Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1024 | 1025 | (Page 1026) | 1027 | 1028 | .... | 1898 | newer

  0 0

  Kijana Mabu Jisinza aliyeishi miaka 16 bila ya sehemu ya kutolea haja kubwa.
  Akina mama wa Wilaya ya Manyoni wakizungumza na Mkuu wa mkoa wa Singida Mhe. Mhandisi Mathew J. Mtigumwe wakisubiri kuonana na daktari bingwa wa magonjwa ya akina mama.
  Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe. Mhandisi Mathew J. Mtigumwe (katikati) akizungumza na wagonjwa waliojitokeza kupata huduma za madaktari bingwa, kushoto kwake ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Singida Daktari John Mwombeki na kulia kwake ni Mkurugenzi wa halmashauri ya Manyoni Charles Fussi.
  Wananchi wa Wilaya ya Manyoni waliojitokeza kupata huduma ya Kliniki tembezi ya madaktari bingwa.

  Mkuu wa Mkoa wa Singida Mheshimiwa Mhandisi Mathew John Mtigumwe amefanya ziara katika hospitali ya Wilaya ya Manyoni kukagua huduma zinazotolewa katika kliniki tembezi ya madaktari bingwa na kuagiza kijana yatima aliyeishi miaka 16 bila sehemu ya haja kubwa kupatiwa matibabu bila malipo.

  Mheshimiwa Mhandisi Mtigumwe ametoa agizo hilo wakati akitembelea wodi ya wanaume ambapo amekutana na kijana yatima Mabu Jisinza mwenye umri wa miaka 16 mkazi wa kijiji cha Mgandu wilayani Manyoni ambaye mara baada ya kuzaliwa bila sehemu ya kutolea haja kubwa alifanyiwa upasuaji wa kuwekewa njia ya muda sehemu ya tumboni na baada ya wazazi wake wote kufariki amekosa msaada wa kuwekewa njia ya kudumu.

  Mheshimiwa Mhandisi Mtigumwe amemuagiza Mganga Mkuu wa Mkoa wa Singida Daktari John Mwombeki kuhakikisha anasimamia kijana huyo anapatiwa matibabu stahiki kwakuwa ameishi kwa kunyanyapaliwa kwa muda wa miaka 16 kutokana na kutoa haja kubwa sehemu ya tumbo huku akisaidiwa na msamaria mwema Lilema Luhumbika mkazi wa kijiji cha Mgandu ambaye amekuwa akimpa chakula na malazi.

  Aidha Mheshimiwa Mhandisi Mtigumwe amemuagiza pia Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manyoni kuchangia fedha endapo kijana huyo atapewa rufaa zaidi na atakapopona apelekwe shule kwakuwa hajui kusoma, kuandika wala lugha ya Kiswahili.

  Wakati huo huo Mheshimiwa Mhandisi Mtigumwe ametoa maelekezo kwa Mganga Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Daktari Fransis Mwanisi kuwa ndani ya mwezi mmoja awe ameanzisha kliniki ya magonjwa yasioambukiza baada ya kupata maombi kutoka kwa mgonjwa wa Kisukari Neema Jakson Mbijima aliyeomba kupatiwa huduma ya ushauri kwa wagonjwa wa kisukari, presha na magonjwa ya moyo.

  Mheshimiwa Mhandisi Mtigumwe ameagiza pia kuongezwa kwa siku za kutolewa huduma hizo za kibingwa zilizoanza kutolewa wilayani Manyoni siku jumatatu ya tarehe 24 Oktoba na kutarajiwa kukamilika tarehe 28 Oktoba 2016 siku ya ijumaa, akielekeza kuwa wagonjwa wote watakaoandikishwa mpaka siku ya ijumaa wahudumiwe wote.

  Naye Mganga Mkuu wa Mkoa wa Singida Daktari John Mwombeki amesema kliniki tembezi ya madaktari bingwa Wilayani Manyoni inao madaktari bingwa wa macho, meno, watoto, daktari bingwa wa magonjwa ya akina mama, daktari bingwa wa magonjwa ya ndani na daktari bingwa wa upasuaji huku kwa muda wa siku tatu madaktari hao wameona wagonjwa 1038.

  Mheshimiwa Mhandisi Mtigumwe amezungumza na wagonjwa waliojitokeza kupata huduma hizo na kuwataka wawataarifu wananchi wengine wajitokeze kwa wingi wasikiapo matangazo ya huduma za kibingwa kwa kuwa huduma za kibingwa kwa ngazi za wilaya ni nadra kupatikana na zitawapunguzia gharama na muda wa kufanya kazi za kuzalisha mali, ameongeza kuwa Mkoa unaweka utaratibu wa kufanya huduma hizo kuwa endelevu.

  Huduma za Kliniki tembezi za madaktari bingwa ukiwa ni utaratibu wa kipekee kufanyika Mkoani Singida umezinduliwa tarehe 14 Agosti 2016 Wilayani Iramba katika hospitali ya Kiomboi ambapo jumla ya wagonjwa 1452 walionwa na mwezi Septemba huduma hiyo imetolewa katika halmashauri ya Wilaya ya Singida ambapo wagonjwa 1064 walinufaikana na sasa ikiwa ni zamu ya halmashauri ya Manyoni ambapo tayari wagonjwa 1038 wamehudumiwa, utaratibu huu utaendelea mwezi Novemba kwa halmashauri ya Ikungi.  Imetolewa na;

  Grace Gwamagobe
  Afisa Habari
  Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
  SINGIDA.
  28 Oktoba, 2016.

  0 0  0 0

  0 0

  Bondia Abdallah  Pazi a.k.a Dullah Mbabe akimsukumia makonde mazito Bondia Chengbo Zheng kutoka nchini China na kupelekea mpambano huo kuisha ndani ya dakika mbili na sekunde kadhaa kwa 'KnockOut' ya kiufundi, katika Ukumbi wa Diamond Jubilee, Jijini Dar es salaam usiku huu.
  Bondia Abdallah  Pazi a.k.a Dullah Mbabe akiendelea kumsukumia makonde mazito Bondia Chengbo Zheng yaliyompelekea kwenda chini na kuomba kutoendelea na mpambani huo.
  Bondia Chengbo Zheng akimuomba msimamizi wake kumtoa 'Groves' baada ya kushindwa kuendelea na mchezo kufuatia makonde mazito na ya haraka haraka aliyoyapata kutoka kwa Bondia Abdallah  Pazi a.k.a Dullah Mbabe
  Bondia Abdallah  Pazi a.k.a Dullah Mbabe (78.2KG) akitangazwa mshindi mara baada ya kumpiga kwa 'KnockOut' Bondia Chengbo Zheng (77.9KG) kutoka nchini China katika raundi kwanza kabisa ya mpambano wao usiokuwa wa Ubingwa uliomalizika usiku huu katika Ukumbi wa Diamond Jubilee, Jijini Dar es salaam.
  Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi akimpongeza
  Bondia Abdallah  Pazi a.k.a Dullah Mbabe kwa ushindi alioupata wa kumpiga Bondia Chengbo Zheng kutoka nchini China, na kufanya heshima ya mchezo huo kuendelea kubaki nchini.
  Bondia Abdallah  Pazi a.k.a Dullah Mbabe akizungumza na vyombo vya habari.,
  Katika mambano ya utangulizi, kulikuwa na pambano hili la raundi nane lililokuwa na mvuto wa aina yake lililowakutanisha mabondia Said Mbelwa (nyeupe) na Shaban Kaoneka. hili lilikuwa na pambano la rusha nirushe, ambapo Bondia Said Mbelwa alifanikiwa kushinda kwa 'KnockOut' ya kiufundi dakika ya saba ya mpambano huo.
  Chukua hiyooooo...

  Bondia Paul Kamata (nyeupe) akimsukumia makonde mithili ya mvua Bondia Buta Obed katika mpambano wao usio na ubingwa wa raundi nani, ulichezwa usiku wa leo katika Ukumbi wa Diamond Jubilee, Jijini Dar es salaam. Bondia Paul Kamata alishinda kwa 'KnockOut' ya kiufundi, katika raundi ya tano ya mchezo hio.
  0 0

  Mbunge wa Kasulu vijijini Mhe Augustine Vuma (Kushoto) akitoa maelezo kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. January Makamba wakati viongozi hao walipotembelea kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu. (Katikati ni Bw. Peter Bulugu Kaimu Mkuu wa Kambi – Nyarugusu
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. January Makamba akihutubia katika Mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Kagera Nkanda, Wilayani Kasulu
  Sehemu ya wawakilishi wa mashirika mbalimbali yanayotoa huduma katika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. January Makamba (hayupo pichani) mara baada ya kutembelea kutembelea kambi ya Nyarugusu na kutoa maelezo katika sekta ya mazingira
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. January Makamba akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Kasulu Kanali Martin Mkisi wakikagua uharibifu wa mazingira katika msitu wa Makere katika Wilaya ya Kasulu

  …………………………………..

  Na Lulu Mussa

  Kasulu

  Imebainika kuwa ongezeko kubwa la idadi ya wakimbizi katika kambi ya Nyarugusu inachangia kwa kiasi kubwa la uharibifu wa mazingira kwa kuongeza matumizi ya rasilimali za asili.

  Hayo yamesemwa leo na Kaimu Mkuu wa Kambi ya Nyarugusu Bw. Peter Bulugu wakati wa kuwasilisha taarifa ya hali mazingira katika kambi hiyo kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia masuala ya Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba

  Kaimu Mkuu wa Kambi wa Nyarugusu Bw. Peter Bulugu amesema kuwa hali ya mazingira katika kambi si nzuri na inakabiliwa na tatizo la uharibufu wa mazingira kwakuwa wengi wa wakimbizi hao hutumia kuni kama nishati ya kupikia.

  Hata hivyo Bw. Bulugu amebainisha kuwa Ofisi yake imeeanda mkakati wa upandaji miti ili kunusuru maeneo yanayozunguka, na kwakuanzia jumla ya miche 900,000 imeoteshwa katika vitalu. Pia Kambi imedhamiria kugawa majiko banifu ambayo yatatumia nishati kidogo na uzalishaji wa nishati kwa kutumia takataka za mashambani unatarajiwa kuanza mwezi Novemba.

  Aidha, mkakati mwingine ni ujenzi wa nyumba za tofali mbichi na kuezeka kwa mabati badala ya miti ambapo jumla ya nyumba 800 zimekamilika na nyumba 542 ziko katika hatua mbalimbali za ujenzi. Alisema Bw. Bulugu

  Akiwa katika Wilaya ya Kasulu Mkoani Kigoma, Waziri Makamba ametembelea kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu na kupata fursa ya kuongea na wawakilishi wa mashirika mbalimbali yanayotoa huduma katika kambi hiyo.

  Waziri Makamba amesema kuwa ni vema uongozi na mashirika yanayotoa misaada katika kambi hiyo kuandaa mpango mzuri wa namna ya kuwapokea na kuwahifadhi wakimbizi ili ujio wao usiathiri watanzania wanaozunguka kambi ili shughuli zao za uzalishaji mali kila siku ziwe na tija.

  Waziri Makamba aliuagiza Ungozi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na wakimbizi kutafuta pesa zaidi ili mpango wa kugawa majiko banifu uwafikie wakimbizi wote. “Kaya zilizopo hapa ni 30,000 ninyi mnataka kugawa majiko hayo kwa kaya 3000 tu, nashauri muangalie uwezekano wa kugawa kwa kaya zote” Makamba alisisitiza.

  Waziri Makamba pia ameagiza kufanyika kwa Ukaguzi wa Mazingira (Environment Audit) ndani ya wiki mbili kwakuwa ni takwa la kisheria. Na kuwataka na kupanda miti kwa wingi. ” Pandeni miti ya aina mbalimbali mfao miti ya matunda, kuni na mbao ili kunusuru mazingira yetu”.

  Waziri Makamba pia alitembelea msitu wa Makere wenye takriban ekari 75,000 ambao kwa upande wa Makere kusini kumekuwa na uharibufu mkubwa wa mazingira na kuagiza doria za mara kwa mara ili kudhibiti wananchi wanaofanya kilimo cha kuhamahama, kukata na kuchoma miti pia kudhibiti ongezeko la mifugo kwa kuiandikisha ili mgogoro uliopo baina ya hifadhi na wananchi uweze kupatiwa ufumbuzi kwa kujenga hoja madhubuti.

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia masuala ya Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba hii leo ameendelea na ziara ya kukagua hali ya mazingira katika Mikoa 10 hapa nchini ambapo leo ni siku ya 13. Waziri Makamba pia atatembelea Mkoa wa Tabora.

  0 0

  Mkurugenzi Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Brigedia.Jen Mbazi Msuya akiwa na Meneja Rasilimaliwatu wa Kampuni ya kutengeneza chuma ya Kamal Bw. Ajay Jha wakati wa kuangalia saruji iliyotolewa na kampuni hiyo kwa waathirika wa tetemeko la ardhi Kagera Oktoba 28, 2016.
  Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya kutengeneza chuma ya Kamal ltd wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Brig.Jen Mbazi Msuya mara baada ya kuangalia msaada wa saruji mifuko 640 uliotolewa na kampuni hiyo tayari kwa kusafirisha mkoani Kagera.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Mkurugenzi Idara ya Kuratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Brigedia.Jen Mbazi Msuya (wa kwanza) akisalimiana na Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya kutengeneza chuma ya Kamal ltd Bw. Gagan Gupta wakati wa uhakiki wa misaada ya saruji iliyotolewa na kampuni hiyo kwaajili ya waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera tarehe 28 Oktoba, 2016.
  Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Brig.Jen Mbazi Msuya (wa kwanza kushoto) akieleza jambo wakati alipotembelea ofisi za kampuni ya Kamal ili kupokea na kuangalia saruji zilizokabidhiwa na ofisi hiyo kwa waathirika wa tetemeko la ardhi Kagera.
  Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya kutengeneza chuma ya Kamal ltd Bw. Gagan Gupta (wa kwanza kulia) akizungumza jambo kwa baadhi ya wafanyakazi wa Ofisi ya Waziri Mkuu walipofika katika ofisi hizo kuangalia msaada wa safuji mifuko 640 unaosafirishwa kwa waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera.
   

  0 0

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Mh. George Simbachawene akizungumza wakati wa mkutano wa kuzindua Bodi mpya ya Mikopo ya Serikali za Mitaa leo mjini Dodoma.
  Naibu Katibu mkuu anayeshughulikia elimu kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Bw. Benard Makali akizungumza katika mkutano wa kuzindua bodi mpya ya Mikopo ya Serikali za Mitaa katika Jengo la Mkapa mkoani Dodoma.

  Baadhi ya wajumbe wa Bodi ya Mikopo ya Serikali za Mitaa wakifuatilia uzinduzi wa Bodi hiyo katika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Mkapa leo mjini Dodoma.

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Mh. George Simbachawene akikata utepe wa nyaraka muhimu zinazohusu Bodi, katika mkutano wa kuzindua bodi mpya ya Mikopo ya Serikali za Mitaa katika Jengo la Mkapa mkoani Dodoma.  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Mh. George Simbachawene kwenye picha ya pamoja na wajumbe wa bodi ya mikopo na baadhi ya watumishi wa bodi hiyo katika mkutano wa kuzindua bodi mpya ya Mikopo ya Serikali za Mitaa katika Jengo la Mkapa mkoani Dodoma.

  Na, Nasra Mwangamilo

  Bodi ya Mikopo ya Serikali za Mitaa yatakiwa kuongeza fursa itakayoziwezesha Serikali za Mitaa nchini kupata fedha za kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi hasa katika miradi ya maendeleo na utoaji wa huduma za kijamii.

  Wito huo umetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Mh. George Simbachawene alipokuwa akizindua rasmi Bodi hiyo leo mjini Dodoma.

  “Natambua kuwa nyenzo muhimu za kutekeleza majukumu ya Bodi ni rasilimali fedha ambazo zinatakiwa zipatikane kupitia vyanzo mbalimbali ambavyo vimeainishwa kwa mujibu wa sheria, kifungu cha 62 cha Sheria ya Bodi ya mikopo kinataja njia mbalimbali ikiwemo kupata fedha kama zitavyoainishwa na Bunge kwa madhumuni ya kuendesha shughuli za Bodi”.Aalisema Mh. Simbachawene.

  Aidha alisisitiza kuwa Bodi hiyo ijitahidi kusimamia kwa ukaribu zaidi uwekezaji kwa kuelekeza rasilimali kwenye vitega uchumi vyenye faida kubwa ikiwa ni njia mojawapo ya kujiongezea mapato huku ikiwa na lengo la kuhakikisha inatoa mikopo kulingana na makubaliano baina ya Bodi na Halmashauri husika.

  Pia aliwataka wa jumbe wa Bodi kusimamia kwa ukaribu utendaji wa Bodi hiyo na kuhakikisha kwamba hesabu zinatunzwa vizuri na taarifa zinatolewa kwa wakati hii ni pamoja na kuweka amana za muda maaalumu kwenye mabenki, umiliki wa hisa katika mabenki, kodi ya pango kutoka kwenye nyumba zinazomilikiwa na Bodi pamoja na malipo ya riba kutoka kwenye mikopo.

  “Nitumie nafasi hii kusisitiza kwamba nanyi kama wa jumbe wa bodi hii lazima kusimamia kwa ukaribu utendaji wa bodi ya mikopo na kuhakikisha kwamba hesabu zinatunzwa vizuri, Ni vizuri taarifa za bodi zipatikane kwa wakati nakuwasilishwa mbele ya bodi na kujadiliwa kwa wakati”. Alisisitiza Waziri.

  Kukosekana kwa mwamko wa kimaendeleo miongoni mwa baadhi ya viongozi na watendaji wa Halmashauri hivyo kuna umuhimu wa bodi hii mpya kusaidia kuchochea ubunifu wa kimaendeleo ili Halmashauri ziinue miradi bora inayokopesheka na yenye faida kubwa.

  0 0


  0 0

  Na Rhoda Ezekiel-Globu ya Jamii Kigoma,

  ASKARI wa Jeshi la Mgambo wametakiwa kuacha kushirikiana na wahalifu katika vitendo viovu na kutumia Mafunzo waliyo yapata kuzuia uhalifu na kuzisaidia mamraka za kiraia katika kuimalisha ulinzi na usalama wa Raia na mali zao.

  Rai hiyo ilitolewa na Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala jana wakati akifunga mafunzo ya Askari Mgambo 65 katika kijiji cha Bukililo kata ya Gwanumbu Wilayani Kakonko Mkoani Kigoma ambapo aliwaomba Askali hao kutumia mafunzo hayo kwa kutumisha ulinzi katika Vijiji vyao na kushirikiana na Serikali kuwaibua wahalifu.

  Ndagala alisema Askari mgambo ni moja kati ya jesi linalo lisaidia Taifa katika ulinzi na usalama na mafunzo mliyo yapata ninaimani yamewajengea uzarendo wa kuipenda Nchi yenu, muyatumie mafunzo haya mlio yapata katika kuhakikisha uhalifu na suala la wahamiaji halamu yana kwisha kabia katika vijiji vyenu.

  Alisema vijiji vya Bukililo na Gwanumbu ni vijiji ambavyo vinapakana na Nchi jirani ya Burundi tumeamua kutoa mafunzo haya ilikuongeza askali wa kutosha ilikukomesha vitendo vya kiuhalifu vilivyo kuwa vikiendelea mipakani ikiwa ni pamoja na kuwazuia Wahamiaji halamu ambao wengi wao wanakuja kushirikiana na wahalifu kufanya vitendo vya kiujambazi na kuingiza siraha mbalimbali Nchini.

  Aidha Ndagala aliwaomba Wananchi kushirikiana na askari hao kuwafichua wahalifu na wahamiaji halamu ambao baadhi yao wamewapokea na kuwahifadhi bilakujua wanaweza kusababisha madhala gani na wengi wao wameingia na siraha ndio wanao jihusisha na vitendo vya utekaji na kuwaibia wananchi mali zao.

  "Niwapongeze kwa kumaliza mafunzo haya ya miezi minne ni mafunzo mazuri na kwamaonyesho mlio yaonyesha ninaimani mtakuwa mabarozi wazuri katika kazi zenu niwaombe msitumie mafunzo hayo kinyume na utaratibu kazi yenu ni kudumisha usalama na kufanya kazi wakati wa vita kama Askali na kulinda maeneo nyeti msikubali kutumiwa na watu kutimiza malengo yao mtakuwa mkikiuka kiapo mlicho kiapa hii leo",alisema Mkuu huyo wa wilaya.

  Kwa upande wake Diwani wa kata ya Gwanumbu Toi Butono alisema kumalizika kwa mafunzo hayo itasaidia Kijiji kupata Askali wa kutosha awali kijiji kilikuwa hakina askali na matukio ya kiuhalifu yalikuwa yamezidi lakini baada ya kuwapata askali hao vitendo hivyo vitapungua.

  Nao Baadhi ya wahitimu wa Mafunzo ya Mgambo,Efron Reuben na Asuman Manase waliishukuru Serikali kwa kuamua vijana nao wapate mafunzo hayo ambayo yatawasaidia katika kuimalisha ulinzi na usalama vijijini na kuishi kizalendo katika Nchi yao.

  Hata hivyo waliiomba Serikali pindi zinapo tokea nafasi za ulinzi katika taasisi za kiserikali na binafsi wapewe kipaumbele pamoja na nafasi za kujiunga na Jeshi la wanachi (JW) wapewe kipaumbele ilikutoa hamasa kwa vijana na watu wengine kuona umuhimu wa kujiunga na jeshi la mgambo.
  Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala akikagua Gwaride la Askari wa jeshi la Mgambo,alipokuwa akifunga mafunzo ya Askari Mgambo 65 katika kijiji cha Bukililo kata ya Gwanumbu Wilayani Kakonko Mkoani Kigoma ambapo aliwaomba Askali hao kutumia mafunzo hayo kwa kutumisha ulinzi katika Vijiji vyao na kushirikiana na Serikali kuwaibua wahalifu.

  Askari wa jeshi la Mgambo,wakiwa kwenye gwaride la kufungwa kwa mafunzo yao,katika kijiji cha Bukililo kata ya Gwanumbu Wilayani Kakonko Mkoani Kigoma

  0 0

  Tarehe kama ya leo, 29 October 1959, takribani miaka 57 iliyopita katika kijiji cha CHATO, alizaliwa mtoto kwenye familia ya mkulima. Mungu alimpa ulinzi na akalelewa kwa misingi ya kitamaduni. Mtoto huyo ndiye kiongozi wa nchi yetu,ni Dkt John Pombe Joseph Magufuli.

  HAPPY BIRTHDAY  RAIS WETU MPENDWA.

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Mathew Mtigumwe akiwapongeza washiriki waliomaliza kwa wastani mzuri wa muda, kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu
  Bi Zaibabu Ramadhani mwenye umri wa miaka 47 akiwasili Katika uwanja wa Shule ya Sekondari Ikungi kumalizia kilomita 21
  Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Mathew Mtigumwe akisalimia na Felix Simbu kijana wa Kitanzania aliyeshika nafasi ya tano katika mashindano ya Olimpiki nchini Brazil mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Shule ya Sekondari Ikungi kwa ajili ya kuhamasisha Ikungi Half Marathon 2016
  Washiriki wa mbio fupi za Mita 100 wakipokea maelekezo ya Mkufunzi wa Ikungi Half Marathon 2016
  Mhariri wa Mtandao wa www.wazo-huru.blogspot.com Mathias Canal akisikitika kwa kushika nafasi ya tano kwenye Mbio fupi za Mita 400
   Mwanzo mgumu lakini ushiriki ni muhimu
   Moja ya washiriki wa mbio fupi za mita 800 akjijiandaa kwa ajili ya kuchomoka kutafuta ushindi
   Washiriki wa Ikungi Half Marathoni 2016 Kilomita 21wakichuana vikali kwenye mchezo wa Riadha
  Viongozi mbalimbali waliokaa Jukwaa kuu wakifatilia kwa makini mashindano ya Ikungi Half Marathon2016
  Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akimuonyesha Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Mathew Mtigumwe jinsi ambavyo washiriki wa Ikungi Half Marathon 2016 walivyokuwa wakichuana kumaliza mbio hizo za Kilomita 21
   Wananchi walivyoitikia kwa wingi katika mashindano ya Ikungi Half Marathon 2016
   Umakini unahitajika katika kubaini muda wa washindi
   Baadhi ya watumishi katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ikungi wakifatilia kwa makini mchuano mkali wa Ikungi Half Marathon 2016
   Washindi wakipokea zawaidi zao
   Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akiwapongeza washindi wa nafasi za juu
   Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Mathew Mtigumwe akiwa kwenye picha ya pamoja na washindi wa nafasi za juu katika mashindano hayo
   Wananchi wakisikiliza kwa makini hotuba ya Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Mathew Mtigumwe
   Muwakilishi wa Meneja wa mgodi wa Shanta Gold Mine Bw Elisante Kanuya akitoa zawadi kwa baadhi ya washindi
  Felix Simbu kijana wa Kitanzania aliyeshika nafasi ya tano katika mashindano ya Olimpiki nchini Brazilakihojiwa na waandishi wa Habari wawakilishi wa East Africa Radio na East Africa Televisheni
  Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Mathew Mtigumwe akimpongeza Bw Elisante kanuya Muwakilishi wa Meneja wa Mgodi wa Shanta Gold Mine 

  Na Mathias Canal, Singida

  Mashindano ya Ikungi Half Marathon yenye lengo la kuibua vipaji kwa vijana na kuviendeleza, Kujenga umoja na mshikamano miongoni mwa vijana na kuwandaa vijana hao katika mashindano mbalimbali ya kitaifa na kimataifa yamehitimishwa hii leo na kutoa taswira nyingine ya Mashindano ya Ikungi Marathon kwa mwaka 2017.

  Mashindano hayo yalianza Septemba 3, 2016 kwa ngazi ya Vijiji, Kata na Tarafa na hatimaye kufikia ngazi ya Wilaya ambapo viongozi wa Wilaya za Mkoa wa Singida wametakiwa kutafakari namna bora ya kuanzisha mchezo wa kipaombele ili kutoa taswira ya manufaa kwa jamii ya wapenda michezo.

  Mgeni Rasmi katika kilele cha mashindano ya Ikungi Half Marathon 2016 Ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Mathew Mtigumwe Ameyasema hayo hii leo huku akimsihi Mkuu wa Wilaya ya Ikungi kuanzisha Tovuti maalumu ya Ikungi Marathon kwa ajili maandalizi ya mbio ndefu zitakazofanyika mwaka 2017.

  Mhe Mtigumwe amempongeza mkuu huyo wa Wilaya hiyo kwa kubuni na kuanzisha mchezo huo ambao umeleta chachu na mafanikio makubwa kwa vijana wa Mkoa wa Singida ambapo ameshauri pia kubadilisha mwezi wa ufanyaji wa mashindano ili kila kijana apate nafasi ya kushiri ambapo amesema kuwa mashindano hayo yamebeba taswira ya Mkoa mzima hivyo ameahidi kuyaongeza nguvu na kutoka kwenye ngazi ya Wilaya na kuwa ngazi ya Mkoa.

  Tangu kuanza kwa Mashindano haya mwanzoni mwa Mwezi Septemba mwaka huu vijana zaidi ya 150 walijitokeza kushiriki ambapo kati yao vijana 60 pekee ndio walifanikiwa kuingia ngazi ya Wilaya ambapo kati yao wanaume ni 52 na wanawake ni 8.

  Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu awali akizungumza kabla ya kumkaribisha mkuu wa mkoa alisema kuwa aliamua kuanzisha mashindano hayo ya Ikungi half Marathon 2016 kutokana na washiriki wengi wazaliwa wa Ikungi kufanya vizuri katika mashindano mbalimbali ya Riadha ngazi ya Kitaifa na Kimataifa akiwemo Bw Felix Simbu aliyeshika nafasi ya tano kwenye mashindano ya Olimpiki nchini Brazil, Na Bi Tausi Said aliyefanya vyema nchini Canada.

  Dc Mtaturu ametumia nafasi hiyo pia kuzitambulisha fursa zilizopo katika Wilaya ya Ikungi katika shughuli za kiuchumi na kijamii katika kuinua kipato cha wananchi wa Wilaya hiyo, Ikiwemo fursa za nyanja mbalimbali katika uwekezaji kama vile Kilimo na mifugo kwa maana yauzalishaji wa mazao ya chakula kama vile uwele, Viazi vitamu, Mahindi na vitunguu, Mazao ya biashara kama vile alizeti na Ulezi.

  Fursa zingine zilizotajwa na Mkuu huyo wa Wilaya ya Ikungi ni pamoja na Msitu ya asili unaowezesha ufugaji wa nyuki na kupata asali bora, Ardhi na maji kwa uwepo wa maeneo chepechepe kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji na mazao ya bustani lakini pia uchimbaji wa madini wakiwemo wachimbaji wadogo na wachimbaji wakubwa.

  Mhe Mtaturu pia alisema kuwa uwepo wa mkondo wa upepo kwa ajili ya uzalishaji wa umeme wa upepo katika vijiji vya Unyankanya na Siuyu Tarafa ya Mungaa.

  Dc Mtaturu amesema kuwa Wilaya ya Ikungi imedhamiria kwa dhati kuwekeza katika michezo kwani itakuwa chachu kwa wawekezaji, Sambamba na kutoa fursa kwa wananchi wake hasa katika kuongeza kipato, Kutoa ajira na kupandisha taaluma ya michezo kwa wakazi wa Wilaya ya Ikungi na Mkoa wa Singida kwa ujumla.

  Naye Felix Simbu kijana wa Kitanzania aliyeshika nafasi ya tano katika mashindano ya Olimpiki nchini Brazil ameiomba serikali kuwaandaa vijana kwa ajili ya mashindano

  0 0  0 0


  0 0
 • 10/29/16--09:55: SHIWATA yandaa mashindano
 • MTANDAO wa Wasanii Tanzania (SHIWATA)umeandaa mashindano ya Sanaa na Michezo litakalofanyika kuanzia Novemba 12,2016 katika viwanja
  mbalimbali jijini Dar es Salaam.

  Mwenyekiti wa SHIWATA,Cassim Taalib alisema jana kuwa michezo
  itakayoshindaniwa ni soka,mpira wa kikapu,ngoma za asili, muziki wa
  dansi, sarakasi, Karate na kaswida.

  Alisema mashindano hayo yatafanyika kuwapata washindi ambao kwa pamoja watakwenda kukabidhiwa zawadi zao kwenye kijiji cha wasanii
  Mwanzega,Mkuranga.

  Mwenyekiti Taalib aliwataja wajumbe wa Kamati ya tamasha hilo kuwa ni
  Deo Kway, na mchezaji wa zamani wa Simba, Kureshi Ufunguo na mchezaji
  wa zamani wa Yanga, Salvatory Edward watakaosimamia mashindano ya
  soka.

  Wengine ni Selemani Pembe, Athumani Bakari maarufu kama Mbegeja katika mchezo wa sarakasi,Abdul Salvador kamati ya muziki wa dansi na Kocha wa timu ya Taifa ya Mpira wa Kikapu, Manase Zablon katika mchezo wa mpira wa kikapu.

  Wajumbe wengine ni Ismail Kambangwa, Kashindye Fundikira na Mariam
  Ismail maarufu kama mama Mipango watakaosimamia ngoma za asili.


  0 0

  Naibu Waziri wa Elimu , Sayansi na Teknolojia Mhandisi Stella Manyanya (kulia) akikata utepe wakati uzinduzi wa program ya JIANDALIE AJIRA inayolenga kupunguza tatizo la ajira nchini. Wengine katika picha ni Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Kimataifa wa Vijana (IYF), Bw. William Reese (wa pili kulia), Mwenyekiti wa bodi wa Taasisi ya Ujasiriamali na Ushindani TECC Bi. Beng’I Issa (kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Ujasiriamali na Ushindani, Bw. Sosthenes Sambua (wa pili kushoto) na Ahmed Makbel Mkurugenzi Msaidizi wa Ajira kutoka ofisi ya Waziri Mkuu (katikati).
  Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa wa Mfuko wa Kimataifa wa Vijana (IYF), Bw. William Reese, akisisitiza jambo wakati wa uzinduzi wa program ya Jiandalie Ajira jana jijini Dar es Salaam, wengine katika picha ni Mwenyekiti wa bodi wa Taasisi ya Ujasiriamali na Ushindani (TECC) Bi. Beng’I Issa (kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa (TECC) Sosthenes Sambua katikati, program hiyo ili zinduliwa na Naibu Waziri wa Elimu , Sayansi na Teknolojia Mhandisi Stella Manyanya kwenye ukumbi wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere Dar es Salaam jana.

  Na Ally Daud-MAELEZO. 

  Mfuko wa Kimataifa wa Vijana( Interanational Youth Foundation) imezindua rasmi programu mpya ya miaka mitano wa JIANDALIE AJIRA unaowalenga vijana hapa nchini kama moja ya jitihaha za kukuwajengea vijana mafunzo ya ufundi stadi na ujasiriamali kuondokana na tatizo la ajira . 

  Akizindua programu hiyo, Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Technolojia ,Mhandisi Stella Manyanya alisema program hiyo ni ukombozi mkubwa kwa vijana hapa nchini kwa kuwa itawawezeshae kutengEneza ajira na kukuza uchumi. 

  “Programu hii imekuja kutengneza vijana kuwa wabunifu na kutengneza ajira ikiwa ni pamoja na kuajiri wengine na siyo kuwa wasaka ajira,”na kwa kufanya hivyo taifa litapiga hatua kiuchumi,aliongeza kusema,Mhandisi huyo ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nyasa” alisema Mhandisi Manyanya 

  Aidha Mhandisi Manyanya aliupongeza mfuko huo wa IYF kwa kuja na mradi ambao utatekelezwa kwa ushirikiano na Taasisi ya Ujasirimali na Ushindani (TECC), Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) na Shirika lisilokuwa la kiserikali la The MasterCard Foundation. 

  Mhandisi Manyanya alisema pia programu hiyo itawezesha kuwaandaa wakufunzi wa chuo cha VETA ili waweze tumika katika kuwafundisha vijana ambao ndio walengwa katika mradi mzima na ambao wanachangamoto kubwa ya ajira. 

  Mbali na hayo Mhandisi Manyanya alikitaka chuo hicho kuendeleza na kupanua wigo wa ushirikiano na waajiri ili kujenga nguvu kazi kukidhi matwakwa ya soko la ajira kwenda sambana na dira ya Maendeleo ya Taifa ya mwaka 2025. 

  Kwa upande wa Rais wa IYF ambaye pia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa mfuko huo Bw.William Reese alisema mfuko wao umeandaa mpango huo kwa nchi za Tanzania na Msumbiji kwa ajili ya kuwaandaa vijana katika elimu ya mafunzo ya ufundi stadi na uujasirimali 

  “Tatizo la ajira siyo la Tanzania tu bali la dunia nzima kwa nchi zilizoendelea na ambazo hazijaendelea”, na hitaji mipango ya pamoja, ya kidunia na yakinchi kwa kushitrikiana na mashirika yasiyokuwa ya kiserikali” alisema Bw. Reese. 

  Pia Mkurugenzi wa Kanda ya Afrika IYF (Regional Director,Africa) , Bw.Mathew Breman alisema mpango wa jiandallie ajira utaendeshwa kwa muda wa miaka mitano na unalenga kuwapatia mafunzo ya ufundi stadi na jasirimali kwa vijana. 

  ” Programu hii inahusu vijana wa miaka 18 hadi 24 na watapata mafunzo na mikoa inayolengwa ni pamoja na Dar es Salaam, Dodoma, Mtwara,na Morogoro,” na vijana 22,500 watanufaika na mradi huu, aliongeza Bw. Breman. 

  Aidha Bw. Breman mradi unaletekezwa katika nchi Msumbiji ambapo kwa pamoja na Tanzania utanufaisha vijana 30,000 kupata mafunzo ya ufundi stadi na ujasiriamali katika kipindi hicho. 

  Mwenyekiti wa Bodi wa Taasisi ya Ujasirimali na Ushindani (TECC),Bi. Issa Beng’I alisema program hiyo ni muhimu kwa vijana. 

  “Tunazo program nyingi hapa nchini Tanzania, ikiwemo kijana jiajiri, vijana wa bodaboda,vijana wa JKT, na sasa program ya jiandalie ajira itawawezesha kujitambua zaidi,” na kufanikiwa kwa hili ni ukombozi mkubwa kwa taiafa letu, aliongeza kusema Bi. Issa. 

  Moja ya vijana , Nuru Mungi akitoa ushuhuda wa biashara yake, alisema mafanikio aliyoyapata katika ujasirimali yamekuja baada ya kupata mafunzo (TECC). 

  “ Kutokana na mafunzo haya sasa namiliki kiwanda kidogo cha kutengneza sabuni na naamini kupitia program ya jiandalie ajira vijana wengi watanufaika na kupanua wigo wa ujasirimali.alisema. 

  Mkurugenzi Msaidizi wa Ajira toka Ofisi ya Waziri Mkuu, Ahamed Makbel,alisema tatizo la ajira hapa nchini kwa kwa sasa limefikia asilimia 10.3. 

  “Tatizo hili kwa vijana limefikia asilimia 11.7 kwa vijana amabyo ni nguvu kazi kubwa inayobeba asilimia 56 kwa nchi nzima, vijana hao wanaumri kati ya miaka 15 hadi 35. 

  Mfuko wa IYF umesha fanya kazi katika mataifa zaidi ya 70 duniani ili kuweza kusaidia vijana mbalimbali kwa ajili ya kukuza uchumi wa kijana na taifa kwa ujumla ili kufikia uchumi wa kati.

  0 0

   Baadhi ya wakazi wa Mji wa Shinyanga wakishiriki katika zoezi la usafi wa mazingira leo, Mjini Shinyanga. 
   Katikati Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina, Kushoto Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Bi Josephine Matiru,  na Bwana Daniel Sagata Pamoja wakijiandaa kuanza zoezi la usafi wa mazingira katika eneo la Binzatana Mjini Shinyanga mapema leo. 
   Naibu Waziri Ofisi ya makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe Luahaga Mpina akishiriki katika zoezi la kupanda miti Mjini Shinyanga leo.
   Viongozi pamoja na baadhi ya wananchi wa mkoa wa Shinyanga katka zoezi la usafi wa mazingira mjini Shinyanga leo.
  Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe Luhaga Mpina akiongea na baadhi ya wananchi wa mkoa wa Shinyaga katika eneo la Binzanata baada ya kukamilisha zoezi la usafi wa mazingira na kupanda miti mapema leo. ( Picha zote na Habari na Evelyn Mkokoi wa OMR).


  EVELYN MKOKOI-SHINYANGA

  Uongozi wa mkoa wa Shinyanga kupitia Mkuu wa Wilaya yake Bi Josephine Matiru umeiomba serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais Kujenga kiwanda kitakacho tengeneza mkaa utokanao na mabaki ya miti ambao ni rafiki kwa mazingira ili kunusuru hali ya mkoa huo kuendelea kuwa jangwa kutokana na ukataji miti ovyo kwa matumizi ya makaa manyumbani, matumizi mengine na athari zitokanazo na mabadiliko ya tabia nchi.

  Mkuu wa wilaya hiyo ametoa ombi hilo leo mbele ya Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina aliposhiriki siku ya usafi kitaifa ya mwisho wa mwezi October ambapo zoezi hilo lilizinduliwa rasmi na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania December Mwaka jana na kuendelea kutekelezwa kila jumamosi ya mwisho wa mwezi kama siku maalum ya usafi nchini.

  Bi Materu aliendelea kusema kuwa, Mkoa wa shinyanga unakumbana na changamoto kubwa ya ukataji miti ovyo ambayo ingeweza kukabiliwa kwa kutumia mabaki ya miti, taka na maranda ya mbao kutengeneza mkaa rafiki kwa mazingira na kusema kuwa mkoa na wilaya ya shinyanga imebarikiwa kuwa na miti ya aina mbali mbali ambazo mazingira yangetunzwa vizuri na kutumia malighafi hiyo ya taka kutengeneza mkaa banifu akitolea mfano kiwanda cha kutengeneza mkaa rafiki wa mazingira cha Zanzibar.

  Kwa Upande wake Naibu Waziri Mpina alikiri kupokea maombi ya mkuu wa wilaya huyo na kueleza kuwa serikali itakuwa tayari kujenga kiwanda cha kutengeneza mkaa mjini shinyanga “Na pengine katika Mbio za Mwenge Mwakani tukijaaliwa tunaweza kuzindua kiwanda hicho kama mradi wa mfano.” Alisisitiza Mpina. “Lazima tuwe na viwanda vya mkaa rafiki kwa mazingira sasa na wafanya biashara wa gas za manyumbani sasa ufike wakati nao washushe bei ili asilimia kubwa ya watanzania waweze kutumia nishati hiyo.” Alifafanua Mpina.

  Akizungumzia suala ya usafi wa Mazingira ambapo sambaba na hilo Naibu Waziri Mpina Pia alishiriki zoezi la upandaji miti katika eneoa la Binzamata, alisema kuwa watanzania wana kila sababu ya kujijengea utamaduni wa usafi wao pamoja na mazingira kwani hata vitabu vitakatifu vinasisitiza usafi wa mazingira akitolea mfano kitabu cha Biblia takatifu cha kumbu kumbu la Torati 23:11-14 na kusema kuwa “Pahala Pachafu hapana Utukufu wa Mungu na hauwezi kuonekana mahali hapo na haya siyo maneno yangu wala ya Rais Magufuli, ni maneno ya biblia hivyo watendaji katika ngazi zote mzingatie utekelezaji wa sheria yya mazingira ya mwaka 2004 na kanuni zake na kuwachulia hatua wale wote watakao kiuka sheria hiyo.”

  “Ni jukumu la kila mtu kufAnya usafi na kila wilaya na Halmashauri ijetengenezee mwongozo na sheria ndogo ndogo katika eneo hili la usafi wa mazingira na lazima watu wawajibike.”

  Naibu Waziri Mpina Pia alisisitiza zoezi la upandaji miti ili kuweza kukabiliana na athari zitokanazo na Mabadiliko ya tabia nchi na kurudisha uoto wa asili.

  Akitolea mfano wa kasi ya serikali ya awamu ya tano katika zoezi la usafi wa mazingira Mpina alisema “ watu walidhani Mhe. Rais alivyozindua siku ya usafi zilikuwa ni nguvu za soda, kasi tuliyonza nayo ndiyo tutakayo maliza nayo, waharibifu wa mazingira lazima sheria iwashughulikie.” Alisisitiza Mpina.

  Akizungumzia wananchi wanaoabudu siku ya Jumamosi Mpina alisema Sheria ndogo ndogo za mazingira za Halmashauri na miji ni vizuri zikaona namna ya kuweza kuwapa nafasi na wao ya kuabudu na kushiriki usafi katika siku hiyo.Siku ya kila Jumamosi ya kila mwisho wa mwezi imetengwa na serikali ikiwa ni maalum kwa ajili ya usafi nchini.

  0 0


  Mkurugenzi Mkuu wa SBL Helene Weesie akitoa hotuba ya ufunguzi kwa wageni waliohudhuria tafrija mchapalo ya maadhimisho ya miaka 20 tangu kuanzishwa kwa bia ya Serengeti Premium Lager (SPL) mwaka 1996.Pia kulizinduliwa chapa mpya ya Bia hiyo .hafla hiyo ilifanyika siku ya alhamisi katikaHOTELI ya Hyatt Regency Jijini Dar es salaam
  Mgeni Rasmi Waziri Wa Viwanda, Biashara Na Uwekezaji, Mh. Charles Mwijage (Mb) akitoa hotuba kwa wageni waliohudhuria hafla ya kutimiza miaka 20 ya bia ya Serengeti premium lager .Hafla ilifanyika katika Hotel ya Hyatt Regency Jijini Dar Es salaam.
  Mwenyekiti wa Bodi ya SBL Nehemiah Mchechu akitoa hotuba yake katika hafla ya kutimiza miaka 20 ya Bia ya Serengeti Premium Lager na pia kuzinduliwa kwa muonekano mupyaa wa bia hiyo mapema siku ya alhamisi.
  Wageni waalikwa katika hafla hiyo wakifurahia jambo
  Mkurugenzi Mkuu wa SBL Helene Weesie (katikati) akijadiliana jambo na Mkurungezi wa Mawasiliano wa SBL John Wanyacha na Mkurungezi wa Masoko wa SBL Ceasar Mloka katka tafrija mchapalo ya kutimiza miaka 20 ya bia ya Serengeti Premium Lager
  Meneja Masoko wa SBL Anitha Msangi akitoa ufafanuzi wa safari ya bia ya serengeti premium lager toka ilipoanzishwa miaka 20 iliyopita ikiwa ni ubunifu wa mtanzania Winston Kagusa
  Burudani maridadi ikiendelea wakati wa tafrija hiyo

  Mgeni Rasmi Waziri Wa Viwanda, Biashara Na Uwekezaji, Mh. Chrles Mwijage (Mb) (wa kwanza kushoto )akifurahia muonekano mpya wa bia ya Serengeti Premium Lager mara baada ya uzinduizi pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya SBL Nehemiah Mchechu (katikati ) na Mkurugenzi Mkuu wa SBL Helene Weesie katika hafla iliyofanyika katika Hotel ya Hyatt Regency Jijini Dar es salaam.
  Baadh ya wageni waalikwa waliohudhuria hafla hiyo wakiifuatilia kwa makini uzinduizi wa muoenkano mupyaa wa Serengeti Premium Lager
  Wadau wakipozi katika picha ya chui ambayo ni nembo ya bia ya serengeti
  Wadau wakifurahia muonekano mpya wa bia ya Serengeti Premium lager


  Wageni waalikwa wakifurahia burudani iiliyotolewa katika hafla ya maadhimisho ya miaka 20 ya Bia ya Serengeti na pia uzinduzi rasmi wa muoenekano mpya wa bia hiyo .Hafla hiyo iliyofanyika katika Hotel ya Hyatt Regency jijini Dar es salaam.

  0 0


   Rais Dkt John Pombe Magufuli akimpongeza kwa kazi nzuri Katibu Mkuu wa  Wizara ya Maliasili na Utalii Meja Jenerali Gaudence Milanzi baada ya kukagua akikagua pembe za ndovu 50 zilizokamatwa katika operesheni maalum ya  ya kusaka majangili alipofanya ziara ya kushtukiza makao makuu ya Wizara ya Maliasili na Utalii (MPINGO HOUSE) jijini Dar es salaam leo Oktoba 29, 2016.  Rais Dkt John Pombe Magufuli akikagua pembe za ndovu 50 zilizokamatwa katika operesheni maalum ya kusaka majangili alipofanya ziara ya kushtukiza makao makuu ya Wizara ya Maliasili na Utalii (MPINGO HOUSE) jijini Dar es salaam leo Oktoba 29, 2016
  Rais Dkt John Pombe Magufuli akimpongeza kwa kazi nzuri Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Meja Jenerali Gaudence Milanzi baada ya kukagua akikagua pembe za ndovu 50 zilizokamatwa katika operesheni maalum ya ya kusaka majangili alipofanya ziara ya kushtukiza makao makuu ya Wizara ya Maliasili na Utalii (MPINGO HOUSE) jijini Dar es salaam leo Oktoba 29, 2016

  0 0

  Aliyekuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa
   Makosa ya Jinai Bw. Diwani Athumani


  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (katikati), akizungumza na wanafunzi wa kidato cha nne wa Shule ya Sekondari ya Jitegemee JKT Mgulani katika mahafali ya 32 yaliyofanyika jana. Makonda alikuwa mgeni rasmi. Kulia ni Mkuu wa Shule hiyo, Luteni Kanali Robert Kessy na kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi wa Shule hiyo, Brigedia Generali Laurance Magere.
  RC Makonda akimkabidhi cheti Mwalimu Bora wa Shule hiyo, Grace Eliyatosha Moshi.
  RC Makonda akimkabidhi zawadi Mwanafunzi Bora,  Samuel Ndebeto.
  RC Makonda akipeana mkono na mhitimu wa kidato cha nne wa Shule ya Sekondari ya Jitegemee JKT, Samina Rajab baada ya kumkabidhi cheti  katika mahafali ya 32 kwa ushiriki wake wa masuala ya Skauti shuleni hapo. Katikati ni Mwenyekiti wa Bodi wa Shule hiyo, Brigedia Generali Laurance Magere.
  Huyu ndiye ni Mwanafunzi Bora wa Shule hiyo,  Samuel Ndebeto.
  Mkuu wa Mkoa Paul Makonda (katikati), akiwa meza kuu na viongozi mbalimbali. Kutoka kulia ni Mkuu wa Shule ya Sekondari Kigamboni, Luteni Kanali, Laurent Mgongolwa, Mkurugenzi wa Mipango ya Huduma Makao Makuu ya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Luteni Kanali Festus Mang'wela, Mkuu wa Shule ya Sekondari Jitegemee, Luteni Kanali, Robert Kessy, Mwenyekiti wa Bodi wa shule hiyo, Brigedia Generali mstaafu, Laurence Magere, Mwakilishi wa Katibu Tawala wa Wilaya ya Temeke, Hashim Komba na Mjumbe wa Bodi wa Shule hiyo, Sebastian Enosh.
  Mgeni rasm Paul Makonda akiwa katika picha ya pamoja na walimu na wafanyakazi wa shule hiyo.
  Wahitimu wakiwa kwenye mahafali hayo.
  Mhitimu wa kidato cha nne akisakata rhumba kwenye mahafali hayo.
  Walimu na wanafunzi wakicheza kwaito.
  Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Jitegemee JKT wakitoa burudani kwenye mahafali hayo.
  Wahitimu ndani ya ukumbi.
  Mgeni rasmi Paul Makonda akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali waliokuwa jukwaa kuu.
  RC Makonda akiwa katika picha ya pamoja na wahitimu hao.
  RC Makonda akiwa katika picha ya pamoja na wahitimu hao.
  Vijana wa Skauti wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi.
  Mgeni rasmi akiwa katika picha ya pamoja na Kwaya ya shule hiyo.

  Na Dotto Mwaibale

  MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amewataka wazazi na walezi kuwaacha huru watoto wao kuendelea na masomo wayapendayo badala ya kuwachagulia.

  Mwito huo ameutoa katika mahafali ya 32 ya kidato cha nne katika Shule ya Sekondari Jitegemee JKT Mgulani Dar es Salaam jana ambapo alikuwa mgeni rasmi.

  "Watoto wapewe uhuru wa kile wanachopenda kukisomea badala ya kuwachagulia kwa kufanya hivyo itawasaidia kupenda kazi watakayoifanya kutokana na masomo waliyosoma" alisema Makonda.

  Alisema hivi sasa kuna changamoto kubwa kwa watumishi kujiingiza katika vitendo vya ubadhirifu kutokana na kutokuwa wazalendo kutokana na kufanya kazi ambayo imetokana na masomo ambayo hawakuyapenda.

  Alisema kama mtoto anapenda kuwa mtaalamu wa kompyuta muache aendelee na masomo ya kompyuta badala ya kumlazimisha kuwa na taaluma nyingine.

  Mkuu wa Shule hiyo, Luteni Kanali Robert Kessy alisema wahitimu hao wameandaliwa vizuri kwa ajili ya kufanya mtihani wao watakao uanza Jumanne wiki ijayo na kuwa wanategemea wote watafanya vizuri.

  Kessy alisema kuhitimu kidato cha nne ni hatua nyingine ya kuendelea na elimu ya juu hivyo aliwataka wahitimu hao kuondoa wasiwasi katika kipindi hiki cha kuelekea kufanya mtihani wa mwisho.

  Wakisoma risala yao kwa mgeni rasmi Paul Makonda wanafunzi hao walisema changaoto kubwa waliyonayo na uchakavu wa miundombinu shuleni hapo kama mapaa ya vyumba vya madarasa kuezekwa kwa mabati aina ya Asbestors ambayo si mazuri kiafya pamoja na uchakavu wa sakafu ambapo Makonda aliahidi kutoa mabati 2,000 kwa ajili ya kuezekea vyumba 25.

  Katika hatua nyingine Makonda amezitaka shule za sekondari za jeshi katika mkoa wa Dar es Salaam kuhakikisha zinaunda kamati kwa ajili ya kurudisha heshima ya michezo mashuleni kama ilivyokuwa awali.

older | 1 | .... | 1024 | 1025 | (Page 1026) | 1027 | 1028 | .... | 1898 | newer