Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1022 | 1023 | (Page 1024) | 1025 | 1026 | .... | 1898 | newer

  0 0


  Mwenyekiti wa Tamasha la Sauti za Busara Zanzibar Ndg Simai Mohammed Said akitiliana saini ya Makubaliano ya kusaidia Tamasha la Sauti za Busara Zanzibar na Balozi wa Ujerumani Tanzania Balozi Egon Kochanke, Ujerumani imekubali kuchangia  €5000 sawa na shilingi za Kitanzania milioni 12,hafla hiyo imefanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Kitalii ya Park Hyyat Shangani Zanzibar leo. Tamasha la Sauti za Busara Zanzibar hufanyika kila mwaka katika mwezi wa Febuary na kuhudhuriwa na Wageni mbalimbali wanaotembelea Zanzibar.
  Mwenyekiti wa Tamasha la Sauti za Busara Zanzibar Mhe Simai Mohammed Said, akibadilishana mkataba na Balozi wa Ujerumani Nchini Tanzania Balozi  Egon Kochanke, baada kumaliza kutiliana saini ya makubaliano ya kuchangia Tamasha hilo kwa mwaka 2017, hafla hiyo imefanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Park Hyyat Shangani Zanzibar, leo mchana. 

  0 0

  ef1
  Mhariri Mkuu wa kituo cha redio cha EFM Radio cha Jijini Dar es Salaam, Scholastica Mazula akisalimiana na Mkurugenzi wa Habari, Hassan Abbas wakati wa ziara yake ya kutembelea ofisi za kituo hicho leo Jijini humo kwa ajili ya kubadilishana mawazo na uzoefu wa kazi.
  ef2
  Mhariri Mkuu wa kituo cha redio cha EFM Radio cha Jijini Dar es Salaam, Scholastica Mazula akitoa ufafanuzi kwa Mkurugenzi wa Habari, Hassan Abbas wakati wa ziara yake ya kutembelea ofisi za redio hiyo leo Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kubadilishana mawazo na uzoefu wa kazi. Kulia ni Mtangazaji wa redio hiyo, Boneventure Kilosa.
  ef3
  Mkurugenzi wa Habari, Hassan Abbas akiwa katika picha ya pamoja na Mtangazaji wa kipindi cha michezo cha redio ya EFM, Ibrahim Masoud “Maestro” wakati wa ziara yake ya kutembelea ofisi za kituo hicho leo Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kubadilishana mawazo na uzoefu wa kazi.
  ef4
  Mkurugenzi wa Habari, Hassan Abbas (mwenye suti) akiwa katika picha ya pamoja na Mtangazaji wa kipindi cha Ubaoni kinachorushwa hewani na kituo cha redio ya EFM,  Silvester Mjuni   (kushoto) wakati wa ziara yake ya kutembelea ofisi za kituo hicho leo Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kubadilishana mawazo na uzoefu wa kazi. Wengine kushoto ni Afisa Habari Mwandamizi wa Idara ya Habari Jonas Kamaleki na Afisa Habari Beatrice Lyimo.
  ef5
  Mtangazaji wa kipindi cha UBAONI kinachorushwa hewani na kituo cha redio cha cha EFM cha Jijini Dar es Salaam, Silvester Mjuni (katikati) akiendesha mahojiano maalum ya kipindi hicho na Mkurugenzi wa Habari, Hassan Abbas (kushoto) wakati wa ziara yake ya kutembelea ofisi za kituo hicho kwa ajili ya kubadilishana mawazo na uzoefu wa kazi. Kulia ni Afisa Habari(MAELEZO), Jonas Kamaleki.
  ef6
  Mkurugenzi wa Habari, Hassan Abbas akizungumza katika mahojiano maalum ya kipindi cha cha UBAONI kinachorushwa hewani na kituo cha redio cha EFM redio cha Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Afisa Habari Mwandamizi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Jonas Kamaleki.
  (PICHA NA ISMAIL NGAYONGA -MAELEZO)

  0 0

  UONGOZI wa kampuni ya DIRA NEWSPAPER COMPANY LTD wachapishaji wa gazeti DIRA YA MTANZANIA unamwomba radhi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama wa nchi na jeshi la wananchi wa Tanzania kwa ujumla kwa habari iliyochapishwa kwa bahati mbaya katika gazeti letu; toleo Na.424 la Juni,20-26 ,2016 iliyokuwa na kichwa cha habari kisemacho “KIFARU CHA KIVITA CHA JWTZ CHAIBWA”.

  Tunapenda kueleza kwa masikitiko kuwa habari hiyo ilichapishwa kwa bahati mbaya baada ya mtayarishaji wa kurasa (graphic designer) kuipanga habari ambayo ilikuwa haijakamilika kiuchunguzi na kuiacha iliyotakiwa ichapishwe siku hiyo.

  Tunapenda JWTZ na watanzania wote kwa ujumla kuwa wafahamu kuwa gazeti la DIRA YA MTANZANIA halikulenga kuchafua Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kama ambavyo baadhi ya watu walivyofikiria.

  Tunafahamu mchango mkubwa wa jeshi la wananchi wa Tanzania kwa taifa letu na namna jeshi hilo linavyoshirikiana kwa kiasi kikubwa na vyombo vya habari hasa utoaji wa taarifa mbalimbali na kamwe jeshi hili tokea kuanzishwa kwake halijawahi kukwaruzana na vyombo vya habari jambo ambalo ni heshima kubwa kwetu na taifa kwa ujumla.

  Hivyo uongozi wa gazeti hili umeonelea kuomba radhi kwa Mkuu wa majeshi (CDF), askari wote wa JWTZ na watanzania wote walioshitushwa na habari hiyo na hasa mkuu wa kikosi cha 83 KJ cha Kiluvya mkoani Pwani ambaye kikosi chake kilitajwa kama chanzo cha habari hiyo.

  Na tunaomba ifahamike kuwa tumeomba radhi kwa ridhaa yetu na tunaamini kuwa “kuomba radhi” ni kitendo cha kiungwana kwa utamaduni wa waafrika na hasa watanzania tuliokulia katika misingi ya amani, upendo na utulivu na pia tunaamini kuomba kwetu radhi kutazidisha mahusiano mema na ya karibu kati yetu na JWTZ.

  Tunatanguliza shukrani zetu.

  Musiba Esaba Meneja utawala na Fedha.

  0 0


  Mhadhiri wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Stella Marios cha Mtwara Padre, Dkt. Charles Kitima akichangia mada katika moja ya Kongamano la Maadhimisho ya Kumbukizi za Mwalimu Julius Nyerere.( PICHA KUTOKA MAKTABA)

  ……………………………………………………

  Na: Frank Shija, MAELEZO

  27.10.2016

  Uanzishwaji wa Bodi ya Ithibati ya Wanahabari kama ilivyoainishwa katika Muswada wa Huduma za Habari wa mwaka 2016 hautaminya uhuru wa kutafuta na kusambaza habari.

  Hayo yamebainishwa na Mhadhiri wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Stella Marios kilichopo Mtwara Dkt. Charles Kitima katika mahojiano maalum na mwandishi wa habari hii leo.

  Dkt. Kitima amesema kuwa msingi wa haki ya kutafuta taarifa na kusambaza habari unatokana ibara ya 18 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hivyo watu wasiwe na hofu ya kuwa Bodi hiyo itawaminya watu kutoa mawazo yao.

  “Bodi ya Ithibati ya Wanahabari haiwezi kuwa kizuizi cha watu kutafuta na kusambaza habari kwani haki hiyo ipo kikatiba kupitia ibara ya 18 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania” Alisema Dkt. Kitima

  Amesema kuwa haoni sababu yoyote ya kupinga uanzishwaji wake kwa kuwa malengo yake ni kuhakikisha inasimamia kanuni za maadili ya wanahabari hapa nchini na kuijengea heshima tasnia.

  Aidha aliongeza kuwa pamoja na kuanzishwa kwa Bodi hiyo hakuna maana kwamba uanzishwaji wake utachukua majukumu ya taasisi zingine za habari zilizopo na kuongeza kuwa waandishi wa habari duniani kote wanafanya kazi kwa kufuata miiko ya maadili ya uandishi wa habari.

  Alisema kuwa suala kubwa kwa mwanahabari ni kuzingatia maadili na weledi wa taaluma yake ili kutekeleza majukumu yake pasipo kusababisha usumbufu kwa mtu au kikundi kingine.

  Bodi ya Ithibati ya Wanahabari ipo katika muswada wa huduma za Habari sehemu ya Tatu na kuelezewa kwa kirefu katika kifungu cha 10 hadi 20 katika muswada huo unaopatikana katika Tovuti ya Bunge ambayo ni www.bunge.go.tz.

  0 0

  Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii Ileje

  BALOZI wa Tanzania nchini Malawi, Victoria Mwakasege, amewataka Polisi kuimarisha ulinzi katika mipaka kati ya Tanzania na Malawi katika Wilaya ya Ileje.

  Balozi Mwakasege amesema hayo wakati wa ziara yake ya ujirani mwema kati ya Wilaya ya Ileje ya Tanzania na Chitipa ya Malawi katika mpaka wa Isongole.

  “lazima tukomeshe na kufunga njia zote za panya hasa zile ambazo zinapitisha bidhaa haramu kwa aupande wetu wa tanzania” amesema Mwakasege.

  Ameongeza kuwa kuna bidhaa zingine nchini Malawi ni halali lakini kwetu ni haramu, jambo ambalo linaleta shida kwa vijana wetu hasa pombe nyingi zinazotoka nchi hiyo, kwetu zimepigwa marufuku.

  Amesema kuwa pombe za viroba na Sukari vimekuwa zikitumia kuvushwa kwa njia za panya hali inayo hatarisha afya ya mlaji na kuikosesha serikali mapato.
    Balozi wa Tanzania nchini Malawi,Victoria Mwakasege, akizungumza na baadhi ya  viongozi wa Wilaya ya  ileje wakati wa ziara yake ya kukagua mpaka kati ya Tanzania na Malawi.
  Balozi wa Tanzania nchini Malawi,Victoria Mwakasege akisaini kitabu cha wageni kilichoshikwa na katibu Tawala wa Wilaya ya Ileje, Mary Joseph.   
   Mkuu wa Wilaya ya Chitipa,Grace Chirwa akizungumza na baadhi ya watendaji wa Tanzania na Malawi wakati wa ziara ya kukagua mipaka.
   Balozi wa Tanzania nchini Malawi,Victoria Mwakasege, akiwa na watendaji wa wa nchi zote mbili katika mpaka wa Tanzania na Malawi.
  Picha ya pamoja ya watendaji wa Tanzania na Malawi.

  0 0

   Afisa Mipango wa Bodi ya Filamu Tanzania Mfaume Said akiwasilisha mada inayohusu historia, majukumu na mipango ya baadae ya bodi hiyo mbele ya wasanii wa kike waliohudhuria mafunzo ya kuongeza ushiriki wao kwenye tasnia ya filamu. Mafunzo hayo ya siku mbili ni mwendelezo wa juhudi za Bodi ya Filamu kuongeza ubora wa filamu za Kitanzania.
  nl2
  Mkufunzi Mwandamizi kutoka Chuo Kikuu cha Dar-es-salaam Dkt. Mona Mwakalinga akisisitiza jambo wakati akiwasilisha mada inayohusu njia mbalimbali zinazotumika kuongeza uwezo wa mwigizaji kuuvaa uhusika kwenye michezo ya kuigiza na filamu.
  nl3
  Baadhi ya waigizaji wanaoshiriki mafunzo ya siku mbili ya kuwaongezea ushiriki waigizaji wa kike wakifuatilia mada inayowasilishwa na Mkufunzi Mwandamizi kutoka Chuo Kikuu cha Dar-es-salaam Dkt. Mona Mwakalinga. Mafunzo hayo ya siku mbili yanafanyika ukumbi wa Habari Maelezo, jijini Dar-es-salaam
  nl4
  Mwigizaji wa michezo ya kuigiza na filamu Bi. Madina Mjatta (Zawadi) akichangia mada wakati wa mafunzo ya siku mbili yanayolenga kuongeza ushiriki wa waigizaji wa kike kwenye tasnia ya filamu nchin

  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akizungumza na Uongozi wa  Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa,Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ katika kikao cha Mpango kazi wa mwaka 2016-2017   katika  utekelezaji wa  robo mwaka ya kwanza ya Julai-Septemba 2016 kilichofanyika leo  Ikulu Mjini Unguja,[Picha na Ikulu.] 27/10 /2016.
  zum2
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akitoa maelekezo wakati alipokuwa akizungumza na Uongozi wa  Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa,Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ katika kikao cha Mpango kazi wa mwaka 2016-2017   katika  utekelezaji wa  robo mwaka ya kwanza ya Julai-Septemba 2016 kilichofanyika leo  Ikulu Mjini Unguja,[Picha na Ikulu.] 27/10 /2016.
  zum3
  Baadhi ya maafisa wa Vikosi vya SMZ wakiwa katika kikao cha Mpango kazi wa mwaka 2016-2017   katika  utekelezaji wa  robo mwaka ya kwanza ya Julai-Septemba 2016 cha Uongozi wa  Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa,Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ,kilichofanyika leo  Ikulu Mjini Unguja chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(hayupo pichani),[Picha na Ikulu.] 27/10 /2016.
  zum4
  Wakuu wa Vikosi vya Ulinzi vya SMZ wakiwa katika kikao cha Mpango kazi wa mwaka 2016-2017   katika  utekelezaji wa  robo mwaka ya kwanza ya Julai-Septemba 2016 cha Uongozi wa  Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa,Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ,kilichofanyika leo  Ikulu Mjini Unguja chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(hayupo pichani),[Picha na Ikulu.] 27/10 /2016.
  zum5
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa,Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ Mhe,Haji Omar  Kheir akisoma taarifa ya  utekelezaji wa Mpango kazi wa mwaka 2016-2017 katika  kikao  cha robo mwaka ya kwanza ya  Julai-Septemba 2016 kilichofanyika leo   Ikulu Mjini Unguja,chini ya mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) (kulia) Katibu Mkuu Kiongozi Dkt.Abdulhamid Yahya Mzee,[Picha na Ikulu.] 27/10 /2016.
  zum6
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa,Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ Radhia Rashid Haroub akisoma vifungu wakati  wa kikao cha utekelezaji wa Mpango kazi wa   mwaka 2016-2017 katika  Wizara hiyo katika  robo mwaka ya kwanza ya  Julai-Septemba 2016, kilichofanyika leo  Ikulu Mjini Unguja,chini ya mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani),(kulia) Naibu Katibu Mkuu Nd,Kai Bushir Mbarouk,[Picha na Ikulu.] 27/10/2016.

  0 0

  Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), akifuatilia kwa makini wakati Mkurugenzi wa Uhamasishaji Uwekezaji kutoka kituo cha uwekezaji Tanzania-TIC, John Mnali, akiwasilisha mada kuhusu fursa za uwekezaji zinazopatikana Tanzania, wakati wa mkutano wa 5 wa ushirikiano wa kiuchumi kati ya Korea ya Kusini na nchi za Afrika (KOAFEC), Mjini Seoul, Korea Kusini. Kulia kwake ni Mkuu wa Kitengo cha Utafutaji Rasilimali kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Zanzibar-Sabra Issa Machano.
  Mkurugenzi wa Uhamasishaji uwekezaji kutoka Kituo cha Uwekezaji Tanzania-TIC, John Mnali (Katikati), akibadilishana mawasiliano na mmoja wa wafanyabiashara walioonesha nia ya kuweka nchini Tanzania baada ya Mkurugenzi huyo kuwasilisha mada kuhusu fursa za uwekezaji zinazopatikana Tanzania, wakati wa mkutano wa 5 wa ushirikiano wa kiuchumi kati ya Korea ya Kusini na nchi za Afrika (KOAFEC), Jijini Seoul, Korea Kusini.
  Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (Mb), akibadilishana mawasiliano na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya MarineBio, Heo Yun-Young, ambaye kampuni yake inataka kuwekeza kiwanda cha kusindika zao la mwani linalopatikana katika Bahari Kuu ya Hindi nchini Tanzania.
  Msaidizi wa Waziri wa Fedha na Mipango, Edwin Makamba, akiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti ambaye pia ni Rais wa Benki ya EXIM ya Korea Kusini, Lee Duk-Hoon baada ya hafla ya usiku ya kuagana kwa washiriki wa mkutano wa Ushirikiano wa Kiuchumi kati ya Korea Kusini na Nchi za Kiafrika, Jijini Seoul, nchini Korea kusini.
  Mkurugenzi wa Uhamasishaji uwekezaji kutoka Kituo cha Uwekezaji Tanzania-TIC, John Mnali, akiwasilisha mada kuhusu fursa za uwekezaji zinazopatikana Tanzania, wakati wa mkutano wa 5 wa ushirikiano wa kiuchumi kati ya Korea ya Kusini na nchi za Afrika (KOAFEC), Jijini Seoul, Korea Kusini
  Maofisa kutoka wizara ya Fedha na Mipango, Edwin Makamba ambaye ni msaidizi wa Waziri wa Fedha na MIpango, kushoto, na Mkuu wa idara ya Sera, Shogolo Msangi, wakifuatilia uwasilishwaji wa mada kuhusu fursa za uwekezaji zilizopo Tanzania Bara na Tanzania Visiwani, wakati wakati wa mkutano wa 5 wa ushirikiano wa Kiuchumi kati ya Korea Kusini na nchi za Kiafrika, uliomalizika leo Jijini Seoul, Korea Kusini
  Mkuu wa kitengo cha utafutaji Rasilimali, kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Zanzibar, Sabra Issa Machano, akiwasilisha mada kuhusu fursa za uwekezaji zinazopatikana Tanzania Zanzibar, wakati wa mkutano wa 5 wa ushirikiano wa kiuchumi kati ya Korea ya Kusini na nchi za Afrika (KOAFEC), Jijini Seoul, Korea Kusini.
  Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), akimpongeza Mkuu wa kitengo cha utafutaji Rasilimali, kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Zanzibar, Sabra Issa Machano, baada ya akiwasilisha mada kuhusu fursa za uwekezaji zinazopatikana Tanzania Zanzibar, wakati wa mkutano wa 5 wa ushirikiano wa kiuchumi kati ya Korea ya Kusini na nchi za Afrika (KOAFEC), Jijini Seoul, Korea Kusini.
  Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (Mb), akisalimiana na mwanafunzi wa Kitanzania anayesomea Chuo Kikuu kimoja nchini Korea Kusini kuhusu masuala ya biashara ya kimataifa na uchumi, Alice Mwamzanya, baada ya kushiriki mkutano wa 5 wa ushirikiano wa kiuchumi kati ya Korea Kusini na Nchi za Afrika (KOAFEC), Jijini Seoul nchini Korea Kusini.(Picha na Benny Mwaipaja-Wizara ya Fedha na Mipango)

  …………………………………………………..


  Benny Mwaipaja,WFM, Seoul, Korea 

  WAFANYABIASHARA wakubwa kutoka KOREA ya Kusini, wamekaribishwa kuja kuwekeza nchini Tanzania katika sekta ya viwanda vitakavyoongeza thamani ya bidhaa za kilimo, mifugo, mazao ya bahari pamoja na kutumia malighafi zinazopatikana nchini ili kusisimua uchumi wa taifa na kukuza ajira. 

  Wito huo umetolewa Jijini Seoul nchini Korea, na Mkurugenzi wa Uhamasishaji uwekezaji kutoka Kituo cha Uwekezaji Tanzania-TIC, JOHN MNALI, wakati akiwasilisha mada kuhusu fursa za uwekezaji zinazopatikana Tanzania, wakati wa mkutano wa 5 wa ushirikiano wa kiuchumi kati ya Korea ya Kusini na nchi za Afrika(KOAFEC). 

  Mnali amesema kuwa Tanzania imeweka mazingira mazuri ya uwekezaji ikiwemo kuondoa urasimu wa upatikanaji wa vibali vya kuwekeza na ardhi kwa ajili ya uwekezaji huo ili kuvutia mitaji na teknolojia kutoka nje ya mipaka yake. 

  Amewashauri wawekezaji hao kufufua viwanda ambavyo havifanyi vizuri nchini, ili kuanza uzalishaji wa bidhaa zitakazotumia malighafi zinazopatikana nchini pamoja na kutumia soko kubwa lililopo katika ukanda wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na soko la AGOA la Marekani. 

  Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Utafutaji Rasilimali, kutoka Wizara ya Fedha na Mipango Zanzibar, Sabra Issa Machano, amewahimiza wawekezaji wa Korea kwenda kuwekeza Visiwani humo na Tanzania kwa ujumla katika sekta za kilimo, viwanda na uvuvi wa samaki na mwani katika Bahari Kuu ili wakazi wa nchi hiyo na wawekezaji waweze kunufaika na rasilimali zilizoko visiwani humo. 

  Amewahimiza wawekezaji hao kujenga hoteli za kisasa kwa ajili ya kuhudumia soko la utalii ambalo ni kubwa nchini humo, pamoja na kutumia mandhari ya Mji Mkongwe wa Zanzibar ambao ni kivutio kikubwa cha watalii baada ya kutangangazwa na Shirika la Kimataifa linaloshughulika na masuala ya sayansi na utamaduni-UNESCO kuwa mji wa urithi wa Dunia. 

  Baadhi ya wawekezaji ikiwemo kampuni ya Youngsan, inayojihusisha na utengenezaji na usambazaji wa vipuri vya magari pamoja na kampuni ya MarineBio inayojihusisha na biashara ya utengenezaji wa bidhaa zinazotokana na mwani, wameonesha nia ya kuwekeza Tanzania baada ya kuvutiwa na mazingira ya uwekezaji nchini Tanzania. 

  “ Kampuni yetu imetafuta kwa muda mrefu fursa ya kuwekeza Tanzania lakini tulikuwa hatufahamu ipasavyo njia za kutumia kufikia uwekezaji huo ambapo sisi tunajihusisha na biashara itokanayo na zao la mwani linalozalishwa kwa wingi Zanzibar ambapo tunatengeneza bidhaa za karatasi, urembo, karatasi na vitu vingine vingi” alisema Yun-Young 

  Amesema kuwa wanatarajia kufungua kiwanda kikubwa ambacho kitazalisha ajira kwa wakulima na wafugaji wa samaki nchini Tanzania kwakuwa kampuni yake itajihusisha na biashara kubwa itakayochangia kukuza ajira na kuwafanya watu wengi hususan wanawake, waondokane na umasikini wa kipato. 

  Katika Mkutano huo uliomalizika leo, Ujumbe wa Tanzania uliongozwa na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango, ambaye amemwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, ambapo, Tanzania imesaini mkataba mmoja pamoja na Makubaliano ya ushirikiano wa pamoja kwa ya upanuzi wa miundombinu ya maji taka katika Jiji la Dar es salaam na ujenzi wa njia ya umeme yenye msongo wa kV400 kutoka Mbeya, Kigoma hadi Nyakanazi.

  0 0

  East Africa’s leading music festival Sauti Za Busara has announced the line-up for the 2017 edition, which will be held between 9 and 12 February 2017 in Zanzibar. The line-up presents a diverse selection from around the continent and the diaspora and includes 25 acts from within East Africa.


  Members of Wahapahapa band from Tanzania. Photo: www.busaramusic.org
  Members of Wahapahapa band from Tanzania. Photo: www.busaramusic.org
  For more CLICK HERE
  For many of the artists, this will be their debut performance at the festival and in East Africa. The line-up includes:
  • Moroccan roots-reggae superstars Bob Maghreb, who reinterpret Bob Marley classics with fresh North African flavours
  • Roland Tchakounté, a rocking African blues musician from Cameroon (now based in France)
  • Kyekyeku, a young, conscious Ghanaian singer-songwriter taking traditional palm wine and highlife music to new directions.

  0 0
 • 10/27/16--09:57: IKUNGI HALF MARATHON 2016


 • 0 0

  Mmoja wa wanafunzi wa Shule ya Msingi Nyarugusu, Juma Edward aliyesaidiwa na Shirika la Plan International kuacha kazi migodini na kurudi shule kuendelea na masomo akilishukuru shirika hilo kwa kuanzisha Mradi wa Uondoaji wa Ajira Hatarishi na Vitendo vya Ukatili kwa Watoto, Mradi huu wa miaka mitatu unaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD), unaratibiwa na Shirika la Plan International na kutekelezwa katika Wilaya 3 za Mkoa wa Geita.

  Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO, Geita

  Shule ya Msingi Nyarugusu iliyopo mkoani Geita imeanzisha kamati ya kudhibiti utoro wa wanafunzi ikiwa ni njia moja wapo ya kuwazuia kwenda kufanya kazi katika migodi iliyopo mkoani humo.

  Maamuzi hayo yametolewa na Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Peter Kitagira alipokuwa akiongea na waandishi wa habari juu ya mchango wa Mradi wa Uondoaji Ajira Hatarishi na Vitendo vya Ukatili kwa Watoto unaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD) na kuratibiwa na Shirika la Plan International. 

  Kitagira amesema kuwa wameamua kuchukua maamuzi hayo baada ya kugundua kuwa asilimia kubwa ya watoto wa mkoa huo wanaacha shule na kukimbilia kufanya kazi za migodini kwa ajili ya kujitafutia kipato bila kufahamu madhara ya shughuli hizo.
  Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Nyarugusu. Peter Kitagira akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya uanzishwaji wa Kamati ya utoro katika shule hiyo. Mradi huu wa miaka mitatu unafadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD), unaratibiwa na Shirika la Plan International na kutekelezwa katika Wilaya 3 za Mkoa wa Geita.

  “Hali ya utoro inaongezeka kwa kasi na ndio maana tumeamua kuanzisha Kamati ya Kudhibiti Utoro wa wanafunzi, kamati hiyo inafanya mawasiliano ya karibu na wamiliki wa migodi ili kuhakikisha hakuna mtoto chini ya umri wa miaka 18 atakayeajiriwa kwa ajili ya kufanya kazi kwenye maeneo hayo”, alisema Kitagira.

  Kitagira ameitaja sababu nyingine inayosababisha kushuka kwa mahudhurio ya wanafunzi wanaosoma katika shule hiyo kuwa ni hali duni ya maisha inayosababisha wazazi kuwaacha watoto majumbani wakilinda nyumba ili wao wakatafute fedha za kujikimu.

  Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati wa Shule hiyo, Philip Edward amesema kuwa ni vigumu sana kuwaelimisha wazazi juu ya athari za watoto kufanya kazi migodini au kuwaacha nyumbani wakilinda nyumba na kulea wadogo zao kwa sababu hawana njia nyingine ya kujipatia kipato zaidi ya kufanya kazi hizo.
  Mwenyekiti wa Kamati wa Shule ya Msingi Nyarugusi, Philip Edward akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu umuhimu wa mradi wa Uondoaji wa Ajira Hatarishi na Vitendo vya Ukatili kwa Watoto unaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD), unaratibiwa na Shirika la Plan International na kutekelezwa katika Wilaya 3 za Mkoa wa Geita.

  “Ili kupunguza utoro shuleni hapa, kamati ya shule ilifanya kikao na wazazi ambapo tulikubaliana kutoa kiasi cha shilingi mia tano kama adhabu kwa kila mwanafunzi ambaye hatokuja shuleni lakini muda mwingine tunawahurumia wazazi kwani kipato chao ni cha shida sana”, alisema Edward.

  Naye Mwalimu wa shule hiyo, Mathias Kato ambaye pia ni mlezi wa watoto wanaohudumiwa na shirika la Plan International amelishukuru shirika hilo kwa jitihada zao wanazozifanya katika kupinga ajira za watoto migodini kwa sababu umechangia kiasi kikubwa kuongeza mahudhurio ya  wanafunzi shuleni hapo.

  Ametoa ushauri kwa Serikali na mashirika mengine kuangalia namna ya kuwasaidia wazazi wenye kipato duni wanaoishi katika maeneo ya migodi kwa sababu ukosefu wa kipato kwa wazazi ndiyo chanzo cha watoto kutoroka shule na kwenda kujitafutia ridhiki migodini.

  0 0   Mkurugenzi Mkuu wa SBL Helene Weesie akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano na waandishi wa habari  ambapo alitangaza maadhimisho ya miaka 20  tangu kuanzishwa kwa bia ya Serengeti Premium Lager (SPL)  mwaka 1996. Anayefuatia ni Meneja masoko wa SBL  Anitha Msangi na kulia  mwishoni ni Mkurungezi wa Masoko wa SBL , Cesear Mloka  .Mkutano huu umefanyika mapema leo katika Hoteli ya Hyatt Regency Jijini Dar es salaam

  Mkurungezi wa Masoko wa SBL , Cesear Mloka akifafanua jambo kwa waandishi wa habari mara baada ya kutangazwa kwa maadhimisho ya miaka 20  tangu kuanzishwa kwa bia ya Serengeti Premium Lager (SPL)  mwaka 1996.Anayefuatia katikati ni Meneja Masoko wa SBL Anitha Msangi na mwishoni kulia ni Mkurungezi mkuu wa SBL  Helene Weesie.Mkutano huu umefanyika mapema leo katika Hyatt Regency Hotel Jijini Dar es salaam.
  Mpishi Mkuu mtanzania  Winston Kagusa aliyefanikiwa kuchanganya mbinu ya utengenezaji wa bia za kijerumani na  vionjo vya hapa nchini kupata  kinywaji hiki  cha Serengeti Premium Lager kinachopendwa na wengi.
   Mkurugenzi Mkuu wa SBL Helene Weesie akiongoza katika kuzindua chapa mpya ya Serengeti Premium Lager sherehe ambazo zinaambatana na maadhimisho ya miaka 20 ya bia hiyo kulia kwake ni Meneja Masoko wa SBL Anitha na kushoto kwake wa kwanza ni Mpishi Mkuu wa kwanza wa Serengeti Premium Lager Winston kagusa na mwishoni ni Mkurungezi wa Masoko  Cesear Mloka.Hafla hii ilifanyika katika hotel ya Hyatt Regency Jijini Dar es salaam.

  Mkurugenzi wa Mawasiliano, SBL John Wanyacha akifafanua jambo kwa waandishi wa habari katika Mkutano wa waandishi wa habari ambapo Bia ya serengeti premium lager inatimiza miaka 20 toka kuanzishwa kwake na pia kuzinduliwa kwa chapa yenye muonekano mpya.Mkutano huu ulifanyika mapema leo katika hotel ya Hyatt Regency
  Waandishi wa habari wakichukua matukio katika mkutano huo uliofanyika mapema leo

  • SBL yaizindua bia hiyo katika muonekano mpya


  • Yashinda zaidi ya medali 10 za ubora wa kimataifa


  Dar es Salaam  Oktoba 27, 2016- Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) leo  imetangaza kuanza kwa sherehe maalumu kuadhimisha miaka 20  tangu kuanzishwa kwa bia ya Serengeti Premium Lager (SPL)  mwaka 1996. Sherehe hizo zinaambatana na uzinduzi upya wa bia hiyo ikiwa katika muonekano mpya.


  Akizungumza  leo jijini Dar es Salaam katika mkutano na waandishi wa habari, Mkurugenzi Mkuu wa SBL Helene Weesie, amesema mbali na kuonesha mafanikio ya bia ya Serengeti kwa kipindi cha miongo miwilil iliyopita, kampuni ya SBL itatumia kipindi hiki kuwashukuru wateja  wake na umma wa Watanzania  kwa kuikubali bia ya Serengeti kama chaguo lao la hivyo kuifanya kuwa mingoni mwa bia zinazoongoza hapa nchini.


   “Tunawashukuru  wateja wetu, wafanya biashara, wasambazaji, mashirika ya sekta binafsi, serikali na wadau wote  ambao kimsingi wametusaidia  na kuwa nasi  katika safari yetu hii ya mafaniko,” amesema Weesie.


  Bia ya Serengeti Premium Lager ni ya kwanza kutengenezwa kwa kimea kwa asilimia 100hapa nchini ikiwa ni ubunifu wa Mpishi Mkuu mtanzania aitwaye Winston Kagusa  ambaye alichanganya mbinu ya utengenezaji wa bia za kijerumani na  vionjo vya hapa nchinikupata kupata kinwaji hiki kinacopendwa na wengi.


  Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu, bia ya Serengeti ilizalishwa kwa mara ya kwanza ikilenga kufikia sehemu ndogo maalumu ya soko lakini azma hii ilibadilishwa na kuzalishwa kwa wingi kutokana na ongezeko kubwa la mahitaji ya bidhaa hiyo jambo ambalo lilisababisha kuanzishwa uzalishaji zaidi katika viwanda vya SBL vilivyoko Moshi na Mwanza.


  Aidha Mkurugenzi huyo ameendelea kusema kwamba katika kipindi chote cha miongo miwili bia ya Serengeti imekuwa na vifungashio vya muonekano tofauti tofauti vinavyoakisi mabadiliko ya kinyakati na mahitaji ya wateja wake. “muonekano mpya tunaouzindua leo hii ni muendelezo wa kielelezo hiki kwamba daima SBL tunajali mahitaji ya wateja wetu na tuko karibu nao, amesema Weesie.


  “Tunaona fahari kuzalisha Bia ya Serengeti Premium Lager  katika  ubora uleule wa hali ya juu katika viwanda vyote vitatu, na huu ni uthibitisho halisi kutokana na kutambuliwa  na wateja wetu wa ndani  pamoja na medali  zaidi ya 10  za kutambulika kimataifa  ambazo bia hii imeshinda. Tunaahidi wateja wetu kwamba tutaendeleakuzalisha Serengeti Premium Lager  katika ubora wa hali ya juu  kwa kuzingatia vigezo vya ubora vilivyoanishwa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) na Shirika la Viwango la Kimataifa (ISO),” amesema Weesie.


  Uzinduzi wa muonekano mpya wa  bia ya Serengeti pia umekuja na kauli mbiu mpya wa kinywaji hicho cha “Taifa Letu. Fahari Yetu. Bia Yetu.” Aidha kampuni hiyo imewakaribisha wateja wake na wadau mbalimbali kutoka sekta za umma na binafsi katika hafla ya maadhimisho ya miaka 20 ya bia ya Serengeti yatakayofanyika leo jijini Dar es Salaam.
  0 0

  Mkufunzi wa Manchester United Jose Mourinho ameshtakiwa na shirikisho la soka nchini Uingereza FA kwa kudai kwamba itakuwa vigumu kwa refa Anthony Taylor kusimamia mechi yao dhidi ya Liverpool.

  Mourinho aliongezeawamba kumteua Taylor kusimamia mechi hiyo ya tarehe 16 Oktoba ilimpatia shinikizo refa huyo mwenye makao yake Manchester.

  Mameneja hawaruhusiwa kuzungumzia kuhusu marefa kabla ya mechi.
  Mourinho ana hadi Oktoba 31 kujibu shtaka la ukosefu wa nidhamu na kusababisha mechi hiyo kuwa na jina baya.

  Taylor alito kadi 4 za njano zote kwa timu ya Manchester United katika sare hiyo ya 0-0.


  0 0

  Moja kati ya wajasiriamali watakaokuwepo katika maonyesho ya wajasiriamali ya Airtel FURSA, Bi Theresia Maliatabu akiandaa bidhaa zake za picha za Sanaa nyumbani kwake mbagala rangi tatu. Theresia ni moja kati ya wafanyafanya biashara waliowezeshwa na mradi wa kuinua vijana wa  Airtel FURSA
   
  Mkuu wa wilaya ya kinondoni Mh. Ally Hapi anatarajiwa kufungua maonyesho ya wajasiliamali mbalimbali wanaodhaminiwa na Mpango wa Airtel FURSA yatakayofanyika ijumaa hii katika viwanja vya ofisi za Airtel makao makuu Morocco jijini Dar es Salaam kuanzia saa nne asubuhi hadi jioni.

  Airtel kupitia mpango wake wa Airtel FURSA tunakuwezesha, umeandaa mpango utakaowawezesha wajasiriamali hao ambao awali waliowazezwa kupitia mpango wake wa Airtel FURSA ili waweze kuonyesha biashara zao kwa lengo la kuwawezesha wafanyabiashara kutangaza na kupata masoko ya biashara zao ili kukuza biashara na mitaji yao.

  Akiongea juu ya maonyesho hayo, Meneja Uhusiano wa Airtel Bwana Jackson Mmbando alisema “ tumeonelea ni vyema kujipanga katika kuendeleza dhamira yetu ya kuwainua vijana na kuhakikisha mpango huu wa Airtel FURSA unaleta tija na kuinua biashara zao. Watakaoshiriki ni zaidi ya wafanyabiashara 28 na vikundi vinne vilivyonufaika kwa kupatiwa vitendea kazi kupitia mradi wetu wa Airtel FURSA ambao kwa sasa wanafanya vizuri katika biashara zao”.

  Airtel tumeona ni vyema tukiendelea kuwawezesha kwa kuwatafutia masoko endelevu ndani na nje ya nchi kwa kuwashirikisha katika maonyesho haya yenye lengo la kutangaza biashara zao na kupata masoko zaidi, tunatoa wito kwa watanzania kuwaunga mkono kwa kufatilia kazi zao kupitia mitandao ya kijamii na kupata fursa ya kutembelea maonyesho haya siku ya kesho.

  Bidhaa zitakazo kuwepo katika maonyesho hayo ni pamoja na Sanaa za picha za ukutani, vifaa vya magari, vyakula mbalimbali kama matunda ,korosho, cake, mifugo kama vile kuku wa kisasa, bidhaa za kiafrika, mapambo ya nyumbani na kadhalika

  0 0

   
  Bwa. Samwel Kamanga -Mkurugenzi Mtendaji wa NIC


  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Maendeleo wa Abu Dhabi Mohamed Al Suwaidi aliyefika Ikulu kwa ajili ya mazungumzo.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Balozi wa Umoja wa Falme za Kiarabu nchini Abdullah Ibrahim Al Suwaidi aliyefika Ikulu pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Maendeleo wa Abu Dhabi Mohamed Al Suwaidi kwa ajili ya mazungumzo.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Maendeleo wa Abu Dhabi Mohamed Al Suwaidi mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU


  0 0

  0 0


  Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala ,akizungumza jambo na baadhi ya wakulima walioko katika bonde la Katengele,wakati alipokuwa akikagua kilimo cha umwagiliaji katika Bonde la Katengela kijiji cha Kinonko Wilayani Kakonko katika mashamba ya Mpunga,mkoani Kigoma.Dc Ndagara aliwaeleza wakulima hao kuwa kuanza kulima mazao yao kwa misimu miwili ya Kiangazi na masika kitaalamu zaidi na kujiunga kwenye vyama vya ushirika na kuacha tabia ya kuuza mazao yote kutokana na hali ya hewa ya mwaka huu inayoweza kupelekea maeneo mengi kukosa chakula.
  Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala ,akiwasikiliza baadhi ya wakulima walioko katika bonde la Katengele,wakati alipokwenda kukagua kilimo cha umwagiliaji katika Bonde la Katengela kijiji cha Kinonko Wilayani Kakonko katika mashamba ya Mpunga,mkoani Kigoma.
  DC Ndagala akishiriki kulima kwenye moja ya shamba linaloandaliwa kwa ajili ya kilimo cha Mpunga,katika Bonde la Katengela kijiji cha Kinonko Wilayani Kakonko katika mashamba ya Mpunga,mkoani Kigoma.


  Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagaa ,akipima kina cha maji yanayotumika katika kilimo cha umwagiliaji kwenye bonde la Katengele,wakati alipokuwa akikagua kilimo cha umwagiliaji katika Bonde hilo kijiji cha Kinonko, Wilayani Kakonko katika mashamba ya Mpunga,mkoani Kigoma.
   
   
  Na Rhoda Ezekiel-Globu ya Jamii, Kigoma.

  MKUU wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala amewaasa wakulima wa Bonde la Mto Katengela Kijiji cha Kinonko Wilayani Kakonko kulima mazao yao kwa misimu miwili ya Kiangazi na masika .Aidha pia amewashauri waanze kulima kwa kitaalamu zaidi ili wapate mazao ya kutosha.pamoja na kuwaeleza yote hayo lakini pia akawasisitizia umuhimu wa kujiunga kujiunga kwenye vyama vya ushirika na kuacha tabia ya kuuza mazao yote kutokana na hali ya hewa ya mwaka huu inayoweza kupelekea maeneo mengi kukosa chakula.

  Akizungumza na wakulima wa Bonde la Mto katengera jana wakati wa ziara yake , vijiji vya Kinonko,Nyamibuye na Rumashi Ndagala alisema wakulima wengi wamekuwa na tabia ya kuuza mazao yote na kupelekea kubaki wakilia njaa baada ya mazao yao waliyo lima kuisha ,pia wakulima wanatakiwa kuunda vikundi vya ushirika vitakavyo wasaidia kupata mikopo,pembejeo na masoko yatakayo wasaidia kuuza bidhaa zao kwa bei ya juu.

  Alisema Wakulima wakiweza kulima misimu yote miwili ya Kiangazi na masika,bonde hilo lina uwezo wa kuhudumia wananchi wote wa Kakonko kutokana na mkulima mmoja kuwa na uhakika wa kulima hekali moja na kuzalisha gunia nane  za mpunga kwa msimu mmoja wa mavuno na hali inayo weza kuikomboa wilaya hiyo isikumbwe na janga la njaa.

  Aidha Ndagala amewaomba maafisa kilimo wa Wilaya hiyo kuwawezesha wakulima kulima kwa misimu miwili na kuwapa mbinu za kulima kitaalamu kwa kutumia pembejeo zinazotolewa na Serikali, ili kuweza kupata Mazao mengi na kuweka tahadhali kutokana na hali ya hewa inayo weza kupelekea ukosefu wa mvua.

  "Nniwaombe wananchi kwa mwaka huu mlime mazao yanayo weza kustahimili ukame kama Vile mihogo, mtama na viazi na yale yanayo stawi haraka kutokana na mabadiliko ya tabia ya Nchi iliyojitokeza, hali inaweza kusababisha mwaka huu chakula kika kosekana kabisa, pia mjenge tabia ya kuhifadhi chakula msikiuze chote tusije tukaanza kuomba misaada wakati uwezo wa kuhifadhi chakula tunao",alisema Ndagala.

  Kwa upande wake Afisa kilimo wa Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko,Muhdin Alfani alisema bonde hilo lina zaidi ya kilomita 29 na linawakulima 310 na mradi wa kukamilisha ujenzi wa bonde hilo la umwagiliaji ni shilingi milioni 312 na kila hekali moja linaweza kuzalisha gunia 18 kwa msimu mmoja wa kilimo.

  Alisema lengo la Halmashauri  kuanzisha mradi huo ni kuwasaidia wananchi wa Wilaya hiyo kulima na kupata mazao ya kutosha yatakayo wasaidia kuilisha wilaya na Nchi jirani ya Burundi ambayo inategemea chakula kingi kutoka kwa Watanzania katika masoko ya ujirani mwema na kuweza kuiongezea serikali pato la taifa.

  Nao baadhi ya wakulima wa bonde hilo,Issa Masumo na Shedrack Milembe wameiomba Halmashauri hiyo kuwawezesha kupata masoko na kupangiwa bei maalumu itakayo wasaidia kuepukana na unyanyasaji wa Wafanya biashara wanaokuja kununua mpunga na kuwapunja wakulima na kukosa haki yao ya msingi wao kama wakulima.

  0 0

  Waziri wa Maji na Umwagiliaji,Mhandisi Gerson Lwenge akiotesha mti katika chanzo cha maji cha Kaloleni mjini Moshi. Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Said Meck Sadiki akiotesha mti katika chanzo cha maji cha Kaloleni. Mwenyekiti wa Bodiya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) Prof Faustine Bee akiotesha mti katika chanzo hicho. Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa MAzingira mjini Moshi (MUWSA) Joyce Msiru akiotesha mti katika chanzo cha maji cha Kaloleni.Mkuu wa wilaya ya Moshi ,Kippi Warioba akiotesha mti katika chanzo cha maji cha Kaloleni. Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

  Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya maji safi na usafi wa Mazingira mjini Moshi,Prof Faustine Bee (kushoto) akimuongoza Waziri wa Maji na Umwagiliaji ,Mhandisi Gerson Lwenge kuelekea katika chanz cha Mkashilingi kilichopo wilyani Hai kwa ajili ya uzinduzi, kulia kwa Waziri ni Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA).Joyce Msiru. Waziri wa Maji na Uwagiliaji ,Mhandisi Gerson Lwenge akizungumza wakati wa uzinduzi wa chanzo cha maji cha Mkashilingi kilichopo wilayani Hai mkoani Kilimanjaro.Baadhi ya wananchi waliohudhuria uzinduzi huo wakimsilikiliza Waziri wa Maji na Umwagiliaji (hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa chanzo cha Mkashilingi. Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Said Meck Sadiki akizungumza katika uzinduzi huo.
  Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) Joyce Msiru akimueleza jambo Waziri wa Maji na Umwagiliaji ,Mhandisi Gerson Lwenge mara baada ya kujionea chanzo cha maji cha Mkashilingi.
  Waziri wa Maji na Umwagiliaji ,Mhandisi Gerson Lwenge akiwasili atika chanzo kingine cha Kaloleni kwa ajili ya uzinduzi rasmi ,kulia kwake ni Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) Joyce Msiru.
  Chanzo cha Maji cha Kaloleni. Chumba maalumu kwa ajili ya matibabu ya maji. Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi,(MUWSA) Joyce Msiru akisoma taarifa ya mradi wa ujenzi wa chanzo cha maji cha Kaloleni. Waziri wa Maji na Umwagiliaji ,Mhandisi Gerson Lwenge akizindua mradi wa maji wa Kaloleni.

  0 0

older | 1 | .... | 1022 | 1023 | (Page 1024) | 1025 | 1026 | .... | 1898 | newer