Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46362 articles
Browse latest View live

WAZIRI WA AFYA ATOA TAMKO JUU YA VIASHIRIA NA MAABUKIZI YA UGONJWA WA UKIMWI NA MARALIA KWA TAKWIMU ZA 2011-2012

$
0
0
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na WatotoMh. Ummy Mwalimu akizungumza na waandishi wa habari wakati alipokuwa akitoa tamko la serikali kuhusu Takwimu za viashiria vya Ukimwi na Maralia mwaka 2011-2012 na kiwango cha maambukizi ya Ukimwi (VVU) kushoto kwake ni Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Mohammed Bakari Kambi.
……………………………………………………………………
Kwa mujibu wa Takwimu za Viashiria vya UKIMWI na Malaria za mwaka 2011-2012, kiwango cha maambukizi ya Virusi vya UKIMWI (VVU) nchini kinakadiriwa kuwa ni asilimia 5.1 miongoni mwa watu wazima wenye umri kati ya miaka 15 – 49. Takwimu hizi zinaashiria kwamba, kwa kila watanzania 1000, watu 51 miongoni mwao wanaoishi na maambukizi ya VVU. Inakadiriwa kuwa, kuna watu 1,400,000 wanaishi na VVU nchini Tanzania ambapo, watu 839,574 wanapatiwa tiba ya dawa za kupunguza makali ya VVU zinazotolewa katika vituo 4,000 vilikuwa vinatoa huduma hiyo nchi nzima hadi kufikia mwezi Juni mwaka huu (2016). 

Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kushirikiana na Wadau wake imechukua hatua za makusudi na za haraka katika kukabiliana na Maambukizi ya Virusi vya UKIMWI na UKIMWI. Serikali imefanikiwa kuanzisha na kutekeleza mipango mbalimbali ya kuzuia maambukizi mapya kwa kutoa huduma za kinga, tiba na matunzo kwa walioambukizwa VVU katika ngazi ya vituo vya huduma za afya na ngazi ya jamii. Mikakati yote hii imelenga kuboresha afya kwa kupunguza maambukizi mapya ya VVU na kutokomeza kabisa UKIMWI. 

Mbali na Mipango mikakati na mbinu madhubuti ambazo zimetekelezwa bado takwimu zinaonesha kuwa kiwango cha maambukizi miongoni mwa makundi maalum na yale yaliyo katika hatari zaidi ya kuambukizwa VVU yapo juu kulinganisha na kiwango kilichopo kwa jamii kwa ujumla.
Kutokana na mazingira yetu makundi maalum ni makundi yaliyo katika hatari zaidi ya kuambukiza na kuambukizwa VVU, kwa kuzingatia takwimu za maambukizi ya VVU kwa makundi haya kuwa juu, Serikali imeainisha makundi haya kama ifuatavyo:- 

Wasichana walio katika umri wa balehe walio katika mazingira hatarishi, vijana walio katika umri wa balehe, watoto yatima na watoto walio katika mazingira hatarishi (yaani watoto wanaoishi mitaani), wanaume wanaofanya ngono na wanaume wenzao, wanawake wanaofanya ngono kinyume na maumbile, watu wanaotumia dawa za kulevya hasa wale wanaotumia dawa za kulevya kwa njia ya kujidunga sindano, wanawake wanaofanya biashara ya ngono na wateja wao, wafungwa, wakimbizi na wafanyakazi wanao hamahama hasa madereva wa malori ya masafa marefu, wachimba madini na jamii zilizopo katika maeneo ya migodi, wavuvi na jamii zilizopo katika maeneo ya uvuvi, wafanyakazi wa kwenye mashamba makubwa, wajenzi wa barabara na watu wenye ulemevu. 

Kuna ushahidi wa kipiedemilojia kwa programu za VVU na UKIMWI kulenga makundi maalum. Katika nchi zilizo Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, vijana balehe wenye umri wa miaka 15 hadi 24 wanachangia asilimia 35 ya maambukizi mapya ya VVU. Aidha, kiwango kikubwa cha maambukizi ya VVU nchini Tanzania, kinaonekana miongoni mwa makundi maalum (asilimia 26 miongoni mwa Wanawake wanaofanya Biashara ya Ngono, asilimia 36 miongoni mwa wajidunga na asilimia 25 miongoni mwa wanaume wanaofanya ngono na wanaume wenzao). 

Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ilianza kutoa huduma za VVU na UKIMWI kwa makundi maalum na yale yaliyo katika hatari zaidi ya kuambukizwa na kuambukiza VVU tangu mwaka 2010 baada ya kufanya tafiti na kugundua kuwa kiwango cha maambukizi ya VVU kiko juu ikilinganishwa na makundi mengine kwenye jamii. Huduma hizi zimekuwa zinatolewa katika vituo vya kutolea huduma za afya katika ngazi ya Jamii katika Mikoa mbalimbali nchini. 

Hivi karibuni kumekuwepo na taarifa kuwa Asasi za Kiraia (za hapa nchini na za Kimataifa) zimekuwa zinapitia katika Afua ya kupambana na UKIMWI ili kuhamasisha mapenzi ya jinsia moja, na hii imepelekea Waziri wa Katiba na Sheria kutamka kupitia vyombo vya habari kuwa atavichukulia hatua za kisheria asasi hizo ambazo zinakiuka taratibu na sheria zilizowekwa na Serikali. 

Napenda kutamka kwamba, Wizara yangu halitalifumbia macho suala hili, na napenda kuziasa asasi zote za kiraia za ndani na nje ya nchi kufanya kazi kwa kufuata taratibu na sheria za nchi na kutoa afua zenye lengo la kupambana na maambukizi mapya ya VVU katika makundi haya na jamii kwa ujumla. Aidha nazitaka asasi hizo kutoa huduma bora zenye kiwango cha kimataifa lakini pia huduma zinaoendana na utamaduni, mila na desturi za Mtanzania huku zikizingatia sheria za nchi kama vile sheria ya kanuni ya adhabu, sura ya 16 kama ilivyofanyiwa marakebisho mwaka 2002. 

Tukumbuke kwamba Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ina jukumu la kutoa huduma za Afya na zile za kupambana na UKIMWI bila ubaguzi, na vilevile bila kujali jinsi, kabila, dini, hali ya kifedha, rangi au chama cha mtu yeyote. 

Baada ya kubaini changamoto katika utoaji wa huduma za Afya na zile za kupambana na UKIMWI kwa asasi zisizo za Serikali, niliitisha kikao na wadau wa maendeleo wanao fadhili na kutoa huduma za kupambana na UKIMWI katika makundi haya maalum ili niweze kutoa ufafanuzi wa mambo kadhaa ya msingi ikiwemo kuweka bayana suala la kutoa huduma za VVU kwa makundi haya huku tukizingatia taratibu na sheria za nchi (Public Health Approach to HIV programming to PK). 

Yafuatayo ni matamko niliyoyatoa na ambayo wote tunapaswa kuyazingatia:
Serikali itaendelea kutoa huduma za Afya na zile za kupambana na UKIMWI bila ubaguzi wa jinsi, kabila, dini, hali ya kifedha, rangi au chama cha mtu yeyote. 

Kwa kuwa maambukizi ya VVU kwa makundi maalum bado yapo juu ukilinganisha na jamii kwa ujumla, Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, JInsia, Wazee na Watoto itaendelea kutoa kitita cha huduma kama kitakavyopitiwa na kuainishwa na miongozo ya kutolea huduma za kupambana na UKIMWI katika makundi maalum. 

Makundi Maalum kwa mantiki ya Tanzania itabaki kuwa ya kiujumla kama yalivyo tajwa hapo juu ambayo yanaendana na mazingira ya Tanzania, hivyo maana na tafsiri hiyo ifuatwe na kuzingatiwa katika huduma au afua zinazotekelezwa na wadau wote wanao shirikiana na Serikali katika kutoa huduma za VVU na UKIMWI nchini. 

Kila mdau wakati wote atoe huduma kwa mujibu na sheria na kanuni ya adhabu sura ya 16 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002 inayotaka mtu kuchukuliwa sheria endapo atathibitika kufanya mapenzi na mtu wa jinsia moja., na kama mdau ni shirika lisilo la Serikali pia ana wajibu wa kuzingatia Sheria Na 24 ya Mwaka 2002 ya Asasi zisizo za Kiserikali, na kufuata maadili ya kazi za NGO (NGO code of conduct). 

Huduma za Makundi maalum na yale yaliyo katika hatari zaidi ya kuambukizwa na kuambukiza VVU zinazotolewa katika vituo vya kutolea huduma za afya zitaendelea kwa makundi yote isipokuwa huduma za ngazi ya jamii kwa wanaume wanaofanya ngono na wanaume wenzao, hizi zitasubiri mwongozo mpya wa utoaji wa huduma ngazi ya jamii. 

Huduma mkoba zinazotolewa na watoa huduma za afya toka vituoni zitaendelea kutolewa kwa mujibu wa miongozo iliyopo. Wizara inaweka msisitizo mkubwa katika kuunganisha huduma zinazofanana na utoaji wa rufaa katika vituo vya huduma za afya kwa mwendelezo wa huduma. Taratibu za utekelezaji zitafafanuliwa na Wizara ndani ya wiki moja. 

Kutokana na kuongezeka kwa idadi ya wadau wanaotaka kushirikiana na kuisaidia Serikali katika kutoa huduma hizi, hasa kwa kuzingatia tabia ya kuhama hama kwa makundi haya kutoka eneo moja hadi jingine, kumekuwa na mwingiliano wa huduma zinazotolewa kwa makundi haya, mwingiliao huu unahatarisha ubora wa huduma. Ili kuleta tija, uwajibikaji na uwazi, Mganga Mkuu wa Serikali ataongoza zoezi la kupanga upya wadau katika Mikoa watakayotoa huduma kwa nchi nzima. 

Asasi zote za kiraia za hapa nchini zinazotekeleza afua za VVU na UKIMWI katika Halmashauri lazima ziidhinishwe na Halmashauri husika kabla hazijaruhusiwa kufanya kazi na asasi zisizo za kiserikali za kimataifa. Kwa maneno mengine, Asasi zisizo za kiserikali za kimataifa zitapewa orodha ya asasi za kiraia zilizoidhinishwa kufanya kazi katika Halmashauri au Wilaya husika. Kanuni za Msingi za Ushirikiano (MOU) zitaandaliwa kati ya wadau watatu, yaani Asasi ya Kimataifa, Asasi ya Kiraia ya hapa nchini na Halmashauri au Wilaya husika. Nakala ya Kanuni za Msingi za Ushirikiano (MOU) ziwasilishwe Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara ya Maendeleo ya Jamii) na Tume ya Taifa ya Kudhibiti UKIMWI. 

Wakati huohuo, mkakati wa usambazaji wa vilainishi hauruhusiwi kutolewa kama afua mojawapo ya kuzuia VVU kwa sasa. Serikali inahitaji muda wa kutosha wa kujiridhisha kuhusu umuhimu wa matumizi yake kama kinga ya kuzuia VVU na pia kuhusu kukubalika katika jamii yetu. Endapo Serikali itaridhia jambo hili, basi hatua stahiki zitachukuliwa ikiwa ni pamoja na kuandaa mipango ya manunuzi na usambazaji wake ikitumia mfumo ya kusambaza vifaa tiba.

MAWAZIRI UGANDA NA TANZANIA WATEMBELEA ENEO LITAKAPOJENGWA GATI ITAKAYOTUMIKA KUPAKIA MAFUTA KUTOKA UGANDA KWENYE MELI

$
0
0
Waziri wa Nishati na Madini nchini, Profesa Sospeter Muhongo (wa Saba kushoto) na Waziri wa Nishati na Maendeleo ya Madini wa Uganda, Mhandisi Irene Muloni (wa Nane kushoto) wakiwa katika Kata ya Chongoleani mkoani Tanga ambako kutajengwa hifadhi ya mafuta pamoja na gati itakayotumika kupakia mafuta kwenye Meli mbalimbali baada ya kusafirishwa na Bomba la Mafuta kutoka nchini Uganda. 
Waziri wa Nishati na Madini nchini, Profesa Sospeter Muhongo (wa Tano kulia) na Waziri wa Nishati na Maendeleo ya Madini wa Uganda, Mhandisi Irene Muloni (wa Nne kulia) wakisalimiana na mmoja wa Wananchi katika Kata ya Chongoleani mkoani Tanga ambako kutajengwa hifadhi ya mafuta pamoja na gati itakayotumika kupakia mafuta kwenye Meli mbalimbali baada ya kusafirishwa na Bomba la Mafuta kutoka nchini Uganda
Waziri wa Nishati na Madini nchini, Profesa Sospeter Muhongo (wa Tatu kushoto mstari wa Mbele) na Waziri wa Nishati na Maendeleo ya Madini wa Uganda, Mhandisi Irene Muloni (wa Pili kushoto mstari wa mbele) wakitoka katika eneo la Chongoleani mkoani Tanga baada ya kukagua sehemu itakayojengwa hifadhi ya mafuta pamoja na gati itakayotumika kupakia mafuta kwenye Meli mbalimbali baada ya kusafirishwa na Bomba la Mafuta kutoka nchini Uganda.



Waziri wa Nishati na Madini wa Tanzania, Profesa Sospeter Muhongo na Waziri wa Nishati na Maendeleo ya Madini wa Uganda, Mhandisi Irene Muloni wametembelea eneo la Chongoleani mkoani Tanga ambako kutajengwa hifadhi ya mafuta pamoja na gati itakayotumika kupakia mafuta kwenye Meli mbalimbali ili kusafirishwa. 

Mafuta hayo yatapakiwa kwenye Meli hizo baada ya kusafirishwa na Bomba kutoka Hoima nchini Uganda kwa ajili ya kusafirishwa nje ya nchi. 

Akiwa katika eneo hilo Waziri wa Nishati na Maendeleo ya Madini wa Uganda aliwaeleza wananchi wa eneo hilo kuwa nchi ya Uganda inaishukuru Tanzania kwa kukubali Bomba hilo lipite katika ardhi ya Tanzania suala ambalo litakuwa na faida mbalimbali kwa Wananchi ikiwemo mabadiliko ya kiuchumi. 

Alisema kuwa lengo ni kuona kuwa mradi huwa huo unaanza kazi mwaka 2020 na ndiyo maagizo ambayo Marais wa nchi mbili wameyatoa kwa watendaji wanaosimamia Mradi huo wa Bomba la Mafuta. 

Mhandisi Muloni alitumia fursa hiyo kuwaasa wananchi kujiandaa kikamilifu kwa fursa za kiuchumi kwani watekelezaji wa mradi watahitaji huduma mbalimbali kama za chakula, malazi na usafiri hivyo kupitia utoaji wa huduma hizo wananchi nao watapata kipato. 

Pia alizishukuru Sekta Binafsi za Uganda na Tanzania kwa kuwa tayari kushirikiana na Serikali ili kuhakikisha kuwa mradi huo unafanikiwa akitolea mfano kampuni ya GBP ya Tanzania ambayo imeonesha nia ya kununua hisa katika kampuni itakayoanzishwa kwa ajili ya usimamizi wa Bomba hilo la Mafuta. 

Pia alizishukuru kampuni za TULLOW ya Uingereza, CNOOC ya China na TOTAL ya Ufaransa kwa kuamua kutekeleza mradi huo ambao utawezesha jumla ya mapipa laki mbili ya mafuta kusafirishwa kwa siku kupitia Bomba hilo la Mafuta lenye urefu wa kilomita 1443. 

Kwa upande Profesa Muhongo alisema kuwa Bomba hilo pia litatumika kusafirisha mafuta kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) baada ya nchi hiyo kugundua mafuta. 

Alisema kuwa Waziri kutoka DRC anayesimamia Nishati hiyo amefika nchini ili kufanya mazungumzo na Tanzania juu ya kutekeleza suala hilo ambapo inakadiriwa kuwa nchi hiyo itakuwa ikisafirisha mapipa 30,000 hadi 100,000 kwa siku kupitia Bomba hilo la Mafuta. 

Alisema kuwa Gati hiyo ya Chongoleani ina uwezo wa kupakua mafuta kwa muda wa mwaka mzima kutokana na kutokumbwa na mawimbi makubwa ya bahari ambayo hupeleka shughuli hiyo kusuasua. 

“ Ndugu zangu shughuli ya upakiaji wa mafuta katika Bandari hii itafanyika kwa muda wa mwaka mzima kwani Bandari hii haina mawimbi makubwa yatakayozuia shughuli hii kufanyika, na ndiyo moja ya vigezo vilivyotumika katika kuchagua Bandari hii kupokea mafuta kutoka Uganda,”alisemaProfesa Muhongo. 

Kwa upande wa Wananchi, baadhi ya Wananchi hao walisema kuwa wamepokea mradi huo kwa matumaini makubwa ambapo wamesema kuwa wana imani kuwa mara mradi utakapoanza wataweza kupata huduma mbalimbali ikiwemo Elimu, Afya, Miundombinu ya barabara n.k. 

Naye Profesa Muhongo aliwaasa wananchi hao kuwa na subira wakati Serikali ikiwa inafanya mipango mbalimbali ili kuhakikisha kuwa mradi huo unafanyika kwa ufanisi.

Umoja wa Walimu na Wazazi (UWW) umeondoa migogoro baina ya walimu na wazazi Mkoani Dodoma

$
0
0
Na: Lilian Lundo - MAELEZO - Dodoma

Uanzishwaji wa Umoja wa Walimu na  Wazazi (UWW) kwa shule za Msingi za Serikali Mkoani Dodoma umefanikiwa kutatua migogoro baina ya walimu na wazazi iliyodumu kwa muda mrefu mkoani humo.

Hayo yamesemwa leo, Mjini Dodoma  na Mratibu Elimu Kata wa Kigwe Wilaya ya Bahi Mkoani Dodoma Elias Milaji katika Mkutano wa Waratibu wa Elimu Kata wa Mkoa huo kuhusu Mafanikio ya uanzishwaji wa UWW katika shule za Msingi za Serikali katika Mkoa huo.

"UWW umeweza kutatua migogoro mingi iliyoko katika kata ya Kigwe, moja ya migogoro hiyo ni wazazi kugoma kushiriki mikutano ya shule kutokana na walimu kukataa kuwafuta watoto wa kike shule ili wakaolewa," alifafanua Milaji.

Aliendelea kwa kusema kuwa, baada ya uanzishwaji wa UWW katika kata hiyo migogoro imepungua kwa kiasi kikubwa na wazazi wamekuwa wakishiriki katika kufuatilia maendeleo ya masomo pamoja na mahudhurio ya watoto wao.

Kwa upande wake Mratibu Elimu Kata wa Chamwino, Chitema Simango amesema kuwa UWW umewezesha kwa kiasi kubwa ushiriki wa wazazi katika maendeleo ya shule ambapo kabla ya uanzishwaji wa Umoja huo walimu walikuwa wakiachiwa ufuatiliaji wa maendeleo ya wanafunzi pamoja na shule lakini kwa sasa wazazi na walimu wanashirikiana kwa pamoja katika kufuatilia maendeleo ya wanafunzi na shule.

Aidha UWW umeleta uwazi katika mapato na matumizi ya shule ambayo  yanabandikwa katika mbao za matangazo za shule husika na wazazi wanapewa nafasi ya kuhoji juu ya mapato na matumizi hayo.

UWW ni mpango ulionzishwa na Serikali kwa kushirikiana na Mpango wa Kuinua Ubora wa Elimu Tanzania (EQUIP-T) ukiwa na lengo la kuboresha mahusiano bora kati ya walimu na wazazi. Umoja huo mpaka sasa umeanzishwa katika mikoa ya Dodoma, Kigoma, Shinyanga, Simiyu, Tabora, Mara na  Lindi.

MUSWADA WA HUDUMA ZA HABARI USIPOTOSHWE-MSEMAJI WA SERIKALI

$
0
0
Na May samba-MAELEZO.

Mapema mwezi September mwaka huu muswada wa huduma za habari ulisomwa kwa Mara ya kwanza bungeni na kutolewa fursa kwa wadau wa habari kutoa maoni ili kuuboresha.

Takribani miezi miwili sasa imepita tangu wadau walipotakiwa kuusoma na kutoa maoni, lakini cha kushangaza wamekuja na sababu lukuki ikiwamo “ETI” kukosa muda wa kuusoma, Muswada wenye kurasa 28 tu.

Kimantiki wachambuzi wa masuala haya wanasema kuwa muswada huu unahistoria ndefu ya zaidi ya miaka 20 ambapo wadau katika sekta ya habari wamekuwa wakipigania kuipa heshima taalum hii na kuifanya kuheshimika kama fani za aina nyingine nchini.

Kwa kujua, kutojua au kwa makusudi wapo baadhi ya watu walio ndani ya tasnia ya habari na wasio wanatasnia wamekuwa wakivipotosha vifungu muhimu ndani ya muswada huu inawezekana kwa maslahi yao binafsi au kutumika na watu wenye nia mbaya na tasnia hii waliosahau maslahi mapana ya tasnia ya habari nchini.

Akizungumza kwa nyakati tofauti Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO  Bw. Hassan Abbas amesema lengo la muswada huu ni kuja na sheria itakayokuza na kuimarisha taaluma na weledi katika tasnia ya habari na kuweka mfumo wa usimamizi wa huduma za habari.

Jambo lingine lililoibua mjadala kwenye muswada huu ni kuhusu taaluma kwa waandishi wa habari ambayo imeibua hofu kwamba wanahabari wasiokuwa na kiwango cha elimu kwa ngazi ya shahada watafukuzwa, kuachishwa kazi au kutotambulika kama wanahabari.

Akilitolea ufafanuzi suala hilo Bw. Abbas amesema kuwa waandishi hawapaswi kuwa na hofu kwani kutakuwa na viwango tofauti vya utambuzi katika fani ya habari na pia kutatolewa muda wa miaka mitano kwa waandishi wa habari kujiendeleza.

Aidha Bw Abbas amesema kuwa masuala yote ya taaluma katika muswada huu yataainishwa katika kanuni zitakazoongoza tasnia hii na sio katika sheria.

Jambo la msingi kwa sasa ni kwa wadau wa habari kuungana kwa pamoja katika kutoa maoni ili kuuboresha muswada kwasababu haukandamizi bali ni muswada utaoleta mabadiliko chanya katika tasnia ya habari.

Mojawapo ya mambo yenye kuleta neema katika tasnia ni pamoja na uundwaji wa Bodi ya Ithibati ambayo lengo lake ni kuwa msimamizi wa kanuni za maadili ya wanahabari, viwango na mienendo ya kitaaluma pamoja na kuendeleza vigezo bora vya maadili na nidhamu miongoni mwa wanahabari.

Aidha, kutakuwa  na Mfuko wa Mafunzo kwa waandishi wa  habari ambao utawawezesha wanahabari kuongeza ujuzi katika fani yao na hatimaye kuleta matokeo chanya ambayo kwa namna moja au nyingine yanaweza kusaidia katika uwajibikaji wa serikali.

Muswada huu pia  utakuza na kuchangia utafiti na maendeleo katika nyanja ya habari na  kuonesha wazi namna gani tasnia hii inaenda kulikomboa taifa kwa matumizi sahihi ya kalamu za waandishi tofauti na ilivyokuwa awali hali itakayopeleka kutoka kwenye uandishi wa mazoea na kufikia uandishi wenye nia ya kuwasaidia watanzania na serikali kwa ujumla kufikia malengo yanayotakiwa.

Mswada huo pia umelenga kumlinda mwandishi wa habari kwa kumtengenezea mazingira ya kuwa na Bima na Hifadhi ya Jamii kwa kuelekeza kila mwajiri aweke Bima na kuchangia katika Mifuko ya Hifadhi za Jamii kwa ajili ya waajiriwa wote wa chombo husika.

Suala hili limekuwa likipigiwa kelele na waandishi wenyewe kwa muda mrefu hasa kutokana na wengi kukosa huduma muhimu hasa za afya kutokana na kutokuwa na bima na imeshuhudiwa waandishi wengi wakipitia wakati mgumu hasa wamapopatwa na magonjwa.

Masuala mengine yaliyomo katika mswada huo ni uanzishwaji wa Baraza huru la Habari ambalo litasaidia kukuza maadili na viwango vya taaluma baina ya wanahabari na kampuni za habari na pia litakuwa kiungo kati ya wanahabari, vyombo vya habari pamoja na wadau wa habari.

Aidha, Muswada huu pia umekusudia kuwa kiungo kati ya serikali na wananchi kwa kiasi kikubwa ambapo wananchi wataweza kueleza hisia zao juu ya utendaji wa serikali.

Rai yangu kwa wanahabari nchini ni kuacha kulalamika na kutoa sababu bila kujenga hoja zitakazoboresha muswada huu kama inavyofanywa na baadhi ya watu, serikali ina nia njema ya kulimaliza suala hili lililodumu kwa takribani miaka 20 ili hatimaye taaluma hii iweze kutambulika rasmi.

HAFLA MCHAPALO YA MIAKA 71 YA UMOJA WA MATAIFA YAFANA JIJINI DAR

$
0
0
Ziafuatazo ni picha za hafla mchapalo (Cocktail Party) ya kukata na shoka ya kusheherekea miaka 71 ya Umoja wa Mataifa tangu ulipoanzishwa iliyofanyika nyumbani kwa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez jijini Dar es Salaam ambapo mgeni rasmi alikuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni na kuhudhuriwa na wageni mbalimbali mashuhuri kutoka taasisi mbalimbali za serikali, binafsi pamoja na mabalozi wa nchi mbalimbali.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akitoa salamu za Umoja wa Mataifa katika hafla mchapalo ya kusheherekea miaka 71 ya umoja huo tangu kuanzishwa kwake kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (hayupo pichani) kuzungumza na wageni waalikwa.
Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika hafla mchapalo ya kusheherekea miaka 71 ya Umoja wa Mataifa iliyofanyika nyumbani kwa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (kulia) jijini Dar es Salaam.
Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez wakigonga 'cheers' ya kutakiana kheri na afya njema katika hafla mchapalo ya kusheherekea miaka 71 ya Umoja wa Mataifa iliyofanyika Oktoba 24, 2016 jijini Dar es Salaam.
Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez baada ya kugonga glass.
Shamra shamra za miaka 71 ya Umoja wa Mataifa zikiendelea jukwaa kuu.
Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati), Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (kulia) pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Celestine Mushy (kushoto) wakitazama 'documentary' fupi kwenye hafla hiyo.
Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati) akibadilishana mawazo na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (kulia) pamoja na Balozi wa Japan nchini Tanzania, Masaharu Yoshida.
MC wa hafla mchapalo ya miaka 71 ya Umoja wa Mataifa, Edgar Kiliba kutoka ofisi ya Mkuu wa Umoja wa Mataifa akiendesha hafla hiyo.
Wafanyakazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa wakibadilishana mawazo Anthony Rutabanzibwa (kushoto) na Amon Manyama katika hafla hiyo.
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) nchini, Awa Dabo (katikati) kwenye hafla mchapalo ya kusheherekea miaka 71 ya Umoja wa Mataifa tangu kuanzishwa kwake.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Emslies Travel Ltd. Jaffer Hirji (kushoto) wakati wa hafla mchapalo ya kusheherekea miaka 71 ya Umoja wa Mataifa tangu kuanzishwa kwake.
Baadhi ya wageni waalikwa na waheshimiwa mabalozi wakibadilishana mawazo kwenye hafla hiyo.

Mtaalamu wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) nchini, Hoyce Temu (kulia) akiwa na baadhi ya wafanyakazi wenzake na wageni waalikwa kwenye hafla hiyo.
Picha juu na chini ni baadhi ya wageni waalikwa na wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa.






Nguse Nyerere akiwa na baadhi ya Maafisa wenzake wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki katika hafla mchapalo ya kusheherekea miaka 71 ya Umoja wa Mataifa.
Edgar Kiliba (katikati) wa ofisi ya Mkuu wa Umoja wa Mataifa akibadilishana mawazo na baadhi ya wageni waalikwa kwenye hafla mchapalo ya kusheherekea miaka 71 ya Umoja wa Mataifa iliyofanyika Oktoba 24, 2016 jijini Dar es Salaam.
Wageni waalikwa wakibadilishana mawazo.
Baadhi ya wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa katika picha ya pamoja.

Baadhi ya Maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki katika picha ya pamoja.
Wafanyakazi wa Ofisi ya Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Edgar Kiliba na Beatrice Mkiramweni katika picha ya pamoja.

Baadhi ya madereva wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa katika picha ya pamoja kwenye hafla hiyo.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez katika picha ya pamoja na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angeline Mabula (Mb) katika hafla ya kushehereka miaka 71 ya Umoja wa Mataifa iliyofanyika Oktoba 24, 2016 jijini Dar es Salaam.
Geofrey Adroph BLOGGER P.O.BOX 24793, Mob: +255 755 274953 /+255 713 363965, Email: pamojapure@gmail.com. Blog: http://www.pamoja.co.tz/ DAR ES SALAAM, TANZANIA 2016-10-26 14:30 GMT+03:00 Zainul Mzige :
Ziafuatazo ni picha za hafla mchapalo (Cocktail Party) ya kukata na shoka ya kusheherekea miaka 71 ya Umoja wa Mataifa tangu ulipoanzishwa iliyofanyika nyumbani kwa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez jijini Dar es Salaam ambapo mgeni rasmi alikuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni na kuhudhuriwa na wageni mbalimbali mashuhuri kutoka taasisi mbalimbali za serikali, binafsi pamoja na mabalozi wa nchi mbalimbali.
img_3816Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akitoa salamu za Umoja wa Mataifa katika hafla mchapalo ya kusheherekea miaka 71 ya umoja huo tangu kuanzishwa kwake kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (hayupo pichani) kuzungumza na wageni waalikwa.
flk_2006Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika hafla mchapalo ya kusheherekea miaka 71 ya Umoja wa Mataifa iliyofanyika nyumbani kwa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (kulia) jijini Dar es Salaam.
flk_2009Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez wakigonga 'cheers' ya kutakiana kheri na afya njema katika hafla mchapalo ya kusheherekea miaka 71 ya Umoja wa Mataifa iliyofanyika Oktoba 24, 2016 jijini Dar es Salaam.
flk_2012Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez baada ya kugonga glass.
flk_2015Shamra shamra za miaka 71 ya Umoja wa Mataifa zikiendelea jukwaa kuu.
img_3790Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati), Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (kulia) pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Celestine Mushy (kushoto) wakitazama 'documentary' fupi kwenye hafla hiyo.
img_3894Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati) akibadilishana mawazo na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (kulia) pamoja na Balozi wa Japan nchini Tanzania, Masaharu Yoshida.
flk_2026MC wa hafla mchapalo ya miaka 71 ya Umoja wa Mataifa, Edgar Kiliba kutoka ofisi ya Mkuu wa Umoja wa Mataifa akiendesha hafla hiyo.
flk_2041Wafanyakazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa wakibadilishana mawazo Anthony Rutabanzibwa (kushoto) na Amon Manyama katika hafla hiyo.
flk_2104Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) nchini, Awa Dabo (katikati) kwenye hafla mchapalo ya kusheherekea miaka 71 ya Umoja wa Mataifa tangu kuanzishwa kwake.
flk_2121Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Emslies Travel Ltd. Jaffer Hirji (kushoto) wakati wa hafla mchapalo ya kusheherekea miaka 71 ya Umoja wa Mataifa tangu kuanzishwa kwake.
flk_2166Baadhi ya wageni waalikwa na waheshimiwa mabalozi wakibadilishana mawazo kwenye hafla hiyo.
flk_2170
flk_2045Mtaalamu wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) nchini, Hoyce Temu (kulia) akiwa na baadhi ya wafanyakazi wenzake na wageni waalikwa kwenye hafla hiyo.
flk_2086Picha juu na chini ni baadhi ya wageni waalikwa na wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa.
flk_2258
flk_2091
flk_2083
flk_2085
flk_2156
flk_2096
flk_2134Nguse Nyerere akiwa na baadhi ya Maafisa wenzake wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki katika hafla mchapalo ya kusheherekea miaka 71 ya Umoja wa Mataifa.
flk_2106Edgar Kiliba (katikati) wa ofisi ya Mkuu wa Umoja wa Mataifa akibadilishana mawazo na baadhi ya wageni waalikwa kwenye hafla mchapalo ya kusheherekea miaka 71 ya Umoja wa Mataifa iliyofanyika Oktoba 24, 2016 jijini Dar es Salaam.
flk_2049Wageni waalikwa wakibadilishana mawazo.
flk_2065Baadhi ya wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa katika picha ya pamoja.
flk_2160
flk_2142Baadhi ya Maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki katika picha ya pamoja.
flk_2070Wafanyakazi wa Ofisi ya Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Edgar Kiliba na Beatrice Mkiramweni katika picha ya pamoja.
flk_2074
flk_2139Baadhi ya madereva wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa katika picha ya pamoja kwenye hafla hiyo.
img_3962Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez katika picha ya pamoja na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angeline Mabula (Mb) katika hafla ya kushehereka miaka 71 ya Umoja wa Mataifa iliyofanyika Oktoba 24, 2016 jijini Dar es Salaam.

WIZARA YA HABARI YAPOKEA VIFAA VYENYE THAMANI ZAIDI YA SH.MILIONI 20 KUTOKA UBALOZI WA CHINA NCHINI.

$
0
0
Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Bw. Petro Lyatuu akipokea Luninga kutoka kwa Mshauri wa masuala ya Utamaduni kutoka Ubalozi wa China hapa nchini Bw Gao Wei wakati wa makabidhiano ya. Vifaa vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 20 kutoka Ubalozi wa China nchini kwa ajili ya maendeleo ya Sekta ya Sanaa leo Jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Wizara hiyo , kulia ni Kaimu Mkurugenzi Maendeleo ya Sanaa Bibi Leah Kihimbi. 

. Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Bw. Petro Lyatuu akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa makabidhiano ya Vifaa vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 20 kutoka Ubalozi wa China nchini kwa ajili ya maendeleo ya Sekta ya Sanaa leo Jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Wizara hiyo ,kushoto ni Mshauri wa masuala ya Utamaduni kutoka Ubalozi wa China Bw.Gao Wei, na Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Maendeleo ya Sanaa Bibi Leah Kihimbi. 





Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Bw. Petro Lyatuu (Katikati ) akimshukuru Mshauri wa Masuala ya Utamaduni kutoka Ubalozi wa China Bw Gao Wei kutokana na msaada wa Vifaa walivyotoa kwa Wizara kwa ajili maendeleo ya Sekta ya Sanaa leo Jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Wizara hiyo, kulia ni Kaimu Mkurugenzi Maendeleo ya Sanaa wa Wizara Bibi Leah Kihimbi.
Kaimu Mkurugenzi Maendeleo ya Sanaa wa Wizara ya Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Bibi Leah Kihimbi (Kulia) akitoa neno la Shukrani kwa Ubalozi wa China hapa nchini baada ya kupokea Vifaa vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 20 kutoka Ubalozi wa China nchini kwa ajili ya maendeleo ya Sekta ya Sanaa leo Jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Wizara hiyo ,katikati ni Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara Bw. Petro Lyatuu, na kulia ni Mshauri wa Masuala ya Utamaduni kutoka Ubalozi wa China Bw. Gao Wei.

…………………………………………………………………..

Na Shamimu Nyaki-WHUSM.

Ubalozi wa China nchini umeipatia Wizara ya Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo vifaa vya ofisi vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 20 ikiwa ni kuendeleza ushirikiano uliopo baina ya Serikali hizo mbili.

Hatua hiyo imekuja ikiwa na lengo la kusaidia katika kukuza na kuendeleza sekta ya sanaa ambayo katika mpango wa miaka mitano ya maendeleo ya Serikiali inatakiwa kuongeza ajira pamoja na pato la taifa kupitia kazi mbalimbali za sanaa.

Akizungumza wakati wa makabidhiano ya vifaa hivyo leo Jijini Dar es Salaam Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Bw. Petro Lyatuu aliushukuru Ubalozi huo kwa mchango wao wa kuhakikisha sekta ya sanaa inakuwa na kuleta mabadiliko nchini.

“Tunashukuru Ubalozi wa China kwa kutupatia vifaa hivi ambavyo vitasaidia sana utendaji katika Sekta ya Sanaa ambayo inaendelea kukua kwa kasi hapa chini na kusaidia kuimarisha ushirikiano mzuri baina ya Serikali yetu na China”Alisema Bw. Petro Lyatuu.

Naye Mshauri wa masuala ya Utamaduni kutoka Ubalozi huo Bw Gao Wei amesema kwamba China itaendelea kutoa ushirikiano kwa Wizara katika kuendeleza Sanaa kwa kutoa misaada mbalimbali kwa kadri itakavyohitajika.

“Tutaendelea na ushirikiano huu sio tu kwa kutoa msaada wa vifaa bali pia kubadilishana uzoefu na taaluma ya Sanaa ili Sekta hii ikue na kuheshimika na kutambulika rasmi kama ajira ”Alisema Bw Gao.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Sanaa Bibi Leah Kihimbi amesema kuwa vifaa hivyo vitaimarisha utendaji kazi wa Sekta ya Sanaa ukizingatia kuwa ni Sekta ambayo imebeba dhamana kubwa ya kutangaza Sanaa ndani na nje ya nchi.

Vifaa vilivyotolewa na Ubalozi wa China ni pamoja na Komputa 4,Komputa Mpakato 1,Kamera ya video moja na Luninga vyote vikiwa na jumla ya dhamani zaidi ya milioni 20.

NI KINYUME CHA SHERIA KUMUWEKA MTU NDANI KWA ZAIDI YA MASAA 24

$
0
0
Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria, Mohamed Mchengerwa akifungua kongamano la siku mbili la kitaifa la msaada wa kisheria kutoka mikoa yote ya Tanzania bara na visiwani linalofanyika mjini Dodoma.

KITENDO cha jeshi la polisi kuwaweka ndani mahabusu zaidi ya saa 24 bila kuwapeleka mahakamani au kuwapa dhamana ni ukiukwaji wa sheria na uvunjifu wa ,katiba ya nchi.Hayo yalisemwana leo Dodoma na Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria, Mohamed Mchengerwa alipokuwa akifungua kongamano la siku mbili la kitaifa la msaada wa kisheria kutoka mikoa yote ya Tanzania bara na visiwani.

“Ni kinyume cha sheria kuweka watu ndani zaidi ya muda uliwekwa kisheria. Lakini watanzania wengi hawajua hili…hii inatokana na uelewa finyu wa naswala ya kisheria,” alisema Mchemgerwa, wakati wa ufunguzi wa kongamano hilo liloandaliwa na Shirika la Legal Services Facility (LSF).
Alisema wapo watu ambao wanakutana na matatizo mbalimbali pamoja na kuwekwa ndani bila ya makosa kutokana na kutokujua sheria.

Mchengerwa alisema watu wengi hawajui kama kuna dhamana ya polisi ambapo mtuhumiwa hatakiwi kukaa mahabusu zaidi ya saa 24 bila kupelekwa mahakamani au kupewa dhamana.Katika kongamano hilo,Mchengerwa alisema watoa msaada wa kisheria wanatakiwa kutoa msaada huo katika kila wilaya hususani maeneo ya mjini na vijijini.

"Wapo watu ambao wako gerezani na hawana kosa lakini kutokana na tatizo la uelewa mdogo wa kisheria wamekuwa wakifungwa.
Abdullkarim Saidi, mmoja watoa msaada wa kisheria kutoka Zanzibar akizungumza kwa niaba ya wasaidizi wa kisheria wa visiwani Zanzibar.

"Jamii bado haijui kama kuna dhamana ya polisi pia ni kosa la kisheria kumweka mahabusu mtuhumiwa zaidi ya saa24 bila kumpeleka mahakamani au kumpatia dhamana"alieleza.

Aliwataja wasaidizi wa kisheria kama nguzo muhimu ya kuwasaidia kuelemisha watanzania kuhusu maswala haya ya kisheria na jinsi ya kupata haki zao pindi wanapopatwa na matatizo mbalimbali ya kisheria.

Kwa upande wake mmoja wa watoa msaada wa kisheria kutoka Zanzibar, Abdullkarim Saidi alisema licha ya kazi kubwa wanayofanya ya kutoa msaada wa kisheria, wasaidizi wa kisheria nchini bado wanakabiliwa na changamoto nyingi.
Washiriki wa Kongamano la Kitaifa la Wasaidizi wa Kisheria walioshiriki kongamano hilo linalomalizika mjini Dodoma leo.

Alisema changamoto hizo ni pamoja na kukosekana kwa usafiri pamoja na fedha za kuendesha shughuli zao kwa ufanisi, na kuongeza kuwa “tunafanya kazi katika mazingira ambayo si rafiki kutokana na kutembea kwa umbali mrefu.”

Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa LSF Bw. Kees Groenendijk amesema shirika lake limeweka mikakati madhubuti ya kuwasaidiza wasaidizi wa kisheria waweze kufanya kazi zao kwa ufanisi zaidi, ikiwa ni pamoja na kuwawezesha kifedha na kitaaluma ili waweze kuwasaidia na kuwafikia watanzania wengi zaidi wenye matatizo mbalimbali ya kisheria.

Kwa mujibu wa Kees, mpaka sasa shirika la LSF limeshatoa zaidi ya shilingi billion 20 kwa mashirika mbalimbali yanajishughulisha na utoaji wa huduma za kisheria—lengo kuu likiwa ni kuwasaidia watanzania kupata haki zao.

Ramadhani Masele, Progamme Meneja wa LSF, akifafanua jambo wakati wa uzinduzi wa Kongamano la wasaidizi wa kisheria Dodoma.
Wasaidizi wa kisheria wakiimba wimbo wa mshikamano wakati wa uzinduzi wa kongomano la wasaidizi wa kisheria Dodoma.
Scholastica Jullu, Programme Meneja wa LSF, akiongea wakati wa Kongamano la wasaidizi wa kisheria Dodoma.
Wasaidizi wa Kisheria wakiwa katika picha ya pamoja baada ya uzinduzi wa Kongamano la wasaidizi wa kisheria lililofanyika siku mbili mjini Dodoma 25-26, 2016 na kumalizika leo.

MUSWADA WA HABARI UTATOA FURSA KWA CHOMBO CHA HABARI KUOMBA RADHI PASIPO KUCHUKULIWA HATUA NA MAMLAKA ZINAZOHUSIKA

$
0
0
Mkurugenzi wa Habari, Hassan Abbas akifanya mahojiano ya kipindi maalum cha heloo Tanzania kinachorushwa hewani na kituo cha redio Uhuru FM cha Jijini Dar es Salaam wakati wa ziara yake ya kutembelea vyombo vya habari leo Jijini humo. Kushoto ni mtangazaji wa kipindi hicho, Sheila Simba.
Mkurugenzi wa Habari, Hassan Abbas akibadilishana mawazo na Mtangazaji wa kipindi cha heloo Tanzania kinachorushwa hewani na kituo cha redio cha Uhuru FM, Sheila Simba wakati wa ziara ya kutembelea vyombo vya habari leo Jijini humo leo Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Habari, Hassan Abbas akibadlishana mawazo na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Redio Uhuru FM cha Jijini Dar es Salaam, Angel Akilimali ikiwa ni sehemu ya mwendelezo ya ziara yake ya kutembelea vyombo vya habari leo Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Habari, Hassan Abbas (katikati) akizungumza na wahariri na waandishi wa gazeti la Uhuru wakati wa ziara yake ya kutembelea vyombo vya habari leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Kaimu Mhariri Mtendaji wa Gazeti hilo, Ramdhani Mkoma na kulia ni Afisa Habari Mwandamizi wa Idara Habari( MAELEZO), Jonas Kamaleki.
Mkurugenzi wa Habari, Hassan Abbas akimsalimu mwandishi mwandamizi wa habari za michezo wa gazeti la uhuru, Sophia Ashery wakati wa ziara yake ya kutembelea vyombo vya habari leo Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Habari, Hassan Abbas akimsalimu mwandishi mwandamizi wa gazeti la uhuru, Njumai Ngota wakati wa ziara yake ya kutembelea vyombo vya habari leo Jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mhariri Mtendaji wa gazeti la Uhuru, Ramadhani Mkoma akimpatia maelezo kuhusu uhifadhi wa magazeti ya zamani kwa Mkurugenzi wa Habari, Hassan Abbas wakati wa ziara yake ya kutembelea vyombo vya habari leo Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Wahariri wa Gazeti la Uhuru wakifuatilia kwa makini mkutano wa mazungumzo baina yao na Mkurugenzi wa Habari, Hassan Abbas wakati wa ziara yake ya kutembelea ofisi za gazeti hilo leo Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Habari, Hassan Abbas akizungumza wakati wa mkutano wake na bodi ya uhariri wa gazeti la uhuru wakati wa ziara yake ya kutembela ofisi za gazeti hilo leo Jijini Dar es Salaam. Wengine kutoka kushoto ni Mhariri wa Picha, Yassin Kayombo na Mhariri wa Habari Abdallah Kimweri.
Mkurugenzi wa Habari, Hassan Abbas akisalamiana na Mhariri msanifu kurasa wa gazeti la Uhuru, Jane Mihanji mara baada ya kumaliza mazungumzo yake na Bodi ya Uhariri ya gazeti hilo leo Jijini Dar es Salaam.

………………………………………..

Na Beatrice Lyimo-MAELEZO.

Dar es Salaam.

SERIKALI imesema muswada wa sheria ya huduma ya habari utatoa fursa kwa vyombo vya habari kuiomba radhi jamii radhi kwa jamii pindi wanapoandika habari zenye upotoshaji na hawatochukuliwa hatua za kisheria kutoka katika mamlaka zinazohusika.

Akizungumza katika mwendelezo wa ziara yake katika vyombo vya habari leo Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Habari, Hassan Abbas alisema hakuna haja ya waandishi wa habari kuuhofia muswada huo kipengele na badala yake wausome na kuelewa na kisha watoe maoni yao ili kuuboresha zaidi.

“Sifa moja ya taaluma ya habari ni kufuata maadili hivyo muswada umetoa fursa kwa mwanahabari kukanusha na kueleza ulichokosea hivyo mwandishi hatashtakiwa endepo akiona amekosea na kusahihisha ikiwemo kuomba radhi” alifafanua Mkurugenzi Abbas.

Kwa mujibu wa Abbas alisema kutakuwa na bodi maalumu itakayosimamia masuala ya maadili kwa waandishi wa habari nchini na hivyo kutoa fursa kwa waandishi hao kuhojiwa na kutoa ufafanuzi wa jambo husika.

Aidha Abbas alisema kuwa ipo misingi ya haki ya habari iliyoanishwa katika mikataba ya kimataifa ikiwemo kifungu cha 19 cha mkataba wa geneva wa mwaka 1966 umeeleza kuhusu haki ya kupata habari na taarifa ingawa upo ukomo katika masuala kadhaa ikiwemo suala la usalama wa taifa.

Aidha Abbas aliongeza kuwa muswada huo umelenga kulinda maslahi na usalama wa wanahabari kwani unazungumzia hali halisi ya mwandishi wa habari ukilinganisha na Sheria ya Magazeti ya mwaka 1976 inayozungumzia haki ya chombo cha habari pekee.

Mkurugenzi Abbas alisema kila taaluma duniani ina bodi yake hivyo imefika wakati kwa Tanzania napo kuwa na bodi ya wanahabari ili kuweza kuitendea haki taaluma ya habari.

WAZIRI MWIGULU NCHEMBA AFANYA MAZUNGUMZO NA MABALOZI WANNE KUTOKA NCHI MBALIMBALI, JIJINI DAR ES SALAAM LEO

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba akimkaribisha ofisini kwake Balozi wa Norway nchini, Hanne-Marie Kaarstad (kushoto) kwa ajili ya kufanya mazungumzo naye kuhusu masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Norway na Tanzania. Mazungumzo hayo yalifanyika katika ofisi ya Waziri huyo, jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Balozi Simba Yahya. Picha na zote Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba akimfafanulia jambo Balozi wa Japan nchini, Ian Myles (wapili kulia) wakati Balozi huyo alipomtembelea ofisini kwake, jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kujadiliana masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na Japan. Wapili kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Balozi Simba Yahya. Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango wa Wizara hiyo, Haji Janabi, na kulia ni Msaidizi wa Balozi huyo, Pascale Julien. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba akimfafanulia jambo Balozi wa Norway hapa nchini, Hanne-Marie Kaarstad (kulia) wakati Balozi huyo alipomtembelea Waziri Nchemba ofisini kwake, jijini Dar es Salaam leo kwa ajili ya kujadili masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na Norway. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba akimsikiliza Balozi wa India hapa nchini, Sandeep Arya (kulia) wakati Balozi huyo alipomtembelea Waziri huyo ofisini kwake, jijini Dar es Salaam leo kwa ajili ya kujadili masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na India. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba akimfafanulia jambo Balozi wa Rwanda, Eugene Kayihura (kulia) wakati Balozi huyo alipomtembelea Waziri Nchemba ofisini kwake, jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kujadili masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na Rwanda. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba akipokea zawadi kutoka kwa Balozi wa India nchini, Sandeep Arya (kulia) mara baada ya Balozi huyo kumaliza mazungumzo na Waziri ambayo yalifanyika ofisini kwake, jijini Dar es Salaam leo. Mazungumzo hayo yalikuwa na lengo la kujadili masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na India. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba akimsindikiza Balozi wa Rwanda, Eugene Kayihura (kulia) mara baada ya kumaliza mazungumzo yao, yaliyofanyika ofisini kwa Waziri huyo, jijini Dar es Salaam leo. Lengo la mazungumzo hayo ni kujadili masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya nchi jirani ya Rwanda na Tanzania. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Pikipiki zawaongeza ufanisi wa kazi Waratibu Elimu Mkoa wa Dodoma

$
0
0
Mratibu elimu kata katika kata ya Litura Halmashauri ya wilaya ya Mbinga vijijini mkoani Ruvuma, Nicodem Hyera akijaribu kuwasha moja kati ya pikipikialiyokabidhiwa na kiongozi wa mbio za Mwenge.

…………………………………

Na Lilian Lundo – MAELEZO – Dodoma

Ugawaji wa Pikipiki kwa Waratibu Elimu Kata Mkoa wa Dodoma umeleta mafanikio makubwa katika nyanja ya elimu na kuongeza kiwango cha ufaulu ndani ya mkoa huo.

Hayo yamesemwa na Mratibu Elimu Kata wa Sanzawa Wilaya ya Chemba Sweetbert Malimi, leo Mjini Dodoma katika semina ya Waratibu Elimu inayoendelea Mjini hapo.

“Pikipiki imeniwezesha kushughulikia kwa wakati matatizo yanayotekea katika shule ninazozisimamia, vilevile kufuatilia kwa wakati maendeleo ya taaluma ya wanafunzi pamoja na ufundishaji wa walimu”, alifafanua Malimi.

Ufuatiliaji huo umeletea mafanikio makubwa katika Mkoa wa Dodoma, ambapo ufaulu wa darasa la saba kwa wilaya ya Chemba peke yake ulipanda kutoka asilimia 30 mwaka 2015 mpaka asilimia 46 mwaka 2016.

Kwa upande wake Mratibu Elimu Kata wa Songambele iliyoko Wilaya ya Kongwa amesema kuwa katika kata yake ana shule Sita za kuzifuatilia ambapo kabla ya kupata pikipiki alikuwa anatumia baiskeli kutembelea shule hizo na aliweza kutembelea shule hizo mara moja kwa wiki.

Aliendelea kwa kusema kuwa, baada ya kupata pikipiki anauwezo wa kutembelea shule hizo mara tatu hadi nne kwa wiki akifuatilia maandalio ya walimu, maazimio ya kazi, utengenezaji wa zana za kufundishia, mahudhurio ya wanafunzi pamoja na kuhudhuria vikao vya kamati ya shule.

Aidha amesema kuwa, kutokana na ufuatiliaji huo wa mara kwa mara katika shule hizo kumepelekea umakini mkubwa wa ufundishaji wa walimu kwa kufuata taratibu za ufundishaji kama vile kuwa na maandalio, maazimio ya kazi pamoja na kuwa na zana za ufundishaji. Serikali kwa kushirikiana na Mpango wa Kuinua Ubora wa Elimu Tanzania (EQUIP-T) ilitoa jumla ya Pikipiki 192 kwa Waratibu Elimu Kata wote wa Mkoa wa Dodoma mwaka 2014 na 2015. Pikipiki hizo zimekuwa zikitumika na Waratibu hao kufuatilia maendeleo ya taaluma ya shule

MTENDAJI MKUU TEMESA AWATAKA WAFANYAKAZI WA MV TANGA KUZINGATIA USALAMA WA ABIRIA.

$
0
0

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dkt. Mussa Mgwatu (katikati) akitoa maelekezo ya kiutendaji kwa Meneja Msaidizi TEMESA Tanga Mhandisi Mahangaiko Ngoroma (kushoto) alipotembelea kituo hicho, kulia ni Mhasibu wa TEMESA Tanga Bw. Lusenga David.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dkt. Mussa Mgwatu (kushoto aliyesimama) akizungumza na watumishi wa TEMESA Tanga wakati alipotembelea kituo hicho kuangalia hali ya utendaji kazi, kulia ni Meneja Msaidizi TEMESA Tanga Mhandisi Mahangaiko Ngoroma.

Picha zote na Theresia Mwami TEMESA Tanga

……………………………………………….

Na Theresia Mwami TEMESA TANGA

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu amewataka wafanyakazi wa kivuko cha Mv Tanga kuzingatia usalama wa abiria kwa kufata kanuni na Sheria za usafirishaji wa abiria kupitia vivuko.

Amesema hayo alipotembelea na kuongea na watumishi wa kivuko cha MV. Tanga kinachosafiri kati ya Pangani na Bweni na kuwasisitiza watumishi hao juu ya suala la usalama wa abiria na kuwa waaminifu katika ukusanyaji wa mapato ya kivuko hicho.

Ndugu zangu hapa tunabeba roho za watanzania wenzetu tuwe makini sana na kuzingatia Sheria na taratibu zilizopo ili kuhakikisha usalama wa hawa abiria tunaowahudumia” Alisisitiza Dkt Mgwatu.

Kwa upande wake Meneja Msaidizi TEMESA Tanga Mhandisi Mahangaiko Ngoroma amemuahakikishaia Mtendaji Mkuu kuwa watazingatia taratibu na Sheria zilizopo ili kuhakikaisha usalama wa abiria wanaowahudumi kupitia kivuko cha Mv Tanga na vivuko vingine vilivyopo mkoani Tanga.

Aidha kwa upande wao watumishi wa Mv Tanga wamemwaomba Mtendaji Mkuu kuwasaidia kutatua changamoto mbalimbali zilizopo zikiwepo uhaba wa vifaa kwa ajili ya kutekeleza majukumu yao ya kila siku.

Mtendaji Mkuu wa TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu yuko katika ziara ya kikazi kutembelea vituo vilivyopo kanda ya Kaskazini kuangalia utendaji kazi wake na kuona changamoto zilizopo ili ziweze kupatiwa ufumbuzi kwa maendeleo ya Wakala huyo.

Mboni Masimba aja na Sauti ya Mwanamke

$
0
0
Mtangazaji wa Kipindi cha "The Mboni Show" kinachoruka kupitia kituo cha televisheni TBC1, Mboni Masimba ameandaa kongamano la kuwahamasisha wanawake aliloliita  Sauti ya Mwanamke lenye lengo la kuwapa uwezo wa kujikomboa kiuchumi.

Katika  kongamano hilo litakalofanyika mkoani Mwanza Novemba 6, mwaka huu katika Hoteli ya Gold Crest,  wanawake mbalimbali waliofanikiwa kiujasiriamali, kibiashara na kielimu watakuwepo kuzungumza na wanawake  wa jiji hilo kwa kiingilio cha Sh40,000.

Masimba anasema kwa kiingilio hicho wanawake wa Mwanza
 watapata elimu, burudani pamoja na chakula.

"Atakuwepo Shekha Nasser ambaye ni mmiliki wa Shear Illusion na Mwanzilishi wa Manjano Foundation huyu amefanikiwa sana kwenye biashara, atakuwepo Mkandarasi Maida Waziri pamoja na Biubwa Ibrahim ambaye ana Kampuni ya  Namaingo Agri_Busness Agency inayowawezesha watu mbalimbali katika masuala ya kilimo," amefafanua Masimba.

Anaongeza kuwa pamoja na kupata elimu ya biashara na ujasiriamali, maarifa kuhusu maisha na nyumba yatatolewa na wawezeshaji maarufu Bi Chau na Bi Fatma.“Wanawake mnapokutana lazima mbadilishane ujuzi wa kila aina, hatutawaacha hivi hivi wanawake wa Mwanza, tumemuandaa Bi Chau na Bi Fatma kuwafunda yale mambo yetu,” anafafanua.

Shughuli yoyote ya wanawake bila burudani haiwezi kunoga ndiyo maana Masimba anawapeleka Mwanza, Isha Mashauzi na mchekeshaji Katarina Karatu kuifanya siku hiyo iwe nzuri.Masimba anasema sherehe itaendeshwa na mshereheshaji maarufu nchini Mc Zipompapompa.

“Tunaanzia Mwanza, lakini kongamano letu litakwenda nchini kote, tunataka kuwakomboa kifikra wanawake wa Kitanzania, Sauti ya Mwanamke ni  sauti ya jamii, ipewe nafasi,” anasema Masimba.

PROF. MBARAWA AZINDUA BODI YA WAKURUGENZI YA SHIRIKA LA POSTA.

$
0
0

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akikata utepe kwenye begi lilobeba vitendea kazi vya wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Posta katika uzinduzi wa bodi hiyo uliofanyika jijini Dar es salaam. Anayeshuhudia kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano), Prof. Faustin Kamuzora.
Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Posta wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa katika uzinduzi wa bodi hiyo uliofanyika jijini Dar es salaam.


Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akifafanua jambo kwa wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Posta katika uzinduzi wa bodi hiyo uliofanyika jijini Dar es salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano), Prof. Faustin Kamuzora akisoma taarifa ya utekelezaji wa Shirika la Posta kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa katika uzinduzi wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika hilo uliofanyika jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Posta Dkt. Haruni Kondo akisoma taarifa ya uendeshaji wa Shirika hilo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa katika uzinduzi wa bodi hiyo uliofanyika jijini Dar es salaam.
Baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Posta wakimsikiliza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa katika uzinduzi wa bodi hiyo uliofanyika jijini Dar es salaam.
…………………………………………………………..

Na Daudi Manongi,MAELEZO

Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa ameitaka Bodi teule ya Shirika la Posta kutumia fursa zilizopo ili kuongeza vyanzo vya mapato vya Shirika hilo.

Profesa Mbarawa ameyasema hayo wakati akizindua Bodi mpya ya wakurugenzi ya Shirika la Posta katika ukumbi wa Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano leo Jijini Dar es Salaam.

“Nashukuru kwa kuwa mmekubali uteuzi wangu,mmekuja katika shirika zuri na hivyo kama mtajipanga mtaweza kufanya mambo mengi makubwa,naitaji mtu anayeweza kutafta mapato na shirika hili la Posta lina vyanzo vingi lakini bado halijatumika vizuri na hivyo naomba mbadilishe mtazamo wa watu wetu ili msonge mbele” Alisema Prof Mbarawa.

Aidha Waziri Mbarawa ameitaka bodi iyo kuisimamia vizuri menejimenti ya Shirika la Posta ili ifanye kazi kwa ufanisi mkubwa na pia amemuagiza mwenyekiti wa bodi hiyo ya wakurugenzi kuwekeana mkakati wa mikataba ya kazi na malengo ili kupata matokeo mazuri na amesisitiza kuboreshwa kwa mahusiano kati ya watendaji wa juu na wafanyakazi wa chini.

Waziri Mbarawa ameagiza bodi iyo teule kusimamia huduma mpya ya Posta mlangoni na Huduma Center kwa uadilifu ili vilete tija kama ilivyokusudiwa na kuihakikishia bodi iyo kuwa serikali imejipanga kulipa Deni la kampuni iyo ili kupunguza mzigo wa utendaji wa shirika hilo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Posta Luteni kanali Msaafu Haruni Kondo amemhakikishia waziri uyo kuwa wataisimamia vyema menejimenti ya Shirika hilo na kuhakikisha vyanzo vya mapato vinapatikana kama alivyoagiza kwani utekezaji wa majukumu ndio msingi wa maendeleo wa shirika hilo.

TRA YAFUNGUA OFISI MPYA KIMARA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania ( TRA) Bw. Alphayo Kidata – (Mwenye suti ya bluu katikati) pamoja na Kamishna wa Kodi za Ndani TRA Bw. Elijah Mwandumbya (Kushoto kwake) wakiwa katika picha ya pamoja na walipakodi waliofika katika Ofisi Mpya ya TRA Kimara ili kuhakiki Namba zao za Utambulisho wa Mlipakodi –TIN. Ofisi hiyo imezinduliwa leo tarehe 26 Oktoba 2016 na Kamishna Mkuu wa TRA ili kuwafikia wananchi kwa karibu zaidi na kuboresha huduma mbalimbali za Kodi.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania ( TRA) Bw. Alphayo Kidata akikata utepe kama ishara rasmi ya uzinduzi wa ofisi mpya ya TRA iliyoko Kimara Mwisho leo Tarehe 26 Oktoba 2016, Kushoto kwake ni Kamishna wa Kodi za Ndani TRA Bw. Elijah Mwandumbya pamoja na Wakurugenzi wengine wa TRA wakishuhudia tukio hilo

Meneja wa TRA Kinondoni Bw. Wallace Mnkande (anayeongea kwa vitendo) akitoa maelezo ya kituo hicho kipya kwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Alphayo Kidata (aliyeketi) wakati wa uzinduzi wa ofisi hiyo. Wengine kutoka kulia ni Kamishna wa Kodi za Ndani TRA Bw. Elijah Mwandumbya, Naibu Kamishna wa Kodi za Ndani Bw. Abdul Zuberi, Meneja wa Majengo Gerald Mwikuka, Mkurugenzi wa Rasilimali Watu Bw. Gerald Mwanilwa na Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi Bw. Richard Kayombo.
:Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania ( TRA) Bw. Alphayo Kidata akisalimiana na baadhi ya walipakodi waliofika katika ofisi mpya ya TRA iliyoko eneo la Kimara Mwisho ili kuhakiki Namba zao za Utambulisho wa Mlipakodi –TIN wakati wa uzinduzi wa ofisi hiyo.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania ( TRA) Bw. Alphayo Kidata akiongea na baadhi ya walipakodi waliofika katika ofisi mpya ya TRA-Kimara Mwisho ili kuhakiki Namba zao za Utambulisho wa Mlipakodi –TIN wakati wa uzinduzi wa ofisi hiyo.
Kamishna wa Kodi za Ndani TRA Bw. Elijah Mwandumbya akimweleza jambo Kamishna Mkuu wa TRA Bw. Alphayo Kidata alipotembelea ofisi mpya za TRA Kimara Mwisho kwa ajili ya uzinduzi rasmi wa ofisi hiyo.
Meneja wa TRA Kinondoni Bw. Wallace Mnkande akimwonesha jambo Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Alphayo Kidata (kushoto kwake) alipotembelea ofisi ya TRA Kimara Mwisho wakati wa uzinduzi huo uliofanyika tarehe 26 Oktoba 2016

…………………………………………………………

Katika jitihada za kuboresha huduma kwa walipakodi na kuzifikisha huduma hizo kwa karibu zaidi Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania ( TRA) Bw. Alphayo Kidata amezindua ofisi mpya ya TRA katika eneo la Kimara Mwisho jijini Dar es Salaam Tarehe 26 Oktoba 2016 itakayotoa huduma zote za kikodi ikiwemo usajili na uhakiki wa Namba za Utambulisho wa Mlipakodi –TIN, Usajili wa Kodi ya Ongezeko la Thamani-VAT, Malipo ya Kodi za Magari, Kodi zote za Mapato zikiwemo Kodi za Makampuni, Watu Binafsi, Wafanyakazi (PAYE), Kuendeleza Ufundi Stadi – SDL, VAT, Ushuru wa Stampu na huduma nyingine za kikodi.

Akizungumza na walipakodi waliofika katika ofisi hiyo kupata huduma wakati wa uzinduzi, Bw. Kidata aliwashukuru kwa mwitikio wao katika zoezi la uhakiki wa taarifa za TIN ambao utaisaidia Mamlaka kupata idadi sahihi ya walipakodi ili kuondoa walipakodi hewa ikiwa ni pamoja na kuboresha huduma za ulipaji kodi.

“Zoezi hili litaongeza ufanisi katika suala zima la usimamizi na ukusanyaji kodi kwa kiwango cha juu” Alisema Bw. Kidata

Kamishna Mkuu wa TRA aliwataka walipakodi hao wanaoishi maeneo ya karibu na ofisi hiyo mpya ya TRA iliyopo Kimara Mwisho kuendelea kujitokeza kwa wingi ili kupata huduma mbalimbali za kikodi ikiwemo uhakiki wa taarifa zao TIN kabla ya tarehe ya mwisho wa zoezi hilo kwa Mkoa wa Dar es Salaam ambayo ni tarehe 30 Novemba 2016.

Aidha Kamishna wa Kodi za Ndani TRA Bw. Elijah Mwandumbya alisema TRA imejipanga kuhakikisha inaendelea kuboresha huduma zake na kuwafikia walipakodi kwa ukaribu zaidi ili kuondoa usumbufu na kuokoa muda wa upatikanaji wa huduma hizo.

“TRA kwa kuhakikisha walipakodi wanapata huduma iliyo bora imeanzisha vituo vingi vya kodi katika jiji la Dar es Salaam na nchi nzima ili walipakodi wapate huduma stahiki na ya haki na kuiwezesha Serikali kupata mapato yake kwa mendeleo ya Taifa letu” Alisema Bw. Mwandubya.

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU

$
0
0


UTOAJI WA MIKOPO KWA WANAFUNZI MWAKA 2016/2017
Baada ya kukamilisha zoezi la Uchambuzi wa maombi ya Mikopo 88,163 yaliyopokelewa hadi kufikia 11 Agosti, 2016. Jumla ya Wanafunzi wapya 20,183 wamepangiwa Mikopo. Upangaji huu umezingatia vigezo vilivyomo katika mwongozo wa  utoaji wa mikopo uliopitishwa na Bodi ya wakurgezi na kuidhinishwa na wizaya ya elimu sayannsi na teknoloji. Vigezo hivyo ni pamoja na
      I.        Vipaumbele vya  kitaifa vinavyoendana na Mpango  wa Maendeleo  wa Taifa wa Miaka mitano, Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 na Mafunzo ambayo yatazalisha wataalamu wanaokidhi mahitaji  ya kitaifa katika fani za kipaumbele ambazo ni;
·         Fani za Sayansi za Tiba na Afya,
·         Ualimu wa Sayansi na Hisabati,
·         Uhandisi wa  Viwanda, Kilimo, Mifugo, Mafuta na Gesi Asilia,
·         Sayansi Asilia, na
·         Sayansi za Ardhi, Usanifu Majengo na Miundombinu.
      i.        Uhitaji wa waombaji hususani wenye mahitaji  maalum kama vile ulemavu na uyatima
  1. Uhitaji wa waombaji wanaotoka katika familia zenye hali duni ya kimaisha
o    Wadahiliwa yatima waliopata mkopo                                                                    873
o    Wadahiliwa wenye ulemavu wa  viungo                                                                 118
o    Wadahiliwa  wahitaji wenye  mzazi mmoja                                                          3,448
o    Wadahiliwa wahitaji waliofadhiliwa na taasisis mbali mbali                                         87
o    Wadahiliwa wahitaji wanaosoma  kozi  za kipaumbele                                           6,159
o    Wadahiliwa wahitaji wanaosoma kozi zingine                                                        9,867
Jumla                                                                                                         20,183

Kiasi cha Fedha zinazohitajika
Bajeti iliyoidhinishwa kwa ajili ya ukopeshaji kwa mwaka wa fedha wa 2016/17 ni shilingi bilioni 483, kwa ajili ya jumla ya wanafunzi wa mwaka wa kwanza wapatao 25,717, na wanaoendelea na masomo wapatao 93, 295.
Hatua zinazofuata:
              I.        Wanufaika wote wanaopungukiwa na sifa watachunguzwa kwa ajili ya kurekebishiwa au kuondolewa katika unufaika wa mkopo
             II.        Waombaji waliwasilisha taarifa zenye upungufu, taarifa zao zitahakikiwa, na wakibainika kuwasilisha taarifa za uongo watachukuiwa hatua stahiki ikiwa ni pamoja na kufutiwa mikopo yao
           III.        Wanufaika wote watatakiwa kuhuisha taarifa kwa kujaza dodoso. Taarifa za ziada za kiuchumi za wazazi au walezi wao zitatumika kutanua uhalisia. Wale watakaokutwa na hadhi zisizo stahili, watapoteza sifa za kuendelea kupata mikopo na kulazimika kurejesha kiasi watakachokuwa wamepokea tayari.

IMETOLEWA NA:
MKURUGENZI MTENDAJI
BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU

Tamasha la Uhondo wa Zantel lazidi kupasua anga

$
0
0


Msanii maarufu wa muziki wa ‘singeli’ Rajabu Selemani ‘virusi mdudu’ (kushoto), akikonga nyoyo za wakazi wa kimara na maeneo ya jirani katika tamasha la Uhondo za Zantel katika viwanja vya Rhino, Kimara, Dar es Salaam juzi, ikiwa ni moja ya kampeni za kampuni ya simu za mkononi ya Zantel kuwa karibu na wateja wake ikiwajulisha bidhaa na huduma zao zilizopo sokoni.
Msanii maarufu wa muziki wa ‘singeli’ Rajabu Selemani ‘virusi mdudu’ (kushoto), akikonga nyoyo za wakazi wa kimara na maeneo ya jirani katika tamasha la Uhondo za Zantel katika viwanja vya Rhino, Kimara, Dar es Salaam juzi, ikiwa ni moja ya kampeni za kampuni ya simu za mkononi ya Zantel kuwa karibu na wateja wake ikiwajulisha bidhaa na huduma zao zilizopo sokoni.
Baadhi ya watu waliojitokeza katika tamasha la Uhondo wa Zantel wakiselebuka wakati mmoja wa wasanii waliopamba tamasha hilo akitumbuiza.

Tamasha la Uhondo wa Zantel linalodhaminiwa na kampuni ya simu za mkononi ya Zantel limeendelea kukonga nyoyo za wakazi wa sehemu mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam mara hii ikiwa ni zamu ya wakazi wa Kimara na maeneo ya jirani kama inavyoonekana katika picha hizi hapa chini.

VIJUSO VYA BAADHI YA MAGAZETI YA LEO ALHAMIS OKTOBA 27

WAZIRI MAKAMBA AKAMILISHA ZIARA KATIKA MKOA WA KATAVI

$
0
0
 Bibi Josephine Rupia, Mkuu wa Idara ya Maliasili Halmashauri ya Mpanda akitoa maelezo ya Mto Katuma kupoteza mwelekeo wa kutiririsha maji katika mkondo wake kama ilivyokuwa hapo awali. Wengine katika picha ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. January Makamba na Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jenerali Mstaafu Raphael Muhuga
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. January Makamba akihutubia wananchi wa kijiji cha Kabage kilichopo Mkoani Katavi na kuwasisitizia umuhimu wa Hifadhi ya Mazingira
Mmiliki wa Kiwanda cha kutengeneza chumvi cha Nyanza Mining akitoa maelezo kwa Waziri Makamba juu uzalishaji wa chumvi hiyo kwa kutumia nishati ya jua.


TAARIFA YA ZIARA YA MHE. JANUARY MAKAMBA KATIKA MKOA WA KATAVI
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na  Mazingira  Mhe January Makamba hii leo ameendelea na ziara yake katika Mkoa wa Katavi kwa kutembelea kijiji cha Kabege ambapo aliangalia mradi Mkubwa wa Umwagiliaji wa Mwamkulu katika Manispaa ya Mpanda ambao kwa sasa umesitisha kutoa huduma zake kwa kukosekana kwa maji ya kutosha katika Mto Katuma.

Katika kikao cha Majumuisho ya Ziara yake ya siku mbili katika Mkoa wa Katavi, Waziri Makamba ameutaka uongozi wa Mkoa huo kudhibiti yafuatayo:
1.    Ongezeko la watu na mifugo ambayo kwa kiasi kikubwa inachangia uharibifu wa mazingira. 
2.    Kusitisha uchepushaji kwa Mto Katuma ambapo taarifa ya Mkoa ilieleza kuna jumla ya mabanio 40 ambayo yanatumiwa na watu kuchepusha maji kwa ajili ya manufaa yao binafsi.
3.    Uchimbaji hatari wa Madini usiofuata taratibu
4.    Kuhuisha sheria ndogo ndogo za mazingira katika ngazi mbalimbali za Serikali za mitaa
5.    Kuanisha maeneo maalumu ambayo yatatangazwa katika Gazeti la Serikali kama mazingira nyeti ili kuyapa ulinzi zaidi
6.    Kusimamia uondoshwaji wa wavamizi katika Vyanzo vya maji 
7.    Kufanyika kwa sensa ya mifugo ili kujua Mkoa una mifugo kiasi gani na kubuni namna bora ya kuhumudimia mifugo hiyo bila kuathiri mazingira 
8.    ameahidi kuaanda andiko maalumu la Mradi wa Ziwa Katuma
9.    Mmiliki wa Jema Sitalike Project kutafutwa popote alipo, leseni yake ya madini isitishwe, apigwe faini na kurekebisha eneo alilokuwa akitumia awali kwa shughuli za uchenjuaji wa dhahabu.
10.  Waziri Makamba meagiza Watendaji kata na Vijiji kutotoa vibali vya uchimbaji wa madini bila kufuata utaratimu wa Wizara ya Nishati na Madini

Mara baada ya Majumuisho Waziri Makamba alipata fursa ya kuongea na wanakijiji cha Kabage na kusisitiza yafutayo:
1.    Wananchi kutunza mazingira kwa kutofanya kilimo cha kuhamahama, Ukataji Ovyo wa Miti na Uchomaji wa misitu.
2.    kuwakumbusha wananchi kuwa rasilimali ya maji ni ya watu wote hivyo isiwanufaishe watu wachache
3.    Serikali inaangalia namna bora ya kurudisha Mto Katuma katika njia yake ya awali ambayo ilipotea baada ya kutokea kwa mafuriko mwaka 1998
4.    Kuundwa kwa jumuiya za watumia maji na kuzingatia Sheria ya Mazingira ya kutofanya shughuli zozote za kibinadamu ndani ya mita sitini za chanzo cha maji
5.    Kuundwa kwa Kamati ya Mazingira katika Kijiji hicho
6.    Kuondokana na Makazi holela kwa kuandaa mpango wa matumizi bora ya ardhi.
Waziri Makamba amewasili Katika Mkoa wa Kigoma na kutembelea kiwanda cha Nyanza Mines na kuwapongeza kwa kuzalisha chumvi kwa kutumia nishati ya jua ambapo awali kiwanda hicho kilifungiwa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kutokana na uharibifu wa Mazingira kwa kutumia magogo mengi mwaka 2015. Kiwanda hicho kwa sasa kinazalisha tani 20,000-25,000 ndani ya miezi mitatu.



TUMPIGIE KURA RAIS WETU DKT JOHN POMBE MAGUFULI KATIKA TUZO YA WATU MASHUHURI DUNIANI

$
0
0
Rais wetu Dkt  John Pombe Magufuli kachaguliwa na FOBES kushindania Tuzo ya Mtu mashuhuri wa Mwaka 2016 Africa!Tumpigie kura kwa wingi ili iatangaze Nchi yetu Duniani Kote,unaweza bofya link chini halafu angalia jina  gonga utakuwa umesha piga kura.uzalendo kwanza

Mtendaji wa Kata aswekwa Rumande kwa Matumizi mabaya ya Fedha za Umma

$
0
0

   Wananchi wa Kijiji cha Esokonoi, Kata ya Gilailumba kata ya Kitumbiine, Wilaya ya Ngorongoro wakionyesha  zana  walizotumia kutengeneza barabara  ya Km 24 kwa nguvu zao wakati wa Ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha  Mhe. Mrisho Gambo  katika  Kijiji hicho.
  Wananchi wa Kijiji cha Esokonoi, Kata ya Gilailumba kata ya Kitumbiine, Wilaya ya Ngorongoro wakishangilia Msafara wa Mkuu wa Mkoa wa Arusha ulipokuwa unawasili katika Kijiji hicho.
 Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe Mrisho Gambo(Mbele kushoto) pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Longido Mhe. Daniel Chongolo(Mbele  Kulia) wakiwasili  kwenye Mkutano wa hadhara  katika Kijiji cha  Esokonoi.
 Mwenyekiti  wa CCM Mkoa wa Arusha  Mhe. Michael Lekule Laizer akiongea na wananchi wa Kijiji cha  Esokonoi wakati wa Ziara ya Mkuu wa Mkoa katika Wilaya hiyo.
 Wananchi wa Kijiji cha Esokonoi wakimskilizia Mkuu wa Mkoa wa Arusha  Mhe. Mrisho Gambo (hayupo pichani) alipokua akizungumza nao kwenye Mkutano wa hadhara.
  Mwenyekiti wa CCM Mkoa Mhe. Michael Lekule Laizer(kushoto), Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo  (Katikati) pamoja na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Longido wakiwa katika mavazi ya asili ya Kimasaai waliyovishwa kwa heshima na wananchi wa Esokonoi.






Nteghenjwa Hosseah – Longido

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Londifo, Juma Mhina ameamuru polisi wa Wilaya hiyo kumkamata na kumuweka ndani Mtendaji wa Kata ya Gilai Lumbwa, Paul Lucas baada ya kutuhumiwa kutumia Fedha za umma vibaya zilizochangwa na wananchi wa maeneo hayo kwa ajili ya kuinua Sekta ya Elimu.

Agizo hilo la Mhina lilifanikiwa baada ya mara kwa mara kushindwa kumkamata Paulo baada ya kumkwepa kila alipokuwa akitafutwa na hatimaye mtendaji huyo kujitokeza kwenye Mkutano wa hadhara wa Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe Mrisgo Gambo uliofanyika kwenye Kijiji cha IIchang Sapukin kata ya Gilailumbwa.

Mmoja kati ya wananchi walioshirki Mkutano huo Bi. Anni Mollel alimshukuru Rc Gambo kufika Kijijini hapo na kujionea hali halisi ya ujenzi wa Shule ya Sekondari ambayo wananchi walichanga Fedha zao zaidi ya Tsh Mil 96 ila hazikutumika kama ilivyokusudiwa badala yake viongozi wa Serikali na Wenyeviti wa Kijiji walitumia Fedha hizo kujinufaisha binafsi badala ya kuwasaidia watoto kukaa kwenye mazingira mazuri ili wapate Elimu.

“Yaan bora umekuja Mkuu hawa viongozi wetu huku kijijini ni Miungu watu wanajipangia mambo yao ya kubadilisha matumizi ya Fedha zilizochangwa na wananchi kaka zao yaan ukiwaangalia wao wana maisha mazuri wakati sisi tunateseka sasa lro uondoke nao na tunamuomba Mkurugenzi wa Halmashauri hii Ndg. Mhina kuwaleta watumishi wengine na wale waliohamishwa hapa baada ya kushirki kula hela zetu wakamatwe pia na waseme wamepeleka wapi hela zetu”

Mara baada ya wananchi kusema hayo Gambo alimhoji Mkurugenzi Mhina ni kwa nini hawajachukua hatua za kisheria kuwakamata watuhumiwa ndipo Mhina aliposema mbele ya hadhara hiyo kwamba zoezi hilo lilishindikana awali baada ya Paulo kumkwepa Mkurugenzi huyo mara kwa mara lakini jana alijileta mwenyewe katika mkutano huo na ndipo imekuwa rahisi kwake kumkamata.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkaguzi wa ndani wa Halmahauri hiyo, Bi. Mwajuma Mndaira kwenye Mkutano huo alidai kuwa alifanya mahojiano na wenyeviti wa vijiji kujua ni kwa nini walikusanya Fedha kwa wananchi bila kutumia stakabadhi za Serikali katika zoezi hilo.

Pia hivi sasa bado wananendelea na uchunguzi wa nyaraka za malalamiko mbalimbali ili kubaini Paulo alihusika na kinanani na kwa nini abadilishe baadhi ya matumizi ya Fedha hizo na kuuza baadhi ya vitu vilivyochangwa bila kuonyesha sababu ya Msingi kwani baadhi ya kampuni za uwindaji wa kitalii ikiwemo Wingert WindroseSafaris na Kampuni ya Kilombero Nothern Safaris zilitoa mifuko ya Saruji 400 kwa ajili ya ujenzi wa shule ya Sekondari hiyo.

Rc Gambo alimuhoji Mtendaji huyo kwanini shule hiyo haijakamilika mpaka leo wakati watoto wa jamii ya kifugaji wana haki ya Kupata Elimu na wazazi wao wanajitoa wa ajili ya watoto wao huku yeye akiendelea kuwarudisha nyuma, Paulo alijitetea kwamba baadhi ya fedha hizo ziliztumika kihalali na fedha zingine alilazimik kubadilisha matumizi yake na kujenga vyumba vya maabara, jiko pamoja na mabweni,

Baada ya utetezi wake kugonga mwamba alijikuta yupo chini ya himaya ya Polisi waliokuwa wakiongoza msafara huo ambapo pia Mkuu wa Wilaya hiyo Chongolo aliahidi wananchi hao kuwa atafuatilia suala la watumishi wengine watakoziba nafasi za wote watakaomatwa na ubadhirifu huu kuletwa haraka iwezekanavyo ili huduma zisizorote na endapo tuhuma hizi zikithibitkka watapelekwa Mahakamani na aliongezwa kuwa atakua karibu nao kuhakikisha kero kama hizo hazijitokezi rena hapo baadae .
Viewing all 46362 articles
Browse latest View live




Latest Images