Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1017 | 1018 | (Page 1019) | 1020 | 1021 | .... | 1897 | newer

  0 0     Prof. Ninatubu Mbora Lema

  Ikulu, Dar es Salaam.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amemteua Prof. Ninatubu Mbora Lema kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA).

  Taarifa iliyotolewa leo tarehe 22 Oktoba, 2016 na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi huu umeanza tarehe 20 Oktoba, 2016.

  Prof. Ninatubu Mbora Lema anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Mhandisi Lambert Ndiwaita aliyefariki dunia tarehe 20 Agosti, 2015.

  Prof. Ninatubu Mbora Lema ni Profesa Mshiriki Usimamizi wa Ujenzi, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Associate Professor of Construction Management - University of Dar es Salaam).


  Gerson Msigwa
  Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
  Dar es Salaam
  22 Oktoba, 2016

  0 0

  Na Ally Daud- MAELEZO

  SERIKALI kupitia mpango wa Taifa Wa kudhibiti Magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele itaanza kugawa kingatiba za ugonjwa Wa matende, mabusha na Minyoo Oktoba 25 mwaka huu ili kuondoa kabisa magonjwa hayo mpaka ifikapo 2020.

  Akizungumza hayo katika semina na waandishi Wa habari kuhusu magonjwa hayo Afisa Mpango wa huduma hiyo Bw. Oscar Kaitaba  amesema kuwa zoezi hilo litaanza Oktoba 25 hadi Oktoba 30 mwaka huu katika maeneo yote ya Dar es salaam.

  "Zoezi la kugawa kingatiba kwa wananchi Wa Dar es salaam litaanza Oktoba 25 na kumalizika Oktoba 30 ili kuweza kupambana na vimelea vya magonjwa hayo na kuendelea na mikoa mingine" alisema Kaitaba.
  Aidha Bw.Kaitaba amesema kuwa kingatiba ambazo zitatolewa ni Ivermectin na Albendazole ili kuondoa magonjwa ya Matende,Mabusha, na Minyoo kwa wakazi wa Dar es salaam na vitongoji vyake.

  Bw.Kaitaba amesema kuwa kingatiba hizo zitatolewa kwa wananchi wote wenye umri kuanzia miaka mitano na kuendelea katika maeneo yote ya Dar es salaam katika stendi za mabasi, Masoko,Hospitalini, Ofisi za Serikali za Mitaa, Ofisi za Wizara, Kambi za majeshi ns Magereza.

  Aidha Bw.Kaitaba ameongeza kuwa wananchi wanatakiwa wajitokeze kwa wingi kupata kingatiba hizo wakiwa wameshakula vizuri chakula na kuondokewa na imani potofu kwamba zinachangia kuzuia mimba ama kwa wanaume kupungukiwa nguvu za kiume.

  Kwa upande wake Muhamasishaji Wa Mpango huo kutoka Wizara ya Afya Bw. Makora Said amesema kuwa Semina hiyo inahusu kuwahamasisha waandishi wa habari kutoa elimu kwa wananchi kuhusu Mpango Wa Taifa wa Kudhibiti Magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele nchini kama vile Matende, Mabusha, Minyoo, Usubi, Trakoma na Kichocho.

  Aidha Bw. Makora amesema kuwa kama waandishi watakavyoielimisha jamii kwa elimu ya kutosha na wananchi wakakubali wito Wa kutumia kinga tiba hizo Serikali itafanikiwa kuepusha ulemavu na udumavu kwa watanzania.

  Aidha Bw. Makora amesema kuwa waandishi wanatakiwa wawe kipaumbele katika kuandika habari za afya ya Binadamu ili kuwapa ufahamu  wananchi na uwezo Wa wa kufanya maamuzi sahihi juu ya afya zao kwa ujumla.                  
        
  Semina hiyo ya siku moja imelenga kuwaelimisha waandishi Wa habari kuhusiana na Mpango Wa Kudhibiti magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele ili elimu ya kutosha ikatolewe kwa wananchi ili kufanikisha lengo la Sera ya Afya ya mwaka 2007 hadi kufikia 2020.

  0 0

  Katibu Mkuu wa Baraza la Waislamu (BAKWATA) Selemani Lolila akizungumza na waandishi wa (habari hawapo pichani) juu ya Tanzania ijiandae kunufaika kibiashara na kukuza uchumi wa Taifa na mtanzania mmoja mmoja ifikapo mwakani leo jijini Dar es Salaam.kulia ni Mkurugenzi Msaidi JAKIM kutoka nchini Malaysia Mohd Amri Bin Abdullah.
  Mkurugenzi Msaidi wa kampuni ya JAKIM kutoka nchini Malaysia,Mohd Amri Bin Abdullah akizungumza na waandi wa habari (hawapo pichani) juu kuzingatia viwango maalum vilivyowekwa na kampuni ya JAKIM nembo ya halali leo jijini Dar es Salaam.kulia ni Katibu Mkuu wa Baraza la Waislamu (BAKWATA) Selemani Lolila Mkurugenzi wa Halal Tanzania Certification (HTC),Muhsin Hussein akifafanua jamb leo jijini Dar es Salaam. kulia ni Katibu Mkuu wa Baraza la Waislamu (BAKWATA) Selemani Lolila.


  Katibu Mkuu wa Baraza la Waislamu (BAKWATA) Selemani Lolila amesema Tanzania ijiandae kunufaika kibiashara na kukuza uchumi wa Taifa na mtanzania mmoja mmoja ifikapo mwakani kwa sababu wapo mbioni kuingia kwenye orodha ya nchi ambazo biadhaa zake za chakula zitawekewa nembo ya Halal ambapo bidhaa hizo zitauzwa kwa nchi 33 kimataifa ikiwemo Malaysia inayotoa nembo ya JAKIM.

  Halal ni nembo ambayo inawekwa katika bidhaa inapoazalishwa hadi kumfikia mlaji kwa kuzingatia viwango maalum vilivyowekwa na kampuni ya JAKIM nembo ya halali.

  Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam Lolila amesema nembo ya Halal itaweza kumhakikishia mlaji muislamu na wasiokuwa waislamu uhakika wa chakula tokea kilipoanzishwa hadi kuuzwa kuwa kimepitia njia inayotakiwa kwa misingi ya dini ya kiislamu.

  "Katika kitabu cha Qur an kinatueleza kuwa tuchinje na tule vyakula vya halal lakini kwa sababu mbali mbali tumekuwa tukila chakula bila kujua kimeanzia wapi na kimepita katika njia gani" Kwa kutambua mchango wa dini yetu tumepata mafunzoambao ndio wamiliki wa nembo ya Halal baada ya mwaka mmoja watakuja kufanya ukaguzi wa kile walichotuachia ili kueza kupata nembo hiyo itakayotusaidia kuuza bidhaa zetu katika nchi za Asia na nyenginezo, "alisema Lolila.

  Ameongeza kuwa nchi nyingi za kiarabu hawali chakula mpaka waone nembo ya Halal ambapo wanaamini chakula hicho kimepita katika njia sashihi inayotakiwa kwa waumini wa kiislamu na wasiokuwa waislmu.

  Huku akieleza kuwa Tanzania zipo bidhaa nyingi zitakazo weza kuingizia pato la Taifa kwa nchi hizo ikiwemo Malaysia endapo kama zitauzwa katika nchi za kimataifa.

  Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halal Tanzania Certification (HTC) Muhsin Hussein amesema wamejifunza mengi kutoka kwa ugeni huo kutoka Malaysia na watayafanyia kazi mafunzo hayo yaliyowapa weledi wa kutambua bidhaa Halali kuanzia kwenye hatua za awali, na kuongeza kuwa wataitisha mafunzo maalum kwa waandishi wa Habari ili waweze kutoa elimu kwa Umma nao ujue kwa undani bidhaa Halal.

  Mkurugenzi huyo amewatoa hofu a kwa kuwaeleza kuwa zile nembo za Serikali zinazotumika katika usimamizi wa bidhaa na chakula ikiwemo TBD na TFDA zitaendelea kuwepo ila nembo hiyo ya Halal itakuwepo ili kuweka Imani kwa waumini wa Dini ya Kiislamu waliokuwa na hofio ya kutumia bidhaa zisizo Halal, zinazokwenda kinyume na mafundisho ya Dini hiyo Tukufu.


  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimkabidhi zawadi Mwanafunzi  Mahira Baraka Hamadi wa kidato cha sita Skuli ya Biashara Mombasa Wilaya ya Magharibi Unguja  akiwa ni mwanafuzi aliyefanya vizuri  katika Mtihani wa Taifa Mei mwaka 2016,hafla iliyofanyika leo Ikulu Mjini Unguja[Picha na Ikulu.] 22/10/2016.
  za9
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimkabidhi zawadi Mwanafunzi  Munawara Abdull-Aziz  Salim wa kidato cha sita Skuli ya SUZA Unguja  akiwa ni mwanafuzi aliyefanya vizuri  katika Mtihani wa Taifa Mei mwaka 2016,hafla iliyofanyika leo Ikulu Mjini Unguja[Picha na Ikulu.] 22/10/2016.
  za10
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimkabidhi zawadi Mwanafunzi Suhayla  Hamad Abubakar wa kidato cha Nne Skuli ya Feza akiwa ni mwanafuzi aliyefanya vizuri katika Mtihani wa Taifa mwezi Octoba mwaka 2015,hafla iliyofanyika leo Ikulu Mjini Unguja[Picha na Ikulu.] 22/10/2016.
  za11
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimkabidhi zawadi Mwanafunzi Hamdoun Sabri Hamdoun wa kidato cha Nne Skuli ya SOS akiwa ni mwanafuzi aliyefanya vizuri katika Mtihani wa Taifa mwezi Octoba mwaka 2015,hafla iliyofanyika leo Ikulu Mjini Unguja[Picha na Ikulu.] 22/10/2016.
  za12
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimkabidhi zawadi Mwanafunzi Suleiman Ali Hamadi wa kidato cha sita Skuli ya Biashara ya Chasasa Pemba akiwa ni mwanafuzi aliyefanya vizuri zaidi kuliko wanafunzi wote hapa Zanzibar na ni mmoja kati ya wanafunzi kumi wa mwanzo Tanzania katika Mtihani wa Taifa mwezi mei mwaka 2016,hafla iliyofanyika leo Ikulu Mjini Unguja
  za1
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akizungumza na Walimu na Wanafunzi wa kidato cha Nne na Sita waliopata daraja la kwanza katika Mtihani wa Taifa katika mwezi Octoba -2015 na Mei mwaka- 2016,sherehe ya kuwazawadia  wanafunzi hao  iliyofanyika leo Ikulu Mjini Unguja,[Picha na Ikulu.] 22/10/2016.
  za3
  Baadhi ya Walimu na Wanafunzi wa kidato cha Nne na Sita waliopata daraja la kwanza katika Mtihani wa Taifa katika mwezi Octoba -2015 na Mei mwaka- 2016,wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akizungumza nao leo katika sherehe maalum ya kuwazawadia  wanafunzi hao  iliyofanyika Ikulu Mjini Unguja,[Picha na Ikulu.] 22/10/2016.
  za4
  Baadhi ya Walimu na Wanafunzi wa kidato cha Nne na Sita waliopata daraja la kwanza katika Mtihani wa Taifa katika mwezi Octoba -2015 na Mei mwaka- 2016,wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akizungumza nao leo katika sherehe maalum ya kuwazawadia  wanafunzi hao  iliyofanyika Ikulu Mjini Unguja,[Picha na Ikulu.] 22/10/2016.
  za5
  Baadhi ya Walimu  wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akizungumza na Wanafunzi wa kidato cha Nne na Sita waliopata daraja la kwanza katika Mtihani wa Taifa katika mwezi Octoba -2015 na Mei mwaka- 2016, katika sherehe maalum ya kuwazawadia  wanafunzi hao  iliyofanyika leo Ikulu Mjini Unguja,[Picha na Ikulu.] 22/10/2016.
  za6
  Baadhi ya Wanafunzi wa kidato cha Nne na Sita waliopata daraja la kwanza katika Mtihani wa Taifa katika mwezi Octoba -2015 na Mei mwaka- 2016,wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) wakati alipokuwa akizungumza nao  katika sherehe maalum ya kuwazawadia iliyofanyika leo Ikulu Mjini Unguja,[Picha na Ikulu.] 22/10/2016.
  za7
  Baadhi ya Wanafunzi wa kidato cha Nne na Sita waliopata daraja la kwanza katika Mtihani wa Taifa katika mwezi Octoba -2015 na Mei mwaka- 2016, wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) wakati alipokuwa akizungumza nao  katika sherehe maalum ya kuwazawadia iliyofanyika leo Ikulu Mjini Unguja,[Picha na Ikulu.] 22/10/2016.


  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia kwenye mkutano wa kwanza wa Wafanyabiashara wa Tanzania na Morocco utakaoainisha fursa za uwekezaji baina ya nchi hizo mbili uliofanyika kwenye Hotel ya Hyatt Regency.
  Wafanyabiashara wa Tanzania na Morocco wakimsikiliza  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mhe. Samia Suluhu Hassan alipokuwa akihutubia kwenye mkutano wa Kwanza wa Wafanyabiashara wa Tanzania na Morocco utakaoainisha fursa za uwekezaji baina ya nchi hizo mbili uliofanyika kwenye Hotel ya Hyatt Regency.


  Katika Hotuba yake ya ufunguzi wa Mkutano wa kwanza wa wafanyabiashara na Wawekezaji wa Tanzania na Morocco Makamu wa Rais aliainisha maeneo mbali mbali ambayo yanaweza kuwa fursa nzuri ya kuwekeza Tanzania.

  Baadhi ya maeneo hayo ni Kilimo,Utalii, Nishati, Mafuta na Gesi, Viwanda,Sekta ya Huduma, na Sekta ya Madini

  Mbali na kuainisha  baadhi ya fursa Makamu wa Rais aliwahakikishia uwepo wa amani na usalama na sheria mbalimbali zinazolinda haki za wawekezaji.
   Rais wa  Chama cha Wafanyabiashara wa Morocco Bi.Miriem Bensalah-Chaqroun, akihutubia kwenye mkutano wa kwanza wa Biashara na Uwekezaji baina ya Tanzania na Morocco uliofanyika kwenye Hotel ya Hyatt Regency.
   Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage akizungumza wakati wa mkutano wa kwanza uliowakutanisha wafanyabiashara wa Tanzania na Morroco.
   Sehemu ya wafanyabiashara kutoka Morocco wakifuatilia kwa makini mkutano huo.
  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI


  0 0

   

   
  Mmiliki wa Mradi wa Hoteli ya Kitalii katika eneo la Matemwe Mkoa wa Kaskazini Unguja, Mkurugenzi wa Mradi huo Brain Thomson, akitowa maelezo kwa waandishi wa habari walipofika kutembelea mradi huo kujionea maendeleo ya matayarisho yake na kuwaonesha michoro ya picha za majengo ya Mradi huo mkubwa utakaokuwa na uwanja vya ndege. na kutengeneza visiwa kwa ajili ya wageni wanaofika katika Visiwa vya Zanzibar. 
  Mmiliki wa Mradi wa Mkubwa wa Hoteli ya Kitalii katika eneo la Matemwe Mkoa wa Kaskazini Unguja Mr. Brian Thomson, akitowa maelezo ya mradi huo kwa kuwaonesha jinsi ya majengo yatakuwa katika eneo hilo na kutoa ajira kwa Wananchi wa Matemwe na vijiji jirani kupitia mradi huo. 
  Mmiliki wa Mradi Mkubwa wa Ujenzi wa Hoteli katika eneo la Matemwe Mkoa wa Kaskazini Unguja Mr. Brian Thomson akizungumza na waandishi wa habari walipofika kuangalia ujenzi wa mradi huo na kusema kukamilika kwakev kutachukua miaka minane kukamilika kwake na kutowa fursa za ajira kwa vijana wa kijiji hicho na kutowa maendeleo katika sekta za jamii kunufaika na mradi huo.
  Sehemu ya mbele ya majengo ya mradi huo kuingia katika eneo la hoteli hiyo.
  Jinsi ya mradi huo utakapokamilika ujenzi wake utakuwa kama hivi na kubadilisha mandhari ya eneo la matemwe mkoa wa kaskazini unguja.

  0 0  0 0


  Bibi Pili Abdallah akielezea kwa kina maisha ya Mabinti wadogo yanayowapelekea kupata Mimba za utotoni na kuolewa wakiwa wadogo, pia alizungumzia Tamaa na Matamanio yalivyo na nguvu ya kuwafanya watoto wakike kujiingiza katika maswala ya ngono wakiwa wadogo na kupelekea kupata mimba, mwisho aliwashauri wazazi wenzake kuwatambua watoto wao. Furahini Michael akiulizwa swali na Bwana Steven Mfuko kuhusu athari za mimba za utotoni na kuolewa katika umri mdogo.
  Mkazi wa Tabata kwa Cecy ambapo kampeni ya Binti wa kitaa ilifanyika Bi.Sheira Mheni akielezea jinsi watoto hususani wa kike wenye umri kati ya Miaka 12-17 walivyoharibika kutokana na mabadikiko ya Teknolijia ambapo imewapekea kufahamu mambo ya wakubwa wakiwa watoto na hatimaye kupata matamanio na kufanya kama walivyo ona katika Mitandao ya kijamii na Runinga jambo linalowasababishia Mimba za Utotoni
  Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Tenge Athuman Mpwenewe akieleza namna ambavyo kumekuwa na Mimba nyingi za utotoni katika mtaa wake na juhudi ambazo zimefanywa na Serikali ya Mtaa kuhakikisha swala hilo linatokomezwa kabisa na mwisho alizungumzia vikao na wanamtaa vinavyosaidia kutatua tatizo hilo.
  Mmoja wa Mabinti ambaye jina lake limehifadhiwa akiwa anatoa ushuhuda wa kuachishwa shule,na hapa alipo hasomi na kampeni ya Binti wa kitaa kupitia wadau watafanya jambo kwa Binti huyu
  Mwanaharakati Kijana Victoria Mwanziva akijibu swali na kuelezea kwa kina tafsiri ya Jinsia
  Mwezeshaji wa Kampeni ya Binti wa Kitaa Steven Mfuko akiwahoji baadhi ya Maswali watoto hawa wenye umri wa miaka 12 kama wanajua maswala mbalimbali kuhusu wao na kusema kwamba hawafahamu, na kuomba wapewe elimu juu ya mabadiko yao ya mwili ili kuepuka Mimba za utotoni
  Bi. Mwama Ajabu akielezea namna Simu zilivyoweza kuwaharibu watoto wa kike na kuongeza kuwa wazazi hawana muda nao ndio mana hizo simu zimawaharibu sana, na mara nyingi hufanya mawasiliano kisiri mida ya usiku wakati watu wamelala na kibaya zaidi watoto hao hupendelea zaidi kufatilia mitandao ambayo sio mizuri, ameshauri wazazi mwenzake kuwa lazima wawe karibu na mabinti zao.
  Baadhi ya wahusika wa Binti Kitaa wakiongea na Bodaboda waliofika katika kampeni ya Binti wa Kitaa
  Anna akizungumzia Jinsi Binti wa Kitaa inavyofanya kazi
  Hii Timu ya Binti wa kitaa Wakimsikiliza Mtoto aliyeachishwa Shule na Mzazi wake
  Baadhi ya wahusika wa Binti wa Kitaa wakiwa katika eneo la tukio
  Baadhi ya watu wakiwa katika Mdahalo huo
  Mhandisi Eliwanjeria James kutoka Kikundi cha Mainjinia wanawake Tanzania akielezea kwa kina juu ya kampeni ya Binti wa Kitaa

  Mkurugenzi Mtendaji wa (CVF) Ndg. George David maarufu kwa Ambassador Angelo akiendela kutoa Mwongozo

  Mwakilishi wa Sunshine Group akipokea Cheti cha Shukurani kutoka kwa Binti wa Kitaa
  Mwakilishi kutoka GW Health World Limited akipokea Cheti cha Shukurani kutoka Binti wa Kitaa
  Bwana Steven Mfuko akitoa Elimu juu ya Mimba za Utotoni na Kuolewa wakiwa chini ya Miaka 18
  Watu mbalimbali wakiwa katika kampeni hiyo
  Kulia ni Binti akitoa ushuhuda wa yeye kupata mimba wakati akiwa na miaka 16 na kusema hiyo ilisababishwa na familia yake
  Aliyemwakilisha Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Tabata Sajenti Geoffrey Kapenejele ambaye pia yupo katika Dawati akielezea namna wanavyotoa elimu kuhusiana na Jinsia katika maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na Mashuleni pia kwa madereva Bodaboda ambao wamekuwa wakilalamikiwa kusababisha Mimba nyingi za utotoni, Mwisho aliomba jamii kwa ujumla kushirikiana ili kupiga vita swala hilo
  Bwana nidhamu wa Madereva wa Bodaboda kituo cha Cecy Bwana Atupele akieleza namna elimu ya maswala ya Jinsia ilivyo wasaidia wao kuunga mkono kupambana na mimba za utotoni ambapo wamejiwekea utaratibu wa adhabu kali kwa yeyote atakayempa mimba binti mwenye umri wa chini ya miaka 18
  Mambinti wakiwa katika Kampeni ya Binti wa Kitaa
  Mwakilishi wa Sunshine Group Fatuma akielezea namna mimba za utotoni zinavyo athiri maisha ya Binti na pia kusababisha matatizo ya kiafya na kumsababisha akose mambo mengi na kuahidi kuendelea kushirikiana na kampeni ya Binti wa Kitaa kupinga swala hilo
  Mwakilishi kutoka TBC FM akielezea majukumu yao ya kuhakikisha kila mtu anapata habari na taarifa pia elimu juu ya kupinga Mimba za utotoni pamoja na ndoa
  Bwana Makundi kuroka Radio France RFI akielezea namna baadhi ya Nchi zenye machafuko zinavyo wanyanyasa mabinti wadogo wenye chini ya umri wa miaka 18 kwa kuwaoa, kufanya nao ngono pia kuwahusisha katika mashambulizi mbalimbali, Pia alieleza kuwa vyombo vya Habari vina jukumu kubwa sana la kuhakikisha jamii inapata taarifa na elimu juu ya kupinga mimba na ndoa za utotoni
  Kila sehemu ambapo Kampeni ya Binti wa Kitaa inapita huwa panaachwa alama inayo onesha kuwa kuna kitu kilifanyika hapa Meneja wa Kampeni ya Binti wa Kitaa Mhandisi Eliwanjeria James (kushoto) akiwa na mtoto ambaye aliachishwa shule na Baba yake , hapa anakabidhiwa rasmi kwa wawakilishi wa Sunshine Group Ltd pamoja na GW Health limited kwa ajili ya kusomeshwa ili amalizie masomo yake

  Picha ya pamoja .Picha zote na Fredy Njeje

  0 0


  Na Lulu Mussa-
  Songwe

  Wakazi wa Wilaya ya Ileje Mkoani Songwe wamehamasishwa kutunza Vyanzo vya Maji kwakuwa Maji hayana mmadala wa kitu chochote. Waziri wa Nchi mwenye dhamana ya Usimamizi wa Masuala ya Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba ameyasema hayo leo katika muendelezo wa ziara yake ya kukagua mazingira nchini.

  Akiwa katika Kijiji cha Ibungu Wilayani Ileje, Waziri Makamba alishuhudia uliochepushwaji wa Mto Kalembo kwa manufaa ya baadhi ya mtu/watu, na haikuweza kufahamika mara moja muhusika. Aidha Waziri Makamba amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Ileje Bw. Joseph Modest Mkude kuhakisha wanambaini mtu/watu hao na kuwafisha katika vyombo vya Sheria.

  Taarifa iliyotolewa na Mkuu wa wilaya ya Ileje ilisema kwamba kumekuwa na uvamizi katika Vyanzo vya Maji na Serikikali imeendelea na juhudi za kuwaondoa kwa kuwapatia maeneo mengine ila baadhi ya wananchi hao wamekuwa wakikaidi. Hali hiyo haikumfurahisha Waziri Makamba na kuagizia kutumika mamlaka ya Dola. “Hatuwezi kuruhusu watu kuharibu Vyanzo vya Maji na kuwabembeleza watoke” Makamba alilisitiza.

  Waziri Makamba amesema ni muhimu watu kutii Sheria na Mamlaka zilizopo, ameagiza wakazi hao kupewa wiki mbili tu na baada ya hapo waondolewe kwa nguvu kwani tayari maeneo mbadala kwa makazi yao yalisha ainishwa. Pia Waziri Makamba ameahidi kutoa muongozo wa Sheria ndogondogo za Mazingira za Vijiji na Vitongoji ili zitumike kama nyenzo za hifadhi ya Mazingira Nchini.

  Katika hatua nyingine Waziri Makamba alitembelea Kijiji cha Lubanda, Kata ya Lubanda na kufanya Mkutano wa hadhara na wananchi na kuwasisitizia, kutokokata miti ovyo, kutochoma misitu na kuepuka uchepushaji wa Vyanzo vya Maji ikiwemo mito na Mabonde.

  Pia Waziri Makamba aliwashauri wakazi wa Lubanda kulima kilimo cha Matuta ama makinga maji ili kuepuka mmomonyoko wa udongo katika miinuko. Aidha Waziri Makamba ameunga mkono jitahada za wananchi wa Kata hiyo za ujenzi wa Kituo cha afya kwa kuchangia bati Ishirini na nane (28). Waziri Makamba anaendelea na ziara yake na leo amewasili katika Mkoa wa Rukwa.
  Uharibifu wa Mazingira unaofanywa na binadamu, pichani ni Mto Kalembo uliopo katika Kijiji cha Ibungu Wilayani Ileje uliochepushwa kwa manufaa ya baadhi ya mtu/watu, haikuweza kufahamika mara moja muhusika. Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba amemuagiza Mkuu wa wilaya ya Ileje Bw. Joseph Modest Mkude kutafuta wahusika na kuwafikishwa kwenye Vyombo vya dola.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akifafanua jambo kwa wananchi mara baada ya kuwapa fursa ya kuuliza maswali katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kata ya Lubada Wilayani Ileje. Kushoto ni Bw. Stanford Kibona aliyeuliza swali.

  0 0

  Miss Talent 2016 ambaye ni Mshiriki wa Miss Tanzania 2016 namba 20,Lisa Mdolo aliibuka kinara katika mpambano huo wa Kusaka Vipaji kwa washiriki wa Miss Tanzania 2016 uliofanyika Jembe Beach jijini Mwanza usiku wa kuamkia leo. Mshindi huyo wa Miss Talent 2016 amecheza ngoma ya asili.Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii Mwanza.
  Mshindi wa Miss Talent 2016 akipongezwa na Mamiss wezake mara baada ya kushinda kinyang’anilo cha Miss Talent leo jijini Mwanza.
  Top 5 Miss Talent 2016 wakiwa wamepozi mara baada ya kushinda nafasi tano Bora ya Miss Talent 2016.
  Hashim Lundenga akitangaza Mshindi wa Kwanza wa Miss Talent 2015 mara baada ya Mamiss Tanzania Kufuana katika Kinyang’anyiro hicho na Miss Talent 2016 No. 20 kuibuka Kidedea.
   Mshindi wa Pili wa Miss Talent 2016 akionesha Kipaji chake.Mshindi wa tatu wa Miss Talent 2016 akifanya yake kwa kujifunga Mtandio kwa Mitindo mbalimbali.
  Kulia ni Mshindi wa Nne namba 13 wa Mshindi wa Miss Talent 2016 akishirikiana na mwenzie kutumbuiza katika hafla ya kutafuta vipaji kwa mwamiss Tanzania 2016.
  Mshindi wa Tano wa Miss Talent 2016 akisoma taarifa ya habari kwa Lugha ya Kiingereza na Kufananisha na watangazaji wa BBC World wakati wa kuonyesha kipaji chake jijini Mwanza Leo.

  0 0


  Baadhi ya madawati yaliyokabidhiwa leo kwa Mkuu wa wilaya ya MuhezaHajat,Mhandisi Mwanasha Tumbo ikiwa ni mkakati wa kukabiliana na upungufu wa madawati kwenye shule za msingi wilayani humo. Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha.

  Mkuu wa wilaya ya Muheza,Hajat,Mhandisi Mwanasha Tumbo kulia akipokea madawati 200 kutoka kwa Meneja wa Shamba la Miti Lunguza, yaliyotolewa na wakala wa huduma za misitu Tanzania (TFS) Abdallah Mchomvu katika halfa iliyofanyika leo
  Mkuu wa wilaya ya Muheza,Hajat,Mhandisi Mwanasha Tumbo wa kwanza kulia mwenye hijabu akikagua madawati hayo kabla ya kuyapokea anayefuata ni Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Muheza,Kahoza Joseph ambaye ni Mhandisi wa Ujenzi wa Halmashauri hiyo
  Mkuu wa wilaya ya Muheza,Hajat,Mhandisi Mwanasha Tumbo wa kwanza kulia mwenye hijabu akitazama baadhi ya madawati hayo kabla ya kuyapokea anayefuata ni Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Muheza,Kahoza Joseph ambaye ni Mhandisi wa Ujenzi wa Halmashauri hiyo
  Meneja wa Shamba la Miti Lunguza,Abdallah Mchomvu akizungumza katika halfa hiyo ya kukabidhi madawati kwa Mkuu wa wilaya ya Muheza,Hajat,Mhandisi Mwanasha Tumbo wa kwanza kushoto aliyekaa ambayo yaliyotolewa na wakala wa huduma za misitu Tanzania (TFS)
  Kaimu Katibu Tawala wa wilaya ya Muheza ambaye ni Afisa Tarafa ya Muheza Khatibu Omari wakati wa halfa hiyo wa pili kutoka kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Muheza,Hajat,Mhandisi Mwanasha Tumbo
  Baadhi ya wafanyakazi wa shamba la miti la Lunguza ambalo ni la serikali linalojishughulisha na uhifadhi wa misitu ya asili na ustawishaji wa miti ya misaji (Teak)

  0 0


  0 0

  Baadhi ya zana haramu za uvuvi zilizokamatwa, Pichani ni Mabomu yanayotumika kulipulia Samakina viumbe vingine Baharini.

  Zana Haramu za vuvi zikiteketea kwa moto. (Picha na :Bernad Mpangala Mchambuzi wa Mifumo Kilwa.)
  Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Ndg; Christopher Ngubiagai akizungumza na wavuvi.
   
  Mkuu wa wilaya ya Kilwa, Chistopher Ngubiagai, ametoa siku 14 kwa wavuvi haramu katika wilaya hiyo wajisalimishe na kukabidhi dhana wanazotumia.

  Mkuu huyo wa wilaya ametoa agizo hilo wakati wa zoezi la uchomaji wa zana za uvuvi haramu lililofanyika mjini Kilwa Masoko.

  Ngubiagai alisema uvuvi haramu nitatizo linalohitaji nguvu na jitihada zinazotokana na uzalendo ili kulikabili. Kwasababu ya mbinu zinazotumiwa na wahalifu katika kuhakikisha hawakamatwi na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.

  Alisema mapambano hayo ni makali na magumu, kwa sababu baadhi ya wahalifu hao kuwa na mtandao mkubwa unaowahusisha baadhi ya viongozi na watendaji wa umma wasiowaadilifu. Hivyo wilaya hiyo imetengeneza mikakati madhubuti itakayotokomeza tatizo hilo linalotishia uwepo wa viumbe hai wa baharini. 

  Ngubiagai aliitaja baadhi ya mikakati hiyo kuwa ni kuhakiki wavuvi wote waliopo katika wilaya hiyo na maeneo wanayofanyia shugulizao, kusajili vyombo vyote vya uvuvi na kuvipa namba za utambuzi na kujua kila chombo mahali kilipo, kuwasajili wavuvi wote walio kwenye kambi za uvuvi na kuainisha bandari maalumu zinazoshushia mazao ya uvuvi ya maeneo mbalimbali.

  "Napenda kuwatahadharisha wasalimishe zana zao za uvuvi haramu haraka iwezekanavyo ndani ya wiki mbili kwani zama zao zimekwisha. Vita hii niliyoianza haitasimama nitahakikisha uvuvi haramu unatokomea kabisa katika wilaya hii,lengo ni kuhakikisha rasilimali za uvuvi zinavinufaisha hata vizazi vijavyo," alisisitiza Ngubiagai.

  Alibainisha kuwa kupitia hatua za awali za mapambano hayo ambayo ni utekelezaji wa maagizo ya Rais Magufuli aliyotoa hivi karibuni jijini Mwanza, naya waziri mkuu, Kassim Majaliwa aliyotoa wilayani Mafia mkoa wa Pwani.

  Wamefanikiwa kukamata kilo 281 za unga wa kutengenezea mabomu tambi 7, vibati 7 na chupa za mabomu ambazo zilikamatwa kutokana na ushiriano mkubwa wa raia wema kwenye kambi za uvuvi za Nyuni, Ukuza na Simaya.
  "Unga uliokamatwa ulikuwa na uwezo wa kutengeneza chupa za mabomu 188,kila chupa ingeweza kuharibu eneo lenye ukubwa wa zaidi ya mita hamsini,maana yake nikwamba zisingekamatwa basi eneo la bahari lenye ukubwa wa zaidi ya mita za mraba 9400 zingeharibiwa kabisa," alisema.

  Mkuu huyo wawilaya alitoa wito kwa serikali kupitia wizara ya maliasili na utalii kwa kusema "Kuna umuhimu wakuangalia na kutafuta uwezekano wa kuunda kikosi maalum cha kwa ajili ya kupambana na wavuvi haramu katika bahari na maziwa,kwa sababu hawa askari ingawa wanajitihidi sana na juhudi zao zinazaa matunda,lakini hawana uelewa mkubwa wa mambo ya bahari na sheria zake," alisema.

  Kwa upande wake ofisa uvuvi wa halmashauri ya wilaya hiyo, Ahmad Mkali. Alisema miongoni mwa changamoto kubwa zinazosababisha kupunguza kasi ya kupambana na uvuvi huo ni uchache wa boti za kufanyia  doria.Akibainisha kuwa halmashauri hiyo inaboti moja tu. Wakati mahitaji halisi ni angalau boti nne."Wavuvi haramu wanavua bahari kuu ni mbali,na eneo la bahari nikubwa sana kwa boti moja inakuwa vigum
   

  0 0

  Mzee Philip Mangula
  Na Bashir Nkoromo, Mkuranga
  MAKAMU Mwenyekiti wa CCM-Bara, Philip Mangula ameelezea kufurahishwa kwake kufukuzwa kwa wanachama 100 mkoani Mwanza kwa kubainika kukisaliti chama wakati wa uchaguzi mkuu uliopita.

  "Haiwezekani, unajiita mwanachama, halafu badala ya kujitolea kwa nguvu zako zote chama kishinde vita ya kushika dola, wewe unakisaliti,  hapo unakuwa si mwanachama bali jeshi la kukodiwa",  Mangula alisema, hayo jana, wakati akizungumza na Vijana wanaosoma na waliohitimu vyuo vikuu 20, ambao wameweka kambi ya kufyatua matofali kwa ajli ya ujenzi wa mabweni na nyumba za walimu katika shule ya Sekondari Nasabagani, Mkuranga mkoa wa Pwani.

   "Taarifa ya Chama kuwafukuza uanachama wale 100 kule Mwanza imenifurahisha sana, ni matumaini yangu kwamba hatua kama hizi zitaendelea kuchukuliwa  kila mahala nchini kote kwa waliokisaliti chama. hivi ni mchezaji gani anayempiga ngwara mchezaji wa timu yake wakati wa mechi ya kutafuta ubingwa halafu akaachwa kuendelea kuwa katika timu?" Mangula alisema na kuhoji kwa mshangao.

  Mangua alisema, wakati mikoa itaendelea kuchukua hatua, lakini pia kwa ngazi ya taifa hatua dhidi ya waliokisaliti chama zitaendelea kuchukuliwa, ikiwa ni pamoja na kuwatupilia mbali watakaojaribu kuomba nafasi za uongozi wakati wa uchaguzi wa Chama mwakani, huku wakiwa wameshabainika kuwa walikisaliti chama wakati wa uchaguzi mkuu ulipita.

  Mangula aliwataka vijana nchini kote hasa wasomi, kuepuka kutumiwa vibaya na wanachama watakaokuwa wanasaka uongozi wakati wa uchaguzi mkuu wa CCM unaotarajiwa kufanyika mwakani, kwa kuwa kijana yeyote atakayekubali kutumiwa vibaya atakuwa amekisaliti na kuchangia kunyong'onyesha nguvu na uhai wa Chama.

  "Hili la kutumiwa vibaya hasa ninyi vijana, nawaasa sana kuepuka nalo, jambo hili ni baya sana, na si kwa Chama tu lakini hata kwa wewe uliyekubali kutumika, maana utatumiwa kama ngazi, halafu akishapita hatakuwa na manufaa kwako na hata kwa taifa maana atakuwa mvurugaji tu, badala ya kushiriki kuleta maendeleo ya chama na taifa", Alisisitiza mangula.

  Alisema, vijana hao 53 waliojitolewa kufyatua matofali kwa ajili ya ujenzi huo wa mabweni na nyumba za walimu, wameonyesha moyo mkubwa wa uzalendo kwa nchi yao, na kwamba huo ndiyo uzalendo wa kweli unaopaswa kuonyeshwa na kila mwananchi hasa viongozi katika ngazi mbalimbali.

  Mangula alisema, vijana hao wameoyesha mwamko ule uliokuwa umejengwa na kuwepo wakati wa Baba wa taifa Mwalimu Nyerere, ambao katika miaka ya hivi karibuni hasa baada ya kuanza kwa mfumo wa vyama vingi umetoweka kwa watu kuanza kujinasibu kwa majina ya vyama vyao vya siasa badala ya kuonyesha uzalendo kwa kuisaidia jamii kwa za kujitoea.

  Alisema, umefikia wakati sasa kipimo cha kwanza kwa yeyote kupata uongozi iwe ni kutazamwa kama kweli ni mzalendo ambaye yupo mstari wa mbele kufanya kazi za kujitolea katika jamii, na siyo kutazama uwezo wake wa kuzungumza na kumwaga hotuba nzuri majukwaani.

  "Sifa za mtu kupewa uongozi isiwe ukasuku wa kutoa talalila za hotuba nzuri za kisiasa majukwaani, kwanza atazwamwe kama amekuwa akitoa mchango gani kwa jamii kwa kufanya kazi za kujitolea katika kusukuma maendeleo ya taifa mbele kama ilivyokuwa wakati wa Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, hongereni sana vijana kwa kuonyesha moyo wa kfufua uzalendo.", alisema  Mangula.

  Mapema, Katibu wa Kambi ya vijana hao, Daniel Sarungi, alisema, tangu walipoanza kambi hiyo, na kuanza kufyatua matofali Septemba 29, 2016, wameshafywatua matofali zaidi ya 30,000, kati ya lengo lao la matofali 45,000, ambalo watahakikisha wamelifikia kesho Oktoba 24, 2016.

  Alisema, vijana hao wamejikusanya kutoka vyuo vikuu 20, vutatu vikiwa ni vya nchi za nje, na wamekuwa wakishirikiana vizuri, tangu kusomba mchanga na kufyatua matofali, kujipikia chakula, kufundisha wanafunzi wa kidato cha tano na sita katika shule hiyo, kutoa huduma ya afya, kushiriki michezo mbalimbali na kufanya semina na mijadala ya kukuza uwezo wa kuleta maendeleo katika jamii.

  Sarungi alisema, vijana hao ambao baadhi wameshahitimu masomo na wengine bado wanasoma katika taaluma mbalimbali wameamua kujitolea kusaidia ujenzi wa mabweni na nyumba za walimu, baada ya kuguswa na adha ya kulala chini wanafunzi wa kidato cha tano na cha sita katika shule hiyo huku walimu na wakiwa hawana nyumba za kutosha kuishi.

  Wakati wanafunzi waliopo sasa wanalala chini katika chumba cha maabara, nyumba moja yeneye nyumba vitatu inatumiwa na walimu saba kuishi katika nyumba hiyo, haliambayo hairidhishi.

  Mapema, Mangula alishiriki kufyatua matofali na baadaye kusema kwamba aliamua kwenda kuwaunga mkono vijana hao baada ya kusikia taarifa zao kwenye vyombo vya habari hatua yao ya kuamua kujitolea kusaidia shule hiyo baada ya kuhamasishwa na Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Filberto Sanga ambaye siyo tu amekuwa akiratibu bali amekuwa pia ashiriki katika ufyatuaji huo wa matofali.

  0 0

  Akina dada walioshiriki katika mashindano ya urembo kwa watu wanaoishi na ulemavu wa ngozi ama Albinos jijini Nairobi, Kenya. Tarehe 21 Oktoba 2016.Mamia walijitokeza kushuhudia maonyesho ya urembo ya Mr na Ms Albino nchini Kenya. Kila siku Albino wanakabiliwa na hatari ya kuuawa na viungo vyao vya mwili kuuzwa kutokana na imani za kishirikina Afrika mashariki na Afrika kusini.Chanzo-BBC SWAHILI
  Malkia mpya! Louise Lihanda, aliyeshinda taji la urembo kwa akina dada atembea jukwani akiwa amevalia vazi la kupendeza lililotengenezwa kwa kutumia puto. Loiuse ambaye ni mwanafunzi, amekuwa mwanamke wa kwanza kushinda taji hilo, katika mashindano yaliyofanyika jijini Nairobi, Kenya tarehe 21 Oktoba 2016
  Wanaume walioshiriki katika mashindano hayo wasimama  jukwaani. walishiriki katika mashindano ya urembo kwa watu wanaoishi na ulemavu wa ngozi ama Albinos jijini Nairobi, Kenya. Tarehe 21 Oktoba 2016.
  Mfalme! Jairus Ongetta, ambaye amekabidhiwa taji ya uanamitindo bora kwa wanaume akiwa jukwaani na mavazi ya kupendeza.
  Erick Thomas, awaongoza wanamitindo wenzake kwenye jukwaa wakati wa mashindano ya urembo kwa watu wanaoishi na ulemavu wa ngozi. Lengo lake ni kuhakikisha kwamba watu walio na ulemavu huo wamejivunia ngozi yao.
  Msichana huyu aliduwazwa na maonyesho hayo! Yeye ni miongoni mwa watu ambao kila siku wanakabiliwa na hatari ya kuuawa kutokana na imani za kishirikina Afrika mashariki na Afrika kusini.
  Miraba minne! John Ngatia, ambaye pia huwa anasakata densi, avalia sare ya mapigano ya ndondi katika maonyesho hayo, jijini Nairobi Kenya tarehe 21 Oktoba 2016
  Majaji walikuwa macho! Waliongozwa na mwanamitindo wa kimataifa Deliah Ipupa (katikati) tarehe 21Oktoba 2016.
  Naomi Wafula, ajitokeza jukwaani akiwa amevalia vazi lililotengenezwa kwa sahani za plastiki katika mashindano ya urembo yaliyofanyika jijini Nairobi, Kenya tarehe 21 Oktoba 2016
  Mamia walihudhuria maonyesho hayo kuonyesha umoja wao na watu wanaoishi na ulemavu wa ngozi katika mgahawa wa Carnivore jijini Nairobi Kenya, tarehe 21, Oktoba 2016
   
   Amina Makokha ajitokeza jukwaani akiwa amevalia sare ya mchezo wa raga  katika mashindano ya urembo yaliyofanyika jijini Nairobi, Kenya tarehe 21 Oktoba 2016
  Kutoka kulia, naibu rais wa Kenya William Ruto, Mbunge Isaack Mwaura na mkurugenzi mkuu wa bodi ya filamu nchini Kenya Ezekiel Mutua pia walikuwemo.

  0 0

  Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mst. Damian Lubuva (kulia) akiungana kuimba wimbo wa Taifa na Mgeni Rasmi wa Maadhimisho ya Kumbukumbu ya Miaka 50 ya Kuanzishwa kwa Tume ya Kudumu ya Uchunguzi (TKU) Mhe. Waziri wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah Kairuki (kushoto) na Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Bahame Nyanduga, kwenye ufunguzi wa maadhimisho hayo liliyofanyika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.
  Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mst. Damian Lubuva (kulia) akieleza uzoefu wake kuhusu shughuli za Tume ya Kudumu ya Uchunguzi (TKU) kwenye kongamano hilo.
  Baadhi ya viongozi wa Serikali waliohudhuria Maadhimisho ya Kumbukumbu ya Miaka 50 ya Kuanzishwa kwa Tume ya Kudumu ya Uchunguzi (TKU) kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam wakiongozwa na Rais Mstafu wa Awamu ya Pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi (wa pili kulia) wakifuatalia taarifa ya Jaji Mst. Lubuva.Wengine ni Mawaziri Wakuu Wastaafu Fredrick Sumaye (kulia), Jaji Mstaafu Joseph Warioba (wa tatu), na Mwanasheria Mkuu Mstaafu Jaji Mack Bomani na Mwenyekiti Mstaafu wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Jaji Kiongozi Mstaafu Amiri Manento.
  Baadhi ya Wageni Waalikwa wakiwemo kutoa Ubalozi wa Sweden nchini Tanzania na Wawakilishi wa Tume ya Kudumu ya Uchunguzi za nchi za Afrika, wakifuatilia taarifa ya Jaji Mst. Lubuva.
  Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Alhaj Ali Hassan Mwinyi akiwa akipokea tuzo ya Heshima ya Utawala Bora kutoka kwa Mgeni Rasmi wa Maadhimisho ya Kumbukumbu ya Miaka 50 ya Kuanzishwa kwa Tume ya Kudumu ya Uchunguzi (TKU) Mhe. Waziri wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah Kairuki kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.
  Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mst. Damian Lubuva (katikati) akiwa amepokea Cheti cha Utambuzi wa Utumishi wake kwenye Tume ya Kudumu ya Uchunguzi (TKU) kutambua mchango wake.Kushoto ni Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), Bahame Tom Nyanduga na kulia ni Katibu Mtendaji wa Tume hiyo Mary Massay.
  Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mst. Damian Lubuva (wa tatu kulia) akiungana na kwenye picha ya pamoja na na Mgeni Rasmi wa Maadhimisho ya Kumbukumbu ya Miaka 50 ya Kuanzishwa kwa Tume ya Kudumu ya Uchunguzi (TKU) Waziri wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angela Kairuki, Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi na Viongozi wengine wa Serikali Wastaafu waliohudhuria maadhimisho hayo kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam..
  Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mst. Damian Lubuva, akisalimiana na Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi.
  Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mst. Damian Lubuva akimueleza jambo Mgeni Rasmi wa Maadhimisho ya Kumbukumbu ya Miaka 50 ya Kuanzishwa kwa Tume ya Kudumu ya Uchunguzi (TKU) Waziri wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angela Kairuki baada ya ufunguzi wa maadhimisho hayo.
  1. Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mst. Damian Lubuva, akibadilisha mawazo na Wanasheria Wakuu wa Serikali Wastaafu wenzake Jaji Mst. Mark Bomani 1965-1976 na Jaji Mst. Joseph Sinde Warioba 1976 -1985.Jaji Mst. Warioba alitumikia nafasi hiyo kuanzia mwaka 1985 hadi 1993.
  Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mst. Damian Lubuva akizungumza na kituo cha Televisheni cha ITV baada ya ufunguzi wa Maadhimisho ya Kumbukumbu ya Miaka 50 ya Kuanzishwa kwa Tume ya Kudumu ya Uchunguzi (TKU).Picha na Hussein Makame-NEC
   
   
  Hussein Makame, NEC

  Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mst. Damian Lubuva ameitaka Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) kujifunza uzoefu wa tendaji wa Tume ya Kudumu ya Uchunguzi (TKU) ili kuimarisha utawala bora nchini.

  Jaji Mst. Lubuva ametoa wito huo wakati akeleza uzoefu wake juu ya utendaji kazi wa Tume ya Kudumu ya Uchunguzi (TKU) wakati wa Maadhimisho ya Miaka 50 ya Tume hiyo yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.

  Alisema pamoja na TKU kukabiliwa na changamoto nyingi katika inatekeleza majukumu yake wakati huo lakini ilifanya kazi zake kwa ufanisi kutokana na malalamiko ya wananchi yaliyoshughulikiwa kwa wakati huo.

  “Katika hali na mazingira ya Tume ya wakati huo, bila kusita nashawishika kusema kuwa Tume ya Kudumu ilianzishwa wakati ambapo si watu wengi kwa bahati mbaya Afrka ambao walijali haki za binadamu na utawala bora” alisema Jaji Mst. Lubuva.

  Aliongeza kuwa itakuwa si kusifia kusema kuwa TKU ilifanya kazi nzuri katika kipindi chake cha miaka 32 kwani ulikuwa wakati ambapo Tanzania ndio ilikuwa imejikomboa kutoka utawala wa Kikoloni na ilijitahidi kuendesha shughuli za maendeleo kwa wananchi.

  Hata hivyo alisisitiza kuwa walithubutu kwa mwalimu kuleta wazo la kuanzisha TKU ili kunusuru wananchi kutakona na madhila ya matumizi mabaya ya madaraka ya viongozi na watendaji kwa wakati huo.

  “Kwa upande mwingine Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora ina kibarua kizito katika kutekeleza majukumu yake katika mazingira ya sasa ambapo tume hii si rahisi kuelezea kwa wananchi kwa nini isifanikiwe zaidi ya TKU”

  Alisema THBUB tofauti na TKU ina bahati ya kujifunza kutokana na uzoefu wa tume hiyo ya kudumu katika mazingira ya sasa kulinganisha maendeleo na uelewa wawananchi kiujumla kuhusu haki zao za kimsingi kisiasa na kiutawala.

  “Hivyo tunaposherehekea miaka 50 ya Tume ya Uchunguzi ni halali kusema kwamba ilikidhi haja na matakwa ya wananchi kwa wakati huo kuweka misingi imara ambayo THBUB itaitumia katika juhudi za kusonga mbele”alisema Jaji Mst. Lubuva.

  Kwa upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejiment ya Utuishi wa Umma Mhe. Angellah Kairuki alisema lengo kubwa la Serikali kuanzisha TKU ilikuwa ni kumlinda mwananchi na lilifanikiwa kwa kushughulikia malalamiko 39,000 kwa kipindi cha miaka 35.

  “Aidha malalamiko yaliyopokelewa katika kipindi cha miaka 15 (2001-2016) ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora ni 32,000 na hivyo kufanya idadi ya malalamiko ya miaka 50 kufikia 71,000” alisema Mhe. Waziri Kairuki na kuongeza kuwa:

  “Idadi hiyo inaonesha jinsi vyombo hivi vilivyo na manufaa kwa wananchi wanyonge.Baadhi ya malalamiko yaliyopokelewa ni kuhusu vitendo vya unyanyasaji, masuala ya utumishi, kuchelewa kutekeleza wajibu, , kukataliwa kuomba rufaa, kutrofuata taratibu za kisheria, mirathi, matumizi mabaya ya mali ya umma na migogoro ya ardhi”

  Naye Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Bahame Nyanduga alisema Maadhimisho ya Miaka 50 ya TKU yamekwenda sanjari na kumuenzi Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere kwa kuanzisha Tume hiyo ikiwa ni taasisi ya kusimamia uwajibikaji wa watumishi wa umma kwa wananchi.

  “Pili ni kujikumbusha huko tulikotoka na kujifunza kutokana na kazi za TKU, changamoto na na mafanikio iliyoyapata na mwelekeo unaotakiwa katika kuhakikisha dhana ya uwajibikaji na utawala bora zinaendelezwa nchini Tanzania” alisema Nyanduga.

  Katika maadhimisho hayo Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere na Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi walipata Tuzo na Cheti cha kutambua mchango wao kuweka misingi ya uwajibika na utawala Bora.


  0 0

  DC-Longido,Mh Chongolo.
  Mkuu wa wilaya ya Longido Daniel Godfrey Chongolo amemtia ndani Mkandarasi anayejenga barabara ya Longido-Kitumbeine-Oldonyolengai Bw. Loserian Sokonei Mollel kutokana na uzembe na kutotimiza matakwa ya mkataba na kuwasababishia usumbufu watumiaji wa barabara hiyo pamoja  na wananchi kwa ujumla. 

  Mkandarasi huyo anayemiliki kampuni ya Genuine Company Limited amekuwa akiendesha shughuli za ujenzi wa drift katika barabara hiyo bila kutengeneza barabara mchepuko (diversion) katika maeneo hayo na kusababisha mara kwa mara wasafiri kukwama na kulala porini. 

  Wakizungumza na mtandao huu, wananchi wa kijiji cha Gelai Lumbwa wamepongeza uamuzi wa DC Chongolo kwa sababu unasaidia kuondosha na kutatua kero zanazowasumbua na kuwakwaza kwenye maisha yao ya kila siku. "Tulichoshwa na watu waliokuwa wakifanya mambo vile wanavyotaka wao. Kwa hakika hii ni awamu ya Kazi Tu, tunamshukuru DC na OCD na tunamuunga mkono" alisema Mesiaki Laizer.

  0 0

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na jeshi la Kujenga Taifa Mh Job Masima aliyeshinda kwa Senior akipiga mpira wakati wa mashindano ya PWC Trophy yaliyofanyika Jumamosi Oktoba 22 katika uwanja wa Golf wa jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania Lugalo Jijini Dar Es Salaam.
  Baadhi ya Watoto (Junior) wa Klabu ya Golf ya Lugalo walioshiriki mashindano ya PWC Jumamosi Oktoba 22 Jijini Dar es Salaam wa Pili Kulia ni Mshindi wa Kwanza wa Kundi hilo Almadius Simon wa Klabu ya Lugalo.
  Wachezaji wa Golf kutoka kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mh Job Masima, Dk Edmund Mndolwa aliyekuwa Mkuu wa majeshi Jenerali Mstaafu George Waitara na Balozi Clemence Sanga wakibadilshana mawazo kabla ya kuanza mashindando ya PWC yaliyofanyika Jumamosi Oktoba 22 katika Uwanja wa Golf Lugalo Jijini Dar es Salaam.
  Mshindi wa Jumla wa mashindano ya PWC yaliyofanyika Jumamosi Oktoba 22 Jijini Dar es Salaam Nicholous Chitanda wa Lugalo aliyeshika Vikombe akiwa katika Picha ya pamoja mara baada ya kukabidhiwa Kushoto ni mwenyekiti wa Klabu ya Lugalo Brigedia Jenerali Michael Luwongo , wa kwanza kulia ni Mwenyekiti wa TGU Joseph Tango na wa pili kulia ni Msuya Mkurugenzi PWC .(Picha na Luteni Selemani Semunyu).

  0 0


  0 0


  Mwenyekiti wa Chama cha Wahudumu wa Baa Tanzania (Chawabata), Ali Hussein (kulia), akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, wakati akitoa ombi kwa serikali la kuomba kufunguliwa baa muda wote ili kunusuru biashara hiyo. Kushoto ni Katibu wa chama hicho, Boniface Lameck.
  Katibu wa chama hicho, Boniface Lameck. akisisitiza jambo kwenye mkutano huo.


  Na Dotto Mwaibale

  CHAMA cha Wahudumu wa Baa Tanzania (Chawabata) kimeiangukia serikali kwa kuiomba iruhusu wenye mabaa kufanya biashara zao wakati wote ili kusaidia kupata fedha za kulipa kodi na mishahara ya wafanyakazi wao.

  Ombi hilo limetolewa na Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho, Ali Huseein wakati akizungumza na mtandao wa www.habarizajamii.com Dar es Salaam leo asubuhi kuhusu changamoto waliyonao wenye mabaa katika kufanya biashara yao hiyo ya uuzaji wa vileo na vinywaji baridi."Tunaiomba serikali kuangalia kwa karibu kuhusu muda wa kufungua baa kwani muda huu wa sasa wa kufungua saa 10 jioni na kufunga saa tano ni mdogo ukilinganisha na ilipokuwa awali wa kufungua wakati wote" alisema Hussein.

  Hussein alisema nia ya serikali haikuwa mbaya ya kufungua baa saa 10 lakini hawakuangalia upande wa pili wa wamiliki wa baa hizo kwani wengi wao kwani katika muda huo wengi wao hawafanyi kabisa biashara.aliongeza kuwa wafanyabiashara hao wanahitaji kupata muda wa siku nzima wa kufanya biashara zao ili waweze kumudu kupata fedha za fedha za kulipa kodi ya serikali na mishahara ya wafanyakazi na wahudumu wa baa ambao ni wengi ambapo hivi sasa wanashindwa kufikia malengo.

  Alisema baadhi ya baa zimepunguza wahudumu wake kutokana na kubanwa na muda huo ambapo wahudumu wamekuwa wakiingia jioni tu baada ya muda wa asubuhi kupigwa marufuku na serikali."Wenye mabaa hivi sasa wapo katika changamoto kubwa ya biashara zao tunaiomba serikali kuangalia jambo hilo kwa sura nyingine ili kuinusuru biashara hiyo kuanzia mmiliki wa baa na viwanda vinavyotengeneza bidhaa hiyo na serikali yenyewe kupata kodi yake.

  Alisema kuwa changamoto hiyo waliibaini baada ya kuzitembea baa kadhaa jijini Dar es Salaam mapema mwezi huu ambapo walipata fursa ya kuzungumza na wamiliki wa baa na wahudumu wa baa hizo.Katibu wa chama hicho, Boniface Lameck alisema kutokana na kubanwa kwa muda wa kufungua baa kumepunguza ajira kwa wahudumu wa baa nyingi hapa nchini ambao ni wadau wao wakubwa wa viwanda vya bia na wamiliki wa baa.

  Alisema bila ya wahudumu wa baa biashara hiyo inakuwa inapoteza kundi muhimu la kuzifanya bia hizo kusambaa katika soko."Tunaiomba serikali kuruhusu baa kufunguliwa wakati wote kama ilivyokuwa zamani jambo litakalosaidia wenye mabaa kupata fedha za kulipa mishahara na kodi " alisema Lameck.

  Lameck aliongeza kuwa muda uliotengwa na serikali ni kama masaa saba tu kuanzia saa 10 hadi saa tano usiku na ndani ya muda huo wateja wengine wanaondoka kuanzia saa moja hadi saa tatu hivyo kuwa changamoto ya biashara hiyo.

older | 1 | .... | 1017 | 1018 | (Page 1019) | 1020 | 1021 | .... | 1897 | newer