada sheria ya huduma za habari unavyoweza kusaidia kukuza diplomasia ya uchumi nchini.

  Dkt. Achiula alisema kuwa vyombo vya habari vina jukumu kubwa la kulinda amani ya nchi na kwa kuwekwa misingi ya uwajibikaji kwa waandishi wa habari itakayosaidia kulinda maslahi ya Taifa.

  “Muswada huu upitishwe ili vyombo vya habari vifanyekazi katika misingi ya taaluma kwa kutoa taarifa zenye kweli kwa jamii, zitakazoitangaza nchi kimataifa ili kujenga diplomasia ya uchumi, itakayosaidia katika kulinda heshima utulivu na amani ya nchi”

  “Muswada huu pia utasaidia waandishi wa habari kuandika habari zitakazoiletea sifa nchi na kuvutia watalii na wawekezaji kwa kuzingatia amani iliyopo nchini, mbali na hapo diplomasia ya uchumi itaweka mazingira rafiki katika kufikia azma ya Serikali ya Awamu ya Tano ya Tanzania ya kufikia uchumi wa kati kupitia viwanda ifikapo mwaka 2020” alisema Dkt. Achiula

  Sehemu hii ya muswada wa huduma za habari unaakisi mikataba ya kimataifa ikiwemo mkataba wa geneva ibara ya 19 inayoainisha haki wa wajibu kwa mwandishi wa habari hasa katika maeneo yanayohusu usalama, utulivu amani na maslahi ya kiuchumi, maadili au afya ya jamii.

  Akizungumzia kuhusu Bodi ya Ithibati iliyopo katika muswada huo, Dkt. Achiula alisema kuwa Bodi hiyo itasaidia kukuza kanuni za maadili kwa wanahabari na kukuza weledi jambo litachochea mahusiano yenye faida katika nyanja za kimataifa.

  Ameongeza kuwa kuwemo kwa Baraza Huru la Habari kutasaidia kuijengea uwezo sekta habari nchini kwa vile muswada huo utazalisha waandishi wa habari waliobobea katika fani mbalimbali, huku akitolea mfano nchi zilizoendelea ikiwemo Ujerumani kwa kuwa na chombo kinachosimamia masuala ya sekta ya habari kwa kufuata misingi na utaratibu maalumu.

  Aidha, wadau wa sekta ya habari nchini, wametakiwa kuendelea kutoa maoni yao ya kuboresha Muswada wa huduma za habari, kabla muswada huo kusomwa tena bungeni ifikapo novemba mosi, mwaka huu.

  0 0

  Mkuu wa Wilaya ya Ileje, Joseph Mkude (kulia) na Mkurugenzi wa Wilaya hiyo, Haji Mnasi wakishiriki zoezi la kuziba mfereji uliochimbwa kuchepusha Mto Kalembo na mmoja wa Wakazi wa kata ya Bupigu kijiji cha Bungu.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Ileje, Haji Mnasi, akiwa na baadhi ya watumishi wa wilaya hiyo kuziba maji katika eneo lilichimbwa na mmoja wa wakazi wa Kata ya Bupigu kwa lengo la kuchepusha mto Kalembo kwenda kwenye Mashamba .
  Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Ileje ,Haji Mnasi, akivuta maji yaliyowekwa kuziba mto Kalembo uende sehemu nyingine hali inayohatarisha mazingira katika eneo hilo.
  Mkuu wa Wilaya ya Ileje ,Joseph Mkude akizungumza jambo na mkurugenzi wa wilaya hiyo Adji Mnasi, juu ya atahari za mfereji huo.

  Na Humphrey Shao,Globu ya Jamii Ileje

  MKUU wa Wilaya ya Ileje, Joseph Mkude ameongoza kamati ya ulinzi na usalama kwenda kufukia mfereji uliochimbwa na wananchi wa kata ya Bupigu kuchepusha maji kutoka mto Kalembo kwenda mashambani.

  DC Mkude amefanya zoezi hilo ikiwa ni siku chache tangu Waziri ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, Janauary Makamba ,kuagiza kusitishwa na kufukiwa kwa mfereji huo.

  wakati wa zoezi hilo la ufukiaji Dc Mkude alimuagiza mkurugenzi wa wilaya hiyo Haji Mnasi kupeleka wataalamu wa umwagiliaji kutoa elimu juu ya ujenzi wa Skim ambazo aziathiri Mazingira.

  Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mtendaji wa Wilaya hiyo amesema kuwa hakuna haja ya wananchi kujichukulia maamuzi wenyewe kwenye vyanzo vya maji na misitu ya Serikali.

  Ametoa wito kwa wananchi wa kata ya Bupigu kuwa wavumilivu kwani serikali hii ni ya Wanyonge hivyo wanafanya mpango wa kuwawezesha kwa namna nyingine kumudu kilimo cha umwagiliaji kupitia Rasilimali walizonazo.


  0 0


  0 0

  Wachezaji wa Azam Fc wakimpongeza Nahodha wao John Bocco dakika ya 86 baada ya kuwapachikia bao la ushindi katika mchezo wao wa Ligi Kuu Vodacom VPL leo kwenye Uwanja wa Kaitaba uliopo Bukoba Mjini. Bao hilo limeiwezesha Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam kuibuka na pointi  tatu muhimu  baada ya kuinyuka Kagera Sugar mabao 3-2 katika mchezo ulifanyika leo Mkoani Kagera.

  Huu ni ushindi wa pili mfululizo kwa Azam FC, ulioifanya Timu hiyo ya Jijini Dar es Salaam kupanda juu  nafasi mbili kwenye msimamo baada ya kufikisha jumla ya pointi 19 katika mechi 12 za Ligi ilizocheza. 

  Mshambuliaji Themi Felix, alianza kuishtukiza Azam FC kwa kuifungia bao la uongozi Kagera Sugar dakika ya 32 kabla ya Mudathir Yahya kusawazisha kwa bao zuri la shuti akimalizia pasi ya kichwa aliyodondoshewa na Bocco kufuatia faulo iliyochongwa na Erasto Nyoni.  Hadi kipindi cha kwanza kinamalizika timu zote zilitoka uwanjani zikiwa nguvu sawa. Kipindi cha pili Azam FC ilikianza kwa kasi kubwa ikitaka kupata bao la uongozi lakini mabeki wa Kagera Sugar walikuwa kizuizi kikubwa kwa washambuliaji wa mabingwa hao wakiokoa hatari zote.
  Mwamuzi wa mchezo wa leo, Mathew Akrama kutoka Mwanza, aliamuru penalti ipigwe langoni mwa Azam FC baada ya beki Aggrey Morris kumfanyia madhambi Ally Nasoro ndani ya eneo la hatari, na penalti hiyo ilifungwa na Felix.

  Baada ya bao hilo, mabadiliko ya wachezaji watatu yaliyofanywa na Kocha Mkuu wa Azam FC kwa nyakati tofauti ya kuwatoa Gonazo Ya Thomas, Gadiel Michael na Jean Mugiraneza na kuingia Shaaban Idd, Frank Domayo na Khamis Mcha, yaliongeza uhai kwa timu hiyo na kupelekea kufunga mabao mawili yaliyoipa ushindi huo.
  Alianza Domayo dakika ya 80 aliyefunga bao zuri kwa shuti kali nje kidogo ya eneo la 18 akimalizia mpira uliotemwa vibaya na mabeki wa Kagera Sugar kabla ya Bocco kufunga la ushindi dakika sita baadaye akifunga kwa kichwa safi kufuatia krosi iliyochongwa na Shaaban Idd.
  Bao hilo linamfanya Bocco kufikisha mabao matano kwenye msimu huu wa ligi akizidiwa mabao mawili na Shiza Kichuya wa Simba, anayeongoza kileleni kwa mabao saba.

  Picha zote na Faustine Ruta, Bukoba


  Timu zilivyokuwa zinaingia Uwanjani
  Kikosi cha Timu ya Kagera Sugar

  Kikosi cha Azam Fc
  Kikosi cha Azam Fc kilichoanza dhidi ya Kagera Sugar leo kwenye Uwanja wa Kaitaba  Kikosi cha Azam Fc leo kilikuwa:
  Aishi Manula, Erasto Nyoni, Gadiel Michael/Khamis Mcha dk 79, Aggrey Morris, Daniel Amoah, Jean Mugiraneza/Frank Domayo dk 70, Ramadhan Singano, Salum Abubakar, John Bocco (C), Mudathir Yahya, Gonazo Ya Thomas/ Shaaban Idd dk 62

  Ushindi huu pia ni wa pili mfululizo baada ya Timu ya Kagera kupoteza mchezo wao uliopita dhidi ya Yanga kwa bao 6-2 na sasa Timu hiyo kupoteza pointi 3 mbele ya Azam Fc kwa bao 3-2. Kitendo kilichowafanya Mashabiki wa Kagera Sugar kuandamana wakionesha Mabango katika Mchezo huo.
  Mashabiki wakiwa na Jazba kubwa Uwanjani Kaitaba

  Mashabiki wa Kagera Sugar wakiwa na Mabango wakionesha ujumbe wao kwa Timu yao inayoongozwa na Maxime.

  Wakidai kuwa ana Tabia ya kuuza Mechi.Baadhi ya Wachezaji wa Kagera Sugar wakijiuliza
  Kagera Sugar wakiwa hoi baada ya Azam Fc kusawazisha bao kwa kufanya 2-2
  John Bocco ‘Adebayor’ akigombea mpira wa kichwa  Kichapo cha pili mfululizo

  Waamuzi wa Mtanange huo

  Mashabiki wa Timu ya Kagera Sugar wakiwa na Ujumbe wao

  Mashabiki wa Timu ya Kagera Sugar

  Juu kwa juu Wanahabri wa Azam Fc wakichukua Picha

  Bocco tena  Penati.... mpira ukipangwa


  0 0

   Vijana wasomi 53 wa grupu la Whatsapp la WAZALENDO wakikamilisha kufyatua matofali 45,000 kwa ajili ya mabweni matano na  nyumba tano za walimu Shule ya Sekondari ya Nasibugani wilayani Mkuranga mkoa wa Pwani, umbali wa kilomita 151 kutoka Dar es salaam, na kilomita 53 kutoka makao makuu ya Wilaya. 
  Leo wamekutwa wakifanya kazi hiyo nzito huku wakihamasika kwa nyimbo wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Mhe. Filbert Sanga (wa pili kulia). Vijana hao, 14 wakiwa wanawake na 39 wanaume, walikubaliana kupiga kambi shuleni hapo toka Septemba 27, 2016  na kufanya kazi hiyo ya kujitolea na bila malipo kwa moyo mmoja na kufanikiwa kufyatua matofali hayo. Kambi hiyo inatarajiwa kufungwa kesho Jumamosi Oktoba 29, 2016 na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Profesa Joyce Ndalichako
   Mmoja wa vijana hao wasomi akielekea kazini
    Sehemu ya vijana hao wasomi 53 wakichota maji ili kukamilisha kufyatua matofali 45,000 kwa ajili ya mabweni matano na  nyumba tano za walimu Shule ya Sekondari ya Nasibugani wilayani Mkuranga mkoa wa Pwani
   Sehemu ya vijana hao wasomi 53 wakichota maji ili kukamilisha kufyatua matofali 45,000 kwa ajili ya mabweni matano na  nyumba tano za walimu Shule ya Sekondari ya Nasibugani wilayani Mkuranga mkoa wa Pwani
   Sehemu ya vijana hao wasomi 53 wakichota maji ili kukamilisha kufyatua matofali 45,000 kwa ajili ya mabweni matano na  nyumba tano za walimu Shule ya Sekondari ya Nasibugani wilayani Mkuranga mkoa wa Pwani
   Sehemu ya vijana hao wasomi 53 wakichota maji ili kukamilisha kufyatua matofali 45,000 kwa ajili ya mabweni matano na  nyumba tano za walimu Shule ya Sekondari ya Nasibugani wilayani Mkuranga mkoa wa Pwani
  Vijana hao wasomi 53 wakikamilisha kufyatua matofali 45,000 kwa ajili ya mabweni matano na  nyumba tano za walimu Shule ya Sekondari ya Nasibugani wilayani Mkuranga mkoa wa Pwani
   Vijana hao wasomi 53 wakikamilisha kufyatua matofali 45,000 kwa ajili ya mabweni matano na  nyumba tano za walimu Shule ya Sekondari ya Nasibugani wilayani Mkuranga mkoa wa Pwani
   Vijana hao wasomi 53 wakikamilisha kufyatua matofali 45,000 kwa ajili ya mabweni matano na  nyumba tano za walimu Shule ya Sekondari ya Nasibugani wilayani Mkuranga mkoa wa Pwani
   Vijana hao wasomi 53 wakikamilisha kufyatua matofali 45,000 kwa ajili ya mabweni matano na  nyumba tano za walimu Shule ya Sekondari ya Nasibugani wilayani Mkuranga mkoa wa Pwani
   Vijana hao wasomi 53 wakikamilisha kufyatua matofali 45,000 kwa ajili ya mabweni matano na  nyumba tano za walimu Shule ya Sekondari ya Nasibugani wilayani Mkuranga mkoa wa Pwani
   Vijana hao wasomi 53 wakikamilisha kufyatua matofali 45,000 kwa ajili ya mabweni matano na  nyumba tano za walimu Shule ya Sekondari ya Nasibugani wilayani Mkuranga mkoa wa Pwani
   Vijana hao wasomi 53 wakikamilisha kufyatua matofali 45,000 kwa ajili ya mabweni matano na  nyumba tano za walimu Shule ya Sekondari ya Nasibugani wilayani Mkuranga mkoa wa Pwani
   Vijana hao wasomi 53 wakikamilisha kufyatua matofali 45,000 kwa ajili ya mabweni matano na  nyumba tano za walimu Shule ya Sekondari ya Nasibugani wilayani Mkuranga mkoa wa Pwani
  Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Mhe. Filbert Sanga akielekeza vijana sehemu ya kuweka matofali 
   Kazi ikiendelea
   Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Mhe. Filbert Sanga akiwa katika picha ya pamoja  na vijana hao wasomi 53 baada ya kukamilisha kufyatua matofali 45,000 kwa ajili ya mabweni matano na  nyumba tano za walimu Shule ya Sekondari ya Nasibugani wilayani Mkuranga mkoa wa Pwani
   Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Mhe. Filbert Sanga akipungia pamoja  na vijana hao wasomi 53 baada ya kukamilisha kufyatua matofali 45,000 kwa ajili ya mabweni matano na  nyumba tano za walimu Shule ya Sekondari ya Nasibugani wilayani Mkuranga mkoa wa Pwani
   Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Mhe. Filbert Sanga akitoa maelekezo kwa vijana hao wasomi 53 baada ya kukamilisha kufyatua matofali 45,000 kwa ajili ya mabweni matano na  nyumba tano za walimu Shule ya Sekondari ya Nasibugani wilayani Mkuranga mkoa wa Pwani
   Baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo wakiwa bwenini
   Baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo wakiwa bwenini ambako kuna uhaba wa nafasi kiasi cha kurundikana namna hiyo
   Huko jikoni msosi unaandaliwa
   Wanafunzi wa shule hiyo wakijipanga kupata chakula cha mchana
   Wanafunzi wanapata chakula na matunda kila mlo
   Mojawapo ya nyumba chache za walimu ambamo wanakaa walimu saba
   Walimu sita kati ya saba wanaoishi kwenye nyumba hiyo
   Nishati mbadala ya solar itumiwayo na walimu hao saba
   Wanafunzi wakipata mlo wa mchana
   Vijana wasomi wanawake wanalala hapa 
   Sehemu ya vijana hao 14 wanawake wakipumzika baada ya kazi nzito
   Pamoja na kufyatua matofali baadhi ya vijana hao wasomi ambao ni walimu walikuwa wakiingia darasani kufundisha. Hapa mwalimu akiandaa kipindi baada ya kufyatua matofali
   Mwalimu akiandaa kipindi
   Sehemu ya vijana hao
   Jiwe la msingi
   Nje ya darasa
   Mandhari ya sehemu ya shule hiyo
   Bweni la vijana wasomi wanaume
   Pamoja na kazi nzito ya kufyatua matofali vijana hawa wazalendo wana nyuso za furaha na kuridhika kwa kujitolea kwao
   "....HAPA KAZI TU!" anasema kijana huyu mzalendo
   Furaha ya kumaliza kazi kwa mafanikio
   Kijana mzalendo Petro Mgoti (suruali ya njano) alikuwa katika ziara ya mafunzo ya wiki sita nchini Ujerumani, na aliporejea nyumbani alienda moja kwa moja kujiunga na wenzie huko Mkuranga.
   Furaha ya ushindi
   Utamu wa uzalendo ni kufanya kazi na kufurahi kwa pamoja
   Vijana mapumzikoni
    Jengo la darasa la maabara ambalo sasa hutumika kama bweni la wanafunzi wa ziada
    Darasa la maabara ambalo sasa hutumika kama bweni la wanafunzi wa ziada
    Darasa la maabara ambalo sasa hutumika kama bweni la wanafunzi wa ziada
   Bweni kwa ajili ya wanafunzi ndani ya darasa la maabara
   Kila sehemu ya stoo ya darasa la maabara  hutumika kama bweni la wanafunzi wa ziada
   Stoo ya darasa la maabara  hutumika kama bweni la wanafunzi wa ziada
   Darasa la maabara ambalo sasa hutumika kama bweni la wanafunzi wa ziada
   Hayo matofali ni alama ya kuwa upande huo wa mbele ni wa Msikiti kwa ajili ya walimu na wanafunzi wa Kiislamu. Wakristo na waumini wa madhehebu mengine hutumia madarasa
   Baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo wakielekea bwenini
   Baada ya kazi na msosi sasa ni wakati wa kuimba wimbo wa kambi
   Wimbo wa kambi ukiimbwa na kuchezwa kwa furaha
   Kijana akishukuru kwa kuhitimishwa kwa kazi hiyo
   Mmoja wa vijana hao akishukuru Mungu kwa kumaliza kazi salama

   Sehemu ya vijana hao
   Vijana wakiwa katika kikao kidogo cha kuhitimisha kazi
    Kijana mzalendo Petro Mgoti (suruali ya njano) akisema machache. Yeye alikuwa katika ziara ya mafunzo ya wiki sita nchini Ujerumani, na aliporejea nyumbani alienda moja kwa moja kujiunga na wenzie huko Mkuranga.
   Baada ya kazi nzito Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Mhe. Filbert Sanga akijiunga kupata msosi na  vijana hao wasomi 53 baada ya kukamilisha kufyatua matofali 45,000 kwa ajili ya mabweni matano na  nyumba tano za walimu Shule ya Sekondari ya Nasibugani wilayani Mkuranga mkoa wa Pwani
  Vijana hao wasomi 53 wakipata msosi baada ya kukamilisha kufyatua matofali 45,000 kwa ajili ya mabweni matano na  nyumba tano za walimu Shule ya Sekondari ya Nasibugani wilayani Mkuranga mkoa wa Pwani.

  0 0


   Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu

  Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu kulia akisistiza jambo wakati akizungumza na washiriki wa Ikungi Half Marathon kulia kwake ni MathiasCanal Mwandishi wa Habari wa mtandao wa Www.wazo-huru.blogspot.com
  Afisa Michezo Wilaya ya Ikungi Aboubakary Kisuda akizungumza na awashiriki wa Ikungi Half Marathon kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu
  Washiriki wa Ikungi Half Marathon wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu

   Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu

  Na Mathias Canal, Singida 

  Mashindano ya kuibua vipaji vya wafukuza upepo kwa mbio ndefu Ikungi Half Marathon yanayotaraji kufika ukomo jumamosi hii Octoba 29, 2016 katika Viwanja vya Shule ya Sekondari Ikungi ambapo Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Methew Mtigumwe anatarajiwa kuwa mgeni Rasmi katika mashindano hayo.

  Vijana takribani 60 shupavu waliochomoza kwenye mchujo wa ngazi ya Vijiji, Kata na Tarafa  wataingia barabarani kuisaka ama heshima ya ushindi au ushiriki kwa ngazi ya Wilaya huku wengine waliokosa nafasi katika awamu hii kusubiri awamu ijayo katika mashindano ya Full Marathon yatakayofanyika Mwaka 2017.

  Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu amezungumza na washiriki wote wa mbio hizo ambapo amewapongeza kwa kujitokeza kwa wingi jambo ambalo linaonyesha kuwa mchezo huo una wahitaji wengi.

  Mtaturu amesema kuwa mashindano haya ya Ikungi Half Marathon yanafanyika kwa mara ya kwanza na yatakuwa endelevu ambapo mwakani yatafanyika pia mashindano yam bio ndefu yatakayojulikana kama Ikungi Marathon 2017.

  Dc Mtaturu alisema kuwa Dhamira ya kuanzishwa kwa mashindano haya ni kuibua vipaji kwa vijana na kuviendeleza, Kujenga umoja na mshikamano miongoni mwa vijana na kuwaandaa vijana katika Wilaya hii kwa ajili ya mashindano mbalimbali ya Kitaifa na Kimataifa.

  Mashindano ya mbio ndefu yenye umbali wa kilomita 21 yatahusisha vijana wenye umri wa kuanzia miaka 17 hadi 30 waishio Wilayani Ikungi na yanatarajiwa kufanyika kila mwaka ili kuinua hamasa ya Mchezo wa riadha huku yakiambatana na mbio fupi za mita 100, mita 400 na mita 800.

  Mashindano haya yalianza Septemba 3, 2016 kwa ngazi ya Vijiji, Octoba Mosi yalifanyika kwa ngazi ya Kata, ambapo mchujo wa ngazi ya Tarafa imemalizika Octoba 15, 2016 na hatimaye kupisha mchuano wa Kiwilaya.

  Mashindano haya yatatoa fursa kwa vijana kuonyesha uwezo wao wa kucheza na miguu kwa kasi ya ushindani kwa maana ya manufaa ya pesa lakini pia itaimarisha ajira kupitia chama cha Riadha mkoa wa Singida na Taifa kwa ujumla lakini pia kuwaondoa vijana wengi katika mawazo ovu ya kushinda vijiweni badala yake kujitokeza kwa ajili ya kujihusisha na Kilimo pamoja na ufugaji.
  Dc Mtaturu amewasihi washiriki wote kukimbia kwa kutumia muda mzuri ili iwe taswira ya rekodi nzuri katika ukimbiaji jambo litakalokifanya chama cha cha Riadha Taifa kuchagua vipaji vitakavyoendelezwa.

  0 0

   Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Profesa Beno Ndulu (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam jioni hii kuhusu kuchukuliwa kwa benki hiyo ambayo ilikuwa ikimilikiwa na serikali kwa asilimia 100.
   Mkurugenzi wa Usimamizi wa Mabenki, Kenedy Nyoni (kushoto), akichangia jambo kwenye mkutano huo. Kulia ni Gavana wa Benki Kuu, Profesa Beno Ndulu.
   Meneja Msaidizi Idara ya Uhusiano wa Umma na Itifaki wa BoT, Victoria  Msina (kulia), akimkaribisha Gavana Beno Ndulu kuzungumza na wanahabari. Wa pili kutoka kulia ni Kaimu Katibu wa Benki, Mustafa Ismail.
   Waandishi wa habari wakichukua taarifa hiyo.
   Wapiga picha wakiwa kazini.
  Taswira ya ukumbi huo wakati wa mkutano.

  Na Dotto Mwaibale

  BENKI Kuu ya Tanzania (BoT), imechukua usimamizi wa Benki ya Twiga 9Twiga Bancop Limited) kuanzia Oktoba 2016 imefahamika.

  Hayo yamebainishwa na Gavana wa Tanzania, Profesa Beno Ndulu Dar es Salaam leo jioni wakati akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kuhusu hatua hiyo ya kuchukuliwa kwa benki hiyo ambayo serikali ilikuwa ikiimiliki kwa asilimia 100.

  "Kwa mamlaka iliyopewa benki kuu chini ya kifungu cha Sheria namba 56 (1) (g) (i) na 56 (2) (a)-(d) cha Sheria ya mabenki na Taasisi za Fedha ya mwaka 2006 benki kuu ya Tanzania imeamua kuchukua usimamizi wa benki hiyo kuanzia tarehe 28 Oktoba 2016" alisema Ndulu.

  Alisema uamuzi huo umechukuliwa baada ya kubaini kuwa benki hiyo ina upungufu mkubwa wa mtaji kinyume na matakwa ya sheria ya Mabenki na Taasisi za Fedha ya mwaka 20016 na kanuni zake.

  Alisema upungufu huo wa mtaji unahatarisha usalama wa sekta ya fedha na pia kuendelea kutoa huduma za kibenki kwa benki hiyo kutahatarisha usalama wa amana za wateja wake.

  Profesa Ndulu alisema kutokana na uamuzio huo Benki Kuu ya Tanzania  imeisimamisha Bodi ya Wakurugenzi na Uongozi wa benki hiyo na imemteua Meneja Msimamizi ambaye atakuwa na jukumu la kusimamia shughuli za benki ya Twiga kwa kipindi ambacho itakuwa chini ya usimamizi wa benki kuu.

  Alisema pia Umma unaarifiwa kuwa katika kipindi kinachokadiriwa kufikia wiki moja kuanzia siku ya taarifa hii, shughuli za utoaji wa huduma za kibenki za benki hiyo zitasimama ili kutoa nafasi kwa ajili ya kupanga taratibu za uendeshaji wa benki hiyo.

  Alisema Benki Kuu ya Tanzania inapenda kuuhakikishia umma kuwa itaendelea kulinda maslahi ya wenye amana katika mabenki kwa lengo la kuleta ustahimilivu katika sekta ya fedha.


  0 0

   Mkuu wa kituo cha polisi Kibaya Patrick Kimaro (sabasita) akizungumza kwenye mafunzo hayo.
  h3h2
  Wafanyakazi wa TCRA Kanda ya Kaskazini wakiendesha mafunzo hayo
  h1
  Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Mkoani Manyara, Tumaini Magessa (kulia) na mkuu wa polisi wa wilaya hiyo Fadhili Luoga wakifutilia mafunzo hayo.
   
  Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Mkoani Manyara, Tumaini Magessa amewaasa askari polisi kuwachukulia hatua kali wahalifu wa mitandao ili kukomesha matukio hayo ambayo yamekuwa kero kwa jamii katika sehemu tofauti hapa nchini.
   
  Magessa alitoa kauli hiyo wakati akifungua mafunzo ya maofisa wa polisi wilaya ya Kiteto juu ya masuala ya uhalifu wa mitandao, yaliyoandaliwa na mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) kanda ya kaskazini na kufanyika kwenye jumba la maendeleo ya jamii mji mdogo wa Kibaya.
   
  Alisema ukuaji wa teknolojia umewezesha kupata mawasiliano ya intaneti kupitia simu, kutuma na kupokea fedha kwa kutumia simu za mikononi na kulipia huduma mbalimbali ila baadhi ya watu wanatumia matumizi hayo vibaya hivyo wachukuliwe hatua kali.
   
  Alisema maendeleo ya matumizi ya simu yamekuja na changamoto hizo pamoja na matumizi mabaya ya teknolojia ya mawasiliano na baadhi ya watumiaji wameibiwa pesa kwenye akaunti zao za fedha kupitia mitandao.
   
  Meneja wa TCRA kanda ya kaskazini Annette Matindi alisema kuna aina nyingi za uhalifu kupitia mitandao ya simu na intaneti ikiwemo kutokusajili laini za simu au kutumia majina bandia kusajili simu.
   
  Matindi alitaja makosa mengine ni kutumia simu kutuma ujumbe wa matusi au kasha na vitisho, utapeli na wizi wa fedha kupitia mtandao na simu ikipoteza mawasilino kwa muda pindi yakirudi unakuta fedha zimeibiwa.
   
  Mkuu wa Kituo cha polisi Kibaya, ASP Patrick Kimaro (Sabasita) alitoa wito kwa jamii kuzingatia na kusisitiziwa kuwa na matendo ya uadilifu ili kukomesha matukio ya makosa ya mitandaoni kupitia ulimwengu huu wa teknolojia.
   
  Kimaro alisema watumiaji wa mitandao ya kijamii wanapaswa kutambua kuwa wakitumiwa picha, sauti au maneo ya kashfa, uchochezi au udhalilishaji, wanapaswa kutoa taarifa kwenye kituo cha polisi ili kukomesha hali hiyo.
   
  Alisema kusambaza picha, sauti au maneno yenye viashiria vya makosa ya mtandao kwa kisingizio kuwa umetuliwa na mtu hakusababishi mtu asichukuliwe hatua hivyo wanapaswa kufuta kuliko kusambaza.
   
  Pia, alisema mafunzo kama hayo yanapaswa kutolewa mara kwa mara kwa askari polisi ili waendelee kukomesha makosa hayo kwani vijana wengi wenye utaalamu wa kompyuta na suala la  IT wanajifunza mbinu mpya kila mara za ualifu wa mitandao.
   
  Kwa upande wake, askari wa kituo hicho Bkari Yusuf alisema kwa sababu TCRA wana uwezo wa kuzima simu feki, pia watu wanaotumia mitandao ya kijamii kwa kuvunja maadili wanapaswa kufungiwa ili kukomesha makosa hayo.

  0 0

  Waziri wa Mambo ya ndani Mh.Mwigulu Nchemba amefanikisha kumrejesha KochaYanga Hans Van Der Pluijm ambaye alitangaza kujiuzulu kuiongoza timu hiyo mapema wiki hii.

  Katika Mazungumzo yaliyodumu takribani siku tatu,Mchana huu Mwigulu amefanikiwa kumrejesha kocha huyo ndani ya viunga vya jangwani na tayari kwa kuendelea na kazi yake ya Ukocha.

  Hii ni mara ya pili kwa Mh.Mwigulu anafanikiwa kuweka mambo sawa ndani ya klabu ya Yanga kwani msimu uliopita alifanikiwa kumrejesha kiungo Haruna Niyonzima kuichezea Yanga.

  Ikumbukwe kuwa Mwigulu Nchemba ni mdau wa michezo nchin na mpenzi wa soka na mwanachama hai wa jangwani “Yanga”

  Tazama hapo Barua kutoka kwenye Uongozi wa Yanga.

  url


older | 1 | .... | 1023 | 1024 | (Page 1025) | 1026 | 1027 | .... | 1897 | newer