Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1018 | 1019 | (Page 1020) | 1021 | 1022 | .... | 1897 | newer

  0 0


  Mkurugenzi Mtendaji wa jarida maarufu nchini la Bang 'Bang Magazine', Emelda Mwamanga (katikati) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa duka jipya kubwa la mavazi ya maharusi 'Precious Wedding House' lililozinduliwa jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni mmiliki wa duka hilo, Mary Monyo pamoja na Mwendeshaji wa duka la Precious Wedding House, Victoria Chuwa (kulia). Uzinduzi huo uliofanyika Sinza Madukani ulikwenda sambamba na maonesha ya mavazi mbalimbali ya maharusi yaliofanywa na wabunifu wa mitindo maarufu kutoka Tanzania na Nigeria na wanamitindo chipukizi toka Tanzania.
  Mmiliki wa duka jipya kubwa la mavazi ya maharusi 'Precious Wedding House' lililozinduliwa jijini Dar es Salaam jana, Mary Monyo (kulia) akimlisha keki Mkurugenzi Mtendaji wa jarida maarufu nchini la Bang 'Bang Magazine', Emelda Mwamanga (kushoto) wakati wa hafla ya uzinduzi huo uliofanyika Sinza Madukani sambamba na maonesha ya mavazi mbalimbali ya maharusi yaliofanywa na wabunifu wa mitindo maarufu kutoka Tanzania na Nigeria.
  Mkurugenzi Mtendaji wa jarida maarufu nchini la Bang 'Bang Magazine', Emelda Mwamanga (kushoto) akimlisha keki Mmiliki wa duka la mavazi ya maharusi 'Precious Wedding House' lililozinduliwa jijini Dar es Salaam jana, Mary Monyo (kulia) wakati wa hafla ya uzinduzi huo uliofanyika Sinza Madukani sambamba na maonesha ya mavazi mbalimbali ya maharusi yaliofanywa na wabunifu wa mitindo maarufu kutoka Tanzania na Nigeria.
  Mmiliki wa duka la Precious Wedding House, Mary Monyo (kushoto) akimlisha keki Mwendeshaji wa duka hilo, Victoria Chuwa (kulia) mara baada ya uzinduzi wa duka la mavazi ya maharusi 'Precious Wedding House' lililozinduliwa jijini Dar es Salaam.
  Mmiliki wa duka la Precious Wedding House, Mary Monyo (kushoto) akimlisha keki mmoja wa wageni waalikwa mara baada ya uzinduzi wa duka la mavazi ya maharusi 'Precious Wedding House' lililozinduliwa jijini Dar es Salaam.
  Mbunifu maarufu wa mitindo kutoka nchini Nigeria, Femi (wa pili kushoto), pamoja na mbunifu maarufu nchini Tanzania, Strayton Mashulano (wa kwanza kulia) wakiwa katika pozi pamoja na baadhi ya wanamitindo chipukizi kutokea nchini Tanzania, kwenye maonesha ya mavazi mbalimbali ya maharusi yaliofanyika katika duka la mavazi ya maharusi 'Precious Wedding House' lililozinduliwa jijini Dar es Salaam.

  Mmiliki wa duka la Precious Wedding House, Mary Monyo akimkabidhi zawadi ya keki Mtangazaji wa Kipindi cha Mitikisiko ya Pwani kupitia Times FM, Khadija Shaibu 'Dida' kwenye uzinduzi wa duka jipya kubwa la mavazi ya maharusi 'Precious Wedding House' lililozinduliwa jijini Dar es Salaam. Uzinduzi huo ulienda sambamba na siku ya kuzaliwa Khadija Shaibu 'Dida'.
  Mmiliki wa duka la Precious Wedding House, Mary Monyo (kushoto) akimwonesha moja ya magauni ya maharusi Mkurugenzi Mtendaji wa jarida maarufu nchini la Bang 'Bang Magazine', Emelda Mwamanga (kulia) mara baada ya uzinduzi wa duka la mavazi ya maharusi 'Precious Wedding House' lililozinduliwa jijini Dar es Salaam jana. Uzinduzi huo uliofanyika Sinza Madukani ulikwenda sambamba na maonesha ya mavazi mbalimbali ya maharusi yaliofanywa na wabunifu wa mitindo maarufu kutoka Tanzania na Nigeria na wanamitindo chipukizi toka Tanzania.
  Mkurugenzi Mtendaji wa jarida maarufu nchini la Bang 'Bang Magazine', Emelda Mwamanga (kushoto) pamoja na Mtangazaji wa Kipindi cha Mitikisiko ya Pwani kupitia Times FM, Khadija Shaibu 'Dida' wakifungua mvinyo kwenye Uzinduzi huo uliofanyika Sinza Madukani.
  Mmiliki wa duka la Precious Wedding House, Mary Monyo (kulia) akigonganisha glasi ya mvinyo na baadhi ya wageni waalikwa kwenye uzinduzi huo.

  Wabunifu mitindo waonesha mavazi uzinduzi duka la maharusi Na Mwandishi Wetu WABUNIFU wa mitindo maarufu kutoka Tanzania na Nigeria na wanamitindo chipukizi wamejitokeza kufanya maonesha ya mavazi mbalimbali ya maharusi katika uzinduzi wa duka jipya kubwa la mavazi ya maharusi 'Precious Wedding House' lililozinduliwa jijini Dar es Salaa. Uzinduzi huo uliofanyika jana eneo la Sinza Madukani ulipambwa na mbunifu wa mitindo kutoka nchini Nigeria ajulikanaye kwa jina la Femi, mbunifu maarufu nchini Tanzania, Strayton Mashulano pamoja na baadhi ya wanamitindo chipukizi kutokea nchini Tanzania.
   
   Akizungumza katika uzinduzi huo, Mwendeshaji wa duka la Precious Wedding House, Victoria Chuwa ambao ni waandaaji wa onesho alisema waliamua kufanya onesho hilo ili kutoa fursa kwa wananchi hasa wanaoelekea kufanya harusi kujua mitindo mbalimbali ya mavazi ambayo wanaweza wakaitumia katika shughuli zao za harusi na kuonekana tofauti kimuonekano.
   
   Alisema wabunifu walifanya maonesho ya mavazi katika mitindo mbalimbali kutumia mavazi ya hali zote ikiwa ni kuonesha jamii harusi si lazima muhusika au maharusi kutumia gharama kubwa bali wanaweza kutumia gharama za chini na kuonekana wenye mvuto kama watapata ushauri kutoka kwa wabunifu na wanamitindo. 
   
  Alisema duka lao pamoja na kuuza nguo za maharusi watakuwa wakitoa ushauri bure kwa maharusi endapo watafika katika duka hilo ambalo limekuja kuleta mabadiliko katika mitindo ya maharusi. Alisema duka hilo litahudumia watu wenye kipato cha chini, cha kati na hata cha juu kulingana na mahitaji ya wahusika huku wakinufaika kwa ushauri bure kila atakaetembelea na kuomba ushauri kwa wataalamu wa mitindo. 
   
  Alisema duka hilo kubwa la mitindo ya maharusi wa kike na kiume linatumia wataalamu wa mitindo kutoka nchi za Uturuki, Marekani, Italia pamoja na Tanzania. Alisema wamekuja kuondoa dhana iliyojengeka kuwa nguo za maharusi ni anasa kutoka na maduka mengi kuuza bei kubwa kuliko inavyotegemewa, hivyo kupitia kwa wataalam wao maharusi wanaweza kufanya shughuli kwa bei ndogo na kuvutia.
   
   "...Watu wengi wanaona mavazi ya maharusi ni kama anasa kutokana na bei kubwa za mavazi haya, sisi tumeamua kuleta mabadiliko hapa dukani kuna nguo za makundi yote, yaani watu wa kipato cha chini, watu wa kipato cha kati na hata watu wa kipato cha juu...unaweza kuandaliwa nguo yako ya harusi na wanamitindo kutoka nchi tulizotaja wewe ukiwa hapa hapa nchini na ukaipata ndani ya siku 21. 
   
  Akizinduwa duka hilo, Mkurugenzi Mtendaji wa jarida maarufu nchini la Bang, Emelda Mwamanga alimpongeza mwanamama mjasiliamali na mmiliki wa duka hilo, Mary Monyo kwa uamuzi wa kusaidia kutoa ushauri kwa maharusi jambo ambalo limekuwa likipasua vichwa kwa wahusika. Alisema kitendo hicho kinatoa changamoto kwa akinamama wajasiliamali kuweza kufanya mambo makubwa kibiashara.

  0 0

  Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Bunge), Dkt. Hamisi Mwinyimvua akimkabidhi Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mafuta ya MOIL, Sharif Mansoor , hati za ujenzi wa shule ya sekondari ya Nyakato,  kutokana na hiyo na  makumpuni ya mafuta mengine ya OILCOM na GBP waliahidi kuijenga shule hiyo iliyobomoka kutokana na tetemeko la ardh mkoani Kagera, Septemba, 2016, makabidhiano hayo yamefanyika tarehe, 23 Oktoba jijini Dar es salaam.
  h2
  Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Bunge), Dkt. Hamisi Mwinyimvua akimkabidhi Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mafuta ya MOIL, Sharif Mansoor , hati za ujenzi wa shule ya sekondari ya Nyakato iliyobomoka kutokana na tetemeko la ardhi mkoani Kagera Septemba , 2016, kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mkuu GBP Badal Sood, Mkurugenzi MOIL, Altaf Mansoor, kushoto kwake ni Katibu Mkuu wizara ya elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi,Maimuna Tarish, tarehe, 23 Oktoba jijini Dar es salaam.


  Serikali imeyakabidhi makampuni ya mafuta ya OILCOM, GBP na MOIL hati za Ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Nyakato iliyobomoka kutokana na tetemeko la ardhi mkoani Kagera lilitokea mwezi Septemba mwaka huu.

  Akizungumza wakati wa makabidhiano wa hati hizo jijini Dar es Salaam leo Tarehe 23 Oktoba, 2016, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu), Dkt. Hamisi Mwinyimvua ameyashukuru makampuni hayo kwa ahadi ya kujenga shule mbili zilizobomoka kutokana na tetemeko hilo.

  “Shule ya sekondari ya Ihungo na Shule ya Sekondari ya Nyakato zilibomoka  kutokana na tetemeko hilo, Kwa kuwa serikali imeanza kujenga shule ya sekondari ya Ihungo ninawakabidhi nyaraka za ujenzi wa shule ya sekondari ya Nyakato na ninaamini mtakamilisha ujenzi kwa wakati ili wanafunzi waweze kurejea shuleni hapo”amesema Mwinyimvua

  Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mafuta ya MOIL, Sharif Mansoor amesema makampuni yao yataendelea kuziunga mkono juhudi za serikali za kukabili na kurejesha hali pindi maafa yanapotokea nchini.

  “Sisi tunaamini nchi yetu ya Tanzania lazima ijengwe na watanzania wenyewe na sisi hatunabudi kuwasaidia ndugu zetu wa Kagera kwa athari walizozipata za tetemeko kwa kujenga shule hiyo kwa ramani ambayo mmetukabidhi” amesema Mansoor

  Naye, Katibu Mkuu wizara ya elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Bi. Maimuna Tarish amesema kuwa jukumu la wizara hiyo ni kutoa elimu bora na ili elimu iwe bora ni lazima iwepo miundo mbinu ya majengo ya shule ambayo ni bora kama itakayojengwa na makampuni hayo ya mafuta.

  “Tutawakabidhi michoro ya shule hiyo ambayo ujenzi wake umezingatia ushauri wa wataalamu wakiwemo wa Jiolojia, aidha katika ujenzi  mtakao kuwa mnaufanya Wakala wa majengo ya serikali (TBA), itasimsmia kazi ya ujenzi ili kuhakikisha ubora unaotakuiwa unafikiwa” amesema Tarish

  Itakumbukwa kuwa nchi yetu ilikumbwa na tetemeko la ardhi katika Kanda ya Ziwa na Hasa Mkoa wa Kagera , Mwezi Septemba mwaka huu. Tetemeko hilo lilikuwa na athari kubwa kwa miundombinu na majengo ya taasisi mbalimbali za serikali na makazi ya wananchi.

  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  2 MTAA WA MAGOGONI,
  S. L. P 3021,
  11410 DAR ES SALAAM
  JUMAPILI, OKTOBA 23, 2016

  0 0

  Ratiba ya mazishi Jacob Elinaza yatakayo fanyika Oktoba 24,2016 nyumbani kwao Segerea jijini Dar es Salaam.

  1. Mwili wa marehemu utafika saa 11:30 am 
  2. Chakula cha mchana kuanzia 12:00pm 
  3. Kuaga mwili wa marehemu kuanzia saa 2:30pm 
  4. Ibada ya mazishi itaanza kuanzia 4:00pm 
  Kila kitu kitakuwa nyumbani kwetu segerea kwa mama 
  *Maelekezo* ya kufika

  Unashuka kituo  cha Oil com segerea anachukua pikipiki unasema wakupeleke kwa msoji mwanajeshi au kwenye msiba kwa Elinaza 
      
  BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA JINA LAKE LIHIMIDIWE.

  0 0


  Balozi wa Japan, Masaharu Yoshida akiangalia gari jipya aina ya Land Cruiser VXR wakati wa uzinduzi wa jumba la maonyesho ya magari la Kampuni ya Toyota Tanzania jijini Dar es Salaam juzi
  Balozi wa Japan, Masaharu Yoshida (kushoto) akimpongeza Mwenyekiti na Afisa Mtendaji Mkuu wa Toyota Tanzania, Mahmood Karimjee wakati wa uzinduzi wa jumba la maonyesho ya magari la kampuni hiyo jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki.
  Mwenyekiti wa Taasisi ya Karimjee Jivanjee, Hatim Karimjee (kushoto) pamoja na Balozi wa Japan nchini, Masaharu Yoshida (kulia) wakifatilia uzinduzi wa jumba jipya la maonyesho ya magari ya Toyota --- Kampuni ya magari ya Toyota Tanzania Limited imezindua jumba la maonyesho la kisasa kwenye makao makuu yake jijini Dar es salam ikiwa ni jitihada za kuboresha huduma kwa wateja. 

  Akizungumza kwenye uzinduzi huo uliofanyika jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki, Mwenyekiti na Afisa Mtendaji Mkuu wa Toyota Tanzania, Bw. Mahmood Karimjee alisema “Uzinduzi wa jumba hilo la maonyesho unaleta zama mpya katika safari ya Toyota Tanzania, inadhiirisha azma ya Karimjee Group katika kutoa huduma bora kwa wateja. Wateja sasa watafaidika na huduma zilizoboreshwa na bora zaidi kimataifa na tunatarajia watafurahia huduma hii kwa miaka mingi ijayo”. 

  Jumba hilo kubwa la magari ya Toyota yanayotumika zaidi hapa nchini limeboreshwa kwa kuwekewa huduma nyingi za kisasa kama kumbi za mikutano zenye vifaa vya kisasa ili kuendana na viwango vya kimataifa na litatumika kama maonyesho ya magari ya Toyota hususani aina mpya za magari hayo yakiwemo yale yaliyozinduliwa hivi karibuni kama Hilux pick mpya, Fortuner SUV na Landcruiser VXR. 

  Kutokana na uwekezaji huu, Toyota Tanzania imelenga kuwapatia huduma mpya na bora wanunuzi wa magari hayo na watu wengine watakaotembelea jumba hilo kujionea huduma na bidhaa mbalimbali zinazotolewa na kampuni hiyo. “Kununua gari ni maamuzi muhimu na sio jambo unaloweza kulifanya kila siku. Hivyo basi Toyota imeamua kuhakikisha kila mnunuzi wa gari anaweza kufurahia huduma za kisasa,” alisema Karimjee. 

  Kufuatia ufunguzi huo, mwakani kampuni hiyo pia itazindua kituo cha huduma baada ya mauzo kwa lengo la kuhakikisha watumiaji wa magari hayo wanaendelea kupata huduma zitakazofanya magari hayo yadumu katika hali nzuri kwa muda mrefu. Vilevile kampuni hiyo itazindua kituo cha kutoa huduma za kuzuia magari yasiharibike na pia itatoa huduma za kukodisha magari kupitia kampuni yake ya Salute Finance Ltd. 

  Karimjee alisema uzinduzi huu ni historia muhimu katika miaka 191 familia ya Karimjee na miaka 50 ya Toyota hapa nchini kwani jumba la mwisho la maonyesho lilizinduliwa miaka 26 iliyopita. Uzinduzi huo ulihudhuriwa na balozi wa Japan nchini, Masaharu Yoshida, mabalozi mbalimbali, wapenzi wa magari ya Toyota na Meneja Mkuu wa Toyota Motor Corporation, Bw. Yu Asano. Ambaye aliipongeza Toyota Tanzania kwa kupiga hatua hii muhimu.

  0 0

  Pichani ndege aina ya Boeing 747 iliyombeba Mfalme Mohammed VI wa Morocco na ujumbe wake ikiwasili katika uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere,jioni hii jijini Dar na kulakiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli.
  Pichani ndege aina ya Boeing 747 iliyombeba Mfalme Mohammed VI wa Morocco na ujumbe wake ikiwasili katika uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere,jioni hii jijini Dar na kulakiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt John Pombe Magufuli akiwa na Mgeni wake,Mfalme Mohammed VI kutoka taifa la Morocco wakipata Gwaride la heshima,mara baada ya kuwasili Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar jioni hii.Mfalme huyo amewasili jioni ya leo kwa ziara ya kikazi ya siku tatu,aidha imeelezwa kuwa Mfalme huyo aliyekuja na ujumbe wa watu takribani 1000,mara baada ya kumaliza ziara yake ya siku tatu,atakuwa na siku nyingine tano za mapumziko hapa nchini ambapo atatembelea maeneo mbalimbali ya vivutio na utalii nchini Tanzania
  Sehemu ya ujumbe alioongozana nae Mfalme Mohamed VI kutoka Taifa la Morocco,aliyewasili jioni ya leo na kulakiwa na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt John Pombe Magufuli   0 0

   Mfalme wa Morocco Mhe. Mohammed VI (aliyetangulia mbele) akishuka katika Ndege mara alipowasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere 23/10/2016 kwa ajili ya ziara rasmi ya siku tatu Jijini Dar es Salaam.
   Mfalme wa Morocco Mohammed VI  akipokea shada la maua alipowasili  Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere 23/10/2016 kwa ziara rasmi ya siku tatu  Jijini Dar es Salaam.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimlaki Mfalme wa Morocco Mohammed VI mara baada ya  kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere 23/10/2016 kwa ziara rasmi ya ya siku tatu  Jijini Dar es Salaam.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na Mfalme wa Morocco Mohammed VI wakisimama kwa nyimbo za Taifa na mizinga 21 mara baada ya  Mfalme huyo kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere 23/10/2016 kwa ziara ya siku tatu  Jijini Dar es Salaam.
   Mfalme wa Morocco Mohammed VI akikagua gwaride mara baada ya  kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere 23/10/2016 kwa ziara ya siku tatu Jijini Dar es Salaam.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimtambulisha Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan kwa Mfalme wa Morocco Mohammed VI mara baada ya  kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere 23/10/2016 kwa ziara ya siku tatu ya kikazi Jijini Dar es Salaam.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimtambulisha Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa  kwa Mfalme wa Morocco Mohammed VI katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere 23/10/2016 kwa ziara rasmi ya siku tatu  Jijini Dar es Salaam.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimtambulishwa sehemu ya ujumbe wa  Mfalme wa Morocco Mohammed VI mara katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere 23/10/2016 kwa ziara rasmi ya siku tatu  Jijini Dar es Salaam.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli  katika maongezi na Mfalme wa Morocco Mhe. Mohammed VI  katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere 23/10/2016 kwa ajili ya ziara rasmi ya siku tatu Jijini Dar es Salaam.
   Sehemu ya ujumbe wa wafanyabiashara walioongozana na mfalme wao
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Mfalme wa Morocco Mhe. Mohammed VI wakifurahia ngoma mara baada ya Mfalme huyo kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere 23/10/2016 kwa ziara rasmi ya siku tatu Jijini Dar es Salaam.
   Mfalme wa Morocco Mhe. Mohammed VI (wa pili kulia) pamoja na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli wakiangalia kikundi cha ngoma cha Usambara mara baada ya Mfalme huyo kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere 23/10/2016 kwa ziara rasmi ya siku tatu  Jijini Dar es Salaam.
  Mfalme wa Morocco Mhe. Mohammed VI (wa pili kulia) pamoja na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli wakiangalia kikundi cha ngoma cha Usambara mara baada ya Mfalme huyo kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere 23/10/2016 kwa ajili ya ziara rasmi ya siku tatu Jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na Mfalme wa Morocco Mohammed VI wakisimama kwa nyimbo za Taifa na mizinga 21 mara baada ya  Mfalme huyo kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere 23/10/2016 kwa ziara ya siku tatu  Jijini Dar es Salaam.

  0 0
   
  0 0

   Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akiwa pamoja na Viongozi wa Mkoa wa Rukwa wakielekea kutembelea fukwe za ziwa Rukwa zilizoharibiwa vibaya
   Sehemu ya wakazi wa Nankanga wakimsikiliza Waziri wa Nchi Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba (hayupo pichani) wakati wa Waziri akiwahimiza juu ya kutuza rasilimali za Mazingira.
   Mifugo ikichungwa pembezoni mwa Ziwa Rukwa Waziri Makamba amegiza shughuli za aina hiyo kufanyika mita 200 kutoka kwenye chanzo cha maji
  Sehemu ya Viongozi wa dini, siasa na wazee wa Mkoa wa Rukwa wakimsikiliza Waziri wa Nchi Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba (hayupo pichani) alipokutana nao na kusisitiza amani na Hifadhi ya mazingira.
   

  Na Lulu Mussa -Sumbawanga

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. January Makamba ameendelea na ziara ya kikazi katika Mkoa wa Rukwa. Katika ziara yake siku ya leo Waziri Makamba ameshuhudia uharibifu mkubwa wa mazingira hususan pembezoni mwa ziwa Rukwa.

  Waziri Makamba amewaambiwa wakazi wa Kijiji cha Nankanga kwamba mwaka 2000 kina cha maji katika ziwa Rukwa kilikuwa ni mita sita, na kwa mwaka 2016 chanzo hicho kimepungua hadi kufikia mita tatu. "Tafiti zinaonyesha kuwa kupungua kwa kina hicho pamoja na mambo mengine kunasababishwa na kilimo cha milimani na kandokando ya ziwa, na ulishaji wa mifugo katika Vyanzo vya maji" Makamba alibainisha

  Katika ziara yake baada ya kushuhudia uharibifu mkubwa kiasi hicho, Waziri Makamba ameazimia kulitangaza eneo la Ziwa Rukwa kama eneo mahsusi kwa mazingira na kanuni za matumizi ya maeno hayo zitaandaliwa ili kunusuru Ziwa Rukwa.

  Pia, wakurugenzi wote wa Halmashauri za Mkoa wa Rukwa wameagizwa kutenga pesa zitokanazo na tozo mbalimbali ili waweze kugharamia uwekaji wa alama maalum 'beacons' ili kuainisha eneo tengefu na kuagiza kuwa zoezi hili lifanyike haraka.

  Aidha, Mhe. Makamba amesisitiza juu ya upandaji wa miti na ameonyesha masikitiko yake kwa Mkoa wa Rukwa kuwa na upungufu wa miti ya asili na ile ya kupanda kwa kiwango kikubwa. "nimetembea zaidi ya kilomita 200 sijaona miti iliyopandwa" Makamba aliongezea.

  Wakazi wa Mkoa wa Rukwa wamefahamishwa na kusisitizwa kuwa kuanzia mwakani itakuwa lazima kwa wanafunzi wa Primary na Sekondari kuwasili na miti na kutakiwa kuitunza mpaka pale watakapomaliza shule. Waziri Makamba ameahidi kuleta wataalamu na kutoa orodha ya miche inayostawi katika kila kijiiji ili kurahisisha uoteshaji wa miti.

  Katika hatua nyingine, Waziri Makamba amekutana na viongozi mbalimbali za dini na wazee wa Mkoa wa Rukwa na kuwataka kuunda Kamati ya Amani, na kuahidi kugharimia Mkutano wa kwanza wa kuundwa kwa baraza hilo na kusisitiza agenda ya Mazingira iwepo.

  Mkoani Rukwa Waziri Makamba ametembelea mwalo wa ziwa Rukwa na kuzungumza na wananchi wa maeneo hayo na Mkutano wa Hadhara katika Kijiji cha Nankanga ambapo wakazi wa maeneo hayo wamempongeza kwakua toka kijiji hicho kianzishwe mwaka 1974, Waziri Makamba ndio amekuwa mgeni wa kwanza Kitaifa kuwatembele.

  0 0

  Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Said mecky Sadiki akishiriki katika uchimbaji wa msingi kwa ajili ya ujenzi wa madarasa matatu katika shule ya msingi Msamadi ,uchimbaji ulioenda sanjari na uzinduzi rasmi wa kampeni ya kuchangia ujenzi wa vyumba vya madarasa katika wilaya ya Hai. Mkuu wa wilaya ya Hai,Gelasius Byakanwa akishiriki kuchimba msingi kwa ajili ya ujenzi wa madarasa matatu katika shule ya msingi Msamadi iliyopo wilayani Hai. Kaimu Katibu Tawala wa wilaya ya Hai,Juliet Mushi akishiriki kuchimba msingi kwa ajili ya ujenzo wa madarasa matatu katika shule ya msingi Msamadi iliyopo wilayani Hai.

  Baadhi ya wananchi wakishiriki katika uchimbaji wa msingi kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule ya msingi Msamadi.  Msingi kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa katika shule ya msingi Msamadi ukiwa umechimbwa na wananchi wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kuchangia ujenzi wa vyumba vya madarasa kwa shule zilizoko wilaya ya Hai. Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro ,Said Mecky Sadiki akizungumza wakati akizindua rasmi kampeni za kuchangia ujenzi wa vyumba vya madarasa katika wilaya ya Hai.

  Baadhi ya wananchi waliohudhuria uzinduzi wa kampeni ya kuchangia ujenzi wa vyumba vya madarasa. Mkuu wa wilaya ya Hai,Gelasius Byakanwa akizungumza na wananchi juu ya wazo la kuanzishwa kwa kampeni ya kuchangia ujenzi wa vyumba vya madarasa katika wilaya ya Hai.

  Baadhi ya wananchi waliohudhuria mkutano wa uzinduzi wa kampeni ya kuchangia fedha kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa wakinyanyua mikono kuashiria kuunga mkono kampeni hiyo. Diwani wa kata ya Masama Kusini Elingaya Masawe (Chadema) akizungumza wakati wa uzinduzi rasmi wa kampeni ya kuchangia ujenzi wa madarasa katika shule za msingi na sekondari wilayani Hai. Diwani wa kata ya Bomang'ombe ,Joe Nkya (Chadema) akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kuchangisha fedha kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa uliofanyika katika shule ya msingi Msamadi wilayani Hai.Makamu mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Hai na Diwani wa kata ya Machame Magharibi Goodluck Kimaro (Chadema) akizungumza katika uzinduzi huo.

  Mkuu wa wilaya akizungumza namna wanavyoshirikiana na Madiwani wa upinzani katika shughuli za menedeleoo ya wananchi wilayani Hai.kulia kwake ni Diwani wa kata ya Masama Mashariki ,John Munis (Chadema).
  Mkuu wa wilaya ya Hai,Gelasius Byakanwa akitoa maelezo juu ya namna wananchi watakavyo changia katika ujenzi wa madarasa kwa njia ya harambee ili kupunguza changamoto ya vyumba vya madarasa katika wilaya ya Hai.  Baadhi ya wananchhi waliofika katika uzinduzi wa kampeni ya kuchangia ujenzi wa vyumba vya madarasa wakitoa ahadi zao wakati wa harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya ujenzi huo.

  Mkuu wa wilaya ya Hai,Gelasius Byakanwa akiongoza harambee ya kuchangia ujenzi wa madarasa katika shule ya msingi Msamadi iliyopo katika kijiji cha kwa sadala.

  Baadhi ya Wafanyakazi wa Kampuni ya Swissport wakifuatilia matukio mbalimbali yaliyojiri wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kuchangia ujenzi wa vyumba vya madarasa.

  Ujenzi wa vyumba vya madarasa ukiendelea katika shule ya msingi Msamadi iliyopo kijiji cha Kwa Sadala wilayani Hai.  Mafundi ujenzi wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Said Mecky Sadiki pamoja na wafanyakazi wa Kampuni ya Swissport.

  Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Swissport wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro ,Said Mecky Sadiki pamoja na Mkuu wa wilaya ya Hai ,Gelasius Byakanwa mara baada ya kumalizika kwa harambee ya kuchangia ujenzi wa vyumba vya madarasa ambapo Swissport wametoa kiasi cha Sh Mil 15. 

  Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Mbulu,Mkoani Manyara,Hudson Stanlay Kamoga,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo Pichani) kuhusiana na mikakati aliyojiwekea katika utendaji wake wa kazi kwa watumishi wa halmashauri hiyo..Picha na Mary Margwe.
   
   
  Na Mary Margwe, Mbulu

  .Ndoto yake ni kuibadilisha Mbulu kuwa nchi ya vitunguu swaumu.(Mbulu the land of garlic).Asisitiza mambo muhimu matatu ya kuleta mabadiliko ya maendeleo yanayotokana na neno P I A

  P---Patriotism---Uzalendo
  I----Integrity. ----Uadirifu na
  A---Accountabiliyt---Uwajibikaji

  Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Vijijini,Mkoani Manyara , Hudson Stanley Kamoga, amewataka watendaji,madiwani na wananchi kwa ujumla kumpa ushirikiano katika utendaji wake wa kazi ya kuwatumikia wananchi Wilayani humo kwa lengo la kusukuma gurudumu la maendeleo.

  Akiongea na waandishi wa habari Jana ofisini kwake, Kamoga alisema ushirikiano katika nyanja yoyote ile inahitajika ili kufikia malengo,hivyo naye anaomba apewe ushirikiano ili kuweza kufikia malengo aliyojiwekea katika kuhakikisha Mbulu unajua na maendeleo ya kweli na si vinginevyo.

  Kamoga alisema ushirikiano huo uende sambamba na kuwataka wakuu wa idara kumpa mpango kazi wake wa mwezi mmoja kuwa mini amefanya kwenye idara yake, kama idara wamekutana na vikwazo / changamoto gani na ni kwa namna gani wamejipanga kukabiliana na changamoto hizo

  Kamoga alisema yeye kama Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Mbulu, angependa kuona madiwani na watendaji wa halmashauri ya wilaya hiyo wakiwa wanazungumza lugha moja tu ya maendeleo na si vinginevyo.

  "Lazima kama Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Mbulu,nihakikishe watendaji na madiwani wanafanya kazi kama timu moja, kwani siku zote umoja ndio hujenga kitu chochote cha maendeleo na msingi wa maendeleo ni ushirikiano yaani umoja,hivyo uwezo ninao wa kulisimamia hili na hatimaye kuweza kuona tuko wapi, tumetoka wapi na tunatarajia kwenda wapi " alisema Kamoga.

  Aidha alisema ili kufikia malengo aliyojiwekea kikamilifu, ametengeneza utaratibu ambapo angependa watendaji wake wote wa halmashauri waufuate na kuuzingatia kikamilifu katika utekelezaji wa majukumu yao ya Kila siku.

  "Wanahabari kuna hili neno lenye herufi tatu tu lakini lina maana kubwa sana katika utekelezaji wa majikumu yetu ya Kila siku ambapo tukilishika kikamilifu hakuna kitakachokwenda mrama,ambalo linasomeka P I A , P ...limesimama kama neno Patriotism (Uzalendo) , herufi ya pili ni I...limesimama kama Integrity (uadirifu) na la tatu ni A...ambalo limesimama kama Accountability (Uwajibikaji).

  Kamoga alifafanua kua kufuatia maana ya neo PIA, anataka kutengeneza halmashauri yenye watendaji wazalendo, na hao wazalendo lazima wabebe uadirifu kisha tatu Uawajibikaji ,hawa wazalendo ambayo ni waadirifu lazima wawe waajibikaji ,ambapo alisema kukishakua hivyo katika Kila idara zote ambazo watendaji wake wako hivyo, halmashauri hiyo itapiga hatua kubwa mbele kimaendeleo katika kukabiliana na changamoto zilizopo.

  " Kwa hiyo wote tuibebe neno P I A ili tuwe wazalendo, waadirifu na pia tuwe waajibikaji Kila mmoja ahakikishe ana anawajibika kwenye nafasi yake wa uwezo wake wote ,hapo tutasonga hatua mbele kimaendeleo,hii ndio misingi yangu ninayotaka tujijengee na watendaji wangu wa halmashauri

  Je? Ni Mikakati gani ambayo itamwezesha Kamoga kufikia malengo yake?

  Kila mmoja atahakikisha anafanya kazi kwa mazingira yake bila kuingiliana na mwingine,ambapo ana amini madiwani kwa moyo na uchu walionao wa kutaka maendeleo katika jamii hususani ndani ya kata zao.

  Aidha alisema kubwa madiwani watashirikiana kwa umakini kabisa na watendaji walipo kwenye kata hadi ngazi ya vitongoji vyao, ili kuhakikisha wanapunguza migogoro iliyopo vijijini na kwenye kata zao katika kuleta maendeleo ndani ya kata na vijiji, " Lakini pia watendaji wangu wafanye kazi kwa uzalendo, uadirifu na Uwajibikaji wa hali ya juu, hii ndiyo mikakati yangu .

  Pamoja na hayo yote lakini je? Nini Ndoto zake za baadaye kwa Halmashauri ya Wilaya hiyo kama Mkurugenzi??

  "Ndoto yangu kubwa nataka na natamani kuona watu wa ndani na nje ya nchi yaani Tanzani na duniani kote ijue kuwa Mbulu ionekane kama nchi ya vitunguu swaumu ( The land of Garlic) kule Bashay na Mbulu kiujumla tunazalisha vitunguu bora huku wananchi wake bado wanaonekana kutonufaishwa na zao hili" alisema Kamoga.

  Alifafanua kuwa lengo vile vitunguu vibadilike kubadilisha maisha wana Bashay ,wakulima wafurahie uwepo wa uzalishaji mkubwa wa vitunguu swaumu,ambapo alibainisha vitunguu vinavyosafirishwa kwenda nje ni vema viende vikishakua vimewekwa lebo kuonyesha hili ni zao la MBULU ( this is the product of Mbulu / Mbulu product) .

  "Hiki ndicho natamani sana sana ,kwa hiyo mtu anakula kitunguu swaumu akiwa anajua kabisa kuwa anakula kitunguu cha wapi , mtu yoyote akienda sokoni moja kwa moja aulize nataka kitunguu cha Mbulu, huu ndio ufahari wangu,nitasimamia kuhakikisha hili linatekelezeka" alisema Kamoga.

  0 0


  Baada ya Isha kuanza kukamua shabiki huyu alikunwa na hivyo kuvamia jukwaa kwenda kumtunza.
  dar-live4
  Sehemu ya umati uliofurika ukumbini hapo kufuatilia mpambano huo.
  dar-live5
  Leyla akifanya yake baada kupanda jukwaani.
  dar-live1
  Kabla ya mpambano Abubakari Soud ‘Amigo’ wa Jahazi alipanda jukwaani kuwanogesha mashabiki.
  dar-live2
  Mtangazaji wa Redio Times FM, Aisha Mbegu (kulia) akirusha sarafu ili kumpata mwanamuziki wa kuanza kukamua kati ya Leyla na Isha. Kushoto ni mshereheshaji MC wa Jahazi, Mwasity Robert, na katikati ni mwakilishi wa Isha na Leyla.

  dar-live6
  Mtangazaji na MC wa shughuli hiyo, Aisha Mbegu wa Redio Times FM, uzalendo ulimshinda na kuanza kubanjuka.
  dar-live7
  Wanenguaji wa Jahazi wakimsindikiza Leyla.
  dar-live8
  Leyla akiwanogesha mashabiki.
  dar-live9
  Isha Mashauzi aliyevamia tena jukwaa akiwa katika na vazi jingine.
  dar-live10
  Isha na kundi lake wakishambulia jukwaa.
  dar-live11
  Wakati Isha akipagawisha mashabiki, Leyla alikunwa na kumvamia Isha jukwaani na kumtunza hali iliyosababisha mayowe ya kushangilia.
  dar-live12
  Uhasama wao ulikuwa ni jukwaani tu, kwani baada ya kushuka jukwaani wote walikuwa kitu kimoja.

  MASHABIKI wa burudani, hususan muziki wa taarab, usiku wa kuamkia jana walipata burudani ya aina yake wakati wakali wa muziki huo, Isha Mashauzi na kundi lake la Mashauzi Classic kwa upande mmoja na Leyla Rashid kwa upande mwingine akiwa na kundi lake la Jahazi Modern Taarab, walipotoana kijasho kwenye onesho maalum la kutaka kujua nani mkali kati yao.

  Kabla ya mpambano huo kulikuwa na ubishani mkali kwa mashabiki ambapo upande fulani ulisema Isha ndiye mkali kuliko Leyla huku wengine wakisema “aaah, wapi bwana Leyla ndiyo mkali zaidi; pale Isha haingii hata kwa nini”!

  Hatma ya ubishi huo ni mpambano uliowakutanisha wawili hao na kuwaacha mashabiki wakijionea na kuamua wenyewe. Kabla ya wakali hao kupanda jukwaani mshereheshaji wa shughuli hiyo, Aisha Mbegu, wa Redio Times ilibidi arushe sarafu hewani ili kumpata mwanamuziki wa kuanza kulivamia jukwaa maana walianza kutegeana. Baada ya sarafu kurushwa Isha ndiye aliyeangukiwa na zali la kuanza kuonesha mavitu vyake jukwaani.

  (PICHA/HABARI: RICHARD BUKOS /GPL)


  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi wa Italia nchini Mhe. Roberto Mengoni (kushoto) ,Ikulu jijini Dar es Salaam
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Balozi wa Italia nchini Mhe. Roberto Mengoni (kushoto) mara baada ya kumaliza mazungumzo ,Ikulu jijini Dar es Salaam .

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiagana na Balozi wa Italia nchini Mhe. Roberto Mengoni (kushoto) aliyemtembelea na kufanya naye mazungumzo  ,Ikulu jijini Dar es Salaam


                                 .....................................................................
  Balozi wa Italia hapa nchini Tanzania Roberto Mengoni amemhakikishia Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kuwa nchi yake itaendelea kudumisha na kuendeleza mahusiano mazuri na ya kihistoria kati ya nchi hizi mbili katika sekta mbalimbali kama hatua ya kuongeza chachu ya maendeleo kwa wananchi wa mataifa hayo mawili.


  Balozi huyo wa Italia hapa nchini ametoa kauli hiyo leo 24-Okt-2016 alipokutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ikulu jijini Dar es Salaam.Balozi huyo Roberto Mengoni ameeleza kuwa nchi yake itaendelea kushirikiana ipasavyo na Tanzania katika sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya afya,utamaduni na elimu.

  Kwa upande wake, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameishukuru Serikali ya Italia kwa kuendelea kusaidia miradi ya maendeleo ikiwemo ya afya hapa nchini.


  Makamu wa Rais amesema Serikali itaendelea kushirikiana na Italia katika sekta mbalimbali ikiwemo uimarishaji wa biashara na shughuli za utalii kati ya Italia na Tanzania.

  Amesisitiza kuwa Serikali ipo tayari wakati wowote kupokea mawazo mazuri ya kimaendeleo kutoka kwa Serikali ya Italia yatakayosaidia kujenga na kuimarisha ustawi mzuri katika jamii hapa nchini.

  0 0

   
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitoa heshima za mwisho kwa Msaidizi wa Mtendaji Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Marehemu Margareth Lwekama katika ibada ya kumuombea marehemu iyoyofanyia kwenye Kanisa la Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam Oktoba 24, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

  0 0


  Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Chama Cha kikomunisti cha China (CPC) Ndugu Liu Yunshan, mjini Chongqing, nchini China hivi karibuni. Katika Mazungumzo hayo, Ndugu Kinana aliwawakilisha Makatibu Wakuu kutoka vyama vya Ukombozi Kusini mwa Afrika, ambao alifuatana nao nchini China.
  Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu Abdulrahman Kinana (Watatu kushoto) akiwa katika kikao na Makatibu Wakuu wa Vyama vya Ukombozi Kusini mwa Afrika, na Waziri wa Mambo ya Nje wa Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC), Song Tao (wanne kushoto), baada ya kuwawakilisha Makatibu Wakuu hao katika mazungumzo na Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya CPC, Liu Yunshan. Kutoka kushoto ni Pedro Sebastiao wa MPLA (Angola, Elisau Joaquim wa FRELIMO (Msumbiji), Waziri wa Mambo ya Nje katika Chama cha Kikomunisti cha China, Song Tao, Gwede Manlashe wa ANC (Afrika Kusini), Nangolo Mbumba wa SWAPO (Namibia), Ignatius Chembo wa ZANU-PF (Zimbabwe).
  Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu Abdulrahman Kinana (Watatu kushoto) akishikana mikono kuonyesha mshikamano na Makatibu Wakuu wa Vyama vya Ukombozi Kusini mwa Afrika, na Waziri wa Mambo ya Nje wa Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC), Song Tao (wanne kushoto), baada ya kuwawakilisha Makatibu Wakuu hao katika mazungumzo na Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya CPC, Liu Yunshan. Kutoka kushoto ni Pedro Sebastiao wa MPLA (Angola, Elisau Joaquim wa FRELIMO (Msumbiji), Waziri wa Mambo ya Nje katika Chama cha Kikomunisti cha China, Song Tao, Gwede Manlashe wa ANC (Afrika Kusini), Nangolo Mbumba wa SWAPO (Namibia), Ignatius Chembo wa ZANU-PF (Zimbabwe). PICHA ZOTE NA OFISIYA KATIBU MKUU WA CCM

  0 0


  Jovita Mchuruza akiongea na waandishi wa habari(hawapo pichani)baada ya kutelekezewa watoto watano na mkewe wenye vichwa vikubwa,wanaondelea na matibabu katika hospitali ya mkoa wa Kagera.

  Timu ya madaktari kutoka Taasisi ya mifupa(MOI)pamoja na wafadhili wao GSM Foundition wakiwa kwenye ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera wakimpa taarifa juu ya upasuaji wa vichwa vikubwa na mgongo wazi jwa watoto walioufanya katika Mkoa huo kwa muda wa siku tatu.Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Salum Kijuu akimpa pole mmoja wa watoto wenye maradhi ya kichwa kikubwa aliyelazwa katika hospital ya Mkoa wa Kagera baada ya kufanyiwa upasuaji na madaktari toka MOI kwa ufadhili wa Taasisi ya GSM Foundation
  Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Salum Kijuu akimpa pole mmoja wa watoto wenye maradhi ya kichwa kikubwa aliyelazwa katika hospital ya Mkoa wa Kagera baada ya kufanyiwa upasuaji na madaktari toka MOI kwa ufadhili wa Taasisi ya GSM Foundation


  Na Editha Karlo,wa blog ya jamii,Kagera.

  MARADHI ya vichwa vikubwa na migongo wazi kwa watoto yanatibika endapo wazazi watachukua tahadhali mapema ya kumpeleka mtoto hospitali kwaajili ya matibabu.

  Dk Hamis Shaabani daktari bingwa wa upasuaji wa mishipa ya fahamu kutoka Taasisi ya mifupa(MOI) ameyasema hayo leo wakati wa zoezi la ufungaji upasuaji wa vichwa vikubwa na migongo wazi katika hospital ya Mkoa wa Kagera.Dk Hamis alisema kuwa utafiti uliofanywa na Taasisi ya MOI mwaka 2002 unaonyesha zaidi ya watoto 4800 huzaliwa kila mwaka wakiwa na maradhi ya vichwa vikubwa na migongo wazi na kati yao 500 pekee ndiyo wanaoweza kufika hospital na kupatiwa matibabu.

  Akizungumzia chimbuko la maradhi hayo Dk Hamisi alisema kuwa watoto wenye vichwa vikubwa na migongo wazi wanaweza kuzaliwa nacho au kupata siku chache baada ya kuzaliwa."Kwa wale wanao zaliwa na maradhi hayo ni kwasababu ya upungufu wa virutubisho ambavyo mama mjamzito anatakiwa avipate kabla ya kushika mimba virutubisho hivo vinapatikana kwenye matunda,mboga za majani,mayai na vyakula vyote vyenye protini,pia maradhi ya mgongo wazi husababisha watoto kupooza na kushindwa kutumia miguu yao,"alisema

  Alisema mpaka sasa kwa Mkoa wa Kagera wameshawafanyia upasuaji jumla ya watoto saba wenye vichwa vikubwa na mmoja wa mgongo wazi.Ofisa habari wa GSM Foundation Khalfani Kiwamba alisema kuwa taasisi yao iliamua kudhamini matibabu ya maradhi ya vichwa vikubwa na migongo wazi baada ya kuelezwa changamoto mbalimbali za matibabu ya maradhi hayo na uongozi wa Taasisi ya MOI.

  Joviti Mchuruza akiongea kwa niaba ya wazazi ambao watoto wao wamefanyiwa upasuaji aliwashukuru timu nzima ya madaktari hao pamoja na Taasisi ya GSM kwa msaada huo wa matibabu waliowapatia wa watoto wao bure.Aliiomba jamii kuacha kuhusisha maradhi hayo na mila potofu za imani za kishirikina au mikosi kwenye familia hali inayofanya akina mama au baba kutelekezewa watoto.

  Aliwaomba pia wataalam hao wasogeze huduma hiyo karibu na jamii hasa maeneo ya vijijini ambapo wapo watoto wengi wenye maradhi hayo wanateseka na hawana msaada."Nawaomba wazazi wenzangu hasa akinamama sababu sisi ndiyo tunakaa na watoto kwa muda mrefu ndiyo tunaoweza kugundua mabadiliko ya mtoto pia tusisikilize maneno ya dhihaka ya watu wa pembeni maradha haya yanatibika kabisa"alisema mzazi huyo

  Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali mstaafu Salum Kijuu aliwashukuru madaktari pamoja na shirika la GSM Foundation kwa udhamini huo wa matibabu bure kwa watoto wenye vichwa vikubwa na migongo wazi.Pia aliwataka wazazi wenye watoto wenye maradhi hayo wasione aibu kuwapeleka hospitali ili waweze kupatiwa matibabu bure.

  0 0

  Mkurugenzi wa Habari, Hassani Abbas (kulia) akizungumza jambo na Mwandishi Mwadamizi wa Gazeti la Jambo Leo, Mashaka Mgeta (kushoto) wakati wa ziara ya kutembelea ofisi za gazeti hilo pamoja na kubadilisha uzoefu wa kazi leo Jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mhariri Mtendaji Anicetus Mwesa.
  Mkurugenzi wa Habari, Hassani Abbas (kushoto), akizungumza na Wahariri Waandamizi wa Gazeti la Jambo Leo, Anicetus Mwesa (katikati), Exuper Kachenje na Kizito Noya wakati wa ziara ya kutembelea ofisi za gazeti hilo pamoja na kubadilisha uzoefu wa kazi leo Jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi wa Habari, Hassani Abbas (kushoto), akizungumza na Wahariri Waandamizi wa Gazeti la Jambo Leo, Joseph Lugendo (kushoto), na Joseph Kulngwa wakati wa ziara ya kutembelea ofisi za gazeti pamoja na kubadilisha uzoefu wa kazi leo Jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi wa Habari, Hassan Abbas (katikati) akizungumza na Bodi ya Uhariri ya gazeti la Jambo Leo wakati wa ziara wakati wa ziara ya kutembelea ofisi za gazeti hilo pamoja na kubadilisha uzoefu wa kazi leo Jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi wa Habari, Hassani Abbas (kulia) akipokelewa na Kaimu Mhariri Mkuu wa gazeti la Majira, Eckland Mwaffisi wakati wa ziara ya kutembelea ofisi za gazeti hilo pamoja na kubadilisha uzoefu wa kazi leo Jijini Dar es Salaam.
  Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Majira, Imma Mbughuni akimkaribisha Mkurugenzi wa Habari, Hassan Abbas wakati wa ziara ya kutembelea ofisi za gazeti hilo pamoja na kubadilisha uzoefu wa kazi leo Jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi wa Habari, Hassan Abbas akizungumza na watendaji wakuu wa gazeti la Majira, akiwemo Mhariri Mtendaji, Imma Mbunghuni wakati wa ziara ya kutembelea ofisi za gazeti hilo pamoja na kubadilisha uzoefu wa kazi leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Afisa Habari Mwandamizi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Jonas Kamaleki.
  Mkurugenzi wa Habari, Hassan Abbas (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na watendaji wakuu wa gazeti la Majira, Imma Mbughuni (kulia) na Kaimu Meneja Mkuu wa kampuni ya Bussines Times Ltd Sophia Mshangama (kushoto).

  …………………………..

  Na Beatrice Lyimo

  SERIKALI imevitaka wadau wa vyombo vya habari nchini kuacha kulalamika na badala yake waendelee kutoa maoni yao kuhusu muswada wa sheria kwa vyombo vya habari ambao unatarajiwa kuwasilishwaa katika Bunge lijalo mjini Dodoma.

  Akizungumza katika wakati tofauti wakati wa ziara yake ya kutembelea Taasisi za Vyombo vya habari nchini, Mkurugenzi wa Idara ya Habari(MAELEZO), Hassan Abbas alisema lengo la Serikali ni kuhakikisha kuwa muswada huo unapitishwa na Bunge ili uweze kuwa sheria kamili na hatimaye kuifanya tansia ya habari kuzidi kuheshimika.

  Mkurugenzi Abbas alisema tangu muswada huo uliposomwa kwa mara ya kwanza Bungeni, mwezi Septemba mwaka huu, wadau wa tasnia ya habari nchini ikiwemo Wahariri na waandishi wa habari wamekuwa mstari wa mbele kupingana katika mitandao ya kijamii badala ya kutoa maoni yao katika mamlaka zinazohusika.

  “Ni aibu kwa maoni ya muswada huu yanayohusu tasnia ya habari kutolewa na watu ambao hawana taaluma ya habari, hivyo tukiwa kama wanataaluma ni vyema tujitokeze kwa wingi kutoa maoni kifungu kwa kifungu ili kuweza kuboresha muswada” alisema Mkurugenzi Abbas.

  Aliongeza kuwa haitopendeza kwa muswada huo kuendelea kutolewa maoni na wananchi wengine na wadau wa muswada kukacha kutoa maoni yao, na hivyo kusababisha muswada huo kuandikwa na watu walio nje ya tasnia ya habari.

  Abbas alisema, muswada huo utakusudia kuiongezea nguvu tasnia ya habari kwa kuweka ikiwemo suala zima la kuzingatia sheria na mipaka ya nchi katika utoaji wa habari na taarifa maalum za Serikali kwa umma kwa kuzingatia ukomo wa kimataifa.

  “Azimio la Umoja wa Mataifa la mwaka 1948, pamoja na kuzungumzia kuhusu haki ya kupata taarifa lakini pia limeanisha sheria mbalimbali ambazo hazina budi kuheshimiwa, na sheria hizo ni pamoja na sheria za ulinzi na usalama” alifafanua Mkurugenzi Abbas.

  Akifafanua zaidi alisema taaluma ya habari ni tasnia muhimu katika maendeleo ya taifa ila kwa upande mwingine inaweza kuharibu maendeleo kwa njia moja au nyingine na hivyo kuwataka wadau wa habari kujitokeza kutoa maoni kwa kujenga hoja za msingi ili kuboresha muswada badala ya kulalamika.

  Aidha kwa upande mwingine, Abbas alisema Ofisi yake ni mlezi na mratibu wa vyombo vya habari na hawana budi kuwasiliana naye pindi wanapopata changamoto mbalimbali ikiwemo utoaji na upatikanaji wa taarifa za Serikali katika Wizara, Taasisi, Idara, Mikoa na halmashauri nchini.

  Pia alisema zipo taarifa ambazo zinahitaji kufanyiwa uhakiki ikiwemo ufundi na takwimu, na hivyo aliwataka waandishi wa habari kuwa wavumilivu pale wanapohitaji taarifa hizo kutoka kwa maafisa habari wa Wizara au Taasisi husika.

  Kwa upande wake, Mhariri Mtendaji wa gazeti la Majira, Imma Mbughuni alisema chombo hicho kimejipanga kutoa maoni yao kuhusu muswada huo na mara baada ya kumaliza wanatarajia kuwasilisha katika kamati ya kudumu ya Bunge.

  Naye Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Jambo Leo, Anicetus Mwesa alisema chombo chao pia kimekusudia kuupitia muswada huo ili kutoa maoni yao na baadae kuyawasilisha katika kamati husika..

  0 0

  Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Gerson Lwenge akipokea maelezo ya ramani ya mradi wa uchimbaji visima vya Kimbiji na Mpera kutoka kwa Mhandisi Mkazi wa mradi, Injinia Charles Kaaya.
  Mashine ikiendelea na kazi ya uchimbaji kisima Kimbiji.
  Baadhi ya mafundi wakiwa eneo la kazi Kimbiji.
  Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Gerson Lwenge akiwa pamoja na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Serengeti, Mehrdad Talebi (kushoto), Mhandisi Mkazi wa mradi, Charles Kaaya, Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA), Archad Mutalemwa na Mkurugenzi wa Maji Mijini, Mhandisi Dkt. Justus Rwetabula.
  Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Gerson Lwenge akionja maji yaliyopatikana katika kisima namba K17.
  Mhandisi Mkazi wa Mradi wa uchimbaji visima vya Kimbiji na Mpera, Charles Kaaya (kushoto) akizungumza na Mwenyekiti wa Kamati ya Miradi na Ufundi ya Bodi ya DAWASA, Prof. Felix Mtalo (katikati) na Waziri Maji na Umwagiliaji, Inj. Gerson Lwenge.

  WAZIRI wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Gerson Lwenge, ameiagiza Kampuni ya Serengeti Limited kukamilisha mradi wa uchimbaji visima 20 vya maji vya Kimbiji na Mpera kwa muda waliokubaliana, vinginevyo itabidi ilipe gharama za ucheleweshaji kama itashindwa.

  Alisema serikali haitavumilia kuona mradi huo wenye manufaa makubwa kwa Jiji la Dar es Salaam unachelewa kukamilika, kwa sababu unahitajika kuhudumia wananchi kwa kuwapatia huduma ya majisafi na salama.

  Waziri Lwenge alitoa agizo hilo mwishoni mwa wiki, baada ya kufanya ziara ya kukagua utekelezaji wa mradi huo mkubwa uliopo Kigamboni, Dar es Salaam ulioanza kutekelezwa tangu mwezi Machi, 2013.

  Alisema mradi huo utagaharimu zaidi ya Sh. bilioni 18, na serikali imeshalipa kwa mkandarasi zaidi ya Sh. bilioni 13, na ulitegemewa kukamilika ifikapo Desemba mwaka huu, lakini utachelewa kutokana na changamoto mbalimbali alizotaja mkandarasi huyo.

  “Pamoja na changamoto alizozitaja mkandarasi, hatutakubali utekelezaji wa mradi huu uendelee kuchelewa, mkandarasi inabidi aongeze kasi ili tumalize kero ya wananchi wa Kigamboni, Mkuranga na Dar es Salaam yote, ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakisubiri mradi huu, hatutavumilia uchelewaji zaidi na itabidi walipie gharama endapo watashindwa”, alisema Inj. Lwenge.

  Alisema mradi umetekelezwa kwa asilimia 56 hadi sasa, visima nane vikiwa vimekamilika, huku vingine saba vikiwa katika hatua mbalimbali za uchimbaji na vitano vikiwa havijaanzwa kazi ya uchimbaji.

  Wakati huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Serengeti Limited, Mehrdad Talebi alikiri kuchelewa kukamilika kwa mradi huo kama mkataba unavyosema, kutokana na changamoto mbalimbali, ikiwemo ukosefu wa vifaa vya kazi na kuahidi ifikapo Machi, 2017 watakuwa wamekamilisha kazi hiyo.

  Aidha, Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA), Archad Mutalemwa, alisema mradi huo hautakamilika kulingana na makubaliano ya awali, lakini ana imani na kukamilika kwa kazi hiyo mara baada ya kutatua changamoto za mkandarasi, ikiwemo kupatikana kwa vifaa vya kazi.

  Uchunguzi wa awali ulionyesha uwepo wa maji mengi na safi katika maeneo ya Kimbiji na Mpera. Hivyo, ikaamuliwa visima kati ya 20-40 vichimbwa kwenye maeneo hayo na vinategemwa kuchangia hadi asilimia 30 ya mahitaji ya maji ya Dar es Salaam, mji unaotarajiwa kuwa na watu wapatao milioni 7.59 ifikapo mwaka 2032.

  Ili kukabiliana na tatizo la maji kati ya sasa na hadi mwaka 2032, visima 12 vitachimbwa maeneo la Kimbiji na 8 maeneo ya Mpera. Visima hivi vitakuwa na kina cha hadi mita 600 na vinategemewa kuzalisha lita za ujazo 260,000 kwa siku.

  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Kilimo,Maliasili,Mifugo na Uvuvi wakati wa  kikao cha Mpango kazi wa mwaka 2016-2017   katika  utekelezaji wa  robo mwaka ya kwanza ya Julai-Septemba 2016 kilichofanyika leo  Ikulu Mjini Unguja.
  2
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisisitiza jambo alipokuwa akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Kilimo,Maliasili,Mifugo na Uvuvi wakati wa  kikao cha Mpango kazi wa mwaka 2016-2017   katika  utekelezaji wa  robo mwaka ya kwanza ya Julai-Septemba 2016 kilichofanyika leo  Ikulu Mjini Unguja
  3
  Waziri wa Wizara wa Kilimo,Maliasili,Mifugo na Uvuvi Mhe,Hamad Rashid  Mohamed (katikati) akisoma taarifa ya  utekelezaji wa Mpango kazi wa mwaka 2016-2017 katika  kikao  cha robo mwaka ya kwanza ya  Julai-Septemba 2016 kilichofanyika leo   Ikulu Mjini Unguja,chini ya mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) (kulia) Katibu Mkuu Kiongozi Dkt.Abdulhamid Yahya Mzee na Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhe.Lulu Msham Abdalla.
  4
  Viongozi wa Idara mbali mbali katika Wizara ya Kilimo,Maliasili,Mifugo na Uvuvi wakiwa katika  mkutano wa  siku moja unaozungumzia  Mpango kazi wa mwaka 2016-2017   katika  utekelezaji wa  robo mwaka ya kwanza ya  Julai-Septemba 2016 uliofanyika leo Ikulu Mjini Unguja,chini ya mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani)
  5
  Baadhi ya Wakurugenzi katika Idara mbali mbali za Wizara ya Kilimo,Maliasili,Mifugo na Uvuvi wakiwa katika  mkutano wa  siku moja unaozungumzia  Mpango kazi wa mwaka 2016-2017   katika  utekelezaji wa  robo mwaka ya kwanza ya  Julai-Septemba 2016 uliofanyika leo Ikulu Mjini Unguja,chini ya mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani.
  6
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Kilimo,Maliasili,Mifugo na Uvuvi wakati wa  kikao cha Mpango kazi wa mwaka 2016-2017   katika  utekelezaji wa  robo mwaka ya kwanza ya Julai-Septemba 2016 kilichofanyika leo  Ikulu Mjini Unguja (kushoto) Waziri wa Kilimo,Maliasili,Mifugo na Uvuvi Mhe,Hamad Rashid  Mohamed,akifuatiwa na Katibu Mkuu Kiongozi Dkt.Abduhamid Yahaya Mzee,
  7
  Baadhi ya Wakurugenzi katika Idara mbali mbali katika Wizara ya Kilimo,Maliasili,Mifugo na Uvuvi wakiwa katika  mkutano wa  siku moja unaozungumzia  Mpango kazi wa mwaka 2016-2017   katika  utekelezaji wa  robo mwaka ya kwanza ya  Julai-Septemba 2016 uliofanyika leo Ikulu Mjini Unguja,chini ya mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani),
  8
  Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo,Maliasili,Mifugu na Uvuvi Nd,Juma Ali Juma akitoa ufafanuzi  wa vifungu  wakati  wa kikao cha utekelezaji wa Mpango kazi wa   mwaka 2016-2017 katika  Wizara ya Kilimo,Maliasili,Mifugu na Uvuvi katika  robo mwaka ya kwanza ya  Julai-Septemba 2016, kilichofanyika leo  Ikulu Mjini Unguja,chini ya mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe,Balozi Seif Ali Iddi,(kushoto).

  [Picha na Ikulu.] 24/10 /2016.

  0 0

  01
  02
  Mkuu wa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika (EASTC) Prof. Innocent Ngalinda akizungumza na washiriki wa mafunzo na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa mafunzo maalumu ya Ukusanyaji Takwimu Rasmi uliofanyika leo katika chuo hicho kilichopo Changanyikeni jijini Dar es salaam.
  03
  Naibu Mkuu wa Chuo, Taaluma, Utafiti na Ushauri wa Kitaalamu wa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika (EASTC) Dkt. Frank Mkumbo akizungumza na washiriki wa mafunzo na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa mafunzo maalumu ya Ukusanyaji Takwimu Rasmi uliofanyika leo katika chuo hicho kilichopo Changanyikeni jijini Dar es salaam.
  04
  Baadhi ya washiriki wa mafunzo maalumu ya Ukusanyaji Takwimu Rasmi wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika (EASTC) Prof. Innocent Ngalinda wakati wa uzinduzi wa mafunzo hayo uliofanyika leo katika chuo hicho kilichopo Changanyikeni jijini Dar es salaam.
  Na: Albert Fen Dar es Salaam

  Mkuu wa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika (EASTC) Prof. Innocent Ngalinda amezindua mafunzo maalumu ya Ukusanyaji Takwimu Rasmi ambayo yalianza tarehe 17 Oktoba mwaka huu chuoni Changanyikeni jijini Dar es Salaam.

  Akizungumza leo wakati wa uzinduzi wa mafunzo hayo, Prof. Ngalinda amesema   mafunzo hayo yameandaliwa kwa nia ya kumpatia mshiriki ujuzi katika ukusanyaji takwimu kwa ajili ya kuzichakata na kuwa takwimu rasmi.

  “Washiriki hawa watafundishwa mbinu shirikishi, utatuzi wa matatizo mbalimbali wakati wa ukusanyaji takwimu, sensa na viwango vya tafiti mbalimbali, utunzaji wa Vifaa vya ukusanyaji takwimu kama vile simu za mkononi  na kumpyuta mpakato pamoja na kubadilisha madodoso ya kawaida na kuwa ya kisasa”, amesema Prof. Ngalinda.

  Akizungumzia malengo ya mafunzo hayo Naibu Mkuu wa Chuo, Taaluma, Utafiti na Ushauri wa Kitaalamu wa chuoni hapo Dkt. Frank Mkumbo amesema lengo ni kuwawezesha wakusanyaji takwimu kukusanya takwimu halisi na zenye ubora kwa ajili ya kupanga mipango mbalimbali ya Maendeleo.

  “Lengo kuu la mafunzo haya ni kuhakikisha kuwa wakusanyaji takwimu rasmi wanakuwa na weledi wa kutosha katika kukusanya takwimu bora na zenye tija kwa taifa” amefafanua Dkt. Mkumbo.

  Jumla ya washiriki 110 wamejiunga na mafunzo hayo maalumu ya muda wa miezi miwili kwa awamu ya kwanza ambayo yatamalizika mwezi Disemba, 2016 na watakaomaliza na kufaulu watapatiwa cheti cha Ukusanyaji Takwimu. Awamu ya pili ya mafunzo hayo yanatarajiwa kuanza Novemba mwaka huu na kumalizika Januari, 2017.

  0 0


older | 1 | .... | 1018 | 1019 | (Page 1020) | 1021 | 1022 | .... | 1897 | newer