Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1020 | 1021 | (Page 1022) | 1023 | 1024 | .... | 1896 | newer

  0 0

  Mtangazaji maarufu aliyewahi kutangaza kituo cha redio cha Clouds Fm nakujiunga na EFM redio na baadaye kurudi tena Clouds Fm amefunguliwa mashtaka katika mahakama ya kazi jijini Dar es salaam na EFM redio kwa kile kinachodaiwa kuwa amekiuka mkataba wa kazi wa kituo hicho.

  Kufuatia mashtaka hayo, Efm inadai fidia ya shilingi milioni 200 kwa mtangazaji huyo ambaye alijiunga na kituo hicho kutoka clouds fm na baadae kudaiwa kukatisha mkataba kiholela na kurudi tena clouds fm bila kufuata makubaliano pamoja na sheria alizokubaliana nazo katika mkataba wake awali wakati  alipojiunga na efm redio.

  Kesi hiyo imepangwa kusikilizwa tarehe 23/11/2016 katika mahakama ya kazi Jijini Dar es salaam.


  0 0

  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa akisisitiza jambo wakati wa uzinduzi wa Bodi mpya ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA). Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Prof. Ninatubu Lema.
  Wajumbe wa Bodi wakimsikiliza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa(hayupo pichani), wakati wa uzinduzi wa bodi hiyo jijini Dar es salaam.
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa (kushoto) akimkabidhi vitendea kazi Mwenyekiti wa Bodi hiyo ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA) Prof. Ninatubu Lema (kulia) wakati wa uzinduzi wa Bodi mpya.
  Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA) Prof. Ninatubu Lema, akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa (kushoto), wakati wa uzinduzi wa bodi hiyo. Kulia kwake ni MKurugenzi wa Miundombinu ya Uchukuzi, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Eng. Hussein Mativila.

  ……………………………………………………

  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, ameitaka Bodi mpya ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) kusimamia Menejimenti ya Mamlaka hiyo katika Idara ya Utawala na Rasilimali watu ili kuhakikisha ajira zote zinazotolewa zinazingatia sifa na vigezo vya kuajiri.

  Akizungumza katika uzinduzi wa Bodi hiyo mpya jijini Dar es salaam pamoja na mambo mengine, Profesa Mbarawa ameisisitiza bodi hiyo kuifanyia kazi Ripoti ya Uchunguzi wa uendeshaji wa Viwanja hivyo nchini na kufanya mabadiliko mara moja.

  “Nataka muipitie ripoti niliyomkabidhi Kaimu Mkurugenzi Mkuu na mufanyie maamuzi, suala la kuajiri watu kiholela, ninataka wote waliandikwa kwenye ripoti hiyo kuwa hawana sifa watolewe wapishwe watu wenye sifa ili waweze kufanya kazi”, amesema Waziri Mbarawa.

  Aidha, Profesa Mbarawa ameitaka Bodi hiyo kusimamia kwa uadilifu miundombinu yote ya viwanja vya ndege nchini na kuhakikisha mashine za ukaguzi zinafanya kazi masaa 24 ili kudhibiti mianya yote ya rushwa.

  Ameitaka Bodi hiyo kusimamia vizuri ukusanyaji wa mapato katika viwanja vyote ili kuweza kufikia lengo lililowekwa na kukuza uchumi wa nchi.

  Aidha, Profesa Mbarawa ameitaka Bodi hiyo kushirikiana na wafanyakazi wa Viwanja hivyo katika mambo mbalimbali ili kuboresha utendaji na kuweka uwazi katika utoaji wa huduma katika viwanja hivyo.

  Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Profesa Ninatubu Lema amemhakikishia Waziri huyo kuwa ataongeza ushirikiano na wafanyakazi wote na kusimamia maagizo yote yaliyotolewa.

  Ameahidi kuboresha huduma katika viwanja vyote nchini na kusema kuwa umuhimu wake utaongeza mapato katika viwanja hivyo na nchi kwa ujumla.

  0 0

  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akimfafanulia jambo Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Kuwahudumia Wakimbizi (UNHCR), Chansa Kapaya (kulia) wakati Mwakilishi huyo alipomtembelea Naibu Waziri ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo, kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali ya kuwahudumia Wakimbizi nchini. Katikati ni Mkurugenzi wa Idara ya wakimbizi wa Wizara hiyo, Harrison Mseke. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 
  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia), akimsikiliza Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Kuwahudumia Wakimbizi (UNHCR), Chansa Kapaya wakati alipokuwa anamfafanulia jambo kuhusu masuala ya wakimbizi nchini. Mwakilishi huyo alipomtembelea Naibu Waziri ofisini kwake, jijini Dar es Salaam leo. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

  0 0

     Boeing 787 Dreamliner offers inatoa huduma bora za daraja la kwanza na kawaida.
    Boeing 787 ndiyo ndege ya kifahari katika Shirika la Ndege la Etihad 
    Kuanza safari yake ya kwanza kutoka Abu Dhabi kwenda Tokyo Narita
    Inahudumiwa na wahudumu mahiri katika fani za upishi, vinywaji na malezi 
  Kuanzia Desemba, mwaka huu Boeing 787 itaanza rasmi safari zake kati ya Abu Dhabi na Tokyo Narita  ikiwa imeboreshwa zaidi. 

  Ndege hiyo yenye daraja la kwanza, kati na daraja la kawaida inachukua nafasi iliyoachwa na ndege ya Airbus A340, ambayo kwa sasa imepangiwa vituo vingine tofauti kwa safari  za kila siku.

  Ofisa mkuu wa Mipango na Mikakati wa Shirika la Etihad Kevin Knight amesema, “Ktumia ndege hiyo katika safari za Tokyo, ni kielelezo cha kutambua umuhimu wa kituo hicho cha Japan, pia ni sehemu ya utekelezaji wa mikakati iliyowekwa na Shirika la Etihad.”

   Aliongeza kuwa “Ubora wa huduma zinazotolewa katika ndege hiyo, unaongeza thamani yetu katika ushindani wa masoko ya huduma za anga.”
  Ndege ya Boeing 787 ina jumla ya viti 235. Kati ya viti hivyo, 8 vipo katika daraja la kwanza, 28 daraja la kati na 199 vya daraja la kawaida.

  Viti katika daraja la kwanza vimeboreshwa kwa kuongezewa nafasi ya kutosha huku zikinakshiwa na kitambaa laini cha Poltrona Frau. Viti hivyo pia huweza kutumika kama vitanda ambavyo huweza kubeba mpaka watu wawili. Huduma zingine katika daraja hilo ni runinga na chakula kinachotolewa kwa oda maalumu.

  Katika daraja la kati, wateja hupewa fursa ya kuchagua aina tatu za vyakula. Wahudumu wa vyakula na vinywaji pia wanatoa ushauri kwa abiria kuhusu aina ya chakula pamoja na vinywaji maalumu.
  Abiria katika daraja hili pia wamewekewa mavazi maalumu pamoja na viatu vya wazi na sanduku maalumu lenye vifaa vya kutumia mtu binafsi.

  Ndege hiyo pia imesheheni vifaa mbalimbali vya burudani kama vile Panasonic eX3 ambayo ina chaneli saba za televisheni, video, michezo na huduma ya mtandao unaotumia Wi-Fi pamoja na mfumo wa USB kwa kila kiti.

  Huduma hii mpya inajumuisha wafnyakazi kutoka mataifa mbalimbali wakiwamo watumiaji wa lugha ya Kijapani. Wasaidizi wa kulea watoto pia wanapatikana katika kila safari ya  Boeing 787 ili kutoa msaada wa malezi.

  Shirika la Etihad lilianzisha safari za kwenda Japan Februari,2010 ikiwa na ndege ya kila wiki kwa safari za AbuDhabi na Nagoya kupitia Beijing. Ratiba hiyo ilibadilishwa na kuwa ya kila siku Machi 2014 wakati safari za Tokyo Narita zikiongezwa katika ratiba ya Japan mwaka 2010 kwa kutumia ndege za kila wiki na kwa safari za kila siku mwaka 2013.
  Ratiba ya ndege kati ya Abu Dhabi na Tokyo Narita, itakayoanza rasmi Desemba 2016.

  Namba ya ndege

  Mwanzo

  Muda wa

  Kutoka

  Kituo

  Muda wa

  Kufika

  Mzunguko

  Aina ya ndege

  EY878

  Abu Dhabi

  04:10

  usiku

  Tokyo Narita

  07:05

  mchana

  Kila siku

  B787-9

  EY871

  Tokyo Narita

  03:25 usiku

  Abu Dhabi

  10:45

  jioni

  Kila siku

  B787-9

  Muhimu: Safari zimeorodheshwa kwa kuzingatia muda wa eneo husika. 

  0 0

  Mkurugenzi wa Habari, Hassan Abbas (mwenye suti) akizungumza katika ya kipindi mahojiano maalum cha 360 kinachorushwa na kituo cha Televisheni cha CLOUD wakati wa ziara yake ya kutembelea vyombo vya habari Jijini Dar es Salaam na kuelezea maudhui mbalimbali yaliyopo katikamuswada ya sheria ya huduma ya Habari. Wengine ni Watangazaji wa Kituo hicho, Babbie Kabae (kushoto) na Hassan Ngoma.
  Mkurugenzi wa Habari, Hassan Abbas akibadilishana mawazo na Watangazaji wa kipindi cha Michezo cha kituo cha Redio cha CLOUDS FM cha Jijini Dar Es Salaam, kutoka kutosho Shafii Dauda (kulia) na Mbwiga mbwiguko (katikati) wakati wa ziara yake ya kutembelea vyombo mbalimbali vya habari leo Jijini Dar es Salaam. Katika ziara hiyo Msemaji huyo wa Serikali alizungumzia maudhui mbalimbali yaliyopo katika muswada wa sheria ya huduma ya habari.
  Mkurugenzi wa Habari, Hassan Abbas (mwenye suti) akiwa katika picha ya pamoja na Wahariri na Waandishi wa Habari wa kituo cha habari cha Redio na Televisheni cha CLOUD wakati wa ziara yake ya kutembelea vyombo vya habari leo Jijini Dar es Salaam. Katika ziara hiyo Msemaji huyo wa Serikali alizungumzia maudhui mbalimbali yaliyopo katika muswada wa sheria ya huduma ya habari.
  Mkurugenzi wa Habari, Hassan Abbas akipokelewa na Meneja vipindi wa kituo cha redio cha Times FM cha Jijini Dar es Salaam, Amani Misana wakati wa ziara yake ya kutembelea vyombo mbalimbali vya habari leo Jijini Dar es Salaam. Katika ziara hiyo Msemaji huyo wa Serikali alizungumzia maudhui mbalimbali yaliyopo katika muswada wa sheria ya huduma ya habari.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Redio cha Times FM cha Jijini Dar es Salaam, Rehure Nyaulawa akifafanua jambo kwa Mkurugenzi wa Habari, Hassan Abbas kuhusu utendaji kazi wa gari la urushaji matangazo ya nje. Katika ziara hiyo Msemaji huyo wa Serikali alizungumzia maudhui mbalimbali yaliyopo katika muswada wa sheria ya huduma ya habari.

  Mkurugenzi wa Habari, Hassan Abbas akizungumza katika ya kipindi mahojiano maalum ya kipindi cha Hatua Tatu kinachorushwa na kituo cha Redio cha Times FM cha Jjijini Dar es Salaam kuelezea maudhui mbalimbali yaliyopo katikamuswada ya sheria ya huduma ya Habari. Anayefuatilia mahojiano hayo ni mahojiano hayo ni mtangazaji wa kituo hicho Stanslaus Lambat.
  Mkurugenzi wa Habari, Hassan Abbas akiwa katika picha ya pamoja na Bodi ya Uhariri ya Kituo cha Redio cha Times FM cha Jijini Dar es Salaam wakati wa ziara yake ya kutembelea vyombo mbalimbali vya habari Jijini Dar es Salaam. Katika ziara hiyo Msemaji huyo wa Serikali alizungumzia maudhui mbalimbali yaliyopo katika muswada wa sheria ya huduma ya habari.

  (PICHA NA ISMAIL NGAYONGA)

  ………………………………………………………………………………

  Na Beatrice Lyimo-MAELEZO-Dar es Salaam

  SERIKALI imesema hakutokuwa na matumizi mabaya ya mamlaka anayopewa Waziri anayesimamia tasnia ya habari katika muswada wa sheria ya huduma ya habari isipokuwa kwa masuala yatakayohatarisha usalama wa Taifa.

  Imesema Serikali haiwazuii waandishi wa habari kukosoa sera, matamko na ahadi mbalimbali zinazotolewa na Viongozi wa kitaifa pindi wanaposhindwa kutekeleza maagizo wanayoyatoa kwa wananchi.

  Akizungumza katika mwendelezo wa ziara yake ya kutembelea vyombo mbalimbali vya habari leo Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Hassan Abbas alisema muswada huo unatoa fursa kwa chombo cha habari kupeleka malalamiko yake mahakamani pindi inapotokea kutokubaliana na hatua itakayoweza kuchuliwa na Waziri mwenye dhamana ya habari.

  Kwa mujibu wa Abbasi alisema yapo masuala kadhaa yanayopaswa kuchuliwa hatua za haraka za maamuzi ikiwemo suala la uchochezi, uasi wa kikundi fulani cha watu kinachotaka kuigombanisha Serikali na wananchi.

  Aliongeza kuwa hata katika mikataba ya kimataifa ikiwemo kifungu cha 19 mkataba wa geneva wa mwaka 1966 umeeleza kuhusu haki ya kupata habari na taarifa ingawa upo ukomo katika masuala kadhaa ikiwemo suala la usalama wa taifa.

  “Uchochezi ni kuhatarisha amani ya nchi, lakini mwandishi akiikosoa Serikali haitokuwa uchochezi bali kwa atakayeleta habari za uchochezi kwa maana ya uasi atatakiwa kuwajibishwa” alifafanua Mkurugenzi Abbas.

  Aidha alisema kuwa muswada huo umekusudia kuanzishwa kwa Baraza la Maadili litakalokuwa na wajumbe saba, ambapo wanne kati yao ni kutoka katika tasnia ya habari ikiwemo mwenyekiti wa Baraza na watakuwa na mamlaka ya kusimamia maslahi na usalama wa waandishi.

  Akifafanua zaidi alisema kuwa lengo la Serikali ni kuhakikisha kuwa mchakato wa kupata Sheria ya huduma ya habari unafika mwisho ambapo mchakato wake umechukua miaka 20 mpaka sasa.

  Alisema kuwa lengo la Serikali ni kuhakikisha kuwa muswada huo unapitishwa na Bunge ili uweze kuwa sheria kamili na hatimaye kuifanya tansia ya habari kuwa taaluma yenye kuheshimika zaidi.

  Pia alisema kuwa muswada huo utasaidia sekta ya habari kuwa muhimili wenye nguvu na taaluma iliyokamilika yenye haki zake kama upatikaji wa bima za afya kwa waandishi wa habari.

  Abbasi alisema iwapo sheria hiyo itapitishwa itatumika upande wa Tanzania Bara pekee na si Zanzibar, kwa kuwa suala la habari halipo katika mambo ya Muungano, ingawa sekta hizo zinashirikiana kwa namna moja au nyingine.

  0 0

  Rais wa Tanzania Christian Deliberation Burea (TCDB) Bw. Carolous Bujimu (kushoto) akielezea mwongozo wa programu ya kusimamia na kukuza vipaji kwa wasanii wakati wa kikao na wadau wa tasnia ya Filamu na Muziki leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo
  Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo (katikati) akizungumza na wadau walioshiriki katika kikao cha uwasilishaji wa mwongozo wa programu ya kusimamia na kukuza vipaji kwa wasanii kutoka TCDB leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Rais wa Tanzania Christian Deliberation Burea (TCDB) Bw. Carolous Bujimu.
  Mjumbe kutoka COSOTA Bw. Paul Makula akichangia mada wakati wa kikao cha uwasilishaji wa mwongozo wa programu ya kusimamia na kukuza vipaji kwa wasanii kutoka TCDB leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Rais wa Shirikisho la Filamu Bw. Simon Mwakifwamba
  Afisa Kodi Mkuu kutoka TRA Bw. Sydney Mkamba (kushoto) akizungumza na wadau wa filamu na muziki wakati wa kikao cha uwasilishaji wa mwongozo wa programu ya kusimamia na kukuza vipaji kwa wasanii kutoka TCDB leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mrakibu Msaidi wa Polisi (ASP) Bw. Mboka Minga
  Rais wa Shirikisho la Filamu Bw. Simon Mwakifwamba (kushoto) akizungumza wakati wa kikao cha uwasilishaji wa mwongozo wa programu ya kusimamia na kukuza vipaji kwa wasanii kutoka TCDB leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Afisa Sanaa kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bibi. Joyce Hagu
  Mrakibu Msaidi wa Polisi (ASP) Bw. Mboka Minga (aliyesimama) akichangia wakati wa kikao cha uwasilishaji wa mwongozo wa programu ya kusimamia na kukuza vipaji kwa wasanii kutoka TCDB leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa Ubunifu kutoka Wanene Studio Bw. Rodgers Charles

  …………………………………………………………

  Na: Genofeva Matemu – WHUSM,

  Wadau wa Tasnia ya Filamu na Muziki wameishauri Taasisi ya Tanzania Christian Deliberation Burea (TCDB) kuandaa upya mwongozo wa programu ya kusimamia na kukuza vipaji kwa kuwa na takwimu kutoka kwa Taasisi zote zinasimamia sekta ya Filamu na Muziki nchini.

  Rai hiyo imetolewa na wadau mbalimbali wa tasnia hizo walioshiriki katika kikao kilichoandaliwa kwa ajili ya kuwasilisha mwongozo huo kwa wadau leo Jijini Dar es Salaam.

  Akizungumza wakati wa kikao hicho Rais wa Shirikisho la Filamu Bw. Simon Mwakifwamba amesema kuwa ni vyema mwongozo wa programu ya kusimamia na kukuza vipaji kutoka TCDB kuzingatia takwimu na taarifa sahihi kutoka kwa wadau ili kuweza kuendana na hali halisi ya tasnia hizo.

  “Katika kutekeleza azma ya Taasisi ya TCDB ni vyema mkaandaa mchakato wa kufikia na kushirikisha vyombo vya wadau kuanziia ngazi ya chini kwa kupitia shirikisho la filamu pamoja na Taasisi za Serikali ambao watachangia katika kuandaa mwongozo ulio bora” amesema Bw. Mwakifwamba.

  Aidha Mrakibu Msaidi wa Polisi (ASP) Bw. Mboka Minga ameitaka Taasisi ya TCDB kuandaa mwongozo wa programu ya kusimamia na kukuza vipaji ili uweze kuendana na jitihada zilizofanywa na Serikali katika kusimamia na kupambana na maharamia wa kazi za sanaa.

  Naye Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo ameitaka Taasisi ya TCDB kushirikisha wataalamu wa tasnia ya Filamu na Muziki ili waweze kuendesha Taasisi hiyo kitaalamu na kwa weledi.

  Tanzania Christian Deliberation Burea (TCDB) ni Taasisi ambayo inalenga kusimamia na kukuza vipaji vya wasanii wa filamu na muziki kuanzia ngazi ya Wilaya kwa kuibua na kusimamia uandaaji wa kazi za sanaa.

  0 0

  Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya YARA Tanzania Ltd, Alexandre Macedo, akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa Usafirishaji wa mbolea kwa njia ya Reli TRL, Uzinduzi huo umefanyika leo kwenye Ofisi za YARA Tanzania zilizopo Kurasini jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Naibu Kaimu Mkurugenzi Uendeshaji wa TRL, Focus Makoye Sahani.
  Azungumzia uzinduzi huo Mkurugenzi huyo alisema kuwa YARA kwa kushirikiana na TRL na SAGCOT, wameamua kuzindua njia hiyo ya usafirishaji ili kupunguza gharama za usafirishaji kwa kutumia barabara na maji ili kuwafikia walengwa kwa wakati na kwa gharama nafuu, ambapo awali kusafirisha Tani moja kutoka Viwandani Ulaya hadi jijini Dar es Salaam, ilikuwa ni Dola za Kimarekani 40, kwa Tani moja na Dar es Salaam hadi Tabora ni Dola za Kimarekani 100 kwa Tani moja kwa njia ya barabara. Aidha Macedo, alisema kuwa kuamua kutumia usafiri wa Treni sasa usafiri utashuka kwa asilimia 35.
  Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya YARA Tanzania Ltd, Alexandre Macedo (katikati) Naibu Kaimu Mkurugenzi Uendeshaji wa TRL, Focus Makoye Sahani (kushoto) na Mratibu wa Program ya SAGCOT Centre, Emmanuely Lyimo, kwa pamoja wakionyesha ushirikiano kwa kushikana mikono kuashiria uzinduzi rasmi wa Usafirishaji wa mbolea kwa njia ya Reli TRL uliofanyika leo kwenye Ofisi za YARA Tanzania zilizopo Kurasini jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya YARA Tanzania Ltd, Alexandre Macedo (katikati) Naibu Kaimu Mkurugenzi Uendeshaji wa TRL, Focus Makoye Sahani (kushoto) na Mratibu wa Program ya SAGCOT Centre, Emmanuely Lyimo (wa pili kulia) na Afisa Habari wa YARA Tanzania, Lynda Byaba (kulia), kwa pamoja wakionyesha ushirikiano kwa kushikana mikono kuashiria uzinduzi rasmi wa Usafirishaji wa mbolea kwa njia ya Reli TRL uliofanyika leo kwenye Ofisi za YARA Tanzania zilizopo Kurasini jijini Dar es Salaam. Picha Zote na Mafoto Blog
  Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya YARA Tanzania Ltd, Alexandre Macedo (aliyenyoosha mkono) akiwaonyesha baadhi ya waandishi wa habari maeneo mbalimbali ya Ofisi kwao wakati walipotembelea kwenye uzinduzi wa usafirishaji kwa njia ya Treni uliofanyika leo.
  Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya YARA Tanzania Ltd, Alexandre Macedo, akionyesha jinsi mbolea inavyopakiliwa kwenye Mabehewa kabla ya kusafirishwa.
  Wafanyakazi wa Kampuni ya YARA wakipakia mifuko ya Mbolea kwenye Mabehewa tayari kwa kusafirishwa.
  Wafanyakazi wa Kampuni ya YARA wakipakia mifuko ya Mbolea kwenye Mabehewa tayari kwa kusafirishwa.

  Bw. Macedo akipanda kwenye Injini ya Treni kuashiria uzinduzi huo leo.

  Bw. Macedo akipanda kwenye Injini ya Treni kuashiria uzinduzi huo leo.
  Mifuko ya Mbolea ikiwa tayari kupakiwa kwenya magari ili kusogezwa eneo la kupakilia kwenye Mabehewa ya Treni
  Wafanyakazi wa YARA wakijiandaa kushusha katika magari na kupakia kwenye Mabehewa.
  Mabehewa yakisubiri kupakiliwa.....

  Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya YARA Tanzania Ltd, Alexandre Macedo, Naibu Kaimu Mkurugenzi Uendeshaji wa TRL, Focus Makoye Sahani wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanahabari waliotembelea Ofisi hizo leo wakati wa uzinduzi huo.

  0 0


    Mfalme Mohammed  VI wa Morocco akibusu Masahaf kabla ya kumkabidhi Waziri Mkuu Kasim Majaliwa katika hafla fupi ya uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa msikiti kwenye eneo la BAKWATA Kinondoni jijini Dar es salaam Oktoba 25, 2016.  Kulia ni Mufti Mkuu wa Tanzania, Abukary Zubeir. Jumla ya Masahaf 10000 zilikabidhiwa na Mfalme huyo
   Mfalme Mohammed  VI wa Morocco na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  wakishuhudia wakati Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakary Zubeir (kulia)  akitia saini Makubaliano ya ujenzi wa Msikiti kwenye eneo la BAKWATA, Kinondoni jijini Dar es salaam Oktoba 25, 2016
   Mfalme Mohammed  VI wa Morocco na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  wakishuhudia wakati Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakary Zubeir (kulia)  akitia saini Makubaliano ya ujenzi wa Msikiti kwenye eneo la BAKWATA, Kinondoni jijini Dar es salaam Oktoba 25, 2016
  Mfalme   Mohammed VI wa Morocco,  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa , Rais Mstaafu Alhaj  Ali Hassan Mwinyi na Makamu wa Rais Mstaafu, Dkt. Mohammed Bilal wakiwa katika hafla fupi ya uwekaji jiwe la msingi la ujenzi wa msiki uliofnywa na Mfalme Mohammed wa Morocco kwenye  eneo la BAKWATA, Kinondoni jijini Dar es salam Oktoba 25, 2016.  Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu
  .

  0 0

  Viboko Katika Hifadhi ya Taifa ya Katavi wakiwa wanaathirika kutokana na upungufu wa maji katika Mto Katuma. Waziri Makamba ametangaza hatua za haraka na za muda mrefu za kurejesha mto huo katika hali yake ya awali.
   
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. January Makamba akiangalia eneo lililokuwa likitumiwa na Jema Sitalike Project ambao walizuiwa kuendelea na shughuli za uchenjuaji wa dhahabu kutokana na kutokuwa na vibali. Wengine katika picha ni pamoja Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jenerali Mstaafu Raphael Muhuga.
  Mashimo yaliyokuwa yakitumiwa na Jema Sitalike Project ambao walizuiwa kuendelea na shughuli za uchenjuaji wa dhahabu kutokana na kutokuwa na vibali, yakiwa yameachwa wazi hali inayotishia usalama wa wananchi wanaozuka maeneo hayo. Waziri Makamba ameagiza kusimamishwa kwa shughuli za Mradi wa Jema ambao kwa sasa wamehamishia shughuli zao Mkoani Mwanza na kuwataka kuchukua hatua za haraka kufunika mashimo yaliyopo Sitalike - Katavi.
   
  Na Lulu Mussa, Katavi 

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba amesema kuwa uharibifu wa Mazingira katika Mto Katuma ni tishio kubwa kwa uhai wa Hifadhi ya Taifa ya Katavi na wakazi wa Mkoa huo. 

  Akiwa katika mwendelezo wa ziara yake ya siku 16 kutembelea Mikoa mbalimbali hapa nchini, Waziri Makamba amesema kuwa Mto Kasuma uko hatarini kutoweka kutokana na ongezeko la shughuli za binadamu, wingi wa mifugo, Uchimbaji wa madini, ukataji wa miti na uchepushaji wa maji kunakopelekea kupoteza mtiririko wa maji yenyewe. 

  Waziri Makamba amesema ni vema kuwa na mikakati na hatua za haraka na zile za muda mrefu ikiwa ni pamoja na kufanya sensa ya mifugo ili kuweza kujua Mkoa una mifugo kiasi gani na kuainisha maeneo ya malisho. "Zoezi hili si hiari, ni lazima na takwa la kisheria' Makamba alisisitiza. 

  Imependekezwa pia kufanyika kwa Ubomoaji wa mabanio yanayokinga maji kama hatua ya haraka ili maji yaweze kutiririka kwa wingi katika kipindi hiki cha kiangazi, na kuagiza kufanyika kwa doria za mara kwa mara ili kubaini watu wanaokiuka taratibu hizo. 

  Waziri Makamba pia amezitaka Mamlaka za bonde kutimiza wajibu wao kwa kutoa vibali stahiki kulingana na ujazo wa maji uliopo katika maeneo yao ili kujenga usawa wa matumizi sahihi ya rasilimali maji. ' Mamlaka za bonde zisitoe vibali ofisini na operesheni ifanyike kwa wote wasio na vibali" Alisema Waziri Makamba. 

  Pia, Waziri Makamba ameagiza kufanyika kwa Tathimini ya athari kwa mazingira kwa Mto Kasuma na kuuagiza uongozi wa Mkoa wa Katavi kuainisha baadhi ya maeneo ambayo yatatangazwa kama maeneo nyeti ili kunusuru mazingira ya Katavi na ustawi wa Mto Katuma.

  "Kuwe na tozo ya uharibifu wa Mazingira na tozo hiyo iendane na kiwango cha uharibifu atakachofonya muhusika" ,Akiongea na Wadau wa Mazingira katika Ukumbi wa Maji Mkoani Katavi Waziri Makamba amekumbusha watumishi wa Umma Nchini kuwa na nidhamu na uwajibikaji wa dhati na kusisitiza kuwa hakuna muda wa kubembelezana. "Fanyeni kazi kwa weledi, nidhamu na uadilifu" alisema Makamba. 

  Katika hatua nyingine Waziri Makamba ametembelea eneo ulipokuwa mradi wa uchenjuaji wa dhahabu wa Jema Sitalike Project ambao ulikua ukifanya shughuli zake bila kibali cha Wizara ya Nishati na Madini na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC). 

  Waziri Makamba ameagiza kusimamishwa kwa shughuli za Mradi wa Jema ambao kwa sasa wamehamishia shughuli zao Mkoani Mwanza na kuwataka kuchukua hatua za haraka kufunika mashimo yaliyopo Sitalike - Katavi ili kunusuru uhai wa viumbe vinavyozunguka maeneo ya Sitalike. 

  Waziri Makamba yuko Mkoani Katavi kwa ziara ya kikazi na hii leo amekutana na Viongozi wa Vikundi vya Mazingira, katembelea eneo lilikokuwa na shughuli za Uchimbaji wa Madini na chanzo cha Mto Katuma.
   

  0 0  Na Kijakazi Abdalla Habari Maelezo


  Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imetumia kiasi ya dola 90 elfu kuifanyia matengenezo ya kawaida Meli ya MV Mapinduzi ll iliyopelekwa Chelezoni Mombasa.

  Akizungumza na waandishi wa Habari Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji Mustafa Abuod Jumbe mara baada ya kuwasili Bandarini Malindi amesema itaanza safari zake za kawaida Pemba kuanzia kesho ili kupunguza usumbufu wa usafiri uliojitokeza baada ya kuondoaka meli hiyo.

  Alisema kuwa meli hiyo imefanyiwa matengenezo ya kawaida na hakuna kitu kilicho badilishwa na baada ya matengenezo hayo itakuwa chini ya Mamlaka ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kutoka kwa udhamini wa mtengenezaji.

  Hata hivyo Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji amesema hivi sasa Serikali imo katika mchakato wa kununua meli nyengine mbili mpya, moja kwa ajili ya abiria na mizigo na nyengine itakuwa ya mafuta

  Mapema Nahodha wa Meli hiyo Abdulrahman Mzee amesema matengenezo ya meli yaliyofanyika yamekwenda sambamba na muda uliopangwa na yamefanywa kwa hali ya ubora kabisa

  Amesema kuwa kufanyika kwa matengenezo ya meli hiyo ni jambo la kawaida kwa chombo chochote cha usafiri jambo linalokipa ubora chombo husika.

  Meli ya MV Mapinduzi ll iliondoka Zanzibar wiki mbili zilizopita kwenda chelezoni Mombasa na imerejea Zanzibar leo kupitia Pemba ikiwa imechukua abiria 1200 pamoja na mizigo.

  0 0

   

  Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) (katikati) akiwa na Mawaziri wenzake kutoka nchi za Kenya, Uganda na Ethiopia (wengine hawako Pichani) wakionesha kwa waandishi wa habari (hawako pichani pia) nyaraka za makubaliano ya uteuzi wa mradi utakao fadhiliwa kwa pamoja kati ya Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) na Serikali ya Korea, wenye thamani ya dola Milioni 50 za Marekani sawa na zaidi ya shilingi Bilioni 100.18 zitakazotumika kujenga njia ya usafirishaji umeme kwa njia ya gridi ya Taifa, yenye msongo wa kV 400 katika ukanda wa kaskazini Magharibi kwa upande wa Tanzania itakayoanzia mkoani Mbeya, Nyakanazi hadi Mkoani Kigoma. wakati wa Mkutano wa 5 wa ushirikiano wa Kiuchumi kati ya Korea Kusini na nchi za Kiafrika, unaoendelea Jijini Seoul Korea Kusini.
  Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), kushoto, na Mwenyekiti ambaye pia ni Rais wa Benki ya EXIM ya Korea Kusini, Lee Duk-Hoon, wakitia saini Mkataba wa mkopo wenye masharti nafuu wa Dola za marekani milioni 90.092 sawa na zaidi ya shilingi Bilioni 194 za Tanzania, kwa ajili ya mradi wa Upanuzi wa Miundombinu ya mfumo wa maji taka Jijini Dar es salaam, wakati wa Mkutano wa Ushirikiano wa Kiuchumi kati ya Korea na nchi za Afrika, unaoendelea Jijini Seoul, Korea Kusini
  Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), kushoto, na Mwenyekiti ambaye pia ni Rais wa Benki ya EXIM ya Korea Kusini, Lee Duk-Hoon, wakipeana mikono baada ya kusaini Mkataba wa mkopo wenye masharti nafuu wa Dola za marekani milioni 90.092 sawa na zaidi ya shilingi Bilioni 194 za Tanzania, kwa ajili ya mradi wa Upanuzi wa Miundombinu ya mfumo wa maji taka Jijini Dar es salaam, wakati wa Mkutano wa Ushirikiano wa Kiuchumi kati ya Korea na nchi za Afrika, unaoendelea Jijini Seoul, Korea Kusini
  Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), kushoto, na Mwenyekiti ambaye pia ni Rais wa Benki ya EXIM ya Korea Kusini, Lee Duk-Hoon, wakionesha mkataba waliousaini wa mkopo wenye masharti nafuu wa Dola za marekani milioni 90.092 sawa na zaidi ya shilingi Bilioni 194 za Tanzania, kwa ajili ya mradi wa Upanuzi wa Miundombinu ya mfumo wa maji taka Jijini Dar es salaam, wakati wa Mkutano wa Ushirikiano wa Kiuchumi kati ya Korea na nchi za Afrika, unaoendelea Jijini Seoul, Korea Kusini
  Baadhi ya wajumbe kutoka Tanzania na Korea walioshuhudia utiawaji saini wa mkataba wa mkopo wenye masharti nafuu wa Dola za marekani milioni 90.092 sawa na zaidi ya shilingi Bilioni 194 za Tanzania, kwa ajili ya mradi wa Upanuzi wa Miundombinu ya mfumo wa maji taka Jijini Dar es salaam, wakati wa Mkutano wa Ushirikiano wa Kiuchumi kati ya Korea na nchi za Afrika (KOAFEC), unaoendelea Jijini Seoul, Korea Kusini

  Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (wa nne kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Mawaziri wenzake wa Fedha kutoka nchi 54 za Kiafrika, wanaohudhuria Mkutano wa 5 wa Ushirikiano wa Kiuchumi kati ya Korea na nchi za Afrika (KOAFEC), unaofanyika Jijini Seoul, Korea Kusini.
  Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo Afrika anayeiwakilisha Tanzania (AfDB) Dkt. Nyamajeje Weggoro (katikati) wakimsikiliza kwa makini Raisi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) kabla ya kuanza kwa mkutano unaojadili namna kilimo na mapinduzi ya viwanda vinavyoweza kuibadili Afrika Kiuchumi na Kijamii wakati wa Mkutano wa 5 wa Ushirikiano wa Kiuchumi kati ya Korea na nchi za Afrika (KOAFEC) unaofanyika Jijini Seoul, Korea Kusini,
  Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (kulia) akitia saini makubaliano ya uteuzi wa mradi utakao fadhiliwa kwa pamoja kati ya Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) na Serikali ya Korea, wenye thamani ya dola Milioni 50 za Marekani sawa na zaidi ya shilingi Bilioni 100.18 zitakazotumika kujenga njia ya usafirishaji umeme kwanjia ya gridi ya Taifa, yenye msongo wa kV 400 katika ukanda wa kaskazini Magharibi itakayoanzia mkoani Mbeya, Nyakanazi hadi Mkoani Kigoma.
  …………………………………………………………………………………..

  Benny Mwaipaja, WFM, Seoul, Korea

  TANZANIA, Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) na Korea ya Kusini zimetiliana saini makubaliano ya pamoja kutekeleza mradi wa ujenzi wa njia ya umeme gridi ya Kaskazini Magharibi inayoanzia mkoani Mbeya, Nyakanazi hadi Kigoma, yenye msongo wa kV 400 mbapo Serikali ya Korea imeahidi kutoa Dola zaMarekani milioni 50 sawa na zaidi ya shilingi Bilioni 100.18, kwa ajili ya kugharamia mradi huo.

  Hali kadhalika, Tanzania na Benki ya Exim ya Korea, zimesaini Mkataba wa mkopo wenye masharti nafuu wa Dola za marekani milioni 90.092 sawa na zaidi ya shilingi Bilioni 194 za Tanzania, kwaajili ya mradi wa Upanuzi waMiundombinu ya mfumo wa maji taka Jijini Dar es salaam.

  Kwa upande wa Tanzania, Makubaliano pamoja na Mkataba vimesainiwa na Mhe. Dkt. Philip Mpango (MB) Waziri wa Fedha na Mipango kwa niaba ya Serikali, Oktoba 25, 2016 Jijini Seoul nchini Korea Kusini huku upande wa AfDB, aliye saini ni Rais wa Benki hiyo Adesina Akinwumi, na kwa upande wa Benki ya Exim, mkataba huo umesainiwa na Mwenyekiti ambaye pia ni Rais wa Benki hiyo Lee Duk-Hoon.

  Akizungumza mara baada ya kutia saini makubaliano na mkataba huo, Dkt. Mpango amesema makubaliano na mkataba vilivyosainiwa vina manufaa makubwa kwa wananchi wa Tanzania.

  “Wananchi wa Upande ule waanze kufurahia kwamba maendeleo yanakuja na hasa tunaposema maendeleo ya viwanda ambavyo nilazima vitumie umeme, na kwamba mradi huu unatarajia kupelekwa hadi Mbeya” Amesisitiza Dkt. Mpango.

  Dkt. Mpango, amesema kuwa mradi huo una umuhimu mkubwa pia kwakuwa serikali imedhamiria kuufungua ukanda wa Magharibi mwa Tanzania, kwa upande wa viwanda vya aina mbalimbali.

  Kwa upande wake, Naibu Mkurugenzi Mtendaji (Uwekezaji) wa Shirika la Ugavi wa Umeme nchini Tanzania-TANESCO, Decklan Mhaiki, amesema mradi wa umeme wa Nyakanazi hadi Kigoma utakuwa na urefu wa kilometa 280 na utakapo kamilika utaondoa changamoto ya shirika hilo kuzalisha umeme unatumika katika ukanda huo wa Magharibi hususan Kigoma, kwa kutumia majenereta ambayo uendeshaji wake ni ghali na umeme wake si wa uhakika.

  “Kuleta laini kama hii, kwanza itapunguza gharama kubwa, na umeme wa ziada utakao zalishwa tunaweza kuuza nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia Congo, upande wa pili wa Ziwa Tanganyika, lakini kikubwa ni kuwahakikishia wananchi wa mkoa wa Kigoma kuwa na umeme wa uhakika” ameongeza Bw. Mhaiki.

  Akizungumzia mkataba wa ujenzi wa miundombinu ya maji taka Jijini Dar es salaam, Dkt. Philip Mpango, amebainisha kuwa mradi huo unatarajia kuwa na tija kwakuwa utatatua changamoto ya majitaka kutuama mitaani hasa wakati wa mvua na kusababisha magonjwa ya mlipuko kikiwemo kipindupindu.

  Akifafanua kuhusu mradi huo, Mchumi ambaye pia ni Afisa anayeshughulika na utafutaji wa Fedha za Nje kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Melckzedek Mbise, amesema kuwa mradi wa maji wa Ruvu unatarajia kuongeza wingi wa maji Jijini Dar es salaam, utakaosababisha uzalishaji wa maji taka pia kuongezeka, hivyo mradi huo wa kuondoa maji taka umekuja wakati muafaka.

  “Mradi huu umekuja wakati muhimu na mkopo una masharti nafuu sana” Amesisitiza Bw. Mbise.

  Naye Afisa Mkuu wa utafutaji rasilimali kutoka Wizara ya Fedha na Mipango Zanzibar, Sabra Issa Machano, amesema kuwa kati ya nchi 54 za Kiafrika zinazohudhuria mkutano wa Tano wa Ushirikiano wa Kiuchumi kati ya Korea naAfrika, Mjini Seoul Korea, ni nchi nne tu zilizopewa mkopo na ufadhili ambazo ni Kenya, Uganda na Ethiopia, huku Tanzania ikipewa kiasi kikubwa zaidi cha fedha jambo linaloonesha kuwa Tanzania inakubalika Kimataifa.

  0 0


  Kaimu Meneja wa Bandari wa Bandari Tanga, Hendry Arika, (kushoto) akimtambulisha kiongozi wa Mabalozi wa Jumuiya ya Ulaya wanaowakilisha nchi zao nchi, Roeland Vande Geer kwa Captain Bandari, Endrew Matiria wakati ulipofanya ziara yake Tanga kuangalia fursa za uwekezaji baada ya ujio wa mradi wa Bomba la Mafuta Tanga.

  Mabalozi 12 kutoka nchi mbalimbali wamefika Tanga kuangalia furasa za uwekezaji kwa kutembelea Bandari ya Tanga, Bohari ya mafuta ya GBP na eneo ambalo litajengwa bombala Mafuta kijiji cha Chongoleani.
  Akizungumza katika mkutano na ujumbe huo, Meneja wa Bandari Tanga, Hendry Arika, alisema ujumbe huo umejionea kasi kuelekea ujenzi wa bomba la Mafuta na kuwataka wawekezaji wa ndani kuangalia namna ambavyo nao watawekeza.
  Kaimu Meneja Bandari Tanga, Hendry Arika, akiwafahamisha mabalozi wa nchi za Ulaya wanaowakilisha nchi zao nchini wakati walipotembelea Bandari ya Tanga kuangalia fursa za uwekezaji kufuatia ujio wa mradi wa bomba la mafuta Tanga.


  Mabalozi wakitembelea bohari ya mafuta bohari ya GBP.

  Mkurugenzi wa halmashauri ya jiji la Tanga, Daudi Mayeji, akiwaonyesha mabalozi wa nchi 12 za Ulaya wanaoziwakilisha nchini zao nchini ramani ya eneo litakapojengwa bomba la mafuta kijiji cha Chongoleani Tanga ziara waliyoifanya leo.
  Kaimu Meneja wa Bandari ya Tanga, Hendry Arika akizungumza na waandishi wa habari leo eneo litakalojengwa bomba la mafuta kijiji cha Chongoleani Tanga wakati wa ziara ya mabalozi 12 kutoka Jumuiya ya Ulaya wanaowakilisha nchini zai nchini.
  Kiongozi wa mabalozi wa nchi 12 Jumuiya ya Ulaya, Roeland Van Geer, akizunguza na waandishi wa habari wakati wa ziara ya mabalozi hao Tanga kuangalia fursa za uwekezaji kufuatia ujio wa bomba la Mafuta,habari hii kwa hisani ya blog ya kijamii ya tangakumekucha 0655 902929

  0 0

  Mkurugenzi wa Jumuiya ya Wanasheria Wanawake Zanzibar (ZAFELA) Jamila Mahmoud akitoa elimu kwa wanafunzi wa darasa la walemavu wa akili liliopo Skuli ya Jang’ombe juu ya kuelewa viashiria vya udhalilishaji wa kijinsia
  zaf2
  Baadhi ya walemavu wa akili wa Skuli ya Jang’ombe wakionyesha kazi walizofanya wakati wa mafunzo yaliyotolewa na Viongozi wa ZAFELA kuhusu kuelewa viashiria vya udhalilishaji wa kijinsia.
  zaf3

  Mratibu wa ZAFELA Saada Salum Issa akifuatilia kazi walizowapa walemavu wa akili wa Skuli ya Jang’obe wakati walipofika kutoa elimu ya kutambua viashiria vya udhalilishaji wa kijinsia.

  0 0


  0 0


  Afisa Mtendaji wa Kata ya Mburahati Jijini Dar es salaam ametakiwa kusimamia kwa uaminifu mapato ya soko Mburahati ili kuimarisha mapato ya Manispaa hiyo ambayo yataimarisha uboreshaji wa huduma mbalimbali kwa wananchi.

  Agizo hilo limetolewa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo wakati alipofanya ziara sokoni hapo kwa lengo la kujionea hali halisi ya soko pamoja na hali ya ukusanyaji wa mapato.

  Sambamba na agizo hilo pia Mkurugenzi amemtaka Afisa Mtendaji huyo kwa kushirikiana na kamati ya soko Kuandaa orodha ya majina ya walipaji wote pamoja na kiasi wamachotakiwa kulipa, kutolewa namba pamoja na kuwepo na orodha ya kiasi kinachotakiwa kukusanywa kutoka katika maduka hayo, Kutoa mapendekezo mapya ya viwango vya tozo, na kuwepo na jina la kila mmiliki wa meza sokoni hapo na kiasi cha ushuru anacholipa.

  MD Kayombo ametoa siku tano kwa Afisa Mtendaji huyo kwa kumtaka Kuwasilisha orodha ya watu wote wanaodaiwa tozo na kodi katika soko na vibanda pamoja na muda wanaodaiwa sambamba na Kutengeneza data base ya wafanyabiashara wote katika soko hilo.
  Pamoja na ukaguzi huo Mkurugenzi alipata maelezo juu ya ukusanyaji mapato katika soko la Mburahati lililopo pembeni ya jengo la soko linalojengwa. Akisomewa taarifa ya soko hilo na katibu wa soko Ndg Fikiri Pazi alisema kuwa wenye meza hulipa kiasi cha shs 200 kwa siku na wenye vibanda (maduka)hulipa shs21000 kwa mwezi viwango ambavyo wamekuwa wakilipa tangu kuanza kwa soko hilo mwaka 1982.

  Mkurugenzi hakuridhika na viwango hivyo kwa ni ni viwango vilivyopitwa na wakati kutokana na hilo ameagiza tozo hizo ziangaliwe upya na walete mapendekezo ya viwango vipya ambapo menejimenti ya Manispaa itavipitia na kulinganisha na mapendekezo ya viwango vya menejimenti na kisha kufanya maamuzi ya viwango vipya.

  Akiendelea kutoa taarifa alisema mashine ya kukatia risiti imeharibika hiyvyo kusababisha ushuru kutokusanywa tangu 6/10/2016,baada ya kusikia hayo Mkurugenzi ameagiza apate jumla ya kiasi kilichotakiwa kulipwa na kumtaka kufuatilia pesa hizo na ziingizwe kwenye akaunti mpya ya Manispaa ya Ubungo na kuwasilisha slip ya benki ofisi za Manispaa.

  Pamoja na ukaguzi wa soko Mkurugenzi alikagua pia Zahanati ya Mburahati iliyopo katika kata hiyo na kujionea kukamilika kwa ujenzi wa Zahanati hiyo na kutoa maagizo yakufanyika usafi ili Zahanati hiyo ianze kufanya kazi na kuhudumia wananchi.

  Kwa upande wake Diwani wa Kata Mburahati Mhe Yusufu Yenga amemshukuru Mkurugenzi huyo kwa kuwatembelea na kujionea hali halisi na changamoto zilizopo.

  Diwanihuyo alisema kuwa NdgKayombo ni Mkurugenzi wa kwanza kufika hapo kwa ajili ya kujionea hali halisi ya ukusanyaji wa mapato na ziara ya kikazi katika eneo hilo ambapo Ameahidi kumpa ushirikiano na kumuunga mkono katika juhudi zake za kusimamia utekelezaji wa shughuli za maendeleo za Halmashauri yake.

  Mkurugenzi huyo ameahidi kurudi tena katika eneo hilo akiwa na timu ya waandisi wanaosimamia ujenzi wa soko hilo kwa ajili ya ukaguzi zaidi.

  0 0

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongozana na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Profesa Rwekaza Mukandala (kulia kwake) kuelekea kwenye ukumbi wa Nkurumah baada ya kuwasili kwenye Chuo Kikuu cha Dar es salaam kuhutubia kwenye kilele cha Maadhimisho ya Miaka 55 ya Chuo hicho Oktoba 25, 2016. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Ally Happy, kushoto ni Rais wa Jumuiya ya Wahitimu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Jaji Joseph Warioba na wapili kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Tekinoloji, Dkt. Leonard Akwilapo.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa na makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Profesa Rwekaza Mukandala baada ya kwasili kwenye ukumbi wa Nkurumah chuoni hapo kuhutubia kwenye kilelele cha Maadhimisho ya Miaka 55 ya Chuo hicho Oktoba 25, 2016.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia kwenye kilele cha Maadhiisho ya miaka 55 ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam kwenye ukumbi wa Nkurumah jijini Dar es salaam Oktoba 25, 2016.
  Baadhi ya waliohudhuria kwenye kilele cha Maadhimisho ya miaka 55 ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipowahutubia kwenye ukmbi wa Nkuruma jijini Dar es salaam Oktoba 25, 2016.


  0 0

  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Moi akifungua rasmi sherehe za kuadhimisha siku ya mtoto wa kichwa kikubwa na Mgongo wazi Duniani,ambapo alisema wanakazi kubwa ya kutoa matibabu kwa watoto wenye matatizo ya mtindio wa ubongo na mifupa na mpaka sasa watoto takribani 202 wameshafanyiwa upasuaji na zoezi linaendelea Nchi nzima.
  Mwenyekiti wa chama cha wazazi wenye watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi Bw. Hakim ambaye nae mtoto wake anamatatizo kama hayo akielezea  kuwa kuna umuhimu wa kutoa elimu kwa kuwa watu wengi wanahusisha tatizo hilo na imani potofu, aliongeza kuwa watoto waliofanyiwa upasuaji mkoa wa Mbeya ni 18, Morogoro 12, Mwanza 50, na Izazi 14. na wamefanikiwa kuokoa Maisha ya watoto 185 katika mikoa 16 Tanzania.
  Meneja wa Nakiete akitoa neno wakati wa Maadhimisho hayo
  Mmoja wa wazazi akiwa na Mwanae mwenye tatizo la Kichwa kikubwa
  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Moi (Kushoto) akipokea Msaada kutoka Duka la madawa la Nakiete
  Madam Sophia Mbeyela (Kulia) akitoa msaada kwa watoto hao
  Baadhi ya wazazi wakiwa na watoto wao wenye vichwa vikubwa
  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Moi wapili kutoka kushoto akipokea Msaada viti 15 vya kutembelea 'wheel chair' watoto kutoka kwa Mohamed Punjan Foundation
  Baadhi ya wauguzi wakiwa katika maadhimisho hayo
  Baadhi ya wazazi na walezi na wazazi wenye kichwa kikubwa na Mgongo wazi wakiwa katika maadhimisho hayo.
  Picha zote na Fredy Njeje.

  0 0  0 0

   Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo aliyekuwa akisikiliza Changamoto mbalimbali walizonazo baada ya kufanya ziara katika wilaya ya Longido,jijini Arusha.

  Mkurugenzi halmashauri ya Longido bwana Juma Mohamed Muhina ameamuru kukamatwa na kuwekwa chini ya ulinzi wa polisi mtendaji wa kata ya Egirai Lumbwa Wilayani Londigo bwana Paulo Luka kwa tuhuma za ubadhilifu wa fedha za ujenzi wa madarasa ya shule ya sekondari Natroni Flamingo.

  Maamuzi hayo yamefikiwa baada ya wananchi wa kijiji cha Meligoi kata ya Egirai Lumbwa kuikata taarifa iliyosomwa na mtendaji wa kata hiyo iliyoonyesha ujenzi mpaka kukamilika utagharimu kiasi cha milioni 50 lakini michango ya awali ilikuwa milioni 12 na kati ya hiyo milioni 4 tu ndio ilikuwa michango ya wananchi.

  Wananchi hao walimweleza Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo aliyekuwa akisikiliza Changamoto mbalimbali walizonazo baada yakufanya ziara katika kijiji hicho , walisema kuwa wao wanavyojua wamechanga zaidi ya fedha zilizotajwa kwenye taarifa hiyo.

  Hivyo Gambo alimtaka Mkaguzi wa ndani wa Halmashauri kufafanua juu ya matumizi ya fedha hizo, akifafanua Bi. Mwajuma mdaira alisema alifanya ukaguzi na kugundua kuwa fedha zilizokusanywa kwa njia ya michango ilikuwa milioni 95 na milioni 50 kati ya hizo zilitumika kwenye marekebisho ya majengo ya shule japo hakukuwa na mikata yoyote iliyoingiwa kati ya shule na mkandarasi.

  Pia fedha hizo zilitumika bila kutumia stakabadhi za malipo za halmashauri, na kuna wawekezaji 2 ambao ni Winget Windros Safari walichangia mifuko 200 ya simenti na mingine 200 ilitolewa na Kilomberong Hunting kusaidia ujenzi lakini mifuko 144 kati ya hiyo iliuzwa na fedha zake hazikujulika matumizi yake lakini bado anaendelea na ukaguzi zaidi.

  Hivyo kumpelekea Mkuu wa Mkoa Mrisho Gambo kutaka kufahamu hatma ya mtendaji huyo kwa Mkurugenzi wa Halmashauri aliyekili kupata taarifa hiyo jana yake tu na hapo hapo akamuamuru kamanda wa polisi Wilaya kumkamata mtendaji huyo nakumpeleka kituoni kwa maelezo na upelelezi zaidi juu ya ubadhilifu huo.
  Badhi ya wananchi wa kijiji cha Meligoi walioikata taarifa ya mtendaji wa kata yao, wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa Mrisho Gambo(hayupo pichani) katika mkutano wa hadhara, kijiji hapo.

  0 0


  Na Jovina Bujulu-MAELEZO,Dar es Salaam


  WANATASNIA ya habari nchini wametakiwa kuukubali muswada wa sheria wa huduma ya habari unaotarajia kuwasilishwa hivi karibuni Bungeni kwa kuwa umekusudia kuifanya taaluma hiyo kuaminika kwa jamii.

  Hayo yamasemwa na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Hassan Abbas Jijini Dar es salaam wakati wa ziara yake ya kutembelea vyombo vya habari vilivyopo Jijini humo.

  Alisema kwa muda mrefu wadau wa Habari na wanatasnia wenyewe wamekuwa na kiu ya kupata sheria mpya baada ya ile ya mwaka 1976, ambayo imepitwa na wakati.

  “Kutokana na teknolojia kubadilika, ni wakati mwafaka wa kuanzishwa kwa taasisi inayosimamia maadili ya wanahabari, hivyo vyombo vya Habari waliona ni muhimu kuwa na sheria mpya itakayokidhi mabadiliko hayo” alisema Abbas.

  Aidha, alisema kuwa sheria hiyo itahusu vyombo vya habari vya mfumo wa machapisho, ambavyo ni pamoja na magazeti na majarida na si mitandao ya kijamii kama wadau wanatafsiri.

  Aliongeza kuwa miongoni mwa masuala yanayozungumziwa katika muswada huo ni pamoja na kuundwa kwa bodi ya ithibati kwa wanahabari, Baraza huru la habari, Ofisi ya mkurugenzi wa habari, na Mfuko wa mafunzo kwa wanahabari.

  Abbas aliongeza Serikali imewashirikisha wadau muhimu wakati wa mchakato wa kuandaa muswada huo ikiwemo Baraza la Habari Tanzania (MCT), Chama cha wamiliki wa vyombo vya habari (MOAT), Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) na baadhi ya wadau wa haki za binadamu. 

  Aidha alitoa wito kwa wadau wote kutoa maoni yao kwa lengo la kuboresha muswada huo sheria kupitia barua pepe ya ofisi ya Bunge can.bunge.go.tz ili kuyawasilisha mbele ya kamati ya kudumu ya bunge ya huduma za maendeleo ya jamii.

older | 1 | .... | 1020 | 1021 | (Page 1022) | 1023 | 1024 | .... | 1896 | newer