Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46384 articles
Browse latest View live

RAIS DK. SHEIN AZUNGUMZA NA UONGOZI WA WIZARA YA AFYA

$
0
0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Afya  katika  kikao cha Mpango kazi wa mwaka 2016-2017   katika  utekelezaji wa  robo mwaka ya kwanza ya Julai-Septemba 2016 kilichofanyika leo  Ikulu Mjini Unguja,[Picha na Ikulu.] 21/10 /2016.
komb2
Waziri wa Afya Mhe,Mahmoud Thabit Kombo   akisoma   utekelezaji wa Mpango kazi wa mwaka 2016-2017 katika  kikao siku moja cha robo mwaka ya kwanza ya  Julai-Septemba 2016 kilichofanyika leo  Ikulu Mjini Unguja,chini ya mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein(hayupo pichani) (kushoto) Naibu Waziri wa Afya Mhe,Harusi Saidi Suleiman,[Picha na Ikulu.] 21/10 /2016.
komb3
Baadhi ya Viongozi wa Idara mbali mbali katika ya Wizara ya Afya   wakiwa katika  kikao siku moja cha Mpango kazi wa mwaka 2016-2017   katika  utekelezaji wa  robo mwaka ya kwanza ya  Julai-Septemba 2016 kilichofanyika leo   Ikulu Mjini Unguja,[Picha na Ikulu.] 21/10 /2016.
komb4
Viongozi katika Wizara ya Afya wakiwa katika  kikao siku moja cha Mpango kazi wa mwaka 2016-2017   katika  utekelezaji wa  robo mwaka ya kwanza ya  Julai-Septemba 2016 kilichofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja,chini ya mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,[Picha na Ikulu.] 21/10 /2016.
komb5
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Afya kuhusu utekelezaji waMpango kazi wa mwaka 2016-2017 katika  kikao siku moja cha robo mwaka ya kwanza ya  Julai-Septemba 2016 kilichofanyika leo  Ikulu Mjini Unguja,[Picha na Ikulu.] 21/10 /2016.
komb6
Baadhi ya Maafisa  wa Idara mbali mbali katika ya Wizara ya Afya   wakiwa katika  kikao siku moja cha Mpango kazi wa mwaka 2016-2017   katika  utekelezaji wa  robo mwaka ya kwanza ya  Julai-Septemba 2016 kilichofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja, [Picha na Ikulu.] 21/10 /2016.
komb7
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt.Juma Malik Akil (katikati) akitoa ufafanuzi wa vifungu wakati wa  kikao siku moja cha Mpango kazi wa mwaka 2016-2017   katika  utekelezaji wa  robo mwaka ya kwanza ya  Julai-Septemba 2016 kilichofanyika leo Ikulu Mjini Unguja,chini ya mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani),wengine (kulia)Mkurugenzi Mkuu wa Wizara ya Afya Dk.Jamala Adam Taib (kulia) na Mshauri wa Rais ushikiano wa Kimataifa,Fedha na Uchumi Ikulu Mhe,Balozi Mohamed Ramia Abdiwawa, [Picha na Ikulu.] 21/10 /2016.
komb8
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Afya kuhusu utekelezaji waMpango kazi wa mwaka 2016-2017 katika  kikao siku moja cha robo mwaka ya kwanza ya  Julai-Septemba 2016 kilichofanyika leo  Ikulu Mjini Unguja,[Picha na Ikulu.] 21/10 /2016. 

MUUGUZI HOSPITAL YA WILAYA YA CHUNYA MBEYA ATIWA MBALONI KWA KUDAIWA KUSABISHA KIFO CHA MTOTO MCHANGA

$
0
0

Mkuu wa Wilaya Chunya Rehema Madusa akiwa na majonzi baada ya kumsikia mama aliyepoteza mtoto wake mara baada ya kujifungua kutokana na uzembe wa muuguzi katika hospital ya Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya.

Mkuu wa Wilaya ya Chunya Rehema Madusa akizungumza na watumishi wa hospital ya Wilaya ya Chunya kufuatia tukio la mama mjamzito kifanyiwa vitendo vya unyanyasaji na mmoja wa watoa huduma hospitalini hapo hali iliyopelekea mtoto kupoteza maisha .
Mkuu wa Wilaya ya Chunya Rehema Madusa akimfariji Maria Solomoni ambaye alipoteza mtoto wake kwa uzembe wa muuguzi katika katika hospital ya Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya.
Patricia Kisoti Muuguzi anayetuhumiwa kufanya uzembe uliosababisha Mama mjamzito kujifungua na mtoto wake kupoteza maisha katika hospital ya Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya. 

Baadhi ya watumishi wa hospital ya Wilaya ya Chunya katika Mkutano na Mkuu wa Wilya y chunya mara baada ya kutokea tukio la mama mjamzito aliyepoteza mtoto wakati akijifungua kutokana na uzembe wa mmoja wa wauguzi hospitalini hapo.

Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo ya Wilaya ya Chunya, Sasita Shabani akizungumza kuhusiana na tukio hilo la kufanyiwa ukatili kwa mama mjamzito na mmoja wa wauguzi .
Wananchi na wanaopata huduma za afya katika Hospita ya Wilaya Chunya wakionesha nyuso za majonzi mara baada ya mmoja wa wananchi kufanyiwa vitendo vya kikatili.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Chunya, Sophia Kumbuli akisisitiza jambo kuhusiana na tukio hilo.
Wananchi na wanaopata huduma za afya katika Hospita ya Wilaya Chunya wakionesha nyuso za majonzi mara baada ya mmoja wa wananchi kufanyiwa vitendo vya kikatili.


Na JamiiMojaBlog

Jeshi la Polisi Wilayani Chunya Mkoani Mbeya linamshikilia muuguzi wa afya katika hospitali ya Wilaya ya Chunya, Patricia Kisoti, kwa kutokana na uzembe uliopekekea mama mjamzito kujifungua mtoto akiwa amekufa.

Akizungumzia tukio la kukamatwa kwa muuguzi huyo Mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Chunya Rehema Madusa amesema kitendo kilicho fanywa na muuguzi huyo nichakinyama na kimetia aibu sekta ya afya.

Amesema September 4, mwaka huu katika hospitali ya Wilaya ya Chunya, mjamzito huyo akiwa ameongozana na mwenzake walifika kituoni hapo usiku, wakihitaji huduma ya haraka kutokana na hali ya mgonjwa kuwa mbaya.

Amesema licha ya mama huyo kufika akiwa katika hali mbaya alijitahidi kujieleza ili apate huduma kwa waaguzi waliokuwa zamu akiwemo mtuhumiwa huyo Patricia Kisoti ambaye ndiye aliyetakiwa kumhudumia mgonjwa huyo lakini alishindwa kutoa ushirikiano badala yake alitoa majibu ya kejeli na kushindwa msaada wowote.

Amesema kama mama huyo angemshughulikiwa kwa haraka ikiwa na muuguzi huyo kutoa taarifa kwa ngazi za juu baada ya kuona tatizo hilo haliwezi, basi mtoto huyo angekuwa hai.

Aidha, Mkuu huyo alimtaka Mkurugenzi wa Halmashauri ya Chunya, Sophia Kumbuli kuhakikisha anachukua hatua za kinidhamu kwa wahusika wote.Amesem kifo cha kichanga hicho, kwa asilimia kubwa kilitokana na uzembe wa muuguzi huyo kutokana na maalezo yaliyotelewa mgonjwa huyo.

Akizungumzia sakata hilo, Maria Solomoni, amesema siku hiyo, yeye akiwa ameongozana na mwenzake aliyemtambulisha kuwa alikuwa ni wifi yake, walifika katika kituo hicho cha afya majira ya usiku, huku akiwa ameshikwa na uchungu, ambapo waligonga mlango wa chumba cha nesi ambao kwa muda huo ulikuwa umefungwa.

Maria, aliendelea kufafanua kuwa aliendelea kuteseka na mates ohayo mpka majira ya saa kumi namoja alifajili ndipo alipoona wanaume wawili wakimuhangaikia na kumuingiza katika chumba cha upasuaji na kufanyiwa oparesheni.

Naye Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo ya Wilaya ya Chunya, Sasita Shabani, alikiri kutokea kwa tukio hilo kituoni hapo na kwamba katika uchunguzi wao wa awali umebaini kwamba katika tukio lililomkuta Maria Solomoni, ndani yake kulikuwa na uzembe.

Ziara ya Mfalme wa Moroko ni Fursa kwa Wafanyabiashara

$
0
0
Immaculata Makilika- MAELEZO

Moroco ni nchi iliyopo Kaskazini Magharibi mwa Afrika, ambayo imepakana na bahari za Atlantiki na Mediteraniani, na upande wa bara imepakana na nchi za Algeria, Mauritania.mpaka wa kusini unatajwa kuwa Sahara Magharibi.

Nchi ya Moroko inakadiriwa kuwa na eneo la Km2 446,550, huku sehemu kubwa ikiwa ni jangwa la Sahara na watu wengi nchini humo huishi kwenye sehemu zilizo na rutuba hasa karibu na maeneo ya pwani.

Nchi hiyo ina milima inayofunika eneo kubwa, ikiwemo milima ya Atlas ambayo ipo katikati ya nchi hiyo kutoka kusini magharibi kuelekea upande wa kaskazini mashariki na mji mkuu wake ukiwa ni Rabat wenye wakazi milioni 2, aidha mji mkubwa ni Casablanka.

Nchi ya Moroco ilipata uhuru wake mwaka 1956 kutoka kwa nchi za Ufaransa na Hispania zilizokuwa zikiitawala, na kikatiba inaongozwa na Mfalme, kwa sasa inaongozwa na mfalme anayeitwa Mohammed wa VI, na Waziri Mkuu ni Abdelilah Benkirane. Watu wa Moroko hutumia lugha rasmi za kiarabu na kiberiberi. Fedha yao inajulikana kama Dirham, zaidi ya 90% ya watu wake ni waislamu. Uchumi wa Moroco unategemea zaidi utalii, sekta ya mawasiliano, viwanda vya nguo pamoja na kilimo.

Hivi karibuni, kwa mara ya kwanza tunashuhudia ziara ya Mfalme wa Moroco Mohammed wa VI aliyewasili nchini wiki hii kwa ziara ya siku tatu hadi Oktoba 25 mwaka huu. Ujio wa Mfalme huyo wa Moroko unaidhihirishia dunia kwa kiasi gani diplomasia ya Tanzania imeendelea kukua kwa kasi, ikiwa ni sambamba na kukuza diplomasia ya uchumi.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Augustine Mahiga anasema kuwa lengo la ziara hiyo ni kukuza uhusiano wa kati ya Tanzania na Moroco hususani katika masuala ya uchumi na biashara kwa faida ya watu wa nchi hizi mbili. “ Ziara hii imejikita zaidi katika kukuza ushirikiano wa kiuchumi na biashara, ikizingatiwa kuwa nchi ya Moroco imefanikiwa katika nyanja mbalimbali kama vile miundombinu, afya, madini na ulinzi”.

“Vile vile wafanyabiashara kutoka Moroko watafanya mazungumzo na wa hapa nchini kwa lengo la kubadilishana uzoefu na ni hatua nzuri itakayoweza itakuza uhusiano wetu pamoja na kuchochea maendeleo ya kiuchumi” anasema Balozi Mahiga. Maroko imepiga hatua katika sekta mbalimbali ikiwemo utalii, uvuvi ,viwanda, kilimo na madini.

Mambo yaliyopo katika mpango huo ni pamoja na maboresho ya reli, na barabara, kuboresha viwanja vya ndege kwa viwango vya kimataifa ikiwa ni pamoja na kuongeza idadi ya ndege zinazoingia Moroco. Sambamba na hilo bandari maarufu zimeandaa utaratibu wa safari za kitalii.

Vitu na Maeneo mbalimbali yamekuwa sehemu ya kuvutia utalii kutoka nchi za Ujerumani, Ufaransa, na Hispania, ambapo huvutiwa na fukwe za bahari,milima ya Atlas, pamoja na miji maarufu ya kama ya Tangie, Marrakech, Casablanka na Tarfaya. Sekta ya madini ni sekta muhimu kwa vile inachangia uchumi wa nchi kwa asilimia 6 ya pato la ndani la taifa na asilimia 35 ya pato la kigeni kwa nchi ya Moroco.

Ili kukuza sekta ya utalii nchini humo, matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) yameimarishwa na kuweza kutangaza vivutio mbalimbali kwa kuhususha sekta binafsi katika kutangaza utalii wa ndani, na kati ya nchi zilizofanikiwa katika hilo ni pamoja na nchi ya Malaysia ambapo mwaka 2011 ilipata watalii milioni 24.7 na mwaka 2012 ilipata watalii milioni 25 kutokana na matumizi ya TEHAMA.

Jitihada mbalimbali zimefanyika katika kusaidia sekta ya utalii nchini kukua na kuchangia zaidi pato la taifa, ambapo kupitia maboresho kuongeza ndege zenye safari ya moja kwa moja hadi nchini, na kuboresha miundombinu ya barabara sekta hiyo imeweza kupata mafanikio.

Tanzania na Uswisi zasaini Mkataba wa Makubaliano kuhusu ushirikiano wa kisheria kwenye masuala ya Jinai

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Augustine Mahiga (Mb.) kwa pamoja na Mhe. Florence Tinguely Mattli, Balozi wa Uswisi hapa nchini wakisaini Mkataba wa Makubaliano kati ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Uswisi kuhusu Ushirikiano wa Kisheria kwenye masuala ya Jinai. Mkataba huu utasaidia kuzijengea uwezo mamlaka zinazohusika na masuala ya Jinai na pia kubadilishana taarifa kuhusu masuala hayo. 
Mhe. Mahiga na Mhe. Mattli wakiendelea na zoezi la kusaini huku Maafisa kutoka Wizarani na Ubalozini wakishuhudia. Kulia aliyesimama ni Bw. John Pangipita, Afisa Mambo ya Nje na Bi. Sheila Ally.  
Dkt. Mahiga pamoja na Balozi Mattli wakibadilishana Mkataba mara baada ya kumaliza kuweka saini.
 
Tukio hilo pia lilishuhudiwa na Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria, Balozi Baraka Luvanda (wa kwanza kushoto), Mkurugenzi wa Idara ya Amerika na Ulaya, Balozi Joseph Sokoine (wa pili kutoka kushoto), Katibu wa Waziri, Bw. Gerald Mbwafu na Bw. Pangipita (wa pili kutoka kulia).

BAADA YA TAMKO LA SERIKALI WATUMISHI WAFURIKA VITUO VYA USAJILI

$
0
0
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira akipokea ripoti ya utekelezaji wa zoezi la Usajili watumishi wa Umma toka kwa Afisa Usajili mkoa wa Dodoma Bwana Khalid Mrisho. 

Afisa Utawala Bi. Salma Mohamed toka ofisi ya Wakala wa Geolojia (GST) akihakiki orodha ya watumishi wake ambao hawajasajiliwa Vitambulisho vya Taifa, kufuatia agizo la Serikali la kila mtumishi wa Umma kuwa amesajiliwa kufikia Oktoba 31, 2016. Pembeni ni Bi.Rehema Kionaumela Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Uratibu Wilaya NIDA 

Afisa Usajili NIDA Bw. Devis Lubago, akimsajili na kuchukua alama za kibaiolojia mtumishi wa Umma aliyefika ofisi za NIDA Dodoma kukamilisha usajili. 

Mmoja wa Watumishi wa Umma akichukuliwa alama za vidole wakati wa zoezi la usajili Watumishi wa Umma linaloendelea mkoani Dodoma. 


Baadhi ya watumishi wa Umma wakisubiri kupata huduma ya usajli kwenye ofisi ya NIDA, jengo la Hazina mkoani Dodoma 

Afisa Usajili Bi. Lucina Ramadhani akikagua taarifa za mtumishi kabla ya kuanza kuingiza taarifa zake kwenye mfumo 

Bi. Aziza Konyo mmoja wa watumishi wa Umma akichukuliwa alama za vidole alipofika kusajiliwa katika zoezi linaloendelea nchi nzima la kusajili Watumishi wa Umma. 

Watumishi wa Umma mkoani Dodoma wamefurika katika vituo vya usajili kufuatia tamko la Serikali la kuongeza muda wa usajili Vitambulisho vya Taifa kufikia Oktoba 31, 2016 ambapo mfanyakazi au mwajiri ambaye atashindwa kutekeleza agizo hilo hatua stahiki zitachukuliwa dhidi yake; tamko lililotolewa na Waziri ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora alipokutana na vyombo vya habari hivi karibuni. 

Watumishi waliojitokeza katika vituo wameonekana kuwa tayari wamejaza fomu za maombi ya Vitambulisho vya Taifa wakiwa wamejipanga kupigwa picha. 

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi amekuwa miongoni mwa viongozi waliotembelea moja wapo ya vituo vya usajili mkoani Dodoma; kushuhudia namna shughuli za usajili zinavyofanyika na kupata taarifa ya mpango wa utekelezaji zoezi hilo ilivyopangwa na mkoa husika, katika kuhakikisha zoezi hilo linakamilika kwa wakati na kila mtumishi anasajiliwa na kuchukuliwa alama za Vidole, saini ya kielektroniki na picha. 

Zoezi la Usajili Watumishi wa Umma linaenda sambamba na kuanza kwa uhakiki wa taarifa za uraia wa waombaji wote walioomba kupatiwa Vitambulisho vya Taifa. 

Tayari mikoa ambayo usajili umekamilika, zoezi la uhakiki wa taarifa na mapingamizi linaanza mara moja ili vitambulisho kuanza kuzalishwa.

UONGOZI HANDENI WAPIGA MARUFUKU UFUGAJI HOLELA

$
0
0

Mkuu wa Wilaya Mh. Godwin Gondwe akizungumza na wannchi wa kijiji cha Chogo  wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Mtendaji Bw. William Makufwe akifutiwa na Mh.Aabdalla Pendeza Diwani wa Kata ya Kabuku Ndani na wa kwanza kushoto ni Mwenyekiti wa kijiji cha chogo.
 Mkuu wa Wilaya ,Mkurugenzi Mtendaji na viongozi wengine kutoka Halmashauri wakitazama moja ya eneo laKitalu cha kuoteshea miti ya malimao mkulima baada ya kupitia shamba na kuona uharibifu uliofanyika.

baadhi ya wananchi kijiji cha Chogo Kata ya Kabuku ndani. 
 Mkurugenzi mtendaji halmashauri ya wilaya ya handeni akizungumza na wananchi wa kijiji cha Chogo kata ya Kabuku Ndani.
 Mmoja kati ya wafugaji waliopo katika kijiji cha ChogoBw. Masanja akifafanua jambo kwa Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi na  wananchi wote kwa ujumla.


 ======  =======  ========
Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mh. Godwin Gondwe  na Mkurugnzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Bw. William Makufwe wamepiga marufuku ufugaji holela. Tamko hilo limetolewa baada ya uongozi wa kijiji cha Chogo Kata ya Kabuku Ndani kuomba Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi Mtendaji kuwasaidia kuondoa wafugaji waliovamia katika kijiji chao na kuharibu mazao ya kilimo ya wananchi wa kijiji hicho.

Akizungumza na wananchi hao Mkuu wa wilaya aliwaeleza wananchi kuwa kila sehemu kuna taratibu na sheria zake namna ya kuishi. “ni marufuku kuchunga mifugo kwenye maeneo ya hifadhi ya misitu ya Serikali au ya Kijiji kwa maana  ni kosa akipatikana mtu wa namna hiyo kamateni peleka polisi na mimi nifahamu”alisema, na pia ni marufuku kuchukua mifugo kwenda kuchunga kwenye shamba  la mwenzako kuwepo na  mazao au  hakuna ni kosa kamateni mtu wa namna hiyo  peleka polisi, hata kama mwenye shamba amekwisha vuna isipokuwa kwa idhini ya mwenye shamba pekeyake.

Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni aliwaeleza wananchi  kwamba ulinzi wa mali za Chogo  ni wanachogo wenyewe, na mgogoro wa wakulima na wafugaji ni wetu sote, Aliwaeleza kwamba walishindwa kuchukua tahadhari mapema pindi wafugaji hao walipoingia miezi mine iliyopita kwa sababu eneo lao lina mpango bora wa matumizi ya ardhi. 

Aidha aliwaeleza wananchi kuwa, amewataka  Watendaji wa Kata na Vijiji kuleta orodha ya mifugo iliyopo kwenye maeneo yao na waeleze uwezo wa ardhi iliyopo kuweza kuhimili idadi ya mifugo iliyopo kwa mujibu wa mpango wa ardhi uliowekwa katika maeneo yao ili kugungua  kama kunamifugo imezidi au haijazidi, “Tarehe 29/10/2016 nitapata orodha ya Halmashauri nzima kwa kata 21 na  Vijiji 91” alisema. 

Mfugaji wa mwanzo ambae atakuwepo katika kijiji husika kwa kumkaribisha ama la kama idadi ya mifugo aliyokuwa nayo inakidhi viwango atabaki, lakini kwa mfugaji atakaye zidisha kiwango cha mifugo basi ataondolewa ili aende  kutafuta mahali kwingine na marufuku kukaribisha mfugaji mwingine alisema Mkurugenzi.

Mwenyekiti wa kijiji cha Chogo aliwaeleza viongozi kuwa wafugaji hao waliingia kwenye maeneo yao bila kufuata utaratibu, wameleta uharibifu wa mazao napindi wanapohitajika kwenye vikao ili wapewe utaratibu wanakaidi kufika. Alieleza kuwa eneo ambalo limetengwa kaajili ya mifugo lipo eneo la Chang’ombe na kwa mujibu wa idadi ya mifugo iliyopo tayari imejitosheleza. Mifugo iliyovamia ni zaidi ya 4000 na kwamba ardhi ya kijiji haiwezi kutunza idadi kubwa ya mifugo.

Bw. Said Mmbelwa mwanakijiji wa Chogo kitongoji cha Kibamba aliwaeleza wananchi wenzake kuwa walifanya makosa kuwakaribisha wafugaji hao bila kufuata utaratibu na kwamba kama wananchi weneyewe wasipobadilika basi migogoro ya wakulima na wafugaji haitakwisha.

Aidha Diwani wa kabuki ndani  Mh. Abdallah Pendeza aliwashukuru Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi Mtendaji na Kuwataka wananchi kutekeleza yale ambayo viongozi wamewaelekeza kwa kushirikiana, kwamba kila mmoja atimize wajibu wake kulingana na sheria, taratibu na kanuni.

Mkuu wa Wilaya aliwataka viongozi wa vijiji kuhuisha kamati za ulinzi na usalama na kuhakikisha wanaripoti kwenye vyombo vya sheria pindi wanapoona kunamtu ameingia kwenye maeneo yao haeleweki ili kulinda amani.

Imetolewa na
Alda Sadango
Afisa Habari
Halamshauri ya Wilaya Handeni

WALIBYA WASAIDIA MRADI WA MAJI

$
0
0
Mkurugenzi wa Taasisi ya World Islamic Call Society ya Libya tawi la Tanzania Ammara Zaiyani kulia aliyeshika ndoo ya maji baada ya kumtwisha ndoo ya maji Saida Ally mkazi wa Kijiji cha Binga-Kisiju kata ya Dondo wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani, kushoto kadhi mkuu wa mkoa wa Pwani Sheikh Hamis Mtupa (Picha na John Gagarini).
Mkurugenzi wa Taasisi ya World Islamic Call Society ya Libya tawi la Tanzania Ammara Zaiyani akifungua bomba la maji baada ya uzinduzi wa kisima cha maji kwenye Kijiji cha Binga-Kisiju wilayani Mkuranga mkoani Pwani kushoto kwake ni mwakililishi wa balozi wa Libya Mohamed Atoumi
Mkurugenzi wa Taasisi ya World Islamic Call Society ya Libya tawi la Tanzania Ammara Zaiyani katikati akielezea jambo kulia ni kadhi mkuu wa mkoa wa Pwani Sheikh Hamis Mtupa na kushoto ni mwakililishi wa balozi wa Libya Mohamed Atoumi wakati wa uzinduzi wa mradi wa maji kwenye Kijiji cha Binga Kisiju- kata ya Dondo wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani Picha na (John Gagarini)



Na John Gagarini, Mkuranga

WANANCHI wametakiwa kuwa na utamaduni wa kulipa kodi mbalimbali za serikali ili ziweze kutumika kwa ajili ya maendeleo kama wanavyofanya wananchi wa Libya.

Hayo yalisemwa wilayani Mkuranga na mkurugenzi wa Taasisi ya World Islamic Call Society iliyopo chini ya ubalozi wa Libya hapa nchini Ammara Zaiyani wakati akikabidhi mradi wa kisima cha maji kwenye Kijiji cha Binga–Kisiju.Zaiyani alisema kuwa fedha ambazo zimesaidia ujenzi wa kisima hicho cha maji ya kunywa chenye thamani ya shilingi milioni 18 zimetokana na kodi za wananchi wa Libya kwa ajili ya kusaidia watu wenye changamoto mbalimbali za kimaendeleo.

“Wananchi wa Libya wanajitolea kuwasaidia wenzao hivyo na nyie mnapaswa kuwa na utamaduni wa kuwasaidia wengine kupitia kwenye malipo mbalimbali ya serikali yenu ambayo ina sema hapa Kazi Tu,” alisema Zaiyani.Naye mwakilishi wa Ubalozi wa Libya hapa nchini Mohamed Atoumi alisema kuwa serikali ya Libya kupitia taasisi hiyo imekuwa ikipokea maombi mbalimbali na imekuwa ikisaidia kadiri ya uwezo unapokuwepo.

Atoumi alisema kuwa wamekuwa wakisaidia kwenye sekta mbalimbali ikiwa ni pamoja kwenye huduma za afya, maji na shughuli nyingine za maendeleo lengo likiwa ni kudumisha ushirikiano uliopo na Tanzania.

Kwa upande wake kadhi mkuu wa mkoa wa Pwani Sheikh Hamis Mtupa alisema kuwa wanashukuru kwa msaada huo kwani umesaidia kuwaondolea adha wananchi wa Kijiji hicho ambao walikuwa wakishinda wakitafuta maji ambayo siyo safi wala salama.

Mtupa alisema kuwa wananchi wanapaswa kulinda miundombinu ya kisima hicho ili isiharibike kwani maji hayo ni kwa wananchi wote bila ya kujali dini ya mtu na ni huduma muhimu kwa binadamu.Naye mkazi wa kijiji hicho Mwanahawa Maulid alisema kuwa wamekuwa wakihangaika kutafuta maji ambayo yanapatikana mbali na wamekuwa wakitumia muda mwingi kusubiria maji.

Maulid alisema kuwa maji waliyokuwa wakiyatumia ni ya kuchimba chini ambayo si salama kiafya na yamekuwa wakiwasababishia magonjwa mbalimbali kama vile kuhara na UTI.

Rais Magufuli aagiza bodi ya Mikopo kuongeza kasi ya ukusanyaji wa madeni.

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Magufuli ameagiza Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu kutumia Sheria zilizopo kuongeza kasi ya ukusanyaji wa madeni kwa wahitimu walionufaika na mikopo.

Rais Magufuli ametoa agizo hilo leo jijini Dar es salaam wakati akiweka jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa hosteli za wanachuo katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam unajengwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) kwa gharama ya shilingi bilioni 10.

Amesema kuwa Serikali inadai takribani shilingi trilioni 2.6 kwa wahitimu walionufaika na mikopo ya Elimu ya juu.“Serikali inawadai wahitimu walionufaika na mikopo ya Elimu ya juu takribani shilingi trillion 2.6 ambazo wanatakiwa kuzirudisha ili ziweze kutolewa kama mikopo kwa wanafunzi wapya na waliopo vyuoni” alifafanua Dkt Magufuli.

Aidha Dkt. Magufuli ameitaka Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi kusimamia ipasavyo suala la utoaji wa mikopo kwa wanafunzi kwa kuzingatia vigezo vilivyopo kwani lengo la mikopo hiyo inawalenga watoto maskini.

Alisema kuwa kumekuwa na baadhi ya malalamiko ya kuwa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu inafanya zoezi la ugawaji wa mikopo hiyo kwa upendeleo hivyo kuzitaka uongozi wa Wizara kushughulikia suala hilo.Mbali na hayo Rais Magufuli amewataka wanufaika wa mikopo hiyo kutimia mikopo hilo kwa malengo mazuri katika kujinufaisha na masuala ya Elimu.

Naye Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Prof. Joyce Ndalichako alisema kuwa mradi wa ujenzi wa hosteli hizo utasaidia kuwahudumia wanafunzi 3,840 ambapo unatarajiwa kuisha mwishoni mwa mwezi Desemba 2016.Katika hatua hiyo Prof. Ndalichako alisema kuwa wanafunzi waliodahuiliwa kwa mwaka huu wapo 58,000 hivyo suala la wanafunzi 66,000 kukosa mikopo hiyo ni upotoshaji unaofanya na baadhi wa watu.

Mradi wa Ujenzi wa Hosteli za wanachuo katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wenye majengo 20 kila jengo gorofa nne zenye vyumba 12 unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa Desemba mwaka huu.

DC BUKOMBE ATOA SEMINA ELEKEZI KWA WAKUU WA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI

JARIDA LA OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU LA MWEZI SEPTEMBA, 2016

TANZANIA SETS TO PARTICIPATE IN 2016 WORLD TRAVEL MARTKET

VYUO VYA HABARI VIJIANDAE KUTOA ELIMU BORA ILI KUENDANA NA MABADILIKO YATAKAYOLETWA NA SHERIA YA HUDUMA ZA HABARI.

$
0
0

Mapema Septemba 2016 kwa mara ya kwanza Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye aliwasilisha kwa mara ya kwanza Bungeni Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari na kuanza kujadiliwa na kutolewa maoni kutoka kwa wadau mbalimbali wa Habari nchini.

Kwa sasa Muswada huu unaendelea kujadiliwa na kuchambuliwa na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii chini ya Mwenyekiti wake Mhe. Peter Serukamba na baada ya mchakato huo kukamilka utapelekwa kwa ajili kuanza kujadiliwa na wabinge.

Sasa hoja yangu naielekeza katika kuangalia Muswada huu hasa katika sehemu ya Tatu (c) Uthibitishwaji wa wanahabari kifungu cha 18 (1) na (2) vinaelezea kuwa Mtu hataruhusiwa kufanya kazi za uandishi wa habari isipokuwa kama mtu amethibitishwa na Sheria hii na (2) inasema mtu ambaye anakusudia kufanya kazi ya uandishi wa habari ataomba kuthibitishwa na Bodi kwa utaratibu wa maombi utakaoainishwa katika kanuni.

Ukisoma kifungu hiki na sehemu zake zote utaona kuwa lazima kutakuwa na vigezo ambavyo mwandishi wa habari atapaswa kuwa navyo ili Bodi iweze kumthibitisha kuwa mwandishi wa habari kamili na baadae kumpatia Press Card.

Tukiangali kwa mifano tu ya taaluma ambazo watu wake wanapata udhititisho kutoka kwa Bodi zao utaona kuwa hata vigezo vyenye ngazi fulani ya kitaaluma na kwa mfano wanasheria ili kudhititishwa kuwa mwanasheria na kupata mhuri wa kuwa Wakili unabidi uwe na Shahada ya Kwanza ya Sheria na kufanya baadhi ya mitihani ya kufuzu ili kudhitishwa.

Kwa waandishi wa Habari pia tutegemee kuwepo kwa vigezo na masharti ambayo kwa vitahitaji kuongeza elimu tulizonazo katia fani yetu na pia hili litasababisha sasa vyuo vya uandishi wa habari na mawasiliano kutoa elimu iliyo bora zaidi ili kuendana na mabadiliko haya.

Tumeshudia uwepo wa vyuo vya uandishi wa habari kila sehemu hata vingine ukiangalia mazingira yake lazima utilie shaka kama vinatoa ile elimu inayostahili na iliyodhibitishwa na mamlaka zilizopo za TCU na NACTE. 
Niwaombe tu wahusika katika vyuo vya uandishi wa habari kuzingatia vigezo na masharti ya utoaji wa elimu ya Habari na Mawasiliano katika vyuo vyao kwani kuja kwa Sheria ya Huduma za Habari ni mwanzo wa kuifanya taaluma ya habari kuwa taalum inayoheshima na kuwa taaluma inayoheshimika sana na sio rahisi kuipata kama sasa watu wanavofikiria tu ukitaka kuwa mwandishi wa habari unaweza kusoma miezi mitatu hivi basi umekuwa mwandishi wa habari.

Ingawa kuna baadhi watu wanasema wanatumia vipaji vyao vya uandishi wa habari na utangazaji lakini tujue kuwa kipaji bila ya kuendelezwa ni kazi bure tunahitaji kuviendeleza vipaji hivyo kwa kupata elimu na ujuzi zaidi wa fani ya habari ili kuendana na mabadiliko ya teknlolojia na Sheria za nchini.

WAZIRI KAIRUKI AMALIZA ZIARA YA SIKU 2, KUWATEMBELEA, KUWASIKILIZA NA KUZUNGUMZA NA WANUFAIKA TASAF WA MANISPAA ZA KINONDONI NA TEMEKE JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah Kairuki, akizungumza na wanufaika wa Tasaf pamoja na wananchi wa Kata ya Sandali, ambao kaya zao bado hazijaingizwa katika mpango huo. 
Baadhi ya watendaji wa Mkoa na waratibu wa Tasaf wa Manispaa ya Temeke wakiwa katika mkutano huo, wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah Kairuki, wakati alipokuwa akizungumza na wanufaika wa Tasaf pamoja na wananchi ambao kaya zao bado hazijaingizwa katika mpango huo. 
Baadhi ya waratibu wa Tasaf wa Manispaa ya Temeke wakiwa katika mkutano huo. 
Mmoja wa wanufaika wa Tasaf, akimpatia zawadi ya kitenge Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah Kairuki (kulia), baada ya kuzitumia fedha za ruzuku anazopewa na Tasaf katika mradi wa kutengeneza bidhaa hizo. 
Naibu Meya wa Manispaa ya Temeke, Feysal Salum, akizungumza na wanufaika pamoja na wananchi ambao hawajanufaika na Tasaf, wakati wa mkutano huo, Mtaa wa Mamboleo, Kata ya Sandali jijini Dar es Saaam.
Diwani wa Kata ya Mtoni, Benard Mwakyembe, akitoa maelezo kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah Kairuki, alipofika na kufanya mkutano na wanufaika wa Tasaf pamoja na wananchi ambao bado hawajaingizwa katika mpango huo, maeneo ya Shule ya Msingi Mtoni, jijini Dar es Salaam jana.
Baadhi ya wanufaika wa Tasaf katika mpango wa Serikali wa kuzinusuru kaya masikini pamoja na wananchi ambao bado hawajaingizwa katika mpango huo wa maeneo ya Kata ya Mtoni, Temeke jijini Dar es Salaam jana, wakisikiliza masuala mbalimbali yaliyokuwa yakielezwa katika mkutano huo.
Mkurugenzi wa Uratibu wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (Tasaf), Alphonce Kyariga, akitoa ufafanuzi katika kuwapa ufahamu wanufaika wa Tasaf pamoja na wananchi wa maeneo hayo ya Kata ya Mtoni, ambao bado hawajaingizwa katika mpango huo wa kunusuru kaya masikini. Kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah Kairuki.
Mmoja wa wananchi wa Kata ya Mtoni, ambaye bado kaya yake haijaingizwa katika mpango huo, Rajab Bakari, akitoa malalamiko yake kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah Kairuki kuhusu kutokufikiwa na mpango huo, ilhali akiwa ni mmoja wa watu wanaostahiki kupata ruzuku hiyo.
Mwananchi wa Kata ya Mtoni, ambaye bado kaya yake haijaingizwa katika mpango huo, Uwesu Thabiti, akitoa malalamiko yake kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah Kairuki kuhusu kutokufikiwa na mpango huo, ilhali akiwa ni mmoja wa watu wanaostahiki kupata ruzuku hiyo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah Kairuki, akipokewa na Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Felix Lyaniva, alipowasili Ofisi za mkuu huyo jana kwa ajili ya kuhitimisha ziara yake ya siku mbili kuwatembelea, kuwasikiliza na kuzungumza na wanufaika hao wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (Tasaf ) wa Manispaa za Kinondoni na Temeke jijini Dar es Salaam. 
Baadhi ya wanufaika wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (Tasaf ) na wakazi wa maeneo ya Sandali, wakiwa katika mkutano na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah Kairuki, kwenye Mtaa wa Mamboleo, Manispaa ya Temeke, jijini Dar es Salaam jana. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Diwani wa Kata ya Sandali, Temeke jijini, Abel Tarimo, akitoa maelezo kuhusu masuala mbalimbali kwenye mtaa wake huo, kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah Kairuki, alipokuwa na mkutano na wanufaika wa Tasaf pamoja na wakazi wa maeneo hayo jana.
Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Felix Lyaniva, akizungumza kabla ya kumkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah Kairuki (kulia), kuzungumza na wanufaika wa Tasaf pamoja na wananchi ambao kaya zao hazijaingizwa katika mpango huo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke, Nasib Mbaga.
 

Rais Mstaafu BENJAMINI MKAPA azindua Filamu ya Utalii NshabaOntwale Nyakijoga "Nipeleke Nyakijoga"

$
0
0

Mgeni rasmi Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Benjamini William Mkapa, akitoa neno kwa Wageni waalikwa kwenye Jioni ya Bwanjai, kabla ya kuzindua rasmi filamu ya NshabaOntwale Nyakijoga ' Nipeleke Nyakijoga ' Uzinduzi wa filamu hiyo ya utalii ulifanyika, katika Ukumbi wa Kardinali Rugambwa Social Centre, Oysterbay Jijini Dar es Salaam.
Mgeni rasmi wa Jioni ya Bwanjai Rais Mstaafu Benjamini William Mkapa, akikabidhiwa filamu ya NshabaOntwale Nyakijoga ' Nipeleke Nyakijoga ' na Mrs Dorina Kilama tayari kwa ajili ya Uzinduzi huo, anayeshuhudia katikati ni Profesa Wenceslaus Kilama, uzinduzi wa filamu hii ya Utalii umefanyika Oktoba 21, 2016 katika ukumbi wa Kardinali Rugambwa Social Centre, Oysterbay Jijini Dar es Salaam.
Mgeni rasmi Rais Mstaafu Benjamini William Mkapa, akikabidhi CD yenye filamu hiyo ' Nipeleke Nyakijoga ' ndugu Salum Salum ambae ni mwakilishi wa DSTV, ikiwa ni ishara ya kutambua mchango wa kampuni hiyo ambayo ilikuwa miongoni mwa wadhamini wa Usiku wa Bwanjai, Uzinduzi wa filamu hii ya Utalii umefanyika Oktoba 21, 2016 katika ukumbi wa Kardinali Rugambwa Social Centre, Oysterbay Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya waalikwa katika Uzinduzi wa filamu hiyo ya NshabaOntwale Nyakijoga ' Nipeleke Nyakijoga ' Uzinduzi wa filamu hii ya Utalii umefanyika Oktoba 21, 2016 katika ukumbi wa Kardinali Rugambwa Social Centre, Oysterbay Jijini Dar es Salaam.
Kikundi cha Ngoma kutoka Kantare, Bwanjai kikitoa Burudani maridhawa wakati wa Uzinduzi wa filamu ya NshabaOntwale Nyakijoga ' Nipeleke Nyakijoga ' Uzinduzi wa filamu hii ya Utalii umefanyika Oktoba 21, 2016 katika ukumbi wa Kardinali Rugambwa Social Centre, Oysterbay Jijini Dar es Salaam.


kwa hisani ya www.habari360.com

MAPOKEZI YA B.G MALISA MKOANI ARUSHA LEO OKTOBA 22,2016

$
0
0
Kiongozi mkuu wa kanisa la Ukombozi ,Nabii B.G Malisa akizungumza na waandishi wa habari mara baada tu ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro(KIA) leo ambapo atakuwa na mkutano wa maombezi wa siku 8 katika viwanja vya reli jijini Arusha.
Nabii B.G Malisa akitia sahihi katika kitabu cha wageni ndani ya uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro(KIA) mara baada ya kuwasili akitokea jijini Dar es salaam ambapo atakuwa na mkutano wa maombezi wa siku 8 katika viwanja vya reli jijini Arusha.
Nabii B.G Malisa akipokea zawadi ya maua mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro(KIA) leo ambapo atakuwa na mkutano wa maombezi wa siku 8 jijini Arusha katika viwanja vya reli.
Nabii B.G Malisa akipokea zawadi ya maua mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro(KIA) leo ambapo atakuwa na mkutano wa maombezi wa siku 8 jijini Arusha katika viwanja vya reli.
Umati wa wakazi wa mkoa wa Arusha waliofurika katika uwanja wa ndege wa kimatifa wa Kilimanjaro(KIA) kumpokea Nabii B.G Malisa ambaye atakuwa na mkutano wa maombezi wa siku 8 katika viwanja vya reli jijini Arusha.
Nabii B.G Malisa akiwa nje ya chumba cha mapokezi ya wageni mashuhuri(VIP) katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA)mara baada ya kuwasili leo mkoani Arusha,pembeni yake kushoto ni mchungaji wa kanisa la Ukombozi tawi la Arusha ,Mwana wa Nabii mchungaji Ushindi na mkewe Grace Ushindi wa tatu kutoka kulia waliosimama.(picha na Moses Mashalla)

YANGA WAWAADHIBU KAGERA SUGAR BAO 6-2 KWENYE UWANJA WA KAITABA MJINI BUKOBA LEO.

$
0
0


Yanga leo wameichakaza Kagera Sugar 6-2 kwenye Mechi ya VPL, Ligi Kuu Vodacom, ilityochezwa huko Uwanja wa Kaitaba, Bukoba na kuchupa hadi Nafasi ya Pili. 

Kagera Sugar ndio waliotangulia kupata Bao katika Dakika ya 3 Mfungaji akiwa Mbaraka Yusuf na Yanga kusawazisha Dakika ya 4 kupitia Straika wao kutoka Zimbabwe Donald Ngoma. 

Yanga walipa Bao la Pili Dakika 21 kupitia Simon Msuva na Straika wa Zambia, Obrey Chirwa, kuipa Bao la 3 Dakika ya 26.
Yanga waliongoza kwa Bao hizo 3 hadi Mapumziko. 

Kipindi cha Pili, Dakika ya 49, Mbaraka Yusuf, kwa mara ya pili, akaipa Kagera Sugar Bao lao la Pili lakini Yanga wakaja juu na kupiga Bao 3 nyingine katika Dakika za 58, 63 na 64 kupitia Deus Kaseke, Chirwa na Ngoma.

Timu ya Pili ni Yanga yenye Pointi 21 kwa Mechi 10 wakifungana na Stand United, waliocheza Mechi 12, lakini wana udhaifu wa Magoli na hivyo kushika Nafasi ya 3. 

Jumapili Oktoba 23 zipo Mechi 2 wakati Simba watakapocheza na Toto Africans ya Mwanza Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam na huko Sokoine, Mbeya ni kati ya Tanzania Prisons na Mbao FC.

Waamuzi wa Mtanange uliochezwa leo hii kwenye Uwanja wa Kaitaba Mjini Bukoba Kagera Sugar Dhidi ya Timu ya jijini Dar es Salaam Yanga.



Viongozi walisalimiana kabla ya kipute kuanza, Picha Zote na Faustine Ruta. Bukoba



Kikosi cha Yanga kilichoanza



Kikosi cha Kagera Sugar kilichoanza



Picha ya pamoja



Ngoma aliisawazishia bao Yanga mapema kipindi cha kwanza



Taswira mtanage ukiendelea

Mchezo huo umezalisha mabao nane ambapo Casillas alifungwa mabao matatu mepesi katika dakika 27 pekee alizokuwa langoni kabla ya Kocha Mecky Mexime kumtoa na kumuingiza David Burhan ambaye nae alifungwa matatu.
Cassilas alishindwa kujiamini langoni ambapo alifanya makosa kadhaa katika dakika chache alizodumu uwanjani ambapo kama washambuliaji wa Yanga wangeongeza umakini kabla ya mlinda mlango huyo kufanyiwa mabadiliko basi wangeweza kufunga zaidi ya mabao hayo kipindi cha kwanza.
Washambuliaji Obrey Chirwa na Donald Ngoma walifunga mabao mawili kila mmoja huku Simon Msuva na Deus Kaseke wakifunga moja moja na kukamilisha karamu hiyo ya mabao.














Shangwe...





































Furaha kwa ocha mkuu wa Yanga SC, Hans van Der Pluijm baada ya kuona Timu yake ikiinyeshea mvua ya mabao Timu ya Kagera Sukari.

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AWATAKA WANAWAKE KUWAFICHUA WAPENDA RUSHWA WANAOKWAMISHA HARAKATI ZAO ZA KUJIKOMBOA KIUCHUMI

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa ufunguzi wa Kongamano la pili la Sauti ya Wanawake Wajasiriamali Tanzania (VoWET) katika ukumbi wa  PH Planes Quality Plaza, Dar es Salaam.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa ufunguzi wa Kongamano la pili la Sauti ya Wanawake Wajasiriamali Tanzania (VoWET) katika ukumbi wa  PH Planes Quality Plaza, Dar es Salaam ambapo

Makamu wa Rais aliwataka Wanawake wajasiriamali kuwafichua watendaji wa mamlaka za kurasimisha biashara watakaowadai rushwa wakati wa kupatiwa huduma ya kurasimisha biashira zao.



Makamu wa Rais alitoa wito huo leo jijini Dar es Salaam wakati kufungua Kongamano la Pili la Sauti ya Wanawake Wajasirimali Tanzania (VoWET).



Alisema wanawake hawapaswi kuogopa kuwafichua watendaji wanaowaomba rushwa kwani wanawakwamisha katika harakati zao (wanawake) za kujiendeleza kibiashara,kiuchumi na pia kukwamisha juhudi za serikali katika kuinua maendeleo ya Wanawake nchini.


 Rais wa VoWET Bi. Maida Waziri (kulia) akihutubia wakati wa Kongamano la Pili la Sauti ya Wanawake Wajasiriamali Tanzania ambapo licha ya kupongeza jitihada za serikali ya awamu ya tano katika masuala mbali mbali ya kumuwezesha mwanamke pia alielezea changamoto ambazo wanawake wanakutana nazo katika shughuli zao za kuwainua kiuchumi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia baadhi ya kazi za ubunifu zilizofanywa na Wanawake Wajasiriamali kabla ya ufunguzi wa Kongamano la pili la Sauti ya Wanawake Wajasiriamali Tanzania (VoWET) katika ukumbi wa  PH Planes Quality Plaza, Dar es Salaam.
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

RC GAMBO APOKEA MSAADA WA BATI 500 NA MIFUKO YA SARUFI 500

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo(kwanza kushoto) akimshkuru Meneja wa Kampuni ya Hanil-Jiangsu Joint Venture Ltd, baada ya kuhakiki msaada wa mabati 500 na mifuko ya saruji 500.
Maneja Mradi wa Kampuni ya Hanil-Jiangsu Joint Venture Ltd, Bw.Xie (kulia mbele) akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo (mbele kushoto) mfuko wa saruji na bati kama sehemu ya msaada wa bati 500 na mifuko ya saruji 500 waliyoitoa kwa ajili ya kuwezesha huduma mbalimbali za Maendeleo katika Mkoa wa Arusha.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Mashaka Gambo (mbele) akishukuru Kampuni ya Hanil-Jiangsu Joint Venture Ltd kwa kutoa msaada kwa wananchi wa Arusha.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Mashaka Gambo(mbele kushoto) akikabidhi Mkuu wa Wilaya ya Arusha mifuko ya saruji 100 na bati 100 kwa ajili ya Ujenzi wa Kituo cha Afya Muriet.
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Arusha kupitia Tiket ya Ccm Catherine Magige(kwanza kushoto) akitoa shukrani kwa kampuni ya Ujenzi iliyotoa msaada kwa ajili ya kuwezesha huduma za kijamii Mkoani Arusha.
Mbunge wa Viti Maalum anayewakilisha Kundi la Walemavu kupitia Tiket ya Ccm Amina Mollel(kwanza kushoto) pia alitoa shukrani zake kwa kwa Kampuni iliyotoa msaada.
Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Athumani Kihamia (pili kulia) akishkuru kwa msaada wa Mabati 100 na Mifuko ya saruji 100 aliyopewa kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Afya Terrat.

Mhandisi wa Wakala wa barabara Mkoa wa Mkoa John Kalupale (kwanza kulia) akiwatambulisha wawakilishi wa Kampuni ya Hanil-Jiangsu Joint Venture Ltd walipokuja kukabidhi msaada wa mabati na Cement kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha. 
 
Kutoka kushoto ni Mbunge wa Viti Maalum Amina Mollel, Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe. Gabriel Daqarro pamoja na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa Mhe. Catherine Magige baada ya makabidhiano ya msaada wa mabati 500 na mifuko ya saruji 500 toka kampuni ya ujenzi wa barabara ya Sakina Tengeru na barabara ya Mchepuko.

…………………………………………….

Nteghenjwa Hosseah – Arusha

MKUU wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amepokea msaada wa bati 500 pamoja na mifuko ya saruji 500 kwa ajili ya kuwezesha huduma mbalimbali za maendeleo ikiwemo ujenzi wa zahanati pamoja na shule za msingi na sekondari za Mkoa wa Arusha.

Mara baada ya kukabidhi wa msaada huo nje ya jengo la Ofisi ya Mkuu huyo, Gambo alimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe. Gabriel Dararro mifuko 100 ya saruji na mabati 100 kwa ajili ya ujenzi kituo cha afya kinachojengwa eneo la kwa mama mbauda kata ya Muriet Jijini Arusha.

Alisema msaada huo utawezesha kila wilaya kunufaika nao kwani kila wilaya za mkoa wa Arusha kuna changamoto za uhaba wa vyumba vya madarasa pamoja na mahitaji ya majengo ya zahanati ili kusogeza huduma kwa wananchi.

Alimshukuru Meneja Mradi wa Kampuni ya ujenzi ya Hanil – Jiangsu Joint Venture Ltd, inayojenga barabara ya Sakina – Tengeru Km 14.1 na barabara ya Mchepuko Km 42.4 , Xie Jianbao ambao wametoa msaada huo kama sehemu ya kurudhisha kwa jamii ya watanzania ili kukuza mahusiano na kujali jamii na Taifa ambalo limewapa kazi kubwa ya ujenzi wa barabar hiyo itakayogharimu takribani Bil. 139.

“Naishukuru kampuni hii kwa kutoa msaada huo kwa ajili ya kuleta maendeleo na naahidi tutautumia ipasavyo katika kuleta maendeleo na kila wilaya nitakayofanya ziara msaada huo nitaupeleka ili ya kupunguza changamoto mbalimbali kwa jamii “.

Naye Meneja Mradi wa kampuni hiyo, Bw. Xie alisema kampuni yao imeona umuhimu wa kuchangia jamii kwani wao ni wajenzi wa barabara na wanastahili kurejesha faida kwa jamii inayowazunguka.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Mhe. Gabriel Daqarro alimshukuru Gambo kwa msaada huo na kusisitiza kuwa mifuko hiyo 100 ya saruji pamoja na bati 100 zitasaidia ujenzi wa kituo cha afya kinachojengwa Kata ya Muriet Jijini Arusha.

Naye Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, Athumani Kihamia alishukuru kwa msaada huo utakaosaidia ujenzi wa kituo cha afya kujengwa na kukamilika ndani ya miezi miwili na kuahidi kwamba atasimamia ipasavyo ili kuhakikisha Kituo kinajengwa katia ubora unaostahili.

Katika makabidhiano hayo yaliyohudhuriwa na wabunge wa Viti maalum wanawake Mkoa wa Arusha, Catherine Magige na Aminah Mollel walitoa rai kwa nyakati tofauti kwa wananchi wa mkoa wa Arusha kumuunga mkono Mhe. Gambo pamoja na Serikali ili kuwezesha maendeleo kusonga mbele.

TANESCO YASEMA NJIA YA KUSAFIRISHA UMEME KUPITA ARDHINI KATIKATI YA JIJI LA DAR ES SALAAM

$
0
0
 Kaimu Meneja Mradi wa uboreshaji wa huduma za umeme jijini Dar es Salaam, Mhandisi Iddi Rashidi, akizungumzia kukamilika kwa ujenzi wa mfumo wa njia ya kusafirisha umeme ardhini, (Underground Transmission Lines), kwenye shule ya sekondaru ya wasichana Jangwani jijini Dar es Salaam, Oktoba 22, 2016.
NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID

SHIRIKA la umeme nchini (TANESCO), limekamilisha ujenzi wa  mfumo wa njia ya usafirishaji umeme chini ya ardhi, (Underground Transmission Lines) ,  kutoka shule ya sekondari ya wasichana ya Jangwani jijini Dar es Salaam na kutoka kituo cha umeme cha Makumbusho kwenda kituo kipya cha kupozea umeme kilichoko katikati ya jiji cha City Centre cha ukubwa wa 100MVA (2X50MVA), 132/33KV.

Akizungumzia maendeleo ya utekelezaji wa mradi wa uboreshaji wa huduma za umeme jijini Dar es Salaam, Kaimu Meneja wa Mradi huo, Mhandisi Iddi Rashidi, alisema, kukamilika kwa ujenzi wa  mfumo huo ambao utahusisha ujenzi wa mfumo wa njia za usambazaji umeme chini ya ardhi (Underground Distribution Lines), wa kilomita 4.3 wa msongo wa kilovolti 33 kwa ajili ya kuunganisha kituo cha City Centre na vituo vingine vitatu vya Kariakoo, Railway na Sokoine.

Akifafanua zaidi, Mhandisi Rashidi alisema, ujenzi wa mfumo wa njia ya usafirishaji umeme chini ya ardhi (Underground Transmision Lines),  kwa msongo wa Kv132 kutoka Makumbusho kwenda kituo cha City Centre tayari umekamilika na ule wa kutoka shule ya sekondari ya wasichana Jangwani kwenye City Centre pia umekamilika.

“Faida kubwa ambayo wakazi wa jiji la Dar es Salaam watarajie ni kupata umeme wa uhakika (reliable power supply ulio kwenye viwango stahiki, (Acceptable quality power supply) hususan kwa wale wa maeneo ya katikati ya jiji,” Aliongeza Meneja wa TANESCO Mkoa wa Ilala, Mhandisi Athanasius Nangali.Akieleza zaidi, Mhandisi Nangai alisema, “Mradi huu unaviwezesha viituo tajwa kuwa na njia mbili za kuvvipatia umeme na hivyo kuwezesha kuwa na njia mbadala ya kupata umeme endapo njia moja kati ya hizo itakuwa na hitilafu.” Alifafanua.

Alisema kuongezeka kwa kituo cha City Centre cha 100MVA, kunafanya jiji la Dar es Salaam pekee kuwa na jumla ya vituo 9 vya aina hiyo.
“Hivi sasa tunaweza kusema, ujenzi umekamilika kwa zaidi ya asilimia 98, kinachoendelea ni kukamilisha ujenzi wa mfumo wa njia ya kusafirisha umeme kupitia juu (Overhead Transmission Lines), wa kilomita 1.3 wa msongo wa kilovolti 132 kutoka kituo kikubwa cha kupozea umeme cha Ilala hadi shule ya sekondari ya wasichana Jangwani ambapo utaungana na mfumo wa usafirishaji umeme chini ya ardhi, (Underground Transmission Lines) kwenda kituo kikubwa cha City Centre.” Alifafanua.

kutoka Makumbusho kwenda kituo cha City Centre, umekamilikakatikati yan jiji utekelezaji wa Mradi huo, unaofadhiliwa kwa pamoja na Serikali ya Tanzania na Finland, unahusisha ujenzi wa kituo cha udhibiti mifumo ya usambazaji umeme (Distribution SCADA System), katika msongo wa kilovolti 33 na 11.

“Tayari ujenzi wa kituo cha City Centre umekamilika kwa asilimia 100 na sasa tuko katika hatua za majaribio.” Alisema Mhandisi Rashidi.
Naye Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO, Bi. Leila Muhaji, amewaomba wakazi wa jiji kuwa wavumilivu wakati zoezi hili la kuboresha miundombinu likiendelea kwani huwa panatokea kukatika kwa umeme sehemu Fulani Fulani ili kutoa nafasi kwa mafundi kufanya kazi kwa usalama zaidi.
 Meneja wa TANESCO Mkoa wa Ilala, Mhandisi Athanasius Nangali, (kulia), akiwa na Kaimu Meneja Mradi, Mhandisi Iddi Rashidi wakati wakizungumza na waandishi wa habari kuhusu mradi huo
 Meneja wa TANESCO Mkoa wa Ilala,  Mhandisi Athanasius Nangali, (katikati), Kaimu Meneja Mradi, Mhandisi Iddi Rashid, (kulia), Afisa Habari na Mawasiliano wa TANESCO, Hendry Kilasila, wakitembelea eneo la ujenzi wa Mfumo huo shule ya sekondari Jangwani jijini Dar es Salaam
 Nguzo ya kusafirisha umeme wa juu kutoka Kituo cha Ilala kuja shule ya sekondari ya wasichana Jangwani, ambapo zitaungana na Mfuko wa njia ya kusafirisha umeme ardhini kupelekea katikati ya jiji

 Mafundi wakiwa kazini
 Mhandisi  Nangali, (mbele), Kaimu Meneja Mradi, Mhandisi Rashid, (kulia), wakiangalia moja ya roller lenye nyaya.

MANGULA ASHIRIKI KUFYATUA MATOFALI KUUNGA MKONO VIJANA WANAOSOMA NA WALIOHITIMU VYUO VIKUU 20

$
0
0
Makamu Mwenyekiti wa CCM-Bara, Philip Mangula akishiriki kufyatua matofali leo, kuunga mkono vijana 53 wanaosoma na waliohitimu Vyuo Vikuu 20, walioweka kambi ya kufyatua matofali 45,000 kwa ajli ya ujenzi wa mabweni na nyumba za walimu, katika shule ya Sekondari ya Nasabagani, iliyopo Kisiju, Wilayani Mkuranga mkoa wa Pwani. Mabweni ni kwa ajili ya Wanafunzi wa Kidato cha tano na cha sita, ambao kwa sasa wanalala chini katika chumba cha maabara ya shule hiyo.
Makamu Mwenyekiti wa CCM-Bara, Philip Mangula akichangaya saruji na mchanga, wakati akishiriki kufyatua matofali leo, kuunga mkono vijana 53 wanaosoma na waliohitimu Vyuo Vikuu 20, walioweka kambi ya kufyatua matofali 45,000 kwa ajli ya ujenzi wa mabweni na nyumba za walimu, katika shule ya Sekondari ya Nasabagani, iliyopo Kisiju, Wilayani Mkuranga mkoa wa Pwani.
Makamu Mwenyekiti wa CCM-Bara, Philip Mangula akishiriki kufyatua matofali leo, kuunga mkono vijana 53 wanaosoma na waliohitimu Vyuo Vikuu 20, walioweka kambi ya kufyatua matofali 45,000 kwa ajli ya ujenzi wa mabweni na nyumba za walimu, katika shule ya Sekondari ya Nasabagani, iliyopo Kisiju, Wilayani Mkuranga mkoa wa Pwani. Aliyevaa shati la kijani ni Katibu Msaidizi wa CCM mkoa wa Pwani, Abihudi Shilla akisaidiana na Mzee Mangula
Makamu Mwenyekiti wa CCM-Bara, Philip Mangula akisaidiana kubeba tofali na Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Filberto Sanga, baada ya kufyatua tofali hilo, wakati akishiriki kufyatua matofali leo, kuunga mkono vijana 53 wanaosoma na waliohitimu Vyuo Vikuu 20, walioweka kambi ya kufyatua matofali 45,000 kwa ajli ya ujenzi wa mabweni na nyumba za walimu, katika shule ya Sekondari ya Nasabagani, iliyopo Kisiju, Wilayani humo mkoa wa Pwani.
Mkuu wa wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani, Filbarto Sanga akimweleza jambo, Makamu Mwenyekiti wa CCM-Bara, Philip Mangula aliyetembelea eneo la ufyatuaji matofali kabla ya kushiriki ufyatuaji huo leo, kuunga mkono vijana 53 wanaosoma na waliohitimu Vyuo Vikuu 20, walioweka kambi ya kufyatua matofali 45,000 kwa ajli ya ujenzi wa mabweni na nyumba za walimu, katika shule ya Sekondari ya Nasabagani, iliyopo Kisiju, Wilayani Mkuranga mkoa wa Pwani. Kulia ni Mwenyekiti wa Kambi ya Vijana hao, Mwita Myamkururu.
Mkuu wa wilaya ya Kisarawe mkoa wa Pwani, Filbarto Sanga akimweleza jambo, Makamu Mwenyekiti wa CCM-Bara, Philip Mangula aliyetembelea eneo la ufyatuaji matofali kabla ya kushiriki ufyatuaji huo leo, kuunga mkono vijana 53 wanaosoma na waliohitimu Vyuo Vikuu 20, walioweka kambi ya kufyatua matofali 45,000 kwa ajli ya jenzi wa mabweni na nyumbaza walimu, katika shule ya Sekondari ya Nasabagani, iliyopo Kisiju, Wilayani Mkuranga mkoa wa Pwani. Kulia ni Mkuu wa Shule hiyo, Hillary Bwagidi
Makamu Mwenyekiti wa CCM-Bara, Philip Mangula, akikagua matofali yaliyokwishafyatuliwa na vijana 53 wanaosoma na waliohitimu Vyuo Vikuu 20, walioweka kambi ya kufyatua matofali 45,000 kwa ajli ya ujenzi wa mabweni na nyumba za walimu, katika shule ya Sekondari ya Nasabagani, iliyopo Kisiju, Wilayani Mkuranga mkoa wa Pwani Mkuu wa wilaya ya Kisarawe mkoa wa Pwani, alipofika kuwaunga mkono vijana hao leo. Nyuma yake ni Mkuuwa wilaya ya Mkuranga, Filbarto Sanga na katibu Msaidizi wa CCM mkoa wa Pwani, Abiudi Shilla. Picha zote na Bashir Nkoromo-Official CCM Blog. PICHA ZINGINE KEM KEM ZA TUKIO HILI/>>BOFYA HAPA
Viewing all 46384 articles
Browse latest View live




Latest Images